Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Zuri Lingine la Mbwana Samatta, Achaguliwa Kwenye Kikosi Bora cha Wiki cha UEFA Europe Leque

$
0
0

Mshambuliaji wa timu ya RC Genk na nahodha wa Taifa stars, Mbwana Samatta amechaguliwa kwenye kikosi bora cha wiki cha UEFA Europe legue.

Neno la pongezi kwa Samatta.

Warioba Apigilia Msumari Baa la Njaa Nchini...

$
0
0

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Sinde Warioba amesema haina haja ya kubishana kama kuna njaa au upungufu wa chakula kwani dalili zinaonyesha tatizo hilo litatupata na haitakuwa mara ya kwanza kwani limeshawahi kutokea.

Amesema kuwa wakati wa nyuma tatizo kama hilo lilipotokea watu walishirikiana kusaidia kuwapa wakulima maarifa na taarifa za hali ya hewa ili waweze kukabiliana na tatizo.

Ametolea mfano njaa inavyoathiri nchi za Somalia, Kenya na Nigeria kwa sasa ambapo watu na mifugo wamefariki na kusema mabishano hayasaidii.

Ameyasema hayo yote katika Kongamano la wanawake katika Uongozi linaloendelea katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kenya Kuajiri Madaktari Kutoka Tanzania..Kisa Mgomo wa Madaktari

$
0
0

KENYA: Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Peter Munya ametangaza kuwa Serikali itaajiri madaktari kutoka Tanzania, Ethiopia na Cuba ndani ya wiki 3 zijazo.

Madaktari hawa wa kigeni wataajiriwa ili kuchukua nafasi ya madaktari walio katika mgomo uliodumu kwa siku zaidi ya 90 wakidai kuongezewa malipo.

Akiongea katika mkutano huko Naivasha, Munya aliwaambia madaktari ambao bado hawajarudi kazini waende kusaini makubaliano ya utambulisho katika Serikali za Kaunti zao.

Haya yamekuja siku moja tu baada ya Rais Kenyatta kusema kuwa wanachofanya madaktari hao ni 'blackmail' na wanachokitaka ni kikubwa mno na hakiwezi kufanywa ndani ya usiku mmoja.

Mabadiliko ya CCM Kusomba Vigogo 11,Wamo Mawaziri,Wabunge na Makada Maarufu..!!!

$
0
0

Wakati mabadiliko ya katiba yatawaengua vigogo 11 katika uongozi wa CCM walio na kofia zaidi ya moja, hatima ya idadi kama hiyo ya wanachama wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, itajulikana kesho.

CCM inatarajia kupitisha mabadiliko makubwa ya katiba, ambayo yatapunguza idadi ya wajumbe katika vikao vya juu na pia kupunguza kofia za uongozi mwanachama mwenye cheo ndani ya chama, ubunge au serikalini.

Mabadiliko hayo yalipendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 13 mwaka jana.

Mabadiliko hayo yalitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliyemaliza muda wake, Nape Nnauye kwamba muundo wa chama umebadilika na mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa CCM, Toleo la 2012, Kifungu cha 22 na 23.

Nape alizitaja nafasi hizo kuwa ni mwenyekiti wa tawi, kijiji au mtaa, kata/wadi, jimbo, wilaya na mkoa. Wengine ni makatibu wa halmashauri kuu wa ngazi zote, mbunge, mwakilishi na diwani.

Mabadiliko hayo pia yamepunguza ukubwa wa Kamati Kuu kutoka wajumbe 34 hadi 24, hali inayofanya wanaoingia kwa kupigiwa kura kupungua hadi wanne kutoka kumi.

Pia nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu zimepungua kutoka 388 hadi 158, huku wengi wakiingia kwa nafasi zao na wajumbe kutoka wilayani kuondolewa.

Kutokana na mabadiliko hayo, baadhi ya viongozi wenye kofia zaidi ya moja wameshaanza kutangaza kutotetea nafasi zao katika uchaguzi ujao wa viongozi wa CCM na jumuiya zake.

Wa kwanza alikuwa Sophia Simba ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba. Simba pia mbunge na mjumbe wa Kamati Kuu.

Mwingine ni Abdallah Bulembo aliyetangaza kuwa hatagombea uenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM. Bulembo ameteuliwa na Rais Rais John Magufuli kuwa mbunge, jambo linalomfanya awe na kofia mbili.

Mbali na hao waliotangaza hadharani, wapo vigogo wengine ambao wana nafasi zaidi ya moja za uongozi, akiwamo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ambaye mbali na uwaziri ni mbunge, mjumbe wa NEC na mjumbe wa Kamati Kuu.

Pia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ni mbunge na mjumbe wa Kamati Kuu, kama ilivyo kwa Profesa Makame Mbarawa (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu wakati Shamsi Vuai Nahodha ni mbunge na mjumbe wa Kamati Kuu.

Mabadiliko hayo pia, yatawakumba wenyeviti wa CCM wa mikoa ambao kwa nafasi zao ni wajumbe wa NEC. Mmojawapo ni Kimbisa, ambaye ni mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma na mjumbe wa Kamati Kuu.

Wenyeviti wa mikoa ambao pia ni wabunge ni Joseph Msukuma (Geita), Martha Mlata (Singida) na Deo Simba (Njombe). Mwenyekiti wa CCM wa Mbeya, Godfrey Zambi pia ni mjumbe wa NEC na mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Mwingine anaonekana kuguswa na mabadiliko hayo ni Salma Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini na ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais kuwa mbunge.


Maoni ya CCM, Mbunge Njombe

Alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo, naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema suala la kofia mbili litajadiliwa na kutolewa uamuzi na Halmashauri Kuu.

“Tusiwahishe ajenda hiyo. Hatuzuii mtu kujiuzulu kwa utashi wake, lakini jambo hilo litajadiliwa na Kamati Kuu na mwishowe kwenye Halmashauri Kuu chama kitaweka wazi nini kitafanyika kwa sababu huko ndipo yatangazwa mabadiliko ya kanuni na ratiba ya uchaguzi ndani ya chama utakavyokuwa kuanzia ngazi ya matawi,” alisema Vuai.

Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga ni miongoni mwa wanachama wenye kofia mbili, akiwa pia mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Njombe. Alipoulizwa atavua kofia gani kati ya ubunge na uenyekiti, alisema anasubiri mwongozo wa Halmashauri Kuu.

“ Mimi ni mjumbe natarajia kwenda huko huko. Mwongozo ukitolewa ndipo nitajua cha kufanya, lakini kwa sasa siwezi kukueleza kwa uhakika,” alisema Sanga.

Wengine waliotafutwa kuzungumzia suala hilo hawakupatikana, isipokuwa Msukuma ambaye alisema yuko kikaoni.


Hatua kali za kinidhamu

Lakini hoja inayotarajiwa kutingisha ni ya kujadili mchakato wa uteuzi wa wagombea wa CCM na mambo yaliyojitokeza katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Miongoni mwa wanachama watakaokuwa katika wakati mgumu ni wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao walipinga hadharani maamuzi ya chombo hicho ya kupitisha majina matano ya wagombea urais kwa maelezo kuwa katiba ya CCM ilikiukwa.

Wajumbe hao ni Sophia Simba, Adam Kimbisa na Emmanuel Nchimbi.

Waliopitishwa walikuwa Bernard Membe, January Makamba, Dk Asha-Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ali na John Magufuli (ambaye alishinda na sasa ndiye Rais).

Chanzo cha habari kililiambia Mwananchi kuwa baadhi ya wanachama hao wameshahojiwa na Kamati ya Maadili na kwamba kinachosubiriwa sasa ni uamuzi.

“Kamati ya maadili imeshamuhoji Sophia Simba na wanachama wengine na NEC inakaa na kupokea mapendekezo ya Kamati ya Maadili, hapo ndiyo hatma yao itajulikana. Lakini nakwambia ndugu yangu hawa watu sasa hawawezi kutoka,” alisisitiza.

Mwananchi ilipomtafuta Simba kuhusu suala hilo alisema hayo ni maneno ya mtaani na kwamba chama kina taratibu zake.

“Chama kina taratibu zake hakiwezi kuyumbishwa na maneno ya mitaani. CCM ina taratibu zake na maamuzi yanapitia vikao halali vya chama,” alisema Simba.

“Kwanini unataka tuvuke mto ilihali hatujafika.”

Alipoulizwa kuhusu taarifa kuwa alihojiwa pamoja na watuhumiwa wengine, alisema hizo ni taratibu za kawaida katika chama chao.

“Ninachofahamu kuhojiwa ni taraibu za kawaida sina kesi yoyote,” alisema.

Juhudi za Mwananchi hazikufanikisha kumpata Kimbisa, hali kadhalika Nchimbi ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa balozi nchini Brazil kutokana na simu zao kutopatikana.

Wengine watakaokuwa katika wakati mgumu ni wanachama wanaodaiwa kukisaliti chama wakati wa kampeni za uchaguzi na ambao walijadiliwa kuanzia ngazi ya wilaya na baadaye mapendekezo kuwasilishwa vikao vya juu na baadaye Kikwete kumkabidhi Rais Magufuli ripoti hiyo.

Mara kadhaa viongozi wa chama hicho walikaririwa wakitaka wasaliti wa chama kuchukuliwa hatua, akiwamo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliwataka viongozi wa CCM wa Mkoa wa Kaskazini A kisiwani Unguja kuwachukulia hatua zinazostahili wanachama wanaokisaliti na kukihujumu chama.

Pia, mara kadhaa wakati wa kampeni, Rais Magufuli alikuwa akituhumu wanachama kuwa walikuwa wakionyesha kuwa CCM mchana na usiku wakipigia kampeni wagombea wa vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Katika uchaguzi huo, vyama vya upinzani viliendelea kuipokonya CCM viti huku mgombea urais aliyeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa akipata takriban asilimia 40 ya kura zote, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi wa vyama vingi urudishwe mwaka 1995.

Wanachama wanaodaiwa kukisaliti chama hicho ni pamoja na mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, ambaye amekuwa akilalamikiwa kutokana na CCM kufanya vibaya katika uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini lililochukuliwa tena na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.


Bulembo ajiuzulu

Katika hatua nyingine, jana katika kikao cha Baraza Kuu Maalum la Jumuiya ya Wazazi, Bulembo alitangaza kutotetea nafasi yake ya unyekiti.

“Kila mmoja ni shahidi, wakati naingia, jumuiya hii ilikuwa inakwenda kufa, jambo lililosababisha aliyekuwa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kutaka kuifuta. Lakini nikamuhakikishia ataona mapinduzi akiniachia,” alisema Bulembo.

“Sasa natoka kifua mbele, yale yote niliyoyaahidi nimetimiza kwa asilimia 75. Tangu nimeingia hatujawahi kuomba hata shilingi moja kwa ajili ya uendeshaji,” alisema.

Hata hivyo, Bulembo alisema ataendelea na vikao vyote mpaka Oktoba atakapomkabidhi rasmi mwenyekiti mpya.

Alisema kwa sasa asiulizwe kwa nini amechukua uamuzi huo na kwamba hoja siyo kuteuliwa kwake kuwa mbunge bali ni utaratibu aliojiwekea katika maisha yake.

Credit - Mwananchi

Serikali Yazidi Kumpendelea Dangote,Baada ya Kupewa Mgodi wa Makaa ya Mawe,Sasa Apewa Tenda ya Kuiuzia Serikali Cement Ili Kukamlilisha Ujenzi wa Dodoma..!!!

$
0
0

Serikali ya mkoa wa Dodoma imeingia makubaliano na kampuni ya saruji ya Dangote kuuza saruji katika ujenzi wa miji mipya ya makao makuu ya nchi (Dodoma).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo mara baada ya kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa kampuni za Dangote Alhaaj Saada Ladan, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema kuwa Serikali ya mkoa wa Dodoma imeipa eneo kampuni hiyo ya Dangote kama eneo la bandari kavu, ambapo saruji inayouzwa nje ya nchi, zitauziwa kutoka Dodoma.

Alhaaj Ladan kwa upande wake aliishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliotoa kwa kampuni hiyo, huku akisema kuwa ikizingatiwa hata mji wa mkuu wa Nigeria Abuja, ulijengwa na wataalamu wa kitanzania, na hivyo hawana budi nao kutoa mchango wao kuijenga Dodoma.

JPM Aongoza Kikao cha Kamati ya Maadili CCM...!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 10 Machi, 2017 ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.

Siku 14 Ngumu kwa Serikali ya Zanzibar...!!!

$
0
0

Hatua ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutoa siku 14 kwa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) na taasisi za Serikali kuhakikisha wanalipa madeni yao ya umeme la sivyo watakatiwa umeme, vitaipa wakati mgumu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka aliwaambia waandishi wa habari kwamba shirika lake linadai wateja hao jumla ya Sh275 bilioni.

“Tunadai kiasi kikubwa sana cha fedha kutoka kwa wateja wakubwa na wadogowadogo, mpaka Zeco, hivyo tunatoa notisi ya siku 14 kuanzia leo (jana) walipe deni lao kwani baada ya hapo tutasitisha huduma pamoja na kuchukua hatua nyingine za kisheria,” alisema Dk Mwinuka.

Katika kiasi hicho, Zeco inadaiwa Sh127 bilioni ambacho ni sawa na asilimia 15 ya Bajeti ya Serikali ya Zanzibar kwa mwaka 2016/17 ambayo ni Sh841.5 bilioni.

Pia kiasi hicho ni kikubwa karibu mara nne ya kile kilichotengwa katika bajeti hiyo kwa ajili ya mikopo ya ndani ambacho ni Sh33.0 bilioni hali inayoonyesha kwamba Zeco na SMZ watalazimika kuandaa mpango mkakati wa kulipa deni hilo ambao utamaanisha kujifunga mkanda ili kulimaliza.

Alipoulizwa kuhusu notisi hiyo ya kulipa deni, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Zanzibar, Salama Aboud Talib ambaye alikuwa ziarani Pemba alisema hadi jana hakuwa amepokea barua kutoka Tanesco hivyo asingeweza kuzungumza chochote.

Wiki iliyopita, akiweka jiwe la msingi katika kituo cha kupoza umeme cha njia ya Kv 132 mkoani Mtwara, Rais John Magufuli aliiagiza Tanesco kuwakatia umeme wadaiwa wote sugu ikiwamo Zanzibar. Alisema shirikia hilo halipo kisiasa, hivyo wadaiwa wote wakatiwe umeme.

Sambamba na hayo, alilitaka shirika hilo kutoingia mikataba na kampuni zinazoweza kusababisha au kuongeza madeni, badala yake mwekezaji yeyote akitaka kuwekeza azalishe umeme wake na kuuza mwenyewe.

Wadaiwa wengine

Kuhusu wadaiwa wengine, Dk Mwinuka alisema hadi kufikia Januari, shirika hilo lilikuwa linazidai wizara na taasisi za Serikali kiasi cha Sh52 bilioni huku kampuni binafsi na wateja wadogo wakidaiwa jumla ya Sh94 bilioni.

Alisema malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya shirika kwa wakati ikiwamo uendeshaji, matengenezo ya miundombinu pamoja na miradi mbalimbali.

Alisema kulipwa kwa malimbikizo hayo ya madeni kutaisaidia Tanesco kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi zaidi, hivyo kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme nchini.

Alipoulizwa kuhusu mashirika na taasisi za umma zinazodaiwa malimbikizo hayo ambayo Tanesco haikuyataja, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alisema mashirika hayo yanatakiwa kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kulipa deni kama wanavyodaiwa.

Shehena Kubwa ya Pombe Aina ya Viroba Kutoka Nchi ya Uganda Yakamatwa Wilayani Muleba...!!!

$
0
0

Shehena kubwa ya pombe haramu iliyofungashwa kwenye mifuko aina ya viroba kutoka nchi ya uganda kwa njia za magendo imekamatwa ikiwa imehifadhiwa kwenye gari lililojengwa nje ya mji kata ya Nshamba wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera huku kiwanda cha kuzalisha pombe kali inayosadikiwa haifai kwa matumizi ya binadamu kimefungiwa.

Kukamatwa kwa ghala lililosheheni pombe kali kutoka nchi jirani ya Uganda na kufungwa kwa kiwanda cha pombe kali ni matokeo ya operesheni inayohusisha jeshi la wananchi, uhamiaji,magereza,polisi na mgambo kwa lengo la kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu hapa nchini ambapo operesheni hiyo imefanikiwa kuwakama ta watuhumi wa watatu wakiwa na katoni 800 za viroba na tani nane za kahawa ikisafilishwa kwa njia za magendo nje ya nchi kinyume cha sheria.

Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Modest Lwakahemula amebainisha madhara ya kutumia pombe kali.

Baadhi ya wananchi wameipongeza serikali kuanzisha operesheni ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na pombe kali hapa nchini.

Ongeza Shape na Kupata Muonekano wa Kuvutia Kwa Kutumia Botcho Mult Plus 10

$
0
0

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu sasa imewasili.
BOTCHO MULT-PLUS 10× ni dawa mpya iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza shepu na kuwa na muonekano wa kuvutia. Imewasaidia wengi ktk nchi mbali mbali duniani na sasa imeingia Tanzania na inasambazwa na MARKSON BEAUTY PRODUCTS pekee.
SIFA ZAKE:-
1.Huongeza hipsi, makalio na mapaja.
2.Huzuia michirizi wakati wa kuongezeka mwili.
3.Huzuia kuongezeka kwa tumbo na mikono
4.Matokeo ya haraka sana na garantii.
5.Ni salama kabisa na imethibitishwa.


BOTCHO MULT-PLUS 10× inapatikana kwa laki mbili tu. @200,000/=.
Kwa bidhaa za tiba na urembo tufuatilie kwenye GOOGLE au instagram @markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr.
(+255) 0767447444 au
0714335378

Umeisikia Hii ya Papa Francis Kuruhusu Wanaume Walio na Wake Kuwa Mapadri?

$
0
0
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema kuwa huenda wakabadili sheria kuwaruhusu wanaume waliooa kuwa mapdri wa kanisa hilo.

Papa Francis alisema hayo akifanya mahojiano na gazeti moja la nchini Ujerumani ambapo alieleza kuwa, ni wakati sasa wa kufikiria jambo hilo kutokana na kanisa kukumbwa na uhaba wa mapadri hasa maeneo ya vijijini katika maeneo mbalimbali duniani.

Kiongozi huyo wa kanisa alisema, yeye yupo tayari kufanya mabadiliko hayo ambayo yataruhusu wanaume waliooa kubarikiwa na kuwa mapadri, lakini kwa wale ambao tayari ni mapadri, hawataruhusiwa kuoa.

Kanisa katoliki tayari limeruhusu baadhi ya watu waliooa kuwa watumishi kanisani. Wakristo ambao tayari wameoa kisha wakabadili dhehebu na kuwa wakatoliki wanaruhusiwa kuendelea kuwa kwenye ndoa na kuwa mapadri wa kanisa Katoliki kama watapa ridhaa kutoka kwa wake zao.

Kanisa Katoliki linaamini kuwa Padri hatakiwi kuoa kulingana na maandiko matakatifu katika biblia, na kwavile inaaminiwa kwamba Padri anatakiwa kuishi kama Kristo, na hivyo hatakiwi kuoa kama ilivyokuwa kwa Kristo Yesu.

Alichokizungumza Mchezaji Samatta Baada ya Kufunga Goli Mbili Europa League

$
0
0
Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ambao walikuwa ugenini usiku wa March 9 kucheza mchezo wao wa kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent, Samatta anarudi katika historia baada ya kufanikiwa kuifungia goli mbili KRC Genk dhidi ya KAA Gent katika ushindi wa 5-2.

Baada ya hapo Samatta ambaye kacheza mechi yake ya 9 ya Europa League ndio kafunga goli, alifanya mahojiano  na Sport Extra ya Clouds FM na kueleza anavyojisikia kufanikiwa kufunga katika michuano ya UEFA Europa League hatua ya 16 bora.

“Nakosa hata cha kusema kwa jinsi ninavyojisikia kwa sababu nilikuwa natafuta sana hilo goli la Europa kuliko kitu chochote, nilikuwa nahangahika na kipindi ambacho natafuta hayo magoli yalikuwa hayaji, kwa hiyo ile game ya jana ilikuwa nimeshatafuta sana magoli kwa hiyo nikaona bora ni relax ikitokea nafasi sawa”

Alichokiandika Ridhiwani Kikwete baada ya Kenya, Uganda kupost Will Smith yupo kwao

$
0
0
March 6 2016 ziliripotiwa stori za staa kutoka Marekani amekuja Tanzania kwa mara ya pili hii ni baada ya picha yake aliyopiga Airport Arusha kusambaa kwenye kitandao ya kijamii, Will Smith alidaiwa kuwa anaelekea mbuga za wanyama Serengeti.

Headlines zimekuwa nyingi kuhusiana na Will Smith kuja Tanzania lakini nchini Kenya Ghetto Radio wameripoti kuwa  ‘Will Smith in Kenya’ ambapo ilikuwa ni March 3 2017, Uganda wameandika ‘Hollywood Movie Star @willsmith has made a call on Uganda Africa #ugandatourism

Post ambazo zimeandikwa na mitandao ya kijamii ya Kenya zinaonekana au zinadaiwa kama kupotosha na kulazimisha ionekane staa huyo amekuja nchini kwao lakini zikitumika zile zile picha ambazo ziliripotiwa kuwa alikuwa ni Tanzania, mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametumia ukurasa wake wa instagram kuyaandika haya…..

“Yaaani ni haya mambo yanaweza sababisha watu wasiongee ! Sasa kila nchi ya ukanda huu inadai alikuwapo kwao. Ninachojua mie alikuwa Arusha,Tanzania na hii picha alipiga Airport. Sasa sijui nn?”

Wanaume Waliochelewa Kuoa Wana Msongo wa Mawazo Kuliko Wanawake

$
0
0
Kuna utafiti nilikuwa nafanya baada ya kufwatilia baada ya kuona topic nyingi zinazowasema single mother's na wanawake waliofika miaka 30s bila kuolewa.

Nilichokigundua;

1. Wanawake waliochelewa kuolewa na na single mother wengi wana amani ya moyo kuliko wanaume waliochelewa kuowa na single dads ndomana awaishi kujaza JF topic za kuwazungumzia wanawake hiyo yote nikujipa moyo ili kupunguza maumivu.

2. Wanaume wengi waliochelewa kuoa mpaka kufika miaka 35 na kuendelea wengi walitegemea kuchelewa kuoa kutawafanya wawe na pesa na maisha mazuri lakini imekuwa tofauti wengi wamefika umri huo wakiwa hawana kitu tofauti na wenzao waliooa mapema wana faraja ambayo ni watoto na wengine wamepata baraka maisha yamewanyookea,asila za kukosa vyote vinawatesa wanajikuta na asila muda wrote poleni kwa hilo.

3. Wanaume wengi waliochelewa kuoa wanatabia zisizovumilika bila kusahau maneno mengi bila vitendo ujuaji mwingi na dharau kwa wanawake wanasahau walizaliwa na mwanamke poleni, mwanamke yoyote anatakiwa kuheshimiwa.

NB; Jirekebisheni tabia njema si kwa mwanamke mtu hata mwanaume unatakiwa ujitambue labda ujitahidi uwe na mapesa kama Mengi ndo utapata mtoto mzuri wakutuliza moyo wako ukifika 40s maana huwa mnajipa moyo wanaume amzeeki.

Nafasi za Kazi World Vision na Zingine zilizotangazwa leo Katika Magazeti

Msami Atamani Kutoka na Wema Sepetu...!!!

$
0
0

Msanii wa bongo fleva ambaye pia ni miongoni mwa ma'dansa' wakali Bongo, Msami Baby ameweka wazi hisia za moyo wake na kusema kuna mastaa wa 'bongo movie' anatamani kutoka nao kimapenzi.

Msanii huyo amesema katika tasnia ya filamu ametokea kuwapenda wadada watatu ambao ni Wema Sepetu, Elizabeth Michael (Lulu) na Jokate Mwegelo japokuwa amekuwa matatani kwa kushindwa kuchagua mmoja kwa kuwa wote ni wazuri.

“Katika mastaa wa bongo ambao ninawapenda sana na ninatamani ningewapata ni pamoja na Jokate Kidoti, Lulu na Wema Sepetu, uzuri wa hawa wadada unanifanya niwapende sana” Alisema Msami

Kwa upande mwingine msanii huyo amesema yeye umri kwake siyo kigezo kikubwa kwakuwa ameshawahi kutoka na mwanamke aliyemzidi umri na wakaishi vizuri bila ya kuwa migogoro ya aina yeyote ile.

Israel Yapiga Marufuku Adhana Misikitini..!!!!

$
0
0

BUNGE la Israel limeridhia muswada wa kwanza wa sheria, ambayo itaweka kikomo cha adhana – wito kwa Waislamu kwenda misikitini kutekeleza ibada ya sala.

Aidha unapiga marufuku matumizi ya vipaza sauti wakati wowote.

Hata hivyo, muswada wa sheria hiyo ulisababisha hasira kubwa miongoni mwa wabunge kutoka jamii ya Waarabu nchini hapa.

Muswada wa kwanza wa sheria hiyo unataka marufuku kwa mwadhini kutumia kipaza sauti kati ya saa tano usiku na saa moja asubuhi, ukilenga adhana kwa sala ya Alfajiri.

Mbali na muswada huo, mwingine unapendekeza marufuku kwa mwadhini kutumia kipaza sauti katika mitaa yenye makazi ya watu, na faini ya kiasi cha euro 2,600 itatozwa kwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo.

Sheria ya kwanza itahusu misikiti katika eneo la Jerusalem Mashariki linalokaliwa na Israel na pia maeneo yote ya nchi hiyo, lakini haigusi viwanja vinavyouzunguka msikiti wa al-Aqsa ambavyo vimo katika mgogoro huo.

Siku Chache Baada ya Kustaafu Jeshi..Jenerali Mwamunyange Afunguka Haya...!!!

$
0
0

Mkuu wa majeshi mstaafu Jeneral Davis Mwamunyange amewetaka watanzania kudumisha uzalendo,mshikamano na umoja wa kitaifa pamoja na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda nchi.

Aidha baada ya ya ukaguzi wa gwaride rasmi lililokuwa na Gads 6 lilitengeneza umbo la Omega ikiwa ni ishara ya kuashiria mwisho ambapo baadae generali mstaafu alishuhudia ndege vita zikipita kutoa salamu za heshima.

Ifahamike kuwa Jeneral Davis Adolf Mwamunyange amehudumu kwa nafasi mbalimbali ndani na nje ya jeshi,aliwahi kuwa mtaalam wa kijeshi kwenye kamati ya ukombozi wa nchi za kiafrika chini ya OAU,mkurugenzi wa idara ya mahusiano ya kimataifa makao makuu ya jeshi,mkuu wa jeshi la kujenga taifa ,chief of staa na baadaye akateuliwa kuwa CDF madaraka aliyohudumu hadi anastaafu utumishi katika jeshi hilo.

Sentensi za Lema Katika Mkutano Wake wa Kwanza Arusha Baada ya Kuachiwa..!!!

$
0
0

Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema jana amefanya mkutano wa hadhara ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipotoka mahabusu wiki moja iliyopita.

Lema amefanya mkutano huo katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro ili kuweza kuzungumza na wapiga kura wake kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo ya maendeleo katika jimbo hilo.

Miongoni mwa mengi aliyoyazungumza, Godbless Lema amezungumzia kukamatwa kwake ambapo amesema kuwa amekaa mahabusu kwa miezi minne pasipo kuwa na kosa kabisa.

Aidha, ameeleza kuwa mahabusu kuwa watu wengi ambao wapo kule kwa kusingiziwa wengine wamewekwa tu kwa uonevu na hawana kosa, hivyo kama kiongozi ataendelea kuwapigania huku akiwasihi wakazi wa Arusha kuwaombea waliopo mahabusu.

Mbali na Lema, mwingine aliyepata nafasi ya kuzungumza na umati huo uliojitokeza leo ni mwanachama mpya wa chama hicho, muigizaji Wema Sepetu.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama mkoani humo akiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro.

Paul Makonda Apigwa Kombora Namba Mbili..

$
0
0

WAKATI nchi ikiwa imelipuka na kumpigia kelele za kutaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aoneshe cheti halisi cha kidato cha nne na kama hana ajiuzulu, wapinzani wake hao wameibuka na kombora namba mbili ambalo ni uraia wa mkewe, Ijumaa linakudadavulia. Awali, hoja ya vyeti feki ilishikiwa bango zaidi na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Josephat Gwajima ambaye alisema ana ushahidi wa cheti halisi cha Makonda chenye matokeo ya Divisheni 0 na kwamba alitumia cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge kilichomwezesha kuendelea na msomo.

NI JUMAPILI ILIYOPITA Gwajima alitoa madai hayo mazito, Jumapili ya Februari 26, mwaka huu, kwenye mahubiri ya ibada ya kanisani kwake, Ubungo ambapo alisema kuwa, Makonda alitumia cheti hicho feki wakati yeye alianza darasa la kwanza mwaka 1988, akitumia jina la Daudi Albert Bashite.

MITANDAONI SASA Baada ya Gwajima kufunguka hayo, mitandao ya kijamii ilianza ‘kumpiga’ Makonda kwa kumsema vibaya huku baadhi Chunguni

KIUJUMBE TOKA

Ukitaka ujue watu wanafahamu ulizaliwa wapi, unaitwa nani, ulisoma wapi, ulifaulu vipi? Wachokoze ama chukua fomu kugombea chochote ndipo utaelewa unaishi kwenye nyumba ya vioo! …Meseji Sent MAKONDA APIGWA… wakimtaka aoneshe vyeti halali na kama hana, ajiuzulu au Rais Dk. John Pombe Magufuli amtumbue.

WAZIDI KUMUANDAMA Kuna wengine walienda mbali zaidi, baada ya mkuu huyo wa mkoa kwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kimara jijini Dar Jumapili iliyopita na kuangua kilio alipokuwa ibadani, wakasema ‘hata akilia wao wanataka vyeti.’

“Hatutaki ulie, toa vyeti baba,” alichangia mmoja wa wafusi wa Mtandao wa Facebook. KUSUDI LA MAKONDA Kwenye ibada hiyo, Makonda alipopewa nafasi ya kuzungumza, alitumia mwanya huo kueleza namna ambavyo ameingia kwenye vita kubwa ya madawa ya kulevya ambayo wengi waliowahi kuianzisha walipoteza maisha ama walifungwa.

Alisema, inahitaji usimame na Mungu wa kweli ili uweze kufanikiwa kuishinda vita ya madawa ya kulevya kwani wanaohusika, wana nguvu kubwa ya kufanya lolote lakini yeye amejitoa mhanga kumsaidia Rais Magufuli aliyemteua.

“Kwenye hii vita, kila aliyeingia ni ama aliuawa au alifungwa au alipotezwa kwa namna yoyote ile,” alisikika Makonda akisema. Kuonesha kwamba yupo tayari kwa lolote, Makonda alisema yeye haoni tatizo kuukosa wadhifa wa ukuu wa mkoa kwa siku moja lakini hawezi kukubali katika utawala wake, vizazi viangamie kwa madawa ya kulevya.

“Hata kama nitakuwa mkuu wa mkoa kwa siku moja lakini ilimradi nimetimiza kusudi la Mungu, nipo tayari,” alisema Makonda.

ALIGUSIA KOMBORA NO. 2 Katika mazungumzo yake kanisani hapo, Makonda alionesha kunusa harufu ya kombora la pili ambalo ameandaliwa ili kukwamisha jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya ukiacha lile namba moja la vyeti ambalo ndilo lilikuwa ‘hot’.

“Baba mchungaji huwezi amini sasa hivi wametoka kwenye suala la vyeti, wamehamia kwa mke wangu. Naye wanasema si raia,” alisema Makonda.

MITANDAO YAKAZIA SASA Baada ya Makonda kusikika hivyo, mitandao ilizidi kuchochea moto suala hilo na kusema kwamba ni kweli mkewe si raia kwani hata uso wake unaonesha.

“Wewe humuoni alivyo? Anaonekana kama raia wa kigeni hivi, wakimfuatilia watajua na ninaamini ushahidi ni rahisi sana kupatikana. Vimepatikana vyeti sembuse uraia, tutashuhudia mengi mwaka huu,” alichangia jamaa aliyejiita Mehans mtandaoni.

MAKONDA AKESHA AKIMUOMBA MUNGU

Taarifa za ndani zimedai kuwa kutokana na makombora hayo, Makonda ameamua kumshtakia Mungu na kumuacha ayashughulikie maana anaamini dhamira yake ilikuwa njema katika mkoa na taifa lake. “Makonda sasa anapambana kiimani, ameamua akeshe kwenye maombi. Anafanya maombi, anaamini mwisho wa siku Mungu wake atamtetea. Mungu hawezi kukubali aangamie.

Wanamsakama kwa maneno, wanasahau ni Makonda huyo aliyejitoa kinaga ubaga kudhibiti mashoga. “Makonda huyohuyo alijitoa kudhibiti matumizi ya shisha, alisimama kidete kuendesha zoezi la kusalimisha silaha ambalo lilichangia kupunguza uhalifu ndani ya jiji.

“Watu wanajiweka pembeni na hoja ya msingi ya madawa ya kulevya ambayo mheshimiwa amejitoa. Amethubutu kuwataja wahalifu wa madawa hayo  yanayowaangamiza vijana, wao wanang’ang’ania suala la vyeti na uraia wa mkewe kweli? Mungu atampigania,” kilisema chanzo kilicho karibu na Makonda.

MADAI MENGINE

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambazo hazijathibitishwa, zinadai kuwa, kuna uwezekano mkuu huyo wa mkoa akawa amemuandikia barua rais kuomba kujiuzulu ili kuondokana na ‘presha’ ya maadui wanaomsakama. Hata hivyo, Makonda na ofisi ya rais, hawajazungumzia lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoenea.

KUTOKA KWA MHARIRI

Makombora anayorushiwa Makonda si jambo la ajabu sana kwani historia inaonesha kuwa, wengi waliojaribu kugusa mambo yenye madhara kwa jamii lakini yaliyo na faida kwa baadhi ya watu waliishia kupingwa na kuzushiwa mambo ya ajabu.

Hata hivyo, makombora yote mawili aliyopigwa Makonda ni mepesi na anayo nafasi ya kuyapangua yasimuathiri endapo ataamua kuweka kila kitu wazi ili kuwaumbua wazushi wanaotaka kumharibia sifa yake nzuri. Kinyume chake, sifa yake aliyojijengea kwa muda mrefu itakuwa imeingia doa.

Mama Salma Kikwete Atumika Kutapeli Watu ...!!!

$
0
0

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu uwepo wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos), inayotapeli watu fedha kwa kutumia majina ya watu maarufu nchini.

Tahadhari hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema Saccos hiyo yenye jina maarufu la Focus Vicoba kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na tovuti inayojulikana kwa jina “http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz. wapka-mob, hutumia majina ya viongozi serikalini na watu maarufu, kwa nia ya kuwatapeli wananchi.

Alisema majina ya viongozi yanayotumiwa na matapeli hao ni pamoja na jina la mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.

Aliongeza kuwa matapeli hao, hutumika kufungua akaunti za facebook na tovuti mbalimbali, ambazo hutumia kuwarubuni watu kwa kuwaaminisha kuwa wanaweza kupata mikopo yenye masharti nafuu na haraka zaidi kwa njia hiyo ya mtandao.

Alisema katika ufuatiliaji wa suala hilo, kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandao cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kimebaini kuwa katika tovuti “http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz. wapka-mob picha na jina la Mama Salma, limetumika huku kwenye ukurasa wa Facebook wakitumia jina la Mengi, likiwa ni pamoja na namba za simu 0757 308381 na 0768 199359 ambazo si za Mama Salma wala Mengi.

Aidha, alisema katika ufuatiliaji wa jambo hilo, Desema 16 mwaka jana alikamatwa mtu aliyefahamika kwa jina la Boniface Ojwando (27) baada ya kubainika kuwa anahusika katika mtandao huo wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kupitia mitandao hiyo ya kijamii, ambapo mpaka sasa mtuhumiwa ameshafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka hayo yanayomkabili.

“Nitoe onyo kwa wale wote wanaondelea kufanya udanganyifu huu wa kujipatia fedha kwa njia isiyo halali kupitia mitandao ya kijamii kuacha mara moja, kwani sheria iko wazi na pindi watakapokamatwa, watachukuliwa hatua kali,”alisema Sirro.

Alitoa rai kwa wananchi wote, kutokuwa wepesi kukubali matangazo ya mikopo, yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii, bila kufika katika ofisi husika ili kujiridhisha kuhusu utolewaji wa mikopo hiyo, ili kuepuka kutapeliwa fedha na mali zao.
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live




Latest Images