Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Kudadeki..Kumbe Daraja la Kigamboni Linaingiza Pesa Ndefu Kiasi Hiki..!!?

0
0

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekusanya Sh. bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane, katika daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Makusanyo hayo, imeelezwa, ni kuanzia katikati ya Mei, mwaka jana hadi mwezi huu na ni juu ya lengo kwa asilimia 20.

NSSF inakuwa taasisi ya pili ndani ya wiki moja kutangaza mapato ya mradi, baada ya Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (Dart) kufanya hivyo Alhamisi.

Akizungumza na Nipashe jana juu ya maendeleo ya mradi wa daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema limeingiza jumla ya Sh. bilioni sita.

Aidha, Prof. Kahyarara alisema gharama za uendeshaji wa daraja hilo katika kipindi hicho ni jumla ya Sh. milioni 800 tu.
Prof. Kahyarara alisema NSSF imemudu kuvuka lengo kwa wastani wa asilimia 20 kutokana na kutumia waajiriwa wake badala ya wakala.

Alisema awali makaridio yalikuwa ni kukusanya Sh. bilioni tano katika kipindi hicho.

“Sera yetu ni kwamba hizi fedha hatuzitumii," alisema Prof. Kahyarara."

"Tunaziwekeza moja kwa moja BoT (Benki Kuu) katika mnada wa dhamana za serikali (treasury bonds) ambayo ni ya asilimia 13.5 ambayo ikiiva miaka 15 ijayo ni Sh. bilioni 18."

Alisema kwa uwekezaji huo, NSSF itarudisha fedha zilizojenga daraja na faida ya kutosha.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, kwa utaratibu wa BoT kila baada ya miezi sita wanaweza kuvuna faida ambayo watawekeza kwenye miradi mingine ya maendeleo.

“Utaratibu huu tumeona unalifanya Shirika kuwa na uhakika, kwamba likihitaji fedha ya haraka wanaweza kuzitumia na taarifa zitaonyesha fedha za daraja zilishapatikana. Ni ubunifu tulioanzisha kwa kuwa tuliona ukiweka sekta binafsi huwezi kupata faida hiyo,” alifafanua.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF alisema iwapo kazi ya kukusanya fedha hizo ingepewa kampuni binafsi wangepata hasara ya Sh. milioni 300.

Prof. Kahyarara alibainisha kuwa NSSF ilitaka tangu siku ya kwanza ya kutumika kwa daraja hilo faida ianze kukusanywa jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Tuna uwezo mkubwa wa kukusanya fedha, tuna madirisha ya kutosha na watu wenye utaalamu kama walioko mabenki. Itakuwa ni kituko kumuita mtu kutukusanyia fedha, hivyo hatuna mpango wa kutumia kampuni binafsi," alisema Prof. Kahyarara.

"Kwa kutumia wafanyakazi wetu wenyewe tuna uhakika mkubwa wa kukusanya zinazoingia na kurudisha fedha zetu kwa wakati.”
Prof. Kahyarara alisema kazi ya NSSF ni kuandikisha wanachama, kukusanya fedha za wanachama, kulipa mafao na kuwekeza ili fedha ziwe na thamani zisikae bila kuwa na thamani.

Ujenzi wa daraja hilo, ambao uligharimu dola za Kimarekani milioni 128, ulianza mwaka 2012 na kufanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Daraja hilo lililozinduliwa Aprili 19, mwaka jana, na Rais John Magufuli, lina urefu wa mita 680 na jumla ya barabara sita.


Ehe..Mashabiki wa Simba Mmesikia Alichokisema Bocco wa Azam Fc Baada ya Kuwafunga..?

0
0

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amesema kwamba utulivu, kutokata tamaa ndiyo siri ya mafanikio yake kuifunga mara nyingi Simba kila wanapokutana nayo.

Bocco alifunga bao pekee la dakika ya 70 jana kwa Azam kwenye mchezo dhidi ya Simba iliyolala kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza  baada ya mchezo wa juzi, Bocco alisema kwamba kufunga kwake kwenye mechi nyingi dhidi ya Simba kunatokana na utulivu na kutokata tamaa muda wote wa mchezo.

“Kila mechi nawekewa ulinzi mkali, lakini sikati tamaa, muda wote ninakuwa na lengo moja tu la kutafuta nafasi ya kufunga, ambalo ndilo jukumu langu nililopewa uwanjani kama mshambuliaji,”alisema Bocco na kuongeza.

“Mfano mechi kama ya leo (juzi) mimi ninapenda niwasifu mabeki wa Simba walicheza vizuri na kutubana kwa muda mrefu, lakini likatokea kosa moja tu na sisi tukalitumia vizuri kujipatia bao,”alisema Bocco.

Bao la juzi linakuwa la nane kwa Bocco msimu huu na kuzidiwa kwa bao moja na Shiza Kichuya wa Simba, Amissi Tambwe na Simon Msuva wa Yanga wanaoongoza kwa pamoja kila mmoja akiwa na mabao tisa.

Aidha, juzi Bocco aliifikisha mabao 19 ya kuifunga Simba tangu Azam ipande Ligi Kuu mwaka 2008, hivyo kuendelea kuongoza kufunga mabao mengi katika mechi baina ya timu hizo.

Huyu Ndiye Golikipa wa Kagera Sugar Aliyefariki Usiku wa Kuamkia Leo..!!!

0
0

Golikipa wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za ligi kuu amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na kifo cha mchezaji huyo.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar. Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani,” alitweet kiongozi huyo wa TFF.

Marehemu David Burhan ameshawahidakia Mbeya City na Majimaji, ikumbukwe kuwa Burhan ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Pan African ya Dar es Salaam, Abdallah Buruhan.

Ubuyu wa Moto Moto.. Penzi la Tunda Ladaiwa kumkosesha Dogo Janja Usingizi..!!!

0
0

Kwa wapenzi wote wa ubuyu, tena ubuyu mtamu, basi hapa ndipo penyewe! Ubuyu uliotufi kia mubashara unatonya kuwa video queen aliyeuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian anadaiwa kumkosesha usingizi staa wa Manzese Music, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni mapenzi aliyonayo kwake.

KUMBE NDIYO CHANZO CHA BIFU!

Chanzo makini kilitoa ubuyu wa motomoto kuwa, Dogo Janja au Janjaro anayekimbiza na Ngoma ya Kidebe, amekuwa akiteseka kutokana na mapenzi aliyonayo kwa Tunda japokuwa waliwahi kuwa wapenzi zamani.
Inadaiwa kuwa, haijulikani Tunda alimpa nini Dogo Janja lakini ukweli ni kwamba anatamani kuwa naye tena na ndiyo chanzo cha bifu lake la mara kwa mara na mwandani wa Tunda ambaye naye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’.
“Unaambiwa Dogo Janja hapati usingizi kwa sababu ya penzi alilonalo kwa Tunda. “Kama utakuwa unamfuatilia, amekuwa akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa, anamuomba Mungu ampe Tunda maisha marefu ili aendelee kumuona milele.
“Hata kwa marafi ki zake amekuwa akisema bado anampenda sana Tunda na ndiyo maana alimtungia wimbo huo wa Kidebe”.
“Nasikia hata video ya wimbo huo Dogo Janja alitaka acheze Tunda lakini siku ambayo walikuwa wanashuti, mwanadada huyo alipata emergency (dharura) ndipo akatafutwa mwingine’.
“Hivi karibuni ndiyo ameweka wazi kwamba huo wimbo amemwimbia Tunda, jambo ambalo lilimfurahisha sana mrembo huyo aliyeuza sura kwenye Wimbo wa Salome wa Diamond Platnumz na Rayvanny.
TUNDA FULL SURPRISE
“Lakini kwa upande wake Tunda amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea kuwa alikuwa hajui kama ndiye aliyeimbiwa lakini anaupenda sana wimbo huo,” alisema mtoa ubuyu wetu.
HUYU HAPA TUNDA
Baada ya kupata ubuyu huo, Wikienda  lilimtafuta Tunda na mazungumzo yalikuwa hivi;
Wikienda: Mambo vipi Tunda, unaongea na Wikienda hapa.
Tunda: Karibu, niambie.
Wikienda: Kuna habari kuwa ule Wimbo wa Kidebe alioimba Dogo Janja amekuimbia wewe, unajua?
Tunda: Nimejua hivi karibuni na nimefurahi sana kiukweli maana aliniomba niwe video queen lakini ikashindikana. Siku aliyokuwa anashuti nilipata emergency, lakini kiukweli nimefurahi sana.
Wikienda: Kilichokufurahisha zaidi ni nini?
Tunda: Nimefurahi kwa sababu ni wimbo ninaoupenda sana kabla hata sijajua kaniimbia mimi.
Wikienda: Mliwahi kuwa wapenzi zamani, je, mna mpango wa kurudiana?
Tunda: Kama tutarudiana mtasikia tu, mapenzi hayajifi chi kwa hiyo wewe sikilizia.
Wikienda: Lakini kuna taarifa kwamba Dogo Janja hapati usingizi analiwewesekea penzi lako, je, unalijua hilo.
Tunda: Hahahaa…sijui ndiyo nasikia kwako maana hajaniambia.
DOGO JANJA AELEKEA DODOMA
Ili kuleta mzani wa habari hiyo, Wikienda lilimgeukia Dogo Janja ambapo baada tu ya kupokea simu alisema yupo kwenye kelele akielekea Dodoma.
Wikienda: Haloo Dogo Janja, kuna habari yako hapa.
Dogo Janja: Samahani niko kwenye kelele naelekea Dodoma mawasiliano siyo mazuri.
KUTOKA MEZA YA UBUYU
Dogo Janja amekuwa akinaswa mara kwa mara na warembo mbalimbali na sasa anadaiwa kumuwewesekea Tunda ambaye ni mpenzi wa Young D hivyo akiingilia penzi hilo ataharibu mambo, namshauri moyo wake ufanye kazi ya kusukuma damu kwa sasa na si vinginevyo.

Goli la John Bocco Laua Shabiki wa Simba Dar...!!!

0
0

BAO la dakika ya 70 alilofunga straika wa Azam FC, John Bocco, juzi Jumamosi dhidi ya Simba, limeua shabiki mmoja wa Simba aliyetajwa kwa jina la Chenje Ramadhan Dogoli mkazi wa Manzese jijini Dar, mwenye umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa nesi wa Hospitali ya Mwananyamala ambaye hakupenda kuanikwa jina lake kwa sababu yeye si msemaji mkuu, alisema shabiki huyo ambaye ni mfanyabiashara katika eneo la Manzese, alifikishwa hospitalini hapo na wenzake akiwa kwenye hali mbaya.

“Alifikishwa hapa na wenzake akiwa kwenye hali mbaya, wenzake wanasema

 wakati wanaangalia mpira huko kwao Manzese, mara bao lilipofungwa, akaonekana anapumua kwa taabu na akaanza kuishiwa nguvu, wakaamua kumkimbiza hospitali ambapo kwa bahati mbaya akafariki dunia muda mfupi baada ya kufika hapa,” alisema nesi huyo ambaye ndiye aliyempokea.

Ikumbukwe kuwa, Simba na Azam zilipambana juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Bocco ukiwa

 ni mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Bara.

Hata hivyo, walipotafutwa madaktari wa Mwananyamala jana, waligoma kuzungumzia ishu hiyo wakidai wafuatwe ofisini leo Jumatatu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Suzan Kaganda alipoulizwa alisema suala hilo haliihusu polisi.

“Ishu hizo kama za kufa pengine kwa shinikizo la damu haziwezi kuripotiwa polisi kwa kuwa ni maradhi ya kawaida, labda ingekuwa ni jambo la mauaji,” alisema Kaganda.

Bilionea wa Facebook Anataka Nawe Ufanikiwe Kama Yeye..!!

0
0
NIANZE kwa kukubaliana na wasomaji ambao wamekuwa wakilalamika kuyumba kiuchumi kwani hata mimi ninapitia kipindi kama hicho. Lakini cha msingi tusikate tamaa, tuendelee kukaza kwa kufanya kazi kwa bidii. Tusisahau ubunifu na kukipenda kile tunachokifanya ambacho mwisho wa siku ndicho kinatupatia mkate wetu wa siku. Baada ya kusema hayo, bila shaka utakuwa umewahi kutumia au kusikia Mitandao ya Kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram.

Mmoja wa wamiliki wa mitandao hiyo anajulikana kwa jina la Mark Zuckeberg, Mmarekani aliyezaliwa huko White Plains, New York nchini Marekani. Jamaa ni bilionea mwenye pesa ndefu ambazo zimemfanya ashike namba tano huku akiwa na utajiri wa dola bilioni 55 (zaidi ya trilioni 110), ndiye tajiri mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 32.

Mkewe anaitwa Priscilla Chan mwenye umri wa miaka 30. Jamaa ametajirishwa na Mtandao wa Facebook. Hakuzaliwa akiwa tajiri, aliangalia dunia inahitaji nini, hivyo akachangamkia fursa. Ni mambo yaleyale ambayo nimekuwa nikiyaeleza kila siku. Alipoona fursa, hakuiacha, akaichangamkia na mpaka kufika hapo. Anapohojiwa na waandishi wa habari, huzungumza mambo mengi sana ambayo kama watu wengine wakiyafanya, basi watafanikiwa na kuwa kama yeye.

Unataka kufanikiwa? Basi fanya mambo haya matano ambayo yamemfanya Zuckerberg kufanikiwa na kuwa hapo alipo. USIOGOPE KUFA NYA MAKOSA Wakati akihojiwa kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni Zuckeberg anasema: “Watu wengi wanaogopa kufanya mambo f’lani kwa kuogopa kukosea. Hakuna mtu aliyekamilika, kila mtu huanza kwa kufanya makosa pia. Wengine wanaogopa kuchekwa, eti nikikosea, akina f’lani watanicheka, ndugu yangu, hutakiwi kuogopa kitu chochote kwani kukosea ni sehemu ya maisha yetu, ni kitu ambacho tumeumbwa nacho.

“Unapofanya makosa ndipo unapopata akili ya kufanya vizuri baadaye na ndiyo maana wakati mwingine unapata utajiri, unafanya makosa na kufilisika lakini unaporekebisha makosa yako na kugundua ulipoangukia, unainuka tena.” JIFUNZE KWA WATU WALIOFANIKIWA Zuckerberg anaendelea: “Unapotaka kufanikiwa ni lazima uwaangalie waliofanikiwa walianzaje? Nilipoanza safari hii, niliwaangalia Bill Gates, Carlos Slim na wengine. Ni mfano bora kwangu. Niliangalia video zao na kuwasikiliza, kwa nini walifanikiwa, waliwezaje?

Kama wao waliweza, kwa nini mimi nishindwe? Nikafanya na hatimaye nikawa hapa nilipo.” T E N GENEZA T I M U NZURI J a m a a anafunguka: “Huwezi kufanya biashara ukiwa peke yako, ni lazima uandae timu kwa ajili ya usimamizi, sasa hiyo timu ni lazima iwe nzuri ambayo itakufanya kusonga mbele na si kurudi nyuma. “Nilipoanzisha Facebook, niliiandaa timu yangu, niliweka watu makini, timu ambayo ilikuwa tayari kupambana.

Walijitoa sana, walipambana na ninakiri kwamba bila timu hiyo makini leo nisingekuwa hapa nilipo.” UWE NA KIU YA MABADILIKO Anasema: “Ndiyo! Unapoamua kufanya biashara mtaani kwako, ni lazima uwe na kiu ya kubadilisha mtaa mzima. Watu wana shida na kitu f’lani waambie kwamba wewe utabadilisha kila kitu. Watu wanapenda mabadiliko, biashara ambayo inafanyika, leta yako ikiwa imeboreshwa au yako iwe mpya kabisa kwa ajili ya kuonesha watu kwamba
una kitu kipya kuliko vya w e n gine. “Niliangalia hilo kipindi cha nyuma.

Niliona kwamba watu wanapenda kuwasiliana, wale wa Marekani wanapenda kuwasiliana na marafiki wapya wa Afrika, Ulaya na sehemu nyingine. “Nilipogundua hilo, nikasema ni lazima nilete mabadiliko, watu watoke kwenye hali ya kutamani na kuingia kwenye hali ya kuwa nacho, hivyo nikawaletea Facebook ambayo leo watu wa sehemu mbalimbali wanatengeneza urafiki.

”FUATILIA KILA SIKU Jamaa anaweka wazi: “Unapokuwa na biashara usijifanye wewe ndiye bosi kwamba huwezi kutoka ofisini, unataka kila kitu uletewe. Haipo hivyo, kwa sasa hivi kila kitu kimebadilika,  hakuna bosi wa kukaa ofisini, kama ni kweli hiyo ni biashara yako ni lazima uifuatilie hatua kwa hatua. “Huwezi kupata mafanikio kwa kukaa ofisini tu, ni lazima ujue leo kimeingia kiasi gani na kimetoka kiasi gani, ni lazima ujue timu yako inaishi vipi, f’lani yupo wapi na anafanya nini. Ni lazima wakati mwingine uende kuzungumza na watu, upate mawazo yao, hawataki nini na wanataka nini.

Ukifanya hivyo na kujitolea, hakika utazidi kufanikiwa.”

Huu Ndio Muonekano Mpya wa Ray C, Mashabiki Wadai Aache Kujikondesha

0
0

Mashabiki wamjia juu Ray c... Wamwambia aache Diet ya kupungua mwili kwani ameanza kuharibika na kukonda...!! Wamtaka aache mara moja.

Umeuona Mjengo Anaojenga Diva? Mwenyewe Adai Hela za Matangaza ya Insta ndo zinajenga

0
0


Diva The Bawse sio mtu wa mchezo mchezo, amewaonesha mashabiki jambo ambalo limewashtua katika mtandao wa Instagram.


Mtangazaji huyo wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, amepost picha katika mtandao huo ya mjengo wake anaodai anaujenga huku akiweka wazi kuwa utakamilika ifikapo mwaka 2018.


“Tusichukuliane POA ila nene Hard work Pays Aisee, don giv Up guys !. focus and Msidharau Online ads , Haya Matangazo ya Insta By 2018 yatamaliza Hii nyumba yangu. Tuseme Inshaallah 💞,” ameandika Diva katika picha ya nyumba hiyo.


Endapo nyumba hiyo itakamilika itamfanya mtangazaji huyo kuwa miongoni mwa mastaa wenye mijengo mikali hapa Bongo.

Waliookolewa Mgodini Watoka Hospitali

0
0


Geita. Wachimbaji 15 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Geita kwa ajili ya matibabu baada ya kuokolewa katika mgodi wa RZ walikokuwa wamefunikwa na kifusi cha udongo kwa siku tano wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya zao kuwa nzuri.


Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Brian Mawala amesema afya za wachimbaji hao zimeimarika na wana uwezo wa kuendelea na kazi.


Baada ya kuruhusiwa leo asubuhi wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga.

Wastara Ataja Mambo 5 Ambayo Hatayasahau Katika Maisha yake

0
0

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma ametaja mambo matano ambayo hatakuja kuyasahau katika maisha yake.


Muigizaji huo amekiambia kipindi cha FNL cha EATV, jambo la kwanza ambalo hata kuja kulisahau maishani mwake kifo cha wazazi wake wote wawili na jambo la pili ni ajali ambayo ilimsababishia ulemavu mpaka sasa hivi.

Jambo la tatu ambalo Wastara ameongeza hatalisahau ni kifo cha mumewe Sajuki na jambo jingine ambalo linamuumiza na hatalisahau wakati alipotumia vyombo vya habari kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya mumewe Sajuki ambaye baadaye alifariki dunia.

Wastara ameweka wazi jambo la tano ambalo linamuumiza zaidi kichwa ni kitendo cha mashabiki wake kumchukulia tofauti na alivyo kiuhalisia.

Hii Inaitwa Kubana Matumizi Bana....Waziri Mkuu Atua Dodoma Kwa Ndege ya Abiria,Soma Hapa livee..!!!!

0
0
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Dodoma leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria vikao vya bunge  ambavyo vinatarajiwa kuanza kesho Jumanne

Waziri Mkuu ameongozana na mkewe Mary Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali ambao wametumia usafri wa ndege ya abiria ya ATCL inayopitia Dodoma kuelekea Kigoma
Katika Uwanja wa Ndege Waziri Mkuu amepokelewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wa serikali na chama wa mkoa wa Dodoma.

Mara baada ya mapokezi hayo, Waziri Mkuu amefungua Kikao cha Baraza la Mashauriano (RCC) mkoani Dodoma ambapo amesema kikao hicho ni chombo muhimu na endapo kitatumika vizuri kitaweza kusaidia kusukuma maendeleo ya Mkoa na kupunguza migogoro kwenye Halmashauri.

Amesema wakati umefika wa kuwa na watumishi wenye weledi wa kutosha kwenye Halmashauri zote nchini na pia hazitakiwi kuwa pango la wezi, wazembe au jalala la kutupa wabadhilifu walioshindikana kwingineko.

Aidha, Waziri Mkuu amesemma Serikali za Mitaa na Halmashauri zote nchini zinatakiwa zianze kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi kuona ni kwa namna gani zitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda vinavyotarajiwa.

Hata hivyo amesema kila Halmashauri iandae mpango wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo makubwa ya kipaumbele kama vile ujenzi wa miundombinu ya shule,  maboresho kwenye sekta ya afya (ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya).

“Endeleeni kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwenu, mfanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.  Kila mmoja kwa nafasi aliyonayo atimize wajibu wake na kuzingatia mipaka ya nafasi yake. Punguzeni migogoro, matusi, dharau, bezo na vitisho. Mshirikiane na jamii ione mpo wamoja,” amesema.

Vikao vya Bunge vinaanza kesho baada ya wiki mbili za shughuli za kamati za kudumu za Bunge, na sasa tayari wabunge wamekwishawasili Dodoma kwa ajili ya vikao hivyo vitakavyodumu kwa takriban wiki 2

Gigy: Mabwana wa Wema Wananishobokea Wenyewe…

0
0

Kufuatia kusambaa kwa video yake akifanya vitendo vya kifuska hadharani na aliyekuwa mpenzi wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Ibrahim Mgimbu ‘Calisah’ mwanadada anayeuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka na kusema wenyewe ndiyo wanaomshobokea.
 Video hiyo chafu ya Gigy na Calisah ilisambaa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wengi walionekana kumshangaa mwanadada huyo huku wakimtolea maneno ya kejeli kuwa hajatulia na amekuwa akipenda kuwa kimapenzi na wanaume waliopitia kwa Wema akiwemo Idris Sultan. Baadhi ya mashabiki waliozungumza na Wikienda walifunguka kuwa, Gigy anatakiwa kubadilika kwani amekuwa mtu wa matukio kila siku na amekuwa akipita kule alikopita Wema kwa sababu alianza na Idris na sasa Calisah.
“Hivi Gigy haoni wanaume wengine hadi ajibebishe kwa wale ambao tayari walishakuwa na uhusiano na Wema? Hata sielewi Gigy anajisikiaje maana hii video yake na wanafanya vitendo vya kimahaba huku akiwa ana uhusiano na mpenzi wake wa siku zote Moj (Mourald Alpha) sijui naye huwa anaonaje na anajisikiaje anapoona mwanamke wake anafanya hivyo,” alisema shabiki mmoja aliyezungumza na Wikienda.
Baada ya kuvutiwa waya na kuulizwa kulikoni kupenda kupita alikopita Wema na kujirekodi video za kimahaba na kuziachia mitandaoni, Gigy alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza niseme hiyo video siku hiyo, Calisah ndiye aliyenishobokea maana ndiye aliyenifuata, kuhusu wanaume aliotoka nao Wema ni kwa sababu labda nyota yangu inamzidi maana wenyewe ndiyo wamekuwa wakinifuata kwa kifupi wanaume wa Wema ndiyo huwa wananishobokea. “Kuhusu Moj, ni mpenzi wangu na ni mume wangu mtarajiwa na ni baba wa mwanangu maana nina ujauzito wake.”

Obama Kuwa Bilionea Baada ya Kustaafu, Anaweza Kulipwa Hadi Shilingi Bilioni 99 Kuandika Kitabu Kipya cha Maisha Yake..!!!

0
0

Barack Obama amepumzika sasa baada ya kuitumikiaa Marekani kwa miaka minane kama Rais. Lakini, hiyo haimaanishi kuwa ametoka kwenye mzunguko wa fedha. Na tena, huenda akaanza kuingiza nyingi zaidi, asante kwa mikataba minono inayomuwinda kutoka kwa wachapishaji wa vitabu.

Yeye na mkewe Michelle, ni uamuzi wao tu, kukubali kusaini mikataba ya vitabu, yenye thamani ya kuanzia dola milioni 20 hadi 45. Fedha hizo, pamoja na matumizi mengine, zitamwezesha kugharamikia bili za ndege binafsi, sababu amewahi kudai kuwa hatopenda kusafiri na ndege za kawaida akistaafu.

Kwa mujibu wa New York Times, mawakala wa masuala ya vitabu wanadai kuwa Obama ana nafasi ya kuandika kitabu chenye thamani kubwa zaidi kuwahi kuandikwa na Rais yeyote.

Wengine wanadai kuwa Obama anaweza kuingiza zaidi ya dola milioni 12, na mkewe zaidi ya dola milioni 10.

Obama amewahi kuandika vitabu vitatu, “Dreams From My Father,” “The Audacity of Hope” na “Of Thee I Sing” ambavyo vimeuza zaidi ya nakala milioni 4 duniani na kumuingiza zaidi ya dola milioni 10.

Kudadeki...!!Zaidi ya Watu Laki Tisa Wasaini Kupinga Ziara ya Trump Uingereza

0
0

Zaidi ya watu 900,000 wamesaini petition ya kutaka kusitishwa kwa ziara ya Donald Trump nchini Uingereza kufuatia uamuzi wake wa kupiga marufuku waislamu kuingia Marekani

Na sasa wabunge wa House of Commons watalazimika kujadili ziara hiyo.

Mipango ya Trump kuzulu nchini Uingereza, ilitangazwa saa 48 zilizopita baada ya waziri mkuu, Theresa May kueleza kuwa Rais huyo ameukubali mwaliko toka kwa malkia.

Petition hiyo inadai kuwa Trump hapaswi kualikwa nchini humo kuepuka kumdhalilisha malkia. Uamuzi wa Trump kuzuia raia wa nchi 7 za Kiislamu kuingia nchini Marekani umepingwa vikali.

Mangwea Awatokea Cpwaa na Noorah,Wafunguka Alichowaambia ..!!!

0
0

Ikiwa sasa ni miaka minne na miezi kadhaa imepita tangu Rapa Albert Mangwea kufariki dunia, wasanii Noorah pamoja na Cpwaa kwa pamoja wamejikuta wakifanya mpango wa kuingia studio na kurudi na nguvu mpya wakidai kuwa ni maagizo aliyowapa ndotoni.

Hatua hiyo ni baada ya wakali hao kwa muda tofauti kumuota rappa huyo na kuamini kuwa huenda alikuwa anawakumbusha kuwa wanapaswa kurudi kwenye muziki na kumuenzi kwa kufanya kazi ya pamoja.
Alianza rapa Noorah kwa kupost picha ya Albert Mangwea na kusema alimuota na jinsi alivyokuwa wakizungumza ni kama alikuwa hai na kitendo kilichomfanya Noorah atamani kuona ile ndoto kama ingekuwa ndiyo uhalisia lakini haikuweza kuwa kwa kuwa ni ndoto tu.

"Nimekuota usiku wa leo (jana) mshkaji wangu. Ilikuwa 'too realistic' kama vile bado upo hai. R.I.P ndugu yangu" aliandika Noorah 

Baada ya hapo aliibuka Cpwaa na kudai hata yeye amemuota Albert Mangwea juzi hivyo ni kama rapa huyo anaongea nao, hivyo Cpwaa alimuomba Noorah warudi kwenye muziki kwani game ni kama imemiss sana ladha zao, hivyo Noorah alisema haina tatizo japo kwa muda huu bado anafanya matibabu kutokana na tatizo lake la kichwa, ila aliahidi kuwa atapita kwa Cpwaa ili wamalize kesi hiyo. 

"Bro huwezi amini I did as well jana! Daah bro is talking to us. Come back my brother game ime miss ladha zetu Babastylz jana nime request sana ngoma za Ngwea kiwanja flani" alisema Cpwaa.

Duh..Noma Sana ..Ben Pol Ageuka 'Mbogo' Story Kuhusu Mtoto Wake(Video)

0
0

Msanii wa bongo fleva Ben Pol amesema hayupo tayari kuelezea sababu ya kuachana na mwanadada ambaye walifanikiwa kupata mtoto mmoja aliyepewa jina la Mali

Akiongea kupitia eNewz Ben Pol amesema kwa sasa hayupo tayari  kabisa kuongelea swala la mwanamke ambaye kwa sasa wameachana  na hayupo tayari kumuelezea mtoto wake na endapo mtu yeyote atahitaji kufanya mahojiano kuhusiana na mtoto wake asubiri mtoto akue ili aweze kumuhoji kuhusiana na maisha yake.

Mtazame hapa:-........

Kwa Faida Yako:Kutafuna Bigijii kwa Muda Mrefu Kunaweza Kukusababishia Vidonda vya Tumbo..!!!

0
0

Kuna athari kubwa sana zinazotokana na utafunaji wa bigijii (chewing gums) kwa muda mrefu

Utafunaji huo husababisha tumbo kuzalisha acid ya kutosha likifikiri kuna chakula ambacho kinatafunwa tayari kumezwa. Kitendo cha kutafuna bigijii husisimua seli linazozunguka ukuta wa ndani wa tumbo kutengeneza juisi (digestive juice) ambayo husaidia kwenye mmeng’enyo wa chakula.

Hii ni njia asilia ambayo husababisha chakula ambacho kimetafunwa kuanza kumeng’enywa punde tu kinapofika tumboni. Kwahiyo utafunaji wa bigijii (chewing gums) husababisha uzalishaji wa aside isiyo na ulazima. Hii ni habari nmbaya kwa walaji wa bigijii kwani aside hii huongeza athari za kupata vidonda vya tumbo.

Lakini risk ni ndogo sana labda uwe unatafuna bigijii (chewing gums) nyingi sana kwa siku, kwahiyo ondoa hofu labda uwe kocha wa mpira wa miguu (football coach).

Njaa na Deni la Tiafa Kutikisa Bunge Kesho..!!!

0
0

Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni la taifa na hali ya uchumi nchini.

Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki.

Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-

KIAPO CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-

    Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo
    Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi
    Mhe. Anne Kilango Malecela
    Mhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)

MASWALI

Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi. 

KAULI ZA MAWAZIRI

Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa  kama ifuatavyo:-
Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.

MISWADA YA SHERIA

Katika mkutano huu, miswada ifuatayo itajadiliwa...

Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).

Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016) 

Kudadadeki..!!Unaikumbuka Ile Chura ya Snura,Sasa Ona hapa Jinsi Wanaijeria Wanavyoicheza na Kuiimba livee(Video)

0
0

Wimbo wa msanii Snura ambao ulifungiwa kwa mara ya kwanza na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) 'Chura' umeonekana kuwakosha baadhi ya raia wa Nigeria baada ya msanii mkubwa wa Nigeria Don Jazzy kujirekodi video huku akiimba na kucheza ngoma hiyo

Baadhi ya mashabiki wa Tanzania pia wamepokea vyema video hiyo na kutoa sifa nyingi kwa Don Jazzy kwa kitendo cha kuimba ngoma hiyo ya Singeli pia wametoa pongezi nyingi kwa Snura kwa ngoma yake hiyo.

"Lol TZ did I get it right?  #255 #Chura" alipost Don Jazzy 

Hii ni sehemu ya video hiyo

Cheka na Mpoki Kwenye Domo Tenga ya EFM Radio(Video)..!!!

Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images