Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Aika (Navy Kenzo): Vanessa Mdee ndiye aliyetufanya turudi kwenye muziki baada ya kukata tamaa

$
0
0
Muimbaji wa kundi la Navy Kenzo, Aika, amedai kuwa Vanessa Mdee ndiye aliyewahamasisha kurudi kwenye muziki baada ya kuwa wamekata tamaa.



Akizungumza jana kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV ambapo yeye na Nahreel walikuwa ma-hosts, Aika amemuelezea Vee Money kama mtu mwenye upendo.

“Ni msichana ambaye ana bidii, ametumotivate vitu vingi sana hata sisi kwenye maisha yetu,” amesema Aika. “Tuseme, yeye ndiye alitufanya sisi turudi kwenye muziki baada ya kuja studio na kusikiliza nyimbo zetu na kusema ‘jamani toeni hii nyimbo ya Bokodo’ by then. Alitupa nguvu sana na ni mtu ambaye amekuwa akituencourage tukisaidiana,” ameongeza.

Vee Money pia aliwahi kuzungumzia story hii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Up Close & Personal cha K24 ya Kenya, Vee alisema alikutana na Nahree na Aika baada ya kupigwa chini na label ya B’Hits.

“Kwahiyo nikasema nahitaji kumpata mtu ambaye anaweza kupatia sauti yangu. Shout out kwa Hermy kwasababu sasa sisi ni familia, ni kaka yangu daima. Kwahiyo nilikuwa naijua hii bendi ya Navy Kenzo toka Arusha na wakati huo walikuwa wakijulikana kama Pah One. Pah One ikaja kuvunjika na wawili kati yao walikuwa wanataka kwenda nje kusoma masters, nilienda kwenye studio yao ambayo wakati huo ilikuwa nyumba yao na nikamuambia Nahreel ‘nakuaminia, nadhani mimi na wewe tunaweza kufanya mambo makubwa pamoja,’” alisema Vanesa.

“Muda huu Nahreel alikuwa tayari kufungasha virago na kuondoka ‘nimechoka na mambo haya ya muziki.’ Na nikamuambia, acha tufanye kazi na nikamuambia ‘nichezee nyimbo zako’ pamoja tulielewana sana na imekuwa ni story tangu hapo na ninajivunia sana Navy Kenzo na Nahreel ni genius na ndiye mtayarishaji mkuu wa album yangu.”

Baada ya Kimya Kirefu..Pro Mark Mwandosya Aibuka na Kutoa Yake ya Moyoni...!!!!

$
0
0

BAADA ya kimya kirefu cha tangu mwishoni mwa mwaka 2015, waziri mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, Prof. Mark Mwandosya, amezungumza kutoka kijijini kwake Lufilyo, katika Halmashauri ya Busokelo, mkoani Mbeya.

Katika salamu zake alizozitoa jana, Prof Mwandosya alitaka vyuo vikuu na taasisi za sayansi na teknolojia kurekebisha uwiano ulio hasi katika usaili wa wanafunzi wa kike, katika fani na masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.

Katika salamu hizo, Prof. Mwandosya ambaye alikuwa mmoja wa watia nia 40 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 pia alipendekeza juhudi za kuhamasisha wanawake kupenda masomo ya sayansi zihusishe wahadhiri.

Alisema wahadhiri hao wanapaswa kutembelea shule za sekondari na kufanya mazungumzo na walimu na wanafunzi wa kike.

Prof. Mwandosya alisema mazungumzo hayo yalenge katika kufafanua misingi na nguzo za sayansi na hisabati na kuwashawishi wanafunzi, hasa wa kike, kutoogopa kuchukua michepuo yenye masomo ya sayansi na hisabati.

“Maendeleo ya taifa lolote line yanatokana na matumizi bora ya sayansi na teknolojia. Hivyo basi ajira nyingi pia zinatokana na matumizi ya sayansi na teknolojia katika maendeleo ya binadamu,”alisema.

Aliongeza kuwa kutokuwa na uwiano mzuri wa kijinsia katika usaili katika elimu ya juu hasa katika sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati ni changamoto kubwa katika maendeleo ya elimu nchini.

“Maneno ya hekima ya Mwalimu, Mwanafalsafa, Mwafrika, mwenye asili ya iliyokuwa Gold Coast ambayo sasa ni Ghana, Mwanzilishi wa Chuo cha Achimota, marehemu James Emmanuel Kwegyr Aggrey, ni muhimu tuyazingatie," alisema Prof. Mwandosya.

Prof. Mwandosya alimnukuu Kwegyr Aggrey akisema, “njia ya uhakika ya kuwafanya watu wasiendelee ni kuwaelimisha wanaume tu na kupuuza elimu ya wanawake. Ukimuelimisha mwanaume una muelimisha yeye tu, lakini unapomuelisha mwanamke, una elimisha taifa lote.”

Aidha, Prof. Mwandosya ambaye alistaafu uwaziri akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais 2015, alisema anaaminia wizara yenye dhamana ya elimu itasaidia kurekebisha uwiano usioridhisha wa udahili wa wanafunzi na ajira za wanawake nyanja hizo.

Prof Mwandosya ambaye alishika nafasi ya pili nyuma ya Jakaya Kikwete katika mapendekezo ya mpeperusha bendera ya CCM kwa uchaguzi wa rais wa 2005, alikuwa mmoja wa makada wa kwanza wa chama hicho kuchukua fomu miaka 10 baadaye lakini akachujwa mapema.

Rais John Magufuli na Waziri wa Ujenzi katika utawala wa Jakaya Kikwete ndiye aliyepitishwa na mkutano mkuu wa CCM kabla ya kumshinda Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kupata asilimia 58.46 ya kura zote halali Oktoba 25, 2015.

Kimenukaa..Aliyemuaa Mke wa Mwanajeshi Kusakwa Nchi Nzima...!!!

$
0
0

JESHI la Polisi limeanza uchunguzi mkali kuwatafuta waliohusika kufanikisha mauaji ya kinyama ya Samira Masoud (34), ambaye ni mke wa mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Samira aliuawa nyumbani kwake, eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam, na kisha mwili wa marehemu kukutwa ukiwa kwenye chombo kikubwa cha kuwekea maji cha namna ya beseni.

Akizungumza  jana, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, SACP Susan Kaganda, alisema mwili wa Samira ulikutwa
Jumanne ya wiki hii baada ya taarifa kupatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu, ambaye ni mke wa mwanajeshi wa JWTZ (jina linahifadhiwa).

Akisimulia zaidi, Kamanda Kaganda alisema kuwa Jumanne ya wiki hii, majira ya saa 11:00 jioni, ndugu wa marehemu walifika katika kituo cha polisi kutoa taarifa kuhusu marehemu ambaye ni dada yao.

Alisema ndugu hao waliwaeleza polisi kuwa, kwa muda mrefu walikuwa hawana mawasiliano na dada yao, lakini siku hiyo (Jumanne), walipokea ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi ya Samira.

Kamanda alisema ujumbe huo ulikuwa ukisomeka kuwa, “Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu… itaozea ndani.”

Alisema baada ya kuona ujumbe huo, ndugu hao walikwenda nyumbani kwa marehemu, lakini hawakuingia ndani baada ya kukuta gari lake lipo nje ya uzio. Waliamua kwenda kutoa taarifa polisi.

Aidha, alisema baada ya taarifa hiyo, polisi kwa kushirikiana na ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kibamba, walifika eneo hilo na kuvunja nyumba na ndipo walipokuta mwili wa marehemu kwenye chombo cha maji huku ukiwa umeharibika vibaya.

“Tumejaribu kila mara kuipiga simu ya marehemu ambayo ilitumika kutuma ujumbe kwa ndugu wa marehemu, lakini imezimwa…mume wake ambaye ni mwanajeshi wa JWTZ, ambaye alikuwa kwenye mafunzo ya kijeshi visiwani Zanzibar, alikuja baada ya kupewa taarifa za kifo cha mke wake. Hivi sasa bado hakuna anayeshikiliwa,” alisema Kamanda Kaganda.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwamba, hivi sasa wanasubiri ripoti ya daktari ili kujua kwa kina namna Samira alivyouawa.

Yanga Mzuka Umepanda,Matajiri Wamwaga Pesa kwa Wachezaji..!!!

$
0
0

MZUKA umekolea Yanga. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya matajiri wa Yanga kumwaga fedha na kuweka mambo sawa kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matajiri wa klabu hiyo wamelipa malimbikizo ya madeni yote waliyokuwa wakidai wachezaji wao akiwamo beki wa kati, Vincent Bossou, kwa lengo la kuwaongezea morali ya ushindi dhidi ya wapinzani wao.

Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema wachezaji waliokuwa wanaidai klabu hiyo wamelipwa.

Mkwasa alisema kwa sasa hakuna mchezaji anayedai na kila mmoja amelipwa kutokana na stahiki yake na kazi iliyobaki ni kusaka ushindi dhidi ya Zanaco.

“Hakuna mchezaji yeyote anayeidai Yanga, Bossou alikuwa anatudai mshahara wa Februari mwaka huu na limbikizo la fedha zake za Agosti mwaka jana,” alisema Mkwasa.

Mkwasa alisema limbikizo la fedha hizo si mshahara nazo amelipwa ili waweze kuitumikia klabu yao kwa asilimia 100.

Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, alisema lengo la kuwaweka sawa wachezaji ni kuhakikisha wanaondoa na kuziba mwanya wa wachezaji wao kulalamika au kuwa na mawazo yatakayowafanya wacheze huku wakiwaza mambo ya nje ya uwanja.

Alisema wamelazimika kufanya hivyo kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wao kupata ushindi mkubwa katika mechi ya kwanza ili kuwarahisishia kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

“Kama utawala tumehakikisha tumeweka mambo yote sawa kwa sababu tunatakiwa kushinda mechi hii ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, kama unavyojua tukishindwa kupata ushindi hapa nyumbani kazi itakuwa ngumu ugenini,” alisema Mkwasa.

Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema wamewasoma wapinzani wao kupitia mikanda ya video (CD) kwa mechi walizocheza, lakini hawataingia uwanjani kwa kutegemea mbinu moja, wamejipanga kupambana kutafuta matokeo mazuri.

“Tuna wachezaji na kocha wametokea Zambia ambako Zanaco wanatoka, lakini soka linabadilika, unaweza kuangalia mechi leo lakini kesho ukacheza ukakuta kikosi kimebadilika, hivyo tunajiandaa kama sisi na si kutegemea mtu wala CD,” alisema Mwambusi.

Mwambusi alisema kwa kawaida Yanga ina kikosi kipana ambapo hata michezo ya nyuma wanakuwa na majeruhi lakini matokeo mazuri yanapatikana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Paulo Malume, alisema kurejea kwa Donald Ngoma na Thaban Kamusoko, kumewafanya wachezaji kuwa na morali ya hali ya juu kuelekea mechi hiyo.

“Tumejiandaa vizuri kama ulivyoona timu iko mazoezini, waliokuwa majeruhi wamerudi, ni raha kwa kweli tuna imani kocha kesho atapanga ‘full muziki’ kama hakutatokea mabadiliko yoyote kikosini,” alisema Malume.

Alisema katika kuhakikisha wanawapa morali vijana wao matajiri wa timu hiyo, wamechanga kiasi cha fedha kuwapa endapo wataibuka na ushindi.

“Kama ilivyo kawaida yetu wachezaji wakifanya vizuri tunawapa tuzo, tumekuwa na utaratibu wa kukutana katika vikao vyetu na tuna fedha zipo tayari siwezi kuzitaja ni kiasi gani ili kuwapa wachezaji wakishinda,” alisema.

Zanaco waliwasili jana tayari kwa mechi huku nahodha wa timu hiyo, Ziyo Tembo, akimtaja kiungo wa Yanga Mzambia, Justine Zullu, kuwa wanamjua uwezo wake ndani na nje ya uwanja.

Akizungumza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Tembo alisema kiungo huyo wa Yanga hawezi kuwasumbua huku kocha wao, Munamba Numba, akitamba kuondoka na ushindi.

Kudadeki...Diamond Azidi Kuwakimbiza,Angia Katika Anga za Kina Jay Z Rasmi,Aja na Tovuti Yake Maalumu ya Kuuza Muziki..!!!

$
0
0

Tovuti namba moja ya kuuzia muziki nchini, Mkito.com, imepata mpinzani mpya, Wasafi.com. Diamond Platnumz ameizindua rasmi website yake ya kuuzia muziki, si tu wa wasanii wa WCB, bali wasanii wengine pia.

Wiki hii, hitmaker huyo wa Marry You, amekuwa akifanya mikutano ofisini kwake na wasanii mbalimbali, kuzungumza namna ya kufanya nao kazi kwenye mradi huo. Tayari amekutana na wasanii kama Ben Pol, Barnaba, Cassim pamoja na Chege na Temba.

Kwa mwelekeo huo, Wasafi.com inakuja kuwa mpinzani mkubwa wa Mkito.com, ambayo hadi sasa ndio website inayotegemewa na wasanii wengi kuuzia nyimbo zao.

Msanii wa WCB, Harmonize anaachia wimbo wake mpya exclusively kupitia website hiyo inayokuja na app yake pia.

Video..Tazama Rais Magufuli Akiimba Wimbo wa Darasa Katika Moja ya Hutuba Yake Huko Mtwara

Kwa Mara ya Kwanza Leo..Wema Sepetu Atapanda Jukwaa la Chadema Kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mhe Godbless Lema Arusha...!!!!

$
0
0

Malkia wa filamu Wema Sepetu atahudhuria mkutano wa hadhara Ijumaa hii wa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema utaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro Arusha jioni ya leo.

Mbunge huyo itakuwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza na wananchi wake ikiwa ni siku chache toka aachiwe na mahakama kwa dhamana baada ya kukaa rumande miezi 4.

Muigizaji huyo tayari yupo Arusha, jana ametoa taarifa kwamba ameshafika katika mji huo kwajili ya mkutano huo ambao unatarajiwa kuwa na watu wengi.

“Glory Be to God…!!! I had a safe Travel…! Back in Arusha ready for tomorrow’s Meeting with Hon. Godbless Lema… Y’all better be there… Im sure he’s got alot to share with Us… Goodmorning World…. Kajua kanapiga,” aliandika Wema Instagram.

Wema pamoja na mama yake walihamia CHADEMA mwezi mmoja uliopita baada ya kudai kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya viongozi wa chama cha CCM.

Mbunge wa Mtera: Wasiporidhika na Vyeti Watasema Sijatahiriwa Nitatoa Nini...!!?

$
0
0

Haya sasa, naona kasi ya vyeti sasa imetua Bungeni,kwa waheshimiwa ambao nao inasemekana hawajakwenda shule.

Zamu hii sakata limetua kwa Mbunge wa Mtera, Mh Livingstone Joseph Lusinde,yeye alisema hivi:-

"Wanaosema sijasoma, nikitoa vyeti wakawa hawajaridhika wakasema pia sijatahiriwa,je nitoe nini?

Haya sasa.

Mheshimiwa Lusinde wakati Wa kampeni za kugombea uraisi Mwaka 2010 walijitokeza wagombea wenza wakatumia hoja ya kuwa Kibajaji hajasoma, wakashawishi wapiga kura wamtake atoe vyeti vyake. Lakini kibajaji Hakuyumbishwa na hizo propaganda akaendelea kupiga kampeni zinazohusu jimbo lake na hatimae wananchi wakamuelewa wakamchagua kwenye kura za maoni na kumpiga chini Mwanasiasa mkongwe Mzee Malecela na baadae wananchi wakachukua wakaweka waaaa!

Siku Moja katika mkutano Wa kampeni baada ya kumaliza kunadi Sera akauliza swali hivi hawa wanaosema sijasoma na wanataka vyeti, Je nikitoa vyeti alafu wasiporidhika wakasema Sijatahiriwa je nitoe nini?

Hatariii..Mzee Warioba Alipukia Serikali ya Magufuli Kuhusu Baa la Njaa..!!!

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Warioba amewataka watanzania wote kuungana na kujiaandaa kukabiliana na baa la njaa ambalo huenda likatokea, huku akikiri kuwa tatizo la upungufu wa chakula kwa mwaka huu, ni kubwa kuliko kawaida.

Akizungumza leo wakati akizindua kongamano la 'Wanawake na Uongozi' katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, Jaji Warioba amesema hakuna haja ya watanzania kubishana na kulumbana kama kuna njaa au upungufu wa chakula, bali kujiandaa ikiwa ni pamoja na kujifunza kujifunza katika nchi ambazo tatizo hilo limetokea ikiwemo Kenya na Somalia.

"'Haijalishi kama njaa ipo au kuna upungufu wa chakula kinachotakiwa ni kuungana  na kujiandaa kwa pamoja ili kujua ni jinsi gani tutaweza kukabiliana na baa la njaa endapo litatokea kama jinsi inavyosemwa, tujifunze kupitia Kenya na Somalia. Siyo sawa kurushiana maneno huyu anasema hivi huyu anamjibu vile, tuungane kwa pamoja" Amesema Warioba ambaye pia alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba a kuongeza “Serikali ijiandae kukabiliana na njaa kwa sababu ingawa tumezoea kwamba kila mwaka zipo sehemu zenye upungufu wa chakula, mwaka huu tatizo ni kubwa”

Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya, Warioba ametaka elimu itolewe kwa watu wanaojishughulisha na dawa za kulevya hususani wanaolima bangi lakini pia wasaidiwe wapate njia mbadala za kuweza kujikimu ili kuachana na shughuli hizo ambazo zinaathiri asilimia kubwa ya vijana.

Ameongeza kuwa tatizo la dawa za kulevya linaripotiwa kawaida kama siyo tatizo kwa sababu limefanywa kama jambo la siasa.

"Tatizo la dawa za kulevya linazungumzwa kama jambo la kawaida, badala yake tumetafuta mchepuo wa kisiasa, ambao ndiyo unazungumzwa, Karibu kila siku utaona taarifa kwamba wameenda askari wameharibu dawa za kulevya katika mashamba ya bangi, inaripotiwa tu kama tukio halafu basi. 

'Tuseme hapana matumizi ya madawa, madawa ni mengi sana yanayoingia , tunajua madhara yake, tuyazuie yanayoingia kutoka nje pamoja na yanayolimwa, tujitahidi kuwasaidia vijana walioathirika. Tunahitaji kujenga nguvu za pamoja" Amemalizia jaji Warioba.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba, ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, na limetumika pia kuzindua kitabu chenye jina 'Nguvu zetu, Sauti zetu, Ajenda katika mchakato wa katiba mpya' kilichoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es salaam, 

Mambo 6 Yanayomponza Paul Makonda...!!!

$
0
0

Bado Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (36) anaendelea kutajwa kwenye vinywa vya Watanzania wengi kufuatia madai ya kutumia vyeti ambavyo vinasemekana si vya kwake, lakini Amani sasa limebaini mambo 6 yanayomponza bosi huyo.

Kwa takriban wiki ya tatu sasa, jina la Makonda limekuwa likiandikwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa ishu hiyo ya vyeti ambapo, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Joseph Gwajima ndiye aliyeibua madai hayo mazito kiasi cha kuifanya jamii kuyavalia njuga madai hayo.

ILIKUWA KWENYE IBADA YA JUMAPILI

Gwajima aliibua sintofahamu ya vyeti hivyo, Jumapili ya Februari 26, mwaka huu, kwenye mahubiri ya ibada ya kanisani kwake, Ubungo ambapo alisema kuwa, Makonda anatumia cheti cha kidato cha nne cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge wakati yeye alianza darasa la kwanza mwaka 1988, akitumia jina la Daudi Albert Bashite.

Akihubiri huku waumini wake wakimsikiliza kwa umakini mkubwa, Mchungaji Gwajima alisema kuwa, mwaka 2001, Makonda alitumia cheti cha mwanafunzi huyo chenye divisheni 3 ya ponti 25 ili aweze kujiunga na Chuo cha Uvuvi Nyegezi (NFTI) na ndiyo akaendelea hivyohivyo mpaka kufi ka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na baadaye kuingia kwenye siasa na leo hii ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

MAKONDA HAPENDWI?

Tangu kuingia kwenye siasa, Makonda amekuwa akikumbwa na ‘bahati mbaya’ ya kuwa na damu ya kunguni kiasi kwamba, kwa tafsiri ya kawaida ni rahisi kusema kuwa, baadhi ya watu hawampendi lakini ni kutokana na utendandaji wake uliotukuka.

AMANI LABAINI MAMBO 6 YANAYOMPONZA

Amani liliweza kuzungumza na baadhi ya watu kuhusu utendaji kazi wa Makonda ambapo wengi walitoa maoni yao kwamba, yapo mambo yaliyosababisha mheshimiwa huyo kuingia kwenye kuonekana na watu ‘ana damu ya kunguni’ na ndiyo yanayomponza.

JAMBO LA KWANZA, WAKATI WA BUNGE LA KATIBA

Mwaka 2014, chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ Tanzania iliingia kwenye mchakato wa Katiba Inayopendekezwa ambayo Jaji Joseph Warioba alikuwa mwenyekiti wa kutafuta maoni mitaani. Baada ya maoni kukamilika, kulikuwa na mijadala mbalimbali ikiendelea, ikiwemo kuundwa kwa Bunge la Katiba ambapo, Makonda alikuwa mmoja wa wajumbe walioteuliwa na JK. Katika mjadala mmoja uliofanyika kwenye Jengo la Ubungo Plaza jijini hapa na Jaji Warioba akiwa mshiriki mkuu, kulitokea vurugu kubwa kiasi kwamba, mzee Warioba alidaiwa kupigwa.

Mengi yalisemwa, baadhi ya watu walidiriki kutamka kwamba, miongoni mwa watu waliompiga mzee Warioba ni Makonda. Ilibidi Makonda atumie nguvu kubwa kukanusha kwamba, yeye siye aliyempiga mzee Warioba bali aliingilia kati kuamua na kumuweka sawa mzee huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu mwaka 1990.

Hata hivyo, licha ya utetezi wake, Warioba mwenyewe alitoa tamko kwamba hakupigwa na Makonda, lakini watu walishindwa kumwelewa mzee huyo na kuendelea na madai kwamba ni Makonda tu. Kuanzia hapo, jamii ilianza kumuona Makonda kama si mjamii kwa tukio la kusema alimpiga mzee Warioba na kukatokea mgawanyiko wa watu, waliomshabikia na waliokataa kumshabikia ambao idadi yao kama iliuelemea mzani.

MKUU WA WILAYA

Nyota ya Makonda licha ya madai ya kumpa kichapo mzee Warioba, ilizidi kung’ara, kufumba na kufumbua JK akampa ukuu  wa wilaya ya Kinondoni ambapo kwa hakika, alijitokeza mstari wa mbele kutatua migogoro ya ardhi na kuonekana kwenye vyombo vya habari kila kukicha kwamba, anatetea wanyonge. Wapo waliomkubali kwa kazi hiyo, wengine waliendelea kuwa na msimamo uleule kwamba hawamkubali.

JAMBO LA PILI, NAULI ZA WALIMU DAR

Bado akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda aliwahi kutoa ofa ya walimu wa Jiji la Dar kupanda bure daladala. Lakini siku ya kwanza ya zoezi hilo hakuna mwalimu aliyekubali kulipiwa nauli wakidai kuwa, wanaweza kujilipia wenyewe. Nyuma ya zeozi hilo ilisemekana kuwa, walimu waliwahi kukerwa na matamshi ya Makonda siku za nyuma kuhusu walimu na madaraja yao ya kazi.

Kwa hiyo walimu nao wakamuona Makonda ni ‘adui’ yao. Mwaka 2015, mwaka mmoja tu baada ya Bunge la Katiba, akaingia madarakani Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ huku Makonda akiendelea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, lakini kabla ya kupepesa macho, JPM akamteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ‘RC’. Hapo ndipo yakaongezeka mambo juu ya mambo.

JAMBO LA TATU, APIGA VITA SHISHA, MASHOGA NA MACHANGU

Makonda aliingia kwenye kiti cha u-RC akiwa na munkari wa kufanya kazi, alihakikisha jiji linakuwa safi  kwa wakazi wake kufuata maadili na kuachana na maisha ya mkato. Kwa hiyo alipiga vita matumizi ya kilevi aina ya shisha, akatangaza vita na wanaume tata ‘mashoga’ lakini pia akawaambia wanawake wanaojiuza ‘machangudoa’ kwamba, waachane na biashara hiyo mara moja.

Makundi ya watu yakaibuka na kudai; ‘Makonda anajifanya ni mchapakazi sana ili rais ampende’. Kwa hiyo akaongeza sababu nyingine ya kuwa na ‘maadui’ kwani wavuta shisha walikasirishwa kwa kuondolewa kwa starehe yao hiyo achilia mbali mashoga na machangu ambao walimuona anawakomalia hivyo kuwahatarishia njia zao haramu za kupata kipato.

JAMBO LA NNE, ZOEZI LA DAR ES SALAAM MPYA

Siyo siri wala hakuna sababu ya kupepesa macho, miongoni mwa mambo ambayo, yalimwongezea ‘maadui’ Makonda ni oparesheni ya Dar Mpya ambayo aliifanya kwa nia  njema ya kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi wa mkoa wake huo wenye watu karibu milioni 6. Zoezi hilo lilifanyika kwa siku karibia saba ambapo Makonda na wasaidizi wake walikuwa wakifanya mikutano ya hadhara kila siku katika maeneo mbalimbali na kusikiliza kero.

Katika kusikiliza kero hizo  baadhi ya watu, hasa viongozi wa serikali za mitaa na wengine, walijikuta wakikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya kutuhumiwa hadharani.

Mbaya zaidi ili watuhumiwa hao wakamatwe, Makonda alikuwa akiamuru kwa sauti na kuwanyooshea vidole mkutanoni huku kituo kimoja cha runinga jijini Dar kikirusha mubashara matukio hayo hivyo wengi kudai ni udhalilishaji.

Baada ya mikutano ya Dar es Salaam Mpya kumalizika, baadhi ya watu walikuwa mahabusu, wengine mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofi si au pesa, lakini huku Makonda mwenyewe akiwa ameongeza idadi ya ‘maadui’.

JAMBO LA TANO, MATAMSHI YAKE

Katika mikutano hiyo, watu wengi walikuwa wakilalamikia kitendo cha Makonda kuwasemea maneno makali viongozi waliokuwa wanatuhumiwa kwamba, hakuwa anajali umri wao na hivyo kusema lolote lile.

“Kwenye ile mikutano ya Dar Mpya hakuna jambo lilikuwa likiniumiza kama matamshi yake Makonda. Unajua wengine walikuwa sawa na wazazi wake, lakini yeye akawa hachagui maneno ya kusema. Unajua ulimi siku zote bwana ndiyo wenye kuleta tatizo.

“Ni vyema kiongozi akawa anaingiza maneno yake kwenye kipimo kwanza kabla ya kutoa sauti. Kipimo cha kazi yake ni kuchuja, kwamba hili niliseme, hili hapana,” alisema Hussein Mohamed, mkazi wa  Buguruni na kuongeza:

“Unajua inawezekana kabisa, kule kupendwa sana na rais ndiyo kumempa ‘kichwa’ cha kutoa kauli kali za namna ile.”

JAMBO LA SITA, MADAWA YA KULEVYA Licha ya kuacha ‘majeruhi’ kibao  kwenye zoezi la Dar Mpya, bado Makonda kama kawaida yake, hakuacha kujipa ujasiri na kufanya kazi ya kutumikia wananchi na kupinga mambo yaliyo kinyume na uadilifu, hivyo Februari 2, mwaka huu, Makonda kwa mara ya kwanza na akiwa mkuu wa mkoa wa kwanza nchini, alijitokeza hadharani na kutaja majina kadhaa ya watu aliodai wanajihusisha na madawa ya kulevya.

Katika majina hayo, yalikuwepo ya watu maarufu, akiwemo Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na askari polisi 12. Makonda aliwataka watu hao kufi ka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar kwa mahojiano ambapo walitii.

Baada ya sakata hilo, Februari 8, mwaka huu, Makonda akaibuka na listi kama siyo orodha ya watu wengine 65 akiwataja majina na kuwataka wafi ke kwenye kituo hichohicho cha polisi kwa ajili ya mahojiano. Miongoni mwa watu hao, walikuwemo wenye majina makubwa nchini kama vile, mfanyabiashara Yusuf Manji, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni (Chama Cha Mapinduzi), Idd Azzan na Gwajima ambaye ndiye aliyeibua hoja ya vyeti.

‘MAADUI’ WAONGEZEKA’ Kitendo cha Makonda kutaja majina ya wadaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya hadharani kiliibua hoja nyingine, wengi walijitokeza wakipinga kwamba, hakuwa sahihi kwa sababu watu hao ni watuhumiwa tu.

Hoja hiyo ilipaa juu zaidi hadi kufi kia kushika mjadala mkubwa nchini kwamba ni sahihi au siyo sahihi? Miongoni mwa watu waliokereka na kutajwa ni Gwajima.

Yeye alisema kuwa, Makonda alimtendea sivyo hivyo akatangaza vita naye. Katika vita hiyo, ndipo Gwajima naye akadai amechimba na kuchimbua na kubaini kuwa, Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine kuingia chuo baada ya yeye kufeli hivyo akamtaka Rais Magufuli  kumwajibisha.

NIA YAKE NI NJEMA

Katika mtazamo wa kawaida, katika yote aliyoyafanya au kuyasimamia Makonda yana njia njema kwa jamii. Nani asiyejua madawa ya kulevya yanavyoathiri jamii? Nani asiyejua shisha inavyoharibu vijana? Nani asiyejua ukahaba unavyoweza kuleta magonjwa? Lakini pengine uwasilishaji wake ndiyo umekuwa ukisumbua wengi.

NDIYO YAMEMPONZA

Makonda leo hii kama asingetaja hadharani majina ya watu wa unga, kama asingejitolea kuwapiga vita machangu na mashoga, kama asingewakera walimu kwa nauli, kama asingefanya mikutano ya Dar Mpya ina maana angekuwa ni mkuu wa mkoa aliyepoa na kuonekana mwema machoni kwa watu. Kumbukumbu ziko hivyo, wale wanaojitoa mhanga kusimama mbele za watu na kupambana kwa dhati kukosoa matatizo hukumbwa na vita kubwa kutoka kwa watu wenye

Mfanyabiashara Akurupushwa Porini Akichinja Mizoga ya Punda

$
0
0

Kweli ni hatari kubwa! Wabongo wanakula vingi ambavyo hawavijui vilikotoka hali inayohatarisha afya zao! Hilo limedhihirika Machi 6, mwaka huu kuuatia mfanyabiashara mmoja ambaye hakujulikana jina mara moja, mkoani hapa kukurupushwa porini baada ya kukutwa akiwa anachuna mizoga ya mnyama punda ambaye haikujuli  kaka aliwaua kwa mtindo gani.     

Tukio hilo la kushangaza, lilijiri kwenye pori la Kijiji cha Kidomole  wilayani Bagamoyo mkoani hapa ambapo, Amani lilibahatika kukuta mizoga hiyo baada ya mtuhumiwa kukimbia.

Kwa mujibu wa wafugaji wa eneo hilo ambao ni Wamasai, siku ya tukio, walipata taarifa kutoka kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Maria kwamba punda wake wawili wamepotea ndipo walipoanza msako wa kuwasaka wanyama hao.

“Sasa tukiwa tunaendelea kuwasaka, mara tukafika kwenye pori hilo na kumkuta bwana mmoja anawachuna wale punda. Khaa! Tukashangaa sana. Lakini kabla hatujamkamata alikimbia. “Kusema ukweli licha ya kwamba alikimbia lakini kwa sura tunamjua vizuri sana. Ni mfanyabiashara wa nyama Bagamoyo. Ni muuza nyama ya ng’ombe.

Sasa kuna uwezekano kumbe zinakuwaga si nyama za ngo’mbe bali ni punda kwani huku wanyama  hao wanapotea mara kwa mara,” alisema mfugaji mmoja bila kutaja jina lake. Mfugaji huyo aliongeza kuwa, mtuhumiwa amekuwa akipeleka nyama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuziuza. Sehemu hizo ni pamoja na Chalinze, Bagamoyo yenyewe na jijini Dar es Salaam.

Mfugaji huyo aliendelea kudai kuwa, kwa sababu wanamfahamu mtuhumiwa huyo hivyo wanajipanga kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Bagamoyo ili akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Akizungumza na Amani, Maria ambaye ndiye mmiliki wa punda hao alisema:

“Kwa kweli nimeumia sana kwani punda walikuwa wakinisaidia kubeba mizigo, kwenda kuchota maji, sasa wamewaua mimi nitafanya nini?” Baadhi ya watu walioshuhudia  tukio hilo walisema kuwa, baadhi ya watu wanakula nyama ya punda, wengine hawali.

Wakasema kuwa wana hofu mtuhumiwa huyo huichukua nyama hiyo na kutangaza kwamba ni ya ng’ombe na kuwalisha watu mishikaki yake.

“Mbaya zaidi, nyama yenyewe hakuna cha kupimwa wala kuangaliwa kama mnyama alikuwa mzima kiafya au la! Hii ni hatari sana.

Huyu mtu akamatwe mara moja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Huwezi kuwalisha binadamu wenzako nyama ambayo wao hawaitumii. Kama kwake ni halali, kwa wengine ni haramu,” alisema Mathayo, mkazi wa Bagamoyo.

Waziri Nape Unastahili Kuwa Waziri Mkuu wa…!!!

$
0
0

NIMESHASEMA mara kadhaa katika makala zangu za nyuma lakini halitakuwa jambo baya kama nikiligusia leo kidogo kwa msomaji mpya wa makala zangu, kuwa mimi siyo mpenzi wa siasa na sifi kirii kufanya siasa katika maisha yangu, japokuwa natambua siasa ndiyo inayoendesha dunia.

Robo tatu ya maisha yako unayoishi wewe unayesoma hapa yamesababishwa na siasa, amani au machafuko ya nchi au jamii nyingi kwa asilimia kubwa yanasababishwa na siasa.

Hiyo inamaanisha hata kama huipendi siasa lazima ‘uiishi’. Nimeanza na utangulizi huo kwa kuwa nitakachokizungumza hapa kinaweza kutafsiriwa kisiasa lakini uhalisia ni kuwa nazungumza ukweli ambao nimekuwa nikiuona kwa muda sasa:

Tangu wajina wangu, Rais John Joseph Magufuli alipoingia madarakani na kutangaza baraza lake la mawaziri niliona wazi mlengo wake ni kupenda wasomi au watu waliofi ka levo fl ani ya juu kielimu.

Katika chaguzi zake za mawaziri, Rais Magufuli alifanya chaguo sahihi katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa kigezo cha usomi kwa waziri husika hakikuwa kipaumbele kikubwa kama zilivyo idara nyingine, huo ulikuwa uamuzi sahihi kwa kuwa wizara hiyo ni ukweli kuwa inahitaji kuongozwa na mtu ambaye anaweza kuzungumza lugha na wahusika wake wakaelewa na siyo lazima awe msomi.

Siyo kwamba wasomi hawatakiwi lakini utendaji wa waziri wa wizara hiyo, Nape Moses Nnauye ambao amekuwa akiufanya umenivutia na ninaamini kuna mamilioni ya watu ambao wanamuelewa anachokifanya. Achana na madongo yake ya kisiasa ya hapa na pale ambayo ni kawaida kwa mwanasiasa lakini haya machache niliyoyaeleza chini yanaweza kukufanya uamini kuwa Waziri Nape anastahili kupata cheo cha kuwa waziri mkuu wa wizara yake kama cheo hicho kingekuwepo.

Nasema hivyo kwa kuwa tukumbuke majukumu ya cheo chake yalipatikana baada ya Rais Magufuli kuunganisha wizara kadhaa alipoingia madarakani, hivyo mzigo alionao ni mkubwa lakini ameonyesha kuumudu:

ANAISHI MAISHA YA WASANII

Amedhuria mara nyingi matukio ya wasanii, pamoja na hivyo ametoa ushauri mzuri, amekuwa akiwapa moyo wa kupambana, anawaonyesha njia ya kupita na kupata mafanikio.

Amewavumilia mara kadhaa walioonyesha utovu wa nidhamu kwa kuwa wasanii ni wasumbufu, mfano hai ni siku alipotakiwa kumkabidhi bendera Diamond, msanii huyo alichelewa sehemu ya tukio, Waziri Nape alifi ka mapema na kumsubiri kitu ambacho ni dharau kwa kiongozi mkubwa kama yeye lakini alivumilia.

Amefanya ziara mitaani kusaidia masoko ya kazi za wasanii lakini ni wasanii wachache wameonyesha kumuunga mkono.

ANAJUA KUISHI NA VIJANA

Mara kadhaa amejichanganya na vijana mtaani akionyesha sapoti ya mambo kadhaa ya kimichezo na kiburudani na wakati mwingine jukwaani, kitu ambacho ni nadra kufanywa na mawaziri wengine ‘wasomi’.

ANASAPOTI MICHEZO

Najua Rais Magufuli siyo mpenzi sana wa michezo lakini ukweli ni kuwa Nape amekuwa ‘link’ muhimu kati ya serikali na michezo. Amesaidia kutoa hamasa katika timu za taifa hasa soka la vijana ambalo ndiyo msingi wa mafanikio.

Kwenye riadha na michezo mingine napo yupo hata kama siyo mjuzi lakini mara kadhaa nimeona akishiriki na kutoa ushauri wa kile anachoona kipo sahihi. Matukio ya kutembelea Uwanja wa Nyamagana na Taifa katika sakata la viti ni mfano wa jinsi alivyo ‘active’.

ANATHAMINI WANAHABARI

Hivi karibuni kulitolewa tamko la kufungwa kwa TV za mtandaoni lakini Nape akapinga hilo kwa kusema huwezi kufungia wakati hakuna sheria, huo ni mfumo hai na aina ya kiongozi anayetambua kile anachokiongoza  pamoja na hofu kubwa iliyopo kwa wanahabari katika serikali iliyopo madarakani, Nape amekuwa mstari wa mbele kusimamia haki za wanahabari na kuwatetea anapoona wana haki na mara kadhaa ameshiriki katika misiba ya wanahabari.

Anapoona kuna wanahabari wanafanya jambo zuri imekuwa kawaida yake kuwapongeza na siyo kusubiri wakosee tu ndiyo azungumze nao. Pia amewatetea wasanii hadharani alipoona wanatendewa ndivyo sivyo.

ANGALIZO KWA NAPE

Pamoja na mazuri yote hayo lakini moja ya udhaifu ambao nauona kwake ni kuwa mara kadhaa amekuwa akitoa ushauri wa mambo kadhaa, namsii sehemu nyingine asitoe ushauri bali atoe maagizo kwa ufupi aongeza kaukali kiduchu na asiruhusu urafi ki ukamuharibia kazi nzuri anayoionyesha.

Jaji Atoa Mpya Amuuliza Aliyebakwa ''Kwa nini Hakufunga Miguu''Canada

$
0
0


Jaji wa mahakama ya juu nchini Canada amemuuliza mwathiriwa wa ubakaji kwa nini hakufunga miguu

Jaji mmoja kutoka Canada aliyemuuliza mwanamke katika kesi ya ubakaji ''kwa nini hakuweka mapaja yake pamoja'' wakati wa tukio hilo amejiuzulu.J

Robin Camp alijiuzulu baada ya kamati ya nidhamu kupendekeza kuwa afutwe kazi.

Bwana Camp alisema kuwa alisikitishwa na matamshi yake lakini jopo la nidhamu lilisema liliona matamshi yake yalikosa hali ya kutopendelea na heshima.

Waziri wa haki katika jimbo hilo amekubalia kujiuzulu kwake.

Matamshi ya bwana Camp yaliotolewa wakati wa keshi ya ubakaji mwaka 2014 yalizua hisia kali na kusababisha ukosoaji mkali kutoka kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono pamoja na mawakili wao.Jaji huyo alichukua msimamo na kuliambia baraza hilo kwamba alifahamishwa kuhusu makosa yake na kwamba aliomba msamaha juu ya matamshi yake.

Baraza hilo ambalo husimamia idara ya haki lilibaini kwamba vitendo vya bwana Camp wakati wa keshi hiyo vilikuwa na uharibifu wa wazi kuhusu sera ya kutoa haki katika idara hiyo na kwamba hawezi kuendesha tena afisi hiyo.

Pia ilibainika kwamba jaji huyo alizungumza na mlalamishi kwa lugha isioheshimika inayofedhehesha na kuonyesha ubabe.

Kamanda Siro Aongea Kuhusu Kukamatwa kwa Vanessa Mdee na Rummy

$
0
0


Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema jeshi hilo bado linawashikilia Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Vanessa Mdee ambaye alikamatwa juzi (Jumatano) na Rummy Shaeli kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.


Akiongea na wana habari Ijumaa hii ofisini kwake kamanda amesema jeshi hilo bado linawashikilia watu hao mpaka uchunguzi utakapo kamilika.

“Juzi tulimkamata Vanesa Mdee napia tunamshikilia Rummy Shaeli taarifa zinaonyesha ni watumiaji na wasambazaji lakini upelelezi unaendelea na ukikamilika tutawafikisha mahakamani au tutamuachia. Na sio hao tu wapo wengine ambao tuna majina baadhi tumewakamata inasemekana huwa wanasafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini,” amesema Siro.


Msanii wa bongo fleva Rummy

Vanessa alikuwa miongoni mwa watuhumiwa wa matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa na Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika orodha yake ya pili na kuwataka kuripoti katika kituo cha kituo kikuu cha polisi. Hata hivyo Vanessa hawakuweza kufika kituoni hapo kwa wakati kwa sababu wakati agizo hilo likitolewa alikuwa nje ya nchi na kumtuma mwanasheria wake kumwakilisha.

Maneno ya Wema Kabla ya Lema Kuhutubia Arusha Leo

$
0
0

MSANII wa filamu na malkia wa mtandao nchini Wema Sepetu ‘Madam’,  amejikita zaidi katika siasa baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni.


Wema ameendelea kuzianika mitandaoni  baadhi ya harakati zake za kisiasa ikiwa ni pamoja na kujihusisha na shughuli za kijamii kama vile upandaji wa miti,  uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na leo kabla ya Lema kuhutubia, ameweka picha na ujumbe mtandaoni unaowahamasisha watu kufika katika mkutano huo.


“All Ready Kwa Ajili ya Mkutano wa Mhe. GodBless Lema… See you there…. Giving MY Chadema A New Look… Y’all Know Black And Khaki Be our Colour…. A lil White to add Flavor wont Hurt Nobody…. #CallMeKamanda cc @upendosimwita1 @_elm_ @blowassa”, alimaliza Wema.

Diamond Akubali Kuwa na Mtoto Kabla ya Tiffah

$
0
0


U-heard ya leo March 10, 2017 inamuhusu Mwimbaji Diamond Platinumz kudaiwa kuwa na mtoto kabla ya Tiffah na Prince Nillan ambapo mtangazaji Soudy Brown kabla ya kuzungumza na kaka wa dada anayedaiwa kuzaa na Diamond aliicheza sauti anayosikika Diamond akikiri kuwa alikuwa na mwanamke Mwanza ambaye aliwahi kusema ana ujauzito wake na mpaka alikuwa akimhudumia  


Kwenye sauti hiyo Diamond amesikika akisema ….>>“Niliwahi kwenda mwanza zamani nilikuwa katika show ya matamasha makubwa nikakutana na mtoto kawaka alikuwa anatokea kwenye chumba cha Brother Dully, akaja kwangu Mimi nikafanya yangu” :-Diamond


“Nilivyorudi huku demu akanambia  ana mimba nikaanza kuhudumia, nikaenda mwanza kumtafuta japo kwao walini-Mind wakaona kama nazingua, nikambana kujua ukweli kama ana mtoto, maana alinidanganya kuwa katoa Mimba,


Nilipomchunguza nikajua kweli amezaa nikamuomba nimuone mwanangu hata kwenye picha ndipo asubuhi akaondoka pale hotelini tulipokuwa ili akaniletee picha nimuone,  alivyoondoka muda wa ndege yangu kuondoka ulikuwa umefika akawa amechelewa kurudi, nilivyompigia simu akakataa kunitumia picha kwa simu” :-Diamond

Soudy brown alipo mtafuta mama wa mtoto pamoja ndugu wa karibu hakufanikiwa zaidi ya kaka wa Dada anayesemekana kazaa na Diamond…..>>“Ni kweli Diamond kazaa na dada yangu, ni mtoto wa mama yangu mdogo, anaitwa Anita anafanya kazi ya Salon na mtoto huyo anafanana na Diamond kila kitu na mtoto ana miaka mitano au sita na mtoto anaitwa Queen yaani ukimuangalia mdomo ule ule japo mama yake kaolewa”

Chuo Cha Oxford cha Uingereza Kinachoongoza Duniani kwa Kuwa na Maswali Magumu Wakati wa Usahili wa Wanafunzi Wapya..

$
0
0


CHUO Kikuu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza ni chuo chenye sifa na heshima katika utoaji wa elimu ya taaluma mbalimbali duniani.

Chuo cha Oxford ambacho kilianzishwa miaka ya 1096 hadi sasa kinaendelea kuwa chuo bora ulimwenguni.

Chuo hicho hutumia mfumo wa usahili katika kuchagua wanafunzi ambao wanataka kujiunga chuoni hapo.

Inafahamika duniani kote kuwa wanafunzi wanaojiunga katika ngazi mbalimbali Oxford huwa na sifa au vipaji maalumu.

Walimu wanaofundisha chuoni hapo huwapima mwanafunzi kwa uwezo wake wa kufikiri, maarifa na kuweza kutatatua changamoto kwa njia mbalimbali.     

Kila mwanafunzi anayedahiliwa Oxford lazima ajielewe vizuri kwa sababu hawahitaji mtu ambaye ana uwezo wa kukariri.

Mwanafunzi kabla haujadahiliwa kwenye chuo hicho hufanyiwa usahili kupima uwezo wake wa kufikiri.

Usahili huo si tu wa kukariri kichwani kitu ambacho unakijua, lakini usahili huo unatungwa kwa lengo la kumpa mwanafunzi nafasi ya kuonyesha uwezo na nguvu ambayo inahamasisha kutumia maarifa katika kutatua matatizo mapya.

Pia maarifa hayo yanamwezesha mwanafunzi kuwa mbunifu katika nyanja mbalimbali kwa namna mbili ambayo inamletea changamoto au kumruhusu kuwa bora.

Mkurungezi wa wanafunzi wa Shahada wa Oxford, Samina Khan anasema wakati wa kujibu maswali hayo si kitu ambacho unajua kipo sahihi, lakini kukabiliana na mawazo mapya.

Hata hivyo, maswali ya usahili huo huwa changamoto kwa wanafunzi wengi kwa sababu yanahitaji maelezo binafsi, mara nyingi watu huyaona maswali hayo ni ya kijinga lakini yanakuwa na tija ndani yake.

Asilimia kubwa ya wanafunzi hushangaa namna ya maswali huulizwa au kuletwa katika mtihani.

Wanafunzi wanajikuta wakifeli katika usahili wa kujiunga na masomo ya juu ya Oxford.  

Mwanafunzi mmoja aliwahi kusema kuwa walimu wa oxford wao wanatafuta mtu ambaye ana akili za kawaida (natural intelligent) na mwanafunzi ambaye mwalimu atakuwa na furaha kumfundisha.

Haya ni baadhi ya maswali ambayo huulizwa katika usahili wa kudahiliwa chuo cha Oxford.



1.       Kinachotofautisha hadithi fupi na riwaya ni nini?

Fikiria hatukuwa na rekodi ya kumbukumbu ya historia ya kipindi cha nyuma, isipokuwa kuna rekodi za kukumbuku ya kila kitu kinachohusiana na michezo. Ni kiasi gani cha kumbukumbu tunaweza kupata kuhusiana na michezo?

Kwanini binadamu huwa ana macho mawili?

Je, ni lazima mashairi yawe magumu kueleweka?

Je, vurugu zinazotokea huwa ni za kisiasa? Je, siasa inamaanisha kitu tofauti katika mazingira tofauti?

 Kama kuegesha gari katika mistari miwili ya njano adhabu yake ni kifo, na hakuna aliyewahi kutenda kosa hilo je, hiyo inaweza kuwa sheria mahususi?

 Ni kitu gani cha kawaida kwa binadamu?

Kama unaweza kugundua chombo kipya cha muziki, ni aina gani ya sauti kitakuwa kinatoa?

Huu ni mti wa cactus. Niambie kuhusu huu mti.

Rasmi.. Dawa ya Ukimwi Yagundulika Nchini Israeli,..!!!

$
0
0

MAMILIONI ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) ulimwenguni, sasa wanaweza kupata tumaini jipya baada ya wanasaynsi wa nchini Isreali kugundua dawa ambayo inasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu Ukimwi.

Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Hebrew kilichopo Jerusalem nchini Israeli wamegundua dawa yenye protini ambayo wanadai inaweza kupunguza virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa mgonjwa kwa asilimia 97 ndani ya siku saba tu, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Times la Israel.

Ugunduzi huu mpya sasa unatoa tumaini jipya katika utafutaji wa dawa ya ungonjwa huu ambao mpaka sasa hauna tiba ukiwa umeshaua watu zaidi  ya milioni moja kwa mwaka 2015 pekee.

Virusi vya Ukimwi hushambulia chembe chembe nyeupe za damu zinazojulikana kama CD4 ambazo husaidia kupigana na magonjwa yanayoingia mwilini.

Virusi vya Ukimwi huingia ndani ya chembe chembe hai nyeupe na kujizalisha kwa wingi jambo ambalo husababisha uharibifu wa CD4.

CD4 zinapokuwa chini ya 200 kwa kyubiki milimita za ujazo wa damu, mgonjwa anahesabika kuwa tayari ameanza kuugua Ukimwi.

Ugunduzi huo mpya umehusisha majarabio ya dawa hiyo mpya ambayo iliwekwa kwenye damu ya wagonjwa 10 wa Ukimwi iliyokuwa kwenye chupa maalumu kwa ajili ya majaribio.

Sehemu kubwa ya dawa hiyo ambayo ilipewa jina la Gammora na watafiti, ilisababisha uzalishaji wa DNA ya virusi hao ndani ya CD4 iliyoathirika kujizalisha kwa wingi badala ya utaratibu wa  kawaida ambao huzalisha moja au mbili.

Hii inasababisha chembe chembe nyeupe zilizojeruhiwa kujiharibu zenyewe na kuzifanya zishindwe kusambaza virusi zaidi.

Majarabia yanahusisha dawa hii mpya ya Gammora yataendelea kukiwa na matumaini makubwa kuwa itaweza kuua asilimia 100 ya seli zilizoathiriwa na Virusi vya Ukimwi.

Abraham Loyter mmoja ya wagunduzi wa dawa hiyo mpya, aliliambia gazeti moja la Israeli kuwa ugunduzi huo mpya unaleta tumaini jipya.

“Tunachokifanya sisi ni kuharibu seli ambazo zimeathirika na kwa hiyo zitakufa moja kwa moja na hazitaweza kusambaza tena virusi,” anasema.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya ya Israeli ilitangaza kwa mara ya kwanza kugawa dawa zenye uwezo wa kuzuia maambukizi kwa makundi yenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya. Dawa hizo zinazojulikana kama prophylactic drugs zinapomezwa mara kwa mara zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi.

Kwa sasa, dawa pekee kwa watu wenye virusi vya ukimwi, ni dawa za kupunguza makali ambazo humezwa kila siku ambazo pia hupunguza uwezekano wa maambukizi mapya.

Historia inaonyesha kuwa VVU ilitokea kwa nyani waliopo katika Afrika ya kati katika miaka ya 1900. Kutokana na mwingiliano kati ya tamaduni tofauti na mataifa, vilianza kusambaa duniani.

Ukimwi uligundulika nchini Marekani miaka ya 1980 na ulijulikana kama Ukosefu wa Kinga kwa Mashoga (GRID). Kadiri muda ulivyokwenda, wagonjwa wengine watano waligundulika nchini humo, wote wakiwa ni mashoga mwaka 1981.

Wakati watafiti na wanasayansi wakiendelea kuumiza  vichwa kupata majibu ya dawa ya ugonjwa huu unaendelea kugharimu maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kila mwaka, bado tiba au kinga yake ya uhakika imekuwa mtihani mkubwa ambao hadi sasa hakuna aliyeufaulu. Hata hivyo, wugunduzi huu wa wanasayansi wa Israeli unaweza kubadilisha matokeo.

Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini zina asilimia ndogo mno ya maambukizi yanayokadiriwa kuwa 0.1. Hii ni tofauti na nchi za Kiafrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo karibu asilimia tano ya watu wake wanakadiriwa kuwa wameaambukizwa VVU.

Kwa sasa tuna watu 7,500 ambao wanaishi na VVU hapa Israeli,” anasema Dk. Margalit Lorber ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Afya cha Haifa's Rambam kinachoshughulika na magonjwa yanayotokana na upungufu wa kinga ya mwili. Wagonjwa wapya 450 huripotiwa kila mwaka,” anaeleza.

Wakati asilimia ya watu walioathirika na VVU nchini Israel ikiwa ni asilimia 0.1, nchi hiyo ilianza tafiti kuhusiana na ugonjwa huo miaka 1990 wakati kulipokuwa na msukumo mkubwa duniani juu ya utafiti wa VVU na Ukimwi.

Wanasansi walioshiriki katika utafiti wa dawa hiyo mpya wanasema, majaribio ya ufanisi wa dawa hiyo yataanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na wanatarajia kuifanya tiba hiyo kuwa ya gharama nafuu kuliko dawa zozote za ugonjwa huo.

Kutana na Kraft:Mbilikimo Anayejiona Mwenye Bahati kwa Kupata Demu Mrefu Zaidi Yake Mara Mbili...!!!

$
0
0

KAMA mwanamume pekee duniani mwenye uwezo wa kunyanyua vitu vizito mara nne wa uzito wake mwenyewe, Anton Kraft, linapokujua suala la ‘uzito kwa uzito’ ni mtu mwenye nguvu zaidi duniani.

Mbilikimo huyo mwenye urefu wa futi 4'4', mkazi wa Florida, ameweza kuinua uzito wa stone 36 sawa na kilo 229.

Kraft , 52, hupenda kutoka na wasichana wenye urefu mkubwa zaidi ya wake na kwa miezi sita iliyopita amekuwa akitoka na China Bell mwenye urefu wa futi 6'3'.

Bell (43), ambaye alizaliwa mwanamume kabla ya kubadili jinsia kuwa  mwanamke, alipoombwa uhusiano na jamaa huyo mwenye nguvu, haraka haraka alijikuta akimkubalia kutokana na kulewa na ujuzi wake wa kunyanyua vitu vizito.

“Nadhani unyanyuaji wa vitu vizito wa Anton umenivutia  mno, lakini pia kwa sababu yeye mwenyewe anavutia pia, wakati unaposhikilia taji la unyanyuaji wa uzito wa juu duniani huwa unamaanisha mengi,” Bell anasema.

“Kamwe nilikuwa sijawahi kutoka na mpenzi mwenye urefu wa futi 4'4", lakini nilikuwa na shauku nilipokutana naye. Nina furaha nimempata kwa bahati kwa sababu yeye yu mtu wa aina yake.

Mimi niko tofauti naye yu tofauti na tunakotoka, tofauti ni nzuri.

Miaka 10 ya kunyanyua vitu vizito, Kraft anadai kuwa na rekodi ya wakati wote kwa daraja lake la uzito.

Lakini inaonekana amezidisha kipimo cha kunyanyua uzito zaidi ya mwili wake.

Anasema ‘kiufundi amekufa’ mara tano kabla ya kufufuka – kutokana na kukumbana na matukio kuanzia kusombwa na mafuriko hadi kuanguka kutokea dirishani.

Madaktari wana wasiwasi kuwa  huenda akapata shambulio la moyo iwapo ataendelea na mfumo wake wa maisha hayo ya unyanyuzi wa vitu vizito visivyoendana na ule wake.

Lakini Kraft haonekani kubabaishwa na hilo.

“Baadhi ya watu wanasema ninachofanya ni udhaifu, lakini nataka kufanya kitu ambacho sina, ninachoweza kuthibitisha kuwa nakiweza.”

“Kwa ujumla mimi ni mmoja wa watu watano wenye nguvu zaidi duniani bila kujali urefu na uzito.

“Na zaidi mimi ni mwanamume pekee duniani kuwahi kunyanyua uzito mara nne zaidi ya ule wa mwili wangu,” anajigamba.

Anayemtia nguvu katika harakati zake hizo, anasema ni rafiki wake huyo wa kike. 

“Florida ni moja ya majimbo yenye ndoa za jinsia moja na sote kimsingi ni wa watu jinsia moja.

“Nafurahia kutoka na mwanamke aliyebadili jinsia kwa sababu alizaliwa mwanaume akaweza kufanya kila linalowezekana kuwa mwanamke.

“Nakutana na sehemu kubwa ya wanawake, ambao wamezaliwa wakiwa wanawake, ambao hata hivyo, sina muda mwingi wa kushughulika nao.

“Kwa sasa kwa mafanikio yangu ukiongeza na kuwa na mpenzi nimpendae wa aina hii, hakika najihisi kuwa mwanaume mwenye bahati kuliko wote duniani.

“Hakika tuna furaha sana na ukweli najisikia vyema kuliko kipindi chote cha maisha yangu. Shukrani hakika zimwendee China,” anasema.

Fahamu Sifa za Lazima Wanazotakiwa Kuwanazo Walinzi wa Papa Fransic Huko Vatican

$
0
0

Sehemu ya walinzi wanao linda makao makuu ya papa (baba mtakatifu) huko Vatican .

Vigezo vya kuwa mlinzi wa Vatican ni kama ifatavyo:

1.Lazima uwe mkatoliki


2.Lazima uwe haujaoa (msela).

3.Lazima uwe lraia wa Uswiswi (Swiss citizen)

4.Uwe na umri wa kati ya miaka 19-30.
5.Uwe na urefu wa anagalau sentimenta 175 .(175 cm) 

6.Wanatumia ndogo ndogo za kisasa na za kienyeji .
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images