Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live

Je Wajua Kwanini kila Unachokionja Baada ya Kupiga Mswaki Huwa na Ladha Mbaya..!!!

0
0

Toka ukiwa mdogo mpaka unazeeka umekuwa ukijiuliza kwanini kila kitu unachokula au kukionja huwa kinakuwa na ladha mbaya mara tu baada ya kusafisha kinywa chako kwa kutumia mswaki ulioweka dawa ya meno.

Dawa nyingi za mswaki huwa zinakemikali zifuatazo Sodium lauryl sulfate, sodium laureth sulfate (SLS) and sodium lauryl ether sulfate (SLES) ambazo hupunguza nguvu ya ukinzani ili kutengeneza povu (foaming action) kwenye dawa ya meno ili kusaidia katika kuondoa mabaki ya vyakula kwenye kinywa chako.

Lakini pia kemikali hizi hukinzana na utendaji kazi wa taste buds (huhusika na utambuzi wa ladha) kwa kuvunja vunja phospholipids kwenye ulimi wako. Matokeo yake husababisha ladha ya uchachu (bitter tastes) nahii ndo sababu kila unachokionja na kukila huonekana kibaya mara baada ya kusafisha meno yako.

Lakini hali hii huondoka mara tu baada ya mda mfupi. Niwatoe hofu watumiaji wa dawa za meno kuwa hali hii ya kuhisi uchachu haina madhara yeyote kiafya.

Your Health, Our Concern

Trump Amfanyia Umafya Waziri Mkuu wa Australia,Amkatia Simu na Kuutukana utawala wa Obama Kwenye Twitter..!!!

0
0

RAIS Donald Trump wa Marekani amemkatia simu Waziri Mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull wakati wakizungumzia makubaliano ya nchi hizo juu ya wakimbizi.

Mawasiliano hayo ya simu kati ya Rais Trump na Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.

Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani.

Australia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.

Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Marekani.

Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.

Alikiambia kituo kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za ukweli

Mtoto wa Mfalme Saudi Arabia Azua Gumzo, Asafiri na Mwewe 80 Kwenye Ndege

0
0

MTOTO wa Mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah bin Abdul Aziz azua gumzo baada ya kusafirisha ndege 80 aina ya mwewe kwa kutumia ndege.

Picha moja katika tovuti ya Reddit iliyotoka jana (Jumatatu) asubuhi, ilizua taharuki kwenye mtandao wa Intanet ambapo ilionyesha ndege 80 waliokuwa wakisafirishwa kwenye ndege wakiwa viti.

Hata hivyo, jambo hilo si la ajabu katika Mashariki ya Kati kuhusiana na kusafirishwa kwa ndege ambao Reddit walisema ni mwewe, lakini wakionekana kuwa ni vipanga.

Usafirishaji wa vipanga katika nchi za Mashariki ya Kati ni jambo la kawaida ambalo limefanywa kwa maelfu ya miaka ikiwa ni pamoja na kuwafundisha ndege hao kuwinda.  Ifahamike pia kwamba kipanga ni alama ya taifa ya Umoja wa Nchi za  Falme za Kiarabu (UAE), hivyo mashirika ya ndege yanayosafiri eneo hilo yanategemewa kutia maanani mahitaji ya ndege hao.

Mtumiaji mmoja wa tovuti ya Reddit amesema katika makala moja kwamba vipanga wanaweza kupewa pasipoti kutoka UAE na kuweza kusafiri kwenda Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, Pakistan, Morocco na Syria.  Hiyo ni kwa mujibu wa makala hiyo ambayo imeongeza kwamba pasipoti hiyo huwa inatumika kwa miaka mitatu.

Mwakilishi wa shirika la ndege la Flydubai alimwambia Frank Kane, mwandishi wa tovuti ya UAE ya ‘The National’,  kwmba vipanga lazima wawe na viti vyao kwenye ndege na kufungwa vitambaa maalum kuwaepusha na matukio ya ajali.

Vilevile, kwa mujibu wa mwandishi huyo, daraja maalum kwenye ndege (business class) la Flydubai mnamo Aprili 2015 lilitengwa maalum kwa vipanga, hivyo kufanya tukio hilo kuwa si la ajabu.

Katika daraja la kawaida la shirika la ndege la Qatar , mtu anaruhusiwa kusafirisha vipanga wasiozidi sita, hii pia inaruhusiwa katika shirika la ndege la Etihad.

Ukatili: Ulemavu wa Viungo Wasababisha Abakwe na Baba kwa Zaidi ya Miaka Miwili..!!!

0
0

BINTI ana miaka 19, hajiwezi kutokana na udhaifu wa mwili wake. Hawezi kutembea bila msaada wa watu angalau wawili, lakini baba yake aliona ndiye anayemfaa kukidhi tamaa zake za kimwili.

Kwa miaka miwili, mkazi wa Kijiji cha Kiwanja katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Lyimo Pesambili amekuwa akimwingilia kimwili binti yake wa kumzaa, bila ya kujali udhaifu wa afya ya mtoto wake huyo.

Pesambili pia anafahamika kwa majina ya Maneno Pesambili Kanjanja ambayo aliyatumia wakati akiishi katika Kijiji cha Chalangwa wilayani humo. Bado haijafahamika sababu za mtuhumiwa huyo kutumia majina tofauti kwa maeneo tofauti aliyoishi.

Binti huyo, ambaye hata hivyo tunahifadhi jina lake, amekiri kufanyiwa vitendo hivyo vya kikatili na mzazi wake. Pamoja na kukiri kuingiliwa kimwili na baba yake, binti huyo alifichua zaidi ukatili wa baba yake huyo ikiwemo kunyimwa chakula, mavazi na huduma zingine muhimu.

Ukatili dhidi ya binti huyo, ambaye kwa miaka yote miwili alifungiwa ndani, ulifahamika wiki mbili zilizopita baada ya kuonekana njiani na baadhi ya kina mama, majira ya saa moja usiku akitambaa kueleke kwenye moja ya majengo kijijini hapo.

“Jumapili ilikuwa mara ya tatu kumuona, nilipomuliza ndipo akanieleza analala kwenye ofisi za CCM, nikaita watu kupata msaada,” anasema mkazi wa kijiji hicho, Maria Mwasaga, aliyemuokota binti huyo.

Pesambili hivi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Chunya, akituhumiwa kumbaka binti yake huyo.

Alifikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha wilaya hiyo mjini Chunya Jumatatu ya Januari 23, mwaka huu baada ya kina mama kijijii hapo kuulazimisha uongozi wa kijiji kuchukua hatua.       

Hata hivyo, katika maelezo ya awali yaliyoandikishwa kituo cha polisi, mtuhumiwa huyo aliandikiwa kosa la kushindwa kulea familia na sio kubaka.

Kina mama katika Kijiji hicho cha Kiwanja ndio walioingilia kati kwa kuulazimisha uongozi wa kijiji hicho kumchukulia hatua za kisheria mzazi huyo.

Hata hivyo, kina mama hao waliwaambia waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kuwa, mazingira waliyoyashuhudia katika kituo cha polisi, yaliwapa mashaka iwapo haki ingetendeka.

Wanasema walibaini suala hilo kutopewa umuhimu na viongozi wa kijiji pamoja na polisi, wakaamua kuvijulisha baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo wa Raia Mwema ambao kufika kwao kijijini hapo mwishoni mwa Juma lililopita kuliibua njama za kulifunika jambo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa aliwaeleza waandishi wa habari waliofuatilia suala hilo kuwa hakuwa na taarifa zozote na kuelezea kushangazwa kwake kwa suala hilo kutokuwemo kwenye taarifa za polisi anazopatiwa kila siku asubuhi.

“Ndio nasikia kutoka kwenu, huu ni zaidi ya ukatili,” alisema Mkuu huyo wa wilaya katika mahojiano yake na waandishi wahabari ofisini kwake.

Binti asimulia:

Mama yake alifariki akiwa bado mtoto mdogo, alimwacha akinyonya, hivyo takribani maisha yake yote ameishi na baba yake huyo, mtuhumiwa wa ubakaji.

Binti anasimulia kuwa baba yake alikuwa na kawaida ya kumfuata anapolala baada ya kuhakikisha kuwa wadogo zake wamelala. Alimwingilia kwa nguvu, kutokana na udhaifu aliokuwa nao, hakuwa na uwezo wa kujitetea.

Mazingira ya malazi ya familia hiyo yanatisha, ni chumba kikubwa chenye kitanda kimoja ukutani kinachotumiwa na baba huku watoto wakilala kwenye sakafu bila kuwepo godoro na kikinuka uvundo.

“Akiona watoto wamelala alikwenda mlangoni, aligonga mlango kama vile mtu yupo nje anataka kuingia ndani, kisha akaja kwangu na kuniingilia,” anasimulia binti huyo katika mahojiano yake na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo.

Kwa mujibu wa binti huyo, baba yao amekuwa akimfanyia ukatili tangu akiwa bado mdogo ambapo mwaka 1998 alilazimika kukatisha masomo yake akiwa darasa la sita kwa kukosa huduma muhimu.

Manyanyaso yalimlazimisha kuacha masomo, alilazimika kufanya vibarua na biashara ndogo ndogo ikiwemo kuuza kuni ili apate fedha kwa ajili ya mahitaji yake ya shule, nguo na chakula.

“Huna mikono,” lilikuwa swali la Pesambili kwa binti yake huyo kila alipomuomba mahitaji, anasema binti huyo.

Anasema baada ya kuacha masomo, aliondoka nyumbani na kuanza kuhangaika kujitafutia maisha ikiwemo kufanya kazi kwenye machimbo ya dhahabu wilayani humo. Akiwa kwenye hizo harakati zake za kutafuta maisha ndipo alipokutana na mwanaume ambaye baadaye alikuja kuishi naye kama mumewe.

Hata hivyo, binti huyo anasimulia kuwa aliishi na mumewe kwa miaka mitatu tu kabla ya kurudishwa nyumbani kwao kutokana na kuugua ambapo alijikuta mwili ukiishiwa nguvu.

Alirudishwa kwa baba yake miaka miwili iliyopita na tangu wakati huo, alimgeuza kuwa mke wake kwa kumuingilia kimwili hata bila ya ridhaa ya binti yake ambaye tayari alikuwa mgonjwa na dhaifu.

Pesambili aliishi peke yake na watoto wake watatu baada ya mke wake, aliyeoa baada ya kufiwa na mke wa kwanza kufariki, kuondoka. Na mke uyo aliondoka kielezwa kuwa alichoshwa na mateso ya mumewe huyo.

Pamoja na mchezo wake huo mchafu kwa binti yake, bado aliendelea kutompatia huduma za muhimu ikiwemo chakula, malazi, mavazi na hata maji, ikizingatiwa kuwa hakuwa na uwezo wa kubeba vitu.

“Nilikuwa nanawa mikojo yangu, akaniambia nanuka, sina soko,” anasimulia binti huyo.

Mkazi wa Kijiji cha Kiwanja, Tunu Kitaba  anasema, wao wakiwa wanawake, tukio hilo limewaumiza ndio maana waliamua kulisimamia hadi waone haki ikitendeka.

“Mwenyekiti wa kijiji alilifahamu tatizo lakini hakuchukua hatua yoyote, ndio maana tumewaita mtusaidie,” alisema Tunu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiwanja, Gideon Kinyamagoha alithibitisha kufahamu binti huyo kufungiwa ndani na kwamba alilazimika kuiagiza Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Serikali ya Kijiji hicho kufuatilia.

“Maelezo ya binti kwa kina mama, alisema baba yake alikuwa akimwingilia kimwili,” alisema Mwenyeiti huyo katika maelezo yake kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Rehema Madusa.         

Polisi, ustawi wa jamii wajichanganya:

Tayari serikali wilayani Chunya imechukua hatua kuhakikisha haki inatendeka. Baada ya mahojiano yake na waandishi wa habari, mkuu wa wilaya hiyo aliamua kulifuatilia mwenyewe siku hiyo hiyo kwa kuwaita Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Chunya na Asifa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo.

Ofisa Upelelezi wa Wilaya hiyo, Mkoma alibainisha kuwa kesi iliyopo kituoni hapo kuhusu Pesambili inahusu kushindwa kulea familia, kwamba wakati wa kutoa maelezo, suala la ubakiji halikutajwa.

Afisa Usatawi wa Jamii Wilaya ya Chunya, Theresia Mwendapole naye alithibitisha tatizo la binti huyo kufahamika na ofisi yake.

“Huyo baba aliwahi kuja ofisini kwangu, kuomba iwapo serikali inatoa msaada kwa watoto kama hawa waliopooza,” alisema Theresia akithibitisha kulifahamu tatizo hilo.

Theresia pia alithibitisha suala la Pesambili kumbaka binti yake huyo lilitajwa wakati wa kutoa maelezo Kituo Kikuu cha Polisi wilayani humo. Hata hivyo afisa huyo alidai kuwa suala la ubakiji lilitajwa baada ya zoezi la utoaji maelezo kukamilika.

Kwa mujibu wa Theresia, wanapokea wastani wa tukio moja la ubakaji kila wiki wilayani humo. Anasema kuwa wenyeji huvihusisha zaidi vitendo hivyo na imani za kishirikina kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu.

Kutokana na mkanganyiko huo wa maelezo ya maafisa wa serikali, Mkuu wa Wilaya aliamua wote, yeye mwenyewe, afisa usatawi wa jamii na afisa upelelezi kwenda kijijini hapo, umbali usiozidi kilometa tano kutoka ofisi za mkuu wa wilaya.

Katika hatua ya kushangaza, tangu wananchi hao wafikishe malalamiko yao polisi na ujirani uliopo, hakuna aliyethubutu kufika kijijini hapo kujionea hali halisi.

Mkuu wa wilaya na ujumbe wake huo walikutana na uongozi wa kijiji, wananchi, kujionea makazi ya mtuhumiwa pamoja na kuonana na binti mwenye.

Mkuu wa Wilaya alimwagiza Afisa Ustawi wa Jamii kusimamia zoezi la uchunguzi wa afya kwa binti na wadogo zake.

Vile vile alimwagiza afisa upelelezi kuandika maeleo sahihi ya suala hilo na kesi isomeke ubakaji na taratibu za kisheria ziendelee ikiwemo mtuhumiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Kina mama kijijini hapo wameweka msimamo wao kwamba hawataki kumuona tena Pesambili kijijini hapo na iwapo ataachiwa na kurudi kijijini basi watajua wao cha kufanya.

Binti huyo hivi sasa anatunzwa na kina mama wa kijiji hicho akiishi kwa mmoja wao, Tunu. Kina mama hao wanaamini kuwa akipata huduma atarudi katika hali yake ya kawaida.

Siri ya Uwezo wa Nazi na Ndimu kwa Kinadada..!!!

0
0


Kinadada wengi huangaika mara kwa mara kwa lengo la kuhitaji kuwa na nywele nzuri zenye muonekano mzuri kila siku, lakini kwa bahati mbaya sana si wote wanabahatika kufanikiwa kuwa na nywele hizo nzuri.

Si ajabu kabisa kumsikia mwanamke akisema ameshakata tamaa kutokana na mwenendo wa makuzi ya nywele zake kutokwenda vizuri na wengi hukata tamaa mara baada ya kutumia dawa mbalimbali za kukuza nywele lakini hujikuta wakikosa hayo mafanikio na baadhi yao hujikuta nywele zinazidi kuisha zaidi au kudumaa.

Kama wewe ni dada ambaye huenda unashida hiyo basi tambua kwamba moja ya sababu ya nywele kushindwa kukua vizuri ni pamoja na hii sababu ya kuwa na mba kichwani mwako.

Sasa leo napenda kukupatia hii mbinu ya kumaliza shida ya mba kwa kutumia mchanganyiko wa mafuta ya nazi na ndimu ili baadaye uweze kuwa na nywele zenye afya bora.

Jambo la kufanya kwanza kabisa utahitajika kuziosha nywele zako vizuri kabisa na uzikaushe kisha tafuta mafuta ya nazi ndimu.

Weka mafuta ya nazi kwenye kibakuli kisha pima kijiko kimoja cha chakula chenye maji ya ndimu na ukoroge vyema. Kisha tumia mchanganyiko huo kwa kuweka kichwani na uhakikishe unafika hadi kwenye mizizi ya nywele kabisa fanya hivyo kwa dakika kadhaa. Kisha kaa na mchanganyiko huo bila kuosha kichwa kwa dakika kama 20 hivi.

Baada ya dakika hizo kupita osha kichwa chako vizuri, kisha ufanye zoezi hilo kwa mara mbili hadi tatu kwa wiki ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kwa wanaume Tu..Jua Mbinu 10 za Kufanya ili Kumfikisha Mpenzi Wako Kileleni Haraka na Akaridhika,Huitaji Madawa Tena Ukizijua Mbinu Hizi..!!!

0
0

Karibuni katika somo jingine ndugu wapenzi wa Udaku Special, kumekuwa na maombi toka kwa watu mbalimbali hasa wanaume wakihoji  juu ya kuweza kumfikisha mwanamke kielelni.

 kama huwezi kumfikisha mwanamke kileleni basi unausika katika hili somo!!!!...Wengi wakitaka kujua ni namna gani ya kumfikisha mwanamke kileleni kwa kuzani hawana nguvu za kuhimiri kufanya tendo kwa muda mrefu bila kufikiri kuwa kumuandaa mwanamke kabla ya tendo kunaweza kukusaidia katika kumridhisha.

Wanaume wengi huwa hawana maandalizi mazuri kwa wanawake wao kabla ya tendo la ndoa yanayoweza kuwasaidia kama kichochezi cha kuwafikisha kileleni mapema.

Basi njia hizi zinaweza kuwa msaada mkubwa endapo zitatumika ipasavyo na hata yule ambaye ulikuwa umridhishi baada ya somo hili utaweza kumlidhisha ipasavyo kwa kumfanyia yafuatayo.


1.Mpe maneno matamu okimtomasa kwa ulimi sikio lake kimahaba zaidi

2. Pitisha ulimi wako shingoni kifuani, tumboni, mapajani ni ikibidi zama chumvini walau kwa dakika kumi hivi

3. Tumia ulim wako ipasavyo kutomasa kitovu chake

4. Mnyonye lita kadhaa za mate na huku ukitumia ulimi wako ipasavyo kuuchanganya ulimi wake

5. Papasa matiti yake huku ukifinya finya chuchu zake na peleka mdomo wako huku ukinyonya kama mtoto

6. Zungusha viganja vyako karibu kila kona ya mwili wake bila kusahau kubinya binya sehemu za mbavu hips na makalio yake

7. Tekenya ki**mi chake kwa vidole vyako au kwa ulimi ikiwezekana

8. Mpe koni ya asili ajilambie kwa raha zake

9. Muweke mkao mzuri wa kupokea zawadi yake

10. Ingiza taratibu mti shimoni

Hata kama huna uwezo wa kumfikisha kileleni hiyo dozi itakusaidia vilivyo.

Naamini kama utayafanyia kazi ipasavyo tatizo la kumridhisha mwanamke litapungua..

ZINGATIA yafuatayo

Maandalizi kwanza:
Tumia muda wa kutosha mwanzoni, wanawake wanapenda kuingiliwa taratibu bila pupa. Mbusu, mfanyie masaji na mchezee kwa muda, huku ukim non'goneza maneno machafu masikioni, na tumia mda kumpapasa sehemu nyeti. Anahitaji kuloana hata kabla hujamvua nguo.

Mtafutie Style anayoipenda:
Najua wengi mnapenda ile ya kumweka juu huku ukimshika matiti yake na makalio. Itunze hiyo utaitumia badae, mwanzoni jaribu kutafuta style ambayo ina mchanganya na kumfurahisha yeye kwanza, kama vipi muulize kwanza.

Rais Magufuli Ateua Mkuu Mpya wa Majeshi

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.

Cameroon Yatinga Fainali AFCON..!!!

0
0

Cameroon imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) baada ya kuwafunga Ghana mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili uliofanyika usiku huu mjini Frenceville nchini Gabon.

Michael Ngadeu-Ngadjui alianza kuipatia Cameroon bao la kuongoza dakika ya 72 ambapo kabla ya sekunde chache refa kupuliza kipenga cha mwisho Christian Bassogog aliipa timu hiyo goli la pili na la ushindi.

Magoli hayo mawili yanawapa Cameroon nafasi ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.

Cameroon itakutana na Misri ambayo ilitinga hatua ya fainali jana baada ya kuwafunga Burkina Faso goli 4-3 kwa mikwaju ya penalti.

Fainali hiyo itachezwa Jumapili ijayo ambapo itatanguliwa na mechi ya kusaka mshimdi wa tatu siku ya Jumamosi kati ya Ghana na Burkina Faso.

JPM Awashukia Polisi, Takukuru,Mahakama,Prof Lipumba Achekelea..!!!

0
0

RAIS John Magufuli amewanyoshea kidole Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwa ndio chanzo cha serikali kupoteza kesi nyingi kutokana na kupindisha na kuwasilisha ushahidi hafifu mahakamani.

Pia ameagiza mamlaka zinazohusika na kusikiliza kesi, mhalifu ambaye anakamatwa na vidhibiti, kesi yake isikilizwe siku hiyo na hukumu kutolewa siku hiyo hiyo badala ya ilivyo sasa waendesha mashitaka wanarefusha kesi hizo kwa kisingizio cha ushahidi kutokamilika.

Alitumia maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika Dar es Salaam jana kuwanyooshea kidogo majaji katika maamuzi yao waliyoyafanya kuhusu mahakimu 28 waliokuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya rushwa kuachiwa huru wote.

Aliziagiza pia ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kuhakikisha kwamba zinaacha kugombana, kwani nazo zimekuwa zinachangia kutengeneza ushahidi hafifu na hivyo kufanya serikali kupoteza kesi mahakamani.

Awapasha Polisi, Takukuru

Alisema Polisi na Takukuru ambao ndio wenye jukumu la kufanya upelelezi wamekuwa hawafanyi upelelezi na wamefikia hatua wanamkamata mtuhumiwa na vidhibiti, lakini mtuhumiwa anashinda kesi.

Alitoa mfano kuwa mtuhumiwa wa dawa za kulevya anakamatwa na dawa za kulevya, lakini akifikishwa mahakamani upande wa mashitaka unashindwa kuendelea na kesi kwa kisingizio kuwa upelelezi haujakamilika.

“Mtuhumiwa anakamatwa na jino la tembo, lakini wanadai upelelezi bado kukamilika, au kakamatwa na dawa za kulevya baada ya muda dawa hizo zikipelekwa kwa mkemia inabainika kuwa ni unga wa muhogo wa huko Sumbawanga,” alisema Rais Magufuli.

Alisema kutokana na ushahidi kutokuwepo, mahakama inalazimika kumwachia huru mtuhumiwa; hivyo akaonya kuwa umefika wakati vyombo hivyo vijitathmini na vibadilike.

Aliagiza kuwa mtu akishikwa na vidhibiti, siku hiyo hiyo kesi yake isikilizwe na imalizike, na kama kuna mtu atajitokeza kumtetea naye aunganishwe kwenye hiyo kesi wote waende jela. Serikali haijalipwa trilioni 7.5/-.

Alisema majaji watafute namna ambavyo wanaweza kutumia sheria watuhumiwa wa namna hiyo wahukumiwe kwenda jela, “sheria huwa inasema kifungo au faini, sasa nyinyi hawa wenye vidhibiti mnawahukumu vyote pamoja.”

Alibainisha kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2016, serikali haijalipwa kiasi cha Sh trilioni 7.5 licha ya kushinda kesi za ukwepaji kodi zilizokuwa zinawakabili washitakiwa mbalimbali.

“Haiwezekani mwekezaji anachimba madini yetu, kodi halipi, anashitakiwa mahakamani anashindwa, halafu pesa haitolewi. Sasa tujiulize, kama utoaji haki unaakisi ujenzi wa uchumi wa nchi ni kwa kiasi gani kesi zenye thamani ya Sh trilioni 7.5 zimeathiri uchumi?” Alihoji Rais Magufuli.

Ugomvi wa AG, DPP

Rais Magufuli alitoboa kwamba ofisi hizo mbili muhimu katika utoaji wa haki nchini watendaji wake wamekuwa wanagombana, jambo ambalo linafanya serikali ishindwe kesi kutokana na ushahidi hafifu unaowasilishwa na watendaji wa ofisi hizo.

Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP), Biswalo Mganga wamekuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe na akawataka watendaji wa ofisi hizo kujitathmini wenyewe, ni wapi wanakosea na wapi wanakwenda kwa kuendekeza ugomvi huo.

“Waziri unafahamu ugomvi wa ofisi hizi mbili, cha ajabu wote hawa wanatoka mkoa mmoja na yawezekana wilaya moja, sijui wanagombea nini. Kama ni madaraka wote ni wateuliwa wa Rais, kama ni kasima tafuteni suluhisho,” alisema Rais Magufuli.

Alionya kuwa bila kutafuta suluhisho, serikali itaendelea kupoteza kesi kutokana na ushahidi laini unaowasilishwa mahakamani.

Alisema wakati mwingine ushahidi unakuwa laini hadi kumfanya jaji aahirishe kesi kutoa nafasi kwa mawakili wa serikali kwenda na ushahidi mzito, lakini hawafanyi hivyo.

“Kwa hali unakuta ushahidi upo, lakini tunashindwa kwa sababu ushahidi unaopelekwa mahakamani ni mwepesi kutokana na matatizo yaliyopo katika ofisi hizi mbili,” alisema.

Ahoji mahakimu kutofungwa Katika hotuba yake, Rais Magufuli alihoji mahakimu 28 walishitakiwa kwa tuhuma za kupokea rushwa, lakini akashangaa kwamba katika kesi zote hizo hakuna hakimu hata mmoja aliyetiwa hatiani na kufungwa.

Alisema kwa hali ya kawaida raia ambao sio wanasheria wanakuwa na maswali mengi kuhusu maamuzi hayo ya mahakama. Alisema yawezekana upelelezi wa polisi haukufanywa vizuri au ushahidi ulikuwepo, lakini haukufikishwa vizuri mahakamani.

“Yawezekana mawakili wa pande zote walikula njama kuhakikisha hakuna ushahidi unaotolewa dhidi ya mahakimu hao au yawezekana majaji au mahakimu wenzao waliamua kuwaachia huru wenzao kuthibitisha ule usemi kuwa kesi ya ngedere unampelekea nyani,” alibainisha Rais Magufuli.

Alisema jambo hilo ni changamoto kwa Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma na alimtaka ashughulikie suala hilo kwani mbele ya wananchi maamuzi hayo ya mahakama yanaleta shaka na akawataka majaji wajipange kuondoa changamoto hizo wanapoanza mwaka mpya wa mahakama.

Alisema Watanzania wangefurahi hata mahakimu wawili wangefungwa.

Rais Magufuli pia alisema kuna madudu mengi yanafanywa ndani ya Idara ya Mahakama, lakini yamekuwa yanapita kimya kimya na akatolea mfano baadhi ya majaji kuhusishwa kupokea fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu (BoT), lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya majaji hao.

Alisema mambo kama hayo yanaumiza kuona yanafanywa na chombo ambacho kina dhamana ya kutoa haki ya kisheria kwa wananchi.

Alisema kuna majaji wachache sio waadilifu ambao wamekuwa wanaichafua sura ya mahakama “Yawezekana hapa asilimia 99.99 ni wasafi, lakini wanachafuliwa na hawa wachache ambao ni asilimia 0.00. Jaji Mkuu tafadhali chukua hatua dhidi ya watendaji hawa wachafu,” alisema Magufuli na kuongeza kuwa ameyasema hayo kwa sababu mahakama haiongozwi na malaika.

Alisema kuna majaji kutokana na uchafu wao, tangu waanze kusikiliza kesi, Serikali haijawahi kushinda kesi zinazofikishwa “Unajiuliza hivi kesi zote huwa hazina ushahidi? Ashangaa kuhusu ajira mpya.

Akijibu maombi ya Jaji Juma kutaka mahakama iruhusiwe kuajiri watumishi wapya wapatao 900, Rais Magufuli alishangaa kwani kwa sasa taasisi hiyo ina watumishi 6,500 ambao ni wengi kuliko idara nyingine serikalini na akahoji iweje watake kuongeza watumishi.

“Ninyi ndio wengi kuliko idara nyingine yoyote, kwa mfano mnataka walinzi wa nini, hivi polisi hawalindi mahakama, kama hawalindi kwa nini msitoe kwa kampuni binafsi za ulinzi?Angalieni nani anahitajika katika mageuzi haya mnayofanya,” alisema Rais Magufuli.

Pia aliishauri idara hiyo kuhakikisha kwamba inaunganisha baadhi ya shughuli ambazo zilikuwa zinafanywa na watu wanne ifanywe na mtu mmoja na aongezewe mshahara badala ya kutaka kuongeza watumishi wengine wapya.

Alisema inamuwia vigumu kuongeza ajira za umma kwa sababu Serikali inatumia Sh bilioni 600 kila mwezi kuwalipa wafanyakazi 546,166 kila mwezi na bado kuna kulipa madeni mengine jambo ambalo linafanya serikali inalemewa.

Alitoa mfano kuwa mwezi uliopita serikali ilifanya malipo ya mishahara na kulipa madeni yenye thamani ya Sh bilioni 955 wakati makusanyo kwa mwezi ni Sh trilioni 1.2. Alitahadharisha kuwa suala la kuongeza watumishi wapya linaweza kufanya Serikali ishindwe kuwalipa mshahara.

Alisema atawaruhusu mahakama kuajiri watumishi wa kada zinazotakiwa tu na akamtaka jaji mkuu kuhakikisha kwamba kwa nafasi ambazo sio muhimu wafanye mageuzi waangalie namna ya kuzijaza nafasi hizo kwa kutumia watumishi waliopo.

Ataka mawakili kuwa wazalendo Rais Magufuli pia aliwaagiza mawakili kuhakikisha wanakuwa wazalendo na wawatose watuhumiwa wabaya na wasiwatetee.

Alisema wahalifu hao wabaya wakitaka wawatetee, mawakili wachukue fedha zao lakini wakifika mahakamani wawaruke “Chukueni fedha zao, lakini mkifika mahakamani wageukeni,” aliwaambia.

Pia aliwataka mawakili hao kupitia chama chao, Tanganyika Law Society (TLS) kuacha kujihusisha na siasa badala yake wasiwe na vyama katika kutekeleza majukumu yao.

Alisema ndani ya TLS kumekuwa kama chama cha siasa, hadi kwenye kampeni za uchaguzi wanapigana mkumbo watu wenye mlengo tofauti wa vyama vya siasa. Alisema yeye hatakuwa tayari kuteua wakili kuwa jaji ambaye anashabikia vyama vya siasa.

“Jijengeeni heshima kwa kuwa neutral (msiwe na upande), hiyo itawajengea heshima,” alisema Rais Magufuli.

Mwanamama azua tafrani, aibukia kwa Rais

Katika hatua nyingine, mwanamke mkazi wa Tanga, Sobha Mohammed alizua tafrani baada ya kuibuka mara tu Rais alipomaliza hotuba yake akiwa na bango, lakini kabla ya kufika mbele ya meza kuu alikumbana na rungu la walinzi wa rais.

Mama huyo alirejeshwa nyuma kuondolewa eneo hilo huku watu waliokuwapo hapo wakishuhudia, na wakati huo Rais Magufuli alikuwa katika mazungumzo na Kaimu Jaji Mkuu, lakini baada ya muda mfupi kulitokea agizo la Rais la kutaka aachwe na apelekwe kwao atoe kilio chake.

Alipofika mbele, mama huyo alianza kutoa kilio, na akielezea madhila ya kudhulumiwa haki zake katika kesi iliyofunguliwa mkoani Tanga na kwamba amefika katika ofisi mbalimbali za wahusika wa masuala ya kisheria kuanzia Polisi hadi kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe.

Baada ya kumsikiliza mama huyo, Rais Magufuli aliagiza, “Ofisi ya DPP, AG na…. Jaji Kiongozi si ndio msimamizi wa kesi zote za chini chini, si ndio bwana. Shughulikie suala la huyu mama. Kama kesi iko Mahakama ya Mwanzo kule muivute huku haraka haraka, ishughulikiwe haraka.

Na AG pia mshughulikie, lakini na pia mumlinde ili asidhuriwe kwa kifo cha aina yoyote. Chukua jina lake, lakini pia mtafutieni Polisi ili amlinde. Lakini mhakikishe usalama wake. Jaji Kiongozi chukua simu yake. Na mama njoo uchukue simu ya Jaji Kiongozi, umpigie moja kwa moja.”

Kauli ya Rais ilipokewa kwa shangwe na nderemo. Profesa Lipumba apongeza Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kitendo cha Rais kuyasema mambo hayo hadharani hapo, kinaonesha kuwa anataka kupata nguvu ya kisiasa ili wananchi wajue kinachoendelea katika mfumo wa utoaji wa haki nchini.

“Kwa mfano, serikali imeshinda kesi na inatakiwa kulipwa shilingi trilioni 7.5, lakini hazijalipwa tatizo liko wapi? Alihoji Lipumba.

Profesa Lipumba alisema kuna haja ya watendaji ndani ya mfumo wa mahakama na vyombo vingine vya serikali kuhakikisha kwamba wanabadilika ili mapungufu aliyoyaainisha Tais yasiwepo tena.

Pitia Vichwa vya Magazeti ya Leo 3/2/2017..!!!

Kitwanga Atishia Kuzima Mitambo ya Maji..!!!

0
0

MBUNGE wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM) ametishia kuwa endapo wananchi wake hawatopata maji kutoka chanzo cha maji cha Ihelele kama walivyoahidiwa na serikali, ataongozana na wananchi hao kwenda kuzima mitambo ya maji katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, chanzo hicho cha maji kwa sasa kinazalisha maji yanayopelekwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Shinyanga na Kahama kupitia Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Kahama na Shinyanga (Kashuwasa).

Akiuliza swali la nyongeza bungeni Dodoma mbunge huyo alisema tangu serikali iwaahidi kuwa jimbo hilo la Misungwi litapata maji kupitia mradi huo wa maji wa Ihelele hadi sasa maji hayo hayatoki wakati maeneo mengine yanapata.

“Naibu Spika nasema wazi kuwa nitaongozana na wananchi wa jimbo langu kwenda kuuzima ule mtambo wa maji Ihelele kama maji haya yataendelea kutotoka kwenye maeneo yetu,” alisema Kitwanga ambaye aliposimama kuuliza swali hilo alishangiliwa sana na wabunge wenzake.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge alimtaka mbunge huyo asiandamane na wananchi wake, kwani kilichokwamisha maji hayo yasifike jimboni kwake ni uhaba wa fedha za kuunganisha bomba la maji hadi eneo hilo ambapo zinahitajika takribani Sh bilioni nne.

Duh..Eti Serikali Itatumia Bilioni 105 kwa Ajili ya Kutunzia Nyayo za Binadamu wa Kale..!!!

0
0

WIZARA Maliasili na Utalii inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufukua nyayo za Laetoli zilizopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro zilizogunduliwa na mtafiti Dk Mary Leakey mwaka 1978.

Jitihada hizo za wizara zinafanywa kutokana na agizo la Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2007, alipoitaka wizara hiyo kufukua nyayo hizo na kuzihifadhi kisasa kwa matumizi ya elimu na utalii kwa Watanzania na wageni.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) aliyetaka kujua serikali inafanya mkakati gani kuajiri wataalamu wa kufukua nyayo hizo.

Makani alisema, mradi huo una gharama kubwa unakadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 50 (sawa na Sh bilioni 105), ambazo zitatumika kwa ajili ya kusomesha wataalamu na kuandaa michoro ya ujenzi wa makumbusho.

Lakini pia fedha hizo zitatumika katika kufufua na kuhifadhi nyayo hizo, kusimamia ujenzi na kuweka mifumo ya uhifadhi wa kisasa wa nyayo hizo.

Alisema fedha hizo ni nyingi, ukilinganisha na mapato na majukumu ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambayo inatakiwa kugharamia, hivyo wizara inaendelea kutafuta fedha ili kugharamia utekelezaji wa mradi huo.

Makani alisema hakuna hali ya kusuasua katika kutekeleza mradi huo kwani baadhi ya kazi tayari zimekwisha kamilika na nyingine zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kazi zilizokamilika ni pamoja na kuundwa kwa idara ya urithi wa utamaduni, kukamilika kwa michoro ya awali ya jengo la mapokezi, jengo la utafiti na jengo la elimu kwa umma.

Pia imewasilishwa tathmini ya athari kwa mazingira kwa mamlaka husika ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa uchambuzi wa kina ili kutoa idhini na kutoa mafunzo ya shahada ya uzamivu kwa watumishi wawili.

Kazi ambazo zinaendelea kutekelezwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za ajira kwa baadhi ya watalaamu wanaopatikana nchini na kukusanya takwimu sahihi kuhusu mazingira rafiki ya nyayo hizo na kazi inafanywa na watalaamu kutoka nje ya nchi inatarajiwa kukamilika Februari mwaka huu.

Wanachama wa Cuf Waviziana ili Kuzichapa,ni Wale Wanaomuunga Mkono Prof Lipumba na Wanaomuunga Mkono Maalim Seif..!!!

0
0

MGOGORO wa CUF umeendelea kupata sura mpya, baada ya upande wa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba, kutoa kauli ikionesha hofu ya usalama wao na ofisi za chama hicho Buguruni, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi hizo jana,   Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF, Masoud Mhina alidai kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, Julius Mtatiro na wenzake, wamepanga kuvamia ofisi za chama hicho.

Mhina alidai tayari walinzi wa chama wamejipanga kukabiliana na kikundi chochote chenye dhamira ya kuhujumu chama hicho.

“Tuna taarifa kuwa kuna vijana wanaandaliwa kuja kuvamia ofisi kuu za chama Buguruni kwa ajili ya kufanya vurugu, nadhani wanatufahamu vizuri, tukianza huwa hatukamatiki na tutahakikisha chama kinabaki salama,” alidai.

Mhina alidai wanawafahamu viongozi waliopanga hujuma hizo na tayari wamewasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu vitisho na vitendo vya udhalimu vinavyokusudiwa kufanywa na wasaliti wa chama hicho, dhidi ya viongozi wa chama upande wa Bara.

Alidai kwa sasa hawawezi kuweka wazi majina ya viongozi hao kwa kuwa wanajijua na vikao wanavyofanya kila kukicha ila ipo siku watawataja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria na kikatiba.

“Tutawashughulikia kisheria na kikatiba wanaotaka kuhujumu chama kokote waliko tutawatafuta hadi maeneo ambayo wanafanyia mikutano na kuwakamata, maana CUF hatuna mgogoro, ulishamalizwa na Msajili wa Vyama vya Siasa,” alidai.

Mhina alitoa onyo kwa wanaojiita viongozi wa CUF wanaozungumzia vichochoroni na kuwataka kama ni halali, waache na badala yake waende ofisi za chama hicho ili wamweleze Profesa Lipumba walipewa uongozi na nani.

“Tumewavumilia sana kiasi cha kutosha, sasa dawa yao ipo jikoni mmoja mmoja baada ya mwingine tutawajibika nao, hivyo nachukua nafasi hii kutoa onyo kwao kama ni viongozi, bora waje ofisini si kuzungumzia vichochoroni,” alisema.

Awali akizungumzia kazi za Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama, Mhina alisema kwa mujibu wa Katiba ya CUF ibara ya 88 (2) (a), Katibu atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati na Ibara ya 87 (1) imeeleza kuwa wajibu wa Kamati hiyo ni kuhakikisha usalama wa chama unakuwapo nchini.

Alitumia nafasi hiyo kumsihi Katibu Mkuu aache vikao vya kuhujumu chama, kwa kuwa havina tija kwake zaidi ya kujenga uhasama dhidi ya wanachama na viongozi hao Bara na Zanzibar.

Akizungumzia tuhuma hizo, Mtatiro alihoji kuwa tangu lini Mwenyekiti wa Chama akachaguliwa na Msajili na kuongeza kuwa Buguruni pamejaa wahuni wanaomlinda Lipumba, hivyo hawawezi kufika eneo hilo.

“Hatuwezi kufanya upuuzi kama huo wa kwenda pale na hakuna anayetaka kuvamia, kwa kuwa hakuna anayetaka kukaa kwenye ofisi ile kimabavu kama Lipumba, tena kwa msaada wa wahuni na Polisi, sasa tunakwenda kuhujumu nini na ili iweje?”Alihoji.

Alihoji wanaojiita wakurugenzi, wameteuliwa na nani wakati hawamtambui Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF.

Kwa mujibu wa Mtatiro, ili mtu awe Mkurugenzi lazima ateuliwe na Mwenyekiti halali wa chama anayetambuliwa na vikao vya kitaifa hivyo haelewi waliteuliwa na nani.

Mbowe Awaita Mameya wa Dar Kujadili Uuzwaji wa UDA..!!

0
0

HISA za Uda zawa kaa la moto. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe kufanya kikao cha dharura na mameya, naibu mameya na viongozi waandamizi wa Ukawa kujadili utata wa uuzwaji wa hisa za Shirika hilo la Usafiri Dar es Salaam.

Mameya hao kutoka Dar es Salaam waliwasili mjini hapa juzi kwa nyakati tofauti, kuhudhuria kikao hicho kilichofanyika jana kwenye ofisi za Bunge.

Taarifa zilizotufikia zilieleza kuwa kikao hicho kilifanyika baada ya kuibuka mvutano kati ya Serikali na uongozi wa Jiji hilo, linaloongozwa na Ukawa kuhusu kuidhinisha Sh bilioni 5.8 za uuzwaji wa hisa asilimia 51 kati ya 100 kwa kampuni ya Simon Group.

Jumamosi iliyopita Baraza la Halmashauri ya Jiji hilo chini ya Meya wake, Isaya Mwita kwenye kikao chake cha kawaida, lilishindwa kufikia mwafaka wa kuzipangia matumizi fedha hizo kwa kilichoelezwa ni sawa na kubariki ufisadi wa uuzwaji wa hisa hizo ambazo wanaona ni kiasi kidogo.

Kikao hicho kilifanyika baada ya agizo la Rais John Magufuli Januari 27 wakati akizindua mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Katika agizo hilo, Rais alitoa siku tano kwa uongozi wa Jiji kuhakikisha kiasi hicho cha fedha zilizolipwa na Simon Group kinapangiwa matumizi.

Lakini jana, Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema alisema nje ya viwanja vya Bunge, kuwa amewaita mameya hao na manaibu wao ili kuzungumzia sakata la hisa hizo.

“Nataka tupate msimamo wa pamoja ili wakazi wa Dar es Salaam wanufaike na na Uda. Sioni sababu ya kuiua wala kulichukia shirika hili,” alisema.

Miongoni mwa mameya walioonekana jana kwenye viwanja vya Bunge ni Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ambaye alikiri kuitwa kuhudhuria kikao licha ya kusisitiza kuwa hajui ajenda.

Mapema jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene aliwaeleza waandishi wa habari kuwa hana la kusema juu ya kushindwa kugawanywa kwa fedha hizo.

Alitaka viongozi hao wapewe muda ili kumaliza tatizo hilo huku akisisitiza kwamba kwa kuwa siku zimepita, anasubiri kauli ya Rais juu ya jambo hilo.

Mwiguli Nchemba Amkataza Makonda Kutembea na Ving'ora vya Polisi

0
0

WAKUU wa Mikoa na Wilaya ni ruksa kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali za utendaji, zikiwamo za ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Ufafanuzi huo ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kujua kama ni itifaki za kiserikali kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora.

Mbowe alishangaa na kuhoji kuwa ni itifaki gani kwa viongozi hao, akatoa mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutembea na kikosi cha polisi chenye watu tisa, pikipiki za polisi za kuongoza msafara na gari lenye king’ora.

Waziri Mwigulu alisema, viongozi hao hawaruhusiwi kutembea na misafara yenye magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda ofisini, labda kama viongozi wa mkoa na polisi wapo ofisi moja, lakini hawakatazwi kwenda navyo wanapoenda eneo la kazi maalumu.

“Viongozi hao wanapokuwa na majukumu ya kwenda kutoa maelekezo au kufanya shughuli zinazohusiana na majukumu ya ulinzi wa maeneo yao, wanaruhiswa kuwa na magari hayo,” alisema.

Wafariki Wakisubiri Mwisho wa Dunia..!!!

0
0

Waumini watano wanaotambulika chini ya mwamvuli wa imani ya Voodoo nchini Benin wamefariki dunia baada ya kuamuliwa kukaa kwenye chumba maalumu na kufanya maombi wakisubiri mwisho wa dunia.

Waumini hao waliamulia kukaa kwenye chumba kilichozibwa sehemu zote kama sehemu ya kudhihirisha imani yao.

Vifo hivyo vilisababishwa na msongamano pamoja na ukosefu wa hewa.

Waumini wengine walionusurika kwenye tukio hilo lililotokea katika Mji wa Adjarra uliopo karibu na Bandari ya Novo, Kaskazini mashariki mwa Benin wamelazwa hospitali.

Mmoja wa walionusurika kwenye tukio hilo alisema waliamuliwa kuingia kwenye chumba cha maombi ili kujisalimisha na adhabu yoyote iwapo dunia ingefikia mwisho wake.

“Tukiwa katika chumba cha maombi tulitumia nguo zilizochakaa kuziba maeneo yote yaliyokuwa wazi na baadaye kutayarisha mkaa ambao ulikuwa kama maandalizi ya kurejea kwa roho mtakatifu,” alisema Yves Aboua akiwa amelazwa katika hospitali ya Porto Novo.

Tukio hilo linakumbusha lile lililotekea nchini Uganda wakati wafuasi wa mtu aliyejiita nabii maarufu kwa jina la Kibwetele walipojitekeza kwa moto wakiamini kuwa mwaka 2000 ulikuwa mwisho wa dunia.

Baada ya tukio hilo iliripotiwa kuwa makumi ya watu walipoteza maisha ndani ya kanisa la Kibwetere.

Kwa muda sasa umekuwapo upinzani mkubwa unaojitokeza kukemea mwenendo unaofanywa na waumini wa Voodoo ambao wanalalamikiwa kwenda kinyume na misingi halisi ya imani.

Moja ya kanisa lililojitokeza wazi kukema imani hiyo ni lile linalojulikana kama Kanisa Takatifu la Yesu Kristo wa Baname.

Nchini Benin, Voodoo ni utamaduni unaotambuliwa na wengi na kuna siku maalumu ya kitaifa inayotambulika kwa jina hilo. Pia, kuna makumbusho ya Taifa ya Voodoo.


Hamorapa, Ney Wamitego lao Moja....!!!

0
0

KIZUNG-UMZIA ishu ‘inayo-trend’ kwa sasa kwenye burudani hususan katika Muziki wa Bongo Fleva bila kupapasa utataja ishu ya msanii chipukizi aliyejizolea umaarufu wa ghafla, Athuman Omary ‘Harmorapa’.

Harmorapa amejizolea umaarufu kutokana na kuhusishwa kufanana muonekano na staa wa muziki huo ambaye ni mmoja kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’. Licha ya kuhusishwa huko, pia jina lake lina ukaribu na Harmonize ila utofauti wa hao wawili, Harmorapa anafanya Muziki wa Hip Hop wakati mwenzake anaimba.

Kimuziki

Harmorapa amefahamika wiki tatu zilizopita kupitia ngoma yake ya Usigawe Pasi ambapo katika video ya ngoma hiyo amemtumia dada anayefananishwa kimuonekano na muigizaji kutoka Bongo Muvi, Jacqueline Wolper. Ikumbukwe kuwa Wolper yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Harmonize.

Tangu kufahamika kwa dogo huyo ambaye anatokea mkoani Mtwara kama ilivyo kwa Harmonize, mashabiki wengi wa muziki wamekuwa wakimuongelea na wengine kumfuatilia kwa ukaribu.

Kushika mkwanja

Moja ya matukio ambayo yamewashtua wengi ni kitendo cha kuonekana na ‘maburungutu’ ya pesa ‘mkwanja’ jambo ambalo limewahi kufanywa na wanamuziki wengine hivi karibuni kama vile Nay wa Mitego na Rayvanny.

Itakumbukwa kuwa, baada ya picha za Nay akiwa amekumbatia maburungutu ya pesa kusambaa mitandaoni, alifanyiwa mahojiano katika kipindi kimoja cha TV, juu ya utajiri wake huo na kusema kuwa biashara pamoja na muziki wake ni vitu vinavyomwingizia pesa nyingi.

Alisema mali zake na kila kitu zinafika bilioni, ukichanganya hela zilizo benki pamoja na biashara anazofanya thamani yake.

Kwa upande wa Harmorapa kwake ameonesha kumbe inawezekana kushika pesa hizo ndani ya muda mfupi. Hivi karibuni naye aliachia picha kibao zikimuonesha akiwa na maburungutu ya pesa.

Swali ni je, pesa hizo ni zake alizozipata ndani ya kipindi kifupi tangu aingie kwenye muziki au kachukua tu ili apigie picha na kutafuta kiki? Kama kafanya kwa lengo la kiki, tuna-wezaje kuamini kwamba zile walizopigia picha akina Nay wa Mitego  ni zao? Jibu utakuwa nalo wewe msomaji?

Kumi-liki gari

Licha ya kuonesha mkwanja huo, Harmorapa pia anadaiwa kuzawadiwa mkoko aina ya Nissan Murano na meneja wake ambapo jambo kama hilo limeshawahi kutokea kwa wasanii wengi wa muziki wa Bongo Fleva kukabidhiwa mkoko na mameneja wao kama vile Rayvanny, Queen Darleen na Dogo Janja.

Katika hili nalo bado kuna siri nyuma ya pazia! Hivi kweli gari hilo kapewa au nalo kaomba apigie picha? Maana alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha TV hivi karibuni, dogo huyo alionekana kutuna kabisa kwenye usukani wa gari hilo kuonesha ni lake lakini baadaye kuna picha kapiga yuko kwenye siti ya abiria.

 Kubadili wana-wake

Alipoanza kuonekana kwenye video alikuwa na Wolper Feki na hata katika ‘interview’ mbalimbali za TV na redio alizokuwa akifanyiwa alikuwa akiongozana na Wolper huyo.

Lakini kwa siku za hivi karibuni alimtambulisha mwanamke mwingine kuwa ndiye aliyenaye baada ya kumpiga chini Wolper Feki. Mwanamke wake mpya ni video queen ambaye yupo katika Video ya Too Much ya Darassa.

Kwa anachokifanya Harmorapa ndani ya muda mfupi kubadili wanawake, ni jambo ambalo wasanii wengi nao wamekuwa wakifanya hivi katika uhusiano wao akiwemo Nay ambaye alishawahi kutoka na Shamsa Ford, Siwema na pia akadaiwa kutoka na Pam D.

Ndiyo maana naweza kusema kuwa, anachokifanya Harmorapa ndicho wanachokifanya wasanii walio wengi na kwa hili niseme tu kwamba ni ulimbukeni!

P funk - Harmorapa ni Level Nyingine Bana..!!!

0
0

Producer mkongwe na mwenye heshima yake P Funk Majani ameibuka na kumzungumzia huku akimsifia msanii anayeibukia kwa kasi katika bongo fleva, Harmorapa na kusema kuwa rapa huyo ni "level nyingine".

Tangu Msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye 'headline' mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine wakifurahishwa na matendo yake huku wengine wakimdhihaki na kuona kuwa hastaili kuwa mwanamuziki.


Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na picha mbalimbali na Harmorapa mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshikilia pesa nyingi jambo ambalo limemfanya producer huyo kuibuka na kumwagia misifa.

"Chezea Harmorapa wewe!!! Levo zingine hizi" alindika P Funk Majani kupitia ukurasa wake wa Instagram



New Video: Diamond Platnumz ft Ne-Yo – Marry You

0
0

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, video ya Diamond Platnumz ya wimbo wake, Marry You aliomshirikisha Ne-Yo imetoka. Kwa mara ya kwanza video hii imewekwa kwenye channel ya Vevo ya staa huyo.

Universal Music Group (UMG) Watangaza Rasmi Kumsainisha Diamond

0
0

Hatimaye record label kubwa duniani, Universal Music Group (UMG), imemtangaza rasmi kumsainisha Diamond Platnumz.

Anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusainishwa kwenye label hiyo.

Wimbo wake, Marry You akiwa na Ne-Yo ni wa kwanza kutoka chini ya mwamvuli wa Universal Music.

“He’s a star, he is talented and full of energy and creatively he’s on par with any international artist I’ve worked with,” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa label hiyo Afrika, Sipho Dlamini.

“He’s focused and determined to succeed. He’s passionate about his country, his people , his language and his culture and I love that. He is a first class performer on stage, his new material is authentic, fresh and African, yet it will touch people across the globe. Artists like him are the reason we do what we do.”
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live




Latest Images