Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

'Askofu Mokiwa ana mashitaka ya jinai'

$
0
0
KATIBU Mkuu Kanisa la Anglikana Tanzania, Johnson Chinyong’ole amesema aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentine Mokiwa anakabiliwa na mashitaka ya jinai kwa kuingia mikatiba mibovu na matumizi mabaya ya fedha za kanisa makosa yanayoangukia kuvunja sheria za nchi.

“Hatujakurupuka kuchukua hatua, ushahidi wote tumeshauwasilisha kwa vyombo vinavyohusika serikalini, sisi tumetimiza wajibu wetu, hivyo tunaviachia vyombo vinavyohusika kufanya kazi yake katika eneo hilo la ubadhirifu wa fedha,” alisema Chinyong’ole.

Alifafanua kuwa wakati wanaenda kutangaza uamuzi wa kumvua uaskofu Dk Mokiwa juzi kanisa la Ilala, walienda kutoa taarifa kwa msajili wa vyama ambaye ndiye anayesajili makanisa, lakini pia wameshatoa taarifa katika ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

Alitaja sheria alizovunja Dk Mokiwa kuwa ni sheria ya miunganiko ya wadhamini sura ya 318, sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 na sheria ya mipango miji sura ya 355 kwa kuruhusu mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika shamba la kanisa la Mtoni Buza na eneo la Kanisa la Mtakatifu Mariam Kurasini.

“Sisi tunasubiri mrejesho kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Rita na kwa Msajili wa vyama vya kiraia,” alisema katibu mkuu huyo wa kanisa la Anglikana Tanzania.

Alifafanua kuwa katika mashitaka 10 anayokabiliwa nayo, shitaka la tatu ndilo ambalo ni la ubadhirifu wa mali za kanisa ndilo ambalo linaifanya serikali kuingilia kati.

Alisema makosa ya Dk Mokiwa yanahusisha pia kughushi na akatoa mfano wa kuingia mikataba kwa kuwatumia watu ambao si wadhamini wa kanisa hilo wakati sheria inamtaka atumie wadhamini wawili wanaosimamia mali za kanisa, pamoja na kutumika kwa muhuri bandia wakati sheria inasisitiza muhuri unaotumika ni ule wa moto.

Katibu Mkuu huyo alisema ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi ya askofu hiyo yenye kurasaa 173 imewasilishwa pia serikalini ili vyombo vinavyohusika kufuatilia tuhuma hizo viweze kujiridhisha wakati vinapoenda kuchukua hatua.

“Hakuna mtua aliyeonewa, wala kuchafuliwa, hizi ni tuhuma za ubadhirifu wa mali ya kanisa, lazima vyombo vya dola vihusike hapa,” alisema katibu mkuu huyo na kuongeza kuwa serikali ndio inayotakiwa kuchukua hatua kwa sababu tume iliyoundwa na kanisa imeshaweka hadharani ushahidi kwa lengo la kuokoa mali za kanisa.

Amevunja kiapo cha utii Kwa hali hiyo jambo hilo tayari wameliwasilisha kwa msajili wa vyama ambaye ndiye msajili wa kanisa hilo na pia wamewasilisha suala hilo kwa wakala wa vizazi na vifo (Rita) kwa kuwa sheria ya nchi iliyovunjwa ni ya udhamini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Chinyong’ole alisema kwa mujibu wa katiba ya kanisa hiyo ya mwaka 1970 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004, pamoja na Dk Mokiwa kugoma kung’oka madarakani baada ya kuvuliwa madaraka yake na askofu mkuu Dk Jacob Chimeledya, kwa sasa katiba haimtambui kama askofu wa kanisa hilo.

Alisema kabla ya marekebisho ya mwaka 2004, sinodi ya dayosisi ndio ilikuwa inakuwa na tamko la mwisho dhidi ya askofu wa dayosisi, lakini baada ya marekebisho kufanyika askofu mkuu ndiye msimamizi wa maaskofu wote wa dayosisi na ana mamlaka ya kuwastaafisha pale wanapokiuka katiba ya kanisa.

“Dk Mokiwa amenyang’anywa utawala wa dayosisi ya Dar es Salaam, katiba inampa mamlaka askofu mkuu kuwastaafisha maaskofu ikibainika wameenda kinyume cha sheria na katiba ya kanisa,” alisema Chinyong’ole.

Aliongeza kuwa baada ya kumvua utawala wa dayosisi, hatua inayofuata ni taratibu zingine za kisheria ambazo zitashughulikiwa na kanisa ikiwa ni pamoja na kumbana Dk Mokiwa kukiuka kiapo chake cha kumtii askofu mkuu wa kanisa.

Alisisitiza kuwa Dk Mokiwa amevunja kifungu namba 7 cha katiba ya kanisa hilo kuhusu kiapo cha utii kwa askofu mkuu aliposema

“Nakubali na kuahidi kumheshimu na kumtii, kama inipasavyo, askofu mkuu wa kanisa Anglikana Tanzania... watakaofuata baada yake...”

Katibu mkuu huyo alisema Dk Mokiwa kutokana na hatua yake kugoma kujiuzulu baada ya kushauriwa na askofu mkuu Tanzania, amevunja kiapo cha utii kwa katiba ya jimbo kinachosema,

“Ninaahidi pia kwamba nitakubali kujiuzulu au kujitoa kwa hukumu yoyote itakaoniachisha madaraka na mapato yanayohusika na dayosisi hii nitakayohukumiwa wakati wowote baada ya uchunguzi wa kutosha wa barza lenye kbali cha sinodi ya kanisa.”

Pia amevunja kiapo cha utii kwa katiba ya dayosisi kinachosema “Ninaahidi pia kwamba nijiuzulu wakati wowote kama ikiazimiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania kwa mujibu wa katiba ya kanisa na ya Dayosisi.”

Wachunguzi wa mambo wanabainisha kuwa kugoma kwa Dk Mokiwa kung’oka madarakani kutaleta mtafaruku mkubwa ndani kanisa hilo kutokana na baadhi ya makanisa katika Dayosisi ya Dar es Salaam kuunga mkono uamuzi wa askofu mkuu na wengine wanamuunga mkono Dk Mokiwa.

Juzi, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya alimvua uaskofu mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Mokiwa baada ya mashitaka 10 yaliyofunguliwa na walei 32 wa kanisa hilo katika dayosisi hiyo kumtuhumu kwa ufisadi wa mali za kanisa hilo.

Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya Askofu Mokiwa kugoma kujiuzulu kama ilivyoshauri nyumba ya maaskofu ambayo ilimkuta na hatia ya ufujaji wa mali za kanisa hilo na kukiuka maadili ya kiuchungaji ambayo yalibainishwa kwenye ripoti ya uchunguzi ya kanis ahilo nchini.

Hata hivyo, Dk Mokiwa amegomea uamuzi huo kwa maelezo kuwa, mwajiri wake ni Sinodi ya Dar es Salaam ambayo ndio yenye uamuzi wa kumfuta kazi na si askofu mkuu au askofu mwingine yeyote wa kanisa la Anglikana Tanzania.

Serikali yashtukia ubia na shule binafsi

$
0
0
WAMILIKI wa shule binafsi sasa wameomba kuingia ubia na Serikali ili wapewe ruzuku kuwezesha shule zao kudahili wanafunzi wa kidato cha kwanza, kwa maelezo kuwa shule hizo zitasaidia kuondokana na kero ya baadhi ya wanafunzi wanaofaulu kukosa nafasi katika shule za serikali.

Hata hivyo, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imekataa ombi hilo kwa maelezo kuwa serikali ina shule za kutosheleza mahitaji yaliyopo na haihitaji msaada wa shule binafsi katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika suala la vyumba vya madarasa.

“Serikali hatuna mpango wa kuingia ubia na shule binafsi katika kudahili wanafunzi wa kidato cha kwanza, sisi tumeamua kutoa elimu bure na tumeboresha mazingira ya shule zetu, wao wanaendesha shule zao kwa kulipisha na waendeshe peke yao,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila.

Ombi la Tamongsco Kupitia Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa shule na Vyuo visivyo vya Serikali (Tamongsco), wamiliki hao wameiandikia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuomba wizara iwashirikishe katika udahili wa wanafunzi 12,000 ambao wamefaulu mitihani ya darasa la saba mwaka jana, lakini kutokana na ukosefu wa madarasa hawataweza kwenda kidato cha kwanza.

“Kila mwaka tunaiomba Serikali ituondolee kodi, badala yake shule binafsi zipewe ruzuku ili watoto wanaokosa nafasi za kusoma katika shule za Serikali kila mwaka wapate elimu hiyo katika shule binafsi kwa mikataba maalumu ya ubia wa sekta ya umma na binafsi,” alisema Katibu Mkuu wa Tamongsco, Benjamin Nkonya katika barua yao waliyoiwasilisha wizarani.

Nkonya alisema baadhi ya madarasa katika shule zisizo za serikali hayana wanafunzi wakati madarasa katika shule za serikali yamefurika wanafunzi hadi 200 kwa darasa moja, jambo ambalo shule hizo binafsi zinaona kwamba ni kuwaweka katika mazingira mabovu kabisa ya kujifunzia na kufundishia wanafunzi hao.

Katibu Mtendaji huyo alisema kama Serikali inatoa ruzuku kwa hospitali binafsi, ifanye hivyo pia kwa shule binafsi za sekondari ili watoto wote wa kitanzania waweze kupata elimu kwa usawa. Majibu ya Serikali

Profesa Msanjila alisema kwamba Serikali imeamua kuboresha shule zake na kutoa elimu bure, jambo ambalo limewavutia wananchi wengi na sasa wanapeleka watoto wao katika shule za serikali tofauti na miaka ya nyuma.

Alisema kutokana na hali hiyo serikali haina mpango wa kuingia ubia na shule binafsi, badala yake itaendelea kutoa miongozo ya elimu inayoelekeza sera za elimu zinazotakiwa kufuatwa na shule ambazo sio za serikali na sio kuingia nazo ubia katika kudahili wanafunzi.

“Hawa tulitaka kuweka ada elekezi, lakini walitumia wanasiasa kupinga, kwa madai kwamba tunaingilia elimu ambayo serikali haihusiki, jambo hilo serikali imeamua kuachana na nalo ili soko liweze kuamua,” alisema Profesa Msanjila.

Aliongeza kuwa serikali imekuwa inaingia ubia katika sekta ya afya katika wilaya au mkoa ambako hakuna hospitali kubwa ya serikali na hivyo kulazimika kuingia ubia na hospitali binafsi au za mashirika ya dini zilizoko katika wilaya hizo.

“Sasa kwenye sekta ya elimu, serikali ina shule kila kata na kila kijiji, sasa huo ubia wanaotaka tuingie kwa sababu zipi? Hakuna sehemu ambako serikali haina shule,” alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo.

Alisema baada ya kukataa ada elekezi, serikali iliona kuwa shule hizo zisizo za serikali zinafanya biashara na hazitoi huduma kama zinavyodai ndio maana zinalipa kodi zote zinatakiwa kulipwa na kampuni nyingine inayofanya biashara.

“Baada ya kukataa ada sisi tuliona kwamba hawa wanafanya biashara, hivyo lazima waendelee kulipa kodi maana hawatoi huduma,” alisema Profesa Msanjila.

Mtazamo wa Tamongsco Alisema Tamongsco inaona kwamba kuwasubirisha wanafunzi wengi hivyo kwa muda uliotajwa na serikali wa kujenga madarasa ndipo wajiunge na kidato cha kwanza kutasababisha malengo ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kutofikiwa.

Katika andiko hilo ambalo limesainiwa na Katibu Mtendaji wa Tamongsco, wanadai kwamba ubia wa sekta ya umma na binafsi katika sekta ya elimu umeleta mafanikio makubwa nchini Uganda ambako serikali inatoa ruzuku kwa shule binafsi ambazo ni asilimia 80.

“Tuna ushahidi kwamba nchi nyingine nyingi duniani hutumia mifumo hii ya PPP na hufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu kuliko gharama ambayo serikali ingetoa bila kutumia mfumo wa PPP,” linasema andiko hilo la Tamongosco.

Wamiliki hao walisema kutokana na tofauti za wamiliki wa shule zetu, wamependekeza njia za ushirikiano kati ya sekta ya umma na isiyo ya umma zitumike katika kuondoa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi 12,422 waliokosa nafasi katika shule za serikali na wale watakaokosa kwa miaka ijayo.

Miongoni mwa njia hizo ni Mfumo wa Udahili Uliowianishwa ambao lengo lake ni kuondoa uwezekano wa mwanafunzi mmoja kudahili zaidi ya mara moja.

Kama ilivyo katika vyuo vikuu. Pia Serikali itenge kiasi cha fedha kwa mwanafunzi mmoja. Shule husika itatoza ada ya ziada kwa makubaliano na serikali.

Njia nyingine ni udhamini katika utaratibu huu, ikokotolewe gharama halisi ya kumsomesha mwanafunzi mmoja kwa mwaka katika shule ya serikali kwa kila kanda kwa kuzingatia nguvu ya fedha ya mahali husika na serikali itoe fedha hizo.

Producer Mr T Touchez Atoboa Siri ya Ngoma zake Kutamba Wakati Huu

$
0
0

Licha ya kufanya ngoma nyingi kali na kubwa mwaka 2016 Producer Mr T Touchez amefunguka na kusema kuwa bado hajafikia malengo yake kwani malengo yake kwenye muziki huu wa bongo fleva ni makubwa zaidi. .
.

Akiongea na EATV MR T Touchez amesema kipindi cha nyuma alikuwa anafanya ngoma kali na hits lakini kipindi hicho alikuwa bado hajalisoma game linataka nini na watu wanataka nini lakini sasa hivi ameshaweza kusoma watu wanapenda nini na game lipoje ndiyo maana kwake inakuwa rahisi sana kutengeneza hits song na kubadili muziki wake awezavyo na bado akaendelea kutoa ngoma kali tu.
.
. "Mwanzo nilikuwa nafanya muziki lakini nilikuwa silisomi 'game' japo nilikuwa naweza kutengeneza hits nyingi lakini si kama ilivyo sasa naweza kusema nataka kutengeneza hits song, au nataka kutengeneza idea ya muziki flani na nikaipeleka ikatiki kutokana na mimi kuisoma vizuri game na kuwa na juhudi zaidi katika kazi nazofanya kwa sababu nilikuja kugundua sijawa mkubwa kama vile mimi nataka kuwa, mpaka saizi bado sijakuwa vile mimi nataka sababu nina malengo makubwa tofauti na haya watu wanayaona" alisema @mrttouchez
#letitshine

Serikali Yaagiza Waliomchapa Viboko Mwanamke Mbele za Watu Wachukuliwe Hatua

$
0
0

Serikali imeviagiza vyombo vyake vya kiuchunguzi kufuatilia chanzo cha picha inayoonyesha mwanamke mmoja akichapwa viboko mbele ya mkutano.

Aidha vyombo vya dola vimetaiwa kufanya uchunguzi ndani ya muda mfupi na kutoa taarifa rasmi na Serikali haitasita kutoa adhabu kali kwa wote waliohusika.

Zimetajwa Aina 10 bora za magari ya kisasa zaidi duniani

$
0
0

Magari ni kati ya vitu vinaundwa kwa ubunifu mkubwa zaidi duniani, magari yamekuwa yakifanya dunia kuwa sehemu rahisi kufikika kwa haraka ingawa ni kwa maeneo yenye barabara tu. Magari sio tena hitaji la wanaume pekee, hata wanawake wanamiliki magari mazuri na ya kisasa kila siku. 

Leo nimekutafutia hii taarifa kuhusu vitu vya kujua kwenye magari; vipo vingi kuanzia kwenye aina ya gari unalotaka kununua, uimara wake, kampuni inayotengeneza n.k; nyingi zimekuwepo tangu zamani sana, na zimekuwa zikishindana kila siku kuunda magari ya kisasa.

Nimekukusanyia hapa leo kampuni 10 zilizotajwa kuwa bora zaidi kwenye kuunda magari ya kisasa duniani. 

10. BMW

Inawezekana ulikuwa haufahamu nini kirefu cha herufi hizi tatu “BMW”, hii inasimama badala ya maneno “Bavarian Motors Work”kampuni ya kuunda magari iliyoanzishwa mwaka 1916 na waanzilishi wake ni marafiki watatu Franz Jozef Popp, Karl Rapp,na Camillo Castiglino; kutoka nchini Ujerumani, BMW haikuanza kama kampuni ya kuunda magari, ilikuwa ikizalisha Injini za ndege.

Baadaye ikaanza kuunda magari na pikipiki zenye speed kubwa. Sasa hivi, magari yanayoundwa na BMW yamekuwa yakitajwa kuwa kati ya magari ya starehe na imara duniani.



9. Mercedes-Benz

Mercedes-Benz pia ni kampuni ya kuunda magari kutoka Ujerumani na ilianzishwa mwaka 1926 na marafiki wawili ambao niGottlieb Daimler pamoja na Karl Benz. Inafahamika sana kwa kuunda magari ya kisasa na starehe, magazi ya mizigo, na mabasi ya abiria. Mercedes-Benz ni kampuni inayounda magari yenye uwezo kugundua kitu kinachosogea karibu yake wakati wa usiku, jambo linalofanya dereva kujiupusha na ajali.

Mbali na sifa za Mercedes-Benz kuwa moja kati ya makampuni yanayounda magari ya kisasa duniani, pia ina sifa ya kuunda magari yanayotajwa kuwa na usalama zaidi kwa watumiaji wake. 


8. Audi

Hapa tena ni aina ya gari ya Kijerumani inaingia kwenye list, Audi. Hii ilianzishwa mwaka 1909 na fundi makenika ajulikanaye kama August Horch. Tafsiri ya Kilatini, Audi ina maana ya “Sikia”, ambayo ni sawa na Kijerumani “Horch”. Jina Audi linawakilishwa na maduara manne kwenye Logo ya magari hayo ambayo yanaundwa na kampuni nne na ndio sababu za kuwekwa maduara manne kwenye Logo yake. 

Audi inatajwa kuwa moja kati ya magari mazuri na ya kisasa, salama na yenye gharama pia; Na katika kuthibitisha hilo, Audi ilikuwa kampuni ya kwanza ya kuunda magari duniani kufanya majaribio ya magari yake kwenye ajali makusudi ili kujua yanaharibika kiasi gani. 


7. Bugatti

Bugatti ni kampuni ya kuunda magari iliyoanzishwa na raia wa Italy aitwaye “Ettore Bugatti” na kwa mara ya kwanza ilianza kuunda magari nchini Ufaransa mwaka 1909. Aina hii ya magari ilipata umaarufu wa kuunda magari yenye speed zaidi duniani pia walihusika na kuunda ndege.

Wanarekodi pia ya kuwa kampuni kongwe zaidi ya uundaji magari; Bugatti wana sifa nyingine kuwa na magari yenye starehe zaidi na ya kipekee. Gharama sio jambo la kushangaa unapouliza bei za magari ya Bugatti na mwaka 1956 Bugatti waliingiza sokoni magari zaidi ya 8000, kitu ambacho kinaweka idadi ya kuwa wameshatengeneza zaidi ya magari 100,000 yaliyoko kwenye matumizi kote duniani.


6. Lamborghini

Lamborghini pia ni kampuni iliyoanziwa na fundi Muitaliano aitwaye “Ferruccio Lamborghini” mwaka 1963. Mwanzo kabisa kampuni hii ilikuwa ikiunda Matrekta kwaajili ya shughuli za kilimo. Baada ya Lamborghini kufariki mwaka 1993, kampuni hii haikuwa tena ya mtu binafsi, mwaka 1998, iliungana na kampuni nyingine mbili Audi pamoja na Volkswagen.


5. Ford

Ford Motor Company ni moja kati ya makampuni ya kuunda magari yanayoheshimika sana duniani ikiwa ni kampuni kongwe zaidi ya Kimarekani inayounda magari yenye sifa ya uimara. Kampuni hii ilianzishwa na Henry Ford mwaka 1903. Kitu cha kushangaza kuhusu Ford kwa kipindi cha miaka 6 haikuwahi kutengeneza magari yenye rangi  nyeusi.

Hayo yalikuwa maamuzi ya mmiliki wake, Henry Ford aliyekuwa akifanya kazi kama Engieer kwenye kampuni ya Edison Illuminating Company akiwa kama Mhandisi Mkuu. Kama ilivyo historia za makampuni mengi ya uunndaji magari, Ford pia walikuwa wakiunda ndege; na kampuni yake iliitwa Ford Airplane Company, lakini haikufanikiwa kupata faida kitu kilichofanya ifungwe kabla haijasababisha hasara.


4. Ferrari

Ferrari pia ni kampuni ya Kiitaliano ambayo imejikita kwenye kuunda magari yanayotumiwa kwenye michezo ya mbio za magari. Kampuni hii ilianzishwa na fundi makenika aitwaye “Enzo Ferarri” mwaka 1939. Ferarri ilianzishwa na mvulana wa miaka 10 tu mwenye jina la Enzo, ambaye alikuwa mpenzi wa mbio za magari aliyekuwa na ndoto za kuja kumiliki kampuni yake na alitimiza ndoto yake.

Brand ya Ferrari inarekoi ya kuwa kampuni inayozaliwa magari ya michezo yenye gharama kubwa, speed, ya kisasa na imara zaidi ya muda wote duniani. Ile logo ya njano yenye picha ya Farasi kwenye magari ya Ferrari ilikuwa inatumiwa na kamanda wa kwanza kutoka jeshi la Italy wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia, Francesco Baracca.

Wakati huo Enzo Ferrari alimuomba Baracca aitumie logo hiyo ili kumtangaza kama mtu mwenye bahati; sasa miaka kadhaa baada ya kifo cha Kamanda wa jeshi Baracca logo hiyo imekuwa ni utambulisho rasmi wa magari ya Ferarri.


3. Porsche

Porsche pia ni kampuni iliyonunuliwa na kampuni ya Kijerumani ya Volkswagen Group.Ilianzishwa mwaka 1931 na fundi mitambo Ferdinand Porsche. Ikiwa moja kati ya kampuni maarufu za kuunda magari, Porsche pia haikuanzia kwenye kutengeneza magari, ilikuwa ikifanya kazi ya kushauri namna nzuri ya kuunda magari.

Miaka 10 baadaye, ikajikita kwenye kuunda magari yanayotumika kwenye michezo. Magari ya Porsche yameweka rekodi  ya kushinda karibia mashindano zaidi ya 30,000 ya mbio za magari, kiwango ambacho hakuna kampuni au brand yoyote ilifikia rekodi hiyo mpaka sasa. Porsche wanajulikana kwa kuwa na magari ya kipekee duniani.



2. Bentley

Bentley Motor Limited, inafahamika zaidi kwa jina la Bentley, ni kampuni ya kuunda magari iliyoanzishwa na raia wawili ambao ni ndugu kutoka Uingereza H. M. Bentley na Walter Owen Bentley mwaka 1919, na baadaye ikanunuliwa na Volkswagen Group mwaka 1998.

Bentley wamejiwekea rekodi ya kuunda magari ya kisasa na mengi yamekuwa yakitumiwa na watu maarufu wakiwemo mastaa wa muziki, filamu, michezo, viongozi wa taasisi n.k.Bentley pia ni kati ya brands zinazoongoza kwa kutoa misaada kwenye maeneo mbalimbali duniani.



1. Volkswagen

Volkswagen, inajulikana kwa ufupisho wa jina lake kama ‘VW’, hii ni gari inayotengenezwa na kampuni kutoka Ujerumani ambayo ilianzishwa mwaka 1937 na chama cha wafanyakazi cha German Labour Front. kitu cha kushangaza kuhusu Volkswagen ni kwamba wazo la kuundwa kwake liliwekewa mkazo na mtawa wa mabavu, Adolf Hitler.

Tafsiri ya neno Volkswagen ni ‘Gari ya Watu’, na slogan yake ni ‘Das Auto’ ikiwa na maana ya ‘Gari’ kwa lugha ya Kijerumani, kinachobebwa kwenye maneno yote hayo ni kumaanisha kwamba gari yao ni mfano sahihi wa jinsi gari inavyotakiwa kuwa.

Inasemekana Volkswagen ndiyo kampuni ya kuunda magari ambayo ni kubwa kuliko zote kwasasa. Kingine ni kwamba VW wanashikilia rekodi ya kuwa kampuni inayounda magari ya kisasa zaidi duniani, pia wanaunda magari ya mizigo; sio tu kubeba mizigo magari yake makubwa yanauwezo wa kufanya mashindano ya mbio.

Ozil otoa sharti la kubaki Arsenal

$
0
0
Mesut Ozil yuko tayari kusaini mkataba mpya na Arsenal lakini anataka kujua kama meneja Arsene Wenger atabaki kwenye klabu hiyo baada ya mwisho wa msimu huu.

Ozil (kushoto) na Wenger kwenye mazoezi

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni wa msimu huu wakati mikataba ya Ozil na mchezaji mwenzake Sanchez inamalizika baada ya miezi 18.

Ozil amesema kuwa anafurahi sana kubaki kwenye klabu ya Arsenal na amewaambia viongozi wa timu hiyo kuwa angependa kuongeza muda wa mkataba wake.

"Nina furaha sana ndani ya Arsenal na nimeiacha klabu itambue hilo kwamba nipo tayari kusaini mkataba mpya."Alisema Ozil akiongea na waandishi wa habari za michezo za Ujerumani.

"Mashabiki wanataka nibaki na sasa ni uamuzi wa klabu.

"Wanajua kwamba nipo hapa kwa sababu ya Arsene Wenger. Yeye ndiye aliyenileta na yeye ndiye anayeamini nilichonacho. Klabu pia inajua kwamba nataka kuwa muwazi na kile meneja anataka kufanya."

Wakenya wamsuta Rais Kenyatta mtandaoni

$
0
0
 Rais Kenyatta akizindua daraja

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakimsuta Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufuatia hatua zake za kuzindua miradi.

Wakosoaji wanasema kuwa baadhi ya miradi ilizinduliwa na Rais Kenyatta ilikuwa ikiendelea au tayari ilikuwa imezinduliwa.

Wengine nao wanasema kuwa hatua hiyo iko chini ya hadhi ya rais.

Wiki iliyopita bwana Kenyatta ambaye atawania urais tena mwezi Agosti alikuwa mjini Mombasa ambape alizindua daraja.

Baadhi wa watumiaji wa mtandao wa Twitter wametumia uzinduzi huo kama chanzo cha kumsuta rais.

Wakitumia #UhuruChallenge, wamechapisha mifano yao ya vitu walikuwa wakizindua.
 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta
 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta
 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta
 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta
 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta
 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta

Maeneo kadha ukiwemo mji mkuu Nairobi, pwani na maeneo ya kaskazini mwa nchi yamekuwa yakikumbwa na ukoseu wa nguvu za umeme hali iliyosababisha rais kusutwa zaidi

Wafanyabiashara ya ‘unga’ wabadili mbinu

$
0
0
Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya kwa kusafirisha na kuingiza nchini, vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kifua) aina ya ephedrine kisha kuvitumia kutengeneza kokeni na heroini.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Dawa za Kulevya, Mihayo Msikhela alisema jana kwamba wafanyabiashara hao husafirisha kemikali hizo kutoka Bara la Asia na wanapozifikisha nchini huzitumia kutengeneza dawa hizo za kulevya.

“Hivi vibashirifu aina ya ephedrine mara nyingi vinatumika kutengenezea dawa za kifua lakini hawa wafanyabiashara haramu wanabadilisha mfumo wake. Wanachofanya wanachanganya na kemikali nyingine ambazo wanatengeneza dawa aina ya heroini na kokeni,” alisema.

Pia, alisema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha Serikali na hudanganya kuwa zitatumika kutengeneza dawa za kifua

Tishio la njaa bei ya vyakula hazikamatiki, wananchi washindia maembe

$
0
0
UKAME, njaa kila kona. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maeneo mengi ya nchi kukumbwa na njaa ambayo imesababishwa na kukosekana mvua muda mrefu.

Baadhi ya mikoa haikupata kabisa mvua za masika na zile za vuli, huku maeneo mengine zikinyesha chini ya wastani.

Katika maeneo hayo, kuna njaa na ukame mkali, mifugo imeanza kufa na wananchi wakishindia maembe kama mlo wao wa siku.

Wakati hali ikiwa hivyo, Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa mkoani Ruvuma wiki iliyopita, iliagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutunza akiba iliyopo hadi msimu ujao wa mavuno.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA kwa baadhi ya mikoa na wilaya, umebaini kuwapo uhaba mkubwa wa chakula, huku mifugo nayo ikikosa malisho na maji jambo ambalo linazidisha uwezekano wa mifugo mingi kuendelea kufa kwa njaa.

Katika Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani na Morogoro ambako kuna wafugaji wengi, ng’ombe zaidi ya 1,000 wameripotiwa kufa kwa njaa.

Kutokana na tatizo hilo, baadhi ya wafugaji wametishia kujiua baada ya kushuhudia mifugo yao ikifa mfululizo kwa kukosa chakula.

Mmoja wa wafugaji katika Kitongoji cha Chaua, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze, Hamisi Meya, aliliambia MTANZANIA kuwa amepoteza ng’ombe zaidi ya 100, wakati mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Karanga kutoka Mdaula, Bagamoyo, akipoteza ng’ombe 220 waliokufa hivi karibuni.

“Hali ni mbaya, baadhi ya wenzetu wanataka kujiua baada ya kushuhudia mifugo yao ikiteketea kwa kukosa chakula na maji.

“Kibaya zaidi, hawa ng’ombe sasa hawauziki, hawana nyama, wamekonda mno, hawawezi hata kutembea, ni hasara kubwa kwetu… sijui ni msaada gani unaweza kutusaidia, tunaelekea kurudi kwenye umasikini, tunamwomba Mungu atupe mvua ili tuponyeshe mifugo yetu,” alisema Meya.

Mfugaji mwingine, Mzee Malimingi wa Kijiji cha Gumba, alisema amepoteza ng’ombe zaidi ya 300 kutokana na ukame.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Chaua, Rashid Maisha, aliliambia gazeti hili kuwa njaa imetokana na ukame wa muda mrefu ulioikumba Chalinze tangu Aprili, mwaka jana.

“Tunategemea zaidi kilimo cha mahindi ambacho kinahitaji mvua za kutosha, tangu Aprili, mwaka jana hatukupata mvua na hata mazao tuliyopanda yaliishia njiani, kilo moja ya sembe inauzwa kati ya Sh 1,600 na 1,700.

“Familia nyingi hivi sasa zinashinda na kulala njaa, ukipatikana unga kidogo watoto wanakorogewa uji, tunaomba Serikali itusaidie chakula vinginevyo baadhi ya watu wasiokuwa na uwezo watakufa,” alisema Maisha.

RIDHIWANI KIKWETE

Akizungumzia hali hiyo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete (CCM), alikiri kuwapo njaa katika jimbo lake.

Alisema unahitajika msaada wa dharura kunusuru hali hiyo.

“Nimekuwa kwenye ziara ya kukagua jimbo langu, nimebaini hali inatisha, njaa ni tishio. Kibaya zaidi wanaochunga mifugo wamechoka sambamba na mifugo yao, bei ya vyakula inazidi kupaa zaidi.

“Tumejaribu kutafuta ufumbuzi kupitia Halmashauri ya Chalinze, tumeomba tani 1,421 za mahindi, tumefanikiwa kupata 600, kati ya hizo tani 250 tumezitawanya kwa kaya masikini sana na zilizobaki tumezisambaza sokoni zinauzwa kwa bei ya chini kidogo,” alisema Ridhiwani.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, alikiri kuwapo njaa na ukame, huku akiahidi kutoa ufafanuzi.

“Niko safarini, unaweza kuja ofisini kuanzia Jumatatu (jana), nitakuwa na nafasi nzuri ya kulitolea ufafanuzi sula hilo,” alisema Mwanga.

MOROGORO

Mkoani Morogoro, zaidi ya ng’ombe 15,000 wamekufa katika vijiji vitano wilayani Mvomero kutokana na ukame.

Katika vijiji vya Dakawa, Sokoine, Kambala, Mera na Melela, MTANZANIA lilishuhudia baadhi ya wafugaji wakilalamikia mifugo yao kuanguka na kufa baada ya kukosa chakula na maji.

Katibu wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Morogoro, Kochocho Mgema, alivitaja vijiji vilivyoathirika zaidi na ukame na idadi ya ng’ombe waliokufa kwenye mabano ni Dakawa (2,723), Sokoine (4,246), Kambala (1,328), Mera (1,284) na Melela (1,057).

Kwa upande wa Wilaya ya Kilosa,  Mgema alisema zaidi ya ng’ombe 3,328 wamekufa.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha  Wafugaji Taifa (CCWT), Joshua Lugasi, aliiomba Serikali kutangaza ukame kama janga la Taifa kutokana na hali halisi ilivyo.

Aidha wafugaji hao wameitaka Idara ya Hali ya Hewa (TMA) kutoa taarifa sahihi na kuhakikisha zinawafikia wadau kwa wakati ili waweze kufanya shughuli zao kwa tahadhari.

TAHARUKI 

Baadhi ya wakulima katika maeneo ya Malinyi, Morogoro, Gairo, Mvomero na Ulanga, wamedai kama hali ya ukame itaendelea, inaweza kusababisha maafa makubwa.

Mkazi wa Kilombero, Said Timbuko, alisema ni jambo la kawaida kwa kaya kula mlo mmoja, huku mfumuko wa bei za vyakula ukizidi kushika kasi.

“Mfuko wa kilo 25 za sembe tulikuwa tunanunua Sh 18,000, sasa umepanda mpaka Sh 35,000,” alisema.

Alisema bei hiyo ya kilo hizo 25 za sembe uuzwa mjini, lakini kwa wilayani imefika hadi Sh 40,000.

MA-DC

Wakizungumzia hali hiyo, wakuu wa wilaya za Mvomero, Ulanga, Malinyi na Kilosa, walisema ukosefu wa mvua katika misimu husika ndiyo chanzo cha ukame.

Hata hivyo, wamewaomba wananchi  kujenga tabia ya kulima mazao yenye  kustahimili ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

ARUSHA

Mkoani Arusha, mahindi na mchele vimeadimika, huku mifugo ikidhoofu na mingine kufa.

Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda na wanyamapori, wameanza kufa kutokana na kukosa malisho na maji baada ya mito, vijito na mabonde yenye maji kukauka.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini bei ya kilo moja ya unga wa sembe na dona katika Soko Kuu la Arusha na Kilombero, inauzwa kati ya Sh 1,600 na 1,800, wakati debe moja la mahindi likiuzwa Sh 15,000 na gunia la kilo 100 Sh 90,000 hadi 110,000.

Masoko ya Arusha na Kilombero, mchele unauzwa Sh 2,200 hadi 2,400 kwa kilo moja, huku mazao mengine kama ngano, maharagwe, mbaazi na kunde nayo yakipanda bei na kusababisha sintofahamu kwa wananchi.

Katika Kijiji cha Kitumbeine wilayani Longido, wananchi wanalazimika kubadilishana mbuzi mmoja mkubwa mwenye thamani kati ya sh 40,000 na 50,000 kwa debe moja la mahindi.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo, alionyesha hofu yake na kuomba Serikali kupeleka chakula ili wananchi wakinunue kwa bei nafuu, baada ya kuuza mifugo yao wakati huu ambao bado mifugo haijadhoofika zaidi.

Akizungumza na MTANZANIA, Mkurugenzi wa Kampuni ya usagishaji na usafirishaji nafaka ya Monaban, Dk. Philemon Mollel, alisema hali katika ghala lake ni mbaya na amebakiwa na tani 2,000 tu kiasi ambacho hakitoshelezi mahitaji.

“Kinga ni bora kuliko tiba, hali ni mbaya, tunaomba Serikali iruhusu tuagize chakula kutoka nje ya nchi ili kuokoa maisha ya Watanzania.

“Pia tunaomba kodi na ushuru wote ufutwe kwenye chakula kilichoko nchini na kile kitakachoingizwa kutoka nje na wafanyabiashara wasiwekewe vikwazo na ucheleweshaji usio wa lazima,” alisema.

Baadhi ya wakulima wa Kata ya Mang’ola wilayani Karatu, walidai upatikanaji wa chakula na hasa mahindi ni mbaya ikilinganishwa na mwaka juzi.

Mkulima Samweli Basso, alisema bei ya gunia la mahindi katika kata hiyo imefikia Sh 70,000 hadi 75,000.

DODOMA

Juma Matokeo ambaye ni mfanyabiashara mkoani Dodoma, alisema Juni, mwaka jana, bei ya mchele ilikuwa kati ya Sh 1,200 na 1,400 kwa kilo moja mkoani Shinyanga, ikiwa ni bei ya jumla huku wao wakiuza kwa Sh 1,500 hadi 1,600 bei ya rejareja.

MTWARA

Meneja wa Umoja wa Ushirika wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mtwara, Said Namata, alisema wakulima wengi wameweka kipaumbele katika kilimo cha mbaazi, hivyo kusababisha kuadimika kwa zao la mahindi.

Alisema mwaka jana pekee, wakulima waliuza mbaazi kwa wastani wa Sh 3,000 na 4,000 kwa kilo moja hivyo waliacha kulima mahindi.

Naye Rajabu Hamis mfanyabishara wa Soko kuu Mtwara alisema mfuko wa kilo 25 wa unga wa sembe unauzwa Sh 40,000 badala ya Sh 27, 000 bei ya zamani.

RUVUMA

Mwananchi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema pamoja na Mkoa wa Ruvuma kulima mahindi, hatua zinapaswa kuchukuliwa, hasa maeneo ya vijijini.

Kilo moja ya mahindi inauzwa wastani wa Sh 730 na 750.

TANGA

Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini bei ya gunia moja la mahindi Tanga mjini linauzwa kati ya Sh 95,000 hadi Sh 97,000 badala ya Sh 67,000 za awali kutokana na kuadimika.

Mfuko wa sembe wa kilo 25 ulikuwa ukiuzwa kati ya Sh 25,000 na 24,000 lakini hivi sasa unauzwa Sh 30,000 hadi 27,000 na ile ya kilo 50 iliyokuwa ikiuzwa Sh 50,000 na Sh 55,000 hivi sasa inauzwa hadi Sh 60,000.

PANGANI

Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi, John Semkande (CCM), alisema mchele unauzwa kilo moja Sh 2,400 wakati awali uliuzwa Sh 1,600, sembe Sh 1,400 badala ya Sh 1,000 na 1,200.

Alisema sababu kubwa inayosababisha hali hiyo ni ukame ambao umechangia kukosekana kwa mahindi.

LUSHOTO

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Malibwi wilayani Lushoto, Mwinjuma Salehe (CCM), alisema hali ya chakula si nzuri kwani unga wa sembe umefikia Sh 1,500 badala ya Sh 1,200 za awali.

Kutokana na hali hiyo, Salehe aliwataka viongozi wa Serikali wilayani humo kuwa wakweli na wawazi kuwaeleza ukweli viongozi wa kitaifa badala ya kukaa kimya na kuogopa kutumbuliwa, huku wananchi wakizidi kuumia.

KILINDI

Wakazi wa Vijiji vya Mvungwe, Kwamba, Kwekivu, Tunguli na maeneo mengine katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, wanakula maembe kama mlo wao wa siku.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, Musa Semdoe, alikiri kuwapo njaa katika baadhi ya maeneo, lakini akasema wamejipanga kukabiliana nayo.

“Ni kweli njaa ipo, tumejipanga kuwapelekea mbegu zitakazovumilia ukame ili ziweze kuwasaidia kukabiliana na njaa hiyo,” alisema.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo, alisema wilaya hiyo haina njaa kama inavyoelezwa na baadhi ya wananchi.

HANDENI

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alisema mabadiliko ya tabianchi yamesababisha wakulima kupata mavuno kidogo.
Alisema kwa wastani wilaya hiyo inazalisha tani 81,000 za mahindi, kunde na muhogo, lakini mabadiliko hayo
yalisababisha ukosefu wa mvua na kuzalisha tani 47,000 pekee.

 IRINGA

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Asia Abdalah, amepiga marufuku utengenezaji wa pombe za kienyeji zinazotumia mahindi (komoni) ili kujihami na njaa inayotishia kuikumba wilaya hiyo.

Kwa kawaida wakulima wilayani humo huanza kuvuna mahindi mabichi kati ya Januari na Februari,  lakini hali imekuwa tofauti    kwani  mahindi yamekauka kabla ya kuzaa.

Mwenyekiti  wa  Kitongoji  cha  Kimala,  Barnabas Nyamoga,   alisema  wananchi  wamejitahidi  kulima, lakini mazao yao  yameishia  kukauka.

Mbunge  wa   Kilolo, Venance Mwamoto (CCM), amewataka watendaji  wa kata zote za  Kilolo  kutoa taarifa  mapema juu ya wananchi wanaokabiliwa na njaa ili  waweze  kusaidiwa na Serikali.

KANDA YA ZIWA

Wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameomba viongozi wa wilaya na mikoa yao kufikisha haraka ujumbe wa njaa Serikali kuu ili iweze kuwapatia chakula cha msaada.

Ili waweze kuweka msisitizo wao, wananchi hao walitumia mabango ya mabua ya mahindi yaliyokauka kumwonyesha Mkuu wa Mkoa, John Mongella hali halisi ya ukame.

Hali hiyo imetokana na ukame wa muda mrefu ambao umesababisha mazao yote kukauka, huku bei za vyakula zikipanda kila kukicha. Gunia la mahindi linauzwa kati ya Sh 100,000 na 125,000.

Akizungumzia hali hiyo, Mongella alisema kilio cha njaa ni kikubwa katika maeneo mengi ya wilaya za mkoa wake, hivyo aliahidi kutuma timu kufanya utafiti wa hali ya chakula.

KWIMBA

Wananchi wa Kijiji cha Mwabilanda wilayani Kwimba, wakiongozwa na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), juzi walimpokea kwa mabua ya mahindi yaliyokauka Mkuu wa Mkoa, Mongella na kuonyesha ukubwa wa tatizo la njaa.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mtemi Msafiri, alisema wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula unaotokana na ukame, hivyo kutishia uhai wa wananchi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Solwe, Joseph Nkonoki, alisema hali ya chakula kijijini hapo ni mbaya.

UKEREWE

Mbunge wa Ukerewe mkoani Mwanza, Joseph Mkundi (Chadema), ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kuchukua hatua haraka ili kuwanusuru wananchi.

Alisema hali ni mbaya na tayari dalili zimeanza kuonekana na kuwataka viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa kuacha kuogopa kauli ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwatumbua iwapo watasema ukweli.

Gunia la mahindi wilayani Ukerewe linauzwa kati ya Sh 105,000 na 120,000 tofauti na mwaka jana ambapo lilikuwa linauzwa kati ya Sh 70,000 na 80,000.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomihn Chang’ah, alisema  wananchi wake wanayo akiba ya kutosha ya chakula huku akiwasisitiza kupanda mazao yanayostahimili ukame.

SENGEREMA

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,  Emmanuel Kipole, alisema hali ya chakula si nzuri kutokana na ukame unaoendelea hivi sasa.

Aliwataka wananchi kutunza akiba ya chakula walinacho, huku akisisitiza walio na fedha kununua chakula sokoni ili kukitunza kwa matumizi ya baadaye.

ILEMELA

Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema licha ya ukame kuwapo, hali ya chakula ni nzuri kwani wakazi wote wanakwenda kukinunua soko kuu la Mwanza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk. Leonard Maselle, alikataa kuzungumzia suala hilo.

SIMIYU

Serikali mkoani Simiyu, imewahakikishi wananchi kuwa hakuna mtu atakayekufa kwa njaa, licha ya kukumbwa na upungufu wa mvua msimu huu wa kilimo wa 2016/2017.

BUNDA

Bei ya mahindi katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imepanda kutoka Sh 14,500 kwa debe moja hadi kufikia Sh 20,000, huku unga wa muhogo (udaga) ukipanda kutoka Sh 12,500 hadi 17,500.

Nafaka nyingine kama mtama zimepanda kutoka Sh 10,000 hadi Sh 17,500 kwa debe, wakati ulezi unauzwa  Sh 30,000 kwa debe moja.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA, maeneo mbalimbali, unaonyesha bei ya chakula imepanda kuanzia Agosti na Septemba, mwaka jana.

Diwani wa Kata ya Nyamuswa, Fyeka Sumera, alisema wakazi wa kata yake wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.

MUSOMA

Mkuu wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Dk. Vicent Naano, alisema hali ya chakula si mbaya, licha ya mvua kuchelewa kunyesha na chakula kinapatikana sokoni.

Mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Mathayo (CCM), alisema hali ya chakula si nzuri na hatua madhubutu zinapaswa kuchukuliwa mapema.

TARIME, RORYA

Diwani wa Kata ya Kitembe, Thomas Lisa (Chadema), alisema hali ni mbaya, lakini cha kushanagza ni pale wakuu wa wilaya wanaposhindwa kuweka wazi kwa hofu ya kutumbuliwa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Dagopa, Kijiji cha Nyambogo, Kata ya Kitembe wilayani Rorya, Elias Amara, alisema hali ya chakula ni mbaya na wanaomba Serikali ipeleke chakula cha msaada.

KAGERA

Wakazi wa Bukoba mkoani Kagera, wamesema hali ya chakula ni mbaya kutokana na ukame.

Wamesema wanategemea zao pekee la ndizi kwa chakula. Mkungu mmoja unauzwa Sh 7,000 hadi Sh 15,000.

Hata hivyo, viongozi wa wilaya na mkoa hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, huku Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denis Mwilla, akidai jambo hilo ni zito, linahitaji takwimu kulizungumzia.

GEITA

Mkuu wa Wilaya ya Geita mkoani Geita, Herman Kapufi, alikataa kuzungumzia hali ya njaa, licha ya wananchi kuiambia MTANZNIA kuwa hali ya chakula ni mbaya.

TMA

Nayo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema msimu wa mvua wa kuanzia Januari hadi Februari, unatarajiwa kuwa chini ya wastani.

Meneja Ofisi Kuu TMA, Samuel Mbuya, alisema jana kuwa kunyesha mvua chini ya wastani kunatokana na kupungua kwa joto la bahari eneo la Ikweta.

UKUAJI KILIMO

Hivi karibuni, wakati akitoa tathimini ya ukuaji wa uchumi kwa nusu mwaka na matarajio ya hadi Juni mwaka huu,  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, aliitaja sekta ya kilimo kuwa ndiyo inayoongoza kwa kukua polepole.

Alisema licha ya kilimo kuwa miongoni mwa sekta inayochangia kukua kwa pato la Taifa, lakini yenyewe inakua kwa asilimia 2.7 hadi 0.3.

KAULI YA MAGUFULI

Taarifa hizi za ukame na njaa, zimekuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kuhutubia wananchi mkoani Kagera na kusema Serikali yake haitatoa chakula cha msaada ili kila mtu afanye kazi.

Rais Magufuli pia aliwaonya wakuu wa mikoa na wilaya wajiandae kuwajibika endapo maeneo wanayoongoza yatakuwa na ukosefu wa chakula na kusababisha wananchi kukumbwa na njaa ilhali maeneo mengi ya nchi yamepata mvua za kutosha.

Source: Mtanzania

Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri mkuu Marekani

$
0
0
Jared Kushner na mke wake

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.

Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.

Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

Kingine Alichokisema Soulja Boy kuhusu Beef yake na Chris Brown

$
0
0

Kumekuwa na majibishano makali kwenye mitandao ya kijamii kati ya rapa Soulja Boy na Chris Brown juu ya kile ambacho kilisemekana kuwa Chris Brown alimpigia Soulja boy simu na kumtishia kumpiga kwasababu tu ali LIKE picha za Karueche ambaye ni mpenzi wa zamani wa Chris.

Muda mfupi baadaye Soulja akaeleza chanzo haswa cha bifu yao ni baada ya Chris kugundua kwamba Rihanna na Soulja Boy walikutana na kuspend time hivyo wivu ukamuingia mpaka akaamua kumpigia simu Soulja.

Imenifikia video ikimuonyesha Soulja Boy akisema kuwa yeye na Chris Brown hawana bifu, na Chris ni kama kaka yake, kama ilivyo kwa watu wengine ndugu hugombana na kupatana hivyo watu wasubirie tu mpambano wa kirafiki kati yake yeye na Chris Brown utakaofanyika March 2017.

Wakenya Wamsuta Rais Kenyatta Mtandaoni

$
0
0

Watumiaje wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakimsuta Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufuatia hatua zake za kuzindua miradi.


Wakosoaji wanasema kuwa baadhi ya miradi ilizinduliwa na Rais Kenyatta ilikuwa ikiendelea au tayari ilikuwa imezinduliwa.


Wengine nao wanasema kuwa hatua hiyo iko chini ya hadhi ya rais.


Wiki iliyopita bwana Kenyatta ambaye atawania urais tena mwezi Agosti alikuwa mjini Mombasa ambape alizindua daraja.


Baadhi wa watumiaji wa mtandao wa Twitter wametumia uzinduzi huo kama chanzo cha kumsuta rais.


Wakitumia #UhuruChallenge, wamechapisha mifano yao ya vitu walikuwa wakizindua.


 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta


 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta


 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta


 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta


 Ujumbe unaomsuta Rais Kenyatta



Maeneo kadha ukiwemo mji mkuu Nairobi, pwani na maeneo ya kaskazini mwa nchi yamekuwa yakikumbwa na ukoseu wa nguvu za umeme hali iliyosababisha rais kusutwa zaidi

Apandishwa Kizimbani kwa Madai ya Kumtukana Rais Magufuli na Makamu wa Rais

$
0
0


Mtunza bustani Maganga Masele, amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu utendaji wao wakuliongoza taifa.

Wakili wa Serikali Lucy Mallya amesema kuwa Desemba 22, mwaka jana Masele akiwa Leaders Club Kinondoni jijini Dar es salaam, alitoa lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli na Samia, maneno ambayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo, Masele alikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Mallya alidai kuwa upelelezi haujakamilika pia hakuna pingamizi la dhamana kwa kuwa kisheria kosa hilo linadhaminika.

Kwa upande wake Hakimu Mwijage amesema kuwa ili mshitakiwa awe nje kwa dhamana ni lazima awe na mdhamini  mwenye barua yenye utambulisho atakayesaini bondi ya sh 500,000.

Masele amekamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana,na kesi yake itatajwa Januari 24

Jengo la Billicanas kujengwa maduka

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kujenga maduka ya kisasa zaidi ya 200 katika eneo lililobomolewa jengo la Billicanas lililokuwa likimilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Jengo la Billicanas lilibomolewa na shirika hilo mwishoni mwa wiki baada Mbowe kuondolewa mwanzoni mwa Septemba mwaka jana kutokana na kushindwa kulipa deni la Sh bilioni 1.3 ambazo zilikuwa pango ya miaka 20.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, alisema ujenzi wa maduka hayo madogo madogo ya kisasa yatakayokuwa katika ghorofa tano, unatarajia kuanza mwakani baada ya kukamilika kwa taratibu za kutafuta mzabuni.

“Tunajenga mall (maduka ya kisasa) ndogo ndogo, maduka yatakuwa 232 yatakayoanzia ghorofa moja mpaka tano,” alisema Mchechu.

Alisema kabla ya kufanyika kwa ujenzi huo, wataalamu wa shirika hilo watapitia michoro iliyoandaliwa na baadae kutangaza tenda ili kupata mzabuni.

Mchechu alisema kuwa mbali ya jengo la Billicanas, kuna majengo mengine manne yanayomilikiwa na shirika hilo yatabomolewa ili kukamilisha ujenzi huo.

“Kuna majengo yanayozunguka eneo la maegesho ya magari ya jiji, tunategemea kuyabomoa kati ya majengo matatu au manne ndani ya mwezi huu, hilo litakuwa eneo la maegesho,” alisema Mchechu.

Alisisitiza kuwa ubomoaji wa majengo hayo utafanyika ndani ya mwezi huu ili kuweza kuharakisha ujenzi huo.

Nyoka apatikana katika ndege ya Emirates ya kwenda Dubai

$
0
0
Maafisa wa Emirates hawajafafanua iwapo nyoka aliyegunduliwa ana sumu

Safari ya ndege ya shirika la Emirates ya kutoka Oman kwenda Dubai imesitishwa baada ya wahudumu wa ndege kumpata nyoka ndani ya ndege.

Safari ya ndege nambari EK0863 kutoka Muscat ilisitishwa baada ya wafanyakazi wa kupakia mizigo kumgundua nyoka kwenye eneo la kubebea mizigo.

Msemaji wa shirika hilo la ndege amenukuliwa na vyombo vya habari Dubai akisema nyoka huyo aligunduliwa kabla ya abiria kuabiri ndege hiyo.

Ndege hiyo ilichunguzwa kwa makini kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari.

Iliwasili Dubai saa chache baadaye.

Emirates hawakusema ni nyoka wa aina gani aliyepatikana kwenye ndege au iwapo ni nyoka hatari.

Wengi wamefananisha kisa hicho na filamu ya Samuel L Jackson ya mwaka 2006 kwa jina Snakes on a Plane (Nyoka kwenye Ndege) ambapo abiria wanakumbana na mamia ya nyoka wadogo wenye sumu ndege ikiwa katikati ya safari. Baadhi ya watu wameanza kujadili filamu hiyo mitandao ya kijamii.

Hii si mara ya kwanza kwa nyoka kugunduliwa kwenye ndege, hasa maeneo yenye joto.

Novemba mwaka jana, nyoka wa urefu wa mita tatu aligunduliwa kwenye ndege Mexico.

Chatu mwingine alionekana akining'inia kwenye ubawa wa ndege iliyokuwa safarini kutoka Cairns, Australia hadi Port Moresby nchini Papua New Guinea mwaka 2013.

Na mwaka 2012, maafisa wa kuwahudumia wanyama walimuokoa nyoka mdogo aliyegunduliwa kwenye ndege iliyowasili Scotland kutoka Mexico.

Mbowe, Besigya Wakaribishwa Ikulu Ghana

$
0
0
mbowe

 Rais wa Ghana Akufo- Addo, Kiongozi mwenye umri wa miaka 72, na ambaye ni wakili wa zamani wa kutetea haki za binadamu,  mara tu baada ya kuapishwa katiaka viwanaja vya Accra nchi humo Janauari 7 2017. Ameanza kuyatekeleza majukumu yake kwa nchi zingine za Afrika ikiwemo kukuza demokrasia ya kweli kwa kuupa ngvu mfumo wa vyama vingi.
rais-ghana

Katika sherehe za kuapishwa Rais huyo mpya alisema ni lazima kurejesha uadilifu serikalini, na kwamba fedha za umma hazipaswi kutumika visivyo na chama kinachoshinda uchaguzi bali kukuza rasrimali za nchi na maendeleo kiuchumi. Na kwa watu waliomchagua, rais Akufo Addo alikuwa na Ujumbe huu.

Aidha Rais Nana Akufo-Addo aliyemshinda John Mahama katika uchaguzi wa rais mwezi jana, leo amewakaribisha viongozi wa vyama vya upinzani, mwenyekiti wa chama cha Demokraia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kutoka Tanzania na Kizza Besigye Kifefe mwnasiasa mashughuli kutoka Uganda, Ikulu nchini humo leo kwa mazungumzo ya kisiasa.

Polisi Washtukia Mbinu Mpya ya "Wauza Unga"

$
0
0

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya kwa kusafirisha na kuingiza nchini, vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kifua) aina ya ephedrine kisha kuvitumia kutengeneza cocaine na Heroin.

Kamanda wa polisi, kikosi cha dawa za kulevya, Mihayo Msikhela amesema kwamba wafanyabiashara hao usafirisha kemikali hizo kutoka bara la Asia na wanapozifikisha nchini hutumia kutengeneza dawa hizo za kulevya.

Kadhalika amesema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha serikali na hudanganya na hudanganya kuwa zitatumika kutengeneza dawa za kifua.


Nay wa Mitego Achukizwa na Video ya Mwanamke Aliyedhalilishwa kwa kuchapwa Viboko

$
0
0


Rapa Nay wa Mitego ameonesha kusikitishwa na moja ya video ambayo inamuonesha mwanamke akiwa amezungukwa na wazee na vijana wengi wakimchapa viboko kama adhabu kutokana na makosa ambayo mwanamke huyo ameyafanya.

Rapa Nay wa Mitego baada ya kuitazama video hiyo amefunguka na kusema licha ya ubabe wake na ukorofi wake lakini katika maisha yake hajawahi kumpiga mwanamke na kusema anawachukia sana wanaume ambao wamekuwa wakiwapiga wanawake.

"Na ubabe wangu wote, sijawahi kumpiga mwanamke, namchukia mwanaume yoyote kwenye hii dunia anaye mpiga mwanamke. Ningekua ni kiongozi kwenye hii nchi hawa mbw*** wote wangeenda jela bila mjadala, acha jela ikajae lakini cha moto wakione. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu. Sijui kabila gani hawa mashetani..!! eeh Mungu walaani hawa binadamu wanaomdhalilisha huyu mama, wageuze ata funza tu. Wahusikaaaaa please chukue hatua kali juu hili". Alisisitiza Nay wa Mitego

Tazama hapa video ya mwanamke huyo, akiadhibiwa na kundi la wanaume...

TANGA: Miili ya Watu 12 yaopolewa Baada ya Boti Kuzama Usiku wa Kuamkia leo

$
0
0

Watu 27 waokolewa na jumla ya miili 12 imeopolewa kutoka Bahari ya Hindi baada ya boti iliyokuwa inaelekea Pemba kuzama leo alfajiri

Flora Mbasha: Naomba Mniache Mimi na Mbasha Tafadhali

$
0
0
Mwanamuziki wa Injili nchini, Flora Mbasha amesema kuwa watu wamuache na maisha yao kati yake na Mbasha kwani mapenzi ni kitu binafsi kati ya watu wawili na anaishi kama anavyotaka na sio kama watu wanavyotaka aishi

Amedai kuna watu wanajifanya wanamjua maisha yake kuliko yeye na kumbe sivyo, pia kwa sasa anataka afahamike kama Madam Flora na sio Flora Mbasha kwa kuwa kuna talaka ipo kwenye process 
Video:
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images