Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Pata Hii:Mchungaji wa Kilokole Amnajisi Mtoto na Kukimbia Kijiji,Alimchukua Kwao Kwa Ahadi ya Kumsomesha..!!

0
0
 
MKUU wa Wilaya, Emmanuel Kipole, ameagiza kukamatwa kwa Mtendaji wa Kijiji cha Luchili, Mathias Njolilo na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Msazibwa Daud kwa tuhuma za kumtorosha Mchungaji wa Kanisa la Agape anayetuhumiwa kunajisi mtoto wa miaka 13 (jina linahifadhiwa).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jana, Kipole alisema, haiwezekani Serikali ikemee vitendo vya ukatili kama hivyo huku baadhi ya watumishi wakipokea fedha ili kuficha watuhumiwa.

"Nafuatilia tukio hilo, lakini kama Mtendaji na Mwenyekiti wamemwacha mtuhumiwa,  naagiza vyombo vya usalama viwakamate na wamtafute aliko mtuhumiwa na watoe maelezo kwa nini amemwacha huku akituhumiwa badala ya kumpeleka kwenye vyombo husika," alisema Mkuu wa Wilaya.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya ilikuja baada ya mwandishi wa habari hizi kufuatilia tukio hilo kijijini na kuzungumza na wananchi, huku Mchungaji naye akidaiwa kutoroka kijijini hapo, baada ya kuachwa na viongozi wa kijiji wanaodaiwa kupokea fedha kutoka kwake.

Ilivyokuwa

Mchungaji huyo baada ya kumnajisi moto huyo, alimsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.  

Tukio la kunajisiwa mtoto huyo lilitokea Januari 10 nyumbani kwa Mchungaji huyo lakini licha ya kuomba msaada serikalini ili akamatwe afikishwe kwenye vyombo vya sharia, hakuna hatua zilizochukuliwa.

Licha ya tukio hilo kufikishwa kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji na mtuhumiwa kukamatwa na viongozi hao, aliachwa katika mazingira ya kutatanisha yaliyojenga shaka kwa wananchi, na hajulikani aliko.

Taarifa kutoka kijijini hapo zilieleza kuwa baada ya kufanyiwa ukatili huo motto huyo alitoa taarifa ofisi ya Mtendaji wa Kijiji na mtuhumiwa akakamatwa lakini aliachwa katika mazingira ya kutatanisha.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Asha Hamud anayeishi jirani na Mchungaji huyo alidai kuwa siku ya tukio mtoto huyo alionekana asubuhi akilia huku akionekana kuvimba mashavu na kutembea kwa shida.

"Nilipomuuliza alisema amefanywa vibaya na Mchungaji usiku kwa kumwingilia  mara tatu na kumsababishia maumivu makali … nilimchukua na kumpeleka ofisi ya Mtendaji wa Kijiji kuomba msaada ili mtuhumiwa akamatwe," alidai mwananchi huyo na kuongeza:

"Baada ya muda Mtendaji wa Kijiji alimtuma Mwenyekiti wa kitongoji cha Luchili Center, Msazibwa Daud ili akamkamate, alimkamata na kumfikisha ofisini hapo na kumfungia kwenye chumba cha mahabusu cha ofisi yake na kusubiri taratibu za kisheria".

Wakiwa wanasubiri taratibu hizo, baada ya nusu saa zilichangwa fedha za nauli ili kumsafirisha mtoto huyo nyumbani kwao mkoani Kagera, ili kupoteza ushahidi wa tukio na kwa taarifa zilizopatikana, aliambiwa anapelekwa hospitalini kumbe alikuwa anasafirishwa.

Mtoto huyo alichukuliwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Daudi hadi Sengerema Mjini na kupandishwa basi la Bukoba, huku akiambiwa anapelekwa hospitalini kwa uchunguzi wa afya yake.

Mtoto asimulia 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi akiwa mkoani Kagera mtoto huyo alidai kuwa Mchungaji huyo alimwomba kwa wazazi wake kijijini Izibwa, Bukoba Vijijini kwa lengo la kumsomesha na siku ya nne alipoulizia kuhusu shule Mchungaji alimjibu:  "Shule utakwenda".

Ikiwa ni siku ya nne akiwa nyumbani kwa Mchungaji huyo, alimlazimisha kufanya naye mapenzi huku akimshambulia kwa kipigo.

Dada aeleza

Dada wa mtoto huyo, Devotha Costantine ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo, alidai kuwa mdogo wake alifika kwake Kashai mjini Bukoba akiwa na maumivu makali akilalamika kunajisiwa.

"Nilimwuliza kulikoni akasema amenajisiwa na Mchungaji; wakati anamchukua alisema anakwenda kumsomesha, lakini kilichotokea ni kunajisiwa, kitendo ambacho ni cha kikatili, tunaiomba Serikali kumchukulia hatua Mchungaji huyo," alisema Devotha huku akibubujikwa na machozi.

Alisema siku mdogo wake anafika, alishangaa kumwona kwani hakumtarajia.

Kuhusu hali ya mdogo wake, alisema walimpeleka kwenye matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Aidha, mmoja wa wananchi wa Luchili ambaye hakutaka jina lake litajwe gezetini alisema siku moja baada ya tukio hilo, Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji hicho kupitia kwa Mtendaji wake, Mathias Njulilo walituhumiwa kumwacha Mchungaji huyo kwa kupewa Sh 13,000.

Baada ya kumwacha baadhi ya wachungaji wa madhehebu ya kikristo kijijini hapo,  walimchangia nauli akatokomea pasipojulikana na huku wananchi wakitupia lawama uongozi wa kijiji kukumbatia uovu kwa kupewa fedha ili kuficha ukweli na kuomba Serikali iwachukulie hatua kali kisheria.

Mchungaji

Mchungaji anayetuhumiwa kumnajisi mtoto huyo alizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili akisema:

“Namwachia Mungu kwa kuwa ndiye muweza wa yote na yote yanapatika kwa wanadamu, siwezi kusemea lolote juu ya suala hilo limetokea, hata mimi sikutegema naomba msamaha msinitangaze manake ni fedheha kwangu na wachungaji wenzangu aombaye msamaha kama ametenda kosa husamehewa," alisema Mchungaji huyo.

Mtendaji

Mtendaji wa Kijiji, Njolilo alipoulizwa kuhusu kumkamata mtuhumiwa na kumwacha, hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo na kusema hajui lolote licha ya Mwenyekiti wa Kjiji Ibrahimu Mbata kukiri kuwa alipewa Sh 20,000 kama Mwenyekiti wa Kijiji wakiwa ofisini lakini akahoji alipewa za nini na Mtendaji.

Mkuu wa Mkoa Awashusha Vyeo Walimu Wakuu 63 Kisa Mkoa Kuwa wa Mwisho Kitaifa Matokeo ya Form Two

0
0
 
SIKU mbili baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kutangaza matokeo ya kidato cha pili na shule tisa za mkoa wa Mtwara kushika mkia, Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendegu ameagiza mamlaka husika kuwavua vyeo walimu wakuu wa shule za msingi 63 kutokana na matokeo hayo.

Akizungumza  juzi Dendegu alisema alichukua aumuzi huo baada ya kujiridhisha kutokana na utafiti ambao waliufanya baada ya matokeo ya darasa la saba yaliyotoka mwaka jana.

Alisema taarifa zilizopo zinaonesha wanafunzi hao wa kidato cha pili waliofeli walifanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba hali ambayo inaibua maswali mengi katika kufeli huko.

Mkuu huyo alisema zipo changamoto mbalimbali ambazo zipo pia katika mikoa mingine ila Mtwara zimekuwa zikitumiwa kama sababu za changamoto za mitihani.

“Hawa wanafunzi walifaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2014/15 hivyo ni jambo la kushangaza kuona leo wanafeli, lazima kuna uzembe kwa wasimamizi wa watoto hao katika ngazi ya msingi,” alisema.

Alisema baada ya kuhoji baadhi ya walimu, walidiriki kusema kuwa walitoa majibu kwa wanafunzi hao hali ambayo ilichangia ufaulu, hivyo kusababisha kilichotokea.

Mkuu wa Mkoa alisema pamoja na walimu wakuu hao kushushwa vyeo, bado wanaendelea na mkakati wa kubaini udhaifu wa walimu wa sekondari na pia maofisa elimu ili wajiandae kuwajibika.

Dendegu alisema zipo changamoto kama ufundishaji wa mazoea, kufanya mambo kwa kufupisha, utoro kwa wanafunzi, wazazi kukosa mwamko na zingine nyingi.

Alisema pamoja na changamoto hizo, wana mikakati ya kutoa chakula na kutaka maofisa elimu kufuatilia shule mbalimbali lakini bado uzembe upo.

Unamkumbuka Yule Mtanzania Aliyewekwa Rehani Pakistani na Ndugu Yake,Mahakama Yaamua Haya Juu ya Kesi Hiyo.!!

0
0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Mfanyabiashara Juma Mwinyi maarufu ‘Neti’ aliyekuwa akidaiwa kumweka reheni mdogo wake nchini Pakistani kwa Sh bilioni 1.5.


Uamuzi huo wa mahakama umetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya kupitia hoja mbalimbali za kisheria na kujiridhisha kwamba mshtakiwa alikamatwa bila kufuata utaratibu.

Juma aliachiwa huru ikiwa ni miezi minne tangu kufikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza akishtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu kwani alishtakiwa Agosti 3, mwaka jana na aliachiwa huru Desemba 19, 2016.

Awali akisoma mashtaka Wakili wa Serikali Mkuu, Peter Njike alidai kati ya Desemba Mosi mwaka 2015 na Julai 15 mwaka 2016 jijini Dar es Salaam mshtakiwa alitenda kosa la kusafirisha binadamu kinyume cha sheria.

Njike alidai Juma alijifanya anakwenda kumpa mafunzo Adam Akida Mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Chemchem na Idrisa na badala yake alimsafirisha kwenda nchini Pakistan kwa ajili ya kumweka reheni.

Mshtakiwa alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Agosti mwaka jana na kufunguliwa kesi namba 276/2016 ambayo ilifutwa Novemba 11, mwaka jana kwa kutumia kifungu cha sheria namba 225 (5) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai na kukamatwa tena.

Juma alikuwa chini ya mikono ya Polisi tangu alipokamatwa tena Novemba 1, mwaka jana hadi Novemba 14 ambapo alishtakiwa tena kwa mashtaka haya hayo katika kesi namba 411 ya mwaka 2016.

Wakili wa mshtakiwa huyo Hudson Ndusyep, aliwasilisha hoja mahakamani hapo Desemba 7, mwaka jana akidai mteja wake ameshtakiwa kimakosa kwa sababu sheria za ukamataji zimekiukwa kwani alikamatwa bila kuwepo kwa hati ya kumkamata, hivyo aliomba kesi ifutwe mshtakiwa aachiwe huru.

Akijibu hoja hizo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hellen Mosha, alipinga hoja za utetezi na kuiomba mahakama isimwachie huru mshtakiwa na kwamba hoja ya hati ya kumkamata itaangaliwa wakati kesi inaendelea na hoja za utetezi haziko katika msingi wa kisheria.

Akisoma uamuzi Desemba 19 mwaka jana baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Mkeha alisema mshtakiwa alishtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu chini ya kifungu namba 4(1)(a)na (5) cha Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu namba 6 ya mwaka 2008.

Katika sheria hiyo kifungu namba 12 (1) kinasema wazi kwamba polisi hawezi kukamata mtu kwa kosa lolote lilipo chini ya sheria hiyo bila kuwa na kibali cha kukamata, hivyo mahakama ilikubaliana na hoja za utetezi kwamba utaratibu wa kumkamata mtuhumiwa ulikiukwa.

“Kwa mujibu wa sheria hakuna njia nyingine zaidi ya kuondoa mashtaka dhidi ya mshtakiwa na kumwachia huru mshtakiwa.

“Naushauri upande wa mashtaka wakati wowote wanapofuata taratibu za ukamataji wamfikishe mshtakiwa mahakamani,” alisema Hakimu Mkeha.

Mwanzo wa sakata la Juma

Hatua ya kukamatwa kwa Juma, ni matokeo ya gazeti hili kuripoti habari za Mtanzania kushikiliwa ughaibuni kutokana na biashara ya dawa za kulevya Julai 18, mwaka jana.

Habari hizo ziliripotiwa baada ya kipande cha video kusambaa katika mitandao ya kijamii Julai 17, mwaka jana ikimwonesha Adamu Akida amewekwa chini ya ulinzi na maharamia hao wenye silaha.

Gazeti la MTANZANIA lilifuatilia tukio hilo na kubaini kuwa Adamu alikuwa amewekwa rehani kwa gharama ya Sh bilioni 1.5 kwa kile kilichoelezwa kuwa ilikuwa ni utekelezaji wa mpango wa biashara ya ‘unga’.

Kutokana na hatua hiyo, timu ya Gazeti la  MTANZANIA iliamua kuchimbua suala hilo ili kujua ukweli wa namna kijana Adamu Akida, alivyokuwa kwenye mateso hayo.

Akisimulia tukio hilo kaka yake aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi) alisema, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu.

Alisema baada ya kueleza shida yake, Juma alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata fedha.

“Awali alikwenda kwa kaka yake mtoto wa mama yake mdogo anaitwa Juma na kuomba asaidiwe mtaji kwani amekuwa na maisha magumu sana. Baada ya hali hiyo aliambiwa kuna safari ya kwenda Pakistan ambayo waliondoka wakiwa wameandamana watu watatu pamoja na Juma na kijana mwengine ambaye jina lake limenitoka, ila anaishi Kinondoni.

“Walipofika kule, Juma akachukua mzigo akiwa na yule kijana wa Kinondoni, huku Adamu akiachwa Pakistan kwa maelezo kuwa baada ya siku tano atakuja nchini na mzigo mwingine. Muda wote hata tukihoji alipo Adamu tunaambiwa yupo anaendelea na kazi huko aliko na angerudi mwezi wa tisa au wa nane.

“Sasa hii video ndiyo imetupa picha halisi ya Adamu, maskini sijui kama tutampata akiwa hai. Hata hivyo kwa kipindi cha hivi karibuni, tulikuwa tukishangazwa na mwenendo wa Juma kwani amekuwa na fedha nyingi sana hadi kufikia kuwajengea nyumba dada zake pamoja na kuwanunulia magari,” alisema Abdallah huku akibubujikwa na machozi.

Mke alivyohama
 
Julai 19, mwaka jana chanzo cha uhakika kilisema kuwa mke wa Adamu ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Sunna, Magomeni, alihamia Kijitonyama.

Mke huyo wa Adamu, alihamishwa na shemeji yake, Juma ambaye ndiye aliyempangia nyumba nyingine Kijitonyama.

Kauli ya Mwenyekiti wa Mtaa

Akizungumza na Mtanzania, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Idrissa, Issa Mpangile, alisema askari kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi walifika katika ofisi yake na kumtaka waongozane kwenda katika nyumba ya baba mdogo wa Adamu.

Alisema walipofika nyumbani kwa Kessy Baharia Mtaa wa Idisa, ambaye ndiye baba mdogo wa Adamu, polisi walichukua maelezo yake na baadaye wakarudi katika ofisi ya Serikali ya Mtaa kuchukua maelezo yake.

Akizungumzia kuhusu kijana huyo, Mpangile alisema kuwa ni mzaliwa wa mtaa huo, lakini baadaye alihamia Mtaa wa Suna ambao ni jirani na Mtaa wa Idrissa, Kata ya Magomeni.

Alisema wakati kijana huyo anahama mtaa huo, alikuwa bado ni kinyozi na hakuwa na rekodi ya kusafiri kwenda nje ya nchi.

Alisema katika mazungumzo na Baharia, alimweleza kuwa amewasiliana na baba wa kijana huyo ambaye anaishi Bagamoyo mkoani Pwani.

Mpangile alisema kwa mujibu wa Baharia, baba wa kijana huyo anayejulikana kwa jina la Akida, amesikia habari za mtoto wake na kwamba atakwenda kuripoti kituo cha polisi.

Naye mama mdogo wa Adamu, aliyetambulika kwa jina la Khadija Katundu, alikiri maofisa wa polisi kumuhoji mume wake.

Alisema wameendelea kutoa ushirikiano kwa watu wanaofika nyumbani kwao kuhoji kuhusu suala hilo, na kwamba wanaamini ufumbuzi utapatikana.

Inasemekana kijana huyo aliwekwa rehani kwa ghamara ya Dola za Marekani 700, 000, sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.5 za Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kupanda Kizimbani Leo Kisa Mbunge Lema..!!!

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo anatarajiwa kuwa Shahidi wa kwanza katika kesi namba 351 ya mwaka jana inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mke wake Neema Lema.


Mbele ya Hakimu Nestory Barro wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, katika kesi hiyo ya uchochezi Lema na mkewe wanadaiwa kutoa kauli za kukashifu dhidi ya Gambo ambapo leo watuhumiwa hao wamesomewa hoja za awali za shitaka linalowabili.

Lema alikuwa akitetewa na Wakili John Mallya na Sheck Mfinanga,huku Serikali ikiwakilishwa na Wakili Alice Mtenga.

Alice alidai Lema na mkewe walituma ujumbe mfupi wa sms, “Karibu tutakudhibiti kama uarabuni wanavyodhibiti mashoga”, ujumbe unaodaiwa wa kumuudhi na kumuumiza Gambo.

Baada ya kusomewa hoja hizo watuhumiwa hao walikana kutenda kosa hilo ambapo pia Wakili Mallya alitoa notisi ya pingamizi la mdomo la kuipinga hati ya mashitaka iliyowashitaki watuhumiwa hao kutokana na kuwa na mapungufu ya kisheria na kuwa baadaye wataiomba Mahakama iitupilie mbali hati hiyo.

Hakimu Barro aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 3 mwaka huu,hoja za pingamizi hilo zitakapowasilishwa kwa njia ya mdomo.

Breaking News!!,Mbowe Atoa Tamko la Chama Baada ya Lowassa Kukamatwa na Polisi..!!!

0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa kitendo cha kumkata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa mkoani Geita kimedhihirisha polisi kutumika na Chama Cha Mapinduzi wakati wa chaguzi mbalimbali.


Mwenyekiti huyo alisema jeshi la polisi limekuwa likiwakamata na kuwaweka ndani viongozi mbalimbali wa chama chake kwa shinikizo la CCM na kuwataka Watanzania kulaani ukamataji huo kwa kuwa ni uhuni wa kisiasa.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo jijini hapa wakati akifungua Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Lowassa pamoja na baadhi ya wabunge.

Hatarii:Mganga wa Kienyeji Mbaroni Kwa Kumbaka Binti wa Miaka 19 ,Pichazz + 18..!!!

0
0

MGANGA wa kienyeji, mkazi wa Kijiji cha Kirungu mkoani Kigoma, Wilson Ndaliheremo (30), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumbaka binti (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 19.


Mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Wakili wa Serikali, Daisy Makakala, alidai kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo Desemba 29, mwaka jana maeneo ya Kawe Ukwamani.

Katika maelezo ya hati ya mashtaka, wakili huyo alidai mtuhumiwa alimwingilia msichana huyo bila ridhaa yake kisha kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Baada ya maelezo hayo, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo.

Wakili alidai upelelezi wa shauri hilo unaendelea hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hata hivyo, Hakimu Mushi alisema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo linadhaminika, hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili walioajiriwa serikalini au katika taasisi inayotambulika kisheria, pia watakaoweka saini ya maandishi ya Sh milioni tano kila mmoja.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Januari 30, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa alirejeshwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hii Yataka Moyo Aisee!! Jeneza Tupu Lazikwa kwa Maiti Kusahaulika Nyumbani..!!!

0
0
 
MAELFU ya wakazi jijini hapa(Mbeya), wamelazimika kusitisha shughuli zao kwa zaidi ya saa tano kushuhudia tukio la aina yake baada ya familia moja kuzika jeneza tupu na kulazimisha Jeshi la Polisi kulifukua.

Akithibitisha tukio hilo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Likula, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4.30 asubuhi Igoma ‘A’, kata ya Isanga.

Alisema Jeshi la Polisi la Mkoa lilipokea taarifa kuwa maiti aliyekuwa azikwe kwenye makaburi ya zamani ya Isanga alikutwa chumbani kwenye godoro na kulazimika kulifukua siku iliyofuata.

Alisema baada ya taarifa hiyo, polisi walifuatilia na kubaini kuwa juzi saa moja asubuhi Jailo Kyando (36) mwosha magari na mkewe Anna Elieza (32) wakazi wa Mtaa wa Igoma ‘A’ waliamka na kukuta mtoto wao wa kwanza Haruni Kyando (9) akiwa amefariki dunia.

Alisema taarifa za awali zilidai kuwa marehemu tangu utotoni alikuwa na matatizo ya   kifafa hali iliyosababisha aishi bila kusoma.

Kaimu Kamanda alisema kwa kifo hicho taratibu za mazishi zilifanyika na saa sita  mchana jeneza lililoletwa msibani liliwekwa sebuleni kando ya mwili wa marehemu uliokuwa umeviringishwa kwenye blanketi na kulazwa kwenye godoro.

Alisema baada ya maombi ya na Walokole wa Bonde la Baraka, vijana walibeba jeneza hadi makaburini na kuzikwa.

Aliongeza kuwa waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa Haruni chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali.

Kutokana na hali hiyo, taarifa zilifikishwa Polisi, askari walifika na kuuchukua mwili wa marehemu na kuhifadhi kwenye mochari ya hospitali ya rufaa ya Mbeya.

Polisi walikwenda makaburini kusimamia ufukuaji kaburi kuanzia saa 4.30 asubuhi hadi saa tano asubuhi.

Baada ya kufukua Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma ‘A’, Fred Mwaiswelo alifunua jeneza na kukuta likiwa tupu hali iliyoashiria kuwa mwili haukuwekwa.

Polisi walibeba jeneza hilo na kwenda nalo kwenye kituo kikuu cha Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kuwakabidhi ndugu kuendelea na taratibu za mazishi kwa mara nyingine.

Hata hivyo, baadhi ya ndugu na majirani wa mtaa huo walisema tukio hilo linaweza kuwa na sura mbili; hujuma za makusudi au bahati mbaya ya kusahau mwili.  

Walisema inaweza kuwa hujuma kutokana na kawaida ya misiba kabla ya mazishi lazima ndugu kutoa heshima za mwisho, lakini msiba huo haukuwa na utaratibu huo na baadhi ya ndugu hawakuhudhuria maziko.

Tetesi;Muda Wowote Kuanzia Sasa Huenda Baraza la Mawaziri Likabadilishwa,Wasomi Wafunguka Haya Makubwa..!!

0
0
KUNA kila dalili kwamba uamuzi wa Rais John Magufuli kuwateua Profesa Palamagamba Kabudi na Abdallah Bulembo kuwa wabunge, ni ishara ya kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri.

Hatua hiyo inatajwa kuchagizwa na taaluma na uzoefu wa wateule hao na utendaji wa mawaziri takribani mwaka mmoja tangu kuteuliwa kushika nyadhifa hizo.

Uchunguzi  na maoni ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini unabainisha, kwamba Rais Magufuli kimfumo na matukio yanayoendelea nchini, yakiwemo yanayozikumba wizara, huenda akafanya mabadiliko hayo ili kuendeleza kasi yake ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Uteuzi wa Kabudi ambaye ni Profesa wa Sheria wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Bulembo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, umefanya idadi ya wabunge walioteuliwa na Rais Magufuli kufikia wanane, huku watano wakiteuliwa kuwa mawaziri, mwingine Dk Tulia Ackson kuwa Naibu Spika wa Bunge.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema: “Siwezi kuwa mtabiri, lakini ukisoma alama za nyakati na uteuzi huu kufanyika sasa, inawezekana si wote, lakini nafikiri anaweza (Rais Magufuli) kufanya mabadiliko katika Baraza lake.

“Mfano Profesa Kabudi ni mzoefu, msomi na anaijua Tanzania. Ana uwezo mkubwa, wa kujieleza na kujenga hoja. Sidhani kama Rais atamwacha hivi hivi awe mbunge tu.”

Alisema Bulembo anaweza asiteuliwe kuwa waziri, lakini akatumika bungeni kuimarisha umoja wa wabunge wa CCM.

“Huenda Magufuli anataka umoja wa CCM usimamiwe vizuri. Binafsi naamini bado Lowassa (Edward) ana ushawishi miongoni mwa wabunge wa CCM wa sasa. Bila kutafuta mbinu za kuhakikisha mizizi yake inakatwa taratibu, italeta shida. Wanaangalia mwaka 2020 maana yeye (Lowassa) ameanza kampeni mapema,” alisema Dk Bana.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inampa Rais mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10 kutoka miongoni mwa wananchi ambao anaona wanaweza kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake kwenye baadhi ya maeneo kama vile afya, elimu, kilimo, nishati na sheria.

Ibara ya 66 (1) inasema, bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za wabunge, yaani (e) wabunge wasiozidi 10 walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67 (1) (b).

Walioteuliwa

Miongoni mwa wateule hao ni Naibu Spika, Dk Tulia. Novemba mwaka juzi Naibu Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani alichukua fomu za kuwania uspika kupitia CCM kabla ya kujitoa dakika za lala salama, na akateuliwa na Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Viti Maalumu.

Baada ya kujitoa, alijitosa kuwania unaibu spika ambapo wabunge 250 walimpigia kura ya ndiyo.

Wengine walioteuliwa kuwa wabunge na kupewa wizara ni, Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustino Mahiga, Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Dk Philip Mpango (Fedha) na Dk Abdallah Posi  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.

Rais Magufuli alipoteua Baraza la Mawaziri Desemba 10 mwaka juzi, walikuwamo Dk Posi, Balozi Mahiga na Profesa Mbarawa ambao waliteuliwa kwanza kuwa wabunge.

Wakati akitangaza Baraza hilo, alisema aliacha viporo wizara nne za Maliasili na Utalii, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Fedha na Mipango na Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, huku akiteua naibu mawaziri kuongoza wizara hizo.

Desemba 23 alimalizia kiporo hicho kwa kumteua Profesa Ndalichako na Dk Mpango kuwa mawaziri ikiwa ni baada ya kuwateua kuwa wabunge.

Akizungumzia uteuzi huo, mhadhiri mwingine wa UDSM, Richard Mbunda alitofautiana na Dk Bana na kusisitiza: “Kwa kuzingatia utendaji wa mawaziri wenyewe na hali ilivyo sasa, sidhani kama kuna sehemu (wizara) imelega. Unajua Magufuli wakati akiteua mawaziri alizingatia sana weledi.

“Ndiyo maana Dk Mwakyembe (Harrison) yuko Wizara ya Katiba na Sheria, hata Mahiga amebobea katika masuala ya uhusiano wa kimataifa na yuko Wizara ya Mambo ya Nje. Huyu Makamba (Januari-Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano), Shahada yake ya Uzamili amesomea masuala ya utatuzi wa migogoro.”

Alisisitiza kuwa iwapo wizara kadhaa zingekuwa zimetetereka, huenda uteuzi wa Profesa Kabudi ungeashiria kuwa anakwenda kuziba pengo katika maeneo hayo.

“Nadhani anajaribu kuongeza idadi ya wabunge bungeni maana nafasi 10 za uteuzi wa Rais huongeza nguvu ya CCM bungeni. Sioni kama kuna kitu chochote kimemsukuma kufanya uteuzi huu,” alisema Mbunda.

Rais Magufuli tangu alipotangaza kuunda wizara 18 zenye mawaziri 19 na manaibu 16, huku sita kati yao wakiwa wanawake, amefanya mabadiliko kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga na kumteua Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo kushika wadhifa huo.

Kupitia mabadiliko hayo, Rais alimteua Dk Charles Tizeba kuziba nafasi ya Mwigulu.

Katika mwaka mmoja wa utawala wake, Rais Magufuli alimtosa waziri mmoja, kuhamisha mmoja na kuteua mmoja wakati mtangulizi wake, Jakaya Kikwete alihamisha mawaziri 18.

Kikwete

Katika muhula wa pili wa utawala wake, Rais Kikwete aliteua wabunge 10, kati yao sita aliwapa wizara za kuongoza, utaratibu ambao Rais Magufuli aliutumia ili kupata mawaziri kulingana na mahitaji ya Serikali yake.

Walioteuliwa na Kikwete kuwa wabunge na kupewa wizara, ni Profesa Mbarawa, Shamsi Vuai Nahodha, Zakhia Meghji, Profesa Sospeter Muhongo, Janet Mbene, Saada Mkuya na Asha-Rose Migiro. Alikamuilisha orodha yake ya uteuzi wa wabunge 10 kwa kuwateua Dk Grace Puja na Innocent Sebba ambao hakuwapa uwaziri.

Kabudi

Profesa Kabudi ambaye alipata kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria UDSM, alihitimu Shahada ya Sheria UDSM akipata daraja la kwanza mwaka 1983 na Shahada ya Uzamili mwaka 1986 katika chuo hicho.

Alisoma Shahada ya Uzamivu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Freie kilichoko Berlin, Ujerumani mwaka 1995. Profesa huyo pia ni Msajili wa Kanisa la Anglikana Tanzania na pia alikuwa mjumbe wa Iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Bulembo

Bulembo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM tangu mwaka 2012, pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Mara (MRFA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka juzi, alikuwa Meneja wa Kampeni wa Mgombea Urais wa CCM.

Duh:Baada ya Madee Kutoa 'HELA' Nay wa Mitego Aamua Kumchana 'Live' Kuwa Wimbo Huo ni Mbaya,..!!

0
0

Wafalme wa Manzese, Madee na Nay wa Mitego, wameirejesha tena bifu yao.


 Imerudi upya baada ya Madee kuandika mstari kwenye wimbo wake mpya, Hela ambao umetafsiriwa kumwendea hasimu wake, Nay.

“Yule kijana wa home sio staa, anatukana hata waliomzaa, wivu tamaa na njaa ukiendekeza ujue kidole utakaa,” Madee amerap kwenye wimbo huo.

Baada ya muda mfupi tangu wimbo huo utoke, Nay aliandika kwenye Instagram, “Leo nimesikia Wimbo Mbayaaaaa kuliko nyimbo mbaya nilizowahi kusikia Mwaka huu.”

“Mtag uyo Msanii mwenye huo wimbo Kama ushausikia..?!”

Huyu Ndiye Mwanamuziki Ghali Zaidi Afrika Kwa Sasa....

0
0


Tekno alilipwa shilingi bilioni 8.8 kusaini na Sony Music

Ili kusaini mkataba wake na Sony Music, hitmaker huyo wa Pana, amelipwa dola milioni 4, ambazo ni takriban shilingi bilioni 8.8 za Tanzania.

Hicho ni kiasi kikubwa zaidi kuwahi kupewa msanii wa Afrika kwenye record label deal. Taarifa za Tekno kuchukua mkwanja huo, zimetolewa na promota wake, Paul O wa kampuni ya Upfront & Personal kama anavyosikika akieleza kwenye video hiyo.

Umaarufu wa Tekno uliongezeka maradufu mwaka jana kufuatia mafanikio ya wimbo wake #Pana.

‘Shishi Food’ ya Shilole Yatoa Deal Kwa Wasichana

0
0

Msanii wa muziki Shilole kupitia kampuni yake ya mapishi ‘Shishi Food’ ametoa deal kwa wasichana wenye uwezo wa kupika pamoja na kutoa huduma.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mtoto Mdogo’ yupo kwenye mpango wa kufungua mgahawa mkubwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Jumatano hii ametoa tangazo rasmi la kuhitaji wafanyakazi kwa ajili ya mgahawa huyo.

“Shishi Food delivery’ inatangaza nafasi ya kazi kwa wasichana tu. Kama unaujuzi wa chakula, na upishi pamoja na huduma kwa mteja.. tafadhari tuma picha pamoja na CV yako suzilitasamson@gmail.com,” aliandika muimbaji huyo Instagram.

Muimbaji huyo alikuwa na mgahawa Mwananyama Kinondoni lakini baadaye ukafungwa.

Rais Wa Zamani wa Marekani George H.W. Bush Akimbizwa Hospitali Baada ya Kuzidiwa Ghafla..!!!

0
0

Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush amekimbizwa katika hospitali ya Houston Methodist ya mjini Texas baada ya kuzidiwa ghafla.


Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mkuu wa wafanyikazi wa rais huyo wa 41 wa nchi hiyo, Jean Becker kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na kuna uwezekano mkubwa akaruhusiwa kutoka hospitalini siku chache zijazo.

Siku chache zilizopita mtoto wake George W. Bush ambaye na yeye aliwahi kuwa Rais Marekani alitoa ripoti kuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa Donald Trump huku akiongeza kuwa baba yake, George H.W., hatohudhuria kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.

Hatari Sana!! Simba Akamatwa Morogoro,Alikuwa Anakatisha Katika Mashamba ya Miwa..!!!

0
0


Timu ya  Mtibwa Sugar imeipunguza kasi Simba katika mbio za Ubingwa baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana 0-0 mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara uliochezwa kwenye dimba la uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kwa matokeo hayo Simba wamebaki katika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 45 nyuma ya mbili dhidi ya  wapinzani wao wakubwa Yanga wenye pointi 43 ambao jana walipata ushindi kwa taabu mkoani Ruvuma dhidi ya timu ya Majimaji.

Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Azam FC watashuka uwanjani kucheza na Mbeya City katika uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Habari Picha: Rais Magufuli Amwapisha Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma..!!

0
0
JAJI1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 
JAJI2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 
JAJI3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi  baada ya kumuapisha  Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
JAJI4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha   Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
JAJI5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan 
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju  wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
JAJI6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama  kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
JAJI7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama baada ya  kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
PICHA NA IKULU

Aibu Ilioje!!Hivi Ndivyo Jose Chameleone Alivyoweza Kumuibia Mtanzania Huyu Milioni 100 Mchana Kweupee..!!

0
0

DAR ES SALAAM: Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya wa Uganda, Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ amejipatia zaidi ya shilingi milioni 100, mali ya mzalishaji nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Paul Matthysse ‘P Funk’,


Chameleone anadaiwa kuuza mdundo (beat) mali ya P Funk bila kumpa hata ‘thumni’ na yeye kutia kibindoni zaidi ya dola 50,000 za Kimarekani, (zaidi ya shilingi milioni 100) baada ya kulipwa na kampuni inayojishughulisha na masuala ya filamu, Walt Disney ili kuruhusu mdundo unaosikika katika kibao cha Profesa Jay cha Nikusaidieje, mali ya P Funk, utumike kwenye sinema ya Queen of Katwe iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana bila ridhaa yake.

Akizungumzia sakata hilo, P Funk alisema, Chameleone si mtu mzuri kwani alianza kumuingiza mjini tangu mwaka 2006 alipoichukua beat  ya Nikusaidieje na kuiingizia mashairi ya wimbo wake na kuuita Bomboclat.

“Unajua zamani tulikuwa tunatoa wimbo katika mfumo wa CD, tunapeleka redioni. Kwenye hiyo CD tulikuwa tunaweka beat tupu, sauti pekee (akapela) na wimbo wenyewe uliokamilika.

“Sasa jamaa (Chameleone) akaiba ile beat, akaingiza mashairi ya Bomboclat bila hata kuniambia chochote. Nikamueleza, akakubali kunilipa dola 2000. Nikamkubalia lakini akaingia mitini. Kama hiyo haitoshi, wimbo huohuo ambao beat yake ameniibia, akaenda kuuza tena Walt Disney, napo nilimcheki akaanza kuleta longolongo zilezile za mwanzoni.

“Akaanza ooh sijui nimefanya ili tuzidi kujitangaza mara ooh sijui wamenipa hela kidogo kama dola 2000, nikaona huyu anataka kuniletea ushenzi, lazima nimfunze adabu, nikazungumza na Cosota (Chama cha Hakimiliki Tanzania), wakawaandikia barua wenzao wa Uganda lakini nao hawakujibu chochote,” alisema P Funk.

Ili kumuonesha kwamba ‘amemaindi’, P Funk kupitia kwa wanasheria wake waliuandikia barua ya kiofisi (official letter) uongozi wa Disney ambao ulishtuka kusikia kwamba yeye ndiye mmiliki halali wa mdundo huo, hivyo ukamuomba suala hilo walimalize kirafiki.

“Wameniambia kwamba watafanya mahesabu yao na kuona natakiwa kulipwa kiasi gani na wao wenyewe watajua Chameleone watamshughulikia vipi,” alisema P Funk.

Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kupata simu ya nyota huyo mkongwe wa Uganda, lakini baada ya kujitambulisha na kumsomea tuhuma hizo, alisema yeye siyo Chameleone, bali ni mtu wa menejimenti yake ambaye alipotakiwa kutoa majibu ya kiofisi kuhusu suala hilo, alisema mwenye majibu ni msanii mwenyewe.

Mtu huyo wa menejimenti alitoa namba binafsi ya mwimbaji huyo wa kibao cha Valuvalu, lakini mara zote kutwa nzima jana, kila alipopigiwa, simu yake iliita bila kupokelewa hadi ilipokatika.
Licha ya kutumiwa pia ujumbe uliojaa tuhuma hizo, Chameleone hakujibu.

Kesi ya Lissu ya Kutumia Lugha ya Uchochezi Yapigwa tena Kalenda...!!!

0
0

Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, leo imeshindwa kusikilizwa kwa mara nyingine kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu na kupigwa kalenda hadi Februari 14, 2017.


Akisoma maelezo ya kesi hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa,  mwendesha mashtaka wa serikali aliiambia mahakama kwamba shahidi wa jamhuri aliyepaswa kuwasilisha ushahidi wake leo dhidi ya mbunge huyo ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema, amepata dharura ya kikazi.

Baada ya kuridhishwa na maelezo hayo, hakimu Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo ambayo inatarajiwa kusikilizwa tena, Februari 14.

Lissu anakabiliwa na mashtaka ya kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Juni 28, 2016.

Wakati huohuo, kesi nyingine inayomkabili Lissu, wahariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapishaji wa gazeti hilo, Ismail Mahbood ambayo leo ilifikishwa mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, imeahirishwa hadi kesho, Januari 19, 2017.

Kwa mujibu wa wakili wa serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba, aliomba kesi hiyo isikilizwe siku nyingine kutokana na  kutokamilika kwa maelezo ya awali ya kesi hiyo.

Ehe,Umemsikia Bahati Bukuku?Adai Hana Mpango wa Kuolewa Kwa Sababu Eti Ndoa Ilimshindaga Toka Kitambo

0
0

Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku amefunguka na kuweka wazi kuwa ndoa ilimshinda na kusema katika harakati za maisha yeye alipishana na aliyekuwa mume wake kufikia hatua ya kutengana na sasa kila mmoja kuishi kivyake. 


Bahati Bukuku akizungumza kwenye  cha Kikaangoni alisema wimbo wake wa 'Dunia haina huruma' si kama alimwimbia huyo aliyekuwa mume wake bali anakiri kuwa ni kisa cha kweli kilichotokea lakini hayo mambo aliyekuwa mumewe alikuwa hayafanyi.

"Aliyewahi kuwa mume wangu hakufanya hilo tukio ila kile kisa ni kweli kilitokea sehemu, lakini aliyekuwa mume wangu hakuwa na matatizo haya, ila tu katika harakati zetu za maisha kuna kupishana hivyo nilipishana naye tu. Siwezi kuongea uongo kwa mtu aliyekuwa mume wangu, hata nikiandika kitabu siwezi kuruka hili popote nikisimama nitasema niliolewa ndoa ikanishinda" alisema Bahati Bukuku 

Baadhi ya mashabiki walitaka kujua endapo alipata watoto katika ndoa hiyo, ambapo Bahati alikataa kuongea chochote kuhusu yeye kuwa na watot au la, na kusema kuwa hayuko tayari kuongea chochote huku akisema kuwa ana watoto wengi

"Hili swala la watoto sitaki kuzungumzia, mimi nina watoto wengi tu, kwahiyo kwenye ndoa yangu nisingependa kuongelea swala la watoto" alisema Bahati

Mbali na hilo Bahati Bukuku anasema watu ambao walimzushia kifo ni watu wake wa karibu ambao anafanya nao kazi na huenda walifanya hivyo ili kutaka kumpunguzia mashabiki wake.

"Walionizushia kifo ni watu ambao nafanya nao kazi, walidhani watanipunguzia mashabiki lakini pia ni kazi ya shetani hiyo, hivyo walijifanya ile taarifa imeanzia Congo lakini ni wa hapahapa ila mamlaka za mawasiliano bado zinaendelea kufuatilia ingawa mpaka sasa tayari wameshafahamika" alisema Bahati Bukuku 

Katika hatua nyingine, Bahati amesema hivi sasa anaandaa movie ambayo pia itakuwa na lengo la kuinjilisha, na kufikisha ujumbe wa Mungu kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye uimbaji.

Ubuyu wa Moto Moto!! Huyu Ndiye Waziri wa Magufuli Anayechepuka na Flora Mvungi,Walikutana Dodoma,Flora Akiri Kila Kitu Bila Kukataa

0
0

HUKU kukiwa na taarifa kwamba ndoa yake na msanii wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan Baba ‘H-Baba’ imeparaganyika, mrembo wa Bongo Movies, Flora Mvungi amedaiwa kunasa kwenye penzi la mmoja wa mawaziri wa serikali ya awamu ya tano.

 
Chanzo kilicho karibu na msanii huyo kimepenyeza habari kuwa, mrembo huyo kwa sasa yupo chini ya himaya ya waziri huyo (jina kapuni kwa kuwa hatujampata) ambapo safari ya uhusiano wao ilianzia mjini Dodoma.

“Nakumbuka ilikuwa ni mwaka jana, Flora alienda Dodoma na wasanii wenzake sasa alipofika mjengoni, waziri aliuona

mzigo hivyo akaomba nafasi na Flora bila hiyana akakubali.

“Mwanzoni kidogo alichomoachomoa lakini waziri alimuahidi maisha mazuri, na kwa kuwa tayari walikuwa kwenye gogoro na mtu wake(H-Baba), ilikuwa ni kama kumsukuma mlevi tu. Mtoto wa kike akaingia mzimamzima, yani sasa hivi Flora, kafa kaoza kwa mheshimiwa,” kilisema chanzo hicho makini.

Jitihada za kumpata waziri huyo ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani. Atakapopatikana, tutaripoti kwa upande wake ili kujua anazungumziaje madai hayo.

Kwa upande wake Flora, alipotafutwa na mwanahabari wetu alikiri kukutana na waziri huyo Dodoma lakini akaomba asizungumzie suala hilo kwani litamweka kwenye nafasi mbaya katika jamii.

“Naomba sana mliache hilo suala, najua aliyevujisha lakini nawaombeni sana mliache kabisa. Litanichafua tafadhalini sana,” alisema Flora.

Hatarii Sana;Tazama Video ya Waziri Nape Nnauye Akiwapaka Mashabiki wa Ali Kiba kwa Kumuonea Wivu Diamond

0
0

Waziri wa sanaa na michezo Nape Nnauye amesema anahisi mashabiki wa upande wa Ali Kiba ndio walikuwa wakiponda kuhusu Diamond kupewa bendera kwa sababu kumekuwa na uhasama na chuki kati ya pande hizo mbili, yeye binafsi amedai hana tatizo na msanii yoyote kati ya hao wawili na wamekuwa marafiki zake kabla hata hajawa waziri


Sikia Alichokisema Diamond Baada ya Picha za Zari Kuzagaa Akiwa analiwa Denda na Mwanaume Mwingine..!!!

0
0

Daimond Platnumz mapema hivi karibuni alivutiwa waya na kituo kimoja cha redio kutaka kujua maoni na mtazamo wake juu ya picha ambazo mama watto wake anaonekana akipigwa denda na mwanaume mwingine.

Alichokijibu Daimond ni hiki hapa ,Sikiliza hapo chini Livee


Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images