Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live

TIMU ya Leicester Wamtimua Kocha Wake...Kisa Kizima Hichi Hapa

$
0
0
Ranieri alikuwa Kocha wa Leicester tangu Julai 2015

Bingwa mtetezi wa ligi kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake muitaliano Claudio Ranieri, ikiwa ni miezi tisa baada ya kuiwezesha kupata ubingwa wa Ligi kuu.

Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu itakuwa kwenye mstari wa kushuka daraja.

Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Seville.

Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.

HII Ndiyo DNA ya Kitamaduni Kabisa Yenye Ukweli 90% Kujua Kama Mtoto ni Wako Au Umebambikiziwa

$
0
0
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Nawasilisha.

BY GENTAMYCINE

Serikali Yawataka Wananchi Kuanzisha Desturi Ya Kununua Kazi Za Wasanii

$
0
0
Serikali imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii, kwakuwa ndiyo njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.

Wito huo umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tovuti a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za muziki za wasanii.

Alisema mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu ya kupambana na wezi wa kazi za wasanii, kwakuwa video za muziki zitakuwa zikipatikana kwenye mtandao huo peke yake kwa kipindi maalum na hivyo kuingiza pesa zinazoenda kwa msanii, serikali na watayarishaji moja kwa moja.

Pia alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili zaidi, itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya lugha elfu sita duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje, wizara yake itawaunganisha na Watanzania waliopo nje ya nchi.

Prof Ole Gabriel amewataka wasanii wao wenyewe kuunga mkono mpango huo sababu ndio njia pekee ya kuufanya ufanikiwe.

“Mpango huu utafanikiwa kama ninyi mkiwa sehemu ya mpango huu, kama ninyi wenyewe tena mkianza kuwa na kona kona na kuupiga vita, basi mpango huu utaonekana feki na utashindikana,” alisema.

Hadi sasa kuna video mbili mpya zilizowekwa kwenye Afro Premiere ambazo ni Go Low ya G-Nako na Jux pamoja na K wa Roma na Baghdad. Mashabiki wanaweza kununua nyimbo hizo kwa shilingi 300 tu kwa kutumia simu zao.

DONALD Trump Atangaza Kujenga Kinu Kikubwa Cha Silaha za Nyuklia Marekani

$
0
0
Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa anataka kujenga kinu kikubwa cha nyuklia nchini humo kuhakikisha kuwa taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani linaendelea kuwa juu zaidi katika silaha za nyuklia.

Akizungumza leo katika mahojiano maalum na shirika la habari la Reuters, Rais Trump amesema kuwa Marekani sasa hivi iko nyuma katika uwezo wake wa silaha za atomiki.

Katika hatua nyingine, Reuters imemnukuu Trump akizungumza baada ya mahojiano hayo, ambapo alieleza kuwa anachukizwa sana na kitendo cha Korea Kaskazini kufanya majaribio ya silaha zake za maangamizi.

Alisema kuwa katika kuidhibiti Korea Kaskazini, Marekani inapaswa kutumia mfumo wa nchi marafiki kama Japani na Korea Kusini.

Ni nchi tisa pekee duniani zilizothibitisha kuwa na silaha za kinyuklia ambazo ni Urusi, Marekani, China, India, Israel, Ufaransa, Korea Kaskazini, Pakistan na Uingereza. Nchi nyingine zinazodaiwa kuwa na silaha hizo zimekua zikikanusha vikali na kudai kuwa zinatumia nyuklia kama nishati.

Kwa mujibu wa shirika linalojihusisha na masuala ya usalama, Ploughshares Fund, linakadiria kuwa kuna zaidi ya silaha za nyuklia 15,000 duniani kote, ambapo Marekani na Urusi pekee zinamiliki zaidi ya asilimia 93 ya silaha hizo.

Dr Harrison Mwakyembe Aonywa na Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki

$
0
0
Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa.

Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha, inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria zote.

“Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru, wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia ni sawa na kuvunja sheria za nchi.

Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa chama chake kimefurahishwa na barua hiyo kwa Waziri na kwamba nao pia wanafanya taratibu kumuona ili kujadili mustakabali wa chama hicho.

Alisema kuwa TLS inaendelea na mchakato wa uchaguzi kama ulivyopangwa na kuwataka wagombea wote kujiandaa kwa uchaguzi huo ambao alisema ni halali.

Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika machi 18 mwaka huu, huku wagombea kutoka vyama vya upinzani wakiwa wamejitokeza kuwania nafasi ya uongozi wa juu.

Wema Afunguka Sababu ya Kukimbilia CHADEMA

$
0
0
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.

Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu

 Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.

"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema

Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu

Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM kusema

"Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki

Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia"

TCRA Yaadhibu Vituo Vinne vya Utangazaji

$
0
0
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji  kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa) kupitia taarifa ya habari.

Akitoa adhabu hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vitio hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake.

Amevitaja vituo  hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.

MWIMBAJI Rosa Ree Kutoka The Industry Aachia Video ya Wimbo wake Mpya..Icheki Hapa

$
0
0
Mwanadada ROSA REE ambaye ndio mkali wa Hip Hop hapa nchini kwa sasa ameachia kichupa kipya kinachokwenda kwa jina la UP IN THE AIR..

Bonyeza Play:

KIMENUKA...Steve Nyerere Atiwa Mbaroni

$
0
0
Utata umeibuka juu ya kukamatwa kwa msanii wa filamu nchini Steven Mengele a.k.a Steve Nyerere, mara baada ya kuwepo kwa taarifa hizo ambazo zimetolewa ufafanuzi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.

Akizungumza jana na wanahabari, Kamishna Sirro alisema yeye hajamuita Steve Nyerere lakini huenda akawa ameitwa na maafisa wake wa upelelezi kwa ajili ya mahojiano, jambo ambalo ni sahihi.

Sirro alisema kuna kikosi maalum alichokipa kazi hiyo na endapo msanii huyo anahojiwa ataweza kuachiwa kama kikosi hicho kitajiridhisha kuwa anastahili dhamana, lakini kama kitaona bado kinamuhitaji, kitaendelea kumshikilia.

Msanii huyo ameingia kwenye 'headline' hasa mitandaoni baada ya kusambaa kwa sauti zinazodaiwa kuwa ni mazungumzo kati yake na Mama wa Msanii Wema Sepetu, kuhusu sakata la dawa za kulevya linalomkabili Wema Sepetu.

Katika hatua nyingine, Mwenyenyiki wa CHADEMA, Freeman Mbowe alifika katika kituo hicho kikuu cha polisi Dar es Salaam, na kisha kupandishwa kwenye gari ya polisi na kupelekwa kusikojulikana.

Kamishna Sirro alipoulizwa kuhusiana na kinachoendelea kwa mwenyekiti huyo, alisema kuwa jeshi hilo lina mamlaka ya kumuita Mbowe wakati wowote kwa ajili ya mahojiano.

Msikilize hapa akifafanua baada ya kuulizwa maswali na waandishi wa habari


ALIYETAKA Kujikata Uume Atiwa Mbaroni Singida

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mkazi wa kijiji cha Maghojoa wilayani Singida kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kukata uume wake kwa panga hadi kuutenganisha na mwili kwa kile alichodai kuelemewa na ugumu wa maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ntandu Mahumbi (60), mkulima katika kijiji hicho na kwamba tukio hilo ni la Februari 23, mwaka huu saa 5 asubuhi.

“Mtuhumiwa alituambia siku ya tukio yeye alitoka nyumbani kwake kwenda shambani na aliporejea majira ya saa tano asubuhi aliingia ndani na kuchukua panga, akajikata uume wake na kujichoma kwa kisu kifuani ikielezwa ni kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili,” amesema Magiligimba.

Amesema polisi inaendelea na uchunguzi ili kufahamu sababu zaidi za mtu huyo kufanya kitendo hicho na mara uchunguzi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani.

Hata hivyo, habari ambazo hazikuthibitishwa zinadai kuwa siku ya tukio, Mahumbi aliporudi kutoka shambani alimkuta mke wake akizini na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake, ndipo aliposhikwa na hasira na kuamua kufanya alichotenda.

Habari Njema Kutoka Markson Beaty, Sasa Wanakuletea Program ya Kuongeza Ukubwa wa Uume...

$
0
0

HABARI NJEMA
MARKSON BEAUTY sasa tumewaletea program inayokuwezesha kuongeza uume kwa size utakayo kama ifuatavyo :-
1.Urefu nch 5 na upana cm 3 @120,000/=.
2.Urefu inch 6 na upana cm 3 @130,000/=
3.Urefu inch 6-7 na upana cm 4 @150,000/=
4.Urefu inch 8 na upana cm 4-5 @170,000/=
Pia tuna Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume @120,000/=.
Spray ya kuchelewesha kufika kileleni kwa wanaume @120,000/=.
Popote ulipo duniani utapata huduma zetu.
Wasiliana nasi kwa no (+255)
0767447444 au 0714335378.
Instagram @marksom_beauty_pr @marksom_beauty_pr

Tahadhari Kwa Wadada Mnaopenda Kuvaa Shanga Kiunoni...

$
0
0
Bwana Yesu asifiwe!!!

Wanawake wengi wanapenda kuvaa shanga kiunoni wakiamini zinawavutia wanaume wengi katika mapenzi.

Napenda kutoa tahadhali kwa wanaopenda kuzivaa hasa kiunoni kuwa asilimia 80% ya shanga zinazouzwa zikiwa zimeshasokotwa zinatengenezwa na waganga WA kienyeji au watu ambao ni mawakala WA shetani na kuzinuizia mapepo kwa malengo yafuatayo:


Kuharibu au kuiba nyota za watu
Kuwafunga wanawake uzazi
Kuwaunganisha na mtandao WA kuzimu
Kuvuruga mfumo WA hedhi WA wanawake
Kuwafanya wanawake kuwa makahaba, kwa sbb unatamani kukutana na wanaume wengi ili wakujue km unavaa shanga na unazitumia
Kuwafunga kimafanikio
Kuwafanya wasidumu kwny ndoa wanapoolewa.
Kuwafanya wafikirie ngono zaidi.


Sasa unaweza usinunue kwa mganga lakn aliyetengeneza ni mganga au agent WA shetani.

Ww unaweza kununua kwa MTU na ukamwona WA kawaida, au yeye anaeuza yamkini hajui lakn alyetengeneza alikuwa na kusudi.

Unahitaji kuwa makini sana Dada zangu na vitu vinavyovaliwa sirini.

Ni unaponunua ukazikomboa kwa damu ya Yesu ili kufuta Yale maagano na manuizo yalyoambatanishwa nayo.

Nami ninazikomboa kwa mamlaka ya Jina la Yesu kwa yeyote mwenye nazo nafuta manuizo yote kwa Damu ya Yesu, km unazo TYPE AMEN.

By Illovo

SIMBA na Yanga Leo Hapatoshi....Watakao Vunju Viti Kukiona, Askari 350 Kuulinda Uwanja wa Taifa leo

$
0
0
Askari Polisi wapatao 350 watamwagwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi kulinda usalama wakati Simba na Yanga zikipambana katika mchezo namba 169 wa Ligi Kuu Bara.

Askari hao watakuwa wakilinda usalama wa ndani na nje ya uwanja huo uliopo Manispaa ya Temeke na mtu yeyote atakayefanya fujo au uharibifu ataishia mikononi mwao.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema, askari hao watashirikiana na watu wengine kutoka majeshi mengine na kampuni binafsi za ulinzi kuhakikisha usalama unatawala uwanjani hapo.

“Kuna polisi 350 ambao leo (jana) jioni watafanya mazoezi uwanjani wakijipanga kwa ajili ya kulinda kesho (leo) kuhakikisha hakuna vurugu au uhalifu wowote utakaotokea.

“Nawasihi wote watakaofika uwanjani kutazama mechi kwa utulivu na kutofuata mkumbo wa kufanya fujo kwani wataishia mikononi mwa polisi na walinzi wengine wa siri.

“Hatuwezi kukubali kuona watu wanajipanga kuharibu miundombinu ya uwanja ambao tulipata tabu kuomba uruhusiwe kwa timu hizi, nawasihi watu wasifanye vurugu,” alisema Lucas.

MAHAKAMA Yabariki Kuvunjika Kwa Ndoa ya Flora Mbasha na Mumewe...Sasa Kugawana Mali

$
0
0
Baada ya msuguano wa miezi kadhaa, hatimaye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imeridhia kuvunja ndoa ya Mwanamuziki wa Injili, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha kisha kugawana mali walizochuma pamoja. Chanzo makini kimefunguka kuwa, Flora aliyekuwa akiidai talaka hiyo ili aweze kuolewa na mwanaume wake mpya, alifanikiwa azma yake hiyo hivi karibuni baada ya mahakama kuridhia.

“Si unajua Flora ameshapata bwana mpya yule Daud Kusekwa na vikao nasikia vimepamba moto. Hivyo alikuwa anapambana kwelikweli kuhakikisha anapewa talaka na mimi ninayo nakala yake kama vipi niwatumie.

“Sasa amefanikiwa, wamegawana mali na mahakama imewapa masharti juu ya malezi ya mtoto wao aitwaye Eliza kwamba Flora ndiye atakayempa mahitaji yote ya msingi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Si unajua wale kuna mali walichuma pamoja? Basi zote wamezipiga pasu. Kuanzia zile zilizokuwa kwenya akaunti ya pamoja na hata ile nyumba yao iliyopo Tabata Kimanga.”

Risasi Jumamosi baada ya kuipata nakala ya hukumu hiyo ya talaka, lilimvutia waya Flora ili kumsikia anazungumziaje hatua hiyo lakini simu yake haikupatikana hewani.

Kwa upande wake Mbasha, alikiri ndoa yao kuvunjika mahakamani na kusema hayuko tayari kuzungumzia mgawanyo wa mali zao. “Wewe elewa tu tumeshaachana, talaka imetoka mahakamani.

Hayo mambo mengine mimi siwezi kuyazungumzia,” alisema Mbasha. Wawili hao kwa sasa kila mmoja ameshampata mwenzi. Flora anatarajia kuolewa Aprili 30, mwaka huu wakati Mbasha bado haijajulikana kama atamuoa mchumba wake wa sasa au la.

USHAURI wa Mange Kimambi Kwa Chadema Baada ya Kumchukua Wema Sepetu.

$
0
0

Mange Kimambi Ameandika haya hapa chini katika ukurasa wake wa Instagram:

From @mangekimambi_ - Mi naomba nitoe nasaha kwa Chadema juu ya Wema mapemaaaa ili baadae tusije kulaumiana.
.

Mi natoa ushauri kwa Chadema kuwa wawe serious na kumshikilia huyu mtoto mpaka 2020. She is a huge asset. Wasifanye mistake waliyoifanya kwa Wolper!!Kuna mtu aliedhani kuna siku Wolper atageuka?Wolper alitupa shida mnooooo kipindi cha kampenii, Yani alikuwa ndo kamanda wao namba 1 online.Ila baada ya kampeni kuisha mlimsahau kabisaaa... Ubunge viti maalum mkawapa mahawara na magirlfiend zenu ambao hawakuwa na mchango hata robo ya mchango wa Wolper.Okay basi acheni viti maalum, hata kumpa kifuta jasho Mbowe jamani?

Ngojeni niwaambieni kitu, tusidanganyane hapa kuwa mtu anaweza kukipenda chama akawa anakufa njaaa ila akakomaa na chama.So Mimi nawaambia Chadema although Wema anaapa Miungu yoooote kuwa kaja kwa roho moja na haitaji pesa, mwisho wa siku hakuna kishawishi kibaya kama njaa.Atajikaza mwaka au miaka miwili ila njaa ikimzidia shetani atamshinda.Na CCM mnawajua mbinu zao.

So Mimi nawaaambia mapemaaa, Mbowe, Mdee , Easter Bulaya and the rest huyu mtoto 'mumshikilie'.She is going to be a huge asset to you kupata kura za watu wengi mnooo.Njaa isikie kwa mwenzio, so don't take her for granted!

Nawapeni wazo tu, sio lazma mumuweke kwenye payroll ya chama Ila Baba Sasha, Lema, Professor Jay, Mdee, Easter, Mbowe, Mnyika,mkisema kila mwezi kila mmoja wenu achange laki 3 tu za kumsaidia Wema kujikimu hamtoshindwa.Haki hizo kidogo zitamsaidia kuishi na kujikimu na kukitumikia chama.Mkimwacha akapauka asije after 2 years 'akaimisss' CCM tukaanza kulaumiana Hapa. Njaa ni kitu kingine aiseee!

Hata Wolper Alivyorudi CCM niliweka posti nikasema tusimlaumu Wolper , tuwalaumu Chadema, hawakumthamini, mtoto wa watu aliwasaidia mno.Asikwambie mtu Hata mtu apende chama vipi mwisho wa siku mkono lazma uende kinywani.


Mimi mwenyewe sometimes naishiwaga nguvu ya kazi Ila ni vile Magufuli ananiogopesha mnooo na issue ya demokrasia na udikteta so najikaza. Ila sometimes huwa natamani niage. So Trust me najua nachoongelea, msaidieni huyo mtoto..

KUTANA na Mtabibu Ostadhi Khamisi Kutoka Mombasa Kenya Kwasasa Yupo Tanzania Kwa Ajili yako

$
0
0

Kutana na ostadhi khamisi kutoka mombasa Kenya kwa sasa yupo Tanzania ni mtabibu na mtafiti Wadawa za asili anatibia kama vile:
Miguu kuuma
Miguu kufagazi
Miguu kuwakamoto
Chango lauzazi kwakina mama
Dawa ya uzazi wakina mama inapatikana
Kusafisha nyota ili uwe namuonekano kwa kila mtu
Kumrudisha mpenzi wako na liekukimbia ndani yasiku 3 bila yapingamizi yoyote
Kumshika mume au mke asitoke nnje ya ndoa
Pata pete ya Bahati inayo endana na nyota yako
Kurudisha mali ilipotea au kudhurumiwa ndani yasiku 3
Pata utajili usiokuwa namashaliti yoyote
Dawa za nguvu za kiume
Dawa ya biashara inapatikana
Dawa ya kuzuia chuma ulete kwenye biashara inapatikana
 Zindiko la nyumba au shamba
 Anatuliza familia zinazogombana DUWA pamoja navisomo vya ufunguzi wa mwili wako njoo ufunguliwe vifungo ulivyo fungwa kutana na ostadhi khamisi utimiziwe ahadi ulizo hadiwa acha kuteseka acha kuhangaika ostadh khamisi yupupo tanzania kwajili yako...

Call +255718746825 +255754765246 kwa what'sapp +255783708487

VIDEO: Mama Wema Sepetu kuhusu simu ya Steve Nyerere na kuhamia CHADEMA

$
0
0
Mama wa Mwigizaji Wema Sepetu ameongea kuhusu yeye na Mtoto wake Wema kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kila kitu alichozungumza pia kuhusu sauti ya simu iliyosambaa akiongea na Steve Nyerere kiko kwenye hii video hapa chini:

KUCHEZA Elimu ya Tanzania ni Tatari zaidi ya Dawa za Kulevya’ -Hussein Bashe

$
0
0
Moja ya habari kubwa hivi sasa Tanzania ni pamoja na hatua ya Serikali kupitia TCU kutoa orodha ya majina ya baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wasio na sifa za kuwa wanafunzi wa vyuo.

Badhi ya watu na taasisi mbalimbali kikiwemo chuo kuku Dar es salaam UDSM kilichoikataa orodha hiyo. Kwenye Exclusive interview ya Ayo TV na millardayo.com tunaye Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe ambaye na yeye ametoa ya moyoni baada ya kuiona taarifa hiyo huku akisisitiza kuwa Serikali imefanya makosa.

Bashe amesema:
’Tunatatizo kubwa la mfumo wa elimu kwenye nchi yetu, toka nimekuwa na ufahamu na kufuatilia mambo nimeona kila Waziri amekuwa akija na movie yake, ukijiuliza swali nani aliwadahili hawa wanafunzi jibu ni TCU‘ –Hussein Bashe

‘Leo mwanafunzi amekaa chuoni na katumia gharama nyingi achilia mbali matarajio yake aliyojiwekea na familia yake alafu unaenda kuzima mshumaa wake, tujiulize mara ya kwanza wakati wanadahiliwa walikuwa na sifa alafu sasa hawana sifa?‘ –Hussein Bashe

‘Hii inatafsiri kwamba mfumo wetu wa elimu unatatizo kubwa lakini la pili wakati unawaadhibu wanafunzi hao kwa kuwaita hawana sifa aliyewadahili umewachukulia hatua gani? leo chuo kikuu Dar es salaam wametofautiana na TCU na umeona‘ –Hussein Bashe

‘Mimi nasema kama Mbunge kwamba hili jambo la kuchezea elimu ya nchi hii ni hatari mno kuliko hata dawa za kulevya, kuifanya elimu hii kama ni sehemu ya kuifanyia majaribio ni hatari‘ –Hussein Bashe

‘Tumekuwa ni watu wa kusukumwa na matukio, Moja kati ya mtu aliyekuwa nilikuwa na matarajio makubwa sana kwenye nchi hii ni Profesa Joyce Ndalichako lakini siku zinavyokwenda naona kama anashusha viwango vya elimu ya Tanzania huyu ni mama ninayemuheshimu lakini kwa hili hatuwezi kucheza na elimu ya nchi hii‘ –Hussein Bashe

‘Mimi nataka nitumie fursa hii kumweleza Rais Magufuli kwamba anakila sababu ya kuwatazama watendaji wake aliyowaamini, anaweza kuwa na nia njema pamoja lakini chakutazama ni je, amewapa watu sahihi kwenye hizo nafasi?‘ –Hussein Bashe

Vipi kuhusu TCU kudaiwa kutaja majina ya wanafunzi ambao hawapo vyuoni? Bashe amesema:
’Hii inaleta tafsiri kwamba ukurupukaji uliopo ndani ya Serikali, hakuna lugha nyingine unaweza tumia na suala la kudahili ni kazi ya vyuo na TCU wao wanafanya kazi ya udalali na ni mambo ya kukurupuka‘ –Hussein Bashe

MREMA Aeleza Haya Kuhusu Vita ya Madawa ya Kulevya

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya Parole, Augustine Mrema amesema kuwa vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya itasaidia kupunguza kwa wingi wa wafungwa magerezani kwakuwa watu wengi watakapoacha kujihusisha na biashara hiyo vitendo vya uhalifu navyo vitapungua.

Akitoa tathmini ya utendaji wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam, Mrema ametoa wito kwa Watanzania wote kwa kutumia majukwaa mbalimbali kukemea matumizi na biashara ya dawa za kulevya .

Mrema alisema,
“Wasiruhusu rais kushindwa hili au Makonda kushindwa hili, hatutakaa tuibuke tena ni kukamatia hapohapo kwahiyo watu wema wajitokeze katika hii vita wasimuachie rais peke yake wasimuachie Makonda na Simon Sirro, tujitokeze tuhakikishe huu mtandao unavunjwa.”

Aliongeza “Mimi nilikuwa napendekeza kwamba kila mkutano wa hadhara utakaofanywa na viongozi wa vyama wasiache hii agenda tukiendelea hivyo watashindwa, tumeona tu kelele kidogo dawa zimekosekana mtaani, Je tukikazana baada ya mwezi madawa yatakuwa ni historia, alihoji?”

TID kumshtaki Steve Nyerere, ni baada ya kutuhumiwa kupokea milioni 2 za RC Makonda

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki Khalid Mohamed ‘TID’ ameahidi kuwachukulia hatua watu wanaosambaza taarifa kuwa alipewa pesa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kama kivuli katika sekeseke la kutaja majina ya wanaohusika na dawa za kulevya.

Muimbaji huyo alisema yeye alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na serikali ilimkamata kwa kosa la kutumia lakini ikaamua kumsaidia kwa kumfanya aachane na dawa hizo pamoja na kumpa nafasi ya kuelimisha vijana wenzake ambao bado wapo katika janga hilo.

Watu wana ushahidi gani kama mimi Mh. Makonda kanipa mimi pesa au wanazungumza tu? mimi nataka huyo sijui Steve nani nani…..aseme kwamba aliniona nikipatiwa hizo pesa bila hivyo mimi nitamshtaki, unaituhumu serikali, bila ushahidi, hili ni kosa ambalo naweza nikampeleka mtu mahakamani,” TID alikiambia kipindi cha Selekt cha EATV.

Msanii anayedaiwa kutoa kauli hiyo ya TID kupewa pesa ni Steve Nyerere, kupitia sauti za simu zilizosambazwa tangu juzi, zikionesha mtu anayedhaniwa kuwa ni Steve Nyerere akiongea na mtu anayedhaniwa kuwa ni Mama wa msanii Wema Sepetu.
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live




Latest Images