Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Update: Chanzo cha moto Uwanja wa Ndege wa JNIA, Dar chajulikana

$
0
0
 DAR ES SALAAM: Moto mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno ameuambia mtandao huu kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.

Aidha Meneja wa Uwanja huo ameeleza kuwa kwa sasa shughuli zote za usafirishaji zimeamishiwa Terminal One na zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika.

“Kwanza naomba niwatoe hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja wetu, ni kweli moto umezuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa kuamkia leo.

“Lakini madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee, hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia kule terminal one (Uwanja wa zamani) zinaendelea kama kawaida”. Amesema Meneja huyo.

“Baada ya kuudhibiti moto huo tumerudi kuangalia chanzo tukakuta, mfumo wa umeme uko sawa, hivyo hatujajua chanzo hasa cha moto huo ila tunajitahidi kufanya utafiti ili tujue.” Aliongeza Meneja na kusema taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.
Raia akichukua picha za tukio hilo huku walinzi wakitaharuki.
Vikosi vya ulinzi na usalama vikiwasili eneo la tukio.
Wasafiri wakitaharuki kuona moto huo ukizuka na kusababisha taharuki kubwa miongozni mwao.

Moto ukiwaka viwanjani hapo.

UPDATES: CHANZO CHA MOTO UWANJA WA NDEGE DAR CHAJULIKANA

Taarifa zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, chanzo cha moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salam na kusababisha shughuli zote za usafirishaji Uwanjani hapo kusimama kwa muda, kimejulikana kuwa ni hitilafu ya umeme.

Akizungumza na mtandao wa Global Publshers mapema asubuhi ya leo, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno amesema kuwa, uchunguzi umebaini kwamba, kulikuwa na tatizo la umeme ambalo hata hivyo lilishughulikiwa mara moja.

“Kulikuwa na tatizo la umeme kwenye eneo la kuhifadhia mizigo lakini moto ulidhibitiwa vizuri na sasa shughuli zinaendelea kama kawaida japokuwa bado tunatumia Terminal One (uwanja wa zamani) kwa kuwabeba abiria kwenye mabasi na kuwapeleka panapohusika.

“Kwa sasa ndege zote zinatua na kuruka bila tatizo lolote na kufuatana na ratiba hivyo hakuna hofu yoyote kwani muda si mrefu eneo hilo la mizigo litakuwa limeshawekwa sana, ” alisema Kamanda Otieno.

Aidha Mamlaka ya Uwanja huo imetoa mabasi kwa ajili ya kubeba abiria kuwapeleka Terminal One ambako shughuli za usafirishaji zinaendelea kama kawaida.


Shule yalia kuelemewa wanafunzi

$
0
0
SHULE ya Msingi Bunju `B' iliyopo Kata ya Mabwe Pande Manispaa ya Kinondoni, imeiomba serikali kujenga shule nyingine ili kuwe na shule mbili kutokana na shule hiyo kuzidiwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Angelina Rweyemera, alisema kwa sasa ina wanafunzi zaidi ya 2,060, idadi iliyovuka idadi ya wananfuzi wa wanaotakiwa kuwapo katika shule moja.

Rweyemera alisema kwa kawaida shule moja kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, hutakiwa kuwa na wanafunzi 990, lakini shule yake ina idadi ya wanafunzi wa zaidi ya shule mbili.

Alisema kutokana na wingi wa wanafunzi katika shule hiyo, walimu wamekuwa katika wakati mgumu kufundisha.

"Tunaiomba serikali itujengee shule nyingine zipatikane shule mbili ili wingi wa wanafunzi tulionao sasa katika shule yetu upungue," alisema.

Rweyemera alisema hiyo itasaidia walimu kufundisha vizuri tofauti na ilivyo sasa.

Alisema licha ya shule hiyo hivi karibuni kujengewa vyumba viwili vya madarasa na Manispaa ya Kinondoni vilivyogharimu Sh. milioni 42 na kufanya kuwa na madarasa 18 huku ikipungukiwa na madarasa manne, bado wingi wa wanafunzi ni tatizo kubwa kwa walimu katika kumudu kuwafundisha vizuri.

"Shule ipo katika usalama mzuri kutokana na kuzungushiwa uzio na pia miundombinu ya maji na umeme ni mizuri, ila tatizo ni wingi wa wanafunzi ambao umepita kiasi, hivyo ikijengwa shule nyingine na wanafunzi wakapunguzwa, nina imani hali ya ufundishaji itakuwa bora katika shule yetu, " alisema Rweyemera.

Vigogo dawa za kulevya waja na mbinu mpya

$
0
0
WAFANYABIASHARA wa dawa za kulevya nchini, wameibuka na mbinu mpya ya kuingiza dawa hizo.

Mbinu hiyo ni kuingiza vibashirifu (kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kifua) aina ya ephedrine,  ambavyo huvitumia kutengenezea dawa za kulevya aina ya cocaine na heroin.

Akizungumza na MTANZANIA mapema wiki hii, Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Mihayo Msikhela, alisema wamebaini mbinu hiyo mpya na kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, wamejipanga kila kona ya nchi kudhibiti dawa hizo.

Kamanda Msikhela alisema wafanyabiashara hao huzisafirisha kemikali hizo kutoka Bara la Asia.

“Kikosi cha kupambana na dawa za kulevya tunapambana na kila njia ili kuweza kuliokoa Taifa. Na katika hili tunawaomba Watanzania wote tushirikiane kwa kukataa matumizi ya dawa za kulevya.

“Vibashirifu aina ya ephedrine hutumika kutengeneza dawa za kifua, lakini hawa wafanyabiashara haramu wanabadilisha mfumo wake. Wanachofanya ni kuchanganya na kemikali nyingine na kutengeneza heroin na cocaine,” alisema Kamanda Msikhela.

Alisema wafanyabiashara hao hununua kemikali hizo bila kuwa na kibali cha Serikali na hudanganya kuwa zinatumika kutengeneza dawa za kifua.

Alisema kwa kipindi cha mwaka jana, kikosi chake kiliwakamata watuhumiwa sita wakiwa na vibashirifu hivyo kilo 22,009. Walikwishafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema wanaoingiza vibashirifu wanatakiwa kufuata taratibu za kisheria, ikiwamo kupata kibali kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

TAKWIMU DAWA KULEVYA
Kamanda Msikhela alisema takwimu za mwaka jana zinaonyesha kuwa kilo 17.33 za dawa za kulevya aina ya cocaine zilikamatwa ikilinganishwa na mwaka 2015 zilipokamatwa kilo 7,696.

Kuhusu heroin, alisema kilo 31.77 zilikamatwa mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2015 ambao zilikamatwa kilo 69,346.

WAATHIRIKA WA DAWA
Matumizi ya dawa za kulevya hivi sasa yameteka kundi kubwa la vijana, wakiwamo wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu.

Kutokana na matumizi ya dawa hizo, baadhi ya watumiaji ambao awali walikuwa na ukwasi wa mali, sasa wamejikuta wakiangukia katika umasikini wa kutupwa.

MTANZANIA ilifanya mazungumzo na baadhi ya watumiaji wa dawa hizo katika vituo vya ushauri nasaha kwa waathirika wa dawa hizo (Sober House).

Akizungumza namna alivyoanza kutumia dawa za kulevya, mmoja wa waathirika ambaye yupo katika Kituo cha Padref of Wisdom kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam, Fatma Hussein, alisema alikuwa mmoja wa wauzaji wa dawa hizo akishirikiana na kigogo mmoja anayeishi Oysterbay, Dar es Salaam.

“Mimi nilikuwa naletewa mzigo na pusha (mfanyabiashara), nami nauchukua naugawa kwa vijana wangu kama watatu hivi, ambao walikuwa wakiusambaza maeneo mbalimbali kama Tandale, Manzese, Magomeni na hata Tandika.

“Nimeendelea na biashara hiyo kwa muda wa miaka kama mitano na kufanikiwa na kuwa na maisha mazuri na niliweza kununua nyumba.

“Siku moja alikuja pusha akaniambia hivi unauzaje biashara bila kujua ubora wake, basi akaniambia nionje kidogo kwa kunusa.

“Sitoisahau siku ile, maana nilitapika sana. Lakini baadaye nikapitiwa na usingizi na kuona raha sana, basi nilikuwa nakunywa bia, lakini nikaona haina starehe nzuri kama unga, ndipo nikajikuta nauza nyumba na magari yangu, hata fedha sijui nilivyotumia,” alisema Fatma.

APONZWA NA SIGARA
Kwa upande wake Witness Paschal, alisema alianza kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya kupitia rafiki yake aliyekuwa mkoani Geita.

“Nilitoka hapa Dar es Salaam na kwenda kwa rafiki yangu Geita kutafuta kazi, nilifanikiwa nilipata, lakini siku moja ‘boy friend’ wa rafiki yangu alikuja pale nyumbani na kuniambia nijaribu kuvuta sigara.

“Baada ya kuvuta nilipata usingizi mzito, basi kila siku nikawa natamani sana kuivuta, ikaendelea hivyo, ufanyaji kazi wangu ukazorota na kujikuta nikiacha kazi kabisa.

“Kwa kuwa yule bwana wa rafiki yangu alikuwa Mhindi, kwa hiyo upataji wa unga kwake haukuwa tatizo, mwisho nikaanza kuiba na hata kuonekana kama mtu aliyechanganyiwa mbele ya jamii,” alisema Witness ambaye ni mmoja wa waathirika wa dawa za kulevya.

MWANAJESHI ATUMBUKIA
Ally Zongo ambaye alikuwa mwanajeshi, alitumia dawa za kulevya kwa miaka 10, lakini sasa ameacha na amekuwa akiwasaidia wenzake walioathirika katika kituo cha Padref of Wisdom.

‘TEJA’ WA ZAMANI ALIYEOKOA ‘MATEJA’ 300
Akizungumza katika kipindi cha Kidani kinachorushwa na Azam Tv, Mkurugenzi wa Kituo cha Padref of Wisdom, Nuru Salehe, alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa dawa za kulevya ambaye alijikuta akiingia katika matumizi hayo kwa miaka 12 baada ya kuolewa na mume wake ambaye alikuwa akizitumia.

Alisema pamoja na wao kuanzisha vituo hivyo, lakini bado anapata shida na namna dawa za kulevya zinavyoingia licha ya vyombo vya dola kulinda mipaka ya nchi.

“Mimi niliathirika na dawa za kulevya na nilipelekwa hadi kwa waganga na wazazi wangu, wakihisi labda nimerogwa, lakini nilikwenda kuacha dawa Zanzibar Sober House na wakati wote nilikuwa na ndoto ya mimi siku moja kuwa na kituo kama hiki, na sasa zaidi ya watu 300 wameacha kupitia hapa.

“Nilianza na wanaume na sasa wapo hadi wanawake ambao tumekuwa tukitoa huduma ya uraghibishi kwao ili waweze kuachana na matumizi ya dawa za kulevya,” alisema Nuru.

Mkurugenzi huyo alisema pamoja na hali hiyo, ni lazima Serikali ije na majibu madhubuti kuhusu kuingia kwa dawa za kulevya nchini, licha ya kuimarishwa ulinzi hadi viwanja vya ndege na maeneo ya bandari.

Alisema licha ya watu wanaohusika na biashara hiyo kukamatwa kwenye baadhi ya maeneo, lakini kasi hiyo inatakiwa kuongezwa kwa kwenda sambamba na utoaji elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuhusu dawa za kulevya.

NANDO ASIMULIA
Kwa upande wake, aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando, akizungumza katika moja ya kipindi kilichorushwa na Clouds Tv, mwishoni mwa mwaka jana, alisema kuwa yeye ni mvutaji wa bangi na sigara ingawa pia anatumia unga.

Alisema akiwa katika nchi za Marekani na Afrika Kusini alitumia sana unga.

“Mimi si mpenzi wa unga kivile, mimi nimesafiri sana na kuona madaraja ya unga A, B… mfano class A unapatikana Los Angeles na class B unapatikana Colombia, kwa hiyo zote ukishazi-test (ukijaribu), ukija huku Afrika unaziita mchanga tu na si unga.

“Nawashauri wasivute unga, mapafu yataishia ‘kunyeka’ au kuwa mateja. Uteja unatokana na kuvuta lakini si ‘kusnifu’ na ukisnifu huwezi kuwa teja. Kwangu mimi nilikuwa situmii sana, mimi ni mwanamichezo, sina muda wa kutoa 3,000/- yangu nikapate kete moja.

“Kinachochangia ni kuwa ‘bored’ sana, mtu kama Chid Benz alitakiwa kutafuta kitu kama michezo, maana ukiruhusu tu hiyo, akili yako itakuwa ndiyo vile tu,” alisema Nando.

VIJANA 400,000 WAATHIRIKA
Inaelezwa kwamba vijana wanaotumia dawa za kulevya kwa sasa wanafikia 200,000 hadi 400,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Arusha na Tanga.

Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu, kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee vijana zaidi ya 30,000 wameathirika.

Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa asilimia 30 wanaotumia dawa hizo kwa kujidunga sindano, wako hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Pamoja na hali hiyo, 20,000 waliotharika na dawa za kulevya wamekuwa wakipatiwa matibabu nchini.

TAARIFA YA WAZIRI
Akitoa taarifa ya athari za dawa za kulevya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood, alisema kuwa watu milioni 200 duniani wameathirika na utumiaji wa dawa za kulevya.

Alisema kwa Zanzibar watu 10,000 wameathirika na utumiaji wa dawa huku 3,200 wakitumia kwa njia ya kujidunga sindano.

UTAFITI WA UN
Utafiti za hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa (UN) unaonyesha kwamba kuna ongezeko kubwa na la kutisha katika matumizi ya dawa za kulevya aina ya heroin na kwa njia ya kujidunga katika nchi za Kenya, Libya, Mauritius, Shelisheli na Tanzania.

Ripoti mpya ya hivi karibuni ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu (UNODC), imetamka bayana kwamba Tanzania ni kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za Afrika Mashariki na Tanga ukitajwa kama mkoa hatari zaidi.

Jumla ya tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroin zilisafirishwa bila kukamatwa kwenda au kupitia Afrika Mashariki, ikiwamo Tanzania kati ya mwaka 2010 na 2013.

WALIOFUNGWA CHINA, BRAZIL
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006 hadi Juni 2015, Watanzania 178 ambao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya wamekamatwa nchini China.

Kutokana na sheria za China, wakitiwa hatiani na mahakama watakuwa hatarini kupoteza maisha.

Sheria za China mtu anayekutwa na hatia ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya hunyongwa.

Na kwa upande wa nchi ya Brazil, waliofungwa ni 113.

Kwa upandewa Hong Kong kuna zaidi ya Watanzania 200 wenye kesi za dawa za kulevya. Kesi 130 zimeshatolewa hukumu na 70 zinaendelea.

Marekani kuanza kudai viza raia wa Cuba

$
0
0
Rais wa Cuba wakielekea Marekani

Marekani imesitisha sera ya muda mrefu ambayo ilikuwa inawapa raia wa Cuba hadhi maalumu ya kuingia na kuishi nchini Marekani bila ya visa.

Serikali ya Cuba imekuwa ikilalamika kwamba, sera hiyo, ijulikanayo kama "wet foot, dry foot," imewafanya maelfu ya raia wa Cuba kukimbia nchini humo kila mwaka.

Rais Obama amesema hatua ya kuondolewa kwa sera hiyo, ni hatua muhimu katika kurudisha uhusiano na Cuba.

Mahasimu hao wa muda mrefu wamerudisha uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 2015 baada ya karne ya uhasama.

Akothee afunguka tetesi za kumlipa Diamond milioni 36 kwaajili ya kolabo

$
0
0
Muimbaji wa Kenya, Akothee amefunguka tetesi zilizosambaa kuwa alimlipa Diamond Platnumz kiasi cha shilingi milioni mbili za Kenya ili ashiriki katika wimbo wake wa ‘Sweet Love’. Kiasi hicho ni takriban shilingi milioni 36 za Tanzania.

Akiongea katika kipindi cha runinga cha Talk Central cha K24, Akothee amekataa kuweka wazi lakini amedai kuwa fedha hiyo ni kitu kidogo kwa kuwa na kama wimbo huo usingekuwa mzuri wangeomba warudishiwe fedha yao.

“What is two million shillings? No! am not saying no but am not saying yes, am saying why 2 million. Is the song good, we don’t have to talk about price if the song is not good then if we have paid we will ask our money back,” amesema Akothee.

“And now the song is doing well let’s just talk about the song,’ ameongeza.

Mpaka sasa wimbo huo umefanikiwa kutazamwa mara 3,383,577 kwenye mtandao wa YouTube na umekuwa wimbo wa kwanza wa muimbaji huyo kutazamwa zaidi katika mtandao huo.

"Ngoma ya Darassa haina ujumbe"

$
0
0
 Darassa

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Prince Dully Sykes amesema wabongo wengi hawapendi nyimbo zenye ujumbe wa kuhamasisha maendeleo, na ndiyo maana ngoma nyingi zisizokuwa na ujumbe wa aina hiyo ikiwemo ya 'Muziki' ya Darassa, huwa zina hit zaidi.

Dully alizungumza hayo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, alipokuwa akizungumzia mikakati yake kwa mwaka 2017 na kutakiwa kuelezea maana ya ngoma yake ya 'Inde' ambayo ilikuwa 'hit' mwaka 2016.

Alisema wimbo wa Darassa hauna ujumbe wowote wa kuhamasisha maendeleo isipokuwa umejaa majigambo na kujisifia, na kwamba nyimbo za aina hiyo ndizo hupendwa na watanzania huku akisema kuwa endapo Darassa angeimba maendeleo, wimbo wake usingependwa.

"Kwani wimbo wa darassa una ujumbe gani? siyo simba, siyo chui, hiyo si ni kujisifia tu, wabongo ukiwaimbia eti sijui twende tukalime, tufanye kazi maendeleo na vitu kama hivyo hawavipendi" Alisema Dully.

Alisema kwa kutambua hivyo, ndiyo maana na yeye hawezi kutunga nyimbo zenye ujumbe wa maendeleo na ataendelea na ngoma kama ilivyo 'inde' na nyingine ambazo zimetikisa anga la bongo fleva

Dully
Hata hivyo, Dully alimpongeza Darassa kwa kazi nzuri na kwa kulishika game la bongo kwa kipindi hiki, na kukiri kuwa kazi yake ni nzuri huku akikataa kuwa ngoma ya Darassa haijamfunika kwa kuwa ngoma yake ya 'inde' ilikuwa hit kabla ya 'Muziki' ya Darassa.

Kuhusu ujumbe uliomo kwenye ngoma ya 'inde' Dully alisema ngoma hiyo aliitengeneza kwa ajili ya kucheza kuburudisha zaidi maana hicho ndicho watanzania wanachokipenda, huku akikanusha kuimba matusi na kusema "Sijaimba matusi, ni jinsi wewe utakavyoutafsiri na kuuelewa, tuliza akili yako utajua nimeimba nini, vitu vingine havisemwi hadharani"

Kuhusu mikakati yake ya mwaka 2017, Dully amesema muda si mrefu atatoa ngoma nyingine ambayo anaamini itakuwa ni kali zaidi ya 'inde' na kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Omog: Ndiyo kwanza kazi imeanza

$
0
0
KOCHA wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog ametamka kuwa wanaanza kutimiza ndoto zao na kuondoa nuksi ndani ya klabu hiyo ya kushindwa kupata mataji kwa kuanza na kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, leo Ijumaa watakapocheza dhidi ya Azam FC.

Omog anatarajiwa kuiongoza Simba katika fainali hiyo baada ya Jumanne ya wiki hii kuiondoa Yanga kwa penalti. Azam ambayo inanolewa na Idd Nassor Cheche kwa muda, yenyewe iliingia fainali hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa kuifunga Taifa Jang’ombe katika nusu fainali. “Ile hali ya kukosa mataji kwa Simba itafika mwisho Ijumaa hii, tumejipanga vizuri kuchukua ubingwa, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini kwa hali ilivyo inabidi

watusamehe kwani lengo letu ni moja tu la kutwaa ubingwa,” alisema Omog. Aidha, Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja naye alisema: “Tunajua Azam ina morali ya ushindi kwa kuwa waliwafunga Yanga mabao manne lakini sisi tuko vizuri na tayari kwa fainali.” Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Azam, Cheche alisema: “Vijana wangu wote wapo vizuri, tunataka kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyapata tulipoifunga Yanga, hilo linawezekana kabisa, lakini ushindi ni ushindi. “Simba walitufunga kwenye ligi, lakini tuwaambie wasitegemee tena kutufunga kwa sababu mchezo wa fainali unakuwa na mipango yake.”

Wafugaji wa Kimasai Kenya wadaiwa kuwajeruhi Watanzania

$
0
0
WANANCHI wa vijiji vya Kirongo Chini na Kiwanda, Wilaya ya Rombo wanaopakana na nchi jirani ya Kenya, wameingia katika mgogoro na wafugaji wa jamii ya Kimasai kutoka nchini Kenya na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa na kulazwa hospitali.

Wafugaji hao wanadaiwa kuwapiga na kuwajeruhi wakulima wa Tanzania, huku wengine wakiwakamata wananchi wa vijiji hivyo na kupelekwa kwenye vituo vya Polisi vya Wilaya ya Taveta.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Agness Hokororo, alithibitisha Wamasai hao waliingiza mifugo yao wiki iliyopita katika moja ya shamba la mkulima na baadaye kuwavamia, kuwashambulia na kuwasababishia majeraha.

“Ni kweli kuna wakulima wa kwetu walijeruhiwa na mmoja alishonwa nyuzi 14 na mwingine amelazwa hadi sasa Hospitali ya Rufani ya KCMC. Hata hivyo, tumeshakutana katika vikao vya ujirani mwema, kati ya Wilaya ya Taveta na Rombo na tukakubaliana kwamba mkulima au mfugaji atakayeingia kwa mwenzake akamatwe,” alisema.

Mashamba yanayodaiwa kuchungiwa mifugo na kusababisha mgogoro huo ni yale yaliyolimwa mahindi, alizeti, maharage, karanga, migomba na mihogo.

Kwa mujibu wa Hokororo, jana (juzi) Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Rombo (SSP), John Mtalima, alikwenda Kaunti ya Taveta nchini Kenya kufuatilia kama wafugaji hao wamekamatwa, kwa kuwa kulishafanyika utambuzi maalumu kwa wahusika ambao walitajwa kwa majina na wakazi wa Taveta.

Mmoja wa majeruhi hao, Protas Sianga, aliimbia Nipashe kuwa Wamasai hao walitokea nchini Kenya na kuingiza makundi makubwa ya mifugo kwa nguvu katika mashamba ya wakulima na kisha kulishia mazao yao.

“Walipokuja na hiyo mifugo tulijaribu kuwaondoa, lakini Wamasai hao wakaanza kutupiga kwa kutumia rungu na sime wakilazimisha kuchungia katika mashamba yetu, na kibaya zaidi wanawalazimisha wakulima kufyeka uzio wa katika mashamba yao ili waingize mifugo yao,” alisema Agatha Akwilini, mmoja wa majeruhi.

Mkazi wa kijiji cha Kiwanda Wilaya ya Rombo, Gervas Tarimo, alisema kama Serikali za Tanzania na Kenya hazitachukua hatua za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo, kuna uwezekano wa kulipuka kwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji wa Kimasai toka Kenya.

China yaisifu Tanzania kwa sera ya uwazi

$
0
0
SERIKALI ya China imeisifu Tanzania kwa kuzingatia sera ya uwazi katika ushindanishaji wa zabuni za miradi ya ujenzi, ikilinganishwa na nchi nyingine zilizopo katika ukanda wa  Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa hivi karibuni mjini hapa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya nchini China, Hu Bo wakati  akizungumza na waandishi wa habari  wa Kituo cha Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo (CCTV) waliofika nchini kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali yao nchini Tanzania.

Mwenyekiti huyo alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zinazoongoza kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za zabuni za ujenzi, ambapo Serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa kipaumbele kwa makampuni ya ukandarasi ya wazawa kwakukubali maombi yao ya zabuni za ujenzi.

“CRJE inafanya shughuli zake katika mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, katika sehemu zote hizoTanzania imekuwa  nchi bora zaidi kwani pamoja na mazingira bora ya kazi zetu lakini pia wakandarasi wazawa wamekuwa wakipewa nafasi katika miradi ya ujenzi,” alisema Hu Bo.

Kwa mujibu wa Hu Bo tangu mwaka 1977 kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi nchini Tanzania, hatua inatokana na ushirikiano na uhusiano wa kirafiki uliopo baina ya Serikali ya China na Tanzania.

Alitaja baadhi ya  miradi ya Serikali iliyokamilishwa  kampuni hiyo nchini ni pamoja na ujenzi wa ukumbi wa Bunge Dodoma, Jengo  la Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Jengo la Ofisi ya Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar, Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Young Killer Afunguka Kuhusu Mstari wake Huu "Atakae Nijibu ni Demu Wangu na Mkiniacha Mnaniogopa"

$
0
0

Baada ya Young Killer kuachia ngoma yake mpya Sinaga
swaga ambayo ina mistari yenye utata mwingi. leo kwenye
XXL ya clouds fm aliombwa kutolea ufafanuzi moja ya
mstari uliopo kwenye wimbo huo

Sasa baada ya kuwachana/diss baadhi ya wasanii wenzake
Rapper huyo aliamua kumaliza na mstari unaosema "atakae
nijibu ni demu wangu na mkiniacha mnaniogopa" ambao ndio
ameutolea majibu haya

"Sihitaji mjadala uje kuendelea nataka uishie hapa, yani
nimeufunga kisaikolojia" alisema @youngkillermsodokii

Rapper huyo pia ameeleza neno #sinagaswaga kwake
inamaana gani na kudai kwamba mtu ambae hana
swaga ni mtu ambae hana mambo mengi hana mbwembwe,
ni mtu ambae yupo straight

G-Nako na Nick wa Pili ‘Wamchenjia’ Young Killer Baada ya Kudai Joh Makini Anabebwa

$
0
0

Ngoma mpya ya Young Killer, Sinaga Swagga ina utata mwingi. Mmoja wa mstari ambao tayari umeanza kumtokea puani rapper huyo ni ule usemao, wanasema Joh anabebwa mpaka nahisi ni ukweli

Joh Makini hana jibu lenye hasira kama wengi wanavyotarajia kwasababu kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, rapper huyo alisema,” Hiyo kamba, hiyo mbeleko hiyo toka 2005 mpaka mpaka 2015 basi hiyo kamba ngumu.”

Jibu lilikuwa tofauti kwa G-Nako aliyesema, “Sometimes watu kama hawa wanakuwa wanaongea tu kwasababu wanataka wasikike kwamba kuna vitu wanaviongea kwenye mistari, inabidi wakifika kwenye interview kama hapa muwe mnawachallenge, kwamba wewe umeongea hivi kwenye mistari yako, umeshafuatilia hiki na hiki? Maake sio mistari tu.”

Kwa upande wake Nick wa Pili alisema, “tatizo ninaloliona katika mstari kama huo ni kwamba unaharibu history sababu Joh amefanya kazi kubwa sana so tunategemea artist wadogo si lazima kumjua Joh Makini ila kuijua historia ya Joh Makini sababu pale ndo kuna mafunzo mengi ya kujifunza.”

Ameongeza, “Kwahiyo anavyokuja mtu akitoa neno kama hilo anaharibu ile historia sio kwa Joh, kwa mtu ambaye anakuja mdogo. Mtu ambaye anatakiwa kumjua Dullah hatakiwi kumjua leo, unatakiwa kujua Dullah alianzaje kufika hapa kwasababu kila mtu anaanza moja, unaweza ukarelate na hiyo story kikawaida.”

Joh alirejea tena kuelezea kwanini mambo kama hayo huwa hajibu akisema, “Katika historia ya interview yangu na jinsi ambavyo nafanya kazi, huwa sitoi nafasi kwenye vitu vya kipuuzi, navipaga tu mgongo naendelea na mambo yangu ya msingi sababu end of the day hata nitakachosema, hakitaleta maana sababu kama hawajui history.”

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Akamatwa Kwa Rushwa ya Ngono Dar es Salaam

$
0
0
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT) amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Konondoni baada ya kunaswa katika mtego wa rushwa ya ngono.

Mhadhiri huyo anayefahamika kwa jina la Samson Jovin Mahimbo (66) mkazi wa Makongo Juu, Dar es Salaam alikamatwa jana Januari 12, 2017 katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Camp David iliyopo eneo la Mlalakua, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Samson Mahimbo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa iliyotolewa na mwanafunzi huyo aliyeombwa rushwa ili aweze kumpatia alama (marks) nzuri  katika mtihani wake wa marudio (supplementary examination) alioufanya tarehe 5 Januari 2017.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017.

Instagram Inayotumika Kumtusi Diamond Yaendelea Kutoa Matusi Wakati Mtuhumiwa Mwenye Akaunti Yupo Selo

$
0
0
November 18, 2016 kijana mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja alikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kutumia akaunti ya ‘Shilolekiuno_official’ kuwatukana watu mbalimbali akiwemo Diamond pamoja na familia yake.

Lakini cha kushangaza akaunti hiyo bado inaendelea kutukana watu wakati mtuhumiwa yupo ndani.

Sallam ambaye ni meneja wa Diamond ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwa kijana huyo mwezi Disemba mwaka jana.

“Kwa watu wote kama ulitukanwa na huyu ambae anaejiita @shilolekiuno_official kwa sasa yupo chini ya mikono ya sheria, Kama una mashitaka yoyote fika Oyster Bay Polisi, Vizuri ametaja watu wanaemtuma afanye hivyo! Na kuwasaidia wale ambao wanajiamini kuwa hawawezi kujulikana basi kwa taarifa yenu Serikali ina mkono mrefu sana! Eti Jana alikuwa anamuita Diamond “Simba” 😂😂😂.” aliandika Sallam Insta baada ya kukamatwa kwa jina hiyo.

Hata hivyo kamanda wa polisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hakuna kijana kama hiyo aliyekamatwa.

“Hatujamkamata na hatuna mtu kama huyo kituoni kwetu. Tuna vijana wengi ambao wamekamatwa wanamakosa kama hayo, jina kama hilo uliloniuliza halipo hapa kituoni kwetu labda kwenye kituo kingine.”

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Kutoka Bagamoyo, Shafisha Nyota na Kurudisha Mausiano yako ya Kimapenzi Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Kutoka Bagamoyo, Shafisha Nyota na Kurudisha Mausiano yako ya Kimapenzi

$
0
0
MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI, (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 48 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI: 

SHEKH SHARIFU RASHIDI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran, dawa za asili, dawa za kiarabu na majini, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango, ngiri maji na n.k, anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, pia anatoa pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali kulingana na nyota yako, anaouwezo mkubwa wa kutumia jina la muhusika kwa kutatua tatizo lako, anaouwezo wa kumrudisha mtu aliepotea kimiujiza, pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo

WASILIANA NAE KWA SIMU NA WHATSAPP NO: 0718-668347 na 0685-224047

au follow@shekh_sharifu_rashid, Email:shekhsharifurashid@gmail.com

Mganga Auawa Kwa Kuchomwa Visu..Kisa ni Kuwatapeli Watu Kwamba Atawapa Utajiri

$
0
0
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTTO MWAIPOPO mkazi wa Kafundo – Ipinda wilayani Kyela Mbeya ameuawa kwa kuchomwa kisu ubavu wa kulia na BONIPHACE KISWAGA Mfanyabiashara na Mkazi Chaugingi Mkoani Njombe kwa madai ya kufanya utapeli.

Taarifa ya Polisi Mkoa wa Mbeya imesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11.01.2017 majira ya saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ipinda – Chini, Kijiji na Kata ya Ipinda, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuwatapeli watuhumiwa pesa ambazo kiasi halisi bado hakijafahamika kwa madai kuwa yeye ni mganga wa kienyeji na atawasaidia kuwa matajiri.

Aidha katika tukio hilo mtuhumiwa huyo BONIPHACE KISWAGA alijeruhiwa kwa kupigwa na wananchi na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa matibabu. Watuhumiwa wengine wawili ambao walikuwa pamoja na mtuhumiwa aliyekamatwa walikimbia na msako mkali unaendelea.

Rais Magufuli: Serikali Yangu Haitayafumbia Macho Magazeti Mawili Yanayoandika Habari za Uchochezi

$
0
0
Rais John Magufuli amesema vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli na kuleta uchochezi siku zake zinahesabiwa kwani Serikali yake anayoiongoza haiwezi kukubali kuvurugwa kwa amani ya nchi.

Amesema mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 chanzo chake ni vyombo vya habari, hivyo hawezi kukubali hali hiyo itokee nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Jambo Food Plant mjini Shinyanga na matangazo yake kurushwa mubashara na Star Tv, Rais Magufuli amesema magazeti yote isipokuwa mawili, vituo vyote vya televisheni na redio nchini vinafanya kazi nzuri ya kuelimisha wananchi.

Rais Magufuli amesema Serikali yake haikatai kukosolewa na kwamba, magazeti mengine yanakosoa na kusaidia kutatua matatizo ya jamii, lakini hayo mawili (bila kuyataja) yamekuwa ni kupindisha kila kitu.

“Hayo magazeti kila ukisema hivi yanapindisha, siyataji kwa sababu yanajifahamu lakini yajue kwamba siku zake zinahesabika. Serikali ninayoiongoza haiwezi kukubali amani kuvurugwa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

Natamani Mpenzi Wangu Achepuke Aweze Kujua Ladha ya Wengine..Mimi sio Mwanaume Sahihi Kwake

$
0
0
Niko kwenye mahusiano na binti mmoja kati ya wengi nilionao.

Kiukweli natamani huyu binti achepuke kwa mwanaume mwingine, huyu binti niko nae kwenye mahusiano zaidi ya mwaka mmoja sasa. Natamani achepuke labda huko atapata mwanaume atakaemfaa katika maisha yake.

Huyu binti ni mwema sana kwangu kiasi kwamba wema wake unageuka kua kero kwangu, mimi ndie mwanaume wake wa kwanza, nina uhakika hajawahi kutoka na mwanamume mwingine kabla yangu na baada yangu.

Nikiri kua nilitumia muda mwingi na gharama nyingi kumshawishi huyu binti kua mimi ndie mwanaume sahihi aliekua amemtunzia mwili wake hadi akakubali kuniruhusu kuchana nyavu.

Natamani achepuke maana huko aanaweza kupata mwanaume mwingine mwema kwake,kwa kweli hutu binti hastahili kua na mimi, ni mwema kiasi kwamba hadi namuonea huruma, anaomba radhi kwa makosa ambayo hakufanya au nimefanya mimi.

Nashindwa huyu binti namuachaje ili aende huko apate mtu anaestahili, namuonea huruma kwamba ameangukia sehemu isiyo salama, nina uhakika kuna watu wengine huko wanaostahili penzi na wema wa huyu binti mimi sistahili.

Polisi Dar Wapiga Marufuku Uuzwaji Holela wa Silaha za Jadi

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam, limepiga marufuku uuzwaji holela wa silaha za jadi kama vile, manati, pinde na mikuki huku likisema tayari limemkamata mtuhumiwa mmoja katika maeneo ya mataa ya Tazara, Mgoli Sakalani(39) akifanya biashara hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema kuwa tabia hiyo imejengeka kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wamekuwa wakiuza silaha mbalimbali zikiwemo mapanga, manati,visu na upinde pembezoni mwa barabara.

Kamanda Siroamewataka wafanyabiashara hao kuacha mara moja biashara hiyo ambayo imeshamiri sana katika Barabara ya Nyerere kwenye Mataa ya Tazara,Mataa ya Chang’ombe na Mataa ya Gerezani.

Alifafanua kuwa miongoni mwa wauzaji wa bidha hizo wengi wao siyo waaminifu kwani hutumia fursa hiyo kuwatishia watu wakiwa kwenye magari binafsi,magari ya umma na kisha kuwaibia mali mbalimbali kama vile simu za mkononi,saa,mikoba na laptop.

Kamanda huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara hao kuifanya biashara hiyo sehemu maalumu kama madukani wakiwa na leseni ya biashara,vinginevyo atakayepatikana akifanya biashara hiyo kiholela atachukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amesema kesho Jumamosi ni siku ya Polisi ijulikanayo kama ‘Polisi Day’ ambapo wataadhimisha siku ya familia katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

Amesema baada ya hafla hiyo fupi, waziri huyo akiambatana na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, wataelekea katika mikoa ya Kipolisi ya Kindondoni,Temeke na Ilala ambapo watatembelea Hospitaliza Mwananyamala, Amana na Temeke kushiriki kufanya usafi wa mazingira maeneo hayo.

Maandhimisho hayo ya siku ya familia pia yataambatana na burudani ya ngoma za asili,kuvuta kamba, kukimbiza kuku na muziki kutoka bendi ya polisi.

Joti Arudia Video ya Darasa...Wadau Wadai Ameitendea Haki Kuliko Darasa, Itazame Hapa

$
0
0
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Joti amerudia wimbo wa mwanamuziki Darassa unaokwenda kwa jina la Muziki.

Huu ni wimbo uliofanya vizuri tangu ulipotoka mwezi Disemba mwaka jana hadi sasa. Wimbo huu ni wa Darassa ambapo amemshirikisha Ben Pol ikiwa ni wimbo wao wa pili kuimba pamoja baada ya ule wa Sikati Tamaa.

Burudika na video hapa chini:

Enyi Wadada wa Mjini Maisha yamebadilika Mwenye Masikio na Asikie

$
0
0
Maisha yamebadilika, nyakati zimebadilika ela za mchezo hazipo tena kila senti inakazi ya kufanya. Enyi wadada mliozoea mizinga jifungeni Mikanda mwafwaaa. Ile ya baby naomba unitumie elfu 30 kwenye MPESA hizo
zama zimepita, hyo ela ukiihitaji itabidi uje uifanyie kazi haswa, itabidi ufue, Utandike kitanda, upike na game uperform Vizuri. Maisha ya ujanja ujanja yamepita nasema na mwenye masikio asikie
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images