Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live

Hatma Kesi ya Godbless Lema Leo...

0
0
RUFAA ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Rufaa hiyo itasikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ambao ni Stella Mugasha, Kipenka Mussa na Bernard Luanda ambaye atakuwa mwenyekiti.

Kesi ya Lema ilikwama kutolewa uamuzi na Jaji Salma Magimbi, Januari 4, mwaka huu, baada ya Wakili wa Serikali, Innocent Njau, kuiomba mahakama hiyo kutoendelea na kesi hiyo kwa sababu wamekata Rufaa Mahakama ya Rufani, kupinga Jaji Dk. Modesta Opiyo, kumwongezea Lema muda wa siku 10 ili akate rufaa ya kunyimwa dhamana, nje ya muda.

Pia katika rufaa hiyo, itasikilizwa kesi ya mawakili wa Lema wanaopinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kukubali kumpa dhamana Lema.

Awali Jaji Salma Magimbi, alisema kwa kuwa upande wa Jamuhuri umekata rufaa hataweza kuendelea kutoa uamuzi wa rufaa ya Lema kulalamikia kunyimwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilimpa dhamana Lema lakini kabla ya kusomewa masharti yake, mawakili wa Jamuhuri waliwasilisha kusudio la mdomo la kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa hakimu.

Jaji Dk. Opiyo alitoa uamuzi Desemba 20 mwaka jana wa kumwongezea Lema muda wa siku 10, ili akate rufaa ya kupinga kupewa dhamana bila masharti ya dhamana, na kutupa pingamizi mbili za wanasheria wa serikali, waliopinga kusikilizwa kwa rufaa hiyo kwa sababu ipo nje ya muda kisheria.

Jaji Dk. Opiyo alisema hoja hizo hazikuwa na mashiko.

Lema alianza kukaa mahabusu Novemba 2, mwaka jana, baada ya kukamatwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kusafirishwa kuletwa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Arusha.

Novemba 8 alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha mbele ya Hakimu Desderi Kamugisha ambapo alisomewa shitaka la uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Hakimu Kamugisha alikubali kutoa dhamana kwa Lema kwa madai kuwa sheria haizuii kutoa haki hiyo kwa mshtakiwa wa kesi ya uchochezi lakini kabla ya kutamka masharti ya dhamana, Mawakili wa Serikali, Paul Kadushi na Materius Marandu walidai wana nia kukata rufaa dhidi ya msimamo huo.

Kutokana na mawakili hao kusema hivyo, Hakimu aliamua kesi hiyo ibaki kama ilivyo, huku mtuhumiwa akisubiri maamuzi ya rufani ya Jamhuri katika Mahakama Kuu.

Jaji Dk. Opiyo alipotupa rufaa ya Jamhuri na kumpa Lema siku 10 zaidi ili akate rufaa ya kupinga kupewa dhamana bila masharti ya dhamana kwa kuwa hoja hizo hazikuwa na mashiko, mawakili wa serikali wakakata rufani Mahakama ya Rufani.

Tangu wakati huo Lema ameendelea kukaa mahabusu katika Gereza la Kisongo.

Donald Trump Apata Pigo Jingine...Waziri Mwigine wa Jeshi Ajiondoa

0
0
Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi.

Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake.

Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.

Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu

Lema Yupo Gerezani Kwa Sababu Isiyo na Msingi..Ila Hawajui Wanazidi Kumkomaza Kisiasa-Rungwe

0
0
Mwenyekiti  wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe, amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), ambaye   bado yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Arusha jana baada ya kuonana na mbunge huyo, Rungwe alisema baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye jamii yanasababishwa na baadhi ya watawala.

Alisema hali hiyo imekuwa ikiibua chuki miongoni mwa wananchi   jambo ambalo si zuri na linahitaji kukemewa.

Kiongozi huyo alimtembelea Lema    akiwa  amefuatana  na viongozi mbalimbali akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Chauma, Kayumbo Kabutali  na wabunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare na Moshi Vijijini, Antony Komu,  wote wa Chadema

“Historia ya zamani inatufunza matatizo yanayotokea katika jamii yanachangiwa na mambo yanayotendwa na baadhi ya watawala  ambayo yanaleta chuki.

“Na chuki siyo kitu kizuri kwa sababu inazidi kuwa kubwa kwenye mioyo ya watu hata kama wako kimya,”alisema na kuongeza:

“Hili limewahi kutokea enzi za mitume hata Nelson Mandela aliwekwa ndani na alipotoka dunia nzima iliamka hivyo tunaona kuna baadhi ya watu wanawekwa ndani bila sababu ya msingi, natoa wito kwa wenye mamlaka kuangalia suala hili.”

Mwenyekiti huyo alisema ni wakati wa watanzania wote kwa ujumla kupigia kelele suala hilo kwa vile  Mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi, anazuiliwa kwa makosa yenye dhamana jambo la kukemewa.

“Tumekuja Arusha   kumuangalia Lema kwa sababu ni mwenzetu na tuna masikitiko na kama walifikiri wakimuweka Lema ndani wanamsimamisha au kumkomesha, wanamkomaza kisiasa.

“Anapata ujasiri wa aina Fulani kwa sababu  haelewi kwa nini yuko ndani, wangemkuta na malori matatu ya silaha sawa,” alisema.

Mbunge wa Bukoba Mjini alisema ameridhishwa na kupata matumaini na hali ya mbunge huyo kwa vile  ni yuleyule na ameongeza ujasiri wa kulisema lile analoamini.

Naye Mbunge wa Moshi Vijiji, Antony Komu,  alisema Lema ameomba wabunge wote bila kuangalia itikadi za vyama vyao wanapaswa kuwa makini wakati wa utungaji wa sheria.

Alisema   kutokana na baadhi ya upungufu wa sheria kuna watu wako gerezani kwa muda mrefu.

Alisema  katika gereza hilo asilimia kubwa wako gerezani kwa muda mrefu kutokana na upungufu wa sheria mbalimbali.

Tembelea Tovuti Pendwa ya ASILI ZETU inayohusiana na Masuala ya Tiba Asilia Kama Kusafisha Nyota na Kumvuta Mpenzi

0
0
Tembelea  tovuti  pendwa  ya ASILI ZETUinayohusiana na masuala ya tiba asilia, kusomewa dua na visomo, kusafisha nyota,  kumvuta mume au mpenzi aliyekuacha, tiba ya magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana,  mvuto wa biashara.

Pia tunatoa dawa za uzazi kwa wale kina mama wenye matatizo ya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote, kupandishwa cheo kazini, mali isiyohuzika kama vile kiwanja, shamba, nyumba, gari n,k.

Bonyeza Hapa: https://asilizetu.wordpress.com

MremboTunda Bata Kama Kawa..Adai Ndio Maisha Aliyochagua Kuishi

0
0
Muuza nyago kwenye video za mastaa wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian ambaye wiki chache zilizopita alikumbwa na msala baada ya kuitwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Sentro’ kwa wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka kuwa, licha ya kukumbwa na sekeseke hilo, hawezi kuacha maisha ya kula bata.



Akipiga stori na Over Ze Weekend baada ya kuulizwa kama amebadili mfumo wa maisha aliyokuwa nayo mwanzo ya kuonekana akijiachia kwenye mahoteli makubwa, Tunda alisema kuwa hayo ndiyo maisha aliyochagua kuishi na kamwe hawezi kubadilika.



“Hayo mambo ya bata ndiyo maisha yangu, siwezi kuacha na wala hayaingiliani na msala nilioupata kwani uzuri situmii pombe. Hata kwenye mambo ya mavazi ndiyo mfumo wa maisha yangu, siwezi kusema kuwa nitaacha kuvaa hivi, bali nitabadilika kuendana na mazingira,” alisema Tunda

Jenerali Ulimwengu Aiomba Mahakama Imuunganishe Katika Kesi ya Mbowe Dhidi ya Makonda

0
0
Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu, leo anatarajia  kuwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba kuungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  katika kesi ya katiba iliyofunguliwa hivi karibuni.

Ulimwengu anaomba kuunganishwa katika kesi ya katiba namba 1 ya 2017 kama mdai dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Maombi ya kumuunganisha yameandaliwa na kesho(leo) yatakuwa mahakamani kuomba naye awe mdai. Anaomba kujiunga kwa kuwa mambo anayopigania Mbowe naye ana maslahi nayo kwa sababu ni mambo muhimu ya katiba,” alisema mmoja wa jopo la Mawakili kutoka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya Chadema, Peter Kibatala.

Katika kesi hiyo ya katiba, Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke   kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na kukamata.

Mbowe pia anaomba mahakama itengue vifungu vya 5 &7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki ya katiba.

Mbowe alifungua kesi hiyo akidai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekiuka sheria na taratibu katika kushughulikia watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini.

Kesi hiyo ya katiba inasikilizwa na majaji watatu, Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday.

Baada ya kufungua kesi hiyo Mbowe pia aliomba mahakama itoe amri asikamatwe mpaka maombi yake ya zuio yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Mahakama ilitoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi  kutomkamata Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani yatakaposikilizwa.

Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki lakini upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata uliwasilisha pingamizi, ukiomba mahakama iyatupilie mbali kwa sababu  hana msingi katika sheria.

Upande wa mdai ulijibu hoja za kupinga maombi yao na Mahakama ilisikiliza hoja za pande zote mbili na kupanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Machi 2, mwaka huu.

Lori Laporomoka Mlimani, Laua Wafanyabiashara 6 na Kujeruhi 12

0
0
Wafanyabiashara sita wamekufa papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa, baada ya lori lililokuwa likiwapeleka mnadani kuacha njia na kuporomoka kwenye mlima wenye kona nyingi zinazofikia 99 wilayani Lushoto.

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba zilisema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili jioni katika mlima wenye idadi hizo za kona zinazoanzia Mng’aro hadi Mlalo wilayani Lushoto, baada ya lori aina ya Mitsubishi Fuso Canter kuporomoka.

Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema lori hilo lilikuwa likitokea Kijiji cha Mng’aro kilichopo uwanda wa chini lilipokuwa likipanda mlima kuelekea Mlalo kwa ajili ya kuwahi soko siku inayofuata.

Walisema lori hilo lilipofika katikati ya mlima liliacha njia na kurudi nyuma hatimaye likaporomoka bondeni, huku mizigo ikiwaangukia watu hao.

Kamanda Wakulyamba aliwataja waliokufa kuwa ni Jamal Hemed (40), mkazi wa Mlalo, Hassan Rashid (33) wa Nyasa, Bisura Seif wa Kifungilo, Hadija Said wa Mhelo, Zuena Juma wa Kwedege na Husna Athumani wa Hemtoye.

Alisema majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa matibabu. Kamanda huyo alisema dereva wa lori hilo, Nassoro Athumani (25) anatafutwa kwa kuwa alitoroka baada ya ajali.

Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva na ubovu wa gari.

Kikwete Aitamani Nafasi ya Kinana CCM

0
0
Mbunge  wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amesema hatamani kuwa rais bali anataka siku moja awe Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam juzi  alipohojiwa katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds.

Jibu hilo la Ridhiwani lilitokana na swali aliloulizwa na watangazaji wa kipindi hicho kama ana ndoto za kuwa rais wa nchi.

“Sijawahi kutamani kuwa rais ila muda ukifika natamani kuwa Katibu Mkuu wa CCM,” alisema.

Ridhiwani alisema mafaniko yake hadi hapo alipofikia ni kutokana na mchango wa baba yake ambaye ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

“Malezi yangu, kuzaliwa na kiongozi kumenisaidia kufika hapa, nisingezaliwa huko labda ningekuwa mtu tofauti na nilivyo, mzee wangu ana mchango mkubwa hata jimboni, ananipa changamoto, ananielekeza, ana nafasi ya kunishauri,” alisema.

Pia alisema katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda, tayari Mkoa wa Pwani una viwanda 164 vikiwamo vinavyojengwa na vilivyokamilika, huku 84 vikiwa ni vikubwa.

Alisema uwekezaji wa viwanda hivyo umegawanyika katika sehemu mbili, chini ya Sh bilioni tano na ule ulio juu zaidi.

“Sehemu kubwa ni viwanda vya kuchakata malighafi, kuna vya matunda, marumaru, nondo, korosho, mabati, saruji na malighafi ya nyumba na vinavyofanya kazi nikivitaja ni zaidi ya 40,” alisema.

Ridhiwani alisema jimbo lake na mkoa wote wa Pwani, unafanya jitihada kuhakikisha bidhaa zilizokuwa zikipatikana China ziweze kupatikana Chalinze ili kuepuka gharama za usafirishaji.

Alisema uwekezaji wa kiwanda cha Twyford Tanzania Ceramics kilichotembelewa wiki hii na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, uligharimu Dola za Marekani milioni 158.

Ridhiwani alisema kiwanda hicho kinachotarajia kukamilika katika kipindi cha Julai hadi Agosti, kitakuwa na uwezo wa kutoa kontena 28 hadi 30 kwa siku.

Alisema kupitia kiwanda hicho, wananchi watapata faida kwa kufanya biashara na kuongezeka kwa ajira.

“Kitakuwa na ajira zaidi ya 2,000 zilizo rasmi, huku zisizo rasmi zikiwa ni zaidi ya 4,000. Hata hivyo, bado nasisitiza ajira izingatie wazawa kwa sababu wananchi tayari wanalalamikia upendeleo katika kupeana ajira, walioajiriwa pale wengi si wakazi wa Chalinze, hata Waziri Mwijage nilimwambia,” alisema.

Pamoja na jitihada hizo, alisema utekelezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda unaweza ukakwamishwa kutokana na uwezo wa kutafsiri neno na nia nzuri ya Rais Dk. John Magufuli.

“Rais hawezi kujenga viwanda peke yake, wasaidizi tutoe tafsiri sahihi ya nia yake nzuri, tutekeleze. Sitokubali kumdhalilisha rais, akisimama mwaka 2020 akiulizwa kuwa viwanda viko wapi aseme viko Pwani, atoe mfano Chalinze,” alisema.

Hali Ilivyo Corner Baa Sinza Baada ya Agizo la Kufungwa Kutokana na Biashara za Machangudoa Kushamiri

0
0
AGIZO la mkuu wa Wilaya ya Kinondini Mkoani Dar es salaam Ali Hapi, kuzitaka baa zote zilizopo ndani Wilaya ya Kinondoni zinazojihusisha na Biashara ya machangudoa kufungwa, Corner Baa ya Sinza Mori Jijini Dar es Salaam imefungwa kwa sasa.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama waliodai kuwa kuna baadhi ya baa zimekuwa zikiwahifadhi wanaouza miili, hali ambayo ni hatari kwa mazingira na makuzi ya watoto.


“Tutashughulika na changudoa na tutashughulika na wenye baa zinazowahifadhi machangudoa, kwa sababu hili ni suala lililo kinyume cha sheria, serikali inapambana na hili tatizo halafu mwingine analikumbatia, hilo haliwezekani, tutawachukulia hatua za kisheria,” amesema.

 Awali, akitoa malalamiko yake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, mkazi mmoja wa Kijitonyama alidai kuna baa zilizogeuka kero kwao.

Salum Milongo/GPL

Wema Sepetu Awa Lulu Chadema....Hivi Ndivyo Wamepanga Kuhusu Wema

0
0

CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), kimesema kipo kwenye maandalizi ya kumkabidhi kadi mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema sepetu, pamoja na kundi lake lenye zaidi ya watu 500.

Wema alikuwa mmoja kati ya wanachama maarufu wa CCM katika kundi la wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka juzi kwa kaulimbiu ya ‘mama ongea na mwanao’.

Akiwa kama kiongozi wa wasanii, alishiriki kumnadi Mgombea Mwenza wa CCM ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano wake na wanahabari mwishoni mwa wiki,  Wema  alisema kwa sasa ameamua kuvaa magwanda na yupo tayari kwa mapambano.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Habari wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene, alisema   wapo kwenye maandalizi na kabla ya Machi 5, mwaka huu watamkabidhi Wema kadi ya uanachama   na kundi lake linalomuunga mkono.

“Wema atakabidhiwa kadi kwa utaratibu maalumu maana ameonyesha heshima na nia ya kujiunga kwenye mapambano ya kweli.

“Kwa kweli Chadema tunafarijika sana na kuja kwake maana kuna timu kubwa inayomuunga mkono pia wanataka kujiunga na chama.

“Tena na wengine wanatoka katika mashirikisho mbalimbali  ikiwamo TFF.  Kwa hiyo hapo unapata picha ya Wema ni mwanachama mpya wa Chadema mwenye mvuto wa aina yake na huwezi kubeza hata kidogo kuja kwake,” alisema Makene

Alisema   wakati wowote chama hicho kitatangaza lini mwanachama huyo atakabidhiwa kadi ya Chadema, tukio ambalo alisema litakuwa la aina yake.

Akizungumza nyumbani kwao Sinza, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Wema alisema amechukua uamuzi wa kuhama CCM baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja katika orodha ya watu wanaotumia dawa za kulevya.

Alisema kitendo hicho kilimdhalilisha kwa kiwango kikubwa.

“Nimeamua kufanya uamuzi wa kuhama CCM na sasa nahamia Chadema.  Sitaki nionekane labda nimepata hasira kulingana na tuhuma zinazonikabili, lakini nataka nionekane nimefanya uamuzi kama binadamu yeyote angeweza kufanya.

“Nimekubali na nimekiri kwamba nilisema nitakufa nikiwa CCM lakini ya Mungu mengi. Natamani ningejua awali, nasema sijachelewa, naamini uamuzi wangu nilioufanya ni sahihi na nimeingia kwenye vita.

“Nipo tayari kupigana, nina imani kwamba kutakuwa na watu wengine wapo nyuma yangu wengi watanifuata,” alisema.

Wema aliyekuwa na mama yake mzazi, Miriam Sepetu ambaye naye   alitangaza kuhama CCM na kuhamia Chadema, alisema alipokuwa kada wa CCM alikuwa mwaminifu na kwa kipindi chote alikipigania kwa uwezo wake wote.

“Nimetuhumiwa hivi karibuni na nilivyokuwa kama kada nilijitoa maisha yangu, utu wangu, nilipoteza muda wangu kupigania kile ambacho nilikiamini ni sahihi lakini siku moja kisinitupe na kinithamini kwa kile nilichokifanya lakini tofauti na nilivyokuwa natarajia havikutokea.

“Sisemi kama nilikuwa nafanya ili nije kubebwa kama princess (binti wa mfalme) ama queen (malkia) kwa sababu Wema ulikuwa unajitoa basi hata ukikosea usiadhibiwe au ukiwa unatuhumiwa usichukuliwe hatua, hapana, sijamaanisha hivyo,” alisema.

Alisema baada ya kushutumiwa aliamua kukaa kimya muda mrefu kwa kuwa alikuwa anatafakari alipokosea.

“Nimekaa kimya muda mrefu si kwamba nimefurahia kilichotokea, nilikuwa bado natafakari na kutathmini where did I go wrong (wapi nilikuwa nimekosea).

“Ni kitu gani ambacho nimekosa na kufanyiwa hichi nilichofanyiwa, nilichogundua ni kitu ambacho najua mwenyewe siwezi kusema nafurahia,” alisema.

Wema alisema kitendo cha kutuhumiwa bila wahusika kuwa na uhakika na tuhuma kimemnyong’onyeza na kumvunja moyo kwa kiasi kikubwa.

“Wanasema wenyewe ‘tenda wema nenda zako usingoje shukrani’, lakini siku ya mwisho siwezi kuwa mnyonge kwa sababu naamini there is something called democracy (kuna kitu kinaitwa demokrasia) katika nchi yangu na hicho ndicho nataka kukipigania,” alisema.

Alisema  uamuzi aliouchukua ni mgumu lakini hatarudi nyuma na anaamini kuna kundi kubwa la watu wasiopungua 500 watamfuata.

Waziri Kigwangalla Amehairisha Mkutano wa Kuwataja Wanaohusika na Mapenzi ya Ushoga

0
0

Naibu Waziri Kigwangalla ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari alipotegemewa kutaja wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Dkt Kigwangalla amesema kuwa ameshindwa kufanya mkutano huo na kuwataja mashoga hao wanaojiuza mtandaoni kutokana na sababu za kiufundi.

Mnamo tarehe 6 mwezi Februari Naibu Waziri huyo alimtaka kijana anayefahamika kama James Delicious kufika kituo cha Polisi kwa kujitangaza kuwa ni Shoga. - #regrann

Mwanamuziki Barnaba Apata Pumziko Jingine Baada ya Kuachana na Mkewe

0
0

Haya sasa Barnabas Naye ameanza taratibu kutuonyesha MTU wake ama Nene? Kama wengi mjuavyo Mwanamuziki Barnaba alizenguana na mkewe na kuachana ambapo aliyekuwa mkewe Siku ya Valentine day alionyesha ulimwengu kuwa AME move on kwa picha iliyosambaa akiwa na mwanaume mwingine..

Sasa Barnaba na yeye amekuja na kupost picha akiwa na msichana mwingine huku akituachia kitendawili...
.

#Repost #barnabaclassic
・・・
Pale Crush brother anapokutaka na crushe sister #iam_just_rakel 😘🌺🔥🗽☀️ Doll metalick Moshi Moshi -Classic Yuko Njiani Jesus is my Power 😊☕️Asante mzazi #@Regrann from @crazyvoicess - Follow @crazyvoicess (me) for more videos like this! ❤😄
Amazing 😍
Tag a friend 👇
🎤
#crazyvoicess #amazing #vocals

Serikali Yasema Makonda Aliingizwa 'Mkenge

0
0


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema itamchukulia hatua muwekezaji aliyetoa ardhi kwa serikali ya mkoa wa dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, kwa madai kuwa ardhi aliyoitoa siyo yake.


Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi, ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa muwekezaji huyo aliidanganya serikali pamoja na kumdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye ndiye aliyekabidhiwa eneo hilo kwa niaba ya serikali.

Mbali na kosa la kuidanganya serikali, Lukuvi pia amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki ardhi kinyume cha sheria.

Kuhusu Mkuu wa Mkoa , Paul Makonda, Lukuvi amesema tayari amekwishafanya naye mawasiliano na kumuelewesha kuwa alidanganywa kwa kuambiwa kuwa anapewa eneo kwa ajili ya viwanda, huku eneo lenyewe likiwa ni mali ya serikali.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita Makonda alikabidhiwa ekari 1500 za ardhi na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vigogo nchini, katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo alisema wameamua kumkabidhi eneo hilo ili kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda na kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.

Kwa upande wake Makonda aalieleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji, utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika na wilaya zote.

Mahakama Yaicharukia Serikali Kesi ya Godbless Lema, Yahoji Sababu za Mbuge Huyo Kunyimwa Dhamana

0
0

Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumnyima haki.


Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu (Lema) kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki.


“Tunaomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikai (DPP) muwe makini sana maana mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua Mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushitua sana,” alisema huku akishauriana na wenzake mara kwa mara kwa masikitiko.


Aliendelea kusema kuwa ofisi ya DPP inaitia najisi taaluma hiyo, kitu kipo wazi ila wanafanya vitu vya ajabu na havipendezi.


Alihoji jaji Luanda kuwa “Tumesoma faili lote tunashangaa hivi kweli ofisi ya mwanasheria mkuu ina wanasheria kweli na kama wapo kwa nini huyu mtu (Lema) awe ndani mpaka leo?”.


Alisema kwa kuwa mikono yao kisheria imefungwa hawawezi kufanya chochote kwa leo na kuwataka Mawakili upande wa Lema kurudi Mahakama Kuu, kuendelea na maamuzi ya dhamana.


Hali hiyo ilitokana na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi kusimama mahakamani hapo na kuomba kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa ipo nje ya uwezo wake.


“Waheshimiwa Majaji baada ya timu yetu ya wanasheria kupitia kwa kina rufaa hii kwa sababu zisizozuilika tumeona hatupo tayari kuendelea na rufaa hii, maana hatukupeleka kusudio (Notisi) kwa msajili muda ulipita, hivyo tunaomba kuiondoa na uamuzi wa kuiondoa rufaa hii tumeufikia Ijumaa muda uliisha kuja mahakamani,”. Alisema Nchimbi.


Baada ya kuwasilisha ombi hilo, Wakili wa Lema Peter Kibatala, alisimama na kusema upande wao hawana pingamizi ila waliomba hoja za awali za rufaa hiyo ziondolewe Mahakamani hapo bila kunakiliwa.


Baada ya ombi hilo Jaji Kipenka Mussa alipokea kwa niaba ya Majaji wenzake na kukubali ombi la kuiondoa rufaa hiyo namba 9/2017.


Aidha Jaji Luanda alimkaribisha jaji Stella Mugasha pia kuongea kwa niaba yao ambapo alisema mahakama imekubali ombi la pili la kuiondoa rufaa namba 10/2017, baada ya Wakili Paul Kadushi kuomba kuiondoa pia.


Wakili wa Lema Peter Kibatala, alilazimika kusimama tena Mahakamani hapo kusema kuwa upande wao unasikitika kuona ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP wanatumia Mahakama kwa njia ya kumnyima haki mteja wao, hivyo aliomba mahakama hiyo iwatatulie tatizo la kisheria lililojitokeza hadi mteja wao awe ndani hadi sasa.


Kibatala aliongea hayo huku akishindwa kujizuia na kumwaga chozi la huzuni mahakamani hapo mbele ya Majaji hao.

Steve Nyerere, Mama Wema Wafika Pabaya

0
0


 DAR ES SALAAM: Hapatoshi na joto la ugomvi linazidi kupanda kila kukicha kufuatia mama wa mwigizaji Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu kuingia kwenye mgogoro mzito na Mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. Wawili hao wameingia kwenye mgogoro huo baada ya Steve kumtuhumu mama Wema kuvujisha mazungumzo yao ya siri yaliyoshusha tuhuma nyingi kwa viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri.

MUVI ILIVYOANZA
Baada ya mazungumzo hayo ya siri kuvuja Alhamisi iliyopita, tathmini za wachangiaji mbalimbali mitandaoni, zilimmwagia lawama mama Wema kwa kuhusika na kusambaa kwa sauti hiyo kwani asilimia kubwa ya mazungumzo yaliyosikika katika ‘clip’ ya sauti hiyo, yalikuwa yakimuaibisha na kumfanya aonekane mmbeya mbele ya jamii hivyo isingekuwa rahisi Steve kuyavujisha.

STEVE NAYE ANENA
Siku hiyohiyo, Steve alizungumza na gazeti dugu na hili, Risasi Jumamosi  ambapo alieleza kwa kifupi kuwa, mama Wema amehusika katika kuvujisha sauti hiyo ili amharibie maisha yake kwani mazungumzo yake yatakuwa yamewachafua mawaziri hao kwa kitendo cha kuwahusisha na suala zima la kumtetea Wema bungeni katika msala wake wa madawa ya kulevya.

WAFIKA PABAYA
Kikizungumza na mwanahabari wetu, chanzo makini ambacho kipo karibu na Steve, kilisema kuwa kitendo cha kuaminika kwamba mama Wema ndiye aliyevujisha sauti hiyo, kilimsikitisha Steve ambapo aliapa kula naye sahani moja kwani bimkubwa huyo alionekana kudhamiria kumharibia maisha. “Steve alikasirika sana. Aliona kabisa mama Wema amemchezea mchezo kwani alipofanya tathmini ya harakaharaka, aligundua kabisa mama Wema alimpigia simu na kumuingiza kwenye mtego makusudi ili yeye aweze kuingia kingi.

“Ndiyo maana ukisikiliza ile sauti, mama Wema alikuwa anamkazania katika eneo lile Odemba aangua kilio Dar muhimu la kumtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (Paul Makonda) ndipo Steve naye akawa anajaa tu bila kujua dhamira ya mama Wema,” kilisema chanzo hicho.

STEVE AJIKOKI

Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, kitendo hicho cha Steve kuamini mama Wema amemwaga mboga, naye alianza kukusanya data zake ili amwage ugali maana ameona hakuna sababu ya kumtendea haki mtu ambaye amedhamiria kumharibia maisha. “Wewe si unajua Steve na mama Wema wemeshafanya mengi, walikuwa karibu, sasa Steve naye hawezi kukubali, atakuja na bonge moja la bomu ambalo akililipua, mama Wema hatakaa asahau maishani mwake,” kilisema chanzo.

MAMA WEMA HAJALI

Wakati chanzo hicho kikieleza kwamba Steve amejikoki kulipuka na jambo, Ijumaa iliyopita, mama Wema na mwanaye waliitisha mkutano wa vyombo vya habari nyumbani kwake na kueleza kwamba wameamua kuingia vitani kupigania ‘haki’ na alipoulizwa kuhusu kuvujisha sauti yake na Steve, hakuonekana kujali.

“Mimi sijashika simu, halafu kwanza Steve ni mwanangu tu…,” alisikika mama Wema ambaye pia alitumia mkutano huo na mwanaye kutangaza kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

WEMA NAYE ALIKINUKISHA

Katika mkutano huo, Wema alisema anatambua kuwa ana kesi lakini kilichomfanya afanye uamuzi huo ni kupigania haki kwa kile alichosema hata kama alikuwa mtuhumiwa, hakupaswa kuchukuliwa kama alivyochukuliwa wakati yeye ana heshima kwenye jamii na alikipigania Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Wema alienda mbali zaidi na kusema, yeye pamoja na wasanii wenzake, wanakidai chama hicho tawala na kwamba licha ya kuongoza dola, hakijamtendea haki hata kama alikuwa mtuhumiwa.


STEVE NAYE ATEMA CHECHE
Juzi Jumamosi, Steve naye aliandaa mkutano wa waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine ya ufafanuzi wa yale yaliyosikika katika ‘audio’ yake na mama Wema, alitumia mkutano huo kupinga mambo aliyoyazungumza Wema aliyoona ni ya uongo likiwemo la kudai hawakulipwa katika kampeni.

“Hakuna msanii ambaye anakidai chama katika Timu ya Mama Ongea na Mwanao ambayo mimi nilikuwa mwenyekiti na Wema akiwa makamu mwenyekiti, sijui labda timu nyingine. Kwanza jamani, ifike mahali tuseme ukweli. Wema ninaweza kusema ndiye msanii pekee ambaye alilipwa hela nyingi kuliko wasanii wengine wote,” alisema Steve katika mkutano huo.

MAMA WEMA KUBURUZWA MAHAKAMANI?
Hata hivyo, chanzo kilicho karibu na Steve, kimeeleza kuwa huenda Steve akamfungulia mashitaka mama Wema kwani Sheria ya Makosa ya Mtandao inamruhusu. “Sheria ya makosa ya mtandao imemkalia vibaya kweli mama Wema kwa sababu inaonesha dhahiri yeye ndiye kahusika kumchafua. Steve nilivyomuona, siku si nyingi atamburuza mahakamani,” kilisema chanzo hicho.

MDAU ANENA
Mdau mkubwa wa sinema za Kibongo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, alisema suala hilo anavyoliangalia limefika pabaya kwani sasa kila upande unajipanga kumtupia mwenzake mashambulizi na ukizingatia suala limeshakuwa la kivyama sasa.

“Wewe si unajua Wema na mama’ke wamehamia Chadema, watafanya kila linalowezekana ‘kumpiga’ Steve aonekane hafai na Steve naye hatakubali, ameandaa mashambulizi ya kila namna kuhakikisha anawabomoa Wema na mama’ke hivyo sasa hivi usitegemee tena Steve akawa na uhusiano mzuri na familia ya Wema,” alisema mdau huyo.

WALIKOTOKA!
Kabla ya kufikia hapo, Wema na Steve walikuwa marafiki wakubwa walioshibana hadi kufikia hatua ya kuwa kama ndugu kwani familia ya mama Wema iliamini Steve ni kama mtoto wao. Steve na Wema wameshirikiana katika dili nyingi mjini zilizowafanya waingize fedha pamoja serikalini na hata sekta binafsi lakini sasa wamegeuka chui na paka.

Zitto Kabwe Aandika Ujumbee Huu Baada Ya Godbless Lema Kunyimwa Dhamana

0
0

Baada ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyokaa Arusha kutupa Rufaa zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusiana na dhamana ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amezungumza.

Kiongozi huyo wa ACT ametumia Facebook kutoa malalamiko yake:
Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana. Serikali inakataa rufaa kuzuia dhamana. Mtu anakaa jela miezi 4, tena mwakilishi wa watu. Siku ya hukumu kuhusu dhamana Serikali inaondoa shauri mbele ya jopo la majaji 3. Lengo? Kumkomoa mtu. Siasa za ukomoaji zinajenga chuki kwenye jamii na chuki inazaa visasi. Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP. Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi.

Zitto Kabwe Ashindwa Kuzuia Hisia Zake Sakata Kushikiliwa Godbless Lema...Ataka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Iwajibishwe

0
0

Kitendo cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe

Katika mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha  Mbunge huyo ambaye ni muwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana  ni siasa za ukomoaji ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi.

"Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi" Ameandika Zitto Kabwe

Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema leo baada ya  majaji watatu  kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipendezi na haingii akilini mtu  kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki ya dhamana.

"Mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua mpaka  mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushtua sana". Alisema Jaji Stella Mugasha.

Mwanamuziki Timbulo Aiponda Label ya QS Mhonda...Adai Haijui Muziki ndio Imempotezea Muda Q Chief

0
0

Timbulo amedai kuwa licha ya wimbo wake hivi karibuni kuvuja ikiwa na ID ya label ya QS Mhonda, haimaanishi kuwa amesainishwa na label hiyo.

Akiongea na Pride FM, Timbulo amedai kuwa wimbo huo ulirekodiwa kipindi ambacho walikuwa na makubaliano ya kufanya kazi pamoja na sio kusainishwa. “Siwezi kusaini na QS, sio label ya muziki ambayo mimi naiona inaweza kukuza muziki wangu,” Timbulo alimuambia mtangazaji wa redio hiyo, Eddy Msafi.

“Sio label ya muziki Tanzania ambayo inafanya hata muziki ambao unatakiwa Tanzania. Hawajui chochote kuhusu muziki, hiyo ni label ambayo labda wangekuwa wanafanya vitu vingine kama masuala ya ujenzi na vitu vingine kibao ambavyo mkurugenzi amesomea,” amesisitiza.

Hivi karibuni label hiyo ya QS Mhonda imeingia kwenye headlines kutokana na kuwa na ugomvi na Q-Chief aliyekuwa amesainishwa mkataba wa maisha. Chief amepigana hadi amefanikiwa kujitoa kwenye label hiyo kwa madai kuwa haikuwa ikimsaidia kwa lolote.

Yenyewe ilidai kuwa imetumia zaidi ya shilingi milioni 200 kwa Q-Chief lakini haijawahi kupata faida. Moja ya kitu kikubwa ambacho kampuni hiyo imefanya ni kumuanganishia collabo na msanii wa Nigeria, Patoranking ‘Koku’ ambayo inaonekana kama ilikuwa ni ya kupoteza muda. Wimbo huo ulivuja mtandaoni na kupotea ndani ya muda mfupi.

Mwanaume Aliyefanya Mapenzi na Maiti ya Mtoto wake Auawa

0
0

Mwanaume mwenye umri wa miaka 45 kutoka Kenya amepigwa na Wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na maiti ya Mtoto wake aliyekuwa na umri wa miaka 15 ambapo ripoti ya K24 TV imeripoti tukio hilo kutokea kwenye kijiji cha Kiwanja Ndege  kaunti ndogo ya Kuresoi Kaskazini.

Mashaidi wanasema baada ya mtoto kufariki kutokana na uvimbe wa Ubongo kichwani walihifadhi mwili kwenye chumba cha pekee lakini mida ya SAA nane usiku baba wa mtoto huyo aliamka na kwenda katika chumba hicho na ndipo alipokutwa akiwa anafanya mapenzi na maiti hiyo kitendo ambacho kiliwakasirisha wananchi na kuanza kumpiga hadi kupelekea kifo chako

Mwenyekiti wa Chadema Mbowe Aifagilia Mahakama Arusha

0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kunyimwa dhamana na kukaa gerezani kwa zaidi ya miezi mine sasa.

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe akiwa nje ya mahakama mjini Arusha baada ya mahakama ya rufaa kufuta rufaa za upande wa Jamhuri, amesema kitendo hicho kiliwafanya waichukie mahakama kuona inapewa maelekezo na serikali, kumbe siyo kweli bali ni mchezo mchafu wa ofisi ya DPP.

“Leo mahakama imetufariji sana na kuturudishia imani yetu kwao kuwa ni chombo kilichosimama kwa miguu yake kama Mhimili wake na haipokei maagizo ya serikali” Amesema Mbowe.

 Amesema sakata hilo linawasababisha kupeleka hoja katika bunge lijalo kuwa waangalie wafungwa na mahabusu walio mo ndani, kwani siyo wote waliokaa kwa sababu za kuhusika na makosa, bali wanaonewa.

Aidha amewapongeza majaji kwa kuitaka ofisi ya DPP kushikilia watu kwa misingi ya sheria na badala ya kuitia najisi mhimili huo kwa sababu ya michezo ya kisiasa.
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live




Latest Images