Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

AFA Baada ya Kufakamia Pombe ya Kienyeji

0
0

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Bahati Mbula (43) mkazi wa Kanindo Kata ya Kishiri amefariki dunia kwenye mkesha wa mwaka mpya baada ya kudaiwa kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema hilo ni tukio pekee lililotokea katika mkesha wa mwaka mpya mkoani Mwanza.

“Nimepata taarifa moja tu ya mtu mmoja kufariki huko Kanindo, marehemu huyo anadaiwa kunywa kwa kuchanganya pombe za aina nyingi za kienyeji.

“Nimeambiwa marehemu huyo alitoka eneo la Sawa Kata ya Lwahnima na kwenda kunywa huko Kanindo, sasa usiku huo wenzake walidhani ameondoka kurudi kwao kumbe alikuwa ameanguka  njiani karibu na pale alipokuwa akinywa pombe hiyo,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema Jeshi la Polisi linafuatilia kwa uchunguzi zaidi kama alikuwa anaumwa au kuna kitu kingine.

“Tuliwaambia wananchi washerekee  mwaka mpya bila kuleta madhara yoyote ikiwamo kuchoma moto matairi, kuendesha magari ovyo,  kurusha mawe nadhani watu walizingatia ndiyo maana hata matukio ya uhalifu hayakuwapo,” alisema.

Njia Rahisi Ya Kuchukua Namba Kutoka Kwa Mwanamke Unayemjua

0
0
Kuchukua namba kutoka kwa mwanamke ni rahisi zaidi kuliko hata kutamka jina lako. Unachohitajika ni kuenda moja kwa moja kwa mwanamke unayetaka kumuomba namba halafu unamwagiza akupatie. Mara nyingi mwanamke hawezi kukataa kukupatia namba yake unless uwe umemuapproach kwa njia isiyofaa ama hakujui.


Mara ya mwisho mimi binafsi nilichukua namba kwa mwanamke chini ya dakika moja ya kukutana na yeye. Nilikuwa nimeandamana na marafiki zangu halafu mwanamke mmoja akapita kando yetu halafu muda wa dakika nikaamua kumuaproach na kunipatia namba yake ya simu hapo hapo.

Kama bado unatatizika ni njia gani za kuchukua namba ya simu kutoka kwa mwanamke basi fuata maagizo haya ya haraka ambayo nitakuelezea.

#1 Jiamini. Kujiamini ni kitu muhimu. Wakati unapoamua kuapproach mwanamke lazima uwe unajiamini. Utajiamini vipi? Kujiamini ni rahisi. Kile unachohitajika kufanya ni kuweka nia kuwa wakati ambapo utamwaproach mwanamke lengwa basi lazima namba yake ya simu atakupatia. Huko ndiko nikujiamini.

#2 Kuwa na mawazo chanya. Mawazo chanya ni mawazo ambayo yanakubaliana na wewe. Mfano unaweza kuwa unataka kufanya kitu, halafu katika akili yako umeweka dhana ya kuwa kile ambacho unakusudia kufanya basi kitafanikiwa. Haya ndio tunayaita mawazo chanya. Ni dhana ambayo unaamini kuwa itatokezea. Ukiweka mawazo chanya kuwa ukiapproach mwanamke flani na atakupa namba yake ya simu basi bila shaka utafanikiwa. Lakini ukiweka mawazo ya kuwa hautafanikiwa basi kweli hautafanikiwa.

#3 Fanya Majaribio. Wakati mwingine inakuwa vigumu kabisa kwa wanaume flani kuongea na mwanamke. Inakuwa vigumu zaidi kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Njia rahisi ya kutatua shida hii haraka ni kuigiza. Kuomba mwanamke namba haichukui zaidi ya dakika mbili, hivyo unaweza kufanya mazoezi jinsi utakavyoongea ukiwa peke yako. Unaweza kuigiza vile rafiki yako anavyoomba namba ya simu ama unaweza kufanya mazoezi kivyako kabla kumuapproach mwanamke kumuomba namba ya simu.

#4  Relax. Wakati unapoach mwanamke lazima uwe umetulia. Punguza wasiwasi, toa kijasho chochote ambacho uko nacho, pumua kiutulivu na uondoe ubabaifu wowote ulio nao. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa umerelax utakuwa na nafasi nzuri ya kukumbuka mambo ambayo umeyapanga kumwambia mwanamke flani. Hivyo ni muhimu kurelax kabla ya kuchukua approach yeyote.

 Njia nzuri ya kumuapproach mwanamke

Njia rahisi ya kuomba namba ya simu kutoka kwa mwanamke ambaye unamjua na anakutambua ni ile ya moja kwa moja. Ukimwona anatembea mtaani halafu wewe umesimama na marafiki zako, mwanzo hakikisha umefuata masharti tuliyoyaeleza hapo juu; jiamini, relax, mawazo chanya na mwigo. Nenda moja kwa moja na umwambie hivi:

"Mambo Mamito. Niko na ishu flani nataka kukuambia lakini sahizi naona si wakati mzuri wa kukuambia... Nipatie namba yako ya simu nitakupigia simu usiku."

AU

"Mambo Mamito. Napatie namba yako ya simu nataka kukupikia simu jioni nikwambie kitu flani"

Hii ndio njia ya moja kwa moja. Mwanamke wa kawaida, ambaye anakutambua hawezi kukataa kukupatia namba yake ya simu. Mwanzo unaweza kuwa na bahati ya kuwa huyu mwanamke alikuwa inteested na wewe tangu kitambo lakini anashindwa jinsi angeweza kuwasiliana na wewe.

Kama ni mwanamke ambaye humjui na hakujui, basi ni vyema kwanza ujitambulishe ili akufahamu. Si lazima uchukue namba yake ya simu siku io hio bali unaweza kungojea muda mpaka mzoeane.

Wanaume wengi wanatatizwa na tatizo la kutojiamini na woga. Lakini naamini kama unaweza kutatua mambo hayo mawili basi kazi yako itakuwa rahisi

MUKANDALA: UDSM Haijaathirika Kwa Teuzi za Rais Kwa Wanataaluma wake

0
0
Rais J.P Magufuli amekuwa akiteua wanaataluma kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hali.iliyopelekea baadhi ya watu kuhoji kama teuzi hizo hazitaathiri uwezo wa chuo hicho kitaaluma.

Akitolea ufafanuzi suala hilo Makamu Mkuu (Deputy Chancellor) Profesa Rwekaza Mukandala amesema kuwa teuzi hizo hazijaathiri chuo hicho kikongwe katika taaluma. Aliongeza kuwa chuo kina uwezo wa kuzalisha rasilimali watu kwa kiwango kikubwa hivyo teuzi chache kwa nafasi mbalimbali katika serikali kuu haziwezi kuathiri chuo.

"Chuo kikuu cha Dar es salaam na serikali vina historia ya mashirikiano kwa miaka mingi na lengo hasa la kuanzishwa kwa chuo hiki ni kuzalisha na kufundisha wataalamu katika nyanja tofauti ili watumike serikalini" alisema Mukandala.
Hivi karibuni rais Magufuli alimteua Dr Tito Esau Mwinuka kuwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO.

Teuzi nyingine zilizofanywa na Rais kwa wanataaluma kutoka UDSM ni kama ifuatavyo:

1. Prof Godius Kahyarara - DG NSSF
2. Prof EGID MUBOFU - DG TBS
3. Prof Adolf Mkenda - PS wizara ya Viwanda na biashara
4. Justine Ntalikwa - Wizara ya Nishati na Madini
5. Dr John Njigu - Mwenyekiti NEEC
6. Dr Ayoub Ryoba - DG TBC
7. Prof Longinusi Rutasitara - Mshauri wa Rais masuala ya kiuchumi

Kwa kumbukumbu tu: UDSM ina wanataaluma wenye Phd wapatao 600.

Wapo wanaohisi kuwa UDSM ndio chanzo cha Think Tank ya Tanzania.
Mafanikio ya wanataaluma hawa katika nyadhifa ni jambo linalohitaji mjadala tofauti na huu.

RAIS Kagame na Mkewe Wapagawa na Wimbo wa Darassa

0
0

Nimekutana na Hii Video Rais Kagame wakiserebuka Vyema Wimbo wa Darasa unaoitwa Mziki....Embu Itazame na wewe Kidogo

MAX 'Mimi Nitaacha Kutoa Machozi Kwa Ajili ya Young Dee, Anguko la Pili Huwa Mara Dufu ya Anguko la Kwanza'

0
0
Meneja wa Young Dee na Mmiliki wa Studio za Authentic siku yakuzaliwa kwa Young Dee aliandika Haya kwa Uchungu akiashiria kuwa Msanii wake huyo ameanza kupotea tena kwenye Madawa ya kulevya baada ya kuhaidi kuacha:

DR. Magufuli Yuko Sahihi na Serikali yake, Watu Walizoea Dezo Sana Tubadilike Jamani

0
0
Juzi hotuba ya Mh.Rais kuna baadhi ya watu wanaiponda, mimi nashangaaa sana hivi watanzania tukoje? Nchi hii jamani tulifikia pabaya sana kwa serikali kuendeshwa kwa ghiliba, uongo, udanganyifu, unafiki, na kupakaziana bila kuwa wakweli, tukaomba tumpate Rais atakae kuwa mkweli, asiyeogopa lawama za ndugu, marafiki, na wananchi ili tusonge na kutoka tulipo.

Juzi Mh.Rais akiwa Kagera amewaambia wanakagera, waanga wa tetemeko na wananchi kwa ujumla ukweli uliyomchungu na usiopingika kuwa serikali haiko kwa ajili ya mtu mmoja mmoja bali kwa maslahi ya jumla ya wananchi wote.

Sisi watanzania tulikuwa tumezoea sana maisha malaini sana, ya msaada, tegemezi na kulialia na kununa, mfn. mtu akiwa mfanyakazi anakuwa na tegemezi wengi sana mjini na kijijini wote wanataka salary yake ika wengine sasa hawafanyi kazi kisa kaka,dada,mjomba n.k yupo bandari, tra,tanesco n.k kila mtu sasa afanye kazi na siyo kumtegemea mtu au mambo ya kona kona ili usawa uwepo na nchi isongeee. Nchi inaendelea kwa kuwa na producers wengi, sisi tuna production man-force kubwa ila wategeaje na wazembe.

Ifike wakati sasa ukweli usemwe hata kama ni chungu na ina kera kiasi gani. Awamu iliyopita watu walipenda kusikia uongo na maneno ya kuremba na kubembelezwa.

By Leo Ojije/JF

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

0
0


Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza Hapa Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

40 Ya Mdogo Wa Tiffah Usipime, Mastaa Wakubwa Afrika Watajwa Kuhudhuria

0
0
STORI: GABRIEL NG’OSHA, GAZETI LA UWAZI, TOLEO 1021, JANUARI 3-9, 2017

DAR ES SALAAM: Habari ya motomoto inaeleza kuwa Januari 16, mwaka huu ndiyo siku ambayo mtoto wa kiume wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ atatimiza siku 40 tangu alipozaliwa Desemba 6, mwaka jana.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa ndani ya familia ya Diamond zilieleza kuwa, Nillan ambaye ni mdogo wa mtoto wa kwanza wa staa huyo, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ anatarajiwa kufanyiwa shughuli hiyo kubwa ya kumtoa ambayo itafanyika nyumbani kwa jamaa huyo huko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Taarifa nyeti zilieleza kuwa, tayari baadhi ya watu wao wa karibu Bongo wamefikishiwa kadi ambapo watakwenda Sauz na kurudi kwa usafiri maalum wa ndege ambapo kila kitu watakuwa wameshalipiwa.

“Tayari Diamond ametoa kadi maalum kwa watu wake wa karibu. Waliopewa kadi wanatakiwa kuthibitisha kama watahudhuria ili kuweka mambo sawa na kujua idadi kamili ya watakaokwenda kwa ajili ya kuwagharamia.

 Mtoto wa kwanza wa Diamond, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’  akiwa kalala na   Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ .

“Unaambiwa siku hiyo (Januari 16), watu watakula bata la kufa mtu maana shughuli ya Chibu Junior itaifunika ile ya Tiffah.

“Mbali na mastaa na watu wa kila aina kualikwa kutoka Bongo lakini pia 40 ya Chibu Junior itahudhuriwa na mastaa wakubwa Afrika ambao wengi ni rafiki zake Diamond hasa wa kutoka Nigeria,” kilifunguka chanzo chetu kikiomba chondechonde kisitajwe popote.


Mbali na chanzo hicho, mtu mwingine ndani ya familia hiyo alipoulizwa juu ya taarifa za mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuhamia Sauz kwa ajili ya shughuli hiyo alisema kuwa, si kwamba tu amehamia lakini kwa sasa mzaa chema huyo ameshakuwa mwenyeji wa mitaa ya Johannesburg kufuatia kuwa huko tangu alipojifungua mkwewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Desemba 16, mwaka jana.

Hata hivyo, alipotafutwa Diamond hakuwa hewani ambapo mmoja wa wanafamilia alisema kuwa yupo nyumbani kwake Sauz kwa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2017.

“Jamaa hayupo Bongo labda umcheki kwa WhatsApp, yupo Sauz home kwake si unajua mambo ya bata za sikukuu ya mwaka mpya? Kwani kuna ishu gani?,” alihoji mwanafamilia huyo kwa sharti la kutotajwa kwani siyo msemaji wa familia ya Diamond.

Alipoulizwa juu ya 40 ya mdogo wa Tiffah na kwamba kuna mwaliko maalum na itakuwa bab’kubwa, jamaa huyo alifunguka:

“Ebana hiyo shughuli achana nayo kabisa lakini unachotakiwa kujua ni kwamba itampaisha Chibu Junior Afrika nzima.”


UJUMBE Mzito Toka Kwa Lemutuz Kuhusu Madawa ya Kulevya Nchini....

0
0

⏩BY@lemutuz_nation -  Wiki hii the National Debate is MADAWA YA KULEVYA kama ulivyo ushoga it is another very sensitive Subject niliwahi huko nyuma kusema kwamba binafsi ninalifahamu sana hili la Drugs kwa sababu nimewahi kuishi at the Source of it New York City nilichokiona kwa macho yangu ni kwamba once binadam akishajikita kwenye kuyatumia madawa ya kulevya huwa anafikia kutumia Cocaine kwa njia ya kujidunga Sindano that is the end of story ni almost impossible kwa yule binadamu kuja ku recover...I am just being realistic na sio kumkatisha anybody tamaa mfumo wa Ubepari Capitalism una tabia moja ya kuheshimu walioshinda tu lakini hauna nafasi kwa walioshindwa tunawahitaji sana Investors like kutoka USA but tatizo ni kwamba wanapokuja kuwekeza wanakuja na utamaduni wao pia au the American Culture ambayo inapokuja haina msalie mtume inasomba everything out na kui replace with its own ...briefly chanzo cha Binadam kutumia drugs ni akili kushindwa kuvumilia maumivu ya kawaida ya maisha kama kuachwa na mpenzi au kupoteza ajira au kupoteza kipato au kupoteza umaarufu au hata preasure za ku maintain umaarufu pia zinaweza kumpelekea binadam kwenye drugs Wazungu wanaita "DRUGS ADDICTION" ....maana yake ni akili yako haiwezi kufanya kazi yenyewe bila msaada wa Drugs na hasa kila inapofikia how to deal na maumivu ya maisha na binafsi ninasikitika sana kusema kwamba hata the Americans kwenye hili la Solutions wamefeli cause tatizo sio kuzuia Drugs zisiingie ila how to instill strong family values to our Society so that people would never think of looking for dependency of substance for their Brain wakati wa kufikiri na hasa kupambana na maumivu ya maisha ...binadam mwenye values hawezi hata kufikiria kutumia Drugs kupigana na maumivu ya kufikiria mambo ya maisha na hasa chanzo cha yote FEAR ambayo behind it ni Shetani I mean rehabs zinasaidia lakini very temporary sio permanent ...Taifa tunahitaji kuwekeza kwenye FAMILY VALUES tupiganie kuwa na Strong Families na tupiganie sana UPENDO kwa wanajamii tupiganie jamii inclusive kwa wote tusiwe na wanajamii wanaojifikiria hawahitajiki na jamii at large ...tuzidishe upendo MAY GOD BLESS TANZANIA!

TUNDA la Tikitimaji Lina Faida Nyingi Mwilini na Hutibu Baadhi ya Maradhi...

0
0
Tunda la tikitimaji au kwa Kiingereza Watermelons lina faida nyingi mwilini na hutibu baadhi ya maradhi.

Tikitimaji pia ni chanzo kikuu cha protini, mafuta, nyuzinyuzi, wanga, calcium, phosphorus, chuma,vitamin A, B6, C. potasium, magnesium, carotene, anthocyanins na virutubisho vingine vingi katika mwili.

Tunda hili linasaidia mtu kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa hatari ya kupata shinikizo la damu.

Tiba au faida 13 za tikitimaji kiafya ni nyingi, asilimia 92 ya tunda hili ni maji, hivyo mtu akila anaongeza maji mwilini, lina vitamini A ndani yake, huboresha afya ya macho, kuna vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili, husaidia kuponya majeraha, hukinga uharibifu wa seli na huboresha afya ya meno na fizi.

Faida nyingine ya tunda hili ni kwamba lina vitamini B6 ambayo  husaidia ubongo kufanya kazi vema, hubadilisha protini kuwa nishati na ni chanzo cha madini ya potasiamu pia husaidia kushusha na kuponya  shinikizo la damu, hurahisisha mtiririko wa damu mwilini, huondoa sumu mwilini, huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake.



Usikose kula tunda hili kila wiki utaona faida yake.

NAY ataja tofauti ya Diamond na Alikiba

0
0

Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa katika wanamuziki watatu wakubwa Tanzania wazuri kwake yeye Alikiba atakuwa namba moja ila katika wanamuziki wakubwa watatu wafanyabiashara basi Diamond Platnumz atakuwa namba moja.


Nay ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi', amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EATV na kusema siku zote yeye amekuwa akimkubali sana Alikiba ingawa anatambua wazi mtaani kuna tetesi kuwa hawezi kufanya naye kazi kutokana na yeye kuwa na uswahiba na Diamond Platnumz.


"Watu wanajenga picha kuwa mimi na Alikiba siwezi kufanya naye kazi sababu tu ya uswahiba wangu na Diamond ni kweli Alikiba si mshikaji wangu lakini leo hii ukiuliza nikutajie wanamuziki watatu wazuri Tanzania wa kwanza nitamtaja Alikiba, lakini pia ukisema nitaje wasanii watatu wakubwa wafanyabiashara basi nitamtaja Diamond Platnumz" alisema Nay wa Mitego.

MTU mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na askari wa wanyamapori Sumbawanga

0
0

Mtu mmoja amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa mguu wa kulia na askari wa wanyamapori wa pori la Akiba la Uwanda kwa madai kuwa alikatisha kwenye hifadhi kinyume cha sheria.

Akizungumza na Channel ten majeruhi huyo, Salaganda Chela amesema ilikuwa jana saa tano asubuhi katika kijiji cha Legeza Kata ya Kipeta wilaya ya Sumbawanga alipigwa risasi katika nyumba ya jirani akinamama wakishuhudia.

Ndugu wa majeruhi wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro baina ya hifadhi ya Uwanda na vijiji vinavyoizunguka hifadhi hiyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema tayari askari anayetuhumiwa kumpiga risasi mwananchi amekamatwa na kumtaja kwa jina la Lemomo Miseyeke mfanyakazi wa hiafdhi ya Uwanda.

HIKI ndicho kilichovunja ndoa ya Mkwasa na TFF

0
0

TFF limesema, kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Charles Boniface Mkwassa “Master” ni makubaliano ya kimkataba kwa pande zote mbili na hakukuwa na tofauti zozote ziliyojitokeza.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, wanatarajia kumalizana kabisa na Mkwasa mpaka ifikapo mwezi wa Machi mwaka huu ikiwemo fidia za kukatisha mkataba.

Alfred amesema, wataendelea kufuata program aliyoiacha Mkwasa huku wakitumia pia programu ya Kocha Salum Mayanga ambaye atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

Mkwasa alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambaye alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi wa Machi, mwaka huu ambapo kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitaanza mapema mwaka huu.

WAZIRI Mkuu Afuta Posho zote kwa Watumishi wa Umma Nchini

0
0
Serikali ya awamu ya tano imeendeleza desturi yake ya kubana matumizi, ambapo leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefuta rasmi posho zote za watumishi wa Umma na kuelekeza posho hizo kufanyiwa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri husika nchini.
Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo 3 Januari 2017, katika ziara yake iliyofanyika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akieleza jambo hilo amebainisha:“Kuanzia Januari hii mtu asipewe posho ya aina yoyote ile, nafuta posho zote ziende katika miradi ya maendeleo,”amesema Majaliwa.
Aidha, Waziri Majaliwa ameagiza Halmashauri zote nchini kusimamia fedha za miradi ya maendeleo za madiwani.

“Sasa hivi madiwani hakuna kupewa fedha za miradi ya maendeleo mkononi, bali wawasilishe vipaumbele vya miradi yao ili halmashauri husika isimamie malipo yake kwa ajili ya kuepuka migogoro,”amesema.
Pia, Majaliwa amezipiga marufuku kampuni za watumishi wa umma kufanya kazi katika halmashauri wanazofanyia kazi.

“Madiwani kama mna kampuni haziruhusiwi kufanya kazi katika halmashauri walizopo ili kuondoa upatikanaji wa dhabuni za upendeleo kitendo kinachoshusha ufanisi wa kazi,”amesema.
Amezitaka halmashauri zote nchini kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya kodi na yasiyo ya kodi.
”Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kwa halmashauri zote nchini kulingana na bajeti itakavyo ruhusu, tunataka halmashauri zitekeleze miradi yake ipasavyo,”amesema.

Amesema kwa sasa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam zinateketeza fedha nyingi kwa ajili ya posho badala ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo Halmashauri za wilaya ya Temeke na Kigamboni zinatumia laki 5 kila mwezi kwa ajili ya posho za kuchochea maendeleo ya madiwani
wakati Ubungo ikitumia milioni 55 ambayo ni sawa na zaidi ya milioni 600 pamoja na posho za vitafunwa milioni 300 kwa mwaka huku Kinondoni ikitumia milioni 780 kwa ajili ya posho ya maendeleo na milioni 390 kwa ajili ya posho ya bites kila mwaka.

JF

MAGUFULI Awashangaa Kagera: UKIMWI nyie, Tetemeko Nyie, Mna mto Unaitwa Ngono na Kijiji cha Katerero

0
0
Magufuli amesema Kagera haipaswi kuwa ya matatizo bali ya mfano na kutolea mfano majanga yaliyotokea Kagera ya Ukimwi na tetemeko.

Pia akawaambia anajua wana kijiji kinaitwa Katerero na mto unaitwa Ngono.

Msikilize:


MWANAMUZIKI Darassa Afunguka "Diamond Hapaswi Kujiita Simba"

0
0
Msanii wa bongo fleva Darasa ameweka wazi ule mstari wake wa "sio simba, sio chui, sio mamba" kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.

Akipiga story kupitia eNewz Darasa amesema Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.

"Ningekuwa Diamond nisingejiita simba, ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana". Amesema Darassa


Darassa amemalizia kwa kusema wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na anajiamini kwa muziki wake anaofanya.

"Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah". Amemalizia Darassa

AINA 10 za Wanawake Zitakazofanya Maisha yako Kuwa Magumu

0
0
Katika kuangalia tabia za wanawake, nakuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

2. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

3. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

4. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

5. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

6. Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

7. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

8. Asie na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

9. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

10. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

POLISI kufukua kaburi la binti aliyezikwa kwa siri Arusha

0
0

Familia moja  jijini Arusha inadaiwa kumzika kwa siri mtoto wao mdogo wa kike wa miaka mitatu katika kaburi lililofichwa, huku majirani wakidanganywa kuwa binti huyo yupo hai.


Taarifa za kisa hicho cha kusikitisha zimevifikia vyombo vya usalama. Kwa sasa kuna mipango ya kuhakikisha kuwa mwili wa binti huyo, Nuru Losipha aliyezikwa kwa siri na familia yake, unafukuliwa kwa uchunguzi zaidi.


Inadaiwa kuwa Losipha alipoteza maisha wakati akifanyiwa tohara au ukeketaji na ngariba, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, huku familia yake ikishuhudia.


Kitendo hicho kilifanyika katika kijiji cha Engutoto Kata ya Mwandeti wilayani Arumeru Desemba 28, mwaka jana, zikiwa zimebaki takriban siku tatu tu, kabla ya mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka mitatu tu, hajaingia mwaka mpya wa 2017.


Mtendaji wa Kata ya Mwandeti, Njivaini Kivuyo awali alikuwa amepitwa na taarifa hizo hadi vyombo vya habari vilipotinga kijijini hapo kwa uchunguzi na ndipo alipolazimika kwenda kuripoti tukio hilo kwenye kituo cha Polisi cha Ngaramtoni.


Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo aliapa kuwa liwalo na liwe na kwamba ikiwezekana kaburi litafukuliwa ili mwili wa malaika huyo asiye na hatia, uchunguzwe upya.


“Ndio kwanza nazipata hizi taarifa, na kama polisi tutaomba kibali cha mahakama ili twende kulifukua kaburi husika tujiridhishe kama kweli mtoto huyo amezikwa humo na iwapo tutaukuta huo mwili, basi tutaanza uchunguzi juu ya kifo chake,” alisema Kamanda arles Mkumbo.


Baba wa marehemu, Losipha Kaiser anadai kuwa mtoto wake alifariki kutokana na ugonjwa wa baridi yabisi na kwamba aliugua kwa kipindi kirefu kabla ya kupoteza maisha Desemba 28, mwaka jana. Lakini madai yake hayo yanapingana na ripoti ya muuguzi katika duka la dawa lililopo kijiji cha jirani cha Kidali, anayeitwa Jane Andrew.


“Walimleta mtoto hapa walitaka nimsaidie tiba, lakini tayari huyo binti alikuwa amezimia na kutokwa na damu nyingi,”alidai.


Muuguzi huyo aliwahimiza wamkimbize mtoto hospitali, na hakufahamu nini kiliendelea hadi ripoti za kifo zilipomfikia.


Huku serikali ikipiga marufuku vitendo vya ukeketaji kwa wasichana, bado kuna familia nyingi kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa, zinaendeleza mila hiyo kwa siri.


Kwa sasa familia hizo zimegundua mbinu mpya ya kuwatahiri watoto wa kike wakiwa wadogo sana, kuepuka kukamatwa.


Ngariba wanaotumika kukeketa watoto, mara nyingi ni akina mama vikongwe wasiokuwa na ujuzi, taaluma za afya na hutumia vifaa butu, ambazo husababisha uvujaji mwingi wa damu na kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa mengine.

FARID Mussa Aliyechukuliwa na Timu nchini Hispania Anatupa Kinachoendelea

0
0


Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Farid Musa amepost ujumbe kwenye account yake ya Insagram (farid_mussa17) akieleza hali ilivyo baada ya kuwasili kwenye klabu yake mpya ya Tenerife ya Hispania.

Farid aliondoka Bongo usiku wa December 28 kuanza safari ya kuelekea Hispania kujiunga na Tenerife baada ya kusubiri kwa muda mrefu kibali cha kufanya kazi nchini huko ambacho mchakato wake ulichukua muda mrefu hadi kukamilika.

“Thanks God nimeanza mazoezi leo na timu yangu mpya wameshanifanyia medical test ninachosubiri sasa ni leseni kutoka chama chao cha mpira cha Spain.”

“Nimeanza maoezi na timu ya U-23 kwa sababu wanajaribu kunifundisha mfumo wanaoutumia kucheza mechi mbalimbali za U-23 huku nikisubiri leseni yangu, kikubwa kwangu namuomba Mungu aendelee kunipa moyo wa subra nina imani kila kitu kitakuwa sawa.”

ZITTO Kabwe Adai Kuna Uhaba Mkubwa wa Chakula Nchini.........Waziri wa Kilimo Ampinga

0
0

Wakati Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akidai kuwa hali ya chakula nchini siyo nzuri kutokana na uhifadhi mbaya, Serikali imesema hali ni shwari licha ya baadhi ya maeneo kutopata mvua za wastani. 


Zitto alidai jana kuwa Ghala la Taifa la Chakula (SGR) lina hifadhi ya chakula kinachotosha kwa siku nane tu wakati Novemba 2015 kulikuwa na chakula cha kutosha miezi miwili. 


Kwa mujibu wa Zitto, taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Novemba inaonyesha kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula (NFRA), imebaki na tani 90,476 tu za chakula ambacho amedai ni cha kutosholeza siku nane.


 Hata hivyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alijibu madai hayo ya Zitto akisema nchi ina chakula cha kutosha wala siyo cha siku nane wala mwezi pekee, bali zaidi. 

Dk Tizeba alisema NFRA inakuwa na akiba ndogo kwa kuwa mwaka 2016 ndiyo ambao nchi ilipata mavuno makubwa ya tani milioni 16 ambazo hazikuwahi kutokea, hivyo maghala ya watu bado yana akiba kubwa ya chakula hivyo wakala haukununua chakula kingi. 


“NFRA inanunua chakula kwa kuangalia mahitaji kwa mwaka huo ukoje, watu wakivuna sana maghala yao yanakuwa yamejaa na mahitaji ya chakula yanakuwa madogo ndiyo maana Serikali hainunui chakula kingi. Miaka miwili iliyopita Serikali ilinunua mahindi kwa wingi lakini yaliishia kuharibika,” alisema Dk Tizeba. 


Aliongeza kuwa Serikali sasa ina mradi wa kujenga ghala jingine lenye uwezo wa kuhifadhi tani 260,000 ili likiungana na la sasa lenye uwezo wa tani 246,000 nchi iwe na uwezo wa kuhifadhi tani zaidi ya 500,000. 


“Kuna maeneo mahindi yameanza kukomaa na wakulima wa huko watavuna kama kawaida, tunachokifanya tutadhibiti uuzaji wa chakula nje ya nchi bila vibali ili chakula kisambae zaidi kwa Watanzania. Japo siwezi kutaja kiasi cha chakula kilichopo kwa sababu za kiusalama, ila kinatosha siyo kwa siku nane wala mwezi mmoja bali ni zaidi,” alisema Tizeba. 


Juzi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za udiwani katika kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, Zitto alisema kauli ya Rais John Magufuli kwa wananachi wa Mkoa wa Kagera kwamba Serikali haina shamba ni kuficha uamuzi unaosababisha kukosekana kwa akiba ya chakula ya kutosha. 


Alidai kuwa hali ya chakula nchini si nzuri, wananchi wanashuhudia namna bei za vyakula zinavyopanda kila siku akidai kuwa bei ya sembe na mchele zimekuwa juu na gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.


 “Hali ya chakula inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya maamuzi mabovu ya Serikali kuhusu hifadhi ya chakula. Serikali zote zilizopita huko nyuma zilikuwa zinanunua chakula cha akiba ili wakati wa ukame kama sasa chakula hicho kiingie sokoni, hivyo kushusha bei na kuwezesha wananchi kumudu gharama za chakula,”alisema Zitto. 


Aliongeza kuwa mpaka sasa NFRA ina tani 90,476 za chakula wakati kipindi kama hicho mwaka 2015 ghala la chakula lilikuwa na tani 459,561. 


Takwimu alizozitoa Zitto Kabwe alizinukuu katika ripoti ya BoT ya Novemba mwaka jana ambayo inaonyesha kuwa tangu Januari 2016 hadi Julai 2016, akiba ya chakula ilipungua kutoka tani 125,668 hadi 49,632, lakini hadi Oktoba mwaka huo iliongezeka hadi 90,476. 


Ripoti hiyo inaonyesha tofauti ya uhifadhi wa chakula kwa mwaka jana na miaka mingine miwili iliyotangulia kwani mwaka 2014 Januari, kulikuwa na tani 235,309 na Desemba, tani 466,583 huku mwaka mwaka 2015 Januari kukiwa na tani 459,561 na Desemba 180,746. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), Steven Ruvuga alisema hali halisi kwa wakulima siyo nzuri kwa kuwa mvua zilinyesha chini ya kiwango, hivyo kuna hofu ya ukosefu wa chakula cha kutosha baadaye. 


“Sasa hivi nipo Kiteto na kwa kawaida mahindi yalipaswa kuwa tayari yameinuka kufikia walau mabega ya mtu mzima, lakini nikiyatizama sasa bado yako chini. 


"Mwaka huu kuna hatari ya ukosefu wa chakula na naishukuru Serikali kwa kuwa imeanza kuchukua hatua katika maeneo yenye uhitaji,” alisema Ruvuga. 


Aliongeza kuwa Ghala la Taifa linapaswa kuwa na wastani wa tani 300,000 za akiba lakini kama sasa zipo 90,476 zinaweza zisikidhi mahitaji ya kila mtu hivyo ni vyema ikabuni mpango mbadala
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images