Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

AUAWA Kwa Kuchomwa Kisu Wakati Wakigombea Soda

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mkazi wa Olasiti, jijini Arusha, Hamisi Amani (17), kwa tuhuma za kumuua mwenzake wakati wakigombea soda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu, saa mbili usiku katika eneo la Kwa Morombo.

Kamanda Mkumbo alimtaja marehemu kuwa ni Novatus Tadei (26), mkazi wa Kwa Morombo na kwamba aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto.

“Marehemu na mtuhumiwa walikuwa wapishi kwenye kampuni inayojulikana kwa jina la ZZ Catering inayomilikiwa na Bashiri Ally.

“Siku ya tukio, marehemu pamoja na wafanyakazi wengine, akiwamo mtuhumiwa, baada ya kumaliza kazi waliyokuwa wanafanya, walipanda gari lenye namba za usajili T 375 CHH, aina ya Toyota Hiace wakirejea nyumbani.

“Wakiwa ndani ya gari hilo, mtuhumiwa Hamis aligundua kuwa soda aliyokuwa ameiweka ndani ya begi lake, haipo na kuanza kuhisi marehemu ndiye aliyeichukua.

“Kwa hiyo, ulizuka ugomvi baina yao na kuanza kutukanana matusi. Wakati ugomvi huo ukiendelea, mtuhumiwa alimkaba marehemu na kuchukua kisu wanachotumia kwenye shughuli zao za mapishi kilichokuwa ndani ya vyombo na kumchoma kifuani.

“Baada ya kuchomwa kisu, Tadei alianguka chini na jitihada za wafanyakazi wenzake waliokuwamo ndani ya gari hilo kuokoa maisha yake zilishindikana, kwani alifariki wakati anapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu,” alisema Kamanda Mkumbo.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.

MREMBO Huddah Monroe aeleza sababu ya kuitosa Wasafi Beach Party ya Diamond

$
0
0
Wasafi Beach Party iliyofanyika Disemba 24, Jangwani Sea Breezy jijini Dar es Salaam, ilikuwa iwakutanishe mahasimu warembo Huddah Monroe na Vera Sidika jukwaani kama mahost.

Wengi tulikuwa tukisubiri kushuhudia drama ya kufungia mwaka kutoka kwa warembo hao wa Kenya, lakini bahati mbaya fahari mmoja hakutokea.

Huddah Monroe ametumia Snapchat kuelezea sababu iliyomfanya ashindwe kuja kwenye party hiyo kuwa ni kushindwa kufikia makubaliano waliyokuwa wamejipangia na Diamond na hivyo ikamlazimu kukatisha kuja katika dakika za mwisho.

Hata hivyo Vera na mrembo mwingine wa Uganda, Anita Fabiola walikuwepo na kila kitu kilienda freshhh…

AUNTY Ezekiel : Siwezi tena 'ku-kiss' Kwenye Movie

$
0
0
Star wa Bongo Movie nchini mwanadada Aunty Ezekiel, amerudi upya kwenye tasnia hiyo huku akiweka wazi baadhi ya mabadiliko aliyoyafanya katika maisha yake kuwa ni pamoja na kutoweza tena 'ku-kiss' kwenye movie atakazocheza.

Aunty ambaye kwa sasa amerejea na movie mpya inayokwenda kwa jina la Chritmass Eve, amesema kilichomfanya afikie maamuzi hayo ni majukumu aliyonayo kwa sasa ya kifamilia ikiwa ni pamoja na malezi ya mtoto.

Akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV Aunty amesema kuanzia sasa akiwa kwenye movie, kabla hajakubali ku-kiss na mtu kwanza anamkumbuka mtoto wake huku akitaja mabadiliko mengine kuwa ni kuweza kuigiza kama 'house girl' uhusika ambao awali aliwahi kusema hawezi kuuigiza.

"Nimechenji baada ya kuzaa, nimekuwa na mawazo tofauti, nimerudi nyuma mara mbili hata ikitokea kwenye movie natakiwa ku-kiss, najifikiria sana hivi mwanangu akiona atafikiria nini" Alisema

Amesema hivi sasa amebadilika kwa kuwa amekuwa mtu mzima na kusisitiza kuwa kwa sasa ameacha mabo yote ya kitoto aliyokuwa akiyafanya ikiwemo kuishi kwa skendo maana ameona hayana faida.

Katika hatua nyingine Aunt alisema anatarajia kupata mtoto wa pili ambaye angependa awe wa kike

UMEWAHI Kusikia Skendo ya Rose Mhando Kutumia Madawa ya Kulevya? Mwenyewe Kafunguka Haya

$
0
0

Msanii mkongwe wa nyimbo za Injili nchini Rose Muhando amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa ameingia katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Muimbaji huyo alidai taarifa hizo zilisambazwa na watu ambao hawamtakii mema katika maisha yake kutokana na kwenda nao tofauti katika makubaliano ya kufanya nao kazi.

“Situmii madawa na sitatumia, kama waliona ndiyo skendo itakayonimaliza wameshindwa, wanaofanya hivyo ni watu wanaotaka kunimaliza walitaka nifanye kazi zao, nikakataa.” Rose aliuambiia mtandao wa gazeti la Mwanaspoti.

Aliongeza, “Sijajiingiza na mambo hayo na wanavyozungumza nasikitika kwa sababu wanaiumiza familia yangu kisaikolojia, mimi ni mama wa watoto watatu na nina ndugu zangu, naambiwa mambo yote hayo kwa sababu sina mtu wa kunitetea,”

Katika katua nyingine muimbaji huyo alizungumzia kuhusu ukimya wake pamoja na ujio wake mpya.

“Nipo hata hivyo kuna kazi nyingine nimeandaa ipo kwa Alex Msama bado haijatoka kutokana na mambo mbalimbali, ingawa naandaa kazi nyingine ninayotegemea kuikamilisha mwezi wa tatu mwakani tutakapojaaliwa. Nimeshaanza kuandaa baadhi ya nyimbo na nyingine naendelea kutunga, unajua kazi hizi huwa nasikiliza sauti ya Mungu aniambie niimbe nini.”

“Pia, nimekuwa nafanya huduma ya kuimba katika mikutano tofauti ndani na nje ya nchi kama hivi jana umenikuta natoka kijiji cha jirani kuimba na wiki iliyopita, nilikuwa Kenya ambako nilifanya huduma, Kisumu na Mombasa, nimeamua kufanya hivyo kwa sababu zangu,” anasema Rose.

DHAMANI ya Mbunge Godbless Lema Yakwaa Kisiki Tena..Arudishwa Rumande

$
0
0
Mbunge Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.

Rufaa hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.

Upande wa mtuhumiwa uliongezea muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda uliokuwa umepangwa awali.

Mbunge Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.

VIDEO:Rais wa Bolivia Anaswa Akitazama Video ya Ngono Mahakamni.....

$
0
0
Rais wa Bolivia, Evo Morales amekumbwa na fedheha kubwa baada ya simu yae kutoa sauti zinazoaminika ni za watu wanaofanya ngono wakati akiwa katika kikao ndani ya mahakama.

Mkasa huo umetokea wakati Rais huyo akiwa katika mazungumzo na wanasheria wa kimataifa kabla ya kuchukua simu yake na muda mfupi sauti za mwanamke na miguno zinasikika kutoka kwenye simu hiyo ndipo ghafla akaitupa chini.

Video hiyo iliyovujishwa na mtandao wa LiveLeak.com  imewaacha watu wengi waliokuwa ndani ya mahakama hiyo wakicheka kufuatia tukio hilo huku baaadhi wakiishia kuguna.

Itazame hapa chini video hiyo ya mkasa wa wa Rais wa Bolivia.


VIDEO:Mashabiki Wadai Fedha zao Baada ya Ali Kiba Kushindwa Kufanya Show Dodoma

$
0
0
Disemba 25, ikiwa ni sikukuu ya Krismasi mashabiki wa mwanamuziki Ali Kiba walibaki wakiwa wamepigwa butwaa bila kuona mtu jukwaani huku muda ukiyoyoma katika tamasha la muziki ambalo Ali Kiba alitakiwa kutumbuiza siku hiyo.

Hadi inafika saa saba usiku mwanamuziki hiyo hakuwepo ukumbini alipotakiwa kuanza kutumbuiza saa nne. Baadhi ya watu waliokuwa ndani ya ukumbi walianza kuleta vurugu na kudai fedha zao ili waondoke kwani muda ulikuwa umekwenda sana.

Akizungumza, mtayarishaji wa tamasha hilo Rashid Adam maarufu Chidi Perugina alisema tatizo kubwa lilikuwa ni suala la usafiri ambapo Ali Kiba alichelewa kufika mkoani Dodoma.

Ali Kiba alikuwa Nairobi na alitegema apande ndege awahi kufika Dar es Salaam na kisha aanze safari ya kuja Dodoma, lakini tatizo lilitokea baada ya Ali Kiba kukosa ndege ya kwanza aliyotakiwa kutoka nayo Nairobi. Ndege ya pili aliyopanda ilichelewa kufika Dar es Salaam na kuanza mchakato wa safari ya kufika Dodoma ulisababisha Ali Kiba kufika hapa saa saba usiku na madakika, alisema Rashid Adam.

Baada ya Ali Kiba kufika aliwaomba radhi mashabiki wake wachache waliokuwa bado wapo ukumbini na hakuweza kutumbuiza sababu ya uchache wao.


Baada ya tamasha hilo kusindwa kufanyika hiyo tarehe 25 Disemba, Ali Kiba anatarajiwa kutumbuiza terehe 28, Januari 2017 ambapo mashabiki walio na tiketi wametakiwa kuzitunza ili kuzitumia kwenye tamasha hilo lingine. Angalia Video:

HUYU Hapa Mwanamuziki wa Bongo Flava Anayetamani Kumuoa Rapper wa Kike Chemical

$
0
0
Rapper Stereo amedai kuwa anatamani rapper Chemical aje kuwa mke wake wa ndoa.
Stereo amesema Chemical ambaye jina lake halisi ni Claudia Lubao ni msichana anayemzimia kupita maelezo. Ameamua kufungua moyo wake kwenye mahojiano na mtangazaji wa CG FM ya Tabora, Manoni MJ wa Pili.

“Nadhani tukioana tutakuwa na familia hivi ya aina yake,” alisema Stereo na kuongeza kuwa bado hajamweleza Chemical takwa la moyo wake.

“Mimi nampenda Chemical kuliko mnavyofikiria,” amesisitiza rapper huyo.

SHILOLE Ashambuliwa Baada ya Kusema ‘Najivunia Mwaka 2016 Nimepata Bwana Mpya’

$
0
0
Msanii wa muziki Shilole amejikuta akishambuliwa na mashabiki wake wa muziki katika mtandao ya Instagram baada ya kuandika kitu cha utani kwamba anachojivunia ndani ya mwaka 2016 ni kupata bwana mpya.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mtoto Mdogo’ akiwa amemshirikisha msanii wa Singeli Man Fongo, hivi karibuni kupitia birthday yake alimtambulisha mpenzi wake huyo.

Katika instagram yake Shilole aliandika

:Mwaka unaenda kuisha je kipi umefanya cha maendeleo.???? Kwa upande wangu mm maendeleo yangu nimepata bwana mpya😂😂😂😂😂 joking

Kauli hiyo iliwafanya mashabiki wa mtandao huo kuanza kumshambulia muimbaji huyo. Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki wao.

Nick.mwenda
Vitu unavyovifanya leo najua baada ya miaka kumi ijayo ndo utaona faida yake au hasari zake hipo usiku hizo tatoo zitakukosti umri auludi nyuma Bali usonga mbele

Piei_raita
Enzi uko bongo movie nilikua nakukubali kinoma ila ulipoingia bongo freva umekua ni mtu wakushobokea mabwana wadogo wadogo mwishoe utanitaka na mimi

Jesikamwalongo
Angalia sana maisha yako usipende kuyumbayumba jua wewe no kioo kwa jamii,

Mbwenitegg
Sihuyo unatuonyeshA bwana Mpya maendeleo kwa upande wako Sasa hatujui kama kakuowa au bado boyfriend na girlfriend zile za usichana bado anyway good for you and life is not fun,

Fkibonde7
Hv mpk ss umekuwa na mabwana wangap na kwa nn unapenda vijana wadogo na unahic watoto wako wanajifunza nn toka kwako.

osca_john
Kunakipindi pesa sikitu jitaidi kuzingatia umakini usipagawe naustaaaa tulia tafakari usileweshwe nasifa

MASHABIKI wa Alikiba Wamvaa Seven Mosha, Wasema Wamechoshwa na Hujuma zake Dhidi ya King

$
0
0
Baada ya seke seka la Msanii Alikiba kushutumiwa kuondoka na pesa za watu na kushindwa kupiga show huko Dodoma...Mashabiki wa Alikiba wameamua kumjia juu Manager wa msanii huyo Bi Seven Mosha na kumtuhumu kuwa anachangia sana msanii huyo kurudi nyuma kimziki.

Baadhi ya mashabiki walimtuhumu Bi Mosha kuruhusu Alikiba kukubali Show ya kiwango cha chini kiasi kile ambapo wengine walisema pale palikuwa ni grocery na wengine wakisema ilikuwa ni bar na wakaongeza hapa speaker zenyewe ziliwekwa juu ya cret la bia kudhihirisha show ilikuwa ya kiwango cha chini sana na hakukuwa na maandalizi.

Wengine mtuhumu manager kuwa ameshindwa kumuongoza Alikiba na kumtafutia show za viwango wakati anajua mashabiki anao na walienda mbele zaidi wakitaka aache kazi ya kummanage msanii Alikiba kwakuwa anamshusha sana..

Mashabiki wa Alikiba hawakuishia hapo walisema wamevumilia na wamechoshwa sana maana hata taarifa za show huwa hawapewi au kinacho fata au kuendelea kwa msanii Alikiba hawapewi updates na Manager amekuwa akitoa kwa kujisikia au anavyo taka yeye na haendani na dunia ya sasa inavyotaka manager awe.

Maoni yangu.

Binafsi naona Seven Mosha ana wakati mgumu sana kuwa manager aina ya wasanii alio nao...
Mfano msanii kama Alikiba ni wazi kabisa ni mvivu na ana kiburi na dharau sana kwa hiyo mashabiki wanaweza kuwa na haki ya kumtuhumu manager lakini wanashindwa kujua wanamshabikia msanii wa aina gani. Alikiba yuko nyuma sana hata kutoa taarifa ambazo anapaswa kuzitoa ni kazi ngumu na anaona uvivu....kwakweli muhurumieni dada Manager.

Pili mashabiki wakitaka kujua Alikiba ni tatizo wamuangalie msanii mwenzie ambaye wako lebel moja Lady jaydee... Lady Jaydee pamoja na kuwa na kiburi sana linapokuja swala la kazi yake hasa muziki yuko shapu sana na hata mashabiki wake hupata taarifa mapema na hana midhaa kwenye kazi na si mtu wa kukubali show za kitoto na anajua ana thamani gani...

Ukweli ni kwamba Alikiba anatakiwa awe wa kwanza kubadilika ajue kuwa yeye anawahitaji zaidi mashabiki na muziki ndio unao muweka mjini na kumtunza. Kuna mwana JF snowhite alisema hivi nalimuelewa sana alisema kuwa "Alikiba anavyo fanya mambo yake utafikiri mashabiki ndio wanatakiwa kuimba na kupiga show na yeye ndio anunue kazi zao"
Hii sentensi niliitafakari nakuona inaongea mengi sana kuhusu Alikiba.

Hivyo tatizo lililokubwa zaidi ni Alikiba kuliko Seven Mosha.

Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki wa Alikiba wakimjia juu Seven Mosha kwenye ukurasa wake wa picha.

Aisee naomba ujitokeze uzungumzie iki kilichotokea meneja@sevenmosha tulipokuwa tumefikia ilikuwa tunaanza kukimbizana na watu wengine ila ii ni aibu kubwa umetuangusha kazidiwa ata akina barakh iv tunaomba uite midia utoeaelezo ila ukikaa kimyaa tutaisi unatumika kiba angekuwa mbali kama menejer ungekuwa unachangamka ninaisi mashabiki umewakatisha tamaaa show gani ile tunaomba maelezo au jiuzulu kiba ni msanii mkubwa jina lake kipata mtu anayejua kazi mbona mtamkoma:



  • fetttyy_POLENI YALIYOTOKEA VYENYE KATIKA SHOW YA DODOMA
  • full__shangweMeneja ulichokifanya usije ukarudia tena umetukera sana mashabiki @sevenmosha
  • sayyidna_ambar@sevenmosha kama umeshindwa kua manager wa @officialalikiba basi achana nae ila si kutushusha hivi eti kweli ww unashindwa kumtengezea show ya mana kiba ah dada ee tushachoka unachotufanyia kila siku unaturudisha nyuma baada ya kwenda mbele unashindwa kumtafutia@officialalikiba collabo za maana show za maana hapa umetuangusha tena umezidi dah kama nini tusamehe tu inafika hatua mpaka wasanii wa niger wanatamka kufanya collabo na kiba kama davido ww hufatilii baada ya kumuimbisha na kina nuh mziwanda ah umezingua mama tena sana@officialalikiba si lazima kuwa na management mbovu kama hi
  • abdallahkhalfan97dada it's your time now if is there any problem just fix it then kila kitu kiende sawa tunakuaminia Malkia wetu wa nguvu
  • eng.zombieMsanii mkubwa Africa ukafanye show pale Kweli dah hii aibu sana @officialalikiba best African artists MTVema akafanye show bar sijui pub manager hapo serious Kweli @sevenmosha mnachosha watu wanaowapa support sasa hapo unapanda au unashuka dah ktk upuuzi ambao ulinikera Leo dah
  • full__shangweNaskia @officialalikiba anakula huu mzigo @sevenmosha ndo maana huyu dem anafanya kaz kwa mazoea
  • 255_queenKumpeleka alikiba kupiga show bar, haikua kitu kizuri!! Hard fans wa kiba lkn ckupendezewa!! International artist kwenda kumpa show kama za local c kitu poa
  • costaleh2@255_queen acha izo usipende kushutumu pasipo hakika ya jambo
  • 255_queen@costaleh2 usiingilie Uhuru wangu wa kuongea please!!! Kwangu mm kingkiba ni international artist hana hadhi ya kwenda kupiga show pale tena ktk kijukwaa ambacho hakina hata hadhi!! Mtu ambaye keshapiga show MTV kisha anaanzaje kwenda kupiga show eneo kama lile. Nafkr haujapaona ile sehemu lkn laiti kama ungeona video ya eneo la tukio ungenielewa naongea nn!
  • jumawendo@sevenmosha we are fade up of you....and shame on you...what the hell are you doing with our talented guy @officialalikiba
  • magaaziDaaaa Hii ya king dodoma not fair si grocery pale et speaker lipo juu ya kret it pain yani sioni unachokifanya me nafikili ungebaki tu nyumbani upike ugali umeneja umekushinda@sevenmosha
  • llovesadam_Mama kwa kile kilichotokea dodoma mashabiki tumemia sana mana hatukutegemea kabisa sasa kama kweli unatujali mashabiik wa msannii wako basi tungeomba ututolee ufafanuz juu ya hilo swala na pia tunaomba uwe unatuweka waz juu ya mipango yenu ya kaz ili muwe mnatupa moyo ss mashabiki na pia uwandae show kubwa ambyo itasababisha habar nzur apa mujin tunaomba sana na pia ujaribu kuzijibu text zetu
  • maggy_dolCan kiba pliz change his management
  • singl34realkaz imekushinda meneja naona huwez pambana na vidume wanakizid akil embu jiuzulu tutafute meneja wa kiume anayechapa kaz kisawasawa maana nimegundua kikwazo kikibwa hapa ni ww unafanya kaz kiuogauoga sana huiwez hii vita walah acha tu kapumzike
  • asnathdavid@ilovesadam_ tatzo nyinyi mnataka kila kitu anachofanya diamond muige, waacheni kiba na management yake wafanye kaz kadri ya uwezo wao, Kama diamond kaandaa show sio lazma na kiba aandae show
  • vankempesKuna vitu mnavipoteza sana huo ukimya unazidi sijui labda ni ujeur au kwa kuwa mshakuwa na maisha yenu mazur labda ila wanaoumia ni mashabiki meneja jaribu kurekebisha tatizo
  • tozzmzeeHakika nawaambieni @sevenmosha @sevenmosha@officialalikiba @officialalikiba najua mpo bize mnakazi nyingi za kufanya ila nawaomba plz jalibuni kupitia hizi coment za mashabiki wanataka nini na mjue ni wap mnakwama na mjue jinsigani mtatatua tatizo kwa namna moja au nyingine hamjui ni jinsgani mashabiki wanu tunaumia paletunapoona uongozi mzima wa juu mnashindwa kufanya kazi yenu vile ipasavyo sisi kama #bloodfans_wa_king_kiba tupo imala mungu mbariki @officialikiba
  • ireneothuman_arsenalYaani duh!kionhozi mkakataa show ya miss TZ mnakuja kutupelekea msanii wetu bar??
  • eggson_Minaona we dada unatumika kumuangusha kiba asitoke zaidi ya alipo saivi kama vipi kaeni mezani mvunje mikataba kiba atafute meneja mwingine akuna cha nimetoka nae mbali saivi dunia imebadirika mziki umebadrika nenda na kasi ya mabadiko kama umechemka kaa pembeni unatuaibisha mtaji wa msanii ni kuwa na mashabiki muhimu ambao unajua ata niende wapi nipo nao sa we uoni mashabiki wamaidi sana au unachukulia kawaida ii inaweza muathiri kiba wetu amashiriki tuzo kiba saivi morari ya kumpigia kura watu imepumgua uoni au tunaomba menejiment ieshimu mashabiki wa kiba ndomtaji wake tunaba utupe ufafanizi wa kinachoendelea juu yako na kiba @sevenmosha
  • 255_queen@costaleh2 nmekutag uone video kule ktk page eti unajifanya haunielewi ile ni video ya kiba show yke ya dom
  • johnhappy592Umeneja umekushinda kaa nyumbani umenejimenti familia yako tuachie @officialalikiba) tumekuchoka meneja gani wewe unashindwa kuwapa ufafanuzi mashabiki? @sevenmosha sisi kama mashabiki tumekuchoka huna nia njema
  • officialollystar1@johnhappy592 some times mashabiki wa tz mnakurupuka kucoment bila kutafakar mambo kiundani ili mrad uonekane umecoment tu .Kama umeneja umemshinda jarb wwe @sevenmosha hakuanza Leo kumanage in shot kama unakumbukumbua nzr kuhusu 0ne 8 utagundua Ali na seven wametoka wap
  • king_benayaNina vidio ya show ya @officialalikiba kubuma dodoma anetaka anione wasap 0717000200. Mm naish dodoma na nilishuhudia kwa macho show ikibuma. Nichek wasap nikutumie vidio
  • official_beca_safari_26Muko watu wengi lkn mawazo yenu mgando siku zote inshu mbaya zote zinatokea kwa @officialalikiba kuanzia Mombasa kuzimiwa mic leo tena Dodoma @sevenmosha tumechoka sisi tunaongea kwa uchungu sababu tunaumia km kz imekushinda pisha watu wingine hapo ndio mwisho wa Uwezo wako
  • wamsumbami napita tu. ..maana niliuliza siku tatu kabla ya show lakini nikaonekana mropokaji. ..wacha muvi iendelee. .seven ww ni mpambanaji sana na umemtoa kiba mbali sana...uko vizuri sana upstairs. .na tunategemea makubwa kutoka kwako ila ushauri wangu kwenu hakikisheni mnapromote show za kiba zote. ..achaneni na mawazo ya tunajaza ukumbi ba
  • wamsumbaAchaneni na mawazo ya tunajaza ukumbi bila hata kupromote show. ..show ni Biashar a kwa muaandaji na mtaji kwenu pia kuwa unapendwa ndio mana watu wanajaa. ..na show ni matangazo
  • macho_official1Nini kilitokea you took too much
  • magaaziIla the truth manager is a person who is responsible for the work of others, thus King ndo boss then seveen ni mwajiliwa hence king why fire huyu mtu ur a boss
  • johnhappy592@officialollystar1 nikweli wametoka mbali sijakataa ila wanaboa sana kukaa kwao kimya kazi yameneja ninini?hivi kwahadhi aliyonayo kiba niyakufanya shoo kwenye ule ukumbi?

Source:Ruttashobolwa/JF

BODI ya Mikopo Kufanya Msako Nchi Nzima Kwa Waajiri Sugu Wasiowasilisha Makato na Majina ya Wadaiwa

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru ameunda kikosi maalumu (Task force) kwa ajili ya msako wa kuwanasa waajiri sugu wote nchini wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Badru amesema kikosi kazi hicho kitaanza kazi Januari 2, mwaka 2017 na kitafanya kazi hiyo kwa siku 14 mfululizo wakipita ofisi moja baada ya nyingine.

MPENZI Wangu Analilia Nimnunulie Gari Kukwepa Miluzi Barabarani

$
0
0
Asikuambie mtu presha ya mwanaume yoyote ipo pale anapojua kuna mbaya wake anataka kufaidi ile raha anayoipata yeye naumia kila niwapo faragha na mpenzi wangu nikiwaza vitu hadimu anavyonipa bila hiyana bila uchoyo na mchezo anavyouweza hadi nachanganyikiwa mtoto kweli mashalaaaa akitembea utadhani kadondoka hajazaliwa.

Mtoto kaja juu kuwa akitembea mitaani watu wanapiga kelele na miluzi sana kwa wingi kitu kinachomkera sasa kaja juu kua nimnunulie gari maana kazichoka hizi kelele nashindwa nifanyeje kwa kweli, naumia sana na nikiwaza tuu nahisi kuchanganyikiwa mimi.

Nifanyeje niudhibiti huu mzigo?

WASSIRA Akimbilia Mahakama ya Rufaa Kumpinga Bulaya

$
0
0
WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

AZAM FC imewafuta kazi makocha wake kutokea Hispania

$
0
0

Azam FC imeamua kuwatimua makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.

Uamuzi wa Azam umekuja baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu tangu ‘wahispaniola’ walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya Stewart Hall kubwaga manyanga.

“Uongozi wa Azam FC umewatimua makocha wao leo mchana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili,” chanzo cha kuaminika toka ndani ya Azam FC kimeiambia shaffihdauda.co.tz.

Katika mechi 17 za VPL ambazo Hernandez alisimama kama kocha mkuu wa Azam FC, timu hiyo imeshinda mechi saba (7), imetoka sare mara sita (6) na kupoteza michezo minne (4).

Hadi sasa Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17. Azam inazidiwa pointi 14 na Simba ambao ndio vinara wa ligi huku wakiwa nyuma kwa pointi 10 dhidi ya Yanga huku wakizidiwa pointi moja na Kagera Sugar.

KESI ya Mmiliki wa Jamii Forums Kuendelea Leo Mahakamani

$
0
0

Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo inatarajiwa kutajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media inayoendesha mitandao ya JamiiForums na Fikra Pevu, anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuendesha tovuti isiyosajiliwa nchini.

PRODUCER Mr T Touch Adai Hataki Kusikia Habari za Nay wa Mitego

$
0
0
Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva Mr T Touch ambaye kwa mwaka 2016 ametengeneza ngoma nyingi kali na zilizofanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari amefunguka na kusema haitaji tena kumzungumzia Nay wa Mitego

Mr T Touch ambaye alikuwa ni moja kati ya maproducer wa Nay wa Mitego ambaye ametengeneza ngoma nyingi za Nay wa Mitego zilizofanya vyema sana kipindi cha nyuma alisema anawashukuru sana watu ambao wamekuwa na mchango kwake katika kufanikiwa na kupiga hatua za maendeleo.

"Nilishasema zihitaji habari za kiuhanagwa kama hizi, mimi sihitaji kumzungumzia huyo Nay wa Mitego, tuzungumzie shughuli yangu na mipango yangu kwa mwaka 2017 kwani mjini usipokuwa na shughuli watu hawawezi kukuelewa kidogo, kwa hiyo tusimzungumzie atakapokuwa na shughuli nadhani hiyo shughuli itanihusu kwa hiyo tusimzungumzie" alisikika Nay wa Mitego kwenye kipindi cha eNEWZ

MITANDAO ya Kijamii Hatari zaidi Kuongeza Ugaidi

$
0
0
Vikundi vya kigaidi vinatumia aina zote mpya za mitandao ya kijamii na teknolojia ya mawasiliano ili kupanua wigo wa mitandao yao sambamba na kufadhili shughuli zao.

Hiyo ni kwa mujibu mwakilishi wa kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi, Delphine Schantz ambapo amesema tovuti na majukwaa mbali mbali kwenye mitandao hiyo inatumika kuchangisha fedha na kununua silaha kupitia kwenye mitandao.

Aidha ameongeza kuwa juhudi za pamoja zahitajika kufuatilia mifumo hiyo kwa kuwa Hakuna nchi mwanachama ambayo ni salama dhidi ya ugaidi au salama dhidi ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya ugaidi.

Bi. Schantz amesema kamati yao hivi sasa inafuatilia tovuti zinazohusika na uandikishaji magaidi na uchangishaji fedha lakini jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wana uelewa wa kutosha kuwa mitandao hiyo inaweza kutumika vibaya kueneza ujumbe mbaya wa kuchangisha fedha kwa ajili ya ugaidi.

WASHINDI wa WatsUPTV African Awards 2016...Watanzania Nao Wamo

$
0
0
Usiku wa December 28 2016 tuzo za WatsUp TV Africa Music Video Awards 2016 ndio zilitangazwa Accra Ghana, washindi 22 walitangazwa kupitia Press Conference wakiwemo wasanii wa Tanzania waliyofanikiwa kushinda tuzo hizo kwa mwaka 2016.

Kama hufahamu WatsUp TV Africa Music Video Awards (WAMVA) ni tuzo ambazo zinaandaliwa na WatsUP TV, zikiwa na lengo la kushawishi au kuhamasisha wasanii kufanya video za viwango vya juu pamoja na ubora.

Wametangazwa washindi 22 wasanii na waongozaji wa video 170 waliyokuwa wametajwa kuwania tuzo hizo wakati zinazinduliwa mwezi September 2016, kwa mujibu wa mtandao wa Zionfelix.net ni kuwa washindi watafanya show katika tamasha la Made in Africa litakalofanyika 2017 Accra Ghana.


List ya washindi wote 22 waliyotangazwa

Best Newcomer Video of the Year
Harmonize ft Diamond Platinium ( Badoo)

Best African Reggae Dancehall Video
Shatta Wale ( Chop Kiss ) Ghana

Best Afro Pop Video
Scientific Ft Quincy B (Rotate) Liberria

Best African Hip Pop Video
Iba One (Dokera) Mali

Best African RnB Video
Alikiba (Aje) Tanzania

Best African Traditional Video
Tay Grin FT 2BABA ( Chipapaa ) Malawi

Best African Dance Video
Oudy 1ER (Lokolo) Guinea

Best African Collabo Video
Diamond ft AKA (Make we sing ) Tanzania

Best African group Video
Navy Kenzo (Kamatia ) Tanzania

Best African Male Video
Diamond Platinium ft Psquare ( Kidogo ) Tanzania

Best African Female Video
Vivian Chidid ( Wuyuma) Senegal

Best African Performance
DJ Arafat (Concert a Korkogo) Cote D’Ivorire

Best International Video
Beyonce – Formation (USA)

Best East African Video
Alikiba (Aje) Tanzania

Best Central African Video
Ferre Gola ft Voctoria Kimani (Tucheze) DR Congo

Best North Africa
Ibtissam Tiskat

Best South African Video
Casper Nyvorvest (War Ready)

West Africa Video
DJ Arafat

Best African Video Director
Godfather Kidogo (Nigeria)

Best African Music of the Year
Diamond Platinium ft PSquare (Kidogo) Tanzania

Special Recognition Award Music Video Africa
Mr Eazi ft Efya (Skin Tight) Nigeria

Viewer’s Choice Awards
Designer Panda (USA)

TATHIMINI Ya show Ya Diamond Dar na Iringa na Mtonyo Alioingiza Ndani ya Siku Mbili

$
0
0
Najua wengi mlikuwa Mkisubiri hili jwa hamu kujua tadhimini nzima ya show mbili za Diamond na Team nzima ya Wasafi zilizo Fanyika Iringa na Dar! Sasa leo nimekuleteeni tathimini ya show zote mbili alizo Fanya Diamond!

Kabla sijatoa tathimini nzima naomba ifahamike hizi show zote mbili za Diamond zilikuwa na Mdhamini mkubwa ambaye ni VODACOM huyu amedhamini show zote mbili Dar na Iringa hadi kupelekea show Hiyo kuitwa VODACOM WASAFI BEACH FESTIVAL! Kama unajua kadhi ya mdhamini basi ujue hicho ndicho walicho Fanya Vodacom moja ya Kazi yao kubwa ni KUANDAA NA KUTEKELEZA MATAYATISHO YOTE YA SHOW ZOTE MBILI.....kuanzia stage na kuwalipa wote walio husika kwa namna moja au nyengine ikiwa ni pamoja na malipo ya wasanii wote walio toka nje ya Tanzania chini ya SALLAM,NA BABU Tale,Malipo ya matangazo yote ikiwa ni pamoja na kuwalipa Clouds Fm na Ebony Fm walio husika katika kutangaza hii show Dar na Iringa!,Kusafirisha na kulipia sehemu ambazo show itafika na wahusika kama vile kulipia Jangwani na Samora! .... Kwa kuwa Diamond ndie alie na Mkataba na Vodacom huenda pia vodacom ilihusika kuwalipa Harmonize,Rich Mavoko,Rayvanny na Queen Darling (JAPO KWA HILI SINA UHAKIKA SANAA ILA MSININUKUU VIBAYA)

Kifupi katika tathimini ninayo ileta Pesa Iliyo patikana ni itaingia moja kwa moja Katika Lebal ya WCB na Itafuata mkataba unavo sema kwa ma meneja!

Tukianzia na Dar Diamond aliingiza Mashabiki zaidi ya 3000 ikiwa sehemu waliyo iindaa ilikuwa na uwezo wa kuchukua watu 1500 hivyo waliingia Mara mbili ya Mategemeo Yao! Na kulikuwa na Tiketi za aina mbili kawaida na VIP.......Tukianza na Kawaida ambayo kiingilio kilikuwa 30,000 waliuza tiketi zaidi ya 2,800

Sasa chukua 2,800+×30,000= Millioni 84+

Kwa VIP waliuza Tiketi 200+ ambapo kila tiketi iliuzwa kwa shilingi 100,000

Sasa chukua 200+x100,000=Millioni 20+

Kwa Dar Jumla ni sh.Millioni 104+

Baada ya Hapo ni Alienda kufanya Show Iringa! Iringa alifanikiwa kuingiza watu 9,000+ kwa kiingilio cha sh 10,000

Sasa chukua 9,000+×10,000=Millioni 90+

Sasa chukua Millioni 104+ + Millioni 90+ =Millioni 194+

Hiyo hela ni kaingiza kwa Siku mbili Tuu!

Kifupi hiyo ndiyo tathimini ya haraka haraka sasa kaaa wewe na Nafsi yako jiulize Ni msanii gani mwingine Tanzania hii anaweza kufanya hivyo? Ifike muda anae Jua apewe heshima yake!

Wasanii wengine waangalie Mikataba ya kuingia..watu walimlaumu Diamond kwa kutokushiriki Fiesta kwa kuwa na Mkataba na Vodacom sasa nafikiri sasa mnaelewa maana ya mkataba alio ingia nao na manufaa anayo yapata! Imagine bila vodacom Diamond hizo millioni 104+ angezigawa vipi?

Sasa kupitia Vodacom wanataka kuzindua Wasafi Festival Ambayo watazunguka mikoa 10 Tanzania wakiaanza na Dar tarehe 14 Feb! Wakiwa na Vodacom means hiyo itakuwa ni zaidi ya Fiesta!

Hiyo Tathimini

DANYA nawasilisha!

MWALIMU Anaswa Akiishi Kinyumba na Mwanafunzi Wake.....

$
0
0
WANANCHI katika kijiji na kata ya Guta, wilaya ya Bunda mkoani Mara, wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya walimu katika kata hiyo, kwa kufanya ngono na wanafunzi na kuishi nao kinyumba kama wake zao.

Hatua hiyo ya kulaani inatokana na hivi karibuni kumkamata mwalimu wa shule ye Msingi Guta, akiishi na mwanafunzi wa shule hiyo kinyumba kama mkewe.

Wananchi wa kata hiyo wakiongozwa na diwani wao, Kigo Nyamhanga, jana waliwaambia waandishi wa habari kwa njia za simu za mkononi kuwa hivi karibuni katika kijiji cha Guta, walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo (jina linahifadhiwa) akiishi na mwanafunzi wa shule hiyo nyumbani kwake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti huku wakioneshwa kusikitishwa kwa vitendo hivyo, walisema kuwa baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari, ambao hawazingatii maadili ya kazi yao, wamekuwa na tabia hiyo chafu na mbaya ya kufanya vitendo vya ngono na wanafunzi wao.

Walisema hivi karibuni saa za usiku walimkamata mwalimu huyo anayefundisha katika shule ya msingi Guta, akiwa na mwanafunzi mmoja wakiishi naye nyumbani kwake kama mke wake.

Walisema kuwa walifanikiwa kumtia mbaroni mwalimu huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema, kwamba mwalimu huyo anaishi na mwanafunzi huyo nyumbani kwake na wanafanya naye vitendo vya ngono. Walisema kuwa baada ya kumkamata polisi walifika na kumpeleka kituo kikuu cha polisi cha wilaya hiyo.

“Baada ya wananchi hao walioongoza na mwenyekiti wa kijiji chao walifanikiwa kumkamata live mwalimu huyo akiwa na mwanafunzi ndani ya nyumba yake” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulsha kwa jina moja la Juma, mwenyekiti wa CCM, tawi la Guta.

Diwani wa kata hiyo, Kigo Nyamhanga, alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwalimu huyo alikamatwa na wananchi walioongoza na mwenyekiti wa kijiji hicho.

Kufuatia tukio hilo, diwani huyo alikemea tabia hiyo na kuwataka walimu katika kata hiyo, kuachana na tabia hiyo chafu, kwani wao wanapewa watoto kuwalea na kuwafundisha na siyo kuwafanyia ukatili huo wa kijinsia.

Aliongeza kamwe tabia hiyo katika kata yake, haiwezi kuvumiliwa ndani ya jamii na hata serikali kwa ujumla.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images