Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Pitia Vichwa vya Magazeti ya Leo 1/2/2017


Shule 6 Dar Hoi Matokeo Kidato cha Nne

0
0

WAKATI Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) likitangaza matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2016 na kuonesha ufaulu wa jumla kwa watahiniwa wa shule umeongezeka kwa asilimia 2.44, idadi ya watahiniwa waliopata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tano imekuwa chini kwa miaka mitatu mfululizo.

Matokeo ya mtihani uliofanyika Novemba, 2016 na kutangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, yanaonesha watahiniwa wa shule 244,762 ambayo ni asilimia 70.35 ya waliofanya mtihani walifaulu mtihani huo.

Ufaulu huo unaonesha kuongezeka kwa asilimia 2.44 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015 ambayo wanafunzi 240,996 ambao ni asilimia 67.91 walifaulu na kwa mwaka 2014 walikuwa ni 169,642 (asilimia 69.76) na mwaka 2013 walikuwa ni 201,152 ambao ni asilimia 57.09.

Jumla ya watahiniwa 408,372 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2016, wakiwemo wasichana 209, 456 sawa na asilimia 51.29 na wavulana 1998, 916 (asilimia 48.71).

Kati yao wote waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 355,822 na wa watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 52,550. Ufaulu kwenda Kidato cha V Pamoja na ufaulu huo kuongezeka, inaonesha kuwa watahiniwa wanaopata madaraja yanayoweza kuwafanya wakaingia kidato cha tano (daraja la I-III), inaonekana kuwa chini ya asilimia 50.

Kwa matokeo ya mwaka jana, watahiniwa 96.018 ambao ni asilimia 27.60 wamepata daraka la I-III, wakati mwaka 2015 walikuwa ni 89,929 ambayo ni asilimia 25.34 na mwaka 2014 walikuwa ni 73,832 ambao ni asilimia 30.72.

Watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 32,521 sawa na asilimia 68.19. mwaka 2015 walikuwa ni 31,1951 sawa na asilimia 64.80, hivyo ufaulu kuongezeka kwa asilimia 3.39. Kwa upande wa maarifa, watahiniwa 8,751 sawa na asilimia 50.48 wamefaulu, mwaka 2015 watahiniwa 7,536 ambao ni asilimia 46.63 hivyo kuwapo ongezeko ya ufaulu kwa asilimia 3.85.

Kuhusu ufaulu wa masomo unaonesha kuwa masomo ya Historia, Jiografia, Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Fizikia, Biolojia, Commerce na Book-Keeping umepanda kwa asilimia 0.12 na asilimia 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Watahiniwa wanaonekana kufanya vizuri zaidi kwenye somo la Kiswahili ambapo ufaulu wake ni asilimia 77.75 ya watahiniwa wote, ingawa ufaulu huo umeonekana kushuka ukilinganisha na mwaka 2015 uliokuwa ni asilimia 77.63 na mwaka 2014 ulikuwa asilimia 69.66.

Aidha, watahiniwa wameshindwa kufanya vizuri katika somo la Hisabati ambalo pamoja na kuonekana ufaulu umeongezeka waliofaulu somo hilo ni asilimia 18.12 ya watahiniwa wote wa shule, mwaka 2015 walikuwa ni asilimia 16.76 na mwaka 2014 ilikuwa ni asilimia 19.58.

“Pamoja na asilimia ya ufaulu wa jumla kuendelea kuimarika, takwimu zinaonesha kuwa bado ufaulu wa masomo na watahiniwa waliopata daraja la I-III ni chini ya asilimia 50, hivyo juhudi za makusudi zinahitajia kuendelea kufanya ili kuinua kiwango cha ufaulu wa masomo na kuongezeka kwa idadi ya watahiniwa kwenye madaraja ya ufaulu,” alisema Dk Msonde.

Shule za binafsi vinara

Kuhusu upangaji wa matokeo kwa shule zenye wanafunzi zaidi ya 40, unaonesha shule za watu binafsi na mashirika ya dini zimeendelea kufanya vizuri katika nafasi za 10 bora kitaifa huku zile zinazomilikiwa serikali zikiendelea kufanya vibaya kwa miaka mitatu mfululizo.

Shule 10 Bora ni Feza Boys (Dar es Salaam), St Francis Girls (Mbeya), Kaizirege Junior (Kagera), Marian Girls, Marian Boys na St Aloysius Girls (Pwani), Shamsiye Boys (Dar es Salaam), Anwarite Girls (Kilimanjaro), Kifungilo Girls (Tanga) na Thomas More Machrina (Dar es Salaam).

Aidha, Mkoa wa Dar es Salaam umezorota kielimu baada ya kuwa na shule sita kati ya 10 zilizoshika nafasi za mwisho. Shule hizo ni Kitonga na Nyeburu (Dar es Salaam), Masaki (Pwani), Mbopo, Mbondole na Somangila Day (Dar es Salaam), Dahani (Kilimanjaro), Ruponda (Lindi), Makiba (Arusha) na Kidete (Dar es Salaam).

Mikoa iliyofanya vizuri katika nafasi ya 10 bora ni Njombe, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Pwani, Ruvuma, Shinyanga, Tabora wakati halmashauri 10 bora ni Bukoba Mjini, Njombe Mjini, Kakonko, Kahama Mji, Wanging’ombe, Ilemela, Iringa Mjini, Mkuranga, Igunga na Kibaha Mji.

Ufaulu kwa watahiniwa 10 bora waliofanya vizuri kitaifa unaonesha kuwa ni asilimia 50-50 kwa wavulana na wasichana huku mwaka 2016 wakiongozwa na mvulana. Mwaka 2015, watahiniwa wa kike walikuwa ni wanne na wavulana sita na mwaka 2014 walikuwa na uwiano sawa, lakini waliongozwa na mwanafunzi wa kike.

Mvulana aongoza, msichana achomoza

Kwa 2016, watahiniwa 10 bora ni Alfred Shauri (Feza Boys), Cynthia Mchechu (St Francis Girls), Erick Mamuya (Marian Boys), Jigna Chavda (St Mary Goreti), Naomi Tundui (Mariam Girls), Victoria Chang’a (St Francis Girls), Brian Johnson (Marian Boys), Esther Mndeme (St Mary’s Mazinde Juu), Ally Koti (ALCP Kilasara) na Emmanuel Kajege (Marian Boys).

Watahiniwa wasichana 10 bora ni Cynthia, Jigna, Naomi, Victoria, Esther, Christa Edward (St Francis Girls), Nelda John (Marian Girls), Mariana Shabani (Kifungilo Girls), Beatrice Mwella (St Mary’s Mazinde Juu) na Rachel Kisasa (Canossa).

Wavulana 10 bora kitaifa ni Alfred, Erick, Brian, Ally, Emmanuel, John Ng’hwaya (Nyegezi Seminary), Clever Yohana (Livingstone Boys Seminary), Desderius Rugabandana (Morning Star), Kennedy Boniface na Assad Msangi (Feza Boys).

126 wafutiwa, 40 matokeo yazuiwa

Katika hatua nyingine, Dk Msonde alisema Necta limezuia matokeo ya watahiniwa 33 waliopata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani katika baadhi ya masomo, pia matokeo ya watahiniwa 124 waliopata matatizo ya kiafya na kufanya masomo yote, watahiniwa wamepewa fursa ya kufanya mitihani wa Kidato cha Nne 2017.

Alisema pia baraza limezuia matokeo ya wanafunzi 40 wa Shule ya Sekondari ya Hellens wanaodaiwa alama endelevu hadi hapo mkuu wa shule atakapowasilisha alama hizo huku likifuta matokeo ya watahiniwa 126 waliobainika kufanya udanganyifu akiwamo mmoja aliyeandika matusi katika karatasi ya majibu.

Kati ya waliofutiwa matokeo 58 ni wa kujitegemea na 58 ni wa shule, 10 watihani wa maarifa. Mvulana kinara anena Akizungumza na gazeti hili, mwanafunzi bora kitaifa, Alfred Shauri alisema siri ya mafanikio yake ni bidii na kumtanguliza Mungu.

Alfred ambaye pia amefanya vizuri kwenye insha ya Afrika Mashariki alisema: “Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufikia ndoto yangu ya kufanya vizuri na nitaendelea kufanya bidii kwenye masomo, ingawa kufanya vizuri kidato cha nne haikupi njia ya kufanya vizuri kwenye mitihani ya elimu ya juu kama hujitumi.”

Kijana huyo ambaye ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto wanne, anasema pamoja na wazazi wake kumtaka kufanya masomo ya sayansi ili kuwa mhandisi, ingawa anapenda fani hiyo, lakini angependa kujikita zaidi katika kuwekeza kwenye biashara na ujasiriamali. Mama yake Alfred, Adela Shauri pamoja na kumpongeza mwanawe, alisema mtoto wake ni kijana mwenye upendo na huruma ambaye anapenda kujibidisha kwenye masomo au kwa kile anachikifanya.

“Yaani mpaka nimetetemeka niliposikia haya matokeo, lakini niseme ni mtoto mwenye bidii katika masomo na anayemtangulia Mungu katika kila jambo. Niwaombe wazazi wenzangu kuhakikisha tunawalea watoto wetu wakiwa na hofu ya Mungu, kwani peke yetu hatutaweza,” alisema.

Kwa upande wa mwanafunzi aliyeshika nafasi ya pili kitaifa na akiwa ni mwanafunzi bora kwa upande wa wasichana, Cynthia Mchechu alisema: “Mpaka sasa siamini haya matokeo, natamani kama nikalale hivi. Lakini nashukuru sana Mungu, kwani bidii katika masomo ndiyo imemfanya kufikia hapo.”

Msichana bora haamini

Cynthia anawashauri wanafunzi wenzake kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kwa kujibidiisha na kuhakikisha wanakamilisha kile wanachotaka kupata katika maisha.

Naye Mercy Mchechu, mama mzazi wa Cynthia ambaye ni mtoto pekee wa kike kwake na mumewe Nehemia Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), anasema mwanawe amekuwa na juhudi ya masomo tangu akiwa anasoma shule ya awali na msingi Rightway ya Dar es Salaam ambayo yeye ndiye mkurugenzi wake.

“Ni binti ambaye ana bidii katika masomo na ana uwezo wa kutambua kile anachokitaka maishani na akaweza kutekeleza,” alisema Mercy.

Siku 153 za Ukimya na 30 za Wapinzani Kupaza Sauti

0
0

JUNI 23 mwaka jana, Rais John Magufuli alipokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kutoka kwa Mwenyekiti (mstaafu) wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva.

Hafla ya kuipokea ripoti hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli akazungumzia masuala tofauti ikiwapo kusitisha shughuli za kisiasa hususani mikutano ya hadhara na maandamano.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli akasema ni wakati wa ‘hapa kazi tu’, hivyo wananchi waachwe wafanye kazi pasipo kuingiliwa na masuala ya siasa, wakati Serikali yake ikitekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu huo.

Hoja nyingi zilitolewa kumsifu na kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua hiyo, kama ilivyokuwa kwa wakosoaji wake walioelezea kukandamizwa kwa misingi ya demokrasia.

Lakini tangu Rais Magufuli apige marufuku mikutano ya hadhara, kisha kutolewa kwa tamko la jeshi la polisi hakuna chama ama mwanasiasa aliyekiuka maagizo hayo, isipokuwa kwa kufanya vikao vya ndani kwa chama husika.

Kutoka Juni 23, mwaka jana Rais Magufuli alipotoa tamko la kuzuia shughuli hizo za siasa, hadi Desemba 23 mwaka jana ilipoanza mikutano ya kampeni za udiwani ikawa takribani siku 30 zilizotoa mwanya kwa wanasiasa wa upinzani angalau kuwa huru kwenda sehemu tofauti za nchi wakishiriki na kuhutubia mikutano ya hadhara.          

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akasema ulikuwa ni wakati muafaka kwa wapinzani kuzitumia kampeni hizo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi masuala ya kitaifa, kwa vile zilipofikia ukomo wake Januari 21, mwaka huu, wangerudi kwenye ukimya kwa maana hapatakuwa na mikutano ya hadhara.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, anathibitisha kuwa agizo la Rais Magufuli na hatua ya polisi kusitisha mikutano ya hadhara ya kisiasa litaendelea kufuatwa baada ya uchaguzi wa udiwani wa marudio wa ubunge katika jimbo la Dimani kufanyika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akakaririwa akisema ukimya wa wapinzani unaotokana na maagizo hayo hauwaathiri wanasiasa pekee bali jamii nzima kwa vile inanyimwa uhuru wa kujieleza.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anasema kampeni za udiwani na ubunge zilitoa mwanya wa uhuru katika kufanyika kwa mikutano ya hadhara isiyoweza kuzuiwa.

Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria, akasema ni kutokana na hali hiyo wanasiasa hasa wa upinzani walizitumia kampeni za uchaguzi huo kuzungumzia masuala tofauti hususani matatizo yanayolikabili Taifa.

MIKUTANO YA NDANI
Mara kadhaa, viongozi wa upinzani akiwamo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Ed-ward Lowassa, wamekuwa wakiisifu kuwa ni yenye kuwaimarisha na kuwajenga zaidi.

Hoja hiyo inaungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, akisema mikutano ya ndani bado inawanufaisha kwa vile inatumuka kuikosoa Serikali na ujumbe kuwafikia wananchi.

Hata hivyo, Mtatiro anaamini kuwa pamoja na katazo la Rais Magufuli na polisi kuhusu mikutano ya hadhara, mabadiliko ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano yanawawezesha (wapinzani) kufikisha ujumbe kwa jamII Pana kama inavyofanyika katika nchi nyingine duniani.

“Tunaweza hata kutumia mitandao ya kijamii na hizi kampeni za uchaguzi mdogo kufikisha ujumbe kwa umma. Sioni kama kuna njia mtu anaweza kuitumia kwa sasa kuvizuia vyama vya upinzani kuzungumzia matatizo ya wananchi,” akasema.

Lakini wapo wanasiasa wanaoamini kwamba kuwapa wapinzani fursa ya kuzungumza na kusikika kwenye jamii, kunasaidia kuyajadili na kupata mawazo mapya ya kukabiliana na kero zilizopo nchini.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo, anasema wapinzani wanapozuiwa kutoyazungumzia matatizo ya nchi ni sawa na kuashiria kutohitaji kadhia hizo kujulikana na kusikika.

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, akasema hakuna haja ya kuwazuia wapinzani kufanya shughuli za siasa hususani mikutano ya kampeni kwa vile baadhi ya mambo yanayotekelezwa na Serikali, yamo kwenye ilani ya uchaguzi.

Sumaye anasema masuala yaliyopo kwenye ilani ya Chadema ya mwaka jana, hayana athari kwa Taifa na ndio maana miongoni mwa hayo yanatekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.          

MIKUTANO ILIVYOZUIWA
Rais Magufuli alitoa kauli ya kupiga marufuku mikutano ya wanasiasa alipokuwa akizungumza Ikulu Dar es Salaam, baada ya kukabidhiwa ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Niwaombe wanasiasa wenzangu wafanye siasa za ushindani kwa nguvu zote baada ya miaka mitano ili wananchi watuhoji tuliyoyaahidi kama tumeyatekeleza au hatujayetekeleza,” akasema.

Rais Magufuli alisema hatua hiyo ni sahihi kwa vile hata nchi zilizobobea kwenye misingi ya demokrasia (hakuzitaja), haziendelezi siasa baada ya uchaguzi na badala yake kuwekeza katika kufanya kazi.

Akasema, “haiwezekani mkawa kila siku ni siasa watu watalima saa ngapi, kila siku ni siasa, ni vema tukatimiza wajibu wetu tuliopewa na wananchi na watatupima kwenye hilo.”

Rais Magufuli akaelezea matumaini yake kuwa Watanzania wanachokihitaji kwa wakati huu ni maendeleo.

Rais Magufuli akasema katika kampeni za 2015, aliahidi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo asingependa kuona mtu yeyote anamchelewesha katika utekelezaji.

USHAURI
Rais Magufuli akashauri kuwa kama kunan hitaji la kuwapo mikutano ya hadhara, isiwe kwa wanasiasa wakiwamo wabunge kutoka majimbo mengine kwenda kuungana na mbunge wa jimbo husika kuwahutubia wananchi.

Badala yake akasema kila mbunge na diwani anapaswa kufanya mkutano ndani ya eneo lake la uwakilishi. Akatoa mfano akisema, “kama ni madiwani wakapeleke hoja kwa nguvu zote kwenye maeneo yao, kama ni wabunge wakazungumze kwa nguvu sana bungeni lakini hata kuziba midomo nayo ni demokrasia, hiyo ni demokrasia ya mwelekeo wa ya aina yake.”

KUSHIRIKIANA NA WAPINZANI
Rais Magufuli akasema Serikali yake imeamua kufanya kazi kwa kushirikiana na vyama vyote vya
siasa ili kuchagiza kasi ya kutatua kero za wananchi.

Katika kuthibitisha hilo, akasema atashirikiana na wanasiasa katika changamoto ambazo utatuzi wake utasaidia kulijenga taifa.

Kinara wa Kidato cha Nne Nchini Afichua Siri ya Kufanya Vizuri,Adai ni Mungu na Wazazi Tu..!!!

0
0
Mwanafunzi wa kwanza katika matokeo ya kidato cha nne nchini kutoka shule ya Sekondari ya Feza Boys jijini Dar es Salaam, Alfred H. Shauri (katikati) akielelzea siri ya mafanikio yake kwa wanahabari.

MWANAFUNZI wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2016, Alfred H. Shauri, ameeleza siri ya mafaniko yake kuwa ilitokana na kusoma kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika kila alichofanya.

Akizungumza na wanahabari katika Shule ya Sekondari ya Feza Boys alikosoma eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam, amesema kitu cha  kwanza katika kila alilofanya ni kumtanguliza Mungu katika masomo yake na cha pili alikuwa sambamba na wazazi wake kuhakikisha anachukua ushauri wao juu ya masomo yake ambapo kwa uapnde wa walimu wake alisema aliwasikilza kwa makini na kuwauliza maswali pale alipokuwa akihitaji msaada na kujisomea vitabu mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus,  alisema kuwa mafaniko ya mwanafunzi huyo yametokana na juhudi zake mwenyewe alizokuwa nazo wakati akiwa shuleni hapo kwani aliweza kuwa wa kwanza pia katika shindano la insha  iliyozikutanisha shule za Afrika Mashariki mwezi Mei mwaka jana.

Umoja wa Afrika Kujiondoa Katika Mahakama ya ICC..!!!!

0
0

Umoja wa Afrika umeunga mkono mpango wa kujiondoa kwa pamoja katika mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya Afrika yanahisi inawalenga viongozi wa Bara la Afrika pekee.

Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo.

Viongozi wa Afrika wanasema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Mpango huo unapendekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki za binaadamu.

CHANZO: BBC SWAHILI

Misri Kujenga Viwanda vya Dawa Tanzania

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi ambaye amekubali nchi hiyo kuja kujenga viwanda vya dawa nchini.

Katika mazungumzo hayo ambayo ni kando ya Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika uliomalizika jana Mjini Addis Ababa Nchini Ethiopia viongozi hao wamezungumzia namna nchi hizo zitakavyoshirikiana katika nyanja mbalimbali zikiwemo afya, kilimo, mifugo na viwanda.

Pamoja na kukubali mwaliko wa Rais Magufuli wa kufanya ziara rasmi nchini Tanzania, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi pia amekubali ombi la kuwaleta wataalamu na wawekezaji wa Misri nchini Tanzania ili wajenge viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba vya binadamu, kuinua teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji, kuwekeza katika viwanda vya nyama na viwanda vingine ambavyo nchi hiyo imepiga hatua kubwa.

“Mhe. Rais El-Sisi nakupongeza sana kwa juhudi zako za kuijenga Misri na nitafurahi sana kuona biashara ya Tanzania na Misri inaongezeka maradufu kwa manufaa ya pande zote mbili” amesisitiza Mhe. Dkt Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli pia amekutana na amekutana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambapo viongozi hao wamezungumzia miradi mbalimbali ya ushirikiano na fursa za biashara ambazo Tanzania na Uganda zinaweza kuzitumia kujiongezea mapato. Mhe. Rais Museven amekubali kufanya ziara nchini Tanzania katika siku za karibuni.

Habari Picha:Rais Magufuli Alivyorejea Tz Kutoka Ethiopia..!!!

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege  katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017. Mbele yake ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Martin.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan va viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017



aw7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Inspecta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu  baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
aw9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt Juma Malewa   baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
aw1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan va viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
aw3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilsalimiana na baadhi ya wafayanyazi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipowasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
aw4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilsalimiana na baadhi ya wafayanyazi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipowasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
aw5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi mikono alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017

Baada ya MwanaHALISI Kumuomba Radhi Rais Magufuli,Serikali Yachukua Hatua Hii Dhidi ya Gazeti Hilo..!!!


Exclusive:Makampuni Yamiminika Kudhamini 40 ya Mtoto wa Diamond..!!!

0
0

Watoto wa Diamond Platnumz huzaliwa wakiwa na harufu za ustaa unaotoka kwa baba na mama yao, Zari The Bosslady. Wakati Tiffah akiendelea kushikilia taji la mtoto staa kuliko wote Afrika, mdogo wake Nillan yuko nyuma kufuata nyayo zake.

Makampuni takriban matano yamejitokeza kudhamini sherehe za Nillan kutimiza siku 40, ambapo kwa mara ya kwanza sura yake itaoneshwa. Sherehe hizo zitafanyika wiki moja ijayo.

Nimekusogezea Picha za Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama Akila Raha na Mkewe Katika Kisiwa cha British Virgin Livee..!!!

0
0

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanaendelea na mapumziko yao huko British Virgin Islands, na Jumanne hii waliungana na mwenyeji wao, bilionea wa Uingereza, Richard Branson.

Obama na mkewe walisafiri kutoka Palm Springs walikokaa siku za wikiendi kwenda kwenye visiwa hivyo kwenye private jet ya Branson.


Wawili hao wanaaminika kuwa wamefikia kwenye moja ya visiwa vinavyomilikiwa na bilionea huyo.

Hamorapa Jeuri Hii Umeitoa Wapi...!!!!?

0
0

DAR ES SALAAM: Akiwa bado anaendelea kutrendi kwa kuitwa ‘Nyani’ katika mitandao ya kijamii, msanii wa kizazi kipya anayefananishwa na msanii kutoka kundi la WCB Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, Athuman Omary maarufu kama Hamorapa leo katika mitandao ya kijamii mashabiki wameibuka na kusema kuwa Hamorapa ametumwa.

Kwa habari ambazo bado hazijathibitika zinadai kuwa Hamorapa anatumiwa na wafanyabiashara wakubwa jiji Dar es salaam, inaonekana wazi kuwa hana uwezo wa kujieleza na anafundishwa jinsi ya kujibu maswali katika mahojiano mbalimbali. Pia hivi karibuni ameonekana katika mitandoa ya kijamii kuweka picha na video zinazomonyesha akiwa napesa nyingi na kazi anayofanya haijulikani.

Akihojiwa na Global Tv mwezi jana, Hamorapa alionekana wazi kuwa ni mtu asiyeweza kujieleza.

Ubuyu wa Moto Moto...!! Kumbe Ray na Chuch Hans Wameshafunga Ndoa Kitambo,Chuch Amefunguka Yiote Hapa Livee..!!!

0
0

KATIKA kila kinachotokea kwa staa kuna mengi huwa yanazungumzwa, mfano mzuri ni baada ya msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans ambaye siku chache zilizopita alibahatika Vicent Kigosi ‘ Ray’ ambapo Gazeti la Championi limepata nafasi ya kuzungumza na Chuchu ambaye ni muigizaji wa fi lamu kama alivyo baba watoto wake na hivi ndivyo anavyofunguka:

Championi: Mambo mama Jaden, vipi mtoto anaendeleaje?

Chuchu: Sote ni wazima wa afya.

Championi: Ni kitu gani kilichosababisha ukafi cha ujauzito, inasemekana ulikuwa unahofi a kulogwa, ni kweli?

Chuchu: Siyo kweli, sikuona kama kuna haja ya kutangaza hicho kitu, ni mambo yangu binafsi hata kama mimi ni staa kuna vitu havihitaji matangazo.

Championi: Ulipanga na Ray mpate mtoto kipindi hiki au ilitokea tu?

Chuchu: (Anacheka),  Usawa huu hamna mimba ya bahati mbaya ni kitu ambacho tulikusudia.

Chuchu: Je, ulipendelea kumzalia Ray mtoto wa kiume kama ilivyotokea?

Chuchu: Mimi sibagui mtoto, yeyote naona sawa, ila baba yake alipenda sana tupate mtoto wa kiume na Mungu kasikia dua yake, ndiyo maana amefurahi kupita maelezo.

Championi: Baada ya kujifungua, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye ni mkurugenzi mwenziye na Ray pale RJ Company, je ameshakuja kumuona mtoto, japo kipindi cha nyuma mlikuwa kwenye mgogoro kwa kuwa inasemekana aliwahi kuwa kwenye uhusiano na Ray ukampindua?

Chuchu: Siwezi kumuongelea Johari kwenye hilo kama kaja kumuona Jaden au la, sababu siyo sehemu ya familia yangu, tuongee mengine, sioni haja ya kumzungumzia.

Championi: Kuna mengi yalisemwa wakati mnaanzisha uhusiano wenu na Ray, hadi kipindi cha ujauzito wako kulikuwa na tetesi za hapa na pale kuwa mimba hiyo siyo ya Ray, uliamini pamoja na yote hayo mngefi ka hapa mlipo leo?

Chuchu: Niliamini tungedumu na tangu tunaanza tulikuwa na malengo mengi, likiwemo hili la kupata mtoto na kufunga ndoa, vitu vingine watu huwa wanazusha hatukuwa na mgogoro wowote.

Championi: Hizi taarifa za kufunga pingu za maisha na Ray zina ukweli upi na kwa nini mlifunga ndoa kimyakimya na hiyo ndoa ilifungwa lini na wapi?

Chuchu: Ni ukweli mtupu kwamba sisi ni wanandoa, tulifunga ndoa ya siri sababu huwa hatupendi kuanika mambo yetu hadi tuamue, muda ukifi ka kila kitu kitakuwa wazi maana bado hatujafanya sherehe.

Championi: Mambo ya malezi yanakuathiri vipi kwenye kazi zako na je, utapumzika kwa muda gani kuigiza?

Chuchu: Hayaniathiri chochote, likitokea dili lolote mtoto akishatoka 40 nitamuachia baba yake amlee, si unajua siku hizi mambo kusaidiana.

Championi: Nini malengo yako kwenye sanaa kwa mwaka huu, baada ya mwaka jana kutwaa tuzo ya msanii bora wa kike iliyoandalia na kituo cha EATV?

Chuchu: Malengo yangu ni makubwa mno, mashabiki watarajie kuniona kwenye kiwango cha juu zaidi, sababu familia imeongezeka lazima nichape kazi ipasavyo.

Championi: Unapenda mtoto wako akue kwenye mazingira yapi, awe msanii kama wewe ama?

Chuchu: Siwezi kumpangia, kikubwa naomba Mungu awe ni mtoto mwema kwa sisi wazazi wake na kwenye jamii pia.

Championi: Kwa upande wa soka unashabikia timu gani na nini kilikushawishi?

Chuchu: Naipenda sana Yanga kwa kuwa mume wangu ni shabiki mkubwa wa timu hiyo, ikifungwa amani yote huwa inatoweka nyumbani.

Mbwana Samatta Aumia Genk Ikipoteza Mbele ya KV Oostende

0
0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta wa klabu ya KRC Genk amejikuta katika wakati mgumu usiku wa Jumanne hii wakati timu yake ya KRC Genk ilipokuwa ikicheza na KV Oostende katika mchezo wa kombe la Ubelgiji.

Samatta aliumia katika daika ya 23 na kulazimika kutolewa nje ya uwanja na kumpisha Jose Naranjo ambaye alikosa p3enati katika mchezo huo.

Katika mchezo huu ambao Genk walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena walijikuta wakipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya KV Oostende na kutolewa katika kombe hilo huku goli hilo likifungwa dakika ya nane na Knowledge Musona ambaye ni raia wa nchini Zimbabwe.

Umeisikia Hii ya Vanessa Mdee,Afunguka Siri ya Mafanikio Yake..!!!

0
0

Msanii wa muziki Vanessa Mdee amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mmoja kati ya wanawake ambao wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha maisha yake yanaenda sawa.

Akiongea katika kipindi cha Wanawake Live cha EATV wiki hii, Vanessa amedai yeye ni mwanawake ambaye wanafanya kazi kwa bidii huku akidai tayari amejipangia ratiba ya kazi zake mpaka mwezi wa nne.

“Mimi nafanya kazi kama kichaa, kwa sababu kuna vitu ambavyo najua natakiwa nivitimize kwa muda fulani. Kwa hiyo najua nikivitimiza, nitakuwa na pesa ya kushoot video, pesa ya kuwekeza kwenye ardhi, na kupendeza kwa saababu kupendeza ni moja kati ya njia ya kuwekeza kwenye brand,” alisema Vanessa.

Aliongeza, “Lakini hayo yote hayaji bila kufanya kazi kwa bidii, kwa sababu mimi ratiba yangu kwa sasa ipo full mpaka mwezi wa nne, nimeshapanga kila kitu ambacho nitafanya kwa kipindi hichi,”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Cash Madame’.

Serikali Yaeleza Hatua Iliyofikiwa Kuhusiana na Walimu Waliompiga Mwanafunzi Mbeya

0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametolea ufafanuzi kuhusu hatua inayochukuliwa na vyombo vya dola dhidi ya watu wanaohusika na vitendo vya unyanyasaji vikiwemo kupiga watu.

Naibu waziri huyo ametoa ufafanuzi huo Jumatano hii mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.

Mbilinyi aliuliza, “Kumekuwa na tabia za watu kupiga watu wengine, vipigo ambavyo vinafikia kiasi cha utesaji matukio kama yaliyotokea Mbeya Day sekondari kwa mwalimu kumshambulia mwanafunzi lakini na lile la mtu kumtoa macho mwingine tukio lililotokea kule Buguruni, Je, Serikali inachukua hatua gani kwa watu wanaowapiga wenzao bila sababu?”

Mheshimiwa Masauni alijibu, “Ni kweli hivi karibuni kumekuwa na vitendo vya kusikitisha katika nchi yetu na kwa jamii ambavyo ni kinyume na sheria na havikubaliki. Aidha serikali haikubaliani na vitendo vya namna hiyo vinavyofanywa na watu, mtu au kikundi kwani vitendo hivyo ni kinyume na sheria na utaratibu mzima wa haki za binadamu. Serikali kupitia jeshi la polisi imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ili kuzuia na kulinda raia na mali zao, aidha serikali kupitia jeshi la polisi tumepokea taarifa za matukio mbalimbali na kuyafanyia uchunguzi wa kina yanapobainika upo ushahidi wa kutosha mtuhumiwa huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.”

Aliendelea, “Nichukue fursa hii kuwaasa wale wote wanaokiuka taratibu, kanuni na sheria za nchi waache tabia hiyo mara moja wizara yangu haitakuwa na suluhu kwa mtu yeyote atakayetenda uhalifu huo.”

Ameongeza “Kuhusiana na suala la walimu ambao wamewanyanyasa wanafunzi kwenye shule ya Mbeya day, suala hili ni suala mtambuka kwahiyo ni hatua mbalimbali zinachukuliwa na mamlaka husika kwa upande wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na mkurugenzi wa mashtaka ni kwamba kuna hatua zinaendelea kuchukuliwa na pale ambapo uchunguzi utakamilika watafikishwa katika vyombo vya sheria.”

Ukiegesha Kiholela Gari Lako Dar, Adhabu Hii ni Halali Yako..!!!

0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo, amesema serikali haitasita kuchukua hatua kwa wote watakaokiuka utaratibu za maegesho ya magari katika jiji la Dar es Salaam, kwasababu kufanya hivyo ni kusababisha msongamano na kero kubwa kwa wengine.

Ufafanuzi huo umetolewa na naibu huyo wa waziri, mjini Dodoma katika mkutano wa sita wa Bunge. Akitoa ufafanuzi juu ya hatua zitakazochukuliwa na serikali juu ya watu wenye maduka wanaopaki magari yao kwa muda mrefu, alisema, “Sheria ndogo ya maegesho ya magari GN namba 60 ya mwaka 1998 kifungu cha (6) kifungu kidogo cha (1) inaipa mamlaka ya halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kudhibiti na kusimamia maegesho ya magari yaliyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ili kuondoa kero, usumbufu na msongamano katika mitaa na katika barabara za umma. Kwa mujibu wa sheria hiyo maegesho yote ya magari ya kulipia na maegesho yaliyohifadhiwa yatumike kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, baada ya muda huo maeneo hayo huwa huru kwa matumizi ya umma pale inapobainika mtu kuhodhi maeneo hayo baada ya kumi na mbili jioni, halmashauri ya jiji huchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza, “Kazi ya ukaguzi na udhibiti na maegesho imetolewa kwa mawakala katika jiji la Dar es Salaam, napenda kutoa wito kwa wamiliki wa magari kuacha kuegesha magari bila utaratibu hasa wakati wa usiku na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine. Serikali haitasika kuchukua hatua kwa wote watakao kiuka utaratibu za maegesho ya magari katika jiji la Dar es Salaam, kwasababu kufanya hivyo ni kusababisha msongamano na kero kubwa kwa wengine.”

Kudadeki..Eti Ng'ombe 150 Watachinjwa siku ya Birthday ya Mugabe...!!!!!

0
0

Chama kinachotawala nchini Zimbawe Zanu-PF, kimeanza kuchangisha pesa kwa sherehe za siku ya kuzaliwa ya Rais Robert Mugabe ambaye anahitimiza miaka 93.

Waandalizi wa sherehe hizo wanasema kuwa wanataka kuchangisha ng’ombe 150 kwa chakula.

Gazeti la serikali la Herald limemnukuu mbunge Never Khanye, akisema kuwa hakuna mtu atalazimishwa kuchanga lakini wakulima wakubwa katika maeneo ya matabeleland ambapo shehere zitafanyika, ni lazima watoe ngombe mmoja kila mmoja, kutoa asante kiongozi huyo wa miaka mingi.

Wakulima wakubwa ni wale walipata mashamba makubwa kutoka kwa serikali kufuata hatua ya serikali ya kunyakua mashamba kutoka wa wazungu wakati wa programu iliyokumbwa na utata nchini Zimbabwe.

Chama cha Zanu-PF kinasema kuwa kinatarajia karibu watu 100,000 kuhudhuria sherehe hizo.

Shere hizo zitafanyika eneo la Matobos nje kidogo ya mji wa Bulawayo.

Acha Papara, Usikubali Wakuachie Majuto..!!!

0
0

NINA hasira kama nini hapa mnaponiona, yaani nimevurugwa kabisa. Mwenyewe nilijua timu yangu ndiyo tunachukua ubingwa msimu huu, mara eti katimu hakana hata historia na huu mchezo kamekuja kutuvurugia. Tangu siku ile sijatoka ndani, maana jirani yangu alikuwa ameweka madebe barazani anapiga ananisubiri! Kama siyo shoga yangu Ma Muhaji kuja nidokeza kisa cha mke wa rafiki wa mwanaye wa kiume, basi nilitaka leo niahirishe hili somo, nikae zangu ndani niendelee kusikilizia maumivu, yanaumajeee!!

Basi, Mama Muhaji kaniambia, eti mke wa rafiki wa mwanaye kaondoka nyumbani kwa ngoma, yaani kajaza watu akimtukana mumewe, matusi makubwamakubwa na watu wanashangilia. Kijana wa watu, nasikia kakaa kimya ndani, kavumilia mvua ya matusi na dharau, mwisho wa siku huyo dada kachukua begi lake, akaondoka kwa mbwembwe, eti wataonana kuzimu! Sasa alichonishangaza shosti, eti huyo bi dada kakaa huko alikokaa wiki tatu tu, karudi anataka waendelee na maisha na kijana wa watu.

Kilichonifurahisha, mvulana kamwambia mkewe, yupo tayari kuendelea kuishi naye ili mradi tu, ajaze watu kama alivyofanya siku ile anaondoka, halafu awaambie kwa nyodo zilezile kwamba anataka kurudi! Fyuutu, unadhani aliweza, akaishia kulialia na hadi jana anaondoka hapa kwangu Ma Muhaji, hata hatujui nini kinaendelea, maana mjumbe kakataa kwenda kusuluhisha, majirani wote hawataki na marafiki ndiyo kabisaa, wenyewe kwanza wanaona aibu wakikumbuka shoga yao alivyokuwa akitamba kwa pozi siku ile! Sasa kwa sababu hiyo ndo nimeona acha niwape kidogo uzoefu, maana nyie wengine mnadhani kubadilisha wanaume, au kuwa wajeuri ndiyo mnaonekana wajanja.

Kwanza shurti mjue, siku zote, pamoja na uzuri walionao, shepu zao na hata majukumu yao, heshima ya mwanamke inatokana na mwanaume. Asikudanganye mtu, achilia mbali kuolewa, ile tu kuishi na mwanaume ndani, ni heshima tosha kwa mwanamke.

Ile inakuonyesha ni kwa kiasi gani wewe una baraka za Mwenyezi Mungu, kwa sababu kuna wanawake na uzuri wao, hakuna mwanaume anafikiria kuishi nao. Na wasikudanganye ukisikia wanasema hawana shida na mwanaume, ni waongo. Mwanamke na hata awe na hela vipi, anaweza kutoka kwenye jumba lake la kifahari, akamfuata mwanaume anayeishi mbavu za mbwa.

Ukimpata mwanaume, shikamana naye. Usije kufanya jambo kwa sababu ya kutaka sifa kutoka kwa mashoga. Kwanza katika hao mashoga wanaoshangilia unapomkosea adabu mwanaume wako, wangapi wanaishi na wanaume? Mwanamke anayeishi na mume, hawezi kukuunga mkono kwenye ujinga huo, labda na yeye awe hamnazo! Kitu kingine ambacho sisi wanawake tunakuwa hatujui ni kwamba wenzetu wanaume, hata waache wanawake mara ngapi, hata hawaonekani kuwa na dosari, lakini sisi sasa, eti umeachika mara tatu tu, nakuambia hata kosa si lako utaonekana wewe ndiyo tatizo! Ninachotaka mjue, kile kitendo tu cha mwanaume kukubali kukuweka ndani, ni heshima kubwa sana.

Kuna maelfu ya mashoga huko mitaani wameshindwa kuwapata, tena wadada wazuri, wanajiremba, wanavaa, lakini ndiyo wanaishia maisha ya klabu, kila mwanaume anaguna ukimuambia amuweke ndani! Cha msingi, ukimpata, kaa naye chini mrekebishane makosa, lakini jivunie kuwa naye! Kwa leo ni hayo tu mashosti, tukutane wiki ijayo ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu!

Wapinzani Kenya Wafuta Maandamano, Wazua Jipya..!!!

0
0

Kambi ya upinzani nchini Kenya imehairisha maandamano ya mtaani na badala yake imeamua kuweka mkazo katika kuwahamasisha wafuasi wao kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

Katika mkutano wao uliohusisha vyama 15, viongozi wa vyama vya upinzani wamesema hawatatumbukia katika mtego wa chama tawala cha Jubilee wa kuandamana kupinga sheria ya uchaguzi iliyopitishwa na bunge na kutiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta.

Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani nchini humo Rais Odinga, amemshutumu bila kumtaja jina, aliyewahi kuwa waziri nchini humo kwa kuendesha kile alichokiita mchezo mchafu katika zoezi la uandikishaji wapiga kura, ambapo amesema kuwa katika zoezi hilo kuna majina kuna vitambulisho vingi bandia (vitambulisho vya wapiga kura hewa) vinatengenezwa, ikiwa ni pamoja na kuandisha watu wasio raia

"Leo tuko hapa kudhihirisha kuwa IEBC inaandikisha watu wasio raia wa Kenya kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa mezi Agosti, 2017" Amesema Odinga huku akionesha namba za vitambulisho 19 vya watu anaodai kuwa hawana sifa

Hatimaye Askofu Mokiwa Amwaga Mboga,Aaanika A - Z Kinachoendelea kati Yake na Askofu Mkuu wa Anglikana Hadi Kufikia Hatua ya Kutaka Kumfukuza...!!!

0
0

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa amejibu tuhuma mbalimbali zikiwamo za wizi wa fedha zilizoelekezwa kwake, akidai ni uzushi wenye lengo la kumchafua ili aondolewe kwenye nafasi hiyo.

Mbali ya kujibu tuhuma hizo, Dk Mokiwa amedai mgogoro huo umezushwa kutokana na hofu ya uchaguzi wa askofu mkuu mpya mwakani na uongozi wa kutojiamini wa Askofu Mkuu, Dk Jacob Chimeledya.

Akizungumza na waandishi wa habari  waliofika ofisini kwake  kujua kiini cha mgogoro katika kanisa hilo ambao umesababisha Dk Chimeledya kumwandikia barua akimtaka ajiuzulu, Dk Mokiwa alisema mzozo uliopo katika kanisa hilo umetengenezwa na ‘wakubwa’ kwa kuwatumia mapadri wawili waliofukuzwa utumishi katika dayosisi ambao waliandaa mashtaka ili aonekane kuwa hafai na aondolewe.

“Ili niondoke, wakatengeneza mashtaka 10 wakitumia mapadri wawili ambao bahati mbaya nimewaondoa kwa utovu wa nidhamu,” alisema. “Kila shtaka lililotengenezwa dhidi yangu linafurahisha, linasikitisha, linachekesha kwa sababu malengo yake ni hatimaye Mokiwa aondolewe. Haya Askofu Mkuu wangu, Dk Chimeledya ameyaamini, ameyafanyia kazi, anaamini kabisa kwamba Mungu, Roho Mtakatifu amemtuma na huduma yake ya uaskofu mkuu itakuwa nzuri ikiwa mimi nitaondolewa kwa mashtaka hayo.”

Akijibu tuhuma moja baada ya nyingine kadri ilivyoandikwa katika mashtaka aliyopelekewa na Dk Chimeledya, Dk Mokiwa alisema: “Kuna shtaka eti nimezuia michango isiende jimboni. Hii ina sababu yake, kuna sheria katika katiba yetu inazuia dayosisi moja isivuke mipaka kwenda kufanya kazi katika dayosisi nyingine. Hapa kuna mwenzetu ametoka huko kwake anakuja kufungua makanisa hapa. Ni ukiukwaji wa katiba tu.”

Alitaja shtaka la pili kuwa ni madai ya kuitoa Dayosisi ya Dar es Salaam katika udhamini wa Kanisa la Anglikana Tanzania. Shtaka hilo linatokana na hoja ya dayosisi kutaka kutumia viwanja vyake katika uwekezaji na kwamba kiwepo kifungu cha kuwa na majadiliano katika uwekezaji huo.

“Hapa wanamaanisha kwamba nilitaka kujitenga niwe mwenyewe. Hata kama ningekuwa nimekula dawa fulani haiwezekani kwa sababu hii siyo taasisi yangu, kama ni kweli nataka kufanya hivyo basi nianzishe kanisa langu na mke wangu anifanye kuwa askofu,” alijibu.

Kuhusu ufujaji wa mali na kuingia mikataba mibovu, alisema havipo na kama ni mikataba iliamuliwa na sinodi na kamati ya dayosisi na kwamba, chombo hicho kina uwezo wa kurekebisha kama kuna makosa na tayari kimetengeneza kamati ya kupitia mikataba hiyo.

Ingawa mashtaka yalionyesha kuwa Dk Mokiwa alifuja mali za dayosisi, ushahidi wa nyaraka na taarifa za fedha za benki aliouweka wazi unaonyesha mapadri wawili walihusika katika akaunti zilizopo kwenye Benki ya Maendeleo, ACB (Benki ya Biashara ya Akiba) pamoja na DCB (Dar es Salaam Commercial Bank) iliyopanga katika jengo la dayosisi hiyo lililopo Magomeni.

Dk Mokiwa alisema kuna miamala inayoonyesha fedha zilikuwa zinaingizwa ACB tawi la Buguruni na kuna nakala za hundi zinazoonyesha fedha zikichotwa na kuingizwa kwenye akaunti binafsi za mapadri hao.

Alisema tangu aanze kazi kwenye dayosisi hiyo ameboresha taasisi alizozikuta na kuanzisha nyingine mpya ili kuinua mapato.

“Sipigi vita mafanikio, nataka maendeleo. Sijisifu ila kanisa hili nimelitoa kimasomaso. Sema tu nabii haheshimiki kwao,” alisema.

Dk Mokiwa alisema ushahidi kwamba mgogoro huo unapaliliwa na wakubwa ni baruapepe aliyodai kiongozi mmoja wa ngazi za juu alimwandikia mmoja wa mapadri waliofukuzwa Desemba 16, 2016 akimjulisha kuhusu tume iliyotumwa kumhoji Dk Mokiwa na kwamba timu nyingine inatumwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Mwezi uliopita, Dk Chimeledya alisambaza waraka kwa makanisa ya Anglikana Dar es Salaam uliomtaka Dk Mokiwa kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali. Hata hivyo, askofu Mokiwa ameutaka uongozi wa Anglikana Taifa kufuata Katiba.


Viewing all 104417 articles
Browse latest View live


Latest Images