Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Diamond Platnumz Ana Roho Mbaya Sana na Kinyongo, Tanzanite Afunguka

$
0
0

Kukumbusha tu Tanzanite alipata jina miaka kadhaa iliyopita baada ya kuurudia wimbo wa Diamond, Mbagala na kudai ulikuwa wake huku pia baadaye akimtuhumu kumroga. Shutuma hizo zilimkera sana Diamond. “Nakutanaga naye [Diamond] lakini si mtu ambaye labda ananipa ushirikiano,” Tanzanite ameiambia Bongo5.

Muimbaji huyo amedai kuwa ugomvi wake na Diamond hadi leo unamwathiri kiasi cha baadhi ya wasanii kukataa kufanya naye kazi. “Lakini pia kitu ambacho kinanishangaza kwamba dah sijui labda tasnia yetu inaenda wapi, sijui sisi Watanzania tunakuwa na roho gani. Kwasababu ile kitu niliyofanya, inafika time sasa hivi kuna msanii nataka nifanye naye kazi anakataa kwasababu hiyo,” ameeleza. “Yupo msanii ambaye niliwahi kutaka kushirikiana naye akasema ‘bwana mimi naogopa uligombana na jamaa [Diamond]. Mimi sijafanya kitu kibaya kiukweli. Ukiangalia cover ni vitu ambavyo vinafanyika, sijui kibaya kilikuwa ni nini.” Tanzanite aongea kwa uchungu na kudai Diamond aache roho ya kinyongo Kwani ni roho Mbaya.. Anahitaji wamalize tofauti.

Toa maoni yako mdau.

Mama Wema Sepetu Matata Polisi..Kisa Kutaka Kumtapeli Nyumba Msama ..

$
0
0

DAR ES SALAAM: Msala tena! Miriam Sepetu, mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu, amejikuta mikononi mwa polisi, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.

Chanzo kimelidokeza gazeti hili kuwa mama huyo amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay, akidaiwa kumtapeli mfanyabiashara Alex Msama, kiasi cha fedha kinachotajwa kufikia shilingi milioni 16.
* “Mama Wema alipatwa na matatizo, akataka kuuza nyumba yake ile ya Sinza Lion, sasa katika kutafuta wateja akakutana na Msama, lakini Msama akamwambia kwa wakati ule alikuwa hana hela, lakini kuna mkopo wake katika benki moja ulikuwa umeiva, hivyo avute subira kidogo angeinunua nyumba hiyo (bei haijatajwa). “Wakakubaliana, sasa mama akamwambia Msama hata hivyo ana shida kidogo ya hela, basi jamaa akawa anampa mara leo milioni mbili, mara tatu hadi zikafika hizo 16, lakini ghafla Msama akaja kusikia ile nyumba imeshauzwa kwa mtu mwingine, alipofuatilia akakuta ni kweli, kumuuliza mama akawa haeleweki hadi jamaa akaamua kwenda polisi,”kilisema chanzo hicho. *

Ili kuweka sawa mambo hayo, Risasi Jumamosi lilifika nyumbani kwa mama Wema, Sinza Mori Jumanne iliyopita, lakini lilizuiwa kuingia ndani kwa maelezo kutoka kwa mlinzi kuwa mama hakuhitaji kuonana na mtu yeyote siku hiyo. Kesho yake, alipigiwa simu yake ya mkononi na akaipokea, lakini mwandishi alipojitambulisha na kuanza kumsomea tuhuma hizo, alisema hana muda wa kuzungumzia jambo hilo kabla ya kukata simu.
*

Kwa upande mwingine, Risasi Jumamosi lilifika ofisini kwa Alex Msama, iliyopo Kinondoni Block 41, lakini mfanyabiashara huyo hakuwepo. Mmoja wa maofisa wa ofisi hiyo, ambaye alikataa utambulisho wake kwa kuwa siyo msemaji wa Kampuni ya Msama Promotions, alikiri kuwahi kumsainisha mama Wema kiasi cha shilingi milioni tatu. Hata hivyo, gazeti hili lilimfikia Msama kwa njia ya simu yake ya mkononi na alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema; “Ni kweli nimetapeliwa na mama Wema, lakini kwa kuwa jambo hili nimeshalifikisha polisi, nadhani mkondo wa sheria utafuatwa,” alisema na kuomba asilizungumzie zaidi suala hilo. Jalada la shauri hilo limefunguliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay kwa namba OB/RB/3358

Hamorapa kuhusu Ishu ya kumpigia Alikiba Magoti

$
0
0


"Mi sijali watu watakaosema mimi ni team Kiba kwa kuwa niliamua kumpigia Alikiba magoti ile ilitokana na heshima na amefanya vitu vikubwa na kuwakilisha nchi yetu vizuri, kwa mimi namuhusudu saana Ali Kiba". Hayo ni Maneno ya Hamorapa Akiongea kupitia eNewz ya EATV, kuhusu maneno ya watu kuwa ameamua kujiweka upande wa Alikiba ingawa ameshindwa kujizuia kuonesha mahaba yake kwa msanii huyo.


Harmorapa aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kufananishwa na msanii kutoka kundi la WCB Hamonize amesema hana mpango wa kubadilisha jina lake "labda iongezeke a.k.a tu"


Hata hivyo Hamorapa amewapa ujumbe watu ambao wamamsema vibaya kwamba hawezi kuimba, wanapaswa kutambua kwamba wanavyomsema vibaya wanamfanya aongeze juhudi na kujua vingi kila siku kwa kutumia zile 'diss' wanazompa.

Serikali ya Guinea Yagundua Wanafunzi Hewa 47,000 Katika Vyuo Vikuu vya Nchi Hiyo..!!

$
0
0

Mamlaka nchini Guinea imesema kuwa kuna zaidi ya wanafunzi bandia 47,000 katika vyuo vikuu vya taifa hilo.

Takwimu hizo zilichapishwa siku ya Alhamisi na waziri wa elimu ya juu baada ya usajili wa kielektroniki.

Mpango huo uliwafutilia mbali wanafunzi hewa.

Mamlaka ya Guinea hutoa ruzuku kwa vyuo vikuu kulingana na idadi ya wanafunzi.

Waandishi wa habari wanasema vyuo vikuu vya umma vimejaa na ruzuku hizo hutolewa kushinikiza upanuzi katika vyuo vikuu vya kibinafsi.

Hatahivyo baadhi ya vyuo vya kibinafsi vimeongeza idadi bandia ya wanafunzi ili kupata ruzuku zaidi.

Hakuna tamko lolote la vile serikali itakavyokabiliana na madai hatua hiyo

Harmorapa Akataa Kata Kata Kubadili Jina Lake...!!!!

$
0
0

Msanii wa Rap Harmorapa aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kufananishwa na msanii kutoka kundi la WCB Hamonize amesema hana mpango wa kubadilisha jina lake "labda iongezeke a.k.a tu".

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Hamorapa amesema maneno ya watu kuwa ameamua kujiweka upande wa Alikiba ingawa ameshindwa kujizuia kuonesha mahaba yake kwa msanii huyo.

"Mi sijali watu watakaosema mimi ni team Kiba kwa kuwa niliamua kumpigia Alikiba magoti ile ilitokana na heshima na amefanya vitu vikubwa na kuwakilisha nchi yetu vizuri, kwa mimi namuhusudu saana Ali Kiba". Alisema Hamorapa".

Hata hivyo Hamorapa amewapa ujumbe watu ambao wamamsema vibaya kwamba hawezi kuimba, wanapaswa kutambua kwamba wanavyomsema vibaya wanamfanya aongeze juhudi na kujua vingi kila siku kwa kutumia zile 'diss' wanazompa.

Jokate Ajibu Baada ya Alikiba na Mama Yake Kumkana,,!!!

$
0
0

Baada ya kuulizwa kwenye kipindi cha clouds 360 anachukuliaje Ali Kiba na mama yake kumkana kwenye mapokezi ya msanii huyo, mrembo Jokate alijibu "Mimi kila kitu nachukulia positive unaambiwa tenda wema nenda zako, kwanza sitaki kuamini kwamba walimaanisha, labda waliteleza au walikosea script."

Jokate aliongeza yupo single na ameanza kutamani kuwa na mtoto.

Alichokisem Muimbaji Gwiji Afrika Yvonne Chaka Chaka wa Afrika Kusini Kuhusu Rais Magufuli...!!!!

$
0
0

Mwimbaji mashuhuri duniani na hasa katika bara la Afrika, Yvonne Chaka Chaka amesema anatamani sana katika maisha yake kukutana na Rais Magufuli. 

Mwimbaji huo amesema Rais Magufuli anaugusa moyo wake kutokana na utendaji kazi wake na ameshauri marais wengine wajifunze kutoka kwake kutokana na utendaji kazi wake.

Amemalizia kwa kumpongeza Mama Salma Kikwete kwa kazi nzuri anazozifanya katika kusaidia watoto hasa wasichana katika kupata elimu.

Rc Makonda Aaanzisha Bifu Jipya na Waziri Lukuvi..Habari za Vichwa vya Magazeti ya Leo 5/3/2017..!!!


Mbeya City Waisafishia Njia Yanga Njia ya Ubingwa

$
0
0

Mbeya City wamaliza mchezo, kazi kwenu Yanga
KLABU ya Simba imeng’ang’aniwa na Mbeya City huku ikilazimishwa sare kutoka sare ya bao 2-2, katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Mbeya City ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Nchimbi baada ya Raphael Alpha kuuacha mpira nyuma na yeye kuuwahi.


Hadi mapumziko, Mbeya City walikuwa wakiongoza kwa bao 1 huku Simba wakiwa hawajapta kitu. Kipindi cha pili Simba walirudi na ari mpya huku wakishambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kusawadhisha kunako dakika ya 65 kupitia kwa Ibrahim Ajib mara baada ya kuchonga mkwaju mzuri wa adhabu.


Mchezo ukawa wa kushambuliana kwa zamu huku Simba wakiongeza nguvu zaidi. Dakika ya 79 Kenny Ally akaiandikia Mbeya City bao la 2 kabla ya Simba kusawadhisha tena kunako dakika ya 85 baada ya kichuya kucheza mkwaju mkali wa penati baada ya Zimbwe kuagushwa na Kabanda na kupigwa kadi ya njano.


Simba wanazidi kuongoza kwa pointi 55 na mabao ya kufunga 40 huku mbele ya Yanga wenye pointi 52  na mabao 49 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.


Sasa Ligi imenoga, sasa kazi kwao Yanga kuhakikisha wanashinda mechi zijazo ili kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Sophia Simba Aiaga UWT..!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sophia Simba leo amesema hana mpango wa kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine katika uchaguzi ujao.

Simba amesema hayo wakati wa mkutano wa wanawake wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Temeke.

Kabla ya mkutano huo yeye pamoja na wajumbe walitembelea wodi ya wazazi  ya hospitali ya Temeke na kufanya usafi.

"Leo wakati tukiadhimisha wiki hii muhimu ya wanawake duniani napenda kutumia fursa hii adhimu kuwatangazia wanachama wanawake wa CCM kwamba kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kutogombea nafasi hii ya uenyekiti taifa katika uchaguzi ujao",amesema.

‘Kada wa Chadema Aliyeuawa Shahidi Kesi Dawa za Kulevya’..!!!!

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amedai kuwa kada wa Chadema,  Anitha Kimario (44) aliyeuawa  alikuwa awe shahidi katika kesi moja dawa za kulevya.

Mutafungwa amesema kiini cha mauaji hayo kinachunguzwa.

Shauri hilo linamhusisha kinara wa usafirishaji wa bangi kwenda nchini Kenya, kupitia njia za panya zilizopo mpakani wilayani Rombo.

 Kamanda Mutafungwa amesema polisi wanachunguza mazingira ya mauaji hayo ili kubaini waliohusika, huku akisema watu wawili wanashikiliwa kwa mahojiano.

Mutafungwa amesema juzi jioni polisi waliokota mwili wa mwanamke huyo ambaye pia ni mfanyabiashara ukiwa umetupwa kwenye mashamba ya miwa.

“Tulipofika eneo la tukio tulikuta mwili wake ukiwa umewekwa kwenye matuta ya kupandia miwa ukiwa umefunikwa na majani na udongo, umevuliwa nguo na kubaki na za ndani,” amesema.

Kimenukaa...Nyumba ya Gwajima Yapigwa Picha na Polisi,Lengo Hili Hapa..!!!!

$
0
0

Wakili  Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu waKanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.

Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na kupekuwa nakupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo.

“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,” amesema Kibatala.

Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.

Mngongolwa amesema baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.

Auawa kwa Kudai Sh10,000..Kisa Kamili Hiki Hapa..!!!

$
0
0

kazi wa Kata ya Daraja Mbili, Mtaa wa Darajani, Baraka Rajabu (25), ameuawa kwa kuchomwa kisu na rafiki yake kwa madai ya deni la Sh10,000.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema Rajabu alichomwa kisu na rafiki yake eneo la Uwanja wa Robikoki hatua chache baada ya kutoka nyumbani kwa mtuhumiwa walikokuwa wakidaina fedha.

Awali, ilidaiwa kuwa Rajabu ambaye ni fundi ujenzi alikwenda nyumbani kwa rafiki yake kumdai fedha hizo za malipo ya viatu alivyomuuzia.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Daraja Mbili, Japhet Mmbinga alisema watu walioshuhudia tukio hilo walisikia majibizano kati ya wawili hao yakihusisha deni la Sh10,000.

 “Saa nane usiku wa kuamkia jana, mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa kwenye bustani za mboga. Hawa walikuwa marafiki na familia zao zote zipo mtaa wangu,” amesema mwenyekiti huyo

Makonda Amtemea Cheche Mange Kimambi na Genge Lake Wanaokesha Kumsema Mitandaoni,Adai Yeye Anainyoosha Dar Yake..!!!

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.

Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya kufa au kupona.

“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,” amesema Makonda.

Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.

“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.

Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.

Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.

Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.

“Nitoe pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.

Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na vijana wachapakazi.

“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na uhalifu,” amesema Makonda.

Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya Kigamboni tulivu na salama.

Amewaasa wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia vijana kuchungana wao wenyewe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya mazoezi.

Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Mbunge asimulia alivyoiba nguo ya ndani ya mama yake ili kujisitiri. Msikilize

$
0
0

Mbunge wa Viti Maalum Mara, Mh. Agness Marwa ameitaka serikali, wabunge pamoja na watu binafsi kuisaidia jamii ya watoto wa kike kupata pedi za kujisitiri, huku akitoa ushuhuda wa jinsi hali hiyo ilivyowahi kumfedhehesha akiwa shuleni.

Agnes amesema kampeni ya Namthamini imemgusa moja kwa moja kwa sababu fedheha za watoto wa kike wa kijijini wanazopitia anazifahamu na kuongeza kwamba yeye ni muhanga aliyewahi kupata mateso pale alipokosa taulo za kujisitiria wakati wa hedhi.

Agnes amesema wakati anaingia katika siku zake kwa mara ya kwanza hali hiyo ilimtokea akiwa shuleni, na hakuwa na vifaa vya kujisitiri kutokana na umasikini uliokuwepo nyumbani kwao.

"Baada ya kusikia kampeni hii ilinigusa sana na kunikumbusha kipindi hali hii imenikuta kwa mara ya kwanza, nilifedheheka sana kwa kuwa ilinikuta shuleni, na wakati huo hata kupata vifaa vya kujisitiria haikuwa kazi rahisi kwa kuwa umasikini ulikuwa mkubwa nyumbani, niliiba nguo ya ndani ya mama kujisitiria lakini bado haikunisaidia"Marwa.

Kutokana na tatizo hilo kuwa na athari kubwa kwa mabiti, mbunge huyo ameitaka jamii nzima ya watanzania kuunga mkono kampeni ya 'Nathamini' inayoendeshwa na kampuni ya East Africa Limited ikishirikiana na taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) iwafikie mabinti wengi zaidi nchini.  

Amesema endapo kampeni hiyo itafanikiwa, itasaidia mabinti hao kukuzwa katika mazingira ya furaha watafikia malengo na hata kuwa viongozi wakubwa wa taifa.

"Siyo kwamba nina fedha nyingi sana lakini nimeona ni vyema kutoa sehemu ya mshara wangu kuelekea siku ya wanawake nimthamini mtoto wa kike hata kama nitakunywa maji na mkate sintojali" - Alisema Marwa huku akikabidhi mchango wake

Gigy Money Afanyiwa Kitu Mbaya Mtandaoni

$
0
0

BAADA ya kuhakiwa akaunti yake Instagram, Msanii wa kuuza nyago kwenye Video Queen wa Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ameendelea kutapeliwa na vijana  wataalamu wa mtandao ambao wanatengeneza akaunti zenye majina yake na kuvuta baadhi ya mikwanja kwa kutumia jina lake.

“Kuna account imefunguliwa eti ina jina la @gigy_pesa, hiyo account siyo yangu. Account yangu ni hii @gigy_money baada ya ku hack ile nyingine. Hiyo ya @gigy_pesa ni matapeli, kuwa nao mbali” alimaliza Gigy

Diamond Ajibu Tuhuma za Wimbo wa ‘Salome’ Kujaa Matusi..!!

$
0
0

Maoni ya baadhi ya wadau wa muziki kuwa kila wanapousikiliza ‘Salome’ wa Diamond na RayVanny wanapata picha ya matusi, yamekutana na majibu ya Boss huyo wa WCB.

Akifunguka jana kwenye kipindi cha Ngazi Kwa Ngazi kinachorushwa na EATV, Diamond alisema kuwa ‘Salome’ haina matusi bali imebeba lugha ya mahaba mazito.

“Ukiangalia wimbo wa Salome, hauna matusi, ila una maneno ya kimahaba,” alisema Mond.

“Unapozungumzia wimbo wa kimahaba, matusi yanatokea pale. Matusi yapo kwenye mahaba. Unapokuwa unaelezea masuala ya kimahaba utaonekana kama unatukana. Lakini sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu mahaba yale kuyazungumza katika lugha ambayo ni ngumu sana mtu kuielewa,” alifafanua.

Kwa upande wake Ray Van, alisema kuwa pamoja na yote yanayosikika kwenye wimbo ule, wamejitahidi kutumia tafsida kuyaficha na ndio sababu wimbo ule unapendwa na watu wa rika zote na unaweza kusikilizwa hata katika jumuiya ya watu wanaoheshimiana.

Salome ni wimbo uliochukua mahadhi ya wimbo wa zamani wa Saida Kalori ‘Chambua Kama Karanga’ na umepata nafasi na mafanikio makubwa katika vituo vya runinga vya kimataifa na kuweka rekodi ya aina yake kwenye mtando wa YouTube.

Video ya Salome imeangaliwa zaidi ya mara milioni 13 na laki 7 kwenye YouTube.

Magufuli: Sitaki Mwekezaji Bandarini...!!!!

$
0
0

John Magufuli ameipiga marufuku Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kuingia ubia na mwekezaji katika uendeshaji wa bandari hiyo ujenzi wa gati namba mbili utakapomalizika kwa kuwa ujenzi huo umetumia fedha za ndani.

Amesema, ujenzi wa gati jipya katika Bandari ya Mtwara utafungua milango ya kiuchumi na kukuza kipato kwa wakazi wa Mtwara na serikali kwa ujumla.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jana alipokuwa anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa gati namba 2 katika Bandari ya Mtwara.

Amesema TPA wakiingia mkataba na mwekezaji katika utendaji kazi mara baada ya ujenzi huo kukamilika watakuwa wanainyonya serikali kwa kuwa imejenga miundombinu kwa fedha za ndani.

"Nisisikie hapa tena mmekaribisha mwekezaji...nitashangaa kweli yaani sisi tujenge kwa fedha zetu kisha mlete mwekezaji baada ya kukamilika kwa ujenzi, sitakueleweni kabisa,” ameonya Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya Mtwara kutaiwezesha kuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa na nyingi kwa wakati mmoja na hivyo kuharakisha shughuli za upakiaji na ushushaji wa shehena.

Amesema ujenzi wa bandari hiyo utagharimu Sh bilioni 137 na kuchukua miezi 21.

“Naipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa kuweza kutekeleza mpango wake wa uboreshaji wa miundombinu ya bandari nchini kwa kuanza na ujenzi wa gati Bandari ya Mtwara" amesema.

“Kukamilika kwa ujenzi wa gati hii kutafungua milango ya kiuchumi na kukuza kipato kwa wakazi wa Mtwara na serikali pia,” amesema Rais Magufuli.

Bandari ya Mtwara ina njia ya kuingilia meli yenye kina cha mita 20 na upana wa mita 250. Meli zenye urefu unaofikia mita 175 zinaweza kutia nanga bandarini bila msaada wa kuvutwa.

Hakuna masharti ya maji kupwa au kujaa kwa meli zinazoingia au kutoka bandarini. Eneo la ndani la kutia nanga lina kina cha mita 20 na uwezo wa kutia nanga meli nne kwa wakati mmoja. Bandari hiyo inayo maeneo ya kuhifadhia mizigo yaliyofunikwa na ya wazi yaliyojengewa ya mita za mraba 11,000 na 15,000 kwa mfuatano huo.

Bandari hiyo pia inashughulikia bidhaa za petroli zilizosafishwa na zisizosafishwa kwa ajili ya kampuni za utafutaji wa mafuta na gesi kupitia kwenye mitambo iliyofungwa upande wa gatini.

Ni kutokana na umuhimu wa bandari hiyo TPA, imeanza kuboresha miundombinu katika bandari hiyo ili kunufaika na fursa kubwa zilizopo katika mkoa huo wa Kusini.

Fursa zilizopo katika mkoa huo na ambazo zinatarajiwa kuinufaisha bandari hiyo ni pamoja na shughuli za watafutaji wa mafuta/gesi, uzalishaji wa gesi asilia na kuhudumia bidhaa zitokanazo na gesi.

Fursa nyingine zilizopo katika mkoa huo ni pamoja na kuhudumia bidhaa za viwanda vinavyojengwa mkoani Mtwara kikiwemo Kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote ambacho kinaendelea na uzalishaji na kuwa tegemeo kubwa kwa uchumi wa Tanzania.

Fursa nyingine ni mazao yanayopatikana Mtwara. Ujenzi wa gati jipya la kisasa katika Bandari ya Mtwara utaiwezesha kuhudumia meli za aina zote zenye urefu wa mita 300.

Ujenzi wa gati hiyopia utasaidia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo na kuiwezesha kuhudumia shehena kubwa zaidi ya mizigo. Hadi sasa imethibitika kuwa Bandari ya Mtwara ni moja kati ya bandari zenye usalama zaidi duniani.

Kuhusu utendaji wa bandari hiyo, katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2015/2016, shehena iliyohudumiwa katika bandari hiyo ni jumla ya tani 356,356 na 273,882.

Bandari ya Mtwara iliyojengwa miaka ya 1950 ni moja ya bandari zenye maajabu makubwa kutokana na kuwa na sifa ambazo bandari nyingi nchini hazina.

Zuio la Magufuli Laitikisa Acacia,Hisa Zake za Uingereza Zaporomoka Kwa Kasi ya Ajabu..!!!

$
0
0

Amri ya Rais John Magufuli ya kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini nje ya nchi umeitingisha kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Acacia inayomiliki migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.

Kila mwaka migodi hiyo husafirisha wastani wa tani 55,000 za mchanga huo unaojumuisha madini ya dhahabu, shaba, chuma, salfa na mekyuri na Rais ameagiza uchenjuaji wa mchanga wa madini ufanyike nchini.

Hii ni mara ya pili Rais Magufuli kutoa zuio hilo. Agosti mwaka jana akiwa Kahama alisema katika uongozi wake, hataki kuona usafirishaji wa mchanga huo. Machi 2 alitoa tena zuio hilo alipotembelea kiwanda cha Vigae cha GoodWill cha Mkuranga, Pwani, kinachotumia teknolojia ya kuchambua baadhi ya madini kwa ajili ya utengenezaji wa vigae.

“Watanzania tumekuwa tunaibiwa kwenye dhahabu, wanachukua mchanga wanausafirisha nje ya nchi, wakifika huko wanachambua dhahabu na mchanga unabaki hukohuko. Ule ni wizi, sasa naagiza hakuna kusafirisha tena mchanga nje ya nchi... tutajenga kiwanda hapahapa,” alisema.

Baada ya zuio hilo, taarifa ya Acacia iliyokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii ambayo ilithibitishwa na Makamu wa Rais wa kampuni hiyo Tanzania, Deo Mwanyika inaeleza kuwa Ijumaa wiki hii hisa za kampuni hiyo iliyoorodheshwa katika Soko la Hisa London, Uingereza zilishuka kwa wastani wa asilimia 20. Hadi jana jioni hisa hizo zilipanda tena kwa asilimia 10.

Mwanyika alisema wamepokea barua ya zuio hilo na kusema Acacia itafanya majadiliano zaidi na Serikali ili kufahamu zaidi juu ya utekelezaji wa agizo hilo.

“Inabidi kufanyike majadiliano, Acacia haikatai kuchenjua mchanga huo hapa ndani lakini siyo suala la kesho, itachukua muda kwa hiyo mchanga unaozalishwa sasa hivi ambao ni sehemu ya shughuli za uchimbaji itakuwaje! Je, utasitisha, utasimamisha mgodi?,” alihoji.

Hata hivyo, utafiti juu ya uwezekano wa Tanzania kuwekeza mtambo wa kuchenjua mchanga huo, uliofanywa na Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA) Februari, 2011 unaonyesha kuwa gharama za kusimika mtambo wenye uwezo wa kuchenjua wastani wa tani 150,000 kwa mwaka ni kati ya dola 500 milioni hadi 800 milioni.

Waziri Muhongo alinukuliwa na gazeti la The Citizen akiagiza kampuni zote kuanza uchenjuaji wa mchanga huo hapa nchini.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Madini na Nishati Tanzania (TCEM), Gerald Mtuli alisema nia ya Rais ni njema lakini inahitaji kampuni hizo kupewa muda.

Pia alisema kuwekeza mtambo huo ni hasara kwa mwekezaji kwa sababu kinachozalishwa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya mchanga unaotakiwa kuchenjuliwa.

“Mwekezaji hawezi kukubali hasara, ni sawa na unalima ekari moja ya nyanya halafu unataka mwekezaji, gharama za uendeshaji wa mtambo ni kubwa kuliko kile tunachozalisha, haina masilahi kwa hapa nchini,” alisema.

Pili, alisema endapo zuio hilo litaendelea, mgodi wa Buzwagi itabidi ufungwe kutokana na asili ya uzalishaji wake.

“Tani moja ya udongo unaochimbwa Buzwagi unatoa gramu mbili tu za dhahabu, maana yake uchafu ni mwingi hivyo ni lazima kusafirisha, Bulyanhulu itabidi kupunguza wafanyakazi ili kuepuka gharama,” alisema.

Aidha, Mtulia alisema upembuzi yakinifu ulifanyika mwanzoni wakati wa uwekezaji wa migodi hiyo na matokeo yalionyesha itahitaji kusafirisha mchanga huo kwa asilimia 30 hadi 40 nje ya nchi.

Pamoja na kuunga mkono zuio hilo la Rais Magufuli, Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti kutoka Taasisi ya Repoa, Dk Abel Kinyondo alisema, linaweza kujenga hofu kwa wawekezaji wengine.

Alisema kabla ya zuio hilo, kulihitajika majadiliano ya kina kati ya Serikali na wawekezaji hao.

“Rais ameibua mjadala mzuri na ametuma ujumbe wa hofu iliyopo kutonufaika na madini, kampuni zimebakiza muda mchache na mikataba iliyoingia inatia shaka, lakini zuio hili ni mara ya pili je, mara ya kwanza ilikuwaje wakaruhusu kuendelea na usafirishaji? Ili kuepuka hatari ya kupoteza wawekezaji wengine na kulinda Serikali ipate kilicho sahihi, ni lazima kukaa pamoja,” alisema.

Salma Kikwete Amefuata Nyayo za Hillary Clinton, Graca Machel...!!!

$
0
0

Uteuzi wa Salma Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais umeibua mjadala katika viunga mbalimbali nchini kutokana na ukweli kwamba hilo halikuwahi kutokea katika historia ya Tanzania, lakini kimataifa si jambo geni hata kidogo.

Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru, Rais John Magufuli alimteua Mama Salma ambaye ni mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa mbunge akiwa mteuliwa wa tisa kati ya nafasi 10 za kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Mama Salma ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, anaungana na wake wengine wa marais duniani kuingia kwenye nafasi za uongozi na siasa.

Hillary Clinton

Mwingine ni Hillary Clinton, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton. Mama huyo ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa na Demoratic kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni Marekani kabla ya kushindwa kwa Donald Trump, ambaye ni Rais.

Miaka minane iliyopita, Hillary alishindwa na Barack Obama katika mchujo wa kumpata mgombea urais wa chama hicho lakini baada ya Obama kuwa Rais, alimteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwanzoni mwa mwaka 2009. Mama huyo pia aliwahi kuwa Seneta wa New York mwaka 2000.

Graça Machel

Katika orodha hiyo pia yumo Graça Machel. Huyu ni mwanamke wa kwanza duniani kuwa ‘first lady’ wa marais wawili tofauti. Alikuwa mke wa Rais wa Msumbiji, Samora Machel kuanzia mwaka 1975 hadi 1986 na mke wa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela tangu 1998 hadi 2013.

Aliteuliwa kuwa waziri wa elimu na utamaduni wa Msumbiji mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru na mwaka huohuo akaolewa na Rais Samora.

Winnie Mandela

Aliyewahi kuwa mke wa Rais wa Afrika Kusini, Winnie Mandela ni kati ya wake za marais wanaoingia kwenye historia ya kuwa wanasiasa na viongozi.

Winnie licha ya kushiriki bega kwa bega katika harakati za ukombozi wa nchi hiyo pia amewahi kushika nafasi mbalimbali za kiuongozi serikalini na pia katika chama tawala nchini humo, ANC akiongoza wanawake.

Rosario Murillo

Nchini Nicaragua, Rais Daniel Ortega aliishangaza dunia aliposhinda nafasi hiyo kwa mara ya nne na mkewe aliyekuwa mgombea mwenza kuwa Makamu wa Rais. Rais Ortega alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 72.5 na kuandika historia katika siasa za dunia ya nchi kuongozwa kidemokrasia na mume na mke.

Suala hilo liliipa shida nchi hiyo kujua ataitwa jina gani? Ni First Lady yaani mke wa rais au makamu wa rais.

Janeth Museveni

Miongoni mwao ni Janet Museveni ambaye mumewe, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimteua kuwa waziri wa elimu na michezo katika baraza lake lenye mawaziri na manaibu waziri 80.

Awali, Mama Janeth alikuwa waziri wa masuala ya eneo la Karamoja lililo Kaskazini – Mashariki mwa Uganda ambalo lilikuwa limegubikwa na migogoro na umaskini uliokithiri.

Wasemavyo wachambuzi

Akizungumzia uteuzi wa Mama Salma, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana alisema kuwa mke wa Rais hakumzuii mtu kuteuliwa katika nafasi nyingine ya uongozi ikiwa anazo sifa stahiki.

Alisema hakuna cheo kinachoitwa ‘first lady’ kwenye Katiba na kwamba kilichomfanya ateuliwe ni utendaji wake mzuri aliouonyesha hasa kuguswa na matatizo ya wananchi jambo linalomuongezea sifa ya ziada ya kuwa msemaji wao bungeni.

“Alimsaidia vizuri Rais Kikwete wakati akiwa madarakani. Rais Magufuli amezingatia vigezo, ni haki yake kikatiba,” alisema.

Mratibu wa Taifa wa Taasisi ya wanawake Ulingo, Dk Ave Maria Semakafu alisema, “Amekuwa kwenye siasa muda mrefu sasa, kwahiyo sioni tatizo lolote katika uteuzi huo tunachopigania ni kuongeza nguvu zaidi katika uwakilishi ndani ya Bunge ili kufanikisha hoja za uongozi.”
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images