Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Mwanasheria wa Wema Sepetu na Vanessa Albert Msando Afunguka Kuhusu Tuhuma Zinazowakabili Wawili Hao

$
0
0
Mwanasheria wa Wema Sepetu pamoja na Vanessa Mdee, Albert Msando amefunguka na kuzungumzia nini kinaendelea kwa wateja wake wawili hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na biashara ya Madawa ya kulevya.


Wawili hao ni miongoni mwa wasanii waliotajwa katika list ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwa wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya.

Wema bado anaendelea kushikiliwa na jeshi lilo huku Vanessa Mdee ambaye alitajwa katika list ya pili ya RC Makonda na kutakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu hii yupo Afrika Kusini na leo amewakilishwa na mwanasheria wake Albert Msando.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Albert Msando amesema kwa upande wa Wema bado jeshi la polisi linaendelea na upelelezi na pindi litakapokamilisha ataeleza nini kinaendelea.

“Mimi nipo hapa kwajili ya Wema Sepetu na Vanessa Mdee,” alisema Albert Msando. “Kwa Wema bado upelelezi unaendelea, kesho baada ya upelelezi kukamilika tutajua anapelekwa mahakamani au la,”

Kwa upande wa Vanessa  Mdee mwanasheria huyo alidai muimbaji huyo wa wimbo Cash Madame bado yupo Afrika Kusini na leo amemwakilisha.

Wasanii wengine ambao bado wanashikiliwa na jeshi hilo ni TID, Nyandu Tozzy pamoja na Recho na Tunda ambao wamefika leo kituoni hapo.

Source:Bongo5

Yote Aliyo Yaongea Makonda leo Akiwa Kituo Kituo Cha Polisi Dar es Salaam

$
0
0
Leo February 5 2017 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza akiwa kituo cha kati cha Polisi Dar es salaam pembeni ya Kamishna Simon Sirro kuhusu ishu ya dawa za kulevya inayoendelea kwenye headlines.

Mambo matatu aliyoyasema mkuu wa mkoa Paul Makonda leo ni kutoa siku kumi kuanzia kesho February 7 2017 kwa Wenyeviti wa mtaa, Wazazi na Watumiaji na Wafanyabiashara.

"Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya"

"Natoa siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarifa….. tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya"

"Natoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao…. hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa hamasa"

Idadi Rasmi ya Watuhumiwa wa Dawa za Kulevya Imetajwa leo

$
0
0
Dar es salaam ni dawa za kulevya ambapo leo February 6 2017 Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro  amezungumza na Waandishi wa habari na kutoa takwimu ya kilichofanyika ndani ya siku 3.

“Tunaendelea vizuri na Oparesheni yatu ya kupambana na dawa za kulevya, tumekamata jumla ya Watuhumiwa 112 na jumla kete 299 zidhaniwazo kuwa ni dawa za kulevya, kwa kawaida tutazipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali na atatuambia ni aina gani”

“Katika Watuhumiwa hao 112, 12 tumewapeleka leo Mahakamani sababu sheria ya mwenendo wa mashtaka iko wazi, huwa inaturuhusu kuomba kuwaombea Watuhumiwa kwa kiapo kwa Hakimu, wawe chini ya uangaliazi wa Jeshi la polisi na Mahakama kwa muda wa miaka miwili wasifanye makosa tena‘

“Wote tuliowakamata wengine wanakiri na wamekwenda kuonyesha hizo dawa za kulevya, kusudio la kwanza ni wawe chini ya uangalizi wetu na kusudio la pili la kiapo chetu ni waache hiyo tabia wawe raia wema, kusudio la tatu wawe wanakuja kuripoti kituo cha polisi angalau mara mbili kwa mwezi…. lengo letu ni kuona je wameacha kutumia dawa za kulevya?” – Kamishna Simon Sirro

Habari Picha..Rais Magufuli Alivyomuapisha Mkuu Mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo..!!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Mabalozi pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma leo jijini Dar es Salaam
  RAI2
Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI3
Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (CDF) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli  akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii wakati wa hafla ya kumwapisha Mkuu wa Majeshi la Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo leo jijini Dar es Salaam.
RAI5
Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akipokea salamu ya  utii kutoka kwa kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Majeshi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
RAI6
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI7
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (CDF) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli  akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii wakati wa hafla ya kumwapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa leo jijini Dar es Salaam.
RAI9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli  akimkabidhi vutendea kazi Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwayo  wakati wa hafla ya kuwapisha wateule hao leo jijini Dar es Salaam.
RAI10
Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa wakati wa hafla ya kuwapisha wateule hao leo jijini Dar es Salaam.
RAI12
Balozi Paul Mella ambaye ataiwakilisha nchi ya Tanzania nchini katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI13
Balozi Samweli William Shelukindo ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Ufaransa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI14
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Nyakimura Mathias Mhoji akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
RAI15
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Boaz Mikomangwa akila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Inspekta Jenerali Ernest Mangu katika hafla ya kuwaapisha baadhi ya viongozi walioteuliwa na Mhe. Rais kushika nyazifa mbalimbali leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
RAI16
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo ( kulia) mara baada ya hafla ya kumuapisha leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mnadhimu wa Jeshi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Shein na Waziri Mkuu wa Kassim Majali.
RAI17
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance S. Mabeyo akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyage wakati wa hafla ya kuapishwa kwake leo jijini Dar es Salaam.
RAI18
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania wakati wa hafla ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Mabalozi pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

Breaking News(Video),Wema Sepetu Amuumbua Makonda,Adai Anatembea na Agnes Masogange na Amempangishia Nyumba Upanga Ndio Maana Hajamtaja Kwenye List..!!!

$
0
0

Sakata la Madawa ya Kulevya limechukua sura mpya kufuatia mwanadada mashuhuri Wema Sepetu, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa, kutoa ya moyoni juu ya sakata zima la kukamatwa kwao na kuhusisha tukio hilo na hila dhidi yake.

Pamoja na mambo mengine, Wema amedai kwamba RC Paul Makonda anatembea na Agnes Masogange na amempangia nyumba Makongo ndio maana hajakamatwa ktk kadhia ya Dawa za Kulevya.

Zaidi Msikie Hapa Wema Sepetu Akifunguka Kila Kitu

ACT-Wazalendo Yamleta Tanzania Julius Malema..!!!

$
0
0

Kiongozi machachari kutoka chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Economic Freedom Fighter – EFF Bw. Julius Malema ni mmoja wa viongozi wanaotarajiwa kuwasili nchini kuhudhuria mkutano utakaondaliwa na chama cha upinzani cha ACT Wazalendo.

Mkutano huo unalenga kujadili mustakbali wa lililokuwa Azimio la Arusha.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo Bw. Ado Shaibu ametaja vyama vingine vilivyoalikwa na ambavyo viongozi wake wanatarajiwa kuwasili nchini kuwa ni chama cha Labour cha nchini Uingereza, Die Link cha nchini Ujerumani na Syriza kutoka nchini Ugiriki.

Shaibu amesema wakiwa nchini, viongozi hao watashiriki mjadala mpana wa maudhui ya lililokuwa Azimio la Arusha ambalo hivi karibuni ACT Wazalengo imeliibua upya na kuliita Azimio la Tabora, ambayo kimsingi maazimio yote yanazungumzia ujenzi wa jamii inayochukia rushwa na aina zote za unyanyasaji huku ajenda kuu ikiwa ni ujamaa na utaifa kwanza.

Breaking News..Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA,Tundu Lissu Amekamatawa Jioni Hii na Polisi,Sababu ...!!!!

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu amekamatwa na Polisi muda huu wa saa 12.00 siku ya jumatatu tarehe 06.02.2017 akiwa anatoka Bungeni huko Dodoma. Haijajulikana hasa sababu za kukamatwa Kwake.

Chanzo. Mkuregenzi wa Itifaki na Mawasiliano ,Uenezi na Mambo ya nje Chadema John Mrema.

Kimenuka..Waziri Aaagiza Bungeni Shoga Maarufu Mitandaoni Akamatwe ,Kisa Hiki Hapa Liveee..!!!

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla, akijibu hoja za wabunge ameviagiza vyombo vya usalama kumtafuta mtu anayejulikana kwenye mitandao ya kijamii kama "James Delicious" kwa kujitangaza kama shoga kinyume cha sheria na kumfikisha mbele ya sheria kujibu tuhuma za kuendesha biashara ya kuuza ngono ya kinyume cha maumbile.

Gigy Money Ampiga Chini Mo J, Ahamishia Penzi Lake kwa Joti

$
0
0
U heard ya CloudsFM Leo, chini ya mtangazaji Soudy Brown imeleta hii  habari inayowahusu Watangazaji wa ChoiceFM, Gigy Money na Mo J ambapo inadaiwa wameachana baada ya Mo J kushtukia.

Inasemekana Mo J ameshtukia mawasiliano ambayo mwenzake alikuwa akiyafanya na mtu mwingine ambayo ikapelekea ugomvi hata mmoja kubeba nguo zake, sasa leo Soudy Brown ameongea na wote wawili.

"Mbali na mimi kuwa naye kwenye mahusiano yeye ana mambo yake anayafanya na alikuwa anayafanya labda amejisikia kumpost Joti au ni mshikaji wake" Amesema Mo J

"Nimeamua tu kumpunguza instagram……..kwani Joti hafai kupendwa na Gigy Money na ninakuambia pale sichomoki na nimefika dada yako, Mo J tushamwagana kipindi kitaenda tu" Amesema Gigy Money

Sikiliza habari kamili hapo chini

Ester Bulaya Apinga Kitendo cha Kuwakamata Waathirika wa Madawa ya Kulevya na Kuwatupa Selo..Ataka Rais Magufuli Ashauriwe Vizuri

$
0
0
Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya amefunguka na kutaka siasa isiingizwe kwenye vita ya madawa ya kulevya na kusema viongozi wasimdanganye Rais Magufuli ili kujihakikishia vyeo vyao au nafasi zao katika uongozi.

Ester Bulaya ametoa rai hiyo leo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa taarifa za kamati na kusema Rais anapaswa kuambiwa ukweli ili waweze kumsaidia kupambambana vyema na madawa ya kulevya.

"Tusifanye siasa kwenye vita hii ya madawa ya kulevya, tusimuongopee Rais kwa kutaka kuhakikisha vyeo vyetu tumwambie ukweli, ili kumsaidia Rais anapaswa kumteua kamishina wa hii tume maana tangu tulipopitisha sheria hiki chombo hakina kamishna, tutakapo hakikisha hicho chombo kinapata kamishna kwa kumsaidia Mhe. Rais tutakamata wale wanaoingiza dawa za kulevya wale mapapa na si hao wanaokamatwa sasa hivi" alisema Bulaya

Mbali na hilo Mbunge Ester Bulaya amesema kuwa hawa watu wanaokamatwa saizi wanapaswa kupelekwa mahospitali kupata matibabu na si vinginevyo kwani hao ni waathirika wa dawa.

"Mdogo wangu Makonda akitaka kupambana na dawa za kulevya aende magerezani akakutana na kina mama Reyla watamwambia mapapa wa madawa ya kulevya, ili tuungane pamoja na tunamkaribisha katika hili lindi kuhakikisha nchi yetu inapambana vikali dhidi ya madawa ya kulevya, kwa sababu mimi mwenyewe nina mdogo wangu anayenifuata yupo Mwananyamala anakunywa dawa methadone, hivyo ninachokisema nina uchungu nacho kwa kuwa nimekifanyia utafiti wa kina" Ester Bulaya 

Msikilize Hapo chini Akiongea

Fahamu Unywaji Pombe Salama Unaoweza Kuimarisha Afya Yako..!!!

$
0
0

Kipimo salama na sahihi kwa afya bora cha unywaji wa pombe kinabadilika kutokana na umri. Ongea na mfamasia wako kujua ni kiasi gani ni mahususi kwa afya yako.

Hakuna shaka umewahi kusikia kwamba unywaji wa wastani wa bia moja hadi mbili kwa siku kwa mwanamme husaidia kuimarisha afya yako na kukuepusha na magonjwa ya moyo. Lakini hata kama pombe ni rafiki au adui wa afya yako inategemea na vitu viwili; Hali yako ya afya ya sasa na ni kiasi gani cha pombe unachotumia. Ushauri kwa mtu mmoja mmoja ni mzuri zaidi.

Kwa baadhi ya watu inategemea na aina ya dawa wanazotumia na mambo mengine, utumiaji wa pombe hata kwa wastani inaweza kuwa ni hatari kwa afya yako.

Unywaji wa wastani kwa afya yako. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa watumiaji wa wastani wa pombe wanapunguza hatari ya kupata shinikizo la moyo na kiharusi, kisukari na huimalisha mifupa kwa wazee zaidi ya watu wanaokunywa kidogo sana au wasiokunywa kabisa.

Ninapozungumzia wastani namaanisha vinywaji viwili kwa siku kwa mwanaume na kimoja kwa wanawake. Watu wengine huepukana na unywaji wa pombe kwa sababu ni wagonjwa au sababu anatumia dawa zinazokinzana na pombe. Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako kwani zinaweza kukusababishia magonjwa ya moyo,kiharusi na aina Fulani za kansa ingawaje watumiaji wengi wa pombe huwa wanavuta sigara pia.

Baadhi ya matatizo yanayoweza kukufanya usinywe pombe;

Kama unatumia dawa zinazosinyaza damu (the blood-thinning medication) warfarin (Coumadin),pombe husababisha tatizo la kutokwa na damu.

Kama unafanya jitihada za kupunguza shinikizo la damu, hata kama utakunywa bia mbili kwa siku inaweza kupandisha BP yako.

Unywaji wa wastani husaidia watu wanaohiyaji kupunguza uzito.

Tafiti nyingi zimeonyesha watu wanaokunywa bia mbili mpaka sita kwa wiki wanapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo (cardiovascular disease) zaidi ya watu wanaokunywa zaidi. Watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 wanaume kwa wanawake inabidi angalau wanywe bia moja kwa siku. Bia mbili kwa siku zinaweza zisiimalishe afya yako licha yakuwa sihatari kwa afya yako.

Ni vigumu sana kusema kuwa kiasi fulani ndo sahihi kwasababu tafiti nyingi za kisayansi zinaonesha utofauti kutokana na utofauti uliopo baina ya mtu na mtu na jamii inayowazunguka.

Kama haunywi pombe usijaribu kuanza kunywa kabisa kwa matarajio ya kuimarisha afya yako. Ni vema ukaanza mazoezi, ukila vyakula vya kujenga mwili na matunda na usijaribu kuvuta sigara kabisa. Ukizingatia vitu hivi utaimalisha afya yako kwa kiasi kikubwa.

“Kwa watu ambao hawanywi pombe kabisa, ushauri wangu wasijaribu kunywa kabisa, kwani kuna njia nyingi za kukufanya kuwa na afya bora kuliko kuanza kutumia pombe na kuanza kukubwa na athari nyingi za kiafya zinazosababishwa na matumizi ya kupindukia ya pombe.”

Kiasi sahihi ya pombe kinachoshauriwa kiafya ni kama kinavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo

Vinywaji vingine vya pombe vina nguvu kuliko vingine. Kwahiyo ni vizuri kuangalia ni kiasi gani kinachokufaa kiafya, kwa mfano cocktile zingine unaweza kuona zipo kwenye glasi ndogo lakini kumbe ina nguvu zaidi ya bia tatu mpaka nne.

Your Health, Our Concern

Je Wajua? Mbu Wamejifunza Mbinu Mpya ya Kujikinga na Chandarua Chenye Dawa..!!!

$
0
0

Jinsi ambavyo baadhi ya bakteria wasivyo na hofu siku hizi kuhusu antibiotics, ndivyo ambavyo mbu wamebuni njia mpya ya kujikinga na chandarua kilichowekwa dawa. Hii ni kutokana na utafiti mpya uliochapishwa na gazeti la ‘infectious Diseases”.

Utafiti huo uliofanywa kwa miaka minne katika nchi ya Papa New Guinea ili kuangalia ni kwa namna gani ugawaji wa vyandarua vyenye dawa vimeweza kusaidia kupiga vita ugonjwa hatari wa malaria.

Vyandarua vilivyopigwa dawa vimeonekana kama njia sahihi na yenye mafanikio kwenye kupunguza vifo zidi ya ugonjwa hatari wa malaria. Kutokana na takwimu zilizotolewa na American Council on Science and Health, kesi (case) tofauti tofauti milioni 451 zimeweza kuzuiwa za malaria katika miaka 15 iliyopita kutokana na utumiaji wa vyandarua vilivyowekwa dawa.

Utafiti huu umeonyesha kuwa mbu sasa hivi wamebadili utaratibu wa kuuma (feeding behavior) katika miaka ya hivi karibuni ili kujiepusha na vyandarua vyenye dawa.

Kabla ya ugawaji wa vyandarua vilivyowekwa dawa mbu walikuwa na tabia ya kung’ata kuanzia usiku wa manane. Lakini baada ya watu kuanza kutumia vyandarua vyenye dawa, mbu wamebadili ratiba yao ya kupata chakula na kuanza kung’ata kuanzia saa nne usiku (10 p.m) na wengine hung’ata kuanzia saa moja(7 p.m) mpaka saa tatu usiku (9 p.m). Ili kuwapata watu kabla hawajaingia ndani ya chandarua chenye dawa.

Kupungua kwa kesi (case) nyingi za malaria kutokana na kung’atwa na mbu kumefuatiwa na kuongezea tena kwa kesi hizo kiama ilivyokuwa awali kabla ya mgao wa vyandarua vilivyowekwa dawa kwa baadhi ya maeneo. Utafiti huo umekuwa unaleta matokeo tofauti tofauti pia katika vijiji tofauti tofauti.

Nitoe wito kwa watanzania tuendelee kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa kwani vimeonyesha kupunguza idadi kubwa ya kesi (case) za malaria, lakini pia tujitahidi kuweka mazingira safi yanayotuzunguka ili kufanya mazingira yetu yasiwe mazingira salama kwa mbu kuzaliana na kuishi. Malaria haikubariki, tuungane kutokomeza ugonjwa huu hatari wa malaria.

Your Health, My Concern

Video : Ay afunguka siri ya kutumia meno ya Dhahabu kama Diamond Platnumz

$
0
0

Kumekua na wimbi kubwa la wasanii hasa wa Bongo Flava kuanza kuvaa meno ya dhahabu. Baadhi ya wasanii ambao wameonekana wakivaa meno hayo ni pamoja na Dogo Janja na Diamond Platnumz.

Lakini siku za karibuni msani AY nae kaanza kuonekana akiwa kavaa meno hayo. Na alipoulizwa kua ilikuaje na yeye akaanza kuvaa meno hayo alifunguka haya ambayo wengi tulikua hatujui. Unaweza tazama video yote kwa kuclick play hapa chini

Kimenuka..CUF ya Maalim Seif Yatoa Majibu Haya kwa Prof Lipumba..!!!

$
0
0

 Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitafanya mazungumzo kusaka suluhu na mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa na kwamba, kipo tayari kwa lolote hata kama kitafutiwa usajili.

Pia, chama hicho kimesema hakijuti kumkaribisha na kumuunga mkono Edward Lowassa, ambaye aliteuliwa kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema na kuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Maelezo hayo yalitolewa juzi na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF,  Mbarala Maharagande kujibu madai yaliyotolewa na Profesa Lipumba alipohojiwa katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Azam.

Katika mahojiano hayo, Profesa Lipumba alidai kuwa mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sasa hautamalizwa na mahakama pekee bali viongozi wa pande mbili na kuzungumza, lakini Maharagande amesema haiwezekani kwa vile Lipumba alishakwisha kukivuruga na hafai tena kuendelea kuwa kiongozi.

“Lipumba anasema tukae tulimalize suala hili kwa kuongea sisi wenyewe. Jambo hilo haliwezekani kwa kuwa kama kupandikiza chuki, uhasama, uharibifu wa chama miongoni mwa wanachama na viongozi ameshafanya na kufanikiwa hilo kwa baadhi ya wanachama na viongozi wake na kuharibu taswira ya chama kwa jamii,” alisema Maharagande.

Kamanda Sirro :Tumemkuta Wema na Misokoto ya Bangi na Makaratasi Yake,Hivyo Naye Atapanda Mahakamani Tu ..!!!!

$
0
0

Sakata la wasanii 12 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi limezidi kukua baada ya watu wengine 100 kukamatwa.

Kati ya watu 112 ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na utumiaji au biashara ya dawa hizo, 12 kati yao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo baada ya kazi hiyo kushindikana jana.

Miongoni mwa watuhumiwa wanaotarajiwa kupandishwa kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ni mwigizaji maarufu wa filamu Wema Sepetu na msanii mwenzake Omary Micheri ambao polisi wamedai walikutwa na vielelezo vya dawa za kulevya na bangi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro alisema watawafungulia watuhumiwa maombi ya kuwaweka chini ya uangalizi wa mahakama na polisi kwa muda wa miaka miwili na watakuwa wakiripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi.

Siro alisema kati ya watuhumiwa 12 waliokamatwa kwanza, 10 walikiri kutumia dawa hizo na kuwataja wauzaji lakini wawili walikutwa na vielelezo nyumbani kwao.

Alisema Wema, ambaye aliwahi kushinda taji la mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania), alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na misokoto ya bangi na makaratasi yake, wakati Micheri alikutwa na kete tatu za dawa za kulevya ambazo hazijajulikana za aina gani hadi zitakapofanyiwa uchunguzi.

Wabunge Wapinga Wizara Kutumia Majengo ya Udom..!!

$
0
0

Siku chache baada ya wabunge kueleza kutoridhishwa na Serikali kuhamia kwenye majengo ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii nayo imepinga hatua hiyo.

Kamati hiyo pia imeshauri Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), kuachana na utaratibu wa kupangia wanafunzi vyuo na ijikite kusimamia ubora wa elimu inayotolewa na vyuo vikuu nchini.

Mapendekezo hayo yalitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2016.

Serukamba ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kamati hiyo ya Bunge inaunga mkono Serikali kuhamia Dodoma, lakini utaratibu wa wizara kuhamishia ofisi zao Udom siyo sawa.

Wizara ambazo zimehamishia ofisi zake Udom kutoka Dar es Salaam ni Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Katiba na Sheria; Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Magufuli Afichua Sababu za Kumwongezea Siku Nne Mwamunyange

$
0
0

Rais John Magufuli amefichua sababu za kumuongezea siku nne zaidi aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, akisema kwa kuwa alikuwa nje ya nchi, hakuwa na mtu anayemwamini kumwachia nafasi hiyo.

Mwamunyange alistaafu rasmi Januari 31, 2017 na alimtaarifu Rais Magufuli wakati akijiandaa kusafiri kwenda Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Akizungumza wakati wa hafla ya kumwapisha mkuu mpya wa majeshi, Jenerali Venance Mabeyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Magufuli alisema alipata wakati mgumu kuteua mrithi wa Jenerali Mwamunyange ndani ya siku nne ambazo alisafiri kwani alikuwa bado hamjui.

 “Nilipokuwa nikienda kwenye mkutano wa AU, Jenerali Mwamunyange aliniambia ‘unajua siku zangu zinaisha tarehe 31 (Januari), sasa ninafanyaje, naomba umteue anayekuja’. Nikasema ‘sasa nikiondoka leo nikamteua (mkuu mpya) tarehe 24 (Januari) na wewe unaondoka tarehe 31 (Januari), si wataanza kusema nimekutumbua? Kwa sababu Watanzania wanajua kubadilisha maneno kweli. Wataanza kusema fulani ametumbuliwa kabla ya wakati wake na hiyo ndiyo itakuwa stori’,” alisema Rais.

“Lakini nikamwambia mimi nasafiri, ninayekujua ni wewe, ninayemteua simjui. Sasa nikishamteua ambaye simjui, hizi siku nne ambazo nitakaa nje itakuwaje?”

Alisema ilibidi amwombe Jenerali Mwamunyange aendelee na wadhifa huo hadi atakaporudi kutoka Ethiopia.


Rais Magufuli alisema akiwa Ethiopia, viongozi wa nchi nyingine walikuwa wakiulizia nani anayerithi baada ya Mwamunyange kuondoka.

“Nikawa naulizwa nani atakuwa mkuu wa majeshi, naulizwa na watu wa nchi nyingine, wala si Watanzania. Nikajua kumbe hii nafasi inaangaliwa na watu wengi,” alisema Rais Magufuli.

Kudadadeki:Wabunge wa CCM na Ukawa Wamshambulian Makonda Baada ya Kuwataja Kina Wema Kuhusika na Madawa ya Kulevya..!!!

$
0
0

Sakata la dawa za kulevya jana lilitikisa Bunge mjini hapa baada ya wabunge kutaka orodha ya ‘wauza unga’ ambayo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema anayo ili ifanyiwe kazi na mrithi wake, John Magufuli.

Akichangia taarifa za Kamati ya Bunge ya Ukimwi na ile ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisema Rais Kikwete aliwahi kuutangazia umma kuwa anayo orodha ya vigogo wa dawa za kulevya hivyo alitaka wakamatwe ili watumiaji waachiwe.

“Kikwete alisema anayo orodha ya wauza dawa za kulevya. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mwigulu Nchemba) amfuate kule Msoga ili ampe hiyo orodha. Naamini watumiaji wataachiwa,” alisema.

“Vita ya dawa za kulevya siyo ya Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam), hii ni vita ya Serikali na naamini itamuunga mkono. Mtu akipimwa akionekana ni mtumiaji atusaidie kumpata muuzaji,” alisema.

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alimtaka Rais Magufuli kuacha kuendesha nchi kwa sanaa na kutafuta habari zake zipewe uzito katika vyombo vya habari, badala ya kushughulika na tatizo.

Mbunge huyo alisema kwa mwaka 2016/2017, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini ambayo ndiyo yenye dhamana ya vita hiyo haikupata fedha za maendeleo. “Leo bajeti ya tume ni sifuri halafu anasimama mkuu wa nchi anasema vita ipiganwe. Tuache kutafuta vichwa vya habari kwenye vyombo habari,” alisema Mdee.


Aliongeza, “Vita hii inahitaji utashi wa kisiasa. Kikwete alisema anawajua wauza unga kwamba ana orodha. Alipoondoka Ikulu si aliacha mafaili? Orodha unayo hapo Ikulu tusicheze na akili za Watanzania,” alisema.

Pitia Vichwa vya Magazeti ya Leo 7/2/2017..!!!

Video... Zitto Kabwe Aaamua Kuingilia Kati Sakata la Wema Sepetu Kukamatwa na Makonda,Haya Ndiyo Aliyosema Bungeni..!!!!

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images