Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Wema Ampongeza Waziri Nape Kwa Ujumbe Alioutoa Dhidi ya Makonda..!!!….

$
0
0

IKIWA bado sekeseke la Madawa ya kulevya linaendelea kuitetemesha nchi kwa sasa, msanii wa Bongo Muvi, Wema Abraham Sepetu, ‘Maddam’ amempa pongezi Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye kutokana na kauli yake kuhusu madawa ya kulevya.

Aidha leo Jumatatu, Feb 13,  Watanzania wengi walitegemea kusikia majina ya wamu ya tatu ya watumiaji, wauzaji, wasafirishaji na wadhamini wa madawa ya kulevya. Kwa sababu ambazo bado hazijulikana orodha ya majina hayo haijatajwa badala yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa amri kwa jeshi polisi kukamatwa kwa mfanyabiashara mmilikiwa wa maduka ya Mapenzi Classic maarufu kama Chiddy Mapenzi.

Zari: Hakuna Kilichonivutia kwa Diamond Nilipomuona Mara ya Kwanza...!!

$
0
0

Akihojiwa na kituo maarufu cha radio mjini, staa na mpenzi wa mwanamuziki maarufu nchini Diamond Platinumz, Zarinah Hassan, amesema kuwa hakuna kilichomvutia kwa mwanamuziki huyo ila wamejikuta tu wakiwa kwenye mawasiliano.

Zari aliendelea kutiririka kuwa hata walivyoonana na Diamond kwa mara ya kwanza hakuvutiwa a nae kimapenzi.

Yanga Waandaliwa Mapokezi ya Kihistoria....!!!

$
0
0

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya soka ya Yanga wanatarajia kurejea nchini mapema kesho wakitokea nchini Comoro ambako walikwenda kucheza mchezo wa awali dhidi ya wenyeji wao Ngaya.

Yanga ambayo itawasili majira ya saa tano asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki wanataraji kupata mapokezi ya aina yake kutoka kwa maelfu ya wanachama na mashabiki wa soka hasa mashabiki wa klabu hiyo ambao watajazana katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuwasubiri mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kuelekea mapokezi hayo makubwa tayari baadhi ya matawi ya wanachama wa klabu hiyo sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam wameshaanza vikao kwa ajili ya kuandaa mapokezi makubwa ya wawakilishi hao wa Tanzania.

Wakiongea na Eatv baadhi ya wanachama hao wamesema lengo la kuwapa mapokezi hayo makubwa na ya aina yake ni katika hali ya kuwapongeza wachezaji kwa kazi nzuri waliyofanya huko ugenini na kuibuka na ushindi mujarabu na pia kuwapa moyo wa uwajibikaji mzuri wakijua kuna mamia ya watu nyuma yao jambo ambalo litawahamasisha zaidi wachezaji kufanya vyema katika mchezo wa marudiano utakaopigwa siku ya Jumamosi Februari 17 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga SC wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya kuwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1 jioni ya jana mjini Moroni, Comoro.

Tundu Lissu Amuumbua Tena Makonda,Achambua Kauli Zake Kisheria na Kukamilisha Kwa Sentesi Hii...!!!!

$
0
0

Kauli ya leo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kwamba ana uwezo wa kumhamisha mtu yeyote kutoka kwenye Mkoa wake ni mfano mwingine wa aina ya wanasiasa waliopewa madaraka na Rais Magufuli ambayo hata hawayaelewi na, kwa sababu hiyo, hata wao wenyewe hawajielewi. 

Nafasi ya Wakuu wa Mikoa imetambuliwa na ibara ya 61 ya Katiba yetu. Ibara ya 61(4) inafafanua kwamba kila Mkuu wa Mkoa atatekeleza kazi na majukumu yaliyofafanuliwa na, au chini ya, sheria yoyote iliyotungwa na Bunge. 

Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili ya kufafanua kazi na majukumu ya Wakuu wa Mikoa ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya 1997. 

Sheria hiyo ndiyo iliyowapa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mamlaka ya kipolisi, yaani mamlaka ya kukamata watu wanaosadikiwa kufanya makosa ya jinai mahali ambapo hakuna askari polisi. 

Mamlaka haya ni madogo sana tofauti na Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina ya Makonda wanavyoamini au kuaminishwa. 

Kwanza, ni mamlaka ya nyongeza (supplementary powers) tu kwa mamlaka ya Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye mamlaka hasa ya kukamata wahalifu. 

Hii ina maana kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya hawezi kutumia mamlaka ya kipolisi pale ambapo tayari kuna askari polisi. Polisi wanatakiwa wafanye kazi yao bila kuamriwa na Mkuu wa Mkoa au Wilaya. 

Pili, mamlaka ya kipolisi yamewekewa masharti ya muda, yaani, mtu aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatakiwa apelekwe mahakamani au aachiliwe huru ndani ya muda wa masaa 48. 

Tatu, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyetoa amri ya kukamata mtu chini ya mamlaka yake ya kipolisi, anatakiwa - haraka iwezekanavyo - kupeleka taarifa ya maandishi kwa hakimu juu ya kukamatwa kwa mtu huyo na sababu zake. 

Sheria imeweka wazi kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya asiyetekeleza masharti haya hataruhusiwa kumkamata mtu huyo kwa kosa hilo hilo na anaweza kushtakiwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake. 

Hakuna mahali popote katika Sheria ya Tawala za Mikoa ambako Mkuu wa Mkoa au Wilaya amepewa mamlaka ya kumwondoa mtu yeyote kwenye Mkoa au Wilaya yake. 

Mamlaka ya kuondoa watu kwenye maeneo yao, yaani deportation, yalikuwa sehemu ya mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Sheria ya Kuondoa Watu (Deportation Ordinance). 

Sheria hii ya kikoloni ilitangazwa kuwa kinyume na Katiba, na kwa hiyo batili, na Jaji James Mwalusanya wa Mahakama Kuu katika kesi maarufu ya Chumchua Marwa na Wenzake ya mwaka 1987. 

Ni wazi Mkuu wa Mkoa wa aina ya Paul Makonda hawezi kufahamu mambo makubwa kama haya. Kwake yeye na kwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina yake, kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni sawa na kuwa Rais wa Mkoa au Wilaya aliyokabidhiwa. 

Wakuu wa aina hii wanahitaji kuelimishwa kwamba wao hawana mamlaka ya kifalme aliyo nayo Magufuli. 

Na namna bora kabisa ya kuwaelimisha ni kuwashtaki kwa madai mahakamani pale wanapoenda nje ya masharti ya madaraka yao. Tutaanza na Paul Makonda.

Kauli ya leo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kwamba ana uwezo wa kumhamisha mtu yeyote kutoka kwenye Mkoa wake ni mfano mwingine wa aina ya wanasiasa waliopewa madaraka na Rais Magufuli ambayo hata hawayaelewi na, kwa sababu hiyo, hata wao wenyewe hawajielewi. 

Nafasi ya Wakuu wa Mikoa imetambuliwa na ibara ya 61 ya Katiba yetu. Ibara ya 61(4) inafafanua kwamba kila Mkuu wa Mkoa atatekeleza kazi na majukumu yaliyofafanuliwa na, au chini ya, sheria yoyote iliyotungwa na Bunge. 

Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili ya kufafanua kazi na majukumu ya Wakuu wa Mikoa ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya 1997. 

Sheria hiyo ndiyo iliyowapa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mamlaka ya kipolisi, yaani mamlaka ya kukamata watu wanaosadikiwa kufanya makosa ya jinai mahali ambapo hakuna askari polisi. 

Mamlaka haya ni madogo sana tofauti na Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina ya Makonda wanavyoamini au kuaminishwa. 

Kwanza, ni mamlaka ya nyongeza (supplementary powers) tu kwa mamlaka ya Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye mamlaka hasa ya kukamata wahalifu. 

Hii ina maana kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya hawezi kutumia mamlaka ya kipolisi pale ambapo tayari kuna askari polisi. Polisi wanatakiwa wafanye kazi yao bila kuamriwa na Mkuu wa Mkoa au Wilaya. 

Pili, mamlaka ya kipolisi yamewekewa masharti ya muda, yaani, mtu aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatakiwa apelekwe mahakamani au aachiliwe huru ndani ya muda wa masaa 48. 

Tatu, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyetoa amri ya kukamata mtu chini ya mamlaka yake ya kipolisi, anatakiwa - haraka iwezekanavyo - kupeleka taarifa ya maandishi kwa hakimu juu ya kukamatwa kwa mtu huyo na sababu zake. 

Sheria imeweka wazi kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya asiyetekeleza masharti haya hataruhusiwa kumkamata mtu huyo kwa kosa hilo hilo na anaweza kushtakiwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake. 

Hakuna mahali popote katika Sheria ya Tawala za Mikoa ambako Mkuu wa Mkoa au Wilaya amepewa mamlaka ya kumwondoa mtu yeyote kwenye Mkoa au Wilaya yake. 

Mamlaka ya kuondoa watu kwenye maeneo yao, yaani deportation, yalikuwa sehemu ya mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Sheria ya Kuondoa Watu (Deportation Ordinance). 

Sheria hii ya kikoloni ilitangazwa kuwa kinyume na Katiba, na kwa hiyo batili, na Jaji James Mwalusanya wa Mahakama Kuu katika kesi maarufu ya Chumchua Marwa na Wenzake ya mwaka 1987. 

Ni wazi Mkuu wa Mkoa wa aina ya Paul Makonda hawezi kufahamu mambo makubwa kama haya. Kwake yeye na kwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina yake, kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni sawa na kuwa Rais wa Mkoa au Wilaya aliyokabidhiwa. 

Wakuu wa aina hii wanahitaji kuelimishwa kwamba wao hawana mamlaka ya kifalme aliyo nayo Magufuli. 

Na namna bora kabisa ya kuwaelimisha ni kuwashtaki kwa madai mahakamani pale wanapoenda nje ya masharti ya madaraka yao. Tutaanza na Paul Makonda.

Kaanza Kazi..Kamishna Mpya a Kudgibiti Madawa ya Kulevya Amkosoa Makonda Redioni,Adai Alikuwa Anakiuka Sheria Kuwataja Wahusika wa Madawa ya Kulevya...!!!

$
0
0

Hatimaye Leo Kamishina mkuu Wa Mamlaka ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini amekosoa mtindo aliokuwa akitumia bwana Makonda kutaja watuhumiwa hadharani kuwa haufuati sheria.

Akihojiwa na redio sauti ya ujerumani jioni hii alipo ulizwa swali ni Kwa nini hawakutangaza Majina ya watuhumiwa Wa madawa ya kulevya Kama hapo awali Bwana Rogers Sianga kamishina mkuu alisema hivi.

Kwanza ktk kupambana na madawa ya kulevya ni lazima uzingatie sheria, Kwa kusema hivyo ana maana kuwa Makonda alikuwa anavunja sheria kutangaza watuhumiwa.

Pili akasema hawawezi kumkamata mtu bila kuwa na ushahidi wowote Kwa kuwa wapo wanaotoa taarifa zisizo sahihi na za chuki jambo linalo weza kuleta uonevu Kwa RAIA wema. Lazima wafanye kwanza uchunguzi kabla ya kumkamata au kumhoji mtuhumiwa.

Jengo la 'Water Front' Lashika Moto...Chanzo Hichi Hapa

$
0
0

DAR: Sehemu ya jengo la 'Water Front' inateketea kwa moto. Jeshi la Polisi lafunga barabara wakati juhudi za uokoaji zikiendelea.
Chanzo cha moto huo kimeelezwa kuwa ni Bajaj iliyokuwa imeegeshwa, kisha kushika moto ulioanzia kwenye betri.

Breaking News: Wachimbaji Sita Wafukiwa na Kifusi Mara...!!!

$
0
0


HABARI zilizotufikia hivi punde zimeelza kuwa wachimbaji sita wa madini wanadaiwa kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba madini kwenye mgodi wa Buhemba ulioko mkoani Mara.

Imeelezwa pia kuwa watu 11 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wamekimbizwa katika Hospitali ya Butiama kwa ajili ya matibabu.

Global Publishers imefanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi ambaye amekiri kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo, na hivi sasa nipo eneo la tukio. Kuhusu takwimu sahihi za watu waliofukiwa kwa sasa sina, mpaka uchunguzi wa jeshi la polisi utakapofanyika ndipo nitatoa ripoti kamili.” Alisema Kamanda Ng’anzi.

Tukio hilo ni la pili ndani ya kipindi kifupi ambapo siku za hivi karibuni, wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa baada ya siku kadhaa katika Mgodi wa RZ, Nyarugusu uliopo Nyarugusu mkoani Geita.

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya: Watoto Hawa Wawasikitisha Wengi (Video)

$
0
0
Moja kati ya jambo lililowasikitisha wengi Jumatatu hii katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni pale walipotajwa watoto wawili wa kike ambapo mmoja ana umri wa miaka 14 na mwingine 16 kuwa walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa takriban miaka mitano.

Wakati huo huo mtoto mmoja mwenye miaka 16 aliongeza kuwa mbali na kutumia madawa hayo lakini pia yamempelekea kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kuwa wakati mwingine ilimlazimu kujiuza ili apate fedha za kununulia dawa hizo.

Wakati huo huo Kamishna mpya wa kupambana na Madawa ya kulevya, Rogers Sianga ameahidi kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia huduma bora za afya ambazo zitawasaidia wasirudi tena kwenye janga hilo.

Orodha hiyo ya tatu iliyotolewa leo na Mh. Makonda ina idadi ya majina 97 ambapo kati yao amedai kuna majina ambayo yatawasha moto zaidi huku akiahidi kuwa kuna awamu nyingine nne zimebakia za kutoa majina hayo.

Kasi ya Paul Makonda Yamfanya TID Akiri Kuwa Anatumia Madawa ya Kulevya....

$
0
0
Hitmaker wa Zeze, Khalid Mohamed maarufu kama TID, amekiri kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza leo kwenye mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, TID amesema yuko tayari kubadilika.

“Nimekuwa muathirika wa madawa ya kulevya, nimekuja kama kijana aliyepotea njia siku za nyuma. Nilikosea sana familia yangu, mama yangu, marafiki na jamii kwa ujumla, naomba mnisamehe. Niko tayari kuunga mkono vita hii, mnyama nimeamua,” alisema muimbaji huyo.

“Hakuna anayejua nimepitia mangapi hadi kufika hapa, lazima nilihitaji nguvu ya dola. Sometimes in life you can mess tu up, you can try again,” ameongeza.

TID amedai kufahamu kuwa wao watu wataoanza kumhisi kuwa atakuwa ‘snitch’ kwa mkuu wa mkoa na huenda akataja watu wengi, lakini amesema madawa ni janga la umma linalopaswa kupigwa vita.

Amewapongeza Rais Magufuli na Makonda kwa kuwaamsha vijana kuachana na matumizi na biashara hiyo akisema ‘hata serikali ipo tayari kumtokeza shetani huyu’ huyu akiahidi ‘Sitorudi nyuma kamwe.’

Uvumilivu Unanishinda, Nashindwa Kutunza Bikira Yangu

$
0
0
Mimi ni msichana 21 aged, nishawahi pitia relationship 3( long distance). I never had sex with any of them tho. (im virgin), lakini siku zinavyozidi kwenda naona uvumilivu unanishinda...Marafiki zangu wanadai hiyo kitu ni tamu sana

Sometimes, natamani niende na mwnaume yoyote tuu.  Ushauri wenu tafadhali. "Ndege mjanja asinase kwenye tundu bovu.

CCM Kimenukaa..Mashabiki wa Lowassa Watupiwa Virago Huko Arusha,Yumo Bilionea Mkubwa Nchini..!!!

$
0
0

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha inadaiwa kimewafukuza uanachama baadhi ya vigogo wake akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Arusha, Wilfred Soileli.

Wanachama hao wanatuhumiwa kukisaliti chama hicho kabla na baada ya uchaguzi mkuu wakidaiwa kuwa wafuasi watiifu kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Wengine waliotimuliwa ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa kutoka jimbo la Arumeru Magharibi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) na mfanyabiashara maarufu wa madini ya vito, Mathias Manga na Julius Mungure wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Wakati vigogo hao mkoani Arusha ikielezwa wamevuliwa uanachama wiki iliyopita, Kamati ndogo ya Maadili ya CCM iliyokutana Dodoma iliwahoji wanachama wake ambao wanadaiwa kukisaliti chama hicho.

Hao ni Profesa Juma Kapuya, Nazir Karamagi na Ally Sumaye ambao wote wanadaiwa kukisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wana CCM hao waliohojiwa na kamati hiyo iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Rodrick Mpogolo, ambaye gazeti hili lilipomtafuta kwa simu, haikupokewa.

Taarifa zilizosambaa jijini hapa jana jioni zilidai uamuzi wa kuwafukuza uanachama viongozi hao ulifanyika katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa chama wa mkoa huo, Lekule Laizer.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walisema kuwa Soileli na Manga walituhumiwa kushirikiana kutoa siri na mikakati ya chama na kuipeleka kwa viongozi wa Ukawa hasa Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Rais.

“Hawa walionywa mara nyingi waache tabia ya kushirikiana na wapinzani hasa Lowassa lakini Manga aliwahi kusema yuko tayari kuchukuliwa hatua lakini asingeacha urafiki wake na Lowassa kwani siasa siyo uadui,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho ambaye hakutata kutwa jina .

Vigogo Watema ‘Moto’ Dawa za Kulevya...!!!

$
0
0

Siku mbili baada ya kuwa madarakani, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema hakuna mtu atakayepona baada ya kubainika akitakatisha fedha zilizopatikana kwa njia ya dawa za kulevya.

Sianga amesema hayo katika mkutano ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo pia alikabidhiwa na Makonda majina 97 ya watu wanaojihusisha na dawa hizo.

Kamishna huyo amesema atakayefanya biashara ya dawa za kulevya au utakatishaji wa fedha atachukuliwa hatua kwa sababu sheria mpya ya udhibiti inawapa uwezo wa kukamata hadi mali ambazo atakayepatikana na hatia amezichuma.

Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Frederick Kibuta amesema katika kutekeleza majukumu ya taasisi hiyo, watazingatia sheria katika kila hatua.

Amewataka wananchi kufahamu sheria kwa sababu kutokujua hakutoi nafasi ya kuzivunja.

“Popote walipo tutawafikia na tutawachukulia hatua, hakuna atakayebaki salama katika hili,” amesema Kibuta.


Awali, akizungumza katika mkutano huo, Makonda amemuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai aweke kipimo maalumu kitakachokuwa kinawapima wabunge kabla hawajaingia bungeni ili wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.

“Kaka yangu Ndugai alisema ana nia ya kuweka kifaa maalumu kuwapima wabunge kama wanatumia dawa za kulevya au la, hivyo atimize nia yake hiyo ili kama na huko wapo tuwanyofoe,” amesisitiza Makonda.


Serikali Yavuna Milioni 466 Katika Mnada wa Tanzanite..!!!

$
0
0

Serikali imepata kodi ya Sh466.4 kutokana na mauzo ya Sh9.3 bilioni ya madini ya Tanzanite kupitia mnada uliofanyika mjini Arusha.

Akizungumza katika mnada huo, Mkurugenzi wa Uthaminishaji wa Almasi na Vito Wizara ya Nishati na Madini (Tansolt), Archard Karugendo amesema katika mauzo hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro imepata Sh27.9 milioni.

Karugendo amesema katika mnada huo wa pili kufanyika nchini, Kampuni ya TanzaniteOne inayomilikiwa kwa ubia kati ya Sky Associate na Stamico, ndiyo iliongoza kwa kuuza madini na kupata Sh8.8 bilioni.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendela amesema licha ya madini hayo kuwa ni ya Taifa, ni muhimu wakazi wa Wilaya ya Simanjiro waone matunda yake.

Bendera amesema ni aibu Tanzanite inatoka Simanjiro, lakini wilaya hiyo ndiyo ya mwisho kwa elimu mkoani Manyara na kuwapo kwa shida kubwa ya maji, huduma za afya na Mererani inaongoza kwa maambukizi ya HIV ambayo yamefikia asilimia 18.

Wakizungumza baada ya mnada huo, wakurugenzi wa TanzaniteOne, Faisal Shabhai na Hussein Gonga wameeleza kuridhishwa na  kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha wanauza madini katika minada nchini.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema wizara hiyo, itaendelea kuwezesha minada ili kuhakikisha wanunuzi wakubwa wa madini wanafika nchini kununua madini katika masoko yanayotambulika kisheria.

Bunge la 11 Laandika Historia ya Aina Yake..!!!

$
0
0

MKUTANO wa Sita wa Bunge la 11 uliomalizika Ijumaa iliyopita mjini hapa, umeandika historia nyingine kutokana na kuwepo kwa mambo makuu matano yaliyolipa Bunge hilo sura tofauti na mikutano mingine iliyopita.

Kwa pamoja wabunge wote bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa walisimamia walichokiamini hivyo kukipa chombo hicho hadhi yake.

Mambo hayo ni pamoja na kupinga wakuu wa mikoa na wilaya kuingilia haki na madaraka ya Bunge, wabunge kukamatwa bila utaratibu, kasoro katika kutaja watu wanaotakiwa kuhojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, kuhoji utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na kusuasua kwa utekelezaji wa sera ya Tanzania kuhusu viwanda.

Tofauti na mikutano iliyopita, mkutano huo ulishuhudia wabunge wakiungana katika hoja hizo bila kujali itikadi zao, jambo ambalo liliwaweka katika wakati mgumu baadhi ya mawaziri huku Spika Job Ndugai akihitimisha kwa kuonya wateule wa Rais wanaojisahau kwa kutoa lugha zisizoeleweka.

Madaraka ya Bunge

Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuita mkutano wa waandishi wa habari na kuwataja watu kadhaa akiwataka kufika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, ndicho kilichoibua hoja ya kuingiliwa na kupuuzwa kwa madaraka ya Bunge.

Mjadala kuhusu suala hilo uliibuliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) kupitia kanuni ya 52.

Katika hoja yake, Waitara alisema  Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti walitoa matamshi yanayoingilia haki na madaraka ya Bunge.

Waitara alisema Makonda wakati akizungumza na wanahabari, alisema wabunge huwa wanakwenda bungeni kusinzia, kauli ambayo inakiuka Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.

Kuhusu Mnyeti, alisema mkanda wa video yake umesambaa katika mtandao wa facebook ukimnukuu akisema; “huu ni upuuzi mtupu, wabunge hawa hawajielewi nawashauri mfanye kazi zenu.”

Hoja ya Waitara ambayo siku moja nyuma iliibuliwa na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM) na Bunge kuazimia Makonda kuandika maelezo ya kujieleza kwa kauli yake hiyo ambapo iliungwa mkono na wabunge wote na kutaka hatua zichukuliwe ili kurejesha hadhi ya mhimili huo.

Baada ya Waitara kutoa maelezo yake, wabunge mbalimbali walichangia na kubainisha kuwa Serikali haiwezi kujengwa na viongozi wenye kiburi.

“Unapotaka kulitoa pepo mheshimiwa mwenyekiti halibembelezwi. Unataka kuyapunga majini huwezi kubembeleza. Lazima ukazane kulipunga jini litoke. Hatuwezi kutoa pepo kwa lugha nyepesi nyepesi (akipunguza sauti) pepo toka, haiwezekani. Kama ni pepo tulikemee litoke,” alisema John Kidutu, Mbunge wa Ulyankulu (CCM).

Hoja hiyo ilihitimishwa kwa Bunge kupitisha maazimio manne bila kusikia sauti ya “siyooo” kutoka miongoni mwa wabunge, likiwemo la kuwaita wateule hao wawili wa Rais kuhojiwa na mhimili huo kwa matamshi yao.

Wabunge kukamatwa

Hoja ya wabunge kukamatwa bila Bunge kuwa na taarifa lilikuwa ni moja ya maazimio hayo manne yaliyopitishwa kwenye mkutano huo, huku Spika wa Bunge, Ndugai wakati akiahirisha Bunge aliagiza mtu anayemtaka mbunge ni lazima atoe taarifa kwake.

Ndugai alionya kuwa,“wakati mwingine akikosekana mbunge mmoja inawezekana mambo kwenye kamati yasitekelezwe. Kwa hiyo kama kuna ofisa yeyote anamhitaji mbunge, lazima aniambie. Hatuwezi kwenda hivyo. Kwa hakika kwenda hivyo kibabebabe kutaivuruga nchi.”

Kutajwa majina

Sakata la kutangaza hadharani majina ya watu wanaotakiwa kuhojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya ililiwaamsha wabunge na kutoa kauli zilizoonesha kutokubaliana na utaratibu unaotumika katika vita dhidi ya dawa hizo haramu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu wakati akihitimisha michango ya wabunge kuhusu taarifa ya kamati hiyo alisema:

“Upelelezi wa kesi za jinai hauwezi kufanywa kwa kutaja majina ya watu hadharani. Kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi mahakamani.”


Utekelezaji bajeti

Katika mkutano huo kamati mbalimbali za Bunge ziliwasilisha taarifa za kuanzia Januari 2016 hadi Januari mwaka huu, huku kukiwa na upungufu mkubwa katika utekelezaji wa bajeti za maendeleo katika wizara mbalimbali.

Katika uchambuzi uliofanywa na gazeti hili hakuna wizara hata moja iliyopata asilimia 45 ya bajeti ya fedha za maendeleo, jambo ambalo wabunge walihoji na kueleza wasiwasi wao kuhusu utekelezaji huo.

Mathalan, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji hadi kufikia Januari mwaka huu imepatiwa sh. bilioni 7.6 ya fedha za maendeleo sawa na asilimia 18.6.

Licha ya fedha hizo kutotolewa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango alilieleza JAMBO LEO kuwa Serikali inatekeleza bajeti yake kulingana na inavyokusanya na kusisitiza kuwa miradi mingine ya maendeleo ni endelevu.

“Utekelezaji wa miradi ya maendeleo unafanyika kwa awamu. Hivyo ndivyo ilivyo, mfano ujenzi wa darasa unakuwaje? ni suala la awamu tu,” alisema Dk. Mpango.

Tanzania ya Viwanda

Suala la Tanzania kuwa nchi ya viwanda nalo lilitikisa Bunge huku wabunge wakionesha wasiwasi hao kama sera hiyo itatekelezeka.

Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), alisema Serikali haiwezi kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kama haijajua sababu zilizoua viwanda vilivyokuwapo.

Alisema badala ya Serikali kusisitiza uanzishwaji wa viwanda vipya, ingeimarisha viwanda vilivyopo ili vizalishe kwa mafanikio zaidi kwa sababu baadhi havina malighafi za kutosha.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage naye alijikuta katika wakati mgumu baada ya Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kusema haina taarifa yoyote ya kuanzishwa kwa viwanda 1,169 nchini.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Dalaly Kafumu alisema, “Viwanda ambavyo vimesemwa na Ulega ni 67, Waziri anasema ana viwanda 1,169. Mimi nataka niseme hili, kamati yangu haina taarifa kabisa,”alisema Dk Kafumu.

 “Tafsiri yetu kama kamati ni kuwa waziri hushirikiani na sisi vizuri kwa sababu tungekuwa tuna habari hata kufunguliwa kwa kiwanda cha Mkuranga. Tungejua angeweza kwenda mwenyekiti wa kamati au hata mjumbe mmoja tu. Habari tungekuwa nazo.”

CCM Wamchokoza Magufuli,Habari Katika Vichwa vya Magazeti ya Leo 14/2/2017..!!!


Wanyongwe...!!!

$
0
0

RAIS John Magufuli amesema serikali haitajishughulisha na Watanzania waliokamatwa ughaibuni na kuhukumiwa kunyongwa kutokana na kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Huku akianika orodha mpya yenye maelfu ya Watanzania walio kwenye magereza ya ughaibuni tofauti na iliyotajwa Ijumaa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Magufuli alisema hukumu dhidi yao zinapaswa kutekelezwa na Tanzania haitahusika kuwatetea.

Rais Magufuli alituma 'salamu' hizo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Dk. Anna Peter na mabalozi watatu.

Rais aliwataka mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi mbalimbali kutojihusisha kwa vyovyote na wafungwa wa makosa ya madawa ya kulevya.

"Watanzania waliohukumiwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya, mabalozi msijihusishe nao... waacheni," Rais Magufuli alisema.

"Kama wamefungwa kifungo cha maisha, waacheni wafungwe, kama wamehukumiwa kunyongwa, wanyongwe tu.

Tukichekacheka, taifa litaathirika na dawa za kulevya." Alisema idadi ya Watanzania waliokamatwa na dawa za kulevya nje ya nchi inatisha kutokana na idadi aliyopatiwa.

Alisema orodha yake inahusisha nchi 17 zenye jumla ya Watanzania 663 huku China ikiongoza kwa kuwa na wafungwa 268 wa dawa za kulevya kutoka nchini.

Rais Magufuli alisema Msumbiji kuna Watanzania 20 waliofungwa baada ya kukamatwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya, Nepal (wanne), India (26) na 268 walioko kwenye magereza ya China.

Nchi nyingine, alitaja Rais Magufuli ni Uturuki (38), Ugiriki (25), Malaysia (16), Indonesia (mmoja) Comoro(watatu), Pakistan (watatu), Japan (60), Nigeria (91), Ghana (mmoja), Uingereza (24), Kenya (66), Misri (wawili) na Uganda (15).

Rais Magufuli alisema vita dhidi ya dawa za kulevya nchini inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake.

Alisema serikali imepewa jukumu la kupambana na kutokomeza biashara ya dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria namba tano ya mwaka 2015 iliyopitishwa na Bunge la 10 na kusainiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete Mei 11, 2015.

"Ninamshukuru sana Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuisaini sheria hiyo pamoja na wabunge," alisema Rais Magufuli na kubainisha: "Kifungu namba 10 katika sheria hiyo kinaeleza mwenye jukumu la kupambana na dawa za kulevya ni serikali."

Alisema alishangazwa kuona hadi Ijumaa alikuwa hajaletewa jina la Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya uteuzi, na kulazimika kumteua kamishna anayemfahamu mwenyewe.

"Unaweza kuona vita hii ilivyokuwa ngumu, hata jina la kamishna mpya ambaye nilipaswa kuletewa ili nimteue lilifichwa," alisema Rais Magufuli.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema pia yeye hakuwa ametaarifiwa kuwa anatakiwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya na kwamba ili kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya, Kamishna Mkuu aliyeapishwa anapaswa kushirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama na wajumbe wa baraza la kudhibiti dawa za kulevya.

Alisema wajumbe wa baraza hilo, ambao pia hakuwa na taarifa, ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.

Wengine ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

WATU 65 Majaliwa alisema serikali haitamwachia mtu yeyote atakayekamatwa na dawa za kulevya hata kama ni 'kigogo'. Alisema kwa mwaka 2016, serikali ilikamata bangi tani 3.4 na kuwapo kwa kesi 934 mahakamani, mirungi tani 1.8 na kesi 135, heroine kilo 50.5 kesi 292, na cocaine kilo 5.4 zenye kesi nne mahakamani.

Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini imepata msukumo mpya tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ataje orodha ya watu 65 ambao alitaka waisaidie polisi kuhusu biashara ya madawa ya kulevya Jumatano.

Kabla ya kutaja orodha hiyo iliyokuwa na viongozi wa dini, wafanyabiashara na wanasiasa, Makonda alikuwa ametoa orodha ya Polisi 12 na wasanii kadhaa ambao walitakiwa pia kufika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa mahojiano.

Lakini harakati za kuwakamata watumiaji, wauzaji na watu wenye taarifa kuhusu biashara ya dawa za kulevya katika jiji la Dar es Salaam ilipata msukumo mkubwa mwanzoni mwa wiki iliyopita baada ya Rais Magufuli kutaka zisiache mtu yeyote.

“Hakuna mtu maarufu, mwanasiasa, waziri au kiongozi yoyote au mtoto wa fulani, askari ambaye anajihusisha na dawa za kulenya aachwe, hata awe mke wangu Janeth... kamata wote weka ndani,” alisema Rais Magufuli.

Alisema biashara ya dawa za kulevya kwa sasa nchini imefikia katika hali mbaya na kwamba zinauzwa kama njugu nchini. Alitaka vyombo vyote vya ulinzi vinavyoendelea kupambana na dawa za kulevya viendelee na mapambano.

Alisema biashara ya dawa za kulenya kwa sasa nchini inapoteza nguvu kazi za Watanzania wengi haswa vijana, na kwamba vyombo vyote vya ulinzi vinapaswa kushirikiana ili kuwakamata hao.

Rais Magufuli aliwataka wahusika kuuwinda mtandao wote unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. “Haiwezekani wauzaji wapo mtaani wanatanua tu, hawakamatwi," alisema Rais Magufuli.

"Kwa mfano kuna muuzaji mkubwa yupo mkoani Lindi, alishikwa na dawa za kulevya, lakini sijasikia hata siku moja akitangulizwa Mahakamani.

"Ninajua kuna viongozi wanamtetea.” Rais Magufuli alikuwa akimzungumzia mtu anayeaminika kuwa 'mzungu wa unga' aliyekuwa akitafutwa zaidi nchini.

Ali Khatibu Haji (47), maarufu kwa jina la Shikuba, alikamtwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Machi, 2014 baada ya kuwindwa kwa miaka miwili kabla ya kuhamishiwa mkoani Lindi.

Anatuhumiwa kuwa kiongozi wa genge lenye makao yake Afrika Mashariki, lakini likiwa na uhusiano wa kibiashara mpaka China, Brazil, Canada, Japan, Marekani na Uingereza.

Rais Magufuli alimwagiza Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma kuhakikisha kesi zote zinazohusu dawa za kulevya zinasikilizwa haraka.

Ijue Methadone Dawa Inayotumika Kutibu Utegemezi wa Dawa za Kulevya...!!

$
0
0

Methadone ni dawa inayotumika kutibu utegemezi wa dawa zingine za kulevya mfano; heroin, codeine, pethidine na morphine. Dawa hii hutolewa kwa kipimo maalumu chini ya usimamizi maalumu.

Methadone huzuia AROSTO na kupunguza au kuondoa utegemezi wa dawa za kulevya. Kwahiyo methadone hutolewa kama tiba na hupewa kwa wale wenye utegemezi wa dawa za kulevya. Kwa wagonjwa wa namna hii kwao ni mbadala salama wa dawa za kulevya wazotumia kama vile heroin.

Inawaweka huru kutoka kwenye kulazimika kutafuta dawa za kulevya na kuwapa fursa ya kuboresha maisha yao. Methadone hutumika kwa watu wote wenye utegemezi wa dawa za kulevya hata wajawazito 
wanaotumia dawa za kulevya hupewa methadone ili kumkinga motto aliyetumboni asipate utegemezi. Hadi sasa hakuna madhara ya methadone yanayojulikana kwa watoto wachanga.

Wakati mwingine methadone hutumika kutuliza maumivu makali ya muda mrefu au maumivu yanayosababishwa na magonjwa yasiyotibika. Watu wakianza kutumia tiba ya methadone, baadhi hujisikia raha iliyozidi na kujiskia kusinzia hali ambayo pia huletwa na baadi ya dawa nyingine za kulevya.

Dozi moja ya methadone hudhibiti arosto kati ya saa 24 hadi 36. Tiba ya kila siku ya methadone inaweza kuendelea bila kikomo ingawa pia inaweza kusitishwa kwa utaratibu maalumu. Iwapo itabidi kusitisha tiba ya methadone, dozi itapunguzwa taratibu kwa muda wa wiki au miezi kadhaa.

Iwapo methadone itasitishwa ghafla dalili kama tumbo kusokota, kuharisha, maumivu ya misuli na mifupa hutokea. Dalili hizi hujitokeza ndani ya siku moja hadi tatu tangu dozi ya mwisho. Na baadaye hupungua polepole ingawa dalili nyingine kama matatizo ya usingizi na hamu kali ya dawa za kulevya zinaweza kuendelea kwa miezi kadhaa.

Na ni muhimu unapopewa dawa yoyote na daktari mwingine hasa zenye kuleta usingizi ni muhimu umjulishe kuhusu matumizi ya methadone. Methadone hunywewa wakati wote. Hata hivyo mjulishe mfamasia wako au daktari wako aina ya chakula unachotumia kabla ya kunywa methadone. Methadone ni dawa yenye nguvu sana na inaweza kuwa na mwingiliano na dawa nyingine na kuleta madhara.

Mweleze mfamasia au daktari kuhusu dawa ulizo kunywa kabla ya kutumia methadone. Ni muhimu kumweleza mfamasia kama umekunywa pombe au dawa ya usingizi kwa mfano valium, fenegan au piriton maana huweza kuleta kifo kama itanywewa na methadone.

Kuchanganya dawa ya methadone na dawa nyingine za kulevya kunaweza kusababisha mwili kuzidiwa na dawa (overdose), hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha.

Kifo cha Denti Chuo Kikuu Chazua Utata,Yadaiwa Alijichinja Au Amechinjwa..!!!

$
0
0

Kifo cha mwanachuo wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Mkwawa kilichopo mkoani Iringa, Matrona Kileo (23), mkazi wa Sanya-Juu, Moshi mkoani Kilimanjaro, kimezua utata baada ya kuwepo madai kuwa amefariki dunia kwa kuchinjwa au kujichinja, kisa kikielezwa ni kukosa mkopo wa elimu ya juu.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni baada ya Matrona kudaiwa kutoweka kuanzia saa 4 asubuhi na kupatikana saa 9 alasiri akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umetupwa kwenye dampo (maarufu mtaa wa Wasomali), eneo la Bomang’ombe, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Baada ya kusimulia mkasa wa kusikitisha wa Matrona,Wikienda lilichimba undani wa kifo cha binti huyo kilichowashangaza ndugu, jamaa na marafiki na kugundua utata kuhusu mambo yafuatayo;

WAKATI ANAFARIKI DUNIA

Habari za kiuchunguzi kutoka kwa vyanzo vyetu vya kuaminika zilieleza kuwa, Matrona amekulia kwa shangazi zake huko SanyaJuu na huko ndiko alikokuwa akiishi siku zote. Ilifahamika kuwa, Matrona hakuwa anaishi na mama yake mzazi na hata wakati mauti inamfika alikuwa anaishi kimyakimya kwa rafiki yake.

KWA NINI RAFIKI YAKE?

Ilidaiwa kuwa, katika kuishi kwake, mwaka juzi Matrona alikutana na mwanamke mmoja kwenye uchaguzi mkuu ndipo wakaanzisha urafiki ingawa mwanamke huyo inasemekana ni mkubwa kiumri ukimlinganisha na marehemu.

MAISHA YA CHUONI

Ilielezwa kuwa, akiwa chuoni, Matrona alionekana kuwa na mawazo mengi lakini haikufahamika kama tatizo lilikuwa ni mkopo au la, lakini baada ya muda, alianza kulalamika kuumwa kichwa.

MAMA, RAFIKI WAMUENDEA IRINGA Ilidaiwa kuwa, baada ya kuumwa kwa muda mrefu, yule mwanamke ambaye anadaiwa kuwa ni rafiki yake, alifunga safari hadi chuoni kwa marehemu mkoani Iringa kwa kutumia gari binafsi akiwa na mama mzazi wa marehemu na kumchukua.

WIKI MBILI KWA RAFIKI YAKE

Iliendelea kusemekana kwamba, kilichoshangaza ni kwa nini mtu ukae na mtoto wa mtu kwa wiki mbili bila kutoa taarifa kwao hadi mauti inamkuta? Ilidaiwa kuwa, ukiangalia kutoka hapo Boma kwa huyo mama hadi Sanya-Juu ni muda wa dakika 45 au saa moja na nauli ni shilingi elfu moja tu lakini kwa nini asiende naye kwao kama aliweza kumfuata Iringa?

RAFIKI HAFAHAMIKI KWENYE FAMILIA

Iliendelea kudaiwa kuwa, rafiki huyo wa Matrona hakuwa anafahamika kwenye familia ya denti huyo.

MAUTI YAMKUTA WAKIJUA YUKO CHUO

Kwa mujibu wa chanzo hicho, familia ilishtushwa kuambiwa kuwa Matrona ameokotwa Boma-Ng’ombe akiwa amefariki dunia wakati wao walikuwa wanajua kuwa binti yao yupo chuoni Iringa.

MASHUHUDA: HAKUJICHINJA, KACHINJWA

Habari nyingine kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zilieleza kuwa, kwa jinsi ambavyo mwili wa marehemu ulikutwa ni vigumu kuamini kuwa alikuwa amejichinja badala yake ilidaiwa alichinjwa kwa sababu mwili wake ulikuwa na majeraha ya visu, bisibisi na kuvunjwa goti moja. Baada ya kuona utata huo, Wikienda liliwasiliana na ndugu wa marehemu lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

MKUU WA CHUO AFUNGUKA Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Profesa Kiliani alipoulizwa juu ya tukio hilo alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli kuna tukio la mwanafunzi wetu Matrona kufariki dunia, lakini mimi sina maelezo mengi zaidi, kama ni kweli ni mkopo au jambo lingine ndiyo limesababisha kifo chake. Kwa sasa liko chini ya vyombo vya dola, hao ndiyo wataweza kutupa majibu sahihi.”

Nionavyo Mimi ya Makonda ni Kama Hadithi ya Mwanakijiji..!!!

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  ameanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya lakini staili yake ni kama hadithi ya mwanakijiji mmoja aliyepambana na chatu kuokoa watu waliokuwa wamemezwa na nyoka huyo. Hadithi hiyo inasema wanakijiji kadhaa walimezwa na chatu, ikatokea kijana mmoja akajitokeza na kusema ni lazima apambane na chatu huyo ili aokoe wale waliomezwa.

Alichukua kisu na kwenda kumpasua tumbo chatu bila tahadhari kwamba anaweza kuumiza walio tumboni, kwa bahati mbaya katika zoezi hilo alimkata kidole kijana mmoja aliyekuwa amemezwa, kijana yule baada ya kutoka tumboni mwa chatu alianza kulaumu kwa nini amemkata kidole na akadai fidia. Naamini katika hawa wanaotajwa na Makonda wapo watakaokuwa kama kijana yule mwanakijiji, wataumia na tayari wengine wanasema watamdai fidia Makonda.

Zoezi hili ni zuri lakini watuhumiwa wangechunguzwa kwanza kabla ya kutajwa. Nimefurahi kuona kuwa Makonda jana hakutaja majina 97 na badala yake kazi hiyo amempa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Nchini, Rogers Sianga.

Utaratibu huo utazuia waliokatwa kidole kulalamika. Ni kweli kwamba Tanzania imechafuka nje ya nchi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa vijana wetu wengi wamekamatwa wakijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya katika nchi mbalimbali duniani, sasa ili kujisafisha lazima kupambana na wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Ziliwahi kutolewa takwimu na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, aliposema kwamba zaidi ya vijana 400 wa Kitanzania wamekamatwa katika nchi mbalimbali duniani kwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Takwimu za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (ilikuwa ikiitwa hivyo 2014) zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2006 na Aprili, 2014, Watanzania 178 walikuwa wakitumikia vifungo mbalimbali nchini China pekee na wengine 113 wakiwa wamefungwa  nchini Brazil, wote wakiwa ni waliojihusisha na biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

Mwaka 2014 taarifa za ukamataji kutoka Jeshi la Polisi, zilionyesha kuwa watuhumiwa 13,846 walikamatwa wakijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nchini kati ya Januari 2009 na Mei 2014.

Pamoja na watuhumiwa hao, taarifa inaonyesha pia kuwa, madawa yaliyokamatwa katika kipindi hicho ni pamoja na kilo 966.06 za heroin, kilo 363.7 za cocain, kilo 45,734 za mirungi na tani 212.071 za bangi, hii ilikuwa idadi kubwa sana.

Vikosikazi vya Kimataifa vya Kupambana na uhalifu katika Bahari ya Hindi, madawa ya kulevya na uharamia (Combined Task Force-150 (CMT-150), navyo vilifanikiwa kukamata shehena ya madawa ya kulevya aina ya heroin kilo 2,300, ikiwa ni katika kipindi cha Januari hadi Mei 2014 pekee. Dawa hizo zilikusudiwa kuingizwa katika  nchi za ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki, zikiwamo Tanzania, Kenya na Somalia.

Sifa ya Tanzania kimataifa imechafuka kutokana na vijana wengi kukamatwa wakijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, hili hakuna anayepinga.

Baadhi ya wananchi, wakiungwa mkono na wataalamu wa masuala ya madawa na uhalifu wenye kuhusisha madawa ya kulevya wanaamini kuwa kukua kwa biashara hiyo nchini pamoja na vijana wengi kujihusisha nayo kunachangiwa zaidi na serikali kupata kigugumizi kuhusu wahusika wakuu wa biashara hiyo ambao wamebatizwa majina kama vigogo wa biashara za madawa ya kulevya au wazungu wa unga.

Inaelezwa kuwa, mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya duniani, ukiwemo ule maarufu kwa jina la “Mafia,” huhakikisha wanawanasa viongozi katika kila ngazi ya uongozi au taasisi ya umma, lengo likiwa kuwatumia kufanikisha biashara yao haramu katika nchi husika.

Kutokana na biashara hiyo kufanyika katika mfumo wa mtandao wa kimataifa, wataalamu ndani ya vyombo vya dola vyenye kushughulikia tatizo hilo wanabainisha umuhimu wa kuikabili biashara hiyo kimtandao pia, katika ngazi ya kikanda kwa nchi jirani kushirikiana, pamoja na ngazi ya kimataifa. Majukwaa kama SADC, kupitia kamati ya yake ya usalama yakitumika itasaidia sana kukabiliana na kuenea kwa biashara hiyo katika nchi wanachama, hata hivyo, tunahitaji kusafisha nyumba yetu kwanza lakini tusafishe kwa kuzingatia sheria.

Madhara yanayoikabili nchi hivi sasa kutokana na vijana wengi kujitumbukiza kwenye biashara hiyo pamoja na utumiaji wa madawa hayo ni pamoja na kupungua kwa nguvu kazi, kuzorota kwa afya za watumiaji na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, madhara yote hayo yakiliathiri zaidi kundi la vijana ambao ni nguvukazi ya taifa.

Kutokana na athari za madawa hayo, taifa linaingia kwenye gharama zisizo za lazima, zikiwemo gharama za matibabu kwa vijana walioathirika. Takwimu zinaonyesha kuwa watumiaji 1,526, wakiwamo wanaume 1,321 na wanawake 205, wa madawa hayo, waliorodheshwa katika kipindi cha mwaka 2011 na Mei,2014, wanapatiwa  tiba ya dawa aina ya “methadone,” katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananyamala na Temeke, gharama inayotumika ingeweza kutumika katika shughuli zingine zenye tija. Watumiaji wa madawa ya kulevya wako katika mazingira hatarishi zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vyenye kusababisha Ukimwi, kutokana na watumiaji hao kufanya ngono zembe pamoja  na kuchangia vifaa kama vile sindano wanazotumia kujidunga.

Magonjwa mengine yenye kusababishwa na madawa ya kulevya ni pamoja na homa ya ini, mapafu, moyo na kifua kikuu, yote yakiwa ni magonjwa hatari kwa maendeleo ya taifa. Uchambuzi zaidi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya unaonyesha kuathiri kilimo cha mazao ya chakula na biashara, kutokana na wakulima katika mikoa mbalimbali nchini kubadili uelekeo kwa kujihusisha zaidi na kilimo cha bangi. Sheria itazame mianya yote yenye kutoa nafasi kuhamasisha matumizi ya madawa ya kulevya.

Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya nchini chini ya bosi mpya Kamishna Mkuu, Rogers Sianga inatakiwa ivalie njuga maeneo yanayotajwa kuathirika zaidi na madawa ya kulevya kama vile Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro na Zanzibar, Nionavyo mimi; ni jukumu la jamii kusimamia kadhia hii ili itokomee kwa kufuata sheria na kamwe isiwe kupakana matope tu.

Ulinzi waimarishwa Taasisi ya Moyo Muhimbili Ambako Yusuf Manji amelazwa

$
0
0
Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.

Manji aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa alipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.

Askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga walionekana wakiimarisha ulinzi.

Ilipofika saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.

Akiwa amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za mgonjwa.

Februari 8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya watu 65, akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu masuala ya dawa za kulevya.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images