Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

Bondi wa Wastara Mbaroni kwa Ujambazi...

$
0
0

TETESI zilizotufikia sasa hivi zinasema Bondi Bin Salim, yule muigizaji wa filamu ambaye pia ni mpenzi wa Wastara Juma, amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na ujambazi. Tunaendelea kufuatilia na tutawajuza kinachoendelea

Maneno ya Profesa J baada ya Kwenda Gereza la Ukonga Alipofungwa Mbunge Lijualikali

$
0
0
January 11 2017 Mbunge wa Jimbo la Kilombero Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Peter Lijualikali alihukumiwa na Mahakama ya wilaya kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini kwa kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

Leo February 19 2017 Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa J amekwenda kumtembelea gerezani Ukonga Dar es salaam na baada ya kutoka hapo akaandika yafuatayo.

‘Nimetoka gereza la Ukonga kumwona Mh. Lijualikali na Patron wa mkoa wa Morogoro kamanda Zinga na wapiga kura wangu watatu kutoka kata ya TINDIGA walifungwa miaka 30, wana afya njema na wanawasalimia sana ila wanalalamika tu hali sio nzuri kabisa kule ndani.. Mungu AWASAIDIE 

Ben Apima Akimbia Majibu ya Ngoma...!!!

$
0
0

MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Abdul Ahmed ‘Ben’ amedaiwa kupima maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ukimwi (Ngoma) na kukimbia akidaiwa kuhofi a majibu.

Chanzo makini kililitonya gazeti hili kuwa muigizaji huyo alionekana kwenye kituo f’lani cha afya maeneo ya Kigogo jijini Dar akipima Ukimwi lakini alipokuwa akisubiri majibu kwenye benchi, ghafl a alitimka na kuondoka eneo hilo.

Alipopigiwa simu na mwanahabari wetu na kuelezwa mchongo mzima, Ben alishtuka na kukiri lakini akadai si kwamba alikimbia bali alipata dharura na atarejea kuyachukua majibu. “Nimepata dharura, pale nitarudi tu kuchukua majibu si kwamba nimekimbia moja kwa moja,” alisema Ben.

Show ya Alikiba South Africa, Iwe Funzo Kwa Wasanii wa Bongo Fleva

$
0
0
Jana nyota wa Tanzania na Mshindi wa MTV EMA african act 2016 Alikiba alianza world Tour yake kwa showJijini Durban South Africa.

Kiwango cha idadi ya watu waliojitokeza na ukumbi aliofanyia show inathibitisha kabisa mziki wa bongo flava bado una safari ndefu kutoboa kimataifa hasa nje ya East Africa.

Collabo ni njia mojawapo ya kutoka kwenye nchi ngumu kama South Africa na Nigeria japo kuna baadhi ya mashabiki wanazibeza.

Sasa kama Alikiba na ukubwa wake huo amepata idadi hiyo ya watu, Billnass, Baraka da Prince au Timbulo atapata watu wangapi? Wakati chipukizi wa Nigeria Tekno akija bongo ndo main Artist.

Jionee picha za jana jijini Durban

Hii Ndio Barua Nzito Aliyoandika Shamsa Ford Kwa Mumewe Ambaye Amehusishwa na Kesi ya Madawa ya Kulevya

$
0
0

Hakika ukipata mwanamke Kama huyu usimuache... Na huu ndio ujumbe wa shamsa kwa mumewe .


Shamsa Ford ameandika Haya:

Nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.

Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..

Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani in shall ah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..

Mwanaume Ukiwa Unafanya Haya Usilalamike Mkeo/Mpenzi Akichepuka

$
0
0
Ikifikia mke kukusaliti kwanza unahitaji kujiuliza kuna tatizo gani mpaka akafikia kukusaliti? Mwanamke anaekupenda sio rahisi kumsaliti ampendae hata akitongozwa na Sharobaro, Mzee Yussuf, Diamond hata Reginal Mengi.

Ikitokea mkeo kakusaliti kuna kitu nyuma ya pazia lako, ingawa wengi wetu tunasema hela na Gari vinawalainisha wanawake. Wengi waliosalitiwa basi hizi ndio kasoro zao:-

1 Kaowa mwanamke wa mtu (mwanamke alikuwa na mpenzi wake lakini jamaa kaingia wakati mwanamke anatamani ndoa)

2 Alikuwa na hela sasa kafulia hana kitu au alijifanya alikuwa na hela lakini baada ya kuowa mke anagutuka mume mchovu.

3 Humtoshelezi kwenye tendo la ndoa( humkojozi) kama umeowa mke ameshawahi kufikishwa kilima cha kilimanjaro pole yako fanya maujuzi umpeleke kilima cha Everest.

4 Ubahili hapa wengi wa wanaume ndio hupigiwa sana wake zao, mke anahitaji matumizi yake binafsi sio kula na kulala tu au kumnunulia madira na chocolate za kichina. kuna matozi wanahonga mpaka malaki na milioni halafu unawacha hela ya ugali unapikiwa pilau ukimaliza kula unakwenda kulala, bwege kama wewe lazima uchapiwe dadeki zako.

5 Huna muda wa maongezi na mkeo hujui hata nini anapenda,nini leo kimemkuta,wala huna future plan kwenye familia wewe ukali,mpira,vijiwe,kazi na marafiki tuu wakati rafiki yako wa kweli(mkeo) huna muda wa maongezi nae.

6 Kuwaachia marafiki kuzoweana sana na shemegi yao, sio kama vibaya kutaniana na shemegi yao lakini kuna mataani mengine hupitiliza. utakuta mpaka baadhi ya rafiki wanampigia simu shemegi yao wanaongea kwa masaa na vicheke kibao.

7 Kujifanya mkali kila wakati wewe uso umeukunja kama ngozi za pumb..u hujulikani kijana au mzee hujulikani leo umefurahi au umenuna. Tokea umuowe mkeo hujawahi kumtania hata siku moja.

8 Kuchepuka kuna baadhi ya wanaume walioowa nishawahi kuwauliza kwanini wanachepuka jibu lao kubwa wanasema hawajui. HUbaki kumalizia kusema eti hawa wanawake watakuwa na sumaku

Kuna baadhi ya mambo husababisha sisi wenyewe wake zetu kufikia kuchukua uamuzi wa kutusaliti, Kama ukali unafanya kazi mbona simba na ukali wake lakini kazungukwa na mabebez kibao

Jokate Akutana na Beyonce, Jay Z na Blue Ivy Kwenye NBA All-Star Game

$
0
0
Kukutana na Jay Z na Beyonce ni suala gumu, kukutana nao na ukashikana nao mikono na kuzungumza mawili matatu nao ni suala gumu zaidi. Lakini bahati hiyo ya mtende imeamuangukia mrembo wa Tanzania, Jokate Mwegelo Jumapili hii.


Siamini: Jokate Mwegelo akisalimia na Jay Z huku mtoto wake, Blue Ivy akiamtazama kwa makini. Pembeni yao ni Queen Bey

Jojo amefanikiwa kukutana na The Carters wakiwa na mtoto wao, Blue Ivy kwenye mchezo wa NBA All-Star Game uliofanyika Jumapili mjini New Orleans, Louisiana kwenye uwanja wa Smoothie King Center.

“So NBA Africa took me courtside and I haaaaaaad to say hello to the Carters,” ameandika Jokate.

“OMG 😭😭😭😭. @beyonce is super cute and I can’t believe she shook my hand and was like nice to meet you. 😍😍🤗🤗. I was like wait I need a picture, I came all the way from Tanzania for this B 😕. She’s so sweeeeeet and I’m so lucky lmao,” ameongeza.

“Thank you @beylite @balleralert for this pic I couldn’t snap one as I was shocked and still in disbelief. 😳 #Beyonce #Beylite #NBAAfricaGame #NBAAllStar

Bongo5

Noma Sanaa..Uhaba wa Madawa ya Kulevya Mitaani Wapelekea Mateja Kuhamia Kwenye Ugoro..!!!!

$
0
0


VITA ya kupambana na dawa za kulevya ikiwa imeshika kasi nchini na kusababisha kupungua kwa mihadarati sokoni baada ya wafanyabiashara hiyo kuhofia kukamatwa, watumiaji 'mateja' wameibuka na vilevi mbadala.


Uchunguzi  umegundua kuwa 'mateja' ambao bado wapo mitaani baada ya watumiaji wengi kuonekana kukimbilia katika nyumba za matibabu, wamelazimika kutumia vileo mbadala ili kukidhi haja ya miili yao.

Uchunguzi katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambayo huwapo watumiaji wengi wa dawa za kulevya, umebaini kuwa 'mateja' wamehamia kwenye vileo kama mafuta ya petrol, ugoro na gundi ya viatu baada ya kukosa dawa za kulevya.

Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini ambayo imepata msukumo mpya tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ataje watu 65 waliotakiwa kuisaidia polisi kuhusu biashara ya mihadarati wiki mbili zilizopita, ilipata nguvu zaidi wiki iliyopita kutoka kwa IGP, Ernest Mangu.


Tembelea Tovuti Pendwa ya ASILI ZETU inayohusiana na Masuala ya Tiba Asilia Kama Kusafisha Nyota na Kumvuta Mpenzi

$
0
0
Tembelea  tovuti  pendwa  ya ASILI ZETUinayohusiana na masuala ya tiba asilia, kusomewa dua na visomo, kusafisha nyota,  kumvuta mume au mpenzi aliyekuacha, tiba ya magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana,  mvuto wa biashara.

Pia tunatoa dawa za uzazi kwa wale kina mama wenye matatizo ya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote, kupandishwa cheo kazini, mali isiyohuzika kama vile kiwanja, shamba, nyumba, gari n,k.

Bonyeza Hapa: https://asilizetu.wordpress.com

Wanasheria wa CHADEMA Wamtaka Mbowe Asijisalimishe Polisi

$
0
0
Wanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamesema wamemshauri Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe, asiende kuripoti polisi leo.

Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, amesema Mbowe hatakwenda kuripoti polisi leo kwa sababu amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na inaanza kusikilizwa Februari 21 mwaka huu.

“Mbowe haendi polisi, tumemshauri asiende kwa sababu kesi yake inaanza kusikilizwa Jumanne (kesho).

“Kama wanamhitaji, waje keshokutwa (kesho) Mahakama Kuu, watampata hapo,”alisema Mallya.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema yuko Mwanza na hajawasiliana na Mbowe.

“Hapa niko Mwanza sijawasiliana na mwenyekiti, lakini kama nikiwasiliana naye, nitamshauri asiende huko polisi.

“Kwa hiyo, naweza kusema kilichofanywa na Kamishna Sirro si wito wa kipolisi bali ni siasa kama ambavyo alifanya Makonda kwa kutangaza majina ya watu hadharani.

“Wito wa polisi huwa ni wa kimaandishi, hawajamwandikia barua, hawajampigia simu.

“Hawa maafande wana namba zetu za simu sisi kama mawakili wa chama, kama wanamhitaji Mbowe kwanini wasitupigie simu mpaka watangaze kwenye vyombo vya habari,”alihoji Lissu.

Alipoulizwa kama Mbowe atakamatwa wakati wowote kuanzia sasa, Lissu alisema watalazimika kulishtaki mahakamani Jeshi la Polisi kwa kitendo hicho.

“Hatuwezi kukubali utaratibu huu, waache kufanya siasa, wakimhitaji mwenyekiti wetu wamwandikie barua,”alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitaja majina 65 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya akiwamo Mbowe.

Pamoja na kutaja majina hayo, Makonda aliwaagiza watuhumiwa hao kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa dhidi ya tuhuma hizo.

Februari 10 mwaka huu, akiwa mjini Dodoma, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alizungumza na waandishi wa habari na kusema hajawahi kujihusisha kwa namna yoyote na biashara ya dawa za kulevya na pia hatakwenda polisi kuhojiwa kama alivyoagizwa na Makonda.

Hata hivyo, alisema atakwenda polisi, kama jeshi hilo litafuata taratibu za kumuita kwa mujibu wa sheria.

“Siwezi kwenda polisi kwa wito wa Makonda kwa sababu hana mamlaka hiyo kisheria. Kama polisi wananihitaji, waniite kwa kufuata utaratibu, nitakwenda kwa sababu mimi siogopi kwenda polisi,”alisema Mbowe.

Wakati Mbowe akisema hayo, juzi Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema Jeshi la Polisi linamtafuta Mbowe na kwamba limeshindwa kumpata kwa sababu amezima simu.

Kutokana na hali hiyo, Kamanda Sirro alitoa saa 48 kwa Mbowe kuripoti polisi na endapo hatafanya hivyo atatafutwa kwa namna ambayo jeshi hilo litaona inafaa.

 “Jumatatu (leo) asiporipoti kutakuwa hakuna namna ya kulizuia tena Jeshi la Polisi kutafuta namna ya kumhoji.

 “Mbaya zaidi juzi tumejitahidi kumtafuta hapatikani, tulikwenda nyumbani kwake hakupatikana, tulikwenda mahali anakoishi sasa, pia hakupatikana,”alisema Sirro

Jumuiya ya Kiisilamu yataka MATEJA Wote washtakiwe na Pia Mali za Paul Makonda Zichunguzwe

$
0
0
Jumuiya  na Taasisi za Kiislamu nchini imevitaka vyombo vya kisheria na uchunguzi kuacha kupuuza kauli zilizotolewa na wabunge zilizomtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumiliki mali zisizoendana na kipato chake halali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa Jumuiya hiyo Sheikh Rajabu Katimba, alisema wakati wa mkutano wa Bunge lililopita baadhi ya wabunge walimtuhumu Makonda hivyo tuhuma hizo zinapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

Alisema vyombo vyenye mamlaka ya uchunguzi vinapaswa  kufanya uhakiki wa mali za Makonda ili kuondoa shaka katika umiliki wa mali aliyonayo na uhalali wa misaada ya kifedha zinazotolewa kwake na taasisi rafiki.

Sheikh Katimba alisema kifungu cha (11) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma inamtaka kiongozi kutaja hadharani mali zake ikiwemo zawadi anazopewa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) wakati akichangia taarifa za Kamati ya Bunge na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alisema Makonda amenunua jengo ‘(Apartment ) lenye thamani ya shilingi mil 600 jijini Dar es  Salaam.

Selesini aliliambia Bunge kuwa Makonda amempa gari mkewe aina ya Mercedez Benzi lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh milioni 550.

Mbali na Selesini, Mbunge mwingine aliyemtuhumu Makonda kujilimbikizia mali ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) ambaye naye wakati akizungumza bungeni alihoji ni wapi  Makonda alipata fedha za kusafiri kwenye ndege  daraja la juu kwenda Marekani.

Wakati huo huo, Sheikh Katimba alisema vita dhidi ya dawa za kulevya inaweza kwenda vibaya iwapo itasimamiwa na wanasiasa.

Alisema ili kuepuka hilo vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kisheria vinapaswa kuifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.

Sheikh Katimba alisema taasisi za kiislamu zinaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kupambana na biashara hiyo na kusisitiza kuwa vyombo vyenye mamlaka kuisimamia kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya nchini ya mwaka 2014.

‘’Hatuoni ni kwa mantiki ipi watumiaji wengine washitakiwe kwa kutumia dawa na wengine waachiwe huku zitumike na fedha za kuwatibia nje ya nchi.

‘’Wasanii kama Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C’  msanii TID nao pia walipaswa kushitakiwa kama walivyofanywa wengine na vilevile watumiaji walioko mitaani na kwenye vituo vya daladala wote wasombwe wakapimwe na kisha washitakiwe.

“Pamoja na nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuongoza na kuendesha vita hiyo lakini vita isimamiwe na vyombo vyenye weledi na si wateule wa kisiasa au wanasiasa,’’ alisema.

Aidha, alizungumza kesi za ugaidi inawakabili baadhi ya viongozi wa dini kwa kueleza kuwa haitakuwa na tija wala heshima iwapo viongozi  hao wataendelea kushikiliwa gerezani.

“Ni kweli serikali inatutaka tuiunge mkono kwenye vita hiyo nasi tuko tayari lakini ni vuziri jitihada hii ikawa kwa watu wote, tunaiona serikali inashindwa kutenda haki kwa viongozi wa dini yetu na ni kesi gani isiyokwisha? inatia aibu masheikh kufungwa bila hatia miaka mitatu ni sawa na kufungwa bila hatia,’’ alisema Sheikh Katimba.

Mzee wa Upako Afunguka Kuhusu yeye Kunywa Pombe.....Atangaza Maamuzi Mapya Kwa Waandishi Aliowatabiria Kifo.

$
0
0
Mchungaji Anthony Lusekelo amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kunywa pombe, na kuweka wazi kuwa hanywi pombe bali anakunywa 'wine' isiyo na kilevi, huku akisita kusema endapo unywaji pombe ni dhambi au siyo dhambi.

Amefunguka hilo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, na kuweka wazi kuwa wanaomtuhumu kuwa yeye anakunywa pombe wanapaswa kutoa ushahidi juu ya tuhuma hizo, na kwamba unywaji pombe unaweza kuwa dhambi ama usiwe dhambi kulingana na imani na dini ya mtu.

"Hao wanaotuhumu kuwa nakunywa pombe, waeleze ni pombe gani nakunywa, nilikuwa nakuywa wapi na aliyeniona ni nani... kuna sehemu nyingine pombe siyo dhambi, dini nyingine mpaka kanisani kuna bar".

Je, kunywa bia kiasi bila kulewa ni dhambi au siyo dhambi?

Hilo ni swali lingine alilokutana nalo kuhusu unywaji Pombe, ambapo katika majibu yake amesema hawezi kusema kama ni dhambi au lah, maana inategemea na imani ya mtu, huku akiongeza kuwa Bibilia haijazuia unywaji pombe

"Inategemea na makanisa, kuna mengine hata kunywa soda ni dhambi. Dhambi ni makubaliano yenu kwenye dini yenu. Bibilia inasema kula kitu chochote hata chakula kama ukila kupitiliza ni dhambi, hata unywaji wa pombe ukinywa ukapitiliza ni dhambi. Biliblia haijaandika moja kwa moja kwamba msinywe pombe, imesema msilewe kwa kuwa ndani ya ulevi kuna ufisadi, cha msingi mbadilishe ulevi wenu uwe ni roho mtakatifu"

Ikumbukwe kuwa sekeseke lililosababisha Mzee wa upako adaiwe kunywa pombe, lilihusisha kurushiana maneno na jirani zake ambapo baada ya hapo vyombo vya habari hasa magazeti yaliripoti tukio hilo kwa namna ambayo Mzee wa Upako hakuipenda, na hata kufikia hatua ya kuwatabiria kifo waandishi walioandika habari hiyo.

Alipoulizwa kuhusiana na ahadi yake hiyo ya kuwatabiria vifo, alisema kuwa tayari amewasamehe ingawa uwezo wa kuwaombea kifo anao.

"Tulisema hatuwezi kutumia nguvu kubwa sana kuwaombea watu kifo, kwa sababu sisi ni wanadamu, na wanadamu tuna mapungufu kwahiyo nikaona ni bora kumuachia Mungu. Uwezo huo wa kuwaombea watu wakafa, mimi ninao, lakini nikaona inasaidia nini mtu kumuombea mabaya, kwahiyo nikaamua kusamehe"

Baadhi ya watu walitaka kujua ni kwanini haendi kuombea wagonjwa hospitalini ili wapone, ambapo alijibu kuwa maombi hufanywa katika mazingira maalum, na kwamba hospitali kila mgonjwa ana imani yake.

"Maombi lazima kuandaa mazingira, na sehemu ambayo Mungu amesema tukutane ni kanisani, ndiyo maana hata wakati wa Yesu wagonjwa ndiyo walimfuata Yesu, siyo Yesu aliwafuata wagonjwa.. Kinachoponya ni imani ya mtu, pale hospitali kila mtu ana imani yake, wakati mwingine hata kumuombea mtu inabidi umuombe kwanza maana wengine hawapendi kuombewa"

Clouds Media Wayachukua Masafa ya BBC ya Dar Es Salaam,Kusaga Akitangaza Ujio wa Redio Mpya ..!!!

$
0
0

Station mpya ya redio imetua jijini Dar es Salaam. Inapatikana kwenye masafa ya 103.3 (zamani yalikuwa yakitumiwa na BBC).

Kwa mujibu wa poster iliyowekwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, station hiyo inaonekana kuwa ya muziki peke yake na tayari imepewa sifa za kuwa ‘Africa’s Number 1 Hits Station.’ Ni wazi kuwa inamilikiwa na kampuni hiyo ambayo hadi sasa ina redio mbili, Clouds FM na Choice FM. Bado haijajulikana itatumia jina gani.

Kwa sasa inapiga muziki peke yake.

Njaa Kali ..Askari Magereza Feki Akamatwa Akiwa na Sare za Polisi Anazozitumia Kuwatishia Watu na Kupanda Nazo Daladala Ili Asilipe Nauli..!!

$
0
0

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata askari feki wa Jeshi la Magereza, Elius Msigwa akiwa amevaa sare za jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alimtaja kama Elius Msigwa aliyekuwa akiwababaisha wananchi wa maeneo ya Kivule anakoishi, alifukuzwa kazi tangu Disemba mwaka jana.

Alisema wakati mtuhumiwa huyo anafukuzwa ndani ya jeshi hilo, alikuwa na cheo cha Koplo, lakini alipokamatwa alikuwa amevaa cheo cha Sajenti na alikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa nia ya kuomba radhi, kijana huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika gereza la Keko, alisema “Bahati mbaya siku ya juzi sikuwa na nauli ya kwenda mjini ndio nikavaa hizi ‘uniform’ (sare). Nilikuwa nawaomba vijana wenzangu hata kama umeacha kazi, umefukuzwa au chochote, msivae ‘uniform’ na baada ya kutoka hapa nazirudisha hizi uniform katika kituo changu kilichokuwa cha kazi,” alisema Msingwa.

Kamishina Sirro pia alisema jeshi hilo lilikamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi katika maeneo ya Kivule, Ukonga wakijihusisha na wizi wa kutumia silaha aina ya mapanga, kuvuta bangi na kunywa gongo.

Huyu Ndiye Trump Bana..Amtumbua Jipu Amshauri Wake wa Karibu Baada ya Kuukosoa Utawala Wake Hadharani..!!!

$
0
0

Mshauri mkuu wa baraza la usalama la taifa la Marekani, amerudishwa kwenye kazi yake ya awali baada ya kukosoa sera za utawala wa Donald Trump zinazohusiana na Latin America.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders, amesema Craig Deare ameondolewa kwenye nafasi hiyo. Deare alidaiwa kuponda jinsi uongozi wa Trump unavyoshughulika na masuala ya Latin America alipokuwa akizungumza huko Washington.

Hii si mara ya kwanza kiongozi wa juu anatumuliwa kwa kumkosoa Trump.

Mbasha, Miss TZ Mapenzi Mubashara...!!!!!

$
0
0

Baada ya kuficha uhusiano wao, Mwimbaji wa Gospo Bongo, Emmanuel Mbasha na Mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa, sasa siyo siri tena kwani Wikienda lina picha zao mubashara wakiwa kwenye mahaba niue. Mtu aliyevujisha picha hizo, aliliambia Wikienda kuwa, Mbasha na Jack kwa sasa hawajifichi tena kwani wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali kama kanisani, sehemu za starehe na hivi karibuni walikuwa wakijiachia Siku ya Wapendanao huku wakiwa kwenye mavazi rasmi ya wapenzi.

“Naona wameamua kuweka mambo mubashara kabisa kwa sababu Mbasha ameshasarenda kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha maana sasa ni malavu kwa kwenda mbele. Ukikutana nao hata hawajifichi baada ya Wikienda kuwaweka hewani,”

kilimwaga ubuyu chanzo chetu. Baada ya kupata ubuyu na picha hizo kutoka kwa sosi, mwanahabari wetu alimwendea hewani Jack ambaye muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania mkoani Kilimanjaro ambapo alifunguka kuwa, hapendi kuzungumzia kiundani mambo yake ya uhusiano lakini anachojua ni kwamba, yeye na Mbasha ni marafiki na muda ukifika, kama kuna kinachoendelea ataweka wazi kila kitu. “Muda ukifika nitaweka wazi kila kitu kama kuna mambo ya ndoa na uchumba, wala msiwe na wasiwasi ninyi mtaona tu, suala hilo huwa halina kificho,” alisema Jack kwa bashasha.

Alipotafutwa Mbasha simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na kwamba ulionesha kupokelewa. Wiki mbili zilizopita, Wikienda ndilo lilikuwa la kwanza kuripoti juu ya uhusiano wa Mbasha na Jack huku wawili hao wakija juu lakini sasa mapenzi yao siyo siri tena.

Pamoja na Kuwa Mgonjwa,Wanachama NCCR -Mageuzi Wamtaka Mbatia Ajiuzulu,Wadai Ni Fisadi Mkubwa Ndani ya Chama Hicho...!!!!!

$
0
0

BAADHI ya wanachama wa NCCR-Mageuzi wamemtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na Katibu Mkuu wa chama hicho, Martin Danda kujiuzulu ndani ya siku tatu kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwamo ubadhirifu wa fedha na kutaka kukiua chama hicho.

Mbatia anadaiwa kuuza mali za chama zikiwamo nyumba mbili zilizoko jijini Dar es Salaam eneo la Bunju B, moja iliyoko Tarime mkoani Mara na shamba la ekari 56 lililoko Bagamoyo mkoani Pwani.

Faustine Sungura mmoja wa wanachama wa chama hicho, amesema mbali na kuuza nyumba pia Mbatia ana mkakati maalumu wa kuiua NCCR na kuhamia Chadema ambako ameahidiwa ukatibu Mkuu.

“Hivi sasa kuna mkakati wa kuuza nyumba nyingine za chama zilizopo mkoani Rukwa na Katavi na mauzo yatakabidhiwa kwake kwa madai kuwa anakidai chama fedha alizokikopesha wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, tunatoa tahadhari kwa watu kutonunua nyumba hizo kwani watapata hasara isiyotibika,” alisema.

Pamoja na mambo mengine Sungura amesema viongozi hao wasipojiuzulu atawafungulia mashtaka mahakamani.

Pamoja na Ahadi ya Kuwajengea Makoa Makuu,Waislamu Wamgeuka Makonda,Wataka Akamatawe Haraka na Polisi Ili Achunguzwe Kama Anauhusika na Madawa ya Kulevya..!!

$
0
0

JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu nchini imevitaka vyombo vya kisheria na uchunguzi kuacha kupuuza kauli zilizotolewa na wabunge zilizomtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumiliki mali zisizoendana na kipato chake halali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa Jumuiya hiyo Sheikh Rajabu Katimba, alisema wakati wa mkutano wa Bunge lililopita baadhi ya wabunge walimtuhumu Makonda hivyo tuhuma hizo zinapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

Alisema vyombo vyenye mamlaka ya uchunguzi vinapaswa  kufanya uhakiki wa mali za Makonda ili kuondoa shaka katika umiliki wa mali aliyonayo na uhalali wa misaada ya kifedha zinazotolewa kwake na taasisi rafiki.

Sheikh Katimba alisema kifungu cha (11) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma inamtaka kiongozi kutaja hadharani mali zake ikiwemo zawadi anazopewa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) wakati akichangia taarifa za Kamati ya Bunge na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alisema Makonda amenunua jengo ‘(Apartment ) lenye thamani ya shilingi mil 600 jijini Dar es  Salaam.

Selesini aliliambia Bunge kuwa Makonda amempa gari mkewe aina ya Mercedez Benzi lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh milioni 550.

Mbali na Selesini, Mbunge mwingine aliyemtuhumu Makonda kujilimbikizia mali ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) ambaye naye wakati akizungumza bungeni alihoji ni wapi  Makonda alipata fedha za kusafiri kwenye ndege  daraja la juu kwenda Marekani.

Wakati huo huo, Sheikh Katimba alisema vita dhidi ya dawa za kulevya inaweza kwenda vibaya iwapo itasimamiwa na wanasiasa.

Alisema ili kuepuka hilo vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kisheria vinapaswa kuifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.

Sheikh Katimba alisema taasisi za kiislamu zinaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kupambana na biashara hiyo na kusisitiza kuwa vyombo vyenye mamlaka kuisimamia kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya nchini ya mwaka 2014.

‘’Hatuoni ni kwa mantiki ipi watumiaji wengine washitakiwe kwa kutumia dawa na wengine waachiwe huku zitumike na fedha za kuwatibia nje ya nchi.

‘’Wasanii kama Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C’  msanii TID nao pia walipaswa kushitakiwa kama walivyofanywa wengine na vilevile watumiaji walioko mitaani na kwenye vituo vya daladala wote wasombwe wakapimwe na kisha washitakiwe.

“Pamoja na nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuongoza na kuendesha vita hiyo lakini vita isimamiwe na vyombo vyenye weledi na si wateule wa kisiasa au wanasiasa,’’ alisema.

Aidha, alizungumza kesi za ugaidi inawakabili baadhi ya viongozi wa dini kwa kueleza kuwa haitakuwa na tija wala heshima iwapo viongozi  hao wataendelea kushikiliwa gerezani.

“Ni kweli serikali inatutaka tuiunge mkono kwenye vita hiyo nasi tuko tayari lakini ni vuziri jitihada hii ikawa kwa watu wote, tunaiona serikali inashindwa kutenda haki kwa viongozi wa dini yetu na ni kesi gani isiyokwisha? inatia aibu masheikh kufungwa bila hatia miaka mitatu ni sawa na kufungwa bila hatia,’’ alisema Sheikh Katimba.

Suala la Mo Dewji Kukabidhiwa Simba Lafikia Hatua Hii...!!!

$
0
0

SUALA la mfanyabiashara maarufu ndani na nje ya nchi, Mohamed Dewji (Mo), kukabidhiwa Simba limefikia patamu baada ya viongozi wa matawi kuutaka uongozi kupeleka mapendekezo ya mchakato huo baraza la wadhamini la klabu hiyo haraka ili mpango huo ukamilike.

Mo alishaweka wazi kuwa anataka kuweka hisa ya asilimia 51 na kilichobaki ni mchakato wa kubadili katiba ili zoezi hilo likamilike kwa muda mwafaka.

Kutokana na umuhimu wa mabadiliko hayo, hivi karibuni uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi ulikutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuangalia namna ya kumaliza jambo hilo haraka iwezekanavyo.

Rais wa Simba, Evans Aveva, juzi alikutana na viongozi wa matawi wa Dar es Salaam, ambapo suala kubwa walilolizungumza ni namna ya kuwafunga Yanga Februari 25, mwaka huu lakini suala la Mo nalo likajitokeza, ambapo viongozi hao wakitaka kujua kinachoendelea.

Licha ya wajumbe waliokaa katika kikao hicho hawakutaka kuweka wazi mambo waliyoyajadili, lakini  kuhusu suala hilo la Mo, viongozi hao wa matawi walimbana Aveva na mwisho wakakubaliana kuwa uongozi upeleke mapendekezo ya mchakato katika baraza la wazee ili wakae na wanasheria wao kujadili suala hilo waone kama litakuwa na faida kwa klabu.

“Hakuna anayekataa mabadiliko, lakini lazima Wanasimba wote kwa kauli moja tukubaliane, hatutaki mtu anung’unike ndiyo maana tumeshauriana na uongozi wakutane na baraza la wazee ili jambo hili tulimalize vema,” alisema mmoja wa waliohudhuria kikao hicho.

Jeshi la Polisi Limemtia Mbaroni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

$
0
0

Jeshi la Polisi limemtia mbaroni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na anapelekwa Kituo Kikuu(Central) cha Polisi jijini Dar.

Siku ya Jumamosi Kamanda Simon Sirro alimpa kiongozi huyo muda wa saa 48 za kujisalimisha vinginevyo watamtafuta kwa njia wanazozijua wao.
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live




Latest Images