Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live

Rais Mstaafu Wa Ureno Afariki Dunia

$
0
0
Rais wa zamani wa nchi ya Ureno, Mario Soares ambaye anaheshimika kama baba wa demokrasia nchini humo amefariki dunia hapo jana akiwa na umri wa miaka 92.

Rais huyo wa zamani ndiye mwanzilishi wa chama cha kisoshalisiti nchini humo na katika kipindi cha uhai wake alitumia miongo kadhaa katika masuala ya siasa ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele wakati wa mchakato wa nchi hiyo kujiunga kwenye Umoja wa Ulaya.

Soares alikuwa rais wa nchi hiyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 1996 baada ya kuwa tayari amelitumikia taifa hilo katika nyadhifa za uwaziri wa mambo ya nchi za nje na Waziri Mkuu.

Ureno imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumatatu kwa ajili ya kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

VIDEO: Ona Mapenzi ya Binadamu kwa Wanyama

$
0
0
VIDEO: Ona Mapenzi ya Binadamu kwa Wanyama...

ANGALIA VIDEO HII..

Maximilian Amzungumzia Aliyehusika Kufuta Video ya Furaha ya Young D Youfube

$
0
0

Aliyekuwa meneja na mlezi wa Young D
amefunguka mengi kwenye FNL ya EATV kumuhusu
Young Dee na ikiwemo aliyehusika kufuta video yake
#furaha

. "Unapofanya vitu kwa kushirikisha management vitu
vikiwa kiofisi haviwezi kuharibika vikiharibika ofisi
itachukua responsibility ya kuvirekebisha" alisema
@maximilianrioba "tuliachia video halafu badae haipo
YouTube lakini badae nikagundua kulikuwa na mtu
ambae alikosana nae akawa na access ya password and
then aka contact YouTube hii video sijui ina violate sheria
baada ya hapo ikatolewa, so tume struggle kuirudisha ikashindikana"


Kwa upande mwingine meneja huyo amedai video mpya
ya sasa ya Young Dee #youngdaddy haipo chini ya MDB
lakini imetengenezwa na kukamilika wakati akiwa MDB

Man Walter Alitaka Diamond Ashirikishwe Kwenye Wimbo wa Mr Blue Mboga Saba Badala ya Ali Kiba

$
0
0

P zone mc msanii kutoka micharazo ya mr blue
amefunguka kwenye FNL ya EATV na kudai Man
water alitaka Diamond ndio ashirikishwe kwenye
ngoma ya Mr blue #mbogasaba

. "Man water alitaka diamond aingize vocal kwenye wimbo
wa mr blue lakini haikuwa hivyo, Mr blue alitaka kiba
afanye kitu zaidi na tulipompigia simu kiba alifanya
heshima kubwa zaidi mimi mwenyewe sikutegemea"

Hata hivyo @pzone_mc aliongeza kwa kusema @man_water
alitaka kifanyike kitu zaidi ya pale alipofanya @officialalikiba
na ndio maana katafutwa mwanadada aingize tena sauti
kwenye kolabo hiyo

Mchungaji Ahubiri Akiwa Kabebwa Mgongoni

$
0
0
Makanisa Siku hizi Usanii Mtupu embu angalia huyu Pastor, Hatakiwi kukanyaga chini akiwa anatoa mahubiri..Anabebwa au kupanda migongoni mwa waumini....

Watch "Wolper ampiga kibuti Harmonize :Afuta picha zake zote na za WASAFI"

$
0
0

KUMBE na Wanaume wa Dar mnapigwa VIBUTI?
Bonyeza Play

Lowassa: Serikali ya CCM ina Watu Wabaya Sana Kwani Walimuombea kifo Wakati wa Kampeni.

$
0
0

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, E. Lowassa amesema Serikali ya CCM ina watu wabaya sana kwani walimuombea kifo wakati wa kampeni.

Adai mabadiliko hayazuiliki kwani ndio muelekeo wa dunia kwa sasa.

Kinadada washtukia ulaji wa Pweza, 40% wanakula kila siku

$
0
0
Baada ya wanaume kusifika kuwa ndio walaji wakubwa wa minofu ya samaki aina ya Pweza na supu yake, hali sasa imebadilika baada ya kinadada kuonekana pia wakichangamkia kwa wingi kitoweo hicho kinachotajwa kuwa na sifa za kipekee kwa mujibu wa watumiaji.

Inaelezwa kwa wastani kupitia wauzaji waliozungumza na Nipashe imebainika kuwa kuna ongezeko la takribani asilimia 40 ya wateja wanawake anbayo ni  karibu kila kwenye wateja 10 wanaoununua vipande vya Pweza au supu yake kuwa wanne ni wanawake.

Wanaume ndiyo walikuwa wakisifika kwa ulaji wa supu ya Pweza uliopamba moto jijini Dar es salaam katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo taarifa kwamba husaidia mambo mengi mwilini hasa katika kuimarisha urijali kwa wanaume.

UTAFITI WA KITABIBU:
Dr. Damas Mahenda ambaye ni Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) amesema ni kweli samaki jamii ya Pweza wanafaida nyingi mwili hivyo si ajabu kusikia watu wakichangamkia matumizi yake wakiwemo akina mama.

Dr. Mahenda amesema Pweza wamejawa na virutubisho vinavyosaidia mengi ikiwemo kuongeza hamu na kuboresha tendo la ndoa huku minofu yake ikiwa virutubishpo vya kumuwezesha mwanamke kuwa na sifa halisi za “Ukike” na pia mwanaume kuimarika afya yake.

Mapacha Waishi na Mwanamme Mmoja Kwa Furaha

$
0
0
 MAPACHA wawili wa kike wanaofanana, waitwao Anna na Lucy,  wameamua kuishi na mwanamme mmoja aitwaye Ben Bryne mwenye umri wa miaka 32 huko Perth, Australia.

 Wanawake hao wanaishi na mwanaume huyo mmoja kwa kipindi kirefu huku wakishiriki tendo la ndoa pamoja kwani wamejichukulia kuwa mwili mmoja kwa kupendana na kutooneana wivu pindi mmoja wao awapo na mwanaume huyo.

“Ni mara yangu ya kwanza kuishi na marafiki wawili wa kike na wamekuwa waaminifu kwangu,” Byrne alimwambia mama yake.

Anna na Lucy wameandika rekodi mpya duniani ambapo vyombo vya habari vimekuwa vikiandika sana habari zao ambapo wamekuwa kivutio kikubwa hasa katika harakati za tasnia ya wanawake duniani. Watu wamekuwa wakishangazwa  na mtindo wao huo wa maisha wa kuishi na mwanamme mmoja.

Watu wengi wamekuwa wakihoji ni jinsi Byrne ameweza kulala na wanawake wawili ambao ni mapacha wenye kufanana na akaweza kuwatofautisha!

Wakati huohuo, Anna na Lucy siku zote wameonekana wenye furaha kwa mtindo wao huo wa maisha ambapo wanavalia nguo sare na kutoka sehemu za burudani wakiwa pamoja na mpenzi wao.

SMG, risasi 30 vyaokotwa kichakani

$
0
0
Kibaha. Silaha ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Silaha hiyo inadaiwa iliibwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventura Mushongi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka lindo getini hapo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo.

“Askari huyu alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana, hivyo alitoka na silaha akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi ndipo ilipoibwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi,” alisema.

AY amtaja R Kelly wa bongo

$
0
0
Rapa mkongwe bongo AY amefunguka na kumtaja msanii wa Rnb kutoka Tanzania Ben Pol kuwa ndiye mfalme wa Rnb kwa Afrika Mashariki, Kusini mwa jangwa la Sahara na Afrika Mashariki na kati.

Mbali na hilo AY amemfananisha Ben Pol na mkali wa Rnb kutoka Marekani R Kelly na kusema Ben Pol ndiye R Kelly wetu hivyo tunapaswa kumpa support tu katika kazi zake ili azidi kufanya mambo makubwa zaidi na kuiwakilisha nchi vyema kupitia muziki wake.

"Imagine unapata ZIGO lenye Moyo mashine .About last night na mdogo wangu King wa RnB East Africa,Kusini mwa Jangwa la Sahara na Mashariki ya Kati..Ndio R Kelly wetu sasa tufanyaje?? Tuzidi kumsupport BEN POL" alisema Ben Pol

Kwa sasa Ben Pol anafanya vyema na wimbo wake 'Phone' ambao amemshirikisha Mr Eazi

Madawati yawaweka mtegoni wakuu wa mikoa saba

$
0
0
Dar\mikoani. Wakuu wa mikoa saba nchini wanapambana kulinda ajira zao kwa kuhakikisha wanatatua tatizo la upungufu wa madawati baada ya kupewa siku 43 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Wakuu hao wa mikoa ya Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma walipewa siku hizo na Simbachawene wawe wametatua tatizo la upungufu wa madawati katika mikoa yao baada ya kuonekana ina upungufu.

Agizo hilo alilitoa Novemba 18, mwaka jana akieleza kushindwa kulitekeleza katika siku hizo watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Rais John Magufuli.

Alitoa siku hizo baada ya kupokea madawati 3,500 yenye thamani ya Sh300 milioni kutoka Benki ya NMB.

Baada Ya Kipigo Cha Yanga, Simba Wasema Wako Makini Kila Mechi

$
0
0
Baada ya Yanga kupoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC, Simba imesema itaendelea kuchukua tahadhari kubwa kwa kila mechi yake ya Kombe la Mapinduzi.

Simba imeshinda mechi zake zote za Mapinduzi lakini haikuwa ikishinda kwa idadi kubwa ya mabao kama ilivyo kwa Yanga.

Simba inashuka dimbani Amaan mjini Zanzibar kuivaa Jang’ombe Boys katika michuano hiyo.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wako tayari na wanachotaka ni kufanya vizuri.

“Kila mechi ni mechi nyingine, lazima kuwa makini kwa lengo la kufanya vizuri,” alisema.

Simba inaongoza Kundi A ikiwa na pointi saba baada ya kushinda mbili na sare moja.


Iwapo itashinda leo, uhakika asilimia mia kuivaa Yanga katika nusu fainali utakuwa umepatikana.

Mke wa Masele Ashauriwa Ajiandae kwa Vicheko

$
0
0
 BI Specioza Malick  mke wa msanii wa vichekesho nchini aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa mtindo wake wa kuchekesha, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’,  ni vyema akajitayarisha kucheka na kuvunjika mbavu kutokana na sanaa hiyo ambayo mumewe anaiweza ilivyo.

 Mrembo huyo, aliyefunga ndoa na msanii huyo mwezi huu wa Januari,  ameshauriwa na mashabiki wa sanaa ya mumewe ajitayarishe kucheka zaidi na wakati huohuo awe na ubavu wa kutenganisha kazi ya Masele na maisha yake halisi.

“Mke wa Masele ajiandae kucheka mpaka kuumwa mbavu siku Masele akiamua kumletea nyumbani vituo anavyofanya kwenye televisheni nyumbani.   Bi Specioza ajiandae kuwa maarufu kwani kwa sasa ameungana mwili mmoja na mtu maarufu nchini,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kama Bondi Masaba wa jijini Dar es Salaam.

Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi-Makabe jijini Dar es Salaam.

Rais wa kwanza wa Ushelisheli aaga dunia

$
0
0
Rais wa kwanza wa Ushelisheli, taifa lililoko katika kisiwa kilicho kwenye Bahari Hindi, James Mancham, amefariki.

Mancham amefariki akiwa na umri wa miaka 77.

Inaripotiwa kuwa alipatikana na wafanyikazi wake akiwa amezirai ndani ya nyumba.

Wakili wake Sir James, baadaye alichukua hatamu ya Urais mnamo mwaka 1976 baada ya kushinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa kwanza nchini humo.

Ushelisheli zamani ilitawaliwa na Uingereza.

VIDEO: MAPENZI SIO PESA ONA HII

$
0
0
VIDEO: MAPENZI SIO PESA ONA HII

 ANGALIA VIDEO HII...
 

Pwani: Bunduki Ya Kivita SMG Iliyokuwa Imeibiwa na Mfanyakazi wa Hifadhi ya Saadani Yakutwa Kichakani

$
0
0
Silaha ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Silaha hiyo inadaiwa iliibiwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bonaventura Mushongi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka zamu ya lindo la geti hilo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo.

“Huyu askari alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana zamu ya ulinzi hivyo alitoka na silaha yake akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi na ndipo ilipoibiwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi hiyo,” alisema.

Mushongi alibainisha kuwa baada ya wizi huo, askari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) walianza msako na kupitia taarifa ya msamaria mwema walimkamata mtuhumiwa huyo, mkazi wa Tegeta Kibaoni ambaye alikwenda kuonyesha alipokuwa ameificha kichakani ikiwa na risasi 30.

Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk James Wakibara alisema wameshtushwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea na kwamba, zaidi ni baada ya kukuta mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa mtumishi wao na aliacha kazi miezi kadhaa iliyopita yeye mwenyewe.

Dk Wakibara alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano lilioutoa toka siku ilipoibiwa silaha hiyo hadi ilipopatikana.

Mtoto wa Faru John Awa Tishio Kwa Wenzake Ngorongoro

$
0
0
Faru dume wanaoishi ndani ya Bonde la Ngorongoro mkoani Arusha wapo katika hatari ya kujeruhiwa au kuuawa na mtoto wa faru John aitwaye Telele.

Mmoja wa wahifadhi (jina tunalihifadhi) wa faru katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), alisema faru huyo amerithi tabia za baba yake za ukorofi, na tayari ni tishio kwa wenzake.

Faru John aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Agosti 21, mwaka jana kutokana na uzee na maradhi, anatajwa kuwa mbabe kiasi cha kuwafukuza faru wengine kutoka Bonde la Ngorongoro na kuua wengine wawili kwa nyakati tofauti.

Kifo cha faru John kilizua utata mkubwa, kiasi cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuagiza ufanyike uchunguzi wa kina ambao bado unaendelea.

Kwa mujibu wa mhifadhi huyo, ubabe wa faru John ulifikia hatua ya kupigana na baba yake aitwaye Rajabu kuanzia mwaka 2000 na baada ya vipigo mfululizo, Rajabu alihama kutoka Ngorongoro na kwenda eneo la Moru katika Hifadhi ya Taifa Serengeti ili kunusuru maisha yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Ngorongoro, faru John anatajwa kuwa faru mwenye umbo kubwa kuliko faru yoyote barani Afrika na mtoto wake Telele amechukua umbo la baba yake.

“Baada ya Rajabu kukimbia na kwenda Moru, Serengeti, walibaki madume watatu ambao ni John, Mikidadi na Runyoro, lakini kadri siku zilivyokuwa zikienda na ugomvi ulikuwa ukizidi, kila mmoja akitaka kuwa mkuu wa himaya, huku madume mengine yakiendelea kukua.

“Madume hayo ni pamoja na Msekwa, Telele, Ndugai na Selelii, na huyu Telele ana umbo kama la John na mkorofi sana.

“Mwaka 2003 mapigano yalizidi hadi pembe ya John ikakatika katika mojawapo ya matukio hayo ya kupigana, na baadaye Mikidadi na Runyoro nao walilazimika kukimbia, lakini baada ya kukatika, pembe hiyo ilianza kuota tena na kurudi kwenye makali yake.

“Baada ya madume hayo mawili kukimbia, mwaka 2012 faru John alimjeruhi kwa pembe mtoto wake mwingine aitwaye Cheusi… pembe ilipenya na kumchoma kwenye mapafu na maini na kumsababishia madhara makubwa,” alisema.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Ngorongoro, mwaka 2014 ilibidi pembe ya John ikatwe na mtaalamu kutoka Afrika Kusini, Peter Morkel, ambaye baada ya kuikata aliweka kifaa maalumu cha utambuzi (transmitter), ambacho kipo ndani ya mojawapo ya pembe alizokabidhiwa Waziri Mkuu Majaliwa usiku wa kuamkia Desemba 8, mwaka jana.

“Kuna wakati vikao vilipendekeza John apelekwe Afrika Kusini, lakini kutokana na historia yake ya ugomvi, wenzetu wa kule walikataa,” alisema mtoa taarifa.

 TABIA NA MAISHA YA FARU

Kwa mujibu wa wahifadhi wa faru waliopo Ngorongoro na Serengeti, faru dume wana tabia ya kupigana kila mmoja akitaka kuwa mtawala wa wengine.

Mapigano ya faru wakati mwingine hudumu hata kwa zaidi ya saa tano na yanaweza kusababisha majeraha makubwa na hata kifo.

Ili kuwaachanisha faru wanaopigana, inabidi itafutwe gari na kuingia kati yao, na kwa kawaida baada ya kazi ya kuwaachanisha, gari huharibiwa vibaya na faru hao.

Pia faru jike akishapandwa, huchukua miezi 18 kuzaa, na kutokana na mazingira asilia mazuri kwa faru katika Bonde la Ngorongoro, anaweza kubeba mimba miezi sita baada ya kuzaa.

Hivi sasa kuna faru zaidi ya 50 Ngorongoro, kutoka faru 10 katika miaka ya 1980 hadi 1990, jambo linalotajwa kuwa limelotokana na juhudi kubwa na umakini katika uhifadhi wa mnyama huyo.

Mashabiki wa muziki Kenya wamlilia Darassa

$
0
0
Mashabiki wa muziki wa nchini Kenya wamemlilia Darassa. Hilo limedhihirika katika ujumbe aliouandika muimbaji wa nchi hiyo, Nyota Ndogo kwenye mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo, Nyota Ndogo aliweka picha ya mashabiki na kuandika, “@darassacmg plz kuna pesa zako kenya zinakungoja.this was my show in malindi.nimemaliza kupiga show mashabiki wanamuomba dj acheze nyimbo yako na mimi ni dance.nipo na video yani mimi ni dance.kimbia huku mara moja kabla nyimbo haijaisha ufanye tour ongea na @gatesmgenge nimzuri wakupiga debe.unamashabiki sio tz pekeake.do it now.”

Hizi ni comment za mashabiki katika mtandao huo:

gatesmgenge: @nyota_ndogo tayari mpangilio wafanywa tayari tushazungumza na @hanscana_ karibuni watu wangu wa #Malindi.

ulomchokoza:_kaja@darassacmg@darassacmg @darassacmg plzzzzzzz bro pitia hapa

cntermourice: Wimbo wa taifa unaliliwa kenya @blaze_tz

omoyut: @darassacmg ukuje huku

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Dr. Valentino Mokiwa Avuliwa uaskofu

$
0
0
Sakata la Mgogoro wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es salaam, linazidi kuchukua sura mpya,kufuatia Askofu wa Dayosisi hiyo,Dokta Valentino Mokiwa,kugoma kujiuzulu na kustaafishwa kwa manufaa ya Kanisa hilo kama alivyotakiwa na Mhasham Askofu wa Jimbo kuu la Tanzania,Dokta Jacob Erasto Chimeledya.

Hatua ya Dokta Mokiwa,kutakiwa kufanya hivyo,ni agizo la nyumba ya maaskofu la kuundwa tume ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,kuchunguza tuhuma kumi zilizokuwa zinamkabili Dokta Mokiwa,pamoja na nyinginezo, za ukosefu wa maadili,ikiwemo kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika maeneo ya Buza,ikiwemo pia kutoa daraja la Ushemasi,Upadre,na Ukanon,kwa katibu wa Dayosisi,Mkristo ambaye ametengana na mkewe na kuoa mke mwingine kiserikali kinyume na kanuni ya kanisa kuhusu ndoa.

Waandishi wa Channel Ten,wamefika katika nyumba zinazodaiwa kutelekezwa na Dokta Mokiwa ikiwemo Silver Oak ya Upanga,na ya Mtaa wa Uganda Ostabei, ambapo imedaiwa kuwa ameiacha na kwenda kupanga huku kanisa likimlipa pango la shilingi milioni 3 kwa mwezi miaka zaidi ya miaka sita.

Dokta Mokiwa jana aligoma kupokea barua yake kutoka kwa Dokta Jacob Erasto Chimeledya,na baadhi ya waamini wa kanisa hilo katika nyakati tofauti,wamezungumzia hatua ya kutakiwa kujiuzulu na kustaafishwa Dokta Mokiwa.

Katika hatua nyingine,Dokta Valentino Leonard Mokiwa,kupitia kwa Afisa habari wake,Yohana Sanha,amedai kuwa mchakato uliotumika kumuhukumu ni batili na kwamba bado yeye ni Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam.

Viewing all 104670 articles
Browse latest View live




Latest Images