Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Amuua mkewe kwa nyundo Kisa Wivu wa Mapenzi

$
0
0
Mwanamke mmoja mkazi wa Mikumi wilayani Keya, Mbeya aliyefahamika kwa jina la HILDA SIGARA  amefariki dunia akiwa anapelekwa Hospitali kwa matibabu baada ya kupigwa nyundo kichwani na mume wake aitwaye REBSON TWEVE umri kati ya miaka 30 – 35

Kamanda wa polisi mkoani humo DCP Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.01.2017 majira ya saa 12:00 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani inasadikiwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Amesema katika eneo la tukio kumekutwa nyundo moja, kisu kimoja na fimbo ya muanzi ambavyo vinasadikiwa kutumika katika tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Kyela ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na upelelezi unaendelea huku mtuhumiwa akiwa ametoroka mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Aidha, katika matukio mengine kamanda huyo amesema kuwa jeshi la polisi limepokea taarifa za kujinyonga kwa watu wawili ambao miili yao imekutwa ndani ya nyumba zao katika maeneo tofauti.

Watu hao ni pamoja EDWARD PETER  mfanyabiashara na Mkazi wa Majengo na aliyekutwa amekufa chumbani kwake huku mwili wake ukiwa hauna majeraha yoyote, na mwingine ni ROBERT MWAISENYE Mkazi wa Mbugani wilayani Chunya ambaye alikuwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila akiwa ndani ya nyumba yake.

TEMBELEA Blog ya Tiba za Asili Kwa Maswala ya Tiba Asilia, Kusomewa Dua na Visomo, Kusafisha Nyota na Kumvuta Mpenzi

$
0
0
Tembelea  tovuti  pendwa  ya ASILI ZETU inayohusiana na masuala ya tiba asilia, kusomewa dua na visomo, kusafisha nyota,  kumvuta mume au mpenzi aliyekuacha, tiba ya magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana,  mvuto wa biashara.

Pia tunatoa dawa za uzazi kwa wale kina mama wenye matatizo ya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote, kupandishwa cheo kazini, mali isiyohuzika kama vile kiwanja, shamba, nyumba, gari n,k.  Ingia HAPA

Jinsi Mfumo wa Kieletroniki wa Malipo ya Faini za Barabarani Unavyofanya Kazi

$
0
0
Mfumo wa ulipaji faini za papo kwa hapo kielekitroniki unafanyakazi kama ifuatavyo:

Dereva aliyetenda kosa akikamatwa na kutakiwa kulipa faini kwa njia ya kielektroniki, askari ataingiza kwenye mashine taarifa za namba ya usajili wa gari, nambari ya leseni ya dereva, eneo kosa lilipofanyika, kosa lililofanyika na kisha askari atatoa tiketi ya kielektroniki kumpa dereva aliyetenda kosa.

Tiketi hiyo pamoja na kuwa na namba ya kumbukumbu ya malipo pia itakuwa na maelekezo kwa dereva yanayosema: Unatakiwa kulipa faini ya kosa ulilotenda kupitia mitandao ya simu ya tigo pesa, M-pesa, Airtel Money, Maxi malipo au kupitia kadi yako ya benki (ATM Card za NMB na UMOJA SWITCH).

Unatakiwa kulipa faini yako ndani ya siku saba. Baada ya siku saba utatozwa ziada ya 25%, baada ya siku kumi na nne na kuendelea utatozwa ziada ya 50% ya tozo la awali na itakuwa ikiongezeka kadiri unavyochelewa kulipa. Kwa wale watakaokamatwa wakati wa oparesheni watafikishwa mahakamani ambapo mbali na kulipa malimbikizo ya tozo watatozwa faini ya TZS 50,000/= au kifungo cha miezi miwili jela.

Ili kulipia kwa njia ya mitandao ya simu namba maalum ya Polisi (USSD Code) itakayotumika ni *152*75#. Namba hii pamoja na kutumika katika kulipia tozo pia unaweza kuangalia iwapo gari lako linadaiwa tozo la notification lililolimbikizwa.

Baada ya kutolewa tiketi hiyo dereva husika atatakiwa kulipa faini yake kwa njia hizo zilizotajwa kisha kuiwasiliha kwa askari mwenye mashine namba ya kumbukumbu ya malipo aliyoipata kupitia mtandao husika. Namba hiyo ya kumbukumbu itaingizwa kwenye mashine ya kutolea tiketi ambapo itatolewa risiti ya malipo kisha kukabidhiwa kwa dereva husika.

Ieleweke kwamba, ulipaji huu wa tozo kielektroniki hauna tofauti na ule unaotumika katika kulipia umeme wa LUKU au ada za Magari zinazotozwa kwa njia ya mtandao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ili kurahisisha zoezi hili la ulipaji faini kwa njia ya kielektroniki, madereva watatakiwa kutembea na leseni zao halisi za udereva vinginevyo watalazimika kupelekwa vituoni kwa ajili ya kupata taarifa zao za leseni kutoka katika computer za mfumo wa leseni za udereva jambo ambalo linaweza kuwapotezea muda.

Aidha ieleweke kwamba dereva anapoandikiwa faini ya kielekroniki akichelewa kulipa katika muda aliopewa, Jeshi la Polisi litakuwa likiendesha oparesheni mara kwa mara kwa kuyamulika magari yote yanayodaiwa faini kwa kutumia mtambo maalum wa kutambua namba za usajili wa magari yanayodaiwa (Automatic Number Plate Recognition System). Watakaokamatwa katika oparesheni hizi kwa kukwepa kulipa faini, mbali na kutakiwa kulipa faini aliyolimbikiza awali pia atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sharia.

ENDESHA SALAMA – OKOA MAISHA.
Imetolewa na:

MOHAMMED R.MPINGA – DCP,
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)

“Gigy Money Hawezi Kuwa na Rafiki Kama Mimi, Atajivunia Sana” – Amber Lulu

$
0
0
‘Video qeen’ kutoka Bongo ambaye naye amejitosa kwenye uimbaji wa Bongo Fleva, Amber Lulu amemshambulia mwenza ambaye pia ni video qeen, Gigy Money, na kusema hata siku moja hawezi kuwa na urafiki na mtu kama huyo.

Amber ametoa mashushu hayo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo amesema licha ya kufanya kazi zinazofanana, hawezi kuwa na ushkaji naye na ikitokea hivo atajivunia sana.

“Gigy Money hawezi kuwa na mwana kama mimi, atajivunia sana, hawezi kuwa mshkaji wangu, sina mahusiano naye wala sina beef naye, hawezi kuwa kwenye cycle yangu”

Msikilize mwenye hapa akifanya mahojiano na Jay R Junior.

Freeman Mbowe: Kauli za Rais Magufuli Kagera Hatari

$
0
0
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani (CHADEMA), ameikosoa hotuba aloitoa Rais Magufuli Mkoani Kagera kwa kusema " Hivi mtu ambae amefiwa, nyumba imebomelewa, hana chakula, hana pesa unakwenda kutoa kauli za kibabe kwamba hutowapa chakula kwakuwa serikali haina shamba! hivyo sio sawasawa"

Helmeti Zatajwa Kuwa Chanzo cha Maradhi ya Ngozi

$
0
0
Wakati Sheria ya Usalama Barabarani inamtaka kila dereva wa bodaboda kuwa na kofia ngumu (helmeti) mbili kwa ajili yake na abiria, watumiaji wa vyombo hivyo wapo hatarini kuambukizwa maradhi ya ngozi.

Hatari hiyo inatokana na matumizi ya helmeti chafu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe alisema watumiaji wa usafiri huo wamekuwa wakitumia helmeti moja bila kujali kama imefanyiwa usafi, huku wengine wakilazimika kuvaa zilizo chafu ili kutekeleza matakwa ya sheria.

Nay wa Mitego: MR T Touch bado ni producer mzuri lakini…

$
0
0

Nay wa Mitego na producer aliyemtambulisha kwenye game, Mr T Touch walikuwa na chemistry ya aina yake na walifanikiwa kutengeneza hits nyingi.

Baada ya kufanya kazi kwa muda katika studio za Free Nation za Nay, Touch aliamua kujiengua na kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe. Huko bado anaendelea kufanya vizuri. Pamoja na kwamba hawafanyi tena kazi pamoja, Nay anakiri kuwa Touch bado ni producer mzuri.

“Ni producer mzuri, nimefanya naye kazi kwa muda mrefu so sidhani kama kutakuwa na kitu kipya cha ajabu toka kwake,” Nay alimuambia mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove.

Hata hivyo Nay anadai tangu aondoke Free Nation bado hajasikiliza ngoma mpya za producer huyo.

Kamanda Mpinga Akanusha Trafiki Kulipwa Bonasi Kwa Kukamata Magari

$
0
0
Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imesema hakuna polisi yeyote wa kikosi hicho anayelipwa bonasi kutokana na ukamataji na ulipaji wa faini zinazotokana na makosa ya usalama barabarani.

Taarifa zinazosambaa kwa watu mbalimbali na katika mitandao ya kijamii, zinadai kuwa trafiki kwa kila kosa analokamata na kutoza faini katika kila sh 30,000, analipwa Sh 5,000 kama bonasi.

Ufafanuzi juu ya suala hilo ulitolewa Jumatano hii na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga wakati akizungumza na Habarileo ofisini kwake. Alisema hakuna ukweli kwamba askari hao wanapata asilimia fulani kutokana na makosa wanayokamata, bali wamepewa maelekezo ya kukamata makosa mengi kadri wanavyoweza.

“Nafikiri hii inatokana na kukamata makosa mengi, lakini niseme hakuna askari anayelipwa bonasi, wanachokifanya ni kukamata kulingana na makosa tu,” alisema Kamanda Mpinga.

Aidha, alisema zipo taarifa kuwa askari hao wamepangiwa idadi ya makosa, jambo alisema si kweli ila wamepewa maelekezo ya kukamata makosa mengi kadri inavyowezekana, ikiwa ni kwa lengo la kudhibiti ajali.

Marekani Yaanza kula Sambamba na Mtoto wa Osama Bin Laden

$
0
0

Marekani imemtangaza Hamza mtoto wa Osama ktk orodha ya Magaidi. Azuiwa kufanya biashara na wamarekani na mali zake kutaifishwa.

Aidha kiongozi mkuu wa usalama wa kundi la Al Qaeda, Ibrahim al-Banna ametajwa katika orodha hiyo pia. Marekani itatoa ofa ya dola Million tano kwa atakayesadia kukamatwa kwa al-Banna.

Meek Mill Amchana Nicki Minaj Baada ya Kumwagana

$
0
0
Muda mfupi baada ya Nicki Minaj kutangaza kupitia Twitter kuwa ameachana na Meek Mill, rapper huyo amemchana demu wake huyo wa zamani kwenye Instagram.


Alhamis hii, Meek aliweka picha Instagram ya viatu vyeupe brand ya Giuseppe Zanotti zenye mistari ya dhahabu na kuandika, “If you walk out don’t wear these, they wack.”



Viatu alivyoviponda Meek ni vile ambalo Nicki Minaj alivivaa kwenye video ya wimbo wa mwaka 2013 alioshirikishwa na Ciara, I’m Out.

Wimbo huo una mashairi ya Minaj yanayosema, “You gon’ play me? / On Instagram, ni**as trying to shade me / But your bitch at home trying to play me.”

Aunty Ezekiel katuachia funzo juu ya mapenzi

$
0
0
Moja kati ya matatizo ya watanzania, ni kushindwa kusimamia yale tunayoayaamini. Linapokuja suala la mapenzi wengi hujikuta kwenye wakati mgumu hasa ikiwa yule anayempenda anaonekana si wa maana mbele za watu kwa hadhi,kipato na muonekano.

Pengine mwaka 2016 mwanadada Aunty Ezekiel alituachia funzo,ukipenda usiangalie wengine wanaonaje fuata moyo wako na wasipooelewa wengine wataelewa mwisho wa safari.

Miaka michache nyuma ilisemekana mmoja kati ya warembo A-list wa bongo movie Aunty Ezekiel amebeba mimba ya dansa wa kutegemewa wa Diamond Platinumz, Mose Iyobo, haikuaminika na wengi wetu. Sio kwa kuwa Iyobo hatakiwi kupendwa, lahasha ila kwa kuWa imezoeleka mastaa hasa wa bongo movie kudate na watu wenye kipato kikubwa pengine na umaarufu mkubwa. Wengi waliamini Iyobo ni kama amewekwa kupoteza maboya ili watu wasimjue muhusika haswa wa mimba ya Aunty!

Miaka imepita Mose na Aunty wana mtoto wa kike anaitwa Cookie! Unajua nini? Ukipitia kwenye mitandao ya kijamii moja kati ya couple ambaye sasa zinazopostiwa sana ni Mose na Aunty,watu wanawatamani,watu wanaona wanapendezana.



Ingekua Aunty amewasikiliza pengine kusingekuwa na uhusiano. Ingekuwa amemuona kwa jicho wanalomuona wengine pengine penzi lingekufa siku nyingi. Lakini kwa kuwa alimua kuufuata moyo wake na kuamini kuwa yule ambaye wengine wanamuona sio sahihi kwake ndiye haswaa anastahili kukabidhiwa mtima wake,ndio sababu wapo walipo.

Kwa yoyote anayehusika, mapenzi ni baina ya nafsi mbili zinazopendana,ni vema kusikiliza ushauri na kuufanyia kazi lakini maaumizi yabaki ya kwako. Mwisho wa siku wewe ndo unajua sababu ya kumpenda uliyenaye. Haijalishi wanasemaje au wanaonaje juu ya uhusiano wako Shika uliposhikilia kama kuelewa,wataelewa mbele wa safari.

Imeandikwa na Eliezer Gibson aka Green City Native

Kinana Arusha Kombora Zito Kwa Maalim Seif na CUF

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amerusha kombora zito kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, huku akimwita mgombea wa urais wa kudumu aliyekata tamaa.

Pamoja na hayo, Kinana amewataka Wazanzibari kuachana na maneno ya mitaani kwani Uchaguzi Mkuu ulishamalizika na Dk. Ali Mohamed Shein ameshaapishwa kuwa rais kwa mujibu wa sheria.

Kauli hiyo aliitoa jana katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Dimani zilizofanyika Maungani, nje kidogo ya mji wa Unguja.

Alisema CCM itaendelea kuchaguliwa na wananchi kwa sababu inatimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi, kutimiza matakwa na sera kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Kinana alishangazwa na CUF kushindwa kutanua wigo wa demokrasia ndani ya chama hicho na kuendelea kumshikilia mgombea urais mmoja wa kudumu kwa zaidi ya miongo minne.

“Kuna mgombea mmoja hapa Zanzibar ameanza kugombea urais tokea akiwa na miaka 30 na sasa ana miaka 80, toka akiwa bado kijana mbichi, sasa amekuwa kikongwe na kupinda mgongo ila bado ana tamaa ya kuwania urais.

“Demokrasia ndani ya chama chetu ni ya aina yake na kwamba kukubalika kwetu mbele ya wananchi kunatokana na misimamo yetu inayotetea masilahi ya umma. Hata demokrasia yetu ndani ya CCM kamwe haifanani na vyama vingine,” alisema Kinana huku akishangiliwa.

Kinana alisema CCM ina umoja imara na katu hazuiwi mwanachama kuwania nafasi ya uongozi na haina sifa ya kuwa na wagombea wa kudumu kama ilivyo CUF ambayo tangu ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hadi sasa, Katibu Mkuu wake Maalim Seif amekuwa mgombea wa kudumu.

Alisema ushiriki wa wana CCM 25 ndani ya chama kuwania nafasi ya uteuzi wa ubunge Jimbo la Dimani ni kielelezo tosha cha kuimarika kwa demkorasi, na mgombea aliyepatikana anaungwa mkono na wanachama wote.

Alieleza kuwa vikao vya CCM vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC) vilikutana na kupitisha jina la mgombea aliyeshinda kura za maoni, huku CUF ikiwa kimya, ikishindwa hata kufanya vikao vyake kwa mujibu wa katiba ya chama chao.

Akizumgumzia kupwaya kwa dhana na misingi ya demokrasia ndani ya CUF, Kinana alisema hivi sasa chama hicho kina wenyeviti watatu, ambao mmoja ni wa muda, mwingine wa mpito na aliyebaki ni wa zamani

Aidha Kinana aliwashangaa wanachama wa CUF ambao wanakubali kudanganywa kirahisi kila siku na kuaminishwa ipo siku mgombea wao wa urais aliyeshindwa uchaguzi atatangazwa na Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Rais wa Zanzibar.

“Tuliambiwa hapa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utafutwa, watakuja watu toka UN, mara tukaelezwa wangekuja   Jumuiya ya Ulaya, wakaambiwa washone nguo mpya kusherehekea ushindi, huku siku zikitaradadi hakuna kinachotokea,” alisema.

Kinana alisema viongozi wa CUF hawana uwezo wowote wa kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo kwani walibahatika kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, lakini bado hakuna walichofanya.

“Kama ni mkate CUF walipata nusu na CCM nusu, wakashika wizara makini za Biashara na Viwanda, Katiba na Sheria, Habari na Utamaduni, Mawasiliano na Miundombinu, lakini kutokana na wao kuwa dhaifu, hawakumudu hata kujenga kiwanda kidogo,” alisema.

Kinana aliwaomba wananchi wa Dimani kumchagua mgombea ubunge wa CCM, Juma Ali Juma kwa sababu ni makini, mchapakazi na mwepesi wa kuwatumikia wananchi.

Akihutubia katika mkutamo huo wa uzinduzi wa kampeni, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Idd, aliwaeleza wananchi wa Dimani kuwa si sifa ya wagombea wa CUF kuwatumikia wananchi na mfano mzuri ni katika majimbo ya Pemba.

Wafugaji 50 Wala Kinyesi, Damu na Mkojo Kunusuru Maisha Yao

$
0
0
Watu 50 wakiwa na watoto wadogo wamenusurika kufa, baada ya kupotea ndani ya Pori la Akiba la Selous kwa siku saba; huku wakikosa chakula na maji na kulazimika kula kinyesi cha ng’ombe, damu na mikojo ya binadamu.

Watu hao ambao ni wafugaji, walikuwa wakihama na mifugo yao inayokadiriwa kufikia 1,780 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, yakiwemo Chumvi na Muhoro waliekea Morogoro, ambako walidai ndiko yalipo makazi yao.

Tukio hilo ambalo si la kawaida kutokea katika pori hilo, lilianzia Jumatano iliyopita wakati wafugaji hao, walipoanza safari ya kuelekea Malinyi mkoani Morogoro, wakiongozwa na mwenyeji wao, waliyemtaja kwa jina la Mzee Mzigua, ambaye hata hivyo wanadai aliwalaghai na kuwatelekeza.

Wafugaji hao walisema walitembea kwa siku tano ndani ya pori hilo, wakitarajia kufika Malinyi, yaliko makazi yao. Lakini hali ilikuwa tofauti, baada ya mwenyeji wao huyo, kuwalaghai kwa kuwapitisha njia sisizo sahihi.

Walisema waliishiwa chakula na maji ya akiba na mwisho walijikuta wanatokea ndani ya Pori la Akiba la Selous; huku hali zao zikiwa zimedhoofu kutokana na njaa na kiu cha maji. Wakiwa safarini, mwenyeji wao huyo, aliwataka kila mmoja alipe fedha ikiwa ni ujira wake kwa kuwaonyesha njia. Walidai kuwa walimlipa fedha nyingi.

Wengine walimlipa Sh milioni mbili, Sh milioni moja na wengine Sh 500,000, wakitarajia angewasaidia. Walitembea usiku na mchana ndani ya pori hilo, wakipishana na wanyama wakali kama simba na nyati, hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yao na watoto wao.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi, baada ya kutimia siku ya tano wakiwa ndani ya pori hilo, pale walipoishiwa chakula na maji, hivyo kuwalazimu kuanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu kwaajili ya kukata kiu. Pia walikula kinyesi chao ili kupunguza njaa. Yule mwenyeji wao aliwatelekeza baada ya kuona hali zao zimekuwa mbaya.

Alitokomea kusikojulikana, akiwaacha wasijue pa kwenda, hivyo kulazimika kutelekeza mifugo yao ili kunusuru kwanza maisha yao. Halikadhalika, wengine walilazimika kunywa mikojo yao na mingine kuwanywesha watoto wao kunusuru maisha yao, hali iliyowafanya kuathirika kiafya na kushindwa kuendelea na safari.

Wengine walianguka na kupoteza fahamu. “Sisi tulikuwa tunataka turudi nyumbani kwetu Morogoro. Huku tulikuja wakati wa operesheni ya Morogoro, huku tulikuja kununua ng’ombe lakini miji yetu ipo kule Morogoro. Tukaambatana na huyo mwenyeji wetu aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Mzigua na mtoto wake.Lakini tunajua mpaka nyumbani kwake”alisema Kiongozi wa msafara wa wafugaji hao, aliyejitambulisha kwa jina la Lisesi Cherahani Bela na kuendelea;

 “Zilitimia kama siku nne tukiwa hatujanywa maji, jua lilikuwa linawaka, tukaanza kuanguka, tukaanza kuchinja ng’ombe na kunywa damu, tulijaribisha kula kinyesi cha ng’ombe, tulikuwa tunakojoa mkojo tunanywesha hata watoto. Mimi nilikunywa mkojo lita moja, ikaniathiri hapa kifuani, kumbe mkojo ni kitu kibaya.”

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, kiongozi huyo alisema baada ya kuona hali inakuwa mbaya zaidi, alitafuta eneo ambalo lina mtandao wa simu na kufanya mawasiliano na watu mbalimbali, ambapo alifanikiwa kuwasiliana na watu wa Kigoma na kuomba msaada wao.

Alisema kuwa watu hao, waliwasiliana na wahifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kuwasiliana na wahifadhi wa Pori hilo la Selous, ambao walianza kazi ya kuwasaka na hatimaye kuwakuta katika eneo la Mlima Luhombelo, lililopo katikati ya Pori hilo wakiwa tayari wameshadhoofika kiafya.

Askari hao wa wanyamapori wa Pori hilo, waliwapatia uji na maji na kuwapa huduma ya kwanza wale wengine ambao walikuwa na hali mbaya.

Baada ya taarifa hizo za kupotea kwa wafugaji hao, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gaudence Milanzi alifika katika eneo hilo juzi, akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Martin Leibooki, Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock Msocha na maofisa wengine wa wizara na pori hilo.

Milanzi alisema Serikali inaangalia namna ya kuwasaidia wafugaji hao, kurejea katika hali zao kiafya pamoja na kuwasaidia kutafuta mifugo yao ili waweze kurejea katika makazi yao na kuendelea na shughuli zao.

“Kwa upande wa Serikali kama Wizara hatuchukulii kama hawa wameingia kwenye hifadhi hapana, muhimu kwanza ni kuokoa maisha ya binadamu, na hicho ndicho tunategemea kukifanya sasa hivi, na baada ya hapo kutakuwa na masuala ya kutafuta hiyo mifugo, kwa sababu wamepata hasara kubwa”alisema Katibu Mkuu huyo.

Aliutaka uongozi wa wilaya ya Rufiji, kutoa ushirikiano na wizara ili kuwabaini waliowadanganya wafugaji hao, kwa kuwaingiza kwenye pori hilo na kuwatapeli kiasi hicho kikubwa cha fedha.

“Hawa waliowadanganya na kupita huko ndani ya pori kwa kweli tutaendelea kuwatafuta na tutaomba tuwe na ushirikiano na uongozi wa Wilaya kwa sababu inaelekea kuna watu kazi yao ndo hiyo, ukiangalia pesa walizowapa ni nyingi sana, sasa watu wamechukua pesa zote na wamewaacha katika hali kama hii, wengine wana watoto wadogo, kwa hiyo tutahakikisha tunashirikiana kuwatafuta ili tukomeshe hili tatizo moja kwa moja”alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA na Mhifadhi Selous kwa juhudi za haraka walizochukua. Alisema wizara yake itaendelea kushirikiana na Mamlaka mbalimbali, kutoa misaada ya haraka, endapo yatatokea tena matukio ya aina hiyo.

Kwa upande wake, Leibooki alisema TAWA ambao ndiyo wamiliki wa hifadhi zote za wanyamapori nchini, haitawachukulia hatua za kisheria wafugaji hao, kwa kuwa waliingia ndani ya pori kwa kudanganywa na watu wenye nia mbaya.

Lakini, alisisitiza kuwa mamlaka yake, itawashughulikia kisheria wawindaji haramu na wafugaji wanaoingiza mifugo yao ndani ya hifadhi zilizo chini ya Mamlaka yake.

Pia alisema Mamlaka yake, inaendelea na utaratibu wa kushirikiana na wananchi waishio pembezeni mwa hifadhi zote, kwa kuwapa elimu ya ufugaji bora kwa kushirikiana na wizara zinazohusika na kuendeleza miradi ya maendeleo, ikiwemo miundombinu ya maji.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji chini (CCWT), Magembe Makoye aliwataka viongozi wa Halmashauri mbalimbali nchini, kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji mahali walipo, bila ya kuondoa watu wengine.

Alisema kuwa wao kama chama, wamesikitishwa na tukio la kuondolewa kwa wafugaji hao katika bonde hilo la Rufiji, kwa kuwaambia warudi walipotoka. Alisema tamko hilo lilitolewa na uongozi wa Halmashauri hiyo na ndilo lililosababisha matatizo hayo.

Makoye alisema kufanya hivyo, hakuondoi migogoro ya wafugaji na wakulima, badala yake ni kuendelea kuzalisha migogoro hiyo katika maeneo mengine, ambayo wafugaji watahamia.

“Tunalaani kweli vitendo hivi vya viongozi na watendaji wengine wa Halmashauri kuwafukuza wafugaji, tena wakati mwingine kwa kuwatisha na matokeo yake wananchi hawa 50 wangepoteza maisha, kama isingekuwa bahati ya mtu mmoja kuwa na simu kati yao” alisema Katibu Mkuu huyo.

“Kwa kweli kwa niaba ya wafugaji wote wa Tanzania naishukuru sana Wizara ya Maliasili kupitia kwa Katibu Mkuu, Gaudence Milanzi.” alisema Katibu huyo.

Alisema kuwa kungeweza kutokea majanga makubwa zaidi kwa kuwa kuwa wafugaji hao walikuwa wakisafiri na watoto wao wadogo katika mazingira hatarishi katikati ya pori hilo, ambalo lina wanyama wakali.

“Kwa kweli ni mazingira ya kusikitisha. Lakini niishukuru sana Serikali kwa maana ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wamefanya kazi yao kwa namna ambavyo mimi ninawiwa kuwashukuru. Tangu jana tumewasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara, leo watu wote wameweza kupatikana, kumefanyika doria ya ndege, doria za magari, doria kwa miguu, wamewatafuta hawa watu, wamewaokoa, wamewaleta kwenye huduma za afya, wamewapa chakula, wamewahifadhi, hawajawadhuru” alisema.

Aliiomba Serikali kuhakikisha tatizo la wafugaji nchini, linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu, kwani jamii haiwezi kuendelea kubaki na tatizo hilo kwa miaka yote. Alitaka wafugaji watafutiwe maeneo ya kudumu ya kufugia, ikiwa ni pamoja na kupimiwa maeneo yao, badala ya hali ilivyo sasa kuafukuza kila kukicha.

Baadhi ya Mzoga wa ngombe uliopatikana ndani ya Pori la Akiba la Selous,  Kanda ya Kaskazini Mashariki  Kingupira  baada ya Wafugaji 50  waliotelekezwa kwa muda wa  siku tano na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo na kisha kuwakimbia( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

Mmoja wa  wafugaji aliyepotea na  kutelekezwa ndani ya Pori la Akiba la Selous,  Bw. Lisesi Cherehani aliyekuwa na ng’ombe 180 na punda mmoja akiangalia mmoja wa ng'ombe wake aliyekufa kwa kukosa  maji ya kunywa kwa muda  wa siku tano kwenye Kanda ya Kaskazini Mashariki katika Pori la Akiba la Selous ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi (katikati) akipata taarifa kutoka kwa  Meneja wa Mradi wa Pori la Akiba la Selous    Bw. Enock Msocha (wa tatu kushoto)  mara baada ya  kuwasili kwa ajili ya kuwatembelea  Wafugaji 50 waliokolewa na Askari wanyamapori baada ya kutelekezwa  na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia ya mkato ndani ya Pori hilo na kisha kuwakimbia ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

Dogo Janja amefata walichokifanya AY, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee

$
0
0
Dogo janja ni msanii anayezidi  kufanya vizuri kwenye mziki wake tangu aliporudi upya amekuwa akionyesha utofauti mkubwa kwenye muziki wake kitu ambacho wasanii wengi wamekuwa wakimpongeza. Dogo janja ametumia ukurasa wake wa Instagram kutuonyesha muonekano wake mpya akiwa amevaa meno ya dhahabu kama walivyofanya, AY, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee.

VIDEO: Hemed PHD azungumzia kudaiwa kutumia dawa za kulevya

$
0
0
Baada ya hivi karibuni kusambaa kwa post kwenye mitandao ya kijamii ikitaja baadhi ya wasanii wa Bongo wanaotumia dawa za kulevya, miongoni mwa wasanii waliotajwa ni pamoja na Hemedy Suleiman.

AyoTV na millardayo.com imempata Hemedy Suleiman kuzugumzia madai hayo……‘Nilipoiona hiyo post nilicheka kwa sababu mimi naujua ukweli, ila nilimfikiria zaidi mama yangu mzazi akisikia hizo habari itakuaje, na kweli alinipigia huku amepanic lakini ukweli ni kwamba mimi si mtumiaji wa dawa za kulevya’

Lowassa Atajwa Kusababisha Deni la Milioni 1

$
0
0
Jina la waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa limetajwa na mkaazi mmoja wa Mbeya mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla kuwa sababu ya deni la shilingi milioni moja kutokana na mapenzi ya wafuasi wake.

Mkaazi huyo wa kata ya Ruanda Nzovwe aliyejitambulisha kwa jina la Amos Mwakyambiki alidai kuwa wafuasi wa Chadema waliharibu paa la nyumba yake walipopanda kwa lengo la kufuatilia mkutano wa Lowassa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, na kwamba chama hicho kilimuahidi kumlipa fidia ya shilingi milioni moja lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

Alimueleza mkuu wa mkoa huo kuwa kutokana na uharibifu huo mkubwa uliofanyika, wapangaji wake waliamua kuhama nyumba yake hivyo kukosa kipato.

“Naomba Serikali ya Mkoa inisaidie kuzungumza na meya (wa Chadema) ili niweze kulipwa stahiki zangu kwani sasa sijui hatma yangu. Kuku niliokuwa nauza kwa ajili ya kupata nauli kwenda ofisi za jiji wamekwisha,” Mkaazi huyo anakaririwa.

Kutokana na madai hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimuagiza Mkuu wa Wilaya kufuatilia suala hilo huku akitahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya nyumba zao wakati wa kampeni.

“Lakini na nyie wananchi msikubali nyumba zenu zibadilishwe kuwa viwanja vya siasa,” alisema Makalla.

Akizungumzia taarifa hizo, Mkuu wa Idara ya Habari ya Chadema, Tumaini Makele alisema kuwa chama hicho kitafuatilia kuona ni nani aliyetoa ahadi hiyo kwa mwananchi huyo na ilikuwa katika mazingira gani ili walifanyie kazi ipasavyo.

Jerry Muro aipigia magoti TFF

$
0
0

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ameomba msamaha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) asamehewa adhabu ya mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.

Julai mwaka jana, Muro alifungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. milioni 3 baada ya kukutwa na hatia katika mashtaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF dhidi yake.

Katika barua yake kwa TFF, Muro amesema kwamba anakiri kupata barua ya kufungiwa kutoka Kamati ya Maadili, lakini anaomba msamaha baada ya kutumikia nusu ya adhabu yake.

Muro ameomba apunguziwe adhabu na kurudi kutekeleza majukumu yake kwa mwajiri wake Yanga kuanzia kipindi hiki cha michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoendelea visiwani Zanzibar.

Mapema wiki iliyopita, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa mahasimu, Simba, Hajji Manara alimwombea msamaha Muro.
Aidha, wasemaji wa timu nyingine akiwemo Massau Bwire wa Ruvu Shooting walimwombea msamaha pia mwenzao huyo, wakiamini atakuwa amejirekebisha.

Muro alifungiwa Julai 8 mwaka jana baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde kilichofanyika mjini Dar es Salaam.

Makosa yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo.

Kwa kosa hilo akahukumiwa kutengana na masuala ya soka kwa mwaka mmoja wakati shtaka lingine lililomtia hatiani ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

Katika shtaka hilo, Jerry anadaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shtaka la kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya televisheni.

Mwigizaji mashuhuri India Om Puri, 66, afariki dunia

$
0
0
 Om Puri aliigiza katika filamu India, Uingereza na Marekani

Mwigizaji mashuhuri nchini India Om Puri, ambaye pia aliigiza kwenye filamu zilizovuma sana nchini Uingereza, amefariki dunia akiwa na miaka 66.

Om Puri aliigiza kwenye filamu ya ucheshi ya East is East nchini Uingereza ambayo ilisimulia kuhusu maisha ya mhamiaji kutoka Pakistan aliyekuwa akizoea maisha kaskazini mwa England.

Taarifa zinasema mwigizaji huyo alifariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake Mumbai mapema Ijumaa.

Om Puri alijulikana sana kwa ustadi na uigizaji wake katika filamu za Kihindi miaka ya 1980.

Aidha, aliigiza kwenye filamu za Kiingereza, zikiwemo Mahatma Gandhi ya Richard Attenborough.
Aliigiza pia katika filamu za Pakistan na Hollywood.

Mwaka 2004, alitunukiwa nishani ya staha ya OBE kwa mchango wake katika tasnia ya filamu Uingereza.

Puri, alizaliwa 1950 jimbo la Haryana, kaskazini mwa India.
 Om Puri akiwa na mwigizaji Helen Mirren katika The Hundred-Foot Journey

Filamu yake ya kwanza kuigiza ilikuwa ya Ghashiram Kotwal mwaka 1976.

Nchini India, anafahamika kwa filamu maarufu za Ardh Satya, Sadgati, Paar na filamu ya ucheshi ya Jaane Bhi Do Yaaro.

Majuzi, alizungumzia marufuku iliyotolewa na India kwa waigizaji wa Pakistan kutokana na kuongezeka kwa uhasama kuhusu umiliki wa eneo la Kashmir.

"Waigizaji wa Pakistan si magaidi," aliambia runinga moja India, hatua iliyomfanya kushutumiwa na baadhi ya vyombo vya habari India.
Om Puri aliigiza katika kipindi cha runinga cha BBC cha The Canterbury Tales akiigiza kama Jetender

Makamu wa Rais wa Marekani Biden amtaka Trump 'akomae'

$
0
0
 Bw Biden amesema wakati umefika Trump "kuwa mtu mzima"

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia Rais mteule wa Marekani Donald Trump kwamba anafaa "kukomaa" na akamshutumu kwa kukosoa majasusi wa Marekani.

Leo Ijumaa, Bw Trump anatarajiwa kupashwa habari za kijasusi kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa Marekani uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana.

Lakini Bw Trump ametilia shaka madai kwamba Urusi ilihusika, na badala yake akawakosoa vikali majasusi wa Marekani kwenye Twitter.

Bw Biden amesema ni jambo la kusikitisha kwa rais mteule kutokuwa na imani na mashirika ya kijasusi.

"Kwa rais kutokuwa na imani na, na kutokuwa tayari kuyasikiliza, mashirika ya ujasusi, kuanzia majasusi wa jeshi hadi majasusi wa CIA, ni jambo la kukosa hekima kabisa," alisema kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha PSB.

"Wazo kwamba unaweza kuwa na ujuzi au ufahamu zaidi ya mashirika ya kijasusi - ni kama kusema kwamba ninafahamu fizikia zaidi ya profesa wangu. Sikusoma kitabu, ninajua tu kwamba ninajua zaidi."

Alipoulizwa anafikiria nini kuhusu hatua ya Bw Trump kushambulia mashirika ya kijasusi na makundi mengine kwenye Twitter mara kwa mara, Bw Biden alisema: "Komaa Donald, komaa, ni wakati wa kukomaa na kuwa mtu mzima, wewe ni rais. NI wakati wa kufanya jambo la busara.

Tuonyeshe sifa zako."

Baadaye, alimweleza Bw Trump kama "mtu mzuri".

Lengo la udukuzi lilikuwa nini?

Bw Biden amesema ameshasoma ripoti ya mashirika ya ujasusi ya Marekani ambayo inaonyesha wazi kuhusika kwa Urusi katika udukuzi kadiri uchaguzi ulivyokaribia.

Bw Trump atapashwa habari kuhusu ripoti hiyo leo Ijumaa.

Baadaye, nakala ya ripoti hiyo - ambayo imetolewa baadhi ya maelezo - itafanywa wazi kwa umma wiki ijayo.

Bw Biden amesema ripoti hiyo inaeleza wazi "walichofanya Warusi, kama sehemu ya sera yao, kujaribu kuathiri na ... kutia doa shughuli za uchaguzi Marekani".

Amesema udukuzi wa barua pepe ulikuwa sehemu ya kampeni ya kutatiza juhudi za kampeni za Hillary Clinton, mpinzani wa Bw Trump kwenye uchaguzi wa urais.

Ameongeza kwamba udukuzi huo ulikuwa umeenea sana kinyume na ilivyodhaniwa awali.

Miongoni mwa watu ambao barua pepe zao zilidukuliwa ni John Podesta, meneja wa kampeni wa Bi Clinton.
 Jenerali Clapper (kulia) amesema azma ya Bw Putin katika udukuzi itafichuliwa kwenye ripoti ya mashirika ya ujasusi

Sava za Kamati Kuu ya Taifa ya chama cha Democratic pia ilidukuliwa.

Nyaraka hizo baadaye zilifichuliwa kwenye mtandao wa Wikileaks.

Alhamisi, mkurugenzi wa Ujasusi wa Taifa Jenerali James Clapper, aliambia kikao cha Kamati ya Huduma za Jeshi katika Seneti kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin aliagiza kufanyika kwa udukuzi huo.

Alisema lengo lake na azma katika udukuzi huo vitafichuliwa wiki ijayo.

Urusi imekanusha tuhuma hizo kwamba ilihusika katika udukuzi huo. Hata hivyo, Marekani tayari imetangaza kuwawekea vikwazo baadhi ya maafisa wakuu wa Urusi.

Bw Trump amesemaje?
Mr Trump alikuwa ameahidi kutoka "maelezo mabya" kuhusu madai hayo ya udukuzi wiki iliyopita.

Bw Trump mara kwa mara amekanusha madai kwamba serikali ya Urusi ilidukua tarakilishi za Bw Podesta na sava ya Kamati Kuu ya Taifa ya chama cha Democratic.

Jumatano, alirejelea pendekezo lake kwamba huenda "mtoto wa miaka 14" alitekeleza udukuzi huo.

Alhamisi, alisema yeye ni "shabiki mkuu" wa mashirika ya ujasusi, baada yake kutilia shaka kwa muda mrefu tuhuma za kuhusika kwa Urusi.

Hata hivyo, baadaye aliibua maswali kuhusu jinsi chama cha Democratic kilishughulikia udukuzi huo.
"Ni jinsi gani na ni kwa nini wana uhakika hivyo kuhusu udukuzi ikiwa hawakuitisha uchunguzi ufanywe kwenye sava zao za kompyuta? Nini kinaendelea hapa?" aliuliza kwenye Twitter.

Mr Trump alikuwa ameahidi kutoka "maelezo mabya" kuhusu madai hayo ya udukuzi wiki iliyopita.
Lakini hilo halikufanyika.

Bw Trump ataapishwa kuwa rais tarehe 20 Januari.

Njemba Amuua Mkewe kwa Nyundo Kisa Wivu wa Mapenzi

$
0
0
Mwanamke mmoja mkazi wa Mikumi wilayani Kyela, Mbeya aliyefahamika kwa jina la HILDA SIGARA  amefariki dunia akiwa anapelekwa Hospitali kwa matibabu baada ya kupigwa nyundo kichwani na mume wake aitwaye REBSON TWEVE umri kati ya miaka 30 – 35

Kamanda wa polisi mkoani humo DCP Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.01.2017 majira ya saa 12:00 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani inasadikiwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Amesema katika eneo la tukio kumekutwa nyundo moja, kisu kimoja na fimbo ya muanzi ambavyo vinasadikiwa kutumika katika tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Kyela ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na upelelezi unaendelea huku mtuhumiwa akiwa ametoroka mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Aidha, katika matukio mengine kamanda huyo amesema kuwa jeshi la polisi limepokea taarifa za kujinyonga kwa watu wawili ambao miili yao imekutwa ndani ya nyumba zao katika maeneo tofauti.

Watu hao ni pamoja EDWARD PETER  mfanyabiashara na Mkazi wa Majengo na aliyekutwa amekufa chumbani kwake huku mwili wake ukiwa hauna majeraha yoyote, na mwingine ni ROBERT MWAISENYE Mkazi wa Mbugani wilayani Chunya ambaye alikuwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila akiwa ndani ya nyumba yake.

Source: Global Publisher
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images