Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Ubuyu wa Moto Moto..Simu yawagombanisha Vanessa na Jux..!!!

0
0

Msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa mara nyingi huwa wanagombana na mpenzi wake huyo Jux kutokana na tabia yake ya kuchelewa kujibu jumbe fupi au hata kupokea simu zake. 

Vanessa Mdee alisema haya kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kudai kuwa Jux kwenye suala la simu amekuwa mvivu sana na ndiyo jambo linaloleta tofauti kati yao.

"Mvivu wa simu amefarakanishwa na simu yake huyu jamaa, hata kwenye kujibu txt au kupokea simu hana ushirikiano na simu kabisaa kwa hiyo tunagombanaga mara nyingi kuhusiana na communication" alisema Vanessa Mdee 

Yeleuwiii..Eti Gigy Money Anataka Kuokoka Ila Sio Sasa..!!!

0
0

MUUZA sura kwenye video za Bongo Fleva ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Choice FM, Gift Stanfod ‘Gigy Money’ hivi karibuni amefunguka kuwa, katika maisha yake, ipo siku ataachana na mambo yote yasiyompendaza Mungu kisha kumtumikia muumba wake.

Akipiga stori mbili tatu na Global Publishers, Gigy aliweka wazi kuwa, katika maisha ya mwanadamu, hasa kijana hukumbana na changamoto nyingi za kimaisha ambazo wakati mwingine humfanya kumkosea muumba wake, lakini inafikia hatua anaamua kuacha kila kitu na kufanya yanayompendeza Mungu.

“Unajua sometimes tunadondoka dhambini, lakini si kwa mapenzi yetu, binafsi ipo siku tu, nitaachana na mambo ya kidunia na kusimama kwa Mungu,” alisema Gigy asiyeishiwa vibwanga.

Hatimaye Serikali Yakiri Bungeni Kuwa Baadhi ya Maeneo Nchini Kuna Njaa

0
0

Jumla ya tani 35,491 za chakula zinahitajika ili kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula na lishe kati ya mwezi Februari na mwezi Aprili mwaka huu unaowakabili watu 1,186,028.

Taarifa hiyo ya serikali imetolewa bungeni leo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini huku akisisitiza kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini bado ni wa kuridhisha pamoja na kuwa baadhi ya maeneo yenye upungufu wa chakula.

Tizeba amesema taarifa hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya tathmini ya serikali iliyobaini kupungufu huo katika halmashauri 55 nchi nzima. 

Aidha amesema kuwa jumla ya watu 118,603 wasio na uwezo wa kupata chakula watahitaji tani 3,549 za chakula cha bei nafuu kwa haraka na tayari serikali imeanza kuchukua hatua za kushusha bei ili wananchi waweze kumudu bei zake.

Amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua na mtawanyiko usioridhisha katika maeneo mengi nchini athari zinazotarajiwa kutokea ni pamoja na matarajio ya malengo ya uzalishaji wa mazao ya chakula huenda yasifikiwe, uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo utapungua, uwezekano wa kuongezeka kwa bei za baadhi ya mazao ya chakula upo, kupungua kwa mapato yatokanayo na ushuru wa mazao kwa baadhi ya halmashauri.

Athari nyingine ni pamoja na kuongezeka kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kutokana na uhaba wa malisho na maji na uwezekano wa kupungua kwa mapato yatokanayo na mazao ya kilimo yanayouzwa nje ya nchi, uwezekano wa kuwa na maeneo mengi yenye upungufu wa chakula na hivyo kuongezeka kwa kiwango cha utapia mlo.

Dkt.Tizeba amesema kuwa ili kukabiliana na athari za ukame tathmini imebainisha kuwa halmashauri za wilaya hizo 55 zinahitaji jumla ya tani 1,969 za mbegu bora za mahindi, mtama na mizizi inayokomaa kwa muda mfupi na kustahimili ukame na mbegu hizo zinahitajika ziwafikie mwezi Februari mwaka huu ili ziweze kupandwa katika msimu wa mwaka 2016 /2017 katika maeneo yanayoendelea kupata mvua wakati huu wa mwaka.

Waganda Kuamua Mechi za Watanzania Kimataifa

0
0

Waamuzi wa Uganda wameteuliwa kusimamia mapambano ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika inayoanza Mwezi Februari mwaka huu.

Kamati ya waamuzi ya CAF, imewateua, Mashood Ssali, Hussein Bugembe, Musa Balikoowa Ngobi na Ali Sabila Chelegat kwa ajili ya mchezo wa Zimamoto dhidi ya Ferroviara da Beira, ya Msumbiji, utakaopigwa Februari pili mwa huu, 2017.

Kwa upande wa Tanzania Bara, Alex Muhambi, Ronald Katenya, Okello Lee na Brian Miiro Nsubuga wameteuliwa kusimamia mchezo wa Yanga dhidi ya Ngaya Club De Mde, ya Comoro, wikiend ya Februari 17 -19, 2017.

Simba SC Wafuata Njia ya Yanga Kuikataa Mamelodi Sundown..!!!

0
0

Klabu ya soka ya Simba SC nayo imeungana na wapinzani wao Yanga kukataa kucheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundown kutoka Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Simba, amekiambia kipindi cha Sports HQ cha EFM, hawatacheza mechi hiyo katikati ya wiki hii na mabingwa hao kutokana na kubanwa na ratiba za ligi kuu ya Tanzania Bara.

Naye mratibu wa ziara ya mabingwa hao hapa nchini, Rahim Zamunda amesema wamepanga timu hiyo ya Mamelodi kuanza kucheza mechi ya kwanza na Azam FC Jumatano hii na alikuwa haoni sababu ya timu za Simba na Yanga kukataa bahati hiyo kwa kuwa hata Barcelona wiki chache zilizopita ilikuwa nchini Qatar wakati ligi yao bado inaendelea.

Mamelodi Sundown walikuja nchini kwa ajili ya ziara ya kupinga mauaji ya tembo ambapo walipangiwa kucheza na timu za Yanga, Simba na Azam FC.

Daktari Aeleza Kilichowaokoa Waliofukiwa na Kifusi Geita..!!!

0
0

Wachimbaji wadogo  15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ, Nyarugusu mkoani hapa jana waliruhusiwa kutoka hospitalini baada ya hali zao kuendelea vizuri. Juzi Jumapili, ilikuwa siku ya muujiza kwa watu hao ambao waliishi chini ya ardhi kwa zaidi ya saa sabini na mbili (72) kabla      ya baadaye kuokolewa katika tukio hilo la kihistoria nchini Tanzania.

Januari 25, 2017, watu hao, akiwemo raia mmoja wa China, Meng Juping walifukiwa na kifusi kwenye mgodi huo na hivyo kuishi ardhini kwa muda huo bila kuona jua wala mwanga, hali ambayo kimaumbile ni vigumu kutokana na kukosa hewa safi ya oksijeni ambayo ndiyo humfanya binadamu kuishi.

Kufuatia muujiza huo ambao wengi wanaamini ni Mungu tu kwa binadamu kuishi chini ya ardhi, Uwazi lilizungumza na daktari wa magonjwa ya binadamu jijini Dar, Godfrey Chale ambaye alitoa sababu zilizowasaidia wahanga hao kukiepuka kifo licha ya kuishi ardhini.

“Kikubwa ni kwamba, inategemea watu walipo. Mfano, kama hao jamaa wote kumi na tano walikuwa eneo lenye nafasi au ‘hall’ kubwa kule ardhini, hiyo ndiyo ilikuwa salama yao.

“Unajua binadamu tunaishi kwa kutegemea hewa ya oksijeni, sasa inapotumiwa na watu halafu haingii nyingine, ni lazima watu wafe. Lakini kama watu watakuwa kwenye eneo lenye uwazi mkubwa kama nilivyosema wanaweza kudumu kwa siku kadhaa kwa sababu oksijeni bado ipo.

 “Lakini kama walikuwa kumi na tano halafu kwenye nafasi ndogo ni vigumu sana kuendelea kuishi. Kwa sababu ushindani wa kuvuta oksijeni ungekuwa mkubwa, wangekufa.

 “Hili sasa linategemea na idadi ya watu kwani pia inawezekana wale walikuwa kumi na tano kwenye nafasi kubwa, wangekuwa zaidi ya idadi hiyo, mfano thelathini na ukubwa wa eneo ni huohuo, lazima wangepoteza maisha kwani oksijeni ingekwisha haraka.

“Kingine kilichowaokoa ni siku za kukaa na kuokolewa, kwani pia kama wangekaa muda zaidi ya siku hizo, lolote lingeweza kutokea kwani oksijeni pia ingeisha. Ndiyo maana utaona watu kama wale wakishatolewa lazima waongezewe maji ili waweze kurejea katika hali ya kawaida kwani miili yao inakuwa imepoteza nguvu kwa kiu, njaa na kuvuta hewa kwa tabu,” alisema Dokta Chale.

Kuhusu madhara yatokanayo na kuishi ardhini kwa siku hizo, Dokta Chale alisema kuwa, ni kusumbuliwa kwa mfumo wa kuvutia hewa.

“Unajua mtu akiwa chini ya ardhi lazima atakuwa anavuta hewa yenye vumbi na uchafu mwingine. Kwa hiyo lazima tiba yao itakuwa pamoja na kuangalia mfumo wa kuvutia hewa,” alisema daktari huyo anayetoa huduma kwenye Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar.

Waliofukiwa katika mgodi huo ni Ezekiel Bujiku (20), mkazi wa Wigo, Yohana Shigangama (34) na Busanda John (20) (mahali wanakoishi hakujajulikana), Aniset Masanja (32), mkazi wa Katoro na Dikson Moris (25) ambaye naye haikujulikana alikokuwa akiishi. Wengine ni Mussa Cosmas (28), mkazi wa Tabora, Raphael Nzubi (26), mkazi wa Bariadi, Amani Sylvester (26), mkazi wa Sengerema, Sheku Butogwa (22), mkazi wa Nyamalulu, Hassan Idd (31) mkazi wa Ilemela, 
Augustino Robert (27), mkazi wa  Nyarugusu, Mgalula Kayanda (23), mkazi wa Ramadi, Sabato Philimon (30), mkazi wa Musoma, Meng Juping (36), raia wa China na mwingine ambaye jina lake halikutambulika mara moja. 

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, ameagiza kurudishwa kwa Afisa Madini wa Mkoa wa  Geita, Fabian Mshai ambaye alihamishwa, ili kutoa maelezo juu ya uzembe uliosababisha tukio hilo.

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Kutoka Bagamoyo , Anarudisha Mapenzi na Kusafisha Nyota

0
0

MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI, (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 48 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI:

SHEKH SHARIFU RASHIDI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran, dawa za asili, dawa za kiarabu na majini, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango, ngiri maji na n.k, anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, pia anatoa pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali kulingana na nyota yako, anaouwezo mkubwa wa kutumia jina la muhusika kwa kutatua tatizo lako, anaouwezo wa kumrudisha mtu aliepotea kimiujiza, pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo,

WASILIANA NAE KWA SIMU NA WHATSAPP NO: 0718-668347. 0685-224047, 0767-204308 na 0627-251404 au follow@shekh_sharifu_rashid, Email:shekhsharifurashid@gmail.com

Belle 9 Afunguka Umaskini Ulivyomfanya Apokonywe Mpenzi Wake

0
0
Wimbo, Sumu ya Penzi uliomtoa Belle 9, ulikuwa ni true story ambayo hatoweza kuisahau kamwe.
Aliuandika baada ya mpenzi wake kummwaga na kuanzisha uhusiano na mtu aliyekuwa akimfahamu.
“Ilinichukua muda sana kuzoea ile hali,” Belle 9 alisema kwenye mahojiano na Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Kwasababu kitu ambacho kilichokuwa kinaniuma ilikuwa katoka kwangu halafu kaenda kwa mtu ambaye namfahamu kabisa, na yule mtu maisha ya kwao na maisha ya nyumbani ni tofauti. Yule alikuwa hata siku tukienda kwenye mpira kila siku anabadilisha six, anabadilisha jezi, sisi ndio tulikuwa wale watu ambao tunarudia hizo hizo kila siku,” aliongeza.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza Hapa Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Mzee Mwenye Wake 86 Afariki Dunia..!!

0
0

NIGERIA: Mzee mmoja(93) aliyekuwa na wake 86 na watoto zaidi ya 170 amefariki dunia kwa maradhi ambayo hayajawekwa wazi.

Mzee huyo ambaye ni Mhubiri wa zamani wa dini ya Kiislamu nchini Nigeria alikuwa akiwaambia Wanawake hao kuwa Mungu alimuagiza kuwaoa.

Shoga Chakula Hakiliwi Gizani....!!!!

0
0

EEE heiiyaaa…shoga yangu ni Jumanne nyingine tamu hadi kumoyo, tumekutana tena. Najua wengi mtakuwa na furaha kwa kuwa leo ndo’ tunaukata mwezi wa kwanza na kesho tunaanza mwingine, si ndiyo!

Basi kiafya shoga yangu ni kama ulivyoniacha wiki jana na najua na wewe ni mzima ila kama mgonjwa ni jambo la kuombeana tu! Shoga si unakumbuka wiki iliyopita niliongea na wale wenzangu na mimi ambao kitu kidogo wanachoshwa na chakula cha usiku? Manung’uniko mengi utadhani analazimishwa kuchomwa sindano, inahuu?

Basi shoga yangu baada ya kuandika tabia za wanaume na wanawake kukataa kula chakula cha usiku kwa kisingizio cha kuchoka, nilipata meseji nyingi, tena wengine wakaniambia wamewaonesha waume/wake zao na wamejirekebisha.

Kuna watu walikuwa na shida jamani hee! Tena kuna wengine walikuwa wameshaanza tabia ya kuchepuka, kisa uvivu wa waume zao, aibu! Shoga sasa wiki hii nimepata meseji kutoka kwa msomaji wangu mmoja anayefahamika kwa jina la Hanifa kutoka Tanga.

Ameniambia anafurahishwa sana na mada zangu na zimekuwa zikimfunza sana. Kikubwa alichotaka niongee na wewe pia ukisome na ufanyie kazi ni hizi tabia za wanaume kupenda kula chakula gizani. Meseji yake ilikuwa inasema hivi; shoga mimi ni mama wa mtoto mmoja lakini tangu nimekuwa na mume wangu sasa yapata miaka mitatu.

Zamani mume wangu alikuwa akipenda sana kula chakula cha usiku na mimi kwenye mwanga lakini hivi ninavyokuambia ana zaidi ya mwaka kila tukila naye chakula cha usiku anataka gizani. Naomba nishauri kwani nikila chakula gizani wala sishibi zaidi ya kushinda na njaa nifanyaje shangazi yangu?

Kwanza nikupe pole yako maana hawa wanaume wetu lol! Hivi jamani mkikimbiwa mtu akaenda kula chakula kwenye mwanga na mtu mwingine mtasema nini? Hamjui raha ya chakula au? Mbona zamani tangu umuoe mlikuwa mkila chakula kwenye mwanga?

RAHA YA CHAKULA

Shoga kwanza nikung’ate sikio kwa wewe ambaye unakaa tu hujui raha ya chakula. Ukiona wengi wapo kwenye ndoa zao na wanapenda kula chakula gizani, ujue wanawatoto lakini ukiona mtu hana watoto au watoto wana chumba chao, yeye kwenye kula chakula cha usiku anataka kula gizani, ujiulize huyo mwenzako vipi?

Shoga raha ya chakula ukile kwenye mwanga peupee peee! Kama kuna minofu uione na uitafune utaona raha yake. Kula chakula gizani ni sawa na kwenda uwanjani kucheza mpira wakati mpira wenyewe umeusahau nyumbani au kwenda bafuni kuoga unavua nguo zote sabuni umeisahau ndani, inahu?

HESHIMU CHAKULA

Chakula shoga yangu kina heshima yake, kama unaheshimu vitu vingine na ndiyo maana ukila chakula kwa wakati wake, matokeo yake yanatokea unaitwa baba ati, upo? Jenga mazoea na tenga muda wa kupeana chakula tena kwa kukiheshimu na kukipangia ratiba kama unavyopanga ukiwa ofisini kwako, umenipata shoga?

HAMA MAZINGIRA

Shoga chakula si lazima kiliwe kwenye meza hiyohiyo kila siku au mna zaidi ya mwaka mnakula chakula kwenye meza hiyohiyo utadhani hamna ‘fenicha’ nyingine mjini loool! Shoga jenga tabia ya kutoka na mwenzako kwenye hoteli au sehemu nzuri ambayo mnaweza kupata chakula chenu cha usiku hata kama hamtalala huko basi kubadilisha mazingira ya meza. Raha ya mbuzi au kuku siyo kumla kwa mkono wa kushoto au kulia bali mikono yote, upo?

SAFISHA UWANJA

Huwezi jua shoga, wengine wanaamua kula chakula gizani kwa kuogopa uwanja. Utakuta mwanamke mwenzangu msafi, akivaa anavyonukia utadhani amezaliwa na pafyumu ila mkalishe kwenye chakula cha usiku, we we weeee!

Utakimbia mbona! Shoga jenga mazingira ya kusafisha uwanja wako kila baada ya siku kadhaa. Uchafu hasa kwa sisi wanawake haufai shoga yangu. Tena ukute siku nzima upo kwenye mihangaiko, ukirudi hata ujisugue na sabuni iliyochanganywa na pafyumu na magadi kutoka wapi shoga lazima utanuka tu. Kwa nini usikimbiwe?

Raha ya chakula, mumeo akikute kwenye sahani ambayo ni safi, haina uchafu wa aina yoyote tena ale peupe bila giza, umenipata? Shoga najua nimeongea mengi sana ila kwa leo nahisi kiu imenibana na naomba niishie hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi ya hapa, upo?

MwanaHalisi Lamuomba Radhi Rais Magufuli. Lakiri Habari ilikuwa na Makosa

0
0

  1. MwanaHalisi Lamuomba Radhi Rais Magufuli. Lakiri Habari ilikuwa na Makosa

Baba Amgeuza Bintiye Mwenye Ulemavu Kuwa Mke, Aanza Kumtesa Baada ya Kumtumia na Kumchoka

0
0
Habari ya simanzi na kusikitisha wilayani Chunya Mbeya, Baba amemgeuza bintie wa kumzaa mwenye ulemavu kuwa mke. Baada ya kumtumia kwa namna awezavyo, ameanza kumfanyia vitimbi ikiwa ni pamoja na kuanza kumnyanyasa kuashiria kuwa amemchoka.

VIDEO:

Jamaa Aliyenyang'anywa Demu na Harmo Rapa Ajitokeza na Kulalamika Kupitia Redio

0
0
Harmo Rapper yule msanii anayejifananisha na Harmonize yadaiwa alimnyanganya Demu presenta na DJ aitwae Msabato na jamaa huyo ameenda studio za EA radio kulalamika na kusema alimnunulia kila kitu na kumpangishia chumba lakini demu huyo ameondoka kwa dharau

Demu mwenyewe jamaa anadai alimtoa Arusha na kumleta Dar kisha kumpangishia chumba na kumpa fedha za saluni na mahitaji mengine

VIDEO:

Noma Sana..Hili Ndio povu Alilotoa Lulu Baada ya Video Inayomuonyesha Akivunja Amri ya Sita Kusambaa Mitandaoni..!!!

0
0

Video ya mtu anayesemekana kuwa ni msanii maarufu wa maigizo nchini, lulu michael, ikimuonyesha msanii huyo akivunja amri ya sita imezagaa mitandaoni. 

Video hyo inasemekana kuwa ya muda, hata hivyo mwenyewe kupitia ukurasa wake wa instagram amekanusha vikali kuwa hyo video sio yake bali ni lulu rappe


U HEAD...Mose Iyobo Afunguka Sababu ya Kumuita Harmorapa Nyani(Video)

Baba wa Kambo Amuua Mtoto wa Mkewe,Kisa Hiki Hapa...!!!

0
0

Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Gwanseri wilayani Muleba kuuawa na baba yake wa kambo kisha kumfukia ndani ya nyumba akiwa amemuweka kwenye mfuko wa plasitiki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amesema tukio la mwanafunzi huyo kuuawa lilitokea jana katika kijiji cha Karutanga wilayani Buleba na kumtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Remijius Poncian(16).

Kamanda Olomi amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni baba wa kambo, Hassan Misigaro (52) anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Serikali - Uzalishaji wa Chakula Nchini Utafikia Tani Milioni 3..!!!

0
0

SERIKALI imefanya tathmini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini na kubaini kwamba uzalishaji wa chakula nchini utakuwa na ziada ya tani 3,013,515.

Akisoma kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula na lishe nchini katika mwaka 2016/17 bungeni Dodoma jana, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alisema tathimini iliyofanywa, imebaini kwamba jumla ya tani 35,491 za chakula zinahitajika katika kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula na lishe kati ya Februari na Aprili mwaka huu kwa ajili ya watu 1,186,028 walioainishwa kuwa na upungufu katika halmashauri 55.

Kwa mujibu wa Dk Tizeba, ziada hiyo ilibainika baada ya Bunge la 10 kutoa kauli ya kufanya tathmini ya upatikanaji na mahitaji ya chakula ambapo tathmini ya awali ya uzalishaji chakula kwa mwaka 2015/16 na upatikanaji wa chakula mwaka 2016/17, ilikamilika.

Alieleza kuwa tathmini hiyo ilionesha kuwa kitaifa, uzalishaji wa chakula utafikia tani 16,172,841 za chakula na mahitaji ya chakula kwa mwaka huo ni tani 13,159,326 na hivyo kuwa na chakula cha ziada cha tani 3,013,515 yaani tani 1,101,341 ni mazao ya nafaka na tani 1,912, 174 ni za mazao yasiyo ya nafaka.

Aliongeza kuwa nchi ilikuwa na utoshelevu wa chakula kwa asilimia 123, lakini pamoja na hali nzuri cha chakula kitaifa, kulikuwa na halmashauri 43 ambazo zilikuwa na maeneo yenye upungufu wa chakula.

Aliongeza kuwa tathmini hiyo ilishirikisha Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Wizara ya Afya kupitia Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC).

Alieleza kuwa tathmini hiyo ilizingatia mihimili minne ya usalama wa chakula ambayo ni upatikanaji wa chakula, ufikiwaji wa chakula, utumiaji wa chakula na uthibiti wa chakula, ilitumia mfumo wa uainishaji madaraja ya usalama wa chakula na lishe.

Aidha, alisema Serikali inafuatilia mwenendo wa bei za mazao ya chakula hususani mahindi, mchele na maharage ili kujiridhisha uwepo wake sokoni.

Tathmini imebaini jumla ya tani 35,491 za chakula zinahitajika katika kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula na lishe kati ya Februari na Aprili mwaka huu kwa ajili ya watu 1,186,028 walioainishwa kuwa na upungufu katika halmashauri 55. Aidha, watu 118,603 wasio na uwezo wa kupata chakula watahitaji tani 3,549 za chakula cha bei nafuu haraka.

Mvua Kubwa Yaangamiza Maisha ya Watu 4

0
0

WATU wanne wakiwamo watatu wa familia moja ambao ni wakazi wa Kijiji cha Isighu kitongoji cha Majumba Sita wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wamekufa maji baada ya makazi yao kusombwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia Januari 31.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wilayani hapa, Dk Said Mawji amekiri kupokea miili ya watu wanne na majeruhi wawili.

Dk Mwaji aliwataja waliokufa kuwa ni Maritha Mabula (60), Shukuru Donald (15) mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mwana Kianga na Bernadeta Mabula(7) mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Ilolo na mwingine ni Jeska Lubeleje (19) mkazi wa Kijiji cha Chinyika katika Kata ya Vighawe.

Aliwataja majeruhi wawili waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni Beka Mlami na Joseph Sumisumi. Aidha, alisema kwamba majeruhi wametibiwa na kuondoka.

Alieleza kuwa katika ajali hiyo, mmoja wa watoto walionusurika na kifo Beca Mrami (10), alisema maji yaliingia ndani ya nyumba na akalazimika kukimbilia darini na ndugu yake, lakini walipoona yamezidi walikimbia wakimwacha bibi yao na dada zake.

“Mimi nilipoona maji yanazidi nikawaambia tukimbie, lakini bibi na akina dada walibaki ndani; mimi na Mandili (Joseph Sumisumi ) tulipanda juu ya paa baada ya nyumba kuanguka nilikimbia na kuwaacha ndani,” alieleza mtoto huyo.

Mzee wa kaya hiyo, Mabula Sumisumi, alisema hakuwapo katika mji huo siku hiyo alienda kulinda mifugo kambini ndipo alipoambiwa familia yake imesombwa na maji.

Hata hivyo, Sumisumi alisema kila kitu kilichokuwamo ndani kimesombwa na maji ikiwamo akiba ya chakula na fedha kiasi alizokuwa amehifadhi ndani ya nyumba ambazo hakuzitaja kiasi chake.

Shuhuda wa tukio hilo, Simon Kazimoto alisema nyumba hiyo imesombwa kutokana na kuwa ilijengwa kwenye mkondo wa maji na kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea umesababisha maji kutawanyika na kuingia katika makazi ya watu na kusababisha vifo.

Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Said Kilungo alisema kwa hatua za awali zilizochukuliwa na serikali ni kuhifadhi maiti kwa kugharamia jeneza na sanda kwa kila maiti baada ya hapo hatua zaidi zitafuata. Kilungo aliwataka wananchi wa kitongoji hicho kuhama katika maeneo hatarishi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa.

Pamoja na mvua hiyo, kusababisha vifo vya watu wanne, lakini tayari baadhi ya miundombinu ya Wilaya ya Mpwapwa iko hatarini kusombwa na maji, ikiwamo daraja la Tanesco na daraja la kwenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Hii Ndio Wizara Nyingine Kubwa Inayofuata Kuhamia Dodoma..!!!

0
0

WAKATI Wizara ya Katiba na Sheria ikiingia rasmi katika ofisi zake mpya mjini Dodoma jana baada ya kuhamia mwishoni mwa wiki, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nayo imetangaza kuhamia mjini humo wiki mbili zijazo, huku ikiwatoa hofu watumishi wanaohamia huko kwa kuwataka kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mathew Mtigumwe jana aliwaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuwa suala la kuhamia Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

Alitoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu kilicholenga kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea kuhamia makao makuu ya nchi, Dodoma.

Alisema awamu ya kwanza ya uhamisho utahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia Februari 14 na 15, mwaka huu huku wengine 47 watahamia muda wowote kati ya mwezi huu na Juni mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amezindua rasmi ofisi za wizara Dodoma na kuwataka watumishi waliohamia kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Makao Makuu ya wizara hiyo yaliyozinduliwa yapo katika Chuo Kikuu cha Dodoma na tayari watumishi wa wizara hiyo 31 wamehamia rasmi wakiongozwa na Dk Mwakyembe, Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju.

Awamu ya pili ya tatu zinatarajiwa kufuata utaratibu uliowekwa na kufikia mapema mwakani, watumisho wote wa wizara hiyo watakuwa wamehamia Dodoma.

Baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa mwelekeo wa kuhamia makao makuu ya nchi kwa makatibu wakuu, manaibu wao pamoja na mawaziri na manaibu wao ifikapo Februari 28, mwaka huu, tayari wizara kadhaa zimehamia ikiwemo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyohamia wiki iliyopita.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images