Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live

Shilole Afunguka Kuhusu Ujauzito Wake...!!!

$
0
0

Msanii filamu na muziki wa bongo fleva, Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana ujauzito wowote bali ameridhika na maisha jambo ambalo limefanya aongezeke mwili na kunenepa licha ya watu kuwa na hisia kuwa huenda ana ujauzito.

Shilole amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka saa kumi na mbili kamili.

"Mimi saizi sina ujauzito wowote sema nimenenepa tu maana nimeridhika na maisha haya haya, ukimya wangu ni kwa sababu nilikuwa nazipa ngoma nafasi saizi nimeamua kuja rasmi na wimbo wangu huu 'sitoi kiki' kwani nimegundua Watanzania wanataka burudani, saizi pesa hakuna hivyo nimeona bora nije kuwaliwaza na muziki mzuri huu" alisema Shilole 

Mbali na hilo Shilole amesema video ya wimbo huo ataifanya na waongozaji kutoka hapa hapa Tanzania. 

Dk Shein :Zanzibar Tukikatiwa Umeme Tutatumia Vibatari..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 10/3/2017..!!!

Mbowe Alivyoshiriki Msiba wa Mama Mdogo wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete...!!!

$
0
0
Msiba wa mama mdogo wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, umewakutanisha kwa mara ya kwanza hadharani kiongozi huyo wa Serikali ya awamu ya nne, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Membe.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, viongozi hao walionekana mahasimu zaidi baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, jina lake kukatwa katika kinyang’anyiro cha mbio za urais ndani ya CCM na kuhamia Chadema.

Baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika, Rais huyo mstaafu hakuwahi kuonekana hadharani akiwa na viongozi hao wa upinzani, huku Membe yeye akiwa haonekani kabisa kwenye mambo ya siasa wala mikusanyiko yoyote ile.

Lakini juzi mazishi ya mama huyo, Nuru Khalfan, mbali ya kuwakutanisha viongozi hao, yaliwakutanisha pia Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye.

Wengine walioudhuria ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, ndiye aliyeongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi hayo yaliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.

Mara baada ya kumalizika kwa mazishi hayo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, aliwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushirikiana nao kwenye msiba huo.

Alisema madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili wamefanya kazi kubwa katika kipindi alichokuwa bibi yake amelazwa.

"Naomba niwashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa sababu wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi chote ambacho mgonjwa amelazwa hadi alipofariki," alisema Ridhiwani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Aisifu Tanzania...!!!!

$
0
0

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameisifu Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake za kutafuta amani nchini Burundi.

Guterres alitoa pongezi hizo wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa jijini Dar es Salaam akitokea enya.

Katibu Mkuu huyo mpya wa UN alisimama kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga.

Pamoja na mambo mengine Guterres alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa serikali kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

“Tanzania imekuwa kinara wa amani Afrika na duniani na naipongeza kwa dhati katika jitihada zake inazozifanya za kutafuta amani ya Burundi na katika nchi nyinge za ukanda huu,” alisema Guterres.

Aidha alisema anatambua mzigo mkubwa inaoupata kama nchi kutokana na kuendelea kupokea wakimbizi kutoka Burundi, na kuahidi UN kuendelea kuunga mkono jitihada za kutafuta suluhu ya kisiasa nchini humo.

Kwa upande wake; Balozi Mahiga aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais John Magufuli kuhusiana na hatua iliyofikiwa ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi na ushiriki wa Tanzania katika vikosi vya Umoja wa Mataifa vya ulinzi wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Balozi Mahiga pia alisema Tanzania imefurahishwa na ujio wake na Rais amempa mwaliko rasmi wa kufanya ziara nchini.

Aidha alimweleza kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano wao ujao wana mpango wa kuwasilisha hoja maalum kuhusu hali ya kisiasa nchini DRC.

Mbali na kufanya ziara nchini Kenya, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitembelea Somalia na kukutana na Rais mpya wa nchi hiyo, Hassan Sheikh Mohamud, ambapo aliagiza Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua kuepusha balaa la njaa nchini humo, kutokana na hali mbaya ya ukame.

Namna Magufuli Anavyojizamisha Taratibu...!!!

$
0
0

UMPENDE usimpende, Rais Dk. John Magufuli ameendelea kushangaza, kufurahisha na kuchanganya wengi ndani na nje ya nchi.

Kati ya mkanganyiko huo, wiki iliyopita akiwa katika ziara ya chini ya wiki katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, Rais Magufuli alitoa kauli ambazo sasa zitakuwa zikiwapeleka mbio watu na watendaji mbalimbali: wamiliki wa kampuni za uwekezaji; wanasiasa; mawaziri hadi watu wa chini kabisa.

Kauli za upendeleo kwa wawekezaji

Katika hatua ya upendeleo wa wazi wa Rais Magufuli kwa baadhi ya wawekezaji nchini, wiki iliyopita akiwa mkoani Mtwara alia aliagiza mfanyabiashara maarufu Alhaj Aliko Dangote anayemiliki kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani humo apewe sehemu ya mgodi wa makaa ya mawe unaomilikiwa na TanCoal ili aweze kupata rasilimali hiyo kwa ajili ya nishati ya kiwanda chake.

Rais Magufuli aliagiza kuwa Dangote apewe mgodi huo wa makaa ya mawe na akatoa siku saba kwa Wizara ya Nishati na Madini na wahusika wengine serikalini   kuhakikisha kwamba agizo hilo linatimia ndani ya muda huo.

Raia Mwema limeelezwa kwamba agizo hilo sasa linawapeleka puta watu serikalini kuhakikisha taratibu zote, zikiwamo za kisheria, zinatimia ndani ya siku saba, muda ambao kwa ugoigoi uliotamalaki serikalini huenda likakwama.

Pamoja na makaa hayo ya mawe, Rais Magufuli aligiza pia kwamba kufikia wiki hii, Dangote apewe gesi ya kuendeshea mitambo yake kiwandani bila kupitia kwa mtu au kampuni ya kati.

Lakini, kumbukumbu zinaonyesha kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuagiza mfanyabiashara kupewa upendeleo wa aina hiyo.

“ Kama mtakumbuka  Oktoba mwaka jana Rais Magufuli alizuru viwanda vya Said Salim Bakhresa na akamwagiza Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Charles Mwijage kumrudishia mfanyabiashara huyo sukari yake iliyozuiwa bandarini kutokana na kile alichodai kuwa ‘biashara” yake ina tija kwa taifa.

“Magufuli huyo huyo alitoa agizo kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha ndani ya miezi miwili wamefikisha huduma ya umeme katika kiwanda cha kusindika matunda na kuzalisha juisi cha Bakhresa Food Products Ltd kilichopo Mwandege wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, “ anasema ofisa mmoja serikalini akieleza kwamba akiamini kwamba suala husika lina manufaa mapana kwa taifa, Rais Magufuli hasiti kukata shauri.

Katika sakata la sukari, bidhaa hiyo ya Bakhresa ilizuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam pamoja na ya wafanyabiashara wengine miezi michache nyuma wakati Rais Magufuli alipotangaza kusitisha vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kwa madai ya kulinda viwanda vya ndani.

Agizo hilo la serikali dhidi ya vibali vya kuagiza bidhaa hiyo lilisababisha uhaba mkubwa wa sukari iliyopanda na kufikia wastani wa Sh 4,500 hadi 6,000 kwa kilo moja katika baadhi ya mikoa nchini.

Kwa wakati huo, mambo matatu yalifanyika yanayoweza kutafsiriwa kuwa ni upendeleo kwa Bakhresa, kwanza, kurejeshewa sukari yake iliyozuiwa sawa na wafanyabiashara wengine, pili, agizo la moja kwa moja la kupatiwa umeme ndani ya miezi miwili, tatu, kupewa eneo la ukubwa wa ekari 10,000 bure ili alime miwa na kufungua kiwanda cha sukari – uamuzi ambao unampa unafuu wa kiuwekezaji Bakhresa ikilinganishwa na wawekezaji wengine watakoamua au waliokwishakuamua kuwekeza kwenye sekta hiyo mahsusi.

Ingawa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bakhresa, Aboubakari Salim, siku hiyo aliweka bayana kwamba kumekuwa na urasimu mwingi katika upatikanaji wa maeneo mapya ya kuanzisha viwanda, lakini bado wapo wawekezaji wanaoamini mwenendo wa Rais Magufuli kwa wawekezaji hautoi fursa sawa kwa wote.

Mtaalamu wa uchumi nchini, Profesa Honest Ngowi, anashauri kwamba serikali ni lazima ijijengee taswira ya kuwaunga mkono kwa usawa wawekezaji wote nchini, na si kuelemea upande mmoja.

“Kimsingi ni vizuri wawekezaji wote wakapata mazingira sawa na ya kuvutia kama Dangote. Wote wakipata uwanja sawa wa kufanya biashara ni bora zaidi,” anasema Profesa Ngowi ambaye katika mazungumzo yake na gazeti hili alikuwa nchini Uswisi.

Pamoja na “upendeleo’ huo wa wazi, Rais Dk Magufuli pia alitoa kauli ambazo zimetafsiriwa kuwa ni tata na huenda nyingine zikazua mijadala ya muda mrefu na ama zisitekelezwe kama alivyoagiza.

Deni la Umeme SMZ

Akiwa bado katika ziara hiyo ya Kusini mwa Tanzania, Rais Magufuli aliliagiza Tanesco kuhakikisha kwamba linawakatia umeme wadaiwa sugu hata kama hao ni serikali, na hata kama ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Kwa muda mrefu kumekuwa na ukakasi kwa Tanesco kuidai SMZ, na kwa miaka mingi, matamko mengi yamekuwa kama maji machemu yasiyounguza nyumba, kwa vile yalibaki kuwa matamko.

Kwa kauli ya wiki iliyopita ya Rais Magufuli, taarifa kutoka Tanesco zimesema kwamba iko mbioni kuandaa mchakato wa jinsi ya kuidai SMZ limbikizo la deni linalokadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 100.

Taarifa zaidi zinasema kwa upande wake SMZ inasema mchakato wa kulipa deni hilo ulikuwa mbioni na kwamba mara kadhaa mazungumzo yamefanyika kati ya SMZ na Bara na Tanesco kufikia muafaka wa ulipaji.

Bila shaka, kama hatimaye Tanesco itaikatia umeme SMZ hatua hiyo itazua changamoto za kisiasa baina ya Bara na Visiwani.

Hata hivyo, wakati Tanesco wakisisitiza utekelezaji wa agizo la Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mohammed Aboud, amenukuriwa na vyombo vya habari akisema wanaendelea na mazungumzo kati ya mawaziri husika wa pande mbili za Muungano juu ya namna ya kulipa deni hilo.

“Lengo letu ni kulipa deni lote kwa sababu ukidaiwa lazima ulipe. Sisi tupo tayari kulipa ndiyo maana tumeanza kufanya mazungumzo na wenzetu wa Tanzania Bara jinsi gani tunaweza kukubaliana juu ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kulipia hatua kwa hatua ili kumaliza deni,” amenukuriwa akisema Aboud.

Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa SMZ Salama Aboud Talib amekaririwa mwanzoni mwa wiki akisema kwamba hadi Januari 2017, ZECO ilikuwa inadaiwa Sh121 bilioni, kwa mujibu wa barua iliyowakilishwa kwake na Tanesco.

Mchanga wa madini

Lakini amri ya hivi karibuni ya kutaka mchanga wa madini kutosafirishwa nje ya nchi nayo imeibua mjadala wa aina yake, na hasa suala la maandalizi ama nchi kujenga uwezo wa kuchenjua mchanga huo wa madini hapa nchini.

Akiwa katika ziara hiyo ya Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, Rais Magufuli aliamuru mchanga wa madini, maarufu kama makinikia (copper concentrate) kutosafirishwa nje ya nchi.

Kwa Tanzania, kampuni moja tu ya Acacia ambayo inamiliki migodi minne ya dhahabu ndiyo inasafirisha makinikia nje ya nchi wakati Anglo-Gold wanaomiliki mgodi wa dhahabu Geita wakiwa hawafanyi hivyo.

Hatua hiyo sasa, kama anavyoripoti mwandishi wetu FELIX MWAKYEMBE imeigawa serikali katika makundi mawili, kundi la wataalamu wa masuala hayo na kundi la wanasiasa.

Kwa mujibu wa amri ya Rais aliyoitoa akiwa Mkuranga mkoani Pwani, uamuzi huo unelenga zaidi kulinda rasilimli za Taifa.

Tayari Kampuni ya Acacia, ambayo ni muathirika mkuu na zuio hilo, imetangaza kusimamisha usafirishaji wa makinikia ya shaba/dhahabu inayozalisha katika migodi yake miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu, ikiwa ni kutii agizo la Rais.

Pamoja na migodi hiyo miwili, Kampuni ya Acacia pia inamiliki mgodi wa North Mara ambao uzalishaji wake wa dhahabu ni tofauti na hiyo migodi miwili.

Wiki iliyopita, Machi 03, 2017, kampuni hiyo ilitoa taarifa rasmi kwa umma inayoelezea kusimamisha usafirishaji wa makinikia ya shaba/dhahabu, muda mfupi baada ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini kutoa taarifa ya serikali kwa umma kuhusu zuio la usafirishaji makinikia na mawe yenye madini kwenda nje.

Hatua hiyo ilisababisha bei ya hisa za kampuni ya Acacia kwenye masoko ya London na Dar es Salaam kupungua kwa takriban asilimia 18.

Mpaka sasa, bei ya hisa za kampuni hiyo bado hazijaimarika na hiyo imeathiri hata mtaji wa soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwani Acacia ndiyo kampuni yenye mtaji mkubwa.

Gazeti la kimataifa ya The Financial Times la Uingereza liliripoti wiki jana kwamba hisa za Acacia zilishuka kwa asilimia 18 kwenye soko la hisa la London, kutokana na kupungua kwa imani ya wawekezaji kwenye kampuni hiyo baada ya kusikia agizo la Rais Magufuli.

Kwa miaka mingi sasa imekuwapo hofu miongoni mwa wananchi kwamba Tanzania inaibiwa kupitia hatua ya kampuni za madini nchini kusafirisha nje ya nchi makinikia kwa ajili ya uyeyushaji kutokana na kukosekana kwa viwanda hivyo nchini.

Lakini wataalamu kwa upande wao wanabainisha kuwa ujenzi wa kiwanda cha kuyeyusha makinikia hayo hautakuwa na faida za kiuchumi kwa Taifa.

Tafiti za kitaalamu zinaonyesha kwamba  makinikia ya shaba (copper concentrate) yanayozalishwa nchini hayakidhi ujenzi wa kiwanda cha kuyeyushia (smelter) kutokana na gharama ya ujenzi kuwa juu ikilinganishwa na kiwango kinachozalishwa kisichokidhi hata mahitaji ya chini ya smelter.

Kwa mujibu wa utafiti wa mwisho kufanywa kuhusu suala hilo, ipo migodi miwili tu ya dhahabu yenye kulisha makinikia hiyo ya shaba na dhahabu, nayo ni Buzwagi na Bulyanhulu.

Taarifa ya utafiti huo uliofanywa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) inabainisha kuwa kiwango cha makinikia hiyo ya shaba na dhahabu kinachozalishwa na migodi hiyo miwili haifiki hata nusu ya kiwango cha chini kinachohitajika kuyeyushwa na kiwanda hicho.

Miongoni mwa mambo ya msingi yaliyomo kwenye taarifa hiyo ya utafiti ya Februari 2011, ni pamoja na kiwango kinachozalishwa na migodi hiyo miwili, Buzwagi na Bulyanhulu ambacho hakizidi tani 60,000 kwa mwaka, wakati mahitaji ya chini ya kiwanda cha kuyeyusha makinikia ni tani 150,000 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya utafiti, mgodi wa Buzwagi huzalisha na kusafirisha makinikia ya shaba kati ya tani 25,000 na 50,000 kwa mwaka wakati ule wa Bulyanhulu huzalisha na kusafirisha tani 10,000 kwa mwaka.

Utafiti huo unaofahamika kama “A Study on Viability to Construct a Copper Concentrate Smelter in Tanzania,” unafichua kuwa takribani wazalishaji wote wa makinikia duniani, sawa na yanayozalishwa nchini, hawana viwanda vyao wenyewe vya kuyeyushia.

Wazalishaji hao nao husafirisha nje, hususan, katika nchi za China, India na Japan kwa ajili ya kutenganisha dhahabu na shaba.

Makinikia ya shaba yanayozalishwa na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu nchini, husafirishwa kwa ajili ya kuyeyushwa, katika viwanda vya Marc Rich Investment nchini China, Sumitomo Metal Mining Co. Ltd na Pacific Co. Ltd vya nchini Japan au Aurubis AG  nchini Ujerumani.

Raia Mwema inazo taarifa zisizo shaka kwamba TMAA haijafanya utafiti mwingine zaidi ya huo wa mwaka 2011.

“Kimsingi hatujafanya study nyingine, na hatuwezi zungumzia kauli ya Rais,” kilisema chanzo chetu cha habari kutoka TMAA kwa sharti la kutotajwa jina.  

Utafiti huo unabainisha pia kwamba gharama ya ujenzi, kwa kiwanda kilichokamilika, ni kati  ya dola za Marekani milioni 500 hadi 800, zaidi ya shilingi trilioni moja.   

Kiuchumi, inabainishwa kuwa kiwanda cha kuyeyusha kinahitaji mzigo wa makinikia usiopungua tani 150,000 kwa mwaka, lakini uzalishaji wa migodi miwili hapa nchini ya Buzwagi na Bulyanhulu hauzidi tani 60,000 kwa mwaka, kiwango ambacho ni asilimia 40 tu ya uwezo wa kiwanda.

Ili kukidhi mahitaji ya kiwanda, Tanzania italazimika kutegemea zaidi asilimia 60 ya makinikia kutoka kwa wazalishaji wa nje, ama sivyo Tanzania ifungue migodi mingine itakayotumia teknolojia hiyo.

Hata hivyo, hoja ya kufunguliwa kwa migodi mipya itakayotumia teknolojia hiyo inakabiliwa na changamoto moja kuu, kwamba hadi wakati utafiti huo unafanyika, hakukuwa na ugunduzi mpya wa madini ya “copper sulphide” ambayo ingesaidia kuongezea katika mahitaji ya makinikia ya shaba.

Wataalamu hao wa masuala ya madini nchini wanabainisha, katika taarifa yao, kwamba suala la gharama na upatikanaji wa umeme wa uhakika ndiyo mambo ya msingi katika kuamua kujenga kiwanda cha kuyeyushia makinikia.

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe katika maoni yake kuhusu suala hilo la makanikia anasema uamuzi huo wa Rais Magufuli ni sahihi, lakini wakati si sahihi.

Anasema Kabwe Zitto: “…kuweka zuio la kusafirisha mchanga wa dhahabu ni uamuzi sahihi uliofanywa bila kuzingatia kwanza uwezo wa ndani wa kuchenjua( refinery).”

 “Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini. Haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa (economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 hivi. Pia tunahitaji umeme zaidi ya 1500mw kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama uwezekano wa eneo letu kuzalisha hizo copper concentrates ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye ukanda huu.

“Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo.  Sasa mjadala hapa ni kwa nini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio alilotoa Rais ndiyo litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa.

Kwa hiyo amri ya Rais iwe ni kuleta mjadala kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana.”

Alisema wataalamu wanaweza kubuni teknolojia yenye uwezo wa kufanya uchenjuaji kwa kiwango cha mchanga tunachozalisha nchini na kusisitiza kuwa, haiwezekani dunia nzima ikawa na teknolojia moja tu ya tani 150,000 la hasha.

“Ushauri wangu ni kwamba serikali ikae na sekta ya madini ili kupata jawabu la kudumu na kuweka azimio la muda maalumu kuendelea kusafirisha mchanga na baada ya muda huo mchanga huo uchenjuliwe nchini kwetu na kuzalisha ajira na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha. Hii sio zero-sum game (kama si kusafirisha basi hakuna lingine). Hapana. Mjadala unaweza kuleta jawabu lenye faida kwa nchi,” alisema.

Licha ya kutafutwa na gazeti hili, uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini umekuwa kimya kuhusu namna gani agizo hilo la Rais Magufuli ‘litatekelezeka, kwa kuzingatia matokeo ya utafiti uliofanywa na TMAA Februari mwaka 2011.

Mradi wa Maji Lindi

Na katika hatua nyingine, akiwa ziarani mkoani Lindi wiki iliyopita, Rais aliagiza pia kupokonywa hati ya kusafiria ya mhandisi mshauri wa Mradi wa Maji Lindi hadi hapo mradi huo utakapokamilika.

Uamuzi wa kumnyang’anya hati ya kusaifiria raia huyo wa India ulitokana na kusuasua kwa uendelezaji wa mradi ambao utatoa huduma ya maji kwa mamia ya maelfu ya Watanzania hasa Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Credit -Raia Mwema

Vipimo vya Faru John Kugharimu ,Mil. 700/- Chuo Kikuu Pretoria..!!!

$
0
0

VINASABA vya faru John vinatarajiwa kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa vipimo vya vinasaba (DNA ) muda wowote kuanzia wiki hii baada kupatikana kwa mfadhili wa kulipia gharama za vipimo hivyo, 

Faru John alizua gumzo nchini mwishoni mwa mwaka jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya ziara katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) na kuwatuhumu maofisa wa shirika hilo na wale wa Idara ya Wanyamapori kwa ‘kumuuza’ faru John kwa kampuni ya Grumeti kwa takriban shilingi milioni 200.

Kutokana na tuhuma hizo maofisa zaidi ya watano kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Idara ya Wanyapori na Tawiri walitiwa mbaroni kwa mahojiano na vyombo vya usalama. Hata hivyo, baada ya muda maofisa hao waliachiwa huru.

Kampuni hiyo ya Grumeti ambayo imewekeza katika shughuli za biashara ya hoteli, utalii na uhifadhi inamiliki hifadhi ndogo (sanctuary) ya Faru Weusi pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Aidha katika mfululizo wa matukio kuhusu sakata la faru huyo baadaye ilibainika alifariki dunia Agosti mwaka jana na waziri mkuu aliunda kamati maalumu kuchunguza kifo chake na pia kupimwa DNA.

Taarifa zilizofika  kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii zimeeleza kuwa tayari nyaraka zote muhimu kuhusu kupelekwa kwa vipimo hivyo nchini humo zimekamilika.

Habari zaidi zinaeleza kuwa pamoja na kukabidhi  nyaraka, maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watakabidhi pia sampuli za vinasaba hivyo kwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali  ili visafirishwe kwenda Afrika Kusini.

Awali ilidaiwa kuwa kulikuwa na hali ya utata kuhusu nani hasa atalipa gharama za vipimo hivyo vya DNA baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kushindwa kupata fedha za kugharimia vipimo hivyo.

“Taarifa ni kwamba kuna mfadhili amepatikana (hakutaja jina) na kulipia gharama za vipimo vya DNA nchini Afrika Kusini katika maabara ya kupima vinasaba ambayo iko kitivo cha wanyama katika Chuo Kikuu cha Pretoria,” kilieleza chanzo chetu ndani ya Wizara hiyo.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa gharama za vipimo hivyo ni katika ya dola za Marekani 300,000 hadi 500,000 ambazo ni zinaweza kufikia kati ya shilingi za Tanzania milioni 700 hadi bilioni moja.

“Kwa kweli gharama za kufanya vipimo vya DNA ziko juu sana na serikali haikuwa na fedha zilizotengwa kwa kazi hiyo, amepatikana mfadhili ambaye atalipia gharama hizo hivyo muda wowote kuanzia sasa vipimo vitapelekwa Afrika Kusini baada ya kukamilika kwa nyaraka zote muhimu,” alieleza mmoja wa maofisa wa wizara hiyo aliyeomba asitajwe jina gazetini kwa kuwa si msemaji wa suala hilo.

Majibu ya vipimo hivyo ndiyo yanayotarajiwa kutengua kitendawili cha iwapo sampuli za vinasaba zilizochukuliwa kutoka katika mabaki ya mnyama huyo zinaoana na zile zilizoko kwenye pembe yake na kujua iwapo faru huyo alikufa kama watendaji wa Idara ya Wanyapori wanavyodai au la.

Juhudi za kumpata msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dorina Makaya hazikuweza kufanikiwa kutokana na simu yake kutokuwa hewani kwa muda mrefu lakini Afisa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Hamza Temba, alisema kwa kifupi kuwa suala hilo liko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na pia Mkemia Mkuu wa Serikali.

 “Sidhani kama jambo hilo liko chini ya wizara kwa kifupi ninavyofahamu suala hilo liko chini ya ofisi ya waziri mkuu na pia mkemia mkuu wa serikali,” alisema ofisa huyo.

Maabara ya Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini ( Veterinary Genetics Laboratory – VGL))  kwa mujibu wa mtandao wa researhmatters.up.ac.za ilianzishwa mwaka 2009 baada ya kuwapo kwa wimbi kubwa la ujangili dhidi ya wanyama hao nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao huo wataalamu wa chuo hicho kitivo cha utafiti na tiba ya wanyama wakiongozwa  na Dk. Cindy Harper walifikia uamuzi wa kuanzisha maabara hiyo kwa lengo la kukusanya sampuli za vinasaba kutoka kwa wanyama hao na kuhifadhi katika kanzidata (database) ya maabara ili zitumike kama sehemu ya ushahidi mahakamani katika kesi za ujangili wa faru.

Ugunduzi na uamuzi wa wataalamu hao ulitokana na kesi nyingi dhidi ya majangili kukwama na wengi kuachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi dhidi yao.

Kwa mujibu wa mtandao huo wataalamu hao wa chuo hicho hutumia sampuli za vinasaba na kuoanisha na alama za vidole vya majangili kisha kuwapa waendesha mashitaka ili kujenga ushahidi thabiti wa kuwatia hatiani washitakiwa.

Takwimu zinaonyesha kuwa dunia ina faru wasiozidi 29,000 kati ya faru 500,000 waliokuwepo mwanzoni mwa karne ya 20 na Afrika Kusini ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama hao kwa sasa.

Kutokana na ujangili wa muda mrefu dhidi ya faru na mahitaji ya pembe zake katika nchi za kiarabu na zile za Asia ya Kusini ambazo wakati mwingine hutumika kama dawa za kiasili kumesababisha dunia kubakiza karibu asilimia moja tu ya faru. 

Nchini Afrika Kusini pekee kati ya mwaka 2010-2015 zaidi ya faru 500 waliuawa na majangili na mwaka 2013 ulivunja rekodi kwa faru 1,008 kuuawa na majangili.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alishindwa kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao cha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili.

Uteuzi wa Mama Salma Kikwete Kuwa Mbunge Unafanya Hesabu za 2025 Kuwa Ngumu...!!!!

$
0
0

KATIKA historia yake ya miaka 50 na ushee, Tanzania haijawahi kuwa na Mke wa Rais, mstaafu au aliye madarakani, bungeni. Wiki iliyopita, Rais John Magufuli akaweka historia mpya kwa kumtangaza Salma Kikwete, mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, kuwa Mbunge wa Kuteuliwa.

Na Mama Salma si First Lady wa kawaida. Kwenye historia ya miaka 50 hiyohiyo, Tanzania haijawahi kuwa na mke wa Rais ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwaka juzi, nilikuwa ndani ya ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma wakati wa kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais kupitia chama hicho.

Mama Salma alikuwa amekaa pembeni ya Benard Membe aliyekuwa  mmoja wa wagombea waliokuwa wakipewa nafasi kubwa kushinda.

Wakati wake wa marais waliopita wa Tanzania walikuwa hawatajwi katika vinyang’anyiro vya namna hii; haikuwa siri kwamba Salma alikuwa akitaka Membe ndiye awe Rais wa Tanzania baada ya Kikwete.

Na ndiyo sababu, ilikuwa ikijulikana kuwa Membe huyohuyo ndiye alikuwa chaguo la Kikwete mwenyewe. Na hii ni kwa sababu, haingewezekana kwa Salma kupiga kampeni hadharani kwa mtu ambaye mumewe hamuungi mkono.

Mara baada ya Magufuli kumtangaza Salma kuwa mbunge, nilichora kwenye karatasi duara moja lililozungukwa na miduara mingine mingi. Lengo langu lilikuwa kutafuta sababu hasa za Rais kufanya uteuzi ambao hakuna aliyekuwa akiutarajia.

Uteuzi wa Salma unahitaji tafakuri ya kipekee. Huyu ni mwanasiasa ambaye tayari ameshiriki katika siasa za juu kabisa za taifa letu. Kama ana ndoto au mpango wowote ule, hauwezi kuwa mpango wa mambo madogo madogo.

Tafakuri yangu ilinifikisha pia katika tukio lilitokea mwishoni mwa wiki hiyohiyo; wakati Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Sofia Simba, alipotangaza kuwa hatawania tena nafasi hiyo.

Salma, anaweza kabisa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa UWT. Hii ni kwa sababu sasa anakijua chama chake vizuri, anajulikana miongoni mwa akinamama nchini na kwa sababu ya mumewe, tayari ana kada maarufu wa chama nyuma yake.

Na kama Salma atakuwa Mwenyekiti wa UWT, maana yake ni kwamba atakuja kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Ukichanganya na nafasi yake bungeni, maana yake ni kwamba atakuwa na fursa pana ya kukutana na watu na makundi mbalimbali.

Hadi sasa, mwanamke mwenye madaraka makubwa kuliko wote hapa nchini ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Kwenye siku za karibuni, ushawishi wake katika jamii umekuwa ukiongezeka kila kukicha.

Kuna wanaoamini kwamba tayari ana sifa za kumrithi Dk. Ali Mohammed Shein kwenye uchaguzi ujao wa Zanzibar na kuna wanaoamini kwamba kama Tanzania iko tayari kwa Rais wa kwanza mwanamke, Samia yuko katika nafasi nzuri sasa kuliko mwanamke mwengine yoyote.

Ujio wa Salma kwenye siasa, unapunguza kidogo nguvu ya ushawishi wa Samia. Ni wazi kwamba Kikwete alipigiwa kura nyingi na wanawake wakati akitafuta urais na ni rahisi kwa mapenzi hayo kuhamia kwa Salma.

Pia, miaka tisa ijayo, watoto wa kike ambao walisomeshwa na Salma kupitia taasisi yake ya Wanawake na Maendeleo (Wama), watakuwa watu wazima ambao wana ushuhuda wa namna mama huyu alivyowasaidia.

Hata hawa wasanii maarufu wa kike na kiume hapa nchini ambao kwa sasa wanaonekana kumuunga mkono Samia, watahamia kwa Salma kirahisi tu kama Kikwete atataka hivyo.

Hii ni kwa sababu, hakuna kiongozi mwengine hapa nchini anayeweza kujidai kuwa na ushawishi mkubwa kwa wasanii hapa nchini kuliko Jakaya.

Kama Magufuli angeacha hali ya sasa (status quo) iendelee, ni wazi kuwa Samia ndiyo angekuwa mwanamke mwenye ushawishi mkubwa kuliko mwengine yeyote hapa nchini kuelekea 2020 na 2025.

Hadi sasa, hakuna anayejua sababu hasa za Magufuli kumteua Salma kuwa mbunge. Kwa wanaofahamu siasa za CCM zilivyo sasa, si siri pia kwamba hatua hii inaonekana kuwa na lengo la kukiweka chama pamoja.

Lakini, wakati nachora duara zangu za kuangalia nje ya boksi, nimeona pia kwamba hatua hii ya Magufuli –hata kama pengine yeye hakuwa na dhamira hiyo, inapunguza ushawishi wa kisiasa wa Makamu wake wa Rais walau kwa Tanzania Bara.

Bila shaka, kuanzia siku ambayo Salma ataapishwa rasmi kuwa mbunge, ramani mpya ya michezo ya kisiasa ndani ya CCM itaanza kuchorwa.

Na kwa kuanzia, wiki ijayo, nitaeleza namna kinyang’anyiro cha kuwania urais kumrithi Magufuli kitakavyoathiriwa na uteuzi huu wa sasa wa Mama Salma Kikwete.

Imeandikwa na Ezekieli Kamwaga wa Raia Mwema

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni


Nyota ya Mbwana Samatta Yazidi Kung'aa Europa League, Hivi Ndivyo Alivyofanya Maajabu Mechi ya Jana

$
0
0
Mashabiki wa soka wa Tanzania ambao wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya soka la nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ataifanyia nini katika mchezo wa kwanza wa UEFA Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent kutoka Ubelgiji pia.

Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk walikuwa ugenini kucheza mchezo wao huo wa kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent, Samatta anarudi katika historia tena baada ya kufanikiwa kuifungia goli mbili KRC Genk dhidi ya KAA Gent katika ushindi wa 5-2.

Mbwana Samatta anafunga goli hizo mbili katika mechi yake ya 9 ya Europa League toka waingie katika hatua ya makundi na alikuwa hajafunga goli lolote, magoli ya Genk yalifungwa na Ruslan Malinovsky dakika ya 21, Omar Colley dakika ya 33, Mbwana Samatta dakika ya 41 na 72 na Jere Uronen dakika ya 45.

KAA Gent ambao watalazimika kuifuata KRC Genk katika mchezo wa marudiano March 16 2017, magoli yao mawili yalifungwa na Samuel Kalu dakika ya 27 na Kalifa Coulibaly dakika ya 61, ushindi huo unawapa matumaini ya zaidi ya asilimiana 50 Genk kucheza robo fainali maana ili watolewe labda KAA Gent ashinde kwa goli 4-0 mchezo wa marudiano. Tazama Video:

VideoFUPI: Rais Magufuli Alivyoirudia Mistari ya Wimbo wa ‘Muziki’ wa Darassa

$
0
0
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amekuwa akisifika kutokana na utendaji kazi wake lakini pia ni moja kati ya viongozi ambao wanaweza kuongea na wananchi na kuchombeza na maneno ya utani.

Licha ya kuwa Rais Magufuli ni mtu makini na mkali kwa watumishi wasiotekeleza majukumu yao lakini alifurahisha umati wa watanzania alipokuwa akiongea nao na kugusia wimbo wa ‘Muziki‘ wa Darassa katika sehemu ya hotuba zake kwa kunukuu mistarii miwili mitatu.

Tundu Lissu, Masha Wataka Kujumuishwa Kesi ya Kupinga Uchaguzi TLS

$
0
0
Wanasheria wawili wa jijini Dar es Salaam, Tundu Lissu na Lawrence Masha wamesema wataiomba mahakama kuwajumuisha kama wadaiwa katika kesi za kupinga uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walizodai zimefunguliwa jijini Dar es Salaam na Dodoma.

Lissu, ambaye ni mbunge wa Iramba na mwanasheria wa Chadema, na Masha (mwanachama wa Chadema na waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani) wamedai kuwa kesi hizo mbili zimefunguliwa Mahakama Kuu na Godfrey Wasonga mjini Dodoma na Onesmo Mpinzile jijini Dar es Salaam, wakitaka uchaguzi huo uzuiliwe.

Mawakili hao wamewahi kupambana katika kesi mbili tofauti zilizohusu vyama vya CCM na Chadema.

Wasonga aliwahi kupambana na Lissu katika kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM mjini Dodoma waliopinga ushindi wa mbunge huyo wa Singida Mashariki katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, wakati Mpinzile alipambana na mwanasheria huyo wa Chadema aliyekuwa akimtetea mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali ambaye amehukumiwa miezi sita jela.

Hata hivyo, Wasonga alisema jana kuwa hajafungua kesi ila anakusudia kufanya hivyo.

Hatua ya Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema, kuchukua fomu ya kuwania urais wa TLS akisema imechagizwa na kauli ya Rais John Magufuli dhidi ya mawakili, ilibadili upepo wa uchaguzi huo na kumlazimu Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kuuzungumzia akisema Serikali haitavumilia kuona chama hicho kinajiingiza katika siasa.

TLS imekuwa ikafanya uchaguzi kila mwaka, lakini umekuwa hauna harakati kubwa kama ulivyo wa mwaka huu. Tayari TLS imepitisha wagombea urais, wakiwamo Lissu na Masha.

Mbali na kuwa mawakili, Masha na Lissu, ambao wote wanawania urais, ni wanachama wa Chadema, jambo linaloonekana kuchochea mjadala wa siasa kuingia katika chama hicho.

Lakini, mgombea mwingine, Godwin Mussa Mwapongo, pia ni kada wa CCM aliyechukua fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea urais mwaka 2015 ingawa hakufanikiwa. Mgombea mwingine ni Victoria Mandari.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Lissu alisema wamepata wasiwasi kuwa huenda kukawa na njama za washtakiwa katika kesi hiyo, ambao ni TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kutojitetea vya kutosha na hivyo kukubali mashtaka ili uchaguzi huo uzuiwe.

Alisema ili hali hiyo isijitokeze, wataiomba masjala ya Mahakama Kuu iliyopo Dar es Salaam, iwaunganishe katika kesi hizo kama wadaiwa.

“Uchaguzi ukizuiwa, maslahi yetu sisi tunaogombea yatakuwa yamevurugwa kwelikweli. Kwa sababu hiyo na kwa mujibu wa taratibu zinazoruhusiwa kisheria, sisi ambao tunagombea na wapigakura wanaotaka, tutapeleka maombi haraka ili tuunganishwe kwenye kesi zile kama wadaiwa,” alisema Lissu.

“Tutanunua ile kesi, kusije kukawa na njama za uongozi wa sasa wa TLS kuendelea kuongoza baada ya muda wao wa kikatiba kuisha na kusije kukawa na njama ya kuzuia uchaguzi na wale ambao wanataka kuvuruga TLS wakafanikiwa.”

Lissu alisema lengo jingine ni kutaka masuala ya uchaguzi huo yasije yakaamuliwa nyuma ya migongo yao au juu ya vichwa vyao na hivyo wanataka kupata fursa kamili ya kuiambia mahakama kwanini maombi hayo ya kuzuia uchaguzi hayana msingi wowote.

Aliongeza kuwa mawakili hao walioamua kuweka mapingamizi ni wanachama wa TLS na walikuwa na nafasi ya kuweka mapingamizi baada ya kamati ya uteuzi kutangaza majina ya wagombea.

“Kulikuwa na kipindi cha karibu wiki mbili cha kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea walioteuliwa, fursa hiyo mwisho wake ilikuwa Machi 15 mwaka huu, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeweka mapingamizi hayo. Itabidi tuwahoji,” alisema.

Kwa upande wake, Masha alisema hakuna mtu hata mmoja kati ya wagombea wote wa urais aliyeamua kuingia na kugombea kwa sababu za kisiasa.

Masha alisema licha ya kuwa hana nafasi ya uongozi Chadema, ni mwanachama aliyekuwa wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kabla Lissu hajachukua fomu hiyo.

Alisema kama kungekuwa na mbinu za kisiasa, yeye na Lissu wasingechukua fomu ya kuwania nafasi moja.

“Lissu alikuja kuchukua fomu baada ya muda wa kushiriki katika uchukuaji wa fomu kuongezwa, kama tungekuwa na njama ya kisiasa isingekuwa rahisi kwa Lissu na mimi wote kuchukua fomu kugombea nafasi moja,” alisema waziri huyo wa mambo ya ndani wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Masha alisema chama hicho kinaongozwa kwa mujibu wa sheria na kwamba hakina uhusiano wowote katika masuala ya kisiasa.

Kuhusu matukio yaliyojitokeza Lissu alisema anashangaa kuona Serikali inaingilia suala la uchaguzi wa TLS, akisema hii ni mara ya kwanza tangu kuundwa kwake, zaidi ya miaka 60 iliyopita.

“Ni mara ya kwanza kwa Serikali kuingia moja kwa moja katika suala la nani anapaswa kuwa kiongozi wa chama hiki. Hii haijawahi kutokea tangu TLS ilipoanzishwa 1954,” alisema.

Alisema chama hicho kinaongozwa kwa mujibu wa sheria na kwamba kuwa wanachama au viongozi wa vyama vya siasa, hakuna maana yoyote ile TLS.

“Linapokuja suala la uchaguzi wa TLS nafasi zangu zote nilizonazo hazina maana. Kitu pekee chenye maana ni je wewe ni wakili mwenye sifa zote zinazotakiwa ili kuweza kugombea nafasi unayotaka kugombea katika chama cha mawakili,” alisema Lissu.

“Nadhani Dk Mwakyembe anayafahamu haya, kama atakuwa hayafahamu ni bahati mbaya sana. Wapiga kura ndio waamuzi wa mwisho kwenye uchaguzi huu. Hatutaki baraka za yeyote.”

Rais wa Zanzibar, Dr. Shein: Mkitaka kuzima umeme zimeni, tutawasha vibatari

$
0
0
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.


Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.

Dkt. Shein katika mazungumzo yake na vyombo vya habari alilezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema mkutano huo utaleta tija na faida kubwa kwa wazanzibari na watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii,uvuvi,ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.

Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya na ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.

Tazame:
Chanzo: ITV

Shilole Afunguka Kuhusu Barnaba

$
0
0
Jana malkia wa muziki Bongo, Shilole ameachia wimbo wake mpya uitwao Hatutoi Kiki. Kama zilivyo ngoma zake zilizopita, ngoma hii pia imeandikwa na Barnaba Classic.

Kwenye interview na kipindi cha Supermega Cha Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove, mrembo huyo ameweka wazi sababu za kupenda kumtumia Barnaba kwenye utunzi wa ngoma zake.

“Barnaba ananijulia sana katika uimbaji wangu, yaani akiandika ngoma,anauvaa uhusika wangu,” amesema Shilole.

Shilole amedai kuwa hiyo ndiyo sababu kubwa ya yeye kupenda kuandikiwa ngoma na mkali huyo wa High Table Sound.

Diamond Aizindua Tovuti ya Kuuzia Muziki Pinzani Kwa Mkito

$
0
0
Tovuti namba moja ya kuuzia muziki nchini, Mkito.com, imepata mpinzani mpya, Wasafi.com. Diamond Platnumz ameizindua rasmi website yake ya kuuzia muziki, si tu wa wasanii wa WCB, bali wasanii wengine pia.

Wiki hii, hitmaker huyo wa Marry You, amekuwa akifanya mikutano ofisini kwake na wasanii mbalimbali, kuzungumza namna ya kufanya nao kazi kwenye mradi huo. Tayari amekutana na wasanii kama Ben Pol, Barnaba, Cassim pamoja na Chege na Temba.

Kwa mwelekeo huo, Wasafi.com inakuja kuwa mpinzani mkubwa wa Mkito.com, ambayo hadi sasa ndio website inayotegemewa na wasanii wengi kuuzia nyimbo zao.

Msanii wa WCB, Harmonize anaachia wimbo wake mpya exclusively kupitia website hiyo inayokuja na app yake pia.

Jokate Akerwa na Matusi kwa Wanawake...!!!

$
0
0

Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo amewataka watu kuacha kutumia lugha za maneno makali (matusi) dhidi ya wanawake kwa kuwa wanawake ni watu wanaohifadhi maumivu na mambo mengi  kwenye moyo zaidi ya wanaume.

Jana wakati akikabidhi mchango wake EATV katika kampeni ya 'Namthamini', Jokate amesema mwanamke ni mtu ambaye anakumbana na mambo makubwa anayopaswa kukabiliana nayo mengine ni mazito lakini anayaweka moyoni mwake ili kufanikisha jambo hivyo anapaswa kuheshimiwa.

"Najisikia vibaya sana pale ambapo mtu namsikia anatoa lugha ya matusi kwa mwanamke, Wanawake tunaumia zaidi ya mara 1000 kwa mwanamke, mwanamke anahifadhi mambo mengi sana moyoni kitu ambacho hakitakiwi, wanawake wanapaswa kuheshimiwa na kulelewa katika jamii na wanastahili kuthaminiwa". Amesema Jokate

Ameongeza kuwa yeye kwa upande wake mwanamke ni mtu mwenye moyo wa ziada ambaye hujitoa kwa ajili ya jamii lakini pia ni mchapa kazi na anajua kitu gani anataka.

Katika kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na EATV kuwachangia mabinti waende shule bila kukosa kwa kigezo cha kuepuka aibu inayosababishwa na ukosefu wa vifaa vya kujisitiri kipindi cha hedhi, Jokate amechangia kiasi cha shilingi laki moja.

Laana Inayoitafuta Familia/Ukoo wa Gwajima..!!!

$
0
0

Family bonding - muunganiko wa kifamilia ni jambo jema sana! Family conflicts - migogoro ya kifamilia ni jambo baya sana... Msingi wa umoja katika ukoo huanza kwenye familia

Tuna familia na koo zenye migogoro mingi sana vinyogo visasi wivu dhuluma kijicho na mambo yanayofanana na hayo vimeharibu familia na koo nyingi 

Familia maarufu ya Gwajima ni mojawapo! Unapoona wanandugu wanatoa siri za familia nje hasa kwenye vyombo vya habari kwa sababu yoyote ile jua kuna shida kubwa ndani yake

Sakata la madawa ya kulevya limetuletea yatokanayo kwenye ukoo huu maarufu wa Gwajima .....kwamba kaka yake Gwajima mchungaji aliugua hadi kufariki na mdogo wake huyu akawaaminisha watoto wa marehemu kaka yake kuwa angemfufua babayao (pengine kwa makubaliano fulani) 

Kaka mtu hakufufuka ! Hakuna mtu aliyeyefufuliwa tena baada ya Yesu Kristo kufufua aliowafufua. Watoto na ndugu wakajenga chuki na familia ya Gwajima mchungaji na pengine hakuna waliohangaika kutatua huo mgogoro kwa sababu wanaozijua wenyewe ama pengine walijaribu wakashindwa

Gwajima mchungaji ana kipaji na karama ya kuhubiri lakini anakitumia vibaya. Gwajima ana uthubutu wa ajabu hayumbishwi na changamoto zake. Ni watu wachache mno wenye hiki kipaji.. Kupitia hili amejijengea umaarufu mkubwa na ni bilionea

Haya anayofanya ni laana kwa familia na ukoo wake, Gwajima ni muongo sana lakini haogopi kuongopa ni mjanjamjanja mwenye viashiria vingi vya utapeli kwa kutumia jina la Mungu na dini.... God is watching...! Kutokana na hili haambiliki na amekuwa na kashfa na migogoro mingi 

Kuna huyu Gwajima mwanasheria msomi asiye na tafakuri wala hekima! Kwa kutaka kufurahisha kaliba Fulani ya watu na pengine kwa malipo kidogo anamponda live kwenye media ndugu yake na kuleta ishu za kifamilia upenuni... Zaidi pengine akiongozwa na wivu juu ya mafanikio ya nduguye ambaye pengine hana elimu kama yake

Gwajima mchungaji hajaongea bado kumjibu lakini wawili hawa wanatupa mwanga wanajifunua wakoje huko kwenye ukoo wake 

Kaka mbabe jeuri Mdogo mtu msomi asiye na hekima wala weledi kila mtu ana watu nyuma yake
Wameanza kumalizana live mpaka nje laana hii itadumu vizazi vingi

Dk Shein Amjibu Rais Magufuli Juu ya Zanzibar Kukatiwa Umeme na Tanesco,Adai Hatishiki Hata Kidogo..!!!!

$
0
0

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.

Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.

Dkt. Shein katika mazungumzo yake na vyombo vya habari alilezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema mkutano huo utaleta tija na faida kubwa kwa wazanzibari na watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii,uvuvi,ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.

Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya na ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.

Harmorapa - Nimeanza Kusumbuliwa na Mademu,Yani Sina Hata Raha..!!!

$
0
0

Rapa anayechipukia kwenye muziki wa hip hop, Harmorapa amefunguka na kusema toka amepata jina amekuwa akipata usumbufu sana kutoka kwa watu wake wa kawaida pamoja na mabinti.

Akiongea na EATV Harmorapa ameweka wazi kuwa sasa hivi amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa mabinti mbalimbali.  

Mapya Yaibuka Kifo Bilionea wa Viroba,Alimtumia Meseji ya Kuaga Mke Wake,Mdogo Wake Afunguka Haya...!!!

$
0
0

WAKATI mwili wa bilionea na mfanyabiashara maarufu wa vinywaji Festo Mselia (58), ukitarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Umbwe Unana mkoani Kilimanjaro, mambo mapya yameibuka kuhusiana na kifo chake kinachodaiwa kutokana na kujipiga risasi.

Mambo mapya yaliyoibuka yakihusishwa na chanzo cha kifo hicho ni pamoja na usumbufu alioupata polisi, kutuma ujumbe wa kumuaga mkewe na kumpigia simu mdogo wake mara tisa bila kupokewa muda mfupi kabla ya umauti kumfika.

Akizungumza na Nipashe jana, mdogo wa marehemu huyo, Anthony Mselia alisema mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi, umekutwa na matundu matatu ya risasi kwenye maeneo ya chini ya kidevu.

"Mazingira yanaonyeshwa kwamba 'brother' (kaka) hajauliwa na mtu, yaani sielewi ni kitu gani kilichomsibu," alisema.
"Lakini kulikuwa na taharuki kuhusu suala la pombe kali aina za viroba, lakini hakuna kitu alichowahi kuniambia zaidi ya kulalamikia suala hilo.

"Tangu siku ya kwanza alipokamatwa Machi 3, mwaka huu, alinipigia simu na kuniambia kwamba serikali haioni namna yeyote ya kuongeza muda na hii ilitokana na kwamba alikuwa na mzigo mkubwa wa bidhaa hiyo katika stoo zake zaidi ya tatu tofauti wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni moja na viroba ndio vilivyokuwa na mzunguko mkubwa wa biashara na ndivyo vilikuwa vimekamata fedha."

Akisimulia zaidi, mdogo huyo wa marehemu alisema kaka yake aliwapeleka polisi zaidi ya stoo tatu.

Alisema kuwa kabla kaka yake hajafikia uamuzi huo Machi 7, yeye alifika nyumbani kwake na kumuaga kuwa anasafiri kwenda Moshi.

"Nilimsalimia na kumuaga kwa safari na akaniruhusu kuondoka na hakuonekana kuwa na mawazo wala kitu chochote alikuwa 'happy' (na furaha) tu. Nakumbuka aliniambia kwamba mdogo wangu ukienda uwahi kurudi kutoka Moshi kwa kuwa mimi naishi hapa hapa Dodoma," alisema.

Aliendelea kueleza kuwa anaamini kaka yake hajafikia uamuzi huo kutokana na kuwa na madeni aliyokuwa nayo ambayo alidai alikuwa ameshayalipa kwa kiasi kikubwa.

"Kwa mfanyabiashara mkubwa kama Mselia ambaye ana mzunguko mkubwa wa biashara, lazima kutakuwa na watu wanaoleta mizigo lakini siyo kesi ya yeye kufikia hatua hiyo, mimi mpaka sasa hivi akili na aliponipigia simu na kulalamika kilichompelekea kufanya uamuzi ni suala la viroba."

Alieleza kuwa awali polisi, maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) walifika dukani kwa kaka yake kumhoji na kumkagua na kwamba marehemu alitoa ushirikiano na kuwapeleka kwenye stoo zake na kuwaonyesha mzigo wote ambao alizuiwa kuuuza.

Alisema kuwa maofisa hao baada ya kumaliza kukagua, waliweka stika lakini alikuwa bado analalamika kwanini mzigo wenye thamani kubwa ya fedha ufungiwe ndani, jambo ambalo lilikuwa linampa wakati mgumu.

Alisema mzigo huo licha ya kuzuiwa kuuzwa, bado umo kwenye stoo zake.

SIMU MARA TISA
Mdogo huyo wa marehemu aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuagana na kaka yake, hakuwasiliana naye lakini baada ya kufika Moshi na kutaka kumjulisha kwamba amefika salama, alibaini kuwa kaka yake alikuwa amempigia simu mara tisa bila kumpokea.

"Muda mfupi baadaye nilipigiwa simu na polisi kwa namba zilizoishia 71 akiuliza kwamba 'wewe unamfahamu Mselia?',

nikamwambia ni kaka yangu, akaniambia mimi ni askari, kaka yako amejipiga risasi, nikamuuliza amejipiga au imemfyatukia bahati mbaya?

"Akasema amejipiga mwenyewe, tafuta watu waende ‘General Hospital’ (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa) kwa ajili ya kumpa msaada."
Alibainisha kuwa baada ya taarifa hiyo, alimpigia mke wa marehemu na baadaye wakawapigia marafiki wa karibu wa familia na wakaungana naye, lakini muda mfupi baadaye akapigiwa simu kuwa kaka yake amefariki.

Alidai kuwa marehemu alikuwa anamshirikisha matatizo yote ya kibiashara.

KWAHERI
Mdogo huyo wa marehemu pia alidai kuwa kaka yake alitumia ujumbe mfupi wa maandishi kwa mkewe uliosomeka "kwaheri" muda mfupi kabla ya tukio la risasi, lakini mke wake hakuutilia maanani akidhani alikosea kuutuma kwake badala yake alikuwa anamuaga mtu mwingine.

"Lakini baadaye, baada ya kupata taarifa kuwa amejipiga risasi, aligundua kuwa kumbe alikuwa anamuaga," alisema Mselia.

"Kinachoonekana ni 'harrasment' ya polisi kwa sababu polisi walifika mara ya kwanza, ya pili na ya tatu, Mselia wa watu maskini hapendi kusumbuliwa."

KAULI YA POLISI
Akizungumza kwa simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alidai maganda ya risasi yaliyokutwa pembeni ya mwa mwili wa marehemu yalitumiwa na marehemu wakati akijaribu kujiua.

“Maganda yale ya risasi aliyatumia kujipiga mwenyewe, unajua alipokuwa akijipiga nadhani hakujilenga vizuri na hii ni kutokana na kupaniki, alijipiga kwenye shigo ikatokea mdomoni, hakufa na yeye alitaka afe sasa kutokana na kujipiga kule alijipiga risasi tano," alidai Kamanda Mambosasa.

Mfanyabiashara huyo alijiua juzi shambani kwake Msalato Manispaa ya Dodoma baada ya kuhojiwa na polisi kuhusu shehena ya viroba aliyokuwa nayo yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni moja.

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid Je? Unapata Pesa Haika? Kusafisha Nyota na Kurudisha Mke/Mume Aliekuacha

$
0
0

MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI. (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 72 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI: SHEKH SHARIFU RASHID ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran dawa za asili dawa za kiarabu, na njiwa, Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k, anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa Pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote, pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu, Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo. WASILIANA NAE KWA WhatsApp na SIMU NO: +255 718-668347 na +255 767-204308 +255 685-224047 Email shekhsharifurashidi@gmail.com.

USHAURI: ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa haraka.
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live




Latest Images