Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104688 articles
Browse latest View live

Video..Hivi Ndivyo Ndoto ya Zitto Kabwe Kutaka Kumtetea Tundu Lissu Bungeni Ilivyokatishwa Bila Huruma na Naibu Spika Dk Tulia


Pitia Vichwa vya Magazeti ya Leo 8/2/2017..!!!

Imefichuka..Kumbe Tundu Lissu Amekamatwa kwa Sababu ya Kusema Maneno Haya Aliyoyaanzisha Zitto Kabwe..!!!

$
0
0

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi kuhusu kuwepo kwa njaa nchini.

Hatua hiyo inafuatiwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kupinga kuwepo kwa njaa nchini na kwamba, wafanyabiashara wachache wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya watu kueneza taarifa hizo.

Simon Siro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam leo amewaambia waandishi wa habari kwamba, wanamshikilia Lissu kutokana na tuhuma hizo.

Si mara ya kwanza Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukamatwa kwa madai yanayofanana na hayo.

Miongoni mwayo ni tarehe 22 Desemba mwaka jana ambapo Lissu aliachwa baada ya saa kadhaa kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kutumia jina la Rais Magufuli kwa dhihaka kwa kumwita rais mtukufu.

Alianza kuulizwa kuhusu mkutano wake na waandishi wa habari alipozungumzia kupotea kwa Ben Saanane, aliyekuwa msaidizi wa karibu wa Mbowe “aliitwa kuhojiwa juu ya Press conference aliyofanya na kuzungumzia suala la Saanane lakini pia wamemuhoji anamaanisha nini kumwita Rais John Magufuli jina la “Mtukufu.”

Lissu amekuwa akimtaja Rais Magufuli kama “mtukufu” mara kadhaa tangu aliposhitakiwa kwa kutamka kuwa “Dikteta uchwara anapaswa kupingwa kwa nguvu zote.”

Lissu alikamatwa jana jioni mjini Dodoma katika vianja vya bunge na kusafirisha moja kwa moja hadi jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukamatwa kwake, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa alieleza kutojua sababu za kukamatwa kwake.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa, Lissu anaendelea kuhojiwa kutokana na tuhuma hizo.

Hii Ndio Video Iliyosababisha Tundu Lissu Akamatwe na Polisi,Alimuita Rais Magufuli Rais wa Hovyo Hovyo..!!

Naibu Spika Amuumbua Kigwangallah Bungeni..!!!

$
0
0

NAIBU Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, `amemuumbua Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla baada ya kukanusha taarifa ya bohari za dawa kuwa haziko chini ya kiwango.

Naibu Spika huyo alilazimika kutoa maelekezo kwa serikali kuangalia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)juu ya ubovu wa bohari za dawa nchini na kuzifanyia kazi kasoro kama watazikuta.

Hatua hiyo ya Dk. Tulia ilitokana na Dk. Kigwangalla kukanusha taarifa ya bohari za dawa kuwa chini ya kiwango zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Halima Ally Mohamed.

Mbunge huyo akiuliza swali la nyongeza, alisema kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya mwaka 2014/15, kuna bohari zisizo na viwango na kutaka kujua msimamo wa serikali ili kuhakikisha afya za Watanzania.

Akijibu swali hilo, Dk. Kigwangalla alisema: “Kwanza, naomba nikanushe vikali sana kwamba kuna bohari za dawa zisizo na viwango. Hiyo ni ripoti ya CAG na hii ni taarifa ya serikali. Kwa hiyo naongea kama serikali kwa mamlaka kamili niliyopewa.”

Alisema bohari zilizopo ni za viwango vya hali ya juu na vimethibitishwa na Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO), na zinakaguliwa kila baada ya miaka mitano na dawa haziwezi kutunzwa kwenye bohari zisizo na viwango kwa sababu zitaharibika.

“Dawa ni ‘high value items’ na hatuwezi kuzitunza ovyo, hivyo kwa sababu tunazitunza kwa gharama kubwa na ndiyo maana katika utunzaji, usambazaji mpaka katika kituo cha afya kijijini, kuna mnyororo uliokamilika unaozingatia viwango vya ubora,” alisema Dk. Kigwangalla.

Kufuatia majibu hayo, Dk. Tulia alisema: “Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kuwa mbunge ameuliza taarifa zinazotokana na Ripoti ya CAG, serikali iangalie katika hiyo ripoti inasema nini ili kama alichosema mbunge kipo sawasawa ama hakipo sawasawa.”

Alisema kama kinachosemwa kipo kwenye ripoti, Wizara ya Afya iliangalie suala hilo.

Baada ya agizo hilo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto, Ummy Mwalimu, alisimama na kusema wamelipokea swali hilo na watalifanyia kazi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje, aliishauri serikali kuiwezesha Bohari ya Dawa nchini (MSD) kuwa na fungu maalum kutoka Hazina.

Akijibu swali hilo, Dk. Kigwangalla alisema MSD haiwezi kupewa fungu la moja kwa moja bila kupitia Wizara ya Afya.

Dr Levy: Ali Kiba ni Dozi ya Kutwa Mara Tatu...!!

$
0
0

Ukimfunika kukata mauno atakushinda kutunga. Ukimfunika umaarufu atakutesa kwa sauti. Ukimsumbua kuhonga media yeye atakuumiza kwa kutojisumbua na hizo media. 

Ni kama kumpenda mwanamke ambaye hajui kama unampenda. Na mbaya zaidi hata hisia juu yako hana. Utaumia sana. 

Ndo Kiba. Hata mashabiki wake wanampenda kuliko yeye anavyowapenda. Anachofanya ni kuwapa kile alichopewa na Mungu. Sauti. Watu wanadata naye.

Wakati watu wengi sana wakimsifia kwa sauti ambayo anayo yeye tu ktk dunia hii. Kuna kitu wanakisahau. Ana tofauti sana katika tungo zake. Sikiliza Mapenzi yana Run Dunia.

Anamuimbia mapenzi mwanaume mwenzake. Ngumu sana mwenye akili ya kisoda kuelewa ule wimbo.
Mchizi anamuimbia mchizi wake ngoma la mapenzi afu lina bamba mbaya. Hata R Kelly na wenzake akili hii waliikosa.

Dem kaenda kwa Kiba kumshitakia ujinga wa bwanaake. Of coz watoto wa kike wanapenda faraja. Kiba akampa faraja.

Mchizi kugundua kaamua kumtosa mtoto. Mtoto kaamua kutangulia mbele ya haki. Alimpenda mchizi wake ila Kiba alimpa faraja tu baada ya ushauri. Hata mimi ningemfariji kwa namna hiyo mtoto mzuri.

Kasikilize hilo ngoma ukiwa na akili timamu usichanganye na mawazo ya hali ya Wema Sepetu kwa sasa. Hutaelewa alichoandika Kiba.

Kiba siyo wa nchi hii. Kinachofanywa na computer yeye anakitoa kwenye koromeo lake.
Kuna sauti kutoka kooni kwake ni ya pekee kuliko upekee wenyewe. Hawezi kusema ila Diamond na wenzake hicho kitu kinawaumiza sana. 

Kiba hajui kujitangaza. Ndo maana hata gari anayotumia haijulikani. Kiba hajui kiki. Ndo maana huwezi kumsikia akiongelea issue zake na madem zake. Hajui kujiongeza ndo maana husikii ana nyumba au shilingi ngapi kwenye account. Na ni ngumu kumkuta news room za udaku. Vyote hivyo hana lakini bado anawaumiza kichwa kundi kubwa la watu. Katikati ya magwiji wa hizi kazi. Fella, Tale na wenzao. Sallam muweke kando hajui fitna za game hili. 

Pamoja na lundo la hao watu Kiba bado anasimama nao katika mstari mmoja. Ogopa sana. Heshimu. Hana anachowaweza zaidi ya lile koo lake na akili ya kuandika kinachotakiwa kuandikwa. 

Hapa siyo suala la team flan. Ukweli uko wazi kuwa kuna upinzani wa wazi na wa siri kati ya Kiba peke yake na Diamond na watu wake. Huwezi kusikia management ya Kiba ikimuongelea Diamond. Ila ni rahisi zaidi kusikia management ya Diamond ikiongea jambo la Kiba. Ndo ukweli.

Watu wanaomzunguka Diamond huwezi kushindana nao hata kwa nusu saa. Game la muziki liko vyumbani mwao. Linawatii kuliko askari wa Dar mbele ya Makonda. Lakini Kiba kaendelea kuwepo kwenye kilele bila kutumia nguvu. Alichonacho Kiba kwenye koo angekuwa nacho Diamond dunia ingesimama. Ni kama Ronaldo angekuwa na kile alichonacho Messi katika miguu yake. 

Mashabiki wanatumia nguvu nyingi sana kupambana na Diamond mitandaoni, wakati Kiba anawauliza wadogo zake vilipo viatu vyake vya michezo akacheze bondeni pale Jangwani. Diamond anajituma sana na muziki wake. Kiba anatufanya tuamini kuwa muziki ni burudani na ufanywe kiburudani. 

Wakati soko la muziki likilazimishwa liwe na muziki unaochezeka. Kiba alikuja na ngoma kama Mac Muga ambao hauchezeki na siyo wa mapenzi. ukakamata vibaya sana. Kasikilize Karim. Utagundua kuwa Kiba ni zaidi ya biti na promo.

Makonda Kataja Majina Mengine 65 ya Wanaohusika na Madawa ya Kulevya......Yumo Freeman Mbowe, Yusuph Manji, Askofu Gwajima

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan.

Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa.

Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.



Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kumkamata Zitto Kabwe Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe jana alijificha ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma  kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mara tu atakapotoka nje ya ukumbi huo.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika  kuwa Polisi wa bunge wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye hafahamu ni lipi


 Zitto Kabwe Ruyagwa
And today it's my turn I've been informed by parliamentary security personnel that police will arrest me for sedition details are not known


Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa  amesema si kweli kwamba Polisi walikuwa Bungeni kumsubiri Zitto atoke wamkamate.

 “Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae

“Unajua watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe… hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai”  Amesema Kamanda Mambosasa.

Mkutano wa Yusuf Manji na Waandishi: Nitamshitaki Makonda Kwa Kunichafulia Jina

$
0
0

Baada ya Jina la Manji kutajwa katika majini 65 yaliyotangazwa leo na Mkuu wa Mkoa Makonda, Yusuph Manji Ameongea na Waandishi wa Habari na Kusema Haya:


Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.

Manji: Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.

Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji: Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji: Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?

Manji: Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.

Manji: Kama unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji: Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja. Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji: Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji: Hivi ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji: Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji: Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji: Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi. Nitakiwa namvunjia heshima.

Manji: Mimi nipo tayari kupimwa na kusearchiwa na Makonda naye apimwe kama anatumia na wamsearch pia.

Manji: Mimi sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Keaho au keshokutwa ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji: Mkuu wa mkoa kuna sehemu nimegongana naye oysterbay na nlienda kuonanana naye kama diwani wa mbagala kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama diwani siwezi kumuandikia rais.

By Figganigga/Jamii Forums

CHADEMA Watoa Kauli Baada ya Mbowe Kutajwa Kwenye Orodha ya Makonda..!!

$
0
0

Muda mchache baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutangaza majina ya baadhi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika mtandao wa biashara ya Madawa ya kulevya akiwemo kiongozi ya juu wa CHADEMA na kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Uongozi wa CHADEMA umefunguka na kueleza namna ambavyo hawakupendezwa jinsi jina la kiongozi wao wa juu lilivyotajwa bila kufuata utaratibu.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii, CHADEMA wamedai wao hawapingi kutajwa kwa mkuu wao ila wanapiga utaratibu iliyotumika kutaja jina la kuingozi huyo wa juu wa chama hicho.

“Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani,” alisema mmoja kati ya viongizi hao.

“Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita,”

Aliongeza, “Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi, tusingependa kuona viongozi wengine waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu,”

Pia katika list hiyo mpya ya Makonda ametajwa aliyekuwa Mbunge wa CCM, Iddi Azzan, mchungaji Gwajima pamoja na watu wengine.

Petit Man Arudi Instagram na Ujumbe ‘Hatutaki Mazoea Kabisa’, Mashabiki Wampa Pole..!!

$
0
0

Mmoja kati ya watu 13 walioachiwa jana na mahakama kwenye sakata la Madawa ya kulevya, Petit Man amepost ujumbe wake wa kwanza katika mtandao wa Instagram huku akiweka sehemu ya wimbo wa msanii wake Billnass ‘hatutaki mazoea kabisa’.

Meneja huyo wa wasanii ndani ya label LFLG alikamatwa na jeshi la polisi mapema wiki iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya pamoja na kutumia.

“Hatutakimazoeakabisa @billnass Feat @mwanafa #TurnOnComment #JahBless #LFLG,” aliandika meneja huyo Insta na kuleta mjadala mkubwa huku wengi wakimpa pole.

Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva na wengine ambao walikuwa kwenye sakata hilo na kuachiwa na mahakama hapo jana, wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.

Huu ni ujumbe wa mashabiki hao wa Instagram.

nhappiness4
Toto nasikia ulipewa Mekong’oto wa haja hivi ni kweli da roho iliniuma kinoma

sherry_4real
Daah pole sn mshakaji wng ndo life ilivo cku azfanani kitu kidogo inaweza ikakuarbia siku au mwez pole sn dady yoo

florah_chiza

Wema Azidi Kuyumbishwa..Apelekwa Kupimwa Kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Kujua Kama Anatumia Madaw Au Lah..!!!

$
0
0

Taarifa zilizotufikia zimeeleza kuwa, msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu hajafikishwa mahakamani Kisutu leo kwa madai kuwa amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwa ajili ya kupimwa na kuthibitisha  iwapo anatumia madawa ya kulevya au la!

Imedaiwa kuwa, Polisi Dar, wamefikia hatua hiyo baada Wema kukana kutumia madawa wakati alipokuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Taarifa zimedai kuwa mastaa wenzake kama TID na wengine walikiri kutumia madawa na kupewa onyo kali huku mahakama ikiwapa masharti matatu likiwemo la kuripoti polisi mara mbili kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja na kuwa chini ya uangalizi wa mahakama, kisha kujidhamini kwa bondi ya shilingi milioni moja na kurudi uraiani wakati Wema akikana kutumia madawa.

Taarifa zaidi zimedai kuwa, polisi wanaendelea kumshikilia Wema huku wakisubiri ripoti ya mkemia mkuu ili waweze kukamilisha upelezi na kumchukulia hatua zinazostahili.

Baada ya Zoazoa ya Wasanii Wanaotumia na kuuza madawa ya kulevya kuwa Kubwa,Kitale Akana Rasmi Jina Lake ya Kitale Rais wa Mateja..!!!

$
0
0

Mchekesheja Maarufu Kitale,Hii leo kupiti ukurasa wake wa kijamii wa instagram amefunguka juu ya kulikana lililokuwa jina lake la awali la kitale Rais wa Mateja.

Hii Hapa Post yake huko Instagram..!!!


A photo posted by MUSA YUSUPH MAHENGE (@mkudesimbaoriginal) on

Alichokisema Mange Kimambi Baada ya Mbowe na Manji Kutajwa Kwenye List ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya..!!!

$
0
0

Operesheni tokomeza upinzani...... 😭😭😭😭 kesho atamtaja Lowassa. 😭😭😭😭
.
.
I'm sorry Sina la kuongea bado nimefreeze kusikia Mbowe ametajwa..., Mwili umekufa ganzi... Mimi sio chadema wala sio fan Wa Mbowe lakini akili imeniruka kusikia Mbowe katajwa, wakifanikiwa kumtake Mbowe down basi na chadema imekwishaaaaa na 2020 hakutakuwa na Upinzani...... Dah nimeishiwa Nguvu kabisaaaaaaaaa... yani ndo maana Magufuli anatujibu kunya kila siku, anajua 2020 atakuwa kaumaliza upinzani......Magufuli na Makonda Mungu Anawaona.😭😭😭😭😭😭😭😭
.
.
Huyo gwajima kama kweli anauza madawa Mungu ndo anaejua sisi hatujui lakini 100% gwajima wanamtaka sababu ndo mfadhili mkubwa wa Chadema..... Anawapaga pesa nyingi sana kwenye kampeni, kuanzia wabunge huwa anawafadhili...Anyways, Mimi Mbowe kutajwa ni kama msiba Yani its means Chadema is over.... Wakiweza kumfunga mbowe Chadema is done.....
.
.
Yusuf Manji ni mtumiaji wa madawa... he is a user sio drug dealer. Ila Yusuf Manji ndo mfadhili mkubwa wa Lowassa....Yani Manji ni mmoja ya watu waliomfadhili Lowassa kwenye kampeni ya 2015. Although yeye ni CCM Ila pesa ya lowassa kwenye siasa kwa kiasi kikubwa mnoooooo ni pesa ya Manji... Manji ni old money , Manji kwao ubilionea ulianzia kwa Babu he is not a drug dealer... Naombeni muingie google msearch Yusuf Manji and Lowassa ndo mtaelewa Manji huwa anampa Lowassa pesa kiasi gani na zamani alikuwa anatoa pesa kwa wagombea wa CCM hata Kikwete alimfadhili for the first time 2015 Manji alimfadhili mgombea wa upinzani na sio Wa CCM....CCM kampeni ya 2015 wamekopa mnoooo waliumia mnooo sababu financial backers waliondoka na Lowassa.....
.
.
Kusema ukweli nimeumia Leo kushinda hata ya Wema sababu hiii ya Leo inawahikikishia CCM ushindi wa 2020 😭😭😭l😭😭... Basi nimekubali CCM ni akili kubwaaaaa. Upinzani hawachomokiiiii 2020 sio kwa mkakati huuu. Dah is soooooo sad!
.
.
Na kawataka Ijumaa ili awalaze ndani mpaka Jumatatu... Aisee Magufuli na Makonda ni dream couple....

Kudadeki..Hivi Ndivyo Makonda Alivyozijibu Tuhuma za Wema Sepetu kuwa Anatoka na Agnes Masogange...!!!

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, “Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama.”

“Hebu wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi hata simu huruhusiwi kuwa nayo,” ameongeza.

“Kwahiyo bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa.”

Majina 65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.

Video:Kamanda Sirro Afunguka Haya Mapya Kuhusu Wema Sepetu na Mustakabali Wake..!!

Video:Rais Magufuli Amefanya Ziara ya Kushtukiza Leo Katika Uwanja Mpya wa Ndege na Kukutana na Mambo Haya..!!!

Uwoya: Napenda Wanaume Wenye Sura Mbaya..!!!

$
0
0

STAR wa Bongo Movie mwenye mvuto wa pekee na mshiriki wa shindano la Ijumaa la Figa Bomba, Irene Uwoya, amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa havutiwi na wanaume wenye muonekano mzuri na hujui ni kwa nini

Aidha staa huyo amewahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa anavutiwa sana na wasanii wa Bongo Fleva hasa wale wadogo kama Msami Baby.

“Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa SIJAWAHI kuvutiwa na wanaume wenye mionekano mizuri, sielewi ni kwa nini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI…’ aliandika Irene


Video : Mh Makonda akitaja majina mengine kuhusiana na mkasa wa adawa ya kulevya

Mamba Mla Watu Ziwa Victoria Auawa Kwa Kuwekewa Ndoano..!!!

$
0
0

Mamba anayesadikiwa kula zaidi ya watu wanane na kuendelea kutishia maisha ya binadamu na mifugo kandokando ya Ziwa Victoria katika Kata ya Mkuyuni jijini Mwanza kwa muda mrefu, hatimaye ameuawa baada ya kunaswa na ndoano iliyotegwa na wananchi kwa siku tatu mfululizo

Mamba huyo ameokotwa na wavuvi hii leo majira ya Alfajiri akiwa amekufa huku akielea juu ya maji katika mwalo wa mswahili uliopo mtaa wa Kang'ata kata ya Mkuyuni jijini Mwanza

Mamba huyo ambaye hakujulikana kama ni dume au jike, anakisiwa kuwa na urefu wa futi 18, sawa na mita tano na nusu.
Viewing all 104688 articles
Browse latest View live




Latest Images