Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

BREAKING NEWS:AZAM WAFANIKIWA KUMSAJILI MCHEZAJI HATARI WA YANGA

$
0
0
Klabu ya Azam FC imeanza rasmi maandalizi ya kutetea ubingwa wao msimu ujao na michuano ya kimataifa kwa kukamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Yanga.
Taarifa rasmi zilizothibitishwa na meneja wa Azam FC Jemedari Said ni kwamba mshambuliaji Didier Kavumbagu amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
“Ni kweli Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini mkataba wa mwaka mmoja. Taarifa zaidi zitatolewa baadae.” Alikaririwa Jemedari.
Kavumbagu alitua nchini Tanzania akitokea Burundi alipokuwa anaitumikia Vital O na kuja kujiunga na Yanga misimu miwili iliyopita.

NEY WA MITEGO AJITOKEZA NA KUJIBU SHUTUMA ZA KUMTEKA MSICHANA

$
0
0
April 14 zilizotoka taarifa juu ya kutekwa kwa msichana mmoja aitwae Neema ambaye ni miongoni mwa watu wanaosemekana walimtukana Ney na Mpenzi wake kupitia akaunti zao za Instagram,Neema alipatikana na kuzungumzia hii bahati mbaya Ney hakuwa nchini aliporudi Soud Brown kaongea nae na hiki ndicho alichokisema.

Bonyeza play kusikiliza.

MKE WANGU ANANIZIDI AKILI NA MBINU..KUTWA NZIMA NA SIMU, YUPO KILA SOCIAL NETWORK

$
0
0
Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo. 

Mke wangu sasa ananizidi akili na mbinu. 

Nilimnunulia smartphone ya bei kama laki 7 aina ya Samsung, yapata miezi minne sasa tangu awe nayo. 

Kinachoniumiza sasa hivi kazi zote ni mschana wa kazi.

Yeye hapiki, hapigi deki na hafui, muda wote yuko bize na simu yake. 

Pia amejiunga social networks zote kama twitter, badoo, facebook, whatsapp, tango, we chat na instagram na nikitaka kupigana naye basi nimuombe pasword zake, hapo yupo tayari kurusha ngumi. 

Usiku analala saa saba na akichelewa ni saa 6 usiku.

Yupo bize. nampenda sana na nahofia kumpoteza. Jamani nifanyeje? Vita nyingne ni pale anapoishiwa pesa ya bando, yani anadai pesa ya vocha kwa lazima mpaka nitaitoa. 

Mitandao yote aweweka profile picture nzuri na tena Mungu alimjalia uzuri kama kabla lake Wairaq (wambulu) walivyo.

Anapotaka kubadilisha profile picture hapo ndo naumiaga zaid sababu anajimek up na kutoa nguo zaidi ya 5 na anavaa moja moja huku msichana wa kazi anampiga picha tofauti tofauti na yeye huangalia ile aliyopendeza.

AINA SITA ZA VITAMBI...JE WEWE CHAKO NI KIPI KATI YA HIVI?

$
0
0
1. Kitambi Mvurugo -- hiki kitambi kimekaa kama O.
Kinapatikana kwa kula sana kitimoto.

2. Kitambi Mchuchumio -- hiki kitambi kimekaa kama
herufi D. Kinatokana na kula sana michemsho na bia za
ofa.

3. Kitambi Mbonyeo -- Akivua shati kitovu hakionekani.
Hiki wanacho wala rushwa. Ila akisimamishwa kazi
kinaisha.

4. Kitambi Mtepeto -- Ni kitambi cha wastani ambacho
ukivaa nguo pana
hakionekani. kinasababishwa na kula mno viporo.

5. Kitambi Mfumanio: hiki mtu anakuwa hana pesa ila
kitambi ni kutokana na minyoo na utapiamlo wa ukubwani.

6. Kitambi Mtunguo: Hiki wanacho sana wadada. Kina
umbo la yai. Hiki kwa 'diet' hakitoki labda Kwa Maombi tu.

HUYU NDO MBOWE KAJA NA PLAN B NA DAIMA HATABIRIKI

$
0
0
Katika kikao kimoja tulichofanyia Mwanza mwaka jana mwishoni Mbowe aliwakuna wajumbe alipotupa siri kwamba alikataa kuwa mwenye kiti wa Chadema mpaka kamati kuu walipokubali mashariti yake. Baadhi ya mashariti ilikuwa kumuomba na kamati kuu ikubali Dr Slaa awe Katibu mkuu badala ya makamu mwenyekiti, kuruhusu kufungua milango ili aingize watu toka vyama vingine na kubadilisha rangi za bendera ya chama. Alitwambia jisi alivyopata shida kuwashawishi wazee wa chama kukubali kombati kuwa vazi la chama na kadhalika. Ilikuwa story ya kuvutia sana!

Leo wakati Ccm wakidhani tuna tofauti kubwa sana na vyama vingine hasa Cuf, na walijitahidi sana kupanda chuki kati yetu. Na zaidi walijitahidi kuivuruga Chadema kwa kutumia mamluki, kumbe Kamanda wa anga anafkiria kitu kikubwa zaidi. Ametoka na plan B amabayo inawafanya Ccm warudi kwenye drawing board kupanga upya mbinu tofauti na hii ya mamluki. Kwa vyovyote sasa mbinu ni kuchonganisha huu muungano maana hauwezi kuwaacha salama.

Mchambuzi yoyote wa siasa anajua kwamba tukiingia kwenye uchaguzi kwa muungano huu Ccm watatoka jasho kweli kweli. Muungano huu utasambaratisha kabisa propaganda ya udini na ukabila, utasambaratisha propaganda ya uchu wa madaraka. Lakini italigawa taifa katika kanda ambazo ni rahisi kupiga kampeini kulingana na sehemu vyama vinavyokubalika. Itapunguza mzigo wa gharama maana utashughulikia eneo dogo kwa ufanisi.

Long live Kamanda Mbowe!

MCHEZAJI WA BARCELONA ARUSHIWA NDIZI UWANJANI..AIKOTA NA KUILA..WATU WAMPONGEZA

$
0
0
Barcelona star Dani Alves responded to a racist taunt in the most incredible way during a match yesterday Sunday April 27th

While playing for his team against Villareal, a spectator threw a banana at him as he tried to take a corner kick. What do you think Dani did? He casually picked up the banana, peeled it, eat the banana, threw away the peel, and then completed the kick...

This move has left many people in shock and Dani is getting a lot of praise for how he handled it.

This is not the first time the Brazilian footballer will face racism on the pitch. He complained about it last year after being taunted by monkey chants from sections of the crowd during a match at Real Madrid.

Racism in football is becoming an issue in Europe and enough is not being done to stop it. Dani is a star! Hopefully, he made the person who threw the banana feel like stupid!

TAZAMA HII PICHA YA RAIS KENYATTA AKIWA AMECHACHAWA NA KALIOZ LA ASKARI

$
0
0
Mtu Mzima ni kama aamini anacho kiona....."Aisee huyu mleteni awe board guard wangu ...Life is Good.....hahah

WARIOBA AWATAJA WASALITI WA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wanasiasa wanaomtuhumu kwa kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Muungano, ndiyo wasaliti kwa kuwa waliingiza kwenye Katiba, mambo yanayokinzana na makubaliano ya Muungano huo.

Jaji Warioba amesema usaliti huo ni pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuondoa mamlaka ya Bunge la Muungano katika utungaji wa sheria, kuitambua Zanzibar kuwa nchi inayojitegemea na kuongeza mambo ya Muungano bila kufuata Katiba.

Ametoa kauli hiyo kujibu mwendelezo wa lugha za kejeli na matusi anazorushiwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wengi kutoka CCM na baadhi ya viongozi wa Serikali baada ya Tume aliyoiongoza kupendekeza muundo wa serikali tatu.

Akizungumza juzi usiku katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Jaji Warioba alisema viongozi wa pande mbili za Muungano wanaomtuhumu, ndiyo waliouvuruga Muungano huo

“Mwalimu aliacha Bunge likiwa na mamlaka kamili, aliacha nchi ni moja, aliacha mambo ya Muungano 11 sasa yamekuwa ni 22, kwa bahati nzuri Rais Jakaya Kikwete alieleza bungeni hilo kwamba mambo hayo yaliongezekaje,” alisema na kuongeza:

“Katika kubaini kuongezeka kwa mambo ya Muungano ndivyo ilikuwa inapunguza mamlaka kwa Zanzibar, mambo 11 yaliyoachwa na mwalimu yaliingizwa kikatiba lakini haya yaliyoongezeka yalipatikana kienyeji.”

Jaji Warioba alisema enzi za uhai wake, Mwalimu Nyerere aliheshimu na kuilinda Katiba hivyo, walioivunja ndiyo wasaliti wa Muungano.

“Sasa kati ya mimi na wao ni nani msaliti kwa Mwalimu, angekuwapo (Mwalimu) ni yupi angeonekana msaliti wa Serikali ya Muungano? Wao ndiyo wameuvuruga, alichokiacha Mwalimu ni tofauti na kinachoonekana kwa sasa,” alisema Jaji Warioba.

Kuhusu Bunge

Jaji Warioba alisema mipango mingi ya maendeleo inayopangwa ndani ya Bunge la Muungano inatekelezwa upande wa Bara pekee.

“Si hivyo tu, Bunge hilo linajadili mambo ya Bara tu na halihusishi upande wa Zanzibar. Zanzibar nayo inajadili mambo yake na kujiamulia lakini jina la Bunge hilo ni Muungano,” alisema Jaji Warioba.

Kutokana na mazingira hayo, Jaji Warioba alisema Zanzibar iliamua kuondoa mamlaka ya Bunge hilo katika utungaji wa sheria kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema sheria zinazotungwa katika Bunge hilo zitatumika ndani ya pande zote za Muungano, lakini Zanzibar wakabadilisha hilo kupitia Katiba yao wakasema sheria zote zitakazotungwa ndani ya Bunge hilo, lazima zipitiwe tena na Baraza la Wawakilishi,” na kuongeza: “(Zanzibar) Hawakuishia hapo, wakafanya mabadiliko ya Katiba mwaka 2010 iliyovunja Katiba ikiitambua Zanzibar kama nchi kamili, ikaondoa mamlaka ya Rais wa Jamhuri kugawa wilaya na mikoa kwa Zanzibar tofauti na Katiba ya Muungano, kwa maana hiyo Zanzibar ikavunja nguvu ya Bunge la Muungano.”

Aidha, alisema hatua hiyo ilionekana kuuvunja Muungano kwa vitendo baada ya kuvunja mamlaka ya Rais na kutambua marais kamili katika nchi mbili tofauti.

“Kwa kawaida nchi inakuwa na amri jeshi mkuu mmoja ambaye anapigiwa mizinga 21, Jeshi la Muungano linapiga mizinga kwa marais wawili kitu ambacho hakiwezekani,” alisema.

Malalamiko ya Watanganyika

Jaji Warioba alisema Kwa upande wa Tanzania Bara, walibaini malalamiko ya Watanganyika kuwa ni pamoja na kukosa fursa mbalimbali ndani ya Zanzibar. “Watu wa bara nao wanasema Zanzibar inashiriki Bunge la Muungano, inakagua miradi ya bara na kuihoji lakini wao hawana nguvu ya kushiriki mambo hayo kwa upande wa Zanzibar,” alisema.

Aliongeza: “Mbaya zaidi wanasema Wazanzibari wanaweza kumiliki ardhi na kupata uraia kwa upande wa bara lakini haki hizo haziwezi kupatikana kwa Mtanganyika, njia pekee tukaona ni vyema Zanzibar nayo ilete mambo yake ndani ya Muungano lakini ikashindikana.”

Hoja ya takwimu

Jaji Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge wasihangaike na takwimu badala yake wajibu maswali yaliyojitokeza kutoka kwa washirika wa Muungano.

“Takwimu siyo tatizo, sisi hatukufanya jambo jipya, ila ilikuwa ni kama marudio tu ya Tume ya Nyalali, wanahoji takwimu hizo je, hawakuona dosari kwa takwimu za maoni ya asilimia 20 kwa jaji Nyalali?

Alisema Tume yake ilizunguka nchi nzima ikiwa na waandishi waliorekodi kwa tepu, video na maandishi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika mtandao wa Tume.

UKAWA RUKSA KUFANYA MKUTANO ZANZIBAR LEO

$
0
0
Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.

Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.

“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.

Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.

“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:

“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.

Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.

BASI LAUWA WATU 18 WALIOKUWA WAKIMSITIRI MAREHEMU KANDO YA BARABARA

$
0
0
WATU 18 wamekufa papo hapo wakiwemo askari Polisi wanne katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Utaho, kilometa 20 nje ya Mji wa Singida katika Barabara Kuu ya Singida Dodoma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Geofrey Kamwela, alisema jana kuwa mbali na askari hao, wengine waliokufa papo hapo ni viongozi watatu wa kijiji hicho na wananchi wanaowaongoza na wengine wanne ambao hawajatambulika. 

Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, askari waliokufa katika ajali hiyo ni Koplo Boniface Magubika, PC Jumanne Mwakihaba, PC Novatus Tarimo na PC Michael Mwakihaba na wote wanatoka katika kituo kimoja cha kazi.

Viongozi wa Kitongoji na Kijiji cha Utaho waliokufa ni Ramadhan Mjengi, ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Paul Hamis, ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji na Ernest Salanga ambaye ni Mwenyekiti Kitongoji.

Wananchi wanaowaongoza katika kijiji hicho waliokufa ni Saidi Rajabu, Ushirika Itambu, Chima Mughenyi, Salim Juma, Abeid Ramadhan, Mwinyi Hamis na Issaha Hussein.

Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, miili ya watu wengine wanne haikuwa rahisi kutambulika mara moja na wote wamehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa mjini Singida.

Kamanda Kamwela alisema ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria lenye usajili namba T.799 BET aina ya Nissan, mali ya Kampuni hiyo ya Sumry, inayomilikiwa na Mohamed Abdallah wa Sumbawanga, lililokuwa likienda jijini Dar es Salaam likitokea Kigoma.

Alisema kuwa basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Paul Njilo, mkazi wa Dar es Salaam, liliwagonga waenda kwa miguu hao waliokuwa wamekusanyika kando ya barabara wakisaidiana na askari Polisi kuondoa mwili wa marehemu Gerald Zephania, aliyekuwa amegongwa na lori lisilofahamika juzi saa moja usiku.

Katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, watu wengine wanane walijeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Misheni Puma ya mjini Singida.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kilichosababisha ajali hiyo huenda ni kuegeshwa vibaya kwa gari la Polisi, wakati likipakia mwili wa marehemu Gerald, aliyekuwa amegongwa na lori mapema kabla ya basi hilo kufika hapo. Inadaiwa gari la Polisi liliziba barabara.

Akizungumzia ajali hiyo katika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam jana, Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alitoa pole kwa wananchi wote waliofiwa na ndugu zao na kuwaombea majeruhi kupona haraka.

Alisema Askari wa Usalama Barabarani hawatakuwa na muhali na dereva yeyote atakayekwenda kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani. Kutokana na hilo, ametoa mwito kwa madereva kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarni, ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

“Polisi iko imara kuchukua hatua zozote za kisheria, kwani kuna baadhi ya watoa huduma wa usafiri hugoma pale wanapotaka kuchukuliwa hatua kwa sababu mbalimbali matokeo yake ni uvunjaji wa sheria kwa makusudi,” alisema.

Alisema Jeshi la Polisi limeanzisha msako mkali wa dereva wa basi hilo ambaye alitoroka ili kufikishwa mahakamani, na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wa aina yeyote ile, ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Imeandikwa na Abby Nkungu, Singida na Theopista Nsanzugwanko, Dar

TUCTA WAPIGANIA PAYE ISHUKE KWA WAFANYAKAZI

$
0
0
  SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeazimia kuendelea kupigania kushushwa kwa Kodi ya Mshahara (PAYE) kutoka asilimia 13 inayokatwa hivi sasa hadi asilimia tisa, ili mfanyakazi apate ahueni ya maisha.

Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Mei Mosi yatakayoambatana na wiki ya wafanyakazi itakayoanza rasmi leo.

Maadhimisho ya Mei Mosi yatafanyika nchini kesho kutwa ambapo kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Mgaya alisema mbali na kupunguzwa kwa kodi, Tucta inayo mambo mengine mawili inayopanga kupigania ili ujumbe ufike serikalini na kupatiwa suluhu.

Suala la pili alitaja kuwa ni kila mfanyakazi kupatiwa malipo mazuri awapo kazini, jambo alilosema wamekuwa wakiliomba mara kwa mara na hadi sasa halijakamilika.

“Kila mfanyakazi ni mstaafu mtarajiwa, hivyo ni vyema waajiri waandaliwe malipo mazuri, ili mfanyakazi atakapostaafu awe na kiwango cha maisha kitakachomsaidia katika maisha yake,” alisema Mgaya.

Pia wamejipanga kupigania mifuko ya pensheni, ilipe kiwango sawa cha kiinua mgongo tofauti na sasa ambapo baadhi ya mifuko inalipa kiwango kidogo na mingine inalipa kiwango kikubwa.

“Ifikie wakati sasa kusiwepo na utitiri wa mifuko, bali ivunjwe na kubaki miwili yaani wa binafsi na wa umma ambayo mengine yanabakia yakijitangaza tu,” alisema Mgaya.

Mgaya alilitaja jambo lingine kuwa ni fidia kwa wafanyakazi ambapo alishauri kuundwe kwa mfuko ambao utawezesha mfanyakazi atakayeumia kazini, kulipwa fidia ambayo itamsaidia.

Kuhusu mabadiliko ambayo yametokea tangu maadhimisho yaliyopita ya Mei Mosi, Mgaya alisema ni kupungua kwa kodi kutoka asilima 14 kwenda 13 ambayo alisisitiza kwamba wafanyakazi wanaomba sasa ifikie asilimia tisa.

Gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka na Naibu wake, Makongoro Mahanga, wazungumzie mpango huo wa Tucta, lakini simu zao ziliita bila majibu.

MR BLUE: WEMA, NAJMA WALINIFILISI

$
0
0
Na Gabriel Ng'osha

NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.

“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.

“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.

Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.

Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.

Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.
GPL

SAMWELI ETOO "SAMAHANI KUNA YOYOTE ANAYETAKA KUWA NYANI KAMA MIMI"

$
0
0
Unaambiwa club ya Villareal imemfungia maisha yule shabiki ambae alionyesha kitendo cha kibaguzi kwa kumrushia ndizi Dani Alves, kitendo ambacho kilitafsiriwa kwa Alves kufananishwa na nyani.
Wachezaji kadhaa wamemsupport kwa ujasiri wake wa haraka na kula ndizi hiyo aliyotupiwa uwanjani alafu akaendelea na game kama kawaida ambapo miongoni mwa waliomsupport ni Neymar.
Mwingine alieonyesha support ni Samuel Eto’o ambae baada ya kuweka picha zake mbili akiwa kwenye magari yake ya kifahari na kuandika ‘samahani nilisahau kuuliza, kuna yeyote anataka kuwa nyani kama mimi?’


SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA STEVE RNB

$
0
0
Mkali toka Tanzania ambaye yupo kwenye list ya Wanamuziki wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Rnb,Watanzania wengi tulimtambua Steve Rnb baada ya kushirikishwa na Mr. Blue kwenye wimbo wa Tabasamu,huu ni wimbo wake mwingine mpya unaitwa She dance,usikilize halafu unaweza andika ulichokisikia juu ya wimbo huu ili baadae nae akipita asome.
Bonyeza play kusikiliza.

JINI KABULA "JINI SIZAI TENA NJE YA NDOA"

$
0
0
MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa hayupo tayari kuzaa tena nje ya ndoa mpaka atakapoolewa.

Akistorisha na paparazi wetu, Jini Kabula alisema hawezi kurudia tena jambo hilo kwani anaogopa kuchanganya damu kwa vile baadaye watoto wanaweza kuja kugombana na kukosa maelewano hivyo anamuomba Mungu atimize ahadi ya kuolewa ndipo azae.

“Nilizaa na Chuz kwa sababu tulikubaliana kuzaa tu na siyo kuoana hivyo kwa sasa nasubiri niingie kwenye ndoa ndipo nizae, sitaki kuwachanganya watoto wangu,”alisema Jini Kabula.

VIDEO IKIONYESHA JINSI BASI LA HOOD LILIVYOKUWA LIKIUNGUA MOTO

$
0
0
Habari za basi la Hood kuteketea kwa moto likitokea Mbeya njiani kuelekea Arusha zimetoka na kusambaa sana April 29 2014 jioni na hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini watu wanaofikia 40 wamejeruhiwa huku 55 wakinusurika kifo.
Hii ni video ikionyesha jinsi basi hilo likiteketea kwa moto Chalinze Pwani.

PICHA:BABY SHOWER YA SHAMIM ZEZE AKA MRS CHONCHI

$
0
0
Haya ndio Yanayojiri mida hii pande za Jiji La Dar Es Salaam, ni ile baby shower ya Blogger Maarufu Shamim Zeze aka Mrs Chonchi, aka Mama wa B2A, aka Mama wa 8020 Fashion,Naona akiwa na Marafiki zake wakaribu Wakipata "Selfie" Kidogo...

AMAZING:DAVIDO, SAMWELI ETO'O, ADEBAYOR NA BALOTELI NAO WAPOST PICHA WAKILA NDIZI

$
0
0

Amazing: Davido, Samuel Eto’o, Adebayor, Balotelli Post Banana Photos In Support

This awesome, this is amazing and breathtaking…. When I personally watched that video I was really touched…
Dani Alves ate the banana that was thrown at him, he started a revolution. Right now, it’s taken over the

social media.

The racist incident happened during Barcelona’s match against Villarreal on Sunday, when a banana was thrown onto the pitch towards Dani Alves as he went to take a corner. Everyone was amazed as Dani picked it up, peeled it back and ate it. And since then, he has been receiving massive support against racism.

Speaking after the match Alves said:

“We have suffered this in Spain for some time, you have to take it with a dose of humour. We aren’t going to change things easily. If you don’t give it importance, they don’t achieve their objective. I don’t know who it was, but thanks to whoever threw the banana, the potassium gave me the energy for the two crosses which led to a goal.”

The banana thrower has been identified and banned for life from games at the El Madrigal Stadium. The banana campaign for Alves has also gone viral. With even Davido sharing his own photo.. This is a nice move from Spanish F.A.. You wouldn’t want to try it in Nigeria, you will be beaten to stupor before banning of life..

SHILOLE AAMUA KUJISIFIA KATIKA MITANDAO"SIJAWAHI KUACHWA MIMI NDIO NAACHA"

$
0
0
STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa katika uhusiano wa kimapenzi hajawahi kuachwa bali huwa anaacha mwenyewe. 



Akistorisha na mwanahabari wetu, Shilole alisema tangu aanze kuwa na uhusiano, amekuwa bingwa wa kupiga ‘vibuti’ wanaume ambao hawaeleweki.


“Ukweli sijui nina nini ila naamini Mungu amenipa kitu cha pekee kwa sababu naweza kumuacha mwanaume kwa kumtukana lakini akataka kurudi, sijawahi kuachwa,” alisema Shilol

SHEIKH PONDA KUSOTA RUMANDE

$
0
0
Kesi inayomkabili kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda imeendelea kupigwa kalenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro.

Ilielezwa mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo haiwezi kusikilizwa kwa sasa kwa kuwa jalada lake bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali ya iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, kutoa maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka jana katika eneo la Uwanja wa Ndege Manispaa ya Morogoro.

Baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mary Moyo alisema kesi hiyo itaendelea kutajwa mpaka jalada hilo lililoitishwa Mahakama Kuu Oktoba 15 litakaporudishwa Mahakama ya Morogoro.

Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo jana chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na sihala za moto, mabomu ya machozi na mbwa huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzito wa mahakama hiyo.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Lilian Lutabula aliyeshirikiana na mwendesha mashtaka wa polisi, Zabron Msusi wakati upande wa utetezi uliwakilishwa na wakili Josephine Jackson kwa niaba ya wakili Bathoromeo Tarimu anayemtetea Sheikh Ponda.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ponda alirudishwa rumande ambako ataendelea kupafanya kuwa maskani yake hadi Mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea kutajwa mahakamani hapo.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images