Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Habari Picha...Rais Magufuli Alivyojiunga na Waumini wa Kikristo Katika Ibada ya Kupata Majivu Leo...!!!


Mange Kimambi Amcharukia Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete Huko Instagram...!!!

$
0
0

Mzee wako alikuwa na busara, Ila huyu jamaa tulienae sasa? Yeye hajajua power yake ndo maana anaitumia vibaya..... .
.
Ila twende mbele turudi nyuma. Ridhwani wewe ulisumbuliwa sanaaaaa na maneno ya mitandaoni mpaka ukamuingiza babako chaka..... Na usiseme kwamba baba yako alimwachia Mungu. Hapana hakumwachia Mungu mwisho alichukua ushauri wako wa kipuuzi Na akatia saini sheria za mitandao ambayo leo Hii ndo huyu kichaaa anatumia kutufunga midomo.... Ridhwani unakumbuka jinsi wewe na January Makamba mlivyoteam up tweeter kuitetea sheria ya Mitandao?? I think pale ndo nilipokutema rasmi. I think nilikuposti wewe na January Na nikawachamba kisawasawa, wewe na January mlidhani sheria ya mitandao itawakinga Na vichambo vya mitandaoni hamkuangalia madhara makubwa ya ile sheria. Sasa oneni Leo mnavyotesa watanzania..... Na niliwaambia wewe Na January , niliwaambia hii sheria inaminya freedom of speech. Sio mimi to kila mtu aliwaambia Ila ndo ilikuwa enzi zile nchi yenu mlikuwa hamsikiiii la mtu.... Enzi zile wewe Na January ndo mahot cake wa mjini mnajifanya mnajua kila kitu, mnajifanya Miungu watu
.
.
Kwa hiyo Ridhwani unakuwa unaongea uwongo ukisema dingi alimwachia Mungu, Hapana dingi hakumwachia Mungu, Dingi alikusikiliza wewe na January Makamba Na akaamua kudo something about it like you asked him to Na akaisaini sheria ya Mitandao....
.
.
Kwa kiasi kikubwa mnoooo wewe umemuwezesha Magufuli kutufunga midomo kwenye mitandao...
.
.
Kwahiyo Riz we piga kimya tuicheze sote hiii ngoma ya mirembe mpaka 2020.....
Source Mange Page

Mmiliki wa Kona Baa Atoa ya Moyoni Baada ya Kufungiwa

$
0
0

DAR ES SALAAM: Mmiliki wa baa maarufu iliyopo katika viunga vya mitaa ya Sinza maarufu kama Kona Baa, Joseph Mushi ametoa ya moyoni kuhusu sakata la kufungiwa kwa baa yake na Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa masikitiko juzi, Mushi alisema anashangazwa na hatua ya serikali kuifunga baa yake kwa kigezo kwamba kuna biashara ya ukahaba kwenye baa hiyo. “Biashara yangu hapa ni kuuza vinywaji mbalimbali, nahudumia wateja tofauti kwa kuzingatia rika na sheria zilizowekwa, siwezi kumjua mtu fulani anajiuza na huyu hajiuzi, jambo hilo linabaki kuwa suala la mtu binafsi.

“Ni kweli nimekuwa nikisikia na wakati mwingine kuona kuna dalili za kuwepo kwa vitendo vya biashara ya namna hiyo, hata hivyo nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha natokomeza uwepo wa shughuli hizo.

“Nimekuwa ni mtu wa kwanza kununua magari mawili pamoja na pikipiki moja na kuzikabidhi kwa jeshi la polisi kanda maalumu enzi hizo kitengo hicho kikiwa chini ya Kamanda Kova (Suleiman) ili kuweza kutusaidia kuwakamata madada poa wote wanaozunguka eneo hili sanjari na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

“Niiombe serikali kutazama njia nyingine za kukabiliana na tatizo la ukahaba nchini pasipo kuathiri shughuli zetu za kiuchumi, ifahamike kupitia kazi hii nimeajiri Watanzania wengi ambao wamekuwa wakijipatia kipato cha kuyaendesha maisha yao, hivyo kwa kufungia biashara hii siyo tu itaniathiri mimi peke yangu lakini pia Watazania wengi,” alisema Mushi.

Aidha, katika hatua nyingine, madereva bodaboda wa eneo hilo wamesema tangu kufungiwa kwa baa hiyo, hali ya biashara imekuwa mbaya kwani wateja wao wengi walikuwa ni wale waliokuwa wanaburudika katika baa hiyo. “Hali ni mbaya kwa sasa, nilikuwa nafanya kazi eneo hili napata shilingi elfu kumi na tano hadi ishirini kwa siku, sasa hivi hata kuipata shilingi elfu kumi ni tabu,” alisema dereva bodaboda mmoja ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini.

Pamoja na hayo, majirani wa mitaa hiyo, waliunga mkono serikali kwa kitendo cha kuifungia baa hiyo kwa madai kwamba hiyo imekuwa chanzo cha kuharibu watoto wao kimaadili. “Hii baa imekuwa kero mtaa huu kwa muda mrefu, wao hawajali huyu ni mtoto, wanachojali wao ni pesa, watoto wadogo wanajiuza, wanacheza muziki na kunywa pombe bila kuogopa chochote, kwa kweli mimi naona ni sahihi kwa uamuzi wa serikali,” alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Tumuamini yupi kati ya Wema Sepetu au Batuli?

$
0
0

Wiki chache zilizopita kumekuwepo na mambo mengi ambayo yamekuwa yakitrend kwenye vichwa vya watu kama madawa ya kulevya, watu kupelekwa kuhojiwa na harakati za wanahabari kutaka kujua msanii gani atapanda mahakamani, lengo ni kutaka kuchukua matukio mbalimbali yatakayotokea maeneo hayo.

Ukiacha na hayo, kumekuwa na habari ambayo msanii wa Filamu Tanzania, Wema Sepetu kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hatua hiyo ilizua mshangao kwa baadhi ya watu kwasababu Wema alikuwa ni kada mahiri wa chama cha Mapinduzi, CCM. Nikisema hivyo simaanishi alivyokuwa CCM asingeweza kuhama chama hicho lahasha, bali ni uhuru wa kidemokrasia tulionao Watanzania mtu kuhamia chama unachokipenda bila kubugudhiwa na mtu.

Safari ya Wema na Freeman Mbowe Mahakama Kuu ya Tanzania 
Kabla ya kujitangaza rasmi, Wema aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika mahakama kuu ya Tanzania ambapo aliwapa sintofahamu watu waliopo katika mahakama hiyo kwa kunyoosha vidole viwili juu.
Kumbuka hapo Wema alikuwa hajatangaza kujiunga rasmi na chama hicho, ila aliongozana tu na viongozi hao. Siku iliyofuata Wema na mama yake (Mariam Sepetu) waliita waandishi wa habari nyumbani kwao Sinza Mori na kutangaza rasmi kuikimbia CCM na kuhamia Chadema na kuanza kujiita kamanda.

Safari ya Wema na waandishi wa habari
Wema alipoita waandishi hao kulikuwa na baadhi ya nukuu ambazo watu walizisikia akizizungumza, moja ya kauli hizo ni kwamba ‘Kipindi cha kampeni 2015 hawakulipwa na CCM, kwa maana hiyo anakidai chama hicho pesa za kampeni. Pia alidai alivyoamua kujiunga CHADEMA, hajapewa hata shilingi kumi akidai kuwa amejiunga nacho wa mapenzi yake mwenyewe.

Batuli na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Protea
Siku kadhaa baada ya Wema kusema anaidai CCM, waliokuwa naye kwenye kampeni hizo za Mama Ongea na Mwanao akiwemo Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli, walipinga kauli yake. Batuli alisema kuwa Wema ni muongo na kudai kiwa wote walilipwa na lengo la maneno hayo ni kumchafua makamu wa Rais huku wakidai kuwa hawatahama katika chama hicho. Waliongeza kuwa kama Wema ameamua kuhama, ahame kimya kimya na si kukichafua chama chao (CCM)..

Hii ni nukuu ya Batuli, “Nikiwa kama makamu mwenyekiti wa group hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama mwenyekiti msaidizi wa muda nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli. Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani,wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo, haiwezekani we staa mkubwa unakaa kwenye media unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa.”

Swali kwako msomaji wa Bongo5 hapa tumuamini nani katika ya hawa watu wawili na ukweli ni upi? Tililika hapa.

Donald Ngoma: Ninaondoka Yanga

$
0
0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma amesema ataondoka katika klabu hiyo kukwepa mambo ya ovyo ya uongozi.


Ngoma amesema hayo wakati akizungumzia tuhuma dhidi yake juu ya kutocheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumamosi, Yanga ikichapwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


“Mimi na klabu tumefikia katika hatua ambayo nitachukua maamuzi muda si mrefu nitakupa taarifa sahihi za kuondoka kwangu kutokana na mambo ya ovyo ya viongozi wa klabu,”ameandika Ngoma katika akaunti yake ya Instagram leo asubuhi.


Aidha, mchezaji huyo amesema kwamba mashabiki na wapenzi wa Yanga wamekuwa wakimshutumu na kumtukana kutokana na taarifa zisizo za kweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu yeye.  


“Nimekuwa kimya wakati wote nikitukanwa juu ya sababu za kutocheza, wakati ukweli ni kwamba mimi nina maumivu ya goti. Taarifa nyingi zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba sitaki kucheza kwa sababu ninataka kuondoka katika timu, nashangaa wapi wanapata hizo taarifa,”amesema Ngoma.


Amesema Daktari ambaye Yanga walimtumia kumtibu yeye alikuwa ‘tapeli’ na ameilia fedha klabu bila kufanya kazi yoyote.


“Daktari alikula fedha za viongozi wa klabu na kuwadanganya kwamba alikuwa ananitibu amenipeleka hospitali, wakati ukweli ni kwamba nilikuwa ninatibiwa katika hospitali nyingine kwa gharama zangu mwenyewe,”amesema Ngoma.


Mchezaji huyo mrefu mwenye nguvu na kasi uwanjani, amesema kwamba baadaye Daktari huyo alipoulizwa alisema kwamba niko fiti kucheza, wakati ukweli ni kwamba sikuwa tayari kabisa kucheza.


“Alikuwa anawaambia watu kwamba maumivu yangu yanaweza kupona ndani ya wiki mbili, wakati Daktari halisi aliyekuwa ananitibu alisema ninahitaji kati ya wiki sita hadi nane kupona. Tazama huyu Daktari feki alivyoleta mtafaruku kati yangu na timu,”amelalamika Ngoma.


Donald Dombo Ngoma anaelekea kukamilisha msimu wake wa pili tangu ajiunge na Yanga akitokea Platinums FC ya Zimbabwe mwaka 2015.


Na amekuwa mchezaji muhimu tangu ajiunge na klabu hiyo yenye maskani yake, Jangwani, Dar es Salaam kiasi kwamba kila alipokosekana pengo lake lilionekana.     

Thamani ya Diamond Platnumz Inayoongozwa na Tamaa

$
0
0

Diamond anaongozwa na tamaa. Anatamani kufika mahali pakubwa zaidi duniani. Na hiyo ndiyo tofauti kubwa iliyopo kati yake na wanamuziki wengine wa daraja lake Tanzania.

Tamaa ya Diamond inamwelekeza kutumia fedha nyingi kuwekeza. Na uwekezaji huo umekuwa ukimpa matokeo makubwa. Huwezi kummudu Ne-Yo, kumweka Tanzania na kurekodi naye wimbo kisha kufanya naye video Marekani bila uwekezaji.

Kuhusu tamaa bila shaka kila mwanamuziki anayo. Hata hivyo tofauti iliyopo kati ya Diamond na wanamuziki wengine ni jinsi ambavyo anashughulikia tamaa zake kuwa kweli. Anafanya uwekezaji mzuri kupata matokeo anayohitaji.

Kufanya ngoma na P-Square kisha kwenda kuwagharamia kukaa nao Afrika Kusini kurekodi video ya Kidogo, inahitaji uwekezaji.

Tofauti ya Diamond na wanamuziki wengine inaonekana pale kila mmoja anaposhika fedha na kutumia. Diamond hutumia fedha anazopata kuwekeza zaidi kwenye muziki, wakati wengine huzitumbua kwa starehe au kufanya uwekezaji mwingine nje ya muziki.

Wahenga walishatwambia kuwa mtu huvuna anachopanda. Diamond anaonekana ni mwanamuziki mwenye thamani kubwa Tanzania na Afrika yote kwa sasa, sababu ni uwekezaji ambao anaufanya kwenye muziki wake.

Hili ni somo ambalo wanamuziki wengine wanatakiwa kulichukua. Wengi ni wazuri na ubora wao studio ni mkubwa kuliko Diamond. Hata hivyo, Diamond anawashinda kwa ubora nje ya studio.

Narudia kwa msisitizo; Wanamuziki wengi Tanzania ni wazuri na wenye thamani kubwa studio kuliko Diamond. Wanaimba vizuri kuliko Diamond. Hata hivyo, Diamond ana thamani kubwa nje ya studio.

Thamani ya Diamond nje ya studio ni jinsi ambavyo hutafsiri tamaa zake za kufanikiwa kwa kuwekeza ili kupata matokeo anayohitaji. Kupata matokeo kama ya Diamond lazima uwekeze.

Ifahamike kuwa kuwekeza ni kujinyima. Kuna vitu utatamani zaidi lakini utalazimika kuviacha ili kuwekeza katika matokeo makubwa ambayo mtu unakuwa unayaota. Diamond alijinyima kwa ajili kuwekeza ndiyo maana anapata tunayoyaona.

Ndimi Luqman MALOTO

Kesi ya Lema...Mahakama Kuamua Hatma ya Dhamana Yake Ijumaa Hii..!!!!!!!

$
0
0

HATIMA ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), itajulikana Ijumaa wiki hii baada ya shauri hilo kurudishwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa.

Hatua hiyo imekuja baafa ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kufuta rufaa mbili za Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), dhidi ya  mbunge huyo juzi mjini hapa.

Mmoja wa mawakili anaomtetea mbunge huyo, Adam Jabir, alisema shauri hilo litaamuliwa Machi 3, mwaka huu mbele ya Jaji Salma Maghimbi kutokana na rufaa ya Jamhuri namba 135 ya mwaka jana, inayopinga uamuzi wa Novemba 11, mwaka jana wa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha kumpa Lema haki ya dhamana.

Novemba 11 mwaka jana, Wakili Mwandamizi wa Serikali Paul Kadushi, alisimama wakati hakimu huyo akijiandaa kuandika masharti ya dhamana na kuieleza mahakama hiyo kuwa wameshasajili notisi ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu wakipinga uamuzi wa hakimu huyo kumpa Lema dhamana.

Hata hivyo,uamuzi huo wa dhamana haukuweza kutekelezwa kwa sababu ya nia ya kukata rufaa waliyoitoa mawakili hao wa Serikali.

Hakimu Kamugisha alishindwa kuendelea na mahsarti ya dhamana kwa mshitakiwa huyo ambapo,alikubaliana na upande wa Jamhuri na kusema kuwa notisi ina hadhi sawa na maombi ya rufaa yaliyowasilishwa Mahakama Kuu hivyo mwenendo na uamuzi wake utasimama mpaka uamuzi utakapotolewa na Mahakama Kuu.

Januari 4 mwaka huu, Jaji Maghimbi alitarajiwa kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusiana na dhamana ya Lema ila ilikwama baada ya  mawakili wa Serikali kukata Rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania,kupinga Jaji huyo  kusikiliza rufaa yao wenyewe.

Jaji Magimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri wakipinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumpa Lema haki ya dhamana.

Uamuzi huo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa jiji la Arusha,hasa ikizingatiwa mbunge huyo anashikiliwa katika mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo kwa zaidi ya miezi mitatu,tangu akamatwe na polisi nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Novemba 2, mwaka jana.

Aidha uamuzi huo ulikuwa unatarajiwa kutoa tafsiri ya kisheria ya notisi ya nia ya kukata rufaa iliyowasilishwa na na mawakili hao wa Jamhuri,notisi iliyosababisha Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi kutokuendelea na hatua ya kuweka masharti ya dhamana.

Akiahirisha uamuzi huo mahakamani hapo,Jaji huyo alisema kuwa mikono yake imefungwa na hawezi kusikiliza na kutoa uamuzi  kutokana na mawakili wa Serikali,kusajili nia ya kusudio la kukata rufaa Desemba 30 mwaka jana,katika Masijala ya Mahakama ya Rufaa Tanzania iliyopo mkoani hapa, kupinga asisikilize rufaa hiyo.

Awali kabla ya mawakili wa serikali kukata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania kupinga kusikilizwa kwa rufaa yao Mahakama Kuu, Jaji Maghimbi,aliwataka mawakili mawakili wa Jamhuri  kuwasilisha hoja zao za rufaa Disemba 29,huku mawakili wa Lema wakitakiwa kujibu hoja hizo Disemba 30 kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa rufaa hiyo jana.

Lema anakabiliwa na kesi mbili za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kesi namba 440 na 441.

Mama Wema, Haujamtendea Haki Steve!

$
0
0

NIMEKUKUMBUKA leo mama wa muigizaji Wema Isaac Sepetu. Habari za hapo Sinza-Mori, familia yako haijambo? Vipi mnaendeleaje? Najua utashangaa kwa nini leo nimekuandikia barua lakini usishtuke, huu ni utaratibu wangu wa kila wiki.    

Huwa nawaandikia watu mbalimbali mashuhuri kama wewe mama. Eeeh! Mwanao amekufanya na wewe usikauke kwenye vyombo vya habari. Hongera yako. Labda tu nikuibie siri kidogo mama, barua hii ni tofauti na zile nyingine ambazo mara nyingi huwa zinasomwa na watu wawili; muandikaji na muandikiwa.

Barua hii inasomwa na mamilioni ya Watanzania ambao watapata fursa ya kujipatia nakala tu ya gazeti hili kwa shilingi mia tano.

Hilo si dhumuni la kukuandikia barua hii. Ngoja nienda moja kwa moja katika hoja. Mama nimekuandikia kwa lengo moja tu, kukuambia kwamba hukupaswa kumfanyia vile muigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ katika sakata lako na mwanao, hata kama ulikuwa una lengo la kumtumia kama ‘silaha’ kwenye vita unayoiendesha.

Mosi, kwa heshima uliyonayo kitendo tu cha kumrekodi (naamini upande wa simu yako ndiyo ulirekodi, yaweza pia kuwa vinginevyo), kilikuwa si cha kiungwana. Kitendo kile pengine kingefanywa na vijana kwa vijana, kidogo kingeeleweka lakini si wewe kama mzazi.

Pili, kama alivyosema Steve, kwa wazo lako la kurekodi limesababisha pia wewe usikike ukifanya masihara ambayo kama ni kweli umehusika kuyasambaza, ukitafakari vizuri utaona jinsi gani yanakurudia wewe mwenyewe.

Yanakudhalilisha maana umesikika ukizungumza mambo yasiyopendeza kutamkwa na mtu mzima mbele ya hadhara. Kitendo cha wewe kuaminika umemrekodi Steve, kimeleta matokeo ya wewe kuvujisha utani wa kijinga usiopendeza kwa mama na mwanaye.

Steve amesikika akikutania kwamba anataka mzae mtoto, utani mbaya ambao kwa namna moja au nyingine, haupendezi kusikika na mamilioni ya Watanzania. Kwa anayewaza vizuri, hawezi kumrekodi mtu katika mambo ya siri kama yale na kwa namna yoyote ile kuyarusha mitandaoni.

Niliposikiliza ile sauti, kwangu niliona ni kama matusi. Mama yangu, jambo lile lingefanywa na vijana wenzake Wema, lingekuwa na picha yenye ahueni lakini wewe kusikika unatoa lugha chafu kwa kijana kama utani, ni aibu.

Jamii nzima itapata tabu sana kukuamini hata kama ulikuwa na lengo jema katika jambo hilo au umevurugwa kiasi gani. Kama mama, hata kama umekosewa, waswahili wanasema huwezi kumfukuza chizi akiwa mtupu na wewe ukiwa mtupu.

Utajistahi kwanza ndipo umkimbize. Kwa namna yoyote, heshima yako inapaswa kubaki palepale. Kama Steve alivyosema, hakutegemea ungeweza kumrekodi kwani anakuheshimu kama mzazi wake. Steve alisema alizungumza na wewe kirafiki kama mama na mwanaye.

Alizungumza na wewe akiamini huwezi kumsaliti au kumfanyia vitendo vitakavyomhatarishia maisha yake ya baadaye kama ulivyofanya. Pamoja na hayo yote, kama vile  mlivyokuwa mnaitaka haki na mwanao, hamkupaswa kuidai kwa kuvunja haki. Maana kwa

mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ni dhahiri itakugusa kwa namna moja au nyingine. Yale ni mazungumzo binafsi, yametokaje kwenye mitandao ya kijamii? Mwisho, nikushauri, wewe ni mzazi kuna mambo ambayo unapaswa kuyazungumza mbele ya jamii mengine weka akiba. Si vyema ukawa unatengeneza picha kwamba kila ukionekana, utamwaga povu kama ulivyosema siku ile kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Naamini mama utakuwa umenielewa. Nimezungumza kiungwana, naomba nawe uwe muungwana katika kila hatua unayopiga kwenye safari yenu na kila unalolifanya, ni vyema kufikiri mara mbilimbili na kujua hatima ya jambo unaloliamua.

VIDEO: Polisi Dodoma limewakamata na Kuwataja Watuhumiwa wa Dawa za Kulevya

$
0
0
Headlines za dawa za kulevya bado zimeendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambapo leo March 1 2017 Kamanda wa polisi Dodoma Lazaro Mambosasa amezungumza na waandishi wa habari na kutoa takwimu ya watuhumiwa waliokamatwa na kufikishwa mahakamani hadi sasa.

Mambosasa amesema:

’Katika operesheni ya kipindi cha miezi minne tangu October 2016 hadi January 2017 tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 88 kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kama vile uuzaji, usafirishaji, usambazaji na ulimaji wa dawa hizo‘ –Lazaro Mambosasa

‘Aina ya dawa tulizofanikiwa kuzikamata ni pamoja na heroine, bangi na mirungi na tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea huku wengine utaratibu ili kuwafikisha mahakamani‘ –Lazaro Mambosasa

‘Nawatahadharisha watu wote wenye nia ya kufanya uhalifu au kuja kufanya biashara haramu ya dawa za kulevya katika mkoa wa Dodoma waache mara moja kwani vita hii ni endelevu hakuna mhalifu atakayebaki salama kama akibainika‘ –Lazaro Mambosasa

Full stori ya Kamanda Lazaro Mambosasa na alivyoyataja majina ya watuhumiwa nimekuwekea kwenye hii video hapa chini…

Nape kawateua Ruge, Diamond, Kitenge, Alikiba, Charles Hilary na wengine

$
0
0
February 28 2017 Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa mkutano na wadau wa michezo leo, alitangaza majina ya watu kumi wanaounda kamati ya kuhamasisha watanzania katika kuiunga mkono timu ya taifa ya vijana ya Serengeti boys kuelekea AFCON 2017 U-17.

Waziri Nape ametangaza kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo mtangazaji mkongwe Charles Hilary wa AzamTV, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba, Mtangazaji wa E-FM Maulid Kitenge, Waimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz na Alikiba wametajwa pia katika list hiyo.
Ameongea zaidi kwenye hii video hapa chini……..

Wanawake Tunakuwa na Thamani Pale Tunapokuwa Nguo

$
0
0
Napenda kuzungumzia thamani ya mwanamke mbele ya mwanaume.

Nimejifunza mengi kupitia kwa marafiki zangu na hata dada zangu na ndugu wa Karibu. Thamani ya mwanamke mbele ya mwanaume ni pala anapokuwa amevaa nguo na si vinginevyo.

Mwanaume akishakuvua nguo haoni thamani yako tena huendelea kumuwazia yule ambae bado hajamvulia.

Nimeshudia wanawake wengi wakiishia kuumizwa kwasababu ya kukubali kuwavulia nguo wanaume kirahisi.

Binafsi baada ya kuushuhudia waliofanyiwa wanawake wenzangu nimeamua kutomvulia nguo mwanaume asiye mume wangu, na hii imenipa thamani kubwa sana.

Wanawake tusijirahisishe kwa hawa viumbe tutaendelea kuumizwa daima.

Mama Diamond Atua Rasmi Bongo Muvi,Hii Ndio Muvi Yake ya Kwanza..!!!

$
0
0

Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ametua rasmi kwenye fani ya uigizaji wa sinema za Kibongo (Bongo Muvi).

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum, mama Diamond alitamba kwenda kimataifa kwenye upande wa filamu kama anavyofanya mwanaye Diamond akiwa ameshiriki katika utayarishaji na uigizaji wa filamu iitwayo Mtepela iliyochezewa huko Kibirizi mkoani Kigoma.

“Nimefanya hiyo filamu na wasanii wa Kigoma, nawajua vizuri lakini kwa sasa siwezi kuizungumzia zaidi,” alisema mama Diamond.

Kwa upande wa mtayarishaji aliyeshirikiana naye aliyejitambulisha kwa jina la Isaya Lazaro almaarufu Zito, alisema mama Diamond mbali na kushiriki katika utayarishaji wa filamu hiyo pia alitoa fedha na ni mmoja wa waigizaji waliofanya vizuri ndani yake.

“Tulimwandalia scene (vipande), akavicheza lakini kabla ya kumaliza alipata safari ya kwenda Afrika Kusini na baada ya kurejea tuendelea kuimalizia”, alisema Zito

Watu Wanamjaribu Rais Magufuli Kupitia Makonda

$
0
0
Rais John Magufuli alipata kueleza kuwa yeye hajaribiwi, hata mimi naamini kuwa Rais wangu hajaribiwi. Rais wangu Magufuli yupo tofauti sana, mwenyewe alishasema hivyo.

Ninachompendea Magufuli wetu ni kuwa hajui kuremba. Hana kawaida ya kulazimisha nyekundu ionekane kijani. Hapana Rais Magufuli yupo tofauti sana. Kwake nyekundu ni nyekundu na kijani ni kijani.

Lipo jambo linalotawala sasa hivi, ni kuhusu uhalali wa cheti cha kidato cha nne ambacho Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikitumia kusomea elimu ya juu.

Hapa ndipo watu wanataka kumjaribu Rais wangu Magufuli. Kwamba afunike kombe mwanaharamu apite ili watu waseme Makonda ni invulnerable prince, yaani mwanamfalme asiyeguswa.

Rais Magufuli siyo kwamba hajui haya, anajua sana, amekaa kimya kama mtu mzima. Bila shaka yupo kwenye kipindi cha kujiridhisha, lipi linalosemwa ni la ukweli na lipi ni la uongo?

Watu wasimjaribu Rais Magufuli, naye hajaribiwi! Rais Magufuli alimtosa swahiba wake kabisa, Charles Kitwanga, kwa kosa moja tu la kuingia bungeni kalewa. Bila hata kuzungumza naye alimtumbua juu kwa juu.

Kitwanga akastaajabu. Akapata mpaka akili ya kwenda kufanya sala ya kuvuka mitihani Israel. Kitwanga kwa kushibana kwake na Magufuli, inadaiwa alianza kujiona Sir Alan Fredrick, aliyekuwa msaidizi wa Mfalme George VI kisha Malkia Elizabeth II.

Sir Alan Fredrick aliogopwa kwa sababu alikuwa karibu mno na mfalme kisha malkia. Na aliaminika kuwa ndani ya kichwa chake kulikuwa na siri nyingi za Uingereza. Unamgusa vipi Sir Alan Fredrick?

Aaah wapi! Rais Magufuli akasema yeye kwenye Serikali yake hana Sir Alan Fredrick, akamtumbua Kitwanga kisha nafasi yake akaijaza. Huyo ndiye Rais wangu Magufuli ninayemfahamu. Yeye anasimama kwenye hasi au chanya, hana katikati.

Rais Magufuli hana hizo za kuchekeana, kwa hiyo Makonda siyo untouchable prince. Rais Magufuli alimpumzisha msaidizi wake wa karibu aliyekuwa anafanya naye kazi Ikulu, Ombeni Sefue, itakuwa Makonda?

TUZUNGUMZE LILILO SAHIHI

Tumeshakubaliana kuwa Rais Magufuli hana tabia ya upendeleo na hana katikati. Hivyo tunakubaliana kuwa Rais Magufuli hawezi kumlinda Makonda kisha ajivunjie sifa yake njema aliyojiwekea.

Baada ya hapo tuzungumze; je, kinachosemwa ni sahihi? Hapo ndipo tunaweza kuuchimba mzizi wa fitina. Basi sasa, kinachozunguzwa kichunguzwe na haki itendeke.

Jina lake halisi ni Paul Christian Makonda au Daud Albert Bashite? Je, ni kweli alisomea elimu ya juu cheti cha kidato cha nne cha Paul Christian Muyenga? Maswali hayo ndiyo yatakayokata na kuuchimbua kabisa mzizi wa fitina.

Makonda asionewe, kwamba watu wenye visasi vyao wasiamue kumpakazia ili kumchafua. Kama kweli yeye ni Paul Christian Makonda na hilo la Daud Albert Bashite anazushiwa, inabidi Makonda awashitaki wanaomchafua.

Ikiwa anasingiziwa, hata Rais Magufuli itabidi awe mkali, maana watu watakuwa wanataka kumyumbisha yeye na utawala wake kisha kupoteza muda kwa vitu vya uzushi.

Ni kweli kuwa Makonda anachukiwa na watu wengi. Sababu ni aina ya ufanyaji kazi wake na uthubutu mkubwa alionao. Ndiyo maana nasema, kama hili la kutumia cheti cha Muyenga anasingiziwa, ni vizuri wanaomsingizia wakashughulikiwa kisheria.

Hata kama Makonda aliwahi kufanya makosa huko nyuma au siku za karibuni kutokana na utekelezaji wake mbaya wa majukumu yake, si sawa kuandamwa kwa tuhuma za uongo. Siku zote uongo haujengi, bali hubomoa.

Jamii nzuri tunayoitaka kwa nchi yetu, ni haki kutendeka na uonevu usipewe nafasi, kuanzia kwa raia wa kawaida chini kabisa mpaka kwa viongozi wao. Mtu akikosea ashughulikiwe kwa haki, siyo kwa kuzushiwa.

HAKI LAZIMA IDHIHIRIKE

Je, ni kweli Makonda anatumia cheti cha Muyenga? Kama ni kweli, siyo sawa kujificha kwenye mwavuli wa kuchukiwa na kudai anachafuliwa na wabaya wake. Haki itendeke na idhihirike.

Suala la Makonda kuwa jina lake ni Daud Albert Bashite na alitumia cheti cha Paul Christian M, kwamba ile M ni Muyenga kisha yeye akaigeuza kuwa Makonda, limeshakuwa mjadala mkubwa. Haupaswi kuachwa hivi! Jipu litumbuliwe.

Hizi tuhuma zimekuwa kubwa na zinazungumzwa mpaka na watu wenye hadhi na ushawishi mkubwa. Zinazungumzwa na watu wenye wafuasi wengi mbele ya wafuasi wao. Hivyo, hili si jambo la chumbani.

Kwa hali ilipofikia, tiba ya jambo hilo ni moja tu; Makonda kutokeza hadharani na kueleza ukweli wa mapito yake ya kielimu. Athibitishe kuwa yeye ni Paul Christian Makonda kwa kuzaliwa na kusoma.

Hata kama ni kweli awali aliitwa Daud Albert Bashite, atokeze na kueleza uhalali wake wa kubadili jina na kuanza kuitwa Paul Christian Makonda. Hivyo ndivyo kukata mzizi wa fitina.

NITATOA MFANO

Mwaka 2005, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, akiwa kijana mdogo, alipewa changamoto kuhusu elimu, wakati akigombea jimbo la Kigoma Kaskazini, kwa tiketi ya Chadema.

Aliyempa changamoto hiyo ni aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Lazaro Matete. Katika mikutano yake, Matete alisema Zitto hajasoma na kwamba alikuwa anawadanganya wapigakura wa Kigoma Kaskazini.

Zitto alikata mzizi wa fitina kwa kuweka wazi vyeti vyake. Matete alikosa hoja nyingine na baada ya Zitto kuanika ukweli wake, haujawahi kuwepo mjadala mwingine wowote kuhusu elimu ya Zitto.

Hivi ndivyo Makonda anatakiwa kuwakata vilimilimi wote wanaomsema kuwa yeye siyo Paul Christian bali jina lake halisi ni Daud Albert Bashite. Makonda akifanya alivyofanya Zitto mbona mambo yatakuwa kimya? Wanaomsema leo hawatakuwa na hoja nyingine.

Upo mfano wa pili; mwaka jana Rais Magufuli alipoteua wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali nchini, aliyeteuliwa kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Luhende Pius, alisemwa kuwa aliishia kidato cha nne na kwamba alikuwa meneja wa Hoteli ya City Style, Sinza, Dar es Salaam.

Hivyo ndivyo ilivumishwa. Ikawa gumzo hasa kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, Rais Magufuli alikata mzizi wa fitina na kuuchimbua kabisa kwa kuonesha hadharani vyeti vya Luhende.

Rais Magufuli alisema: “Huyo mnayemsema ni wa kwenu, ninayemfahamu na niliyemteua ana master (shahada ya uzamili).” Baada ya hapo Luhende aliweka wazi cheti chake, kamera za vyombo vya habari zikarekodi. Ubishi ukaishia hapo.

Ndivyo ambavyo Makonda anapaswa kufanya. Unajua njia ya uongo ni fupi. Ikiwa yote yanasemwa ni kumsingizia, basi atokeze aweke wazi vyeti vyake. Aseme alisomea wapi darasa la kwanza mpaka alipofikia na kwa majina yapi. Akate mzizi wa fitina.

Rais Magufuli hana kupindapinda, ndiyo maana suala la Luhende japo halikuwa kubwa, lakini aliamua kulitolea ufafanuzi. Hili la Makonda limekuwa kubwa mno. Ufafanuzi wake unahitajika.

TUELEWE MANTIKI

Mjadala wa Makonda na vyeti vyake lisichukuliwe kishabiki. Wale wanaomshambulia na hata wanaomtetea. Hili jambo linahusu maadili ya utumishi wa umma, vilevile makosa ya kisheria.

Hivyo basi, washambuliaji wasipayuke tu, bali wawe wanatoa vielelezo vyenye kuthibitisha hoja zao. Na wanaomtetea, nao wasirushe maneno mithili ya wanaopiga ngumi hewani, bali nao watoe vielelezo.

Unamtetea Makonda? Unakuja ni jibu, Makonda unamfahamu vipi? Ulikutana naye wapi? Unajua shule alizosoma? Alikuwa anatumia majina gani? Kwa nini unaamini Paul Makonda uliyemjua ndiye huyu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam? Unazungumza kwa kunyoosha maneno.

Unataka Makonda awajibike? Unasema Makonda unamfahamu vipi? Ulianza kumjua lini? Shule alizosomea ni zipi? Alikuwa anatumia majina yapi? Na kwa nini unasema Paul Makonda alitumia cheti cha mtu mwingine? Kwa nini unaamini Daud Bashite wako ndiye Paul Makonda? Majibu yawe na ujazo.

Narudia tena hili suala halitaki ushabiki. Ni suala nyeti kabisa. Makonda ni kiongozi, anayo dhamana kubwa ambayo ameibeba, kwa hiyo kumsingizia jambo la kughushi cheti ni kumvunjia heshima na kumdhalilisha kwa watu anaowaongoza na taifa kwa jumla.

Hili pia lieleweke; kama ni kweli Makonda alighushi cheti cha kidato cha nne ili apate uhalali wa kujiunga na masomo ya elimu ya juu, hapaswi kutetewa wala kuhurumiwa, maana ni mdanganyifu. Mtu mdanganyifu hapaswi kuhurumiwa.

Inapotokea mtu huyo mdanganyifu anakuwa kiongozi, hatari yake ni kubwa mno. Hivyo suala hili litafutiwe tiba. Makonda ndiye tibabu wa suala hili. Tiba ni kutoka hadharani na kujibu kila kinachozungumzwa.

Na hapa tatizo siyo kufeli. Wengi walifeli na wakajituma kusafisha vyeti vyao. Mjadala wa Makonda ni udanganyifu. Kufeli siyo kuvunja sheria za nchi. Udanganyifu wa cheti ni kosa kisheria.

Je, Makonda ni Jitender Singh Tomar wa Tanzania? Tomar alipata kuwa Waziri wa Sheria wa Delhi, nchini India. Aliwahi kusema yeye ni msomi wa shahada ya sayansi, kutoka Chuo Kikuu cha Avadh. Baadaye Avadh wakatoa taarifa hujasoma kwao.

Alipokataliwa Avadh, Tomar akasema alisoma Chuo Kikuu cha Chaudhary Charan Singh. Huko nako alikataliwa. Waziri Mkuu wa Delhi, Arvind Kejriwal, baadaye aliingilia kati kumlinda Tomar na kumbakiza kazini.

Hata hivyo, baada ya uchaguzi mwaka juzi, Tomar aliondolewa kwenye Baraza la Mawaziri lakini bado ni mbunge.

Makonda naye aseme, halafu shule ambazo atazitaja zitathibitisha. Zisipothibitisha au zikimkana tutajua ni yaleyale ya Tomar. Na akichwa kazini, basi Rais Magufuli atakuwa Kejriwal.

MAKONDA AMASAIDIE MAGUFULI

Kila mmoja anaona sasa, kwamba Rais Magufuli ndiye ambaye anatazamwa katika hili suala la Makonda. Watu wanaulizana, je, atamchukulia hatua au atamlinda kijana wake mpendwa?

Mimi msisitizo wangu upo palepale, Rais Magufuli hana tabia ya kulindana. Kama aliweza kumwondoa kazini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ndani ya siku 27 kwa ripoti ya watumishi hewa, atamwachaje Makonda kama atathibitisha ni kweli alighushi cheti?

Rais Magufuli ndiye mwanzilishi wa uhakiki wa vyeti bandia. Kuna watumishi wengi wa umma wamepoteza kazi kwa sababu ya kuhakikiwa vyeti vyao. Rais Magufuli anachukia tabia ya kughushi, kwa hiyo hili la Makonda hawezi kuliacha hivihivi.

Hivyo, shaka ondoa, Rais Magufuli atamalizana vizuri tu na Makonda kama atambaini kweli alighushi cheti. Rais Magufuli hachezewi.

Hata hivyo, Makonda anatakiwa amsaidie Rais Magufuli. Msaada wenyewe ni kwa kufanya mambo moja kati ya mawili. Bila shaka hapo ataweza kumfanya Rais wetu apumue.

Mosi; kutokeza mbele na kuwajibu wote wanaomsakama kuhusu mapito yake ya kielimu. Akiweza kuondoa utata, atamsaidia Rais Magufuli na haya maneno kuwa anamlinda.

Njia hiyo ndiyo ambayo Luhende aliitumia kumsaidia Rais Magufuli kwa kutokeza na cheti chake Ikulu. Na Rais Magufuli akakitumia cheti cha Luhende kufunga mjadala.

Pili; kama yote yanayosemwa ni sahihi kuwa alighushi cheti, basi anapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu. Makonda akijiuzulu atamsaidia Rais Magufuli ili asichukue uamuzi wa kumfukuza kazi.

Kujiuzulu kwa Makonda kisha kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kufanya udanganyifu, itakuwa hatua muhimu ya kuijengea heshima ya Rais Magufuli na Serikali yake kuwa inaukabili uovu wa aina zote bila woga wala haya.

Vinginevyo, kukaa kimya watu wataona Makonda analindwa. Na itaonekana nchi haina haki, maana kuna watu walilitumikia taifa hili kwa miaka, lakini wamepoteza kazi na stahiki zao kwa sababu ya ukakiki wa vyeti. Kwa nini wao yawakumbe na Makonda aachwe? Haki itendeke na ionekane imetendeka.

Ndimi Luqman MALOTO

Shinda Gari Bure Kutoka Kampuni ya Magari Hapa Tanzania

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi Hawa Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..


Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Mwisho wa Kujisajili ni 22 / 3 / 2017

Picha Mpya ya Jack Wolper yazua Gumzo Mitandaoni.

$
0
0
Hii ndio picha ya wolper inayoongoza kupostiwa kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na fb, picha hii inaonekana kuwavutia wengi zaidi ,salute zimfikie wolper wereva.... I phone 7 plus wereva kwenye ubora wake

Makato Bodi ya Mikopo: TUCTA Yatoa Siku 14 kwa Serikali Kuwarudishia Wafanyakazi Fedha Walizokatwa Kinyume na Mkataba wa 8%

$
0
0
Shirikisho  la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limetoa siku 14 kwa Serikali kurejesha fedha za makato ya mikopo ya asilimia 15 zilizokatwa kikamakosa kupitia Bodi ya Mikopo, likisema sera inayotumika imejaa utata.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, alisema  Serikali lazima irekebishe sheria hiyo ya Bodi ya Mikopo kupitia Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi Stadi kutokana na kuwajumuisha wafanyakazi wote katika makato ya asilimia 15 wakati imetungwa hivi karibuni.

Nyamhokya alisema kuwa wakati sheria hiyo inatungwa, baadhi ya wafanyakazi walikwishaingia makubaliano mengine ya kukatwa asilimia 8 katika mishahara yao.

Alisema wamesikitishwa na hatua hiyo ya Serikali, ingawa wanaamini haitalifumbia macho suala hilo.

Aidha Nyamhokya alisema kuna milolongo mingi ya makato katika mishahara ya wafanyakazi ambayo ni zaidi ya asilimia 57, huku pia mazingira ya kufanyia kazi yakiendelea kuwa magumu na Serikali ikishindwa kuongeza mishahara wala kuwapandisha vyeo kwa muda mrefu.

Aidha alisema kwa kawaida mtumishi mwenye mkopo serikalini analipa kwa makubaliano maalumu, lakini mtindo wa bodi hiyo kukusanya fedha za wanufaika kabla ya kuanza kwa sheria husika kumeleta athari kwa watu wengine.

Tofauti 8 Kati ya Wasichana na Wanawake...!!!

$
0
0

1. Wasichana wanatafuta wanaume wenye pesa ila Wanawake wanatafuta wanaume wanaojali na kupenda.

2. Wasichana hupima thamani ya wanaume wao kwa kuangalia ukubwa wa mifuko yao ila Wanawake hupima thamani ya wanaume wao kwa kuangalia kiwango cha busara na hofu ya mungu na kwa vipi wanajiheshimu mbele ya wapenzi wao.

3. Wasichana huvunja mahusiano kwa sabubu zisizo na mashiko ila Wanawake wana uvumilivu wakifahamu kwamba kila jambo hutokea kwa sababu.

4. Wasichana hufikilia kuhusu mambo yaliyopo sasa ila Wanawake hufikilia kuhusu yajayo.

5. Wasichana wanapenda kuwa na wanaume wengi wanaowafuata ila Wanawake wanafahamu sheria ya uhitaji (Vitu rahisi vina wateja wengi).

6. Wasichana wanahitaji pesa ili kununua make-ups ila Wanawake wanahitaji pesa kwa ajili ya kufanyia mipango ya maendeleo.

7. Wasichana huumizwa na mwanaume mmoja na kuwa na kinyongo na wanaume wote ila Wanawake wanajua kwamba wanaume wote sio sawa.

8. Msichana "anajifunza" ila Mwanamke "anajua"

Wala Sio Makonda; Aliyeleta Balaa Hili la Madawa ya Kulevya ni Huyu ....!!!

$
0
0

KILA kona hivi sasa katika nchi yetu, mjadala mkubwa ni vita dhidi ya madawa ya kulevya. Ni vita aliyoianzisha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda lakini sasa imesambaa nchi nzima na duniani pia, ni kama moto wa kiangazi kwenye pori lenye majani makavu.

Nani amesababisha madawa haya kusambaa dunia nzima? Nionavyo mimi leo niwaletee mtu aliyechangia sana dunia kutikisika kutokana na madawa ya kulevya, msome mtu huyo hapa.

Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari ndani ya milima hiyo ambayo sasa yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa Colombia.

Gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe na hata askari magereza ambao walikuwa wanalinda gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogelea gereza hilo hata umbali wa maili 12.

Kwenye gereza hilo pia kulikuwa na chumba maalumu cha michezo ya watoto maalumu kwa ajili ya watoto wa mfungwa huyo pindi akitembelewa na familia yake. Na pia ndani ya gereza kuliwekwa darubini (Telescope) ya kumuwezesha mfungwa huyo kuangalia katika mji wa Medellín ambako familia yake iliishi na kila siku jioni alitoka nje kibarazani kuongea naye kwenye simu huku akiwatazama kwa darubini hiyo.

Gereza hili lilijulikana kama La Catedral (The Cathedral) na lilimuhifadhi mfungwa huyo ninayemzungumzia aliyesababisha biashara ya mihadarati iwe jinsi ilivyo hivi leo duniani, mtu huyo ni Pablo Emilio Escober Gaviria au kwa kifupi Pablo Escobar kama ulimwengu ulivyomtambua.

Akiwa bado kwenye umri mdogo, Pablo mara kwa mara aliwaambia ndugu na marafiki zake kuwa anataka awe na utajiri wa kiasi cha pesa milioni moja za Colombia atakapofikisha umri wa miaka 22.

Ndoto hizi zilimfanya ashindwe kumaliza chuo kikuu alipokuwa anasoma Universidad Autónoma Latino Americana of Madellín na kujiingiza katika biashara za halali na haramu na hatimaye aliacha masomo chuoni. Moja ya biashara zake haramu za kwanza kabisa akiwa kijana chini ya miaka 21 ilikuwa ni kutengeneza vyeti bandia vya stashahada vya chuo alichokuwa anasoma na kuwauzia watu waliohitaji kwa ajili ya kwenda kupata ajira.

Pamoja na biashara hiyo pia Pablo alijihusisha na kusambaza mizigo ya sigara zilizokuwa haziruhusiwi nchini Colombia (Marlboro), akawa mhalifu. Kutokana na uzoefu wake wa ulimwengu wa kihalifu, Pablo aligundua kuwa zao la coca linalimwa nchini Bolivia ambalo linatumika kutengeneza Cocaine ni bora zaidi kuliko Coca inayolimwa nchini kwake Colombia.

Hivyo basi, Pablo akadhamiria kuwa kama anaingia kwenye biashara hii ya kusafirisha Cocaine ni lazima mihadarati yake iwe tofauti na bora zaidi kuliko Cocaine nyingine watu waliyozoea kutumia.

Akadhamiria kufanya Cocaine yake iwe daraja la kwanza ili kuvutia watumiaji na kufanya soko likue kwa haraka. Mwaka 1975 Pablo alisafiri mpaka nchini Bolivia kukutana na Roberto Suaréz Goméz ambaye marafiki zake walipenda kumuita El Padrino (The Godfather), kiongozi wa genge lililoitwa La Corparacíon (The Corporation).

Pablo alimpata na kumpa wazo Suaréz kuwa atumie ushawishi wake alionao serikalini akutane na kiongozi wa Cuba, Fidel Castro ili wamuombe aruhusu ndege zao za mizigo zitue kwenye viwanja vya ndege vya Cuba na kujaza mafuta, Castro aliwakubalia kwa sharti la  mihadarati hiyo isiuzwe ndani ya Amerika ya Kusini bali isafirishwe na kuuzwa Marekani ambapo alisisitiza kuwa atafurahi akiona vijana wa mabepari wakiharibika akili kwa mihadarati.

Baada ya Cocaine ya Pablo kuingia kwenye soko Marekani uhitaji na biashara ya mihadarati ya Cocaine ilipaa kwa kasi ya ajabu na Pablo Escobar akaanzisha rasmi genge lake la biashara ya mihadarati na akaliita Medellíne Cartel. Ili kufanikisha usafirishaji wa mihadarati yake kwa ufasaha na uhakika, Pablo alinunua ndege za mizigo 15 za ukubwa wa kati na helikopta sita.

Pia alinunua nyambizi (submarines) ndogo. Hadi kufikia mwaka 1985 Pablo alikuwa anasafirisha takriban tani 70 mpaka 80 za Cocaine kwa mwezi na alikuwa ameshikilia asilimia 80 ya soko la mihadarati la Marekani. Katika miaka ya 1990 utajiri wake ulifikia Dola za Kimarekani bilioni 30 na Jarida maarufu la Forbes lilimuorodhesha Pablo Escobar kama mtu namba tano tajiri zaidi duniani.

Moja ya vitu muhimu vya kihalifu alivyovifanya Pablo na kufanikiwa kuibuka kinara wa uhalifu Amerika ya Kusini ilikuwa ni kutekeleza sera yake aliyoianzisha ili kuidhibiti serikali na vyombo vya ulinzi ambapo sera hii aliita “Plata o Plomo”  (fedha au risasi)). Akiwa na maana kwamba kama wewe ni mtu wa serikali na ikitokea mmesigana basi atakupa fedha (rushwa) kama ukikataa kupokea basi anakupiga risasi kwa kutumia watu wake.

Aliwahi kukamatwa na alitoroka jela akawa anatafutwa. Baada ya mwaka mzima wa msako mkali hatimaye Desemba 2, 1993 jeshi la Colombia lilifanikiwa kunasa mawasiliano ya simu kati ya Pablo na wasaidizi wake.

Wakatumia ‘triangulation technology’ kung’amua mahali alipo katika Mtaa wa Los Olivos katika mji wa Madellín. Baada ya kufanikiwa kufahamu nyumba aliyojihifadhi pasipo kupoteza muda wakafanya shambulio la kushitukiza. Mlinzi wa Pablo alipigwa risasi na kufariki papo hapo na Pablo alipigwa risasi mguuni na akajikongoja mpaka juu ya paa.

Wanajeshi waliingia ndani walipanda juu ya paa na walimkuta Pablo amelala chini amefariki dunia akiwa na tundu la risasi aliyopigwa kwenye sikio na kutokea upande wa pili wa kichwa.

Marafiki zake wa karibu pamoja na kaka yake wa kuzaliwa wanasema kwamba siku zote Pablo alikuwa anasema kuwa hatakubali kupigwa risasi ya mwisho na adui yake, kama ikitokea ameshambuliwa na adui na hana namna ya kujiokoa basi atajipiga risasi sikioni itokee upande wa pili.

Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa Pablo katika dunia hii kwa kifupi sana,  ndiye aliyesababisha leo Makonda afanye anayoyafanya katika Dar yake mpya dhidi ya madawa ya kulevya.]

Polisi Watinga Nyumbani kwa Gwajima....Mwenyewe Agoma Kufungua Mlango › Jeshi  la Polisi kwa mara nyingine jana lilizingira nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima...

$
0
0
Jeshi  la Polisi kwa mara nyingine jana lilizingira nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa kile lilichodai kuwa lilifika kufanya uangalizi.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Askofu Gwajima mwenyewe, zinaeleza kuwa polisi walifika nyumbani kwake wakiwa katika gari lao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, polisi hao walipojaribu kutaka kuingia nyumbani kwa askofu huyo, walizuiwa mlangoni kwa sababu hawakuwa na kibali chochote wala maelezo yanayojitosheleza ya kutaka kukutana na kiongozi huyo wa kiroho.

Askofu Gwajima  jana alikiri polisi hao kumfuata nyumbani kwake na hivyo kulazimika kumtafuta wakili wake mara moja.

“Ni kweli walikuja wakiwa na gari la polisi, lakini walipofika nami nilimpigia mwanasheria wangu ambaye aliniambia tuwaulize wametumwa na nani na kama wana ‘search warrant’ (kibali cha kufanya upekuzi) au ‘arrest warrant’ (kibali cha kukamata),” alisema.

Askofu Gwajima alisema walipowauliza, walimtaja Afande Kingai kama ndiye mtu aliyewatuma, lakini hawakuwa na kibali chochote.

Kwa mujibu wa Askofu Gwajima, mwanasheria wake alifanya mawasiliano ya simu na Afande Kingai ambaye amepewa jukumu la kuwafuatilia wale wote waliotuhumiwa katika sakata la dawa za kulevya na kumuuliza sababu za kumfuata nyumbani.

“Afande Kingai amemweleza mwanasheria wangu kuwa walikuwa wamekuja kwa ajili ya ‘observation’ (uangalizi) tu, kwa hiyo mwanasheria wangu akasema kama ni ‘observation’ tu tusiwaruhusu kuingia ndani kwa sababu sheria ya hivyo hakuna, na sisi tumewazuia hawakuingia ndani,” alisema Askofu Gwajima.

Alipoulizwa kama kufuatwa kwake sasa na polisi kuna uhusiano wowote na kauli alizozitoa kanisani kwake hivi karibuni kuhusu elimu ya Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Gwajima alisema huenda ikawa hivyo, lakini akasisitiza kuwa hana uhakika kwa sababu hajazungumza na askari waliomfuata.

Na alipoulizwa kama anadhani ujio huo pia unatokana na andiko ambalo linasambaa kwenye mitandao ya kijamii ambalo linasema Jumapili ijayo mwalimu aliyemfundisha mtu mmoja anayetajwa kwa jina la Bashite atakuwapo kanisani kutoa ushuhuda, Askofu Gwajima alikana akisema andiko hilo si lake.

Pamoja na hayo, Askofu Gwajima alikwenda mbali na kuhoji: “Hata kama ni kweli, sasa unaogopa mwalimu kuja… kanisani kwangu wapo watu wengi waliosoma naye Bashite kuanzia shule ya msingi na Sekondari ya Pamba… vyeti kama huna huna tu.”

Alipoulizwa haoni kauli yake kwamba Rais Magufuli ni tofauti kabisa na Makonda ilikuwa na nia ya kuwatenganisha viongozi hao, Askofu Gwajima alisema aliyemtaja kwa kumshambulia ni Makonda na si Rais.

“Aliyenitaja kwa kunishambulia katika sakata la dawa za kulevya ni Makonda na si Rais, mimi nimemuongelea Makonda, mimi ni mtumishi wa Mungu siwezi kuongozwa kwa ‘speculation’, si unajua hata Yesu alisema kama wewe huna dhambi basi uwe wa kwanza kushika jiwe,” alisema Askofu Gwajima.

Alipoelezwa kuwa katika mahubiri yake ni kama anaonekana kumshtaki Makonda, askofu huyo alisema:“Nilisema nitamshtaki kwa mahakama iliyo juu yake na nilisema Makonda aombe radhi, angekuwa mstaarabu baada ya sakata lile yeye mwenyewe angenipigia simu na kuniambia Gwajima nilikengeuka, lakini hajafanya hivyo.”
 
Pamoja na hayo, Askofu Gwajima alisema kwa aliyoyafanya Makonda tayari amekwishamsamehe na ndiyo maana hajampeleka mahakamani.

Hali ya Rais Robert Mugabe Yazidi Kuwa Mbaya, Apelekwa Singapore

$
0
0
 Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe ameenda nchini Singapore kufanya vipimo vya Afya yake, siku chache baada ya sherehe ya kufikisha miaka 93.

Afya ya kiongozi huyo imekua dhaifu zaidi, na sasa anapata shida hata kutembea wakati wa matukio mbalimbali ya kitaifa.

Msemaji wa rais huyo alisema kuwa vipimo hivyo ni vya mara kwa mara na Rais anatarajiwa kurejea nchini Zimbabwe wiki ijayo.



Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images