Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

U HEARD: Dancer wa Diamond Platnumz adaiwa kumtelekeza mtoto

$
0
0
Ni kawaida yangu kila siku kukuletea sori zote za Entertaiment zinazotokea na leo January 10 2016 nakukutanisha na hii kutoka kwenye U Heard ya Soudy Brown kuhusu dancer wa Diamond Platnumz anayefahamika kwa jina la Zungu kumtelekeza mtoto wake, Soudy Brown kapiga stori na mama wa mtoto huyo…..

’Mimi nimezaa na Dancer wa Diamond anaitwa Zungu nilikuwa naishi nae na tukapata nae mtoto anaitwa Faisali lakini kukatokea mizozo kati yangu na yake kulikuwa na msichana mmoja alikuwa anatoka naye anaitwa Rukia Ruki alishawahi kutoka na Rayvany‘;-Swaumu
Source:Millard

Wasichana wa kiislamu kuogelea na wavulana Uswizi

$
0
0
Kesi hiyo iliamuliwa kwenye mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya

Uswizi imeshinda kesi kwenye mahakama ya haki ya ulaya, ambapo wazazi waislamu watahitajika kupeleka watoto wao kushirika mafunzo ya pamoja ya kuogelea.

Mahakama ilisema kuwa utawala una jukumu la kuhakikisha uwepo mfumo kamili wa masomo na kujumuishwa kwa wanafunzi.

Hata hivyo mahakama hiyo imekiri kuwa uhuru wa kuabudu umekiukwa.

Kesi hiyo iliwasilishwa na raia wawili wa Uswisi wenye asili ya Uturuki ambao walikataa kuwapeleka wasichana wao kwa mafunzo ya lazima ya pamoja.

Maafisa wa elimu hata hivyo wanasema kuwa wasichana waliofikisha umri wa kubalege hawatalazimishwa kuhudhuria mafuzo hayo.

Mwaka 2010 baada ya mzozo uliodumu muda mrefu, wazazi hao waliamrishwa kulipa faini ya takriban pauni 1,100 wa kukiuka majukumu yao kama wazazi.

Walisema kuwa hatua hiyo inakiuka kipengee cha haki za bianadamu cha tume ya ulaya kinachojumuisha haki ya kuabudu.

Mahakama ilisema kuwa Uswisi ilikuwa huru kubadili mifumo yake ya elimu kuambatana na mahitaji na tamaduni.

Pia ilisema kuwa shule zina jukumu kubwa la kuwepo mchanganyiko wa kijamii.

Wezi waiba laptop ya skrini tatu Las Vegas Marekani

$
0
0
 Razer walidai laptop hiyo ya skrini tatu waliyoipatia jina Project Valerie ni ya kwanza ya aina yake duniani

Kampuni ya Razer imetangaza kwamba mbili kati kompyuta mpakato maarufu kama laptop ambazo zina skrini tatu badala ya moja ambazo zilikuwa zimeundwa na kampuni hiyo zimeibiwa.

Laptop hizo za maonesho, ambazo sana zinawalenga watu wanaopenda michezo ya kompyuta, ziliibiwa wakati wa maonesho ya teknolojia ya CES yaliyokuwa yakifanyika mjini Las Vegas, Marekani.

Kompyuta hizo zilionyeshwa hadharani kwa umma mara ya kwanza wakati wa maonesho hayo.

Kampuni ya Razer inasema ilikuwa imebeba kompyuta tatu za aina hiyo lakini waligundua Jumapili kwamba laptop mbili kati ya hizo zilikuwa zimetoweka kutoka kwenye kibanda cha kampuni hiyo siku ya Jumapili.

Skrini zote tatu za laptop hiyo, ambayo imetajwa kuwa ya kwanza ya aina yake duniani, ni za kiwango cha kuonyesha pikzeli 4,000 (4k) na ni za ukubwa wa inchi 17 (43cm).

Skrini mbili huchomoza kila upande kutoka kwa skrini kubwa ya kati, moja kwa moja.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Min-Liang Tan amesema kisa hicho kinachukuliwa "kwa uzito sana".

Msemaji wa Razer amesema kampuni hiyo imeahidi kutoa $25,000 (£20,600) kwa atakayetoa habari za kusaidia "kutambuliwa, kukamatwa na kuadhibiwa" kwa waliohusika katika uhalifu huo.

"Maafisa wetu walifanya kazi kwa miezi mingi kuunda kompyuta hizi," Bw Tan alisema kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook.

"Huu ni udanganyifu, ni wivi na haujatufurahisha. Yeyote aliyefanya hivi bila shaka ni mtu mjanja sana."

Msemaji wa Chama cha Watumiaji wa Teknolojia, shirika linaoandaa maonesho ya CES, ameambia BBC kwamba ni kweli kisa cha kuibiwa kwa laptop hizo mbili kimeripotiwa
Razer, kampuni ambayo ina makao makuu yake California, ilianzishwa na mjasiriamali kutoka Singapore Min-Liang Tan.

Ni kampuni inayosifika na kuheshimiwa sana katika tasnia ya michezo ya kompyuta.

Mashabiki wa michezo ya kompyuta duniani walikuwa wamefurahia sana habari za kuzinduliwa kwa kompyuta hiyo mpya ya skrini tatu ambayo imepewa jina Project Valerie.

Museveni amteua mwanawe kuwa mshauri mkuu Uganda

$
0
0
 Mwana wa Rais Yoweri Museveni, Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba na mkewe Charlotte Kutesa Kainerugaba alipokuwa anapandishwa cheo kuwa meja jenerali Mei 25, 2016.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu operesheni maalum.

Mke wa Museveni, Bi Janet Kataaha Museveni ni Waziri wa Elimu na Michezo, wadhifa ambao alikabidhiwa Juni mwaka jana.

Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.

Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.

Luteni kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu kamanda wa SFC.

Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.

Mkuu wa majeshi wa awali, Jenerali Edward Katumba Wamala amehamishwa na kuteuliwa waziri wa ujenzi.
Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba (kati) amekuwa kamanda wa kikosi maalum Uganda

Kwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF)

Luteni Kanali, Rais Museveni amempandisha afisa mkuu wa majeshi aliyeongoza operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa Rwenzururu, magharibi mwa nchi hiyo.

Watu 100 walifariki wakati wa operesheni hiyo. Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alikamatwa na bado anazuiliwa

Brigidia Peter Elwelu, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha wanajeshi hao wenye kambi yao kuu Mbarara, amepandishwa cheo na kuwa meja jenerali na akateuliwa kamanda wa majeshi ya nchi kavu.

Wafanyakazi wa serikali za mitaa walia na udhalilishwaji

$
0
0

Chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU)kimewatata viongozi wa kisiasa kuacha udhalilishaji kwa watendaji ngazi za kata,vijiji na mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari,Katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Mtima alisema tayari wameshapeleka barua kwa makatibu tawala kwa lengo la kukusanya matukio hayo ya udhalilishaji.

“Kwa mfano tunakumbuka lile tukio la afisa ardhi aliyedhalilishwa na Makonda hivi karibuni, basi huko kwenye halmashauri, watendaji wa serikali za mitaa wananyanyasika sana,” alisema Mtima.

“Akikosea achukuliwe hatua lakini ni vyema akiachwa akajieleza, zipo taratibu za kufuata na sio kufuata umaarufu kwa njia hizo, tunaamini njia ya mazungumzo ndiyo njia sahihi tunaamini hali kama hiyo haitajitokeza tena”.

Lissu Aeleza Kwanini Waliamua Kumchagua Lowassa Kugombea Urais

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiliamua kumchukua aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, ajiunge na chama hicho baada ya kubaini katika utafiti maalum uliofanywa na shirika moja kutoka nchi za nje kwamba alikuwa na uwezo wa kubeba asilimia 18 ya kura zote katika uchaguzi mkuu kuliko mgombea mwingine wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita.

Hayo yalizungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akihojiwa na Global TV Online ambapo alisema pia Lowassa aliongoza wagombea wote katika utafiti huo.

“Wazungu wakatuambia hivi political personalities zote za Tanzania walimfanyia kila mmoja wao walimfanyia uchunguzi wake, wakatuambia hivi ‘katika wote hao ukimweka huyu na huyu, huyu bwana mkubwa Lowassa huyu yeye peke yake anatembea na asilimia 18 ya Tanzania voters,’ aliyekuwa anamfuata alikuwa na asilimia 11 tu. Kwahiyo Lowassa as Lowassa alikuwa na eighteen percent ya likeability ya kupendwa na hao Watanzania akienda huku anaenda na asilimia 18 ya ziada, akienda huku anaenda na asilimia 18 za ziada nyingine ongezeeni,” alisema Lissu.

“Tukasema hivi, ‘tunataka kushinda uchaguzi eeh tuzungumze na Lowassa’ na Dkt Slaa akasema tuzungumze na Lowassa tukamwambia ‘Dkt una mawasiliano naye’ akasema ‘sina mawasiliano naye, ila kuna mtu ambaye anaweza akawezesha mawasiliano naye ni nani? Askofu Gwajima’ tunaelewana, so this how we got Edward Lowassa.”

Joh Makini Ataja Sababu ya Kuchelewa Kuachiwa Kwa Wimbo wa Weusi na Sauti Sol

$
0
0
Rapper wa kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka sababu ya kuchelewa kwa wimbo wao na Sauti Sol kutoka Kenya.

Mwezi Septemba mwaka jana, Joh alithibitisha kupitia mtandao wa Instagram kuwa wimbo huo ungetoka kabla mwaka huo haujaisha lakini mpaka sasa bado haujatoka.

Akiongea na Bongo5, Joh amesema sababu ya kuchelewa kutoka kwa wimbo huo ni kutokana na baadhi ya marekebisho yaliyokuwa yanatakiwa kufanyika katika wimbo huo ambapo wote kwa pamoja walikuwa busy na kazi nyingine.

“Sauti Sol kama ambavyo unawafuatilia utagundua ni watu ambao wako busy sana na sisi pia hivyo hivyo. Ngoma tulishaifanya lakini kama wasanii pia tuligundua kuna vitu turekebishe. Hiyo ndio sababu kubwa na sasa ipo tayari,” amesema Joh.

“Mipango ya video ikiwa tayari na vile ambavyo sote tutakua tayari itoke. I mean sisi na Sauti Sol ili tuweze kupromote kwa pamoja isiwe kwa upande mmoja,” ameongeza.

Sakata la Nuh Mziwanda na Shilole Kukutana Mwanza na Kukiss...Nuh Afunguka Haya

$
0
0

Nuhmziwanda amefunguka kuhusu taarifa ya jana(jumatatu) usiku Nuh na Ex wake #Shilole ,walikutana maisha club jijini Mwanza na kuonekana wakiwa wana kiss.
.
#nuhmziwanda amekiri kukutana na #Shilole maisha club mwanza lakini amekanusha vikali kuwa walikiss au kufanya chochote.
.
#nuhmziwanda amesema alikuwa kwenye mishe zake za kufanya show na #shilole alikuja na wasanii wengine kikazi na ndipo wakakutana ila hayo maneno mengine hayana ukweli hata kidogo.

Amesema yeye tayari ameoa na anamheshimu mkewe ambaye alimuacha Dar kutokana na Hali yake ya sasa (ujauzito)hivyo alikwenda kutafuta na si vinginevyo

KRC Genk Wamemletea Changamoto Mpya Mbwana Samatta

$
0
0
Siku 14 zimepita toka mshambuliaji wa KRC Genk Nikolaos Karelis ambaye alikuwa anashindania namba na mtanzania Mbwana Samatta atangazwe kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 8 hadi 9 kufuatia jeraha la goti la kushoto alilolipata wakati wa mchezo dhidi ya KAA Gent dakika ya 51 December 27.

January 10 2017 KRC Genk imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji Jose Naranjo kutokea Celta Vigo ya Hispania, hiyo itakuwa ni changamoto mpya kwa Mbwana Samatta kuendelea kupambania namba ya kucheza na Naranjo katika kipindi ambacho Karelis atakuwa nje.
Jose Naranjo

Jose Naranjo amejiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea Celta Vigo ya Hispania kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu, Naranjo mwenye umri wa miaka 22 amewahi kuichezea Villarreal kwa mkopo mwaka 2014 akitokea Recreativo.

VIDEO: Askofu Mokiwa afafanua mgogoro unaoendelea kwenye kanisa la Anglikana

$
0
0
Mchezo wa Yanga na Simba kwa dakika 90 ulimalizika pasipo kufungana, hivyo ililazimika kupigwa mikwaju ya penati ili kupata mshindi atakayecheza fainali na Azam FC Ijumaa ya January 13 2017, Simba wamekuwa vinara kwa Yanga kwa kuifunga kwa penati 4-2.

VIDEO:

Anglikana Bado Ngoma Nzito, Askofu Mokiwa Atoa Utetezi Wake, Asisitiza Hatang'oka Hata Kwa Dawa

$
0
0
Hali  ya amani ndani ya Kanisa la Anglikana nchini, bado si nzuri baada ya Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa aliyevuliwa uaskofu kutoa msimamo wake na kudai kuwa yeye ni msafi, na ndio Askofu wa Dar es Salaam, hang’oki hata kwa dawa, na amewasamehe wanaompinga.

Askofu Mokiwa aliyasema hayo kwenye Kanisa la Anglikana Ilala jana, alipozungumza na waandishi wa habari. Alisema licha ya kusemwa mambo magumu, lakini yeye kama Askofu, kazi yake ni kuwaombea waliomkosea na hana matatizo nao, kwani amekwisha wasamehe.

Askofu Mokiwa pia alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Dayosisi ya Anglikana Dar es Salaam haina mgogoro, bali viongozi watano wa dayosisi hiyo ndio wanatengeneza mgogoro huo kwa maslahi binafsi, wakitumia Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni kama njia ya kupitishia migogoro yao.

“Siogopi kusema baba askofu kapotoka katika hili, ameshauriwa vibaya na washauri wake wa kisheria,”alisema Askofu Dk Mokiwa ambaye alimtaja Profesa Palamagamba Kabudi kuwa mshauri wa kisheria wa askofu mkuu.

Kauli hiyo ya Mokiwa imekuja siku chache baada ya kuvuliwa uaskofu, kwa kile kilichoelezwa mashtaka 10 yaliyofunguliwa na walei 32 wa Kanisa hilo Dayosisi ya Dar es Salaam, yakiwemo ya ufisadi wa mali za kanisa, ndio sababu ya Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledya kumvua uaskofu.

Hata hivyo, Dk Mokiwa amegomea uamuzi huo, kwa maelezo kuwa mwajiri wake ni Sinodi ya Dar es Saalam, ambayo ndiyo yenye uamuzi wa kumfuta kazi na si askofu mkuu; au askofu mwingine yeyote wa kanisa hilo Tanzania.

Uamuzi wa kumvua uaskofu, ulichukuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Askofu Chimeledya baada ya Askofu Mokiwa kugoma kujiuzulu, kama ilivyoshauriwa na Nyumba ya Maaskofu, ambayo ilimkuta na hatia ya kufuja mali za kanisa hilo na kukiuka maadili ya kichungaji, ambayo yalibainishwa kwenye ripoti ya uchunguzi iliyoundwa na kiongozi mkuu wa kanisa hilo nchini.

Akizungumzia suala hilo, Mokiwa alisema, “Alikuja na maaskari zaidi ya 12 ambao wamevaa sare, na wengine ambao hawakuvaa sare sijawajui idadi yake, askofu mkuu alidai amekuja kuleta mrejesho wa halmashauri kuu, na matokeo yake akaishia kusema ameniondoa kwenye huduma ya uaskofu.

"Nimesema siondoki, na nimeona wanasema wataweka kila kitu hadharani, nawambia hivi, mimi ni msafi na sina uchafu sehemu yoyote ile, wawe huru na amani kuanika madudu yangu kama yapo, waweke tu hadharani wala siogopi.

“Ninavyo vyombo  halali kwenye Dayosisi hii ambayo hakutaka kukutana navyo ambavyo ni Halmashauri ya Kudumu, hakuwahi kutaka kuwasiliana na sisi, sisi tulitaka kuwasiliana na yeye, angejibu mawasiliano yetu ya kujenga mahusiano na kutekeleza yaliyoamuliwa, hukutaka kutekeleza leo unakuja na hoja ya kuniaondoa.

“Halmashauri ya Kudumu inamwambia hatujawahi kumpelekea mgogoro sisi kama Dayosisi ya Dar es Salaam, waswahili wanasema ‘jipu linamsumbua mwenye mwili wake’, hujawahi kupelekewa neno lolote la machafuko, ni nani aliyekwambia Dayosisi ya Dar es Salaam ina migogoro?

 “Askofu anafanya kazi na sisi, askofu ana vyombo vya kutawala, hana mamlaka ya kujiamulia mambo yake mwenyewe, ukisema Dar es Salaam kuna machafuko wewe Askofu Mkuu tunajua unasimama na watu na makundi katika Dayosisi hii.

“ Yeye ni askofu kama mimi, yeye yupo Mpwapwa, tuna taratibu zetu kama za bendera ukiingia mahali unashusha bendera kidogo, kwa nini Askofu Mkuu afanye kazi na watu ambao sio sehemu ya mamlaka ya Dayosisi ya Dar es Salaam.

“Halmashauri Kuu inamwambia kwa kuwa amekuja na tamko lake bila ya kuwashirikisha, wamemwambia Dar es Salama kuna askofu mmoja tu ni Mokiwa.

“Yeye kama Askofu Mkuu hakupaswa kucheza nje ya Nyumba ya Maaskofu, mimi pia naingia kwenye Nyumba ya Maaskofu, kuchomoka na kufanya kazi nje ya taratibu, hii sio sawa.

"Askofu Mkuu ana timu yake ya maofisa ambao wamemshauri vibaya, na yote yaliyonukuliwa yote yamekosewa katika kusimamia taasisi, kila taasisi ina uhuru wa kurekebisha pale palipoharibika pasipo kuingiliwa.

“Dayosisi ya Dar es Salaam haina mgogoro na mimi ndio Askofu wake, mgogoro uliopo ni wa kutengeneza, katika timu yake kuna watu wenye ‘interest maalum’ ambao ni Profesa Palamagamba Kabudi, yeye ndio mshauri mkuu wa askofu lakini amekuwa akimpotosha, askofu akikosea na yule ni mwanasheria aliyebobea na ndiye anayeingiza kanisa kwenye migogoro iliyobobea.

“Tumewahi kuandikiwa barua na serikali Kanisa letu ndio vinara wa migogoro, wamekuwa wakitengeneza mgogoro kati ya waumini na maaskofu wasielewane, wakubwa waingie kushika hatamu za uongozi hapa.

“Nina kibali cha kuzungumzia Dayosisi ya Victoria Nyanza Mwanza, uongozi wa kanisa umeingia pia na kufanya kazi na makundi, kando ya taratibu, kugombanisha askofu na watu wanaowangoza na kusababisha maumivu makubwa, lakini nasema bila kufuata taratibu yeye akiwa kiongozi mkuu, ni hatari sana kiongozi anayeacha kuongoza kwa taratibu na kufuata matakwa yake mwenyewe. "

Ataja majipu 5 ndani ya Kanisa
Askofu Mokiwa alisema kuwa ndani ya Kanisa hilo, kuna majipu ambayo yamekuwa kiini cha migogoro kila kukicha na kuchafua taswira nzima ya kanisa hilo.

“Askofu Mkuu anashauriwa na Mwanasheria (Profesa Kabudi) anayeheshimiwa na watu wengi, aliyezalisha wanasheria wengi zaidi katika nchi hii lakini halitendei haki kanisa, halisaiidi kusimama sawa sawa, kuliokoa kanisa na mvurugiko, haonekani mara zote kwa kuwa amejificha nyuma ya taratibu hizo.

“Mwingine ni askofu Oscar Mnung’a, Makamu Askofu Mkuu, huyu anakuja kufanya kazi na makundi Dar ili aje kuwa askofu mkuu, alikuwa padri wangu na ni askofu wa Newala, naamini watu wa Mpwapwa na Newala wanawafahamu, kuwa ndio viongozi wao ndio chanzo cha maumivu kwenye kanisa hili.

“Mwingine ni Johnson Chinyong’ole ni Katibu Mkuu, Padri wa Dayosisi ya Morogoro, moyoni mwake anaamini mimi ndiye niliyebana asiwe askofu mkuu, nataka kusema Kanisa Anglikana ni Kanisa kubwa nchi hii, alipaswi kuonekana na dalili yoyote ya migogoro, lina uwezo wa kufanya mambo yake ndani bila ya kuvuana nguo kama ilivyo sasa tena bila ya sababu za msingi.

“Askofu mkuu anafanya kazi na Kanisa la Andrea Mtakatifu Magomeni, kule kuna mtu anaitwa John Mhina, yule alikuwa Padri katika dayosisi yangu na tulimuondolea haki za sakramenti na huduma za kichungaji mikononi mwake, tulifanya hivyo kwa sababu ya kukiuka jambo moja tu la utii.

“Tulifanya uhamisho katika Dayosisi ya Dar akagoma, akatengeneza tuhuma kwa taasisi moja kubwa ambayo naiheshimu, na sitaki kukosea ikavurugikiwa kwa sababu ya maneno ya kinywa changu, taasisi hiyo sina uchafu nao, na sina uchafu popote.

“Sababu ya Mhina kumuondoa ni kwamba haifai, mtu ni kuhani wa Mungu halafu anaenda kukopa benki na kukimbia vielelezo ninavyo, benki alizokopa ni BOA, Akiba Commercial Bank na Tanzania Investment ambayo iliwahi kumtoa mpaka picha zake.

“Mwingine ni Paul Mtweve alikuwa mkuu wa idara ya Uinjilisti, naye nilimuondoa kwa sababu za kiuaminifu, kulikuwa na Saccos ambayo alijikopesha na sasa imefungwa, wamechafua taswira nzima ya Dar es Salaam na ndio wamekuwa wakitumika na askofu mkuu, ndio wamekuwa vinara wa kutengeneza mashaka. Kuthibitisha kuwa wanafanya kazi na Askofu mkuu, uhamisho wa Mhina, alipopinga kuhama, askofu Mkuu ‘alisapoti’, kwangu mimi kwa Dar es Salama sio tena Askofu, mwaka jana sikukuu ya Matende alisema amehamina Mpwapwa sasa sijui amebaki huko au vipi maana hapa sijamuona.

“Nilisali Ubungo siku ya Krismasi, e-mail zilinaswa ambazo zilikuwa zikisambazwa kwa wanangu wa Magomeni ambao hawakusali Krismasi kwa sababu walipewa taarifa kupinduliwa kwangu, hivyo walijua kutakuwa na mapinduzi.

“Taasisi za dini hazipaswi kufanya kama hivi ni aibu, waumini wakimbilie wapi wakati wanaamini Kanisa ndio mahali salama.

“Waumini watulie, kwa jimbo la Dar es Salaam hawatatusikia katika migogoro yoyote, bado nina imani na waumini wa Dayosisi hii, tushikane pamoja, kuifanya kazi ya Mungu.

“Tuna shule, vituo vya watoto yatima, nataka ninaofanya nao kazi bila njaa, na wale wanaocheza nje ya zizi, warudi kundini nitawakaribisha,” alisema.

Mokiwa alifunguliwa mashtaka 10 Machi 2015 ambayo ni kuizuia dayosisi ya Dar es Salaam, kupeleka michango pasipo maelekezo ya Sinodi ya Dayosisi ya Dar es Salaam, kuhamasisha dayosisi kujitoa katika udhamini wa Kanisa la Anglikana Tanzania (KAT) kwa lengo la kuifarakanisha dayosisi na Jimbo, kinyume na katiba ya dayosisi.

Mashitaka mengine ni kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika eneo la kanisa la Mtoni Buza na miradi mingine, kushindwa kutatua migogoro inayohusu uwekezaji na maadili baina ya dayosisi na mitaa ya Magomeni ambao kuna mgogoro na Benki ya DCB, kanisa la Kurasini na mengine.

Askofu huyo pia anadaiwa kushindwa kutatua migogoro baina ya mapadiri na waumini na kutunza mali za kanisa katika mtaa wa Watakatifu wote Temeke na kutelekeza nyumba ya askofu iliyopo Oysterbay ambako imegeuzwa kuwa yadi ya kuuza magari.

Pia alilalamikiwa kushitakiwa mahakamani na Marehemu Christopher Mtikila na watu wengine watatu kwa kosa la kuwatishia silaha ya moto na kuwapapasa maungoni mwao bila ridhaa yao kinyume na maadili ya kikanisa.

Askofu Mokiwa pia analalamikiwa kuanzisha taasisi ya MEA Foundation iliyomwezesha kupokea fedha nyingi za wafadhili kwa ajili ya maendeleo ya dayosisi, lakini fedha zimefujwa na hesabu za chombo hazikuwahi kukaguliwa.

Tuhuma zingine ni kurejea kwa mchakato wa mapitio ya katiba mpya na kuvuruga mchakato wa awali wa maandalizi ya katiba mpya ya dayosisi kwa kutumia fedha za dayosisi na kutekelezwa askofu msaidizi dayososi ya Katanga Kalemi .

Hata hivyo akijibu tuhuma hizo Mokiwa alisema; Nyumba ya Maskofu Oysterbay

“Ile nyumba haijatekelezwa bali vigae vilikuwa vinaanguka, nina kijana wangu ambae ana matatizo mpaka sasa ni mkubwa lakini hasemi vizuri kuna siku nilimkuta anacheza na nyoka, paa linavuja mvua zikinyesha, ndio niliamua kuhama na sasa naishi nyumbani kwangu Mbezi Luisi.

“Kuna fedha Sh milioni 60 ambazo zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba hiyo ikikamilika nitarudi kukaa.

“Silverhok iliyopo Upanga, nyumba haikuwa kwenye hali nzuri jengo halikua salama, ndio maana tuliwahamisha na jengo halijatekelezwa kwani tunataka kulifanya la kisasa kama majengo mengine yanayozunguka eneo lile la Mindu.

"Fedha za DCB Kuna watu wanaeneza nimekuwa nikilipwa Shilingi bilioni 6 na DCB, huku ndani mimi nimewahi kuunda chombo ambacho kinahusisha DCB Magomeni, wa wawakilishi wa dayosisi, lakini Magomeni wenyewe ndio wanakimbia vikao, DCB ndio waliojenga na ndio wanaolipa Kanisa Dayosisi ya Anglikana.

“Kama ni vita yenye maslahi, fanyeni uchunguzi mjue anayepokea fedha kutoka DCB ni nani, mtapa ukweli kuwa ni Magomeni wenyewe, inashangaza wao ndio wanakula na kushiba lakini ndio wamekuwa wakipiga kelele na kupotosha watu.

“Kwa mikono yangu niliwaidhinishia Sh milioni 200 za ujenzi wa Kanisa lakini mpaka leo halijajengwa, mabati yapo pale yamesimama kama kaburi, hakuna kilichofanyika na hela zimeliwa, waseme yote kwa ukweli na sio kuweka siasa. "

Bodi ya Mikopo yatua Precision, Mantrac na Pepsi

$
0
0
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imeendelea kufuatilia waajiri wasiotekeleza sheria ya bodi ya kuwataka kupeleka makato ya wanufaika wa mikopo waliopo katika ofisi katika taasisi na kampuni mbalimbali Dar es Salaam.

Katika ufuatiliaji huo, jana bodi hiyo ilikwenda katika kampuni tatu, Kampuni ya ndege ya Precision, Kampuni ya Mantrac na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi (SBC Tanzania Limited ).

Wakiwa katika ofisi za Precision, walishindwa kuonana na uongozi baada ya katibu muhtasi kukataa kutoa ushirikiano kwa madai hawakuwa na miadi na uongozi wa kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa HELSB, Phidelis Joseph alisema, amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Precision.

Alisema licha ya kampuni hiyo kugoma kutoa ushirikiano, lakini wamekuwa na tabia ya kulimbikiza marejesho, jambo ambalo sio sahihi na kupeleka baadhi ya majina huku mengine wakiyaacha.

“Leo (jana) tumekosa ushirikiano wamegoma kuonana na sisi, kampuni hii ni moja ya ambazo zimekuwa na usumbufu na kushindwa kuleta marejesho kwa wakati wanapaswa kulipa Sh milioni saba kwa mwezi wameshindwa kufanya hivyo na kusababisha kuwa na deni la Sh milioni 31 kama faini kwa kuchelewa kupeleka marejesho kwa kipindi cha miezi 20,” alisema.

Aidha alisema idadi iliyotolewa na kampuni hiyo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watumishi katika kampuni hiyo ambayo vyanzo vya bodi hiyo imebaini uwepo wa wanufaika wengine katika kampuni hiyo lakini majina yao hayajapelekwa na mwajiri katika bodi hiyo.

“Haiwezekani kampuni kama Precision iwe na wanufaika saba tu shirika zima, sisi tunatambua wapo zaidi ya hao saba tunachokitaka walete majina ya wanufaika wote na pia walete marejesho kwa wakati ili fedha hizo zitumike kwa wanafunzi wengine wanaohitaji kupata mkopo na kama wakishindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria,”aliongeza.

Akiwa Pepsi, Joseph alisema, kampuni hiyo imekuwa ikisumbua kwa muda mrefu, kwani wametengeneza bili ya watu zaidi 45 waliorodheshwa kama wanufaika tangu Septemba mwaka 2015, lakini hawajapeleka fedha na kila mara wamekuwa wakiwasiliana na kiongozi wa kampuni hiyo, lakini amekuwa akionesha dharau bila kutoa ushirikiano, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Tunashangaa hapa makao makuu hawaleti fedha hizo lakini katika matawi yao ya Moshi na Arusha wamekuwa wakilipa tunataka leo wamtume mtu ofisini kwetu kuchukua majina ambayo tumeyaorodhesha na majibu ya kwanini wameshindwa kulipa kwa muda mrefu pamoja na majina halali ya wanufaika na wakishindwa tutawachukulia hatua,”alisema.

Katika Kampuni ya Mantrac, Joseph alisema kampuni hiyo imeonekana kuorodhesha majina machache, ili hali vyanzo vya bodi hiyo vinafahamu uwepo wa wanufaika wengine wanaofanya kazi hapo.

Pia alisema kampuni hiyo imeshindwa kulipa marejesho tangu mwezi Julai mwaka jana, hivyo amewataka kuhakikisha wanalipa malimbikizo hayo kwa wakati ili kuepuka faini.

“Tumezungumza na Meneja rasilimali watu na tumemueleza ameahidi kufuatilia na kuhakikisha wanaleta marejesho ambayo wameyalimbikiza kwa wakati na kufuatilia kuona kama kuna wanufaika zaidi walioajiriwa lakini majina hayajatufikia,”aliongeza.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa bodi hiyo, Wambura Mkono alisema, waajiri wanatakiwa kuwasilisha majina ya wafanyakazi wao ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri ili waweze kuwaangalia endapo ni wanufaika au la; na atakapojulishwa kuwa ni wanufaika, anatakiwa kumkata asilimia 15 ya mshahara wake na kuiwasilisha bodi ya mkopo kabla ya tarehe 15 ya mwezi unaofuata katika kalenda.

Shirika la Fedha Duniani (IMF) Lafunguka Kuhusu Hali ya Uchumi ya Tanzania Kipindi Hichi cha Magufuli..

$
0
0
BODI ya Utendaji ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeeleza kuwa hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri.

Bodi hiyo imeeleza hayo baada ya kumaliza kufanya tathmini ya hali ya uchumi hapa nchini, chini ya Mradi wa miaka mitatu wa Kuwezesha Sera (PSI).

Katika taarifa yao iliyochapishwa katika tovuti, bodi ilisema kuwa ukuaji wa uchumi, ulikuwa vizuri katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na hivyo kuleta matumaini ya kubaki katika ukuaji wa asilimia saba kwa mwaka huu wa fedha.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa bei za bidhaa zilishuka kufikia chini ya malengo ya asilimia tano. Hata hivyo, imetahadharisha kuwa kuna madhara ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa uchumi, ikiwemo msimamo mkali wa sasa juu ya sera zinazohusu uchumi mdogo.

Aidha, bodi imependekeza kuwa hali uchumi mdogo kwa sasa inapaswa kutafutiwa ufumbuzi, ikiwemo kulegeza msimamo katika sera za muda mfupi.

Hata hivyo, taarifa ya bodi hiyo inasema baada ya kupata ongezeko dogo kufikia Julai hadi Septemba, serikali ijizatiti kuongeza juhudi katika kutekeleza bajeti, na hasa katika uwekezaji wa kijamii.

Aidha imeeleza kuwa juhudi zilizofanywa na serikali katika kupambana na rushwa na ukwepaji wa kulipa kodi, zimesaidia kuweka msingi mzuri kwa kuongeza uwekezaji katika miundombinu kuanzia bajeti ya mwaka 2016/17.

Mradi wa PSI kwa kipindi kilichoishia Juni mwaka jana, umekuwa wa kuridhisha na malengo yote kufikia Septemba 2016 yalifikiwa.

Chanzo:Habarileo.

Mambo Haya Usimfanyie Mkeo, Okoa Nyumba yako

$
0
0
Mpende mke wako mzuri
Usimkaripie mke wako ukiwa unaongea nae. Inamuumiza sana.
Mithali 15:1

Usimuongelee ubaya kwa mtu yeyote. Mke wako atakua kile ambacho unamuita
Mwanzo 2:19

Usimpe mwanamke mwingine upendo anaostahili mke wako. Huo ni uasherati.
Matayo 5:28

Usimlinganishe mke wako na mwanamke mwingine. Kama huyo mwanamke alikua anakufaa basi Mungu angekupa umuoe
2wakorinto 10:2

Uwe mpole, mvumilivu na msikivu. Amevumilia mengi na amejitolea na ameacha vingi ili awe pamoja nawe. Inamuumiza sana unapokua mkali na kumkera
Waefeso 4:2

Usimfiche chochote. Mmekua kitu kimoja na hivyo ni msaidizi wako, usiweke siri yoyotr kati yenu
Mwanzo 2:25

Usiseme kitu kibaya kuukosoa mwili wake. Amejitolea uzuri wake na mwili wake kukuzalia ww watoto. Ni binadam pia mwenye moyo, sio mwili tu.
Mithali 18:22

Usiulinganishe mwili wake na thamani yake. Mthamini hata pale mtakapofikia uzee
Waefeso 5:29

Usimkaripie kwenye umati wa watu. Suluhisheni matatizo yenu chumbani mkiwa wenyewe.
Matayo 1:19

Mshukuru kwa kuwalea watoto wenu vizuri, nyumba yako pamoja na wewe. Kwani amejitolea kufanya hayo yote.
1wathesalonike 5:18

Mapishi ya wanawake hayafanani. Furahia mapishi ya mke wako. Sio rahisi kumpikia mtu milo mitatu kwa siku kwa siku 365 kwa mwaka kwa miaka mingi mlioishi wote
Mithali 31:14

Usiwaweke ndugu zako kabla yake. Yeye ni mke wako. Ndiye anaekaa na ww. Lazma umpe kipaombele kabla ya ndugu zako.
Mwanzo 2:24

Wekeza katika ukuaji wake kiroho. Mnunulie vitabu, na chochote ambacho kitamsaidia kukua kiroho atembee na Mungu siku zake zote. Hicho ndicho kitu cha pekee unachoweza kumfanyia mke wako.
Waefeso 5:26

Tumia mda wako ukiwa nae kujifunza bibilia na kusali
James 5:16

Tenga mda wa kukaa nae, kucheza nae na kufurahia uwepo wake. Kumbuka, utakapofariki, yeye ndiye ataaesimama pembeni ya kaburi lako. Huenda marafiki zako wakawa na kazi nyingi na kushindwa kuhudhuria.
Mhubiri 9:9

Usitumie pesa zako kumrubuni au kumpelekesha. Pesa zako ni za kwake pia. Mmekua kitu kimoja na ni mrithi wa kila ulicho nacho ulieunganishwa nae na Mungu.
1peter 3:7

Usifichue madhaifu yake. Utakua unajifichua na ww. Mlinde.
Ephesians 5:30

Waheshimu wazazi wake na kuwa na moyo wa upole kwa ndugu zake.
Wimbo ulio bora 8:2

Usiache kumuambia ni jinsi gani unampenda kila siku ya maisha yake. Mwanamke hachoki kusikia hilo.
Ephesians 5:25

Kua katika njia ya Mungu, ndicho kitu kitakacho kufanya uwe mume bora na mwenye hofu ya Mungu.
Warumi 8:29.

OKOA NYUMBA LEO

Askofu Mokiwa: Mimi ni Askofu Halali wa Jimbo la Dar

$
0
0
ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam Dkt. Valentine Mokiwa amesema kuwa yeye anatambua bado ni ndiye askofu wa Dar na  hakuna mtu wa kumfukuza bali mtu wa kumfuta kazi ni Sinodi ya Dar, Kanisa la Anglikana lina kanuni na taratibu zake wala  sio askofu mkuu au askofu mwingine yeyote wa kanisa la Anglikana Tanzania.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na vyombo vya habari baada ya tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi yake yanayodaiwa kufunguliwa na walei 32 (waumini) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam yakiwemo ya ufisadi wa mali za kanisa.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya ndiye anayedaiwa kumvua uaskofu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.

Dkt. Mokiwa amesema kuwa tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake ni za  kumchafua na kulenga kumchonganisha dhidi ya waumini wake na wanaofanya hivyo ni wale waliokiuka miiko ya kanisa  akawavua vyeo, huku akiwataja kuwa ni Mchungaji John Mhina, mchungaji Johnson  Chinyong’ole wa kanisa la Newala na Paul Mtweve aliyemtaja kuwa alikuwa katibu wa uinjilisti Dayosisi ya Magomeni.

Alisema kuwa hao ndio wavunjifu wa amani katika dayosisi hiyo ndio maana akaamua kuwatimua na hivi sasa wamerudi kivingine ndio hao hao ambao wamesababisha mgogoro huu unaojitokeza hivi sasa.


Dk. Mokiwa alisema kuwa alishangazwa, askofu mkuu Dk. Chimeledya na ujumbe wake kuhudhuria kikao cha hivi karibuni cha Halmashauri ya kudumu ya dayosisi ya Dar es Salaam na kutangaza uamuzi wa kumvua uaskofu tena kukiwa na  ulinzi wa polisi kinyume na utaratibu wa kanisa kuja na askali kanisani.

 “Mwenye mamlaka ya kunifukuza kazi ni yule aliyeniajiri, na mwajiri wangu ni Sinodi ya Dar es Salaam na wote wanasambaza habari hizi za uchochezi ni wale niliowavulisha madaraka ya kuwa viongozi. alisema


Mwandishi wa mtandao huu, Denis Mtima akimpa tuhuma zake mchungaji, John Mhina wa kainisa la magomeni zilizotolewa na Askofu Mokiwa.

Alisema waraka ambao umesambazwa na askofu mkuu wa Tanzania haujapitia kwenye halmashauri ya kudumu ya dayosisi ili kupata baraka zake na wala hauna baraka kutoka kwa sinodi ya dayosisi jambo ambalo linaufanya waraka huo ukose sifa za kutekelezeka.

“Ninachowaambia ndugu waandishi wa habari mlifanya makosa kusambaza taarifa bila kuninukuu mimi ili muweze kuandika kilicho bora tofauti na kuandika vitu visivyokuwa vya kweli na  askofu wa dayosisi ya Dar es Salaam bado ni mimi, hatuzitambui barua zilizosomwa katika baadhi ya makanisa,” alisema

Askofu Mokiwa alisema baada ya kikao kilichofanyika hivi karibuni katika kanisa la ilala Dar na kuhudhuriwa na viongozi wakuu huku wakisoma walaka wa kumvua cheo hicho mbele ya halmashauri, lakini maamuzi hayo yaligomewa na wajumbe wa halmashauri ya Dayosisi ya Dar es Salaam.


 “Ule waraka tuliupitia na kubaini kuwa hauna baraza za nyumba ya maakofu, wala hauna baraka za halmashauri ya kudumu na Sinodi ya dayosisi,” alisema na kuongeza kuwa maamuzi ya kumvua uaskofu Dk Mokiwa yamefanywa na askofu mkuu wa Tanzania kwa kushinikizwa na watu wachache aliowavua vyeo na sio vikao vya kanisa.

Lakini alipoulizwa askofu mokiwa swali na waandishi wa habari kuhusu kudaiwa kutelekeza Nyumba iliyopo Osyterbay na nyingine iliyopo Upanga jijini Dar alisema kuwa nyumba hizo siyo za kwake bali ni mali ya kanisa na sio zimetelekezwa bali zipo katika hatua ya ujenzi wa nyumba za kisasa.

Risasi liliwatafuta baadhi ya watuhumiwa waliolalamikiwa na Mokiwa kwa kusababisha mgogoro huo ambao ni Mchungaji John Muhina wa Magomeni na Paul Mtweve ambae alikuwa katibu wa Uinjiristi  ambao kwa upande wao kwanza walikataa kumtambua Mokiwa kama askofu tena kwani kasha vuliwa wazifa huo.

“ Sisi ni viongozi halali wa kanisa la Anglikana Magomeni Mokiwa alitusimamisha kipindi cha uongozi wake lakini tukaamua kukata rufaa sehemu husika tukashinda.

Askofu hana uwezo wa kutuondolea uchungaji, anauwezo wa kutuvua uaskofu laikini kikatiba tuliamua kwenda kukata rufaa katika mamlaka ya juu ambayo yeye hana mamlka nayo ambayo ni kwa askofu Mkuu na alilidhia rufaa yetu tukashinda,’’ alisema na kuongeza.

“Mbona yeye analalamika kuondolewa uaskofu, wakati sisi anatusimamisha alisema amefanya mabadiliko ya kawaida tu,tukakubali laikini tukaenda kukata rufaa kwenye mamlka za juu tunaona asiweke visingizio vyovyote dhidi yetu bali akubali uamuzi uliotolewa na Askofu wetu mkuu.

CUF Wakanusha Wizi wa Fedha, Wadai Taaifa Hizo ni Kelele

$
0
0
THE CIVIC UNITED FRONT
CUF – Chama cha Wananchi

CUF – Chama cha Wananchi hakina sababu ya kumjibu Mtatiro na Genge lake, bali kwa kua kumeibuliwa hoja inayohusu Viongozi halali wa Cuf, tunaona Kuna haja ya kutoa ufafanuzi Kuhusu Jambo hili.

Chama cha Wananchi kinaongozwa na Utaratibu wake wa Kikatiba. Kwa hivyo anaejiona kua ni Kiongozi wa Kitaifa wa Chama hiki ni vyema aje kwenye Vikao vya Chama ili aweze kupata ufafanuzi wa hoja hii badala ya kulalama kwenye Vyombo vya Habari. Katibu Mkuu wa Chama hiki ni Maalim Seif Shariff Hamad na Mwenyekiti wa Chama hiki ni Prof Ibrahim Haruna Lipumba. Ni kweli Cuf tumeomba Fedha zetu za Ruzuku ili ziweze kutusaidia kwenye Uchaguzi huu wa Madiwani katika Kata 20 kwa upande wa Tanzania Bara.

Ni vyema Watanzania wakafahamu kwamba kupitia kwa Shaweji Mketo, upande wa Maalim Seif Shariff Hamad umetamka bayana kwamba haujasimamisha Mgombea kwenye Kata yoyote katika Uchaguzi huu Mdogo unaotarajiwa kufanyika January 22 Mwaka huu. Upande wa Bara Cuf imesimamisha Wagombea kwenye Kata 14 kati ya Kata 20 zinazopaswa kurudia Uchaguzi.

CUF, Chama cha Wananchi upande wa Bara hatuwezi kuacha kusimamisha Wagombea na kuamua kuunga Mkono Wagombea wa Chadema kama ilivyoelekezwa na Katibu Mkuu tu, kupitia Shaweji Mketo. Kuhusu suala la Ruzuku ni kweli kwamba Ofisi ya Msajili ilisimamisha Ruzuku kwakua, ilipokea Malalamiko toka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na baadhi ya viongozi Kuhusu kuvurugika kwa Mkutano huo kulikotokana na ukiukwaji wa Katiba ya Cuf. Kwa sasa Mgogoro huo haupo, kwa hivyo sisi tumeomba Ruzuku hiyo ambayo ni Haki yetu kama Chama, na kwakua Mgogoro umekwisha, Msajili hana sababu ya kuendelea kusimamisha Ruzuku hiyo.

Ni kweli pesa hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya Chama na zinatumika kwenye Shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Udiwani unaorudiwa katika Kata 20 hapa Tanzania Bara. Lakini Maalim Seif Shariff Hamad na Genge lake kama wakweli, basi waeleze pia kua Mwezi October wametoa Milioni 86 kwenye akaunti ya NBC bila ya kuhusisha upande wa pili wala kumuhusisha Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya ambae ni Mmoja ya watia saini kwenye akaunti hiyo.

Kwa upande wetu hatukuona shida pamoja na kutojuliswhwa kwakua tunajua kua pesa hizo zinaenda kwenye Uchaguzi wa Jimbo la Dimani. Mtatiro hawezi kuyafahamu haya kwakua si Kiongozi wa Chama hiki.

Tunawataka Wanacuf kupuuza kelele hizo kwakuwa zinalenga kuwatoa kwenye Harakati za kutafuta ushindi wa Chama na Wagombea wetu kwenye Uchaguzi huu wa Madiwani. Si kosa na wala hakuna shida yoyote kwa Ofisi ya Msajili kutupatia Ruzuku hiyo na kama Kuna Kiongozi yeyote ambae yupo kwa mujibu wa Katiba yetu na anataka kujua Matumizi yake basi asubiri Vikao vya Chama.

Abdul Kambaya

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

HAKI SAWA KWA WOTE

CUF yadai kuibiwa mil. 369/- za ruzuku

$
0
0
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuibiwa fedha za ruzuku zaidi ya Sh milioni 369 huku chama hicho kikiwahusisha waliokuwa viongozi wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba na Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya.

Aidha chama hicho kimemuomba Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na vyombo vingine vinavyohusika, kuchukua hatua za dharura za kuokoa fedha hizo.

Hata hivyo, Sakaya ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Bara, alisema fedha hizo hazijaibiwa kama ambavyo inadaiwa, isipokuwa kwa nafasi aliyonayo ndani ya chama alimuandikia Msajili kuomba fedha hizo kwa ajili ya chama kuingia katika uchaguzi, ndipo zikaingizwa katika akaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, Julius Mtatiro alisema CUF imeibiwa Sh 369,378,502.64 za ruzuku.

“Fedha hizo zilitoroshwa kutoka Hazina ya Serikali Januari 5 mwaka huu na kuingizwa kwenye Akaunti ya NMB tawi la Temeke yenye jina la The Civic United Front ikiwa na akaunti namba 2072300456,” alisema Mtatiro.

Alisema katika tukio hilo la wizi, Hazina imetorosha ruzuku hiyo kwa kumuamini Lipumba, Sakaya, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Thomas Malima na genge lao ambao walishavuliwa uongozi na pia uanachama.

Hata hivyo, Mtatiro alisema kuwa baada ya kugundua utoroshwaji huo, CUF imejiridhisha kuwa akaunti ambayo Hazina wameshiriki kuitumia kutorosha fedha za umma na mali ya CUF ni akaunti ya CUF, ambayo hutumiwa na Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kupokea mgawo wa ruzuku kutoka kwa Chama Taifa.

Aidha, Mtatiro alisema vikao vya kitaifa vya CUF, yaani Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, havikuwahi kupitisha maamuzi yoyote kwamba fedha za CUF ziwekwe katika akaunti hiyo ya wilaya iliyoko NMB Temeke.

Mtatiro alisema siku mbili kabla ya utoroshaji wa fedha hizo, ulisukwa mpango wa kuwaondoa baadhi ya viongozi wa CUF wa Wilaya ya Temeke kwenye utiaji saini unaoihusu akaunti tajwa; na kuwafanya watu wa Profesa Lipumba kuwa watia saini, ambao ni Sakaya na Malima.

Alisema watia saini hao wapya, waliulizia kiasi cha fedha kilichomo kwenye akaunti hiyo na walifanya hivyo katika tawi la NMB Mandela Road.

Alisema kesho yake, wakiongozwa na Malima walikwenda katika Benki ya NMB tawi la Temeke na wakatoa Sh milioni 69 na kuhamisha Sh milioni 300 kwenda kwenye akaunti ya mtu binafsi kwenye akaunti ya NMB 41401600207 ikimilikiwa na Diwani wa CUF wa Handeni mkoani Tanga.

“Mtu huyu ni wa karibu na Lipumba na ni mmoja kati ya wanachama wanane waliosimamishwa uanachama na Baraza Kuu, jana (juzi) akaunti hii ilikuwa kwenye mchakato wa kuondoa fedha hizo kutoka kwenye akaunti hiyo, na kubaki na Sh 207,907 tu,” alisema Mtatiro.

Alisema mtu huyo alitoa Sh milioni 100 kutokea Benki ya NMB tawi la Magomeni, kisha akiwa hapo Magomeni akatoa Sh milioni 50, tawi la Kariakoo alitoa Sh milioni 100 na mwisho akatoa tena Sh milioni 49.5 huku wakiwa na ulinzi wa polisi na gari ya chama hicho akiwa na Sakaya na wengine.

“Hadi tuongeavyo sasa miezi mitano CUF inadai ruzuku ya Shilingi milioni 635 na kwa kuwa fedha zilizotoroshwa Hazina zimepelekwa kwenye akaunti isiyotambuliwa Bodi ya Wadhamini ya chama inatamka kuwa hadi sasa ruzuku yake ni Shilingi 635,000,000,” alisema Mtatiro.

Ntatiro alisema Bodi ya Wadhamini ya CUF inakutana na pia Kamati ya Utendaji ya Taifa ya CUF pia kwa ajili ya kutafakari tukio hilo kubwa la chama na kuelekeza hatua za kiutawala na kisheria za kuchukua haraka.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sakaya alisema chama kimepata nafasi ya kushiriki uchaguzi mdogo katika kata 14 kati ya 20 za Tanzania Bara, hivyo fedha zinahitajika kwaajili ya maandalizi hayo hivyo aliamua kumuandikia Msajili kuomba fedha.

“Hizo fedha hazijaibwa wala nini, hao wanaoongea hawajui wanaongea nini, mimi niliandika barua kwa nafasi yangu kulingana na uchaguzi tulionao mbele yetu nikaomba hizo fedha na zimetolewa kwaajili ya kusambazwa zinakohitajika,” alisema Sakaya ambaye alisema yuko jimboni kwake.

Sakaya alisema taarifa zilizotolewa na Mtatiro, hazina ukweli na kwamba Mtatiro hana nafasi yoyote ndani ya chama. Alisema ukweli ni kwamba Msajili kuweka fedha kwenye akaunti hiyo ya tawi la Temeke ni sahihi, kwani ana maamuzi ya kuweka popote ili mradi zinaingia katika akaunti zinazomilikiwa na chama.

Aidha alisema pia kuwa ni kweli fedha hizo zimetolewa na ni kwa ajili ya kusambazwa katika halmashauri ambazo zinahitajika kuendelea na kampeni za uchaguzi. Uchaguzi huo mdogo wa viti vya udiwani utafanyika Januari 22 mwaka huu.

Lipumba pamoja na viongozi na wanachama wengine 10 Agosti mwaka jana walisimamishwa uanachama na Baraza kuu la Uongozi la Taifa lililokutana katika kikao cha dharura huko visiwani Zanzibar hata hivyo maamuzi hayo yalitenguliwa na Msajili wa vyama vya Siasa.

Kikao hicho pia kilimteua Mtatiro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi itakayokuwa na wajumbe wawili ambao ni Katani Ahmed Katani na Severina Mwijage, ambayo itafanya kazi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hadi hapo utakapoitishwa Uchaguzi mwingine wa kujaza nafasi hizo.

Amjeruhi vibaya mwanawe kwa kumtahiri kwa kisu

$
0
0
MKAZI wa Kijiji cha Mihingo wilayani Bunda mkoani Mara, Marwa Elias (28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda kwa tuhuma ya kumtahiri vibaya kwa kutumia kisu, kukata kipande kikubwa cha uume wa mtoto huyo na kumsababishia madhara makubwa mwilini mwake.

Mtoto huyo mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Mihingo, amefanyiwa ukatili huo na mwanaume huyo, na kumsababishia ulemavu huo. Kwa sasa mtoto huyo anajisaidia haja ndogo kwa shida huku akisikia maumivu makali kutokana na kukatwa sehemu hiyo ya siri vibaya.

Elias alifikishwa katika mahakama hiyo na kushitakiwa kwa kosa la kumfanyia madhara makubwa mwilini mtoto huyo.

Mwendesha mashitaka wa Polisi, Masoud Mohamed, alisema kuwa mtu huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo Aprili 10, mwaka jana, saa nne asubuhi katika eneo la kijiji hicho kinyume cha sheria.

Mohamed alidai mbele ya Hakimu Abelina Kashushura kuwa mtuhumiwa huyo, alitenda kosa hilo wakati akimtahiri kwa kutumia kisu mwanafunzi huyo wakiwa nyumbani kwa mtoto huyo katika kijiji hicho cha Mihingo.

Ilidaiwa kuwa wakati mwanaume huyo akiendelea na kazi hiyo, alimjeruhi vibaya mwanafunzi huyo (jina lake limehifadhiwa) kwa kumkata sehemu kubwa isivyo kawaida ya eneo hilo. Aidha, ilidaiwa kuwa baada ya tendo hilo, mtuhumiwa huyo alitoweka na kwenda kwenye shughuli zake, akimuacha mtoto huyo akiwa na hali hiyo.

Kwamba, baadaye hivi karibuni alikamatwa na kufikishwa polisi na kisha mahakamani hapo.

Baada ya kusomewa shitaka lake mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na kupelekwa mahabusu katika gereza la Nyasura, nje kidogo ya mji wa Bunda, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 23 mwaka huu, itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Kesi hiyo iliahirishwa na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya mjini Bunda, Abelina Kashushura, kutokana na mahakimu wa mahakama ya wilaya hiyo, kutokuwepo siku hiyo mahakamani hapo kwa sababu ya kuwa dharura.

Mbaroni kwa kumchapa mwanamke viboko 30

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawashikilia watu 10 kwa udhalilishaji wa kumchapa viboko mwanamke hadharani.

Watu hao ni wa kijiji cha Kinesi tarafa ya Suba wilayani Rorya. Miongoni mwa watu hao, wamo viongozi watano wa baraza la mila liitwalo Irienyi ndogo la kabila la Wasimbiti.

Watu hao wanatuhumiwa kumchapa viboko zaidi ya 30 hadharani mwanamke huyo, kitendo kilichomdhalilisha mbele ya jamii.

Mapema wiki hii, baadhi ya video ilisambaa katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha mwanamke akichapwa viboko na wanaume kwa zamu huku akilia mbele ya hadhara na sauti za wanaume zilisikika zikishabikia kitendo hicho.

Kamanda wa Polisi Tarime/ Rorya, Andrew Satta alisema kuwa tukio hilo ni la Desemba 23 mwaka jana mchana katika kitongoji cha Migutu kijiji cha Kinesi tarafa hiyo ya Suba wilayani Rorya katika maeneo ya Mastooni, ambako kulikuwa na mkutano wa Ritongo wa mila.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa kijiji hicho (jina limehifadhiwa) aliitwa na kufuatwa na vijana na kupelekwa katika mkutano huo wa mila, uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa kijiji hicho. Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alimtuhumu mama yake mzazi wa umri wa miaka 55 kuwa ni mchawi.

Kwamba hamtambui na kumkana kuwa si mama yake mzazi; huku akidai kuwa mama huyo anataka kumuua kwa uchawi. Kamanda Satta alisema katika mkutano huo wa baraza la mila la Irienyi, vijana sita waliamriwa kumchapa kila mmoja viboko vitano makalioni mwanamke huyo, hali iliyomsababishia majeraha, kumuathiri, kumdhalilisha na kumshushia utu wake kwa jamii.

“Tumewakamata mwenyekiti wa baraza hilo, viongozi wenzake wanne na vijana sita walioshiriki kumkamata na kuadhibu kwa kumlaza chini, kumchapa viboko na kumsababishia madhara makubwa mwilini na kumdhalilisha,” alisema Kamanda. Alisema watuhumiwa hao wanahojiwa na jeshi hilo linaendelea kuwasaka wengine waliohusika.

Pambano la Chris Brown na Soulja Boy kufanyika Dubai

$
0
0
Drama ya pambano la Chris Brown na Soulja Boy inazidi kushika kasi. Imedaiwa kuwa pambano la ngumi la wawili hao lipigwa katika ulingo huko Dubai.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa TMZ, wawili hao wamekubali kupigana kwenye pambano hilo ila wanachotaka ni kupata fedha zaidi kupitia kwa watu ambao watataka kuangalia pambano hilo [Pay-Per-View].

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika mjini Las Vegas lakini kutokana na sheria zilizopo katika mji huo kutokana na mapambano kama hayo ndio imesababisha kubadilishwa kwa ratiba hiyo. Hata hivyo imedaiwa kuwa pambano hilo litakuwa ni kwa ajili ya kujitolea na fedha zitakazopatikana zitatolewa kama msaada.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>