Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Ya Young Dee na Meneja Wake Max Rioba, Muda Utatuambia!

$
0
0

Ukweli na muda ni ndugu, tena ndugu haswa waloshibana. Muda haujawahi kuacha ukweli upite bila kujulikana – inaweza kufika kipindi ukahisi pengine muda na ukweli vimetengana lakini pale inapobidi ukweli kudhihirika muda huacha ukweli udhihirike.


Miezi michache iliyopita rapa Young Dee pamoja na meneja wake Max Rioba waliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwa kile walichokiita Young Dee kuomba radhi kwa kujiingiza kwenye madawa ya kulevya na kuahidi kurudi katika hali ya kawaida na kufanya muziki.

Ilikua habari nzuri kwa mashabiki wa Young Dee na watanzania kwa ujumla kuona Young Dee amesanuka kabla mambo hayajaenda kombo zaidi. Lakini habari ni kuwa Max yule aloenda naye kwenye vyombo vya habari amenukuliwa akisema eti Young Dee amerudia kutumia, ngada!

Yananijia mambo mengi kichwani, mosi; inaweza kuwa Max anamchukia Young Dee,lakini amchukie kwa kwa sababu gani? Kwa lipi analolipata kwa yeye kumchukia? Au pengine kuna watu wanampelekea Max maneno yasiyo ya kweli? Yes hili ni jibu sahihi kwangu nahisi. Pengine naweza kuonekana mwendawazimu kwa kuamini eti kuna watu wasiompenda Young Dee wanamharibia kwa Max, kwa kumpelekea uzushi na maneno yasiyo ya kweli

Kwanini naamini hivyo? Kwa sababu sitaki kuamini Young Dee ameamua kucheza na akili za watanzania kuwaambia ameacha kutumia Ngada halafu eti miezi michache mbele arudie kule?! Sitaki kuamini kuwa ni kweli kwa sababu siamini Young Dee haoni jinsi ambavyo wasanii wanaotajwa kutumia madawa wanavyodhalilika na kudhihakiwa kwenye mitandao ya kijamii. Naamini vipi kijana alotoka kuitwa baba juzi tu hapa akasahau kuwa ana jukumu la kumlea mwanaye na kujitumbukiza kwenye madawa siamini kama youngdee anaweza akasahau hilo!

Lakini kama alivyo sema yeye Young Dee, “time will tell” ngoja tusubiri na tuone,japo sitamani muda unapokuja kutuambia ukweli awe kwenye hali mbaya. Sitamani kuona ukweli ukiniacha nikijiona mwendawazimu kwa kumwamini Young Dee kiasi hicho. Lakini angalizo ndugu yangu kama yanayosemwa ni kweli usiogope kuupokea ukweli mchungu,mwanadamu anapoendelea kuvuta pumzi anakuWa ana nafasi zisizo na idadi za kujisahihisha. Umri na wakati bado ni rafiki kwako unaweza ukajisahihisha bila hata Dongo Janja kujua kuwa ulikosea. Kazi kwako Daudi.

By Eliezer Gibson ”greencitynative

IG:gibson_elly

Walio Mwibia Young Dee Account ya Instagram Wairudisha....Young Dee Afunguka Haya

$
0
0

Rapper Young alihakiwa akaunti yake ya Instagram yenye followers Milioni Moja na kuibadili jina kisha kuanza kutangaza matangazo ya biashara mbali mbali ila leo ameweza kuipata account hiyo

Meseji kutoka kwa Young Daresalaama hii hapa chini:

"YoungDaddyIsBack .
I got my account back!!! Sijui hata nianzie wapi kuwashukuru, You guys are more than fans, you are family to me now... Account nisingeipata bila support yenu!!! I Thank God for giving me the strength to Stand Positive! 🙏🏽Thank you guys for supporting me!!🙏🏽 Thanks to the Media Supporting my Music!!!🙏🏽Bila Support yenu kiukweli sijui, only God knows. Shukran za dhati ziende kwa kila mmoja wenu!!! 🙏🏽🙏🏽🙏🏽 #YoungDaddyIsBack #GodBlessThisHustle "

Label Kubwa za Nje Zinazowasaini Wasanii wa Afrika Kwa Lengo la Kuwapoteza Kwenye Ramani ya Muziki

$
0
0


⏩Rapper na mwanazuoni Nikki wa Pili, amefunguka kwa kudai kuwa label kubwa kutoka ugaibuni zinakuja Afrika kusaini wasanii kwa lengo la kuwanyonya na baadae kuwapoteza kwenye ramani ya muziki.

Rapper huyo wa Kundi la Weusi amezifananisha label hizo na makampuni ya madini kutoka Ulaya ambayo amedai mara nyingi yakuja nchi za Afrika kwaajili ya kupora rasilimali.
.
. “Ujio wa makampuni makubwa ya muziki Africa toka ugaibuni, hauna tofauti na makampuni ya madini, lengo ni lile lile uporaji..time will tell,” alitweet Nikki wa Pili.

Aliongeza kupitia Instagram kwa kusema, “Afrika Kusini na Nigeria muziki wao wameukuza na kuutangaza wenyewe, toka enzi za P Square mpaka Wizkid, au toka Marium Makeba mpaka Mafikizolo. Ujio wa wageni ndiyo unakuja kuushusha. Mtazame #Davido toka amesainiwa na Sony na kabla ya hapo au #Keko wa Uganda, au #RoseMhando. Hawa walisainiwa Sony na pili makampuni hayo lengo ni kufungua milango ya huku kwa muziki wa nje ndiyo maana Mtv Awards main artist alikuwa Future”


Hapa nchini Tanzania kwa sasa ni @officialalikiba pekee ndiyo ambaye yupo chini kampuni ya Sony.

⏩KARIBU KUTOA MAONI YAKO7

VIDEO:Obama Atoa Hotuba ya Kuwaaga Wamarekani iliyowaliza Wengi

$
0
0
Obama anaondoka na historia ya kuwa Mmarekani Mweusi wa kwanza kuwa Rais wa nchi hiyo. Ameshika nafasi hiyo kwa mihula miwili

Kwenye hotuba hiyo iliyokuwa imejaa hisia na simanzi, Rais Obama amewataka Wamarekani kulinda demokrasia yao.

Kuhusu masuala ya rangi kwenye hotuba yake Obama amesema: After my election, there was talk of a post-racial America. Such a vision, however well-intended, was never realistic. For race remains a potent and often divisive force in our society. I’ve lived long enough to know that race relations are better than they were 10, or 20, or 30 years ago

Amewataka Wamarekani wa kila kundi kufikiria mambo kwa mtazamo wa kila mmoja na kuwataka wasikilizane. Wafuasi wake walisikika wakipiga kelele ‘miaka mine tena’ lakini kwa tabasamu akawajibu ‘siwezi kufanya hivyo.’


Michelle akimkumbatia kwa hisia kali mume wake Barack Obama baada ya kupanda jukwaani kuungana naye


Kwenye hotuba hiyo, Obama amemuelezea mkewe Michelle: Michelle LaVaughn Robinson, girl of the South Side, for the past 25 years, you’ve been not only my wife and mother of my children, you have been my best friend. You took on a role you didn’t ask for and you made it your own with grace and grit and style and good humour. You made the White House a place that belongs to everybody.

Mastaa wengi wa Marekani wameonesha kumlilia Obama kupitia mitandao ya kijamii na kumpongeza kwa utawala wake. Chini ni miongoni mwao:

Karrueche
Please don’t go 😢

Jamie fox
will never forget when you became our president… there will never be another one like you…. class… Compassion… And courage!!!

Martin Lawrence
Sad to see you go. You served our country with such class and dignity. #Obama #MichelleObama #Hope #YesWeCan #YesWeDid #BlackHistory



Anthony Hamilton

This Is Embedded in My Soul. The Image Of True Black Love. Go On Y’all! Represented Us Well. Let’s continue the legacy.

Young Jeezy

My President was Black! Congrats on 2 Great terms.. You got 10 more days in office. If you could free meech on your way out that would complete 8 years of Legendary run.. @barackobama 💯 Good luck on your future endeavors🙏

Nas

Barack Obama is one of the Brightest human beings I have ever met. Such an inspiration. The realest human being. The coolest of the cool, always kept his head high through the bad. Fair, strong, wise, a HERO to all people everywhere. Loved by many, missed by all. #salute #HSTRY

Marlon Wayans
Thank you @barackobama for always being a pilar of hope, a conduit for communication, a good hearted, strong willed, example of a man. You and your family have blessed us to dream outside the velvet rope. Thank you so much for your service. You will be missed


Ludacris
History has been made. #farewell

Justine Skye
😭😩💔 Thank you for showing the world that anything is possible #YesWeCan #YesWeDid


Madonna
Good-bye Mr. President! 🇺🇸There will never be another one like you! 🙏🏻 Barak Obama you are a King amongst Men

Drake

As a Canadian that calls America home for part of the year I will always carry your words and the memory of your time in office with me as inspiration. Big up yaself O.

Mwanaume Ataka Kumlipa Mungu Pesa Ili Amsamehe Dhambi zake...Azikwa na Dola Elfu Tano

$
0
0
Charles Obong alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake

Mwanamume mmoja nchini Uganda amezikwa pamoja na dola 5,700 pesa taslim, ambazo alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake na kumuokoa kutoka kwa moto wa ahera.

Charles Obong, mfanyakazi wa zamani wa serikali ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 52, aliomba hilo kwenye wosia wake, kwa mujibu wa familia yake.

Licha hiyo kutekelezwa, kaburi lake lilifukuliwa na pesa hizo kuondolewa kutoka wa jeneza lake, baada ya wazee wa jamii kufahamu kilichotokea, kwa mujibu wa gazeti la the Daily Monitor.

Gazeti hilo lilimnukuu askofu mmoja wa kiangilikana Joel Agel, akisema hakuna pesa zinazoweza kununu uzima wa milele na Mungu hawezia kupokea pesa kama malipo.

Emmanuel Mbasha Atoboa Siri ya Flora Mbasha Kuzaa Nje ya Ndoa...Adai Bado Anamuitaji Warudiane

$
0
0
Msanii wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji aliyekuwa mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya ndoa na mwanaume mwingine.

Muimbaji huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa kipindi cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo.

“Moyo wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo yametokea 2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani tuendelee na maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee na maisha. Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado amekuwa mgumu lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana akaamua yeye kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV..

“Mimi sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata mtoto labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza.

Muimbaji huyo alishinda kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada ya Mahakama kuthibitisha muimbaji huyo hakuwa na hatia.

Kesi hiyo ilifunguliwa na mke wake huyo akimtuhumu aliyekuwa mume wake huyo kumbaka binti yatima ambaye walikuwa wanaishi naye.

Jerry Muro Adai Simba Wasinge Shinda Wangeweza Vunja Hata Muungano

$
0
0
Baada ya klabu ya Yanga kuambulia kichapo cha penati nne kwa mbili katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi Jumanne hii, aliyekuwa afisa habari wa klabu ya Young Africans Jerry Muro ambaye kwa sasa bado anatumikia adhabu ya kufungiwa na TFF, amewatupia dongo watani wake wa klabu ya Simba.


Mashabiki wa Klabu ya Simba amekuwa wakitaniwa mara kwa mara na mashabiki wa Yanga baada ya kufanya tukio la kuvunja viti katika uwanja wa Taifa wakati wa kicheza na watani wao wajadi Yanga.

Muro amerusha kijembe hicho kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuandika
‘Sikilizeni nyinyi…Bora hata Simba mmeshinda, maana mlivyo watata mngeweza hata vunja Muungano’

Watani hao wa jadi wanatarajiwa kukutana tena katika mzunguko wa pili wa ligi kuu wa Tanzania bara ambayo sasa hivi imesimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi.

Rosa Ree: Wasanii wa Hip Hop Wananitaka! (Video)

$
0
0
MKALI wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rosa Ree kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa, kuna wanamuziki wengi wa Hip Hop wanamtaka kimapenzi kupitia Global TV Online. Rosa Ree anayebamba na Ngoma ya One Time alisema kuwa, kwa sasa hana uhusiano na mwanaume yeyote japo kuna wakali kibao wa Muziki wa Hip Hop wamekuwa wakimtaka kimapenzi.

 “Nilishawahi kutongozwa na wasanii wenzangu wengi tu lakini kikubwa sitaki kuingia katika uhusiano kwani naamini kuwa na mtu unayemtaka ni mipango ya Mungu na siku ikitokea nitakuwa naye,” alisema Rosa Ree ambaye pia ni memba wa Lebo ya The

Industry. Tazama Video:
Stori: Credit to Andrew Carlos

Mama Kanumba: Huyu Ndiye Mrithi wa Kanumba, Naamini Atanifuta Machozi!

$
0
0
DAR ES SALAAM: Wakati ikiwa inakaribia miaka mitano tangu  Aprili 7, 2012, ambapo aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, alipoaga dunia, mama yake mzazi Bi. Flora Mtegoa ametembelea kaburini kwa marehemu mwanaye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake akiwa ameambatana na kijana aliyemuanika kuwa ndiye mrithi wa muigizaji huyo nambari one nchini.


Katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita, mama huyo alisema siku ya kwanza kuonana na kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Fredy Swai, alipatwa na mshtuko mkubwa kwa sababu alimuona anafanana mno na mwanaye, tofauti na watu wengine ambao mara kadhaa wamekuwa wakifananishwa na mkali huyo wa filamu Tanzania.


Fredy ambaye ni msanii wa Tamthilia ya Dhamira inayorushwa katika kituo cha televisheni cha ITV, ameelezewa na mama huyo kuwa anafanana mno na mwanaye na kwamba anaamini atamfuta machozi siku zote za maisha yake.

Akimzungumzia kijana huyo, alisema alipigiwa simu na kuambiwa juu ya mfanano huo na siku alivyokwenda nyumbani kwake Kimara Temboni, aliamini faraja yake iliyopotea imerejea upya.

“Nimeona ninunue kadi niweke kwenye kaburi la mwanangu kumuenzi kwa maombi, sikutaka kusumbua watu ndiyo maana unaona nimeambatana na vijana wangu wawili tu, huyu Fredy tangu nimfahamu najihisi kama namuona mwanangu, nimekubali kuwa wanafanana sana hao wengine sijawapitisha.fredy-mrithi-wa-kanumba-6

“Kila ninapofika hapa kaburini huwa machozi hayakauki, lakini leo ni tofauti na siku zote, chozi langu halijadondoka, sababu nimempata mrithi wake, mtu ambaye ananifanya nisilie tena, nampenda kama Kanumba, naamini atafuata nyayo zake kwenye sanaa,” alisema mama huyo
Wakiwa makaburini hapo, mambo matatu muhimu yalifanyika, ikiwa ni kusafisha kaburi hilo, kufanya maombi ya kumtakia mema huko aliko, sambamba na kuweka shada la maua na kadi kwa kumuenzi.

Kwa upande wake, Fredy alisema, amekuwa akipata usumbufu mkubwa kwa kufananishwa na Kanumba na mara nyingi amekuwa akiitwa jina la Steve, ndipo watu wakamshauri amtafute mama huyo kwa kuamini anaweza kufarijika akimuona.

“Tangu utotoni, watu walikuwa wanawaambia wazazi wangu wanipeleke kwa Kanumba nikacheze kama mdogo wake, nikawa naogopa kuonana naye kutokana na ustaa aliokuwa nao marehemu,” alisema chipukizi huyo.

Diamondplatnumz amekabidhiwa bendera kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya #AFCON2017

$
0
0

diamondplatnumz amekabidhiwa bendera ya Tanzania na waziri wa habari sanaa na michezo mh Nape nnauye ili kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya #AFCON2017 nchini Gabon ambapo atatumbuiza katika ufungizi wa mechi ya kichuano hiyo.

Emanuel Mbasha Aomba Mungu Amfanyie maajabu Apate Mke Mwingine

$
0
0

Emanuel Mbasha ameandika haya baada kukutana na Masanja akiwa na mke wake.

Embasha - "Bahari beach batani kidogo Masanja na wake ila mie peke yangu duuu Mungu Fanya Muujiza.siitaji ushauri "

Nani ni Muhimu Katika Maisha yako? Soma Hichi Kistori Kifupi cha Kufundisha

$
0
0

Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi;

"Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele"

Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake.

Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake.

Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu.

Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano.

Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee.

Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa.

Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine mawili kati ya yale manne yaliyobaki. Ulikuwa uamuzi mgumu mno kwa Cathy. Bila hiyari akafuta majina ya wazazi wake.

"Futa jingine zaidi tafadhali" mwalimu alimwambia.

Cathy akaishiwa pozi, na huku mikono ikimtetemeka na machozi katika macho yake akafuta jina la mwanae wa pekee. Na kubakiza jina la mume wake, Cathy alilia mno!!!

Mwalimu akamwambia Cathy aende akakae. Baada ya muda kidogo mwalimu akamuuliza Cathy "kwanini mume wako? Wazazi wako ndio waliokulea na kukuza, Mtoto wako ndio huyo tu mmoja uliyenae!! Na unaweza ukapata mume mwingine!!! Kwanini??"

Darasa likawa na ukimya wa hali ya juu, kila mmoja akitamani asikie ni nini Cathy atajibu.

Cathy kwa ujasiri na utulivu akainuka na kusema, "siku moja wazazi wangu watafariki (Mungu anisamehe), mtoto wangu pia ataondoka pale atakapokua mkubwa kwenda kuanzisha familia yake.

Mtu nitakayebaki nae kumaliza nae maisha hasa uzeeni ni mume wangu tu!! Yeye ndiye niliyeunganishwa nae na Mungu, mimi na yeye ni mwili mmoja."

Wanafunzi wote wakasimama na kumpigia makofi kwa kushare nao ukweli na msimamo wa maisha yake.

Huu ulikuwa uamuzi wa Cathy, yeye kwa mtazamo wake alimchagua mumewe.

Je wewe ungechagua nani?

Mwanamke Akamatwa Akitaka Kumtorosha Mpenzi Wake Gerezani Kwa Kumweka Kwenye Begi

$
0
0

VENEZUELA: Mwanamke mmoja(Antonieta Saouda) akamtwa akiwa katika harakati za kujaribu kumtorosha mpenzi wake(Ibrain Garcia) kutoka katika gereza la Jose Antonio Anzoategui.

Mwanamke huyo alikwenda kumtembelea mpenzi wake huyo akiwa na mtoto wao mwenye umri wa miaka 6 ndipo aliamua kumuweka katika begi la nguo na kuanza harakati za kumtorosha.

Mbunge Peter Lijualikali wa CHADEMA Atupwa Jela Miezi Sita Bila Faini

$
0
0

KILOMBERO: Mbunge Peter Lijualikali wa CHADEMA pamoja na dereva wake John Bikasa wamehukumiwa miezi 6 jela bila ya faini.
Wawili hao walikuwa na mashtaka ya kuwashambulia Askari wa Jeshi la Polisi.

Rais Magufuli: Magazeti Yanayoandika Kuna Njaa Yamenunuliwa na Wanasiasa na Wafanyabiashara

$
0
0
Anaejua kuna njaa nchi hii ni Rais, mimi ndio ninayejua wapi kuna njaa na wapi hakuna. Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa,anasema Rais JPM kutoka Simiyu

Wanaotangaza kuna njaa ni watu wanaolipwa pesa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema nchi ina njaa na ukame wa kuuwa watu na mifugo.

Yapo magazeti yanayotumiwa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema Tanzania kuna njaa. Kuna mfanyabiashara mmoja ana tani 25,000 za mahindi bandarini anataka aingize bila kodi kwa kisingizio cha njaa Tanzania. Rais anasema ameagiza alipe kodi na asipitishe mahindi hayo bure kwa kisingizio cha njaa, Tanzania haina njaa.

Kuna mfugaji mwingine walimlipa hela wanasiasa huko Mvomelo, akaenda mbele ya Tv na kusema ana mifugo inakufa kwa ukame.

"Nimeagiza wamwambie auze hizo ng'ombe ili aepukane na ukame. Huwezi kuwa na ng'ombe karibu elfu na zaidi na wanakufa ng'ombe 16 unaanza kulialia badala ya kuuza upate hela ya kula na ujikimu kimaisha."

Rais anasema hatapeleka chakula Simiyu na Bariadi eti kisa ukame. Wananchi walitakiwa kujua kama mvua ni ndogo basi walime mazao yanayostahimili ukame na si kulazimisha kulima mahindi yanayohitaji mvua nyingi. JPM anasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu na yeye anasema ukweli kuwa hataleta chakula popote kwa sababu ni wanasiasa na wafanyabiashara ndio wananunua magazeti kutangaza njaa.

Rais kamuumbua Dr Kamani, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu anayemtaka Rais aruhusu kuingiza mifugo kwenye hifadhi, wakati yeye akiwa waziri wa Mifugo wakati wa JK hakufanya hivyo, sasa kama sio unafiki ni nini? JPM anasema yeye sio mnafiki, hataruhusu mifugo kuingia kwenye hifadhi kwa sbb ya sifa za kisiasa huku akiharibu mazingira.

Rais anasema Watanzania walizoea kuambiwa maneno "matamu matamu" na wanasiasa huku muda ukienda bila kuwa na maendeleo. Yeye anataka watanzania wasahau maneno matamumatamu. Ataongea ukweli tu,tena ukweli mchungu hata kama utawaudhi watu, kama ni jiwe atasema jiwe na sio mchanga mgumu uliokusanyika pamoja.

Rais amewaomba Watanzania wazidi kumuombea, wapo "wapinzani" wake wanamsimanga kwa kununua ndege, na wakati kwa miaka mingi Tanzania haikuwa na ndege, na hao wanaomkosoa ndio hao hao wanaokimbilia kuzipanda.

Baadae Rais akamuita mhandisi Maji wa Mkoa wa Simiyu ili aje aelezee mpango wa Maji kutoka Ziwa Victoria kuja mkoa wa Simiyu na Wilaya zake... Mhandisi hakutoa majibu mazuri, akaja RAS ambaye akasema kikwazo ni mlima wa Ngasamo ambao una madini ya Nikel(?) ambao ndio ilipaswa kuwa na tank la kuleta maji. Eneo hilo tayari kuna muwekezaji na hawawezi kuweka tank.

Rais ameamuru mgodi huo usipewe leseni na huyo muwekezaji apewe taarifa kuwa huo mgodi haupo tena na watu wapewe eneo la kuweka Tank. Amemuagiza Kamishna wa madini aifute leseni na ujumbe umfikie Waziri wa Madini na autekeleze.

Na mwisho Rais amesisitiza watu wafanye kazi,hakuna wa kugawiwa chakula bure.Hawezi akawasomeshea watoto bure,ajenge barabara, anunue ndege, ajenge hospitali na kuweka madawa ktk hospital, alete huduma ya maji na bado watu wakae tu na kusubiri eti serikali itawatafutia chakula.Watu wafanye kazi ili wapate chakula na si kusubiri chakula cha serikali.

"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA, NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI, WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI, MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU" alisisitiza Rais Magufuli.

Mwishoni Rais amemalizia kwa kusema: "Naweza kuwa sio mwanasiasa mzuri sana, Lakini ipo siku mtakuja kunikumbuka"

Chuchu wa Ray Ajifungua Mtoto wa Kiume

$
0
0


 STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans, hatimaye amejifungua mtoto wa kiume katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili,  akiwa mwanamke wa kwanza kumpatia muigizaji mkubwa kiume  Vincent Kigosi ‘Ray’, mtoto.


Akizungumza Mtanda huu ndugu wa karibu na mastaa hao alithibitisha kujifungua kwa Chuchu na kusema kuwa ujio wa mtoto huyo ambaye wamempa jina la kwanza la Vincent Junior, kuwa ameleta furaha kubwa kwa  Ray.

“Yaani Ray, alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kungalia mpira lakini alipopata habari hiyo alionekana mwenye furaha sana huku baadhi ya mastaa wenzake wakimpongeza,” alisema ndugu  huyo

Daktari Asogeza Mbele Kesi Ya ‘Scorpion’

$
0
0


Kesi ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’, leo imeshindwa kuendelea baada ya daktari aliyemtibu majeruhi anayetajwa katika kesi hiyo, Said Mrisho kushindwa kutokea mahakamani.

Katika viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kama kawaida umati uliokuwa ukitaka kusikiliza kesi hiyo ulifurika mapema asubuhi kutaka kujua kinachoendelea.

Ilipofika mishale ya saa mbili na nusu, Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Ukonga na kuhifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya mahakama hiyo.

Saa tatu kamili chumba cha mahakama kilikuwa tayari kimeandaliwa kwa ajili ya kesi hiyo ambapo Wakili wa Scorpion, Juma Nasoro, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga, Hakimu anayeendesha kesi hiyo, Frola Haule na makarani wote walikuwa tayari kwenye chumba inapoendeshwa kesi hiyo wakimsubiri mtuhumiwa huyo apelekwe ili kesi iendelee.

Saa tatu na robo maafande wa magereza zaidi ya nane wengine wakiwa na silaha nzito walimchomoa Scorpion na kumpeleka kwenye chumba cha mashitaka mbele ya hakimu, Frola Haule.

Scorpion akiwa kizimbani, Wakili Katuga aliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa nne upande wa Jamhuri ambaye ni daktari aliyemtibu majeruhi kutoa ushahidi wake.

Wakili huyo alisema shahidi huyo alitoa udhuru mahakani hapo kuwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa yuko nje ya kituo cha kazi hivyo ameomba kesi hiyo iahirishwe na shahidi huyo apewe wiki mbili au tatu.

Baada ya ombi la wakili huyo, mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo mpaka Januari 25 mwaka huu ambapo Scorpion alirudishwa rumande.

Magufuli "Naweza Kuwa Sio Mwanasiasa Mzuri ila ipo siku Nitakumbukwa"

$
0
0

RAIS John Magufuli amesema inawezekana asiwe mwanasiasa mzuri, lakini siku moja atakumbukwa kwa mambo ambayo anayafanya, kwa sababu dhamira yake ni nzuri katika kusimamia ubadhirifu wa fedha za umma na kusimamia miradi ya maendeleo ili watanzania wote wanufaike.

Pia amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi. Aidha, katika kusimamia kauli zake mkoani Simiyu, Rais Magufuli ameagiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu ambayo aliweka jiwe la msingi, ujenzi wake jana kujengwa kwa Sh bilioni 10 na kukataa kiwango kilichokuwa kimekadiriwa cha Sh bilioni 46.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Somanda wilayani Bariadi, kabla ya kwenda kuzindua ujenzi wa barabara.

Awali Rais alikuwa na mikutano mingine katika vijiji vya Nyashimo, Masanzakona, Lamadi na Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Nimeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali, ujenzi wake wamesema ni Shilingi bilioni 46, nimesema kitu hicho hakiwezekani, tena wamekosea sana kuniita mimi kuja kuweka jiwe la msingi,” alisema Rais Magufuli.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inajengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), Rais Magufuli alikataa gharama alizoelezwa, kwa maelezo kuwa ni kubwa.

“Haiwezekani pale Chuo Kikuu Dar es Salaam majengo yote yale yalijengwa kwa Sh bilioni 10, hapa jengo moja Sh bilioni 46, haiwezekani hata kidogo, nitaleta shilingi bilioni 10 kutoka ndani ya Serikali na hospitali hiyo ikamilike,” alisema.

Rais Magufuli alisema amekaa katika sekta ya ujenzi kwa zaidi ya miaka kumi, ambapo alisema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ina majengo 20 yenye ghorofa nne ambazo zilijengwa kwa Sh bilioni 10.

“Mkitaka mkalete majengo yale ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mbandike hapo, mtajua, nyie jengo hilo moja tena la ajabu ajabu, mnasema bilioni zote hizo, haiwezekani na siku ya kuzindua nitakuja mimi,” alisema.

Rais Magufuli alisema fedha za ujenzi wa barabara hiyo zote, zimetolewa na Serikali ambapo alimuagiza Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kilometa 48.9 zilizobaki katika barabara hiyo ndani ya wiki moja, ziwe zimetangazwa kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.

Alisema kwa kujengwa barabara hiyo, wananchi wa mkoa huo wataweza kufanya biashara kwa urahisi, ambapo amewaomba wananchi kuitumia vizuri barabara hiyo na kuilinda.

“Imekuwa ni kawaida barabara ikijengwa inakuwa chanzo cha ajali, watu wanaendesha kwa fujo, badala ya barabara kuwatunza inakuwa ndio chanzo cha mauaji, natoa mwito tuzingatie sheria za barabarani nisije kusikia baada ya siku chache imeua,” alisema.

Rais Magufuli aliwataka wananchi ambao wako ndani ya mita 2.5 kila upande, eneo ambalo barabara hiyo itapita, waanze kuondoka, wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mradi huo.

Rais alisema pia kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa, wanadai kuwa kuna njaa nchini, ambapo alisema kuwa kama kuna njaa, ni yeye atatoa tamko hilo.

“Wapo wafanyabiashara wachache waliokuwa wamezoea panatokea ukame kidogo, wanatumia vyombo vya habari vichache na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa, lengo lao wasamehewe kodi,” alisema.

Alisema wafanyabiashara hao, wameleta mahindi yaliyo katika ubora usiofaa kwa lengo la kuuza bila kulipa kodi ili wapate faida.

“Yupo mfanyabiashara mmoja ameleta tani 25,000 za mahindi, anataka tumsamehe kodi, tumeshamkata kodi na huo ndio mchezo wao, wanawaambia andikeni kuna njaa, anayejua kuna njaa ni Rais,” alisema Rais Magufuli.

Alisema wabunge mwaka jana wakiwa katika vikao vya Bunge, walisema chakula ni kingi na kushauri kiuzwe nchini Uganda, lakini sasa hivi wanadai kuwa chakula hakitoshi.

Hivi karibuni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto, aliitaka Serikali itangaze rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria.

Zitto alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita kupitia ACT-Wazalendo, ambapo alisema bei ya chakula inazidi kupanda kutokana na uhaba wa chakula.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi hata kidogo, na kueleza kuwa jukumu la serikali siyo kugawa chakula cha bure kwa wananchi.

Alisema kuwa serikali haiwezi kutoa chakula cha msaada kwa watanzania zaidi ya milioni 50 nchi nzima, huku akiwataka wananchi kutowasikiliza wanasiasa ambao wanafanya siasa za kizamani.

“Jukumu la Serikali sio kuleta chakula kwa sababu serikali haina shamba la kulima, ni lazima niwaambie ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli, na wanasema asiyefanya kazi na asile…. maana yake na asipokula si afe, niwaombe mfanye kazi,” alisema Rais Magufuli.

Alibainisha kuwa kazi kubwa ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za fya, barabara, maji, umeme pamoja na elimu, na siyo kutoa chakula cha bure.

Rais alisema kuna maeneo hapa nchini, ambayo mvua zimenyesha na hazikutosha, hivyo wananchi wajipange kulima mazao ambayo hayatahitaji maji mengi na pia kuchukua muda mrefu kabla ya kuvunwa na sio kwamba kuna njaa.

“Ninafahamu wapo wanasiasa wachache ambao wanafikiri mzee bure hajatoka kichwani kwao, kila kitu kikitokea serikali ifanye, serikali ninayoiongoza mimi haitatoa kitu, mlinichagua niwaeleze ukweli na mimi nawaeleza ukweli,” alisema Magufuli.

Aliongeza kuwa bado hajachoka kuendelea kutumbua watumishi wanaowanyonya wananchi wanyonge, ambao wanakula rushwa bila huruma pamoja na mafisadi.

Alisema ataendelea na utaratibu huo. Rais Magufuli leo anaendelea na ziara yake mkoani humo kwa siku ya pili, ambapo atatembelea kiwanda cha chaki wilayani Maswa, ikiwemo kuweka jiwe la msingi barabara ya Maswa – Mwigumbi, Shinyanga.

Awali katika mikutano yake mkoani humo, Rais Magufuli akiwa Busisi mkoani Mwanza, alisisitiza kutotoa msaada wa chakula kwa kaya zinazokabiliwa na tatizo la njaa nchini.

Aliwataka wananchi kuzitumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao yanayostahimili ukame, badala ya kutegemea msaada wa chakula kutoka serikalini.

Wakati huo huo, viongozi wa Wilaya ya Kongwa walitakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kulima mazao yanayostahili ukame ya mtama na muhogo ili kuondokana na njaa inayotaka kuanza kunyemelea wilaya hiyo.

Rugimbana alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara wilayani humo, ambapo alizungumza na kada mbalimbali za viongozi ikiwamo kamati ya ulinzi na usalama, w0atendaji wa halmashauri, viongozi wa CCM na walimu.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Fadhili Nkurlu akizungumza na waandishi wa habari naye aliwataka wananchi wa wilaya yake kutunza chakula pamoja na kukitumia vizuri kiasi kidogo kilichopo na kuwataka wananchi kupanda mazao yanayostahimil ukame.

Mke wa Bilionea Msuya Aomba Mahakama imwachie huru

$
0
0

Mke wa bilionea Erasto Msuya (marehemu), Miriam Mrita na mwenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, iwaachie huru kwa kuwa hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia mahakamani hapo.

Miriam na mshtakiwa mwenzake, Revocatus Muyela, waliwasilisha ombi hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mwambapa, kupitia kwa wakili wao, John Mallya.

Wakili Mallya aliwasilisha ombi hilo baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuiomba mahakama iwape muda ili watekeleze amri, iliyowataka wabadilishe hati ya mashtaka. Hivi karibuni mahakama ilitoa siku mbili kwa upande wa Jamhuri, kubadilisha hati ya mashtaka, kwa kuwa ilibaini hati hiyo ilikuwa na mapungufu.

Baada ya wakili Kishenyi kuomba aongezewe muda wa kurekebisha hati, Mallya alidai amri ya mahakama ni sheria na kama hawatekeleza sheria hiyo, hakuna hati yoyote inayowashikilia washtakiwa hao, hivyo aliomba waachiwe huru.

Hata hivyo, Kishenyi alidai kuwa hawajakataa kutekeleza amri ya mahakama, lakini wanaomba muda, pia wanaweza kuiarifu mahakama kama wanakata rufaa au la. Aidha aliiomba mahakama isikubali ombi la washtakiwa, bali iendelee kuwashikilia kwa mujibu wa sheria.

Hakimu Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 23, mwaka huu ili aweze kutoa uamuzi wa hoja hizo.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa Mei 25 mwaka jana katika eneo la Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, kwa makusudi walimuua Aneth Msuya kwa kumchinja akiwa nyumbani kwake.

Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni mke wa aliyekuwa kaka wa Aneth, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama bilionea Msuya.

Dk Shein Akanusha Kuwa na Ugomvi na Maalim Seif

$
0
0

Wakati Wazanzibari leo wakiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, amesema hana ugomvi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi na kubainisha kuwa wanatofautiana kisiasa na kwamba ni jambo la kawaida na mazungumzo ya muafaka yalishafanyika.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Dk Shein aliyasema hayo mjini Zanzibar Jumatano hii wakati akihojiwa na televisheni ya Azam katika kipindi cha Funguka kuhusu maandalizi ya mapinduzi, utendaji wake kama Rais wa saba Zanzibar, uchaguzi wa Zanzibar na maendeleo ya mchakato wa Katiba.

Pamoja na hayo, Rais huyo amebainisha kuwa anaamini amechaguliwa kihalali na Wanzanzibari, ambapo kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015, hakukuwa na shinikizo lolote kutoka serikalini bali ni maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kubaini mchezo mchafu kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo alisema harakati za kuandaliwa kwa Katiba mpya ya Tanzania, zimefuata taratibu zote kwa mujibu wa Sheria na Katiba katika kipindi chake cha uongozi na Rais mstaafu Jakaya Kikwete na sasa kilichobaki ni kuendelea na mchakato wa kura za maoni na kutungwa kwa Katiba hiyo.

Aidha Dkt Shein alizungumzia Kuhusu sherehe za Mapinduzi, Rais huyo alisema Wazanzibari wanapaswa kujivunia kupatikana kwa mapinduzi hayo kwa kuwa ndio mkombozi na uhuru wao, hasa baada ya kupata mateso na manyanyaso ya kutawaliwa kutoka kwa watawala mbalimbali wakiwemo waarabu kutoka Oman.

Alisema Wazanzibari walitawaliwa tangu mwaka 1553 na Wareno kwa muda wa takribani karne mbili na baadaye Waarabu kutoka Oman kwa takribani miaka 40 hadi pale waasisi akiwemo Abeid Amani Karume, chini ya chama cha Afro Shiraz walipofanikisha mapinduzi na kuikomboa nchi hiyo.

Alisema enzi za ukoloni, Wazanzibari waliteseka ambapo pamoja na kuteswa pia walinyimwa haki ya kupata elimu, kumiliki ardhi ya nchi yao na kukosa fursa ya kupatiwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo afya.

“Hii ni miaka 53 ya uhuru na ukombozi wa Wazanzibari, kwetu sisi mapinduzi haya ni alama yetu, ndio sifa yetu, ndio uhuru na ukombozi wetu. Mapinduzi ndio ishara na njia iliyotukomboa na kutuweka huru na sasa tunajitawala wenyewe,” alisisitiza.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images