Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Kupoteza Pesa, ni Hatua Moja Wapo ya Kujifunza Namna ya Kuitunza na Kuizalisha

$
0
0

*Kupoteza pesa, ni hatua moja wapo ya kujifunza namna ya kuitunza na kuizalisha*_



Hii ni moja kati ya kanuni muhimu Sana'a katika kuelekea Uhuru wa kifedha,

Nayo inatafsri hii.

Katika mapato yako ya changanue kama ifuatavyo.

*Mfano Unalipwa Tshs 300,000, kwa mwezi au kama faida katika Biashara yako*

10% × 300,000=30,000 hii ni lazima uitoe kwa wasiojiweza au kama Fungu la kumi.

-- 10% × 300, 000= 30000/= hii unaweka kama akiba ya kuanzishia Biashara

10%×300,000= 30,000/= hii inatumika kwa ajili ya kuongeza maarifa yako kama kununua vitabu au kuhudhuria seminar nk.

Na kiasi kingine kinacho baki 70% ya mapato yako hii ndiyo unatakiwa kuingiza kwenye matumizi yako ya kawaida.

Na hii kanuni ndiyo inayotengeneza matajiri duniania kote kwa kujua na kutambua matumizi yao.

*Ukweli ni kwamba watu wengi hatujui bajeti zetu kamili ila tunaishi kulingana na tunavyo pata*

Ili uweze pia kufikia malengo yako makubwa kiuchumi kuwa tayari kuvunja kanuni hii ya kiuchumi
Inayoitwa

*PARKINSON LAW*

" *_A MANS EXPENSES WILL ALWAYS RISE TO MEET HIS INCOME AND MAKE HIM STAY THE SAME_*

( Matumizi ya mtu yana kwenda kulingana na kipato chake, jambo linalo mfanya aendelee kuwa vilevile)

Na ndiyo maana nataka nikwambie jambo hili ukitaka kufanikiwa hakikisha *UNAKUWA NA MATUMIZI MADOGO KULIKO KIPATO CHAKO* ili u-violate hii law ndipo utaona mpenyo wa kiuchumi.

Zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza
Ujifunze namna ya kuongeza vyanzo vya kipato chako.

Kama inacho kimoja hakikisha mwaka huu unatengeneza chanzo kingine cha mapato ili kupata mpenyo wa kifedha.


Nb.
Mafanikio live clinic ni trh 28/01/2017 Temeke Mwisho ukumbi kata 15.

-- MAFANIKIO AWARDS , endelea kupendekeza jina la mwandishi, msemaji na muhasishaji alie gusa maisha yako na kutoa mchango kwa jamii kuinuka kimafanikio.


🙏🙏🙏🙏🙏
*Facebook* Mafanikio Live Awards
Instagram: *Amka_Jitambue*
YouTube channel: *Amka Jitambae*
*EFM 93.7- Ushauri wa Bure*
Amkajitambue.blogspot.com
+255 653 206 053

Diva ndani ya Penzi Jipya na Mwanamuziki wa Bongo Flava.....

$
0
0


Diva ndani ya Penzi Jipya na mwanamuziki wa Bongo Flava anayejulikana kama Heri Muziki, penzi la wawili hao lilianza baada ya Diva kumwalika Mwanamuziki huyo katika kipindi cha Ala za roho kinachorushwa na Redio ya Clouds Fm.

Diva amepost ushahidi wa penzi lao kw kupost video wakidendeka na kuandika haya hapa chini
.
#Regrann from @divathebawse - @herimuziki is The Key to My Happiness .. i chose to be Happy 💞

Ushahidi..!! Rais Magufuli Hajawahi Kubadilika Kikauli,Kuanzia Alipokuwa Waziri Hadi Hivi Sasa,Soma Hapa Kauli zake Tata..!!!

$
0
0

RAIS Dk. John Magufuli ni yule yule. Ndivyo unavyoweza kumtafsiri kupitia misimamo na kauli zake mbalimbali ambazo amepata kuzitoa kabla na baada ya kupewa dhamana ya kuliongoza Taifa hili.

Kwa uhalisia baadhi ya kauli zake huzaa misimamo thabiti inayobebwa na sheria za nchi. Kwa maana nyingine kauli na misimamo yake husimamia kile anachokiamini kuwa ni ukweli na haki.

Ujumla wa misimamo na kauli zake zimekuwa zikigusa hisia miongoni mwa watu wengi na kusababisha mitazamo chanya na hasi kulingana na mtu mmoja mmoja anavyotafsiri.

Pamoja na hali hiyo, misimamo na kauli zake anazozitoa hajawahi kuyumba hata mara moja.

Kwa watu waliopata kufuatilia aina ya kauli za Rais Dk. Magufuli tangu anaingia kwenye ulingo wa siasa za nchi (enzi akiwa waziri), wanafahamu bayana kwamba siku zote amekuwa ni mtu mwenye kauli za misisitizo na msimamo thabiti.

Mtazamo huo unadhihirisha kwamba tangu awali Dk. Magufuli amejipambanua kuusemea ukweli pasipo kujalisha kama ukweli huo ni mtamu au mchungu kwa wengi.

Historia inaonyesha kwamba, wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na Miundombinu chini ya utawala wa awamu ya tatu, aligoma kupelekwa kwa boti mbili za mwendo kasi katika Ziwa Victoria kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa madai kwamba uzito wa boti hizo unaweza kuvunja madaraja ya barabara zitakazotumiwa kupitishwa kwa boti hizo.

Waziri mwenzake aliyekuwa anahusika na Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo, Profesa Mark Mwandosya, alijaribu kuingilia kati suala hilo kwa kutetea kwamba boti hizo ni muhimu kwa usafirishaji ndani ya Ziwa Victoria na  hazikuwa na uzito wa kuweza kuharibu madaraja kutokana na takwimu walizokuwa nazo.

Dk. Magufuli kwa upande wake alikataa utetezi huo wa waziri mwenzake kwa kusema: “Kama mnataka zikateni vipande vipande hizo boti mkaziunganishe Mwanza.”

Kwa msingi huo ililazimu boti hizo zipitishwe nchini Kenya kwa kupitia Bandari Kuu ya Mombasa na kubebwa kwa magari hadi Bandari ya Kisumu  ndiko zikaweza kuingizwa ndani ya Ziwa Victoria.
Pia, msimamo wake wa kuzuia mabasi marefu (Megabus) ya Zambia yaliyokuwa yanatoka Bandari ya Dar es Salaam nao uliwahi kutikisa diplomasia baina ya Tanzania na nchi hiyo.

Inaelezwa kwamba, Dk. Magufuli aliyazuia mabasi hayo Kibaha mkoani Pwani, akidai kwamba sheria za Tanzania haziruhusu mabasi marefu ya kiwango kile kupita katika barabara za hapa nchini.

Pamoja na kuwapo kwa maelezo kwamba mabasi yatakuwa ‘transit’ bila abiria na hayafikii urefu wa malori kama semitrailers ambazo zinaruhusiwa kupita katika barabara zetu, bado Dk. Magufuli alishikilia msimamo wake kwa kusema: “Wazambia watafute namna nyingine ya kuyapeleka mabasi yao Zambia, si katika barabara zetu hata kama hayana abiria yako transit tu.”

Sakata hilo lilikuwa kubwa sana hadi ikabidi ngazi za juu upande wa Zambia na Tanzania ziingilie kati ndipo mabasi yakaruhusiwa kwenda Zambia.

Tukio la kupandishwa kwa nauli ya Kivuko cha Kigamboni pia ni sehemu ya misimamo ya Dk. Magufuli, alisema: “Nauli mpya lazima zilipwe na mtu asiyetaka ni vyema akapiga mbizi kutoka Kigamboni hadi ng’ambo ya pili au apite Kongowe kuingia katikati ya jiji.” Kauli hiyo iliibua mjadala mpana na kugusa hisia za wengi.

Msimamo huo ambao aliutoa mwishoni mwa mwaka 2011, ulionekana dhahiri kutoungwa mkono na wananchi walio wengi lakini aliusimamia kwa nguvu zake zote.

Kwa mantiki hiyo, misimamo na kauli zake alizopata kuzitoa siku za nyuma wakati akitumikia nafasi za uwaziri ukalinganisha na misimamo na kauli zake za sasa akiwa kwenye nafasi ya ukuu wa nchi ni dhahiri unabaini kuwa Dk. Magufuli ni yule yule aliyezoeleka katika msisitizo na kauli zenye kutafsiriwa kwa utata na baadhi ya watu.

Duru zaidi za mambo zinatanabaisha kwamba, kinachoonekana kuisisimua zaidi jamii katika mtazamo wa hofu juu ya kauli za Dk. Magufuli kwa sasa ni nafasi aliyonayo kwamba anatoa kauli au msimamo kama Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa msisitizo wa kauli au msimamo wake unamaanisha kwamba, ni amri na lazima ifuatwe kwa sababu chini ya mamlaka yake kuna vyombo vinavyolinda utekelezaji wa amri yake.

Mfano mapema mwezi huu wakati alipotembelea wakazi zaidi ya 200 wa Mkoa wa Kagera waliokumbwa na tetemeko la ardhi Septemba mwaka jana, aliwaambia bayana kwamba kila mtu atabeba msalaba wake.

Katika maelezo yake alisema kwa uwazi kuwa Serikali haitamjengea nyumba mtu yeyote aliyeathirika na tetemeko hilo kwa sababu si jukumu lake.

Akaongeza kuwa watu wote ambao nyumba zao ziliharibika wanatakiwa kujenga wenyewe kwa sababu hakuna sehemu yoyote duniani ambako Serikali inabeba jukumu la kuwajengea nyumba waathirika wa maafa kama hayo kwa maana kwamba maafa hayo ni ya asili.

“Kuna nchi kama Japan na Italia zimekuwa zikikumbwa na matetemeko mengi, haijawahi kutokea Serikali yao ikawajengea nyumba upya isipokuwa inarejesha miundombinu ya taasisi za umma kama vituo vya afya, shule na barabara.

“Mwaka jana (mwaka juzi) nilipokuwa naomba kura kwenu, sikuomba tetemeko la ardhi litokee hapa, hili ni jambo  ambalo liko nje ya uwezo wangu, tunaomba kila mmoja aweze kutumia msaada uliotolewa ili kurejesha miundombinu ya makazi yenu…Wapo wanasiasa ambao watainuka  na kuanza kuwadanganya eti Serikali itawajengea nyumba, hilo halipo kama wanaona wanajiweza wawejengee wenyewe,” alisema.

Akaeleza kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wananchi wa Kagera kudai tetemeko limesababisha njaa, alihoji kama mazao yao yakiwamo migomba ilipandwa kwenye nyumba.

Baada ya hapo, akiwa katika eneo la Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza, nako alisema: “Ninafahamu wapo wanasiasa wachache ambao wanafikiri mzee bure, kila kitu kikitokea Serikali ifanye, Serikali ninayoiongoza mimi haitatoa kitu, mlinichagua niwaeleze ukweli na mimi nawaeleza ukweli.

“Sasa hivi wakati wa kulima mahindi umebadilika, tusijilazimishe kulima mahindi ambayo yanahitaji mvua nyingi, mvua zinaponyesha tulime na asiyefanya kazi na asile, msije kamwe mkadanganywa na mtu yeyote kwamba patakuwa na chakula cha Serikali, nataka niwaambie hakuna shamba la Serikali.

“Nani anaweza akanionyesha shamba la Serikali, hakuna shamba la Serikali, mlinichagua niwaambie ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli ni lazima tufanye kazi tujipange.”

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, wakati akifungua mkutano wa mashauriano wa Bodi ya Makandarasi, Mei mwaka jana, Rais Dk. John Magufuli, aliwahi kutoa kauli ambazo pia ziliwashtua watu wengi na kuibua mjadala mkubwa.

Kauli mojawapo ni kwamba kiti chake cha urais hajapewa na mtu yeyote bali kimetoka kwa Mungu, hivyo yupo tayari kutoa sadaka mwili wake kwa ajili ya Watanzania wengi ambao ni masikini.

Katika kuweka kumbukumbu sawa, Rais         aliitoa kauli hiyo mwezi mmoja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kukutana na wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam.

Tofauti na kauli hiyo, Rais Magufuli alikwenda mbali na kuwaambia wafanyabiashara hao kama miongoni mwao yupo aliyemchangia fedha wakati wa kampeni ajitokeze na aliwasisitiza walipe kodi.

Pia, Rais amewahi kutoa kauli nzito kwamba, ni mara kumi akachunge ndege kuliko awe rais halafu anavumilia uozo unaofanyika.

Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ni mmoja wa watu ambao wameguswa na kuipambanua misimamo pamoja na kauli zinazotolewa na Rais Dk. Magufuli.

Licha ya maoni yake mengi kuhusu Rais, hivi karibuni aliandika ujumbe kwenye akaunti ya twitter ya Chadema na kusema: “Rais sio Chief Commander tu, ni Chief Comforter, Rais anatakiwa aongee vizuri ni mfariji mkuu tunapokuwa kwenye majanga”.

Tafsiri ya ujumbe huo wa Lissu inawezekana alilenga kumshauri Rais atoe kauli za matumaini na kuwafariji wenye matatizo kwamba kama kuwaambia ukweli basi usiwe ukweli mchungu.

Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu, amewahi kukaririwa mwaka jana na gazeti hili akizungumzia baadhi ya kauli za rais kuwa zinaibua tafsiri ya kutia wasiwasi kwa wananchi na kuwajengea taswira hasi wale wanaomlinda.

Muktadha huo wa mtazamo wa Profesa Baregu ambao ulionyesha ugeni wake juu ya kauli za Dk. Magufuli kabla hajawa rais, ulijikita zaidi kuziangalia kauli chache zenye mrengo wa kutafuta huruma ya wananchi ili apate wigo wa kuwabana baadhi ya Watanzania ambao anahisi hawakubaliani naye.

“Anatakiwa ajue kuwa yeye ndiye Commander in Chief (Amiri Jeshi Mkuu), ana vyombo vyote, hivyo kauli zake zinaweza kuweka msukumo wa kuumiza watu wengi kwa kuwahisi tu,” alisema Profesa Baregu.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, naye amewahi kuchambua kauli za Rais Dk. Magufuli kuwa zinaonyesha udhati  wa kupambana na vitendo vya rushwa.

Profesa Bana alisema kwa nafasi aliyonayo Rais kama mkuu wa nchi, anatoa kauli hizo kwa dhamira ya dhati kuwaambia wananchi kwamba hawezi kurudi nyuma katika vita.

Alisema Rais anatumia kauli za aina hiyo ili kufikisha ujumbe kwa wale wanaosema jitihada zake anazozifanya katika utawala wake ni nguvu ya soda.

“Anajua hatari zilizopo ndio maana anasema yuko tayari kujitoa mhanga, si mara ya kwanza tunaona viongozi wa aina yake ambao wamejitoa muhanga kutafuta haki ya wengi wanahujumiwa, lakini pia najua ajenda hii itamvusha 2020 na hilo sitoona ajabu kama ataendelea na mapambano hayo maana najua Watanzania watamuunga mkono,” alisema Profesa Bana.

Nyumba ya Mbunge wa CCM Yabambwa Kwa Wizi wa Umeme..!!!

$
0
0

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limebaini wizi wa umeme katika nyumba ya aliyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasnain Murji.

Mhandisi wa Tanesco Mkoa wa Mtwara, Fabiani Ruhumbika, alisema mita ya nyumba ya Murji ilibainika kuchezewa baada ya kuona umeme unaotoka kwenda kwa mteja ni kidogo.

Alisema matumizi ya mteja yanaonekana kuwa ni makubwa kuliko kiasi kinachotumiwa hali iliyowatia shaka kwamba kutakuwa na kuchezewa kwa mita.

Ruhumbika alisema kitendo cha mteja kupindisha mita kutoka kushoto kwenda kulia inaonyesha wazi kuwa ilipoteza kumbukumbu katika usomaji wake.

Mwakilishi wa mbunge huyo wa zamani, Mohamed Haji, alisema kitendo cha kubaini wizi huo hakijui kwa sababu yeye hana ufahamu wa masuala ya umeme.

Akizungumza mjini hapa jana, Mwenyekiti wa Ukaguzi wa Miundombinu ya Umeme kutoka Makao Makuu ya Tanesco, John Manyama, alisema wizi huo umekuwa ukilirudi
sha nyuma shirika hilo na kufifisha mipango yake ya kujiendesha.

Alisema ukaguzi huo ulibaini kuwapo na uchezewaji mita katika nyumba hiyo, huku kukiwa na vifaa vingi vinavyotumia umeme.

Manyama alisema wataalamu wa ukaguzi waligundua wizi wa umeme huo kutokana na kutumia vifaa vya kisasa vya kupimia bila kumwonea mtumiaji wa huduma hiyo.

Alisema mtumiaji anayekamatwa huanza kwa kukatiwa umeme katika mtandao wa Tanesco kisha wanapiga hesabu ili kujua wamepoteza kiasi gani cha fedha na kumtaka kulipa.

“Tumebaini kuwa watu wengi wanatumia umeme bila kulipa (wezi wa umeme) hatua inayosababisha shirika kuchukua hatua kwa kuwakamata na kuwapeleka katika vyombo vya sheria ili kuruhusu liweze kukusanya mapato halisi na kuwa katika hali nzuri ya utoaji wa huduma.

Umeshaisoma Hii..!!! Hawa Ndiyo Watoto wa Mastaa Bongo Wanaotikisa Mitandao ya Kijamii,Tueleze Wewe Unamkubali Tupi?

$
0
0

HAPO awali ushindani kwa mastaa ulikuwa ni ufahari katika maisha kama vile kushindana kuvaa, pesa, majumba ya thamani na magari. Hali imebadilika hivi sasa, mastaa wanashindana watoto, kila mmoja anataka mwanaye awe juu kumzidi mwingine.screenshot_2017-01-22-11-38-09-1
Tukianza na mtoto wa Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’,  Princess Tiffa amekuwa gumzo kila kukicha kwa mtoto mdogo kuwa na jina kubwa kuwashinda watoto wengine kutokana na ustaa wa wazazi wake.screenshot_2017-01-21-21-34-22-1
Mtoto wa Hemed Suleiman (PHD)
Hali hiyo imekuwa pia kwa mastaa wengine ambao nao wanawaandaa watoto wao kuwa mastaa. Mtoto wa staa wa filamu Bongo, Hemed Suleiman, anaonekana kuwa gumzo kwa kusifiwa na mashabiki wa Hemed (PHD) kuwa mtoto huyo ni mzuri kuwashinda watoto wengine kwa muonekano.screenshot_2017-01-22-11-39-56-1
Dina Marious na mwanaye.
Aidha Babu Tale ameonekana mara nyingi katika mitandao ya kijamii akiweka alama za mitihani ya mwanaye zikionesha ufaulu wa mtoto wake. Mtoto wa Aunt Ezekiel na Moze Iyobo dansa wa Diamond naye ametajwa katika watoto gumzo mtandaoni ambao wanafuatiliwa na mashabiki wengi zaidi kutokana na ustaa wa wazazi wake.screenshot_2017-01-22-11-37-07-1
Watoto was Zamaradi Mketema.
Wapo watoto wengi kama vile Mariam mtoto wa MC Pilipili, Juju mtoto wa Zamaradi Mketema, mtoto wa Munaa Love, mtoto wa Esma Platnumz na mzazi mwenzake Petit Man Wakuache, Mtoto wa Tudd Thomas, mtoto wa Kajala, mtoto wa Faiza Ally, mtoto wa DJ Choka, mtoto wa Dina Marious na wengine wengi.screenshot_2017-01-22-11-41-07-1
Paula Paul mtoto wa ‘Kajala’ akiwana rafiki yake.

Huyu Ndiye Trump Bana..!! Atangaza Mwelekea Mpya wa Dunia Huku Masikini wa Marekani Wakianza Kuisoma Namba

$
0
0

DONALD Trump ameapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani. Alivalia suti nyeusi na kufunga tai nyekundu, huku Rais Mstaafu Barack Obama, akiwa amevalia suti nyeusi na tai ya rangi ya bluu. Waling’ara. Ilikuwa siku ya kupewa heshima zaidi kwa bilionea huyo wa biashara za majengo na nyinginezo.

Kabla ya kuapishwa Capitol Hall, Rais mteule, Donald Trump, alikwenda kuhudhuria ibada katika Kanisa la Mtakatifu John mjini Washington. Maelfu ya wananchi waliungana na kiongozi huyo, huku wengine .
wakiandamana kupinga urais wake kitendo ambacho kiliwafanya askari kutumia muda wa ziada kuwazuia.

Marais wastaafu walihudhuria sherehe hizo ikiwa ni ishara ya umoja wa kitaifa bila kujali itikadi za vyama vyao. Miongoni mwa waliokuwepo, George W. Bush, Bill Clinton, Jimmy Carter pamoja na waziri Dick Cheney na wengineo.

Katika hotuba yake, Trump alisema huu si wakati wa maneno bali vitendo na kwamba Marekani inatakiwa kufaidi matunda ya kazi zao na kufufua viwanda vilivyofilisiwa. Tafsiri iliyopo kwenye hotuba hiyo inaonyesha wazi kuwa dunia inakwenda katika mwelekeo mpya.

Katika tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi, Trump alianza kwa kusifu utamaduni wa kisiasa uliowekwa nchini mwao pamoja na kummwagia sifa Rais Obama. “Tutakabiliana na changamoto. Tutakabiliana na nyakati ngumu. Lakini tutafanikiwa malengo yetu. Kila baada ya miaka minne, tunakutana hapa, tunatekeleza wajibu na kukabidhiana madaraka kwa mujibu wa katiba na kwa amani, tunamshukuru Rais Obama na mkewe Michelle kwa juhudi zao ili kufanikisha tukio hili.”

Akizungumzia juu ya msimamo wake katika utawala wa miaka minne ya kwanza, Trump alisema: “Kimsingi suala si chama gani kinachoongoza Serikali kwa sasa, bila kujali Serikali yetu inaongozwa na watu. Januari 20, 2017 itakumbukwa kama siku ambayo wananchi walichukua madaraka ya kuongoza nchi yao tena. Wanaume na wanawake waliosahaulika katika nchi yetu, hawatasahaulika tena.

“Kwa miongo mingi tumevinufaisha viwanda vya nje kwa gharama za kuua viwanda vyetu. Tumetuma majeshi yetu kwenye nchi mbalimbali na kuyadhoofisha; tumetetea mipaka ya mataifa mengine wakati tumeshindwa kutetea kwetu. Tumetumia trilioni ya dola kwa masuala ya nje ya Marekani, wakati miundombinu yetu nchini imeharibiwa na kupoteza mvuto wake,

“Kuanzia siku ya leo na zijazo, mtazamo mpya wa Serikali ni kujali mambo yetu. Toka wakati huu, tutaanza na Marekani kwanza. Kila uamuzi utakaofanywa katika masuala ya biashara, kodi, uhamiaji, sera za nje, utakuwa kwa manufaa ya wafanyakazi na familia za wananchi wa Marekani.

“Tunapaswa kulinda mipaka yetu inayotumiwa na nchi nyingi kutengeneza bidhaa zetu, kuibia kampuni zetu na kupora ajira zetu. Kuyalinda hayo kutakuwa na manufaa na kuibua nguvu mpya,” alisema Trump.

Katika hotuba hiyo, Trump alidhihirisha uzalendo wa hali ya juu baada ya kutamka wazi kuwa kila taifa litapewa nafasi katika majadiliano na Marekani lakini kitakachopewa kipaumbele ni utaifa wa Marekani kwanza kuliko chochote.

Hata hivyo, kabla ya sherehe hizo mamia ya watu walibeba mabango tangu saa mbili asubuhi wakitaka kuelekea kwenye eneo la tukio la Capitol Hall. Miongoni mwa mabango hayo yalisema: “Make racist, Afraid Again”. Pia walibomoa majengo mbalimbali na kuwashambulia waandishi wa habari waliokuwa wakiripoti na kupiga picha kwenye matukio ya kabla, wakati na baada ya kuapishwa.

Atoa amri ya kwanza akiwa Rais

Ikiwa ni saa chache tangu kuapishwa kuwa Rais wa Marekani, Trump ametia saini amri za Serikali mojawapo ikiwa ni agizo linalolenga kuifuta bima ya afya iliyoanzishwa na mtangulizi wake, Barack Obama maarufu kama Obamacare.

Agizo hilo lenye lengo la kuipunguzia Serikali mzigo wa kiuchumi, linaziamuru taasisi za kiserikali kukomesha hatua zitakazoendeleza bima hiyo inayofadhiliwa na Serikali. Badala yake linataka taasisi hizo kupunguza, kuchelewesha au kufutilia mbali gharama za matibabu ambazo zilishughulikiwa na bima hiyo.

Hatua ambayo itaweka gharama hiyo kwa Serikali za majimbo na watu binafsi. Bima hiyo huwawezesha mamilioni ya Wamarekani wasiojiweza kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu. Kuiondoa kabisa bima hiyo kutahitaji muswada kupitishwa katika Bunge la Marekani.

Wasiwasi wa mataifa ya kigeni

Wakati Trump akijinasibu kama bingwa  wa Wamarekani wafanyakazi, kituo cha  sera za kodi ambacho ni  kituo kinachotoa ushauri  bila  kujali  chama, kinakadiria  kwamba  mapendekezo  yake ya  kodi hayataongeza deni la kiasi  cha  dola trilioni 7.2 la Serikali ya  Marekani katika kipindi  cha miaka  10  ya mwanzo, lakini mapendekezo hayo  yanatarajiwa kuwasaidia tu Wamarekani matajiri.

Kuchaguliwa kwake kulipokelewa kwa  wasiwasi  na  wengi duniani  kote, kutokana  na  sera  za  kujitenga  za mambo  ya  kigeni.

Katika  mahojiano  baada  ya Trump  kuapishwa, Makamu  Kansela wa  Ujerumani, Sigmar Gabriel, alisema: “Kile tulichokisikia leo ni matamshi  mazito ya siasa za kizalendo.”

Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto,  alimpongeza Trump  kwa kuampishwa, lakini  alitahadharisha kwamba  utaifa, masilahi  ya kitaifa na ulinzi wa Mexico  ni masuala ya juu kabisa.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa  Francis, alimtaka Trump kuongozwa na mfumo wa maadili akisema ni lazima  kuwaangalia masikini na waliotengwa.

Putin amsubiri Trump

Siku moja baada ya kuapishwa Trump, Rais wa Urusi, Vladimir Putin, yupo tayari kukutana na kiongozi huyo mpya wa Marekani.

Msemaji wa Serikali ya Urusi, Dmitry Peskov, amenukuliwa na shirika la habari la nchi hiyo, TASS akisema hayo siku moja tu baada ya kuapishwa kwa Trump.

Uhusiano kati ya Marekani na Urusi haujawa mzuri katika miaka ya hivi karibuni, huku Marekani chini ya utawala wa rais aliyemaliza hatamu yake juzi, Barack Obama, ikiilaumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wake wa Novemba mwaka jana.

CCM Yawaomba Radhi Watanzania Kwa Waliyoyafanya,Wahaidi Kutorudia Tena..!!!

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaangukia Watanzania kwa kuomba msamaha kutokana na makosa yaliyojitokeza kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi.

Msamaha huo umeombwa Dar es Salaam juzi usiku na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, alipozungumza katika kipindi cha ‘Mada Moto’ kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Channel Ten.

Akiwa katika kipindi hicho ambacho mada ilikuwa ‘Mwaka mmoja wa Serikali ya CCM’, Polepole pamoja na mambo mengine, alizungumzia pia mwelekeo wa CCM kwa miaka 40, itakayodhimishwa Februari 4, kwa kusema kuwa ilifikia hatua baadhi ya wananchi walivunjika moyo kutokana na matendo ya chama hicho.

“Chama Cha Mapinduzi kimejifunza sana katika hii miaka 40, lakini kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015, inawezekana kabisa tumekosea sana na kweli ilifika pahala wananchi walivunjika moyo kwa baadhi ya matendo tuliyoyafanya, na mimi kama kiongozi nabeba dhamana ya wote, watusamehe,” alisema.

Pasipo kufafanua zaidi makosa yaliyojitokeza kabla ya uchaguzi huo na kufikia hatua hiyo ya kuomba msamaha, alisema CCM ni sikivu na kwamba ilisikia pale Watanzania waliposema igeuke.

“CCM ni sikivu, kimesikia pahala ambapo Watanzania walituambia geukeni hapo, na uongozi wa awamu ya tano, chini ya CCM na uongozi wa chama chetu chini ya uenyekti wa Dk. John Magufuli, Makamu wa Mwenyekiti Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu Kinana (Abdulrahman), Naibu Katibu Mkuu Bara na Zanzibar na sisi katika sekretarieti na pia vikao vyote vya chama, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu, Kamati Kuu walifika wakasema imetosha, hatuwezi kuendelea kutosikiliza sauti za Watanzania. CCM si tu kinapendwa na wanachama, bali na umma wa Watanzania,” alisema Polepole.

Hata hivyo, Polepole katika kipindi hicho alisema baada ya kujitazama ndani ya CCM wameamua kutumia msingi wa kujikosoa, kujisahihisha na kwamba imekuwa desturi ya chama hicho kuja na mageuzi makubwa yanayotazama maeneo matatu.

Polepole aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na mageuzi ya kiuongozi kwa kutaka chama hicho kiwe cha mfano.

“Tunataka kiongozi wa CCM ukimtazama unasema huyu ndiye. Ni mwadilifu, ni mwaminifu, mchapakazi, anapiga vita rushwa, ni mkweli, anaamini katika haki, usawa na mambo yanayofanana na hayo,” alisema na kuongeza:

“Ni mtu ambaye kwa hakika miongoni mwetu ni bora kuliko sisi, huyu ndiye kiongozi wa chama, mzalendo wa kweli anayejiweka yeye nyuma na kuweka wengine mbele. Si mbadhirifu, mnyenyekevu, si mwenye mwenendo usiofaa, hayo ndiyo mageuzi ya CCM.”

Polepole alisema licha ya sifa hizo, hata mtindo wa kiuongozi ni shirikishi unaosikiliza wanachama ili kukirejesha chama kwa wanachama.

Hivi Ndivyo Aliyekuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh Alivyoikimbia Nchi Yake..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh.
Aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini humo baada ya mvutano wa muda kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Disemba Mosi mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ECOWAS, kiongozi huyo aliyeiongoza Gambia kwa miaka 22 alipanda ndege kuelekea nchini Guinea ambapo akifika atasafiri kwenda nchini Equatorial Guinea atakapoishi uhamishoni.jammeh2
Akiwa ndani ya ndege.
Jammeh alishindwa na kiongozi wa upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi nchini Senegal na kueleza kuwa atarudi Gambia usalama ukiimarika.
gambia
Barrow aliyeapishwa katika Ubalozi wa Gambia nchini Senegal, alisema kuwa akiingia madarakani ataunda tume kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Yahya Jammeh katika kipindi cha miaka 22 ya utawala wake. Rais wa ECOWAS, Marcel de Souza pia ameeleza kuwa wanajeshi waliokuwa wametumwa kutoka nchi wanachama kwenye kumuondoa Jammeh madarakani sasa wataondolewa japo wachache watabaki kuendelea kuimarisha usalama.jammeh3

Wananchi wa Gambia wamekuwa na hisia tofauti kuhusu kuondoka kwa Jammeh ambapo wanaoaminika kuwa ni wafuasi wake walisikitika kwa majonzi alipokuwa akiwaaga katika uwanja wa ndege huku wengine wakishangili kuamini kuwa ni mwisho wa utawala wa kidikteta uliokuwa hauheshimu haki za binadamu.gambiaRais wa Gambia Adama Barrow alipokuwa akiapishwa kuwa rais wa nchi hiyo katika ubalozi wa nchi hiyo Senegal.

Kitu alichoahidiwa Jammeh kuweza kuachia madaraka baada ya kukutana na baadhi ya viongozi wa mataifa mengine bado hakijafahamika.

Yahya Jammeh anakuwa Rais wa kwanza wa Gambia kuondoka madarakani kwa amani tangu walipopata uhuru mwaka 1965.

Huyu Kikwete Huyu,Tazama Hapa Jinsi Alivyowaweka Mtu Kati Mabilionea Dangote na Bill Gates na Kuteta Nao..!!!

$
0
0

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepata nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani Davos nchini Uswisi.

Rais Jakaya Kikwete alikutana na  tajiria namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote  kutoka nchini Nigeria na tajiria namba moja duniani, Bill Gates kutoka nchini Marekani.

Viongozi hao wamekutana nchini Uswisi katika Mkutano wa Dunia wa Uchumi (World Economic Forum) wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo wa uchumi wa dunia.

Mbali na masuala ya uchumi, mkutano au kongamano hilo pia hujadili kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa sasa yamekuwa ni tishio kubwa kwa viumbe mbalimbali.

Mkutano huu huudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na asasi nyingine za kuraia zikiwa na lengo la kuweka nguvu pamoja na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

Samatta Azidi Kutisha Ubeligiji,Afunga Goli la Ushindi Kwa Timu Yake..!!!!

$
0
0

Mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe ambaye ni Nahodha wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mbwana Samatta ameifungia KRC Genk bao la ushindi dhidi ya wenyeji p Eupen katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Genk imeshinda 1-0 baada ya Samatta kufunga bao hilo katika dakika ya 82 akiunganisha basi safi ya Ruslan Malinovysky.

Samatta ambaye amecheza kwa dakika zote 90, alionyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Eupen.

Kama si juhudi za kipa wa Eupen Hendrik van Crombrugge, Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars angeweza kufunga mabao mengine.

Kwa ushindi huo Genk imesogea hadi katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 31, huku Club Brugge ikiendelea kuwa kinara wa Ligi Kuu Ubelgiji ikiwa na pointi 43.

Beki wa Simba Method Mwanjali Awa Mchezaji Bora wa Mwezi wa 12..!!!

$
0
0

Sentahafu wa Simba, Method Mwanjale amechaguliwa kuwa mchezaji bora Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017. 

Beki huyo wa kati, aliwashinda kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima na beki Yakubu Mohamed wa Azam FC. Mwezi Desemba ulichezwa raundi tatu za Ligi hiyo, huku Simba ikicheza mechi mbili ugenini na moja nyumbani. Raundi hizo ni ya 16, 17 na 18.

Mwanjali aliiongoza Simba kushinda mechi zote tatu, hivyo timu yake kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kunyakua pointi zote tisa, na kubaki katika nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi, nafasi ambayo walikuwa nayo wakati wanaingia raundi ya 16.

Pia katika raundi hizo tatu ambapo Simba haikufungwa bao hata moja, Mwanjali alicheza dakika zote 270, na bila kuonyeshwa kadi yoyote. Alichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya timu yake huku akiongoza safu ya ulinzi.

Kwa kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora, Mwanjali atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wakuu wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora kwa msimu wa 2016/2017 hadi sasa ni John Raphael Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Ramadhan Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Happygod Msuva wa Yanga (Oktoba), na Rifati Hamisi wa Ndanda (Novemba).

Hii Ndiyo Simbaah..Yaigagadua Polisi Dar Bila Huruma..!!!

$
0
0

Simba imeanza vizuri hatua ya kuwania Kombe la Shirikisho kwa kuitwanga Polisi Dar es Salaam kwa mabao 2-0.

Polisi ilionyesha soka safi lakini ikashindwa kuhimili vishindo vya Simba, hadi mapumziko ilikuwa imefungwa kwa bao moja lililofungwa na Patory Athanas.

Kipindi cha pili, Simba waliingia na kasi lakini kipa wa Polisi Dar ndiye alikuwa shujaa kutokana na kuokoa michomo mingi ya hatari.

Laudit Mavugo na Shiza Kichuya, walipoteza nafasi nyingi kwa upande wa Simba huku wakishindwa kuutegua mtego wa offside wa Polisi mara kwa mara.

Dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho, Mohamed Zimbwe Jr, aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa baada ya shuti lake kugonga mwamba baada ya kuuvunja mtego wa kuotea wa Polisi. Halafu ukamkuta na kuupachika wavuni.

Duh Simba si wa Mchezo Mchezo Aisee,Wamebadili Muonekano wa Gari lao na Sasa Lipo Kama Basi la Man United..Tazama Pichazz

$
0
0

Basi la klabu ya Simba aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya wadhamini TBL kupitia Kilimanjaro kutoongeza mkataba mpya.


Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali. Je, una maoni kuhusiana na mwonekano wake?

Huu Ndio Upasuaji wa kurudisha Bikra Kwa Mwanamke Unavyofanywa ..!!!!

$
0
0

bikra ni nini?

hii ni ngozi laini sana inayofunika uke kwa wanawake ambao hawajawahi kushiriki ngono kabisa, kikawaida mwanamke anaacha kuitwa bikra pale ngozi hii inapoondolewa.... ngozi hii kitaaamu inaitwa hymen.

hymenorrhaphy ni nini?

huu ni upasuaji unaofanyika kuirudisha bikra ya mwanamke ambayo imeshatoka tayari kwa sababu mbalimbali.

aina hii ya upasuaji mara nyingi hazipatikani kweye hospitali za kawaida kwani hazina umuhimu wowote kwenye matibabu na zinaweka kwenye kikundi cha plastic au cosmetic surgery,hivyo mara nyingi hufanyika kwenye hospitali au clinic binafsi na mabingwa wa magonjwa ya akina mama yaani gynacologist..

idadi ya wanawake wanaofanyiwa aina hizi za upasuaji inazidi kuongezeka miaka inavyozidi kwenda mbele kutokana na watu kuanza ngono mapema sana.

watu gani wanatakiwa wafanyiwe aina hizi za upasuaji?

wanawake ambao wanataka kurudisha bikra zao ambazo zimeshatoka wanatakiwa kufanya upasuaji huu kwani hakuna dawa yeyote inayoweza kurudisha bikra na ukiisikia ujue ni utapeli.

katika hali ya kawaida bikra inaweza kutoka kwa kushiriki ngono, kupata ajali na kuumia, tabia ya kujichua, mazoezi kama kuendesha baiskeli au farasi, matumizi ya aina fulani za pedi  au magonjwa fulani fulani.

wakati mwingine ngozi ila ya bikra inaweza kua ngumu sana kiasi kwamba ikakataa kuchanika hata kwa kuingiliwa kingono. hivyo mwanamke kutotoka damu wakati wa ngono kwa mara ya kwanza haimaanishi kwamba mwanamke sio bikra.

kwanini wanawake wanafanya aina hizi za upasuaji?

wanawake hua wanasababu mbalimbali kama ifuatavyo

   1 kuwaonyesha wanaume zao au jamii zao kwamba wao ni mabikra kipindi cha ndoa hasa kwenye jamii fulani fulani ambazo bikra ni muhimu sana siku ya ndoa.

  2  kuwasaidia wenye maumivu ya kisaikolojia baada ya kubakwa, hii inawafanye wapate amani kidogo baada ya upasuaji huu.

   3 kurudisha bikra ambayo imeharibika sababu ya kuumia kwa ajari.

upasuaji huu unafanyikaje?

hii ni aina ya upasuaji mdogo ambayo inafanyika kwa kuchoma sindano ya ganzi tu na wala haihitaji kwanamke kupewa dawa za usingizi, japokua kuna wakati mwingine kutokana na mazingira ya mgonjwa daktari anaweza kulazimika kutoa dawa ya usingizi.

kuna aina tatu za upasuji za kurudisha bikra kama ifuatavyo.

  1  kuishona tena ngozi ile ya ya hymen ambayo inamfanya mwanamke aitwe bikra kwa kuirudisha pamoja na kuiacha ipone kisha kurudi kama zamani

  2  kuweka ngozi ya hymen ya bandia na kuishonea pale kisha kuweka ndani yake aina fulani ya kimiminika kinachofanana kabisa na damu ili damu ionekane ikitoka  wakati wa ngono

  3  kuikata ngozi ya hymen ambayo ilichanika mwanzoni na kuitoa nje kisha kuirudishia upya na kuishona kabisa kama mwanzo.

wanawake wanaofanya aina hii za upasuaji wanatakiwa wafahamu kwamba wanatakiwa wakae bila kushiriki ngono wiki tatu mpaka miezi mitatu ili bikra ishike vizuri hivyo ni vizuri kuifanya mapema kabla ya ndoa sio unataka ufanyiwe leo afu wiki ijayo uolewe.

nyuzi zinazotumika kushona ngozi ile ya bikra hua haziondolewi yaani baadae huyeyuka ndani kwa ndani.

madhara ya upasuaji huu

upasuaji huu ni salama kabisa ila hua una madhara madogo madogoambayo ni kawaida hata kwa uparesheni zingine kama ifuatavyo.

kutokwa damu; hii ni kawaida hata kwa uparesheni zingine lakini damu hii inatakiwa ikauke na kuondoka baada ya siku chache.

kubana sana; wakati mwingine daktari anaweza akaishona ngozi ile na kuibana sana kiasi kwamba ikawa ngumu sana siku ya kuitoa wakati wa kushiriki ngono. hua na maumivu makali ambayo huisha bila dawa yeyote baadae.

infection; hii husababishwa na kushambuliwa na bacteria baada ya upasuaji lakini huweza kuzuiliwa kwa kupewa dawa za kuzuia hali hii mfano antibiotics

mwisho; aina za upasuji hizi zinapatikana nje ya nchi kwa wingi, kwa nchini tanzania na afrika kwa ujumla zipo pia lakini ni sehemu chache sana.

dunia inakwenda kwa kasi sana hivyo mwanaume ukijikuta umeoa bikra mwenye watoto wanne usishangae...

SIMANZI: Ajinyonga Baada ya kusalitiwa na Mpenzi Wake, Aacha Barua Yenye Ujumbe Mzito..!!!

$
0
0

Kijana mmoja kwa Jina la Fredrick Richard amefikia hatua ya kujinyonga baada ya mpenzi wake (Rose) kumsaliti na kugawa tunda kwa rafiki yake kwa jina Robert.


 Kabla ya kufikia maamuzi ya kujitoa uhai, kijana huyo aliandika barua ya simanzi kusikitishwa kwa kitendo alichofanyiwa na wawili hao.



Kwa Walevi Waliopindukia: Kama Unataka Kuacha Pombe Kabisa Hii Inakuhusu,Soma Hapa...!!!

$
0
0

 makala iliyopita nilizungumzia madhara ya unywaji wa pombe na kama hukuipata makala hiyo basi isome hapa........, watu wengi ambao ni walevi sana kwenye jamii hudharauliwa na kulaumiwa sana kwa kuendekeza tabia hizo, ni kweli wanaweza kua wanapaswa kulaumiwa lakini upande wa pili ni kwamba watu hawa pia hawapendi kua hivyo na wanashindwa kuacha kwasababu pombe ina kitu kinaitwa addiction yaani mazoea na sio rahisi kuacha kirahisi kwani mwili umeshazoea na unataka zaidi, ikitokea umeacha ghafla hata shughuli zako zitakushinda kwani utapata dalili kitaalamu kama withdraw syndrome ambazo ni kutetemeka, kichwa kuuma, kutapika , kushindwa kula na kua mgonjwa muda wote.

maana yangu ni kwamba mlevi aonekane kama mgonjwa kwenye jamii na kama anataka kuacha pombe basi mpeni msaada na sio kumtenga, swala la kuacha pombe linawezekana kabisa kwa walevi waliopindukia au watu wanaokunywa kawaida tu. yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa kuacha pombe..

amua kutoka moyoni; hakikisha maamuzi haya yametoka moyoni mwako kulingana na wewe unavyoona na sio kwamba unataka ili kuacha kuridhisha kikundi fulani au mtu fulani, hii itakupa nguvu ya kupambana na majaribu ya kutaka kunywa pombe tena.

wajulishe wanywaji wenzako nia yako; waambie rafiki zako kwamba umeamua kuacha pombe kwa muda fulani, wape sababu zako za msingi na kama huna waambie ni sababu binafsi za kifamilia, wajulishe kwamba inaweza kua ngumu na utaomba msaada wao iwapo ukiwaka tamaa ya kunywa pombe tena.

jiwekee malengo mafupi; anza kwa kujiwekea kwamba sitakunywa pombe mwezi huu wote wa kwanza, ukifanikisha ongeza mwezi mwingine...hii itakuapa motisha ya kuendelea kuacha kuliko kusema kwanzia leo sinywi tena kwani utajikuta unakunywa. kama mwezi ukiisha na kujikuta umesevu pesa nyingi kwa kutokunywa basi jinunulie zawadi yeyote.

pangilia starehe zako; kama starehe zako nyingi zinahusisha kunywa pombe basi pangilia starehe zingine ambazo hazitaki pombe mfano kwenda bichi, kwenda kuangalia sinema, kungalia mpira uwanjani na kadhalika. epuka kwenda disko na bar kwa kipindi hiki cha mwanzo.

jitoe nje ya raundi za pombe
; kama umeacha pombe usijihusishe na kuwanunulia watu pombe kwa kuzungusha kama wanywaji wanavyofanyiana wakiwa bar, nunua kinywaji chako kimoja kama ni soda au juisi kisha kaa pembeni ukinywa. kuwanunulia watu utajikuta na wewe unanunuliwa pombe.

kama mnatoka kwenda kwenye starehe basi endesha gari; kuendesha gari ni sababu kubwa ya wewe kutokunywa pombe kama sheria inavyotaka na hata ukilazimishwa kunywa utawaambia rafiki zako kwamba mimi ni dereva leo.

kua tayari kuzungumzia swala lako; watu wengi watakua wanakuuliza kwanini umeamua kuacha pombe, basi andaa sababu za msingi za kuwaambia kama jinsi pombe inavyoharibu maisha yako ya kijamii, kiuchumi na kiafya na wakati mwingine ukiona umezidiwa waambie ni sababu za kifamilia zaidi.

badilisha sehemu za kukutana na watu;
kama ulikua ukipanga kuonana na mtu, unaenda bar basi badilisha sehemu ili ue unaenda kuonana nao kwenye mgahawa au sehemu zingine za wazi ambapo pombe haziuzwi.

furahia faida za kuacha kwa muda huo;
angalia ni kaisi gani cha fedha umesevu kwa kuacha pombe, unajisikiaje kukaa muda mrefu bila kupata hangover, unajisikiaje jamii iliyokudharau sasa inakuheshimu na hii itakupa nguvu zaidi a kusonga mbele.

dawa za kuacha pombe kwa walevi sana;
kuna dawa maalumu ambazo zimetengenezwa kuwatibu watu ambao wanataka kuacha pombe hasa wale ambao wameshindwa kuacha kwa njia nilizotaja hapo juu, utaratibu huu hufanyika chini ya uangalizi wa daktari hasa kwa nchi zilizoendelea...dawa hizi hufanya kazi kwa kukosesha mtu hamu ya kunywa pombe, kuongeza muda wa hangover mpaka siku tatu, na kuzuia madhara mtu anayopata kwa kuacha pombe haraka mfano disulfiram.[sina uhakika kama zinapatikana nchini], pia unawea kutumia virutubisho mbalimbali vya kuondoa sumu mwilini baada ya kuacha pombe, hivyo unaweza kuvipata hapa nchini.

CUF Mmemsikia Jecha Huku?Amesema Kuwa Eti Alikuwa Sahihi Kufuta Uchaguzi Mkuu Kwa Sababu Hizi Tu..!!!

$
0
0

BAADA ya kimya kirefu, hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha amefunguka na kuelezea kuwa uamuzi aliouchukua wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2015 baada ya kubainika kuwa na dosari, ulifanyika kwa kufuata taratibu, kanuni, Sheria na Katiba ya Zanzibar.

Jecha aliyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha Funguka, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Azam na kusisitiza kuwa, hana wasiwasi wala hofu yoyote kwa hatua hiyo, aliyoichukua ya kufuta uchaguzi kwa kuwa ilifuata misingi yote ya Sheria na Katiba.

Pamoja na kwamba alikataa kujibu kwa undani kuhusu hatua yake hiyo na kusisitiza kuwa mengi atayabainisha kwenye taarifa ya tume, alisisitiza kuwa hakuwahi kutumika na chama chochote wala kuwasiliana na Rais Ali Mohammed Shein kama inavyodhaniwa na wengi.

“Haya yote yataonekana kwenye taarifa ya uchaguzi, siwezi kuongea hapa sasa ila kiukweli utaratibu ulifuatwa. Matokeo yalifutwa kutokana na dosari zilizojitokeza ikiwemo baadhi ya matokeo kujulikana kabla na kusababisha baadhi ya vyama kulalamika,” alisisitiza Jecha.

Alieleza kuwa matatizo na dosari za uchaguzi huo, yalianza kujitokea katika kipindi cha kupokea matokeo ambapo matokeo yalitoka katika maeneo ya Unguja, hayakubainika kuwa na matatizo, isipokuwa kwa matokeo yalitoka katika maeneo ya Pemba.

Alisema katika kura hizo za Pemba, ilibainika kuwa utaratibu wa kiufundi ulifanyika kuharibu matokeo ya hesabu za kura baada ya kufanyika urekebishaji wa kasoro wa mambo, ambayo hayakutakiwa yafanywe nje ya sheria za uchaguzi.

Alisema baada ya kutokea kwa dosari hizo, kwa upande wa tume kupitia yeye, iliamua kufuta uchaguzi mzima ili kuepusha vurugu na mgongano wa kisiasa huku Polisi ikifanya uchunguzi kuwabaini wahusika waliosababisha dosari hizo katika matokeo ya uchaguzi.

Kuhusu kushirikisha wajumbe wengine wa tume katika kufanya maamuzi ya kuufuta uchaguzi, Jecha alibainisha kuwa tume nzima ya ZEC ilihusika katika kufutwa kwa uchaguzi huo na ndio maana baada ya kufutwa taratibu za uchaguzi mwingine zilitekelezwa vyema na tume hiyo.

Hata hivyo, alibainisha kuwa katika kutangaza uamuzi wa kufuta uchaguzi huo, alilazimika kufanya hivyo binafsi baada ya kuona hali ya matokeo hayo inazidi kuwa mbaya na kwenda kinyume cha taratibu za uchaguzi.

Alibainisha kuwa baada ya kufuta uchaguzi huo, ili kuleta usawa kwa vyama vyote, tume hiyo ilisubiria vikao vya kutafuta mustakabali wa kisiasa visiwani humo vilivyokuwa vikifanyika baina ya viongozi wa kisiasa wa vyama vyote ndipo itangaze tarehe ya uchaguzi mpya.

“Tulikaa kimya kwa takribani mwezi mmoja tukisubiri hatua zichukuliwe na viongozi kupitia hivyo vikao vyao. Tulisubiri katika ule muda bila kuvunja sheria, na baada ya kuona hakuna hatua zinachokuliwa dhidi ya maamuzi yetu tulitangaza tarehe ya uchaguzi,” alieleza Jecha.

Mwenyekiti huyo alikanusha madai kuwa ametumika kufuta uchaguzi huo kwa maslahi ya CCM na Dk Shein. “Hapana, Sijawahi hata mara moja kuitwa au kutafutwa na kiongozi yeyote wa serikali, wala Rais sijawahi kuwasiliana na hata namba yake sina,” alifafanua.

Alisema ingawa hajawahi kukutana na mtu yeyote anayemlaumu kuhusu uamuzi wa tume hiyo wa kufuta uchaguzi, endapo kuna mtu bado ana malalamiko, anaruhusiwa kuiandikia ZEC malalamiko yake na si yeye binafsi, yatafanyiwa kazi.

Pamoja na hayo, mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa hata baada ya kuufuta uchaguzi huo, kwa kuwa anaamini alifuata taratibu na sheria zote, hakujificha wala kuogopa kitu, kwani aliendelea na shughuli zake kama kawaida.

“Hadithi zilikuwa nyingi, kila mmoja alifikiri alivyotaka yeye, mie nilikuwepo Zanzibar natembea, lakini si kila mtu alikuwa ananiona. Redio za kijamii kila moja ilikuwa inazungumza vyake, mwenyekiti yuko hivi, mwenyekiti yuko wapi, mwenyekiti kesho ananyongwa mara nimepelekwa mahakama za kimataifa yote hayo yalizungumzwa lakini mie nipo,” alisema.

CCM Yaibuka Kidedea Uchaguzi Wa Marudio Jimbo la Dimani Zanzibar.Yaigaragaza CUF Kwa Kura 4860..!!!

$
0
0

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar na kushinda viti vya udiwani katika maeneo mengi Tanzania Bara katika majimbo yaliyotoa matokeo yake mpaka jana usiku.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na vingine vilivyo nje ya umoja huo vimejikuta katika wakati mgumu katika uchaguzi huo mdogo.

CCM iliibuka mshindi katika uchaguzi wa Dimani uliotokana na jimbo kuwa wazi baada ya kifo cha mbunge wake Hafidh Ally Tahri kilichotokea Novemba mwaka jana mjini Dodoma, alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge.

Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Dimani, Fatma Gharib Haji alimtangaza mgombea wa CCM, Juma Ali Juma kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 4,860 dhidi ya mpinzani wake Abdulrazak Khatib Ramadhani wa CUF aliyepata kura 1,234.

Ehee!! Umemsikia Lowassa Alichosema?Amesema Eti 2020 Atashinda Uchaguzi Kiulaini ,Unadhani Hilo Litawezekana Kweli?

$
0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema njia ni  nyeupe kwa Chadema kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu  na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa  hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa Chadema, James Lembeli katika kijiji cha  Mseki, Kahama, Lowassa (pichani) alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na  wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Kudadeki..!!Kanisa la Anglikana Lamwandalia Adhabu Kali Askofu Mokiwa kwa Kuwa Mkaidi..!!!!

$
0
0

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya amesema watachukua hatua zaidi dhidi ya Askofu Valentino Mokiwa wa kanisa hilo Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kuwa bado anaendelea kutoa huduma licha ya kutakiwa kujiuzulu.

Wiki tatu zilizopita Mokiwa aliandikiwa barua na Askofu Chimeledya akitakiwa kujiuzulu akidaiwa kuvunja miiko ya kanisa hilo na kutumia madaraka yake vibaya ikiwamo kufanya ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, Dk Mokiwa amekuwa akikana tuhuma dhidi yake akisema mgogoro wa kanisa hilo ni wa kutengenezwa na adui zake.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi jana, Askofu Chimeledya hakuzitaja hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Askofu Mokiwa, akisema hakuna ulazima wa kuziweka hadharani hadi pale zitakapochukuliwa na kanisa hilo.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images