Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live

Prof Muhongo afunguka juu ya tuhuma za kuhusika na kushiriki kikao cha kupandisha bei yaUmeme..!!

$
0
0

WIZARA ya Nishati na Madini imekanusha taarifa kwamba Waziri wake Profesa Sospeter Muhongo katika kikao chake na Benki ya Dunia (WB) kilichofanyika Septemba 28 mwaka jana kilijadilii mchakato wa kupandisha bei ya umeme nchini.


Imeeleza katika taarifa yake kwamba katika kikao hicho walijadili masuala ya upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi , kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) na kupunguza deni la TANESCO.

Aidha katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Wizara hiyo ilieleza kuwa taarifa iliyotolewa na gazeti moja la kila siku  kwa siku mbili mfululizo kuwa Waziri Muhongo alishiriki katika kikao na ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika siku hiyo kilichojadili kupandishwa kwa bei ya umeme, si ya kweli.

Wizara ilieleza kuwa wamekuwa wakifanya vikao na wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi za Umma, Binafsi na Washirika wa Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Kifedha ya Kimataifa kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji katika Sekta za Nishati na Madini nchini.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba siku hiyo ya Septemba 28 mwaka jana kulifanyika kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya majadiliano kuhusu upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kuboresha uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO).

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kikao hicho pia kilihudhuriwa na taasisi nyingine zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Katika kikao hicho walijadili masuala ya upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma za jamii, kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) na Kupunguza deni la TANESCO.

Taarifa hiyo ya wizara ilieleza kuwa katika kulipunguza deni la TANESCO ambalo linakaribia Sh bilioni 800 (takriban Dola za Marekani milioni 363) na kuboresha shughuli za utendaji za TANESCO, Benki ya Dunia ilijadiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara hiyo ili kupata mkopo wa Dola za Marekani milioni 200.

“Hivyo, katika kikao hicho, hakukuwa na makubaliano ya kupandisha bei ya Umeme kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo,Vile vile, tunaomba kuutaarifu Umma kwamba Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya Serikali inafanya majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Umoja wa Ulaya (EU), JICA (Japan), na Mashirika mengine ya fedha kwa lengo la kutafuta fedha za kuboresha Sekta ya Nishati,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Shule zapigwa ‘stop’ kuwaondoa wanaoshindwa kufikia wasani wa ufaulu..!!

$
0
0

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezitaka shule zote zilizowataka wazazi/walezi kuwahamisha watoto wao kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu, kufuta agizo hilo na kuendelea na wanafunzi hao bila masharti yoyote.


Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicolas Buretta imeeleza kuwa wazazi wenye wanafunzi waliorudishwa nyumbani kwa sababu hiyo wahakikishe wanawarudisha kwenye shule walizokuwa wakisoma ili waendelee na masomo yao kama kawaida.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubainika kuwa bado kuna shule nyingi za msingi na sekondari hususani zisizo za Serikali na zaidi za kidini zinazoendelea kukaririsha, kuhamishia shule nyingine au kuwafukuza wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Badala ya shule hizo kuchukua hatua hiyo, wizara hiyo imesema, “...Ziwe na utaratibu wa kuinua viwango vya taaluma kwa wanafunzi wenye ufaulu mdogo na hivyo siyo ruhusa kukaririsha darasa wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu uliowekwa na shule. Ikitokea, ni lazima kufanya hivyo, taratibu zilizopo zifuatwe.”

Taarifa hiyo imeelekeza wadhibiti ubora wa shule, kanda na wilaya, maofisa elimu wa mikoa na wilaya kusimamia utekelezaji wa agizo hilo katika maeneo yao.

“Shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria zilizopo.”

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa


12 kuchunguza chanzo cha moto Uwanja wa JNIA,Waziri Mbarawa akikataa majibu ya 'BAHATI MBAYA'..!!!

$
0
0

SIKU moja baada ya kutokea kwa moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeunda timu ya watu 12 kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha moto huo.


Moto ulizuka juzi majira ya saa tano usiku katika chumba cha kuhifadhi mizigo kwenye jengo namba mbili (terminal II) na kuteketeza mizigo yote iliyokuwamo katika chumba hicho kidogo.

Tume hiyo imeundwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ambaye alifika katika uwanja huo majira ya saa sita mchana akitokea mkoani Mwanza na kwenda moja kwa moja katika chumba hicho kilichoteketea ili kuona uharibifu uliojitokeza.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo, Mbarawa alisema, baada ya kutokea kwa moto huo hatua za haraka za kuuzima zilichukuliwa na kwamba wakati moto huo unatokea hakukuwa na mtu yeyote katika eneo hilo ambaye amedhurika.

Alisema baada ya kuzimwa kwa moto huo hatua ya pili ili kuwa ni kurejesha huduma ambapo walihamisha huduma kutoka katika jengo hilo kwenda katika jengo namba moja (terminal I) kwa kuwa kulikuwa na ndege ambazo zilikuwa uwanjani hapo.

“Tuliendelea kupeleka huduma zetu katika jengo la abiria namba moja na huduma ikaendelea kama kawaida, kwanza tulizima moto lakini pia tukawa tunaendelea na huduma kule. Huduma ziliendelea kule na wakati huo huo tukaja huku kutayarisha mifumo mingine kuhakikisha jengo hili liweze kutoa huduma muda mfupi baadaye,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema jambo la tatu ni kutafuta chanzo cha moto kwa kuwa moto hauwezi kutokea bila kuwa na sababu ya kitaalamu, hivyo timu hiyo itafanya kazi ya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha moto huo.

Alifafanua kuwa timu hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja na itaoa majibu ya uhakika ya chanzo cha moto hiyo ambayo itasaidia kuweka mikakati ambayo itazuia matatizo ya moto katika viwanja vya ndege vyote nchini. “...ni timu ambayo ina watu wenye uwezo na ujuzi, ninaamini watatupa majibu ya uhakika, hawataupa majibu ya bahati mbaya ilitokea, kwenye utaalamu hakuna kitu bahati mbaya kuna sababu ya msingi, nategemea kupata ripoti ya kitaalamu inayosema chanzo ni nini,” alisema.

Alisema baada ya kupata ripoti hiyo wataweka mikakati ya kuzuia majanga ya moto katika viwanja vyote vya ndege nchini ili tukio hilo lisijirudie tena. Alisema kuwa kwa sasa hawawezi kumnyooshea mtu kidole, kwa kuwa kuna sababu ya kitaalamu.

Tume hiyo inaongozwa na Joseph Nyahende kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imepewa kazi ya kutoa taarifa ya sababu za moto huo.

Hadi sasa thamani ya mizigo hiyo bado haijafahamika.

Moto huo ulizuka katika chumba kidogo kinachotumika kuhifadhia mizigo ya abiria wanaotoka nje ambayo huhifadhiwa hapo kutokana na mmiliki wake au mzigo huo kuchelewa kufika, inayohudumiwa na kampuni ya Swissport ambao ni wasimamizi wa mizigo yote inayopitia katika uwanja huo wa ndege.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa

Kwa mambo haya, Belle 9 hawezi kumsahau kamwe Triss,haya ndiyo aliyofunguka 'live'..!!!

$
0
0

Msanii wa muziki wa bongo fleva Belle 9 kupitia kipindi cha Kikaangoni kilichofanyika siku ya Jumatano  amefunguka na kusema hawezi kumsahau producer Triss ambaye ndiye aliyemtengenezea ngoma yake Sumu ya Penz. 


Belle 9 amesema licha ya maisha ya muziki Triss amemsaidia mambo mengi sana ikiwemo kumfundisha namna nzuri ya kutamka maneno hata kumkumbusha katika mambo mbalimbali pindi anapochepuka kwenye mstari.

"Huwa napenda watu wajue namna gani producer Triss amekuwa msaada kwangu kwenye muziki hata nje ya maisha ya muziki, Triss ndiye mtu aliyekuwa akinifundisha namna nzuri ya kutamka maneno licha ya kuwa nilikuwa naona kwa watu wengine lakini msisitizo mkubwa nilikuwa napata kwake, Triss hata pale alipoona imani yangu kidini inapungua alinisisitiza kwenda kanisani sana. Hivyo amenisaidia mambo mengi sana hata nje ya muziki na hiki kitu napenda watanzania wajue" alisema Belle 9.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa


Ushindi wa Azam Fc jana waikosesha Simba mamilioni ya Mo Dewji...!!!!

$
0
0

Shuti la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika mjni Zanzibar.


Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.

Wakinolewa na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa Stars, Himid.

Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.

Katika mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.

Mfungaji bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne, wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.

Hata Hivyo kwa kipigo hicho ni dhahiri shari Simba watakuwa si wanakosa mamilioni ya ubingwa huo,bali pia wanakosa mamilioni yaliyokuwa yanatolewa na wafadhili wao mbalimbali ,ambao walikuwa wanatoa mamilioni hayo kama kuwapa motisha wachezaji wa Simba.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa


Povu la mwigizaji Gabo Zigamba baada ya mtandao wa Kenya kumuandika kama Mkenya..!!!

$
0
0

Muigizaji anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu, Gabo Zigamba ameujia juu mtandao mmoja wa Kenya ambao umedai kuwa yeye ni raia wa Kenya.


Mtandao huo uliandika stori yenye kichwa cha habari “Gabo Kenyan-talented movie actor” . 

Hata hivyo Ijumaa hii mtandao huyo uliamua kurekesha habari hiyo.
Jinsi kichwa cha habari hiyo kilivyokuwa kabla ya kubadilishwa

Muigizaji huyo baada ya kuona taarifa hiyo, kupitia instagram aliandika:
Kinachoweza kuondoa makucha haya ya majirani ni film tuu. Film is the best method of propaganda spreading. Na ili tufikie hapo ni kufanya kazi zenye ubora wa kidunia ili ziende duniani kufikisha ujumbe.. bado tuna deni kubwa la kuwavua nguo hawa wadhalimu.. hii vita ya nyenyenye za jirani viongozi wengi wana nafasi ya kuishiriki ila sioni ushirika wao. Nna hofu hata tukianza kutengeneza films za kuuambia ulimwengu juu ya machache yanayotangazwa na majirani mmh zisijeishia studio kisa ujirani mwema.. hio ni hofu yangu tuu.. kama trump anamuongelea Puttin on media vipi viongozi wa serikali yetu hawayaoni haya yote..? Mimi naamini serikali yetu inauwezo wa kuita press na media house za dunia na kuorodhesha yote yaliyodaiwa na wakenya kuwa yao na kuipa ujumbe serikali ya kenya . Mfano.. Tunajua mengi yatadaiwa kuwa ni raia tu binafsi na taasisi ndio zinajitamkia haya mambo. Yaani si kenyan government.
Lakini mimi najiuliz raia anapoongelea vitu kama Olduvai gorge ipo kenya mimi najiuliza darasani somo la historia kenya wanafundisha nini?
bado najiuliza wakenya wanafundishwa georaphia ya wapi mpaka waseme kilimanjaro iko kwao?
Mrisho mpoto miaka michache ilopita huko ughaibuni alishikishwa bendera ya kenya na wakenya,akaishusha bendera stegini. Hongera kwako mjomba. Sikupoteza nguvu zangu wakati wa kutoa mchango wangu kwako mjomba.. Ukitaka kuusimamisha moto nenda kwenye chanzo.. haya mambo ni ya history na geographia yaani namaanisha hutokana na elimu wanayopewa.. sasa swali ni kwamba kama oldivai na kilimanjaro ni viko kwao unashangaa nn wakisema Gabo ni wao au mpaka waseme Arusha nayo ni ya kwao

Vikao vya Bunge kuanza Jumatatu..!!

$
0
0

KAMATI za Kudumu za Bunge zitaanza vikao vyake Jumatatu, Januari 16 hadi 29, mwaka huu, mjini Dodoma.


Taarifa ya Bunge iliyotolewa jana mjini hapa na Kitengo cha Hahari, Elimu na Mawasiliano kwa vyombo vya habari, inaonesha kwamba, vikao hivyo vitafanyika kwa mujibu wa utekelezaji wa majukumu ya kamati hizo, kabla ya kuanza Mkutano wa Sita wa Bunge, Januari 31, mwaka huu.

Wabunge wote wanatakiwa kuwasili mjini hapa, Januari, 15, mwaka huu, tayari kwa kuanza vikao kamati hizo siku inayofuata.

Katika kipindi cha vikao hivyo, kamati 12 za wabunge zitafanya ziara, kati ya Januari 17 hadi 21, mwaka huu, kukagua miradi ya maendeleo nchini inayotekelezwa na wizara au idara zinazosimamiwa na kamati husika kabla ya kamati hizo kuendelea na vikao, Januari 23, mwaka huu.

Katika kipindi hicho, Kamati mbili za kisekta zitajadili miswada mitatu ya sheria; Kamati ya kwanza ni ya Katiba na Sheria ambayo itajadili muswada wa sheria za marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2016 na muswada wa sheria wa huduma ya msaada wa kisheria ya mwaka 2016.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa


Maskini… Snura alizwa na mwanaye ..!!!

$
0
0

MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Snura Mushi, amefunguka kuwa amekuwa akilizwa kila mara na mtoto wake wa kwanza Talha, kutokana na maneno anayomueleza kwa kitendo cha baba yake kutompa huduma yoyote.


Akizungumza  Snura alisema kila mara mtoto wake anamuambia asikate tamaa ya kuwalea na kumuombea kwa Mungu, aweze kumsaidia ili waendelee kusoma na kupata huduma japo baba zao hawawajali yeye na mdogo wake kitu kinachomliza mara kwa mara.

“Yaani nasikiaga maumivu makali sana  mtoto wangu mdogo wa miaka sita tu ananiambia maneno hayo yananiumiza kuliko kitu chochote kile huwa yananifanya nijitahidi kila kukicha ili nisimuangushe na nitaendelea kukatika ili mtoto wangu apate elimu aitakayo,” alisema Snura ambaye amezalishwa watoto wawili na baba tofauti.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa



Hatarii:Dada wa Diamond Platnumz afunguka kuwa huwa hatongozwaji bali huwa anatongoza..!!!

$
0
0

MWANAMUZIKI ambaye ni memba wa Kundi la WCB, Mwanaisha Abdul ‘Queen Darleen’ aliye  pia dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ametoa kali ya mwaka baada ya kufunguka kuwa katika mapenzi kitu ambacho hakipendi ni kutongozwa na mwanaume hivyo huwa anapenda kutongoza.


Akistorisha na Mikito Nusunusu Darleen, alisema kitendo cha yeye kumtongoza mwanaume anaamini kwamba anakuwa  amempenda kutoka ndani ya moyo wake lakini akitongozwa wakati mwingine wanaume wanakuwa ni waongo hawana nia ya dhati. 

“Katika maisha yangu yote huwa sipendi kutongozwa napenda nitongoze kwa sababu naamini nikifanya hivyo nakuwa nimempenda mwanaume kweli kwani watongozaji wengi ni waongo na ninajijua kabisa  kwamba sina bahati kwenye mapenzi,” alisema.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa

Mahakama yaiamuru kampuni ya Kenya kuilipa kampuni ya kitanzania fidia ya bilioni 6.2..!!!

$
0
0

Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara imeiamuru kampuni ya Uingereza yenye makao yake Kenya, British American Tobacco Kenya Limited (BAT), kuilipa fidia ya Sh6.2 bilioni kampuni ya Mohan’s Oysterbay Drinks Limited ya nchini.


Uamuzi huo unatokana na Mahakama kuridhika kuwa kulikuwa na makubaliano ya kibiashara kati ya Mohan’s na  BAT ambayo iliyavunja.

Mohan’s iliomba kulipwa Sh12 bilioni zikiwa ni fidia ya uwekezaji iliofanya kutokana na makubaliano hayo, hasara ya kibiashara, faida waliyoitarajia, hasara ya jumla na riba. Makubaliano hayo yalihusu usambazaji wa sigara zinazozalishwa na BAT aina ya Dunhill na Benson & Hedges.

BAT ilikana kuwa na uhusiano wa kibiashara na Mohan’s kama msambazaji wa bidhaa zake kwa madai kuwa hapakuwa na mkataba wa maandishi, bali uhusianao wao ulikuwa ni muuzaji na mnunuzi.

Jaji Latifa Mansoor katika hukumu ya kesi hiyo, amesema vielelezo vilivyowasilishwa na Mohan’s mahakamani vinabainisha kulikuwa na makubaliano ya kibiashara ya mtengenezaji na msambazaji na si muuzaji na mnunuzi.

Amesema BAT haikuwa na sababu ya msingi kuvunja makubaliano kwa kuwa haikuonyesha kuwa Mohan’s ilitenda kosa la ukiukaji wa makubaliano lililosababisha kuyasitisha baada ya kuwapo uhusiano wa kibiashara wa miaka 19.

Jaji Mansoor amesema BAT ingeweza kujadiliana na Mohan’s kuhusu masharti yenye manufaa kwa makubaliano ya usambaji bidhaa hizo, huku wakiweka kifungu cha kuyasitisha jambo ambalo lingewezesha kuendeleza biashara kwa muda mrefu.

Licha ya kukubaliana na madai ya Mohan’s kuhusu uhusiano wake na BAT, hata hivyo Jaji Mansoor hakukubaliana na kiwango cha fidia ambacho kampuni hiyo ya Mohan’s ilikuwa imekiomba cha Sh12,079,000,000.

Badala yake Jaji Mansoor ameamuru kampuni hiyo ya BAT kuilipa Mohan’s fidia ya jumla ya Sh6,234,835,855 (zaidi ya Sh6.2 bilioni), ikiwa ni fidia ya hasara ya gharama za uwekezaji, hasara ya kibiashara, hasara ya jumla,

Pia ameiamuru BAT kulipa asilimia 12 ya kiasi hicho tangu siku ya hukumu hadi itakapokamilisha malipo hayo na pia kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Jaji amesema katika hukumu hiyo kuwa kampuni hiyo imeshindwa kuthibitisha madai mengine kiasi cha Sh12 bilioni ilichokuwa ikiomba, kama vile mapato ya mauzo waliyokuwa wakiyatarajia, malipo ya fidia na malipo ya bima kwa wafanyakazi waliowapunguza.

Mohan’s kupitia kwa Wakili wake Dillip Kesaria ililieleza Mwananchi kuwa ingawa madai yake ya fidia ya zaidi ya Sh12 bilioni iliyokuwa ikiiomba hayakukubaliwa, lakini wameridhika na hukumu hiyo na kiasi cha zaidi ya Sh6.2 bilioni walizopewa na Mahakama.

Wakati Mohan’s ikieelezea kuridhika na hukumu hiyo, BAT kwa upande wake kupitia kwa Wakili wake, Karume, ililieleza kuwa haikuridhika na hukumu hiyo na kwamba itakata rufaa katika Mahakama ya Rufani kuipinga.

Wakili Karume alibainisha kuwa tayari wameshachukua hatua za awali za kukata rufaa kuipinga hukumu hiyo, kwa kuwasilisha mahakamani taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

“Hivyo kwa sasa tunasubiri tu kupata mwenendo wa kesi hiyo ili tuweze kukata rufaa rasmi kwa kuwasilisha mahakamani sababu za rufaa yetu,”amesema Wakili Karume.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa

Asuswa na Wazazi kwa Kuwa na Mahusiano na Kijana Mweusi ..!!!

$
0
0

Mwanafunzi mmoja Allie Dowdl (18) amechangisha zaidi ya dola 10,000 kupitia mchango wa raia baada ya kudai kwamba wazazi wake walikata uhusiano na yeye kwa kuwa na mpenzi ambaye ni mweusi aliyetambulika kwa jina la Michael Swift.

mweusi1Allie Dowdle
Allie Dowdle amesema wazazi wake walikataa kumpatia fedha kwa sababu hawakupenda uhusiano wake na kijana huyo mweusi.
mweusi2Akiandika katika ukurasa wake wa GoFundMe, Allie alisema: Nikiwa na umri wa miaka 18 wazazi wangu wamekataa kunifadhili katika maisha yangu ya baadaye, na kunipokonya raslimali zangu zote.

Baba’ke msichana huyo hata hivyo amekana kwamba sababu ya kukata uhusiano huo ni ile ya ubaguzi wa rangi.
mweusi3Allie anasema kuwa yeye na Michael Swift wamekuwa katika husiano wa kimapenzi kwa takribani mwaka mmoja baada ya kuwaelezea wazazi wake lakini swala hilo likazuka tena baada ya Michael kukutana na wazazi wake msichana huyo.

Anadai kwamba baada ya mkutano huo wazazi wake walimtenga na sasa hawezi kupata fedha alizohifadhiwa, gari, simu na hawezi kulipia masomo yake.
mweusi4”Babangu hakunipa sababu nyingine, aliniambia kwamba siruhusiwi kumuona Michael tena”, alisema. Kwa nini? kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.

”Sitasahau vile wazazi wangu walivyonikaripia walipoelezea vile walivyokasirishwa nami kwamba ningeweza kutafuta mtu 

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa

mwengine mzuri zaidi”.

Bodi ya Mikopo Yacharuka..15% Kuanza Kukatwa Kwenye Basic Salary kwa Wadaiwa

$
0
0

Baada ya Rais kusaini Mabadiliko ya Sheria, 15% ya Bodi ya Mikopo kuanza kukatwa kwenye mshahara ghafi(basic) kuanzia mwezi huu.

Aidha taarifa hiyo ya Bodi ya Mikopo imebainisha kuwa ulipaji huo unapaswa kufanywa kwa wakati kwani kuchelewesha malipo hayo kutapelekea kutakuwa na adhabu(Penalty) ya asilimia 100.

Simfagilii Barack Obama Hata Kidogo, Hana Utu-Nikki wa Pili

$
0
0

Rapa Niki wa Pili amefunguka na kusema yeye hana cha kukumbuka kwa Rais wa Marekani Barack Obama ambaye tarehe 20 mwezi huu anamaliza muda wake kuitumikia Marekani kama Rais 44 na kukabidhi ofisi kwa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump.


Niki wa Pili aliweka wazi sababu kubwa inayomfanya asiwe na cha kukumbuka kutoka kwa Rais Barack Obama kwanza ni kutokana na Rais kutokuwa na utu na serikali yake kushiriki katika mauaji ya watu na kukatisha haki za watu kuishi katika baadhi ya maeneo.

"Mimi kwangu sina cha kumkumba Obama kwa sababu mimi kwanza ni mtu naye amini katika utu na naamini kila binadamu ana haki ya kuishi hivyo nikimkumbuka Obama namkumbuka madrone yamedondoshwa huko na kuuwa watu wasio na hatia zaidi ya elfu saba, ukienda Afghanistan amesambaratisha taifa la Iraq ukiangalia Libya.

Kutokana na kitendo hicho Niki wa Pili anasema yeye kama mfuasi wa utu hawezi kumkumbuka Barack Obama na wala hawezi kumuunga mkono.

"Mimi kama mfuasi wa utu niko against na mtu yoyote anayekandamiza utu sehemu yoyote duniani.

Hivyo siwezi kumuunga mkono Obama sababu mimi namuona hakuwa mfuasi wa utu kwa hiyo mimi si mtu wangu kabisa" alisema Niki Wa Pili

Isabela Atoa Kali.. Adai Mwili Wake ni Kwaajili ya Wazungu tu, Wabongo Wana Maumbile ya Siri Makubwa

$
0
0

Mrembo Isabela aliyekuwa mpenzi wa Luteni Kalama miaka kadhaa na kupigana chini mwaka jana ametoa kali kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema haya:

"@belafasta - Huu mwili mtam sana. Ni wa kutiwa na wazungu tuuuu. Wa bongo mb**oo zao kubwa sizitaki"


Isabela Atoa Kali.. Adai Mwili Wake ni Kwaajili ya Wazungu tu, Wabongo Wana Maumbile ya Siri Makubwa

Mambo Kumi Ninayojifunza January ya Mwaka huu....

$
0
0


1. Kumbe waweza shinda njaa bila kufa.

2.Kumbe waweza beba chakula na kwenda nacho kazini.

3. Bila boda, Bila bajaj unaweza tembea na kufika Kazini.

4. Tafadhali nipigie ni huduma ya msingi

5.Nyama ni mbaya kwa Afya yako.

6. Jiko la mkaa linapika chakula kizuri sanaa.

7. Kumbe ukisaga Mahindi yasiyokobolewa yanatoa unga safii

8.Maji ya kuchemsha ni matamu na mazuri sana zaidi ya Dasani.

9. Waweza kula ugali kama kifungua kinywa( breakfast)

10. Ukioga na sabuni ya Kipande, bado utakuwa msafi... ASANTE JANUARI.

Ray Kigosi Afunguka Juu ya Mimba ya Chuchu Hans

$
0
0
Zikiwa zimebaki siku kadhaa msanii wa filamu nchini Chuchu Hans kujifungua msanii Ray Kigosi amefunguka na kumuomba Mungu mpenzi wake huyo ajifungue salama.

Ray amesema licha ya kupitia mambo mengi lakini Mungu amewapigania mpka sasa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kati ya mwezi huu wa kwanza kama siyo wa pili mwanzoni.
Ray Kigosi anasema ulikuwa ni kama utani vile lakini tayari leo umeshafika mwezi wa tisa toka mchumba wake huyo amepata ujauzito huo.  

"Kwanza kabisa napenda kumrudishia sifa na utukufu Mungu baba Muumba wa mbingu na ardhi tumepitia vingi vikwazo lakini yeye atutiaye nguvu aliendelea kusimama na sisi imara asante sana Mungu kwa kuwa mwema kwetu mengi yalisemwa juu yetu lakini Mungu baba umejibu ulikuwa mwezi mmoja kama utani vile hatimaye imefika miezi tisa na sasa kubaki siku chache. Nakuombea my lovely Mzungu Mungu akufanyie wepesi". Ray Kigosi 

Kocha Lwandamina na Pluijm, Hali Tete Yanga

$
0
0
Si kila tabasamu linamaanisha furaha au amani, ndivyo navyoweza kusema, ukiwaona machoni ni watu wenye sura zenye amani na furaha lakini mioyoni mwao wanajua wenyewe, hawa ni Hans van Pluijm na George Lwandamina.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimenifikia, Pluijm na Lwandamina hawana maelewano mazuri.

Hali hiyo imesababisha kutokuwepo na utulivu kwa baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanadai Pluijm anasababisha makundi kwa wachezaji na kupelekea baadhi yao kutojituma kwenye timu.

“Hans haelewani na Lwandamina, kuna ‘bifu’ zito kati ya wawili hao,” ni maneno ya jamaa aliyenitonya kuhusu hali ilivyo ndani ya Yanga yeye akiwa ni miongoni mwa viongozi wa kamati ya usajili ya usajili ya klabu hiyo.

“Bifu hilo limepelekea uongozi wa Yanga kukaa kikao cha kutaka kumwondoa Pluijm lakini kuna baadhi ya viongozi bado wanamtaka Pluijm, lakini wapo ambao wanasema kwamba akiendelea watajiuzulu nafasi zao.”

Tangu Lwandamina alipowasili ndani ya Yanga kama kocha mkuu, Hans van Pluijm alipewa jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo.

Lowassa na Mbowe Walia Njaa Kagera,Wamtaka Magufuli kuwa na Huruma..!!!

$
0
0

SIKU mbili baada ya Rais Dk. John Magufuli kukanusha taarifa za kuwako kwa tishio la njaa nchini akisema anayejua hilo ni yeye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema hali ya chakula hivi sasa ni mbaya.


Mbali na Lowassa, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya na wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, wamesema hali ya njaa katika maeneo yao ni mbaya.

Kauli za wanasiasa hao wa upinzani zimekuja wakati juzi Rais Magufuli akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu alikaririwa akisema: “Anayejua kuna njaa ni Rais wala si gazeti fulani, mimi ndiye nimepewa dhamana ya kuongoza Watanzania wote.”

Zaidi alikwenda mbali na kusema wafanyabiashara wanatumia magazeti kusema kuna njaa ili wasamehewe kodi ya mahindi yao waliyoyatoa Brazil kuja kuyauza hapa nchini.

Wakati Rais Magufuli akisema hayo, jana gazeti moja (Si Mtanzania) lilimkariri mmoja wa wateule wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba, akisema zaidi ya mifugo 3,000 imekufa wilayani kwake kwa kukosa malisho na maji kutokana na ukame.

Akizungumza katika mkutano mkuu maalumu wa Chadema Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera uliofanyika katika eneo la Bunazi, Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, alimtaka Rais Magufuli kutozipuuza hoja zinazotolewa kuhusiana na masuala mbalimbali ya nchi.

Kuhusiana na hali ya ukame nchini, Lowassa amesema hali ya chakula nchini hivi sasa ni mbaya sana.

“Tunamwomba Rais atafakari kwa uungwana hoja za watu wengine. Tunamheshimu ni rais lakini tunamwomba atafakari hoja hizi watu wasiendelee kuumia sana,” alisema Lowassa.

“Eneo moja ambalo hakika rais anatakiwa kusikia hoja za watu wengine ni suala la njaa. Nimeshuhudia mwenyewe pale Longido na maeneo mengine…hali ya mvua ni mbaya, hali ya chakula ni mbaya, watu wako hoi bin taaban halafu wanaambiwa hakuna kuwapelekea chakula!!” alishangaa Lowassa.

Akizungumzia juu ya madhila na wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Lowassa alielezea kushangazwa kwake na hatua ya rais kuamua kutopeleka misaada kwa wahanga hao akisema hata Mungu anashangaa.

“Mimi nakaa nasema mfano kama ni mama yako pale kijijini, halafu amekumbwa na janga hili, anaambiwa ajisaidie mwenyewe si atakushangaa, hata Mungu atashangaa,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare, amesema hali ya chakula katika Mkoa wa Kagera ni mbaya.

Kama ilivyo kwa Lwakatare kwa upande wake Bulaya alimwambia Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuwa amekuwa akipokea ujumbe kutoka kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali wakilia matatizo ya njaa.

Katika hilo, Bulaya alimwomba Mbowe kulisemea jambo hilo kwenye ngazi ya Taifa.

Bulaya aliyasema hayo jana kwenye kikao cha Mkutano Mkuu wa chama hicho kilichofanyika wilayani Bunda.

Alisema licha ya ukame uliopo lakini  tembo wamechangia tatizo la njaa kutokana na kuharibu mazao mashambani.

“Mwenyekiti, hapa wananchi wana njaa na nimekuwa nikitumiwa ujumbe na wananchi wa jimbo langu wakilalamika kukosa chakula kutoka maeneo mbalimbali,” alisema Bulaya.

Katika ufunguzi wa kikao hicho, Mbowe alisema Taifa lina msiba wa njaa na amekuwa akipokea taarifa kutoka kwa wabunge wengi na ni vyema Serikali ikalifanyia kazi.

Alisema Watanzania waliwachagua viongozi si kwa kuwafanya watumwa bali kuendeleza nchi kwa misingi ya utu.

Mbowe alisema Watanzania wanalia njaa si kwamba ni wavivu bali ni hali ya ukame iliyopo na kwamba tatizo hilo halitaendeshwa kwa kauli za kukatisha tamaa kama zinavyotolewa na viongozi.

“Hili tatizo lipo na pale unapokuwa unawazuia binadamu kusema ipo siku mawe yatazungumza na ukweli utabainika kile ambacho Watanzania walikuwa wanakizungumzia kipo. Hifadhi ya chakula hapa nchini ilianzishwa ili kusaidia wakati wa majanga ya njaa, sasa leo kuna tatizo na wananchi wanasema lakini maneno yao yanakuwa yanapuuzwa, si jambo la kiungwana,” alisema Mbowe.

Akizungumzia hali ya kisiasa hapa nchini, Mbowe alisema yanayotokea sasa ya kuwafunga na kuwaweka mahabusu viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge si suluhisho la kuendelea kupambana katika kuwazungumzia wananchi.

Alisema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anasota mahabusu zaidi ya miezi miwili kwa kosa ambalo linastahili dhamana.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa

Alichokisema Martin Kadinda Juu ya Tabia za Wema Sepetu,Adai zimembadilisha Kabisa..!!

$
0
0

ALIYEKUWA Meneja wa Mrembo wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Martin Kadinda, amempongeza mwanadada huyo kwa kubadilisha mfumo wa maisha yake.


Akizungumza  jana, Martin alisema kitendo cha Wema kufuta picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kubadili tabia za kuweka wazi maisha yake ni hatua ya kupongezwa.

“Uamuzi alioufanya Wema ni hatua nzuri na ya kupongezwa, mimi na familia yake hatukuwa tukipendezwa nayo kwa kuwa ilikuwa ikichafua jina lake,” alieleza Martin.

Martin aliongeza kwamba Wema ambaye amebadili meneja kwa sasa, amekuwa tofauti na alivyozoeleka maana amekuwa muelewa na msikivu kwa anachoelekezwa.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa

Baada ya Prof Lipumba Kung'ang;ania Ofisi za Buguuni,Cuf ya Maalim Seif Wafungua Ofisi Zao Leo..!!!

$
0
0

CHAMA cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, leo wanatarajia kuzindua jengo jipya la ofisi lililopo eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.


Taarifa za ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa ofisi hizo zitatumiwa na viongozi wakiwemo wabunge wanaomuunga mkono Maalim Seif.

Akithibitisha taarifa hizo, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Mbarara Maharagande, alisema uzinduzi wa ofisi hiyo mpya utafanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Hatua ya kuzindua jengo hilo imekuja wakati ambapo chama hicho kikiwa katika mgogoro mkubwa wa uongozi uliotokana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kumrudisha katika nafasi yake ya uenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba na kisha kutwaa jengo lenye ofisi za chama hicho lililopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

“Tutazindua jengo jipya iwe leo au kesho au muda wowote kuanzia sasa, lakini ni jengo la wabunge wote kufanyia shughuli zao hapo na kupanga mikakati mbalimbali ya kukitangaza na kukiimarisha chama,” alisema Maharagande.

Wakati Maharagande akisema hayo, taarifa  toka kwa vyanzo vyake ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa jengo hilo pia litakuwa na ofisi ambazo zitatumiwa na viongozi wa CUF akiwemo Maalim Seif mwenyewe.

Kwa muda wa miezi sita sasa pande mbili za uongozi zimekuwa zikilumbana juu ya uhalali wa maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho uliofanyika Agosti mwaka jana ambao pamoja na mambo mengine ulilenga kumwondoa Profesa Lipumba.

Hatua hiyo ilizua tafrani na hata wajumbe kurushiana masumbwi ndani ya ukumbi hali iliyosababisha kuvunjika kwa mkutano huo.

Siku chache baadaye Baraza Kuu la uongozi lilikutana na kutangaza kumvua uanachama wa CUF Profesa Lipumba jambo ambalo lilipingwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Mutungi ambaye alisema taratibu za kufukuzwa kwa Mwenyekiti huyo hazikufuatwa.

Mapema wiki hii upande wa uongozi wa CUF, chini ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Lipumba, ulidaiwa kulamba Sh milioni 369.378 za ruzuku kinyume na utaratibu.

Ilielezwa kuwa fedha hizo zilitolewa ndani ya siku moja katika matawi matatu tofauti ya Benki ya NMB kwa kutumia akaunti ya chama na baadaye kuhamishiwa kwa mtu binafsi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF ambaye hatambuliwi na Msajili, Julius Mtatiro, alisema fedha hizo zilitolewa kutoka Hazina na kupelekwa NMB tawi la Temeke.

Wakati Mtatiro akidai hayo, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya, ambaye yupo upande wa Lipumba, alidai fedha hizo zimetolewa kihalali kama walivyofanya upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ambao nao walitoa Sh milioni 80 kupitia Benki ya NBC.

Pamoja na hali hiyo, Mtatiro alisema fedha hizo ziliingizwa katika akaunti binafsi ya mtu aliyetambulika katika muamala kwa jina la Mhina Masoud Omary.

Alisema kwa niaba ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF ambalo limemteua yeye kuongoza, hana budi kuwajulisha wanachama kuwa CUF imeibiwa fedha hizo za ruzuku ambazo alidai zimetoroshwa na watu wasiojulikana. 

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live




Latest Images