Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

HUU NDIO UTATU WENYE TOFAUTI ULIO KATIKA CHADEMA..SLAA, ZITTO NA MBOWE

0
0
NAKUMBUKA vema kana kwamba ilitokea jana tu. Takribani miaka kumi iliyopita, kijana mmoja mwembamba alisimama katika mojawapo ya kumbi zilizopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Alikuwa akiomba nafasi ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA.

Baadaye aliniambia kwamba hadi wakati ule hakuwahi kuvaa suti maishani mwake. Suti kwake ilikuwa ishara ya ubepari. Watu aliokuwa akiwapenda wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); Profesa Chachage Seith Chachage, Profesa Issa Shivji na Dk. Azaveli Feza Lwaitama hawakuwa wapenzi wa suti.

Lakini kwenye siku hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alijitolea kununua suti mpya ili walau kijana wake huyo kipenzi wakati huo aonekane vema mbele ya wajumbe.

Kijana huyo akaja baadaye kupata ujumbe wa Baraza Kuu. Baadaye, akifanya kazi kwa karibu sana na Mbowe, alipanda ngazi hadi kufikia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho. CHADEMA haikuwahi kuwa na kijana mdogo namna ile kwenye nafasi kubwa namna hiyo.

Kijana huyo ndiye huyu Zitto Kabwe ambaye leo hii yuko kwenye mgogoro mzito na chama hicho ambacho alijiunga nacho tangu akiwa na umri mchanga wa miaka 16.

Unaweza kudhani kwamba pengine ujumbe huo na unaibu ndiyo pengine matukio yaliyombadilisha Zitto na kumfanya afikie alipo leo. Hapana, mwanasiasa huyu alianza kupata heshima kutokana na tukio moja la kihistoria.

E pluribus unum ya Zitto

Neno hili la kilatini linatumika kwa maana nyingi. Katika ngao ya Serikali ya Marekani maandishi haya humaanisha “Mmoja Kutoka Katika Wengi” kwamba taifa hilo limeundwa na muunganiko wa majimbo mengi.

Hata hivyo, maana ninayoipenda zaidi ni ile nyingine, inayozungumzia tukio au wakati mmoja katika maisha ya mtu ambayo hubadilisha maisha yake.

Kwa mfano, E pluribus unum ya Rais Jakaya Kikwete ilikuwa ni wakati ule alipoamua kwenda kufanya kazi katika chama badala ya kutafuta ajira serikali ilhali tayari akiwa msomi wa shahada ya kwanza katika kipindi ambacho wasomi walikuwa haba.

Leo hii, Kikwete amepanda na kufanikiwa kuwa rais kwa sababu ya maamuzi aliyoyafanya wakati huo.

Kwa Zitto, E pluribus unum yake ni hoja ya Buzwagi. Julai mwaka 2007, Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini alihoji sababu za aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kwenda kusaini mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi katika kipindi ambacho taifa lilikuwa likifanya mapitio ya sheria zake.

Hoja hii ilizua mjadala mkali ambao ulidakwa na taifa zima. Tangu hapo, Zitto akawa ameingia katika nyoyo za Watanzania na kuanzia hapo, hoja zake nyingi zikawa zinafuatiliwa kwa makini na wahusika.

Kuanzia hapo ameibuka na masuala mbalimbali ambayo yameibua mijadala mingi ya kitaifa. Alikwenda kinyume na msimamo wa chama chake baada ya kukubali kuingia kwenye Tume ya Madini iliyoteuliwa na Kikwete na ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini hapa nchini.

Yeye ndiye mtoa hoja ya kusaka mali na fedha zilizofichwa nje ya nchi, mtoa hoja ya kutokuwa na imani na serikali iliyosababisha kufanyika kwa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na sasa anashiriki sana katika kutafuta haki kwa nchi masikini kwenye masuala ya ukwepaji kodi wa makampuni makubwa.

Mgogoro wake mkubwa kabisa na chama chake ulikuja mwaka 2009 wakati alipotangaza nia ya kutaka kuwania uenyekiti wa chama hicho dhidi ya Mbowe. Nia yake hiyo ndiyo msingi wa matatizo yake yote yanayomkuta sasa ndani ya chama chake.

Wakosoaji wake wanasema kosa la kwanza la Zitto kisiasa lilikuwa ni kuwania uenyekiti na Mbowe ambaye ni mtu aliyemlea ndani ya chama. Uamuzi huo wa Zitto umemletea madhara kwa sababu umempotezea marafiki ambao walifukuzwa kwa kumuunga mkono lakini pia kupoteza sapoti ya Mbowe. Hii ni kasoro ya kutokuwa na subira.

Katika miaka ya nyuma, Zitto angeweza kufanya chochote na asihofu kwa vile alijua Mbowe angemtetea. Lakini, kwa uamuzi wake huo, akawa amekata kamba iliyokuwa ikimuunganisha na bosi wake huyo chamani.

Kama angeweza kusubiri kidogo pengine hadi wakati huu, huenda Zitto angeweza kupata uenyekiti pasipo kutumia nguvu nyingi na kuwa si Mwenyekiti wa chama hicho pekee, bali pia mwanasiasa wa upinzani mwenye nguvu kuliko mwingine yeyote kimamlaka hapa nchini.

Pia, tofauti na wanasiasa wengi wa upinzani hapa nchini, Zitto ana mahusiano ya karibu na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM, serikali na vyombo vya dola na hivyo amekuwa mwathirika wa mara kwa mara wa tuhuma za kutumiwa na taasisi hizo.

Hata hivyo, kwa jicho lingine, hii pia inaweza kuelezwa kama mojawapo ya nguvu za mwanasiasa huyu.

Dk. Slaa na orodha ya mafisadi

Huyu ni miongoni mwa wabunge walioingia bungeni katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 akipitia jimbo la kwao Karatu. Hakuwa maarufu sana kwenye miaka ya 1990 na watetezi wake wanasema utawala wa kiimla wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Pius Msekwa, ulichangia zaidi hali hiyo.

Kwa upande wake, E pluribus unum yake ilitokea siku moja ya Septemba 15, mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembeyanga vilivyopo wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam pale alipotangaza iliyokuja kufahamika sana kama “Orodha ya Mafisadi.”

Habari hiyo ilipata sapoti kubwa kutoka kwenye vyombo vya habari kwani, kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Tanzania, vyama vya upinzani vilitaja hadharani majina ya watu wanaotajwa kuwa vinara wa rushwa hapa nchini.

Mafisadi hao walikuwa muhimu kipindi hicho kwani tayari CHADEMA ilikuwa imeanza kujenga hoja kama chama kuhusu upotevu wa mabilioni ya shilingi katika iliyokuwa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Katika Bunge lililopita chini ya Spika Samuel Sitta, Slaa alijipambanua kama mmoja wa wapinga ufisadi na nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, ulimpa fursa ya kuibua ufisadi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akiwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk. Slaa alikuwa kivutio kwa wengi kutokana na tabia yake ya kupenda kuzungumza kwa kutumia takwimu na kuongoza chama ambacho kilikuwa kinaonyesha ujana, staili na mawazo ya mbali kisiasa.

Wapo wanaoamini kwamba CHADEMA kilipata wabunge wengi kuliko katika wakati mwingine wowote tangu kianzishwe kutokana na mvuto au ufuasi aliokuwa nao mgombea huyo kwa wananchi.

Kuna kipindi, kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2011, Dk. Slaa alikuwa ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi ndani ya chama hicho kuliko mwingine yeyote.

Hata hivyo, kwa sababu mbalimbali, umaarufu wa Dk. Slaa umeshuka katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu hadi miwili iliyopita. Kutokuwepo kwake ndani ya Bunge kumeondoa eneo lake moja muhimu la kujieleza.

Wakosoaji wa Slaa wanaeleza kwamba amekuwa na tatizo la kutotaka kushaurika na pia mara nyingi si mtu wa kuonekana kwenye matukio makubwa ambayo huwa yanawasaidia wanasiasa kuonekana.

Mfano unaotolewa mara kwa mara ni kukosekana kwake hivi karibuni katika tukio la kuaga mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi lililofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam –tukio lililohudhuriwa na watu wengine maarufu kutokana na umaarufu wa marehemu.

Kwamba kama hana hoja ya kuzungumza, ni rahisi sana kwa Slaa kupotea kwenye jamii kwa vile si mtu anayependa kujichanganya. Tabia hii, wanasema, watu wanaomfahamu kwa karibu, pengine inatokana zaidi na malezi yake kilei aliyoyapata wakati akiwa padre wa Kanisa Katoliki.

Wanasiasa mahiri hutafuta njia za kuonekana mara kwa mara ili wasipotee. Rais Kikwete anaweza asiwe na habari kubwa ya kufanya lakini anaweza kuonekana akiwa msibani, mpirani, mkutanoni na au safarini. Ni sanaa ambayo Dk. Slaa ameshindwa kuimanya.

Freeman Mbowe

CHADEMA hii inayoonekana leo ina mkono wa Mbowe katika eneo zaidi ya moja. Katika wakati wake, CHADEMA imepata mafanikio makubwa ambayo wengine hawayakuwazia wakati alipopewa madaraka.

Mbowe alipokea uenyekiti wa CHADEMA wakati chama kikiwa na wabunge wasiozidi watano na kikiwa na kila dalili ya uchovu. Aliyemwachia madaraka alikuwa ni Bob Nyanga Makani aliyewahi kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ambaye naye alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Gavana wa BoT.

Ingawa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, tayari alikuwa ameonyesha kuvutiwa na sera za CHADEMA, lakini kilionekana ni chama cha wastaafu, wasiotaka ugomvi na serikali na wasio na shida. Matajiri. Yote yakabadilishwa na Mbowe.

Kubwa kuliko yote ambalo Mbowe amelifanya kwa CHADEMA ni namna alivyoweza kuwaamini vijana na kuwapa majukumu mazito.

Huwezi kutaja vijana kama Zitto, John Mnyika, John Mrema, Halima Mdee, David Kafulila na Muhonga Said Ruhwanya pasipo kutaja mchango.

Hata kama vijana hawa wana akili za kutosha vichwani mwao, walihitaji fursa kuweza kuonyesha umahiri na ni Mbowe pekee, miongoni mwa viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini, ndiye aliyeweza kucheza kamari na vijana na amevuna matunda ya uamuzi wake huo.

Kwa sasa, CHADEMA, pengine, ndiyo chama kinachoweza kujivunia kama tumaini la vijana wengi hapa nchini ambao wanaamini watapata fursa endapo tu watajiunga au kujihusisha na chama hicho.

Freeman pia ni miongoni mwa wanasiasa ambao wamejaaliwa uwezo mzuri wa kuzungumza kwenya majukwaa ya kisiasa.

Ni wanasiasa wachache hapa nchini wenye uwezo wa kushindana naye pindi anapopanda kuzungumza na wananchi.

Ni Mbowe huyuhuyu ambaye utaratibu wake wa kutumia helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi umebadili kabisa namna ya ufanyaji wa kampeni. Sasa karibu vyama vyote vimeona umuhimu wa kutumia chombo hicho katika kampeni zake.

Pia, CHADEMA ni chama pekee nchini ambacho kina ubunifu wake wa mavazi na hili pia linahusishwa naye kwa vile limetokea chini ya utawala wake.

Hata hivyo, wakosoaji wa Mbowe wanataja kasoro zake kubwa mbili. Mosi ni ile ya kutokuwa na uwezo wa kuibua hoja binafsi zitakazomtambulisha yeye binafsi. Wakati Slaa anaweza kujigamba kwa mambo ya EPA na Orodha ya Mafisadi, huku Zitto akijitapa kwa Buzwagi na mabilioni ya Uswisi, Mwenyekiti huyu hadi sasa hana hoja ya binafsi anayoweza kuisimamia kwamba ni yake.

Matokeo yake ni kwamba amekuwa mwanasiasa wa matukio. Jina la Mbowe limekuwa likitajwa sana kwenye matukio ya fujo, purukushani za kisiasa na mikutano ya kisiasa bila ya kuwa na hoja anayoisimamia.

Kasoro ya pili imetajwa kuwa ni tabia yake ya kuhofia upinzani kutoka ndani ya chama chake au jimboni. Wakosoaji wake wanasema hata tofauti zake na Zitto zimesababishwa zaidi na kilichotokea mwaka 2009 kuliko kitu kingine chochote.

Watetezi wake wanasema tabia hii huenda inatokana na ukweli anatoka katika familia ya kitajiri na hivyo ubongo wake umetengenezewa dhana ya kumiliki na ndiyo maana si rahisi kwake kuvumilia upinzani.

Huo ndiyo utatu wenye utata ulio kwenye CHADEMA.

-RAI

VENESSA MDEE KUPAMBANA NA NAZIZI ARUSHA TAMASHA LA KUPAMBANA NA RUSHWA TAR 7 DEC

0
0
Mkali kutoka Kenya, Naziz anatarajia kuumana vilivyo na Mbongo Venessa Mdee ndani ya jukwaa la kupambana na Rushwa....Wakali hao wanatarajia kuchuana kwa kushusha Mistari katika tamasha la MIMI NI AFRICA NA AFRICA NI MIMI litakalo fanyika Tarehe 7 Mwezi huu wa December katika Viwanja vya General Tyre Pande za Arusha.

Tamasha hilo litaanza Mida ya saa saba , Baadhi ya Wasanii watao pamba onyesho hilo ni Kundi la Weusi , Roma, Chindo, Linah , Fid Q na Stamina...
Kama upo Arusha basi Usikose kwenda ......

ZITTO MATATANI BAADA YA KUSHINDWA KESI YAKE YA KUTOA KASHFA DHIDI YA MFANYABIASHARA RAIA WA AFRIKA KUSINI

0
0
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara nyingine ameingia matatani baada ya kushindwa kesi iliyofunguliwa na mfanyabiashara raia wa Afrika Kusini.

Katika kesi hiyo, Zitto alituhumiwa kutoa madai kupitia tovuti yake www.zittokabwe.wordpress.com kuwa mlalamikaji, Moto Mabanga alitoa rushwa ya mabilioni ya fedha kwa maofisa wa Serikali ya Tanzania ili kufanikisha kampuni ya Ophir Energy kupata vitalu vitatu vya gesi mkoani Mtwara kati ya mwaka 2004/2005.

Katika kesi hiyo ya madai Namba 153 ya 2013 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara huyo pamoja na mambo mengine alidai kulipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 5 ambazo ni sawa na Sh bilioni 8 za Tanzania.

Katika hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Sundi Fimbo, Novemba 21 mwaka huu bila Zitto kuwapo, Mahakama ilijiridhisha kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye tovuti binafsi ya Zitto na kwenye mitandao ya jamii yalimkashifu mlalamikaji na mlalamikiwa ameshindwa kuyathibitisha.

Mahakama hiyo imemtaka Zitto kuomba radhi kwenye tovuti yake na mitandao ya jamii ambako aliandika kashfa dhidi ya mfanyabiashara huyo.

Pia imemuamuru mlalamikiwa pamoja na washirika wake kuacha kwa njia yoyote ile kuendelea kuandika na kusambaza habari zenye kumkashifu mlalamikaji.

Mwanasiasa huyo kijana ambaye katika siku za karibu amekumbwa na misukosuko ya kisiasa, pia ameamriwa kumlipa mlalamikaji jumla ya Sh milioni 3 kutokana na madhara yaliyotokana na kashfa husika.

Awali, mlalamikaji alitaka kulipwa Dola za Marekani milioni 5, lakini akashindwa kuithibitishia Mahakama ni jinsi gani alipata hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kashfa hiyo. Pia Zitto ametakiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Alipoulizwa jana kama anakubaliana na hukumu hiyo au anakusudia kukata rufaa, Zitto alijibu kwa ufupi; “Sijaona hukumu wala sijawahi kufika mahakamani.”

Julai mwaka jana, Mabanga alifikisha malalamiko mahakamani akidai Zitto ameandika taarifa zenye kumkashifu kwa kumhusisha na utoaji mkubwa wa rushwa.

Mbali na kujihusisha na biashara sehemu mbalimbali duniani, Mabanga amekuwa akitumika kama kiunganishi kati ya wawekezaji wakubwa na Serikali mbalimbali ikiwamo Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika madai yake, aliitaka Mahakama kumuamuru Zitto kutoka uthibitisho dhidi ya madai ya kuwapa rushwa maofisa wa Serikali katika mchakato wa kupata vitalu vya gesi wa kampuni ya Ophir Energy.

Pia aliiomba Mahakama kutamka kuwa maneno yaliyoandikwa na Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha kwenye tovuti yake na mitandao ya jamii si ya kweli bali ni kashfa.

Wakati hali ikiwa hivyo, wiki mbili zilizopita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilimvua nyadhifa zote Zitto Kabwe ikiwamo ile ya Naibu Katibu Mkuu.
  

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya Chadema uliofanyika Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu, alisema Zitto na wenzake wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha mpango unaoitwa Mkakati 2013 ukilenga kukisambaratisha chama hicho, ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake.

Wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, ambapo walipewa siku 14 wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwamo kuvuliwa uanachama.

-Mtanzania

"WALIOHUSIKA KUCHOMA MOTO OFISI ZA CHADEMA NI CHADEMA WENYEWE..." TAMKO LA POLISI BAADA YA UCHUNGUZI KUKAMILIKA

0
0
Polisi mkoani Arusha imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na kuungua kwa Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kusema wanachama wa chama hicho ndio waliohusika. 

Hata hivyo, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amepinga kauli hiyo na kulipa jeshi hilo siku nne kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa watano baada ya kulipatia majina hayo akidai kuwa ndio wanaohusika na uchomaji moto ofisi za chama hicho.

“Tumewapatia polisi majina... tunaamini walihusika moja kwa moja la sivyo, chama kitatumia vijana wetu wa Red Brigade kuwakamata na kuwafikisha polisi,” Lema aliwaambia waandishi wa habari jana.

Ofisi za Chadema zilizoko katika eneo la Ngarenaro, zilinusurika kuteketea kwa moto juzi baada ya watu wasiojulikana kuwasha moto katika moja ya vyumba vyake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Japhet Lusinga alisema:

“Katika uchunguzi wetu, tumebaini kuwa hakuna mahali palipovunjwa kutoka nje ya uzio na kuruhusu watu kuingia ndani... tumegundua kuna tundu dogo darini eneo la kuelekea bafuni la upana wa futi moja na nusu kiasi haliwezi kuruhusu mtu kupita.

“Tumejiridhisha kuwa hakuna mtu anayeweza kupita hapo na ndani tulikuta majivu na baadhi ya vitu vilivyoungua na vifaa vingine.”

Lema akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema: “Tumebaini polisi wanataka kulifanya jambo hili kama la siasa ndiyo sababu juzi badala ya kuanza kuchunguza waliohusika, waliwakamata Mtunza Ofisi na mlinzi wetu na kuwalaza rumande hadi leo (jana) asubuhi kwa madai eti wanawahoji.

“Hatukubaliani na taarifa yao, hii ni siasa. Kulitokea mauaji ya bomu, wakasema Chadema wamejilipua, leo ofisi imechomwa wanasema Chadema wenyewe, hili hatukubali, “ alisema.

Msajili alaani
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amelaani tukio la kuchomwa moto ofisi hizo za Chadema na kusisitiza kuwa wananchi hususan wanasiasa wasiwe wepesi kuingiza hisia kwenye makosa ya kijinai.

Alisema kuwa tukio hilo linapaswa kukemewa kwa hali yoyote ile kwa kuwa linavuruga na kuhatarisha amani ya nchi.

"MGOGORO ULIOPO NDANI YA CHADEMA NI KAZI YA MAKACHERO..." DR SLAA AFUNGUKA

0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa amesema mgogoro uliopo ndani ya chama ni kazi ya makachero. Alitoa kauli hiyo jana jioni alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar es Salaam akiwa njia kuelekea mkoani Kigoma kwa ziara ya wiki moja.
  

Dk. Slaa ambaye alifika saa 12 jioni alitumia muda dakika zisizozidi 20 kuhutubia ambapo alisema chama hicho kina taarifa za ushiriki wa makachero, lengo likiwa kukidhoofisha na hatimaye kukisambaratisha chama hicho.

“Tunazo tayari taarifa kuwa makachero ndio wapo nyuma ya mgogoro ndani ya chama, wameingia kwa nia ya kutuvuruga, lakini tupo imara.

“Nawasihi Watanzania waache kushabikia vitu visivyo vya msingi, badala watumie muda wao kufikiri na kufanya mambo ya msingi kwa Taifa.

“Yote yanayotokea katika chama chetu kwa sasa yanatuandaa na kutukomaza kwa ajiri ya kuchukua madaraka ya nchi mwaka 2015,” alisema.

Alisema kuwa, wanachama wote wa Chadema wanapaswa kujua hakuna aliye juu ya Katiba ya chama hicho, kwa hiyo Katiba italindwa na kusimamiwa bila woga kwa maslahi mapana ya chama.

Leo anatarajiwa kuondoka na msafara wake kuelekea mkoani Kigoma, ambako kituo chake cha kwanza kitakuwa eneo la Kakonko na baadae ataelekea Muhambwe.

Katika ziara hiyo ya kukagua uhai wa chama atatembelea mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.
-Mtanzania

TIGO YANYAKUWA TUZO YA MTANDAO BORA WA SIMU AFRICA

0
0
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tigo Tanzania Bw. Deon Geyser akionyeshea  waandishi wa habari tuzo ya mtandao bora wa mwaka 2013 walioshinda kutoka kwa umoja wa makampuni ya simu GSMA katika kongamano la mawasiliano na mitandao ya simu Africa Com, iliyofanyika Capetown Afrika Kusini mwezi Novemba. Kushoto ni Mkuu wa Mipango na Uboreshaji wa mitandao kutoka Tigo Bi. Halima Idd..
Kampuni ya Tigo Tanzania imeshinda tuzo ya kuwa mtandao wa simu ulioboreshwa zaidi katika mwaka 2013 barani Afrika. Tuzo hiyo iliyotolewa katika kongamano la umoja wa makampuni za mawasiliano duniani, GSMA, liliyofanyika mwezi Novemba mjini Capetown, Afrika Kusini.

SAKATA LA RAY NA WAREMBO LAFIKA PABAYA-MAINDA AMCHANA JOHARI LIVE BILA CHENGA-HATARII

0
0
Hapo majuzi kupitia mtandao mmoja wa kijamii mwanadada Mainda aliamua kuvunja ukimya baada ya kuamua kuwachana live ‘wabaya’ waka Chuchu hans, na Johari kuhusu sakata linaloendelea la wao kumgombania mwigizaji Vicent kigosi ambaye anadaiwa alikuwa mpenzi wa mrembo huyo. Bila kupoteza muda soma hapo chini alivyofunguka mwanadada huyu…

"...Hizi salamu zako Johari, ni hivi naomba usinitaje kwenye huo upumbavu wenu, Huyo mwanaume mnae mzungumzia mimi kwangu namuona mtu wa kawaida tu ndio maana nikatupa kule. Nadhani umenipata alafu sitaki kumpandisha mtu jina sawa?. Ni hivi mimi si mpinzani wako, nadhani mpinzani wako unamjua mliopiganana (Sakata la Johari na Chuchu hans kupigana)  mkataka kutoana roho kisa shingo ya kuku mlivyokuwa wajinga na malimbukeni wa mapenzi wanaume hapawiganiwi. Nimewakalia kimya naona wewe mwenye kilanga umejitoa kimasomaso ukaenda kiu ukasema Mainda amebip wewe unataka kumpigia, ni hivi usiniweke kwenye upumbavu wenu, mimi huyo mwanaume wenu kwangu ni kuku kama kumtafuna nimemtafuna mpaka mifupa alafu nikatupa kwenye shimo la taka, sasa nyiyni mbwa koko mlio kosa wafugaji ndio mnaruka ovyo hamjui mle nini, pumbavu kabisa wewe na mke mwenzio sindio amkauki kunisema me mgonjwa, sasa kama me mgonjwa huyo bwana wenu ni hivi wewe mwenye shape kama ubao usiejielewa nakushauri achaha na mimi nenda sinza…..(Itaendelea)

TRENI YA MWAKYEMBE YAOKOA SHILINGI BILION 3

0
0
Wakati taarifa mbalimbali zikieleza kuwa treni ya usafiri jijini Dar es Salaam, maarufu kama ‘Treni ya Mwakyembe’ inaingia hasara ya milioni 2.1 kwa siku kutokana na gharama za uendeshaji, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa hizo na kusema, treni hiyo imepunguza hasara ya zaidi ya Sh3 bilioni.

Mwakyembe alisema uwepo wa usafiri huo umesaidia kupunguza msongamano mkubwa jijini, ambao unasababisha hasara ya Sh3 bilioni ambazo ni matokeo ya kukaa barabarani kwa muda mrefu, kuchelewa kazini na katika majukumu mengine pamoja na upotevu wa nishati.

Akizungumza katika Kongamano la miundombinu na uchukuzi katika Nchi za Mabonde ya Ufa uliofanyika jana jijini, Mwakyembe alisema hatasita kuendelea kuwekeza fedha zaidi katika reli, kwani ana uhakika ina faida kubwa na imesaidia katika uchumi na kijamii.

“Ukitaka kujua reli ni ya muhimu, tangaza leo kuwa unasitisha usafiri huo, utaona jinsi ambavyo watu watahangika na shida ya usafiri,” alisema.

Mwakyembe alisema, ukilinganisha hasara inayopatikana katika gharama za uendeshaji zinazotajwa na kiwango cha hasara kinachopunguzwa katika mtazamo wa uchumi na shughuli za maendeleo jijini, ni bora reli hiyo iwepo daima.

Waziri Mwakyembe alisema ana mipango mikubwa ya kuuboresha usafiri huo ingawa ni mapema mno kuiweka wazi kwa sasa.

Alisema mabasi zaidi ya 500 yameondoka barabarani, hivyo kupunguza msongamano.

Alisema treni hiyo itaimarishwa ambapo mabehewa mapya ya kisasa yanatarajiwa kuletwa.

Hata hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti, Wizara ya Uchukuzi inatazamia kupata mwekezaji, ambaye anaweza kuwekeza katika treni hiyo na kusaidia kupatikana kwa treni ya kisasa zaidi inayofaa kwa matumizi ya mjini.

Kwa sasa mabahewa yaliyopo ni ya kizamani, ingawa yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha za usafiri.

Julai mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania, Kipalo Kisamfu alisema treni hiyo inaingiza hasara ya 1.2 milioni kwa siku kutokana na gharama kubwa za uendeshaji, ikiwemo vitendea kazi ambavyo siyo maalum kwa treni za mijini.

DR SLAA ALAKIWA KIGOMA KWA SHANGWE NA MASHAM SHAM

0
0
Msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa umeingia Kigoma tayari, ukianzia Wilaya ya Kakonko. 

Hivi sasa ni mkutano wa kwanza Kijiji cha Muhange, Kata ya Muhange. Amepata mapokezi mazuri sana huku akina mama, watoto, vijana na wazee wako mkutanoni. 

Mkutano wa pili utakuwa jioni Kakonko mjini. 

Source:Afisa Mwandamizi Habari CHADEMA Tumaini Makene

NIMETUKANWA NA MKE WA JIRANI YANGU

0
0
Kuna familia moja imejengea karibu kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi nikamshauri kwamba Wkend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.

From there onward inapotokea mmoja wetu amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya Weekends au public holidays. 

Majuzi nilikuwa na Business moja ya kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni Bar moja ya karibu mtaani kwetu.

Mida ya saa moja na nusu usiku tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi 'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.

Baadaye jamaa akazima simu yake, tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani, akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.

Nimeumia sana kwasababu hata siku moja huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama 
-Jamii Forums

WASANII WAMTAKA RAY AACHIE UONGOZI KWENYE UCHAGUZI UTAKAOFANYIKA LEO KUTOKANA NA SKENDO ZAKE CHAFU

0
0
Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kulipasua Kundi la Bongo Movie kutokana na uchaguzi wa kundi hilo unaotarajiwa kufanyika leo katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya wasanii wa filamu wanaounda kundi hilo wanadai Ray hafai kuliongoza kutokana na skendo ya kuwagonganisha mademu inayomtafuna huku wengine wakimuunga mkono.
“Kuna baadhi yetu wamekuwa wakikaa vikao ili kutaka kumweka pembeni Ray kwa kuwa ameshindwa kuleta umoja ndani ya Bongo Movie na amekuwa akifanya mambo yasiyokubalika…” alisema mmoja wa wasanii ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Chanzo hicho kimesema kwamba wasanii wasiomtaka Ray wamekuwa wakiweka vikao usiku katika kumbi mbalimbali za burudani za jijini Dar kwa ajili ya kumng’oa kwenye cheo hicho.
Wasanii wanaomkubali  Ray wanadai anastahili  kuendelea kuliongoza kundi hilo kwa kuwa ana msimamo thabiti na hakuna mwingine anayeweza kuliongoza.
Msanii wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere, amesema uongozi wa Ray unafika kikomo na wanatakiwa kumchagua kiongozi mpya au  kuendelea naye na jukumu hilo liko mikononi mwa wasanii wenyewe.
“Kimtazamo Bongo Movie linaenda vibaya na hii siyo kwa sababu ya Ray, bali wasanii wote  ni jukumu letu kulijengea heshima kundi hilo, katika uchaguzi wa leo Ray anaweza kuchaguliwa au asichaguliwe kwani kura ni demokrasia…” alisema Steve Nyerere.
Ray hakuweza kupatikana mara moja kuuzungumzia mpasuko huo ndani ya Kundi la Bongo Muvi. 

 GPL

RAIS WA ZAMANI WA AFRIKA KUSINI NELSON MANDELA AMEFARIKI DUNIA

0
0
Rais wa zamani wa Afrika Kuisni Nelson Mandela, amefariki dunia huko Johannesburg, Afrika Kusini usiku wa jana Alhamisi (December 5) akiwa na umri wa miaka 95.

Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.

Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.

Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.

Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.

Pumzika kwa amani Nelson Mandela

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MZEE MANDELA ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO KITAIFA, BENDERA KUPEPEA NUSU MLINGOTI

0
0
Taarifa: Rais Kikwete aagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu za maombolezo ya Kitaifa ya Rais Mstaafu Nelson Mandela wa Afrika Kusini aliyefariki jana.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini  na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea  tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa  machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na
mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea  Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa  taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela  ni mfano bora kwa wanadamu wa  jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela  mahali pema peponi".

Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013. 

Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza  kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee  nusu mlingoti.

Mwisho.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

06 Desemba,2013

TWEET ZA WANAMUZIKI WA NJE BAADA YA KIFO CHA NELSON MANDELA

0
0

  Wasanii Wakubwa wa Nje wakitoa ya Moyoni kuhusu kifo cha Mandela

WEMA SEPETU AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI MITATU AMA KULIPA FINE

0
0
Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Sepetu imetolewa hukumu yake baada ya Wema kuomba iharakishwe kwakuwa alikuwa anasafari.

Kwa mujibu wa mtandao wa Global Publishers, Wema sepetu amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani ama faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.

Baada ya kusomewa hukumu hiyo wema alitoa laki moja hiyo iliyokuwa ikihitajiwa na mahakama kabla ya kuachiwa huru kuendelea na mishe zake nyingine

BIFU LAZIDI KUPAMBA MOTO: BABY MADAHA AMCHANA TENA DIAMOND BAADA YA DIAMOND KUMDISS

0
0

Baada ya mwanamuziki wa kizazi kipya kufunguka na  kuamua kumdiss mwanadada baby Madaha a.k.a The Bad Gul kuwa hawalingani hivyo hana muda muda wa kuwa na beef na mrembo huyu wa filamu na muziki bongo, hatimaye tumeweza kumpata baby Madaha na kufanya naye EXCLUSIVE interview na mwanadada huyu kuhusu hayo mazito aliyoyasema bwana platnumz. Na kwakuwa mwaka huu ni mwaka wa kufunguka bila kuficha chochote binti huyu aliamua kuanika yake ya moyoni kama yanavyosomeka hapo chini….
Baby alianza kwa kusema

“….Kwanza nitafute keeck kwa diamond kwa lipi,wakati anakuja kuniomba kuperfome 2010  akiwa ana single moja ya mbagala pale maisha plus mimi nikiwa judge na kina masoud,tayari nishafanya album ya amore india na nishapiga show kibao,wakati yeye akifikiria amkamate demu gani ili a hit kimuziki mimi tayari nishafanya  movie tatu na moja imeshinda ziff tz na ziff berlin,akiendelea kuwapanda kama farasi hao wajinga wajinga wenzie mie tayari nina tuzo tatu ziff ambazo hata marehemu kanumba angefurahi kupata japo moja(rip)….”

“…..Wakati sasa anaongea blah blah akiwa na single yake moja mpya akihangaika kwenda nigeria kuonyesha skin tight yake ya mistari na kuomba omba collarbo, mi tayari nina single tatu hit na najiandaa kushusha movie kali mpya,tatizo ni kutotaka kukosolewa na kujiona mungu mtu kwenye muziki lakini ukweli anaujua na hata yeye anauogopa kama anabisha afanye nao collarbo anahangaika nini na wote wanaimba bongo flava??upuuzi na ujanja ujanja tu wa mjini unafanyika huku wale punda wake wakikubali kumbeba kwa malipo gani umaarufu???mi sijautafuta kwa nguvu hiyo, nimepikwa bss na watu wakaniona na wakanitambua.kama ni suala la pesa hata asiongee launching yangu ya (kempinsky)hyatt regency 2010 hakuna msanii yeyote wa bongo flava including na yeye ameweza kufanya jeuri hiyo,aliyejaribun labda yule demu wake wa zamani aliyemshit pia kwa vihela vyake mbuzi…”

“….Akiwa bado anastruggle kupata mkwanja awatishe tishe watoto wenzake wa tandale..mimi nishazindua brandy yangu ya manukato na gift bagz zangu ambazo zinaingia sokoni rasmi 31 december…bado anachanja na prado old model,asogee kwenye audi tt yangu apunge upepo yani ye anatafutaa..mi nishapata so wa nini???wanaompapatikia ni wale drama queens wenzie, mi ama bad gul sijali kama kumchana namchana tu so wat??,scandal kitu gani?ye sukari guru ata survive si tandale bwana eeh, vipi wale kwenye list za kubadilishwa kama nguo za ndani je watapata wa kuwaoa???/… wakija forbes hapa watu wataumbuka ooh na hekalu langu kuubwa unakaaje kwenye nyumba ya kupanga?haliishi??hahahaha na kuhusu ati mimi nimesema ana paja la mtoto wapi na wapi he is not ma type at all si hook na little mama’s boy na hook up na big boys tu…”

“…. Mi sio wale farasi zake wanaopokezana kupandwa na yeye after role kuambiwa ukweli sio bif kweli mzinzi na hajui kuimba kama sio kweli atulie tu asipande pande hapo tutamwona mfalme kweli kama mzee yussuf,mimi naimba aina yangu ya muziki tanzania nzima nipo peke yangu hakuna demu anapiga riddim,ragga sasa natafutaje keeck kwa bongo flava????anaeimba nyimbo zake za kipuuzi kutaja taja farasi wake ana (tusi kali sana) angekuwa ameni***** sawa but mpaka anakufa i think atakuwa ananiota mimi na lulu……….kama mbwai mbwai  mjini hapa kila nyumba ina namba..adios…”
Hatuna la kuongezea hapo, kazi yetu ni kuwajulisha kinachotokea tu mjini hapa.
Source:Bongomovies

STORY YA KUPIGANA KATI YA MSANII H-BABA NA CHEKI BUDI HII HAPA

0
0
Headlines kwenye U heard ya Clouds FM zinahusu stori za kupigana kati ya msanii wa bongofleva H Baba pamoja na mwigizaji Cheki Budi ambae amehojiwa na gossip cop Soudy Brown. sikiliza hapa:

ANTI LULU ATUNDIKWA MIMBA..

0
0
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya 
MSANII wa filamu, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ baada ya kurukaruka sana, sasa inadaiwa ni mjamzito wa takribani miezi mitano.

Akilinyetishia Ijumaa juu ya ishu hiyo, rafiki wa karibu wa Anti Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, msanii huyo sasa amekuwa mtumiaji mzuri wa maembe mabichi huku magauni mapana yakiwa ndiyo mavazi yake.

“Mwanzo alikuwa anaficha lakini sasa siyo siri na mwenyewe ameona ni bora kuwataarifu ndugu na marafiki zake,” alisema mtoa habari huyo.

Katika kujua undani wa hilo, waandishi wetu walimsaka Anti Lulu na kufanikiwa kumuona akiwa na kitumbo chake lakini akaomba asipigwe picha ila akasema: “Mmechelewa kujua, mbona inakwenda mwezi wa tano sasa, mwenye mzigo mtamjua nikishajifungua jamani,”alisema msanii huyo.
GPL

NICK MINAJ ASIKITISHWA NA KIFO CHA MANDELA MPAKA AKAJIKUTA KAONGEA KISWAHILI

0
0
Kifo cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini kimewasikitisha watu wengi sana wakiwemo watu wa maarufu duniani lakini rapper Nicki Minaj mwenye wafuasi milioni tatu na nusu kwenye instagram amevunja rekodi ya kuwa staa pekee wa dunia ambae nimemuona ameandika yake ya moyoni na kuongezea kwa lugha ya Kiswahili pia.

Kupitia akaunti hiyo minaj aliandika 
A complete and fulfilled life of a King. We could never repay you for your dedicated, passionate fight against injustice. We enjoy the very liberties you gave your freedom for. Your legacy will never die. Thank you, and may God bless your soul. ***Madaraka kwa watu*** 

DK SLAA APOKEWA NA MABANGO KIGOMA YANAYOMTAKA YEYE NA MBOWE WAJIUZULU

0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amepokewa kwa mabango katika mkutano wake wa hadhara wilayani Kakonko, Kigoma lakini akawaambia waliofanya hivyo kuwa chama chake hakitayumbishwa huku akiwataka wanaosimama na mabango kumtetea Zitto Kabwe kung’oka naye ndani ya chama. 
Dk Slaa yuko mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 11 kutembelea Mikoa ya Shinyanga na Kigoma kukagua na kuimarisha uhai wa chama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwenge Kakonko, Dk Slaa alisema Chadema ni chama imara na kinaendeshwa kwa misingi ya katiba na kanuni.
“Hakuna kiongozi aliye juu ya katiba, ninawaasa wote wanaobeba mabango kujiangalia kwa kuwa ninafahamu wanatumiwa.”

Kabla ya kupokewa kwa mabango hayo, Dk Slaa aliyewasili Kakonko saa 5:11 asubuhi akitokea Wilaya ya Kahama, Shinyanga alikwenda moja kwa moja katika Kata ya Mhange ambako alifanya mkutano wa hadhara.
Dk Slaa alikumbana na mabango hayo saa 8:45 mchana msafara wake ulipowasili Kakonko Mjini ukitokea Mhange.
Wakati Dk Slaa akiingia katika uwanja wa mkutano, ulio jirani na Ofisi za CCM Wilaya ya Kakonko, kuliibuka kundi la vijana wapatao watano wakiwa na mabango mkononi na kuanza kukimbia kuyafuata magari matatu ya msafara wa Dk Slaa huku wakionyesha mabango yao. Hatua hiyo iliwafanya polisi waliokuwapo eneo hilo la mkutano kuwazuia na kuanza kuwatimua lakini mara baada ya Dk Slaa kuteremka katika gari yake na kuingia uwanjani hapo, aliomba kipaza sauti na kuwataka askari hao kuacha kuwatimua wenye mabango. “Naomba msiwaondoe waacheni waje... waruhusuni kwenye mkutano na mabango yao. Waacheni waje hapa … msiwazuie, waacheni waonyeshe mabango yao na muwaruhusu tu wapite hapa mbele, msiwapige tafadhali,” alisema Dk Slaa.
Baada ya kauli hiyo, polisi waliwaruhusu vijana hao watano ambao walibakiwa na mabango manne, moja likiwa limechanika walipokuwa wanawazuia.
Mabango hayo yaliyokuwa na maandishi ya aina moja, yalikuwa na ujumbe uliosomeka: “Tanzania Kigoma Kakonko bila Zitto Haiwezekani”, ‘Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe mnatakiwa kujiuzuru mara moja” na jingine lilisomeka; “Hatupo tayari kwa kusikiliza lolote bila ya Zitto”.
Mara baada ya kupanda jukwaani Dk Slaa aliwataka tena wenye mabango kusogea karibu na jukwaa kuu alipokuwa amesimama na kuanza kuwauliza maswali vijana hao iwapo wanajua Katiba ya Chadema na kama wana kadi za chama. “Naomba niwaulize, hivi nyie wenye mabango mnaijua Katiba ya Chadema?” Walimjibu: “Hapana.” Dk Slaa akawauliza tena: “Sasa mnadai nini kwa mabango yenu kama hamjui Katiba ya Chadema?”
Mmoja wa walioshika mabango hayo alijibu: “Mtetezi wetu Zitto.”
Kutokana na hali hiyo Dk Slaa aliwauliza, atakuwa amekosea akiwakabidhi kwa Polisi kuwa siyo wanachama wa Chadema lakini wanafanya vurugu katika mkutano halali?

Credit: Mwananchi.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images