Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

CAF yamteua Millard Ayo Kuripoti Moja Kwa Moja Michauno ya AFCON2017 Kutoka Uwanjani

$
0
0
Mtanzania Millard Ayo achaguliwa na shirikisho la soka Afrika katika list ya Waandishi watakaoripoti michuano ya Afrika kutoka uwanjani

Michuano hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Januari 14 2014 nchini Gabon.Katika nchi za Afrika Mashariki na CECAFA kwa ujumla,Uganda ndio atakuwa muwakilishi.

Kila la heri #MilladyAyo


U Heard: Camera ilivyosababisha Beef kati ya Q Chilla na MB Dog

$
0
0
Jana January 11 2016 kwenye U Heard ya Clouds FM kuna taarifa kutoka kwa Soudy Brown kama wewe ni mpenzi wa stori zote za Entertaiment nisingependa upitwe na hii ya kinachoelezwa kuwa ni beef kati ya wasanii Qchilla na MB Dog kutoka kwenye kampuni ya QS Muhonda.

Chanzo cha beef zinaripotiwa kuwa ni upotevu wa Camera ambayo taarifa za mwanzo zinasema kuwa Q Chilla ni muhusika kwenye wizi huo, baada ya Soudy Brown kumtafuta Q Chilla na haya ndiyo yalikuwa majibu yake kutokana na wizi huo wa Camera.

‘Mimi nakaa na wadogo zangu pale nyumbani na hawana tabia ya udokozi ila najua kuna watu wamewekwa kwa ajili ya kunifuatilia na unajua matatizo mimi na MB Dog yalianza kuanzia wake zetu, kwa sababu mimi na Mb Dog tunakaa Apartment moja na haya ni makosa ya QS kutuweka wasanii sehemu moja’ kuhusu camera sisi hatuna shida na camera‘>>>Q Chilla

Pata Kifaa Chenye Uwezo Asilimia 99% wa Kuongeza Ukubwa wa Uume....

$
0
0
Handsome up ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara. Inapatikana kwa @200,000/=tu. PIA kuna Gely ya kupaka @ 120,000/= na Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume @120,000/=.
Na spray ya kuchelewesha kufika kileleni kwa mwanaume @120,000/=

NB.Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON $ CO. Wasiliana nasi kwa no (+255) 0767447444 au
0714335378.
Follow us
@Markson_beauty_pr

Mpira Umetushinda Kabisa. Sasa Tunatoa Bendera Kwa Wanaokwenda Kuburudisha na sio Wanamichezo Tena

$
0
0
Zikiwa zimepita saa chache toka Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Nape Nnauye amkabidhi bendera ya taifa Diamond Platnumz kwenda nayo Gabon kwenye uzinduzi wa kombe la mataifa Afrika kumekua na maoni tofauti kwa namna ilivyopokelewa hatua hiyo hasa kwenye upande wa michezo kwa nchi ya Tanzania.

Mmoja kati ya watu waliotoa maoni yao ni pamoja na Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya nne,Ridhiwani Kikwete ameandika :

‘TFF nadhani mnajua kuwa Mungu wa Watanzania anawaona. Tumefika hapa baada ya Mpira kutushinda kabisa. Sasa tunatoa Bendera kwa wanaokwenda Kuburudisha na sio wanamichezo tena…….. Ngashindwa mie’.

Chuchu wa Ray Ajifungua Mtoto wa Kiume

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans, hatimaye amejifungua mtoto wa kiume katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili,  akiwa mwanamke wa kwanza kumpatia muigizaji mkubwa kiume  Vincent Kigosi ‘Ray’, mtoto.


Akizungumza Mtanda huu ndugu wa karibu na mastaa hao alithibitisha kujifungua kwa Chuchu na kusema kuwa ujio wa mtoto huyo ambaye wamempa jina la kwanza la Vincent Junior, kuwa ameleta furaha kubwa kwa  Ray.

“Yaani Ray, alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kungalia mpira lakini alipopata habari hiyo alionekana mwenye furaha sana huku baadhi ya mastaa wenzake wakimpongeza,” alisema ndugu  huyo

Watanzania waadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Z'bar

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akikagua gwaride la vikosi mbalimbali vya kijeshi katika sherehe za mapinduzi, miaka iliyopita

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein, leo anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sherehe za maadhimisho hayo ambazo mwaka huu zimeanza mapema zinafikia kilele hii leo katika uwanja wa amani visiwani humo huku ukitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali za pande zote mbili, mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.

Pamoja na mambo mengi uwanjani hapo Rais Shein anatarajiwa kukagua gwaride maalum lilioandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo ya mapinduzi matukufu katika visiwa hivyo.

Kwa upande wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, yeye ataongoza wananchi wa Tanzania Bara katika maadhimisho hayo akiwa mjini Shinyanga kwa mkutano mkubwa wa hadhara unaofanyika katika uwanja wa Kambarage.

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12 mwaka 1964, yakiongozwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume.

Dudu Baya afunguka asema ajafulia kama watu wanavyodhani

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amedai ukimya wake kwenye muziki umesababishwa na kuwa busy kwenye biashara na siyo kwamba amefulia kama baadhi ya watu wanavyodai.

Rapper huyo amedai kwa sasa maisha yake yako Mwanza na Kampala akija Dar anakuja kufanya kazi za kisanaa japo alishaamua kupotezea muziki na kufanya biashara zake mbalimbali kwa kuwa haishi kwa kutegemea mziki pekee.

“Dudu Baya sijafulia kama watu wanavyodhani mimi na biashara zangu nyingine na muda mwingi sipo Dar es Salaam. Watanzania ndiyo tabia yao hiyo wakiona msanii haonekani wanadhani amefulia mfano watu walipoona King Crazy GK amepotea walidhani amefulia kumbe alikuwa chimbo anapiga kitabu na saizi tayari ana masters yake” Dudu Baya alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Pia Dudu amesema kauli ya Darasa kuimba kwamba ‘siyo chui, simba wala mamba ngozi yake inamtosha kujigamba’ haijamsumbua kwa kuwa Darasa ni kijana wake na ni msanii ambaye amepambana kwa muda mrefu ila kwa sasa kafanikiwa hivyo anampongeza kwa mafanikio

Watumishi Waliotimuliwa Hospitalini kwa kukosa sifa, wazua sokomoko

$
0
0
Related imageWATUMISHI 10 wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Mbeya (Ifisi) waliotimuliwa kazi na Bodi ya hospitali hiyo kwa maelezo kuwa hawana sifa, wamezua sokomoko hospitalini hapo baada ya kuorodhesha majina ya zaidi ya watumishi 20 wakidai walinunua vyeti.

Watumishi hao walifikisha orodha hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, wakidai kuwa watumishi hao walifanyiwa mpango na baadhi ya viongozi wa hospitali hiyo kuwasaidia kununua vyeti hivyo.

Kwa mujibu wa watumishi hao, vyeti hivyo vilikuwa vinanunuliwa kwa Sh. 200,000 kutoka katika moja ya chuo cha uuguzi jijini hapa.

Mmoja wa watumishi hao walioondolewa hospitalini hapo, Subira Mwanjali, alithibitisha kwenye mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Kanisa la Uinjilisti ambao ni wabia wa hospitali hiyo, kuwa yeye ni miongoni mwa walioombwa fedha hizo kwa ajili ya kununuliwa cheti.

“Mimi ni miongoni mwa watu tulioambiwa tutoe Sh. 200,000 ili nikanunuliwe cheti, lakini nilikataa kwa sababu ninacho cheti changu halisi cha taaluma ya uuguzi. Walituondoa sisi na wakiwaacha watu ambao tunaamini hawana vyeti ila wamenunuliwa,” alidai Mwanjali.

Naye Anne Mwangindwa, alidai kuwa uongozi wa hospitali hiyo uliwaondoa kazini bila kufuata taratibu za kazi ikiwamo kutowalipa stahiki zao.

Alidai kwamba baada ya kuona hawatendewi haki, waliamua kupeleka malalamiko yao kwenye Chama cha Wafanyakazi wa Afya nchini (Tughe) ili wapate haki zao, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.

“Sisi hatukatai kupunguzwa kazini, lakini tunachotaka ni kulipwa stahiki zetu kama zinavyoelekezwa kwa mujibu wa sheria za kazi, wamekuwa wakituzungusha hivyo hatuna imani na hawa watu japo ni watu wa Kanisa,” alisema Mwangindwa.

Kwa upande wake, Esther Mwaswalwiba, ambaye yupo upande wa kundi la waliopunguzwa mishahara, alidai kuwa wamepunguzwa mishahara kutoka Sh. 320,000 mpaka 50,000, kiasi alichosema hakiwezi kuwasaidia kuendesha maisha yao.

Alisema kupunguza mishahara hiyo ni sehemu ya kutaka kuwatengenezea mazingira ya kufukuzwa kabisa kama wenzao walioondolewa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Mchungaji Tito Nduka, alikataa tuhuma zilizoelekezwa kwa uongozi wa hospitali hiyo kwa maelezo kuwa watumishi hao wameondolewa kutokana na agizo la Rais la kuwaondoa kazini watumishi wasio na vyeti.

Alisema watumishi hao waliondolewa na Bodi ya hospitali hiyo baada ya kubainika kuwa hawana vyeti vya kidato cha nne na hivyo hakuna uonevu wowote uliofanyika.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Makalla, aliunda timu ya watu wanane kuchunguza mambo makuu matatu yaliyotajwa kwenye malalamiko hayo.

Timu hiyo inaundwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya, Xavery Mhywela, Maofisa Usalama wa Taifa, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya na baadhi ya maofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Alisema kuwa timu hiyo itafanya kazi ndani ya siku 10 na majibu yatakayofanya hatma ya watumishi hao ijulikane pamoja na waliotuhumiwa kuhusika.

Alikabidhi timu hiyo baadhi ya nyaraka ambazo watazitumia kwenye uchunguzi ikiwa ni pamoja na orodha ya watumishi 21 wanaodaiwa kununuliwa vyeti, majina ya watu 10 waliopunguzwa kazini pamoja na nyaraka zinazoonyesha stahiki zao.

Nchi hii Afrika imeripotiwa kuwepo na ugonjwa wa Zika

$
0
0
Ugonjwa wa Zika husambazwa na mbuAngola imeripoti visa viwili vya kwanza vya ugonjwa wa Zika kwa mujibu wa shirika la Reuters.

"Hadi miezi miwili iliyopita, hatukuwa na kisa chochote, lakini sasa tuna visa viwili vya Zika," Reuters ilimnukuu waziri wa afya wa nchi hiyo José Luis Gomes Sambo.

Lazima tuchukue hatua za kuzuia, hasa katika kukabiliana mbu."

Zika ni ugonjwa unaosambazwa na mbu na umesembaa kwenda nchi kadha tangu uibuke nchini Brazil mwaka 2015.

Ugonjwa huo unaaminiwa kusababisha madhara kwa watota wanaozaliwa.

Trump ayalaumu mashirika ya kijasusi Marekani

$
0
0
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameshambulia mashirikia ya kijasusi nchini humo, huku akisema kwamba wangeweza kusababisha uvujaji wa tuhuma kwamba Urusi imekusanya taarifa hatari kumhusu.
Donald Trump
Trump ameyasema hayo katika mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa habari.

Amevituhumu vile vile vyombo vya habari kwa kutoa taarifa alizoziita kuwa hazina ukweli ambazo amesema zimekusanywa na wagonjwa.

Mashirika hayo ya kijasusi yalimuarifu Trump na rais Obama kuhusu tuhuma hizo wiki iliyopita.

Trump ameendelea kusema kuwa, anatarajia kutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na Vladimir Putin, lakini atahakikisha kwamba Marekani inaheshimika kimataifa kuliko ilivyo sasa.

Alichokisema Lipumba akiwa Morogoro

$
0
0
Morogoro. CUF ndiyo chama cha siasa kinachoweza kupambana na mafisadi, dhuluma na uonevu na siyo vyama vingine.

Hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahimu Lipumba aliyoitoa

kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini  Morogoro.

Profesa Lipumba amesema CCM na Chadema haviwezi kupambana na ufisadi kwa sababu bado vina baadhi ya viongozi waliowahi kutuhumiwa kuhusishwa na ubadhirifu.

Pia, amewataka wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea udiwani kupitia chama hicho, Abeid Mlapakolo ili alete mabadiliko ndani ya kata yao.

Download Application ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza Hapa Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Shehe Mkuu Dar: Diamond Acha Utani na Mungu

$
0
0
DAR ES SALAAM: Kufuatia kauli ya msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba kabla ya kuachia video zake huwa anasali rakaa mbili ndiyo maana huwa zinakubalika kwa watazamaji wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amemjia juu na kumtaka kuacha utani na Mungu.


Kwa kauli yake, wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga, Diamond alisema huwa anafanya maombi maalum usiku kwa kuswali rakaa mbili kabla ya kuachia video yoyote, jambo alilosema kwamba ndiyo siri ya mafanikio yake.

“Unajua mimi huwa nafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye video zangu kwa sababu huwa nasali rakaa mbili usiku na kumuomba Mungu ili nifanikiwe kwa video nzuri, nashukuru Mungu anasikia maombi yangu,” alisema Diamond.


Amani lilipomtafuta Shehe Alhadi na kumuuliza kama alichokisema Diamond kina mashiko yoyote kidini, alisema katika dini ya Uislam, muziki wa kidunia ni dhambi na haukubaliki ndiyo maana wasanii kama Mzee Yusuf, wameamua kujiweka nao mbali kwa sababu ni kumkosea Mwenyezi Mungu.

Akaongeza kuwa, alichokisema Diamond ni kama kumfanyia Mungu utani kwa sababu huwezi kuswali, ukamuomba baraka zake ili uende kufanya jambo ambalo ni chukizo mbele zake. Akasema dua za namna hiyo huwa hazipokelewi na Mungu na yeyote anayefanya hivyo, huzidi kumkosea Mungu.

Shehe mwingine aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutochorwa jina gazetini, alisema anachokifanya Diamond ni sawa na mtu ambaye anamuomba Mungu kabla ya kwenda kuiba, jambo ambalo ni tofauti kabisa na misingi ya dini.

Rayvanny Adai Wasanii Wengi Hupotezwa Kwenye Game na Wanawake Zao

$
0
0

Kwa muda mrefu wasanii wamekuwa wakituhumiwa kuwatumia wanawake hususan wenye majina makubwa kama njia ya kutafuta kiki ili majina yao yaendelee kuwa mdomoni mwa mashabiki.

Hali hiyo imesababisha kutokuwepo na imani kuhusiana na ukweli katika mahusiano mengi ya mastaa wa Bongo ambapo wengi huhusishwa na kutafuta kiki.

Hata hivyo Ray Vanny amedai kuwa kwa msanii, mwanamke sio kiki bali ni stress tu. Akizungumza na Dizzim Online Jumanne hii, @rayvanny alidai kuwa wanawake wamekuwa wakiwapa zaidi stress wasanii na wengi wakijikuta wakipotea kabisa.

Alidai kuwa uhusiano hasa pale unapoanza kuingia kwenye migogoro humfanya msanii apoteze concentration kwenye muziki wake na kupoteza vingi.

Alitolea mfano hata habari za udaku kuhusu girlfriend wa staa fulani kuhusishwa kuwa na uhusiano na mtu mwingine huwachanganya wasanii sababu huonekana kama wana udhaifu.

Izzo Business Aeleza Jinsi Alivyosaidiwa na Chid Benz Kifedha na Kimuziki

$
0
0


Nimewahi kuzungumza na Ditto kwa ufupi na akanieleza kuwa katika watu wenye roho nzuri katika kusaidia watu, Chidi Benz ni namba moja.

Alisema kipindi ambacho rapper huyo ana fedha, washkaji wengi wa karibu yake walifaidika sababu hana tabia ya uchoyo. Izzo Bizness amekiri kuwa mmoja wa watu walionufaika na ukarimu wa Chidi Benz.

“Hata mimi wakati sina kitu yaani, unakuta unampigia simu ‘ebana eh inakuaje uko wapi? Hebu njoo tukutane Ubungo.’ Unaenda unachezea labda shilingi 50 fulani, shilingi 30,” alisema @izzo_biznesss kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha @timesfmtz.

Izzo anadai kuwa pamoja na misaada ya kifedha ya hapa na pale, Chidi alikuwa mtu aliyekuwa akimpa ushauri mwingi uliomjenga kimuziki.

“Chidi atabaki kuwa big brother, kuna mambo ya duniani kila mtu ana mitihani yake lakini hata mimi namuombea, nammiss, game imepoa Chidi ni bonge ya rapper, hamna ambaye hajui, kuna vijana wengi sana ametusaidia,” amesisitiza Izzo biznesss.

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Kutoka Bagamoyo, Shafisha Nyota na Kurudisha Mausiano yako ya Kimapenzi

$
0
0

MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI, (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 48 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI: SHEKH SHARIFU RASHIDI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran, dawa za asili, dawa za kiarabu na majini, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango, ngiri maji na n.k, anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, pia anatoa pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali kulingana na nyota yako, anaouwezo mkubwa wa kutumia jina la muhusika kwa kutatua tatizo lako, anaouwezo wa kumrudisha mtu aliepotea kimiujiza, pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo, WASILIANA NAE KWA SIMU NA WHATSAPP NO: 0718-668347 na 0685-224047, au follow@shekh_sharifu_rashid, Email:shekhsharifurashid@gmail.com

Darassa aweka wazi mpango wa kuachia albamu

$
0
0

Hit maker wa wimbo ‘Muziki’ Darassa amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya albamu yake mpya.

Rapper huyo amedai hatua hiyo itawafanya mashabiki wa muziki wake kupata nyimbo zake nyingi kwa pamoja.

“Tutakuwa na albamu mwaka huu ambayo itarahisisha watu kupata muziki wote wanaouhitaji, tupo kwenye kipindi cha mabadiliko na nafanya ninachoweza kwa watu wangu,” Darassa alikiambia kipindi cha 3600 cha EFM.

Katika hatua ngingine rapper huyo amezungumzia kauli za baadhi ya wasanii wa hip hip ambao wanadai hawajaelewa alishokifanya kwenye wimbo Muziki.

“Na deal na mtu ambae yupo tayari kupokea muziki wangu sitakuwa na comment kwa atakaenipinga. Changamoto zinanijenga badala ya kufikiria kitu chako ukanifikiria mimi kwenye kitu chako maana yake nimekuchallenge,” alisema Darassa.

Wimbo huo wa Darassa bado unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio huku katika mtandao wa YouTube ikikaribia kufikisha views milioni 5.

Shehe Mkuu Dar: Diamond Acha Utani na Mungu

$
0
0
DAR ES SALAAM: Kufuatia kauli ya msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba kabla ya kuachia video zake huwa anasali rakaa mbili ndiyo maana huwa zinakubalika kwa watazamaji wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amemjia juu na kumtaka kuacha utani na Mungu.


Kwa kauli yake, wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga, Diamond alisema huwa anafanya maombi maalum usiku kwa kuswali rakaa mbili kabla ya kuachia video yoyote, jambo alilosema kwamba ndiyo siri ya mafanikio yake.

“Unajua mimi huwa nafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye video zangu kwa sababu huwa nasali rakaa mbili usiku na kumuomba Mungu ili nifanikiwe kwa video nzuri, nashukuru Mungu anasikia maombi yangu,” alisema Diamond.


Amani lilipomtafuta Shehe Alhadi na kumuuliza kama alichokisema Diamond kina mashiko yoyote kidini, alisema katika dini ya Uislam, muziki wa kidunia ni dhambi na haukubaliki ndiyo maana wasanii kama Mzee Yusuf, wameamua kujiweka nao mbali kwa sababu ni kumkosea Mwenyezi Mungu.

Akaongeza kuwa, alichokisema Diamond ni kama kumfanyia Mungu utani kwa sababu huwezi kuswali, ukamuomba baraka zake ili uende kufanya jambo ambalo ni chukizo mbele zake. Akasema dua za namna hiyo huwa hazipokelewi na Mungu na yeyote anayefanya hivyo, huzidi kumkosea Mungu.

Shehe mwingine aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutochorwa jina gazetini, alisema anachokifanya Diamond ni sawa na mtu ambaye anamuomba Mungu kabla ya kwenda kuiba, jambo ambalo ni tofauti kabisa na misingi ya dini.

Ripoti yasema Wanawake wa Ulaya wanapata watoto wachache

$
0
0
 Matukio mengi ya kiuchumi na kitamaduni katika kipindi cha nusu karne iliyopita vinaonekana kusababisha wanawake na wanaume kuepuka kupata watoto

Wanawake barani Ulaya wanapata watoto wachache, hususan kusini mwa bara hilo, ripoti ya Ufaransa imebaini.

Zaidi ya asilimia 5% ya wanawake waliozaliwa miaka ya 1970 huenda wakabakia kutokuwa na watoto kusini mwa Ulaya , ikilinganishwa na asilimia 15% katika mataifa ya kaskazini mwa Ulaya na asilimia 18% katika nchi za magharibi mwa Ulaya.

Sababu zinazochangia ni ukosefu wa soko la ajira na ukosefu wa sera bora za kazi zinazozingatia maisha ya kifamilia, jambo linalosababisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaojitolea kutokuwa na watoto, imeelezea ripoti hiyo.

Lakini ripoti imeelezea kwamba viwango vya watu wasio kuwa na watoto pia vilikuwa vya juu yapata karne moja iliyopita.
 Upungufu wa watoto unaonekana zaidi kusini mwa bara Ulaya

Kiasi cha asilimia 17 hadi 25% ya wanawake waliozaliwa katika karne ya 20 walibakia kutokuwa na watoto, kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vifo vya wanaume wengi wa umri wa kuoa kufa katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, uhamiaji wa vijana wa kiume katika nchi maskini, na athari za mfadhaiko mkubwa wa mwaka 1929.

Tangu wakati huo kulikuwa na idadi kubwa ya watu wasiokuwa na watoto, inasema Taasisi ya masuala ya Idadi ya watu nchini Ufaransa.
Mashariki mwa Ulaya , ongezeko kubwa la idadi ya watoto wanaozaliwa lilidumu zaidi kuliko magharibi

Upungufu wa watoto ulifikia viwango vya chini zaidi miongoni mwa wanawake waliozaliwa kati ya miaka ya 1930 na 1940 - wazazi wa kizazi cha "baby boom" ambacho kiliishi na kunufaika na mafanikio ya baada ya vita kama vile viwango vya chini vya ukosefu wa ajira na hali ya mifumo bora ya kijamii iliyotolewa na serikali za wakati huo.

"Matukio mengi ya kiuchumi na kitamaduni katika kipindi cha nusu karne iliyopita vinaonekana kusababisha wanawake na wanaume kuepuka kupata watoto.

Wanawake wachache imeeleza ripoti kuhusu kupungua kwa watoto barani Ulaya , kutokuwa na mpango wa kupata watoto - badala yake , wengi wao "wamekuwa wakiahirisha uzazi" hadi kujipata mud..

Tovuti ya Man Utd Yaongoza Kutembelewa Duniani

$
0
0
Tovuti ya  Klabu ya Manchester United imeongoza kwa kutembelewa na watembeleaji wengi kwa mwezi  kwa mujibu wa ripoti ya UEFA.

Msimu uliopita Man Utd ilikuwa ikitembelewa na watu milioni 8.6 kwa mwezi ikifuatiwa na Arsenal yenye iliyotembelewa na watu 8.5 na nafasi ya tatu imechukuliwa na Klabu ya Liverpool.

Klabu 20 zinazotembelewa sana kwa mwezi ni:

1.Man Utd – 8.6m
2.Arsenal – 8.5m
3.Liverpool 7.7m
4.Real Madrid – 7.2m
5. Barcelona – 6.3m
6.Fenerbahce – 3.3m
7. Chelsea – 3.2m
8. Dynamo Kiev -3.1m
9.Bayern Munich – 2.9m
10. B Dortmund – 2.7m
11. Al Ahly -2.6m
12. PSG – 2.6m
13.Leicester – 1.9m
14. Tottenham – 1.8m
15. Marseille – 1.8m
16. Sao Paulo – 1.7m
17. Man City – 1.7m
18.Zenit – 1.6m
19. Galatasaray -1.6m
20.Juventus – 1.5m
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images