Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Diamond Aaamua Kumfanyia Baba Yake Jambo Hili Ambalo Hatakuja Kulisahau Maishani Kamwe..!!!

$
0
0
baba-diamond-1 
DA ES SALAAM: Baada ya juzikati kupatikana taarifa kuwa mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatana na baba yake mzazi, Abdul Juma, inadaiwa kuwa katika sherehe ya kutimiza siku 40 ya mtoto wa Diamond aitwaye Nillan ‘Chibu Junior’, babu mtu huyo naye atatinga Sauzi.


Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake, baba Diamond ni kati ya watu watakaopata nafasi ya kukwea pipa kwenda Sauzi kwenye tukio hilo linalotarajiwa kuchukua nafasi Januari 16, mwaka huu.
diamond-na-zari“Sherehe ya kumtoa Nillan inatarajiwa kufanya Johannesburg, kule kwenye mjengo wa Diamond. Watu kadhaa kutoka Bongo wakiwemo mastaa wamepewa mualiko na utakuwepo usafiri maalum wa ndege wa kwenda na kurudi Sauzi.

“Nilimsikia Diamond akisema hata mzee Abdul atapata fursa ya kwenda kuwaona wajukuu zake, kwa hiyo tusubiri tuone,” alisema mtoa habari huyo.

Katika kuweka uzani wa habari hii, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpata Diamond lakini simu yake haikuweza kupatikana mara moja.

Ijumaa lilipata fursa ya kuzungumza na baba Diamond na kuulizwa kama ana taarifa juu ya safari hiyo ambapo alisema: “Hata mimi nasikiasikia ila kama itakuwa hivyo litakuwa ni jambo zuri kwani nitapata nafasi ya kuwaona wajukuu zangu. Kama nilivyosema, mimi na Diamond hakuna shida tena kwa hiyo hata hilo la kwenda Sauzi linawezekana kabisa.”

Duh Hii Ndiyo Kik Ya Mwaka: Harmonize Feki Aaamua Kutoka na Wolper Feki Ili Wafanane na Harmonize Halisi,Tazama Pichaz Hapa..!!

$
0
0
wolper-na-hamonie
Harmorapa na Wolper Feki.

Msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka WCB, Harmonize kiasi cha kubatizwa jina la ‘Pacha wa Harmonize’, Harmorapa, leo ametinga kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar ambapo mbali na mambo mengine, amefungukia uhusiano wake wa kimapenzi na ‘Wolper’.



Harmorapa amesema kuwa kutokana na kufanana sana na Harmonize, aliamua kutafuta msichana anayefanana sana na mpenzi wa Harmonize, mwanadada Jacqueline Wolper ambaye naye kwa jinsi anavyofanana naye, ukikutana nao unaweza kudhani umekutana na Harmonize na Wolper ‘orijino’.
harmo-rapa-2Harmorapa
“Prodyuza wangu, Khalfan ndiye aliyenikutanisha na mwanadada huyu ambaye watu wanamuita Wolper kutokana na jinsi alivyofanana naye, alinikutanisha kwa lengo la kufanya naye kazi akiwa kama video queen, akatokea kuwa rafiki yangu sana na mara kwa mara nakuwa naye sehemu mbalimbali.harmo-rapa-3
“Kiukweli uhusiano wetu ni wa kikazi tu tofauti na Harmonize na Wolper ambao ni wapenzi kweli.”
   

Zitto Azidi Kuichokonoa Serikali ya Magufuli,Leo Kaibua Hoja Hizi Nzito,Soma Hapa Kuzijua..!!!

$
0
0

Serikali ilitangaza kuwa ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa utaanza mwezi Disemba mwaka jana kwa msaada kutoka nchi ya China. Leo ni mwezi Januari hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali haijatangaza. Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika) wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao.


Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50.

Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo. Madhara ya kuchelewa kujenga Reli ya Kati ni makubwa mno kwani washindani wetu wa kibiashara, Kenya, wanamaliza Reli yao sasa kuunganisha na nchi za Rwanda na Mashariki ya Kongo.

Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote. Juzi juzi kwa mara ya kwanza tumewasaidia Israel kwenye Umoja wa Mataifa bila ya kujali msimamo wetu wa 'Two States Solution' kati ya Palestine na Israel.

Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya. Tanzania haikuanza na awamu ya Tano, nchi hii imekuwapo na itaendelea kuwapo. Hatuwezi kukaa kimya tukiendelea kuona misingi ya nchi yetu inavunjwa vunjwa. Lazima tukemee.

Kudadeki..!!! Serikali Yaufyata Juu ya Hali ya Njaa Nchini,Huu Ndio Uamuzi Uliotolewa Kuikabili Hali Hiyo..!!!

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeruhusu tani milioni 1.5 za chakula zilizokuwa zimehifadhiwa zianze kuuzwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei za vyakula.


Pia, Majaliwa amesema kupanda kwa bei ya vyakula nchini kulichangiwa na ukosefu uliojitokeza nchi jirani, lakini akawataka wananchi wasiwe na hofu kwani  chakula kipo cha kutosha.

Kauli ya Waziri Mkuu imekuja wakati mjadala wa upungufu wa chakula nchini ukizidi kupamba moto na kusababisha baadhi ya wadau kudai kuwa, Serikali inachelea kutangaza kuwa kuna njaa nchini.

Tayari, Rais John Magufuli ameshaeleza kuwa hakuna baa la njaa na kama litatokea,  yeye ndiye pekee mwenye mamlaka ya kutangaza na kufafanua kuwa tatizo hilo linakuzwa na wafanyabiashara wachache na wanasiasa wanaotaka kujinufaisha na hali hiyo.

Jana, Majaliwa aliyezungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili mjini hapa na ndege ya kwanza ya Bombadier kufanya safari za kibiashara kati ya Dar es Salaam na Dodoma, alisema hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.



Spika Ndugai Awamulia Mawaziri wa Magufuli,Awachimba Mkwara wa Kufakuzisha Kazi,Soma Hapa Livee..!!

$
0
0

Wabunge na mawaziri wametii agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai lililowataka kuzingatia mahudhurio ya vikao vya kamati za Bunge, vinginevyo majina yao yangewasilishwa kwa mamlaka wanazowajibika ikiwamo kwa Rais  John Magufuli.


Katika mkutano wa nne wa Bunge mwaka jana, Spika Ndugai alisikitishwa na mahudhurio hafifu ya mawaziri na wabunge katika vikao vya kamati vilivyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 2 mjini Dodoma.

Amesema katika vikao hivyo vya kamati ilitengenezwa orodha ya wabunge na mawaziri watoro,  ambayo ataitunza hadi vikao vingine vya kamati.

Spika Ndugai aliwaonya kuwa  iwapo wataendelea na tabia ya utoro kwa vikao vya kamati vilivyofanyika kati ya Oktoba 17, 2016  angewashtaki kwa wapigakura, vyama vyao na mawaziri angewafikisha kwa Rais Magufuli.

Umesikia Polisi Walichokisema Kama Sababu ya Kumkamata Lowassa?Soma Hapa Livee..!!!

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea wa Urais 2015 kupitia CHADEMA, Edward Lowassa leo alikamatwa na jeshi la Polisi  wakati akiwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome na baadaye aliachiwa  huru ambapo taarifa za polisi zinadai kuwa walimzuia kwa sababu za kiusalama.
 
Kupitia kituo cha Television cha Azam wameripoti habari ya kukamtwa kwa Lowassa ambapo baadhi wa wananchi wameeleza tukio lilivyotokea.
 
“Tulikuwa kwenye msafara ya kumpokea Lowassa lakini tulipofika hapa stendi wananchi walitaka kuongea na Lowassa, kabla hata hajashuka kwenye gari askari walituvamia wakasema tuondoke moja kwa moja twende kituoni”shuhuda.
 
Mbali na hivyo, Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wanaoandamana kwenda kituo cha polisi baada ya Lowassa kukamatwa.
 
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita amesema kuwa hawakuwa wamemkamata Edward Lowassa bali walikuwa wakijadiliana naye kuhusu usalama wake na jamii.

Haya Fursa Hiyo,Polisi Watangaza Milioni 5 Kwa Atakayetoa Taarifa za Muuaji Huyu Sugu..!!!

$
0
0

Polisi wanamtafuta kijana anayetuhumiwa kuwa muuaji sugu maarufu  Mpemba ambaye pia anakabiliwa na makosa mengine mbalimbali.


Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametangaza dau la Sh5 milioni kwa mtu yeyote atakayempata mtuhumiwa huyo au kutoa taarifa zitakazowawezesha kukamatwa.

“Ni jambazi sugu na anafanya mauaji,  hovyo ameanza muda mrefu tangu kipindi cha Kamanda (Suleiman) Kova ametangazwa lakini hadi leo hii hajakamatwa,” amedai.

Licha ya Mpemba, jeshi hilo linamtafuta kijana mwingine wa Mkuranga mkoani Pwani ambaye anatuhumiwa kuchukua wake wa majambazi wenzake ambao wamekamatwa na Polisi na kuwaozesha kwa wahalifu wengine.

Hii Ni Kubwa Kuliko!! Zitto Adai ACT - Wazalendo kinamuunga mkono Rais Magufuli..!!!

$
0
0

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kinaunga mkono kazi zinazofanywa na Rais John Magufuli pamoja na serikali yake kwa sababu kuna mambo mazuri yanafanyika.


Akihutubia katika mkutano wa kampeni za udiwani jana, katika kata ya Kijichi Dar es Salaam, Kiongozi wa chama hicho, Kabwe Zitto alisema hawajutii kumuunga mkono Rais Magufuli.

Katika mkutano huo, Zitto amewaomba pia wananchi wa Kijichi kumchagua mgombea udiwani wa chama hicho, Edgar Mkosamali katika uchaguzi utakaofanyika Januari 22 mwaka huu.

“Sisi kama chama, ACT Wazalendo tulimuunga mkono Rais tangu mwanzo wa utawala wake na kumkabidhi Ilani ya uchaguzi ya chama chetu kama ishara ya kwamba uchaguzi umekwisha na sasa tujenge nchi yetu. Hatujutii kumuunga mkono kwa sababu kuna mambo mazuri amefanya kuhusu nchi yetu,” alisema Zitto.

Zitto alizitaja kazi ambazo chama chake kinaunga mkono rais kuwa ni pamoja na kupambana na rushwa na ufisadi nchini.

“Ameondoa hali ya ‘impunity’ iliyokuwa imeshika mizizi nchini na kuwawajibisha watendaji na waziri aliyekiuka maadili ya kazi”.

Hata hivyo, Zitto alisema chama chake kinamuomba Rais Magufuli na serikali yake kuwa wasikivu katika matatizo yanayowakumba watanzania, ikiwa ni pamoja na upugufu wa chakula nchini jambo ambalo hivi karibuni alilizungumza na kusema kuwa nchi haina njaa na kwamba hayuko tayari kugawa chakula.

Mange Kimambi Afunguka Jinsi Alavyompata Mtoto Wake wa Kwanza....Amtakia Happy Birthday

$
0
0


From Mange kimambi_ - 15 years ago today at 22 years old I was in Highland Hospital in Oakland, California giving birth to my very first child who I named Cassandrah Cutiey. Yes her middle name is Cutiey, she hates it..I dont know what I was thinking 😂.....I was alone and scared in a foreign country, no family, no boyfriend just one friend Natalia Bakilana and her husband Daniel were in the room holding my hand.....I remember a few hours later being asked by child services if I wanted to give her up for adoption since I was alone, a foreign college student with no support what so ever. I remember looking at them in disbelief like really? You think I would go through 9 months of pregnancy, get disowned and financially cut off by my father and all the time knowing full well another woman was a few months pregnant with the same guy, I would go through all that only to give her away???😭😭. I told them if I didnt want her I would had an abortion..... She truly is my first 💖 and I hope one day she will realize as crazy, as controlling, as bossy, as mkaliiiiii, as ' planning her future' , as untrusting as her mom is no one in this world will ever love her as much as I do. No one....... .
.
.
Happy 15th Birthday Dada Kubwa. We miss You and We Love You..........

Neno Gani Linaumiza Zaidi Kutoka Kwa Mpenzi Wako Unaempenda Kwa dhati Kati ya Haya:-

$
0
0

Neno Gani Linaumiza Zaidi Kutoka Kwa Mpenzi Wako Unaempenda Kwa dhati Kati ya Haya:-

1. Tuachane,
2. Sikutaki tena,
3. Nimepata mwngne,
4. Mbona king'ang'anizi wewe?,
5. Sikupendi,
6. Wazazi wangu hawakutaki,
7. Siwezi kuwa na wewe,
8. Kwako nilikosea njia tu,
9. Huna mvuto naona aibu,
10. Najuta kuwa na ww,
11. Huwezi kunihudumia fuata wajinga wenzio,
12. Wewe sio type yangu,
13. Dini zetu ni tofauti hivyo siwezi kuwa nawe...

FUNGUKA HAPA MDAU

Nogesha Upendo Ya Vodacom Yaja Na Tsh Bilioni 32 Za M-pesa

$
0
0
Wakati wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao, sasa malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.

Awamu hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio hilo kampuni hiyo  imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya wateja wetu.

“Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake. Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa “zaidi la faida” Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.

Kuona kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako. Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.

Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200 washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa moja.

Nyoshi Ataka Mashabiki wa Muziki Wamkate Miguu

$
0
0
Msanii wa  band ya FM Academia Nyoshi El Sadaat amesema wanategemea kuachia nyimbo mbili ambazo zimepewa majina 'Nakuita' na 'mama wa Kambo' ambazo ndizo zitakuwa kwa ajili ya mwaka huu 2017.

Akionge kupitia eNEWZ Nyoshi amesema kama media zitatoa sapoti ya kutosha kwa  nyimbo hizo na kukosa kufanya vizuri basi mashabiki zake wamkate mikono  na miguu ili kuweza kuficha aibu ya uso wake kwa kuwa wamejipanga vizuri na wanahakikisha wanarudisha muziki wa dansi kuwa kwenye chart.

Hata hivyo Nyoshi amesema nyimbo walizoachia kwa mwaka 2016 hazikufanya vizuri kwa kuwa hawakupata sapoti ya kutosha kutoka katika media mbalimbali hali  iliyopelekea muziki wa dansi kushuka chart kwa mwaka 2016.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza Hapa Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Pitia Vichwa Vya Magazeti Leo 17/1/2017..!!!!

Duh!! Eti Mtoto wa Rais Mteule Gambia Amefariki Dunia kwa Kuumwa na Mbwa..!!

$
0
0

Mtoto wa kiume wa rais mteule wa Gambia, Adama Barrow amefariki akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuumwa na mbwa.


Habibou Barrow alifariki Jumapili baada ya kukumbwa na mkasa huo katika  eneo la Manjai karibu na Mji mkuu Banjul ambapo mazishi yake tayari yashafanyika.

Rais Mteule, Barrow ambaye ana wake wawili na watoto wengine wanne, yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa kuwa rais wa Gambia siku ya Alhamisi.

Mo Dewji Azidi Kuapsua Anga Kimataifa,Azoa Tuzo Nyingine Kubwa Afrika..!!!

$
0
0

Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year (ALM) 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania.

 
Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata asilimia 38.3.

Kwasasa bado Jarida la African Leadership hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.

Oh Nooh!! Mamilioni ya Mtoto wa Pili wa Diamond Yatoweka Kimiujiza,Mwenyewe Asema Hilo Halimsumbui..!!

$
0
0
diamond
Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Matarajio ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya kumtumia mwanaye Nillan kupata mamilioni ya pesa kutoka kwa wadhamini yanadaiwa kubuma kufuatia maelezo kuwa, baadhi ya makampuni yaliyokuwa yamezungumza naye yameamua kujiweka pembeni kutokana na ukata wa pesa.


Awali, akizungumza  hivi karibuni, Diamond aliweka wazi kuwa, kabla hata mtoto hajazaliwa kuna benki mbili ambazo zilimwaga dau la mamilioni ya pesa kwa ajili ya kutumia picha ya mtoto huyo kwenye huduma zao lakini yeye alikuwa hajaweka wazi ipi aingie nayo mkataba na kwa mkwanja upi.

Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Hata hivyo wakati mtoto huyo akikaribia kufikisha mwezi mmoja, taarifa zilizotufikia zinadai kwamba baadhi ya makampuni yaliyojitutumua kutaka kutoa mamilioni kwa ajili ya sura ya mtoto huyo yameingia mitini.

Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kilidai kuwa, awali Diamond alikuwa amefanya mazungumzo na makampuni na mabenki tofauti lakini kutokana na hali ngumu, baadhi wamekaa kimya mpaka sasa.

“Kimsingi yale mamilioni ambayo Diamond na Zari walitarajia kuyapata kutoka kwa makampuni na benki kama ilivyokuwa kwa Tiffah, yamebuma. Mambo yamekuwa siyo.

“Inavyoonekana huku kubana pesa za dili kwa Rais John Magufuli kumewafanya hata wale waliokuwa wakitaka kutoa pesa ili wanunue sura ya Nillan wafanye uamuzi wa kupotezea.”
zari-na-mond-kidZari (aliyelala) ikiwa ni saa chache baadea ya kujifungua

Umaarufu wa Nillan umechangia?

Aidha, wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa, kubuma kwa mapesa hayo kunaweza kuwa kumetokana na mtoto huyo kutovuma kama ilivyokuwa Tiffah hivyo kuna ambao wameona kutoa pesa kwa ajili ya sura yake ni sawa na kuzitupa.

“Kipindi cha Tiffah ilikuwa rahisi sana benki na makampuni mbalimbali kutoa pesa ili kununua sura yake kwa kuwa alikuwa ‘hot’ na pia fedha ilikuwa inapatikana kirahisi lakini ikimbukwe huu ni utawala na Magu, pesa haitoki kirahisi.

“Pia Nillan mpaka sasa hawezi kuishawishi benki yoyote itoe mamilioni kununua sura yake kwa kuwa hana kiki kivile. Kwa mfano Tiffah alipozaliwa na kufunguliwa ukurasa wake wa Insta, ndani ya siku mbili tu alikuwa na followers (wafuasi) 200,000 lakini kwa Nillan akiwa anakaribia kufikisha mwezi mmoja ana followers 69,000, hiyo inaonesha watu hawamshobokei na hata kibiashara sura yake haiwezi kuwa kivile,” alisema Rashid Maguli wa Kinondoni ambaye ni shabiki mkubwa wa Diamond.
zari-na-diamondDiamond na mpenzi wake, Zari
Hili linaweza kutokea pia
Ikazidi kudaiwa kuwa, kuna uwezekano kwa mara ya kwanza Diamond akaamua kuionesha picha ya Nillan bila kuwa na mdhamini au akapata wadhamini lakini akapewa ‘pesa mbuzi’ tofauti na matarajio yake.

Diamond anasemaje?

Kufuatia kumwagika kwa ubuyu huo, paparazi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Diamond ambapo alipopatikana alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kirefu kwa kuwa bado mazungumzo yanaendelea na anaamini kila kitu kitaenda sawa.

“Kila kitu kinaenda sawa, niliongea na baadhi ya wadhamini na kuwaambia wasubiri mtoto azaliwe, sasa amezaliwa naamini kila kitu kitaenda sawa, hayo mambo ya kubuma siyajui,” alisema Diamond.

Tujikumbushe kidogo

Mwaka jana, Agosti 6, Tiffah alizaliwa na siku chache baadaye akalamba mkataba mnono wa Ubalozi wa Benki ya NMB na maduka makubwa ya vitu vya watoto.

Mfahamu Zoadic Killer.Muuaji Aliyetikisa Marekani Nzima..!!!

$
0
0

Kuanzia mwaka 1968 mpaka mwanzoni ya miaka ya 70 taifa kubwa la Marekani lilikubwa na mtu mmoja hatari sana,si mwingine bali ni muuaji tambulishi(serial killer) ambaye yeye kama yeye alipendelea kuitwa zodiac killer. Mpaka mtu apate sifa ya kuitwa serial killer anatakiwa awe ametekeleza mauaji wa watu si chini ya watatu katika matukio tofauti tofauti, na pawe na muda wa mapumziko(cooling off period) kati ya tukio moja na jingine.


Hii ni tofauti kidogo na FBI ambao wao wanamtambua 'serial killer' kama mtu aliyetekeleza mauaji ya kuanzia watu wawili katika matukio tofauti. Rekodi za vyombo vya usalama zinaonyesha huyu zodiac killer aliua watu watano waliodhibitishwa(zodiac's confirmed victims) na kujeruhi wengine wawili kwa vipindi tofauti,huku rekodi hizo hizo zikiinisha kua anaweza kua ameua watu 20 mpaka 28. Watu wengi wanaamini hii ni janja ya vyombo vya usalama kuficha aibu maana zodiac mwenyewe anadai kua ameua watu 37.

Muuaji tambulishi huyu alijizolea umaarufu mkubwa mpaka ikafika mahali kuna mtu aliyekua na umajinuni(obsession) na mapigo ya huyu zodiac killer akaanza kuiga na kutekeleza mauaji kama ya zodiac killer miaka ya tisini. Huyu bwana mdogo aliyekua anamuiga 'MASTER' zodiac killer(zodiac killer's copycat) alikua anaitwa Heriberto eddie seda,.

Seda alifanikiwa kuua watu watatu na kujeruhi wengine sita vibaya sana katika kipindi cha miaka mitatu, kutokana na ujuzi kuwa mdogo ukilinganisha na zodiac killer,Bwana mdogo Seda alikamatwa mwaka 1996 na kupigwa 'mvua' ya miaka 232 jela bila msamaha. Turejee kwa 'MASTER' zodiac killer ambaye alikua akifanya mauaji yake katika jimbo la Carlifonia japo pia inasadikika alifanya na matukio mengine jimbo la Nevada.....



TUKIO LA KWANZA 'LAKE HERMAN ROAD ATTACK'
Tarehe 20 disemba mwaka 1968, Binti Betty Jensen mwenye miaka 16 anaonekana kua mwenye furaha kuliko watu wote duniani, Hii ni kutokana na sababu ya kupewa ruhusa kwa mara ya kwanza na wazazi wake kutoka na mpenzi wake David Faraday mwenye miaka 17 usiku(first date)...

Baada ya kufanya matanuzi ya hapa na pale wapenzi hawa wanaamua kwenda sehemu moja tulivu(lover's lane) ambayo ilikua mahususi kwa ajili ya wapendanao. kufika pale wapenzi hawa wakapaki gari yao, baada ya muda ikaja gari nyingine nyuma yao nayo ikapaki. Akatoka mtu akawaamuru washuke kwenye gari...

Bila ya kelewa nini kinaendelea akaanza kushuka bidada Betty Jensen, ile David nae akiwa anashuka mtu huyu aliyekuja akatoa bastola na kumpiga David risasi ya kichwani iliyopelekea mauti yake papo hapo. Kuona vile bidada betty akawa hana namna zaidi ya kukimbia ili kunusuru maisha yake, Alipofika hatua 28 kutoka pale walipokua wamepaki gari nae aliuliwa kwa kupigwa risasi tano mgongoni.. muuaji akawasha gari lake akaondoka zake..

Picha ya tukio zima ndio hiyo, ila swali la msingi sana(critical question) ni kwamba inawezekanaje jopo hili la wanausalama kupata picha kamili ya tukio zima ilihali hawa wapenzi walikutwa wameshakufa na muuaji hajulikani???walichokuta ni miili ya marehemu na gari lao na wakadai wamekuta alama ya matairi ya gari lingine likiwa linaondoka. Lakini je,hii inatosha kupata tukio zima la haya mauaji? je, kuna mtu alishuhudia hili tukio?



TUKIO LA PILI 'BLUE ROCK SPRINGS ATTACK'

Kwa wajuzi wa historia mtakubaliana na mimi kwamba tarehe 4 ya mwezi wa saba ni siku kubwa sana nchini marekani, hii ndio tarehe wamarekani walipata uhuru na ndio mwanzo wa kuzaliwa kwa taifa kubwa duniani,hii ilikua mwaka 1776. Ni tarehe 4 mwezi wa saba 1969 mida ya usiku,watu wakiwa kwenye shamra shamra za hapa na pale, hii ni tofauti kwa wapenzi wawili Michael Mageau na Darlene Ferrin ambao walikua wamekaa kwenye gari kwa utulivu kabisa mahali panapoitwa 'Blue rock springs'(Maili nne kutoka Lake herman sehemu ya tukio la kwanza)...

Baada ya muda wanakuja vijana kwenye gari lingine wanaanza kupiga baruti(fireworks) nyingi huku wakizisindikiza na vicheko..hii ni kawaida sana kwa siku hii ya kipekee,hawakai sana hapo baada ya dakika kadhaa wanaondoka na kuwaacha hawa wapenzi wawili kwenye utulivu tena..
Wakiwa bado kwenye gari, Mara linakuja gari lingine karibu yao lakini linaondoka, baada ya muda kidogo gari lile lile linarudi kwa mara nyingine, anashuka dereva wa hili gari na kuanza kuelekea kwenye gari walilokaa Michael na Darlene. Mtu huyu aliyekuja anawafata huku akiwa kawamulika na tochi yenye mwanga mkali(flashlight) wapenzi hawa.

Michael anamtoa woga mpenzi wake kwa kumuambia kua huyu atakua ni polisi hivyo watoe vitambulisho vyao maana atahitaji kuviona, kwa mshangao mtu huyu aliyekuja alivyofika karibu bila ya kuongea lolote alitoa bastola na kuwafyatulia wapenzi hawa risasi tano kisha akageuka kuondoka zake...

Akiwa anaelekea kwenye gari lake, Michael alitoa kilio cha kuashiria kuugulia maumivu hali iliyopelekea mtu huyu kurudi tena na kuwapiga wapenzi hawa risasi mbili mbili nyingine kisha kuondoka zake.. Michael alikufa hospitalini lakini kwa bahati sana bidada Darlene alipona licha ya kupigwa risasi usoni,shingoni na kifuani. Yeye ndio alioelezea hili tukio licha ya kutoona sura ya muuaji.



ZODIAC KILLER ANAHUSISHWAJE NA MATUKIO HAYA MAWILI?
Kesho yake(05/07) 'Mnyama' zodiac killer kwa mbwembe kabisa anawapigia simu polisi kwa kutumia simu za vibandani(phone booth) kuwa yeye ndio kahusika na mauaji yaliyotokea jana yake, polisi wanafanya jitihada wanajua sehemu simu ilipotoka lakini mtu huyu alishaondoka muda sana...


BARUA ZA ZODIAC
Mwezi wa nane mwaka huo huo Zodaic anaandika barua moja moja kwa vyombo vitatu vya habari tofauti, na katika kila barua akaweka kipande cha fumbo(cipher) huku akibainisha kua wakiunganisha hayo mafumbo matatu na kuweza kung'amua(crack) fumbo hilo litawapa mwanga ye ni nani. pia alielezea kuhusika na matukio yote mawili hapo juu.

Zodiac akaenda mbali zaidi na kuwatumia ujumbe wa sauti akieleza hatua moja baada ya nyingine jinsi alivyotelekeza mauaji hayo, hii inapelekea kuaminiwa kwa kua taarifa za kina za haya mauaji hazikua zimetolewa kwa jamii(confidental information)
Kuonyesha ubabe zodiac anawaamuru wachapishe barua zake katika ukurasa wa mbele wa magazeti yao la sivyo ataua watu mfululizo wiki nzima, Mpaka hapa vyombo vya usalama washaelewa kua zodiac si mtu wa 'Mchezo Mchezo' hivyo basi kesho yake wanachapisha barua zake katika ukurusa wa nne wa gazeti.
Juhudi zinafanyika wataalamu wanang'amua fumbo la zodiac baada ya wiki na kugundua alikua anadhamiria kutoa ujumbe kama ilivyoonekana pichani

[​IMG](solved zodiac cipher) photo credit; biography.com

TUKIO LINGINE LA ZODIAC 'LAKE BERRYESSA ATTACK'

Hili ziwa la kutengeneza(man made) lilipendwa sana na watu kwa ajili ya kwenda kupumzika au kuvua, tarehe 27 septemba 1969,Wanachuo wawili ambao walikua ni marafiki Bryan Hartnell na Cecilia Shepard walikua ziwani hapa kwa ajili ya mandhari(picnic), ndipo alipotokea mtu mmoja akiwa amevaa sweta linalofunika kichwa(hood) na miwani.

Mtu huyu alikuja akiwa kawashikilia bastola marafiki hawa na kudai kua anahitaji gari lao na pesa ili atoreke maana alikua amefanya mauaji. Baada ya kupata anachohitaji mtu huyu aliwafunga mikono marafiki hawa lakini kabla ya kuondoka aliwachoma choma na kisu kirefu kisha akaondoka na gari lao.

Hili gari lilikuja kukutwa limetelekezwa mahali likiwa na ujumbe mlangoni uliosomeka sept 27 'S6:30/by knife'.... Kuonyesha ubabe wake tena, Zodiac aliwapigia simu polisi tena akitumia simu za vibandani na kuwaeleza juu ya tukio alilolifanya na kuwaelekeza mahali,Huku akijigamba kwa sauti 'I did it,I did it'(nimefanya,nimefanya) Lakini kwa bahati nzuri marafiki wale wawili waliokolewa na wasamaria wema na kupelekwa hospitali ambako bryan alipona na cecilia kufariki... Bryan ndo alielezea hiki kisa na kusaidia katika kuchora mchoro unaotoa picha ya huyu muuaji. Mpaka hapo juhudi za kumpata zodiac zimegonga mwamba


ZODIAC ANASHAMBULIA TENA 'PRESIDIO HEIGHT ATTACK'
Baada ya wiki mbili, mtu mmoja anachukua teksi na kuomba kupelekwa mahali panapoitwa "presidio heights', lakini wakiwa njiani mtu huyu anatoa risasi na kumuua dreva teksi huyu, tukio hili linashuhudiwa na watoto watatu ambao walikua mbali kidogo na lile eneo, wanapiga simu polisi na polisi wa karibu anafatilia mahali pale..

Taarifa kutoka kwa hawa watoto ni kwamba japokua hawajamuona vizuri muuaji ila wanahisi ni kama mtu mweusi, polisi aliyekua anafatalia hili tukio anakuja badae kudai kua alipishana na mwanamme mzungu ambaye alionekana kama ana haraka na wasiwasi mwingi karibu na eneo la tukio lakini hakumtilia maanani maana alipewa maelekezo ya kumtafuta mtuhumiwa mweusi. Mchanganyo huo wa rangi mpaka leo umeshindwa kuelezewa

Siku tatu baada ya tukio, 'Mbabe' Zodiac anawatumia polisi barua yenye maelezo kua yeye ndie aliyemuua yule dreva teksi, ili kudhibitisha hili akawatumia na kipisi kidogo cha nguo(swath) ambacho alikikata kutoka kwenye shati alilovaa yule dreva. Watoto wale watatu wanasaidiana na watalaamu kuchora picha ya muonekano wa zodiac(composite sketch)

ZODIAC ANAWATEKA MAMA MJAMZITO NA MTOTO WAKE MCHANGA
Mwezi machi 22 1970, mwanamke mjamzito kathleen jones akiwa na mwanae mchanga wa miezi kumi yupo ndani ya gari akiwa anaenda kumtembelea mama yake, ghafla kwa nyuma linatokea gari lingine likiwapigia honi na kuwawashia taa.. Mwanamke huyu anaamua kupaki gari pembeni. Anakuja mwanaume kutoka kwenye lile gari lingine na kumwambia huyu mwanamke kua tairi lake na mbele linacheza cheza kama limelegea.

Mwanaume huyu anajitolea kumpa msaada Kathleen wa kukaza nati za tairi lake, Anachukua vifaa na kuanza kukaza nati kisha anamwambia " you are good to go"(unaweza kwenda).... Kathleen anashukuru kwa usamaria na kurudi kwenye gari, lakini anashangaa pale anapotaka kuondoka lile tairi linakua limelegea zaidi kiasi cha kutaka kuchomoka kabisaa..
Kuona vile yule mwanamme anaamua kuwapa lifti mpaka kituo cha karibu cha mafuta ili waweze kupata msaada zaidi, lakini cha ajabu mwanamme huyu akawa anaendesha gari kwa zaidi ya lisaa huku akiwa amevipita vituo vingi vya mafuta. Kathleen ameshapata wasiwasi na kila akiuliza akawa anapewa majibu yasioridhisha... Wakafika sehemu yule mwanamme akasimamisha gari kisha Kathleen akachoropoka kutoka kwenye gari na kichanga chake na kukimbia, yule mwanamme akawatafuta bila mafanikio maana ilikua usiku akaamua kuondoka zake.

Kathleen alivyotoa taarifa polisi wakamuonesha michoro ya mfanano wa zodiac(composite sketches) na akadhibitisha kua yule mwanamme alikua Zodiac, Japo wanausalama wengi walipata na wasiwasi na maelezo ya Kathleen maana huu mfumo sio wa Zodiac, yeye anafahamika kama mtu hatari sana na walishangaa jinsi huyu Kathleen alivyotoka mikononi mwake kirahisi, hii ilipelekea wao kuhisi huenda Zodiac nae ana ka 'Hofu' ka MUNGU hivyo aliamua tu kuwaacha


ZODIAC ANAZIDI KUWASILIANA NA POLISI NA VYOMBO VYA HABARI

Zodiac alikua ashakua 'supastaa' na alikua anapenda sana kujulikana(attention seeker)... Aliwaandikia barua polisi kuwaeleza alivyohusika na kutekwa kwa Kathleen, Pia aliandika barua nyingine yenye ujumbe uliosomeka 'My name is ....... ikifuatiwa na fumbo lenye alama 13.. Ambalo wataalamu walishindwa kuling'amua. Vyombo vya usalama wakajiuliza kwanini Zodiac anapendelea kutuma ujumbe kwa mafumbo? hali hii ilipelekea kuwapa mwanga kua wanamtafuta mtu ambaye ni mtaalamu wa hisabati...

Katika barua nyingine Zodiac aliwapa pole polisi maana kulikua na tukio la kulipulia kwa kituo cha polisi siku si nyingi lakini alienda mbele zaidi na kusema " it's more glory to kill a cop than a sic, because cops can shoot back" (ni furaha zaidi kuua polisi kuliko mtu wa kawaida maana polisi wanaweza kujihami)

Zodaic anaendelea kuwaandikia 'Marafiki' zake polisi pamoja na vyombo vya habari barua huku mara kwa mara akiambatanisha na kadi za salamu(greeting cards).. katika barua moja anawaamuru polisi wahamasishe watu mtaani kuvaa nguo zenye vifungo vyenye alama ya zodiac, pamoja na vitu mbalimbali venye alama yake( ikumbukwe hapa watu walishaanza kutengeneza vitu venye alama ya Zodiac), anawaambia washipofanya hivyo atalipua gari lenye watoto wa shule na kuwaua wote, kwa dharau na kujiamini kabisa anaandika" it's easy, you just shoot the fucking tires and watch the kids fly out" (ni rahisi sana,unapiga risasi matairi na kuangalia watoto wanavyodondoka)

Pia anaelezea jinsi anavyopanga kuwatesa watumwa wake(slaves) wakifika paradiso. (kama inavyoonesha pale juu kwenye picha,Zodiac anaamini watu wote aliowaua watakuja kuwa mateka wake paradiso)... Anamwaandikia barua pia Paul Avery ambaye alikua mwanahabari aliyekua anaifatilia kesi ya Zodiac kwa karibu ujumbe akimwambia "pick a boo, you are doomed"(umekwisha)

Zodiac pia anaandika barua kuonyesha kusikitishwa na uwezo mdogo(incompetence) ya vyombo vya usalama huku akibainisha kua inawezekanaje wamegundukua matukio yake machache tu wakati yeye amefanya mengi sana.. hapa 'mbabe' Zodiac aliwaandikia "Why are you only finding the easy ones?? there are hell lot more down there" (kwanini mnagundua matukio marahisi tu? kuna mengi sana mbona)...

Kudhibitisha hili anawaeleza kuhusu matukio mbali mbali ambapo kuna watu walikua wanaripotiwa kupotea kua yeye ndiye aliyewaua, pia anaelezea kuhusika na vifo vingine ambavyo polisi walikua hawamuhusishi navyo yeye.


BARUA YA MWISHO YA ZODIAC
Baada ya kua kimya kwa muda mrefu Zodiac anaandika barua yake ya mwisho huku sehemu kubwa akiisifia filamu ya kutisha ya 'THE EXORCIST' iliyotoka mwaka 1973. Hapa anawaandikia kwamba "its the best sateral comidy i have ever seen". anamalizia barua yake kwa kujigamba na namba ya watu aliowaua akisema " ME=37 POLICE=0

WATUHUMIWA KESI YA ZODIAC

Watuhumiwa walikua wengi ila aliyewavutia sana vyombo vya usalama alikua Leign Allen, hawakua na ushahidi mzuri sana (solid evidence) wa kuweza kubaini kama ndiye Zodiac killer zaidi ya hisia na ushahidi wa mazingira(circumstantial evidence).. Walikuja kumuachia Allen baada ya kupima vinasibu(dna) yake wakilinganisha na sampuli ya vinasibu walivyopata kwenye mate ya kufungia bahasha katika mfululizo wa barua za Zodiac na kukuta havifanani

HITIMISHO
Mpaka leo 'Bingwa' huyu Zodiac hajulikani ni nani, Mwaka 2004 waliamua kufunga hii kesi, 2007 wakaifungua tena lakini hakuna chochote kilichoendelea ikabidi waifunge tena. Kuna vitabu vingi sana vimeandikwa kwa kutumia matukio haya na filamu mbalimbali,mfano ni filamu ya ZODIAC yenyewe. Wanasema huenda Zodiac bado yupo hai.


[​IMG]
(zodiac composite sketch) photo credit: biography.com

Mwanadamu wa Mwisho Kutembea Mwezini Gene Cernan Afariki Dunia.

$
0
0

MAREKANI: Mwanadamu wa mwisho kutembea mwezini Gene Cernan afariki dunia. Alirejea kutoka mwezini na ujumbe wa amani na tumaini kwa watu wote ulimwenguni.
Bwana Gene Cernan ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 82, siku zote aliwasisitiza vijana kufika mwezini ili wasimuache yeye pekee kubakia na sifa hiyo.

Tembelea Tovuti Pendwa ya ASILI ZETU inayohusiana na Masuala ya Tiba Asilia Kama Kusafisha Nyota na Kumvuta Mpenzi

$
0
0
Tembelea  tovuti  pendwa  ya ASILI ZETUinayohusiana na masuala ya tiba asilia, kusomewa dua na visomo, kusafisha nyota,  kumvuta mume au mpenzi aliyekuacha, tiba ya magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana,  mvuto wa biashara.

Pia tunatoa dawa za uzazi kwa wale kina mama wenye matatizo ya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote, kupandishwa cheo kazini, mali isiyohuzika kama vile kiwanja, shamba, nyumba, gari n,k.

Bonyeza Hapa: https://asilizetu.wordpress.com
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images