Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Mada ya Leo ..Je..Ngono Ndiyo Silaha ya Mapenzi?...!!!

$
0
0

KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii ya mahusiano ambayo huwajia kila Jumanne na Jumamosi, ikilenga kufahamishana hili au lile kuhusiana na mambo ya mapenzi, wengine wakiita mahaba.

 nigeukie mada ya leo ambayo inajadili suala zima la uhusiano baina ya ngono na mapenzi ambayo ilianzia Jumamosi iliyopita.

Leo nimewaletea maoni ya wasomaji wangu kuhusiana na mada hiyo kama ifuatavyo:

 Juliana  Mgulu wa Same, Kilimanjaro:  Kwa upande wangu, siamini kuwa ngono ni silaha ya mapenzi na kamwe sitaamini kwasababu  muhimu mi naelewa ilo tendo la ndoa si tendo la wachumba, mi nimesimama katika imani na mbona niko katika mahusiano muda mrefu na ninafurahia uhusiano wangu.

Rama wa Kimara kwa Komba, Dar es Salaam: Kwangu ngono ndoyo silaha ya mapenzi.

Doa Vitras wa Dar es Salaam: Unaweza ukawa na mwenzio na msifanye ngono na mambo yakawa sawa, siku zote ngono ni haja ya kimwili na si ugonjwa ukamfanya mtu akafa, mapenzi ni hisia na si matamanio ya mwili.

Mujuni wa Ubungo, Dar es Salaam: Kama mnapendana kwa dhati, tendo la ngono lazima ndio kiunganishi.

Nuru Shariff wa Tabata Matumbi, Dar es Salaam: Ngoni sio silaha ya kukupenda mtu. Hisia za mtu anayekupenda utazijua kwa vitendo vyake na si tabia. Ngono si mapenzi, wangapi wapo kwenye madanguro na kujirusha na watu, ina maana wanawapenda?

Bakari wa Kondoa: Ngono ni tendo lakini mapenzi ni zaidi ya ngono, kama wawili wana mapenzi toka moyoni, ngono si lolote si chochote. Ngoni ni sawa na kiu ya maji, ukinywa tu basi inakatika. Mapenzi ni mwili na roho.

Raymond Matenga: Kuwa na mwanamke au mpenzi anayekukatalia kufanya tendo la ngono eti mpaka muoane ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege.

Maleck wa Sinza, Dar es Salaam: Mtu mwenye mapenzi ya kweli atakuwa tayari kwa chochote kwa mwenza wake kama anakuwa hataki, basi ujue anaye wake sio wewe. Ukiangalia hali ya sasa huwezi ukawa unamuhudumia mwenzio halafu haja zako hakutimizii, huyo hakufai.

Atambue kuwa manjonjo yake na mahaba atakayonifanyia tukiwa faragha, ndio zitanifanya name ninogewe nimng’ang’anie. Sasa kama hataki nitajuaje kuwa ni mwanamke aliyekamilika? Au atanijuaje kuwa mume aliyenaye yupo sawa? Aliye na malengo nawe  atakufanyia utakavyomuomba.

Tatizo la madada zetu wa siku hizi wana tamaa sana, pesa mbele kuliko utu ndio maana kuna anayemfaidisha kimwili na wengine wa kuwachuna. Hata mimi nimeachana na mwenzangu kwa jambo hilo, hataki kukutana na mimi kila muda ni mtu ambaye hana muda, siwezi kutoka.

 By Lydia wa Same, Kilimanjaro: Ngono sio silaha ya mapenzi kinachotakiwa ni upendo wa dhati, kama mtu hujampenda kutoka moyoni ni bora ukamwambia kuliko kumpotezea muda.

Baba Rooney wa Mbalizi Mbeya: Si kweli kuwa mpenzi ambaye hakupi mapenzi ndio hana mapenzi na wewe. Mbona wapo ambao anakupa mapenzi lakini hana maepnzi na wewe?

Sylvia Lucas wa Maduka Tisa, Mwanza: Ni kweli mtu akikataa kukutana kimwili huyo hakupendi, yupo anayempenda anakupotezea muda tu.

Athanas K wa Mbande, Dodoma: Ngono ni silaha kubwa katika mahusiano na ndio msingi wa halisi wa mapenzi kwa wawili waliokubaliana.

Wewe unamoani gani?tafadhali tuandikie hapo chini ,zingatia lugha nzuri

Makonda na Sirro Wakataa Wito wa Kufika Mahakamani..!!!

$
0
0

HATUA ya kutaja hadharani majina ya watu wanaodaiwa kutumia na kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, imechukua sura mpya baada ya Mahakama Kuu nchini kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro.

Mwingine aliyetakiwa kufika mahakamani hapo leo ni Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO) Kamilius Wambura, huku taarifa zikibainisha kwamba viongozi hao wamepelekewa mwito wa kufika mahakamani hapo kutokana na kesi yaKikatiba iliyofunguliwa dhidi yao na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Kesi hiyo ya Mbowe ni namba moja ya mwaka 2017, imepangwa kutajwa leo, ambapo pamoja na mambo mengine anapinga mamlaka ya Makonda kumkamata na kudhalilisha watu.

Katika kesi hiyo Mbowe anaiomba Mahakama itamke kuwa vifungu vya Sheria ya Tawala za Mikoa vinavyowapa mamlaka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwakamata watu na kuwatia mbaroni, viko kinyume cha Katiba.

Jopo la majaji watatu litasikiliza kesi hiyo akiwamo, Sekieti Kihiyo (Mwenyekiti wa jopo), Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Kaday.

Hata hivyo taarifa zaidi zinaeleza kuwa mwito huo wa Mahakama haukupokelewa na Makonda wala Wambura, ikielezwa hawakuwepo ofisini na wasaidizi wao walikataa kusaini ili kuzipokea huku Kamanda Siro akidaiwa kukataa kupokea mwito huo.

Ofisa wa mahakama aliyepeleka mwito huo, Yusuph Juma, baada ya kuelekezwa na Kamanda Sirro kuwa ampelekee mwito huo Wambura, alipokwenda kwa Wambura, hakumkuta.

Kwenye hati hiyo ya mwito kwenda kwa Kamanda Siro, Juma aliandika: “Kwa hiyo wito haujapokelewa.”

Katika hatua nyingine jana Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alifungua maombi mengine mahakamani hapo akipinga kusudio la Kamanda Siro la kumkamata kama hatajisalimisha katika kituo cha Polisi kwa mahijiano.

Katika maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017, Mbowe anaiomba Mahakama iwazuie wadaiwa kutekeleza azma yake ya kumtia mbaroni pamoja na mambo mengine akidai kuwa kuna kesi ya kikatiba ambayo tayari ameifungua mahakani hapo.

Hivyo aliiomba Mahakama itoe amri ya kuwazuia kumkamata hadi hapo kesi hiyo ya kikatiba itakapomalizika na kwamba Mahakama Kuu imwachie na Polisi wasiendelee na mchakato wowote dhidi yake hadi hapo kesi hiyo itakapomalizika.

Katika kesi ya msingi ya Kikatiba, Mbowe anapinga kitendo cha Polisi kumtaka afike kituoni kwa madai kuwa ni utekelezaji wa amri ya Mkuu wa Mkoa.

Alidai kuwa sheria inayompa Mkuu wa Mkoa mamlaka ya kutoa amri ya kumkamata na kumweka ndani mtu, yako kinyume cha Katiba kwa madai kuwa ilitungwa katika mazingira ambayo hapakuwa na vituo vya Polisi vya kutosha.

Hivyo alidai kuwa kwa mazingira ya sasa sheria hiyo imeshapitwa na wakati na anaiomba Mahakama itamke kuwa ni kinyume cha Katiba.

Hata hivyo alisema kuwa hata kama Mkuu wa Mkoa alikuwa anatekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa sheria hiyo, basi hakutimiza matakwa ya kisheria, ambayo ni pamoja na kutoa taarifa kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi.

Hivyo aliiomba Mahakama kama itaona kuwa Mkuu wa Mkoa alikuwa sawa kutoa amri hiyo, basi imwamuru afuate matakwa ya kisheria, ikiawa ni pamoja na kulinda haki za binadamu katika kutekeleza madaraka yake hayo.

Rais Mugabe Aongoza List ya Marais Wenye Umri Mkubwa Duniani, Atimiza Miaka 93..!!!

$
0
0

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe leo hii anatimiza miaka 93 na kuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi Duniani.

Alizaliwa mnamo mwaka 1924 pia aliwahi kufungwa jela mwaka 1964 na kutoka mwaka 1974 kwa kosa la kutoa hotuba ya kuihujumu Serikali.

Lakini pia Umoja wa Ulaya(EU) umemuongezea muda wa vikwazo Mugabe, yeye pamoja na Mkewe Grace kwa mwaka 1 hadi tarehe 20 Februari mwakani.

Hata hivyo Rais Mugabe amesema kuwa Donald Trump hakuwa chaguo lake upande urais wa Marekani lakini pia hakupenda

Bi. Clinton ashinde kwakuwa angekuja kusimamia na kuviendeleza vikwazo iliyopewa nchi ya Zimbabwe.

Mzee wa Upako Aichambua Muziki ya Darassa ...!!!

$
0
0

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' ameichambua ngoma wa msanii wa bongo fleva, Darassa inayokwenda kwa jina la Muziki, na kusema kuwa msanii huyo ameimba vitu vya maana sana kwenye ngoma hiyo.

Mchungaji Lusekelo ambaye amewahi kunukuliwa akitumia maneno ya wimbo huo na nyingine kadhaa za bongo fleva katika mahubiri yake, alikumbana na maswali katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, ambapo watu walitaka kujua ni kwanini anatumia muziki wa kidunia katika mahubiri yake, badala ya nyimbo za injili.

Akijibu maswali hayo, Mzee wa Upako amesema yeye kama mwanajamii, anaishi duniani pamoja na wana jamii wengine, hivyo ni lazima ajue matatizo yanayowazunguka watu wake ili aweze kuwasaidia na ndiyo maana anajaribu kufuatilia mambo yanayopendwa na watanzanie ikiwemo muziki wa kidunia.

"Muziki ni muziki, hakuna wa kanisani wala duaniani, cha msingi ni ujumbe tu... Sasa ukisema wacha maneno weka muziki, kuna shida shida gani? Ule muziki mi naupenda sana, anasema hakuna jambo gumu kama kumfundisha chizi, na pia ni ujinga sana kusubiri embe chini ya mnazi. Mimi nina nyimbo nyingi hata za kihindi nasikilizaga sana" Alisema

Mbali na ngoma ya Darassa, pia ametoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya kuimba wimbo wa Navy Kenzo unaokwenda kwa jina la 'Kamatia Chini', huku akishauri wasanii wa bongo fleva kuimba nyimbo zenye mafunzo badala ya nyimbo za mapenzi pekee.

"Wasiimbe nyimbo za mapenzi tu, walipe pia sadaka kwa taifa... wakati mwingine waimbe na nyimbo ambazo zinaasa maadili"

Kuhusu Diamond na Alikiba, Mzee wa Upako amesita kusema ni yupi anayemkubali zaidi, na kusema kuwa wote ni wa Mungu, na vipaji vyao vimetoka kwa Mungu.

Huyu hapa Mzee wa Upako, akiimba ngoma ya Muziki, Kamatia chini, pamoja na nyimbo kadhaa za zamani

Wema Aikataa Rasmi CCM Ajiunga Chadema..!!!

$
0
0

Hatimaye mwana dada Wema Sepenga ameonesha kwa namna moja ama nyingine kuamishia majeshi Chadema mara baada ya kuona huko alikokuwa mwanzoni (CCM)alikuwa hayupo sehemu sahihi 

Hapo mwanzoni zilianza kama tetesi lakini taratibu ukweli wa mambo unaanza kudhihirika siku baada ya siku kuwa Wema si kada tena wa CCM na hivyo basi CCM wamepata pigo kubwa sana kumkosa huyu mtu kwa kuwa anawafuasi wengi saana ambao wapo tayali kumfata kokote kule aendako 

Na kwa kuonesha msisistizo zaidi Wema ameonesha mahaba mazito kwa mheshimiwa Freemaan Mbowe ikiwemo ku like picha zake nyiiingi huko Instagram 


Zitto kabwe: Nimepata Kitu Juu ya Mahakama na Kesi ya Mbowe...!!!!

$
0
0

Nimetambua ( taken note ) uamuzi wa mahakama kuzuia amri ya kukamatwa ya mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA. 

Nimefurahi kuwa Mwanasheria wa Act Wazalendo ndg. Albert Msando ni mmoja wa jopo la wanasheria wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA ndg. Freeman Aikaeli Mbowe.

Mfumo wa Vyama vingi nchini upo hatarini, ni LAZIMA wana mageuzi wote kuweka tofauti pembeni na kupambana kulinda Demokrasia yetu. 

Tukiendekeza tofauti zetu ambazo nyengine ni za kijinga jinga tu, tutakuja shtuka hata hicho kinachotupa tofauti ( vyama ) hakipo.

Ray C Akumbana na 'Majanga' Mengine...Lebo Yamtupia Virago Vyake

$
0
0
Msanii wa bongo fleva Ray C amefukuzwa kwenye lebo ya wanene Enterteiment baada ya kauli ya yake aliyodai  kwamba hajasaini na lebo yeyote.


Akionge kupitia eNewz ya EATV, Maneja wa Wanene Enteriment Gentris amesema kuwa Ray C alikuwa kwenye hatua za mwisho kuweza kusajiliwa katika lebo ya Wanene ila alikosea baada ya kupewa demo ya nyimbo yake ambayo ilikuwa haijawa tayari na kuivujisha hali iliyopelekea uongozi wa wanene kukasirika na kuamua kumtimua.

Hata hivyo Ray C alivyoongea kupitia eNewz alisema sababu iliyopelekea yeye kufanya kazi na wanene ni baada ya kupewa ofa ya kurekodi na lebo hiyo ya Wanene hali iliyompelekea kushindwa kukataa kwa kuwa wanene ni lebo kubwa na yenye vyombo vya kisasa zaidi.
Itazame hapa....

Mzee wa Upako Aichambua Muziki ya Darassa, Aulizwa Kuhusu Ali Kiba na Diamond

$
0
0
Mchungaji Lusekelo ambaye amewahi kunukuliwa akitumia maneno ya wimbo huo na nyingine kadhaa za bongo fleva katika mahubiri yake, alikumbana na maswali katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, ambapo watu walitaka kujua ni kwanini anatumia muziki wa kidunia katika mahubiri yake, badala ya nyimbo za injili.

Akijibu maswali hayo, Mzee wa Upako amesema yeye kama mwanajamii, anaishi duniani pamoja na wana jamii wengine, hivyo ni lazima ajue matatizo yanayowazunguka watu wake ili aweze kuwasaidia na ndiyo maana anajaribu kufuatilia mambo yanayopendwa na watanzanie ikiwemo muziki wa kidunia.

"Muziki ni muziki, hakuna wa kanisani wala duaniani, cha msingi ni ujumbe tu... Sasa ukisema wacha maneno weka muziki, kuna shida shida gani? Ule muziki mi naupenda sana, anasema hakuna jambo gumu kama kumfundisha chizi, na pia ni ujinga sana kusubiri embe chini ya mnazi. Mimi nina nyimbo nyingi hata za kihindi nasikilizaga sana" Alisema

Mbali na ngoma ya Darassa, pia ametoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya kuimba wimbo wa Navy Kenzo unaokwenda kwa jina la 'Kamatia Chini', huku akishauri wasanii wa bongo fleva kuimba nyimbo zenye mafunzo badala ya nyimbo za mapenzi pekee.

"Wasiimbe nyimbo za mapenzi tu, walipe pia sadaka kwa taifa... wakati mwingine waimbe na nyimbo ambazo zinaasa maadili"

Kuhusu Diamond na Alikiba, Mzee wa Upako amesita kusema ni yupi anayemkubali zaidi, na kusema kuwa wote ni wa Mungu, na vipaji vyao vimetoka kwa Mungu.
Huyu hapa Mzee wa Upako, akiimba ngoma ya Muziki, Kamatia chini, pamoja na nyimbo kadhaa za zamani

Mwanaume Kudharaulika na Mwanamke ni Uzembe

$
0
0
Ipo hivi mwanamke hata akikuzidi elimu, kipato au chochote kile sio sababu ya kukudharau, wanaume tumepewa siraha directly kutoka kwa Mungu tangu siku ile ambapo nucleus ya sperm ilipoungana na nucleus ya ovum through fertilization na kuunda male zygote, silaha tuliyopewa ni KUTAWALA, Biblia inasema wazi paleambapo Mungu anampa adhabu Eva alimwambia hivi''tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye ATAKUTAWALA'',

Hata mtume Paulo kt nyaraka zake alisema''MWANAUME AMPENDE MKE WAKE KAMA KRISTO ANAVYOLIPENDA KANISA'' alafu akasema kwa wanawake''MWANAMKE 'MTII' MUMEO KAMA UNAVYOMTII KRISTO'', unaweza ona mwenyewe utofauti wa 'kupenda' na 'kutii', kutii ni kuwa chini ya mamlaka inayokupa amri.

Sasa wanaume wengi siku hizi wanakosa hayo mamlaka ya'KUTAWALA' na sababu kubwa ni kutojiamini tu, wewe ni mwanaume, wewe ni kichwa acha kupelekwa pelekwa, ipo hivi unatakiwa kutoa maamuzia ambayo mke wako anatakiwa either afuate au aondoke sio unabadili badili maamuzi eti kisa mkeo amenuna, itageuka yeye ndo atakutawala wewe.

Ukisema familia yangu inaenda this way ni this way kweli, kama hataki aende zake kuliko kumpa mtoto wa kike akutawale tawale baadae unakuja na thread ndefu kulalamika humu, acha kuwapa wapa nafasi ya maamuzi hawa viumbe vitakusumbua sana.

Na kikubwa nikuwa maamuzi yako yawe yenye weledi, lazima atakuheshimu na ukisema kitu huyoooo ananyoosha kufuata, sio unabishana bishana na mkeo kama we ni mke mwenzake bhana, hata wao wanapenda wanaume wenye mamlaka ndani ya nyumba, usiige ulaya wale wamefundishwa hivyo tangu utoto lakini hawa wa kwetu ukiwapa nafasi kidogo tu ya kukutawala you are finished.

''HAKUNA NDOA YENYE DEMOKRASIA IKADUMU''
hawa viumbe ukiwapa nafasi moja ya kukuendesha watataka na nyingine, na nyingine, na nyingine zaidi mwisho unakuwa we mwanamke alafu yeye mwanaume a.k.a unakuwa mume bwege.... USISEMA HUKUAMBIWA........

Shilole Aeleza Kwanini Mgahawa Wake Ameupa Jina ‘Trump Food’ (Video)

$
0
0
Msanii wa muziki na filamu Shilole amefungua mgahawa wake mpya Kinondoni jijini Dar es saalam na kuupa jina ‘Trump Food’.

Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Shilole amedai amelipenda jina hilo kwa kuwa yeye anapenda harakati za Rais wa Marekani Donald Trump.

“Mgahawa unaitwa ‘Trump Food’ kwa sabubu Shishi kama Shishi ni super woman, Trump hana shobo na mtu, akitaka kufanya kitu anafanya kama mimi nafanya na naendelea kufanya, kwa hiyo aim Trump baby,” alisema Shilole.

Muimbaji huyo alisema toka aufungue mgahawa huyo mambo yanaenda vizuri.

Idris Sultan: Kwa Sasa Siko Kwenye Mahusiano ya Mapenzi (Video)

$
0
0
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Hotshots Idris Sultan, amedai kwa sasa hana mpenzi.

Akiongea Bongo5 wiki hii, Idris amedai misukosuko aliyoipata baada ya kuweka wazi maisha ya mahusiano yake na malkia wa filamu, Wema Sepetu, imetosha.

“Mimi niko single, na siwezi kuweka wazi mahusiano yangu kwa sababu fulani kaweka wazi mahusiano yake,” alisema Idris Sultan.

Aliongeza,
“Mahusiano yako ya mapenzi ukiyafanya kila mtu ajue inakuwa ni tatizo, nikipata mpenzi na nikiona kuna umuhimu kwa mashabiki wangu kujua nitafanya, lakini kwa sasa hivi siwezi kufanya hivyo,”

Kwa sasa mchekeshaji huyo ni balazi wa amani nchini Tanzania.

Bongo5

Kocha wa Timu ya taifa ya Ubelgiji Asema Samatta Anauwezo wa Kucheza ligi Kuu Uingereza

$
0
0
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amekiri kuwa, mshambuliaji na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ana-ubora wa kucheza ligi kuu ya  England maarufu kama EPL.

Shaffihdauda ilifanya juhudi za kumtafuta kocha huyo ambaye amewahi kufundisha soka England katika vilabu vya Wigan kabla haijashuka daraja pamoja na Everton kabla ya kupewa majukumu ya kuifundisha timu ya taifa ya Ubelgiji.

Juhudi zilifanywa na Mbwana Samatta kuiunganisha shaffihdauda.co.tz na Martinez, hatimaye kocha huyo akatoa ushirikiano. Martinez amesema, Samatta ni mshambuliaji mwenye kiwango kikubwa na uwezo wa kucheza soka kwenye ligi yoyote ikiwemo EPL, pia amesema ameongea na kushauriana vitu vingi na Samagoal.

Shaffihdauda.co.tz: Umeshawahi kumshuhudia Samatta akiwa uwanjani akiitumikia klabu yake ya Genk?

Martinez: Mimi ni kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji kwa hiyo nafatilia kwa karibu sana ligi za hapa kwa hiyo nimeshamuona mara kadhaa akiwa uwanjani.

Shaffihdauda.co.tz: Unaonaje uwezo wake, anaweza kucheza kwenye ligi kubwa zaidi ya Ubelgiji au timu kubwa zaidi ya Genk?

Martinez: Samatta ni mchezaji mzuri mwenye ubora wa kucheza EPL na anaweza kukupa vitu tofautitofauti kwa ubora wa hali ya juu. Lakini anatakiwa achague baadhi ya vitu ambavyo anaweza kuvifanya kwa ubora wa juu zaidi.

Shaffihdauda.co.tz: Kwa jicho lako la kiufundi, unadhi Samatta anatakiwa afanye nini ili kuongeza ubora wake ambao utafanya atoke hapo alipo na kusonga mbele zaidi?

Martinez: Ili kuwa bora sio lazima utumie kila kitu ulichonacho au unachoweza kufanya, kuna wakati inabidi uamue kipi ukipe kipaumbele halafu kingine kifate nyuma.

Shaffihdauda.co.tz: Ni kitu gani kimekuvutia kwake ambacho kama ungekuwa kocha wa klabu kingekufanya umsajili kwenye timu yako?

Martinez: Anajua namna ya uwakimbia mabeki, anatakiwa kufanya zaidi mazoezi ya spidi na akiwa uwanjani anatakiwa kufanya hivyo.

Shaffihdauda.co.tz: Kama Samatta akikuomba ushauri, utamshauri afanye nini ili kuongeza uwezo wake na kumfanya awe bora zaidi ya alivyo sasa kitu kitakachomfanya aonekane na vilabu vikubwa

Martinez: Anaweza kucheza kama target man kwa sababu anaweza ku-drible na kupangua mabeki lakini anatakiwa kuwa na nguvu kwa hiyo anatakiwa kufanyia kazi jambo hilo, pia inabidi achezee sana mpira mazoezini ili kuimarisha uwezo wake wa kumiliki mpira.

Kwa upande wake Mbwana Samatta amesema, amefurahi kukutana na Martinez moja ya makocha wenye mafanikio makubwa kwenye soka. Amepewa ushauri baada ya kuzungumza na kocha huyo na atafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa. Kikubwa zaidi ni kocha huyo kuonekana kuvutiwa na uwezo wa Samatta ikiwa ni pamoja na kukiri anaubora wa kucheza EPL ambayo haswa ndio ndoto ya Samatta.

“Kwangu ni bahati kubwa sana kukutana na kocha mkubwa kama Martinez ambaye amewahi kuwa kocha wa Wigan na Everton zote amezifundisha zikiwa EPL na sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji akiwaongoza wachezaji wenye majina na mafanikio makubwa kwenye soka duniani. Hata ukiangalia kwenye viwango vya FIFA utaona Ubelgiji ni taifa lenye mafanikio kwa sababu lipo kwenye nafasi nzuri.”

“Niliongea nae mambo kadhaa akanishauri vitu vingi vya kuvifanyia kazi mazoezini na kwenye mechi, kwakweli nimefurahi kwa sababu ni mara chache unaweza kupata fusra kama hii ya kukutana na makocha wenye mafanikio kwenye soka duniani halafu wakakubali kukupa ushauri ufanye nini ili ufanikiwe zaidi.”

Maneno ya Zitto Baada ya IPTL Kuamriwa Kulipa Dola Milioni 168.8

$
0
0

Kupitia ukurasa wake Facebook Zitto kabwe amendika maneno hayo hapo chini...

Mahakama Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa. Mfano mzuri ni kesi kuhusu umiliki wa Kampuni ya Simu ya Tigo ambayo ipo mahakamani Sasa SUO MOTO. 


Ni hatua nzuri Mahakama kuchukua ili kuhakikisha kuna HAKI na pia kuzuia UTAPELI kwenye biashara na kuweka heshima kwenye uwekezaji.


Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m kila siku izalishe au isizalishe umeme ? Ushahidi wote ulionyesha utapeli wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha uamuzi wa Mahakama umefanya MATAPELI hawa kuendelea kunyonya fedha kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc? Ama ni JIPU la Mgongoni?



MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeiamuru Kampuni ya Kufua Umeme IPTL kuilipa Benki ya Standard Chartered Hong Kong na Benki ya Standard Chartered Malaysia Dola za Marekani 168,800,063.87.


Uamuzi huo   ulitolewa na mahakama hiyo baada ya kukubali kuisajili hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ikiitaka kampuni hiyo kulipa fedha hizo.


Jaji Baker Sehel alitoa uamuzi huo baada ya kuisajili hukumu hiyo hivi karibuni na kuamuru IPTL kulipa fedha hizo.


Alisema  walalamikiwa wanaweza kuwasilisha maombi ndani ya siku 21 ya kutaka usajili huo uwekwe pambeni na taarifa ya kusajili hukumu iwasilishwe kwa walamikiwa ikionyesha haitatekelezwa mpaka zipite siku 21.


Novemba 16 mwaka jana, Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ilisikiliza kesi  hiyo baada ya walalamikiwa kushindwa kuwasilisha utetezi wao.


Walalamikaji katika kesi hiyo walikuwa Standard Chartered Bank Hong Kong Limited na Standard Chartered Bank Malaysia wakati walalamikiwa ni IPTL, VIP Engeneering and Marketing Limited na Pan Africa Power Limited.


Katika shauri hilo walalamikiwa walishindwa kuwasilisha utetezi kwa madai kwamba mtambo wa IPTL na yote yanayohusu kampuni hiyo yako Tanzania na kwamba kabla ya kesi hiyo kuna kesi nyingine mbili nchini.


Inadaiwa msingi wa kesi hizo ni kuhusu uhalali wa Standard Chartered Bank kuwa mdai halalali wa IPTL.


Katika kesi   moja, IPTL na PAP wanaidai Standard Chartered Bank Sh trilioni sita na ya pili, VIP wanaidai benki hiyo Sh trilioni moja.


Pamoja na kuwasilisha pingamizi, mahakama ilitupilia mbali na kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.

Mchungaji Aambulia Kichapo Kanisani Huko Sengerema Akituhumiwa ni Freemason

$
0
0
Waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana, Dayosisi ya Victoria Nyanza, Parishi ya Bomani wilayani Sengerema, mkoai Mwanza wamemshushia kipigo Mchungaji wa kanisa hilo, Joseph Kwangu wakati wa ibada ya jumapili ikiendelea, baada ya waumini hao kumtuhumu mchungaji kufanya mambo yanayoendana na ishara wanazozitumia Freemason. Waumini hao waliamua kubandika matangazo ndani ya kanisa, vyooni, milango ya kuingilia kanisani kumtaka mchungaji huyo asiingie ndani ya kanisa hilo.

Waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana, Dayosisi ya Victoria Nyanza, Parishi ya Bomani wilayani Sengerema, mkoai Mwanza wamemshushia kipigo Mchungaji wa kanisa hilo, Joseph Kwangu wakati wa ibada ya jumapili ikiendelea,…

Gigy Money Afunguka Kisa cha Kugombana na Mpenzi Wake...Michepuko Yahusika

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha ChoiceFm, Gigy Money amefunguka kwa kueleza kilichosababisha yeye na aliyekuwa mpenzi wake Mo J wakagombana na kuachana licha ya kuwa alivalishwa pete ya uchumba siku za hivi karibuni.

Akifanya mahojiano wiki hii, Gigy amedai aliumizwa na kitendo cha kupigwa na mpenzi wake huyo baada ya kugundua amechepuka.

“Kuna mambo yalitokea, Mo J alichepuka mimi nikamshtukia, kwa baada ya kumwambia akaanza kunigiga,” alisema Gigy Money.

Aidha,  Gigy Money alisema kuwa anamshukuru Mungu kuwa sasa yeye na mpenzi wake huyo wapo sawa.

“Lakini namshukuru mungu yameisha baada ya mimi pia kuchepuka, kwa sababu labda alikuwa hajui maumivu ya kuchepuka, kwahiyo sasa hivi tupo sawa” alisema Gidy.

Mwalimu Afumaniwa na Mwanafunzi Wake Kitandani

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agness Hokororo amemuweka rumande Mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondani Matolo kwa madai ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo.

Hokororo alisema kuwa tukio lilitokea jana baada ya Mwalimu huyo kuwekewa mitego na wazazi wa mwanafunzi huyo. Ilidaiwa kuwa siku ya tukio , mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani usiku na kwenda kulala na kwenda kulala nyumbani kwa Mwalimu huyo.

Alisema wazazi na baadhi ya majirani waliizingira nyumba ya Mwalimu huyo na kisha walimpigia simu ili akashuhudie tukio hilo. “Kwakweli ni jambo la kusikitisha. Nilifika katika nyumba ya Mwalimu asubuhi saa 12 na kukuta akiwa na mwanafunzi huyo ambaye alikiri kuwa amekuwa akitoroka mara kwa mara na kuja kulala kwa Mwalimu wake,” alisema Hokororo.

Mwanafunzi huyo amesema huwa analala huko, alfajiri huwa anawahi nyumbani kwa ajili ya kujiandaa kwenda shuleni. Mwalimu huyo pia anadaiwa kumpa mimba mwanafunzi aliyetakiwa kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

Jalada La Masogange Lakwama Kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

$
0
0
Msanii  maarufu anayepamba  video za wasanii wa muziki wa bongo Fleva (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange ameendelea kusota rumande, huku jalada lake likiendelea kuwa mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Masogange (25), alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji, usafirisha na kutumia dawa za kulevya.

Masogange alitarajiwa kupandishwa kizimbani Ijumaa wiki iliyopita lakini ilishindikana kutokana na majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali dhidi ya vipimo vyake kuonesha kama anatumia au hatumii dawa hizo kutokamilika.

Hata hivyo alitarajiwa kufikishwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ambapo alikwama tena kutokana na jalada lake kupelekwa kwa AG.

Wakili wa Masogange, Nick Kitege  amesema bado jalada la Masogange lipo kwa AG na anaendelea kulifanyia kazi na pindi litakapokamilika muda wowote anaweza kupelekwa mahakamani.

Alisema jalada hilo limechelewa kutokana na taratibu za kisheria zinazofanywa ili kukamilisha uchunguzi.

 “Bado tupo tunafuatilia na jalada la kesi yake kwa sasa lipo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pindi taratibu zitakapokamilika atafikishwa mahakamani kati ya leo au kesho.

“Kuhusu ucheleweshwaji wa kesi hiyo ni kutokana na taratibu za kisheria, hivyo  Polisi waachwe wafanye kazi yao na sisi tunaangalia hatua zinazoendelea.

“Unajua hivi ni vyombo vya sheria na wanafanya kazi yao, wanahitaji muda kuchunguza na kutoa hoja zilizojitosheleza, bado wanahangaika kushughulikia suala hilo naamini leo tutapata jibu kamili,” alisema Kitege.

Julai mwaka 2013 Masogange alikamatwa Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, akiwa na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Melisa Edward wakiwa na mzigo wa dawa za kulevya wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.8.

Paul Makonda Kujibu Tuhuma Zilizoelekezwa Kwake Kupitia PB ya Clouds FM Kesho Februari 23, 2017

$
0
0
Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa siku kadhaa, kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, PAUL MAKONDA. Tuhuma hizo zimeanza kutolewa mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuasisi mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ambayo yameshika kasi sasa baada ya Rais MAGUFULI kumteua ROGERS SIANGA kuwa kamishna Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini. Miongoni mwa tuhuma hizo ni pamoja na;

1. Kutumia Jina lisilo lake la PAUL CHRISTIAN ambapo mwenye jina hilo ni Mtangazaji wa Radio huko Tabora. Kwa mujibu wa tuhuma hizo, PAUL MAKONDA majina yake halisi ni DAUDI ALBERT BASHITE. Jina la PAUL CHRISTIAN lilikuja baada ya MAKONDA kutumia cheti cha mwenzake ili aingie Jeshi la Polisi kwa vile yeye alifeli mtihani wa kidato cha nne. Kwa vile PAUL CHRISTIAN halisi alifaulu division One, Busweru Sekondari na kupangiwa Tabora Boys ambako alishindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano kwa kukosa ada, MAKONDA akatumia cheti hicho kujiendeleza kitaaluma. Tuhuma hizi zimezushwa na MANGE KIMAMBI ambaye mpaka sasa ameshindwa kuweka ushahidi wa hoja zake.

2. Kununuliwa na wauza madawa ya kulevya gari la kifahari aina ya LEXUS lenye thamani ya zaidi ya milioni 400.....Tuhuma ya Bungeni

3. Kumnunulia mke wake gari ya kifahari aina ya Benz lenye thamani ya zaidi ya milioni 500 na kumkabidhi wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa...Tuhuma ya Bungeni

4. Kununua Appartment Viva Tower, Dar es Salaam....Tuhuma ya Bungeni

6. Kujenga jengo la ghorofa huko Mwanza ambalo limekamilika ndani ya mwaka mmoja. Hata hivyo watoa tuhuma hizi waliingia mkenge baada ya kuweka picha ya jengo ambalo ni Hotel iliyopo Kigoma.

7. Kusafiri kwenda Marekani na Ufaransa na kukaa siku 21 huku akipanda ndege Daraja la Kwanza ambapo gharama ya nauli kwa yeye na mkewe ni Dola za Kimarekani 14,000 kwenda pekee. Kwamba, kwa mshahara wa Mkuu wa Mkoa, usingetosha kugharamia safari hiyo.....Tuhuma ya Bungeni

8. Kumpangishia nyumba ya kifahari AGNES MASOGANGE eneo la Makongo, Dar es Salaam kwa vile ni mpenzi wake na ndio maana hakumtaja kwenye orodha ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya......Tuhuma ya Wema Sepetu.

9. Kukarabati jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam bila kufuata taratibu za manunuzi kwa gharama ya Milioni 400.....Tuhuma ya Bungeni

10. Kumpigia simu Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya na kumtishia kuwa yeye pamoja na wabunge wengine kama PETER MSIGWA, JOSEPH MBILINYI aka SUGU, HALIMA MADEE, JOSEPH KASHEKU aka MSUKUMA atawashughulikia na kwamba wabunge hao si lolote, si chochote.....Tuhuma za Bungeni.

11. Tuhuma ya kumporomoshe matusi Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo baada ya kumuuliza swali kuhusu tuhuma za kutumia cheti kisicho chake cha kidato cha nne.........Tuhuma ya Jambo Leo

Tuhuma ni nyingi na naamini wadau mtaongezea na mimi nitaedit uzi huu ili kuleta mtiririko sawia. Hata hivyo, pamoja na shutuma hizo kuporomoshwa juu yake, PAUL MAKONDA aliamua kutumia busara ya kukaa kimya ili kuepusha mijadala isiyohitajika na hivyo kumtoa kwenye harakati za kupambana na madawa ya kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa hewani na Clouds FM Radio, Mtangazaji wa kipindi hicho, BARBARA HASSAN ametoa taarifa kuwa amempigia simu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam PAUL MAKONDA na kumuomba ajitokeze kupitia kipindi hicho na kujibu tuhuma dhidi yake. Habari njema ni kwamba, PAUL MAKONDA amekubali wito huo na kwamba kesho tarehe 23 Februari 2017 atakuwa hewani 'LIVE' kuanzia saa 12.30 Asubuhi kupitia KAKAKUONA na kuendelea hadi mwisho wa kipindi cha POWER BREAKFAST cha Clouds FM Radio.

By Lizaboni/Jamii Forums

FULL VIDEO: Kutoka Mahakama Kuu, Freeman Mbowe Asikamatwe

$
0
0
Ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe jana Mahakama kuu kufuatia kesi aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda, Kamishna Sirro na ZCO Wambura kwenye sakata la tuhuma za dawa za kulevya.

Mahakama kuu leo imetoa maamuzi ambayo Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu ameyasema yote kwenye hii video hapa chini.

MREMBO Agness Gerald (Masogange) Afikishwa Mahakamani Kisutu Aachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Video queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepandishwa kizimbani Jumatano hii katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya.


Mrembo huyo ambaye ni maarufu kwa kupamba video za muziki wa wasanii wa bongo fleva, amekana tuhuma hizo na kesi yake kuahirishwa hadi Machi 21 mwaka huu.

Katika mashtaka yake mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine Kokulwa, Agnes anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepan. kwa nyakati tofauti.

Mara baada ya kusomewa mashtaka yake, ameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.

Pia mrembo huyo ambaye amewahi kukamatwa nchini Afrika Kusini akihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya, ametakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam kwa kipindi chote cha kesi bila kibali cha mahakama
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images