Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Mwanangu Alikuwa Ananiuliza Baba Nifanye Kosa Gani ili Nije Tuishi Wote Gerezani – Godbless Lema

$
0
0

Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema ambaye amesota gerezani kwa zaidi ya miezi minne, amefunguka kwa mara ya kwanza kuwashukuru wale waliompigania huku akieleza stori ya kusisimua kuhusu mtoto wake.

Lema amedai anaenda kumuona mwanaye ambaye alitaka kufikia uwamuzi wa kutaka kufanya kosa ili na yeye aingie gerezani kukaa na baba yake.

“Leo nina mambo machache sana ya kuongea, ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani,” alisema Lema.

Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1.

Haya Ndio Aliyosema Mama Salma Kikwete Baada ya Kuteuliwa Kuwa Mbunge,Azungumzia Pia Heshima Yake kwa Jamii..!!!

$
0
0

Baada ya kupewa muda kuwasalimia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Mjini Lindi, Ilulu leo tarehe 3 Machi 2017; Pamoja na mambo mengine Mama Salma Kikwete amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge. Kwamba, tukio alilofanya Rais tarehe 1 Machi 2017 kwa kumteua kuwa mbunge limempa heshima kwake na mkoa wa Lindi kwa ujumla.

Utafiti;Huu Ndio Uwiano Sahihi wa Uke na Uume Wakati wa Kufanya Mapenzi ili Kila Mmoja Kufurahia Tendo

$
0
0

Huko nchini Canada wataalamu wa afya ya mapenzi wamefanya utafiti ili kubaini Uwiano sahihi wa papuchi na dushe unaoweza kuwafikisha wahusika kileleni.

Matokeo yameonyesha kuwa Uwiano huo lazima uwe 1:1 kwamba Ukiingiza uume kwenye uke inatakiwa ijae kwenye uke. Kusiwe na nafasi inayobaki, hata ya kuingiza kidole. Katika Wapenzi waliobainika kuwa na uwiano huu, wanamke waliohojiwa, 87% walikiri kufika kileleni wanapo fanya tendo la ngono. 13% iliyobaki walibainisha kuweka mkazo zaidi kuwa wangehitaji mda mrefu wa maandalizi kabla ya tendo kutokana na msongo wa mawazo walionayo.

Aidha, wataalam hao walibaini pia kwamba kwa wale wapenzi ambao uwiano wao wa uke na uume ni 1:2 na kuendelea (yaani uume ukiingizwa kwenye uke, bado kuna nafasi inabaki ya kuingiza kidole), ni 25% pekee ya wanawake ndio wanaofika kileleni wakati wa tendo. Tena zaidi kazi kubwa hufanywa na wapenzi wao wakati wa maandalizi.

Wataalamu pia walitafuta chanzo cha baadhi ya wanawake kutumia vifaa bandia vya uume. Walibaini kuwa wengi wao walinunua vile vifaa kwa saivi inayolingana na papuchi zao. Walipo wahoji hao wanawake, 72% walieleza kuwa walihitaji size ambayo inafiti kwenye maumbile yao. 

Hivyo, wataalamu walihitimisha kuwa uwiano wa 1:1 kati ya papuchi na dushe, unampa mwanamke nafasi kubwa ya kufurahia tendo na kufika kileleni.

Lakini pia kwa upande wa mwanaume, Japo utafiti ulionyesha kuwa wao wangeweza kufika kileleni hata kama uwiano ungekuwa 1:4. Lakini 94% ya wanaume walipendelea zaidi uwiano wa 1:1 kwa maelezo kuwa inaleta raha zaidi.

Vile vile utafiti ulionyesha kuwa sababu kuu ya wanaume kuwatongoza mabinti wadogo au hata wanafunzi ni katika harakati za kutafuta uwiano wa 1:1. Ambapo walidhani watapata maraha ya hali ya juu kulinganisha na uwiano wa 1:2 na kuendelea.

Awamu ya pili ya utafiti huu unaendelea ili kubaini njia zisizo na madhara zitakazo wasaidia wapenzi wawili kuwa na uwiano wa 1:1

Fahamu Wanachama wa Freemason Tanzania,Wako Wanasiasa,Wasanii na Madaktari Bingwa Nchini..!!!

$
0
0

Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali.

Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande.

Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo.

Alisisitiza kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba wenyewe wanakutana katika vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.

Alisema nchini kuna wanachama zaidi ya 600 wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli.

Alisema idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.

Chande alizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema duniani kuna watu wazito wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.

Akizungumzia masharti ya kujiunga na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.

Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.

“Unajua katika imani hii kuna michango mbalimbali ambayo unatakiwa kutoa ambayo ni zaidi ya dola milioni sita (karibu Sh bilioni 10), hivyo ni lazima ndugu wafahamu ili kuepuka matatizo utakapotakiwa kutoa,” alisisitiza.

Alisema si kweli kuwa wenye fedha wengi ni wanachama wa kundi hilo huku akikanusha wanachama wanajiunga kwa ajili ya kupata fedha, bali ni dini kama imani nyingine.

Alisisitiza kuwa hakuna ukweli kwamba wanaopata mafanikio katika maisha wakiwa ndani ya imani ya Freemasons kuwa wanatoa kafara watu wao wa karibu kwa lengo la kupata utajiri.

Chande pia alisema hairuhusiwi kutumia jina la kundi hilo kwa nia ya kujipatia nafasi sehemu mbalimbali au kuongeza nafasi katika chuo au shule.

Hizi Hapa Staili Mbalimbali za Mapenzi...!!!

$
0
0
Nimepita Sehemu fulani, nimeona kuna mzozo eti ni ipi staili nzuri saa ya kufanya mapenzi, kweli hili suala lina mitazamo mingi. Mimi nasema hivii, staili nzuri ya kufanya Mapenzi inategemea na Mwenza wako, mathalani mwenzio ni mnene au ana umbile kubwa huwezi ukamwambia ulale chini halafu akulalie juu, nadhani utakuwa unataka kuvunjwa kiuno kama sio kuteguka kabisa. Kiukweli ziwezi weka picha fulani hapa directly kwa ajili ya kulinda maadili, hivyo basi staili kulingana na umbile lako na la mwenza wako hutegemea na umri wenu pia, na ndio maana vijana hadi umri wa miaka 38 hivi ni wafanyaji wazuri wa mapenzi ukilinganishwa na watu wazima au wazee kabisa.

Yanga Yamtimua Rasmi Hans van Pluijm..

$
0
0

Leo Ijumaa February 3, 2017 uongozi wa Yanga umesitisha mkataba na mkurugenzi wao wa ufundi Hans van Pluijm.

Van Pluijm alikuwa kocha wa timu hiyo kabla ya kubadilishiwa majukumu kuwa mkurugenzi wa ufundi baada ya ujio wa George Lwandamina ambaye ndio kocha mkuu wa sasa.

Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinataja kuwa chanzo cha kuondoshwa kwa kocha huyo ni uhaba wa pesa unaoikabili klabu hiyo kwa sasa.

Udaku Blog inaendelea kupambana kutafuta sababu zilizopelekea Pluijm kupigwa chini na Yanga na habari kamili utaipata hapahapa.

Vyeti Kumng`oa Rc Makonda?

$
0
0

Sintofahamu! Jumapili iliyopita kwenye mahubiri ya ibada ya Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima alitoa madai mazito sana kwamba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda (36) anatumia cheti cha kidato cha nne cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge wakati yeye alianza darasa la kwanza mwaka 1988, akitumia jina la Daudi Albert Bushite.

Akihubiri huku waumini wake wakimsikiliza kwa umakini mkubwa, Mchungaji Gwajima alisema kuwa, mwaka 2001, Makonda alitumia cheti cha mwanafunzi huyo chenye divisheni 3 ya ponti 25 ili aweze kujiunga na Chuo cha Uvuvi Nyegezi (NFTI).

AMCHAMBUA KWA VYUO

Alisema kuwa, alisoma masomo ya certificate  na kuhitimu mwaka 2002 ambapo mwaka huohuo, akiendelea kutumia jina la Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo Cha Uvuvi Mbegani, Bagamoyo mkoani Pwani kwa masomo ya Diploma ya Uvuvi (ODMF, NTA LEV. 6) na kuhitimu mwaka 2005.

Gwajima alizidi kusema kuwa, mwaka 2006, Makonda alipata udahili Chuo cha Ushirika na Biashara, Moshi (wakati huo kikiwa Chuo Kikuu Kishiriki cha SUA) akiendelea kutumia vyeti vyake vya certificate ya Nyegezi na diploma ya Mbegani na akijulikana kama Paul Christian Muyenge.

NI JINA LA MAHAKAMANI?

Mchungaji Gwajima alizidi kudai kuwa, jina la Paul C.  Makonda, analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina na kwa hiyo, cheti cha kidato cha nne cha mheshimiwa kinasomeka, Paul C. Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C. Makonda baada ya kuapa mahakamani.

Kwa mujibu wa maelezo ya Gwajima, ana maana jina la Daudi lilikufa rasmi kwenye makahama na kuanza kuchipuka kwa jina la Paul.

NANI ANAINGIA?

Kwa mujibu wa Mchungaji Gwajima, mwanafunzi aliyeuza cheti hicho (Paul Christian Muyenge) anaingia kwenye kashfa ya kuuza cheti kama kweli mtu huyo yupo na ndiye mwanafunzi halali aliyekuwa akilitumia jina hilo mpaka mwaka 2001.

MKANGANYIKO WA GWAJIMA, PAUL CHRISTIAN

Wakati Gwajima akidai kuwa na nakala za vyeti vyote viwili vya Paul Makonda, vikiwemo vile alivyotumia kuanzia kidato cha nne, upo mkanganyiko mkubwa kutokana na maelezo ya Paul Christian (mtu aliyedaiwa kumpa vyeti Makonda) aliyoyatoa kwa gazeti moja la kila siku la hapa nchini.

Paul Christian, anayedaiwa kuwa ndiye ambaye cheti chake kilitumiwa na Paul Makonda aliliambia gazeti hilo;

“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari na jina wanavyolitaja (waliotunga taarifa ya mtandaoni) wanakosea kwani mimi naitwa Paul Pierre Christian Kagezi, hatuna uhusiano, mimi Mhaya yeye Msukuma.”

“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu?”Alihoji.

Cristian aliendelea kudai kuwa katika kidato cha tano na sita, alichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani angeshindwa kumudu huko alikokwenda.

Alihoji kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?

Alifafanua kuwa watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina yao, huku akiendelea kukanusha kuhusu taarifa hizo.

“Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa, kwani kwa mantiki nimekuuliza ukipata daraja la kwanza kidato cha sita lazima uende chuo kikuu?” alihoji.

“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mashiko.”

  

MKANGANYIKO (CONFUSSION) MKUBWA

Kufuatia madai hayo ya Gwajima ambayo yalikuwa ndani ya mahubiri yake, mitandao ya kijamii na mazungumzo ya watu mitaani, sehemu mbalimbali ya nchi, gumzo kuu likawa ni jina la; ‘Paul Muyenge na Daudi Bashite.’

Baadhi ya watu walionesha kushangaa kwao kama kweli Makonda anatumia cheti cha mtu mwingine huku akijua kuwa, serikali ya awamu ya tano chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli ilitangaza kupambana na watumishi wenye vyeti vya bandia.

“Hivi inawezekanaje Makonda akaendelea kutumia cheti cha mtu mwingine wakati mkuu wake wa nchi ni mkali kwenye eneo hilo? Hili jambo si la kulifumbia macho kirahisi tu, ni jambo zito. Gwajima akae na kujua kuwa, alitoa tuhuma nzito sana ambazo kama zinathibitika zina ukweli, Makonda anaweza kung’oka kwenye nafasi yake” alisema Bakar Msumari, mkazi wa Mbezi Mwisho.

HOTUBA YA MAGUFULI KUHUSU VYETI FEKI

Katika moja ya hotuba zake za kuonesha mwelekeo wa serikali yake, Rais Magufuli alisema kuwa, atakapogundua, mtumishi yeyote katika serikali yake anatumia vyeti feki, basi atamfukuza mara moja bila kujali ni nani (akimaanisha hatajali cheo). Na tangu aanze utawala wake, Magufuli amekuwa ni mtu anayesimamia kile anachokiongea.

“Ndugu zangu Watanzania katika hili la vyeti wala hawana sababu ya kuwa na hofu, tunachotaka sisi ni kujua je, huyu mtu anayelipwa kwa sababu ana masters, kweli ni yake? Kwa sababu kuna watu wanalipwa mishahara mikubwa kwa sababu ya vyeti vyao ambavyo kiuhalisia siyo vya kwao. Wewe kama umeishia darasa la saba, usihofu, utaendelea na kazi kama kawaida,” alisema Magufuli akimaanisha kuwa, hataki watumishi wenye vyeti feki.

Baada ya hotuba hiyo, watumishi wa umma wenye vyeti feki walianza kusakwa kote nchini, wakiwemo wa Mkoa wa Dar es Salaam na wale ambao wamebainika, walichukuliwa hatua na zoezi bado linaendelea.

UFUMBUZI NI UPI?

Baadhi ya watu waliamini kuwa, maneno ya Gwajima si jambo la kuwafanya waamini ni kweli kutokana na historia ya mtumishi huyo wa Mungu ambapo, amewahi kukwaa kesi mahakamani kufuatia kudaiwa kumtusi Kadinali Polycarp Pengo katika ibada moja aliyoifanya kwenye kanisa lake (wakati huo, Kawe).

Wengi walisema kuwa, alichokiongea Gwajima si ukweli kwa asilimia mia moja, bali mwenye ukweli ni Makonda mwenyewe ambaye wasomaji wanaamini ndiyo mwenye uwezo wa kuanika ukweli na kufuta madai ya Gwajima na ufumbuzi wa madai yake kujulikana.

Ijumaa liliweza kuongea na baadhi ya wasomaji ambao walisema kuwa, ni wakati muafaka kabisa kwa Makonda kuibuka na kuweka wazi au kujibu tuhuma za Gwajima ili mambo yaishe na maisha yaendelee.

“Gwajima si msemaji wa mheshimiwa Makonda, aliyoyasema si kwamba ndiyo ukweli. Kwani mara ngapi watu wanaibuka na kujifanya wanawajua wengine lakini baadaye inabainika kuwa si kweli?” alisema msomaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la David Mashaka, mkazi wa Salasala, Dar.

“Nilimsikia Gwajima, lakini sijakubaliana naye moja kwa moja. Makonda ndiye mwenye ukweli wote. Ufumbuzi wake ni kwamba, Makonda ajitokeze na kuweka wazi anachokijua yeye, siyo mtu mwingine tu amsemee,” alisema Omar Kishapu, mkazi wa Kimara Suka.

FAIDA ZA MAKONDA KUTOBOA UKWELI

Baadhi ya watu wamesema kuwa, Makonda kujitokeza na kutatua fumbo hilo kutaleta faida kwani atakuwa ameilinda serikali yake ya awamu ya tano lakini pia atakuwa amemsaidia Rais Magufuli katika kukitimiza kile anachokisimamia kama rais wa nchi.

“Inawezekana Makonda kuendelea kukaa kimya kukawapa watu neno la kumsema rais kwamba mbona hamchukulii hatua. Lakini kumbe hamchukulii hatua kwa sababu anaujua ukweli, lakini je wananchi wanaujua ukweli? Si mpaka Makonda mwenyewe auseme, akiuanika ukweli itampa heshima Magufuli na yeye mwenyewe pia ataendelea kuheshimika na kuaminika,” alisema  Maria Kaparasule, mkazi wa Boko, Dar.

IJUMAA NA VIONGOZI

Juzi, Ijumaa liliwatafuta baadhi ya viongozi ili wazungumzie madai ya Gwajima ambapo, awali Msemaji wa Tume ya Maadili ya Watumishi wa Umma, Honoratus Ishengoma alisema:

“Mimi kwanza kabisa nipo likizo. Lakini madai ya Gwajima kusema ule ukweli ni mazito sana. Hayo madai yanatakiwa kusemewa na Mkurugenzi wa Tume ya Maadili.”

Ijumaa lilimpigia simu, bosi wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma lakini hakupatikana hewani mara moja.

MEYA WA KINONDONI

Ijumaa lilimpigia simu, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta ambaye Gwajima alimtaja kuwa rafiki kipenzi wa Makonda lakini simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa hata iliporudiwa tena na tena.

PROFESA SEMBOJA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja yeye alipoulizwa kuhusu madai ya Gwajima alisema:

“Kosa la Makonda ni kutaja majina ya watu na kuwatuhumu kufanya hivi wakati hawajathibitika, sasa na sisi hatupaswi kurudia makosa hayo ya kumtaja kwa jambo ambalo hatuna uhakika nalo. Ni jukumu lenu nyinyi kama waandishi wa habari kuchimbua na kuja na majibu, je, vyeti hivyo ni feki au la.

“Hapa kuna hoja mbili, ya kuwa na vyeti feki au kutumia jina la mtu katika masomo yake. Mimi ni mtu mzima, wakati wetu, lilikuwa ni jambo la kawaida mtu kusomea jina la mtu mwingine, ambaye alishindwa kuendelea na masoma kwa sababu mbalimbali. Kama alisomea jina la mtu mwingine, lakini masomo alisoma yeye, sioni kama kuna tatizo, ila kama elimu aliyonayo hajawahi kuipata darasani, hilo ndilo tatizo.

“Mimi nadhani tujikite katika kumsaidia rais kwenye mambo magumu anayofanya, kwa sababu ndiye rais anayesimamia vitu kikamilifu, tusimchoshe kwa vitu vidogovidogo, kwangu mimi Makonda ni mchapakazi, huenda ndiyo maana anakutana na vigingi, lakini kwa kweli siwezi kusema lolote hadi ithibitike kosa lake hasa ni lipi.”

TUMEFIKAJE HAPA?

Februari 2 na 9, mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alianza zoezi la kutangaza majina ya watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya ‘unga’ kwa maana ya kuuza au kutumia. Kila aliyemtaja alitakiwa kufika Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ kwa mahojiano na polisi. Miongoni mwa watu waliotajwa ni Gwajima.

Gwajima alifika kituoni hapo na kuwekwa ndani kwa siku kadhaa kisha akaachiwa. Baada ya kuachiwa, alifanya mkutano na waandishi wa habari akionesha kusikitishwa kwake kwa Makonda kumtaja jina yeye akidai kuwa, hajawahi kutumia unga wala kuuza.

Kwa hiyo kumtaja kwake kwamba anatumia vyeti feki inaweza kuwa ni katika kutoa hasira au ‘kulipa kisasi’ dhidi ya Makonda.


Serikali Ivunje Ukimya Kuhusu Manji

$
0
0

Hakuna taarifa rasmi kutoka vyombo vya usalama kuhusu Manji, zaidi ya ile ya uhamiaji kuwa walikuwa wakimsubiri atoke hospitali Muhimbili ili wamlaze mahabusu. Wakati huo Manji alikuwa amelazwa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Manji alilazwa Muhimbili baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Dar es Salaam, alipowekwa mahabusu baada ya kutajwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, ingawa alifunguliwa kesi ya kutumia na siyo kuuza.

Habari zinasema Manji anaumwa matatizo ya moyo na amelazwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.

Wakati huohuo, zipo habari kuwa akaunti zake zimezuiwa. Nyingine zinasema Manji amekutwa na uraia wa nchi mbili.
Kampuni zake zinashindwa kujiendesha. Gazeti lake la Jambo Leo halijachapwa na kuingia mitaani kwa wiki nzima sasa. Angalau hili linathibitishika kwa urahisi.

Hapa ndipo kwenye utata kuhusu Manji na lazima tujadili kwa sababu Manji akiathirika, wanaothirika ni Watanzania wengi mno ambao maisha yao yapo kwenye ajira kupitia kampuni za Manji.

Shida ni kuwa Serikali haisemi kitu. Je, watu wa Manji wanaisingizia Serikali, kwamba yenyewe haijafunga akaunti hata moja ya Manji? Serikali inatakiwa itoke na kukanusha kusingiziwa huku.

Kama ni kweli akaunti za Manji zimezuiwa, maana yake hiyo ni kesi nzito mno. Na inapaswa kuelezwa kinagaubaga ili Watanzania wengine wajue kuwa nini ambacho kinamsibu Mtanzania mwenzao. Izingatiwe kuwa Manji ni mwekezaji mkubwa nchini.

Maana kama ni ile kesi ya uhamiaji mbona watuhumiwa walishapandishwa kizimbani na dhamana yao kuwekwa wazi?

Kilichosababisha akaunti za Manji zizuiwe ni nini? Je, ni ile kesi yake ya matumizi ya dawa za kulevya au ya uhamiaji? Mbona kesi hizo hazina uzito wowote wa kusababisha akaunti za mfanyabiashara mkubwa kama Manji zifungwe?

Nini kimesababisha? Serikali iseme, kufanya vitu kimyakimya si vizuri kwa uendeshaji wa nchi. Manji ni Mtanzania, hata kama angekuwa siyo Mtanzania, vema kama anakuwa na matatizo ya kisheria yasemwe na mchakato uonekane ukitendeka.

Serikali ijiepushe na nyenendo ambazo itaonekana inafanya vita binafsi na raia wake.

Ndimi Luqman
@luqmanmaloto

Kamanda Wema Sepetu kwenda Arusha kuonana na Godbless Lema

$
0
0


Kamanda Wema Sepetu Jumamosi hii ataelekea mkoani Arusha kwajili ya kuonana na mbunge wa Arusha, Godbless Lema ambaye ameachiwa kwa dhamana Ijumaa hii baada ya kusota gerezaji kwa miezi nne.

Muigizaji huyo ambaye ana wiki moja na nusu ndani ya Chadema toka arudishe kadi ya CCM, amedai kesho atasafiri kwenda mkoani Arusha kuonyesha ushirikiano.

“Mungu ni mkubwa, ni furaha kusikia Mh. Godbless Lema amepewa dhamana. Najua ulipitia wakati mgumu sana, najua ulikuwa mbali na familia yako, watoto wako, rafiki zako, makamanda wenzako na zaidi wananchi wako wa Arusha na Watanzania kwa ujumla. Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano,” aliandika Wema Instagram.

Aliongeza, “Kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho i’ll be in Arusha kuonyesha Solidarity “FOR TO BE FREE IS NOT MERELY TO CAST OFF ONE’s CHAINS, BUT TO LIVE IN A WAY THAT RESPECTS AND ENHANCES THE FREEDOM OF OTHERS” – NELSON MANDELA #CallMeKamanda,”.

Rais Magufuli "Ampa Adhabu" Nzito Mkandarasi...!!!

$
0
0

Akiendelea na ziara yake mkoani Lindi, Rais Dkt Magufuli  amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo na kutoa maagizo ili kuhakikisha wananchi wananufaika na jitihada za serikali za kuboresha maisha yao.

Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Godfrey Zambi kumnyang’anya pasi ya kusafiria (passport) Mkandarasi anayeshughulikia Mradi wa Maji wa Ngapa hadi hapo atakapokamilisha mradi huo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokwenda kukagua mradi huo wa maji ambao hadi sasa umetumia miaka 6 kujengwa lakini bado haijakamilika. Pamoja na kuagiza pasi ya mkandarasi ichukuliwe, Rais Magufuli amempa miezi miwili mkandarasi huyo kuhakikisha mradi unakamili huku RC Zambi akiwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mkandarasi hatoki eneo hilo la mradi.

Mradi huo unaotarajiwa kumaliza tatizo la maji mkoani Lindi umegharimu TZS bilioni 29 ambapo hadi sasa mkandarasi amelipwa bilioni 21. Rais Magufuli amesema kuwa kama tatizo ni fedha ndio sababu mradi haumaliziki aambiwe ili atoe fedha serikali kuu kukamilisha wananchi waweze kupata maji.

Mradi huo wa maji ukikamilika unatarajiwa kuzaliwa maji zaidi ya lita milioni 6 kwa siku.

Rais Magufuli anatarajiwa kukamilisha ziara yake mkoani Lindi leo jioni ambapo ataanza safari ya kwenda mkoani Mtwara atapofanya ziara yake Jumamosi na Jumapili. Katika kuhitimisha ziara yake ya siku nne katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, Rais Magufuli atahutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Makada wa Chadema Watimkia CCM..!!!

$
0
0

Makada 15 wa Chadema waliojitambulisha kuwa viongozi wa chama hicho Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza  wamehama chana hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Makada hao wakiongozwa na Damas Kimenyi aliyejitambulisha kuwa Katibu Chadema wa Wilaya hiyo walitaja kuridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli na mbunge wa jimbo la Ilemela, Angelina Mabula kuwa miongoni mwa sababu za kujiunga na CCM.

Wanachama hao wapya walipokelewa katika ofisi za CCM Wilaya ya Ilemela leo (Alhamisi) jioni wakati wa hafla iliyoongozwa na Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Nelson Mesha.

Hata hivyo, Katibu Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Meshack Micus amesema waliohamia CCM walishavuliwa uongozi tangu Januari 18, mwaka huu wakati wa kikao cha Mkutano Mkuu wa wilaya ambacho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.

“Hao ni wanachama wa kawaida na pengine wameondoka kwa hasira ya kuvuliwa madaraka baada ya Mkutano Mkuu kuunda kamati ya muda ya uongozi chini ya uenyekiti wa Warioba Wanzagi na Katibu wake Peter Kaiza,” amesema Micus.

Wengine waliojiunga na CCM ni Lukas Syrilo (Katibu wa Baraza la Vijana Bavicha), Agnes Majora (Katibu wa Baraza la Wanawake, Bawacha), Lucy Kazungu (Mwenyekiti Bawacha), na Edwine Sarung aliyejitambulisha kuwa Mweka Hazina.

Pia wamo Philipo Richard Mjumbe wa kamati tendaji wa Wilaya, Ester Ayoub Makamu Mwenyekiti wa wazee Wilaya, John Haule Mwenyekiti Bavicha, Vestina Johnson Mjumbe wa Bawacha Wilaya na Yohana Emanuel Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya.

Mwanangu Alikuwa Ananiuliza Baba Nifanye Kosa Gani ili Nije Tuishi Wote Gerezani – Lema

$
0
0

Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema ambaye amesota gerezani kwa zaidi ya miezi minne, amefunguka kwa mara ya kwanza kuwashukuru wale waliompigania huku akieleza stori ya kusisimua kuhusu mtoto wake.

Lema amedai anaenda kumuona mwanaye ambaye alitaka kufikia uwamuzi wa kutaka kufanya kosa ili na yeye aingie gerezani kukaa na baba yake.

“Leo nina mambo machache sana ya kuongea, ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani,” alisema Lema.

Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1.

Mbunge Asusa Akipinga Zawadi ya Pikipikii...!!!!

$
0
0
MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM) amelazimika kutoka katika kikao cha baraza la madiwani, ikiwa ni hatua yake ya kupinga Kaimu Mtendaji wa kata ya Kipili, Justine Jordan, kukabidhiwa zawadi ya pikipiki akitaka chombo hicho cha usafiri kiwe mali ya serikali na si ya mtu binafsi.

Tukio hilo lilitokea kabla ya kuahirishwa kwa baraza hilo la madiwani lililoketi katika Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi wakati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sumuni Mwanakulya alipokuwa akimkabidhi Jordan pikipiki aina ya SNLG namba MC 611BNP ya thamani ya zaidi ya Sh milioni mbili.

Jordan ambaye pia ni Ofisa Ugani alizawadiwa na halmashauri ya wilaya hiyo pikipiki hiyo baada ya kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kata yake.

Alikusanya zaidi ya Sh milioni 50 kati ya Sh milioni 100 alizopangiwa.

Mwenyekiti Mwanakulya alipolitangazia baraza hilo la madiwani kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imeamua kumzawadia Jordan pikipiki hiyo, baadhi ya madiwani walihoji uhalali wa zawadi hiyo wakitaka isiwe mali ya mtu binafsi bali iwe mali ya serikali.

Kutokana na hali hiyo, mbunge Keissy alisusa tukio hilo kwa kutoka ukumbini.

Mwanakulya alisisitiza kuwa halmashauri imemzawadia pikipiki hiyo Jordan na inakuwa mali yake huku akiwataka madiwani wasiwe na roho za kwa nini.

“Huyu mtendaji ametukusanyia zaidi ya Sh milioni 50 kati ya Sh milioni 100 aliyopangiwa, kumzawadia pipikipi ya thamani ya Sh milioni mbili imekuwa nongwa, hivi hizi roho za kwa nini zinatokea wapi? Pikipiki hii ni mali yake binafsi,” alisisitiza.

Pamoja na mjadala kuibuka ukumbini kwa baadhi ya madiwani kutokubaliana na hatua ya mtendaji huyo kupewa pikipiki, madiwani wengine walimmwagia Jordan sifa kwa kuweza kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika kata yake ya Kipili kwa uaminifu huku wakiwataka wengine waige mfano wake.

Akichangia, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo aliwakumbusha madiwani hao kuwa uamuzi wa kumzawadia Jordan pikipiki hiyo ulifikiwa katika vikao halali vya halmashauri hiyo.

Jordan licha ya kuishukuru halmashauri hiyo alisema kuwa mafanikio yake hayo yanatokana na yeye kuzingatia sheria na viwango vya ukusanyaji wa mapato ya ndani.

“Nilikuwa naamka usiku wa manane nawaomba wenzangu wajitume, kazi hii ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ina lawama nyingi ila wasiogope kutekeleza majukumu yao,” amesema Jordan.

Magufuli: Majambazi Lazima Watakamatwa..!!!

$
0
0

RAIS John Magufuli amesema kundi la majambazi linaloendesha mauaji mkoani Pwani hasa katika wilaya za Mkuranga na Kibiti halitapenya, bali litakamatwa kokote waliko.

Amesema amani ni jambo la msingi katika uwekezaji na akawataka wananchi kuwaambia ndugu zao ambao wanawafahamu kwamba wanafanya vitendo hivyo, kuacha mara moja.

“Hawatapenya, vyombo vya ulinzi na usalama viko imara, hapo walikuwa wanajaribu kupiga mruzi tu,” alisema Rais Magufuli jana asubuhi alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga wakati wa kuweka jiwe la msingi la Kiwanda cha Vigae cha Good Will.

Alisema nchi inahitaji amani ili wawekezaji waje kwa wingi, kuwekeza miradi mbalimbali.

Alisema Mkoa wa Pwani umebadilika kutokana na viwanda vingi kujengwa mkoani humo na kusaidia kupunguza tatizo la ajira. “Wilaya ya Mkuranga peke yake ina viwanda 83, naambiwa Mkoa wa Pwani una viwanda zaidi ya 200, haya ndio maendeleo tunayotaka, akitokea mtu anahatarisha uwekezaji huu lazima tushughulike naye,” alisema Rais Magufuli.

Aliwahakikishia wawekezaji wa kiwanda hicho cha GoodWill Tanzania Ceramic Co. Ltd kuwa amani itakuwepo eneo hilo na wasifikirie kwenda kujenga viwanda vingine nje ya Tanzania, bali waendelee kujenga viwanda vingine vingi katika wilaya hiyo.

“Jengeni hapa viwanda vingi, bahati nzuri sisi ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, soko la ukanda huu ni kama watu milioni 500, hivyo kuna uhakika wa soko la bidhaa zenu, hivyo jengeni viwanda vingi hadi huko baharini,” alisema Rais Magufuli.

Kiwanda cha Vigae cha Good- Will kinatumia gesi asilia na asilimia 95 ya malighafi ya kiwanda hicho, inapatikana eneo hilo na asilimia tano tu ndio inayoagizwa kutoka China.

Kina uwezo wa kuajiri watu kati ya 1,000 na 1,500. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesisitiza kwamba kama kuna wananchi wanasubiri chakula cha bure kupelekewa na serikali, watakufa kwa njaa kwani hakuna vya bure chini ya utawala wake.

“Hizi kauli zilizokuwa zinatolewa huko nyuma eti hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa, mimi siiungi mkono. Sasa nasema chini ya utawala wangu kuna watu watakufa kwa njaa wasipofanya kazi. Lazima tuambiane ukweli,” alisema Rais Magufuli.

Makonda, Cheti Feki na Dawa za Kulevya...

$
0
0


Zipo sauti nyingi zinapazwa kuwa kelele za cheti zinasababishwa na vita ya wauza dawa za kulevya. Sikubaliani na hoja hiyo, ingawa naweza kukubali kwamba watu wasiompenda Makonda kwa sasa wamepata fimbo ya kumcharaza hasimu wao.

Usiseme vita ya wauza dawa za kulevya ni ngumu ili kuhalalisha cheti bandia cha Makonda kama kweli anacho. Mtetee Makonda kwa kujibu hoja zote zinazotolewa. Kwamba safari nzima ya kielimu ya Makonda ni halali na haina doa. Huo ndiyo utetezi unaopaswa kutolewa kwa wakati huu.

Hao wauza dawa za kulevya ni akina nani mpaka wawe huru kumshambulia Makonda? Huu ni utoto ambao kwa watu wenye fikra timamu wanajisikia vibaya kuusikia ukisemwa kumtetea Makonda.

Kama kweli Makonda alighushi cheti, basi dhambi yake isifunikwe kwa kisingizio cha wauza dawa za kulevya. Uhalifu mmoja siyo pepo ya uhalifu mwingine.

Uhalifu wa kughushi cheti siyo pepo dhidi ya uhalifu wa biashara haramu ya dawa za kulevya. Wote ni uhalifu. Kwa hiyo dhambi ya kughushi cheti ya Makonda (kama kweli ameitenda), haipaswi kufichwa kwenye kivuli cha mapambano ya dawa za kulevya.

Kwanza muuza unga gani huyo anayepambana na Makonda? Maana wote aliowataja wapo mitaani, hakuna hata mmoja ambaye alithibitika.

Hivyo basi, kusema Makonda anashambuliwa na wauza unga ni kuwaonea wale waliotajwa kisha wakabainika kuwa hawahusiki. Watu wasihukumiwe kwa makosa ambayo hayajathibitishwa na mahakama.

Tena kwa maneno haya ni matusi hata kwa Serikali, kwamba wauza unga walikamatwa, wakaishinda Serikali na sasa wanaendesha vita dhidi ya Makonda. Haya siyo maneno mazuri kuzungumzwa.

Nayasema haya kuweka sawa huu mjadala. Ni vizuri hasa Makonda ajitetee na ashinde hii vita dhidi yake ili kama kijana awe na safari njema ya kiuongozi. Na kama ni kweli dhambi inayotajwa kaitenda, basi vita ya dawa za kulevya isiwe chimbo la kujifichia.

Ndimi Luqman MALOTO

Magufuli Asifia Uzuri wa Mama Salma Kikwete..Vichwa vya Habari Magazeti ya Leo 4/3/2017..!!!

Shinda Gari Bure Kutoka Kampuni ya Magari Hapa Tanzania

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi Hawa Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..


Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Mwisho wa Kujisajili ni 22 / 3 / 2017

Hali ya uchumi Yaifanya Yanga Kuachana na Hans Pluijm...!!

$
0
0

Matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Yanga, yamesababisha timu hiyo kuachana na mkurugenzi wake wa ufundi, Hans Pluijm.

, Pluijm amethibitisha kupokea barua kutoka kwa uongozi wa timu hiyo ambao umeamua kuachana naye ili kupunguza gharama.

“Ni kweli nimepokea barua kutoka kwa uongozi ya kutoendelea kuhitaji huduma yangu kutokana na matatizo ya kifedha yayonaikabili klabu hiyo kwa sasa,” alisema Pluijm.

Aliongeza, “Kuhusu mipango iliyo mbele yangu siwezi kuiweka wazi kwa sasa ila nitawafahamisha nini kitafuata ndani ya muda mfupi ujao. Ninawashukuru kwa ushirikiano mkubwa nilioonyeshwa kwa siku zote nilizokuwepo hapa.”

Alipotafutwa ili kuthibitisha taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa aliomba atafutwe baadaye kwani alikuwa kikaoni.

Watumishi 2,059 Watinga Dodoma Awamu ya Kwanza..!!!

$
0
0

Jumla ya watumishi wa umma 2,059 wameripoti Dodoma katika awamu ya kwanza ya kuhamia mjini humo  ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati akikabidhiwa uenyekiti wa CCM, Julai 22, mwaka jana.

Awamu ya kwanza ya Serikali kuhamia makao makuu Dodoma inajumuisha mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao, baadhi ya wakurugenzi pamoja na wasaidizi wachache.

Hayo yamebainishwa jana (Ijumaa) katika kikao cha kazi cha mawaziri na naibu mawaziri kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma chini ya uwenyekiti wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wanajeshi Wanywa Damu ya Cobra Kambini...!!!

$
0
0

Wanajeshi wa Kimarekani zaidi ya 3000, wapo katika mafunzo ya kijeshi huko Sattahip, Thailand yanayohusisha kunywa damu ya nyoka aina ya Cobra na kumchinja kuku hai kwa mdomo.

Wanajeshi hao wa jeshi la Wanamaji na mabaharia walioshiriki mafunzo ya siku kumi walifanya jaribio la kukata kichwa cha kuku mzima kwa mdomo na wanyama wengine jamii ya reptilia.

Kiongozi wa Jeshi la Wanamaji, Harry B. Harris alisema katika taarifa yake kuwa mafunzo hayo yanajumuisha namna ya kukabiliana na wanyama wa porini, kujihami na wanyama mazoezi makali ya moto.

“Kunywa damu ya cobra ni sehemu ya mafunzo ya kukabiliana na mazingira ya porini.” alisema Harris

Pamoja na Marekani, nchi nyingine zilizoshiriki katika mafunzo hayo makali ni Thailand, Singapore, Japana, Indonesia na Malaysia.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images