Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Unatamani Kumuacha ila Unashindwa? Ngoja Nikwambie Kitu

$
0
0
Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu kwanini nisiweze kuishi wewe ukiondoka??

Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua kufanya Maamuzi magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart. Wengi wamegeuzwa watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani, kisa wamezoeana, au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama hutaweza... Hamna kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona maumivu na utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya maamuzi magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu fulani ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako kukutesa maisha yote...

Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life

Exclusive..Baada ya Kutemwa Yanga,Pluijm Kutua Taifa Stars,Mpango Mzima Uko Hivi..!!!

$
0
0

UNAAMBIWA ukiona cha nini mwenzako anasema nitakipata lini, kwani baada ya Yanga kuamua kumtema kocha wao za zamani, Hans van der Pluijm, nyota ya Mholanzi huyo imezidi kung’aa na sasa ana ofa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikimiminika kila kukicha.

Pluijm alibadilishwa kutoka kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo na kupewa cheo cha ukurugenzi wa benchi la ufundi muda mfupi baada ya waajiri wake, Yanga, kumwajiri kocha mwingine, George Lwandamina, aliyekuwa akiinoa timu ya Zanaco ya Zambia, lakini hakudumu muda mrefu, baadaye alitimuliwa kabisa kutokana na kile kilichodaiwa na uongozi kuwa ni ukosefu wa fedha.

DIMBA Jumatano limezungumza na Pluijm kuhusu mustakabali wake ambapo amesema anamshukuru Mungu kwa kuendelea kumpigania, kwani kwa sasa amekuwa akipata ofa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zinampa wakati mgumu wa kuamua aende wapi.

Alisema kwa sasa bado yupo Tanzania na wala hajaondoka kwenda kwao Ghana, ambapo amedai kuwa, anafanya mambo yake kimyakimya na yakishakaa sawa atawekakila kitu bayana ili Watanzania na wadau wanaomuunga mkono wafahamu.

“Kama kuna watu wanauliza, kama nipo Tanzania au nimeshakwenda Ghana waambie bado nipo hapa nchini, na kuhusu mustakabali wangu niseme kwamba siwezi kuzungumza mengi kwa sasa ila kwa kifupi nimepata ofa mbalimbali za hapa Tanzania na nje ya nchi.

“Kwa sasa nachukua muda kutafakari na kutuliza akili yangu halafu nitafanya maamuzi sahihi,” alisema kocha huyo, aliyeiletea heshima Yanga kutokana na kuwapa vikombe mbalimbali, huku pia akijenga mashikamano ndani ya timu.

Taarifa zaidi kutoka vyanzo mbalimbali zinadai kuwa, moja ya timu ambazo Pluijm anatajwa kujiunga nazo hapa nchini ni timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambayo kwa sasa ipo chini ya Jackson Mayanja.

Kimenukaa,,Lissu Ataka Rais Dk Shein na Maalim Seif Wapelekwe Mahakamani,Ahoji Iweje Apelekwe Yeye Tu ....!!!!

$
0
0

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kuchapisha taarifa ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi Salum Hamidu amedai mahakamani kuwa makala nzima iliyotolewa kwenye gazeti la Mawio ni ya uchochezi.

Pia, shahidi huyo alidai mahakamani jana katika kesi hiyo kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Hassan Nassoro Moyo ni miongoni mwa waliohojiwa katika makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi.

Kamada Hamidu alitoa madai hayo wakati akihojiwa na mshtakiwa Lissu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Alidai kuwa katika malaka hiyo iliyochapishwa na gazeti la Mawio toleo la Januari 12-14, mwaka jana, Lissu alitajwa katika aya nane, Maalim Seif alitajwa katika aya 37, Dk. Alli Mohamed Shein alitajwa aya tatu na Moyo aya nne lakini hawapo kizimbani pamoja na washtakiwa wa kesi hiyo.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Lissu na shahidi:

Lissu: Shahidi, Rais wa Zanzibar ametajwa aya ngapi katika mahakama hiyo?

Shahidi: Ametajwa aya tatu.

Lissu: Maalim je?

Shahidi: Aya 37.

Lissu: Moyo naye ametajwa aya ngapi?

Shahidi: Moyo ametajwa aya nne.

Lissu: Je, makala nzima ni ya uchochezi?

Shahidi: Ndiyo.

Lissu: Kama ni hivyo mbona hapa kizimbani watu watatu hawajaungana na sisi kushtakiwa, Dk. Shein, Moyo na Maalim?
Shahidi: Mimi sihusiki na kuandaa mashtaka.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri April 3, mwaka huu.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine ni wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka jana, Dar es Salaam, Lisu na wenzake walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Pia Lissu na wenzake walidaiwa Januari 14, mwaka jana, Dar es Salaam, kwa nia ya kuleta chuki na uchochezi kati ya wananchi na mamlaka halali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walichapisha chapisho hilo lenye uchochezi.

Aidha, Lissu alidaiwa siku hiyo kinyume cha sheria na bila ya mamlaka waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo na wako nje kwa dhamana.

Kesi hiyo iliposikilizwa mara ya mwisho, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimzuia shahidi huyo kuhojiwa na Lissu kuhusu Katiba ya Zanzibar na mamlaka ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya huko, Jecha Salum Jecha, kwa kuwa haina mamlaka ya kuzungumzia katiba hiyo.

Kadhalika mahakama hiyo ilisema haina mamlaka wala uhalali wa kuzungumzia majukumu ya Jecha na kwamba imekubali ombi la upande wa Jamhuri la kusitisha kumhoji shahidi wake kuhusu suala hilo.

Lissu alitaka kumhoji Hamidu, kuhusu Katiba ya Zanzibar.

Msanii Mkubwa Marekani Will Smith Atua Bongo Kimya Kimya na Kujichimbia Zake Katika Mbuga ya Serengeti Akila Bata na Kushangaa Tembo..!!!

$
0
0



Tanzania ina ugeni mzito wiki hii.Muigizaji mashuhuri wa filamu, Will Smith amekuja nchini kwaajili ya mapumziko. Staa huyo wa Suicide Squad, yupo kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti akifurahi uumbaji wa Mungu.

Hata hivyo imebainika kuwa Smith si staa pekee wa Marekani aliyepo Tanzania. Supermodel wa Marekani, Chanel Iman naye amejumuika.
Kwenye Instagram, amepost picha akiwa na Will Smith mbugani Serengeti na kuandika: Great places with great friends and Will is One of the coolest.”

Noma Sana Hii..Diamonda Awachana Clouds Fm na EFM,Adai Hategemei Kiki Kutoka Kwao Ili Afanikiwe...!!!

$
0
0

Diamond Platnumz amesema kwa sasa redio na TV si vyombo anavyovitegemea sana kwaajili ya promotion pindi anapokuwa akiachia nyimbo.

“Mimi nikiwa natoa nyimbo yangu, promotion yangu siwazi redio wala siwazi TV, ever. Promotion yangu ya kwanza mimi nawaza nyimbo iwafikiaje watu, kuna mitandao ya kijamii, kuna digital platform nyingi,” staa huyo alisema kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz.

Alidai kuwa zama za kundi Fulani la watu likiamua kumrudisha nyuma msanii, halipo tena kwa wasanii wenye nguvu kama yeye.

“Tufute zile ‘naweza nikamdhuru mtu fulani ninavyotaka mimi’ vile vitu havipo tena,” aliongeza.

Ukweli Mchungu..Uwepo wa WCB; Bongo Fleva Inachungulia Kaburi...!!!

$
0
0

Hayo yote nayasema kuhusu nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Adul Juma au maarufu zaidi kwa jina la Diamond. Siku za hivi karibuni, Diamond ameanzisha zoezi la kuwachukua wanamuziki na kuwaingiza kwenye kundi lake maarufu sana la Wasafi Classic Baby ‘WCB’ ambalo limetokea kupata jina kubwa katika Muziki wa Kizazi Kipya Bongo.

Lebo hii ya Wasafi kwa sasa inaundwa na watu wanne, Queen Darleen, Rayvanny, Rich Mavoko na Harmonize. Awali, alianza na akina Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko na mwisho ni Queen Darleen. Harmonize na Rayvanny walikuwa hawakutamba sana kabla ya kwenda Wasafi. Mimi kwa hao, naona ni sawa kabisa na wala sina tatizo nao.

ANAINUA VIPAJI

Katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari hapa Bongo, Diamond amekuwa akisema kwamba, anafanya hivyo ili kukuza muziki na kuinua vipaji vya wanamuziki wachanga wa Tanzania. Mimi kwa hilo pia sina tatizo naye. Pia, watu au wadau mbalimbali wa muziki huo wakawa wanampongeza Diamond kwa kuwa, zoezi lake la kuwabeba akina Harmonize linaongeza ushindani mkubwa katika Muziki wa Kizazi Kipya, kwamba kama yeye anawainua hawa, wengine wakainuliwa kule, muziki utapaa. Na kwa hili pia mimi sina tatizo nalo hata kidogo.

NI HOJA ZA MSINGI SANA

Kuna hoja za msingi kwamba, kama si Diamond, hawa akina Rayvanny wasingekuwa hivi walivyo leo. Wasingejulikana kama wanavyojulikana wakiwa kwa Diamond. Hiyo ni hoja ya msingi sana, tena sana. Na kwa hilo mimi sina tatizo na hoja husika.

KUHUSU RICH MAVOKO

Katika zoezi lake la kuendelea kuchukua wasanii, Diamond akamchukua Mbongo Fleva, Rich Mavoko ndani ya kundi lake la Wasafi. Hapa kidogo baadhi ya watu wakahoji uhalali wa usahihi wake. Wengi waliamini kuwa, Diamond kumchukua msanii huyo ambaye alishajenga jina kubwa katika muziki huo ni sawa na kumpoteza njia kwani Rich Mavoko kuwa chini ya Wasafi kunaweza kumfanya afifie kama siyo kufa kabisa kisanii.

NINACHOKIONA

Sasa ninachokiona mimi ni kwamba, nia ya Diamond inaweza kuwa nzuri sana lakini kukatokea makosa madogomadogo kwenye kuchukua aina ya wasanii. Yapo madai ya chini kwa chini kwamba, pia ana mpango wa kumchukua msanii anayevuma sana kwa sasa, Darassa ambaye kibao chake cha Muziki kimeishika nchi kwa kupigwa maeneo mbalimbali. Kama kuna ukweli wa madai haya, naamini kuna siku tutakuja kusikia, hata Ali Kiba, Ommy Dimpoz nani sijui, wote wana mpango wa kujiunga Wasafi. Katika hili, ninatia shaka kwamba, lengo la Diamond kuwakusanya wasanii niliowataja na kumchukua pia Rich Mavoko ni njia moja kwake ya kuelekea kwenye kuudidimiza muziki wa Bongo Fleva.

Wasafi linajiimarisha kuwa kundi kubwa la muziki huo nchini. Sasa je, ikitokea hivyo, upinzani utatoka wapi? Ninavyojua mimi siku zote, palipo na ushindani ndipo panapokuza kitu. Ni sawa na timu za mpira wa miguu wa Tanzani, piga mahesabu kwamba, kuna siku Simba itashuka daraja. Je, Yanga atabaki na mshidani gani? Na kilele cha raha ya mpira wa Tanzania ni kucheza kwa Simba na Yanga.

Ndiyo maana, makocha wa timu hizo bora wafungwe na timu nyingine zote, lakini siyo Simba au Yanga. Hata shule wanazosoma watoto wetu siku hizi, ubora wake inatokana na kuwepo kwa shule bora nyingine. Kama ingekuwa shule moja tu ndiyo bora sifa yake isingekuwa na maana. Sifa  ya mtu mrefu duniani kote inatokana na kuwepo kwa mtu mfupi. Kama watu wote wangekuwa na kimo sawa isingejulikana kama urefu ni bora.

Kuwepo kwa Wasafi kusiwe sababu ya kuwakusanya wanamuziki wengine hawa wenye majina makubwa kwani na wao uwepo wao ndiyo changamoto ya kuwepo kwa Wasafi. Inawezekana nia ya Diamond ikawa nzuri sana lakini mimi naamini anakokwenda, kunaweza kuwa ndiyo kaburi la muziki wenyewe.


Video...Mdogo wa Gwajima Amtetea Makonda, Asema Josephat Apuuzwe kwa Kuwa ni Muongo Mkubwa ,Asema Gwajima Hajawahi Kufufua Hata Kuku...!!!

$
0
0

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

Picha: Bilioni 10 za Rais Magufuli kwa UDSM Zakamilisha Kazi..!!!!

$
0
0

Ujenzi wa majengo 20 yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 3,840 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kila jengo lina ghorofa nne umekamilika baada ya kuchukua muda wa miezi minane.

Suala kubwa nililojifunza katika siasa za Tanzania ni kuwa na kiongozi shupavu anayesimamia kile anachokiamini na kukiamua bila kujali kelele za wanasiasa wanafiki na wale wasioamini.

Ikumbukwe kuwa kuna wakandarasi walitaka kulipwa bilioni 100 katika mradi huu.

Kuna wengine walileta thread hapa na kuwaaminisha baadhi ya wana JF kuwa wataleta gharama kamili ya ujenzi lakini mpaka sasa ''wameingia mitini'' kwa sababu uwongo wao ulitumia lifti kuwafikia walengwa lakini kwa sasa ukweli unafika kwa kutumia ngazi.

Picha hizi pia zinatoa fundisho kwa wasioamini ambao pia wameainishwa kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu ndani ya Quran na Biblia.

Kwa wale wanaojua Quran wanaweza kuelewa maana ya maneno yangu kupitia verse 44 ya Surah Fussilat (41).

Kwa wale wanaojua Biblia wanaweza kuelewa maana ya hoja yangu kupitia Yohana 20:24.

Kuna msemo usemao, Kama hujui kusoma, hata picha huwezi kutazama?

Focus and perseverance is what separates winners from losers.

Uchaguzi TLS: Tundu Lissu Amshukia Mwakyembe, Aahidi Kufungua Kesi Mahakamani...!!!

$
0
0


MBUNGE na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo(CHADEMA), Tundu Lissu amemshukia Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe akimtuhumu kuwa anataka kuharibu uchaguzi wao wa uraisi wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) uliopangwa kufanyika Machi 18 mwaka huu.​

Tundu Lissu ametaka ajumuishwe katika kesi ya Godfrey Sabato Wasonga dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu uchaguzi wa TLS.

Akizungumza na wanahabari katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam, Lissu amesema kuwa Mwakyembe anamtuhumu kuhusika kuwashawishi wanasheria wawili waliofungua kesi mbili za kupinga kutokufanyila uchaguzi huo kwa madai y akuwa uchaguzi huo unaingiliwa na masuala ya kisiasa jambo ambalo lisu amelikataa akisema:

“Uchaguzi wetu wala hauhusiki na masuala ya kisiasa kwani sheria ya Chama cha Wanasheria inavyovigezo vya kuzingatia na kuheshimu Katiba yake na ndipo mwanachama anaruhusiwa kuomba uongozi pale anapokuwa amekidhi vigezo.”

“Katika kugombea Urais wa Chama cha Wanasheria, mimi sijatumia vyeo vyangu katika chama bali nimetumia vigezo vya kisheria ya chama cha wanasheria ndio maana hata ukiangalia mwenzangu Laurence Masha naye ametokea chadema.

“Kwa hiyo kama tungeingiza mambo ya siasa asingegombea yeye tukawa wawili ndani ya chama, Mawakili waliofungua Kesi mkoa wa Dodoma na wengine wa Dar es Salaam tutahakikisha tunanunua kesi hiyo kwa kwenda Mahakamani kufungua kesi inayopinga kutokufanyika kwa uchaguzi huo, na hilo tutalitekeleza kabla ya kufanyika kwa uchanguzi huo ili uchaguzi wetu hauvurugiki,” Alisema Lissu

WhatsApp Yasaidia Ndugu Kutambua Maiti Wao...!!!

$
0
0

Mwili uliokataliwa na ndugu kuchukuliwa katika Hospitali ya KCMC baada ya kukuta umeandikwa jina la mtu mwingine hatimaye umepatiwa ufumbuzi.

Maiti huyo ambaye alibaki hospitalini hapo kwa saa 12, juzi ndugu zake walithibitisha kwamba alikuwa ni ndugu yao baada ya picha iliyopigwa na kutumwa kwenye mtandao wa WhatsApp kusaidia kutambuliwa.

Ndugu hao waliichukua maiti hiyo juzi saa 2:00 usiku na kwenda kuizika eneo la Marangu Samanga.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Roman Mongi, ambaye ni ndugu wa marehemu Frank Mongi, alisema awali waliukataa mwili huo kwa kuwa ndugu yao alikuwa mwembamba lakini maiti ilionyesha alikuwa mnene.

Alisema walipokuta maiti imewekewa lebo yenye jina la Ibrahim Msuya, waliwasiliana na ndugu wa marehemu huyo waliokuwa wilayani Mwanga.

“Walitutaka tuupige picha huo mwili uliokuwa na jina la Ibrahim Msuya, halafu tuwatumie picha kwa WhatsApp. Ndipo wakasema hakuwa ndugu yao na kwamba waliouchukua ndiyo wa kwao,” alisema.

Diva Love Afunguka 'Ningekuwa Mwanaume Ningetoka na Jokate Kimapenzi'

$
0
0


Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM Diva amesema kama angekuwa ni Mwanaume angem’date Jokate kwani anavutiwa sana na muonekano wake wa baby face,pia amekiri kuwa alishawahi kumchangia Charity yake.

Mbali na hilo Diva amefunguka na kusema kuwa hawezi kumuomba msamaha Jokate Mwegelo ingawaje yeye alishawahi kumuona mrembo huyo akimrushia maneno kwenye mitandao ya kijamii.
.
.
. “Siwezi kumuomba msamaha Jokate kwa sababu sijamkosea chochote kama yeye alinikosea aje yeye kuniomba msamaha“Alisema Diva

Miezi kadhaa iliyopita @Divathebawse aliwahi kumtaka Alikiba aachane na @Jokatemwegelo akidai kuwa mwanadada Huyo ndio anamtia gundu king wa bongo fleva

Harmo Rappa Azidi Kutembelea Nyota za Wasanii Wakubwa...Amchokoza AY

$
0
0

Msanii Ay mzee wa commercial ameamua kumuachia jina lake Rapa anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva HamoRappa.

Jina la Legend alikuwa akitumia mzee wa commercial kwenye mtandao wa Twitter lakini sasa ameliachia rasmi kwa rapa huyo mwenye vituko vingi bongo anayeongoza kwa kufuatiliwa kwenye 411 news.

Baada ya HamoRappa kuitambulisha akaunti yake ya Twitter ikiwa na jina la Legend Harmo, jambo liloshtua ulimwengu vipi kwa Zee Legend aliyokuwa akitumia AY.

Mzee wa commercial ameamua kutumia jina la Masta badala ya Lile la Zee Legend ambalo Harmo amelichukua la Legend!

Ukweli Mchungu Kuhusu Anayejiita Mdogo wa Gwajima...!!!!

$
0
0

Amejitokeza mtu mmoja na kufanya press conference kwa jina anajulikana kama Methusela Gwajima , huyu Bwana ni Mwanasheria na ameajiriwa kwenye law firm ya Francis Stolla ambaye anagombea Urais wa TLS .

Huyu Mwanasheria sio mdogo wake na Gwajima wa kuzaliwa , bali ni ndugu katika Ukoo wao huo, naye ni wa KOLOMIJE .

Historia yake ya Kazi inaonyesha kuwa Aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCM Wilaya ya Singida na katika Wilaya ya Nzega katika cheo hichohicho kwa nyakati tofauti. Kwa sasa ni miongoni mwa wanasheria wa CCM .

CCM wameamua kumtuma kada wao wakifikiri kuwa anaweza kuaminika au kunyamazisha mjadala wa kudai vyeti halisi vya BASHITE ambaye kwa sasa ana stress nyingi sana na amezidiwa kabisa kabisa , baada ya watanzania kuamua kumuunga mkono Rais Magufuli katika zoezi la kuhakiki Vyeti linaloendelea.

Mjadala wa BASHITE utashika kasi sana kwenye vikao vya CCM na hasa kwenye Halimashauri Kuu ambako tayari yule Mbunge wa kule Geita ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa ameomba kuwasilisha hoja mahususi kwenye kikao cha Halimashauri Kuu kuwa Bashite anakichafua Chama , hivyo anataka waazimie kuwa aondolewe na kama halitafanyika basi hoja itawasilishwa Bungeni ili kumwazimia PM ambaye yuko kwenye Mamlaka yao.

Kama Umeteseka kwa Muda Mrefu,Hizi Hapa Mbinu za Kuamsha Nguvu za Kiume Kwa Muda Mrefu..!!!!

$
0
0

Suala la nguvu za kiume kwa sasa limeshakuwa ishu kubwa kwa vijana wengi wa sasa,kwa utafiti uliofanywa mwaka 2013 na shirika la Afya duniani unaonesha kuwa zaidi ya asilimia themanini ya wanawake hawatoshelezwi kimapenzi. Moja ya sababu kubwa inayochangia kutotoshelezwa huku kwa hawa wadada ni tatizo la upungufu wa uwezo wa mwanaume kumnyuka mwanamke kisawasawa ili kumkata nyege kabisa kwa kufika kileleni.

Wanaume wengi wa sasa wamekuwa wabovu kabisa katika kusimamisha mashine zao kiasi cha kuwa hata mdada awe mkali na mwenye mvuto namna gani amejitahidi sana kumtandika basi bao tatu kisha kitu inalala kabisaaa,tena kila bao huchukua dakika mbili tayari amekojoaLoo!

Zifuatazo ni njia chache na salama kabisa za kuamsha nguvu za kiume maradufu.

*AINA ZA VYAKULA

 Tusidanganyane chakula ndio kila kitu mwilini,vyakula vya nafaka zisizokobolewa ni vizuri sana kuupa uume nguvu kuliko unavyodhani. Hivyo kama ni ugali basi penda sana kula ugali wa dona na sio sembe kwani sembe huwa haina kiini cha njano chenye protini na wanga ambacho ni silaha sana katika kuutia nguvu uume na mwili kwa ujumla.

Matunda pia kama matango,karoti ni muhimu sana katika kujenga nguvu za kiume.Vyakula vingine ni kama mihogo mibichi,magimbi nk. Lazima uwe na utamaduni wa kutumia aina hii ya vyakula katika maisha yako ya kila siku, sio eti leo una mechi na mdada ndio unajifanya kufakamia mamihogo loo siku hiyo!

*MAZOEZI
Mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwani hufanya mwili uwe fit na hivyo huimarisha hata uume na kuufanya usilale kirahisi pale unapokuwa katika show na mrembo. Push up, kukimbia, kurukaruka na mazoezi mengine mengi ni muhimu sana.

*ACHANA NA UNYWAJI WA POMBE ULIOPITA KIASI
Pombe ni hatari sana na inadhoofisha sana nguvu za kiume hivyo chunga sana unywaji wa pombe uliopitiliza kwani ipo siku utajikuta unamwangalia tu mkeo kama dada ako vile wakati yeye nyege zimempanda balaa,matokeo yake itabidi achapwe na njemba zinazojua shughuli huko nje.

*ACHANA NA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME
Hizi dawa ni hatari sana hasahasa zile za hospitali kwani maranyingi zimetengenezwa kwa kemikali ambazo huamsha vichocheo mwili kwa muda flani lakini baada ya muda tatizo litaongezeka maradufu kwani ni tiba kwa muda mfupi tu.

*UWE MAKINI NA UPIGAJI PUNYETO
Hii kitu ni hatari sana hususani kwa wale wanaosugua sana mishipa ya uume hivyo huifanya isiwe ngangari kiasi cha kukusaidia kumshughulikia vizuri mtoto wa kike mwenye nyege zake. Hivyo kama unafanya haka ka mchezo inabidi uwe makini sana usijejutia.


CHANGIA MTAZAMO NA MAONI YAKO JUU YA HII MADA..

Ishara Za Kujua Iwapo Umemkuna Mwanamke Wako Vizuri Kunako 6 X 6..!!!

$
0
0


 Leo acha niwape dondoo
kadhaa kuhusu namna ya kujua kama umemkuna ipasavyo mwanamke wakati wa tendo la ndoa.

1.Kufinya shuka kwa nguvu au kitanda kwa nguvu wakati unampa mambo
ni ishara mojawapo ya
kuonyesha kwamba inamkuna vizuri.

2.Kukukumbatia kwa nguvu au kukufinya:
Hii pia ni moja kati ya ishara nyingi anazoonyesha
mwanamke pindi anapo
----- vizuri.

3.Kutokwa na jasho ndani ya
sekunde chache:
Ukiona anatokwa na jasho ndani ya sekunde chache na katika hali isiyo ya kawaida basi jua kua utendaji wako ni mzuri na
unamridhisha.
Acha niishie hapo kwa leo, lakini sina maana kwamba kama mwanamke wako haonyeshi moja kati ya ishara hizo au zote
basi ndio inamaanisha
haumridhishi, hapana. Hizi ni baadhi tu, zipo nyingi tu.

Jamani Nitoke Nnje ya Ndoa..?Nahitaji Ushauri Wenu...!!!

$
0
0

Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa! 

Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana lakini huwa anadai hakuna tatizo! Najiuliza sana hivi kutoka nje ya ndoa kutanosaidia nini? Nitachinwa pesa bure na ndo matatizo yataongezeka lakini pia kiimani hairuhusiwi nami naogopa kukutwa katika dhambi na Mungu wangu!

Nimesali sana lakini kama hakuna badiliko lolote! Nimuache? Yaani kila kitu tabu tupu! Wasichana nawaogopa mno nahisi wataniongeza machungu je, nitamfute mmama wa wastani kama miaka 34 ila awe mzuri? mi nina 25. Kwakweli sijitambui niko njia panda!

Nilikuwa mwajiriwa wa kampuni fulani na nilikuwa nikilipwa laki 5 kwa mwezi sasa nina miezi 2 nkmeacha kazi sababu ya matatizo ya ndoa yangu!

Sijielewi nahisi naelekea kufa ningepata mwanamke wa umri huo na anaishi tofauti na.mji wangu na akanipenda ningeenda kukaa kwake hata kwa miezi 3.
Nahisi maisha yangu yanaharibika sasa,

Nina uchungu sana usiku huu nilikuwa safari nimerudi na zawadi zimepokelewa na kutupwa sitting rum, ninahamu nimemsogelea kitandani kanipiga pepisi jichoni nomeumia sana maana tangu tuoane sijawahi ifurahia ndoa!

Hapa najiuliza nifanyeje napanga nitoke nikalale guest lakini sina hata wakunifariji natoka naenda guest hata nikifika nikaamua kujitoa duniani inatosha.

Kuna wanawake wazuri sana, wapoleee sauti za upole akikukosea kidogo tu utasikia samahani baba yangu, nakupenda haikuwa nia yangu, jaman namimi si nipate mmoja wa hivi?

Kudadeki..Amri ya Magufuli Kuwalaza Giza Totoro Wazanzibar kwa Muda wa Wiki Mbili Mfululizo,Tanesco Yaanza Kuitekeleza Mara Moja..!!!

$
0
0

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa siku 14 kwa Shirika la Visiwani Zanzibar (ZECO) kulipa deni lote la ankara za umeme wanalodaiwa na endapo halitafanya hivyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukatiwa umeme.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2017, Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) lilikuwa linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 127.8.

“Shirika la umeme linashindwa kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa wakati ikiwemo uendeshaji wa shirika, matengenezo ya miundombinu pamoja na utekelezaji wa miradi, hayo yote yanasababishwa na malimbikizo ya madeni kwa wadaiwa sugu hivyo tunatoa siku 14, wasipoweza kulipa tutawakatia huduma ya umeme”. Alisema Dkt Mwinuka

Aidha mbali na ZECO, Tanesco imewataja wadaiwa sugu wengine ikihusisha Wizara na Taasisi za serikali zikiwa zinadaiwa zaidi ya bilioni 52.5, makampuni binafsi pamoja na wateja wadogo wanaodaiwa zaidi ya bilioni 94.9

Kwa upande mwingine Dkt. Mwinuka amesema shirika hilo linatarajia kuanza oparesheni maalum ya kukusanya madeni hayo na matarajio yao ni kulipwa kwa malikimbizo yote ili yalisaidie kujiendesha kiushandani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegema nishati ya umeme nchini.

Hatua hii imekuja ikiwa ni takriban siku 4 tangu Rais Magufuli kuagiza TANESCO kufuatilia madeni yote ikiwemo deni ambalo TANESCO inalidai ZECO, na kuitaka kuwakatia umeme wote watakaoshindwa kulipa kwa wakati.

Lissu Jeuri Jamani..Eti Amenunua Kesi Ili Akapambane na Serikali Mahakamani..!!!

$
0
0

Baadhi ya wagombea wa nafasi ya  urais kupitia kwa chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS wanatarajia kuwasilisha maombi ya kujumuishwa kama wadaiwa katika kesi ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika tarehe 18  ya mwezi huu.

Wamefikia hatua hiyo ili kuuongezea nguvu upande wa wadaiwa kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa chama hicho ambao wamefungua kesi katika mahakama kuu kupitia mkoa wa Dodoma na Dar es salaamu .

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam  mgombea TUNDU LISSU amesema uchaguzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na watu wengi huku akibainisha kuwa kuna kile alichokiita njama dhidi ya kuuharibu uchaguzi huo

Lissu ameongeza kuwa wanachama wa chama hicho hawatakuwa tayari kuona uchaguzi unasitishwa kutokana na sheria za chama hicho kusisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya sheria nchini.

Katika kesi ya msingi ya kupinga uchaguzi huo iliyofunguliwa na wanachama hao, washtakiwa ni mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na chama chenyewe (TLS).

Kwa upande wake mgombea mwingine wa nafasi ya urais ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani  mheshimiwa LAWRENCE MASHA amebainisha kuwa chama chao hakina kipengele chochote kinachozuia wanasiasa kugombea nafasi ya uongozi katika chama hicho huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika mkaoni Arusha siku ya tarehe 18 ya mwezi huu

Stars Nyang'anyang'a Viwango wa Fifa...!!!

$
0
0

Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango vya soka vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kutoka nafasi ya 158 mwezi Februari hadi nafasi ya 157 mwezi Machi, kati ya wanachama 211 wa FIFA

Kwa mujibu wa viwango hivyo vilivyotolewa , Argentina imeendelea kubaki katika nafasi yake ya kwanza ikifuatiwa na Brazil, huku Ujerumani ikibaki nafasi ya tatu ikifuatiwa na Chile, Ubelgiji, Ufaransa, Colombia, Ureno, Uruguay, na Hispania ikiwa katika nafasi ya 10

Bara la Afrika linaongozwa na Misri ikiwa imepanda nafasi 3 hadi nafasi ya 20, ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 28 na mabingwa wa Afrika Cameroon wanafuata wakiwa nafasi ya 32 ambapo wamepanda kwa nafasi moja.

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda inakamata nafasi ya 74 ikiwa imekwea kwa nafasi moja, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 88, Rwanda nafasi ya 93, Ethiopia nafasi ya 104, Sudan 138, Tanzania 157 huku Somalia, Djibout na Eritrea zote zikiwa mkiani katika nafasi ya 205.

Habari Picha..Rais Magufuli Akiongoza Kikao Cha Baraza La Mawaziri Mjini Dodoma...!!!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU.
Rais Dkt Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mapema leo mchana mara baada ya kumaliza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma,kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawazili,kilichofanyika leo mjini Dodoma
Waziri wa habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Nape Nnauye akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo.PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images