Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Makato ya Bodi ya Mikopo Yawa Kaa la Moto kwa Waajirwa...!!!

0
0

Kaimu Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Chunya mkoani Songwe, Benedict Polycap amesema  baadhi ya watumishi wanashindwa kufanya kazi kwa utulivu kutokana na kipato chao kupungua baada ya kuanza kukatwa malimbikizo ya mkopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Polycap alitoa taarifa hiyo juzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, kwamba hali hiyo imesbabisha  baadhi ya watumishi kupokea mishahara midogo isiyokidhi mahitaji yao hata kwa wiki mbili.

Alisema baadhi ya watumishi wanapokea mishahara kuanzia Sh100,000 hadi  Sh200,000, hivyo huamua kujiingiza kwenye shughuli nyingine kutafuta kipato cha ziada ili kujikimu.

Katika tukio jingine, Galawa aliagiza kukamatwa mara moja kwa watumishi wanne wanaodaiwa kugoma kuhamia Halmashauri ya Songwe na kubaki Chunya, huku wakiendelea kupokea mishahara.

Galawa alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa za idara za halmashauri hiyo. Taarifa hiyo ilibainisha kuwa watumishi wanne hawajaripoti tangu kuanzishwa kwake Septemba 2016.

Agizo la Rais Magufuli Lainyima Usingizi Zanzibar

0
0

Wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likijipanga kuikatia umeme Zanzibar kama alivyoagiza Rais John Magufuli, SMZ inajipanga kuzungumza na shirika hilo ili kuona namna ya kulipa.

Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema yupo safarini na hakuzungumza kutokana na mawasiliano kuwa mabaya. 
Baadaye mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi, lakini Dk Mwinuka hakujibu.

Baada ya kukwama kupata maelezo ya Dk Mwinuka, mwandishi wetu alimtafuta kwa simu, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ambaye alisema shirika hilo litatekeleza agizo la Rais kama alivyoagiza. 

“Rais ametoa kauli na kuagiza… lazima tutekeleze,” alisema Muhaji ambaye hakubainisha siku ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mohamed Aboud Mohamed  alipoulizwa kuhusu deni hilo, alisema wamejiandaa kufanya mazungumzo kati ya mawaziri husika wa pande mbili za Muungano kuona namna wanavyoweza kufanikisha ulipaji wa deni hilo.

“Lengo letu ni kulipa deni lote kwa sababu ukidaiwa lazima ulipe. Tupo tayari kulipa ndiyo maana tumeanza kufanya mazungumzo na wenzetu wa Tanzania Bara, ili kuona namna tunavyoweza kukubaliana juu ya Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kulipa hatua kwa hatua ili kumaliza deni lote,” alisema.

Lissu Aachiwa Kwa Dhamana ya Aina Yake..!!!

0
0

Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana (ya polisi) iliyowekwa na wanasheria wawili, Hekima Mwasipu na Nashon Nkungu baada ya kushikiliwa na polisi  kwa saa kadhaa .

Lissu alikamatwa ghafla jana alipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mashitaka yake ya uchochezo katika moja ya kesi zinazomkabili, kufutwa.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lissu alikamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi ambayo yangeweza kuibua mtafaruku wa kidini katika jamii wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Dimani, Zanzibar, mwezi Januari mwaka huu.

Baada ya mahojiano ya jana, Lissu ameachiwa kwa sharti la kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Machi 13, mwaka huu.

Kigwangalla Ashindwa Kujizuia kwa Diamond...!!!

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya vijana, Dkt. Hamis Kigwangalla ameshindwa kujizuia na kufunguka jinsi anavyomuhusudu mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nzega, ametumia ukurasa wake wa twitter kutamka rasmi kuwa hajawahi kuwa shabiki wa Diamond, lakini kazi zake anazikubali hasa zile zilizokaa kimikakati ya biashara.

"Sikuwahi kuwa mshabiki wa Diamond Platnumz, japokuwa ni mwimbaji mzuri, ila nakubali sana kipaji chake kwenye 'biashara' ya muziki" Amesema Kigwangalla

Ametaja ngoma iliyomfanya aanze kumkubali tena Diamond, mbali na ile ya Mbagala, kuwa ni Marry You aliyoshirikiana na Ne-Yo kutoka nchini marekani.

"Zaidi ya nyimbo ya Diamond Platnumz Mbagala (ambayo naipenda mpaka kesho), na juzi hapa nyimbo za Ngololo, Salome, hii ya Marry You" Aliandika Kigwangalla

Aunty Ezekieli -Mose Hakukosea Kumuita Harmorapa 'NYANI' ...!!!!

0
0

Muigizaji Aunty Ezekiel amemtetea mpenzi wake (Mose Iyobo) kwa kumfananisha na nyani msanii chipukizi anayefananishwa na mmoja wa wasanii kutoka WCB  (Harmo Rappa) kwa kusema ni sawa kabisa na Mose hakufanya makosa

Hivi karibuni akiwa kwenye Kipindi cha KIKAANGONI cha Facebook EATV Aunty amesema kwamba watu walimnukuu vibaya Mose na kumhukumu moja kwa moja huku akiongeza kwamba hakuwa na nia mbaya.

“Sikuona shida yoyote Mose kumuita Harmorappa nyani kwa kuwa ni majina ambayo vijana wa kisasa wanajipa, mfano kama Nasibu anavyojiita Simba, asilimia kubwa ya watu hawakujua kwa nini alijiita hivyo, wangemuuliza kwa nini ameamua kumfananisha na nyani ndipo wangehukumu, yule si msanii? basi inawezekana Mose labda baada ya kusikiliza wimbo wake  kaona kwenye kuimba ana kisauti kama cha nyani au labda anarukaruka kama kinyani, kwa hiyo ni sawa kumuita nyani" Amesema Aunty.

Aunty amesema alichokifanya Mose ni kumsaidia Harmorapa kujiita nyani na kwamba Mose alichokosea ni kumuita kabla yeye (Hamorapa) hajajiita mwenyewe.

Aidha Aunty amesema kwa upande wake hamkubali kabisa Harmorapa kwa kuwa analazimisha kujulikana na hana kipaji

"Yule mshikaji simkubali kabisa anatumia nguvu nyingi na sababu kutafuta kujulikana kiufupi hajajipanga, hana kipaji" Amesema Aunty

Steve Nyerere - TID ni Panya Tu...!!!

0
0

Msanii wa vichekesho Steve Nyerere ameibuka na kumjibu msanii TID huku akieleza kufurahishwa na hatua ya TID kumfananisha na panya kwa kuwa inaonesha jinsi alivyo mjanja ambaye anaweza kujitafutia na kusema

Wakati akifurahi kufananishwa na panya, Steve amemfananisha TID na paka ambaye husubiri kutengewa kila kitu.

Steve Nyerere alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kudai kuwa yeye hawezi kuanza kujibishana na TID sababu kwake TID si kitu chochote.

Mboto: Ningetembea na Aunt Ningefurahi Sana..!!!

0
0

Mwigizaji wa Vichekesho Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ ameibuka na kufunguka kuwa iwapo angetembea na Aunt Ezekil angefurahi na angeweka wazi kwa sababu yeye ni rijali.  

Mboto alisema hayo baada ya kuibuka maneno mtandaoni kuwa, Aunt aliwahi kuwa na ujauzito wake na akautoa, ishu ambayo Mboto aliikana vikali. Mboto aliliambia Wikienda kuwa, yeye na Aunt hawajawahi kuwa na uhusiano na endapo wangeingia kwenye uhusiano angefurahi na angetangaza wazi kwani yeye ni rijali anayejiamini.

“Hili suala ndiyo kwanza nimelisikia lakini kiukweli kungekuwa na ukweli wowote ningeanika kwani ni suala la kujivunia,” alisema Mboto

Lipumba Afanya Maamuzi Magumu CUF… Atimua Wakurugenzi 6..!!!

0
0

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ametengua uteuzi wa wakurugenzi sita kwa mara nyingine.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya inasema uamuzi huo umefikiwa kutokana na viongozi hao kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na kutohudhuria mkutano wa kamati ya utendaji, licha ya kupelekewa taarifa.

Ilielezwa kuwa Profesa Lipumba Februari 17, alimuagiza Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Magdalena Sakaya kuwapa taarifa ya mkutano wa kamati ya utendaji   uliofanyika Februari 18 na walipelekewa mwaliko kwa posta.

Wakurugenzi waliotenguliwa na nafasi zao kwenye mabano ni Omar Ali Shehe (Mipango na Uchaguzi); Salim Abdallah Bimani (Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma); 
Abdallah Bakar Hassan, (Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi); Pavu Juma Abdallah (Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria);  Yusuf Salim (Naibu Katibu Kamati ya Ulinzi na Usalama) na  Mahmoud Ali Mahinda (Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana).

Akizungumzia uamuzi huo, Bimani alisema hawamtambui Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa chama hicho.

“Lipumba anafahamu kama alifukuzwa uanachama ndiyo maana alikata rufaa kupinga uamuzi wa mkutano mkuu,” alisema Bimani.

Rais Trump Atia Sahihi Amri Mpya ya Kuzuia Wahamiaji wa Kiislamu Kuingia Marekani, Iraq Yaondolewa..!!

0
0

Rais wa Marekani Donald Trump ametia sahihi amri mpya kuu ya uhamiaji ambayo itawazuia wahamiaji kutoka nchi sita zenye waislamu wengi kuingia Marekani kwa muda wa siku 90.

Iraq imeondolewa kutoka kwa orodha ya nchi saba zilizoorodheshwa awali. Watu wenye visa halali wataruhusiwa kuingia Marekani.

Hatua hiyo ambayo pia inajumuisha marufuku ya siku 120 kwa wakimzi wote, itaaza kutekelezwa tarehe 16 Machi.

Amri ya awali ilifutilia mbali mpango mzima wa uhamiaji wa Marekani, na kuwazuia raia kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

Hatua hiyo ilizua fujo kwenye viwanja vya ndege wakati watu wenye stakabadhi halali walizuiwa kuingia Marekani na pia kusababisha maandamano makubwa.

Uongozi wa bwana Trump ulisema kuwa amri hiyo ni muhimu kuwalinda Marekani kutokana na ugaidi.

Ilani ya siku 10 imetolewa ili kusaidia kuzuia fujo zilizoshuhudiwa kwenye viwanja vya ndege tarehe 27 mwezi Januari wakati amri ya kwanza ilipotangazwa.

Wasafiri waliokuwa na visa halali waliokua hewani wakati huo walijipata wakizuiwa na maafisa wa mipaka walipowasili.

Ubuyu wa Moto Moto..Pamoja na Kuwa Mke Halali Katika Ndoa.Kajala Adaiwa Kutesa na Bwana Mpya...!!!.

0
0

Ubuyu mtamu wa Wikienda! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ anadaiwa kupata bwana mpya ambaye kutwa, kucha amekuwa akimposti kwenye mitandao ya kijamii hasa Snap Chat akitamba kuwakomesha wambeya wa Instagram.

Kwa mujibu wa sosi makini, Kajala kwa sasa ana mpenzi mpya ambaye amekuwa akitesa naye kwa kutupia mapichapicha mitandaoni akijiachia kwa kufanya naye mazoezi ‘gym’.

MSIKIE SOSI

Sosi: Hivi jamani Wikienda mna ubuyu mpya mjini?

Wikienda: Ubuyu upo wa kila aina hapa sema tu wewe kama una wa kwako sisi tutaufanyia kazi na kuurusha hewani.

Sosi: Ubuyu mpya ni kwamba sasa hivi Kajala ana bwana mpya ambaye anatokana naye, unaambiwa watu hatunywi maji.

Wikienda: Ni bwana gani huyo? Je, ni staa au ana jina mjini?

Sosi: Nasikia ana asili ya Kisomali. Kuna watu wanasema anacheza kikapu maana ameenda hewani. Fuatilieni mtapata ubuyu freshi kabisa kabla hamjapigwa skupu.

PICHA ZA SNAP CHAT

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilianza kunyapianyapia ambapo lilielezwa kuwa, kulikuwa na picha za Kajala na jamaa huyo ambazo ziliibwa kwenye Snap Chat na wambeya kisha kuzitupia kwenye Instagram, jambo lililomfanya Kajala aumbuke kwani hakuwa na namna zaidi ya kupiga kimya.

WIKIENDA KAZINI KUICHIMBA

Baada ya picha hizo kutupiwa Instagram, Wikienda lilizama kazini kuchimba ukweli ambapo lilibaini moja kwa moja kuwa Kajala na bwana huyo ambaye jina lake bado lipo kwenye mabano ni wapenzi kutokana na jinsi mwanamama huyo anavyotupia picha zao.

Ilibainika kuwa, Kajala amekuwa akitupia picha nyingi zikiwaonesha wakiwa wamekumbatiana na kushikana viuno na maeneo mengi

BETHIDEI YA JAMAA

Hata hivyo, siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa jamaa huyo hivi karibuni, Wikienda lilibaini kuwa, jamaa huyo ni mtu wa Kajala kwani staa huyo alitupia picha za jamaa huyo akimtakia heri ya kuzaliwa ambapo aliandika maneno yaliyoweka wazi kuwa ni  mpenzi wake ambayo yalisomeka:

“Happy birthday my heart beat!” Kama hiyo haitoshi, mmoja wa watu wa karibu wa Kajala alitupia picha za wawili hao akimuwishi jamaa huyo heri ya kuzaliwa, jambo lililofunua kila kitu kwani wana ubuyu walifafanua kuwa, aliyezaliwa ndiye bwana mpya wa Kajala.

Baada ya ubuyu huo kukaa kwenye kilo, Wikienda lilianza kusaka mzani wake kwa kumtafuta Kalala kwa njia ya simu ambapo hakutaka kuzungumza zaidi ya kuomba habari hiyo isiandikwe.

MSIKIE KAJALA

“Naomba usiandike lolote juu ya habari hiyo,” aliomba Kajala, ombi ambalo lilitupiliwa mbali. Kama hiyo haitoshi, Wikienda halikuishia hapo kwani siku iliyofuata Kajala aliombwa tena kuzungumzia ubuyu huo ambapo alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulioonesha umesomwa lakini haukuwa na majibu.

NENO LA MHARIRI

Kama Kajala amepata mchumba inabidi ajitafakari kwani ni katika kipindi ambacho mumewe, Faraji Agustino ametoka gerezani na wengi walitarajia aungane naye tena kwa ajili ya kusongesha gurudumu la maisha kwa sababu ndoa yao bado haijavunjika.

Jay Z Na Beyonce Kununua Nyumba Ya Bei Ghali ($200 Million) Zaidi Jijini Los Angeles...!!!!

0
0

Kuwa superstar sometimes ni raha sana… why? Ukiwa kama Jay Z na Beyonce unakuwa na uwezo wa kununua kitu chochote kile upendacho ikiwemo nyumba ya bei ghali kuliko zote jijini Los Angeles nchini Marekani!

 leo jumanne ya March 7 2017 imenipeleka moja kwa moja mamtoni ambapo mtandao wa PEOPLE umeripoti kuwa weekend iliyopita The Carters walikuwa jijini Los Angeles wakitafuta nyumba ya kuanzia maisha mapya na kuvutiwa zaidi na nyumba ya bei kubwa kuliko zote jijini humo.

Nyumba hiyo yenye ukubwa wa mraba 57,000 inapatikana maeneo ya Holmby Hills ambapo awali ilikuwa inamilikiwa na Television Producer Aaron Speeling na mke wake Candy toka mwaka 1991. Baada ya kufariki kwa Aaron Spelling mwaka 2006 ambaye ndiye aliyeijenga nyumba hiyo, mkewe aliamua kuiweka nyumba hiyo sokoni kwa bei ya $150 Million lakini kufikia October mwaka 2016 nyumba hiyo ilikuwa inauzwa kwa bei ya $200 Million.

Ndani ya nyumba hiyo, kuna vitu mbalimbali ikiwemo maktaba ya kusomea, chumba kikubwa cha sinema, gym ya mazoezi, chumba cha midoli, studio ya kucheza mchezo wa bowling, hifadhi kubwa ya wine, vyumba vya kulala visivyo pungua sita, jiko sita, na bafu 26 . Mbali na vile vinavyopatikana ndani ya nyumba hiyo, nje ya nyumba hiyo kuna uwanja zaidi ya mmoja wa tennis, bustani yenye ukubwa wa ekari 5  pamoja na swimming pool.

Sources karibu na The Carters wanadai kuwa familia hiyo inataka kuhamia jijini LA moja kwa moja na wangependa kuimiliki nyumba hiyo haraka iwezekanavyo.

KUTANA na Mtabibu Ostadhi Khamisi Kutoka Mombasa Kenya Kwasasa Yupo Tanzania Kwa Ajili yako

0
0

Kutana na ostadhi khamisi kutoka mombasa Kenya kwa sasa yupo Tanzania ni mtabibu na mtafiti Wadawa za asili anatibia kama vile:
Miguu kuuma
Miguu kufagazi
Miguu kuwakamoto
Chango lauzazi kwakina mama
Dawa ya uzazi wakina mama inapatikana
Kusafisha nyota ili uwe namuonekano kwa kila mtu
Kumrudisha mpenzi wako na liekukimbia ndani yasiku 3 bila yapingamizi yoyote
Kumshika mume au mke asitoke nnje ya ndoa
Pata pete ya Bahati inayo endana na nyota yako
Kurudisha mali ilipotea au kudhurumiwa ndani yasiku 3
Pata utajili usiokuwa namashaliti yoyote
Dawa za nguvu za kiume
Dawa ya biashara inapatikana
Dawa ya kuzuia chuma ulete kwenye biashara inapatikana
 Zindiko la nyumba au shamba
 Anatuliza familia zinazogombana DUWA pamoja navisomo vya ufunguzi wa mwili wako njoo ufunguliwe vifungo ulivyo fungwa kutana na ostadhi khamisi utimiziwe ahadi ulizo hadiwa acha kuteseka acha kuhangaika ostadh khamisi yupupo tanzania kwajili yako...

Call +255718746825 +255754765246 kwa what'sapp +255783708487

Familia ya Kikwete Yapata Msiba Mzito...!!!

0
0

Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo.

Kupitia mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru jamii kwa salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri.

"Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo". Kauli ya Jakaya Kikwete

Naye Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya leo.

"Ndugu na marafiki nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha Bibi yetu Bi. Nuru Khalfan Kikwete kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana" Amesema Ridhiwan Kikwete.

CCM Waja na Mpango wa Kujenga Chuo Kikuu Cha Chama..!!

0
0

Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho kina mpango wa kufungua Chuo Kikuu cha chama hicho.

Akizungumza katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na Channel Ten ambapo amesema chuo hicho kitatoa mafunzo kwa wanachama, makada na viongozi wote wa chama na hata waliopo serikalini kupitia chama ili kuwafundisha itikadi za chama hicho.

Alisema, “Unajua chama cha Mapinduzi na chama cha kikominist (Uchina) ni marafiki, tumeamua tujenge chuo kikuu cha chama cha mapinduzi ambacho kitakuwa na kazi ya kuwafundisha wanachama, makada,viongozi na wale waliopata dhamana serikalini. Kupitia chama cha mapinduzi tutawafundisha ili tuelewane itikadi yetu, watu hujiunga na chama si kwa ajili ya ushabiki ila watu wanajiunga na chama kwa sababu wanaamini wameielewa itikadi ya chama hiki ni nini.”

Chadema Watoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Kikwete...!!!

0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa salama za rambirambi kwa familia ya raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwa msiba wa mama yake mdogo Bi. Nuru Khalfan Kikwete aliefariki asubuhi ya leo.

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe amesema familia ya Kikwete imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na nguzo muhimu katika familia na ukoo.

Hamorapa :Toka Nimepata Umaarufu Nime Kwichi Kwichi na Mademu 76

Kimenukaaa..Mama Wema Awatimua Mashoga wa Wema Nyumbani Kwake,...!!!

0
0

Bado sakata la mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu  , Mariam Sepetu  kudaiwa kumrekodi bila ridhaa yake mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kisha sauti hiyo kuitupia mitandaoni, kuna siri mpya imebainika ndani yake ya kuwatimua wanaume tata ‘mashoga’ nyumbani kwa mwanaye huyo.

Katika sauti hiyo ambayo, mama Wema alisikika akimshushia lawama nzito Steve kwa kitendo chake cha kutokwenda kumuona Wema aliposhikiliwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ na Steve kujitetea kwamba alifanya hivyo kwa sababu alikwenda Dodoma kuonana na wabunge ili wamsaidie Wema kutoka, lakini jambo jipya ni mama Wema kukiri kuwafukuza mashoga hao nyumbani kwa mwanae.

Mama Wema katika mazungumzo yake kwenye sauti hiyo, alisema kuwa yeye hapatani au hafugi ujinga na ndiyo maana hata ‘wale’ mashoga waliokuwa nyumbani kwa Wema, Ununio, aliwatimulia kwa mbali. “Mimi sipendagi ujinga. Wale mashoga nimewafukuza wote pale, hawapo tena…” alisikika mama Wema akimwambia Steve Nyerere huku akitumia sauti ya kujigamba. Kumekuwa na madai kwamba, baadhi ya mastaa Bongo wamekuwa wakiishi na wanaume ‘tata’ (mashoga) bila kujulikana madhumuni yake.

“Unaweza kukuta staa anaishi na mashoga watatu mpaka wanne na imekuwa fasheni sasa, kila staa anao nyumbani kwao, sijui kwa madhumuni gani?” kilihoji chanzo kimoja baada ya kumsikia mama Wema akidai kuwatimua mashoga hao nyumbani kwa binti yake. “Kwa sauti hii, nimeamua mama Wema si wa mchezomchezo.

Unajua mama kufunga safari mpaka nyumbani kwa binti yake na kutibua utaratibu wake si jambo dogo.

“Wa mama wengine wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu wanaamini binti au mtoto kwa vile ameshafikisha miaka 18 basi ni mkubwa anatakiwa kujitawala. Noo! Mtoto ni mtoto tu, kwa mama hakui hata angekuwa mkubwa,” kilizidi kusema chanzo hicho.

Miezi ya nyuma, msanii wa filamu aliyewahi pia kuwa mtangazaji, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ aliwahi kuandikwa kwa habari za kudaiwa kuishi na mashoga. Lakini pia baadhi ya mastaa wamewahi kuandikwa kwa madai ya kuwa karibu sana na

Nimejaribu kujiua zaidi ya mara nne- Saida Karoli

0
0


Saida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Mapenzi kizunguzungu’, Kaisiki, Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, amefunguka kuwa amewahi kujaribu kuataka kujiua.

Akizungumza katika Promo ya mahojiano ya kipindi cha #TakeOne kinachorushwa na CloudsTv Saida karoli amesikika akisema kuwa ameshawahi kufanya majaribio ya kutaka kujiua zaidi ya mara nne.


Hata hivyo kupitia Promo hiyo amesikika akisema akisema yeye ni Mama wa watoto watano ambapo kila mtoto ana baba yake na kongeza kuwa hana mpango kutoa kizazi hivyo ataendelea kuzaa mpaka Mungu atakapowambia basi.

Faham Usiyoyajua Juu ya Uwezo wa Hali ya Juu wa Mbegu za Maboga Katika Kutibu Magonjwa Haya 10..!!!

0
0

ULAJI wa maboga ni muhimu lakini ni Watanzania wachache wanaojua faida ya boga na mbegu zake. Mbegu za maboga zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna kila wakati baada ya kuzikaanga au zikiwa mbichi au kama zimepikwa na boga lenyewe kwani imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10.

KIBOFU CHA MKOJO

Mbegu za maboga zimekuwa zikitumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo Urinery Bladder. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.

KINGA YA MWILI

Mbegu za maboga zenye kiasi kingi cha madini ya Zinc yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha kwenye damu sukari na huboresha nguvu za kiume pia huongeza uwezo wa kufikiri. Upungufu wa madini ya  Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, mwanamke au mwanaume kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo wa kuelewa wanachofundishwa darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.

MAFUTA YA OMEGA -3

Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.

UGONJWA WA MOYO

Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia Magnesium ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.

KINGA DHIDI YA SARATANI

Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu, hivyo unapokula mbegu hizi husaidia mambo hayo na mengine mengi.

UGONJWA WA KISUKARI

Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha  Insulin mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa hatari wa kisukari.

MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI

Mara nyingi akina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo, wataalamu wamegundua kwamba ulaji wa mbegu umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.

AFYA YA MOYO NA MAINI

Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe Fibre na virutubisho vinavyoimarisha
kinga ya mwili Antioxidants, zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.

DAWA YA USINGIZI

Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri mwororo.

DAWA YA UVIMBE

Wataalamu wamethibitisha kwamba mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe Inflamatory Diseases sawa na dawa aina ya Indomethacin lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa, ndiyo maana tunahimiza kutumia mbegu za maboga ambazo huwa ni dawa asili.

JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA

Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga japokuwa zilizokaangwa bila kuunguzwa nazo siyo mbaya. USHAURI Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu.


Dully Sykes - Jina Analotumia Baraka ni Langu ....!!!

0
0

Mwanamuziki mkongwe Prince Dully Sykesy ameweka wazi yeye ndiye aliyempatia jina la kisanii Baraka The Prince miaka kadhaa iliyopita kabla hata msanii huyo hajatoa wimbo hata mmoja.

Katika ukurasa wake wa instagram Dully ameandika kwamba baraka aliwahi kumpigia simu na kumwomba amchagulie jina ambalo litamfanya awe maarufu.

"Kuna siku ila mwaka sikumbuki nilipata simu kutoka kwa kijana aliejitambulisha kwa jina la BARAKA. Akanisalimia na kunambia anahitaji nimpatie jina ili alitumie kwenye sanaa....nikamuuliza anaishi wapi?...akanambia anaishi MWANZA...nikamwambia nitampatia jina moja kati ya majina yangu.....ndipo nikampatia 'PRINCE' nikamwambia ajiite ....BARAKA DA PRINCE, na kweli....nashukuru mungu yamekuwa na amekuwa mmoja kati ya wasanii wanaonipenda na kuniheshimu ..... @barakahtheprince_ nakupenda sana mdogo wangu!.." Amefichua Dully Sykes

Hata hivyo Baraka amesikika akisema kuwa ni kweli aliwahi kufanya kitendo hicho na kwamba ni miaka mingi sana imepita na anashangaa kitendo  cha Dully kutunza kumbukumbu za muda mrefu kiasi hicho.

"Niliwahi kusikia Dully akikupa jina lazima uwe maarufu , nilimpigiaga simu nikajitambulisha kwake nikamueleza shida yangu akanambia nimpigie baadaye, sikukata tamaa baadaye nikampigia akaniambia mimi natoka kwenye ukoo wa kifalme kwa hiyo nakupatia jina langu la 'Prince' hivyo utakuwa 'Baraka Da prince'. Namuheshimu sana ni kaka anayenijali mimi na kazi yangu". Amesema Baraka

Pamoja na hayo Baraka baada ya kusaini mkataba wa lebo ya Rockstar4000 inayosimamia kazi za wasanii Alikiba na Lady Jaydee, ilimbadilisha jina kutoka kwenye 'Baraka  Da Prince' na kuwa 'Baraka The Prince'.
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images