Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Wajanja Hatulindi Demu, Bali Tunafanya Hivi..!!!!

$
0
0

Mpe Mpenzi wako sababu ya yeye kujilinda akiwa mwenyewe hata kama haupo...Usitumie Nguvu na
Ubabe kumlinda kama hana sababu ya yeye kujilinda mwenyewe.

Mpende na ajue anapendwa ili asiwe na sababu ya kuuchakachua upendo unaompa maana unamtosha kumlinda dhidi ya maupendo feki ya mtaani. Sasa wewe badala ya ku-invest muda wako kumpa Upendo wa kutosha, umejigeuza Alarm, kwamba unaweza kumlinda asiibiwe au asikusaliti...

Unapoteza muda kumfuatilia anaenda wapi, na nani, na kwa nini hajaaga,unamfuatilia nani kamtumia meseji na nani anaongea nae kwa simu mpaka unaenda kuprint statement kwenye mtandao anaotumia... Unapoteza muda wako Kama hujawahi kumiliki hata Shina la Mgomba utawezaje kumiliki mtu??? 

Mpenzi halindwi kama alarm, watu watai-Snooze na watamuiba kama kawa,Mpe sababu za kujiona anapendwa ili ajilinde mwenyewe. Kumlinda Mpenzi ni sawa na kulinda Bahari,wewe unalinda Coco Beach wenzio wanavua samaki Bagamoyo

Mambo Matano ya Kujifunza Kuhusu Mapenzi Kupitia Move ya TITANIC...!!!!

$
0
0

'Titanic is sinking' Ilikuwa ni title ya kitabu tulichosoma form one mwishoni mwa miaka ya 80...hadithi ya kweli yenye mafunzo mengi baadae ilikuja kutengenezwa sinema iliyojivunia umaarufu mkubwa duniani, sinema ya TITANIC  ndani ya ile sinema iliyobeba hisia nyingi za mapenzi usaliti ubabe na dharau kuna mafunzo na darasa kubwa tuliloachiwa

√KUKOSA UMAKINI

Nahodha mahiri akiwa anaongoza meli kubwa duniani isiyozama, ananasa tukio la DiCaprio na mpenzi wake wakiwa kwenye pozi la mahaba mazito.. Badala ya kuangalia kazi yako anajisahau kabisa na kukodoa macho ya utamanifu

√DHARAU

Nahodha kuja kushtuka naona kitu Kama Kichuguu cha barafu lakini anadharau akidhani kile ni Kichuguu kidogo na si mwamba mkubwa...kwakuwa tu TITANIC IS UNSINKABLE...!!!

√USALITI 

yule binti baada ya kulazimishwa kuolewa na tajiri mwenye kila kitu alikuja kusaliti ndoa yake kwa kijana mdogo kapuku 

√UBABE NA PESA SI KILA KITU MAISHANI

tajiri yule aliamini kuwa kwa pesa yake angeweza kupendwa na yoyote.... Lakini matokeo tuliyaona. Mapenzi ya kweli hayachagui 

√UPWEKE NA KUHUKUMIWA NA ROHO

yule binti alikuja kuishi mpweke Mpaka anakufa miaka michache iliyopita..true love happens once in the life time

Kuna mengi yaliyo hai ya kujifunza hata katika maisha yetu ya leo hii.... Yaliyojiri wiki nzima iliyopita na hitimisho lake pale ubungo leo havitofautiani sana na habari ya Titanic 

Tuliokuwa tunadhani kile ni kisiki tulikosea sana.... Kumbe ule ni mwamba mkubwa na kwa dharau zetu na kiburi kilichopitiliza our TITANIC IS SINKING... =======

Naomba Kuongea na Wadogo Zangu wa Kiume 18-30 Years...!!!

$
0
0

Utu uzima dawa! Mnakopita sasa sisi tulishapita salama, lakini kuna uhitaji wa kukumbushana machache, kupeana mbinu na kutiana moyo pia (hapa kwa sehemu hata wadogo zangu wa kike watahusika). Naongelea mabadiliko ya makuzi kihomoni, kimtazamo, kimahusiano na kifikra pia. 

Niwapongeze pia wengi wenu kwa kuwa wawazi kwa yale mnayopitia, wengi wenu hamfahamu kuwa ni sehemu ya makuzi hivyo kujaa hofu na woga mwingi hasa kwenye maeneo haya;

1. Haiba - hapa kila mmoja anajitahidi awezavyo ili aonekane wa kisasa kwa mavazi lugha na hata mikogo mingineyo, kukosa baadhi ya hivyo vitu husababisha maumivu makubwa sana bila kutambua kuwa wakati wako wa kupata bado

2. Ukakamavu/confidence ya kuongea na hadhira au jinsia tofauti, hapa ni kimbembe, wengi hujichukia na kujistukia na hivyo kusababisha kujitenga na jamii muda mwingi kwa kudhani wengine wanajiona bora au ni mahiri kuliko wao! Hiki ni kipindi tu na kitapita lakini siri ya kuongea na hadhira ni kutowaangalia watu machoni bali kuwaangalia juu ya macho yao kwenye paji la uso.

3. Mahusiano kipengele hiki ni muhimu sana na hapa namaanisha kwenye ishu nzima ya kufanya mapenzi. Asikudanganye mtu, mapenzi utayajua baada ya kuvuka miaka 30, hapo utakuwa umewazoea na kuwafahamu wanawake na utakuwa huna hofu tena. wengi sana hapa wanalalamika kukosa nguvu au kumaliza haraka hii yote inaletwa na hofu na mara nyingi kudate mpenzi ambaye tayari keshakutana na wataalam, usitegemee kamwe katika miaka yako 26 umridhishe mwanamke wa 18-23 atakuwa anakuibia tuu. 

Mabinti wengi below 25 wapenzi wao ni 35+years. Hapo huwezi weka ligi.
Kinachowatisha wengi ni story za wanawake kufikishwa kileleni au kupiga show 30 nonstop wakati wewe dak5 nyingi. Usihofu, muda wako bado, wewe bado mchanga hujakomaa.

Lakini vile vile kuna wakati maungo yako huhitaji mapumziko. Hii hutokea yenyewe automatically, ndio maana kuna wakati unakuwa na ashiki sana na kuna wakati unakuwa kama hanithi. Usitishike, jitahidi mazoezi, epuka vyakula vya mafuta na makopo, jizuie kadiri uwezavyo kupiga punyeto labda mpaka uzidiwe sana.

4. Uko kwenye kipindi cha kuingia ukubwani, kwahiyo akili ya kiutu uzima inafunguka, hii hali huja na side effects kama za mama mjamzito. Hasira za ghafla, kukata tamaa, kulia au kutamani kulia, kuzira, kujitenga, kuwa mtu wa mawazo muda mwingi ni vitu visivyoepukika.

Hapa ndipo unapojishape kuwa wewe wa kesho, kwahiyo jitahidi sana yanapokutokea haya usiyaendekeze, vijana wengi huwin na kushindwa hapa. Ukiyapuuza na kusonga mbele mafanikio yako yataanzia hapo, utayachukulia kuwa ndio sehemu ya maisha yako, kushindwa kwako kutaanzia hapo.

Kama bado uko below 30 usiangalie mwili ulionao bali jipange kwa kuwa hii ndio hatua muhimu ya kuwa wewe wa kesho. Mustakabali wako umeubeba mwenyewe.

Ishara Kumi Kwamba Wewe ni “Mwanaume Suruali” Mbele ya Wanawake!...!!!

$
0
0

Hakuna mwanaume asiyependa kuonekana yeye ni mwanaume bora, rijali na anaekubalika mbele ya jamii. Lakini mara nyingi tunapojaribu kufanya kila tuwezalo ili tuwe wanaume bora,mara nyingine tumejikuta Tunaharibu zaidi na kuonekana “wanaume suruali”, “nice guy” na majina mengi yakiwa na maana ya mwanaume mdhaifu, na asiye na sauti mbele ya wanawake au mpenzi wake.

Ukiona una ishara hizi, Tafuta namna ya Kubadilika.

a) Huna Mpenzi na una marafiki wengi sana wa kike. Na wamekuwa wakikuelezea matatizo ya wapenzi wao, na wewe unajiona ni mshauri wao bora!



b) Kama una mpenzi, Unakubaliana na kila anachokisema au anachokitaka unasahau kuwa, wakati mwingine wanawake hufanya vitu kwa majaribio kuona utakubali? Na ukikubali, basi ushakuwa “uchochoro” atakulazimisha ufanye kila anachokitaka kwa gia ya “mimi si ni mpenzi/mke wako??”

c) Huna muda na Marafiki zako tena! Wakati mwingine unakataa mialiko yao kutokana na Pengine mpenzi wako kakuomba umsindikize rafiki yake shopping, au saluni

d) Una rafiki mwanamke ambae si mpenzi wako, unamjua mpenzi wake, lakini wewe ndo unaongea nae zaidi kwenye simu (hasa usiku) kuliko mpenzi wake, wakiwa pamoja wewe ni mpiga picha wao (cameraman) na kuwanunulia maji nk.

e) Unapenda sana kioo kuliko vitu vingine! Na mara nyingi unajipiga picha mbele ya kioo

f) Ni mtu wa Kujitolea mno hasa kwenye kazi ambazo hakuna anayependa kuzifanya. kama kuwabebea wengine mizigo mnapotembea nk!

g) Siku zote wewe ni mtu unayeweka maslahi ya watu wengine mbele kabla yako. Unatumwa mno na mtu yeyote na Hujui Kusema hapana

h) Mpenzi wako ndiye mwenye maamuzi ya mwisho “mi nakusikiliza wewe!”

i) Baada ya party, siku zote wewe ni mstari wa mbele kusafisha meza pamoja na wanawake! Na wanawake wanakupenda kwa hilo.


k) Mkitoka “out” , mpenzi wako analeta marafiki zake kibao na unawalipia pia

Rais wa TLS Tundu Lissu Atuma waraka kwa Rais Magufuli kuhusu sakata la RC Makonda

$
0
0

Rais wa TLS Tundu Lissu Atuma waraka kwa Rais Magufuli kuhusu sakata la RC Makonda


Serikali Yakana Kumshikilia Yusuf Manji

$
0
0
Sakata la kushikiliwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Yusufu Manji limeendelea kuchukua sura mpya, safari hii yakiibuka mabishano Mahakama Kuu baada ya Serikali kukana kumshikilia.

Mabishano hayo yameibuka jana kati ya mawakili wa Serikali na mawakili wa Manji baada ya mfanyabiashara huyo kufungua maombi juma lililopita akihoji uhalali wa kushikiliwa na Uhamiaji.

Manji aliyefungua maombi hayo mahakamani hapo kupitia Wakili wake Hudson Ndusyepo, anaiomba mahakama iiagize Uhamiaji afikishwe mahakamani ili mahakama iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kisha iamuru aachiwe huru.

Kutokana na maombi hayo, Jaji Ama-Isario Munisi, aliwaamuru wajibu maombi kuwasilisha hati zao za kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo na kupanga kuyasikiliza jana mchana.

Wajibu maombi ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.

Hata hivyo jana Serikali katika majibu yake kupitia  hati ya kiapo kinzani cha Ofisa Uhamiaji, Anorld Munuo, ilikana kumshikilia mfanyabiashara huyo. Mbali na kiapo hicho, Wakili Mkuu wa Serikali, Oswald Tibabyekoma, alisisitiza kuwa mfanyabiashara huyo hashikiliwi na yuko huru.

Maelezo hayo ya Serikali yalipingwa vikali na mawakili wa Manji, Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, ambao kwa nyakati tofauti walisisitiza kuwa hadi jana mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwa matibabu, akiwa chini ya ulinzi wa maafisa Uhamiaji.

Kimenukaaa..Kitwanga Aibuka na Kuwachana 'Live' Makonda na Gwajima...!!!!

$
0
0

Figisufisu na ugomvi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Christian Makonda na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (GCTC), Josephat Mathias Gwajima, zimepamba moto na joto lake linapanda na kushuka kila kukicha.

CHANZO CHA UGOMVI WA MAKONDA NA GWAJIMA

Nyuma ya ugomvi huo unaotajwa kuwa wa kihistoria huku mmoja akimwaga mboga na mwingine anamwaga ugali, duru za kisiasa zinadai kwamba, chanzo cha yote hayo ni Ubunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Uwazi limedokezwa.

Jimbo la Misungwi kwa sasa linaongozwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Muhangwa Kitwanga.

KITWANGA NA UWAZI

Akizungumza na Uwazi katika mahojiano maalum na kutoa la moyoni juu ya sakata hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Kitwanga aliwavaa wawili hao akiwashangaa kusikia kwamba wanalitaka jimbo lake hilo.

Kitwanga alikiri kuwa, amezisikia habari hizo lakini kinachomshangaza ni kwamba, ni mapema mno kwani ni mwaka wa pili tu, tangu uchaguzi ulipomalizika mwaka 2015 na uchaguzi mwingine upo mbali kwani ni hadi mwaka 2020.

KITWANGA AFUNGUKA

“Taarifa hizo nimezisikia lakini kinachonishangaza ndiyo kwanza tumetoka kwenye uchaguzi na uchaguzi mwingine bado sana.

“Kwani tayari umeshafika muda wa kugombea?

Wameshapitishwa na vyama vyao?

Ninachojua ni kwamba, sisi tumemaliza uchaguzi na sasa tunafanya kazi, mimi natekeleza ilani ya chama changu (CCM).

WAACHE KUVURUGA WANANCHI

“Kama wanagombana na wao wanataka jimbo langu, wasubiri muda utakapofika tufanye kampeni na siyo kuvuruga wananchi wangu. Katika taratibu zetu ndani ya chama ziko tofauti sana.

“ Najua Gwajima ni mwanachama wa Chadema na Makonda anaiami n i CCM, wao wana taratibu zao lakini wasivuruge wananchi wangu ninaowatumikia, wao waendelee na hayo mambo yao.

WANAKARIBISHWA ULINGONI

“Hata hivyo, simzuii mtu kugombea katika jimbo langu, wanakaribishwa ulingoni lakini wafuate taratibu za vyama vyao muda utakapofika tutajua, huu ni muda wa kuchapa kazi kama ilivyo kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu na ndicho ninachokifanya kwa wananchi wangu na si vingine na wala sitaki kuwaingilia kwenye huo ugomvi wao,” alisema Kitwanga.

YATOKANAYO

Katika uchunguzi wake, Uwazi lilidokezwa na vyanzo vyake kuwa, Makonda anatajwa kutaka ubunge wa jimbo hilo ili kupandisha kiwango chake cha kisiasa na hata kufikia ngazi ya uwaziri baada ya 2020.

Hata hivyo, suala la wawili hao kuhusishwa na jimbo hilo iliwahi kuelezwa na Askofu Gwajima siku chache baada ya kutajwa na Makonda kwenye kuhusika na mambo ya dawa za kulevya hivyo kudai kuwa ni vita ya kisiasa.

Gwajima anayetoka kijiji kimoja na Makonda cha Koromije jimboni Misungwi alikaririwa kanisani kwake akisema kuwa zipo taarifa za Makonda kumsakama kwa sababu anadhani na yeye (Gwajima) analitaka jimbo hilo.

“Nilipata msiba nyumbani Koromije nilikozaliwa, kwa kuwa nilitoka muda mrefu huko hivyo nilikwenda msibani kwa helikopta.

“Kule kuna shangazi yangu, nilitua kwa ndugu wengine na kama unavyojua helikopta ikitua kijijini, lazima watu waje wengi kuitazama.

GWAJIMA NA KITWANGA

“Nilipoondoka, watu wakabaki wakiita Gwajima… Gwajima. Baada ya wiki tatu, nne, kaka yangu ambaye ni mtoto wa shangazi alifariki dunia, nikaona safari hii nikiwa ninakwenda kule nimpigie Mbunge wa Misungwi (Kitwanga), nikamweleza kuwa nitakwenda kule tena kwenye jimbo lako, naomba ukiwa na nafasi twende wote… sitaki unione ninakwenda kwa madhumuni ya kisiasa.

“Nilipokwenda, Kitwanga alikuwa bize, akasema nenda na katibu wangu, nikamchukua na mbunge mwingine wa zamani wa jimbo hilo nikasema twende wote ili wasifikiri kwamba Gwajima anataka kufanya kitu.

“Nikatua na helikopta pale msibani, si unajua tena, wakaniambia ongea lakini sikuhutubia lolote. Nikakaa na mapailoti wetu na baada ya msiba nikaondoka.

GWAJIMA NA MAKONDA

“Sasa baadaye ndiyo watu wakasema yule kiumbe (Makonda) alikuwa anataka lile jimbo, ulipokwenda wewe alihisi unataka kulichukua mwaka 2020, nikasema angeniuliza, kwa mimi siwezi kuwa mbunge, nikiwa mbunge ni kujishusha, mimi ni mtumishi wa Bwana ambaye ni zaidi ya mbunge, waziri na rais, siwezi kugombea urais uwaziri au ubunge, nitakuwa nimejishusha, mimi ni mtumishi wa Mungu aliye hai.

“Kwa hiyo Makonda alidanganyika na kujikuta akinitaja kwenye madawa ya kulevya akijua atakuwa amenimaliza kwa wananchi bila kujua sina ndoto hiyo,” alidai Gwajima lakini Makonda yeye hajawahi kulizungumzia hilo.

Jumapili iliyopita Uwazi lilimtafuta Makonda ili kusikia upande wake lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

KINACHOENDELEA

Jumapili iliyopita Gwajima aliendelea kutumia kanisa lake kumshambulia Makonda juu ya suala ya vyeti feki huku akiweka hadharani ‘document’ aliyodai ni cheti cha kidato cha nne cha Makoda cha Shule ya Sekondari ya Pamba iliyopo Mwanza.

Hata hivyo, Makonda wiki iliyopita akiwa na watu waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya alizungumzia elimu yake kwa kujigamba kwamba akiwa rais wa wanafunzi wa vyuo vikuu alifanya makubwa na hakuzungumza chochote kuhusu vyeti feki anavyodai Askofu Gwajima.

Bill Gates Azidi Kuongoza kwa Utajiri Duniani...

$
0
0

Bill Gates hakamatiki – ameendelea kuongoza orodha ya matajiri duniani. Muanzilishi huyo wa Microsoft ametajwa na jarida la Forbes kuwa na utajiri wa dola bilioni 86 kutoka dola bilioni 75 ambao alikuwa nao mwaka jana.

Forbes imetanganza kuongezeka kwa idadi ya matajiri zaidi katika orodha hiyo ambao wamefikia 2043 huku Marekani katika orodha hiyo imeingiza matajiri, China inashika nafasi ya pili ikiwa na mabilionea 319 na Ujerumani ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na mabilionea 114.

Hii ni orodha ya matajiri kumi zaidi duniani:

1.Bill Gates – $86bn
2.Warren Buffett – $75.6bn
3.Jeff Bezos – $72.8bn
4.Amancio Ortega – $71.3bn
5.Mark Zuckerberg – $56bn
6.Carlos Slim – $54.5bn
7.Larry Ellison – $52.2bn
8.Charles Koch – $48.3bn
9.David Koch – $48.3bn
10.Michael Bloomberg – $47.5bn

Imefichukaa...Huu Ndio Uchawi Anaoutumia Diamond Kufanikiwa Kimuziki,Wengi Hawajui....!!!!

$
0
0

MUZIKI unachukua sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku, umekuwa ukitupa faraja pale tunapoonekana kukata tamaa, ukitajiririsha ile furaha tuliyonayo katika nafsi zetu na kuturejeshea kumbukumbu za kitambo.

Basi muziki ni nini?. Muziki ni mpangilio ala na uimbaji unaoleta athari fulani kwa kiumbe, twende pole pole hapa, yaani naweza kusema kama msanii hawezi kupangilia ala na kuimba kwa ufundi hapo hakuna muziki. Tusimame hapo. Kwa hapa nchi muziki wa Bongo Fleva ndio umetawala sana ukilinganisha na aina nyingine za muziki. Bongo Fleva inasikika kila kona kuanzia majumbani, mtaani, mtandaoni, kwenye vyombo vya usafiri na vyombo vya habari.

Ukitaja majina matatu ya wasanii wanaofanya vizuri katika Bongo Fleva huwezi kuacha kumtaja Diamond Platnumz, kwa kipindi cha miaka saba aliyodumu katika muziki huu amekuwa na mchango mkubwa sana. Kwa miaka hiyo amekuwa akidondosha burudani ya uhakika, hakuwahi kusimama sehemu yoyote ile, ni yeye na kazi, kazi yeye, yaani bampa to bampa kama anavyoeleza Darassa katika wimbo wake wa muziki.

Sote tumekuwa mashuhuda wa mafanikio yake toka alipoanza, tumeshudia akibeba tuzo mbali mbali kama KTMA, AFRIMMA, MTV EMA na nyinginezo.

Kwanini leo Diamond?

Leo nimevutiwa kuandika makala haya mara baada ya msanii huyu kuanzisha wavuti ya kuuza nyimbo za wasanii ijulikanayo kama Wasafi.com. Hii ni hatua kubwa katika muziki wa Bongo Fleva.
Nadhubutu kusema ni hatua kubwa kwa sababu hakuna msanii mwingine aliyewahi kufanya hivyo, yeye ameiona hiyo fursa na kuamua kuifanyia kazi. Pongezi za kutosha kwake.

Mtandao huu unakuja kuleta ushindani mkubwa kwa mitandao kama Mdundo, Mkito na Muziki ambayo ilitangulia kufanya biashara hiyo. Wasanii ni wengi hadi sasa waliyokubali kuweka kazi zao katika mtandao huo. Nimemuona Prof Jay, Navy Kenzo, Barnaba, Kasimu Mganga, Harmonize, Billnas, Saida Karoli, Ray C, Belle 9, Chenge na Temba, Ben Pol na wengineo.

Ni wazi Diamond anazidi kujitunua kisanaa na kibiashara pia, kwa mantiki hiyo hakuna ubishi kuwa ataendelea kuwepo katika muziki huu kwa kipindi kirefu kutoka anafanya kazi na kundi kubwa la watu ambalo linahudumu katika ‘sekta’ ya muziki. Kwa hiyo usitengemee jamaa atashuka kimuziki miaka ya hivi karibuni, hilo sahau kwa sasa na ni vema ukaendelea na mambo mengine kuliko kukaa na kuwaza hilo. Narudia teno hilo sahau kwa sasa.

Mambo anayofanya ndiyo yanamfanya kuendelea kusalia juu. ‘Hakuna uchawi wala ndumba’ alijisemea Prof Jay katika wimbo wake wa Zali la Mentali. Kiufupi Diamond mwenye ametaka iwe hivyo.
Unawekeza kutoka moyoni Aliyekuwa mtangazaji wa redio na mwandishi wa vitabu nchini Marekani (1938-1946) Earl Nightingale aliinua mkono wake na kuandika maneo yasemayo “watu wenye malengo hufanikiwa kwa sababu wanajua kule wanakoelekea kimaisha.”

Wakati Diamond anaondoka Sharobaro Records kwa Bob Junior, sehemu iliyomtoa kimuziki alienda kuanzisha kitu kinaitwa ‘Wasafi’. Neno Wasafi lilikuwa likisikika kwenye nyimbo zake nyingi lakini wengi walizani zilikuwa mbwembe tu. Nani kakudanganya, tena nikupe pole sana. Diamond alikuwa akiishi katika maneno ya Earl Nightingale, alikuwa anajua anapoelekea na Wasafi hakuitaja tu bure, alijiona hapa alipo sasa.

Hakuna aliyetengemea kuwaWasafi itakuja kuwa lebo kubwa nchi ya kusamimia wasanii na kufanya biashara mbali mbali za muziki lakini ndilo tunaishi nalo kwa sasa. Kwani ameenda kwa mganga?, wee!, tena ishia hapo hapo. Siri ni moja tu, Diamond ni msanii aliyewekeza sana katika muziki wake, tunapozungumzia uwekezaji si fedha pekee bali hata muda.

Kuna baadhi ya wasanii wana uwezo mkubwa sana lakini wamekuwa wagumu kuwekeza, mikono yao imekuwa migumu kuzama mfukoni na muda wao mwengi umekuwa ukichukulia baadhi ya mambo yasiyokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na muziki wao. Moja ya nukuu kutoka kwa Anna Kleimer ni ile inayosema, “fanya unachopenda, na penda unachofanya”. Hii kanuni rahisi sana ambayo inawezesha watu kufikia malengo yao. Kwa asilimia kubwa watu mwenye mafanikio makubwa dunia ni wale wanafanya yale wanayoyapenda kutoka ndani.

Diamond anapenda muziki wake ndio maana anamwaga fedha kuwekeza, kuna wasanii wanafanya uwekezaji mkubwa nje ya muziki wao na wamefanikiwa huko, si jambo baya lakini kufanya hivyo ni kumuhakikishia Diamond kuzidi kutawala Bongo Fleva kwa kipindi kirefu zaidi, wala hakuna uchawi.

Chukua hii kwanza

Kuna mambo huwa nikikumbuka naishia kucheka tu. Miaka kadhaa nyuma kulikuwa kunaripotiwa visa vya mganga fulani aliyekuwa akidai ni mganga wake ni Diamond. Mganga alikuwa akidai kuwa yeye ndiye aliyemtoa Diamond na mafanikio yake anahusika hata ushindi wa tuzo saba za KTMA mwaka 2015 anahusika. Sikumshangaa kwa sababu hii imeshakuwa ni tabia kwa baadhi yetu kuamini mtu anapofikia mafanikio fulani katika umri mdogo lazima kuna jambo nyuma ya pazia.

Kiufupi hatuamini katika juhudi binafsi. Sikuwahi kuamini katika maneno ya mganga yule, ila nilijua hata Diamond akitetea vipi hatu hawawezi kumuamini, lakini niliamini kuwa muda na juhudi zake ipo siku zitatupa jibu. Muda hutoa majibu ya baadhi ya maswali yanayoshindikani katika nyakati fulani. James Richardson raia wa Marekani alifungwa jela kwa kusingiziwa lakini baada ya kutumikia kifungo chake kwa miaka 21 ilibainika hakuwa na hatia hivyo akaachiwa huru.

Hivi ndivyo muda hutoa majibu yake. Sasa tunamuona Diamond katika ‘level’ za mbali zaidi kuliko kile kipindi cha hayo maneno, je yule mganga yupo wapi?, akiibuka tena leo wangapi watakaomuamini. Bila shaka jibu litakuwa ‘Acha maneno weka muziki.’ Ndiyo, hilo ndilo jibu pekee kwa sasa, kwani Diamond tunamuona jinsi anawekeza, anatengeneza ‘connection’ na watu mbali mbali wa ndani na nje na vile anavyobrand muziki wake. Tusimame hapo kwanza.

Biashara ni wateja

Biashara yoyote dunia inatengemea wateja ili iweze kujiendesha na kumletea faida yule anayeimiliki au kuisimamia. Biashara ya kuuza muziki kupitia mdandao wa Wasafi.com naiona ikimuugiza Diamond fedha nyingi kwa kuuza tu nyimbo zake binafsi kutokana na ‘fun base’ (followers) kubwa aliyonayo katika mitandao ya kijamii.

Diamond ndio msanii anayeongoza kufuatiliwa na watu wengi mtandaoni kwa hapa Bongo, watu zaidi ya milioni tano wanamfuatilia. Katika mtandao wa instagram ana watu milioni 3.4, twitter 363,000 na Facebook milioni 2.9 (takribani milioni tatu).

Idadi hii ya watu ndio inampa Diamond ‘kiburi’ cha kusema kwa sasa hatengemei radio na TV kama njia ya kutangaza muziki wake. Watu milioni tano ni wengi sana na kila siku wanaongezeka, uzuri ni kwamba jamaa mwenye kaona fursa ndani yao. Kama nusu ya watu hao, yaani milioni 2.5 wataamua kununua wimbo wake mmoja kupitia Wasafi.com kwa sh. 300, Diamond atakuwa ameingiza sh, 750,000,000 (milioni mia 750). Nimegawa idadi hiyo ya watu nusu kwa kuwa wapo wanamfuatilia katika mitandao yote mitatu.

Kwa hesabu vilivyo wazi kiasi hiki bado mtasema ameloga au anafanya biashara fulani ya magendo, bila shaka huu utakuwa ujinga wa kiwango cha PhD, si bure. Hapo bado hatujaangalia ‘show’ zake anazofanya kuanzia Bongo hadi nje, kampuni mbali mbali anazofanya nazo biashara ya matangazo na kadhalika, kiufupi jamaa ‘kajiloga’ mwenyewe tu na hii iwe fundisho kwa wasanii wengine.

Davido: Sipimi Tena DNA...!!!

$
0
0

MKALI wa Miondoko ya Afro Pop, kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ hivi karibuni ameweka wazi kuwa hawezi kufanya tena vipimo vya DNA ili kuthibitisha kuwa mtoto wa kike Veronica ni wake baada ya vipimo alivyofanya awali kuonyesha kuwa si damu yake.

 Akizungumza na vyombo vya habari Nigeria hivi karibuni, Davido aliongeza kuwa mama wa mtoto huyo, anayefahamika kwa jina la Abadan alimpakazia juu ya ujauzito huo na kwamba haukuwa wake jambo alilolielewa tangu awali lakini alitaka tu kuwaridhisha watu ambao hawakuwa wanaamini juu ya hilo kwa kupima DNA.

“Vipimo vya DNA haviwezi kudanganya, huyo mwanaume ni mpigaji tu, anataka pesa za haraka na umaarufu, siwezi kurudia kufanya vipimo hivyo, kwa sasa nipo bize na mambo yangu binafsi,” alimaliza Davido.

Jipatie Water Dispenser Mpya Kwa Bei Nafuu

$
0
0

JIPATIE WATER DISPENSER MPYA kwa bei Nafuu sanaa,Kwa matumizi ya OFISINI NA NYUMBANI, Upate Maji baridi na Moto.

Tunakuletea Oda yako kwa Wakati na Mikoani tunatuma Oda zenu pia.

Tunatoa DHAMANA ya Mwaka 1.

BEI 195000/= TU HAINA FRIJI.

BEI 290000/= INA FRIJI CHINI

TUPIGIE SASA0743757575

More Items/Products follow us Instagram
@beinafuu_shop
@beinafuu_shop
@beinafuu_shop
@beinafuu_shop

Alichosema Waziri Nape Kuhusu Ripoti ya Kamati inayochunguza Tukio la Makonda

$
0
0
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye jana March 20, 2017 alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake.

Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe.

Baasa ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi sasa Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema


’Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!‘



‘Msikubali Kuangushwa na Sisi Wachache, Nyinyi ni Wengi’ -Hussein Bashe

$
0
0

March 21, 2017 Mbunge wa Nzega mjini kupitia CCM Hussein Bashe amepost ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno yaliyosomeka…

’Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo‘

‘Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu‘ –Hussein Bashe

‘Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru‘ –Hussein Bashe

‘Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu.‘-Hussein Bashe

‘Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu‘ -Hussein Bashe

‘Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania UHURU wa taifa letu. TUJISAHIHISHE‘ –Hussein Bashe

KUTANA na Mtabibu Ostadhi Khamisi Kutoka Mombasa Kenya Kwasasa Yupo Tanzania Kwa Ajili yako

$
0
0



Kutana na ostadhi khamisi kutoka mombasa Kenya kwa sasa yupo Tanzania ni mtabibu na mtafiti Wadawa za asili anatibia kama vile:
Miguu kuuma
Miguu kufagazi
Miguu kuwakamoto
Chango lauzazi kwakina mama
Dawa ya uzazi wakina mama inapatikana
Kusafisha nyota ili uwe namuonekano kwa kila mtu
Kumrudisha mpenzi wako na liekukimbia ndani yasiku 3 bila yapingamizi yoyote
Kumshika mume au mke asitoke nnje ya ndoa
Pata pete ya Bahati inayo endana na nyota yako
Kurudisha mali ilipotea au kudhurumiwa ndani yasiku 3
Pata utajili usiokuwa namashaliti yoyote
Dawa za nguvu za kiume
Dawa ya biashara inapatikana
Dawa ya kuzuia chuma ulete kwenye biashara inapatikana
 Zindiko la nyumba au shamba
 Anatuliza familia zinazogombana DUWA pamoja navisomo vya ufunguzi wa mwili wako njoo ufunguliwe vifungo ulivyo fungwa kutana na ostadhi khamisi utimiziwe ahadi ulizo hadiwa acha kuteseka acha kuhangaika ostadh khamisi yupupo tanzania kwajili yako...

Call +255718746825 +255754765246 kwa what'sapp +255783708487

Rais wa Zambia Apigiwa Magoti na Waziri Wake...!!!

$
0
0
Rais wa Zambia Edgar Lungu akinyenyekewa na waziri wake wa Mifugo na uvuvi,

Ummy Asema Maombi ya Madaktari Kwenda Kenya Yanamiminika Wizarani...

$
0
0



Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewahakikishia madaktari wa Tanzania usalama wakiwa nchini humo.

Alisema Serikali haina uwezo wa kibajeti wa kuajiri madaktari wote waliopo nchini licha ya kuwa kuna upungufu kwenye hospitali na vituo vya afya.
“Hiyo ni fursa kwa madaktari wasio na ajira kuichangamkia, ni hiari yao kuomba au kutoomba,” alisema.

Siku Tatu za Makonda Zilivyotikisa Dar es Salaam...!!!

$
0
0

 Kwa siku tatu mfululizo, mjadala mkubwa umekuwa ni jina la mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Aliingia studio za Clouds TV Ijumaa usiku akiwa na askari waliokuwa na silaha za moto, akajadiliwa katika mitandao ya kijamii kutokana na kitendo hicho, Jumapili akawa sehemu ya mahubiri ndani ya Kanisa la Uzima na Ufufuo, lakini jana Rais John Magufuli akamhakikishia kibarua chake, jambo lililoongeza kasi ya mjadala.

“Makonda Amtega Rais Magufuli”, “Makonda Katika Moto kwa Kuvamia Clouds Usiku”, Makonda, Gwajima Waanza Vita Upya”, na “Makonda ‘Ateka’ Clouds Media” ni baadhi ya vichwa vya habari vya magazeti ya jana kuonyesha kitendo cha mkuu huyo wa mkoa kilivyotikisa nchi.

Habari hizo zote zinazungumzia kitendo cha Makonda kuingia studio za Clouds TV inayomilikiwa na Clouds Media Ijumaa usiku, akiwa na askari waliovalia sare na kiraia na ambao walishika silaha za moto na kukariri wadau wakitaka Rais amchukulie hatua.

Na jana asubuhi wadau wa habari, Waziri Nape Nnauye, mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (Moat), Jukwaa la Wahariri (TEF), wahariri, wasanii na vyombo vingine vya habari vilikuwa vikitoa pole kwa uongozi wa Clouds na kulaani kitendo hicho cha Makonda.

Huku wananchi wakiendelea kupaza sauti kutaka atengue uteuzi wa mkuu huyo, Rais Magufuli alitumia ufunguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu za kupishana magari katika makutano ya Barabara ya Sam Nujoma na Morogoro kueleza ya moyoni kuhusu mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam.

Rais alizungumzia taarifa zinazoendelea kujadiliwa mitandaoni kuwa hazina tija na kumtaka “Makonda aendelee kuchapa kazi”.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa mtandaoni kuhusu Makonda na utata wa elimu yake, utajiri wa ghafla na tukio la Ijumaa usiku. Ilikuwa ni takriban saa tatu baada ya mkurugenzi wa vipindi na uendeshaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba kuzungumza kuhusu tukio hilo katika kipindi cha televisheni cha 360, ambacho Rais Magufuli ameshapiga simu mara tatu kueleza jinsi anavyokifuatilia.

Ruge alikuwa akithibitisha habari zilizoenea mitandaoni tangu Jumamosi kuwa Makonda alifika studio za Clouds TV Ijumaa usiku, akiwa ameambatana na askari wenye silaha za moto na kuchukua kwa nguvu sehemu ya kipindi cha Shilawadu kilichokuwa kimezuiwa kurushwa kutokana na kutokidhi matakwa ya kitaaluma.

Shilawadu ni kifupisho cha Shirikisho la Wambea Duniani na ni kipindi ambacho kinazungumzia tuhuma za watu mbalimbali maarufu na katika mahojiano ya 360, Ruge alisema alihisi habari ambayo aliizuia isitoke hadi itakapokidhi vigezo vya kitaaluma, ilikuwa ina uhusiano na Makonda baada ya kuambiwa na mmoja wa watangazaji wa Shilawadu kuwa inamuhusu mwanamke ambaye anadai amezaa na Askofu Josephat Gwajima, mpinzani mkubwa wa mkuu huyo wa mkoa.

Taarifa kuhusu Makonda kuhusika katika sakata hilo zilipamba moto Jumapili asubuhi na zikafuatiwa na video zinazomuonyesha mkuu huyo wa mkoa akiingia ofisi hizo akiwa na askari wenye silaha.

Kusambaa kwa video hizo kuliibua mjadala mkubwa kutokana na wengi kuhoji sababu za Rais Magufuli kutochukua hatua haraka kama alivyofanya kwa watumishi wengine wa umma, akiwemo Charles Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kuingia bungeni akiwa amelewa.

Kutokana na maswali mbalimbali kuibuka, huku Clouds ikitakiwa ieleze ukweli, Ruge alilazimika kueleza kilichotokea, akitumia kipindi cha televisheni ya Clouds TV cha 360 kinachorushwa kila siku asubuhi.

“Paul (Makonda) ni rafiki yetu, lakini ametukosea, huwezi kuja ofisini kwetu ukiwa na mabunduki tena usiku,” alisema Ruge ambaye vituo vyake vya redio na televisheni vimekuwa vikirusha moja kwa moja shughuli za Makonda.

“Sijutii urafiki wetu na mkuu wa mkoa, bali nalaumu vitendo vyake na anapokosea lazima aambiwe ukweli kuwa kakosea. Makonda ni rafiki yetu, lakini mimi urafiki na bunduki siutaki kabisa. Urafiki wa wali na maharage freshi.”

Ruge, ambaye usoni alionekana kuwa asiyetaka masihara, alisema hakutaka kumtafuta Makonda baada ya tukio hilo kwa kuwa mkuu huyo wa mkoa ndiye aliyewakosea.

“Nataka nirudie kwamba urafiki unatengeneza mazingira ya kwamba, ok. Hii unataka kuifanya vizuri zaidi, kitengenezee mazingira mazuri zaidi. Tutakuruhusu ufanye, sio hapa atafanya hata kule kama ambavyo tunaruhusu watu wengine pia wafanye,” alisema Ruge.

“Mimi kwa kweli nampongeza upande mmoja; ni mtu ambaye kwa kweli amekuwa akitumia nafasi vizuri, kwa sababu sio kosa kusema kwamba mimi nina hiki, naomba niki-edit vizuri mnisaidie kukirusha, sio kosa. Kosa ni pale ambapo unapotaka kupanda watu kichwani.

“Kosa ni pale ambapo unapotumia nafasi yako kwa ubaya.”

Ruge alisema yeye anasimamia chombo kilicho na watu zaidi ya 200 na ambao ni vijana wadogo, kulinganisha na Makonda ambaye anasimamia watu milioni tano.

“Kwa bahati mbaya wale mia mbili wananitazama kama mtu ambaye ni mfano. Nisipowatetea wao, huyu atakuja leo. Akija kila siku kiongozi mwingine?” alihoji Ruge.

“Tubadilishe mtazamo wetu sasa maana viongozi wanashindana na wasanii kutafuta kiki kwenye mitandao ya kijamii. Viongozi wetu wanapenda kumzungumzia Mwenyezi Mungu, lakini hawajui kuwa dhambi za binadamu zinaumiza zaidi kuliko kumuudhi Mungu.”

Msimamo wa Magufuli

Hata hivyo, Rais John Magufuli alimtaka Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao.

Magufuli, ambaye wakati mwingi wa hotuba yake alionekana akisoma, alionekana kuanza kutotegemea alichokiandaa alipoanza kuzungumzia suala la Makonda.

Alisema kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.

“Tunaendekeza mambo ya udaku wakati hayatusaidii kupata chakula, kupunguza foleni Dar es Salaam, kupeleka watoto shule, kupata maji ya kunywa, kupata maendeleo. Tuzungumze uchumi na maendeleo ya wana-Dar es Salaam,” alisema Rais Magufuli.

“Mnahangaika kupost (kutuma) mara hili, mara lile, mpaka watu wengine wananiingilia nifanye mambo wanayotaka. Ukinipangia ndiyo unapoteza. Mimi ni Rais ninayejiamini.”

Kwa wiki takriban tatu, kumekuwa na habari katika mitandao zikimuhusisha Makonda na mtu anayeitwa Daudi Bashite aliyesoma Shule ya Msingi Koromije na Sekondari ya Pamba na kumaliza kidato cha nne kwa kupata daraja la sifuri.

Mmoja kati ya watu wanaoongoza kushamirisha habari hizo ni Askofu Gwajima, ambaye amesema anamfahamu na anao ushahidi wa vyeti na watu waliosoma na Bashite na hivyo kumtaka Makonda athibitishe utambulisho wake, la sivyo ataweka bayana kila kitu.

Lakini Rais Magufuli, ambaye Serikali yake imekuwa ikifanya uhakiki wa wafanyakazi wa umma na elimu yao, alisema habari za mitandaoni hazina tija kwake na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo badala ya kupoteza muda kufuatilia udaku kwenye mitandao.

Alisema hawezi kupangiwa nini cha kufanya.

“Najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi, akae wapi, ni mimi ninayepanga. Ninajua wamenielewa,” alisema Rais.

“Kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi. Nasema chapa kazi. Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu. Hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao, kwa hiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi,” alisema Rais akimuangalia Makonda, ambaye alisimama na kuinamisha kichwa kuonyesha kukubali.

“Kwa hiyo niwaombe ndugu zangu Watanzania, tunapoteza muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi. Tuwatumikie Watanzania. Watanzania wana shida nyingi za kufanya. Wanahitaji maji, wanahitaji barabara, wanahitaji elimu, wanafunzi wa chuo kikuu wanahitaji wapate mikopo, Ni mambo yote. wanahitaji afya nzuri. Hilo ndilo jukumu letu sisi viongozi.

“Kwa hiyo niwaombe Watanzania wenzangu wa vyama vyote, tusijisumbue na mambo yasiyo na msingi.”

Ruge asimulia

Kabla ya kutoa hotuba hiyo, Ruge alieleza mkasa wote ulivyokuwa tangu Alhamisi wakati Makonda alipoenda makao makuu ya Clouds na kuongea na watangazaji wa kipindi cha Shilawadu.

Ruge alisema siku hiyo walikuwa na kikao na watu wa TCRA na baada ya hapo alitoka nje ambako alimkuta Makonda akiwa pamoja na vijana wanaofanya kipindi cha Shilawadu na alipowauliza kuwa ni kwema alijibiwa kuwa walikuwa katika mazungumzo ya kawaida tu.

“Nikiwa kwenye gari nikijiandaa kutoka, kijana mmoja wa Shilawadu alinifuata na kuniambia kuna mahojiano amefanya na mtu anaedai amezaa na Gwajima nikamuuliza kwa hiyo,” alisema Ruge.

Alisema kijana huyo alimwambia kuwa wameshindwa kumpata Gwajima na hivyo akawaambia wasirushe hicho kipindi hadi wampate askofu huyo.

Na kwa kuweka msisitizo, Ruge alimwambia meneja wa vipindi anayeitwa Kerry kuwa kama Askofu Gwajima hajapatikana, kipindi hicho kisirushwe na baadaye kumpigia simu ofisa rasilimali watu kumweleza suala hilo.

Pia, Ruge aliwaambia waandaaji wa kipindi hicho wamueleze hata Makonda kuwa hawangeweza kukirusha kutokana na upande wa pili kutopatikana.

“Tena nikamwambia Kerry kwa masihara kuwa ikiwezekana ayapoteze kabisa hayo ‘material’ kwa sababu hata Shilawadu wenyewe walikuwa wanavutana juu ya habari hiyo,” alisema Ruge.

Ruge aliendelea kuwa siku hiyo hiyo saa 10:00 jioni alipigiwa simu na Askofu Gwajima akimueleza kuwepo kwa habari inayomuhusu, lakini akamhakikishia kuwa habari hiyo haipo na haitaruka kwa sababu haijakidhi vigezo.

Mkurugenzi huyo alisema jambo la kushangaza majira ya saa 4:45 usiku Ijumaa alipokea simu kutoka kwa ofisa rasilimali watu akimueleza kuwa mkuu wa mkoa ameingia ofisini akiwa na askari sita wenye silaha.

Alisema baada ya simu hiyo ilifuatia simu ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Joseph Kusaga akimueleza kuwa analaumiwa na Makonda kuwa amezuia kipindi chake.

Mtangazaji mualikwa wa 360, Masoud Kipanya aliuliza kama Makonda huwa ana vipindi vyake Clouds, lakini Ruge alisema hakuna kitu kama hicho.

Alisema baadaye Kusaga alitaka wafanye mazungumzo na Makonda kuhusu suala hilo.

“Mimi nikamwambia siwezi kwenda kwa sababu hata mkuu wa mkoa hajaonyesha heshima kwa sababu anao uwezo wa kunipigia simu muda wowote. Kwa nini hajafanya hivyo mpaka avamie,” alisema Ruge.

Ruge alisema baadaye alimpigia simu Makonda na akamuuliza sababu za kwenda ofisi za Clouds na watu wenye bunduki, lakini Makonda akamjibu kuwa amefanya hivyo kwa sababu amezuia kipindi chake.

“Kwanza sio kipindi chako (Makonda). Mimi ndiye mkurugenzi wa vipindi, na hivi vipindi viko chini yangu,” alisema Ruge akikumbuka mazungumzo yake na Makonda kwenye simu.

Ruge alisema Makonda alimuelezea kuhusu kipindi kinachomuhusu mwanamke anayedai amezaa na Askofu Gwajima, lakini akamjibu kuwa upande wa pili haujapatikana na kumueleza umuhimu wa kusimamia weledi kwa kila mtu kupewa nafasi.

Alisema Clouds kama chombo cha habari wameumia kuona tukio hilo linafanywa na rafiki yao ambaye angeweza kuhoji kwa namna nzuri  lakini sasa amesababisha vijana wa Shilawadu kutokuwa sawa mpaka wamefikia hatua ya kuomba likizo ili watulize akili zao kwa kuwa tayari washaingiwa uoga.

“Tubadilishe mtazamo wetu sasa maana viongozi wanashindana na wasanii kutafuta kiki kwenye mitandao ya kijamii. Viongozi wetu wanapenda kumzungumzia Mwenyezi Mungu lakini hawajui kuwa dhambi za binadamu zinaumiza zaidi kuliko kumuudhi Mungu,” alisema Ruge.

Alisema video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii likihusisha tukio lile ni za kweli, lakini hajui ni nani aliyezitoa kwa sababu pale kuna CCTV kamera na kila mfanyakazi anajua wapi zinafanyia kazi.

Pia alizungumzia habari zilizosambaa kuwa alishikiliwa na polisi Jumapili.

“Watu walisema eti niliwekwa ndani polisi lakini sio kweli nilienda tu kuripoti kwa ajili ya taarifa maana linapotokea jambo lolote linalohusu uvamizi wa silaha ni lazima maelezo yachukuliwe ili kuepusha upotoshaji,” alisema Ruge.

Pia, Ruge alisifu vyombo vya habari kwa kumuonyesha mshikamano, akisifu hata wapinzani wao wakubwa kwamba wamesikitishwa na tukio hilo na kuomba wadau wote wa habari kusimama pamoja katika hilo kuhoji haki na heshima ya vyombo vya habari.

Nape awatembelea

Katika tukio jingine, hata kabla ya Rais Magufuli kuonyesha kumuunga mkono Makonda, Waziri Nape alifika ofisi za Clouds Media zilizopo Mikocheni saa 3:25 asubuhi, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbas pamoja na mwenyekiti wa Moat, Reginald Mengi.

Akiwa katika kituo hicho, Nape alisema Serikali inalaani kitendo kilichotokea katika nchi ambayo imesaini mikataba ya kimataifa ya kulinda uhuru wa habari na kwamba sheria zipo na zinapaswa kufuatwa

“Tumeunda timu ya watu watano kufanya kazi kwa saa 24 ili wapate maelezo ya RC baada ya hapo tutaeleza hatua tutakazozichukua kama Serikali. Lakini kabla ya kuchukua hatua zozote, tunataka kusikia kutoka kwa mkuu huyo,” alisema Nape.

Waziri Nape alikifananisha kitendo hicho kama mapinduzi ya kijeshi na kusema anaanza kuona dalili za wanasiasa kukosa ngozi ngumu.

“Kwakweli inatisha, haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Hii inatokea tu kwenye nchi zenye mapinduzi ambako wanaopindua huvamia redio na kujitangaza,” alisema Nape.

Alisema huwezi kuzungumzia suala la ulinzi mdogo kuwepo Clouds kwa sababu unaweza ukawepo hata wa polisi, lakini akishakuwepo mkuu wa mkoa hawana cha kufanya.

“Nimeteua kamati ndogo inayoongozwa na mkurugenzi wa habari. Nimewaagiza wamhoji leo (jana) mkuu wa mkoa ili tupate nini kiliwasukuma wafanye walichofanya, halafu kesho (leo) mchana tutakuwa na press conference (mkutano na waandishi) kueleza hatua tutakazochukua,” alisema Nape.

Mengi azungumza

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Moat alisema wako pamoja na Clouds na watashirikiana kupambana na unyanyasaji kwa vyombo vya habari na kuwataka waandishi kuendelea kufanya kazi bila woga.

Alisema sura moja ya mwandishi wa habari ni kutokuwa mwoga hivyo jambo lililotokea lisiwatie hofu.

“Jambo lililofanyika ni la hatari sana. Na lazima tujiulize mtu huyu (Makonda) anapata wapi ujasiri huu?. Kama alikuja na bunduki hapa anaweza kwenda nazo popote na pengine kuna siku atazitumia,” alisema Mengi.

Alisema ana imani kuwa Rais Magufuli na waziri wa habari wana upendo kwa vyombo vya habari lakini mapenzi hayo lazima yaonyeshwe kwa vitendo.

Kamati ya Bunge yatinga Clouds

Katika hatua nyingine, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilitembelea ofisi za Clouds Media na mwenyekiti wake, Peter Serukamba alisema wametumwa na Spika wa Bunge.

“Alichofanya mkuu wa mkoa kwa namna yoyote ni matumizi mabaya ya madaraka. Sisi kama kamati tunasubiri Serikali wameunda kamati na sisi tutashauri baada ya kupata maoni ya hiyo kamati,” alisema Serukamba.

Huku akisisitiza haja ya waandishi wa habari kulindwa wanapotimiza majukumu yao, Serukamba alisema viongozi wa Serikali hawapaswi kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya lolote wanalotaka kinyume cha sheria.

“Leo (jana) amekuja kwenye vyombo vya habari, kesho atakwenda kwenye restaurant, keshokutwa atakwenda kwenye nyumba zetu. Niviombe sana vyombo vya usalama, fanyeni kazi kulingana na sheria zilizowaweka madarakani. Nchi inaendeshwa na sheria,” alisema Serukamba.

Alisema jambo hilo ni gumu kulifikiria na ni dalili za ulevi wa madaraka.

“Nilikuwa najiuliza, wakipanda hapa na mabunduki ingetokea bahati mbaya bunduki ile kukatokea lolote, risasi ikafyatuka akafa mtu, leo tungeongea nini? Huku ndiyo kuchapa kazi?” alihoji.

“Lakini kwa vyovyote vile kilichofanyika hakikubaliki kwa jamii ya Watanzania. Kutoka miaka 50 ya uhuru, hakuna mkuu wa mkoa amewahi kufanya haya. Tumepitisha sheria ile ya habari, lakini na waandishi wa habari walindwe,” alisema.

Hata hivyo, Serukamba aliwataka waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari kuepuka kutumiwa na wanasiasa kwa masilahi yao.

“Jambo hili ni fundisho kwa waandishi wa habari. Msikubali kutumiwa na sisi wanasiasa. Inawezekana matokeo ya jambo hili ni kwa sababu sisi wanasiasa tunakuja kwenye vyombo vya habari, tunatengeneza ujamaa na tunaweza kulazimisha mambo ambayo ni nje ya utaratibu,” alisema Serukamba.

Sugu alaani

Akizungumzia tukio hilo, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi alisema walioguswa si Clouds Media peke bali tasnia nzima ya habari.

“Kwa kweli kitendo kilichotokea ni cha kulaaniwa. Hii siyo Tanzania tuliyokuwa tukiitarajia na ndiyo maana tuko hapa kunyoosha mambo kama viongozi. Shambulio lililofanywa jana (juzi) si kwa Clouds peke yake, bali ni kwa industry nzima,” alisema Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alimtaka Makonda kuomba radhi kwa jambo alilofanya ili kulinda uadilifu wake.

“Makonda kama kijana anafanya makosa ya kimkakati yanayomharibia sifa kila kukicha. Naamini kiustaarabu si dhambi ukikosea ukaja hadharani kuwaomba radhi Clouds. Ana wajibu wa kuja kuomba radhi kwa kitendo cha kuingia na askari wakiwa na silaha na kutengeneza taharuki hii,” alisema Bashe.

UTPC kuchukua hatua

Nao Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) umeonya kuwa unaweza kumchukulia hatua Makonda, ikiwemo kumtenga katika kazi zake iwapo mamlaka yake ya nidhamu haitamchukulia hatua.

Rais wa UTPC, Deogratias Nsokolo alisema kitendo cha kiongozi wa Serikali kuvamia ofisi akiambatana na askari wenye silaha ni cha jinai na hakijawahi kutokea nchini.

“Mtu yeyote anayetaka kulazimisha habari gani itoke au isitoke anafinya uhuru wa habari kwani kazi ya uandishi wa habari ina miiko yake hiyo na inayotumika kuamua ni habari gani itumie au isitumike,” alisema Nsokolo.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan alisema hivi karibuni Serikali imepitisha sheria inayoitwa uhuru wa habari na moja kati ya vipengele katika sheria hiyo inawapa mamlaka Serikali kuchagua habari gani itoke au isitoke, kwa maana hiyo kitendo cha mkuu wa mkoa kuvamia kituo hicho cha habari swali la kujiuliza je, sheria hiyo imeanza kutekelezeka?

TLS watoa kauli

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amemshauri Rais Magufuli atengue uteuzi wa Makonda haraka iwezekanavyo kabla hajachafua zaidi taswira ya Serikali yake.

Pia amemshauri Rais Magufuli kumchukulia hatua stahiki kamanda au mkuu wa kikosi chochote cha jeshi lolote aliyeruhusu askari wake kutumiwa na Makonda kwa namna iliyoripotiwa.

Katika taarifa yake kwa umma, Lissu amesema Makonda hastahili kuendelea kwenye madaraka hayo kwa siku moja zaidi.

Kesi ya Masogange Yafikia Hatua Hii...!!!!!

$
0
0

 Upelelezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili  Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange(28) katika Mahakama ya Kisutu bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini ameeleza hayo leo wakati kesi ilipotajwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.

Mkini alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.

Baada ya kueleza hayo, wakili wa Masogange, Nictogen Itege ameiambia Mahakama kuwa mteja wako hiyo alikuwa njiani kuelekea mahakamani lakini alikwama katika foleni eneo la Jangwani.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Wabunge CCM Wajiuzulu Kisa Kuzuiwa Kumuona Lema Alipokuwa Gerezani..!!!!

$
0
0

UONGOZI wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, umejiuzulu katika nafasi hiyo kwa madai ya kuwapo kwa ushirikiano hafifu miongoni mwa wabunge na serikali.

Aidha, taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo zinaeleza kuwa viongozi wa kamati hiyo wamejikuta wakikosa ushirikiano kutoka serikalini kutokana na kusudio lao la kutaka kwenda Gereza Kuu la Arusha (Kisongo) kumuona Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati akiwa amewekwa mahabusu.

Waliojizulu ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Peter Kafumu na Makamu wake, Vicky Kamata, wote wakiwa ni wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku uongozi wa Bunge ukithibitisha kupokea barua zao za kuachia ngazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Dk. Kafumu alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na changamoto mbalimbali.

Dk. Kafumu ambaye pia ni Mbunge wa Igunga, alisema kamati hiyo imekuwa ikifanya kazi kubwa na mara nyingi inakumbana na changamoto lukuki.

"Mtakumbuka tumetembelea bandari, tumeenda Arusha na vituo vingi vya uwekezaji, lakini pia mtakumbuka wakati tunahitimisha taarifa ya mwaka," Dk. Kafumu alisema. "Kwa kweli nilieleza changamoto nyingi ambazo serikali inazo katika kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda."

Alisema kamati iliona inahitaji kuwa na mtazamo wa pamoja zaidi kama kamati kwa serikali badala ya kuwa na mtazamo wa mtu mmoja mmoja.

"Kulikuwa na changamoto nyingi, nyingine ni uelewa wa viongozi na wananchi wenyewe. Jambo la viwanda ni la kufa na kupona, nilisema na kuna wengine hawaelewi sawasawa. Kwa hiyo, unaposhauri kuna wengine wanaona tofauti," alisema.

Aliongeza kuwa wamekuwa na changamoto hiyo na wakati mwingine wanapishana kimtazamo na serikali na kuonekana kama wanaisema vibaya serikali hata pale lengo lao linapokuwa kuieleza serikali ili kufanikisha dhamira hiyo.

"Nimeona ni vizuri tunapoanza mwaka wa pili wa bajeti (ya serikali ya awamu ya tano), niyaseme haya maneno. Kumekuwa na ushirikiano hafifu miongoni mwa sisi wabunge na serikali na wakati mwingine unasema jambo, mwingine anakuwa tofauti na wewe," alisema.

Kamishna wa madini wa zamani huyo alisema kutokana na changamoto hizo, yeye na makamu wake wameona kuna haja waachie nafasi zao.

Mbali na kutopata ushirikiano, Dk. Kafumu alitaja sababu nyingine kuwa ni kukosa muda wa kukaa jimboni kwake na kushindwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani na kamati za fedha.

“Ukiwa mwenyekiti (wa kamati ya kudumu za Bunge), unapewa kazi kubwa, zingine za kuiwakilisha nchi ambazo unapewa na Spika.

Nimejikuta jimboni napungukiwa nafasi ya kufanya na hii imenifanya nitazame upya kwenye nafasi yangu hii nyeti yenye kuhitaji nchi ifike kwenye viwanda," alisema.

"Nimekosa nafasi mimi kama mbunge wa Igunga ya kukaa na wananchi wangu na kumekuwapo na malalamiko mengi kule ya kwamba 'umepewa kazi kubwa umekaa huko huko'.

"Hii nafasi ya uenyekiti nataka niache na nimeshazungumza na Spika na nikitoka hapa naenda kuwasilisha barua yangu ya kuacha uenyekiti wa kamati ili nipate nafasi ya kutumikia nchi hii nikiwa Mbunge wa Igunga.

"Moja ya sababu ni kama wananchi nimewaacha kidogo, nikirudi nitakuwa na uhakika wa kugombea 2020/25 lakini nikiacha, wapo vijana wanapita kule tena kwa nguvu sana, hivyo ningependa niwe karibu na wananchi.

“Kwenye viwanda nilishasema tusipotengeneza mkakati wa pamoja kama serikali wa kuipeleka nchi kwenye Tanzania ya viwanda, hatutaweza."

Alisema viongozi wa kamati hiyo waliingia madarakani Novemba 2015 na wameifanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu kuisaidia nchi kufikia malengo ya kuwa nchi ya viwanda.

"Tulipewa kazi kubwa mno. Kati ya kamati ambazo zina kazi kubwa, ni sisi (Kamati ya Viwanda) kwa sababu mpango wa maendeleo wa miaka mitano, dhamira yake kubwa ni kuipeleka nchi kuwa ya viwanda na Bunge kwa kusaidiana na serikali kuhakikisha tunaipeleka nchi huko," alisema Dk. Kafumu.

Alisema wapo wabunge wengi wazuri ambao wanaweza kushika nafasi aliyoiacha na kuongoza vizuri huku akikiri kuwa uamuzi wake unaweza kuwakatisha tamaa wajumbe kwa muda lakini hautakuwa na madhara makubwa.

Dk. Kafumu aliishauri serikali kuwa ni lazima kuwapo na mazingira mazuri kwa wawekezaji wanapokuja kuwekeza nchini kwa kuwa bado kuna changamoto ambazo zinawafanya wengine kushindwa kuwekeza.

Kwa upande wake, Kamata ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki, alisema katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kuiongoza kamati hiyo, kazi yao ilikuwa kuishauri serikali kazi ambayo wameifanya.

"Kutokana na changamoto mbalimbali ambazo si vizuri kuzisemea hapa, binafsi nimeona nijiuzulu nafasi hii ili kutoa nafasi kwa wabunge wengine kuongoza," alisema Kamata ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu.

Kafumu anakuwa mwenyekiti wa pili wa kamati kujiuzulu baada ya Andrew Chenge.

Chenge alijiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Bajeti Januari 2015 akidai kulinda heshima yake baada ya kuibuka kwa kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya sh. bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

KUMUONA LEMA 'SELO'
Taarifa ambazo Nipashe ilizipata kutoka ndani ya kamati hiyo jana jioni, zilieleza kuwa mbali na sababu walizozitoa, Dk. Kafumu na Kamata hawajafurahishwa na shutuma za usaliti dhidi ya CCM kutokana na kutaka kwao kwenda kumsalimia Lema wakati akiwa mahabusi wa gereza la Kisongo.

"Lema ni mjumbe wa kamati yetu. Kwa hiyo viongozi wetu (Dk. Kafumu na Kamata) waliona kulikuwa na haja ya kutumia busara kwenda kumuona na kumjulia hali mjumbe mwenzetu wa kamati ambaye alikuwa mahabusu jijini Arusha," mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo (jina tunalihifadhi) aliiambia Nipashe jana.

"Hakuna aliyekwenda kumuona Lema, lakini ikaonekana kitendo kumbe ilikuwa ni usaliti kwa CCM. Imetushangaza maana lengo halikuwa kumuona Lema kama mbunge wa upinzani, bali mjumbe wa kamati yetu," aliongeza mjumbe huyo.

Alipotafutwa na Nipashe jana kuzungumzia suala hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alithibitisha kupokea barua za viongozi hao kumtaarifu kuwa wamejiuzulu katika nyadhifa zao.

"Ni kweli, nimepokea barua za kujiuzulu kwao. Sababu za kujiuzulu kwao ni vyema wakaulizwa wao wenyewe," Ndugai alisema.

Katika mkutano uliopita wa Bunge, Dk. Kafumu alikiambia chombo hicho cha kutunga sheria kuwa kamati yake haipati ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kushauri mamlaka ya uteuzi imuongezee Naibu Waziri.

Akihitimisha mjadala wa taarifa ya kamati hiyo bungeni Februari 9, Dk. Kafumu alishauri Rais John Magufuli amuongezee msaidizi waziri huyo ili kumpunguzia majukumu aliyo nayo ambayo pengine yanamlazimu kutoipa ushirikiano kamati yake.

"Waheshimiwa wabunge, mimi labda nimuombe Rais amuongezee msaidizi, inawezekana Mwijage ana shughuli nyingi sana.

Tuweze kumpata waziri kirahisi, vinginevyo kamati inafanya kazi peke yake na hii siyo sawasawa," Dk. Kafumu alisema siku hiyo.

Alisema kamati ilikuwa haina taarifa yoyote kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa viwanda zaidi ya 1,000 vilivyobainishwa na waziri.

“Waziri hashirikiani na kamati vizuri kwa sababu tungekuwa na habari ya kufunguliwa hata Kiwanda cha Mkuranga, Mwenyekiti wa kamati angeenda au mjumbe mmoja (na) habari tungekuwa nazo," alibainisha.

Video: Hii Ndiyo Sababu ya Wabunge Dalaly Kafumu na Vicky Kamata Kujiuzulu

$
0
0
BAADA ya jana Machi 20, 2017, Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda na Biashara, Dkt. Dalaly Peter Kafumu, makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vicky Kamata  kujiuzulu nyadhifa zao hizo, mbele uya kamera za Global TV Online, wabunge hao wametoa kauli zao kuhusu kiini cha wao kufanya maamuzi hayo magumu.

Kafumu ni Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM) ambapo Vicky Kamata ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akiwakilisha wanawake wa Mkoa wa Geita.

WASIKILIZE WENYEWE WAKIFUNGUKA
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images