Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Maneno ya Nape baada ya taarifa ya kutumbuliwa Uwaziri asubuhi hii

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri ambapo sehemu ya mabadiliko hayo ni kumteua Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo… na taarifa kamili ndio hii hapa chini kutoka IKULU.


Aliyekuwa Waziri wa Habari Nape Nnauye ameandika kupitia account yake ya Twitter ‘Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!’

Kauli ya TFF Baada ya Mwakyembe kupewa uwaziri wa Michezo

$
0
0


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limempongeza Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Katika taarifa iliyotolewa leo kwa wana habari, imesema kuwa shirikisho hilo linaamini chini ya uongozi wake mahiri Tanzania itapiga hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya michezo.


Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi kupitia mtandao wa twitter amesema "TFF inampongenza Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Tunakuombea mafanikio makubwa.Amina."

Kuhusu Nape Nnauye, CUF kutangaza hatua nzito

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI


Chama cha Wananchi CUF kimepokea taarifa ya hatua ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kumuondoa Mheshimiwa Nape Nnauye katika nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa mshtuko na masikitiko makubwa.


Mhe. Nape ameondolewa kwenye Baraza la Mawaziri kibabe na bila aibu kutokana na kusimamia Haki, Uhuru, Uwajibikaji, Nidhamu na Maadlili ya uendeshaji wa vyombo vya habari nchini jambo ambalo ni jukumu la msingi la Wizara yake.


Sote tunatambua kwamba Utenguzi huo unatokana na Mhe. Nape kufuatilia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha Clouds Media Group kinyume na taratibu, maadili na Nidhamu ya utendaji wa majukumu yake. kitendo hicho pia ni kosa la jinai lisilovumilika.


Kwa niaba ya Chama cha Wananchi CUF, napenda kutumia fursa hii kulaani mwenendo wa Rais Magufuli wa kuitumia nafasi yake kwa namna inayokosa BUSARA na HEKIMA ya uongozi kwa TAASISI ya URAIS.


Kitendo cha Rais kumlinda mtuhumiwa ambaye amefanya makosa ya wazi kabisa kinadhihirisha namna Rais asivyo na utayari wa dhati na uwezo wa kusimamia nidhamu ya watendaji serikalini.


Huko nyuma na mara kadhaa, Rais Magufuli alichukua hatua za haraka sana kuwafuta kazi watumishi na watendaji wa serikali waliofanya makosa madogo mno hata kama ilikuwa ni kimatamshi tu au maamuzi ya bahati mbaya.


Mifano mizuri ni pamoja na Mhe. Anne Killango (aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga), Dr. Mwele Malecela (aliyekuwa anaongoza taasisi muhimu ya utafiti wa magonjwa ya binadamu), Wilson Kabwe (Mkurugenzi wa Jiji la Dar Es Salaam) ambaye alituhumiwa mkutanoni na kufukuzwa hapo hapo bila kuwepo wala nafasi ya kujitetea.


The Civic United Front (CUF) inashangazwa na maamuzi ya sasa ya Rais Magufuli ya kumlinda mtuhumiwa wa makosa makubwa na ya wazi kabisa na kisha kumfukuza kazi Waziri aliyekuwa akitekeleza wajibu wake ili kulinda heshima ya serikali.


Kwa kitendo hiki cha Rais, CUF inaungana na watanzania wote kuamini kuwa Rais Magufuli hana nia njema ya kurejesha nidhamu serikalini, na kwamba yuko tayari kuwalinda vijana wake wachache kuliko kuilinda serikali na heshima ya nchi na Taasisi ya Urais. Rais anashusha hadhi ya Ikulu na sasa ikulu imegeuka kuwa mtetezi mkuu wa watumishi waovu wa umma.


CUF itatangaza hatua nzito hapo baadaye, kwa niaba ya chama natumia fursa hii kumfariji na kumtia nguvu Mhe. Nape kwa ujasiri aliouonyesha na kusimamia kile ambacho ni haki kwa Taifa, wananchi na sekta ya habari.


Namuomba asirudi nyuma kutetea haki za watanzania wote na kamwe asikatishwe tamaa na kitendo hicho kilichokosa utu na heshima, na kujali mchango mkubwa wa kisiasa ndani ya Chama chake na serikali ya awamu ya Tano.


CUF inaungana na watanzania wote kulaani kitendo hicho na kwamba tutakutana pia na vyama washirika katika UKAWA ili kuamua hatua kubwa za pamoja dhidi ya ukosefu wa haki na Demokrasia nchini na matumizi mabaya ya mamlaka.


"CUF NI TAASISI IMARA YENYE VIONGOZI MAKINI"

HAKI SAWA KWA WOTE


JULIUS MTATIRO

MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI 

CUF-TAIFA.

23 Machi, 2017.

Hatimaye Barnaba Akubali Tetesi za Kuwa Ameachana na Mkewe

$
0
0

Barnaba amefunguka kuhusiana na mahusiano yake na mama Steve kwa sasa.

Wiki chache zilizopita muimbaji huyo alidaiwa kuachana na mzazi mwenzake huyo ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, hitmaker huyo wa Lover Boy amesema, “Kwa sasa siko kwenye maelewano mazuri na mama watoto wangu. Sio kwamba tumeachana au tumetengana sitaki kusema hivyo.”

“Siwezi kusema simpendi mwanamke niliyepata nae mtoto [mama Steve],yule ameshakua kama ndugu yangu.Namrespect sana mama Steve ila kila mtu anaendelea na maisha yake na hatutaki kutengeneza picha mbaya kwa mwanetu,” ameongeza.

Wakati huo huo Barnaba amesisitiza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Lonely’ ambao ameuachia leo haujamgusa mtu yoyote na wala hausiani na maisha yake.

Nape - Hawa ni Wapuuzi tu,Wananizuia Kuongoea Kwa Kunitolea Bastola,Nimepigana Kuiweka CCM Madarakani Alafu Mnaleta Ujinga Hapa...!!!

$
0
0

Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.

Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu 

Mimi ndo nlisimama kuiinua CCM, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, mimi nlishawahikufukuzwa CCM

Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepandambegu ya kupigania haki, Tanzania ni yetu nchini yetu. Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka. 

Lengo la kuja hapa ni kumshukuru rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari. 

Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli 
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia 

Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni 
Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena

Tundu Lissu: Jeshi la Polisi Lirudishe Simu Yangu, Liache Kuingilia Mawasiliano Yangu...!!!

$
0
0

Nimetoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar sasa hivi. Polisi wamekataa kunirudishia simu yangu waliyoinyang'anya kwa nguvu tarehe 6 Machi, siku waliyonikamata nikiwa mahakamani Kisutu.

Mimi sijatuhumiwa wala kushtakiwa kwa kosa lolote la mtandao chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao au Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Kiposta.

Badala yake nimeshtakiwa kwa makosa ya uchochezi yanayohusiana na kauli zangu juu ya Serikali ya Rais Magufuli. Aidha, nimeshtakiwa kutokana na msimamo wangu na kauli zangu juu ya siasa za Zanzibar na masuala ya Muungano.

Kwa sababu hizi, Jeshi la Polisi halikuwa na, na halina, sababu wala haki ya kuchukua simu yangu na kuendelea kukaa nayo hadi sasa, siku 17 baadae.

Nimepata taarifa kwamba tangu walipoichukua kwa nguvu karibu wiki tatu zilizopita, simu hiyo imekuwa inaonekana inatumika kwa mawasiliano ya whatsapp.

Maana yake ni kwamba polisi wanasoma na au kusikiliza mawasiliano yangu ya simu na ya kielektroniki. Hii ni kinyume cha sheria za nchi yetu.

Simu hiyo ni chombo changu cha mawasiliano ya kikazi na binafsi. Kama mbunge, ninaitumia simu hiyo kwa ajili ya mawasiliano yangu na wananchi walionichagua na viongozi wengine wa kiserikali na kichama.

Jeshi la Polisi halina haki ya kujua au kuingilia mawasiliano hayo.

Kama wakili ninatumia simu hiyo kwa ajili ya mawasiliano na wateja wangu, wengi wao wakiwa na kesi mahakamani dhidi ya Jeshi la Polisi au Serikali hii.

Mawasiliano hayo yanalindwa kwa mujibu wa sheria na polisi hawana sababu wala haki ya kujua au kuingilia mawasiliano hayo na wateja wangu.

Vile vile ninatumia simu yangu kwa mawasiliano yangu binafsi na familia yangu, marafiki zangu na jamaa zangu wengine.

Mawasiliano haya nayo yanalindwa na Katiba yetu na polisi hawana sababu wala haki ya kujua au kuingilia mawasiliano hayo binafsi.

Kwa vyovyote vile, kitendo cha Jeshi la Polisi kuchukua na kuendelea kuishikilia simu yangu bila sababu wala haki ni mfano mwingine wa matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi ya Jeshi hili la Polisi.

Badala ya kushughulikia wahalifu wa wazi kama akina Daudi Bashite na wenzake, polisi wetu wanahangaika na viongozi waliochaguliwa na wananchi wanaotumia haki na wajibu wao kikatiba kuikosoa serikali ya Rais Magufuli kwa sababu ya matendo yake ya hovyo.

Ninafahamu polisi wanafikiri kwamba kwa kunifanyia vitendo hivi basi nitaogopa na kulegeza msimamo wangu katika masuala mbali mbali yanayolisibu taifa letu.

Ninawaomba wajiulize kwa nini imeshindikana hadi sasa kulegeza msimamo wangu huo kwenye masuala hayo, licha ya kunikamata na kuninyanyasa mara nyingi kwenye vituo vya polisi na mahakamani. Sitishiki na sitatishika na mambo yao haya.

Hata hivyo, naomba niseme wazi ili mwenye kusikia na asikie. Vitendo hivi vya Jeshi la Polisi havifai na vinatakiwa kukoma kabisa. Polisi wanirudishie simu yangu mara moja na bila masharti yoyote.

Ninaendelea kutafuta mawasiliano ya IGP Mangu na wakubwa wenzake ili wanieleze kwa nini simu yangu inashikiliwa na maofisa wao.

Endapo na wao watashindwa kutoa maelekezo sahihi kwa waliochukua simu yangu na wanaendelea kukaa nayo, nitalazimika kwenda Mahakama Kuu ili kuomba mahakama iingilie kati na kutamka kama ni sahihi kisheria kwa mapolisi wa nchi hii kuingilia mawasiliano ya sisi wananchi kwa namna ya hovyo namna hii.

Naomba mnaopata ujumbe huu mnisaidie kupaza sauti zetu ili matendo haya mabaya yakome katika nchi yetu.

Wasalaam,

Mh. Tundu AM Lissu

Nape Afanya Mkutano Kiana..Adai 'Niliikuta CCM iko Shimoni Nikaitoa Huko'

$
0
0

Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba nafasi yake ya Waziri wa Habari amepewa Dr. Mwakyembe, hii ni Sentensi hapa chini ya jinsi ilivyokua


"Nataka aliyeinua bastola hapa aje aseme ameiinua kwa sababu gani" - Nape Nnauye


"Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia."- Nape


 "We have nothing to fear, but fear itself."- Nape


"Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola. Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo. Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa."- Nape


"Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka. Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?"- Nape


"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape


"Vijana naomba msimamie haki yenu"- Mbunge Nape Nnauye


"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape


"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape


"Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke."-Nape


"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape

Duh..Huu Hapa Ujumbe Aliopost Bashe Mara Baada ya Nape Nnauye Kutumbuliwa Leo..!!!

$
0
0

You will never walk Alone, I know you, we know you, Justice will prevail no matter how long it will take.

Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It's just beginning of a New journey.
@Nnauye_Nape

Kimenukaa..Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema Atoa Povu Hili Baada ya Nape Kutumbuliwa Leo Asubuhi...!!!

$
0
0

Mchungaji Peter Msigwa Leo Kupitia Ukurasa wake wa Twitter Ameweka azi jinsi alivyolipokea suala la Aliyekuwa WAZIRI  wa Habari sanaa,Utamaduni na Michezo Mhe Nape Nnauye Kutumbuliwa na Rais Magufuli.

Kwa Magufuli bashite ni mhimu  na ni bora kuliko Nape ndani ya chama na serikali! Hongera JPM!

Zitto Kabwe: Rais Magufuli Amemzuia RC Makonda Kutokea Mbele ya Kamati ya Bunge...!!!

$
0
0

Anaandika Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini Mhe Zitto Kabwe. 
Rais Magufuli amemzuia RC Makonda kutokea mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka kujibu tuhuma zake dhidi kudharau wabunge Kama Bunge lilivyoazimia

Hatariii..Wema Sepetu Atoa Povu Hili Baada ya Nape Kuvuliwa Uwaziri na Magufuli...!!!

$
0
0

Kada Mpya wa Chadema,Wema Sepetu naye hakubaki nyuma katika kuonyesha hisia zake ,ambapo kupitia ukurasa ake wa kijamii wa instagram amepot ujumbe unaoonyesha kuwa ameshtusha na tukio la Rais Magufuli Kumvua Uwaziri Mhe Nape Nnauye


A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on

Kimenukaa..Gwajima Ajitwika Msalaba wa Nape Kutumbuliwa,Ataja Chanzo cha Magufuli Kumtumbua Nape Haraka Haraka..!!!

$
0
0

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.

Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha Efm,Gwajima amesema Mkuu wa Mkoa alivamia ofisi za Clouds kwa lengo la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.

"Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.

Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.

Uchambuzi Wa Habari: Nape Hakwenda Na Midundo, Ilikuwa Lazima Aondoke..!!!

$
0
0

Ndugu zangu,

Habari kubwa leo ni Nape Nnauye. Ameondoka kwenye Baraza la Mawaziri.

Kwa tunaofuatilia mambo hii ni habari iliyokuja kwa kuchelewa. Kwangu mimi ni siku ile Rais wa Jamhuri alipoongea Ubungo kwamba Mkuu wa Mkoa Makonda aendelee kuchapa kazi, na baadae Waziri wake wa Habari anatangaza tume kumchunguza Makonda. Nape angemsaidia Rais kwa kuvunja alichokiunda kwa maana ya Tume. Kisha kujiuzuru, basi.

Maana, kwenye Jamhuri, hakuna uwezekano wa jambo kama lile kufanywa na Waziri na akabaki kuwa Waziri. Nape ambaye alipaswa, Kama Waziri wa Habari, kuwapo pia kwenye tukio kubwa kitaifa kama lile la uzinduzi wa ujenzi wa flyovers pale Ubungo mbele ya Rais wa Benki ya Dunia. Angeshiriki, angesikia msimamo wa Rais wake kuhusu RC Makonda, na angekuwa na mawili tu ya kuchagua, kumuunga mkono Rais wake au kujiuzuru.

Nayaona manne makubwa:

1. Kutofautiana kwa Nape na Makonda katika suala la Wema kutajwa kwenye orodha hadi kufikia kupigana vijembe kumekuwa na athari kubwa. Hakuna dhambi ya kutofautiana, lakini, kulikuwa hakuna maana ya kuendelea kupigana vijembe.

2. Tume ya Nape kumjumuisha mhariri ( Balile) ambaye gazeti analoliongoza lilibeba habari dhidi ya Makonda katika siku hiyo hiyo ya kutajwa kwa Kamati na ni mhariri huyo huyo ndiye aliyesoma ripoti. Hilo lilikuwa na walakini mkubwa.

3. Umoja wa ghafla wa watu wasiopikika chungu kimoja kutaka Makonda atumbuliwe ( Rejea goli la mkono). Hili linaleta mitazamo mipya kwamba huenda suala zima lina siasa ndani yake. Kwa pamoja inajengeka dhana ambayo haipaswi kupuuzwa, kuwa zoezi zima lilichukuliwa kwa maslahi binafsi zaidi kuliko linavyoelezwa hadharani. Ni kweli, na tumesikitishwa sana na kitendo cha RC Makonda alichofanya pale Clouds TV.

RC Makonda alilikoroga na alistahili Kukemewa, lakini, hiyo usitutie upofu kushindwa kuyaona mashimo kwenye mchakato wa kushuhulika na mapungufu ya RC Makonda. Mchakato usiwe uliojaa mashaka, na mashaka haya huondolewa kwa wenye kuyashuhulikia kutanguliza weledi na kuweka kando yasiyohusika.

Hata tunapozungumzia dhana ya kugomea habari za RC Makonda si sahihi. Kimsingi tunaweza kugomea habari za Makonda lakini si RC Makonda. Habari za RC Makonda ni habari zenye kuhusu Serikali na Wananchi. Habari za Makonda kama Makonda, iwe amekwenda kucheza muziki au harusini hizo zinabaki kuwa habari za Makonda.

4. Hili la nne ndio kosa kubwa alilofanya Nape; Kuendelea na zoezi lake hata baada ya Rais 'kufunga mjadala'. Kama Waziri wa Habari, Nape ni Msemaji Mkuu wa Serikali inayoongozwa na aliye madarakani. Katika kazi hiyo, na kwenye Jamhuri, wakati mwingine Waziri wa Habari husema ' Kama kasuku' , kile kilichosemwa na Rais, hata kama ukikaa naye pembeni anaweza kukwambia kuwa hakubaliani nacho.

Hitimisho, uamuzi wa kumtoa Nape kwenye Baraza ni sahihi ili kurudisha nidhamu na mtiririko mzuri wa utendaji kiserikali.

Nape Nnauye ameshindwa kuendana na midundo au kusaidia kupanga midundo ya kwenda pamoja na aliye juu kwenye Jamhuri na Serikali kwa ujumla.

Katika wakati nchi iko kwenye utekelezaji wa miradi mingi midogo na mikubwa huku ikikopa kugharamia hayo. Ni mikopo ya Watanzania kuilipa, si ya Magufuli. Inahitajika hamasa kubwa ya kuwafanya Watanzania wafanye kazi. Waziri wa Habari ni mmoja wa watu wa kuifanya kazi hiyo.

Ni imani yangu, kuwa Nape ni kijana, mahiri na mwenye ushawishi mkubwa. Anahitaji kutulia na kutafakari namna atakavyoweza kuisaidia Chama chake na nchi kwa nyakati zijazo.

Maggid Mjengwa.

Viongozi, Mastaa Watoa ya Moyoni Kufuatia Nape Kupokonywa Uwaziri, Wengi Wamuita ‘Shujaa’...!!!

$
0
0

Alhamis hii jua limechomoza likiambatana na mshtuko mkubwa kwa wananchi wengi wa Tanzania.

Mshtuko huo umetokana na taarifa ya mheshimiwa Nape Nnauye kupokonywa nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii imekuwa habari yenye mpasuko mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nape ameonekana kuwa mtetezi muhimu wa vyombo vya habari kufuatia kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha nzito.

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokea ripoti toka kwenye kamati aliyokuwa ameiteua kufanya uchunguzi wa tukio hilo, Nape ameondolewa na kuacha sintofahamu kubwa kwenye mkasa huo.

Mastaa, viongozi na wananchi wametoa maoni yao ambao mengi yanafanana – hawajependezwa na kilichotokea huku wengi wakimwelezea Nape kama shujaaa.

Haya ni baadhi yao:

Zitto Kabwe

Nimezungumza na mbunge wa Mchinga @Nnauye_Nape na kuthibitisha kuwa Ni Kweli ameondolewa kwenye Uwaziri. Nape ni Shujaa wa kizazi chetu

Irene Kiwia

The key resource of ordinary citizens is numbers. And justice will reign on earth and truly will the voice of the people be the voice of God. When there is true awakening of the people, in numbers, it forms the real and conscious public opinion.

B12

Nitakua naota eti……. Ngoja nilale tena then niamke! Maana hii si mara ya kwanza kukutana na ndoto mbaya ya kutisha!!

Nchakalih

Kaka @Nnauye_Nape nakushukuru kwa kunipa mfano wa kutumia kumfundishia mwanangu zion somo la uzalendo! HISTORY will JUDGE you RIGHT!! 👊👊

Halima Mdee

Naamini ni UZUSHI!!

Edo Kumwembe
Sidhani kama Nape anajali…alilitafuta hili kwa nguvu zote…sidhani kama anajali

Bonge la Nyau

Huyu ni shujaa wangu……

Wema Sepetu

We will Surely Miss U as Our Minister… Tulishakuzoea. Such a way to start Your Morning.. Lets wait for what’s NEXT…. This Is Tooo Much Jamani. This Country Be Full of Surprises Nowadays…. Smh.. Never Knew Nchi ina MaRais wawili… Now I know…. Smh…

Idris Sultan

Raisi akashika Jiwe na Almasi akavipimaaaaaaaa aksema embu katupeni almasi ina’ngaa kijinga jinga tu nimeiambia ing’ae kwani.

Madee‏ 
Sad newz😭😭

Masoud Kipanya

Haya ni mawazo yangu… Ningekuwa @Nnauye_Nape ningekaa KIMYA kabisa

Diva

Nimepata mshtuko wa mwaka 🤥. Kama Kijana Mpenda Haki na Mpenda Maendeleo na Ninaejitegemea Nimepata Mshtuko wa Mwaka , Nimejiuliza maswal Kwa uchungu Chozi limetoka 🤥🤧

Peter Msigwa

Kwa Magufuli bashite ni mhimu na ni bora kuliko Nape ndani ya chama na serikali! Hongera JPM!

Mwana FA

(Alitweet muda mfupi kabla ya habari za kuondolewa uwaziri (Toka mwanzo kabisa wa haya maswahibu,kaka yangu @Nnauye_Nape anaonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa..kisiasa na kibinadamu. Anajua umuhimu wa kufanya ‘vita’ dhidi ya mambo yasiyo sahihi kwa jamii bila dhulma na ukiukwaji wa sheria,na hayumbi kwy kusimamia ukweli.
NA HARINGI 😀..SALUTE kaka @Nnauye_Nape …najivunia kusema nakujua,ubarikiwe ndugu yangu)

Baada ya habari hiyo kufahamika alitweet: Aisee..

Aika

Its not dictactorship its being a coward #JustSaying running frm people challenging u 🇹🇿


Quick Rocka

I don’t feel proud kuwa mtanzania anymore….Tunatangazaje na kusifia nchi ambayo viongozi wanaosimamia ukweli na sheria wanaondolewa…Huku wanaozingua wanaendelea kupeta…Nape alikuwa waziri sahihi kabisa kwetu wasanii,wanamichezo na wanahabari.

Harmorapa Atimua Mbio Baada ya Kuiona Bastola Aaliyotishiwa Nape..!!!

$
0
0

Harmorapa ni bingwa wa kumendea headlines kwenye matukio makubwa yanayowahusu watu wenye majina. Hata hivyo Alhamis hii mambo yalitaka kumtokea puani.

Rapper huyo mwenye visa alitimba Protea Hotel jijini Dar es Salaam ambako mheshimiwa Nape Nnaye alikuwa ameenda kuzungumza na waandishi wa habari, lengo lake kumpa pole kwa masahibu yaliyompata – kuvuliwa uwaziri.

Hata hivyo wakati anakimbia kwenda kumpa mkono wa pole Nape aliyekuwa kwenye kukuru kukara na wana usalama wasiokuwa na magwanda waliokuwa wakimzuia waziri huyo wa zamani kutimiza azma yake, macho ya Harmorapa yalitua katika chombo cha hatari chenye uwezo wa kutoa pumzi ya mwanadamu – bastola aka cha moto na kujikuta akitimua mbio kuokoa maisha yake.

Video inaonesha mwanausalama huyo akichomoa cha moto na kuwafanya watu waliokuwa jirani kupata hofu ingawa ni Harmorapa ndiye aliyeonesha kuogopa zaidi kiasi cha kutamani kupaa kutoka kwenye eneo hilo.

Haijulikani ‘Kiboko huyo wa Mabishoo’ alisimamia wapi baada ya kutimua mbio hizo, lakini mashuhuda waliokuwepo wanatonya kuwa jamaa alilala mbele kwa speed za Usain Bolt – chezea bastola wewe!

Kutokana na kitisho hicho, Harmorapa alishindwa kumpa mkono wa pole mheshimiwa Nape japo alifanikiwa kupata interview mbili tatu za waandishi waliomshuhudia – mission accomplished.

Hiyo si mara ya kwanza kwa mkali huyo wa social media kutinga kwenye matukio ya watu wengine na kuchukua spotlight. Hivi karibuni rapper huyo alienda pia kwenye studio za Clouds FM kuwapa pole baada ya studio zao kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Nimeona Utupu wa Mke wa Mpangaji Mwenzangu..Sasa Imekuwa Tabu kwa Usumbufu Anaonipa..Ushauri Jamani Nifanyaje....!!!

$
0
0


Ilikuwa wiki moja iliyopita.Wakati wa asubuhi naingia bafuni kuoga kumbe kulikuwa na mke wa jirani yangu ambaye pengine hakusikia ujio wangu nami sikujua kama yumo.
  
Ile anataka kutoka tu pale mlangoni,kanga yake ikaanguka na akabaki mtupu Macho hayana pazia niliona utupu wake nae aliona kuwa nimeona.Ile tu anajizoazoa kujisitiri akateleza akaanguka ikabidi nimsaidie kumuinua , nikamwinua huku akiwa uchi wa myama na kuhakikisha hajaumia popote ...then nikamfunika na kumwambia pole nikaondoka kiistaarabu.
  
Ila sasa naona ustaarabu wangu uliniponza sasa naona ananifanyia vituko Mwanzo nilifikiri yameisha,alianza kwa kukwepesha macho na mimi,,mara akajenga mazoea na mimi.Na sasa vituko vimezidi,mara sms za ajab,wakati wote anataka kujua niko wapi na nafanya nini, siku ingine ananiletea chakula alichopika nile..
  
Kwa tabia na msimamo wangu naheshimu sana ndoa za watu.Nishaurini nifanye nini kumuepuka ? Nimepanga chumba hapa na nimelipa kodi ya mwaka mzima,ni jirani tu chumba cha nne toka kwangu...

Tiririka Upendavyo..Nini Kinawafanya Wanaume Kugeuka Pindi Wnapopishana na Mwanamke Mwenye Makalio makubwa?..!!!!

$
0
0

Natumaini mu wazima wa afya njema.

hili ni swali linalonitatiza kila siku ni sababu zipi zinazopelekea mwanaume kugeuka na kumwangalia tena mwanamke mara tu wanapopishana hasa kwa wale wenye makalio makubwa...??

je ni sababu zipi zinazopelekea kutokea na  kuendelea kwa hali hiyo?

Mada Tujadili..Ni Kweli Mke Asipopewa Heshima Hawezi Kumthamini Mumewe Hata Iweje..?Karibu Kuchangia...!!!!

$
0
0

Kuna wanaume ambao kwa kutokujua wanadhani mwanamke anachohitaji ni ‘fidia’ baada ya kuvunjiwa heshima, hivyo huwa wanawavunjia heshima wake zao na baadae kujitoza ‘fidia’ kwa kuwanunulia zawadi kubwakubwa wanawake hao.
  
Wanawake huwa wanapokea zawadi hizi, lakini hii haina maana kwamba ndoa itaendelea kuwa ya amani na upendo. Mwanamke hata kama atapewa dhahabu yote duniani, kama atajua kwamba mumewe hamheshimu, ni wazi kwamba hatakuwa na furaha ya ndoa. Miongoni mwa mambo sita ambayo mwanamke akiyakosa huhisi kutindikiwa na kukosa furaha ya uhusiano ni heshima.
  
Kama haki ya mwanamke hailindwi na mwanaume, hata kama kuna kitu gani, ndoa ni lazima itakuwa ni ya kubahatisha. Mwanume anapokuwa na uhusiano wa kipapenzi nje ya ndoa yake, mwanaume anapomzuia mkewe kuamua masuala yake mwenyewe ambayo ni haki yake, kamwe mwanamke hawezi kuridhishwa na hayo na hata kama ndoa imejaa watoto wazuri wenye afya na akili na fedha nyingi zimeipamba nyumba yake.
  
Kama mwanaume ataonyesha kutojali kuhusu matamanio au ndoto za mkewe kamwe mwanaume huyo asitarajie kuwa mkewe atakuwa na upendo naye. Mwanamke huwa anatamani sana kuona mumewe anajali na kuyapa uzito matamanio au ndoto za mkewe. Kwa mfano mwanamke anapoonyesha kwamba, angependa kuanzisha shughuli labda ya biashara au wangependa wapate mtoto na mwanaume akaonyesha kutojali kuhusu matamanio hayo, kamwe mwanamke hawezi kutulia na kuwa na amani.
  
Kuna vitu au mambo ambayo mwanmke anayahitaji maishani, mahitaji hayo ni mengi yakiwemo yale ya msingi katika maisha na yale ya kawaida. Inatosha kusema kwamba, mwanamke anapogundua kwamba mumewe hajali juu ya mahitaji yake huwa hajisikii vizuri.
  
Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba mwanamke huhitaji heshima katika utashi na matamanio yake. Anapogundua kwamba utashi na matamanio yake havizingatiwi na mumewe hawezi hata mara moja kumkubali mume huyo. Kumkubali hapa ina maana ya kumkubali na kumtambua.
  
Hapo ndipo tatizo ambalo ni la upande wa pili huanza. Kwa maumbile mwanaume huwa anataka sana mkewe akimuonyesha kwamba anamthamini na kumtambua. Labda hii inatokana na ubabe wa asili wa wanaume ambapo kila wakati angependa kuona mwanamke akimgwaya na kuonyesha kwamba anamtambua kama ‘mwokozi’ wa aina fulani.
  
Kama mwanamke anataka kumfanya mumewe amsikilize na kujali matamanio na ndoto zake anachotakiwa kufanya ni kumuonyesha mumewe kwamba anamthamini na kumtambua. Kwa mfano mwanaume anapofanya jambo ambalo hata kama halina faida, lakini halina madhara, inabidi mkewe aonyeshe kuzitambua juhudi hizo na kuonyesha kwamba, mume huyo anajitahidi sana katika kufanya mambo yake.
  
Mwanaume anahitaji sana kuona mwanamke akimsifu kwa juhudi anazofanya, iwe ni za kitabia au za shughuli. Mwanaume anapokuwa na tabia nzuri, ni lazima mwanamke atafute kila njia ya kumuonyesha kwamba ameitambua tabia yake hiyo, kamwe asimuonyeshe kwamba juhudi anazofanya ni kupoteza muda. 

Pale ambapo mwanaume huonyesha heshima kwa mkewe kwa kuzijali ndoto na matamanio yake ya kimaisha, huhitaji sana kuonyeshwa kwamba heshima yake hiyo imepokelewa. Kwa kawaida mume anapotimiza wajibu wake lazima mke naye atimize wajibu wake.
  
Kuna wakati na karibu mara zote, mwanamke huwa anamlaumu mwanaume na mwanaume kumlaumu mwanamke kwa kila mmoja kudhani kwamba mwenzake ndio chanzo cha matatizo. Hii ni kwa sababu wote wawili hawajui namna nadharia hii inavyofanya kazi. Huyu anataka kuthaminiwa wakati hampi mwenzake heshima na huyu anataka kupewa heshima wakati hamthamini mwenzake.
  
Ili kuondoa kulaumiana huko inabidi kila mmoja ajue wajibu wake, kwani kama mmoja ataanza kumpa mwingine kile anachohitaji ni wazi huyu mwingine atajibu kwa kumpa mwenzake kile kinachomstahili mwenzake ambacho ni heshima.

Fahamu Vigezo Sita Vikubwa Vinavyoweza Kumfanya Mwanamke Kukukimbia Au Kukuacha Kabisa...!!!

$
0
0

1. Wakikosa attention yako. Wasichana hupenda pale wanapofahamu kuwa unawasikiliza na unafahamu nini wao wanahitaji. Kama kutakosekana mawasiliano mazuri na atagundua hilo atauona uhusiano huo haumtimilizii haja zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize anapoongea. Kama akiona hapati penzi analolihitaji atatafuta mwingine ambaye yupo tayari kumtimizia.

2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo katika mahusiano hivyo anategemea mvulana uheshimu hata kwa chochote kidogo anachokufanyia. Mfanye agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.

3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa katika mahusiano yako hata kama una uwezo wa kushughulikia lakini wewe unaona njia sahihi ni kutoka nje kuwa na mahusiano na msichana mwingine ukidhani ndio unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.

4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda kuona kuwa wanapendwa wanathaminwa na wapenzi wao wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna conection ya hisia za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo

5. Hawapendi kusikia kuhusu mapenzi mara kwa mara wasichana hupenda kutumia muda mrefu na wapenzi wao bila kusikia neno la kuwataka wafanye mapenzi kama ukiwa nao na ukawataka kimapenzi mara kwa mara watakuwa wanakuavoid hata utakapokuwa ukiwagusa.

6. Unapomcontrol sana
msichana humpenda mvulana atakayemlinda na kujiona yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake mengine anapenda uhuru.

Katuni 5 Bora za Leo

$
0
0

Bonyeza hapa kuzitazama katuni hizo tano bora za Siku Leo
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images