Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

MKURUGENZI wa Tanesco Atumbuliwa Sakata la Kupandisha Bei ya Umeme

$
0
0

Breaking News : Habari zimezagaa kuwa amkurugenzi wa Tanesco Bwana Mramba ametumbuliwa ....

‘NILIKWEPA Mawe Manne Kabla ya Kuchomwa Mkuki Mdomoni’-Augustine Mtitu

$
0
0

Moja ya tukio lililomake headline wiki hii ni kuhusu mkulima, Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na ukatokea shingoni kwa kile kilichoelezwa ni mgogoro wa wakulima na wafugaji huko kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Manzese wilaya ya Kilosa Mororgoro.

Ameongea haya:

‘Kuna wafugaji waliingiza ng’ombe kwenye shamba la jirani, kijana mmoja akatoka wakamchapa fimbo, nilipoenda kusaidia wakaanza kunishambulia kwa mawe, nikakwepa mawe manne na nilipotaka kugeuka nikimbie nikashtukia mkuki umenichoma mdomoni’;-Augustino Mtitu

JINSI Mramba wa Tanesco Alivyotumbuliwa..Sababu Zatajwa

$
0
0

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba.

Taarifa ya Ikulu ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa ilisema uamuzi huo ulichukuliwa na jana na papo hapo akamteua msomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Tito Esau kukaimu nafasi hiyo.

Uamuzi huo ambao haukueleza sababu, umechukuliwa muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwaweka kikaangoni vigogo waliotangaza kupandisha bei ya umeme, akisema hatua hiyo ni ushahidi kuwa bado kuna majipu na ataendelea kuyatumbua.

Juzi, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ilikubali maombi ya Tanesco ya kupandia bei ya umeme kuanzia Januari Mosi kwa asilimia 8.5, hatua ambayo ilizuiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo huku Rais Magufuli akisema hatua hiyo ilikuwa inakwamisha mipango ya Serikali inayojiandaa kuelekea katika uchumi wa viwanda.

ZITTO Kabwe 'Mwaka 2016 Ulikuwa wa Utumbuaji Majipu na Kusahau Kuboresha Maisha ya Mtanzania'

$
0
0


Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mwaka 2016 ulikuwa wa utumbuaji na majipu na kusahau kuongoza na kuboresha maisha ya wananchi.

Akizindua kampeni za chama hicho katika Kata ya Kijichi, Dar es Salaam, Zitto alisema Serikali inapaswa kuendelea mapambano dhidi ya ufisadi lakini pia kuimarisha hali za wananchi.

Akimnadi mgombea wa chama hicho, Edgar Mkosamali, mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema,“Sisi kama chama hatuna tatizo na mapambano ya Serikali dhidi ya ufisadi na rushwa, lakini ni vyema mapambano hayo yakaenda sambamba na kuimarisha hali za watu na hilo ndilo tatizo la walio wengi.”

INASIKITISHA Hii Ndio Hali ya Nando (Mshiriki wa BBA) Baada ya Kuathirika na Matumizi ya Madawa ya Kulevya

$
0
0

Hii kitu ya madawa ya kulevya inatuharibia kabisa watoto wetu. 

Huyu kijana nafikiri alishiriki Big Brother mwaka fulani na kuiwakilisha Tanzania. Na kwa sasa hii ndio hali ya afya ya Nando, zaidi ya Chiddy Benzino.

Huyu ndio kijana mwingine anayetoa "alarm" kwa vijana wa kisasa kuwa dawa za kulevya sio "ujanja" ni majanga. Unaweza kuanza na kuvuta kisirisiri, lkn majibu ya madhara yake yakawa hadharani na unapotoka hadharani basi muda unakuwa umekwisha kwenda.

Tuwasaidie vijana wetu waepukane na matumizi ya madawa ya kulevya.

KUTENGULIWA Mramba Sio Dawa' Habibu Mchange

$
0
0

Nafikiri kama taifa tumekwama.
Wanasiasa wetu hasa viongozi wa serikali hawaheshimu wataalam wala utaalam na wataalam wetu pamoja na wasomi wanaanza kuingia hofu na kutaka kuwafurahisha Wanasiasa.

Kwa mtazamo wangu, kumuondoa Mramba Tanesco sio suluhisho la tatizo la uendeshaji wa Tanesco.

Tanesco wanasema Gharama za uendeshaji wa shirika Hilo ni kubwa na linaizidi uwezo management.

Tanesco wanasema na ripoti kadhaa zinaonyesha kuwa Wana madeni makubwa.

Na bahati mbaya madeni hayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.

Ipo haja mahsusi ya serikali kuainisha chanzo kikuu cha kukua Kwa Gharama za uendeshaji Tanesco.

Ipo haja pia ya serikali kuangalia ukubwa huu wa madeni wanayodaiwa Tanesco na vyanzo vyake.

Hii kufurahia Fulani katumbuliwa bado haitoi jibu sahihi la Sababu za Tanesco kutaka kupandisha bei ya umeme.

Kama serikali isipochukua hatua mahsusi na madhubuti lazima bei ipande tu, kama sio Leo kesho na kama sio kesho kesho kutwa, itapanda tu.

Itapanda Kwa Sababu Tanesco wanahisi hiyo inaweza kuwa sehemu ya wao kuwasaidia kupunguza deni na kugharamia uendeshaji wao.

Ushauri wangu ni Serikali kupitia upya mikataba yote inayoipa mzigo wa madeni Tanesco.

Waipitie na watujulishe Watanzania kupitia wawakilishi wetu au moja Kwa moja kila aina ya mkataba na changamoto zake.

Kisha kama taifa tupige mstari na kuweka way foward ya pamoja.

Kinyume na hapo Leo Mramba katenguliwa, na kesho mwengine atatenguliwa na kutenguliwa na kutenguliwa.

Lakini je kutenguliwa huku kunajibu Sababu za wao kupandisha bei? ...

Kuna haja Sasa ya sisi kama Taifa kutibu chanzo cha tatizo sio kuhangaika na matokeo ya tatizo.

Habibu Mchange
Mwananchi.

TANZIA: Bongo Movies Wapata Piga la Kuondokewa na Mmoja wao

$
0
0

Muigizaji  kijakaz pazi shabani (ZAMZAM) Amefariki jana mkoani kigoma

Mwili wake unasafirishwa kuja mkoani Dar city

Msiba upo Sokota karibu na sheli. Temeke

Kwa wale.waliomsaau  alikuwa kundi la kidedea alicheza tamthilia ya  mchezo wa kidedea yeye na marehemu Tabia baba yao alikuwa mzee jengua,

Nawaomba wasanii wote tujumuike kwa pamoja kwenye msiba tukawafariji wafiwa

Taratibu za mazishi tutataarifiana

KILICHOMPONZA Boss wa Tanesco Kutumbuliwa Hichi Hapa

$
0
0

HATUA ya Shirika la Umeme ya kupandisha bei ya umeme bila kushirikisha mamlaka nyingine za Serikali, zimemgharimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Felchesmi Mramba, ambaye jana amefutwa kazi na Rais John Magufuli.

Kabla ya kutengua uteuzi wa Mramba, Rais Magufuli ambaye jana alisali mjini Bukoba katika kanisa la Bikira Maria, Mama mwenye Huruma la mjini Bukoba, alisema Tanesco haikumshirikisha yeye, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Ewura juzi ilitangaza kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 8.5 baada ya Tanesco kuomba gharama zipande kwa asilimia 18.19, lakini hatua hiyo ilisitishwa na Profesa Muhongo. “Waliopandisha umeme hawakuja kuniuliza hata mimi kiongozi wa nchi, hawakuuliza hata waziri mwenye dhamana, ya nishati hawakumuuliza hata Makamu wa Rais, Waziri Mkuu haiwezekani mtu akae pekee yake na afanye maamuzi yake pekee bila kushirikisha mamlaka nyingine,” alisema Rais.

Ateua bosi mpya

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa ilieleza kuwa Rais Magufuli baada ya kutengua uteuzi wa Mramba, amemteua Dk Tito Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco.

Mwinuka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na hadi uteuzi wa jana, alikuwa ni Mkuu wa Idara ya Mekanika na Uhandisi wa Viwanda Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. #HabariLeo

Job Opportunity at Azania Bank, Managing Director

$
0
0

Ref. Na EA.7/96/01/I/84 30thDecember, 2016
VACANCIES ANNOUNCEMENT
On behalf of Azania Bank Limited, Public Service Recruitment Secretariat invites qualified
Tanzanians to fill 1 vacant post as shown below.
1.0 AZANIA BANK LIMITED
Azania Bank Limited is the first indigenous private bank in the United Republic of
Tanzania, formerly known as 1st Adili Bancorp Limited established in 1995 following the
liberalization of the banking sector. The Bank is currently owned over 90% by Pension
Funds.
Azania Bank Limited being a full commercial bank offers a range of banking services,
which includes funds transfers domestically and internationally through TISS, Western
union and Money gram. At Azania Bank Limited Customers can open Current
(Business/ Cheque) accounts and various savings accounts for SMEs, Children and
students. Azania Bank Ltd offers a wide range of loan products, such as business loans,
Consumer loans and Mortgage facilities.
1.1 MANAGING DIRECTOR
1.1.1 REPORTING
Reporting to the Board of Directors, the Managing Director is responsible for providing a
strategic direction to the bank by ensuring effective and efficient operations across the
bank network.
1.1.2 DUTIES AND RESPONSIBILITIES
. Provide strategic advice and guidance to the Chairman and the members of the Board, to keep them aware of development within the Industry and ensure that the appropriate policies are developed to meet the bank’s mission and objectives whiles complying with all relevant statutory and other regulations;
. Provide leadership in the provision of effective and efficient operations across the bank’s network;
. Prepare a corporate plan and annual business plans and monitor progress against these plans to ensure that the bank attains its objectives at cost-effectively and efficiently as possible;
. Oversee the preparation of the Annual Reports and Accounts of the bank and ensure their timely submission and approval by the Board;
. Familiarize with the regulatory guidelines framework of Bank of Tanzania;
. Coordinate and propose the delivery of technology based solutions which enable and support all aspects of the bank’s business plan in a timely and cost effective manner;
. Develop and maintain an effective marketing and public relations strategy to promote the products, services and image of the bank;
. Develop a performance based management culture and assume full responsibilities for the bank’s day-to day-operations;
. Oversee and monitor the implementation of the annual budget to ensure that budget targets are met and that revenue flows are maximized;
. Manage the risk arising from frauds to ensure that they are eliminated by proactively examining the process environment in which the bank operates and providing strategic guidance on future operations; and
. Plan and direct cash Operations in the bank’s Central Currency Unit and ensure branches are served and risk of keeping idle cash is minimized.

1.1.3 QUALIFICATION AND EXPERIENCE
. Master’s Degree either in Business Administration, Strategic Management, Financial Management, Marketing or related field from recognized university.
. Bachelor’s Degree either in Banking, Business Administration, Accounting, Marketing or related field from recognized university.
. Must be either an Associate Member of the Chartered Institute of Bankers (ACIB), Certified Public Accountants (CPA), Association of Chartered Certified Accountants (ACCA) or related qualification.
. A Minimum of 10 years working experience in banking operations 5 years of which should be in a senior managerial position in banking operations.
. Demonstrable experience in leadership and strategic management.
. Ability to handle numerous diverse projects to tight timescale in a rapidly changing environment.
. A sound knowledge in IT management systems.
. A wide knowledge of the banking Industry.
. Must be familiar with corporate banking law, regulations and management best practices.
. Excellent people leadership and management skills.
. Self-driven and results-oriented, ability to work conscientiously independently, efficiently and effectively.
. Good interpersonal and communications skills (English & Swahili)
. Willingness to live and practice the core values of the bank.
. Detailed knowledge of financial accounting, banking operations and risk management practices.
. High level of integrity and honesty.
. Awareness and investigative behavior of the bank’s operations.
. Proficiency in Microsoft Operations.
. Excellent analytical and problem-solving skills.
. Age between 35 to 45 years.
1.1.4 NATURE OF EMPLOYMENT
. Fixed term contract renewable once subject to good performance and delivery.
1.1.5 REMUNERATION
. Attractive remuneration package in accordance with the Institution’s Salary Scale.
NB: GENERAL CONDITIONS
i. All applicants must be Citizens of Tanzania;
ii. Applicants must attach up-to-date Curriculum Vitae (CV) having reliable contact, postal address/post code, e-mail and telephone numbers;
iii. Applicants should apply on the strength of the information given in this advertisement;
iv. Applicants must attach their certified copies of academic certificates;
.Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates;
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma transcripts;
.Form IV and Form VI National Examination Certificates;
.Computer Certificate;
.Professional certificates from relevant Authorities;
v. Form VI and form VI results slips are strictly not accepted;
vi. Testimonials and all Partial Transcripts will not be accepted;
vii. Presentation of forged certificates and other information will necessitate to legal action;
viii. Applicants employed in the Public Service should route their application letters through their respective employers;
ix. Applicants who have/were retired from the Public Service for whatever reason should not apply;
x. Applicants should indicate three reputable referees with their reliable contacts;
xi. Certificates from Foreign Examination Bodies for Ordinary or Advanced level education should be certified by The National Examination Council of Tanzania (NECTA) and National Council for Technical Education (NACTE);
xii. Certificates from Foreign Universities should be verified by The Tanzania Commission for Universities (TCU),
xiii. The attachments shall include one recent passport size photo, certified copies of academic certificates, transcripts and the applicant’s birth certificate.
xiv. Deadline for application is 14 January, 2017.
xv. Only short listed candidates will be informed on a date for interview,
xvi. Application letters should be written in Swahili or English.

i. All applications must be sent through Recruitment Portal by using the following address;http://portal.ajira.go.tz/ (This address can also be found at PSRS Website, Click‘RecruitmentPortal’)

ii. IMPORTANT: REMEMBER TO ATTACH YOUR APPLICATION LETTER AND IT SHOULD BE ADDRESSED TO:
THE SECRETARY,
PRESIDENTS OFFICE, PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT
MAKTABA COMPLEX, 11102 DAR ES SALAAM.
27 BIBI TITI MOHAMED ROAD,
P.O.BOX 63100, DAR ES SALAAM.
X.M. DAUDI
Secretary
Public Service Recruitment Secretariat.

NINI Kimemkuta WEMA Sepetu....Afuta Picha Zote Kwenye Account ya Instagram

$
0
0

Nini tena kimemkuta malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu? Ama labda ameamua kutoingia mwaka 2017 kwa kumbukumbu za mwaka 2016?

Ni kwa sababu mrembo huyo ameamua kufuta picha zote kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram yenye followers milioni 2.5.


Japo haijajulikana sababu ya kuamua kufanya hivyo, uwezekano kwamba ameamua kuukaribisha mwaka mpya kwa kupost picha mpya ni mkubwa.

MAHAKAMA yaiamuru Serikali kurekebisha kifungu Sheria ya Mtandao

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kilichobatilishwa.

Hata hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.

Uamuzi huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.

Katika hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.

PICHA: Alikiba alivyofunga mwaka kwenye show yake ya Mombasa

$
0
0
Hitmaker wa Aje, Alikiba alifanya show wikiendi hii mjini Mombasa, Kenya ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.

Show hiyo ilihudhuriwa na mashabiki lukuki wa mji huo na sehemu nyingine tofauti tofauti. Tazama picha zaidi hapa chini.

RAIS Magufuli azuia chakula cha msaada Misenyi.....Awataka Wananchi Wachape Kazi

$
0
0
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amezuia serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Misenyi mkoani Kagera kwa madai kuwa wilaya hiyo haina sababu ya kukumbwa na tatizo la njaa.

Rais Magufuli amekataa serikali kupeleka chakula cha msaada katika wilaya hiyo na kusema haikubaliki kwa eneo hilo lenye mvua za kutosha na hali nzuri ya kilimo na kwamba haiwezekani kulia njaa wakati kuna uwezekano wa kuzalisha kwa ajili ya chakula.

Amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha kata ya Ishozi Wilayani Misenyi Mkoani Kagera ambapo yupo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua maendeleo mbalimbali.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli, amesema kuwa serikali haitaweza kujenga makazi ya kila mwathirika wa tetemeko mkoani Kagera kwa kuwa ina jukumu la kujenga miundombinu itakayokuwa na manufaa kwa jamii nzima kama Zahanati, Shule na barabara.

Amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao nyumba zao hazikuharibika kiasi kikubwa lakini wakadanganywa na baadhi ya watu kuwa watajengewa hivyo wakazibomoa kwa kutaka kujengewa nyumba mpya.

WAZIRI wa Burundi apigwa risasi na kufariki siku ya mwaka mpya

$
0
0
Wakati dunia ikisherehekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2017, nchi ya Burundi imeingia kwenye majonzi baada ya kumpoteza Waziri wake wa Mazingira aliyefariki kwa kupigwa risasi saa chache baada ya kuukaribisha mwaka mpya.

Jeshi la polisi la nchi hiyo limedai kuwa waziri huyo amepigwa risasi wakati akielekea nyumbani kwake huko Rohero. Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ameahidi kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayefahamika kuhusika na mauaji hayo.

Hili ni tukio la kwanza nchini humo kuuawa kwa kiongozi wa serikali lakini tayari wameshawahi kuwapoteza maafisa kadhaa kutoka kwenye jeshi la nchi hiyo.

FEZA Kessy Atoa ya Moyoni Kwa Chidd Benz na Nando

$
0
0

⏩ BY @fezakessy - Let's pray for our brothers and sisters who are caught up in drug addiction. Chidi ni rafiki yangu for many years Na Nando mdogo wangu, I will Not Post how they look like Now cos kwangu haijakaa sawa. #MadawaYaKulevya sio mchezo it's time tuache kunong'ona Na tuwe wazi! Hashtags Na Repost won't help jamaniiiii A plan is needed as a society to fight this devil.

Kwa wale ambao wanasema "wakafie mbali" mara "wameyataka wenyewe" let me tell you something;

Kuna watu wamezaliwa Na addictive personality, wanajaribu Mara moja na ndo mwanzo wa kujiuwa, wengine wanajaribu na wanaacha tu so muache kuhukumu watu kama vile nyie ni Mungu. There is nothing fair about addiction wao wenyewe wanakata tamaa.

We need to stop this drug business "Sisi" kama society, we need to teach about it and make our kids fear these drugs, and we also need to love the ones affected, pray for them because huijui Kesho it might come to your house.
Ni hayo tu for now.

HICHI Hapa Ndicho Kinakwamisha Collabo ya Lady Jay Dee na Diamond

$
0
0

Mkongwe katika anga la bongo fleva, mwanadada Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee amesema yuko tayari kufanya kazi na staa wa muziki huo Diamond Platnumz, endapo atahitaji lakini kinachoweza kukwamisha ni ratiba yake ya kazi.


Jay Dee amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na kuongezeka kwa minong'ono kuwa wawili hao wanakwepana, na hawataki kufanya kazi kwa pamoja, ambapo amekuwa akikabiliwa na mambo mengi kwenye ratiba yake.

Akiwa katika Kitengo ya Planet Bongo ya EATV, Jay amesema hana tatizo na msanii yoyote nchini na yuko wazi wakati wowote, lakini akasita kutaja ni wakati gani atafanya kazi na Diamond.

"Kwa sasa nina ratiba za mambo mengine, lakini akinihitaji niko tayari na tutafanya kazi wakati muafaka nikiwa na na nafasi" Alisema Jay Dee.

Mwezi Novemba mwaka jana, Diamond alipozungumza na EATV kuhusu suala hilo alisema yuko tayari kufanya kazi na mwanadada huyo, lakini tatizo ni kubanwa na ratiba ambayo imekuwa haimpi nafasi.

Kwa kauli hizo, sasa ni dhahiri kuwa wawili hao hawana shida kufanya kazi pamoja lakini huenda wanaogopana, huku kila mmoja akisubiri mwenzake amuanze, maana hadi sasa hakuna ambaye ameomba kufanya kazi na mwezake huku wote wawili wakidai kukwamishwa na ratiba ya kazi zao.

MAPENZI ya Jeniffer Lopez na Drake Yazidi..Lopez Akataa Mwaliko na Kumfuata Drake Las Vegas

$
0
0

Drama ya Drake na Jennifer Lopez imezidi kuendelea wikiendi hii.

Wawili hao wamezidi kuibua maswali juu ya mahusiano yao baada Jennifer kusitisha kuhudhuria kwenye tamasha aliloalikwa la NEW YEAR’S EVE mjini Miami na badala yake alikwenda Las Vegas kwenye show ya Drake aliyokuwa akitumbuiza kwenye ukumbi wa Hakkasan nightclub.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Us Weekly, “Jennifer watched and had the best time at Drake’s show.”

Ni wiki ya pili sasa wawili hao wamekuwa wakihusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi japo hakuna aliyethibitisha kati yao huku wakionekana kushirikiana kwenye wimbo wao mpya.

MAMBO ya kuzingatia kabla ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi

$
0
0

Mapenzi ni moja ya mahitaji muhimu ya wanadamu, kila mmoja wetu ahahitaji kupenda na kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba.

Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvumiliana na kuweza kuishi pamoja ni mkubwa zaidi.

1. ni lengo (ambition),
kama mmoja kati wa wapenzi (nazungumzia wapenzi ambao wanampango wa kuishi pamoja kama mke na mume) ni mtu wa kuwa na malengo na anataka kufanya kitu fulani au kuwa mtu fulani katika maisha yake na mwenzake anachukulia siku kama inavyokuja (laid back), huyu ambaye ana malengo atamchukulia ambaye ni “laid back” kama ni mvivu. Wapenzi wanatakiwa wasipishane sana katika malengo yao hata kama wana kazi mbali mbali.

2. ni uwazi (openness), 
kama mpenzi wako ni “open minded” anapenda kujifunza vitu tofauti, kujaribu vyakula tofauti, kusafiri n.k. Yule ambaye anapenda kujifunza mambo mapya kila siku atamuona mwenzake anaboa.

3. wapenzi wanaweza kuwa tofauti katika ujuzi wa hisia (emotional intelligence). 
Hapa kama tofauti sio kubwa, watu wanaweza kuvumiliana na kuishi pamoja, ila kama tofauti ni kubwa sana, yule ambaye hana ujuzi wa hisia, atakuwa anamburuza na kumharibia mudi yule ambaye amesimama imara kwenye mambo ya hisia. Onyo kwa wanaume ambao wana ujuzi au utaalam wa kusoma hisia za wanawake, wanawake ambao wana F katika ujuzi wa hisia huwa wanavutiwa sana na watu kama ninyi.

4.  ni usosho,
kama mmoja wenu ni mtu wa watu anapenda kuongea na watu na anamarafiki kibao, utamkwaza ambae ni mtu ambaye anapenda maisha “private” na ya utulivu. Mwenzako atakuwa bize anaweka picha zenu na status zinazowahusu facebook wakati wewe unataka mambo ya ndani yawe ya ndani tu. Kama tofauti si kubwa sana mnaweza vumiliana kama tofauti ni kubwa, muda si mrefu mtashindwana

5.  ni wivu.
Wivu ni kitu kibaya sana, kama mpenzi mmoja ana wivu ni ngumu kuekewana na ambaye hana wivu. Kama wote mna wivu, sawa kwani kila mmoja ataepuka kufanya mambo ambayo yanamuumiza mwenzake, ila kama mmoja ndio ana wivu ataona mwenzake hajali, basi ukimuona mwenzako anaongea na classmate wake wa zamani au ukiona mtu amepiga picha na mpenzi wako ameshikwa bega basi inakuwa fujo tupu. Kama upo tayari kwenye uhusiano, na mwenzako ana wivu, jaribu kumuelewesha kwamba kum-kumbatia rafiki yako sio kwamba ndio una mipango mingine ya siri.

Kikubwa katika yote ni uaminifu, kama hamna uaminifu katika mapenzi au ndoa. Usipasue kichwa, ondoka na tafuta mtu ambaye anakuamini au kama haupo tayari kuwa mwaminifu usijiingize katika mahusiano, utajiumiza mwenyewe na mwenzako. Msome mwenzako kabla ya kuanza kuitana wachumba, kama tangu siku ya kwanza mwenzako ana wasiwasi na wewe ukikaribia simu yake, ni afadhali umuulize mapema, kulikoni? Kama umepoteza uaminifu katika mahusiano yako, usihofu, muonyeshe mweza wako kwamba umebadilika na jinsi muda unavyoenda atajifunza kukuamini tena.

Hizi sifa zilizotajwa hapo juu sio za kina sana, lakini ni moja wapo ya mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wako wa maisha(kama basi mapenzi yana macho) kabla ya kujizamisha katika mapenzi. Je wewe unaona ni mambo gani ya kuzingatia katika mahusiano na ni mambo gani yanasababisha ndoa kuvunjika? Usisite kuandika maoni yako.

BREAKING News ; Boniface Mkwasa sio kocha tena wa Taifa Stars

$
0
0

Kocha mzawa ambae ameiongoza timu ya taifa kwa muda mrefu Chalres Boniface Mkwassa, sasa hivi sio tena kocha wa timu yetu ya taifa.

Taarifa hivi zimethibitishwa na rais wa TFF ndugu Jamal Malinzi kupitia ukurasa wa twitter. Jamal Malinzi ametoa taarifa hiyo kwa kuandika,“Mkataba wa TFF na Kocha Mkwassa,kwa makubaliano,umefikia mwisho leo.Salum Mayanga ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda wa Taifa Stars.”.



Ikumbukwe kamba kocha huyu alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambae alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015. 

Endelea kufatilia shaffih dauda website utajua zaidi kuhusu kusitishwa kwa mkataba huu na sababu zake kama zitawekwa wazi na moja kati ya pande hizi mbili

TFF Imemteua Huyu Hapa Kuwa Kocha wa Taifa Stars

$
0
0

TFF imemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda, wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kuchukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.

Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images