Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

ASKARI wa wanyama pori mbaroni kwa kuua na kuficha maiti

$
0
0

olisi mkoani Dodoma, linawashikilia askari watatu wa wanyamapori wa pori la akiba Swagaswaga wilayani Kondoa, wakituhumiwa kumuua mkazi wa kijiji cha Olimba wilaya ya Chemba kwa kumpiga risasi mgongoni wakimtuhumu kubeba nyama pori.


Akizungumza ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lazaro Mambosasa, alisema tukio hilo lilitokea Disemba 31,mwaka jana saa 7:30 mchana katika kijiji cha Selya kata ya Selya wilayani humo.


“Marehemu ambaye hakufahamika jina lake lakini mkazi wa kijiji hicho, alikuwa akiendesha pikipiki huku akiwa amepakia kiroba kilichokuwa na sukari guru ndani yake, lakini askari wanyamapori hao walimhisi amebeba nyama pori na bila kumsimamisha na kumhoji waliamua kutumia bunduki zao kumuua papo hapo,” alisema Kamanda Mambosasa.


Aidha Kamanda huyo amesema baada ya kufanya mauaji hayo, askari hao waliubeba mwili huo kwenye gari walilokuwa nalo pamoja na pikipiki ya marehemu na kiroba cha sukari guru, kisha kwenda kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo la Swagaswaga.


“Baada ya kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo, walichukua pia pikipiki na kiroba na kuvificha kila kimoja mahali pake kwa lengo la kupoteza ushahidi wa tukio hilo”.


Kamanda Mambosasa alisema wakati askari hao wanafanya tukio hilo, walishuhudiwa na mwananchi mmoja wa kijiji hicho ambaye alijificha porini ambaye aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi Kondoa.


Wahusika wa tukio hilo ambao  wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ni George Grefee (26), Chini Paulo (40) na Christopher Waunko (36).

WASANII Wetu na Mtego wa Tuzo za Kimataifa

$
0
0
Naomba wakati tunakaribisha mwaka mpya 2017 tujadili kidogo hizi tuzo za kimataifa. Kwa sasa kumekuwa na wimbi la wasanii wetu kuwa nominated kwenye tuzo za nchi za wenzetu katika hii miaka miwili iliyopita.

Tumeona wasanii wetu wa muziki, movie na ata wanamitindo wakiwania tuzo na wengine kupata hizo tuzo ambazo tunaziita za kimataifa.

Mimi concern yangu ni moja tu. Hivi hizi tuzo mbona tumekuwa tunazipata kirahisi sana siku hizi.

Ukawii kusikia Harmonize ni msanii bora anaechipukia ndani ya Africa yote, au Wema Sepetu ni muigizaji bora east africa kwenye tuzo huko Uganda.

Hivi hizi tuzo uwa tunastahili au kwa kuwa zinaitaji wapiga kula ndio maana tunazibeba kirahisi?

Awa watu wanaotupa hizi tuzo kirahisi Hivi ni sababu wanaukubali muziki wetu au wanafanya kutafuta kufahamika na kutanua tuzo zao mpaka huku East Africa na wanaona Tanzania kwenye entertainment tupo vizuri hivyo ni kama wananatutumia kufanya biashara!?

Hivi mnaamini kuna msanii toka Tanzania amefanya vizuri mwaka huu kuliko Wizkid na Techno? Kama kuna wanaofanya vizuri kuliko awa mbona hatuwaoni wakipata mialiko ya kutumbuiza kama awa wanaijeria tunaochukua tuzo mbele yao? Mbona hatuoni muziki wetu ukipata rotation ya kutosha kwenye stations za radio na tv za nchi za wenzetu?

Hizi tuzo zinapeleka mbele muziki wetu au zinatudumaza? Maana tusije kudhani muziki wetu unakuwa sababu tunapata tuzo kirahisi kumbe zinatupumbaza!

Mimi binafsi naamini sana tuzo za Mama mtv na BET maana zinatoa atleast watu wanaoeleweka ila hizi tuzo zingine siziamni kabisa sijui kwa nini.

Naona sasa hivi mpaka kina Martin Kadinda nao wanapata tuzo za kudesign.

Okay ebu kama kuna mtu ana maoni tuweze kushare kuhusu huu utitiri wa tuzo.

By Gado/JF

JE Young Dee bado anatumia madawa ya Kulevya? Maneja wake Apost Meseji yenye Utata

$
0
0

Je Young Dee bado anatumia madawa ya kulevya? Ni swali la kujiuliza baada ya meneja wa Young Dee kupost picha hiyo yenye maneno aliyoambiwa kuhusu mtu wake anayeishi naye nyumbani ambao wengi tunajua ni Mwanamuziki Young, kuwa mtu huyu anaendelea kutumia madawa kwa siri...

Katika caption ya picha hiyo Max ameandika haya:

From @maximilianrioba - Sina cha kusema! I will never feel sorry again! Never, ever!

Rubani Mtanzania Aliyekuwa Ametekwa Huko Sudani Kusini Aachiwa Huru Bila Masharti

$
0
0
Mitandao ya Sudan Kusini inamuonyesha Rubani Mtanzania aliyekuwa "ametekwa" huko Juba kutokana na ugomvi wa upande mmoja na Serikali iliyopo madarakani.Ikihisiwa kuwa Tanzania ipo nyuma ya ugomvi wa pande mbili za mahasimu wa nchi hiyo.

Kutekwa kwa rubani huyo,kulichagizwa zaidi na ujio wa mke wa Garang na ujumbe wake kwa Rais John Pombe Magufuri,ukiambatana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa nchi hiyo Ndugu Garang Mabior de Garang.

Kwa "udadisi" wa picha hiyo,anayeonekana bila shaka ni Captain Mazrui,mmiliki wa kampuni ya Zenith Aviation yenye makazi yake Zanzibar.Ndege iliyokamatwa ni aina ya C208 yenye usajili wa 5H-MZA ambao ni wa Tanzania.

Kukamatwa na hadi kuachiwa kwake ni kama pamekuwa "kimyakimya".Tungojee tamko la Serikali juu ya kukamatwa na hadi kuachiwa kwa rubani huyu.(Na uhakika wa Rubani).Kwani hata vyombo vya habari vya Sudani Kusini vinasema rubani huyo hana mawasiliano na wanaserikali huko Juba.

Captain Mohammed Nassor Saul (Mazrui) anamiliki kampuni hiyo ambayo hufanya huduma ya ndege za kukodi toka Zanz-Dsm,Znz to Mafia na Znz to Mombasa,yawezekana safari yake kwenda Sudan Kusini ilikuwa ni ya kukodiwa kibiashara kwa ndege yake.

MPANGAJI Mwenzangu Ananitega Kila Akiniona Ananigeuzua Wezele Lake

$
0
0
Huyu ni mpangaji mwenzangu, ameolewa nami nina mke, kwa siku kadhaa mke wangu ambae nampenda sana yuko likizo hivo kila nikurudi au napokuwa nafanyafanya vishughuli vya hapa nyumbani huchukua nguo na kuanza kufua huku akiwa ameelekeza kwangu wowo lake kama inavoonekana kwenye picha hii.

Sasa naombeni ushauri maana nahisi mwaka huu mpya sitaweza kuvumilia huu ujinga, lakini kabla ya yote naomba ushauri 

KERO za Michango ya Sherehe Katika Jamii ya Watanzania

$
0
0
Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.

Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.

Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.

Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.

MWANAMKE Akamatwa Akitaka Kumsafirisha Kijana Kwenye Ulaya Kwa Kumficha Kwenye Begi

$
0
0
A woman has been arrested after she was caught trying to smuggle a teenager over the border into Europe in a suitcase.

The Moroccan was stopped at the border with Spain on December 30, 2016, after the civil guard became suspicious about her package.


They found the 19-year-old from Gabon curled up inside the suitcase in Ceuta, a Spanish enclave in northern Africa.

On Sunday, 1st January, more than 1,100 migrants tried to jump a high double fence between Morocco and Ceuta in violent assault that saw one officer lose an eye. A regional government spokesman said 50 Moroccan and five Spanish officers were injured when hundreds of migrants tried to enter Spanish territory.

The spokesman said two migrants managed to reach Spanish soil. Both were injured scaling the 20ft border fence and were taken to hospital by Spanish police. Another 100 migrants climbed the fence, but Spanish agents sent them straight back to Morocco.

MAJAMBAZI Yapora Mamilioni Mbele ya Askari polisi Dar

$
0
0
WATU wanaodaiwa majambazi wamepora kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 25 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Gazeti hili lilishuhudia tukio hilo jana, saa 4 asubuhi wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari eneo hilo la taa za Tazara.

Watu hao wameporwa katika eneo ambalo huwa askari doria wametanda, lakini wakikamata pikipiki zinazotokea eneo la Buguruni.

Aidha taa za Tazara yaliko makutano ya barabara kutokea Buguruni, Temeke, Kariakoo/Posta na Gongo la Mboto ndilo eneo lenye askari wengi wakiwemo wa usalama barabarani.

Wakati tukio likifanyika kulikuwepo askari wenye magwanda maalumu ya askari doria zaidi ya watano wakivurumushana na waendesha pikipiki upande wa Barabara ya Mandela kutokesa Buguruni. Hata hivyo imeelezwa kuwa watu hao waliokuwa wakipeleka benki hawakuwa na ulinzi kama inavyoshauriwa na Jeshi la Polisi.

Majambazi hao waliokuwa watatu, walipora fedha hizo katika gari ndogo aina ya Toyota Rav4 yenye namba za usajili T 455 DFN mali ya kampuni ya kutengeneza mabati ya Sun Share iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Richard Charles.

Kwenye gari pia alikuwepo mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo, mwenye asili ya China, aliyetambulika kwa jina la Cheng Deng.

Kwa mujibu wa dereva wa gari hiyo, Charles, walikuwa wakizipeleka fedha hizo benki eneo la Quality Centre na ndipo walipovamiwa na watu hao wakiwa na pikipiki aina ya boxer wakati magari yakiwa kwenye foleni wakisubiri taa ziwaruhusu kupita kutoka barabara ya Mandela.

Charles alisema majambazi hao walimwamrisha kufungua mlango na kuwapatia begi la fedha lililokuwa limewekwa katika kiti cha nyuma huku wakimtishia kwa bastola kabla ya kuvunja kioo cha nyuma cha gari hilo na kubeba fedha hizo na kutokomea nazo.

“Kwa kweli hata sielewi mpaka sasa hivi kilichotokea. Walikuja watu wawili mmoja upande wangu mwingine wa bosi wangu wakinitishia kwa bastola nifungue mlango niwape begi la fedha. Ghafla mtu mwingine akavunja kioo cha nyuma kwa kutumia kitako cha bastola na kubeba begi la fedha na kutokomea” alisema Richard.

Askari wenye silaha walifika katika eneo la tukio dakika 20 baada ya tukio hilo wakaishia kuhoji. Hata hivyo askari mmoja ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake alilaumu tabia ya baadhi ya watu kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha pasipo kuomba ulinzi wa polisi jambo linalohatarisha usalama wao na mali zao.

“Kama walijua wanasafirisha kiasi kikubwa hicho cha fedha kwa nini wasingeomba hata ‘escort’ (kusindikizwa kwa ulinzi) ya polisi? Hili ni tatizo, hasa katika kipindi hiki kigumu cha upatikanaji wa fedha, watu wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema.” alisema askari huyo.

Hata hivyo mwandishi wa habari alipokwenda katika ofisi za kampuni hiyo kujua kwa undani tukio hilo lilivyotokea, alimkuta mlinzi ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo.

Hata hivyo mlinzi huyo alimwelekeza mwandishi kuongea na mmoja wa wahusika wa kampuni hiyo mwenye asili ya China ambaye baada ya mwandishi kujitambulisha, alikataa kutokea kwa wizi huo.

Pamoja na kukataa alimwamuru mwandishi aondoke katika ofisi zao huku akisisitiza hakuna tukio hilo na hakutaka kuzungumza zaidi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro alipopigiwa simu na gazeti hili jana ili kupata ufafanuzi zaidi wa tukio hilo simu yake iliita bila majibu na baadae alipokea na kusema yupo kwenye kikao.

Mwandishi alimtumia ujumbe mfupi wa simu kueleza tukio hilo akimuuliza kama ana taarifa lakini hakujibu ujumbe huo na alipopigiwa tena baadae jana, simu iliita bila majibu.

HATIMAYE Aliyechomwa Mkuki Mdomoni Areja Nyumbani

$
0
0
MKULIMA na mkazi wa kitongoji cha Upangwani , Kijiji cha Dodoma Isanga , Kata ya Masanze, wilaya ya Kilosa , mkoani Morogoro , Augustino Mtitu,(35),ameruhusiwa kutoka Hospitalini alikolazwa.

Madaktari wamesema kwamba kuruhusiwa kwa mgonjwa huyo kumetokana na yeye kupona kufuatia kufanyiwa upasuaji mkubwa mara baada ya kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni. Mtitu , alichomwa mkuki na kutokea shingoni Desemba 25, mwaka jana na watu wa jamii ya wafugaji wa kimasai.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa tano asubuhi mwaka jana wakati alipokuwa shambani kuzuia vurugu zilizokuwa zimetokea baada ya wafugaji wa jamii ya kimasai kulisha mifugo yao kwenye shamba la maharage na mahindi yaliyopo katika kijiji hicho.

Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Frank Jacob , akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana alisema kuwa Mtitu ambaye alilazwa wodi namba moja ya wagonjwa wa majeruhi wa ajali na nyinginezo katika hospitali hiyo tangu Desemba 25 mwaka jana aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo kwenda nyumbani baada ya kupona jeraha lilolotokana na mkuki na kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Hata hivyo, Dk Jacob alimshukuru Mungu na madaktari , wauguzi kuwezesha kufanikisha upasuaji wa mgonjwa huyo uliofanikisha kuondolewa kwa mkuki aliochomwa mdomoni na kutokea upande wa shingoni .

Kwa upande wake Mtitu, akizungumza kwa njia ya simu akiwa Kilosa , alimshukuru Mungu , madaktari , uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa na wananchi wa kijiji hicho kwa kuwezesha kunusuru maisha yake baada ya kuchomwa mkuki mdomoni uliotokea shingoni na kuweza kupona.

Mtitu amekaa wodini siku nane a baada ya kuruhusiwa , sasa anakwenda nyumbani kuungana na familia , ndugu na jamaa katika kijiji chao cha Dodoma Isanga , Kata ya Masanze, wilayani Kilosa.

Naye ndugu wa Mtitu, Mwalongo Sanga, akizungumza kwa njia ya simu kutoka kijiji cha Dodoma Isanga , alisema ndugu yao alifika mjini Kilosa ambapo familia yake ilikuwa inaishi kwa muda baada ya Mtitu kulazwa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Watu 12 wanashikiliwa na Polisi na kati yao saba wameshafikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kilosa kujibu mashitaka ya kumchoma mkuki mkulima huyo na kufanya ghasia.

NCHI Ambazo Mtanzania Anaingia Bila Visa

$
0
0
Nchi 73 ambazo Mtanzania anaweza kuingia bila visa.
Afrika Kusini
Antigua & Barbuda
Albania
Armenia
Azerbaijan
British virgins Island
Barbados
Bangladesh
Botswana
Burundi
Bahamas
Belize
Bermuda
Bolivia
Cambodia
Cayman Island
Cape Verde
Comoros
Cook Islands
Djibout
Dominica
Ethiopia
Ecuador
Egypt
Fiji
Grenada
Guinea
Georgia
Haiti
Hong Kong
Jamaica
Jordan
Kenya
Kosovo
Laos
Lebanon
Libya
Liberia
Macau
Malaysia
Madagascar
Maldives
Malawi
Mauritius
Micronesia
Mozambique
Monserrat
Mongolia
Nauru
Niue
Nepal
Namibia
Nicaragua
Palau
Philipines
Qatar
Rwanda
Samoa
Suriname
St. Kitts & Nevis
St. Vincent & Grenadines
St. Lucia
Sierra Leone
Singapore
Swaziland
Tuvalu
Togo
Turkmenistan
Trinidad & Tobago
Timor-Leste
Uganda
Vanuatu
Zambia
Zimbabwe

Serikali Yanunua Shule ya CCM

$
0
0
Hatimaye Rais John Magufuli amehitimisha mjadala wa matumizi ya fedha za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwa kukarabati Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na CCM kisha Serikali kuinunua.

Novemba mwaka jana, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronicus Karumuna alilalamikia zaidi ya Sh70 milioni za tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 mwaka jana na  kusababisha vifo vya watu 17 na kuharibu miundombinu mbalimbali, kutumika kukarabati shule hiyo ya Jumuiya ya Wazazi huku waathirika wakiwa hawajapata msaada wa maana.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1966 ikiwa ya kwanza ya Wazazi nchini, ilikarabatiwa na Serikali ili kuiwezesha kupokea wanafunzi wa Sekondari ya Ihungo baada ya shule yao kuharibika kwa tetemeko.

UTAFITI: Wanawake Weupe Wanaringa Kuliko Weusi

$
0
0
Kutokana na utafiti niliofanya mimi mwenyewe sasa ni dhahiri wanawake weupe wanaringa sana kuliko wale weusi...

Utafiti huu ulijumuisha kuwatokea moja kwa moja, asilimia kubwa kati yao hata ilipotokea kuwaita wengi walionesha dharau sana kuliko wale weusi. 

Sasa kama na wewe ulishawai kutokewa na hali hii unga tela ili nione kama utafiti wangu uko sahihi kias gani

DIWANI Asiyejua Kusoma na Kuandika Aibuka Tena...Adai Anajua Kusoma

$
0
0
Zikiwa zimepita wiki chache tangu diwani wa Boma katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Julist Kisoma asimamishwe kufanya shughuli za udiwani akidaiwa kutojua kusoma, amefunguka akisema alisoma hadi darasa la saba lakini hakufanya mtihani wa mwisho.

Kisoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Mafinga, amesema anafahamu kusoma na kwamba, tuhuma dhidi yake zimetokana na msimamo wake wa kusimamia rasilimali za kata yake na halmashauri.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Mkoga alitangaza kumsimamisha diwani huyo wa Chadema kufanya shughuli za udiwani ikiwamo kuhudhuria vikao hadi suala lake litakapopatiwa ufumbuzi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


RAIS Magufuli Asisitiza Serikali Haitawajengea Nyumba Wananchi Walioathirika na Tetemeko

$
0
0

BUKOBA: Rais Magufuli asisitiza Serikali haitawajengea nyumba wananchi walioathirika na tetemeko

Asema hakuna nchi duniani imejenga nyumba za wananchi baada ya kukumbwa na tetemeko.

Aitaifisha shule ya Omumwani iliyokuwa ikimilikiwa na jumuiya ya wazazi(CCM).

MASHABIKI wamlilia Young Dee baada ya meneja kudai amerudia tena unga

$
0
0

wa mujibu wa meneja wa Young Dee, Maximillian Rioba, rapper huyo amerejea tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.


Taarifa hiyo imekuja katika wakati ambao mashabiki wengi wa muziki waliamini kuwa rapper huyo ameachana na matumizi ya unga

Max anadai amejaribu kila awezalo, lakini sasa ameamua kunawa mikono. Amezitoa taarifa hizo Instagram alipokuwa akichat na msichana aitwaye Wendy Eliah.


Kwenye post yake ya Instagram, Max aliandika ujumbe toka kwenye biblia: Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung`uta mavazi yake mbele yao akisema, “Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine.” Matendo Ya Mitume 18:6 NENO LA BWANA LIMENENA. KILA MWENYE SIKIO NA ASIKIE….



Baada ya kuenea kwa taarifa hizo, mashabiki wameenda kwenye ukurasa wa Instagram wa rapper huyo kumpa ushauri.

Crown_princess_shorla

Munaoleta hiki kiama kwa wapendwa wetu na kutusonononesha kiasi hiki, roho wa Mungu yu mbele yenu, kiama kitawaangamiza soon, kumbukeni mnaowaumiza walizaliwa, wanawazazi wana mama ambao waliteseka miezi Tisa tumboni na mwisho kuingia labour kwa uchungu wa kufa kupona kuwazaa hao watoto, nawaapia chozi la mama hawa Mungu hatolipa mgongo atawaadhibu, kazaneni kuwauwa watoto wa wenzenu kwa kutaka utajiri wa haraka, moto na hasira ya Mungu I juu yenu, @youngdaresalama my brother don’t do that to your poor daughter and her mother, they really need you more than anyone in this world, plz stop this stupid act, grow up brother we don’t wanna loose you, it’s not too late to change my dear! @maximilianrioba don’t give up on him brother at least pray more for him najua lililo gumu kwa mwanadamu Mungu anajua utatizi wake, even if hatokuelewa na nguvu za Mungu atasimama kutete naye. Tuwaombee zaidi kuliko kuwakatia tamaa, najua inavunja moyo but tutambue hata Mungu hajawahi kutukatia tamaa wanadamu na maudhi yetu yote, let us pray for them! For really inaumiza Sana but they our people, our brothers and our family too.


spycedollydoll

Please don’t go back in Da hell that brought you so much regreats u a good man please do the best and prove wrong people who thought you can’t take care of ur baby princess

ireneemoshi

We mtoto wewe, kwann mnapenda kuwapa.shida wazaz.wenu unafkir mama aliye kubeba miez TSA tumbon anajickiaje ukiharbika wewe, yan kma umerudia matapishi acha aisee unapotea kabsaaa umepata mtoto hem mleee huyo, ukiwa kichaa nan atamuhudumiaa, mbona ujana unakupeleka pabaya namna hyo unapte ujue ur still young, kwan shida n nn mpaka uanze kula vtu vya ajabu watu tunaumia kuona vjana mnaharbikiwa bado wadogo jenga maisha yako acha makundi yasiyo na msng hao wanakupotoshaa tuu hem kuwa kioo cha jamii, au una umekumbwa na pepo, hem mkatae shetan cmama mtoto wa kiumee jenga familia wewe ushakuwa baba, kama ni kweli unaapiga hzo mambo kisr achaaaa, wapote dogoo hem angalia picha za jinsi ulivokuw mwanzo na sasa, je unataka kurud ulpotokaaa.

ms._wise_always

@youngdaresalama Acha ujinga dogo , ww ni baba now … ww sio mtu wakutoa watu machozi tena? wewe hujui unathamani gani? au ni makusudi unataka kijana wa watu ajute?@maximilianrioba Kweli unamtia kwenye majonzi namna hii acha upuuzi ww ni mtu mzima now , You shud standup and be ambassdor of others like Nando and Chidy and also stand for your Tamar also
but WHY?

syper_jr

I cant judge you niggha mwenye haki ya kuongelea your lyf n watu ka kna max wanaokufaham vzuri ila yo still a great rapper af una Tamar baharia langu sooo watever u du all remember is yu have a life n a beautiful babydaughter…..nakumbuka max once cried kweny interview clouds sooo no body can make him change his mind kukusupport mpaka ue back again in line siamin if max iz that dumb mpk kupost hii issue yenu insta a only hope he meant by postin uku atha ppo gotta try tu b on yo side bruh..all the best mwanangu D don give up on your kid

wavy_lord_

@youngdaresalama nigga you started cool unataka utuangushe get the fuck out that shit brother Again get the fuck out nigga that shit aint cool i feel like crying right now @maximilianrioba this shit is fVCkn sad

Jitihada za kumtafuta Young Dee ili aelezee kinachozungumzwa zinaendelea.

ZAMARADI na Kipindi Chake Kurudi Hewani Baada ya Kifungo cha TCRA

$
0
0

Kipindi cha runinga cha Take One cha Clouds TV kitarudi hewani mwezi huu baada ya hukumu yake ya kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iyotolewa Octoba mwaka 2016 kumalizika mwezi huu.


Zamaradi Mketema

Kipindi hicho kilifungiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

Mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema ametangaza ujio wa kipindi hicho huku akiwataka mashabiki wa kipindi hicho kutoa maoni juu ya mabadiliko ya kipindi hicho.

“Tukiwa tumemaliza likizo yetu tuliyopewa na TCRA, kipindi chetu kinarudi rasmi January hii 2017 namaanisha Take One mtangazaji wako nikiwa yuleyule Zamaradi H. Mketema,” aliandika Instagram Zamaradi.

Aliongeza, “Hebu niambie katika msimu wetu mpya unatamani kuona nini kwenye kipindi!!? Unatamani irudi vipi ili kuboreshwa!!? Nini kiongezwe!? Nini kipunguzwe!? Nipe maoni yako tafadhali nami nitayafanyia kazi,”

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yaliyorushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

MANENO ya dogo aliyetangazwa ‘man of the match’ vs Yanga

$
0
0

Nimefanikiwa kufanya mazungumzo mafupi na kijana mdogo Greyson Gerald ambaye alitangazwa kuwa man of the match wa mechi kati ya Yanga dhidi ya Jamhuri .

Licha ya timu yake kupoteza kwa idadi kubwa ya magoli (ilifungwa 6-0) kijana huyu anavalia jezi namba 6 kwenye kikosi cha Jamhuri alikuwa bora katika mchezo huo kwa kuonesha kiwango bora katika eneo la kiungo licha ya kupambana na wachezaji wakongwe na wazoefu kama Kamusoko, Zulu, Niyonzima na wengine wengi.

Nashawishika kumuuliza nini hasa kilichopelekea utulivu wake uwanjani na kujiamini mbele ya Yanga ambayo ndio mara ya kwanza alikuwa anakutana nayo tangu alipoanza kucheza soka.

Sikuwa na presha kabisa, niliona ni kawaida licha ya kucheza na timu kubwa,” anasema Greyson ambaye anaitumikia Jamhuri kwa msimu wa pili.

Kinda huyo ambaye aling’ara mbele ya mibaba ya Yanga anasema alianza kucheza ligi daraja la kwanza akiwa na Kurugenzi ya Mafinga, Iringa alipocheza kwa msimu mmoja kabla ya kuvuka maji na kujiunga na Jamhuri ya visiwani Zanzibar.

“Najisikia furaha kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo dhidi ya Yanga, lakini kwa idadi ya magoli tuliyofungwa leo nadhani ilikuwa ni presha kwa wachezaji wenzangu kwa sababu tulikuwa tunacheza na timu kubwa kwahiyo wakapoteza kujiamini.”

Watu wengi huenda wanadhani dogo ni mzaliwa wa Zanzibar, lakini kumbe anatokea Ifakara mkoani Morogoro: “Mimi ni mzaliwa wa Ifakara, Kilombero mkoani Morogoro.”

RAPPER Feature auanza mwaka mpya kwa style ya Wema Sepetu

$
0
0

Rapper wa Marekani, Future ameamua kuuanza mwaka mpya wa 2017 kwa kufuta picha zote kwenye mtandao wa Instagram.

Akaunti ya rapper huyo ina followers wapatao milioni 8.7 huku akiwa amemfollow mtu mmoja pekee ambaye ni Dj Esco.


Future anaungana na malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ambaye na yeye aliamua kuuanza mwaka kwa kitendo kama hicho cha kufuta picha zake kwenye mtandao huo

NIVA akiri kupika 'bifu' na Nay wa Mitego

$
0
0

Msanii wa bongo movie Niva amesema madongo yote waliyokuwa wanatupiana na Nay wa Mitego kwa mwaka 2016 ilikuwa ni 'bifu' za kimuziki na mipango ya kibiashara kwa upande wa movie lakini hawana bifu lolote kati yao.

Akiongea kupitia eNewz Niva amesema hawajawahi kugombana na wala hawana tatizo lolote na Nay kwa kuwa ni watu ambao wamekuwa sehemu moja wamesoma shule moja na wamekuwa wakisaidiana kwenye mambo mbalimbali hata wakati Niva anafunga ndoa Nay alimsaidia kwa kiasi kukubwa.

Hata hivyo Niva ameweka wazi kuwa mambo hayo ya kudanganya mashabiki zao wameyaacha mwaka 2016 na mwaka huu hawatakuwa na mambo kama hayo kwa kuwa ni mwaka wa mafanikio zaidi kisanaa

TUHESHIMU tu Wataalam na Wanataaluma-Habib Mchange

$
0
0

iki hii nimekumbuka namna Dr. Idrissa Rashid mwaka 2008 alipoishauri Tanesco kiuchumi iinunue mitambo ya Dowans tena kipindi hicho ilikuwa inauzwa bei ya 'kutupwa'.

Wachumi wenzake kina Zitto Kabwe wakamuunga mkono tuinunue itatusaidia huko mbeleni.

Wanasiasa wakapinga kwa kelele nyingi, wakasema mitambo mibovu, chakavu haifai na wakaenda mbali wakasema Kina Zitto wanatetea kisa wamehongwa na Kina Rostam.

Wakaongeza kuwa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inatukataza kununua vitu vya mtumba

Waliosema haya Leo wengine ni mawaziri waandamizi wa serikali ya JPM na wengine ni viongozi na wabunge machachari wa UPINZANI.

Wanasiasa wakashinda. Mitambo tukaiachia, na kesi tukashindwa, tukalipa zaidi ya Bilioni 90 kwa kosa la kuvunja mkataba bila kufuata utaratibu. .

Mitambo Ile Ile mibovu, chakavu na ya kifisadi.

Marekani wakainunua, ikabadilishwa Jina ikaitwa Symbion.

Ikaanza kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco.

Obama akaja kutoka Marekani akaizindua.

Wale wale Waliosema mibovu wakaisifia na kuipongeza Marekani.

Mitambo ambayo tungeinunua tungeimiliki wenyewe wala tusingeuziwa umeme.

Leo tunauziwa umeme ghali kutokana na mitambo tuliyoruhusu wanasiasa wawapuuze wataalam.

Hivi ninavyoandika Symbion wanatuuzia umeme kutoka kwenye mitambo ya mtumba.

Sheria inatukataza kununua mitambo ya mtumba lakini inaturuhusu kununua umeme unaotokana na mitambo ya mtumba.

Tuwaheshimu wataalam wetu.
Habib Mchange
Mwananchi
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images