Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104780 articles
Browse latest View live

Mpya Zakunyapia Nyapia..Kisa Wema Kulala Lupango, Mama Wema Hali Mbaya….!!!!

$
0
0

 Hali ni tete! Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja majina ya wanaotuhumiwa kujihusisha biashara na matumizi ya madawa ya kulevya wakiwemo mastaa ambapo Ijumaa iliyopita baadhi yao walitii wito na kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar ‘Sentro’ kwa ajili ya mahojiano akiwemo Wema Isaac Sepetu, mama yake mzazi, Mariam Sepetu anaelezwa kuwa katika hali mbaya kutokana na mwanaye huyo kulala lupango.

Chanzo makini kilicho karibu na mama Wema kilieleza kuwa, baada ya Ijumaa, Wema kwenda kuhojiwa Sentro na kulala lupango, hali ya hewa ilibadilika nyumbani kwa mama yake, Sinza-Mori, Dar kwani mzazi huyo presha ilikuwa juu na kusababisha akeshe akilia usiku kucha.

“Yaani siku ya Ijumaa ambayo Wema na wenzake waliotajwa walikwenda kuhojiwa Sentro kisha kulala lupango, ilikuwa ni siku ngumu sana kwa mama Wema kwani alikuwa akilia siku nzima na usiku wake hakulala kabisa hadi kunakucha.

“Alfajiri ya Jumamosi, ilibidi ndugu zake wamfuate na kumchukua, haikujulikana kama walimpeleka hospitali au wapi lakini hali yake ilikuwa mbaya huku akimlilia mwanaye Wema ambaye alilala lupango ,” kilisema chanzo hicho.

WIKIENDA KWA MAMA WEMA

Baada ya habari hizo kutua kwenye meza ya Wikienda, wanahabari wetu walitinga nyumbani kwa mama Wema na kukutana na kijana ambaye alifungua geti kwa nafasi ndogo huku akiwa anaonesha wasiwasi mkubwa na kutetemeka.

Kijana huyo alipoulizwa kama mama Wema alikuwepo alijibu hakuwepo. Alipoulizwa alikokwenda alisema: “Alichukuliwa alfajiri na ndugu zake.” Alipoulizwa hao ndugu zake walimpeleka wapi alijibu: “Sijui’. Alipoulizwa hali yake kiafya ilikuwaje, alifunguka: “Mama yuko kawaida tu.”

Alipoulizwa juu ya Wema kutoka lupango au la, alijibu:

“Kuhusu Wema haishi hapa, yeye anaishi Ununio.”

Alipoona anabanwa zaidi na maswali, alibamiza geti kisha alikaa kimya.

Wakati Akiiacha White House Obama Anakupa Njia 6 za Kufanikiwa

$
0
0

Obama si mchoyo, amekuwa akizungumza katika vituo mbalimbali vya televisheni na hata kwenye majukwaa kuwaeleza watu ni mambo gani wanatakiwa kufanya ili wafanikiwe.
Haya hapa chini ni miongoni mwa mambo hayo ambayo kama ukiyafanya, hakika utafanikiwa;

JUA UTAFANIKIWA TU.

Kuhusu mafanikio, Obama anasema kama unataka kufanikiwa ni lazima ujue na kuamini kwamba utafanikiwa tu.

Wengine wamekuwa hawafanikiwi kwa kuwa hawajui kama watafanikiwa. Alitolea mfano hai kwamba mwaka 1962, aliyekuwa Rais wa Marekani, John Kennedy aliwaambia Wamarekani kwamba hawawezi kwenda mwezini kwa kuwa ni mbali sana.

Lakini miaka saba baadaye Neil Armstrong akawa mwanadamu wa kwanza kufika huko. Hivyo ndiyo ilivyo, wengine wameambiwa maneno mabaya kwamba hawawezi kufika kwenye mafanikio kwa sababu tu wanaambiwa kwamba ni vigumu, ndugu yangu, kuanzia leo jua kwamba utafanikiwa hata kama kutakuwa na watu wengi wakizungumza maneno ya kukukatisha tamaa.

HUTAKIWI KURIDHIKA.

Obama anaendelea kusema kwamba ili ufanikiwe, hutakiwi kuridhika hata kidogo. Wengine wamekuwa wakianguka au kutokufanikiwa kwa kuwa tu waliridhika, waliingiza kiasi fulani cha fedha, wakajenga nyumba na kununua magari wakaridhika.
Mafanikio si kununua gari tu, si kununua nyumba tu, bali ni kuwa na biashara nyingi ambazo zitakuingizia fedha kila siku.

UWE NA MALENGO.

Obama anasema kuwa, huwezi kufanikiwa bila kuwa na malengo. Ni lazima unapoianza safari yako ujiwekee malengo kwani utakuwa ukifanya vitu kuendana na malengo uliyojiwekea.

Kama hutaweka malengo, utakuwa unafanya vitu bila mpangilio wala mwelekeo. Maisha ya mfanyabiashara ni lazima yawe na malengo ambayo ndiyo ramani ya biashara yako na mafanikio yako kwa jumla.

HUWEZI KUFANYA PEKE YAKO.

Kwa mujibu wa Obama kama walivyo wengine wote wenye mafanikio, safari ya mafanikio ni ndefu. Wengine wamekuwa wakihisi kwamba wanaweza kusimama wakiwa
peke peke yao.

 Ndugu zangu anachokisema Obama ni ukweli, huwezi kusimama peke yako hasa kwenye masuala ya biashara na ndiyo maana mara kwa mara unasikia kuna vikao vya wafanyabiashara. Utakapofanya kila kitu peke yako, hutapata mawazo mapya kwa sababu utakuwa unaiamini akili yako pekee katika kukufikisha sehemu f’lani.

Ili ufanikiwe, unatakiwa kuwashirikisha wafanyabiashara wenzako na ikiwezekana, ukianzisha jambo, unaweza kuwaita na kuhitaji ushauri wao, watakuwa msaada mkubwa kwako.

ACHA VISINGIZO.

Anasema kuwa wafanyabiashara wengine wamekuwa na kawaida ya kulalamika hovyo. Wanaanzisha malengo yao, lakini mwisho wa siku wanakuja na visingizio kwamba hawakufanikiwa kwa sababu fulani, hawakufanikiwa kwa kuwa kulikuwa na watu waliowavuta nyuma kutoka kule walipokuwa wakielekea.

Mfanyabiashara ukianza kutafuta visingizio, hutafika kwa sababu hakuna mfanyabishara anayefanya biashara bila kupitia vikwazo mbalimbali ambavyo usipokuwa makini ndivyo vitakavyokuwa visingizio. Kwamba, hujafanikiwa kwa kuwa haukuwa na muda mrefu wa kazi au visingizio vingine.
Unachokipata, kifanye tena kwa umakini mkubwa na kujitolea, achana na visingizio.

IFANYE BIASHARA YAKO IWE SERIOUS.

Obama anasema kwenye biashara kuna watu wanahisi kwamba wakiwa serious mno ndiyo wanaweza kufanikiwa. Huwezi kufanikiwa kama utayafanya maisha yako kuwa serious.

Matajiri wengi wanakuwa serious kwenye biashara na si maisha yao binafsi ndiyo maana wanacheka na watu, wanataniana ili maisha yasonge lakini kwenye biashara, huko ndipo unapotakiwa kuleta u-serious kupita kawaida, kwani ukileta utani, utafeli.

Idris Sultan Achukizwa na Wanafiki Waliomrekodi Wema Sepetu Bila yeye Kujua Akiwa Selo....Adai Hawajui Wanamuumiza Kiasi Gani

$
0
0

BY@idrissultan - Na muendelee kupiga kelele kutembelea watu central na recording people bila wao kujua. Kwakua tunachukulia maisha ya watu kama mfumo wa likes na following bila kujua tunawaumiza kiasi gani kwa tunachokifanya basi let us proceed na tutaona kama tunaowapenda kama tunavyosema tutakua tumewatendea haki. Kwa hili nimeshindwa kunyamaza, you claim to be friends and true people kumbe unafki unatujaa 🙈. We will kill our families and be the 1st to cry kwenye msiba WHERE IS HUMANITY ? 😒 Kama hamjaenda kutoa moral support basi kaeni majumbani kwenu na mposti posti vimachozi na unafki wenu sio kutuchafulia hata pale pasafi padogo palipobaki 😡😡😡

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Kutoka Bagamoyo , Anarudisha Mapenzi na Kusafisha Nyota

$
0
0

MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI, (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 48 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI:

SHEKH SHARIFU RASHIDI ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran, dawa za asili, dawa za kiarabu na majini, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango, ngiri maji na n.k, anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, pia anatoa pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali kulingana na nyota yako, anaouwezo mkubwa wa kutumia jina la muhusika kwa kutatua tatizo lako, anaouwezo wa kumrudisha mtu aliepotea kimiujiza, pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo,

WASILIANA NAE KWA SIMU NA WHATSAPP NO: 0718-668347. 0685-224047, 0767-204308 au follow@shekh_sharifu_rashid, Email:shekhsharifurashid@gmail.com

Producer P Funk Amesema Haya Baada ya Kumualika Harmorapa Kumtembelea Studio Kwake

$
0
0
Harmorapa umaarufu wake umeanzia tu kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii akijifananisha na mwimbaji wa WCB Harmonize na baada ya hapo ndio akaanza ku-trend.

Leo jana Producer maarufu wa Bongo Records P Funk Majani ambaye anazo sifa nyingi za kuwa hodari wa kuwatoa Wasanii wengi, amemualika Harmorapa kwenye studio yake na kuipost picha wakiwa pamoja na ikazua maswali mengi.

P Funk Ameongea Haya:

“Amekuja kiushkaji tu alitaka kuja kuniona kupata ushauri kwahiyo nimemualika tu amefika fresh nimemuelekezamuelekeza“
“Nimesikiliza nyimbo zake nimemuweka sawa tu na kumwambia ukweli, anaonekana kama anaandika… uwezo wa kuandika anao lakini anachana zile za kizamani, sasa nikawa nampa mbinu za kisasa jinsi ya kudandia kwenye beat na kucheza nazo”
“Kila mtu ameanza sehemu flani, hata mimi siku za kwanza nilikua nagonga beat mbaya… ni kitu tu kukitaka na kukijenga moyoni utakipata…. kwasababu watu wote wanamtolea macho nimemwambia usifanye kitu cha kipuuzi, utapoteza mashabiki wote ukifanya kitu takataka”
“Ni mtu ambaye anaelewa sana na ana roho nzuri, ana heshima sana…. ni baraka za Mungu ndio maana naona watu wanampenda sana, ana heshima sana…. tumsaidie bwana !! kuhusu kurekodi nae studio kwangu hapana…. bado hajafika hapo nimemwambia kabisa kuna siku itafika lakini sio sasa hivi… mpaka ukajirekebishe”

VIDEO: Mbunge Aliyetayari Kutaja Wabunge Wanaouza Dawa za Kulevya Tanzania

$
0
0
Mjadala wa Watuhumiwa wa biashara na watumiaji wa dawa za kulevya umeendelea kuchukua nafasi baada ya kuibuliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Mjadala umefika mpaka Bungeni Dodoma na baadhi ya Wabunge waliosikika wakichangia ni pamoja na Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga aliyesema yupo tayari hata kuwataja baadhi ya wabunge wanaohusika na bishara hiyo.

Tazama hii Video hapa chini akichangia ishu mbalimbali ikiwemo na hiyo:

Babu Tale Awashukia Waongozaji Video wa Tanzania...Atoa Mifano Kwa Video Zilizofanana Location

$
0
0
Babu Tale
Babutale ni meneja maarufu wa kundi la bongofleva la Tip Top connection lakini pia ni meneja wa mwimbaji Diamond Platnumz ambapo leo Tale ameguswa na baadhi ya video kadhaa za bongofleva baada ya kuzitazama akaandika haya.

"Hii ni kwa ndugu zetu madirector wa nyumbani tanzania, tunaomba angalau muwe mnajishugulisha kuangalia vitu ambavyo havijatumika ili kuepuka kufananisha video zetu,sababu inapelekea wasanii kukimbia na kwenda kufanya kazi zao nje ya nchi"
"Mfano kuna video ya dogo janja na roma zote location moja,madee bilnas na wengine wote wametumia vitoa moshi,chege na ben paul wote wametumia gari moja,hilikosa ni la msanii au director? #kelele_za_chura@chegechigunda"

Picha: Wema Sepetu na Wenzake Wafikishwa Mahakamani Leo...

$
0
0
Wasanii akiwemo Tunda, Wema na Rachael na baadhi ya watu wanaoshikiliwa na kituo cha polisi kati kwa tuhuma ya dawa za kulevya wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wameshushwa nyuma ya majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku baadhi ya wakijifunika nyuso zao kukwepa camera za mapaparazi...

Video : Ben Pol afunguka kuhusu kuwepo kwa bifu kati yake na Baraka Da Prince

$
0
0
Siku za hivi karibuni kumetokea wimbi kubwa la baadhi ya wasanii kuwatuhumu wasanii wenzao kua wamewaibia mashairi au wimbo mzima. Wengi hujitokeza mda mchache baada ya nyimbo hiyo kuachiwa.

Habari zilizopo kitaani ni kua kuna bifu la chinichini kati ya Baraka Da Prince na Ben Pol kuhusiana na tuhuma kua Ben Pol aliiba wimbo wa Moyo Mashine kwa Baraka. Ben Pol ameamua kujibu tuhuma hizo kwa kukanusha na kusema hayaaa, bonyeza play hapa chini kutazama alichokisema

Mbunge Msukuma Acharuka Bungeni..Adai Paul Makonda Aseme Anatoa Wapi Hela za Kwenda Kupumzika Paris na Marekani

$
0
0
Vyanzo vya Taarifa katika Kikao cha Bunge kilichoendelea jana jioni, Mbunge wa Geita Ndugu Musukuma amemtuhumu RC Makonda kuwa naye anahusika na dawa za kulevya.

Amedai kawa RC Makonda kwa mshahara wa U RC aeleze ni akina nani walimsafirisha kwenda Marekani na PARIS.

Musukuma ameenda mbele zaidi kasema Makonda aanze na wakwake aliyowapangishia majengo

Tuhuma za Makonda kusafirishwa likizo Nje ya Nchi na kuwa waliomsafirisha wanahusika na madawa ya kulevya hivyo anawalinda inaibua maswali mapya. Je nani anagharimia safari za Makonda Nje ya Nchi.

Hii vita ni kubwa ndugu zangu.

Sikiliza Hotuba ya Halima Mdee Hapa Akitoa Povu Kuhusu Madawa ya Kulevya...Adai Wauza Unga Wanajulikana na List Ipo Ikulu

$
0
0

Sikiliza Hotuba ya Halima Mdee Hapa Akitoa Povu Kuhusu Madawa ya Kulevya...Adai Wauza Unga Wanajulikana na List Ipo Ikulu ilishafanyiwa kazi na waliopita

Bonyeza Play

James Delicious Amlilia Mungu. Adai Hana Raha ya Maisha Kufuatia Agizo la Waziri

$
0
0

Ameandika James Delicious Baada la Agizo kutoka kwa waziri kuwa akaripoti polisi kutokana na kujihusisha na vitendo vya ushoga:

"Oooh my God NAPIGIWA SIMU KAMA MWEHU..KUMBE NAPEWA TALIFA MBAYA TENA NATAKIWA KUKAMATWAA Okay.. Yupo msemaji wangu Wa mwisho. Na nimunguuu.. Pekeeee .. Coz only God can judge me Sito ogopa chochote.

Naiman ntayashinda ya DuniiiaWhy nikamatweee Dunia nzimaaa Niko peke yangu. And kwa ushahid upiii ??? Ooooh.. Wanataka nikose aman na maisha yangu

Kwan kuna anae nilishaa ??? Kuna anaenijuaa chimbuko langu ??? Why wanataka nikoseee rahaa ya maishaaa. Ooooh my God sina lakuongea kwakweli siiiinaaaaa yaaaan mwili wotee umeshikwaa ganziii Sjuuui mama angu akizskiaa talifa hiz atapata halii Gan uko alikoo .sjuui kesho kwenye media nyaandikwajee.

Najuuuta nandomana roho yangu tokaaa mwanzo ilikuwa inasitaa kujiungaa instaa. hasara zakee ndohiiiz.

Okay..

Nasubili hukumuuu. #sinarahayamaisha "

Wema Sepetu Hakupandishwa Mahakamani Leo..Aendelea Kushikiliwa..Wengine Wapata Dhamana

$
0
0
Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi hii.

Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Watuhumiwa wote wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo upande wa Jamuhuri umeomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi
               
Wakili wa upande wa utetezi amedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangalizi wa nidhamu.

‘Mnamuonea Wema Sepetu’, Mashabiki Wake Nchini Kenya Walalama

$
0
0
Wema Sepetu ni miongoni mwa mastaa wakubwa wa Tanzania walioitwa na kufika katika kituo cha polisi cha central jijini Dar es Salaam ili kujibu tuhuma za kuhusishwa na dawa za kulevya.

Habari hizi ambazo zimesambaa kwa nguvu kama vile moto kwenye mbuga ya wanyama wakati wa kiangazi na kuzagaa kwenye vyombo mbambali vya habari Afrika Mashariki, zimewashutua wengi haswa mashabiki wa malkia huyo wa filamu Afrika.

Si ndani ya nchi ya Tanzania pekee ambapo mashabiki wa Wema Sepetu wameteta kuhusu staa huyo kudhalilishwa kwa kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya bali hadi hapa ndani ya nchi ya Kenya.

Naziangazia baadhi ya nukuu za waziri Nape ambazo zimeonyesha kuwa waziri huyo hakufurahishwa wala haungi mkono jinsi zoezi hilo lilivyofanyika, “Lazima itumike busara, tusiwahukumu watu kwa tuhuma, kutengeneza brand ni kazi kubwa sana wakati kuibomoa ni jambo la sekunde tu. Kama wizara tunaunga mkono juhudi za kupambana na dawa za kulevya, tatizo ni namna ya kushughulika na wahusika ikiwemo busara. Tunaunga jitihada za mapambano lakini ni vizuri lifanywe katika namna ya kulinda haki ya mtuhumiwa ili heshima yake isipotee.”

Huu ulikuwa ukweli mtupu kutoka kwa waziri Nape, maana alijua athari za kuwatuhumu wahusika hasa ikizingatiwa baadhi yao ni watu mashuhuri nchini Tanzania.

Athari hizo zimeaanza kuonekana si Tanzania pekee bali Afrika Mashariki labda na bara zima la afrika. Kwenye mitandao ya kijamii, vituo vya redio na hata runinga Afrika Mashariki, habari hizo zimetengeza headlines zenye uzito.

Katika mchakato huo, tovuti moja maarufu nchini Kenya kwa jina, ”Nairobi News” kama vyombo vingine vya habari nchini Kenya liliitumia fursa yake kuwasilisha kwa mashabiki wake habari hizi kwa kichwa kilichosem, ‘Top Tanzanian celebrities linked to drug trafficking’ nakushare habari hii kwenye Fan-page yao ya Facebook.

Wengi walio tupia comments zao, walionekana kuegemea kukashfu vikali kutajwa kwa jina la Wema Sepetu kwenye kashfa hiyo. Hii ni ishara ya kuwa Wema Sepetu anakubalika na kupendwa na halaiki ya mashabiki hapa nchini Kenya, na nikiwakumbusha tu, kuna wakati mwaka jana 2016 Sepetu alizulu Kenya na akakaribishwa vizuri hadi akaeleza kupitia mtandao wa kijamii jinsi alivyo karibishwa Kenya na huenda akafikiria kuhamia nchini humu.

Hizi hapa chini ni baadhi ya comments za wakenya na headline kutoka kwa ukurasa wa Facebook wa tovuti ya Nairobi News.

Maggie Nyawi

mmmh……..when will u stop interfering with others pples international
affairs?……if it’s true or into what will ugain
by gossiping n telling public?

Annitah Walcoltt

Wema ain’t this crap…..Spare my Wema

Omar Elmy

its not true

Sharon Phiny
Even Wema Sepetu and Idriss have been mentioned and they look innocent?


Makala ya: Changez Ndzai

Serikali Kupiga Marufuku Pombe za Viroba....

$
0
0
Serikali inatarajia kupiga marufuku utengenezaji na uingizaji wa pombe za bei rahisi maarufu kama “Viroba” Nchini, ndani ya miezi mitatu ijayo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakilalamikia  kilevi hicho kinavyopunguza nguvu kazi ya Taifa, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi pamoja na Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2016/17.

Dkt. Kigwangalla amesema kuwa baada ya miezi mitatu kilevi hicho kitapigwa marufuku kutengenezwa au kuingizwa nchini pamoja na kuziba mianya yote ya uingizaji wa kilevi hicho ambacho kimekuwa kikitumiwa na vijana wengi, hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko amesema kwamba pombe hiyo inasababisha vifo vya vijana wengi nchini ambao ndio tegemeo kubwa na nguvu kazi ya Taifa.

“Katika kipindi hiki kifupi cha likizo yangu, nilikuwa jimboni kwangu na tumezika vijana wanne ambao wamefariki kutokana na matumizi ya viroba. Hivyo wananchi wa jimbo langu wameniagiza kuja kulieleza Bunge athari za pombe hiyo ili tuweze kujadili na kuona namna gani  ya kuliokoa Taifa hasa vijana kutoka katika janga hilo,” alifafanua Matiko.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Kamati imebaini uwepo wa uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya pombe hizo na kuongezeka kwa tabia hatarishi zinazochangia ongezeko la vijana katika matumizi ya dawa za kulevya.

Aidha amesema kuwa hali hiyo inaathiri ufanisi wa nguvu kazi ya Taifa kutokana na madhara ya matumizi ya dawa za kulevya. Hivyo Kamati imeishauri Serikali kufungia kabisa uzalishaji na uuzwaji wa pombe hizo za viroba ili kulinusuru Taifa

Maamuzi ya Mahakama Kuhusu Wasanii Wanaoshtakiwa Kwa Dawa za Kulevya

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imetoa maamuzi kwa baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.


Mahakama hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili Petitman na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 20 na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa muda wa miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.

Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi  watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani

Sad Story:Siwezi Wachukia Wanawake wote..Ila Wamenitenda Sana

$
0
0

Mimi ni kijana wa kiume nina miaka 24, makazi yangu ni jijini mwanza,nimeamua kushea story yangu ili niweze kupata ushauri kwa watu mbali mbali juu ya nini nifanye baada ya kutendwa katika kila uhusiano ninao anzisha naweza nikasema nilichelewa kidogo kujihusisha na mapenzi kwa mujibu wa Dunia ya sasa,na hii ni kwa sababu nimelelewa na kukua katika familia yenye maadili.

Siwez nikasema nina mvuto mkubwa saana , niko simpo tu kama profile pictures zangu zinavyojieleza lakini siku zote nimejikuta nikiwa kipenzi cha kinadada wengi kulingana na mazingira husika ntakayokua nikiishi, na binafsi me ni mwanamume mtanashati naejpenda sana, mpole na zaid ni mcheshi haswa pengine hizo ndiyo sababu..na story yangu ya mahusiano inaanza nikiwa na miaka 20,kipindi nilipojiunga katika chuo kimoja hapa mwanza.

Baada ya kufika pale chuoni nilijijengea idadi kubwa tu ya marafi na kama unavyojua mtu mcheshi hua ana malafiki wengi ,pamoja na hayo, ckua na mawazo kabisa ya kuwa na msichana kimapenzi richa ya kua nlikua nina miaka 20,na kiukweli nilikua kama naogopa ogopa coz ckuwahi kabla richa ya kua wasichana wengi walikua wakijiweka karibu sana tu na wengi walihisi natoka nao au mmoja wapo..ila baada ya mda kuna mdada mrembo ambae nilimkuta pale chuoni alikua amenizd umri kama miaka 3 hivi,alitokea kunizoea sana,kama kunichukulia chakula.

kuja chumbani kwangu n.k hivyo akatokea kua mtu wangu wa karibu lakini kumbe alikua ananitaka kimapenzi na mwisho wa siku baada ya kua amenitamkia mwenyewe akaja kua galfriend wangu wa kwanza...kiukweli niliyafurahia sdana mahusiano yale,na yeye akawa ndiye mwalimu wangu katika mapenzi.

furaha yangu na huyo dada ilidumu kwa takribani miezi 9,na mambo yalikuja badirika alipokalibia kumaliza chuo, maana alikua
amenitangulia,kidogo kidogo vituko vikaanza mara hapokei cmu,hataki story na mimi,akitoka hataki tuongozane na anatoka akiwa ameupala kupita kiadi,kama mtu mzima kengere ya hatari ikaanza kugonga kua kuna kitu na pengine no more love tena.

Kiukweli nilikua naumia sana,sana tu,coz kuna kipindi alikua ananifokea hata mbele za class mates na ukizingatia mimi ni mpole sana,nilivumilia lakini mambo yalipozidi ikafika hatua nikasema NO,nami nikakata kamba baada ya kugundua kumbe alikua akimegwa na limtu lingine,hivyo nami nikajitahidi kukaa mbali nae ingawa nilikua naumia sana nimwonapo,na hatimae ukafika mda wao wa kufanya mtiani wa mwisho,ila kwa bahati mbaya yeye na baadhi ya wanafunzi walifutiwa mtiani kwa kosa flani kwenye chumba cha mtiani hivyo iliwabidi wabaki wfanye mtiani upya,na hawakuruhusiwa kukaa hostel za chuo,kiukweli nilimhurumia sana EX wangu ,coz ckua na kinyongo na nilikua bdo nampenda,nilimsaidia kumtafutia mahali pa kuishi akifanya mtihani na gharama zingine

Na kwa kipindi hicho alionyesha kubadilika sana ikawa kama mapenzi yameanza upya ila alipomaliza tu mtihani nyodo zikaanza,dharau na kuniumiza kimaksudi(wnawake!!!!)mpaka alipoondoka na mimi nika giv-up kabisaa (COZ MATUKIO NI MENGI CWEZI KUSIMLIA KILA KITU,NAOMBA NILUKE BAADHI YA MATUKIO NA NISIMLIE TU YALIYONIGUSA ZAIDI) ilipita miezi kadhaa nikiwa alone nisitake mwanamke kabisa ila nikaja kukutana na mdada mmoja tulokua tukisali nae -kanisani,nilimvutia,- alinivutia,tukaanzisha mahusiano, (HAPA KATI KATI YALIPITA MAMBO MENGI TU) lakini nikiwa chuoni tulikua tukiwasiliana vzuri tu lakini likizo moja nikiwa kwenye mtanda wa facbook,nikawa napitia plofile yake nikashaangaa kukuta plofile pics yake kuna pic ya mwanaume nasiemjua na relationship status yake inasomeka yumo in relationship na huyo mwanamume,nilimtafuta kujua kinachoendelea akasema ni kweli yuko na mwanaume mwingine ,kumuliza sababu akasema ameamua tu COZ HAWEZI KUA NA MWANAMUME WA KUPIGIANA CMU TU..na kama utani uo ndiyo ukawa mwisho na huu ukawa ni uhusiano wangu wa pili (RICHA YA KUA NILIKUA NI MWANAUME MWENYE MAPENZI HALISI,MWENYE KUJARI
NA KILA KITU ANACHOKIPENDA MWANAMKE) UHUSIANO WA 3:

huyu alikua ni mganda aliekua akisoma chuo jirani na nilichokua nikisoma mimi na nilikutana nae wakati wa maonesho yaliyohusisha vyuo vya maeneo yale,na moja ya maonesho yalikua ni onesho la mavazi na moja wa wahiriki toka chuo nilichokua nilikua ni mimi na siku mbili baada ya tamasha, nilipata friend request kadhaa kwenye facebook na mojawapo alikua ni mdada toka hicho chuo ..MWANZO NILIMPUUZIA SANA LAKINI CKU NDIYO NAMUONA BAADA YA KUPANGA TUONANE,CKUAMINI,NA CWEZI NIKAELEZEA NI KIASI GANI YULE BINT ALIKUA MREMBO,MREMBO HASWAA WA ASILI, so tukawa malafiki,na yeye kama alivyokua yule wa kwanza,alianza kunionesha ishara zote za kua urafiki wa kawaida cyo anao uhitaji,bali ni mapenzi na baada ya kupita mda kidogo nazani kwa kuona celekei aliamu kunifungukia yeye mwenyewe,kama waliotangulia alininiambia kua alinipenda siku nyingi tangu cku ile nimeonesha mavazi chuoni kwao na tangu kipindi hcho alipenda siku moja ajenge mahusiano na mimi..

Nazani hakuna mwanaume alie singo na Rijari then akakataa bahati kam hii,hivyo uhusiano mpya ukazaliwa,akawa msichana wangu wa 3 kimahusiano(SIKUA NAPENDA NA KILA NILIPOANZISHA UHUSIANO RENGO LILIKUA NI LONG TERM RELATIONSHIP BUT CKU ZOTE NILIKUA NIKIANGUKIA KWA GIRLS WASIYO SAHIHI) tulifanya mambo mengi SANA ya kufulahisha katika mapenzi KIASI KWAMBA HAKUKUA NA MWANYA WA KUFIKILIA KUA SIKU MOJA MWENZANGU ATAGEUKA,NA UKWELI KABISA RICHA YA KUA CKUA NA
CKU NYINGI KATIKA MAHUSIANO LAKINI NILIKUA NAJUA NINI MWANAMKE ANATAKA ,NINI NAPASWA NIFANYE NA WAPI NIMFANYE AWE NA FURAHA NA NILIKUA NINAWAPA REASONS ZA KUJIVUNIA KUA THEY GOT A REALY PERFECT MEN..

LAKINI baada ya miezi 5 ya uhusiano alianza kuwa tofauti..mawasiliano akapunguza..mara nyingi akawa hapokei simu zangu NA HATA AKIKUTA MICD CALL ZANGU HASHITUKI KABISA na nilipojaribu kumdadisi kulikoni,alinijbu kua yuko kawaida (NA MARA NYINGI ALIKUA AKINIJBU KUA"KWANI UNATAKA TUZUNGUMZE KUTWA NZIMA AU MMARA KWA MARA NDIYO UJUE KIASI GANI NAKUPENDA" )na zaid alikua akidai ni masomo tu yanamtait,,nilijilazimisha kumwelewa lakin sikulizika na hali ile.

Siku moja nisiyopenda kuikumbuka..na ambayo inaonesha ni kias gani kuna watu wameteswa na mapenzi....nakumbuka cku hiyo nilimtafuta nikawa namsihi abadilike,awe kama zamani coz sikutaka kabisa nimuache au tuacheni coz skua na mpango wa kua na girlfriend mwingine(kama nilivyotangulia kusema kua napenda kua na msimamo kwa msichana mmoja) ..aliniahid kua atabadilika na kwa kuanza akaniomba usiku nimpigie tuongee vizuri kam zamani kwani hata yeye aliyamis sana maongezi yetu matamu ya usiku..niliflahi sana nikijua furaha yangu inaenda kurud tena..na siku hiyo nilijiunga cheka ya 2000 kabisa ili tu maongezi yetu yasijekatishwa njiani.

Usiku wake nilimpigia akapokea lakini kwa sauti kama mtu asiyetaka mtu aliekaribu asikie,akaniambia kua nimtafute baadae,sikujari sana maana nilijua pengine anajisomea Na baada ya nusu saa nilimpigia tena,simu iliita sana pasipo majibu..kwa baadae ikipokelew lakini sauti
niliyoiskia sikuitalajia.. ILIK UA NI SAUTI YA MPENZI WANGU HUYO AKITOA SAUTI KAMA YA MTU ANAEFANYA TENDO LA NGONO msituko na maumivu niliyopata ni siri yangu na nilichofanya badara ya kukata simu,nilitoa kabisa battery ya simu na nikaiwasha kwa baadae wakati nikijaribu kuutafuta usingizi maana kawaida ya kuzima simu kwa mda mlefunikiwa na maumivu makari kabisa simu yangu ilianza kuita na mpigaj akiwa ni huyo mpenzi wangu,nilishtuka na sikupenda kuipokea ila baada ya kuita sana nilipokea na sauti niliyoiskia si ile niliyoitegemea,alikua ni mwanaume,AKINIONYA KUA NI KOME KUENDELEA KUMSUMBUA MSICHANA WAKE,NILIJIKUTA MACHOZI YAKINITOKA KWA UCHUNGU NIKIFKILIA MWENENDO WA MAHUSIANO YANGU YALIYOPITA NA HIKI NINACHOKIPITIA.

Nilikata kabisamawasiliano na huyo binti ila alikuja kunitumia meseji akisema kua nimsamehe kwni kitendo kile hakufanya kwa makusudi ingawa ni kweli yuko ndani ya mahusiano mapya hivyo nimuwie radhi..iliniuma sana NIKIKUMBUKA NILIVYOMPENDA KWA MOYO WOTE NIKAMPA KILA 7BABU YA KUNIPENDA KILA SIKU KIASI WATU WALIOKUA WAKITUONA WALITAMANI WAWE SISI ,NA PIA MAMBO MENGI YA KUSISIMUA NILIYOSHIRIKIANA BUT KAMA MSHUMAA UNAVYOWAKA MPAKA KUZIMA,NDIVYO ILIVYOKUA,KWA MAUMIVU MAKARI SANA ,NIKAACHANA NA YULE (COZ WAT GOES AROUND COMES BACK AROUND DADA YULE AKIWA KWAO UGANDA ALIKUJA NIKUMBUKA NA KUNISUMBUA KILA SIKU,LAKIN KWA KILE ALIKFANYA SIKUTAMANI KABISA KURUDI MAANA NGOZI YA CHUI SIKU ZOTE HAIBADIRIK SO ANGEKUJA KURUDIA TENA niliamua niachane kabisa na mapenzi richa ya wasicha na kazaa kutaka ukaribu na mimi,lakini sikua na hamu nao tena mana kikubwa ilikua ni kulinda heshima yangu,sikupenda nilivoonekana kwa watu kua nabadili wanawake..hivo nilikaa mda mlefu bila kua na mahusiano ya kimapenz na mwanamke yeyote na sasa nikiwa nimeajiriwa kwenye kampun flan hapa mwanza bado kama hitaj la binadam yeyote anaejtambua..nahitaj niwe na mwenzangu..mwanamke tutakaeanzisha mahusiano yenye furaha na upendo...

CWEZ KUWACHUKIA WANAWAKE WOTE SABABU NAJUA C WOTE..NAJUA KUNA BINT SEHEM MWENYE HITAJ KAMA LANGU...LAKIN HAJAWAI PATA NAFAS NA MWANAMUME ANAEMSTAHILI HIVO KUPITIA PAGE HII..NAAMIN KUNA WATU WAZIMA.GREAT THINKERS NA WANAOJITAMBUA NINGEPENDA NIPATE MAWZO NA HTA USHAURI AMBAO UTANJENGA LAKIN PIA KMA YUPO BINT MWENYE MAPENZ YA KWELI ANAEJITAMBUA BAS ANITAFUTE FOR HAPPY N LONG LASTIN RELATIONSHIP CFA:mapenz ya kweli.
rangi yoyote. mvumilivu/mwenye heshima. mcha mungu. ili tusipishane sana kimawazo ni vizuri akiwa na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea. namba yangu ni:0786696226 NI VIZURI UKINITEXT NAMI NITAKUTAFUTA..AHSANTENI

Zitto Aibua Tafrani Bungeni,Aongoza Wenzake Kutoka Nje ya Bunge...!!!

$
0
0

Wabunge wa upinzani watoka nje ya Bunge kumpinga kukamatwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)  Tundu Lissu.

Wabunge hao wametoka nje ya Bunge hivi punde baada ya Naibu Spika kumtaka Mbunge wa Serengeti kutoka nje baada ya kutokea mabishano yaliyotokana na hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) ya kutaka Bunge lijadili swala Haki na Madaraka ya Bunge kukiukwa kwa wabunge kukamatwa ndani ya viwanja vya Bunge kinyume na utaratibu.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amewatoa nje ya Bunge, wabunge watatu wa CHADEMA, Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda) na Marwa Ryoba (Serengeti).

Livee Kutoka Mahakamani...Hivi Ndivyo Wasanii Wahusika wa Dawa za Kulevya Walivyojikuta Katika Wakati Mgumu Leo Wakiwa Mahakamani..!!!

$
0
0

Wasanii akiwemo TID, Recho,  Tunda na baadhi ya watu wanaoshikiliwa na kituo cha polisi kati kwa tuhuma ya dawa za kulevya wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wameshushwa nyuma ya majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku baadhi ya wakijifunika nyuso zao kukwepa camera za mapaparazi.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa Jumatatu hii ilidai watuhumiwa 12 watasomewa kiapo cha kutorudia Matumizi ya Madawa ya kulevya na kuwa katika uangalizi wa mahakama na jeshi la polisi kwa miaka 2.

Aidha jeshi hilo lilidai baada ya kiapo hicho watuhumiwa wawili kati ya hao watarudishwa polisi aliwemo Wema Sepetu kujibu tuhuma za kukutwa na msokoto wa bangi.

Kudadadeki..Halima Mdee Amefunguka Tena Mapya Juu ya Issue ya Wema Kukamatwa na Makonda,Awatupia Dongo Hili CCM..!!!!

$
0
0

wa upinzani Jumatatu hii wameikosoa vikali njia aliyoitumia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa kuwajumuisha mastaa wakiwemo Wema Sepetu kwenye orodha yake.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amedai kuwa kinachofanyika ni ‘usanii’ kwakuwa anaamini Makonda anawajua vyema mapapa wa biashara hiyo wanaotakia kutajwa na sio kuwakamata akina Wema.

Mdee alimuingiza pia Makonda kwenye picha na kuikosoa safari yake ya siku 20 nchini Marekani huku akihoji nani aliifadhili. “Hakuna anayejua aliyemfadhili kwa siku 20, hana ubavu wa kuishi Marekani siku 20. Inawezekana hawa wauza unga ndio wanampeleka huko, anakuja anawakamata akina Wema, Wema kweli?”

“Alizunguka na nyie kwenye kampeni mlikuwa hamjui? Alikuwa na makamu wa Rais, miezi mitatu sijui mama na mtoto, mkapata kura za mateenagers kupitia huyo mtoto, kwahiyo siku zote kumbe ananusa kitu kama wa rais hajui!”

Wabunge wengine wa upinzani nao wamekosoa njia iliyotumika.
Viewing all 104780 articles
Browse latest View live




Latest Images