Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Gwajima Afunguka Saa 72 Mahabusu,Adai Anamuandalia Makonda Dawa Yake..!!!

$
0
0

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati sakata la kutangaza na kushikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Pia alieleza kushangazwa kwake na baadhi ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa nchini kuingizwa katika sakata hilo hata kabla uchunguzi kufanyika.

Gwajima ambaye alikuwa ameshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam alikokwenda baada ya kutangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya, alisema hana mpango wa kumshtaki mkuu huyo wa mkoa.

Askofu Gwajima alisema badala yake anakata rufaa kwa Rais Magufuli akimtaka kufuatilia tuhuma hizo kwa undani kwa watu wanaoendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi ili waweze kupata haki.

Akizungumza kanisani kwake Dar es Salaam jana, Gwajima alisema alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kwenda kuitikia mwito uliotolewa na Makonda kwa ajili ya kutoa ushirikiano kuhusu tuhuma za dawa za kulevya

Alisema baada ya kufika kituoni hapo na kufanyiwa mahojiano alikutana na mfanyabishara na Diwani wa Mbagala Kuu, Yusuph Manji ambaye naye alikuwa amefika kituoni hapo kwa ajili ya kuitika mwito huo wa Makonda.

"Kwenye chumba changu tulikuwa mimi na Yusuph Manji, huyu ana kampuni zaidi ya 23 ameajiri Watanzania zaidi ya 5,000, sasa mtu kama huyo imeshindikanaje kumuita kwa kumpelekea hati ya kuitwa kuhojiwa, badala yake anatangazwa?"

"Imeshindikanaje mtu kama Manji kumuita kwa kumuandikia barua ili aende ahojiwe na ikigundulika achukuliwe hatua, kwa nini atangazwe kabla ya kuchukuliwa hatua?  Ilipaswa aandikiwe barua ya wito kisha uchunguzi ufanyike na kama akibainika ndiyo achukuliwe hatua, ila kwa sababu mkuu wa mkoa hakuwa na nia nzuri hata kwa Manji ndiyo maana hakufanya hivyo," alisema Gwajima.

Alisema hadi alipoachiwa katika kituo hicho bado Manji alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi, ambapo alihoji sababu ya Manji na wengine wanaoendelea kushikiliwa kituoni hapo kutofanyiwa uchunguzi na ukaguzi kama aliyofanyiwa yeye ili waachiwe kama yeye au kuchukuliwa hatua kama wakibainika kujihusisha na biashara hiyo.

"Sioni sababu ya kuendelea kuwashikilia watu wale bila kuchukuliwa hatua. Kama mimi nilituhumiwa tena kwa kutangazwa lakini mwishowe ikabainika hakuna ukweli, nitaamini vipi kama wale waliobaki ndani mikononi mwa Polisi nao wanahusika?"Alihoji Gwajima.

Gwajima alisema mbali na Manji na wafanyabishara wengine waliotajwa kuhusika na biashara hiyo, wamo pia askari wa Polisi ambao nao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara hiyo na wameendelea kushikiliwa kwa amri ya mkuu wa mkoa.

Kutokana na hali hiyo, Gwajima alisema ameamua kukata rufaa kwa Rais ili aweze kuwaangalia watu hao kwa jicho la tatu na tuhuma dhidi yao ziweze kuchunguzwa na ukweli ujulikane.

"Mheshimiwa Rais ninakuomba sana, kuna wale watu wengine ambao nilikuwa nao, ambao ni wafanyabishara na walitangazwa kama mimi, naomba uwatazame kwa macho ya huruma ili tuhuma zao zishughulikiwe, kuliko kuendelea kukaa kwenye giza chini mule, kwa niaba yao ninakata rufaa kwako naomba uwahurumie.

"Kuna askari Polisi wapo ndani kwa wiki ya pili sasa kwa amri ya Makonda, mimi naomba niwasemee leo, kama mimi imeonekana kuwa sina makosa, vipi kuhusu wao? Nampongeza mheshimiwa Rais kwa kuingia katika vita ya dawa za kulevya naomba atazame jambo hili, "alisisitiza Askofu Gwajima.

Alisema kuwa alichogundua ni kuwa Rais anahitaji msaada wake hivyo anaingia katika kazi ya kumsaidia Rais kwa maelezo kuwa inawezekana anapata taarifa zisizo za ukweli.

Gwajima alisema kuwa leo amepanga kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuwaona watuhumiwa wengine ambao wanaendelea kushikiliwa.

Aeleza alivyokaguliwa

Katika hatua nyingine, Gwajima alisimulia waumini wa kanisa lake namna shughuli ya ukaguzi dhidi yake ilivyoendeshwa na Jeshi la Polisi, huku akidai amechiwa baada ya kubainika tuhuma dhidi yake hazikuwa na ukweli.

Alisema baada ya kuhojiwa alielezwa anatakiwa kwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ili kubaini kama anajihusisha na  utumiaji wa dawa za kulevya ama la, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake ambapo alieleza kuwa licha ya kufanyiwa yote hayo Polisi walifikia pia hatua ya kukagua akaunti zake za fedha.

"Kwa sababu mimi tangu kuzaliwa sijawahi kuonja mambo hayo, lakini walivyopima wakakuta hamna chochote na wakanipa fomu kuonesha hawajakuta kitu.

"Niliwaambia kwangu mkikuta hata kipisi cha sigara andikeni dawa za kulevya, tulifika kwangu nyumba yangu ina ghorofa tatu wakakagua zote na hawakukuta kitu walichotaka," alisema

Aliongeza kuwa,"wakaona haitoshi, wakahamia kwenye akaunti zangu za benki na mimi nikawaruhusu waendelee walipofanya uchunguzi wao wakabaini hakuna kitu cha kuweza kunikamatia, hawakupata kitu wakaamua kuniachia,".
Gwajima alisema hana mpango wa kumshtaki Makonda ama kumfungulia kesi bali anajua cha kumfanya.

Dk Slaa aibuka
Aidha, Gwajima aliwaeleza waumini wa kanisa hilo kuwa wakati akiwa mikononi mwa Polisi, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willibrod Slaa alimtumia ujumbe wa kumpa pole na kumweleza kuwa hakubaliani na tuhuma hizo na atakuwa tayari kutoa ushirikiano wa ushahidi kumhusu.

PAUL Makonda Kusoma Orodha ya Tatu ya Vinara wa Unga leo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo anatarajia kutaja majina mengine ya vinara wanaotuhumiwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya.



Katika awamu ya pili, watu mashuhuri wakiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima na mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan walitajwa.

“Awamu ya tatu imekamilika naomba tukutane kesho katika ukumbi wa mwalimu nyerere kuanzia saa 4 asbh,” mkuu huyo wa mkoa aliandika jana kwenye Instagram.

Jana Rais Dkt John Magufuli aliwataka viongozi kuongeza nguvu kwenye mapambano ya biashara hiyo haramu

Chadema Watoa Tamko Rasmi Juu ya Anayoyafanya Makonda,Wamtaka Magufuli Amuonye,La Sivyo...!!!

$
0
0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa Victoria kimemuomba Rais John Magufuli kumkanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ili asije kuliangamiza Taifa kwa ilichodai kutafuta sifa za kisiasa.

Pia, chama hicho kimesema Taifa kwa sasa linakumbwa na ugonjwa wa kisiasa hali inayoweza kuliangamiza kama isipokemewa na anachofanya Makonda kinapaswa kupingwa vikali na asasi zote ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia.

Akizungumza kwa na wanahabari kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ansebert Ngurumo alisema kinachofanywa na  Makonda ni kutafuta vyeo kwa sifa kwani tangu mwanzo amekuwa akipata vyeo kupitia 'propoganda' za kisiasa bila kutambua yeye ni kiongozi wa kiserikali kwa sasa.

Ngurumo ambaye aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, alisema Taifa imekumbwa na ugonjwa wa ukakasi unaowapata viongozi wa kisiasa wanaoitwa Demagobi.

"Demagogi ni neno la kigiriki, Demo- watu halafu Gogi- viongozi wanaongoza watu kwa kutafuta sifa kama akina Makonda. Namuomba Rais Magufuli amkanye asije liingiza taifa sehemu mbaya kwa kutafuta sifa," alisema.

Akizungumza kwa kutoa mfano, Ngurumo alisema Joseph McCarthy ambaye alikuwa Senator katika Bunge la juu Marekani (Senate) 1947 wakati vita baridi ilipopamba moto, alibuni mbinu ya kupata umaarufu.

Alisema ana orodha ya Wamarekani wanaoisaliti nchi yao kwa kuwa Wakomunisti na pengine kufanya upelelezi (espionage) kwa niaba ya Urusi kitu ambacho kipindi kile si tu kinamaliza wengine kiheshima, lakini pia kinaweza kusababisha hata kunyang'anywa uraia.

Ngurumo alisema McCarthy alitaja majina kutoka katika vikaratasi na alipambwa na kupendwa na sehemu ya umma wa Marekani kwa kuwa kipindi hicho vita dhidi ya USSR ilibeba hisia kali, ambapo watu hukuweza kuwaambia kitu.

“Huo ndiyo 'ujasiri' aliojifanya anao Senator McCarthy, mpaka kujifaragua kumtaja Waziri Mkuu wa nchi nyingine, huku baadhi ya wananchi wa US hadi waliandamana kutaka Senator McCarthy apewe tuzo kwa 'kuongoza mapambano yaliyotukuka dhidi ya maadui wa US',” alisema.

Katika hatua nyingine, Ngurumo alivitaka vyombo vya habari kuacha kukuza jambo hilo kwani si mara ya kwanza taifa kuwa na matukio ya maajabu.

"Mwaka 2013 aliibuka babu wa Loliondo kuwa anatibu magonjwa sugu na taifa zima lilihamia kwa babu wakiwemo viongozi wakubwa kisiasa, dini na wengineo, huku jambo hilo likiwa imekuzwa na ‘media’ hivyo nawaomba wanahabari wenzangu fanyeni utafiti kwanza," alisema.

Tembelea Tovuti Pendwa ya ASILI ZETU inayohusiana na Masuala ya Tiba Asilia Kama Kusafisha Nyota na Kumvuta Mpenzi

$
0
0
Tembelea  tovuti  pendwa  ya ASILI ZETUinayohusiana na masuala ya tiba asilia, kusomewa dua na visomo, kusafisha nyota,  kumvuta mume au mpenzi aliyekuacha, tiba ya magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana,  mvuto wa biashara.

Pia tunatoa dawa za uzazi kwa wale kina mama wenye matatizo ya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote, kupandishwa cheo kazini, mali isiyohuzika kama vile kiwanja, shamba, nyumba, gari n,k.

Bonyeza Hapa: https://asilizetu.wordpress.com

Rais Magufuli Akerwa na Kitendo cha Manji na Gwajima Kwenda na Mashabiki wao Polisi

$
0
0
Inaonyesha kila kinachoendelea huwa kinamfikia Rais Magufuli ambapo leo kwenye hotuba yake IKULU Dar es salaam ameongea kuhusu wale Mashabiki wa Yanga walioonekana kulifutafuta vumbi gari la Mfanyabiashara Yusuph Manji baada ya kuingia kuhojiwa Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.
Pamoja na hilo, rais  pia ameongelea ishu ya Wanakwaya wa Askofu Gwajima kwenda na kusimama nje ya kituo cha kati cha Polisi baada ya Askofu huyo kuingia kuhojiwa na Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.


MSIKILIZE HAPA:

Kidato cha Kwanza Kupimwa Upya Uwezo,Watafanya Mtihani Mwingine wa Taifa..!!!

$
0
0

BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta), linatarajia kuanza upimaji maalumu wa stadi na maarifa kwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu shule za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana jana kutoka Necta na kusainiwa na Kaimu Mtendaji, Dk. Richard Kasuga, makatibu tawala Tanzania Bara wanajulishwa kuanza kufanikisha mchakato huo na upimaji huo unatarajiwa kuanza Februari 28, mwaka huu.

Ilifafanua kuwa wanafunzi wote waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu wanatakiwa kufanyiwa mtihani maalumu kwa ajili ya kuwapima ili kubaini uwezo wao waliouonesha katika mitihani yao ya shule ya msingi.

Iliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuwabaini wanafunzi waliofaulu kwa njia ya udanganyifu na watakaobainika wataondolewa shuleni.

“Baraza la Mitihani linawajulisha makatibu tawala kuwa litafanya upimaji maalumu wa stadi na maarifa kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za umma, Februari 28, mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.

Pia taarifa hiyo iliwataka makatibu tawala wote kuwasilisha idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kwa Katibu Mtendaji wa baraza hilo kabla ya Februari 10, mwaka huu.

Wakati huo huo, maofisa elimu wa shule za sekondari na wakuu wa shule za umma walitakiwa kujulishwa kuhusu mchakato huo ili kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza.  

Rasmi..Mwigulu Nchemba Afunguka Juu ya Uhusika Wake Katika Vita vya Madawa ya Kulevya...!!!

$
0
0

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ametaja mambo matano makubwa, ikiwemo dawa za kulevya akisema wizara yake haina mjadala na suala hilo kwani linagusa maisha ya Watanzania wote.

Nchemba alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam baada ya kushuhudia viongozi mbalimbali wakiapishwa na Rais John Magufuli.

Walioapishwa ni pamoja na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.

Wengine ni Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Omar Yusuph Mzee, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Joseph Sokoine na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgovano.

Waziri Mwigulu alitaja mambo mengine ni kupambana na ugaidi, ujangili wa rasimali za nchi, uhalifu wa kutumia silaha na ubakaji.

Alisema wamejipanga kukabiliana mambo hayo kutokana na ukweli kuwa yamekuwa yakiongezeka kila kukicha hali ambayo inahatarisha amani ya nchi.

Mwigulu alisema wizara yake kwa sasa imekamilika kila idara hivyo ni wakati mwafaka wa kuhakikisha mapambano yote yanayohusika na mambo hayo matano yanafanikiwa.

Alisema dawa za kulevya ni janga linalohitaji ushirikiano wa kada zote hivyo wao wapo tayari kuhakikisha vita hiyo inakabiliwa kwa njia yoyote.

Waziri huyo alisema kwa siku za karibuni kumekuwepo na matukio ya ubakaji na ujangili hasa nyara za Serikali akisema waanamini kwa pamoja wataweza kupambana na wahusika.

“Tumejipanga kwa mambo makubwa matano ambayo ni dawa za kulevya, ujangili, ubakaji, uhalifu wa kutumia silaha na ugaidi ambapo vyote kwa pamoja vinashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu,” alisema.

Alitoa mwito kwa Watanzania kutoa ushirikiano wa mapambano mbalimbali ambayo yanafanywa na Serikali ili kudumisha amani ya nchi.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani imekuwa katika mkakati wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu ambapo kwa siku za karibuni mapambano hayo yameonekana kushika kasi hususan kwenye dawa za kulevya ambayo yalianzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amber Rose na Wiz Khalifa Warudiana Mapenzi Yamewashinda

$
0
0

Amber Rose na Wiz warudiana mapenzi yamewashinda.......Amber Rose and ex-husband Wiz Khalifah are officially back together. The couple showed up to Clive Davs pre-Grammy brunch together holding hands and making out on the red carpet.

Accordign to E! News Amber broke things off with Val a few days ago . . . and ran back to Wiz.
#mapenzimubashara

Hii Ndiyo 'Message Sent' ya Nape Kwa Makonda Kupitia Twitter..!!!

Kero za Michango ya Sherehe Katika Jamii ya Watanzania

$
0
0
Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.

Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.

Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.

Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.

MJ

Askofu Gwajima: Makonda ni Kombora Ambalo Halijaelekezwa pa Kutua, linaweza Kutua Sehemu Yoyote!

$
0
0
Askofu Josephat Gwajima amesema akimpeleka Makonda mahakamani, atakuwa amepeleka serikali mahakamani. Hivyo atamshtaki Makonda kwa Rais ili achukue hatua zinazostahili na hatokubali akiendelea kuwa mkuu wa mkoa.

Gwajima amedai watu wasiwalaumu jeshi la polisi kwani na wenyewe wanateswa kama wanavyoteswa wao. Amesema alipoenda polisi amekuta nao wameswekwa ndani kwa amri ya Makonda. Amedai matatizo yote yamesababishwa na 'kiumbe mmoja'.

Amempongeza Rais kwa kumchagua mkurugenzi husika na amemshauri asiache kuamini vijana kwa kuwa kijana mmoja ameharibu.

Baadhi ya Maneno yake Haya Hapa:

Gwajima: Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe.

Askofu Gwajima: Askari walipekuwa nyumba yangu chumba hadi chumba lakini hawakukuta kitu chochote.

Askofu Gwajima: Mimi nitawaambia kitu, msilaumu Polisi wala Ofisi ya Rais. Wao hawahusiki na hili ila ni kiumbe mmoja tu ameibuka katikati.

Askofu Gwajima: Waliniambia wakanipime kwa Mkemia na walinipima kwa uwazi kabisa. Niliwaambia hata wakikuta pombe wasema ni dawa za kulevya.

Askofu Gwajima: Polisi nao wanateswa kama tunavyoteswa sisi. Wanaambiwa wakapekuwe nyumba yangu japo wanajua hamna kitu ila inabidi waende.

Askofu Gwajima: Baada ya kukosa walichokuwa wanatafuta nyumbani kwangu tukarudi polisi usiku ule ule kuendelee na mahojiano.

Askofu Gwajima: Kamanda Sirro akaniuliza kwa nini nimewekwa kwenye orodha hiyo, nikamwambia ni chuki tu za mtu aliyekaa kwenye kiti chake.

Askofu Gwajima: Sijawahi kuvuta sigari, kunywa pombe wala kwenda disko tangu nimezaliwa mimi.

Gwajima: Chumba nilichowekwa polisi nilikuwa mimi na manji. Nikasema 'kumbe na mimi nina pesa kiasi hiki hadi nawekwa na huyu?'

Askofu Gwajima: Kwanini kina Manji wao hadi leo hawajafanyiwa kama nilivyofanyiwa mimi ili nao watoke mule ndani?

Askofu Gwajima: Manji ana kampuni 23, na ameajiri watu zaidi ya 5000. Unashindwaje kumpelekea hati ya kumuita umhoji kabla ya kumtangaza?

Askofu Gwajima: Baada ya kukosa madawa, utalisafishaje jina langu nililolijenga kwa jasho kubwa kwa miaka 29?

 TAZAMA VIDEO:

Zitto Kabwe Amtaka Rais Avunje Bunge

$
0
0

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amemshauri Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo analiona ni kikwazo kwake.

Ushauri huo ameutoa jana ikiwa ni saa chache baada ya Rais Magufuli kukosoa uamuzi wa Bunge kumuita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kujieleza mbele ya Kamati ya Bunge, kutokana na kilichodaiwa na wabunge kuwa ni kauli ya kulidhalilisha Bunge.

Katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kuapishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rais Magufuli amewataka viongozi wengine kumuunga mkono mtu anayejitokeza kupiga vita dawa za kulevya badala ya kumdhalilisha.

"Tunapomuona mtu anajitokeza kupambana na haya madawa ya kulevya, badala ya kumdhalilisha tumuombee na kumtia moyo, hawa wanaweza hata kubadilisha maneno uliyoyazungumza wakabadilisha wakatengeneza kwenye clip wakatupa, na wakajitokeza wengine wakasema wameingilia mamlaka yao, wakati wao wanaingilia mamlaka ya kuwaita wengine, hii ni vita". Amesema Magufuli

Baada ya kauli hiyo ya Rais, Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook ameonesha kushangazwa na kile alichodai  kuwa Rais hakujua kuwa sheria ya kuundwa kwa mamlaka hiyo, ilitungwa, na kwamba anashangaa kuona Rais hakuwa akijua kuwa alipaswa kumteua Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo
Ujumbe wa Zitto unasema

"Wabunge walitoa Hoja Binafsi kuhusu Madawa ya kulevya ( Esther Bulaya na Faustine Ndugulile ) na kufuatia hoja hiyo Serikali ikaleta Muswada bungeni na Bunge likatunga Sheria ya Kupambana na Madawa ya kulevya mwaka 2015.

Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi."

Ujumbe huo umeendelea kusema..
"Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya?
Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje".

Kajala Afunguka Kutomuona Wema Sepetu Selo

$
0
0
Baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni Mwigizaji wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu kusota lupango kwa siku kadhaa kufuatia kutajwa kwenye tuhuma za madawa ya kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kabla ya kupandishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana, staa mwenzake, Kajala Masanja ameibuka na kufunguka sababu ya kutokwenda kumuona mahabusu.


  Kajala, akiwa ni rafiki wa Wema, aliwahi kuokolewa kwenda jela na mrembo huyo baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13, anadaiwa kutofika lupango katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central’ jijini Dar alikokuwa ameshikiliwa Wema, jambo ambalo liliwashangaza wengi. Chanzo makini kililieleza Wikienda kuwa, kitendo cha kutokwenda kumuona wala kufika mahakamani siku aliyopandishwa kizimbani, kilimuumiza Wema na ndugu zake kwani hawakutegemea mtu kama Kajala angeshindwa kufika kumuona na kumsapoti shosti wake huyo.


Katika mitandao ya kijamii, gumzo lilikuwa ni Kajala kutokwenda selo kumuona Wema hadi akatoka huku watu wengine wakimporomoshea matusi.

Katika kuujua ukweli na sababu za kutokwenda kumuona rafiki yake huyo, Wikienda lilimtafuta Kajala ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Nimeshazoea kutukanwa bila sababu lakini mimi sikuwepo, nilisafiri ndiyo maana sikwenda na nimeumia sana kutokwenda.”

Wema ni miongoni mwa mastaa na watu mbalimbali waliotajwa hivi karibuni na Makonda wakituhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ambapo Jumatano iliyopita alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na dada wawili wa kazi ambapo walitoka kwa dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja.

Kimenuka..Chid Mapenzi Mme Halali wa Muigizaji Shamsa Ford Aitwa Kurepoti Polisi na Paul Makonda

$
0
0

Wakati Makonda Akifunga mkutano aliyoufanga leo na waandishi wa habari kuhusu Madawa ya kulevya Amewataja Chid Mapenzi na Ayoub Kuripoti polisi Central..
..
"Namtaka Chid Mapenzi Polisi leo, ikiwezekana nimkute huku Muda huu"

Waziri Nape Afunguka..Adai Watu Wametafsiri Ujumbe Wake wa Twitter Vibaya

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zilisambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodaiwa kutaka kumgombanisha yeye na baadhi ya viongozi wenzake wa serikali.

Kupitia ukurasa wake wa Tweeter Waziri Nape aliandika…>>

‘Tujifunze kusoma biblia, Nasoma masomo ya Mwakasege watu wanachukua na kutafsiri watakavyo kwa faida zao.Nimesikitishwa sana. Si SAWA!‘


Hii imekuja mara baada ya usiku wa February 14 2017 kupitia ukurasa wake huohuo Waziri Nape alinukuliwa kwa kaundika >>’Ujinga ni mzigo mkubwa sana!! Omba busara ya Mungu kwa kila jambo kuliko utajiri na kiburi!‘



Huku akiambatanisha na kipande cha video cha Mchungaji Christopher Mwakasege aliyenukuliwa akisema ‘Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu, sio kwamba hana akili bali amepungukiwa‘

Kwa ufupi ni kwamba Waziri Nape amesema alichokiandika hakijamlenga na wala hajakiweka kwa makusudi yoyote yenye nia ya kumsema kiongozi yeyote, ni utaratibu wake kusoma masomo ya Mwakasege.

Majina Yaliyotajwa leo na Makonda Pamoja na Yaliyokabithiwa kwa Kamishna wa Madawa ya Kulevya

$
0
0

Leo yametajwa majina mawili tu ya Chid mapenzi na Ayubu Mfaume Kiboko.

Majina mengine 97 ameyakabidhi ya kwa Kamishna mpya wa Madawa ya Kulevya ili ayafanyie kazi.....Je ni sahihi alivyofanya hivyo????

Kwa Mara ya Kwanza Toka Atoke Polisi,Wema Sepetu Kayazungumza Haya Makubwa...!!!

$
0
0

Wema Sepetu ametoa shukrani kwa watu wote waliokuwa naye bega kwa bega tangu ashikiliwe rumande kufuatia kutajwa kwenye orodha ya kwanza ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya watu wanaohusishwa na biashara ya matumizi ya dawa za kulevya.

Wema alitoka kwa dhamana ya shilingi milioni 5 wiki iliyopita baada ya kupandishwa kizimbani kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambako alisomewa mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na msokoto wa bangi.

“Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia,” ameandika kwenye Instagram.

“Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu. Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote,” aneongeza.

“Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana. Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu tunasema asanteni sana.”

Hizi Hapa Kauli 20 za Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya Wakati Akitangaza Vita Mpya...!!!

$
0
0

Kamishna wa kupambana na dawa za kulevya, Rogers William Sianga amelipigilia msumari kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya.

Alikuwa akiongea leo jiji Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa Mkoa, Paul Makonda baada ya kukabidhiwa orodha ya tatu ya majina ya watu wanaohusishwa kwenye biashara hiyo.

Kamishna Sianga amesema hawatamuonea huruma mtu yeyote anayejihusisha kwenye biashara hiyo. Ameomba vita hiyo kuendelea nchi nzima na Dar es Saalam peke yake akidai itaendelea hadi visiwani Zanzibar.

Pia amempongeza Paul Makonda kuanzisha mapambano hayo.

Hizi ni baadhi ya nukuu kutoka kwa Kamishna Sianga kutoka kwenye mkutano huo.

1.Sisi waliotukabidhi kazi hii tutaifanya kwa bidii

2.Wauzaji wa dawa za kulevya wanasababisha HIV, kukosa uwezo wa kuzaa, ugonjwa ini na TB

3.Muuzaji wa dawa za kulevya anasabisha watu wasilime chakula, anasabibisha njaa

4.Biashara ya madawa ya kulevya inasababisha ‘inflation’ (kupanda bei kwa bidhaa)

5.Suala la madawa ya kulevya hakuna mtu ambaye yupo salama Atakapotokea muathirika nyumbani kwako ndio utajua madhara yake

6.Tumepokea orodha tuliyopewa na Mkuu wa Mkoa, tempo ni hiyo hiyo
7.Kumekuwepo na mahakimu au majaji wanaovuruga kesi zetu za madawa ya kulevya, tunaanda orodha yao

8.Kumkatisha ghafla mtu aliyeathirika na dawa za kulevya atakufa. Ukimweka jela atapata maumivu makubwa

9.Tutakutana na wamiliki wa sober houses ili kuweka utaratibu wa namna ya kuwasaiia waathirika wa dawa za kulevya

10.Mtu ambaye anafanya biashara ya dawa za kulevya au utakatishaji wa fedha huyo tunakwenda naye

11.Sheria mpya inatupa uwezo wa kukukamata hadi mali ambazo umezichuma kutokana na biashara ya dawa za kulevya

12.Tutakuelezea namna ya kukutoa kwenye dawa za kulevya. Lakini utatuambia nani anayekuuzia hayo madawa

13.Tutaanzaisha kampeni za dawa ya kulevya kuanzia shuleni hadi vyuoni

14.Vita vya dawa ya kulevya sio vya Dar tu. Alichokianzisha Makonda tunataka nchi nzima moto uwake, hatobakia mtu

15.Heroin inaharibu mwili na kisaikolijoa, uraibu wake ni mbaya zaidi

16.Mirungi inamfanya mwanaume asiwe mwanaume, mirungi inaua ndoa

17.Wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameleta huzuni nyingi katika familia, hatutokuwa na huruma nao

18.Mtumiaji wa madawa ya kulevya hutesa familia na kuirudisha nyuma

19.Uzuri wa muuza dawa za kulevya anatamba

20.Tutakuwa na kitengo cha kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya

Kawaumbuaaa..TID Akiri Kutumua Madawa ya Kulevya Mbele ya Makonda,Alia Asemehewe...!!!

$
0
0

Hitmaker wa Zeze, Khalid Mohamed maarufu kama TID, amekiri kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza leo kwenye mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, TID amesema yuko tayari kubadilika.

“Nimekuwa muathirika wa madawa ya kulevya, nimekuja kama kijana aliyepotea njia siku za nyuma. Nilikosea sana familia yangu, mama yangu, marafiki na jamii kwa ujumla, naomba mnisamehe. Niko tayari kuunga mkono vita hii, mnyama nimeamua,” alisema muimbaji huyo.

“Hakuna anayejua nimepitia mangapi hadi kufika hapa, lazima nilihitaji nguvu ya dola. Sometimes in life you can mess tu up, you can try again,” ameongeza.

TID amedai kufahamu kuwa wao watu wataoanza kumhisi kuwa atakuwa ‘snitch’ kwa mkuu wa mkoa na huenda akataja watu wengi, lakini amesema madawa ni janga la umma linalopaswa kupigwa vita.

Amewapongeza Rais Magufuli na Makonda kwa kuwaamsha vijana kuachana na matumizi na biashara hiyo akisema ‘hata serikali ipo tayari kumtokeza shetani huyu’ huyu akiahidi ‘Sitorudi nyuma kamwe.’

Makonda Aagiza Chid Mapenzi, Mume wa Shamsa Ford Akamatwe Haraka..!!!

$
0
0

Mume wa msanii wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford waliyefunga ndoa hivi karibuni, Chid Mapenzi ametajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kuagiza akakamatwe na polisi haraka iwezekanavyo.

Makonda ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar ambapo ametangaza kwamba anayo orodha nyingine ya watu 97 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Pia mtu mwingine aliyetajwa ni Ayubu Mfaume ambapo naye anatakiwa kukamatwa haraka iwezekanavyo.
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images