Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Huu Ndio Msikiti ambao Diamond Anapang Kuujenga..!!!

0
0

Diamond amejitolea kujenga msikiti.

Hitmaker huyo wa ‘Marry You’ amesema kwa sasa anajenga msikiti huo lakini upo mkoani Mtwara.

“Mimi nakushukuru sana mama yangu, asante sana. Naamini kabisa nitakuja Mtwara, Mtwara kule sasa hivi kuna msikiti ninaujenga na inshallah nikimaliza nitaenda kuuzindua,” alisema Diamond Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wake Nillan iliyofanyika nyumbani kwake Madale.

Diamond alisema maneno hayo wakati akimshukuru mama mmoja ambaye alimkabidhi viwanja viwili vya hekta 17 kwa kila kimoja huku kimoja kikiwa ni kitalu cha gypsum.

Hana Hamu ya Kufanya Mapenzi na Mimi..Naomba Ushauri

0
0

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30, nina mpenzi wangu wa muda mrefu toka 2014 japo mapenzi yetu yamekuwa hayana muendelezo muzuri kutokana na tabia za huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano yetu vizuri sana baadae mwenzangu alibadilika ghafla, nikaja kugundua alikuwa na mahusiano na wanaume wengine (zaidi ya mmoja) tukawa tumepotezana kwa mda kidogo coz alikuwa hapokei simu wala kujib text zangu alafu akawa ni mtu wa kusafiri sana kumbe alikuwa anasafiri na hao mabwana zake, siku nimekutana nae nilimuona na dalili za mimba roho iliniuma sana, mwanzoni alidanganya baadae akakubali akawa ametoa hiyo mimba akaomaba nimsamehe kwa sababu nampenda sana tena sana nikawa nmemsamehe. 

Tukawa pamoja kwa mda mfupi baadae alianza tabia yake ya kuruka ruka na starehe kwa sana, niliamua kumuacha japo roho ilikuwa inaniuma alafu yeye hata hajali kila kitu kwake poa tu. Baadae alirudi akaanza kunitafuta akaomba msamaha kama kawaida yake, kupenda ni hatari sana jamani nilimsamehe tukaanza kuwa pamoja, alikaa kwangu kwa muda wa week, nikaanza michakato kwenda kutoa posa na mahari kwao.

Sasa alivyorudi nyumbani kwao akaanza tena unaweza mpgia simu anakuambia sipo nyumbani nipo kwa dada angu fulani, au kwa bibi nitarudi kesho, au nipo hospitali bibi anaumwa baadae simu inapotea hewani hata siku mbili akipatika anakuambia huku kijijini simu ilizima charge. Sasa kilichonichosha zaidi sasahivi hana hata hamu ya mapenzi kabisa tofauti na navyomjua mimi, huyu mpenzi wangu hapo awali alikuwa akiniona tu hutumii nguvu nyingi kumuandaa, lakini sasa hivi hata ukifanyeje hawezi kuwa tiyari hadi umpake mafuta kidogo. na unaweza kumuomba hata mwezi nzima anakuambia sijisikii, sina hamu.

Naomba ushauri wadau, nifanje ili aweze thamini hisia zangu, au hata kama nikimuacha nifanyeje coz nampenda sana huyu dada natamani awe mke wangu wa ndoa, kuna vitu huwa vinanifanya nimpende sana ni rafiki, mnataniana na kucheka, mpole ila sasa ndo hayo mambo yake, nilishajaribu kumuacha nashindwa nafuta namba kila kitu ila akinipigia tu au nikumuona tu nabadilisha mawazo.

By Von G

Baada ya Kulianzisha,,Makonda Yupo Hatarini Kuuawa,Vigogo wa Madawa ya Kulevya Wapanga Mikakati ya Kummaliza kwa Gharama Yeyote Ile..!!!!

0
0

Wakati vita dhidi ya madawa ya kulevya jijini Dar vikipanuka na kugeuka kuwa suala la kitaifa, kuna kila dalili kuwa usalama wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda upo hatarini, Risasi Mchanganyiko limebaini.

Juzi Jumatatu, Paul Makonda alijitokeza tena hadharani na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yanayohusiana na vita alivyovianzisha, huku ikiwa ni mara yake ya tatu kutaja majina ya wanaojihusisha na madawa ya kulevya, safari hii, akitoa orodha ya watu 97.

HATARI YAKE IKOJE?

Biashara ya ‘unga’ ni moja kati ya biashara chache zenye fedha nyingi duniani, ambayo bahati mbaya inapigwa vita na serikali nyingi. Watu wanaojihusisha na shughuli hii, wana fedha nyingi na wako tayari kufanya lolote linalowezekana kuifanya biashara yao kuwa salama.

Kwa Paul Makonda kutangaza vita hadharani, tena akitaja majina ya watu na njia zinazotumika kuuleta, kuusambaza na kuusafirisha, anajiweka katika nafasi mbaya ya kuwa mlengwa wa wafanyabiashara hao, hasa kwa kuwa kukamatwa kwao siyo tu kutaharibu biashara yao hiyo, bali pia wao wenyewe watapotea.

Mfano mmojawapo wa jinsi watu wanaojihusisha na biashara hiyo walivyo na uwezo mkubwa, ni kesi ya bilionea wa unga wa Colombia, Pablo Escobar, aliyeuawa Disemba 2, 1993, baada ya mahakimu zaidi ya 30 waliosimamia shauri hilo kuuawa, licha ya kuendesha kesi hiyo wakiwa mafichoni, tena sauti zao zikiwa zimewekwa mawimbi ya kutofahamika.

MAADUI ZAKE WAMEONGEZEKA

Awali, ilionekana ni wauza madawa ya kulevya pekee ndiyo ambao wanaweza kusemwa kuwa ni maadui zake, lakini baada ya mazungumzo yake na vyombo vya habari Jumatatu iliyopita, watu ambao watafurahia kuona kiongozi huyo kijana anapatwa na matatizo, wameongezeka.

Watu hao ni pamoja na wamiliki wa maduka ya kubadilishia fedha maarufu kama Bureau de Change, wafanyabiashara wa mitungi ya gesi, wamiliki wa mahoteli na klabu za kamari (Casino), achilia mbali watoto wa viongozi wakubwa tokea serikali ya awamu ya tatu, chini ya Benjamin Mkapa.

KWA NINI HAWA?

Licha ya kushangazwa na wingi wa maduka ya kubadilishia fedha (alisema yapo zaidi ya 200 kwa Dar pekee), lakini pia aliyatuhumu kufanya miamala inayozidi kiwango kinachotakiwa kisheria, hivyo kuufanya mzunguko wa fedha zinazopitia hapo kuwa mkubwa.

Alisema wingi huo wa fedha, unatia shaka kuwa huenda unatumiwa na watu wa biashara ya madawa ya kulevya katika kutakatisha fedha. Kwa vyovyote, wenye maduka hawa hawajapendezwa na tuhuma dhidi yao na hivyo nao kuingia vitani kimyakimya.

Biashara ya mitungi ya gesi nayo ilitajwa kuwa ni mojawapo ya njia zinazotumiwa na wafanyabiashara hao kuficha madawa hayo wakati wakisafirisha kutoka au kwenda ughaibuni.

Aidha, alidai kuna hoteli kadhaa kubwa zenye wakazi wa kudumu, ambao wanatambuliwa na wamiliki wake, hivyo atahakikisha anawafanyia kazi, kitu ambacho kinaongeza idadi ya maadui, kama ilivyo kwa wamiliki wa nyumba 200 waliosemwa kuwa wanaruhusu biashara hiyo kufanywa ilhali wakijua ni kosa kisheria.

MBINU ZINAZODAIWA KUANDALIWA

Baadhi ya wanaharakati wanaopinga biashara ya madawa ya kulevya, ambao waliomba hifadhi ya majina yao, wamesema mbinu mbalimbali zinaweza kutumika ili kumdhuru kiongozi huyo, aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Mbinu hizo ni pamoja na kumwinda na kumuua kwa risasi, kitu ambacho ili kukidhibiti, wameomba kuimarishwa kwa ulinzi wake, nyumbani, kazini na hata awapo barabarani.

VIDOSHO, AJALI ZA KUTENGENEZWA

Eneo lingine alilotahadharishwa kujihadhari nalo ni pamoja na wasichana warembo, kwani wanaweza kutumiwa na maadui ili kumtia matatizoni, ikiwemo kumwekea sumu katika chakula, kinywaji au hata kumdhuru kwa namna nyingine.

Wadau hao wamelitaja eneo lingine la hatari linalopaswa kuangaliwa zaidi, ni kwa maadui zake hao kuweza kumtengenezea ajali ya kumdhuru, ili mradi wafanikiwe kuzima harakati zake za madawa ya kulevya alizoanzisha na kuungwa mkono na watu wengi.

KUHUSU ULINZI, HUYU HAPA SIRRO

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alizungumza na Risasi Mchanganyiko juu ya ulinzi wa kiongozi huyo. Akionyesha mshangao, alisema suala hilo siyo jambo la kuuliza kwa sababu wao wanaelewa nini kinapaswa kufanyika.

“Tunajua ukubwa wa vita hivi na madhara yake pia tunajua, huyu ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, tunampatia ulinzi imara kabisa na kwa hili wala watu wasiwe na wasiwasi.”

Kimenukaaa..Spika Ndugai Ajibu Tamko la Makonda,Adai Makonda Ni....!!!

0
0

SIKU moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutakiwa kutimiza ahadi yake ya kuweka vifaa vya kupima wabunge kama wametumia kilevi ama dawa za kulevya kabla ya kuingia Ukumbi wa Bunge,  amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mtani wake, hivyo watu wasijali maneno yake.

Juzi Makonda alimwomba Spika Ndugai kuweka kipimo hicho ili kabla wabunge hawajasimama kuchangia hoja wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.

“Kaka yangu Ndugai alisema ana nia ya kuweka kifaa maalumu kuwapima wabunge kama wanatumia dawa za kulevya au la, hivyo atimize nia yake hiyo ili kama na huko wapo tuwanyofoe,” alisema Makonda.

Akizungumza  kwa simu,  Ndugai alisema: “Makonda ni mtani wangu, mimi ni Mgogo yeye ni Msukuma, kwahiyo tunataniana… msijali maneno yake, alikuwa ananichapa tu kidogo.”

Wakati wa mkutano wa tatu wa Bunge la 11 Mei mwaka jana, Spika Ndugai alipata kulieleza Bunge kuwa anafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa wabunge.

Ndugai alitoa kauli hiyo siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga baada ya kuingia bungeni akiwa amelewa.

Alisema kuwa kuna wabunge kadhaa huingia bungeni wakiwa wametumia vilevi vikali.

“Tunajaribu ku-identify (kuwatambua) watu maalumu wanaoweza kutusaidia kuzungumza na hawa watu ili waondokane na matatizo yale ambayo tutaweza kuyagundua.

“Lakini wale wanaofanya kwa kificho itakuwa tabu kidogo. Lakini huko mbele tutakwenda kwenye vifaa, maana si ulevi tu, kuna sigara kubwa (bangi), unga (dawa za kulevya)… watu wanapiga konyagi hadi mchana, kimsingi mambo ni mengi.

“Simaanishi wabunge wote, maana mtu anaweza kufikiri ni wote, hapana. Hili ni kundi dogo mno la wabunge na hawajai hata mkononi. Lakini wabunge walio wengi ni wazuri sana, hawanywi pombe wala nini. Kikundi hiki kinahitaji msaada wa ushauri,” alisema Ndugai.

MAONI YA WABUNGE

Kauli ya Makonda ya kuwataka wabunge kupimwa akili ili kubaini kama wanatumia aina yoyote ya dawa za kulevya au la, imepokewa tofauti na baadhi ya wabunge.

Akitoa maoni jana kwa simu, Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema), alisema wabunge tayari   wameshapimwa akili na wananchi wao na ndio maana wakapewa ridhaa ya kuwaongoza.

Alisema kulikuwa na michakato mingi hadi wao kuchaguliwa, ikiwa ni pamoja na ya ndani ya chama, majimboni na hata kwenye Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), hivyo wao wako safi hadi wakapitishwa na wananchi wao.

“Anayetakiwa kupimwa akili kama anatumia dawa au la au kama aliugua au la ni mtu ambaye aliwahi kumfunga viatu mtoto wa rais, kulala kwenye sebule ya Sitta, na hata kumpiga mzee Warioba na kutukana waliomzidi umri bila sababu,” alisema Kubenea.

Aliongeza kuwa anaamini kwa wasiopimwa sehemu yoyote akiwemo Mkuu wa Mkoa na wateule wengine wa rais ndio ambao wanatakiwa kupimwa.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu, alisema Bunge ni mhimili mwingine, hivyo Makonda hana nguvu ya kuwataka wao kupima. 

Alisema kama ni mawazo ya kutakiwa kupima au kutopimwa, anayetakiwa kusema hiyo ni Spika wa Bunge Ndugai na kama yeye ataafiki wao watakubali kupimwa.

“Sisi mhimili wetu unasimamiwa na Spika ndiye mkuu wetu, lakini alishawahi kusema hilo siku nyingi  kwamba mhimili wake usiingiliwe hovyo hovyo, lakini mtu mmoja mdogo sana anajiongelesha, ambaye hana hata mamlaka,” alisema Sugu.

Alisema yeye mwenyewe Makonda ana matatizo yake na kama akihitaji wao wapimwe, watatakiwa kwenda wote.

Hata hivyo, Sugu ambaye ni Waziri Kivuli wa Habari Utamaduni na Sanaa, aliwalalamikia waandishi wa habari kwa kumpa nafasi Makonda na kuacha kuandika maoni wanayotoa wao kama wazo lake alilotoa bungeni siku ya kufunga Bunge.

Mbunge huyo alisema anatamani siku moja Makonda apelekwe Mkoa wa Mbeya na akawaongoze kwa miezi sita tu aone na si kukaa Dar es Salaam peke yake huku akiingilia kazi za Spika.

Sugu alisema Serikali ya awamu ya tano inaonyesha wazi kwamba inalichukia Bunge kutokana na matamshi mbalimbali yanayotolewa.

Alisema kama angekuwa yeye badala ya kushauri Bunge kwenda kupima, basi anashauri viongozi wote kupimwa wakiwamo wakuu wa wilaya, mikoa na wengine wa Serikali ili nchi iwe salama kwa kila mtu.

Noma Sanaa..Mateja Mitaani Walalamika Madawa ya Kulevya Kupanda Bei,Walia Bei Ishushwe..!!!

0
0

IKIWA ni takribani siku 13 tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Jeshi la Polisi kuanza kampeni ya kukamata na kutangaza majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya, baadhi ya watumiaji wa dawa hizo (mateja), wamelalamika kuadimika kwa bidhaa hiyo na ikipatikana bei yake inakuwa juu mara mbili.

Taarifa hizo ambazo ni njema kwa viongozi wanaoendesha vita hiyo iliyotangazwa na Rais Dk. John Magufuli alipokuwa akizindua Bunge la 11, zilipatikana baada ya gazeti hili kutembelea baadhi ya maeneo maarufu Dar es Salaam wanapopatikana watumiji wa dawa hizo.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watumiaji hao, zilisema bei ya dawa hizo za aina ya heroin kwa kete moja, imepanda mara tano zaidi ya bei ya awali iliyokuwa ikiuzwa kabla ya kuanza kwa kamata kamata. Tumeacha kutaja bei kwa sababu za kitaalamu.

Walisema licha ya kupanda kwa bei hiyo, hata wauzaji sasa hawamuuzii mtu wasiyemjua kwa hofu ya kukamatwa.

Katika kituo cha Manyanya Kinondoni, baadhi ya mateja walisema kuwa kwa sasa tangu sakata la kuwakamata wauzaji, waingizaji na watumiaji, unga umepanda bei kutokana na kuadimika kwani wauzaji wanauza kwa kujificha.

Mmoja wa mateja hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, alisema kwa sasa si rahisi kupata unga kwa sababu wauzaji wanauza kwa kujificha na kama ukipatikana bei yake imepanda maradufu.

“Ni shida kupata unga sasa hivi maana waliokuwa wanatuuzia wanajificha ili wasikamatwe, kwahiyo ukibahatika kuupata utauziwa kwa bei ya juu kwa sababu siku za nyuma kete ulikuwa unapata kwa Sh 1,000 hadi 2,000  lakini sasa hivi unaanzia 3,500 hadi 5,000.

“Mfano kulikuwa na muuzaji hapo upande wa pili wa barabara, lakini amekamatwa na hakuna tena dawa hapo,” alisema Aisha.

BADO WAPO

Hata hivyo, mateja hao waliendelea kuwapo katika maeneo hayo tofauti na ilivyodaiwa kuwa wakilewa watakamatwa na kupelekwa kituo cha polisi ili wawataje wanaowauzia.

Katika vituo vya daladala vya Mwananyamala Hospitali, A, Tandale, Magomeni Kagera, Kinondoni Mkwajuni na Studio, mateja walikuwapo japo walionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.

WAOMBA KUPELEKWA SOBER HOUSE

Mmoja wa mateja waliokuwapo katika kituo cha daladala cha Magomeni Kagera aliyejitambulisha kwa jina moja la  Juma, alisema wanaiomba Serikali kuwasaidia kwa kuwapeleka katika vituo vya tiba za waathirika (sober house) ili wakapate matibabu kwa kuwa baadhi yao wameanza kupata madhara kutokana na kuadimika kwa dawa hizo.

“Tunaiomba Serikali itusaidie kwa kuwa wenzetu ambao wanakosa ‘unga’ wanapata shida sana kwa kutapika na kuharisha na hali zao si nzuri,” alisema.

WAFANYABIASHARA WAPONGEZA

Baadhi ya wafanyabiashara katika maduka yaliyo jirani na vituo vya daladala, wamesema hatua iliyochukuliwa na Serikali kupambana na dawa za kulevya itapunguza wizi katika mitaa yao.

Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Mama Winnie katika kituo cha Mwananyamala A, alisema kuwa wimbi la wizi lilikuwa likiongezeka siku hadi siku kutokana na mateja kutafuta fedha za kuvutia.

“Hapa tulikuwa tunaibiwa sana na unaweza kuletewa nguo mbichi iliyoanuliwa kwenye kamba na kuuziwa kwa bei rahisi tofauti na bei yake halisi, ili mradi tu apate fedha ya kununulia unga,” alisema Mama Winnie.

Wabunge Zanibar Wamuamulia Maalim Seif,Wataka Apewe Adhabu Kali, Sababu Hii Hapa..!!!!

0
0

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wameshauri kuwekwa adhabu kali kwa atakayejitangazia ushindi katika Uchaguzi Mkuu.

Kauli ya wawakilishi hao imekuja baada ya aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Maalim Seif Sharif Hamad kujitangaza mshindi wa uchaguzi huo.

 Wajumbe hao walishauri adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa mgombea wa nafasi ya kisiasa atakayejitangazia ushindi, kabla ya matokeo kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Wakichangia Muswada wa Sheria wa Kufuta Sheria ya Tume ya mwaka 1992 na kutunga sheria ya kuanzisha Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), majukumu na uwezo, wajumbe hao walisema muswada huo unapaswa kutekelezwa haraka.

Katika kikao kilichoendelea jana Chukwani nje kidogo ya mji wa Unguja, Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani, Ali Salim amesema adhabu iliyomo ndani ya muswada huo faini ya Sh500,000 au Sh1 milioni ni ndogo ukilinganisha na kosa la kujitangaza mshindi.

Tenaaa..Mfumo Mpya wa Kutumia Namba za Simbu Kuanzishwa Mwezi Ujao,Utaruhusu Kuhama Mtandao Mmjoa Kwenda Mwingine Bila Kununua Laini Mpya..!!!

0
0

Mfumo mpya wa matumizi ya namba za simu (Number Portability) unatarajiwa kuanzishwa ifikapo Machi Mosi kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za simu nchini.

Kampuni za simu zilizoingia katika mkataba huo ni pamoja na Tigo, Vodacom, Airtel, TTCL, Zantel, Smile, Smart na Halotel.

Jana, TCRA ilitangaza huduma hiyo mpya kwa watumiaji wa simu nchini, itakayomwezesha mteja kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine na kuendelea kutumia namba yake ya awali.

Mpango huo tayari umeshatekelezwa kwenye nchi nyingi za Ulaya na hata Afrika Kusini.

Mmoja wa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi, Musa Aziz amesema pamoja na faida zilizopo bado kuna hofu kwa watumiaji kutokana na usumbufu wa mawasiliano.

“Nafikiri kutakuwa na gharama za ziada mimi nikimpigia mwenzangu sitajua kwa wakati huo anatumia mtandao gani, hapo ninaweza kuingia gharama kubwa zaidi, sina hakika kama italeta unafuu japokuwa ni mpango mzuri,” amesema Aziz.

Kudadeki..Diamond Naye Ajisalimisha Polisi ,Aachiwa Kwa Faini ya 60,000 Tu..!!!

0
0

Baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kuonekana kukiuka Sheria za Usalama Barabarani, ametozwa  faini ya Sh60,000 katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Usalama Barabarani kwa makosa mawili ya kutofunga mkanda na kuachia usukani wakati akiendesha gari lake akiwa na familia.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema walimuita Diamond baada ya kuona kipande kifupi cha video kwenye mtandao wa Instagram.

“Alitii wito na alikuja juzi ila nilikuwa na kazi nyingi sikuweza kuonana naye na leo (jana) aliweza kufika tena tukaonana, akalipa faini na tukamuonya kufanya kitendo kile alihatarisha maisha ya familia yake,” amesema Mpinga.

Mpinga amesema kutokana na umaarufu wake ndani na nje ya nchi kitendo hicho kingesababisha mashabiki wake kumuiga na kusababisha ajali.

Makonda Hachomoki,Akabiliwa na Kesi Sita Nzito...Habari Katika Vichwa vya Magazeti ya Leo 16/2/2017..!!!

Manji na Wafanyakazi Wake 25 Kupanda Kizimbani Leo...!!!!

0
0

Wafanyakazi 25 wa Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na  mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, wanaodaiwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini, leo wataanza kujieleza kwa maandishi katika ofisi za uhamiaji.

Ofisa uhamiaji wa mkoa, John Msumule  amesema uhamiaji haijawakamata wafanyakazi hao, isipokuwa inashikilia hati zao za kusafiria. 

“Kesho (leo) tunatarajia kuanza kuwahoji ili watoe maelezo yao, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kuwapeleka mahakamani Jumatatu ili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukua nafasi yake.”

Mbali na wafanyakazi hao, Manji anasubiriwa na sekeseke jingine la uhamiaji baada ya kuitwa ili aunganishwe na wafanyakazi hao kushtakiwa kwa madai ya kuajiri wageni wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Manji amekuwa akishikiliwa na polisi tangu Februari 9 alipoitikia wito wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kuripoti kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Ofisa uhusiano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Anna Nkinda amesema Manji aliruhusiwa hospitali jana saa 10:00 jioni baada ya kupatiwa matibabu kwa siku tatu. Hata hivyo haikufahamika alikokwenda.

Picha ya Mwimbaji Linah Sanga Ikionyesha Ana Ujauzito Yavuja

0
0

Wambea Kumekucha na picha inayoonyesha mwimbaji Linah Sanga ikiwa na ujauzito na Kwa waliokua hawamjui Shemela ndo huyo hapo anaitwa "Sheby Sanga"

Video: Eric Omondi Alivyoigiza Filamu ya ‘Adam and Eva’

0
0
Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Eric Omondi amekuwa na utaratibu wa kufanya parody ya nyimbo mbalimbali ambazo zifanya vizuri pamoja na filamu ambazo zimewahi kufanywa zamani. Baada ya kuachia filamu yake fupi aliyoigiza kutoka kwenye ‘God Must Be Crazy’ sasa amekuja na filamu ya ‘Adam na Eva’ yenye urefu wa dakika 15 na sekunde 10.

Msumbiji Inafahamu Tanzania ina Wasumbiji Haramu Wangapi?

0
0
Ama kweli nyani hajui wala haoni kundule. Ni ajabu kusikia eti Msumbuji inafukuza kwa mbwembwe wahamiaji haramu kutoka Tanzania. Mbona Tanzania ina maelfu wa raia wa msumbiji wa aina hiyo ambao sisi tumewakumbatia kama ndugu zetu? Tena wamepewa hadhi hata ya kupigia kura baadhi ya vyama vya siasa nchini? Tukiamua na sisi kuwatimua pia Msumbiji na dunia nzima itatikisika.

Umeipata Hii ya Mwimbaji Barnaba Kumfumania Mkewe na Mwanaume Mwingine?

0
0
Mke wa Barnaba Akiwa na Bwana Mwigine 
Jana February 15 2017 kupitia XXL ya clouds FM, Soudy Bwown ametuletea U Heard inayohusu mwimbaji staa wa Bongofleva Barnaba kudaiwa kuachana na mke wake.

Kwa mujibu Soudy Brown inadaiwa Barnaba amefikia hatua ya kuachana na mke wake baada ya kumfumania mke wake hivyo ikabidi ahame nyumbani na kutafuta sehemu nyingine. Soudy Brown kapiga stori na msanii wa Bongofleva kumuuliza kuhusu taarifa hizo za rafiki yake Barnaba.

‘Mimi nakaa karibu na Barnaba, taarifa hizo ningekuwa nimeshazisikia kwa hiyo ngoja nizifuatilie’ – Amini

Serikali Yafunguka Kuhusu Watanzania Wanaofukuzwa Nchini Msumbuji

0
0
Kumekuwepo na taarifa mpaka za video Watanzania mbalimbali wakiongea baada ya kuondolewa kwa lazima nchini Msumbiji na kurudishwa Tanzania kwa Malori huku wengine wakisema Polisi wa Msumbiji wamewanyang’anya simu na pesa walizokua nazo.

Leo Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kupitia Naibu waziri wake imetoa ufafanuzi kuhusu ishu hii kwa kusema “Mnajua kabisa uhusiano wa Tanzania na Msumbiji sio mbaya na hata December 2016 tulifanya mkutano na kutazamia maswala ya uhusiano na biashara“

“Baada ya kusikia taarifa za kukamatwa na kuondolewa kwa Watanzania, tulituma ubalozi wetu kujua ni kitu gani kinaendelea na wameambiwa Serikali ya nchi hiyo inawaondoa walioingia kwenye taifa hilo isivyo halali“

“Ubalozi wetu kwa Msumbiji wako pale wanashirikiana na serikali ya Msumbiji, uongozi wa Mtwara na UHAMIAJI Mtwara pia wako pale wanashughulikia… tunachokifanya sasa hivi ni kuhakikisha kama ni kweli yale yaliyosemwa na Watanzania ikiwemo kunyang’anywa hati za kusafiria“

“Tumeambiwa zoezi hilo la Msumbiji sio tu kwa raia wa Tanzania bali raia wa nchi mbalimbali walioingia nchini humo bila vibali au kufata taratibu za kuishi na kufanya kazi nchini humo“

Naibu Waziri ameahidi kutoa taarifa kamili baadae lakini ya kufahamu kwa sasa ndio hayo hapo juu

Aliyekuwa Mume wa Zamani wa Zari Hassan Azidiwa na Pesa Aamua Kuzigawa Mtaani

0
0

Mume wa zamani wa Mrembo Zari Hassan Anayeitwa Ivan Amenaswa Mtaani akigawa Pesa kwa watu wasiojiweza huko nchini Uganda....Inasemekana jamaa huyu anamkwaja wa kutosha mpaka hajui pa kuupeleka kiasi ambacho ameamua kuzigawa barabarani...

Tazama Video Hapa:

Nikki Mbishi Atoa Onyo Kwa Vyombo vya Habari Kwa Watakao Sambaza na Kupiga Wimbo wake wa "I am Sorry JK"

0
0
Ikiwa ni saa zisizodi ishirini na nne (24) toka itoke taarifa ya MwanaHiphop Tanzania Nikki Mbishi kutoa taarifa ya kuitwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuhojiwa kuhusu wimbo wake unaomzungumzia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ‘I am sorry JK‘ Rapper huyo ameandika sentensi kadhaa.

“Salaam, baada ya salamu naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia‘

Ameendelea kuandika kuwa
’Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA, naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili‘

Nikki alitoa tahadhari pia
 ‘Kwa yeyote atakae endelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote Duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ulishasambaa, hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria [​IMG] .

#Asanteni sana, naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k. MUZIKI NI AJIRA,MUZIKI NI KAZI YANGU #Mungu_Simama_Kweli_Idhihirike

Ni wako mtanzania mvumilivu:
Nikki Mbishi @2017
With no offence!

Watumia Unga Waanza Kukiona cha Moto..Wadai Unga Umeadimika Mtaani

0
0


IKIWA ni takribani siku 13 tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Jeshi la Polisi kuanza kampeni ya kukamata na kutangaza majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya, baadhi ya watumiaji wa dawa hizo (mateja), wamelalamika kuadimika kwa bidhaa hiyo na ikipatikana bei yake inakuwa juu mara mbili.


Taarifa hizo ambazo ni njema kwa viongozi wanaoendesha vita hiyo iliyotangazwa na Rais Dk. John Magufuli alipokuwa akizindua Bunge la 11, zilipatikana baada ya gazeti hili kutembelea baadhi ya maeneo maarufu Dar es Salaam wanapopatikana watumiji wa dawa hizo.


Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watumiaji hao, zilisema bei ya dawa hizo za aina ya heroin kwa kete moja, imepanda mara tano zaidi ya bei ya awali iliyokuwa ikiuzwa kabla ya kuanza kwa kamata kamata. Tumeacha kutaja bei kwa sababu za kitaalamu.


Walisema licha ya kupanda kwa bei hiyo, hata wauzaji sasa hawamuuzii mtu wasiyemjua kwa hofu ya kukamatwa.


Katika kituo cha Manyanya Kinondoni, baadhi ya mateja walisema kuwa kwa sasa tangu sakata la kuwakamata wauzaji, waingizaji na watumiaji, unga umepanda bei kutokana na kuadimika kwani wauzaji wanauza kwa kujificha.


Mmoja wa mateja hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, alisema kwa sasa si rahisi kupata unga kwa sababu wauzaji wanauza kwa kujificha na kama ukipatikana bei yake imepanda maradufu.


“Ni shida kupata unga sasa hivi maana waliokuwa wanatuuzia wanajificha ili wasikamatwe, kwahiyo ukibahatika kuupata utauziwa kwa bei ya juu kwa sababu siku za nyuma kete ulikuwa unapata kwa Sh 1,000 hadi 2,000  lakini sasa hivi unaanzia 3,500 hadi 5,000.


“Mfano kulikuwa na muuzaji hapo upande wa pili wa barabara, lakini amekamatwa na hakuna tena dawa hapo,” alisema Aisha.


BADO WAPO


Hata hivyo, MTANZANIA iliwakuta mateja hao wakiendelea kuwapo katika maeneo hayo tofauti na ilivyodaiwa kuwa wakilewa watakamatwa na kupelekwa kituo cha polisi ili wawataje wanaowauzia.


Katika vituo vya daladala vya Mwananyamala Hospitali, A, Tandale, Magomeni Kagera, Kinondoni Mkwajuni na Studio, mateja walikuwapo japo walionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.


WAOMBA KUPELEKWA SOBER HOUSE


Mmoja wa mateja waliokuwapo katika kituo cha daladala cha Magomeni Kagera aliyejitambulisha kwa jina moja la  Juma, alisema wanaiomba Serikali kuwasaidia kwa kuwapeleka katika vituo vya tiba za waathirika (sober house) ili wakapate matibabu kwa kuwa baadhi yao wameanza kupata madhara kutokana na kuadimika kwa dawa hizo.


“Tunaiomba Serikali itusaidie kwa kuwa wenzetu ambao wanakosa ‘unga’ wanapata shida sana kwa kutapika na kuharisha na hali zao si nzuri,” alisema.


WAFANYABIASHARA WAPONGEZA


Baadhi ya wafanyabiashara katika maduka yaliyo jirani na vituo vya daladala, wamesema hatua iliyochukuliwa na Serikali kupambana na dawa za kulevya itapunguza wizi katika mitaa yao.


Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Mama Winnie katika kituo cha Mwananyamala A, alisema kuwa wimbi la wizi lilikuwa likiongezeka siku hadi siku kutokana na mateja kutafuta fedha za kuvutia.


“Hapa tulikuwa tunaibiwa sana na unaweza kuletewa nguo mbichi iliyoanuliwa kwenye kamba na kuuziwa kwa bei rahisi tofauti na bei yake halisi, ili mradi tu apate fedha ya kununulia unga,” alisema Mama Winnie.

Mastaa Bongo Wadaiwa Kukauka Kwenye Viwanja vya Starehe...Kisa Hichi Hapa

0
0

DAR ES SALAAM: Kufuatia msala wa kutuhumiwa kujihusisha na utumiaji au biashara ya madawa ya kulevya unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, sasa baadhi ya mastaa wanadaiwa kukauka kwenye viwanja vya starehe.


Chanzo makini ambacho ni mmoja wa mastaa, alifunguka kuwa tangu sakata la kutajwa majina lilipoanza hali ni mbaya kwa mastaa hasa wa kike kwani waliokuwa wakiwapa fedha za kufanya mbwembwe mjini wengi wanahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa tayari.


“Ukweli hali ni mbaya kwa sisi mastaa ndiyo maana unaona hata zile mbwembwe za mjini hazipo tena, wengi tunahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa au wadhamini wao.


“Wasanii wa kike ndiyo wenye hali mbaya zaidi kwani wale mapedeshee waliokuwa wakiwapa jeuri wamepunguza kuwapa fedha huku wengine wakiwa wameshatajwa majina hali ambayo inaendelea kuzua hofu zaidi,” kilisema chanzo hicho.


Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, ni kweli hali ni mbaya kwa mastaa na wengi wao wakiwa na hofu kubwa baada ya kuona wenzao au watu wao wa karibu, wametajwa kwani hata wakipigiwa simu zao za mikononi wana hofu kuzipokea au hata wanapofuatwa majumbani mwao husemekana wamesafiri.


Uchunguzi huo ulibaini kuwa, kwenye kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar, hivi sasa pamekauka kwani wahudhuriaji ni wachache huku mastaa wakiwa hawaonekani kama ilivyokuwa zamani walipokuwa wakijirusha.


Siyo kwenye viwanja tu, lakini pia hata ngoma mpya zilizoachiwa hivi karibuni hazina msisimko kwenye kumbi hizo kama zamani, mfano ukiwa ni wimbo mpya wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake wa Mary You akimshirikisha mwanamuziki wa Marekani, Ne-Yo.


Pia siku kadhaa zilizopita wasanii wakali kwenye Bongo Fleva, Diamond, Ali Kiba na Navy Kenzo walipata tuzo zilizotolewa Kampala nchini Uganda zilizojulikana kwa jina la Hapipo Awards, lakini hazikuwa gumzo kama kipindi kingine zinavyokuwa na hii yote ni kutokana na sakata la madawa ya kulevya.


Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, nako kumepoa kwani ishu kubwa inayojadiliwa ni masuala ya madawa ya kulevya jinsi watu wanavyotajw a , wale mastaa wa liozoea kuposti picha na mambo yao mbalimbali kwa sasa wanaonekana kupoa, jambo ambalo ni tofauti na zamani.


Baadhi mastaa ambao kabla ya ishu ya madawa ya kulevya walikuwa hawakosi klabu lakini sasa hawaonekani ni pamoja na Gigy Money, Amber Lulu, Aunty Lulu, Isabela Mpanda, Shilole, Wema, Uwoya, Baby Madaha na wengine kibao. Akizungumzia ishu hiyo, Amber Lulu alisema:


“Naona maisha yako vilevile, sina wasiwasi kwani wale waliokuwa wanategemea wanaume waliotajwa ndo’ wenye shida.”


Naye Isabela Mpanda alifunguka:


“Ni kweli, hali inazidi kuwa ngumu japokuwa huwa sipendi kwenda klabu kwani mimi ni mwanamuziki na sipendi kuonekana sana ili nisizoeleke.”


Aunty Lulu yeye alisema: “Mimi nilishabadilika hata kabla ya ishu za madawa ya kulevya ila kwa wale waliokuwa wanategemea wanaume wa madawa ya kulevya ndiyo wana hali mbaya na lazima mwaka huu tuheshimiane.”

Duh..Hii Ni Zaidi ya Hatari..Wataka Watoto wao Wafundishwe Ukatili....!!!

0
0

SERIKALI imeshauriwa kuanzisha mtaala wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kuwafundisha na kuwaandaa wanafunzi na namna ya kukabiliana na kuepukana na vitendo hivyo.

Akizungumza katika mdahalo wa kujadili vitendo vya ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria(WLAC), Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii, Fortunata Mtobi alisema kuingiza unyanyasaji wa kijinsia katika mitaala ya elimu kuanzia kwa watoto wa shule za msingi kutasaidia kujenga jamii yenye usawa na upendo.

Mtobi alisema kwa namna moja ama nyingine ukatili wa kijinsia umekuwa kama tatizo mtambuka kwa sababu unatoka na kurithishana.

“Kama mtoto anazaliwa, anakua anashuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia, baba anampiga mkewe au mtoto wa kike anafanyishwa kazi kuliko mtoto wa kiume, unafikiri akiwa mkubwa na yeye atafanya nini kama si kufuata yale aliyojifunza kutoka kwa waliomtangulia?” Alihoji Mtobi.

“Na ndio maana tunasema kama hakutafanyika jitihada za dhati kutokomeza hili, ikiwamo kuanza kuweka mfumo mzuri, kwa mfano mtaala wa kufundisha watoto kuanzia katika umri mdogo," alisema Mtobi na kufafanua, "itakuwa ni kazi kubwa kulitokomeza.”

Mratibu wa Kampeni ya Kupambana na Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Tunaweza) kutoka WLAC, Abia Richard alisema kwa kutumia pendekezo la Idara ya Ustawi wa Jamii, wasichana ambao ndio waathirika wakubwa na tatizo hilo watakuwa wamesaidiwa kuondolewa katika janga.

Alisema kuanzisha mtaala huo katika shule na vyuo, pia utasaidia wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa wawazi katika kutoa taarifa za vitendo hivyo.

“Pamoja na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na wadau mbalimbali kupambana na suala hilo, ikiwamo kuielimisha jamii namna ya kupambana na tatizo hilo, lakini bado vinaendelea japo kuwa vimepungua tofauti na ilivyo kuwa hapo awali," alisema Richard.

"Tatizo ni kwa sababu wengine wanafundishwa kwamba vitendo hivyo ni vibaya ukubwani wakati katika maisha yao yote katika jamii zao wamekua wakishuhudia vitendo hivyo na ndio maana hata kuacha kwake ni hatua.

“Lakini tunaamini kwamba kama utakuwa ni utaratibu kuwaeleza watoto katika umri mdogo, itazoeleka na jamii itabadilika zaidi.

"Hakutakuwa tena na kusema hiki ni cha mwanamke au hiki ni cha mwanamke, wasichana na wavulana ama wanaume na wanawake wote watakuwa sawa.”

Serikali imetunga sera, sheria, miongozo na kuandaa mikakati mbalimbali katika jitihada za kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia, ikiwemo ukeketaji.

Mikakati hiyo ni pamoja na Sera ya Wanawake na Maendeleo ya Jinsia (2000), Mkakati wa Maendeleo ya Jinsia (2005) na Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008).

Mingine ni Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (1998) na Sheria ya Mtoto (2009), vyote vikiwa na lengo la kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images