Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Exclusivee..Alichokisema Diamond Kuhusu Harmorapa ....!!!!!

0
0

Mkali wa Bongo Fleva Diamond Platinums Amefunguka Kuwa Hawezi Kumkandamiza Harmorapa kwa kutumia jina linalofanana na harmonize kwani staa huyu naye anatafuta maisha.

Diamond Amesema kuwa anampongeza Harmonize kwa kazi nzuri anazofanya hali iliyopelekea kupata shabiki anayevutiwa naye na kutamani kuwa kama yeye .

Aidha Staa huyo anayeweka na trak yake ya Marry You amesema kuwa Harmorapa Anatakiwa Kuungwa Mkono kama wasanii wengine kwani huenda alitafuta sana nafasi hii kwa muda mrefu.



Bongo Muvi Mnazingua Mjue...!!!!

0
0

SOKO la filamu za Kibongo lipo hoi, linasuasua. Sababu za kusuasua huko zimetajwa nyingi, lakini hivi karibuni kuna kundi kubwa limeibuka na kudai kuwa eti wasanii kujiingiza katika siasa kumesababisha anguko hilo.

Hoja ya ajabu kabisa. Wanadai eti kwa sababu mastaa kadhaa wa Bongo Muvi walionyesha upande wao wa kisiasa na ama kushiriki kwenye kampeni za kambi mbalimbali za vyama vya siasa kulichangia kurudisha nyuma soko la filamu nchini.

Si kweli. Wasanii wenyewe ndiyo wanaozingua. Nitajenga hoja.



TUANZE NA WEMA SEPETU

Hivi karibuni actress mwenye mashabiki lukuki, Wema  Sepetu aliamua kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Staa huyo ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbali ya kuwa mstari wa mbele katika kuwanadi wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka juzi, pia aligombea Ubunge wa Viti Maalum mkoani Singida – kura hazikutosha.

Akiwa CCM, katika kipindi cha kampeni, Wema alikuwa na wenzake wengine kama Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Steven Mengele ‘Nyerere’, Vincent Kigosi (awali alikuwa Chadema – Ukawa) na wengine wengi.



MASTAA NA SIASA

Mbali na hao, wasanii wengine walioshiriki kwenye kampeni na kujitanabaisha wazi kuwa ni wanachama wa vyama mbalimbali na hasa CCM na Ukawa ni pamoja na Jacob Stephen ‘JB’ na Wellu Sengo.

Wengine ni Single Mtambalike ‘Richie’, Deogratius Shija, Chuchu Hans, Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Aunt Ezekiel, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’, Jacqueline Wolper na wengineo.

Ukiacha mastaa hao wa filamu, wapo wanamuziki kadhaa ambao nao walishiriki kwenye kampeni hizo, miongoni mwao ni staa wa Bongo Fleva anayeendelea kupasua anga za kimataifa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ na Kala Jeremiah.

Lakini wapo waliojitosa kugombea katika majimbo  mbalimbali kama Afande Sele (Morogoro Mjini – ACT – Wazalendo), Mohamed Mwikongi ‘Frank’ (Segerea – ACT – Wazalendo), Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ (Kisarawe – CUF) na wengineo.



WALIOTUSUA KWENYE SIASA

Ipo mifano kadhaa ya wasanii wa sanaa mbalimbali duniani ambao waliingia kwenye siasa na kufanya vizuri. Kwa hapa kwetu mfano mzuri ni wabunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Joseph Haule ‘Profesa Jay’ (Mikumi), wote wa Chadema.

Profesa Jay ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni, lakini Sugu aliingia tangu bunge lililopita ambapo takwimu zinasema, alikuwa mgombea pekee aliyeshinda kwa kura nyingi zaidi kuliko mgombea yeyote!

Tuwaache hawa, twende kimataifa. Msanii maarufu wa filamu nchini Nigeria, Desmond Elliot ni mbunge na alimshinda mshindani wake wa karibu Bayo Smith kwa karibu zaidi ya nusu ya kura zote.

Lakini mwigizaji wa Hollywood Arnold Schwarzenegger, amepata kuwa Gavana wa Jimbo la California.

Je, ni kweli kwamba wasanii hao wote baada ya kuonyesha upande wao wa kisiasa, waliwagawa mashabiki, hawakubaliki na wamepoteza mvuto? Jibu ni hapana.



UKWELI NI HUU

Siasa ni maisha. Kupenda chama fulani au kuwa shabiki wa chama fulani ni haki ya kila binadamu. Jambo la msingi ni kuridhika na sera za chama husika. Sioni tatizo kwa Steve Nyerere kuwa CCM huku akiwa mchekeshaji. Hakuna dhambi kwa JB kuwa CCM wakati akifanya sinema zenye viwango.

Hakuna uhusiano wowote kati ya ubunge wa Sugu na muziki wake kama msanii. Kuwa mwanasiasa ni kuchagua kuwawakilisha wananchi. Hakuhusiani na sanaa.

Kinachopendwa na mashabiki ni namna msanii anavyofanya vizuri kwenye sanaa yake na siyo dini, itikadi ya chama wala jina lake.

Kama ingekuwa kuonyesha upande kisiasa ni kujiua kisanii bila shaka Diamond (CCM) angekuwa ameshapotea kwenye soko la muziki, lakini ndiyo kwanza anapeta na Marry You – kibao alichomshirikisha mkali wa sauti kutoka Marekani, Ne-YO.


TATIZO NI LILELILE

Kinachoitafuna Bongo Muvi ni kilekile. Ubunifu, skendo (kiki), kuvamiwa kwa sanaa na watu wasio wasanii na mengine kama hayo.

Kamwe Bongo Muvi haitarudi kwenye heshima yake ikiwa hadithi zitaendelea kuwa mbovu, wasanii hawatajitambua na kuwa na ushindani. Msijifiche kwenye hoja ya siasa.

Natamani enzi za Shakira, Sikitiko Langu, Born Again,  Oprah, Agano la Urithi, Misukosuko, Girlfriend, Simu ya Kifo, Odama na  Fungu la Kukosa.

Nimezikumbuka sana enzi za White Maria, Fake Pastors, Village Pastor, Hostel, Behind the Scene, Swahiba, Gentlemen na Red Valentine.

Rudini hapo. Acheni maneno, fanyeni kazi. Wapo wachache wanaojitahidi, lakini wengi wanaoharibu wanalididimiza soko la filamu nchini. Ni tamaa yangu siku moja muinuke tena.

Gwajima aendelea kumshambulia Makonda

0
0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai  kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema

Gwajima alisema  kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki  ni kifungo cha miaka mitatu.

Kosa jingine  alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye   na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

Gwajima Azidi Kumfukunyua Makonda,Ataja Makosa ya Kisheria Yaliyomfanya Akimbie Nchi na Adhabu Anazostaili Kupata...!!!,

0
0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.


Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.


“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema


Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.


Kosa jingine alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

Anahitaji Ushauri...Sina Raha Kinyesi Changu Kinatoa Harufu Mbaya Sana..!!!

0
0

Habari za jioni ndugu zangu kwa kwl mwenzenu naadhirika kutokana na harufu ninayoitoa nkienda haja kubwa ni mbya kupita maelezo hata nitumie manukato vipi badoo yani sina raha nkitoka chooni nakuta watu wametoka nje kupunga upepo pia nnakuwa na harufu mbya jaman mke mpk anataaka kurud kwao tatz nn wakuu maana sasa iv nakata gogo saa tisa kila mtu kalala

Kudadeki...Lema Amchokoza Tena Rais Magufuli,Amtaka Amtimue CCM Waziri Mkuu kwa kuwa na Yeye Aliimba Kuwa na Imani na Lowassa...!!!

0
0

Leo kulikuwa na Mkutano wa Mbunge wa Arusha Mjini Kamanda Godbless J. Lema Katika viwanja ya Tindigani vilivyopo kata ya kimandolu. mkutano huo umeudhuriwa na Maelfu ya wakazi wa Arusha na viunga vyake. majawapo lema alichokisema ni Mheshimiwa Rais kwenye ile video ya watu waliokuwa wanaimba wana imani na Lowassa nimemuona na Waziri Mkuu Majaliwa pia akiimba kwa nguvu zote, na yeye mlete huku kwetu"*

Unataka Kolabo na Diamond? Amesema Fanya Hivi...

0
0

Msanii Diamond Platnumz anasema toka ameanza kufanya muziki ameweza kufanya kazi na wasanii wengi lakini anadai ili akushirikishe kwenye wimbo wake lazima umuonyeshe uwezo wako na sababu za kuitaka kolabo yaje, hata kama upo chini ya uongozi wake haiwezi kuwa sababu yeye kukupa shavu.


Msanii Diamond Platnumz akiwa na RayVanny wakiwa kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' Diamond Platnumz alisema hayo kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kusema toka ameanza muziki wasanii ambao amewahi washirikishia kwenye nyimbo zake ni watatu, yupo Chid Benz, Maua, pamoja na RayVanny.

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana Asema Mabadiliko ya CCM Hayalengi Mtu

0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema mabadiliko ya ndani ya chama yanayofanyika hivi sasa hayalengi mtu wala kikundi bali yanalenga katika kukipa uhai, kuongeza ubora na ushindi.

Akizungumza katika mkutano mkuu maalum wa CCM, Kinana amesema kuna upotoshaji unafanyika kuwa mabadiliko yanayofanyika yanalenga mtu jambo ambalo si la kweli.

“Mabadiliko haya hayalengi mtu wala kikundi bali yanalenga katika kukipa uhai chama, ushindi na ubora,”amesema.

Amesema mabadiliko hayo ya kimuundo na kisera yapo tangu CCM imezaliwa miaka 40 iliyopita

Fahamu Maajabu ya Nywele Ambayo Ni Vigumu Kuyajua Katika Hali ya Kawaida..!!!

0
0

Maajabu haya ya nywele! Usipeleke mawazo yako kwenye yale majina yake kwamba zote ni nywele lakini zinatofautiana majina kutokana na mahali zilipo(ota)

Maajabu ya nywele ninayotaka kuzungumzia ni haya 

-akili hulinganishwa na nywele kwenye muktadha wa methali za kiswahili

-nywele hutumika kama malighafi bora kabisa kwenye ulimwengu wa giza 

-nywele huendelea kuota kwa muda fulani hata baada ya mwili kufa 

-nywele hubaki bila kuharibika hata baada ya mwili kuoza kabisa

-rohochafu mapepo hata baadhi ya majini hupenda kukaa kwenye nywele ndio maana baadhi ya vichaa wakinyolewa tu hupata nafuu

Kwa akina dada zangu unapovaa wigi halisi la nywele za mtu unabeba usisoyajua hasa kama mwenyewe keshatangulia kaburini

Kwa Niliyoyaona Wodi ya Wazazi ,Si Mtii Mimba Tena Mke Wangu..!!!

0
0

Aisee wakuu muwe mna waheshimu sana mama zenu kwa kweli ,kwa niliyoyaona wodi ya wazazi aiseee nimeathirika kisaikolojia sitamani tena kumtia mimba mke wangu nahisi kama atakufa kwa kweli.

Roho ilikuwa juu juu kipindi mke wangu anaenda kujifungua ,nilivyoingia wodi ya wazazi ndio kabisa nikaishiwa nguvu kwa kuwaonea huruma.

Jamani jamani wanawake wanateseka sana wakiwa wanajifungua yani nilihisi mke wangu hatoki akiwa hai lazima afe.

Kwa kweli hata nikipita mtaani minions mwanamke ana ujauzito natamani kulia kwa kumuonea huruma ,Sitamani kabisa kumpa mke wangu mimba kama kungekuwa na uwezekano wa kufunga kizazi kwa mwanaume ningeenda walai 

Maana wanawake wanapitia mateso makubwa sana.

Ushauri wenu wakuu niondokane na hii hali .

Hotuba Fupi ya Kitwete Yamuumbua Magufuli na Kinana: Ukata Ndio Umesababisha Mabadiliko Yaliyofanywa CCM..!!!

0
0

Ikikumbukwe wakati anamkabidhi mwenyekiti Magu, Kikwete aliitaja changamoto kubwa inayokikabili chama kuwa ni wanachama kutolipa ada.

Leo katika hotuba yake ameonekana kushangazwa na sababu walizotoa Mwenyekiti na Katibu wake Kinana na kuiacha sababu kubwa na ya msingi wa mabadiliko waliyopendekeza . Ndiyo maana mwanzo amesema "wamekuwa wastaarabu kidogo" !! wameacha sababu ya msingi ya Ukata katika chama.

Suluhisho walilochukua la kukabili tatizo hili na kujificha nyuma eti kuleta ufanisi, limeonekana kumkera Kikwete.

Badala ya kutafuta mbinu ya kuwashawishi wanachama kulipa Ada, wameamua kuwapiga panga wajumbe ili wabaki wachache watakaoweza kulipana posho. Badala ya kutafuta vyanzo vya mapato ili kuweza kugharimia mikutano wameamua kupunguza mikutano na kusema eti wanalenga ufanisi.

Mbinu hii inaonekana kutumiwa Sana na mtawala huyu katika utawala wake: tujiuliza ni wafanyakazi wangapi walikuwa hewa wameondolewa na wangapi walioajiriwa ili hewa isiwe hewa bali wafanyakazi halali.

Baada ya CCM Kutimua Makada Wake 12 Waliokuwa Wanaimba Kuwa na Imani na Lowassa,Lowassa Aibuka na Kuwakaribisha Ukawa...!!!!

0
0

Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.


Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema

Jifunze Njia Sahihi ya Kutengeneza Jiuce ya Embe Iwe Kama ya Bakhresa..!!!!

0
0

Mahitaji
1. Maembe
2.sukari
3. Tangawizi
5. Iriki

HATUA

1. Chemsha maji ya kutosha mf lita 2 hadi 5 kulingana na wingi wa matunda

2.chukua matunda yako na uyaoshe vizuri kwa kutumia maji ya vuguvugu yaliyowekwa chumvi kiasi ili kuua vijidudu

3. Menya matunda yako taratiibuuu bila kujikata vidole

4.katakata matunda katika vipande vidogo vidogo ili kuiwezesha blender yako kusaga matunda kwa urahisi.

5.chukua matunda, iriki na tangawizi kisha weka ktk brenda na anza kusaga kwa kasi uipendayo. Unaweza kuongeza maji yaliyochemshwa wakati wa kusaga ili kupata mchanganyiko wa wastani usio mzito sana.

6. Chukua maji yaliyochemshwa changanya na rojo la matunda kwa kiasi kulingana na wingi wa matunda kisha koroga.

7. Chukua chujio safi na chuja mchanganyiko wako huo. 

8. Chukua sukari na uitie katika mchanganyiko wako. Kisha koroga hadi sukari yote iyayuke.

9. Chukua chombo safi maalum kwa kuwekea juice na anza kuitia juice ktk vyombo hivyo mf. Chupa za plastiki

10. Weka juice yako katika friji. Unaweza kunywa juice yako na vitafunwa mbalimbali unavyopenda

Kinana Amjibu Kikwete Juu ya Mabadiliko ya CCM..!!!

0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ndugu Abdurhaman Kinana amesema mabadiliko wanayoyafanya ndani ya chama hicho yatakuwa yanagusa sehemu muhimu kama Katiba ndani ya CCM, kanuni za uchaguzi pamoja na kanuni za Jumuiya.

Hayo aliyabaanisha katika mkutano Maalum wa mabadiliko uliofanyikia Jijini Dodoma, huku akibainisha baadhi ya vitu na kusema mageuzi hayo hayamlengi mtu wala kikundi chochote bali yanalenga kutoa ufanisi ndani ya chama hicho.

“CCM imekuwa na utamaduni wa mabadilko na imeshafanya hivyo mara 15 na awamu hii ni mara ya 16 sasa dhamira ikiwa ni kuweka uhai, ubora na ushindi wa CCM”. Alisema Kinana

Aidha Katibu huyo ametaja mabadiliko waliyoyakusudia kuyafanya kuwa ni kupunguza utitiri wa vyeo, idadi ya vikao viwe vichache ambavyo vitakuwa na tija kwao pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe.

Kwa upande mwingine Kinana amefananisha mabadiliko hayo na vyama vingine vikongwe duniani ikiwemo chama cha Kikomunist cha China ambacho wanachama wengi lakini idadi ya wajumbe wa mikutano yao wakiwa wachache pamoja na chama cha African National Congress (ANC) cha nchini Afrika ya Kusini.

Ikumbukwe Jana Wakati Alipopewa nafasi ya kusalimia Mhe Kikwete Alionyesha Wasiwasi wake juu ya mabadiliko yaliyofanywa na chama hiko ambapo alidai kupunguza wajumbe kutoka 388 hadi 163 ni panga kali kuliko kawaida.

Magufuli Amtunuku Kikwete Ukumbi wa CCM...!!!

0
0

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wamekubaliana kuita ukumbi mpya uliopo eneo la Dodoma Makulu ‘Kikwete Hall’.

Makubaliano hayo yametokana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Dk John Magufuli kupendekeza kwa wajumbe hao ukumbi huo uitwe Kikwete.

“Leo tumekaa katika ukumbi huu mzuri kuna watu wamefanya kazi na miongoni mwao atakuwa ni Mzee wetu Jakaya Kikwete (Rais Mstaafu wa awamu ya nne). Mtakumbuka kabla ya hapa tulikuwa tukikaa kule yanatolewa magunia tunakaa,”amesema.

Wajumbe hao walikubaliana na wazo hilo na baadaye Rais Magufuli walishikana mkono na Rais Kikwete.

Wajanja wa Mjini Wamliza Mhe Temba Mamilioni ya Pesa Mchana Kweupe...!!!

0
0

Msanii Temba kutoka TMK Wanaume amefunguka na kuweza wazi kuwa alikwama katika muziki na kushindwa kuachia kazi zake mwenyewe baada ya kutapeliwa pesa zake na mtu ambaye alikuwa akifanya naye biashara za magari.

Mh. Temba alisema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live  na kudai kuwa alimuamini sana Mustafa lakini hakujua kuwa alikuwa anatengenezwa ili aje kupigwa pesa zake.

Wafanyabiashara Wasalimisha Vroba vya 140 Mlioni..!!!

0
0

Wafanyabiashara 13 wa Wilaya za Babati na Hanang’ Mkoani Manyara, wamesalimisha katoni 1,540 za pombe zilizofungashwa kwenye karatasi (viroba) zenye thamani ya sh140 milioni.

Wafanyabiashara hao walisalimisha katoni hizo za pombe za viroba kabla ya upekuzi ulioendeshwa na polisi, maofisa wa usalama wa Taifa, chakula na dawa (TFDA) na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

Akizungumza jana na waandishi wa habari, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Francis Massawe alisema wafanyabiashara hao walisalimisha wenyewe viroba hivyo bila kushurutishwa.


Kamanda Massawe alisema katika wilaya ya Hanang’ zilisalimishwa katoni 871 na kwa wilaya ya Babati zilisalimishwa katoni 669 na wafanyabiashara hao wanaopaswa kupongezwa kwa hatua hiyo.

Alichokisema Wabogojo Baada ya Kuoa ...!!!!

0
0

Mchekeshaji ambaye aliwahi kujizolea umaarufu mkubwa kwa kucheza kwenye nyimbo za msanii Mr. Nice enzi hizo Wabogojo jana ameuaga ukapela kwa kuvuta jiko ndani na kuachana na maisha ya u bachelor.

Wabogojo ambaye muda mwingi sasa amekuwa nje ya nchi baada ya kufanikiwa kufunga ndoa aliweza kuwashukuru ndugu jamaa na marafiki kwa kuweza kumpa support katika jambo hilo ambalo ni muhimu katika maisha yake. 

"Hatimaye ni mume na mke. Ahsante Mungu nimebarikiwa kwa jambo hili, familia yangu kwa ujumla sina cha kulipa kwa upendo wenu kwangu kwa jinsi mlivyoweza kuniunga mkono katika jambo hili, nawapenda sana wote marafiki, ndugu, wafanyakazi wenzangu, nashukuruni sana. Nashukuru sana mke wangu kwa kunikubali katika maisha yako kwa hivi nilivyo, nakupenda sana na upendo wangu kwako hauna mwisho" alisema Wabogojo 

Makonda Kwisha Habari Yake,Spika Ndugai Abaiki Kikaango Chake Bungeni..Hbari Vichwa Vya Magazeti ya Leo 13/3/2017..!!!!

Noma Sana ..Ujerumani Yaomba Msaada Tanzania...!!!

0
0

Ujerumani imeiomba Tanzania kuiunga mkono katika harakati zake za kutafuta nafasi katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa uchaguzi utakaofanyika mapema mwaka 2018.

Ujumbe wa Ujerumani umewasilishwa Tanzania na mjumbe maalum wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa Rais Dkt John Magufuli na balozi Harro Adt,na kusema nchi yake inaomba nafasi hiyo huku ikiwa na agenda nne muhimu.

Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo maalum kutoka Ujerumani kwa Niaba ya Rais Dkt John Magufuli,Waziri wa mashauri ya kigeni wa Tanzania Dkt Agustine mahiga amesema wanatambau mchango wa Ujerumani kwa taifa na afrika kwa Afrika kwa ujumla.

Katika kutafuta nafasi hiyo katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa nchi tatu zitakuwa zikiwania nafasi moja huku Isarel na Ujerumani zikipigiwa upatu zaidi.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images