Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

VIDEO: Top 10 ya Viumbe Hatari Duniani


Alikiba aanza mwaka mpya na Tour za Kimataifa

$
0
0
Mkali wa wimbo Aje na mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa EATV Award 2016, Alikiba amefungua mwaka kwa kutangaza tour yake ya kimataifa.

Muimbaji huyo ambaye mwaka 2016 ulikuwa mzuri kwa upande wake baada ya kuchukua tuzo 13 za kitaifa na kimataifa, tour yake itaanza February nchini Afrika Kusini.

“Happy New Year. It’s time to meet my fans across the world. I start with South Africa in February 2017! . KING KIBA LIVE ON TOUR IN SOUTH AFRICA. Contact Exclusive Agent & PR @matthewmensah for additional bookings & endorsements in SA/Southern Africa. #MTVEMABestAfricanAct#AlikibaSATour2K17#KingKibaWorldTour2K17 #KingKiba,” aliandika Alikiba kupitia facebook yake.

Muimbaji huyo hivi karibuni alifanya show ya funga mwaka nchini Uganda, show ambao ilidaiwa kuweka historia nchini humo kutokana na kuhudhuriwa na watu wengi.

Sababu ya YOUNG Dee Kurudia Madawa ya Kulevya ya Fichuka NYANDU TOZI Akana Kujua.

$
0
0

Sababu ya YOUNG Dee Kurudia Madawa ya Kulevya ya Fichuka NYANDU TOZI Akana Kujua.

Trump kukutana na wakuu wa mashirika ya upelelezi Marekani

$
0
0
Wakuu wa mashirika ya upelelezi nchini Marekani wanatarajiwa kukutana na Rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump na kumwonyesha ushahidi kuwa Urusi ilifanya jaribio lisilokifani kuvuruga uchaguzi wa Marekani kwa kufanya udukuzi katika chama cha wapinzani wake cha Democratic.

Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na mvutano mkubwa kati ya viongozi wa mashirika ya ujasusi ya Marekani na rais huyo ajaye, ambaye anapinga vikali madai yoyote kuwa Urusi ilimsaidia kushinda uchaguzi wa rais.

Baada ya Trump kuonyesha wasiwasi kwa mara ya kwanza mapema mwezi uliopita, Rais Barack Obama aliyaamuru mashirika ya upelelezi kutoa ripoti ya kina kuhusu mashambulizi ya mtandaoni na uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa rais.
Obama alifahamishwa kuhusu ripoti hiyo jana na wakuu wa ujasusi na wanatarajiwa kuzungumza na Trump hii leo.

Aliyewaua watu 5 Marekani akamatwa

$
0
0
Mshukiwa alikuwa mwanachama wa kikosi cha ulinzi cha Puerto Rico na Alaska

 Polisi katika jimbo la Florida wanamzuilia mwuaji mshukiwa baada ya watu watano kupigwa risasi na kuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika uwanja wa ndege wa Lauderdale.

Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la kupokea mizigo. Lengo la shambulizi hilo halijulikani.

Mshukiwa ametajwa kama Estaban Santago aliyepatikana na kitambulisho cha kijeshi na ambaye amewahi kufanya kazi Iraq.

Maafisa wa FBI katika afisi ya Alaska wamekuwa na hali ya wasiwasi kumhusu kwa sababu ya tabia zake za zisizoeleweka na mnamo Novemba walimwelekeza kwa daktari bingwa wa akili.

Polisi wanasema mshukiwa huyo hakusema lo lote kabla ya mashambulizi au baadaye. Alipoishiwa na risasi alilala chine kwa upole.
 Mshukiwa alikamatwa akiwa bila silaha
 
Watu wakitumia magari kujikinga
 

Mwanafunzi aliyepewa mimba atishiwa kuuawa

$
0
0
MKAZI wa kijiji cha Karukekere, kata ya Namhura, wilayani Bunda, Mkoani Mara Godfrey Mgaya ambaye ni mzazi wa mwanafunzi aliyepewa ujauzito, amesema sasa binti yake anatishiwa kuuwawa na ndugu wa mtuhumiwa huyo iwapo atang’ang’ania suala hilo kulifikisha kwenye vyombo vya sheria.

Mgaya alisema hayo jana kwa njia ya simu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, akisema kuwa mtoto wake anaishi kwa wasiwasi akihofia maisha yake.

Alisema licha ya Mkuu wa wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili kuagiza polisi wilayani humo, kuhakikisha wanamkamata mtuhumiwa Zephania Mfungo pamoja na mwenyekiti wa kijiji hicho Nyandago Magesa, aliyewazuia askari mgambo kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni rafiki yake, lakini bado watu hao hawajakamatwa.

Mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa binti yake ambaye ni mwanafunzi aliyekuwa anasoma kidato cha pili katika shule ya sekondari Muranda, iliyoko katika kata hiyo alifukuzwa shule mwaka jana kutokana na kupewa ujauzito na mwanaume huyo na sasa anaishi maisha ya wasiwasi kutokana na vitisho anavyopewa vya kutaka kuuwawa.

Alisema baada ya mtoto wake kupewa ujauzito na mtuhumiwa, alikwenda kutoa tarifa katika ofisi ya kijiji na ofisi ya kata, ambapo alipewa askari mgambo ili waweze kumkamata mtuhumiwa huyo, lakini mwenyekiti wa kijiji hicho aliwazuia mgambo hao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni rafiki yake.

Aidha, alisema kuwa pamoja kufuatilia suala hilo ili mtuhumiwa huyo aweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani, kumekuwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na binti yake kutishiwa maisha yake kuwa iwapo akithubutu kusema ukweli hiyo mimba yake hawezi kujifungua salama na ataondolewa uhai wake.

“Sasa kibaya zaidi tangu tukio hilo, kuna ndugu yake mtuhumiwa amekuwa akimtishia mwanangu kwamba akitoa taarifa juu ya mimba yake hatajifungua salama, hata wanaweza kumkodishia gari iweze kumgonga wakati akitembea barabarani,” alisema.

Baada ya kubaini ndoto ya kusoma ya mtoto wake imekatishwa, alimuomba diwani wa kata hiyo, Jogoro Amoni kuingilia kati suala hilo, ambaye pia alitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, aliyeagiza polisi wilayani hapa, kumkamata mtuhumiwa huyo pamoja na mwenyekiti wa kijiji hicho.

Kutokana na vitisho hivyo, baba mzazi wa binti huyo mwenye ujauzito wa miezi minne, aliamua kutoa taarifa kituo kidogo cha polisi Bulamba kuhusiana na vitisho hivyo.

Mgaya ameiomba serikali kumsaidia, ili watuhumiwa hao waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na pia alimuomba Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuingilia kati suala hilo, kwani watuhumiwa hao wamesababisha mtoto wake kukatisha masomo yake.

Laptop iliyo na skrini tatu yazinduliwa Las Vegas

$
0
0
 Razer wamesema laptop yao yenye skrini tatu ni ya kwanza kabisa duniani

Kampuni inayotayarisha michezo ya kompyuta ya Razer imezindua kipakatalishi (kompyuta ya kupakata/laptop) mpya ambayo ina skrini tatu wenye maonyesho ya teknolojia mpya mjini Las Vegas.

Kampuni hiyo imesema laptop hiyo ambayo imeundwa kupitia mradi uliopewa jina Valerie, ndiyo ya kwanza ya aina yake duniani.

Skrini zote tatu ni za kiwango cha kuonyesha pikzeli 4,000 (4k).

Zote ni za ukubwa wa inchi 17 (43cm).

Skrini mbili huchomoza kila upande kutoka kwa skrini kubwa ya kati, moja kwa moja.

Mmoja wa wachanganuzi wa teknolojia mpya amesifu sana laptop hiyo na ksuema wachezaji wa michezo ya kompyuta siku hizi wamekuwa wakitafuta kompyuta za kisasa zaidi, ghali na zenye uwezo wa kipekee.

Kompyuta hiyo inapozimwa na kufungwa, ina upana wa inchi 1.5.

Razer wamesema inalingana na laptop nyingi sana zinazotumiwa kwenye michezo ya kompyuta, ambao kawaida huwa kubwa kidogo kuliko kompyuta zinazotumiwa nyumbani na afisini.
 Project Valerie ina bawaba maalum ambazo hufungua moja kwa moja skrini mbili, moja kila upande
"Tulifikiria, 'Huu ni kama wendawazimu, tunaweza kufanya hivi," msemaji wa kampuni hiyo aliambia BBC.

"Jibu lilikuwa: 'Naam, tuna kichaa vya kutosha, tunaweza'."

Laptop iliyozinduliwa ni ya maonesho tu na Razer hawajasema ni lini wataanza kuunda kompyuta kama hizo za kuuza.

Project Valerie ni moja tu ya laptop za michezo ya kompyuta zilizozinduliwa kwenye maonesho ya CES.

Acer walizindua laptop kubwa ya inchi 21 ambayo inaitwa Predator 21X, ambayo inagharimu $8,999 (£7,250).

Samsung nao wamezindua laptop yao ya kwanza ya michezo iitwayo Samsung Notebook Odyssey, ambazo ni za ukubwa mara mbili - za inchi 17 na za inchi 15.

Gigy Money amshika uchawi Amber Lulu

$
0
0
 VIDEO Queen matata Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameanza mwaka mpya kwa kushusha madai makali kuwa Video Queen mwenzake Lulu Euggen ‘Amber Lulu’, anamroga na anaishi kwa kutumia nyota yake.

Akizungumza na gazeti hili Gigy alisema kuwa kuna vitu vingi sana amekuwa akifanyiwa na mrembo huyo kitu ambacho alikivumilia muda mrefu hivyo kwa sasa ameona ni bora kuviweka wazi.


“Unajua Lulu, mimi nilikuwa nampenda sana kama ndugu yangu kabisa lakini naona vitu vyangu vingi haviko sawa ukifuatilia kwa wataalam unaambiwa ni yeye (Amber),” alisema Gigy.

Alipoulizwa Amber kuhusu tuhuma hizo, alisema: “Sijamroga yule, ana kipi? Aseme tu nimemzidi maarifa na kujitambua.”

Kala Jeremiah: Sakata la Faru John Limeniogopesha

$
0
0
RAPA anayetamba na ngoma ya ‘Wana Ndoto’ Kala Jeremiah amesema sakata la Faru John ambalo limeteka hisia za watu wengi kwa sasa  alipolisikia kwa mara ya kwanza, mapigo yake ya moyo yalimdunda hadi akaogopa.

Akipiga stori na Over Ze Weeked Rapa huyo amesema amekuwa   akisikia kashfa mbalimbali za ufisadi  kwa muda mrefu, lakini hili la Faru John limekuwa la aina yake.

“Nimekuwa nikijaribu  kufuatilia ishu hiyo kwa kina ajabu nakutana na habari  zisizo eleweka kila mtu anamaelezo yake, sakata la Faru John linanifanya niamini uwepo wa sakata la Twiga waliyowahi kupandishwa Ndege  na kusafirishwa Ughaibuni kinyamela.

“Naendelea kujiuliza maswali ambayo sijui majibu yake nitayapata wapi, miongoni mwa yale ninayo jiuliza ni je kuna Faru wangapi wanaokufa huko  katika mbuga za wanyama, na je kwanini kutoweka kwa Faru John kuibue gumzo kiasi hicho, huyo Faru alikuwa na kitu gani kikubwa cha ajabu, lakini kubwa kuliko vyote nimetaharuki baada ya kubaini kuwa kumbe Wanyama huwa wanapewa Majina ya Binadamu.” Alisema Kala Jerimiah

Mashabiki wa muziki Kenya wamlilia Darassa

$
0
0
 Mashabiki wa muziki wa nchini Kenya wamemlilia Darassa. Hilo limedhihirika katika ujumbe aliouandika muimbaji wa nchi hiyo, Nyota Ndogo kwenye mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo, Nyota Ndogo aliweka picha ya mashabiki na kuandika, “@darassacmg plz kuna pesa zako kenya zinakungoja.this was my show in malindi.nimemaliza kupiga show mashabiki wanamuomba dj acheze nyimbo yako na mimi ni dance.nipo na video yani mimi ni dance.kimbia huku mara moja kabla nyimbo haijaisha ufanye tour ongea na @gatesmgenge nimzuri wakupiga debe.unamashabiki sio tz pekeake.do it now.”


Hizi ni comment za mashabiki katika mtandao huo:

gatesmgenge: @nyota_ndogo tayari mpangilio wafanywa tayari tushazungumza na @hanscana_ karibuni watu wangu wa #Malindi.

ulomchokoza:_kaja@darassacmg@darassacmg @darassacmg plzzzzzzz bro pitia hapa

cntermourice: Wimbo wa taifa unaliliwa kenya @blaze_tz

omoyut: @darassacmg ukuje huku

Mwaka 2016 nilikuwa najiimarisha kwenye biashara, 2017 narudi rasmi kwenye filamu – Nisha

$
0
0
 Msanii wa filamu za vichekesho Salma Jabu aka Nisha amedai mwaka uliopita alifanya filamu chache na kuutumia muda mwingi kwenye kujiimarisha zaidi katika biashara.

Muigizaji huyo ambaye ni mfanyabishara wa vipodozi pamoja na nguo, amedai alikuwa anaweza mazingira ya biashara zake safi kwa kuwa anaamini hawezi kuigiza kwa miaka yote.

“Hakika 2016 ulikuwa ni mwaka wangu wa kufanya biashara tofauti na movie, 75% nimefanya biashara huku movie nikafanya 25% na yote hayo nilifanya ili kuweza kuweka msingi imara wa kujiingizia kipato bila kutumia ‘UNisha’ maana naimani kuna maisha baada ya haya na umri unasonga,” aliandika Nisha kupitia Instagram.

“Mwaka mpya 2017 ni mwaka wa kuziba pengo la filamu nikiwa na Nishasfilmproduction. Ahsante Mungu aliye mwema kwenye biashara ndoto kubwa nliyokuwa naiwaza tangu mdogo soon inaenda kutimia ikifika juu. No time to waste and drama zimeishia hapa.,” aliongeza Nisha.

Pia muigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kusahau skendo zote zilizotokea mwaka 2016 huku akidai zilikuwa ni mbinu za kibiashara.

Disemba 2016 muigizaji huyo alidai kupewa mimba na mwanaume ambaye hakumtaja na baadaye kukataliwa.
Moja kati ya biashara za malkia huyo wa filamu

Kocha wa Azam Ameitaja Sehemu Alipoikamata Yanga

$
0
0

Yanga wanategemea sana mipira ya pembeni, sasa tulijaribu kuangalia watu wanaowachezesha wale watu wa pembeni, tukawakamata na ukiwakamata Yanga kwenye midfield basi unakuwa umeua plan zao wakaishiwa maarifa wakawa hawajui nini cha kufanya sisi tukawa tunatengeneza nafasi na kuzitumia,” anasema kocha wa muda wa Azam Idd Cheche baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi wa kihistoria dhidi ya Yanga.

Kwenye michezo miwili iliyopita Azam haikuonesha kiwango kizuri kiuchezaji huku washambuliaji wake wakishindwa kutumia vizuri nafasi, Cheche amesema tatizo lilikuwa ni umaliziaji na walilifanyia marekebisho ndio maana safu ya ushambuliaji ilikuwa hatari dhidi ya Yanga.

“Tumerekebisha safu ya shambuliaji ndio ilikuwa inasumbua kidogo, tulikuwa tunapata nafasi lakini tuikuwa tunashindwa kuzitumia, movements zilikuwa ndogo kwa hiyo tumelifanyia kazi hili suala la finishing ndio limeleta haya matunda yaliyotokea.”

Azam imefuzu hatua ya nusu fainali na inatarajia kukutana na timu itakayomaliza nafasi ya pili kutoka Kundi A lenye timu za Simba, Taifa Jang’ombe, Jang’ombe Boys na URA ambazo zote zina nafasi.

Hii ndio kauli ya Cheche kuelekea mechi ya nusu fainali: “Yoyote atakaekuja kwenye nusu fainali atakuwa ni mzuri na sisi tumejiandaa kupambana nae tuhakikishe tunavuka tunaingia fainali na kuchukua kombe.”

Diamond kufunika ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2017’

$
0
0

Ule wimbo unaosikika mtaani wa ‘pesa kupotea mifukoni’ haumhusu Bosi wa WCB, Diamond Platinumz anayeendelea kuzihesabu ‘deals’ kubwa zaidi za matukio ambayo dunia nzima inayaangalia kwa macho yote.


Siku chache baada ya kutumbuiza kwa ustadi mkubwa kwenye tuzo za CAF jijini Abuja nchini Nigeria, Diamond amealikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Africa 2017 (AFCON 2017), Januari 14 nchini Gabon.


Chibu Dangote amewapa habari hiyo njema mashabiki wake kupitia mitandao ya twitter na Instagram, kwa kupost taarifa ya show yake hiyo iliyowekwa kwenye akaunti maalum ya AFCON 2017.


“GABON!!! You know we gat to make a World History on the 14th January right?? See you this this Coming Weekend then…👈 #WcbWasafi” aliandika.


Ingawa Tanzania haipo miongoni mwa nchi zinazoshiriki kombe hilo kubwa zaidi la soka barani Afrika, mwaka huu bendera itapeperushwa kupitia tasnia ya Muziki na kuiacha alama ya Tanzania kwenye mashindano hayo.

Mwanamke wa Kitanzania Akamatwa na Mzigo wa Madawa ya Kulevya Tumboni

$
0
0

INDONESIA: Mwanamke Mtanzania akamatwa akiwa na Wanigeria wawili wakijaribu kuingiza mihadarati. Mnigeria mmoja ameuawa akijaribu kutoroka. Mtanzania huyo alikamatwa siku ya jumatano katika Jiji la Jakarta.

Baada ya upekuzi Mtanzania huyo akutwa na gramu 138 za Crystal Methamphetamine, kete nyingine 66 za Crystal Methamphetamine alikuwa amezimeza na gramu 3 za bangi alizoficha kwenye nguo yake ya ndani.

Wakati huo huo, polisi nchini Namibia wanadai kukamata watu 135 kati ya Novemba 1 na Disemba 2016 kwa tuhuma za dawa za kulevya aina ya Mandrax, Cocaine, Crack Cocaine, Heroin na Bangi. Kati ya waliokamatwa na dawa hizo wapo Watanzania watano.

Baada ya Soulja Boy Kumpata Mwalimu Mayweather, 50 Cent Amvuta Mike Tyson Kumtrain Chris Brown

$
0
0

BAADA YA SOULJA BOY KUMPATA MWALIMU
MAYWEATHER, 50 CENT AMVUTA MIKE TYSON
KWA AJILI YA KUMTRAIN CHRIS BROWN

It’s going down for real, pambano la ngumi kati ya Chris Brown na Soulja Boy linazidi kuwashawishi watu maarufu kibao, Sasa ni zamu ya Mike Tyson.

Baada ya Soulja Boy kuthibitisha kwamba trainer wake ni Floyd Mayweather, 50 Cent ameamua kumsaidia Chris Brown kwa kumvuta Mike Tyson kwa ajili ya kumtrain Breezy.

Kupitia kurasa ya Instagram ya 50 Cent ameposti vipande vya clip akiongelea kuhusu pambano hilo la Chris Brown na Soulja Boy kwa kusema kwamba, ‘“Floyd is supposed to be training him, but I kind of feel like Floyd want to train him and shit so he can beat me, How you gonna train this nia, all of a sudden? You is the promoter. You ain’t supposed to be training the fighter…But since he got Floyd Mayweather, I just got off the phone with Iron Mike Tyson. Iron Mike is gonna train Chris Brown.”

50 Cent hakuishia hapo akatusibitishia maongezi yake na Mike Tyson ambapo Mike Tyson alifunguka nakusema kwamba “Soulja Boy’s gon’ get fucked up by a yellow ni
a, hris Brown’s yellow ass gon’ fuck Soulja Boy up.”


Lakini tukirudi pia upande wa pili wa jamaa anaitwa Adrien Broner, maarufu kwa ndondi na promoter wa ngumi, yeye amesema atajitolea kumfundisha Chris Brown, na ametaka pambano lisogezwe mbele mpaka tarehe 28 mwezi huu

Pata Kifaa Chenye Uwezo Asilimia 99% wa Kuongeza Ukubwa wa Uume....

$
0
0

Handsome up ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara. Inapatikana kwa @200,000/=tu. PIA kuna Gely ya kupaka @ 120,000/= na Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume @120,000/=.
Na spray ya kuchelewesha kufika kileleni kwa mwanaume @120,000/=
NB.Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON $ CO. Wasiliana nasi kwa no (+255) 0767447444 au
0714335378.
Follow us
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr

Lowassa Atoa Neno Kwa Waliomtabiria Kifo

$
0
0

Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa, amesema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ina watu wenye roho mbaya kwani waliwahi kumuombea kifo,lakini hadi leo anadunda.

 

Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), amesema baadhi ya waliomwombea kifo leo hawapo duniani,kwani mungu ndiye anayepanga maisha ya mwanadamu.

 

“Kule kwa wenzetu kuna watu wenye roho mbaya,kwani hata mimi waliniombea kifo,waliniombea kifo muda mrefu kweli lakini mpaka sasa bado nadunda tu wakati baadhi ya walioniombea hivyo,leo hawapo duniani kwa mapenzi ya mungu”alisema Lowassa.

 

Lowassa aliyasema hayo jana baada ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa ufunguzi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Matevezi jimbo la Arumeru Magharibi,kupaza sauti wakimuuliza juu ya hatima ya mbunge wao Lema ambaye yupo Gereza la kisongo kwa miezi miwili sasa.

 

Katika hatua nyingine, Lowassa  aliwataka timu ya kampeni na wananchi kuhakikisha kura haziibiwi kwa kile alichoeleza kuwa Chadema ina nguvu.

Ningekuwa Rais ningewekeza kwa watoto- Rama Dee

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Rama Dee amefunguka na kusema kama angekuwa Rais wa Tanzania yeye angawekeza kwa watoto

kwani anaamini huwezi kuinyoosha bila ya kuangalia kizazi cha kesho akiamini kizazi cha sasa tayari kimesha athirika kwa msongo wa mawazo.

"Kwa mfano mimi nigekuwa Rais wa Tanzania, ningewekeza kwa watoto mana hauwezi kuinyoosha nchi bila kuangalia kizazi cha kesho, hiki chetu tayari kimeathirika, nchi ya Australia iligundua stress nyingi sana za wazazi zinaaribu maisha ya Watoto, hivyo walicho kifanya walitengeneza sheria ya mtoto, na kama mzazi ukipindisha unapelekwa mahakamani bila shaka. Waliweza kutengeneza mfumo wa "childcare" so hata kama mzazi hana kipato lakini serikali inaweza kusaidia mtoto akapata msingi mzuri wa kimaisha na kishule" alisema Rama Dee

Mbali na hilo Rama Dee anasema Child Care kwa nchi za wenzetu zinasaidia kuondoa utofauti wa mtoto wa mtu masikini na mtu tajiri kwani ukiwaweka pamoja wote wanakuwa sawa na kulingana kwa mambo mengi.

"Child care wanajaribu kusaidia wazazi wafanye kazi na mtoto apate malezi mazuri kupitia watu walio na uzoefu wa kulea watoto! ndio maana ukimsimamisha mtoto wa masikini wa mzungu na tajiri wote wapo sehemu sawa tu! hivyo dhumuni la serikali hapa ni kukamilisha au kutimiza ndoto za watoto" Rama Dee

Njia za kuwakomesha majambazi

$
0
0
Dar es Salaam. Matukio ya watu kuvamiwa na majambazi na kuporwa fedha yamekuwa yakiripotiwa kila kukicha.

Idadi kubwa ya wananchi wamekuwa wakivamiwa na kuporwa fedha. Katika matukio hayo wapo ambao wameuawa, kujeruhiwa na wengine kupata ulemavu wa maisha.

Kutokana na kushamiri kwa matukio hayo mwandishi wetu amefanya utafiti wa jinsi ya kujiepusha kuingia katika janga hilo.

Usitembee na fedha nyingi

Unapobeba fedha nyingi unajiweka katika hatari ya kudhurika au hata kuuawa. Mhalifu anapofika kwako anachotaka ni kupata fedha, hivyo kumchelewesha maana yake ni kuhatarisha maisha.

Wahalifu wanaweza kupewa taarifa za wewe kuwa na fedha nyingi wakati fulani, au kutokana na kiwewe wahalifu wanaweza kukugundua kuwa umebeba kiasi kikubwa cha fedha na kukuvamia.

Epuka kubeba fedha nyingi, fanya malipo kwa mafungu kidogokidogo mpaka ukamilishe malipo au ununuzi uliotaka kuufanya.

 Hakikisha uko salama

Uhalifu unaweza kutekelezwa mahali popote, hivyo ni vyema kila wakati kuhakikisha mazingira uliyopo ni salama. Kwa mfano unapohisi kuna mtu anakufuatilia, chukua hatua haraka ya kuondoka mahali hapo na kujisogeza unapoweza kupata msaada.

Fanya malipo kwa kadi, simu

Malipo kwa njia za simu au kadi ni namna mojawapo ya kujikinga kwa sababu wahalifu hawawezi kuwa na muda wa kuchukua fedha iliyopo kwenye simu.

Wahalifu wanahitaji fedha za haraka ambazo haziwezi kuacha alama ya wao kukamatwa, mlolongo wa kutoa au kuhamisha fedha ndiyo usalama wako.

Kuwa makini na watu usiowajua

Unaweza kukutana na mtu mgeni anayeonekana kutaka kukuzoea ghafla. Anaweza kuwa anakufahamu kwa kiasi fulani lakini unapotaka kumjua yeye anakupa hadithi ambazo kila ukijitahidi kuzielewa akili yako inakataa.

Watu hawa ni hatari, wanaweza kuwa ndiyo wezi wenyewe au wamekuja kutafuta uhakika wa taarifa za uhalifu wanaotaka kuutekeleza kwako.

Kama unafanya biashara, mtu anayetaka kukuibia anaweza kuja zaidi ya mara moja. Huwa ni mwenye wasiwasi na anayependa kuuliza maswali mengi.

 Epuka kuzungumzia mipango yako

Unapokaa na watu iwe kazini, sehemu za starehe au mkusanyiko wa aina yoyote usizungumzie mipango yako hasa ile inayohusiana na fedha.

Unapozungumza na simu kuhusu mipango ya fedha hakikisha hakuna anayekusikiliza kwani anaweza kutoa taarifa hizo kwa wahalifu nao wakapanga mbinu ya kukupora au kukudhuru.

 Kuwa makini unapotumia mashine za ATM

Usimwamini mtu hasa unapoingia katika mashine za kutolea fedha. Angalia watu waliotangulia au waliopo karibu na eneo la mashine hiyo.

Baada ya kutoa fedha kuwa makini. Ukimuona mtu unayemtilia shaka, badilisha uelekeo. Kama yupo nyuma au mbele yako, vuka upande wa pili wa barabara na ondoka haraka.

 Vibanda vya miamala ya fedha

Wafanyabiashara wa miamala ya fedha ni waathirika wa uporaji kwa kuwa wanaaminika kuwa na fedha wakati wote. Mbinu ya kuepuka kuporwa ni kufunga mapema maduka au vibanda vyao.

Njia nyingine ni kuwa makini na watu wanaofika kuulizia kama wana kiasi fulani cha fedha wakijifanya wanataka kutoa lakini huondoka bila kufanya hivyo.

Hawa ni wahalifu ambao hujihakikishia kwanza kama mlengwa ana fedha za kutosha kabla hawajamvamia kwa hiyo, anapotokea mtu kama huyu ni vyema kumfuatilia na ikibidi kufunga kibanda kabla hajarudi na wenzake kufanya uhalifu.

Kadhalika, ikiwa umekusanya kiwango kikubwa cha fedha, hakikisha unazihamisha na kubaki na kiasi ambacho kitahitajika kwa miamala katika muda wa kazi uliobaki.

Ripoti Mpya Ya Mashirika Ya Kijasusi Marekani Yadai Rais Putin Wa Urusi Aliingilia Uchaguzi Wa Marekani

$
0
0
Ripoti mpya iliyotolewa na mashirika ya kijasusi nchini Marekani Ijumaa wiki hii imedaiwa kumtaja Rais Vladimir Putin wa Urusi kuwa aliagiza kufanyika kampeni maalumu kupitia katika vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kufanya udukuzi kwa lengo la kuingilia uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Novemba mwaka jana.

Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa Rais Putin alifanya hivyo kwa makusudi akilenga kumdhoofisha kisiasa mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton katika kampeni zake za kuwania kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Maafisa wa mashirika hayo ya kijasusi ya Marekani walitoa kurasa 25 za ripoti hiyo kwa umma Ijumaa wiki hii baada ya kuwa tayari wamewasilisha ripoti ndefu kuhusiana na uchunguzi huo kwa Rais Barack Obama, Rais Mteule Donald Trump pamoja na wabunge waandamizi nchini humo.

Aidha ripoti hiyo inaeleza kuwa Rais Putin na serikali ya Urusi walionyesha upendeleo maalumu kwa Rais Mteule Donald Trump. Hata hivyo licha ya ripoti hiyo kuwekwa wazi Trump bado ameendelea kutetea uhalali wa kuchaguliwa kwake.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live


Latest Images