Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

TUCTA "KIMA CHA CHINI CHA MFANYAKAZI KIWE 750,000"

$
0
0
Wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kuhutubia wafanyakazi katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeitaka Serikali kupandisha kima cha chini hadi kufikia Sh750,000.

Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya alisema jana kuwa wanahitaji kuona wafanyakazi wakipata kiwango cha mshahara kinachokidhi mahitaji.

Alisema kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumuko mkubwa wa bei uliopo kwa sasa, kiwango hicho angalau kinaweza kukidhi mahitaji muhimu ya wafanyakazi wa kima cha chini, ikiwamo malazi, mavazi, chakula na mahitaji ya afya.

“Katika hali halisi, tunaona namna bei za vitu muhimu ikiwamo umeme, maji, mafuta, gharama za vifaa vya ujenzi, nyumba vyakula na gharama nyingine za maisha zimekuwa zikipanda maradufu katika miaka ya karibuni, lakini hakuna namna inayofanyika kuleta unafuu kwa wafanyakazi.

Kimsingi kima cha chini lazima kiongezwe ili kikidhi mahitaji ya maisha ya wakati huu,” alisema.

WASANII WA BONGO NA WANASIASA NAO WALA NDIZI KUPINGA UBAGUZI WA RANGI

$
0
0

Mtangazaji wa MKASI TV Salama Jabir kupitia page yake ya instagram @ecejay amepost picha ya mastaa kadhaa wa bongo wakiwemo wasanii D-Knob, Godzilla Producer Marco Chali na wengine wakiungana na wabongo kama Mbunge Zitto Kabwe na wengine duniani kupinga ubaguzi wa mchezaji wa Barcelona Dani Alves wa kutupiwa ndizi uwanjani.

LE MUTUZ AFANYA KWELI KWA YULE KIJANA ALIYE SAMBAZA PICHA NA VIDEO ZA UCHI ZA ALIYEKUWA DEMU WAKE.

$
0
0
HUYU NDIYE KIJANA WA MIAKA 27 ANAYEITWA ELIMRINGI MOSHI MWANAFUNZI WA MWAKA 3 IFM ALIYEMREKODI KWA SIRI BILA KUJUA MSICHANA WAKE ANAYESOMA NAYE NA KISHA KUTOA PICHA NA VIDEO YA UCHI WA MNYAMA WA MSICHANA HUYO HUKU YEYE AKIJIFICHA BILA KUONEKANA ILI KUMKOMOA BAADA YA KUMUACHA. KAMA UMECHUKIZWA NA THIS PLEASE ISAMBAZE KILA KONA YA MITANDAO ILI HUYU KIJANA NAYE AINJE JOTO YA JIWE ALIYOMFANYIA MWENZIWE AMBAO NI UNYAMA WA AJABU SANA HUYU KIJANA NI MNYAMAM ANAYESTAHILI KUOZA JELA TU, AMESHALALA RUMANDE SIKU 2 YUPO KWA DHAMANA KESI YAKE INAKUJA SOON NITAWAJULISHA MIMI NINAYE HUYU KIJANA MPAKA NIONE MWISHO!! - LE MUTUZ

KAMA ULIPITWA NA HUO MKASA UNAWEZA TEMBELEA HAPA CHINI..
<<MKASA>>


USHINDI WA NGORONGORO HEROES NI KAMA ZALI LA METANTALI

$
0
0
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ juzi Jumapili ilivuka hatua ya awali ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana lakini timu hiyo haikubahatika kufunga bao hata la kuotea kwenye mechi mbili ilizocheza na Kenya.

Ngorongoro Heroes na Kenya zilitoka suluhu mjini Nairobi wiki chache zilizopita kabla ya kutoka sare ya aina hiyo hiyo kwenye mechi ya marudiano Jijini Dar es Salam. Ngorongoro ilishinda kwa penati 4-3 na kufuzu kwenye hatua inayofuata na ratiba inaonyesha kuwa itavaana na Nigeria katika hatua hiyo ya pili.

Akizungumzia ubutu unaoikabili timu hiyo, Kocha John Simkoko aliliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitafutia timu hiyo mechi nyingi za kirafiki ili iweze kujiandaa vizuri kabla ya mechi ya marudiano na kuwatengenezea vijana hao hali ya kujiamini pindi wanapofika kwenye eneo la hatari la timu pinzani na kuweza kufunga.

Kwa upande wake, Kocha wa zamani wa Azam FC, Stewart Hall aliyekwepo pia kwenye benchi la Ngorongoro Heroes alisema kuwa tatizo la ushambuliaji limekua sugu hapa nchini hivyo kuwataka waalimu na wakufunzi wa michezo kuanzisha program mbalimbali zitakazosaidia kutatua tatizo hilo.

“Ushambuliaji ni tatizo kubwa katika medani ya soka hususani hapa nchini Tanzania, ni vyema walimu wakalitazama hili kwa jicho la pili ili kuweza kulitatua,” alisema Hall anayefanya kazi kwenye Mradi wa Symbion unaohusika zaidi na soka la vijana hapa nchini chini ya usimamizi wa klabu ya Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

WEMA NA DIAMOND WAPEANA MAHABA LIVE BARABARANI..DENDA NJE NJE

$
0
0

Wema Sepetu na Mpenzi wake Diamond Platnumz walionekana maeneo ya Bamaga wakipeana mahaba niuwe live live , Wema alikuwa nje ya gari huku diamond akiwa ndani ya gari Wema alikuja Dirishani na Diamond kuanza kumshika Sehemu za Makalio kabla ya kumvuta na kuanza kudendeka live live huku watu wakishuhudia tukio hilo....Mtajajiju wale wa Team naniino....Team Wema Mpo?

TIMU GANI HAPA BONGO HUWEZI KUISHABIKIA HATA SIKU MOJA?

$
0
0
Timu gani hapa Bongo huwezi kuishabikia hata siku moja?

A: Mbeya City
B: Yanga
C: Simba
D:Azam
E: Nyingineyo, itaje

HII NDIO BONGO, WALIO TIMULIWA MALIASILI WARUDISHWA KAZINI

$
0
0
VIGOGO wa Wizara ya Maliasili na Utalii, waliotimuliwa kazi hivi karibuni na Waziri Lazaro Nyalandu, wamerejeshwa kazini.

Taarifa za ndani ya Wizara zilizofikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa vigogo hao, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Jafari Kidegesho, walikabidhiwa barua za kurejea kazini jana.

Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Wizara hiyo, Nurdin Chamuya ambaye hakukanusha wala kukubali kuhusu hatua hiyo, na badala yake alisema alikuwa katika kikao tangu asubuhi hivyo apewe muda amtafute Katibu Mkuu, Maimuna Tarishi.

Baada ya muda, Chamuya aliwasiliana na gazeti hili na kusema kuwa ameshindwa kuwasiliana na Katibu Mkuu, kwa kuwa yuko katika vikao vya Bajeti na hivyo atatoa taarifa kama suala hilo lipo baadaye. Nyalandu alimuondoa Profesa Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Alisema amechukua hatua hiyo kutokana na kutokuridhishwa na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini. “Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.

“Aidha, ninamuondoa Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dk Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo,” alisema Nyalandu wakati akitangaza hatua hiyo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa watendaji wote waliokaimishwa nafasi za vigogo hao wamepewa barua na Katibu Mkuu kurejea kwenye nafasi zao za zamani. Gazeti hili lilimtafuta Katibu Mkuu, lakini simu yake iliita bila majibu huku simu ya Nyalandu ikikosekana.

"HAIWEZEKANI BADO TUNAMUHITAJI DIDIER KAVUMBAGU YANGA" CHARLES MKWASA

$
0
0
KOCHA Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amesema aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Didier Kavumbagu amefanya haraka kusaini Azam kwani alipaswa kusubiri hadi uongozi wa klabu hiyo kumpa nafasi hiyo.

Kavumbagu ambaye mkataba wake uliisha msimu uliopita, alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Azam juzi kwa ajili ya kuwatumikia mabingwa hao msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkwasa alisema Kavumbagu bado mchezaji mzuri anayemwamini, ndio maana walikuwa wakimtumia katika mechi nyingi msimu uliopita na bado walikuwa wakimhitaji.

“Ni mchezaji mzuri, alikuwa akifanya vizuri na bado tulikuwa tunamhitaji ndio maana tuliweza kumtumia msimu mzima wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amefanya haraka mno,”alisema.

Mkwasa alisema walihitaji kuwa naye lakini kama mwenyewe ameshindwa kuvuta subira na kukimbilia Azam, basi, hawawezi kumlazimisha.

Alisema kwa utaratibu wa Yanga huwa mchezaji anapomaliza mkataba wake, humwita na kuzungumza kumpa mwingine, hivyo, kama angeendelea kusubiri angeitwa na kuongezewa mkataba mwingine.

Kavumbagu alimaliza msimu wa Ligi Kuu akiwa amepachika mabao 13, nyuma ya Mrundi mwenzake anayecheza Simba Amis Tambwe aliyeibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 19.

UNDANI VIFO VYA WATOTO 3 NDANI YA BWANA LA KUOGELEA LANDMARK HOTEL

$
0
0
KUFUATIA vifo vya watoto watatu waliokufa kwa pamoja ndani ya bwawa la kuogelea ‘swimming pool’ kwenye Hoteli ya Landmark, Mbezi Beach jijini Dar, undani  wa vifo hivyo umejulikana, Amani lina kisa kamili.

CHANZO 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, watoto walionusurika kufa ambao  walikuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwenzao ‘bethidei’ aliyejulikana kwa jina la Derrick Mboka, waliwaona marehemu wakielea kwenye maji ya bwawa hilo walilosema kuwa ni la kuogelea watu wazima.

Chanzo kiliendelea kuweka wazi kwamba baada ya kuwaona wenzao wakielea, watoto hao walipiga kelele jambo lililowashtua walinzi wa hoteli hiyo upande wa bwawa ambao walifika haraka kuwatoa marehemu wakiwa tayari wameshafariki dunia huku mtoto mmoja akihangaika kujiokoa.

“Unajua wale watoto sijui nisemeje? Waliingia mle kwenye bwawa, inaonekana walizama, hakuna aliyeweza kuja juu, maji yaliwazidi. Walipokata roho ndipo miili ikaibuka na kuelea, ndipo wenzao wakapiga kelele,” kilisema chanzo kwa masikitiko makubwa.

UZEMBE WATAJWA
Habari zaidi zinadai kuwa sababu kubwa iliyosababisha vifo vya watoto wote watatu ni uzembe uliofanywa na walinzi wa bwawa hilo ambao walidaiwa kutokuwa makini kuwadhibiti watoto wengi waliokuwa wakiogelea karibu na bwawa la watu wazima kiasi cha kutoka na kuingia huko.

MAMA WA MTOTO MWENYE BETHIDEI ATUPIWA LAWAMA
Uzembe mwingine ulitajwa kufanywa na mama wa mtoto aliyekuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa aliyetajwa kwa jina la Anita Mboka kwa kuwachukua watoto wasio wake na kuondoka nao bila kutoa taarifa kwa wazazi wao japo kuwa mama wa marehemu Janeth Zakaria (9), Devotha Mbutwa alikiri kupokea taarifa kuwa mwanaye anakwenda kwenye bethidei ya mwenzake beach (baharini).

Inadaiwa mama huyo alipinga mwanaye kwenda kuogelea baharini, lakini alipoambiwa ni hotelini alikubali bila kujua kuwa nako walikuwa wakienda kupiga mbizi kwenye bwawa na baadaye kupewa taarifa za kifo chake. Marehemu alizikwa jana, Iringa Vijijini.

TAARIFA ZA MTOTO WA PILI
Kwa upande wao, ndugu wa karibu wa marehemu Ndimbumi Bahati (9) walisema hawakupata taarifa yoyote kuhusiana na mzazi huyo kumchukua mtoto huyo, wakadai siku ya tukio, marehemu alipelekwa na baba yake kula chipsi jirani na alipomaliza, baba aliondoka akimuahidi kuwa atakaporejea angemchukua kumpeleka matembezini, lakini jioni akapata taarifa amefariki dunia.
Marehemu alizikwa jana jijini Mbeya.

KUHUSU MTOTO WA TATU
Nao ndugu wa mtoto marehemu Eva Nicholaus (11) hawakupatikana mara moja kwa kuwa hadi gazeti hili linaelekea mtamboni hakukuwa na msemaji rasmi wa familia hiyo ambayo  msiba wake ulikuwa Kijitonyama-Mpakani, Dar. Alizikwa jana Makaburi ya Sinza jijini Dar.

WAZAZI WAVIPOKEA VIFO KWA MTAZAMO TOFAUTI
Inadaiwa baada ya vifo vya watoto hao wa mtaa mmoja, kuna wazazi  walivipokea vifo hivyo kwa mtazamo tofauti ambapo kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa familia ya Ndimbumi, baba wa mtoto huyo, Bahati Sisala alikuwa amechanganyikiwa kiasi cha kupoteza fahamu kwa siku nzima.

Naye mama mzazi wa mtoto Janeth, Devotha yeye alionekana kuzidi kudhoofu hali yake kwa kuwa alizipokea taarifa za kifo cha mwanaye akiwa anaumwa (ugonjwa haikujulikana).


KIJITONYAMA YAZIZIMA 
Waandishi wetu walishuhudia wakazi wa Kijitonyama mahali walipokuwa wakiishi watoto hao wakiwa katika majonzi makubwa ambapo umati uligawanyika kuaga watoto hao.

Msiba wa marehemu Ndimbumi uliagwa nyumbani Kijitonyama huku mwili wa mtoto Janeth ukiagwa katika Hospitali ya Mkoa Kutabibu Kinondoni, Mwananyamala kabla ya miili hiyo kusafirishwa mmoja kuelekea Mbeya na mwingine mkoani Iringa.


WANAFUNZI WAMLILIA MWENZAO MSIBANI
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijitonyama ambao walikuwa wakisoma na Ndimbumi walifika katika msiba huo na kusikitisha waombolezaji waliohudhuria msibani hapo baada ya kuangua vilio jambo lililoongeza simanzi. Marehemu alikuwa akisoma darasa la nne. 


MWENYEKITI, AFISA ELIMU NA KIONGOZI WA DINI WANENA
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Mtaa wa Kijitonyama, Alhaus Magoha alisema amesikitishwa sana na vifo hivyo vilivyotokea ndani ya mtaa wake na kuongeza kuwa hilo ni pigo kubwa.

Naye Afisa Elimu wa Kijitonyama, Alexandrina Kahando na Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mwenge jijini Dar, John Adolf walifika msibani hapo kuwafariji wazazi wa mtoto Ndimbumi ambao walikuwa wameishiwa nguvu kutokana na kumpoteza mtoto wao mpendwa.

HOTELI YAGHARAMIA USAFIRI
Habari zilizopatikana wakati gazeti hili linakwenda mitamboni zilisema kuwa, uongozi wa Hoteli ya Landmark ndiyo uliojitolea kubeba jukumu la kuisafirisha miili ya Ndimbumi na Janet.
Juzi waandishi wetu walifika kwenye hoteli hiyo kwa lengo ka kuzungumza na uongozi lakini waliambiwa kuwa viongozi wote walikuwa kwenye vikao.

Stori: Chande Abdallah, Shani Ramadhani, Denis Mtima na Mayasa Mariwata.
GPL

HIZI NDIO AINA TATU ZA MICHEPUKO HAPA BONGO

$
0
0
1. Mchepuko wa Lami: huu ni ule ambao
hauombi pesa, upo njema unajua designer
zote, katulia hana mapepe, uwe nae usiwe
nae maisha yake yanaendelea.

2. Mchepuko wa Vumbi: huu ni ule ooh sina
pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa,
charge iko low, ooh nipo saloon nadaiwa elfu
thelathini nitumie kwa tigopesa, naomba
nauli, nadaiwa kodi, mtoto wa shangazi kaja,
nrushie dompo, nk. Na hii ndio noma maana
njia kuu lazima washtukie mchepuko vumbi
unachafua na unasumbua fulltime!

3. Mchepuko kokoto: huu ni mkali zaidi ya
njia kuu kila mara huuliza upo wapi? na nani?
Why hupokei simu yangu? Nomaaaa!
Baki njia Kuu!

WOLPER: NATAKA SERIKALI MBILI, SERIKALI TATU MZIGO

$
0
0
MWIGIZAJI staa Bongo, Jacqueline Wolper ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema yeye matakwa yake ni kuwepo kwa serikali mbili na si tatu wala ya mkataba.
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar, Wolper alisema anaamini serikali ya tatu itakuwa mzigo kwa wananchi ambao ndiyo walipa kodi.

“Serikali mbili ndiyo mpango mzima, ya tatu ni mzigo, ya mkataba sioni maana yake. Halafu nataka muungano udumu, pia nitafurahi sana kama Ukawa watarudi bungeni litakapoanza tena Agosti mwaka huu,” alisema Wolper.

WANAFUNZI WA CBE DOM WACHAFUANA KWA PICHA CHAFU NA MATUSI JUU INSTARGRAM

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi wa CBE Dodoma  wamekerwa na kitendo cha kuchafuliwa kwenye mtandao wa Intagram  na mtu ambaye hawajamfamu kwa jina ingawa baadhi yao wanadai kuwa ni mwanafunzi mwenzao ambaye anatumia jina tofauti kabisa na lake na pia yupo miongoni mwao lkn bado hawajamfahamu....



Mwanafunzi huyo anayetumia Ac Feki ya Instar anaposti picha za wanafunzi wenzake na kuwaponda kuwa ni malaya wanaouza K.... pamoja na kuwachafua wengine kuwa ni mashoga. Baadhi ya wanafunzi walio wengi wa CBE wamechukizwa na kitendo hicho cha kuchafuliwa bila sababu yoyote na wamedhamiria kumsaka huyo mtu kwa gharama yoyote ili aweze kuwajibishwa:Instargram anatumia jina  LEE_IN_BOY


GARI LA GURUMO ALILO PEWA NA DIAMOND LAZUA UTATA KWENYE FAMILIA

$
0
0
AMA kweli asiyekuwepo na lake halipo! Lile gari la aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyefariki dunia hivi karibuni, Muhidin ‘Maalim’ Gurumo alilopewa na nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeibua utata mtupu ndani ya familia ya marehemu huyo baada ya kubainika kwamba kumbe hakupewa kadi yake

Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka ndani ya familia hiyo jambo hilo lilifahamika kufuatia mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta miongoni mwa wanandugu hao ambao sasa wamechangukana kutokana na mgawanyo wa mali za marehemu.
Ilijulikanaje kama hakuna kadi?
Chanzo hicho kilimtaja mtoto wa kike wa marehemu Gurumo aitwaye Mariam ambaye anataka nyumba na gari hilo aina ya Toyota FunCargo viuzwe ili watoto wagawane fedha.

“Yule binti alikwenda nyumbani kwa mama yake (mke wa mwisho wa mzee Gurumo aliyekuwa akiishi naye kwenye nyumba yake Mabibo, Dar) na kumtaka ampe kadi ya gari akidai ni la kwake na anataka kuliuza.
“Mama mtu alimwambia mwanaye kuwa baba yao hakupewa kadi hiyo siku alipokabidhiwa gari hilo.
“Hata hivyo, mama huyo alisema siku moja mzee Gurumo alimfuata Diamond alipokuwa akifanya shoo pale Coco Beach (Dar) kwa ajili ya kuulizia kadi hiyo ndipo Diamond akamwambia kwamba akitaka kadi amuulize mtu mmoja aliyesema ni kiongozi mmoja, anafanya kazi maeneo ya Posta Mpya jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa),” kilisema chanzo.


Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya Gurumo kuambiwa maneno hayo, hakutoa jibu lolote kwa mke wake kama alipewa kadi hiyo au la, lakini mama huyo hakuwahi kuiona.
Kukosekana kwa kadi hiyo kumesababisha kuendelea kuwepo kwa gari hilo, kwani kama ingekuwepo, lingeshauzwa.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Diamond zilisema kuwa tukio la kutoa gari kwa mkongwe huyo mwanzilishi wa Bendi za  Mlimani Park Orchestra na Msondo Music Band ulikuwa ni mpango maalum wa kumpromoti msanii huyo ili aweze kung’ara zaidi katika vyombo vya habari ambao uliratibiwa na kiongozi huyo mwenye kulalamikiwa na wasanii mara kwa mara.

KUHUSU MLELA KUWA TEJA LA MADAWA YA KULEVYA..

$
0
0
NYOTA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kugeuka teja (mbwia madawa ya kulevya) hali inayomsababishia ashindwe kujichanganya na wasanii wenzake katika shughuli mbalimbali.

Kikizungumza na Amani juzikati, chanzo  kilisema msanii huyo kwa sasa anavuta unga kiasi cha uteja kujionesha waziwazi na kupoteza mwonekano wake wa zamani.
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Mlela na kufanikiwa kumpata nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Katika maisha yangu sijawahi kutumia madawa ya kulevya na huwa nayapinga sana. Wanaosema navuta ni waongo, mimi sasa hivi naitwa baba, hivyo majukumu yameongezeka ndiyo maana sijichanganyi kivile.”


ACHENI BWANA MATITI YAKO KAMUONYESHE MUMEO HUKOOO ALAHAAA

$
0
0
Hivi haka kamtindo ka kuacha maziwa watu wayachungulie mnavyofanya wakina dada mna maana gani? 

Yaani utakuta mtu hadi wa ofisini matiti kayaacha nje au wengine wamevaa nguo zenye V yaani maziwa kila mtu anayaona.

Halafu myebana mpaka mnatupa majaribu kufanya kazi na nyie. 

Acheni bwana matiti yako kamuonyeshe mumeo huko alaaaaaah

RIPOTI:IMEBAINIKA KUWA WAWINDAJI HALALI NDIO WANAO UA TEMBO

$
0
0
 Ongezeko la kasi ya ujangili nchini limedaiwa kusababishwa na vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mfumo dhaifu wa usimamizi wa sheria katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kwa mujibu wa ripoti iliyopewa jina la Urasimishaji wa Ujangili wa Kitaalamu Afrika, tangu mwaka 2000 wizara hiyo imejikuta katika kashfa za rushwa na kusababisha mawaziri na watendaji wakuu kuvuliwa nyadhifa zao.

Katika ripoti hiyo, Taasisi ya Kimarekani ya Utunzaji Wanyamapori ya Born Free USA kwa ushirikiano na Shirika la Ripoti za Kichambuzi na Takwimu la C4ADS, imeeleza pia jinsi vikundi vya waasi barani Afrika wanavyoendesha shughuli za ujangili.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa mwezi huu nchini Kenya, inaitaja Tanzania kama kitovu cha kusafirisha pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikishindana na ile ya Mombasa katika kutumia bandari kibiashara.

Kutoka mwaka 2008 mpaka 2013, inaelezwa zaidi ya tani 20 za pembe za ndovu ama zilikamatwa zikisafirishwa kuingia au kutolewa katika Jiji la Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya C4ADS.

Ripoti hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).

Uchunguzi huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.

“Kuna udhaifu mkubwa katika usimamizi wa uwindaji halali na wawindaji wenye vibali hawasimamiwi ipasavyo kufanya uwindaji kwa taratibu zilizowekwa kisheria. Hivyo hutumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya ujangili,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Serikali yakanusha

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba wawindaji halali huachwa bila usimamizi, bali wana mifumo ya kusimamia shughuli hiyo.

“Sikubaliani na ripoti hiyo, tumeshaongea sana juu ya suala hili, Rais alishalizungumzia na waziri pia. Ufafanuzi ndio huo, hamna ukweli wowote katika ripoti hiyo,” alisisitiza Sarakikya.

Salakikya alisema idadi ya tembo nchini inazidi kuongezeka katika hifadhi tofauti na upungufu unaoelezwa katika ripoti hiyo.

VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISAIDIE WAFANYA KAZI

$
0
0

Kumekuwa na vyama vingi vya wafanyakazi, lakini kero za wafanyakazi bado zinaendelea kuwapo.

Kwa mfano kuna vyama vya wafanyakazi vyenye lengo la kutetea walimu, hata hivyo bado walimu wengi wanaendelea kuteseka.

Hivi karibuni nilikuwa nazungumza na mwalimu mmoja, anasema anashindwa kuelewa maana hasa ya kuwapo kwa vyama vya wafanyakazi.

Hoja hiyo inaungwa mkono na mwalimu wa Shule ya Sekondari Mbalizi ambaye hakutaka kutajwa jina lake huku akifafanua kwamba kama kweli Chama cha Wafanyakazi (CWT) ingekuwa ni kwa ajili ya wafanyakazi ingefungua kesi kudai madeni ya walimu.

Mwalimu huyo anasema pamoja na kwamba CWT inaongoza kwa kukusanya fedha za wanachama wake, walimu wanaongoza kwa kukopa na kuishi kwenye mazingira magumu zaidi nchini.

Imefikia hatua baadhi ya wafanyakazi wanaona kama vyama vya wafanyakazi vipo kwa ajili ya matumbo yao.

Mfanyakazi wa kampuni ya usafirishaji, Juma Hamisi anasema pamoja na kuwapo kwa chama chao cha Cotwu, lakini waajiri wanawakandamiza wafanyakazi.

Anasema madereva wamekuwa wakipewa Sh20,000 za posho ya safari ya kwenda kulala nje ya kituo cha kazi, je hiyo ni haki?

Pamoja na hoja hizo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu, Utafiti na Kazi zinginezo (Raawu), Kanda ya Nyanda za Juu, Joseph Sayo anasema wafanyakazi wengi wamefaidi matunda ya kazi za vyama vya wafanyakazi.

Anataja moja ya faida kuwa ni Serikali kuondoa kodi kwa mishahara ya kima cha chini na pia kupunguza walau asilimia moja ya kodi kwa mishahara mingine yote.

Hata hivyo, anasema pamoja na faida hizo ukweli ni kwamba wafanyakazi wengi hawajajiunga kwenye vyama vya wafanyakazi.

Anasema vyama vya wafanyakazi vimefanya mambo mengi mazuri, yakiwamo ya kutetea sheria za kazi zirekebishwe na pia vyama vinasaidia kuendesha kesi nyingi za wafanyakazi.

UKAWA ZANZIBAR INATISHA WAITEKA ZANZIBAR KIWANJA CHA KUBANDA MAITI

$
0
0
WAKAZI WA KUTOKA KISIWA CHA TUMBATU WALIFIKA KWENYE UKAWA NA MABANGO YAOKIWANJA CHA KIBANDA MAITI
MUASISI MZEE NASORO MOYOALIFIKA KWENYE UKAWA
MAKAMU WA KWANZA WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMADI AKIKUMBATIANA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROD SLAA KULIA KATIBU MKUU WA NCCRMAGEUZI MUSONA

MAKAMU WA KWANZA ZANZIBAR SHARIFF HAMAD AKISALIMIANA NA KATIBU MKUU CHADEMA DR  SLAA

KATUIBU MKUU WA CUF MAALIM SEFU HAMADI AKIWASALIMIA WANANCHI
WANANCHI WAKISHANGILA
WANANCHI WAKIWA KATIKA MKUTANO WA UKAAWA

WENYEVITI WA UKAWA  JAMES MBATIA NCCR MAGEUZI KUSHOTO PROFES IBRAHIM LIPUMBA CUF KATIKATI NA KULIA NI MWENYEKITI FREEMAN MBOWE CHADEMA WAKIWASALIMIA WANANCHI

ASKARI  WA KIKOSZI CHA FFU AKIWA KATIKA ULINZI

WANANCHI WAKIWA NA MABANGO YENYE UJUMBE WA KUONYESHA SERIKALI TAU

EMMANUEL MAKAID AKIWA ANASALIMIANA NA MZEE NASORO MOYO MUASISI

WANANCHI WAKIWA MABANGO YAO

MWANANCHI HUYU AKIONYESHA PICHA ALIYOIWEKA MGONGONI KWA YA RAIS MSTAAF WA ZANZIBAR NAYE ANATAKA TATU

TANESCO HII NI AKILI AU MATOPE-KUFUNGA NYAYA JUU YA MTI BAADA YA NGUZO KUVUNJIKA.

$
0
0
Nguzo iliyovunjika

Njia Mbadala Baada ya Nguzo kuvunjika

Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni   jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na  miundo mbinu mbalimbali .

Uharibifu mkubwa na wahatari  ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika  na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.

Katika eneo la Mlalakuwa  mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe  pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika  kabisa na nyingine mbili zimelegea  katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni  mti huo si mkavu ni mbichi.

Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?

Tunaomba  muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae  kwani ni hatari sana

KIGOGO USALAMA WA TAIFA AUWAWA KINYAMA DAR

$
0
0
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?
Last edited by Mohamedi Mtoi; Today at 13:54.
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images