Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Habari za Hivi Punde..Mbowe Afunguka ya Moyoni Baada ya Jana Kutajwa na Makonda,Afichua Njama Hizi za CCM kwa Chama Chake..!!!

0
0

Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaita polisi kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, baadhi ya walioitwa wamelaani hatua hiyo wakisema inalenga kuwachafulia majina na heshima mbele ya jamii.

Miongoni mwa waliotwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amezungumza na kueleza kutofurahishwa na hatua hiyo.

Mbowe aliyekuwa safarini kwenda bungeni Dodoma, alisema ameshangazwa kutuhumiwa kwa jambo asilolijua.

“Kama amemtaja mbunge wa Hai anajulikana ni mmoja, hata kama asingesema Freeman, Mbunge wa Hai anajulikana ni Freeman Mbowe.

“The only thing (kitu pekee) ninaweza kusema nchi haiendeshwi hivyo. Yametajwa majina mengi ambayo sijui Makonda ana evidence (ushahidi) gani!

“Anasema tukiwaita tukiridhika na maelezo yao tutawaachia. Huwezi kusema tu, yaani kwa kusema ni Mbowe... mimi ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mimi ni mbunge, mimi ni mzazi, nina wanachama, maaskofu, mapadri, mashehe na viongozi mbalimbali.

“Unapokuwa unamhusisha kiongozi na ‘drug trafficking au drug business’ (usafirishaji wa dawa au biashara ya dawa za kulevya), sijui ana ushahidi gani hadi akanihusisha na jambo hilo, mimi sielewi, kwa hivyo siwezi kusema kwa kitu ambacho sielewi,”alisisitiza Mbowe.

Mbowe aliendelea kusema kuwa kesi za dawa za kulevya hazina dhamana, hivyo alimtaka Makonda awe na ushahidi wa kutosha anapowataja watuhumiwa.

“Tuache habari ya kuitwa, wewe umepata tuhuma, hujafanya uchunguzi, hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini unatakiwa kufanya uchunguzi ili ukimkamata mtu unamshtaki, siyo unataja mtu unachafua hadhi yake. Halafu ukija kusema hatuna ushahidi juu yako umeshaharibu jina lake,” alisema na kuongeza:

“Mimi sijui kama jeshi la polisi linafanya kazi hii au ni Makonda amejipa kazi ya kuwa mpelelezi. Au labda yeye kwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndiyo amejipa kazi ya kutaja majina kwenye mambo yenye kashfa kama haya? Sielewi. This is very wrong precedence (Hii ni rejea mbaya) kwa utawala wa sheria.”

Mbowe alisema inawezekana ni mikakati ya Serikali kuendelea kukandamiza upinzani kwa kuwakamata viongozi wake.

“Sijui kama kuna watu wanaolengwa, lakini tumeona viongozi wetu wanakamatwa hawapewi dhamana, (Tundu) Lissu amekamatwa, (Godbless) Lema amekamatwa ... mtu anakaa miezi minne, kwa hiyo wanaweza kufanya lolote. Inawezekana ni mkakati wa kutesa wapinzani. Wamenitafuta kwenye biashara wameona haitoshi... sina uhakika lakini sioni kama wana nia njema na sisi,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa kama ataitikia wito wa Makonda, Mbowe alisema bado anawasiliana na wanasheria wake kabla ya kuchukua hatua.

Hivi Punde Kutoka Center Polisi..Manji Awasili Akiwa na Kikosi cha Mawakili Kutoka Uingereza na Tanzania..!!!

0
0

Ameongazana na mawakili 8. 6 wa nchini Tanzania na 2 kutoka Uingereza

Taarifa Zaidi Inakuja...!!!

Gwajima Atema Cheche,Amtaka Makonda Amtaje Ridhiwani Kikwete Kwenye List Yake...!!!!

0
0

Gwajima: Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media?

Gwajima: Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii.

Gwajima: Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi;

1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi

2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya.

Gwajima: Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote.

Gwajima: Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge Mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza makonda kwa sababu kafanya Vizuri. Makonda anaujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi Muu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya Hitilafu.

Gwajima: Makonda angeweza kunipigia simu au Kuwagiza Polisi wakaniletea samasi au kuniita.

Gwajima: Nia ya Makonda ni kutaka jina la Gwajima liharibike. Kama Gwajima hafanyi na hajihusishi na Madawa ya kulevya watu wa Usalama wanajua. Nmefanya hii kazi ya Uchungaji kwa Miaka 20.

Gwajima: Si kweli kwamba makonda anatumwa na Rais Magufuli, rais ana tabia ya kupongeza saa nyingine anapiga simu Clouds kupongeza pale wanapofanya Vizuri.

Gwajima: Sisi tunamuunga mkono Mheshimiwa rais hata kama kwenye uchaguzi hatujamuunga mkono, Lakini kwa kuwa amechaguliwa yeye tunamuunga mkono

Gwajima: Naamin Makonda hajajificha kwenye "Usukuma" wake.

Gwajima: Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya Serikali, ni hatari sana

Gwajima: Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze.

Gwajima: Chini yangu kuna Maaskofu 125. Kesho wataogopa nao watasemwa

Gwajima: Kuna siku Paul Makonda, Sitta na Mwakyembe walikuja kanisani kwangu hata CD ninazo na alihutubia hapa kwenye Madhabahu akinisifia sana, Leo ni kitu gani kimemfanya anichafue?

Gwajima: Je ikiwa Gwajima hahusiki, itakuwaje?

Gwajima: Mimi nlikuwa mkali sana juu ya utawala wa awamu ya nne. Miaka kwa miaka Tembo walikuwa wanakufa na hakuna hatua zilizokuwa zinachukuliwa.

Gwajima: Kuna Kipindi Ridhiwani Kikwete aliwapeleka Mahakamani Dr. Slaa na Mch. Mtikila akitaka wakanushe habari kuhusu utajiri wake, hiyo kesi sijui iliishia wapi.

Gwajima: Nani anamtumia Makonda?

Gwajima: Makonda ana nia ovu juu yangu na juu ya Wakristo. Anataka kuwaaminisha watu kwamba wokovu haupo.

Gwajima: Mimi nataka kununua ndege nyingine ili nianzishe chuo cha ndege, mbona sipongezwi kwa hilo?

Gwajima: Jambo hili alilofanya si sawa na si sahihi.

Gwajima: Wabunge wamepiga kelele juu ya jambo hili, sisi wananchi tusio na sehemu ya kuongea tufanyeje?

Gwajima: Namfahamu rais Magufuli, hawezi kumpendelea kwa kuwa ni mtu wa kwao (Msukuma). Rais anawapenda watu wote anawapenda Mawaziri wote na watendaji wote wa Serikali. Naamin rais hajamtuma Makonda.

Gwajima: Nguvu katika mikono isiyo sahihi ni hatari sana.

Gwajima: Juzi kati tulikuwa na mechi kati ya maasikofu na viongozi, Mimi nlikuwa namba tia yeye namba 10. Alikuwa ananiangalia jicho baya sana. Mimi, Makonda, kamanda Sirro Spika wa Bunge tulikuwa tunamechi si angenikamata hapo?

*Kuna watu walikuwa wanauza madawa ya kulevya, katika uongozi huu wale walikuwa wanauza madawa ya kulevya wamebadili majina na wanafanya biashara nyingine. Walikuwa na jina B sasa wamebadilisha jina.

Zari Afunguka Jinsi Harusi Yake na Diamond Itakavyokuwa..!!!

0
0

Zari The Bosslady amedai kuwa anataka harusi yake na Diamond Platnumz iwe kubwa na yenye gharama kuwahi kufanyika Afrika Mashariki.Hata hivyo, itafanyika baada ya kuwa wamefanya mambo ya muhimu zaidi ikiwemo kujijenga zaidi walivyo sasa. 

Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Zari amedai kuwa suala la kufunga ndoa sio kitu kinachowapa pressure.

Amedai kuwa hawajawahi kukaa chini na kuwa na majadiliano ya kina kuhusu ndoa, licha ya hadi sasa kuwa na watoto wawili, Tiffah na Nillan. Staa huyo wa Uganda amedai kuwa moja ya mambo ambayo wanataka kufanya ni kuhakikisha kwanza wanawajengea watoto wao apartments zao zitakazowasaidia katika maisha yao hata kama wazazi wao wasipokuwepo.

Hata hivyo Zari amedai kuwa mwezi March mwaka huu Diamond ataenda rasmi kujitambulisha kwa baba yake na kuhalalisha uhusiano wao pamoja na kuomba mkono wa ndoa.


Video..Gwajima Akijibu Tuhuma za Kuhusika na Madwa ya Kulevya..!!!

Breaking News..Hatimaye Wema Sepetu Apewa Dhamana.

0
0



Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, Alhamis hii alipandishwa kizimbani kwenye mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


Mrembo huyo amesomewa mashtaka matatu. Ameachiwa kwa dhamana hadi February 28 kesi yake itakaposomwa tena. Wema alikuwa anaendelea kushikiliwa na polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za dawa za kulevya ambapo awali alinyimwa dhamana.

Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jeshi lake bado lilimshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo na kuwa jalada lao lilipelekwa kwa wakili wa serikali alipitie ili aone ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa mkemia mkuu wa selikali kubaini kama kweli ni mtuamiji wa madawa ya kulevya.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkali Wema Sepetu ni kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake.

BREAKING NEWS: Manji akamatwa tena wakati akitoka sentro, arudishwa ndani

0
0


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amerudishwa na kushikiliwa ndani ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.


Manji alirudishwa kituoni hapo akiwa tayari amefika nje akiwa tayari kuondoka.

BREAKING NEWS: Askofu Gwajima naye atinga na wafuasi wake kituo cha kati cha Polisi Dar

0
0


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongozana na wafuasi wake, kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.

Video..Pamoja na Kuwa na Bifu la Chini kwa Chini,Zari Afunguka Haya Kuhusu Wema Kuhudhuria 40 ya Prince Nillan..!!!

0
0

Leo February 9 kupitia kipindi cha LEO TENA kinachorushwa na CloudsFM Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari walikuwa Mubashara kuzungumzia arobaini ya Mtoto wao Prince Nillan pamoja na hayo wameongelea mengine pia.

Zaidi tazama Video Hapo Chini

Kutoka Mahakamni..Ombi la Serikali la Kutaka Lissu Anyimwe Dhamana Latupwa,Lissu Akipewa Dhamana ya Milioni 20

0
0

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.

Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20

Video..Msukuma Azidi kumwashia Moto Makonda Bungeni,Awaambia Wabunge Wenzake Wamwachie Makonda Apambane Nae Mtaani Ili Amuonyeshe Fresh..!!

0
0

Pia Mbunge Ester Bulaya Alisema kuwa makonda amempigia simu na kuwatukana wabunge wote

Zaidi tazama Video Hapo Chini

Huwa Napata Shida sana Nikikutana na Wanawake Wenye Hii Tabia

0
0

Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela,ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi!

Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45??Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga,amefanya kazi ana hela,unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu,,,Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani,msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti hes caring uone inavyouma,utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers,waone kwanza,msione gesi mtwara mshaanza kuandamana!45years guy waiting for u student of 23 years,ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??

By  Seth De Jesus Giovanni

Lissu Awaonyesha Polisi Kuwa Yeye Ni Zaidi ya Kiburi,Adai Maneno ya Uchochezi Katamka Kweli na Hajafanya Kosa..!!!

0
0

Baada ya kukaa mahabusu kwa siku nne, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa maneno anayoshtakiwa kwa kuyatamka ni ya kweli na kuwa siyo kosa.

Lissu ambaye yupo nje kwa dhamana, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka manne ya kutoa maneno ya uchochezi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.

Awali, kabla ya kupandishwa kizimbani mbunge huyo aligoma kula akiwa mahabusu ya polisi kwa mujibu wa wakili wake, Peter Kibatala.

Kutoka kwa Lissu kulifuatia kasoro za kuandaa kiapo kuwa mojawapo wa sababu zilizoifanya Mahakama hiyo kutupa pingamizi la dhamana lililowekwa na upande wa Serikali.

Mbunge huyo amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka manne ya kutoa kauli za uchochezi, ambapo upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la zuio la dhamana lililoambatana na kiapo cha Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya Ilala, Mrakabu Msaidizi (ASP), Denis Mjumba.

Hata hivyo, mahakama hiyo imetupa pingamizi la dhamana pamoja na mambo mengine kutokana na kasoro katika kiapo hicho.

Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo, Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi ameainisha mambo matatu yaliyomfanya kulikataa pingamizi hilo na kuamua kumwachia kwa dhamana mtuhumiwa.

Lissu ametimiza masharti hayo na kudhaminiwa na Diwani wa Kata ya Tabata wa chama hicho, Patrick Asenga hivyo akaachiwa huru.

Viongozi wa Dini Wamuunga Mkono Makonda...!!

0
0
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema dawa za kulevya zinateketeza nguvukazi ya Taifa, jambo ambalo halipaswi kuachwa liendelee kumea.


Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sheikh Alhad amesema baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini linaunga mkono juhudi zifanywazo na Serikali kupambana na jambo hilo.

“Suala la matumizi ya dawa za kulevya limekuwa kikwazo cha maendeleo nchini kutokana na nguvu kubwa ya Taifa ambayo ni vijana kujihusisha na utumiaji wa dawa hizo,” amesema.


Amesema kuwa wanawataka viongozi wengine wa umma kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wa kupambana na uovu wa uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya ambao ni janga kwa Taifa.

“Tunawaomba wananchi wote kuunga mkono suala hili pamoja na kuonyesha ushirikiano wa kutosha kwa wale walioamua kujitoa kwa ajili ya nchi yetu.”

Katibu wa baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini, Padri John Solomoni ameitaka Serikali kushughulikia suala hilo kwa umakini ili lisiibue manung’uniko miongoni mwa wananchi ambao hawana hatia.

Padri huyo amewataka viongozi wanaochunguza suala hilo kuwa makini ili wasiharibu haki ya mtuhumiwa.

“Ikumbukwe kwamba wanaotajwa ni watuhumiwa, huenda baada ya uchunguzi wakabainika kuwa hawakuhusika. Baada ya kugundulika kuwa hawana hatia na itakuwa vigumu kurudisha waliyokuwa nayo hapo mwanzoni,” amesema.

Kwa takriban wiki moja sasa, watu mbalimbali wamehojiwa na polisi kuhusiana na ama utumiaji wa dawa hizo au uuzaji katika vita inayoendeshwa na mkuu wa mkoa huo.

Mzee wa Upako Amfurumushia Lundo la Tuhuma TB Joshua wa Nigeria,Adai ni Tapeli wa Kimataifa..

0
0

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

 Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako
Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.

Hatarii..Zitto Aokolewa Usiku wa Manane na Spika Ndugai...!!!

0
0

KITENDO cha Jeshi la Polisi kutaka kumkamata Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, juzi baada ya kutoka bungeni, kilimfanya mbunge huyo kuondoka bungeni usiku wa manane kuamkia jana kwa msaada wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Juzi, wakati Zitto akiwasilisha hoja bungeni kuhusu utaratibu wa wabunge, hasa wa upinzani kukamatwa na polisi bila utaratibu, alibainisha kuwa hata yeye amepewa taarifa kuwa akitoka nje ya viwanja vya Bunge atakamatwa, kuahidi kulala bungeni ili kuwakwepa polisi.

Baada ya wabunge wa upinzani kususia kikao cha Bunge juzi saa 10:30 jioni kutokana na hoja hiyo kupingwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson,  Zitto aliendelea kuwepo ndan  ya eneo la Bunge hadi jana saa 6:25 usiku alipoondoka kwa msaada wa Ndugai aliyempatia usafiri.

Hata hivyo, kususia kikao kwa wabunge hao wa upinzani sambamba na Zitto kusakwa na polisi, jana asubuhi kulimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kutaka Serikali na Bunge kufanya kazi kwa pamoja, huku akisema taarifa ya kukamatwa hovyo kwa wabunge ataifikisha kwa Ndugai  aliyedai kuwa ataitolea tamko rasmi leo.

Zitto asimulia

“Niliondoka saa 6 usiku ikiwa ni baada ya mashauriano kati yangu na Katibu wa Bunge (Dk Thomas Kashilillah) na Spika Ndugai  ambaye aliwasiliana na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi-Ernest Mangu),” alisema Zitto.

“Nilivyokuwa nawasilisha hoja yangu bungeni nilikuwa najua kila kitu juu ya kukamatwa kwangu ndio maana nikaamua kutotoka bungeni kwani walikuwa wakinisubiri nje ya viwanja wa bunge.”

Alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu, IGP aliwasiliana na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa ambaye alibainisha kuwa mbunge huyo alikuwa akitafutwa kwa kutoa kauli uchochezi alipokuwa mkoani Shinyanga, kubainisha kuwa polisi ilikiri kutoona kosa lake.

Alisema baada ya mashauriano hayo alihakikishiwa kuwa akitoa hatokamatwa na polisi lakini kwa kujihami zaidi Spika Ndugai alituma usafiri wa kumchukua.

“Spika aliwasiliana na mkuu wa ulinzi wa Bunge ili kuniwezesha kutoka salama ila pamoja na kuwasiliana naye bado alinitumia gari ambalo lilinitoa ndani ya viwanja vya Bunge,” alisema.

Juzi mpaka saa tatu baadhi ya mageti ya kutoka na kuingilia ndani ya Bunge kulikuwa na magari ya polisi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kwa kiwango kikubwa.

Kauli ya Mwenyekiti wa Bunge

Jana wakati akijibu mwongozo wa mbunge wa Tarime Vijijini(Chadema), John Heche kuhusu polisi kuwakamata wabunge bila utaratibu, Chenge alisema polisi wanaweza wasiwakamate wabunge pindi vikao vya Bunge vinapokuwa vikiendelea, badala yake kufanya hivyo wakati mwingine.

Katika maelezo yake, Chenge alisema kuna haja pia ya kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na Bunge kwa kuwa mihimili hiyo ina majukumu yanayofanana.
“Heche nimekusikia ingawa hukueleza kwa undani, lakini najua suala hili lilianza jana na Naibu Spika akalitolea ufafanuzi,” alisema.

“Ushauri wangu katika hili, kuna haja ya kuwa na mahusiano mazuri kati ya Bunge na Serikali, lakini pia nakuomba Heche umwandikie Katibu wa Bunge umweleze mapendekezo yako ili yafikishwe katika Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa mjadala zaidi.

Alisema baada yah apo uongozi wa Bunge unaweza kujadiliana na Serikali kwa sababu kama polisi wanamhitaji mbunge, wanaweza kusema wa wakamkamata wakati mwingine kwa sababu wanajua anapoishi.

Awali, Heche alisema kama Bunge halitachukua hatua pindi wabunge wanapodharirishwa, utafika wakati Bunge litaanza kudharirishwa.

Alisema Bunge ni chombo kinachoheshimika duniani kwa sababu kinatunga sheria na kupitisha bajeti ya Serikali lakini hivi sasa heshima yake.

 “Hii tabia ya wabunge kukamatwa ovyo, tena bila taarifa ya Spika, haipendezi na hata wakuu wa wilaya wanawanyanyasa sana wabunge huko majimboni. Kwa hiyo, naomba mwongozo wako mheshimiwa mwenyekiti ili uniruhusu niwasilishe hoja yangu ili Bunge liijadili,” alisema Heche.

Wabunge walivyotoka bungeni

Juzi, wabunge wa upinzani, walitoka nje ya Bunge wakionyesha kutoridhishwa na majibu ya Naibu Spika, Dk. Tulia Akson, aliyoyatoa wakati alipokuwa akijibu taarifa ya kukamatwa kwa wabunge wa upinzani iliyowasilishwa na Zitto.

Katika taarifa hiyo, Zitto aliwataja wabunge wa Chadema, Godbless Lema wa Arusha Mjini aliyeko mahabusu katika Gereza la Kisongo, Arusha kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali anayetumikia kifungo cha miezi sita katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, wakati Dk. Tulia akijibu taarifa hiyo, alisema kanuni za Bunge zinataka Spika wa Bunge apewe taarifa za kukamatwa mbunge aliyetenda makosa ya madai na kama siyo makosa ya madai, hakuna haja ya spika kupewa taarifa.

Simba Washtukia Janja ya Wazungu Katika Dili la Kumaka Said Ndemla..!!

0
0

Simba inaonekana haitamuachia kiungo wake Said Ndemla kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.
Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza kwamba uongozi wa klabu ya AFC inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden anakocheza Thomas Ulimwengu haujawa wazi sana katika maelezo yake.

“Unajua wamesema wanamtaka Ndemla, lakini hakuna maelezo ya kutosha na ku
eleza biashara hii inafanyika vipi,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.

“Wanamtaka, Simba inapata kiasi gani? Inafaidikaje sasa na baadaye? Maana isiwe mnakuza wachezaji halafu watu wanaingiza maneno mengi wanakwenda kufaidika wao.

“Hatuna shida na kuachia watu lakini tunachotaka ni uhakika wa mambo. Simba tumeumizwa sana na hata hapa Tanzania imekuwa hivyo. Tunasumbuka kuwakuza, halafu faida kwa wengine, hii sis awa.”

AFC imeonyesha nia ya kumtaka Ndemla lakini taarifa zinaeleza wameshindwa kulipa chochote zaidi ya kusema wamchukue halafu baadaye wakimuuza, Simba itafaidika pia.

Gwajima na Yusuf Manji Wakesha na Polisi Dar, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Ya February 10

Mke Wangu Anunuliwa Nguo za Ndani na Mwanaume

0
0
Baada yakudakua mawasiliano ya mke wangu na kukuta Jamaa akimwambia zawadi yako ipo tayari hivyo watafutane ampatie..

Baada ya siku mbili tatu nakaona kimfuko kipo na chupi nne na brazia mbili, sikuuliza ila nikahisi hii ndio ile zawadi. Nikaamua kudakua mawasiliano yake tena.

Nikakutana tena na mawasiliano wakiulizana vip ameipenda zawadi na je zimemtosha.

Kiumweli ni zaidi ya wiki tatu sasa sijamuuliza au kuonyesha tofauti yoyote kwake, ila bado najiuliza ni sahihi kwa mwanamke tena mke wa mtu kupewa zawadi ya chupi au brazia na mwanaume tofauti na Mume/Mpenzi wake..!

Lakini pia je huyu mwanamke anaweza kuendelea kua na vigezo vya kuendelea kua mke.

Lamwisho ni mwanamke / Mwanaume anapokua anaamua kumnunulia mwenzake nguo za ndani anakua anamaanisha nini?

Natumai mawazo yenu yatanisaidia Asante.!

Wema, Zari Kuonana 'Live' Kwenye Arobaini ya Mtoto Nillan

0
0
Akizungumza live kutoka Clouds Fm, Diamond ametamka rasmi kuwa staa Wema Sepetu ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo, kwa upande wa Zari Hassan nae amesema hana shida na ujio wa Wema Sepetu Kwenye Arobaini ya Nillan ambaye waliwahi kuingia kwenye bifu kipindi cha nyuma.

Kama kweli Wema akifanikiwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo itakua ndo mara ya kwanza kwa mafahari hao wawili kuonana, na itakua sherehe ya aina yake kwa uwepo wa mastaa hao waliowahi kuingia kwenye vita nzito na kurushiana maneno mtandaoni.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images