Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mange Kimambi :Nimepata Kiki ya Kutosha..!!!

$
0
0



Ngachoka mie, kwa hiyo drama zote zile ulikua unatafuta kiki? Sasa kumbe ulikua unamuonea wivu makonda alivyokua anatoka kwenye magazeti kila siku eeh? Ukaamua sasa umchafue weee, dah tutajionea mengi mwaka huu, dah hizi kiki mwaka huu hatari, na umefanikiwa kwa kweli, kazana kuitukana serikali, but remember karma is around the corner 


Hivi Ndivyo Ilivyokuwa Baada ya Mwakyembe na Nape Kukutana Uwanja wa Taifa Leo(Pichazz)....!!!!

Kimenukaaa.. : Joshua Nassari Aibuka Sakata la Nape na Kuandika Ujumbe ‘Tata’..!!!

$
0
0

Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nasari ameandika ujumbe mzito sana kwa ajili ya kuwakumbusha watanzania hasa Mwakyembe ni Mtu wa namna gani hasa baada ya kusema kuwa Ripoti ya Nape Nnauye juu ya Uvamizi wa RC Makonda alioufanya katika kituo cha Clouds tv.

Nasarri Ambae ni mbunge Machachari sana, kupitia Ukurasa wake wa Facebook ameandika yafuatayo; “Dunia inazunguka kwa Kasi, Leo Mwakyembe anasema hawezi kuifanyia kazi Ripoti ya kamati ya Nape Nnauye kwa sababu ni ya upande moja na upande wa pili haikusikilizwa,Mwaka 2008 Mwakyembe aliwasilisha Bungeni Ripoti ya Richmond iliyomtuhumu Edward Lowassa bila ya kumhoji Mhusika Mkuu kwenye ripoti ya Richmond Edward Lowassa.”

Nini Maoni yako juu ya hili?

Makosa ya Kitaalamu Aliyoyafanya Askari Aliyemuonyesha Bastola Nape..!!!

$
0
0

Tukio la kuzuiwa Mkutano wa Mh Nape kuzungumza na wanahabari ni jambo mtambuka, mimi leo nataka nilichambue tukio la askari kumtishia bunduki bwana Nape Nnauye. Naliangalia katika mtazamo wa kitaalamu zaidi.

Kwanza tujifunze mambo machache,
Polisi nini? Hili watu wamekuwa wakilichanganya, Kuwasaidia maana ya neno POLICE ni People's Oorder, Law, lnvestigation and Criminal Enforcements kwamjibu wa Wagiriki, lakini Wazungu wanasema ni Law enforcement and criminal investigation..not vice Verser. Kisha tujifunze utendaji kazi wa huyu mtu aitwaye polisi upoje hapa Tanzania na duniani kote, kwakuwa sheria ni moja japo zinaweza kutofautia kidogo tu kimaumbile na kiutekelezaji lakini msingi wake ni mmoja.

Criminal investigation procedure kupitia criminal investigation Act inamruhusu askari kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anapoonesha ubishi wa kutotii.

Pia sheria hiyohiyo inamtaka, hii ni lazima sio ombi, askari kujitambulisha ikiwa ni Pamoja na kuonesha kitambulisho kabla "hajaanza" utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa dhana na uhalisia wa video hii ninayoitumia kama msingi wa uchambuzi, Mh Nape alikuwa sahihi kumuuliza yeye ni nani na akaomba kitambulisho. Kwa hatua hiyo tu, yule askari ana makosa hata kama ni askari uliyevaa sare au umevaa kiraia kama huyu, ukitaka kumkamata mtu lazima ujitambulishe wewe nani na unatokea kituo gani kisha ufanye yako kwa raia sio kwa kwa utaratibu ule hata kwa mazingira gani, Nape pia ana haki yakujua huyo polisi ni nani.

Suala la kutoa silaha lina mambo mengi ya kitaalamu, Kisheria askari popote ulipo katika misheni yoyote unatakiwa kuwa armed muda wote, lakini kuwa armed si kumpoint mtu gun ambaye ni unarmed wala hajaonesha dalili ya madhara kwako. Hili ni kosa kubwa kwa askari huyu.

Polisi yule anaweza kuwa na utetezi wenye hoja na usipokuwa makini unakubaliana naye kwamba aliona Nape yupo peke yake ndio lakini alikuwa amezungukwa na watu anaoamini ni wafuasi wake. Katika mazingira kama yale ambayo watu wengi wamejaa ambao kwa tafsiri ya kawaida ni watu wanaomuunga mkono nape, unategemea silaha itoke baada ya vurugu kuanza? Hii ni hoja nzito na inamruhusu askari kutoa silaha, lakini hoja hiyo inakufa kwenye kitendo cha kumuelekeza silaha mtu aliyesimama na hana silaha yoyote,

Askari huyu anaweza kujitetea tena kwamba alipomuona mtuhumiwa huyu kasimama alikuwa ameweka mikono mfukoni mwa suruali yake hali iliyomfanya yeye askari afikiri huyu mtu ana silaha,hivyo akamuwahi kwakunyooshea silaha.

Lakini utetezi huu unafutwa na kitendo cha yeye awali kwenda moja kwa moja kwa mtuhumiwa na kumshika na kumsukuma arudi kwenye gari, sauti ya video inasikika mtuhumiwa akimtaka mtu huyu anayedhaniwa ni askari ajitambulishe kwa kuonyesha kitambulisho jambo ambalo lilikuwa rahisi tu lakini ghafla akachomoa silaha na kumnyooshea mtuhumiwa.

Lakini nikitumia video hii namuona askari huyu anatumia silaha kizembe sana huyo angekutana na wenye mafunzo angekuwa chini silaha ingenyang'anywa,.

Kwaasili ukimtazama anaonekana akiihamisha silaha mkono wa kulia baada ya kuitoa kwa mkono wa kushoto,hii inamaana anatumia mkono wa kulia, lakini silaha aliweke kiunoni upande wa kushoto, hali inayomfanya achelewe kuichomoa kiunoni, silaha inatolewa zaidi ya sekunde 60 mpaka anapigwa picha nyingi, tazama hiyo picha Nape angekuwa mtaalamu wa mapigano ya kujihami kijasusi alikuwa anaweza kupiga teke au kifuti na kushika mkono wenye silaha na kumpora.

Kosa la pili ni la polisi waliomzunguka huyu aliyetoa silaha mpaka wakaacha raia Maulidi Kitenge kumvaa yule askari.

Tena Maulid Kitenge japo huenda hajui sheria lakini kafanya kosa kubwa sana kuwaingia wakati wakitimiza kazi zao. Kwa askari makini huyu Kitenge tungeimba iyena iyena leo. Ni kwa kosa la baadhi ya Wanausalama kuwa Wabaridi kumwacha Maulid amsukume Afisa active katika situations ile. Ukweli Maulid kawaponza askari walio Dormant hadi akaingilia mission kiasi cha kuhatarisha Usalama wa mwenzao ambae Silaha yake tayari alikwisha weka kwenye chamber

Kwa minajiri hii, Askari waliokuaa kwenye opaesheni hii wanatakiwa kuwajibishwa kwa ukiukwaji kwa sheria kanuni na taratibu za kazi ya uaskari wao,

Lakini askari aliyetishia kwa silaha atakiwa kuadhibiwa kwa uzembe, suala lake ninadhani huwezi kulipeleka kwenye mahakama ya kiraia labda ya kijeshi, kwa mtazamo wangu, yale ni makosa katika oparesheni za kiusalama ambapo anaweza kushitakiwa katika mahakama ya kijeshi. Msingi wa kesi ya kiraia unaweza kuita ni kvamiwa na mtu mwenye silaha anayedhaniwa ni jambazi. Wataalamu wa sheria za kiraia kina Tundu Lissu, Peter Kibatala, John Mallya, Ben Alex Ishabakaki, Jebra Kambole Sr. Na wengine mnaweza kulifafanua vizuri hili...

Na Yericko Nyerere

Fahamu Mambo Matano ya Kushangaza Kuhusu Tangawizi

$
0
0

TANGAWIZI ni kati ya viungo mahili vinavyochochea ladha nzuri katika vyakula vya aina mbalimbali na hivyo kuwavutia walaji kula chakula husika.

Tangawizi pia inapowekwa kwenye vyakula vigumu kama nyama huifanya ilainike na hivyo kuweza kuiva kwa haraka zaidi. Hivyo kwa point hiyo tu kwanza utagundua kiungo hiki pia kinaweza kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni pia

Wakati tangawizi ikiwa inafahamika zaidi kama kiungo, kwa upande mwingine kiungo hicho huweza kupunguza athari za matatizo mbalimbali ya kiafya pia kama ifuatavyo kwenye orodha hii hapa chini:-

1. Hupunguza maumivu kwa wanawake wakati wa kipindi cha hedhi (Period)

2. Huppunguza maumivu ya mifupa pamoja na misuli kwa ujumla.

3.Inaelezwa kusaidia kuimarisha uwezo wa utunzaji wa kumbukumbu kwa binadamu.

4. Husaidia kutuliza maumivu ya tumbo pia

5. Husifika kwa kuimarisha kinga za mwili na kuufanya mwili kupambana vizuri dhidi ya magonjwa.

Tabia Hizi 5 Zitakufanya Uwe na Maisha Mafupi Sana Hapa Duniani..!!!

$
0
0

Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.

Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na sababu tofauti tofauti.

Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na  hizi zifuatazo.

1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.

2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.

3. Kushinda umekaa siku nzima
Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.

4. Unywaji wa pombe
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo mawili makuu

a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.

b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.

5. Ulaji wa vyakula vya viwandani
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao

Mambo 6 Muhimu Unayotakiwa Kuyafanya Katika Weekend Yako..!!!

$
0
0

Ikiwa tunaelekea kwenye wekeend yaani Jumamosi na Jumapili ambapo watu wengi hupata nafasi ya kupumzika na kufanya mambo yao binafsi. 

Wapo ambao hutumia siku za weekend kwa kutulia nyumbani tu, huku wakijiandaa na kujipanga vyema ili kuanza wiki ijayo vizuri. 

Siku kama ya kesho yaani Jumamosi itapendeza kama ukiitumi kwa kukamirisha kazi zako muhimu hasa zile za nyumbani. 

1. Tumia weekend yako kufanya usafi kwa ujumla

Inawezekekana ikawa ni usafi wa kufua nguo, kusafisha nyumba, vyombo pamoja na kufagia, ni vyema ukajitahidi siku za weekend ukawa unafanya usafi wa kutosha na wakuridhisha kabisa kwasababu mara nyingi katikati ya wiki huwa ni ngumu kupata muda wa kuyafanya hayo tena.

2. Tumia weekend yako pia kukamirisha zile kazi zako ambazo ulishindwa kuzikamirisha katikati ya wiki. 

3. Ikiwa mambo yako yote muhimu na ya lazima uliyakamirisha katikati ya wiki na yote yapo sawa, basi weekend yako itumie kwa kufanya mambo mapya unayopendelea kufanya au kujifunza. Mfano kupika, kuogelea n.k

4. Kwa wanafunzi wao  ni vyema wakatumia wikeend zao kumalizia kazi za shuleni kama ni homework / assignments.

5. Pia hakikisha unatumia weekend yako kwa kupanga ratiba yako yote utakayofanya juma lijalo. Panga kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa utafanya nini, huku ukizingatia muda maalum wa kufanya mambo hayo.

6. Ukiwa na nafasi pia unaweza kuwakumbuka watu wako wa karibu kama ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwatembelea au kuwasiliana nao. Weekend hii kama una nafasi waoneshe ndugu, jamaa na marafiki kuwa unawajali na kuwapenda kwa kuwatembelea au hata kuwatumia salamu kwa njia ya SMS na kuwapigia simu.

Acha Kuteseka na Maumivu ya Jino Tumia Mbinu Hii..!!!

$
0
0

Maumivu ya meno huwa makali sana na huweza kukusababisha hata kushindwa kufanya kazi nyingine endapo yatakuwa ya muda mrefu.

Mbaya zaidi unaweza usilale kabisa endapo utapatwa na maumivu ya jino usiku kama hauna uvumilivu unaweza kutoka usiku huo huo na kukimbia hospitali kwenda kung'oa.

Hata hivyo, hapa ninayo orodha za vyakula na viungo ambavyo huweza kusaidia kupambana na matatizo ya meno.

Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.

Saga majani makavu ya 'mint' kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino linalouma.

Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka pamba hiyo kwenye jino linalouma.

Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma.

Sababu 4 Zinazochangia Kuhisi Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa..!!!

$
0
0

Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakipatwa na maumivu makali kila wanaposhiriki tendo la ndoa (kujamiana).

Kutokana na tatizo hilo kuna baadhi ya wanawake wamejikuta wakilichukia tendo hilo na baadhi yao hata kuhatarisha ndoa zao.

Leo nimeona niweze kukueleza msomaji wangu hasa wewe mwanamama mwenye tatizo hili kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia hali hiyo ya maumivu ni pamoja na hizi zifuatazo hapa chini:-

1. Ukosefu wa ute ute sehemu za siri ambao husaidia kupunguza msuguano wakati wa tendo hilo. Mara nyingi uteute huo hutokana na maandalizi ya kutosha ambayo huweza kufanyiwa mwanamke na mwenzi wake.

2. Maambukizi, mfano fangasi, U.T.I pamoja na magonjwa mengine ya zinaa huweza kupelekea hali hiyo pia ya kuhisi maumivu wakati wa tendo. Hivyo unapoona hali hiyo ni vyema kufika hospitali iliyokaribu nawe ili uweze kufanyiwa uchunguzi zaidi.

3. Pia kuhisi maumivu hayo huweza kuashiria uwepo wa vijiuvimbe vidogovidogo kwenye njia ya uzazi 'fibroid' hivyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi unapohisi hali hiyo.

4. Kwa wale ambao huenda hutumia kinga (kondom) nao huweza kupatwa na tatizo hili la maumivu wakati wa tendo, hivyo unapohisi hali hiyo unaweza kubadilisha aina ya kondomu kwani baadhi ya kondomu zinaweza kutowafaha aina fulani ya watu kwa sababu mbalimbali zikiwemo za mzio 'allergy'.

Lipumba: Inakuaje Syria Wanapigana Vita Lakini Wanatuzidi kwa Furaha..!!!?

$
0
0

Profesa Lipumba ameshangazwa na ripoti iliyotolewa na umoja wa mataifa ikitaja Tanzania kuwa nchi ya 3 kutoka mwisho kwa furaha huku ikipitwa na nchi kama Burundi na Syria

Amesema hii ianaonyesha tupo katika hali mbaya sana ya maisha hadi tunapitwa na nchi zenye vita

Kimenukaa...Makontena Mengine 262 ya Mchanga wa Dhahabu Yanaswa..!!!

$
0
0

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam.

Makontena hayo yalikuwa yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS.

Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ya Rais Magufuli kutembelea bandari ya Dar es salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa madini kutoka migodi mbalimbali iliyopo Kanda ya Ziwa.       

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema makontena hayo yaliyokuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kiforodha yamebainika jana tarehe 25 Machi, 2017 katika msako mkali unaoendeshwa na Mamlaka yake.

Mhandisi Kakoko amesema makontena yote hayo yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), na yalikuwa yanashughulikiwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya Freight Forwarders Tanzania Limited iliyopo Dar es salaam.

Amesema jumla ya makontena 256 yalikuwa katika bandari kavu ya MOFED, wakati makontena mengine sita yalikuwa tayari yameshaingizwa bandarini tayari kwa kusafirishwa.

Ametoa wito kwa makampuni yote ya madini yenye shehena za mchanga yajitokeze yenyewe na kuonesha mizigo yao popote ilipo nchini kabla haijabainika katika msako kabambe unaondeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Orodha ya makontena hayo yaliyobainika inaonesha yalifika bandarini hapo katika nyakati tofauti kutoka migodi ya Buzwagi na Pange Mines.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Bw. Ramadhani Mungi amesema bandari zote nchini ziko salama na kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kuwekwa askari na vifaa vya kisasa vya ulinzi zikiwemo kamera.

Noma Sana..Samatta Alivyoonyesha Vitu Alivyopata Ulaya Jana ...!!!!!

$
0
0

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta jana ameing'arisha Taifa Stars kwa kuifungia mabao mawili na kuipa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.

Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa ulio katika kalenda ya FIFA, umepigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam na kushuhudiwa na maelfu ya watanzania wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi, akiambatana na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye.

Katika mchezo wa leo ambao umejumuisha kikosi kipya kabisa cha Taifa Stars, chini ya kocha mpya Salum Mayanga, kimeanza kwa kasi ya aina yake na kufanikiwa kupata bao la mapema kabisa kunako dakika ya 2 mchezo kupitia kwa nahodha Mbwana Samatta aliyeitendea haki pasi ya Mohamed Hussein.

Taifa Stars iliendelea kuonesha kandanda safi, licha ya ubora na uimara wa Botswana, lakini ikashindwa kutumia nafasi kadhaa ilizopata kupitia kwa Samatta, Ajibu na Msuva.

Kipindi cha pili kilianza kwa Botswana kuongea nguvu na kufanya mashambulizi mengi ambayo hata hivyo ukuta wa Taifa Stars uliokuwa ukiongozwa na Abdi Banda, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein na Shomary Kapombe uliweza kutulia na kuhimili.

Mabadiliko ya kuwatoa Shiza Kichuya, Frank Domayo, Ibrahim Ajibu na Himid Mao na nafasi zao kuchukuliwa na Farid Musa, Mzamiru Yasin, Salum Aboubakary na Jonas Mkude, yaliweza kuzaa matunda ambapo katika dakika ya 77 Mwana Samatta akaifungia Taifa Stars bao la pili kwa mpira wa adhabu alioupiga baada ya kuangushwa nje kidogo ya eneo la 18.

Hadi mwisho wa mchezo, Tanzania inaondoka na ushindi wa mabao 2-0, ushindi ambao una faida katika viwango wa vya ubora ambavyo hutolewa naFIFA kila mwezi.

Ehe..Prof Jay Awachana Diamond na Kiba,Adai Wanaua Muziki wa Bongo Fleva...!!!

$
0
0

MKONGWE kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ameibuka na kusema kuwa, wasanii  mahasimu wakubwa, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba ndiyo wanauoa muziki wa Bongo Fleva.

Profesa Jay ambaye ni Mbunge wa Mikumi, akiwa ameachia ngoma yake mpya ya Kibabe hivi karibuni  amefanya mahojiano na Polisi wa Swaggaz na kuzungumza mengi kuhusiana  na muziki wa Bongo na sanaa kwa jumla.

Fuatilia sehemu ya mahojiano hayo;

SWAGGAZ: Umeachia ngoma mpya Kibabe, nini kimo ndani ya ngoma hiyo? Kwanini umeiita Kibabe?

PROFESA JAY: Nimeuita Kibabe kwa sababu mimi ni msanii mkongwe na nimefanya mengi kwenye huu muziki… na kama nilivyosema humo ndani (ya wimbo), nimechonga barabara ambayo mafanikio hayo (ya muziki) wasanii wengi sasa hivi wanayapata.

Mimi ni msanii wa muziki wa juu yaani heavy weight Mc, nimeona kuna baadhi ya mapungufu yapo kwenye game yetu, yakiwemo uandishi, kiki ambazo hazina kichwa wala miguu na vitu vingi vilivyofanya sanaa yetu idorore au ipunguze ule uhalisia wake ambao tulikuwa tunautegemea kila siku.

Ndiyo maana nikasema niuite wimbo wa Kibabe, kwa sababu mimi ni msanii mbabe na kama unavyojua hii ni Hip Hop… Hip Hop imejaa majigambo… unajisikia nini moyoni mwako na kupeleka kwa hadhira ambayo ni jamii.

Muziki wa sasa hivi ni tofauti sana na zamani sababu mwanzo platforms zilikuwa chache, radio stations zilikuwa chache lakini pia TV zilikuwa chache, studio zilikuwa chache na hata sapoti haikuwa kama ya sasa, lakini sasa hivi kila mtu anasapoti muziki wetu, kuanzia viongozi mpaka mashabiki wa chini, wote wanajitahidi kuwa wazalendo na kusapoti muziki wetu.

SWAGGAZ: Unaonaje sanaa yetu na hasa muziki ambao wewe ni msanii wake. Vipi, kuna hatua tunapiga kwenye muziki au unaona tupo palepale?

PROFESA JAY: Muziki unakua, lakini wasanii hawapo serious kwenye utendaji wao wa kazi. Unaweza kuona wasanii wakubwa kama Diamond na Kiba ambao wana platform kubwa, lakini hawaongei, mashabiki wao hawasaidiani, hawashirikiani, inachangia sana kuufanya muziki wetu udorore.

Naamini kwa nguvu kubwa waliyonayo Kiba na Diamond, wangekuwa pamoja, mashabiki wao nao wangeungana, kama taifa tungeweza kwenda mbele kwa haraka zaidi.

Wenzetu Nigeria wameshirikiana sana, watu walikuwa walidhani kuna bifu kati ya WizKid na Davido au D Banj na P Square, lakini baadaye unawakuta pamoja wanakunywa kahawa.

Naamini siku moja Diamond na Kiba watamaliza bifu zao na kutengeneza taifa lililo bora na wao kama kioo, kama wasanii ambao tunawaangalia sana, wanaweza kufanya kitu kizuri zaidi. Ushindani ubaki wa kimuziki na siyo wa kishabiki na chuki.

SWAGGAZ: Tangu umekuwa mbunge kuna mchango gani mkubwa ulioleta katika sanaa kwa ujumla?

PROFESA JAY: Nimefanya mambo mengi ya kuwasaidia wasanii lakini zaidi ni kupaza sauti ya wasanii ndani ya Bunge kutetea haki yetu. Changamoto za wasanii sasa zinajulikana na namna gani ya kubana ili jasho lao liwafikie moja kwa moja.

SWAGGAZ: Nje ya bunge, hakuna kitu cha moja kwa moja ulichofanya kwa wasanii?

PROFESA JAY: Kama nilivyosema, kazi kubwa nimeifanya kwa kushirikiana na wenzangu, lakini pia studio yangu ya Mwanalizombe nimeihamishia Mikumi na sasa matengenezo yanaendelea ikiwa kwenye hatua za mwisho kabisa.

Hii studio itawasaidia wasanii wa Mikumi na hasa wa vijijini kurekodi kazi zao katika quality ya juu. Naamini itakuwa msaada mkubwa sana kwa wasanii wa Morogoro kwa ujumla na wasanii wengine walio katika mikoa ya  karibu kama Dodoma na Iringa na kufanya kazi zao katika viwango bora.

SWAGGAZ: Mwelekeo wa muziki wa Tanzania unauonaje kwa sasa hasa katika ushindani wa kimataifa?

PROFESA JAY: Mwelekezo ni mzuri, na naamini Kiswahili kinazidi kupasua anga na sisi tunaeleweka. Unaweza kuona sasa hivi wasanii zaidi ya kumi, nyimbo zao zinapigwa kwenye stations kubwa za kimataifa kama Trace, MTV, Channel O nk.

Hata Blogs za kimataifa zinaripoti habari zetu, naamini tukiwa wengi, tutazidi kuwa na mafanikio makubwa zaidi. Nayaona mafanikio makubwa mbele yetu. Tukiwa wasanii wengi na channels zikafunguka zaidi, naamini tutazidi kufanya vema kwenye tuzo za kimataifa kama nchi nyingine.

Mfano Nigeria unakuta kwenye tuzo nyingi wao wanakuwa 25, Mtanzania mmoja au wawili ndiyo maana wanatushinda, naamini wasanii tukiongezeka tutasaidia zaidi kupasua kimataifa.

SWAGGAZ: Unatengaje muda wa muziki na kuwatumikia wananchi bila kuathiri upande wowote?

PROFESA JAY: Nasema kila siku, mimi ni mtu wa kutumikia Jimbo la Mikumi kwa asilimia zote. Hii talent nipo nayo, na ninayo kila siku. Nalala nayo, naamka nayo, naoga nayo, nakunywa nayo chai, natembea nayo.

Kwahiyo hainizuii hata kidogo kutimiza majukumu yangu jimboni. Muziki ni kipaji, kipo ndani, ninacho siku zote.

SWAGGAZ: Vipi kuhusu ndoa yako, baada ya kumvisha mpenzi wako wa muda mrefu pete ya uchumba?

PROFESA JAY: Ni kweli Desemba 31, mwaka jana nilimvalisha pete mchumba wangu wa muda mrefu, mama Lissa, anaitwa Grace ambaye nimezaa naye mtoto mmoja Lissa mwenye miaka 11 na Mungu akipenda mwezi wa saba mwaka huu, nitafunga naye ndoa. Naombeni sana baraka zenu, naombeni mniombee ili niweze kulikamilisha jambo hili mbele za Mungu.

Rasmi..Okwi Kutua Simba ..Kaburu Afunguka Haya Mazito Juu ya Ujio Wake..!!!

$
0
0

MAKAMU wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, ameonekana kuwaweka gizani mashabiki wa Yanga kutokana na kitendo chake cha kila wakati kumtaja Mganda Emmanuel Okwi.

Okwi ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwatia tumbo joto Yanga, zaidi ikiwa ni kutokana na kile alichowafanyia wakali hao wa Jangwani Septemba 2012 alipoiongoza Simba kuwapiga watani wao hao wa jadi mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa kufahamu hilo, kwa muda wote ambao Okwi amekuwa nje ya kikosi cha Simba, mabosi wa klabu hiyo wamekuwa wakilitaja jina lake kwamba wapo mbioni kumrejesha kama sehemu ya kuwatisha Yanga.

Hali hiyo ilijirudia kwa mara nyingine juzi kupitia kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Kaburu aliposti video ya mechi waliyoichapa Yanga mabao 5-0 na kuweka ujumbe uliosomeka: ‘Usiyemtaka anakuja’.

Ujumbe huo ulionekana kama kutuma salamu Yanga kwa wakati huu ambao timu hizo zinafukuzana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa kileleni kwa pointi zake 55, huku wapinzani wao hao wakifuatia na pointi 53.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Okwi anatarajiwa kurejea Msimbazi baada ya klabu yake hiyo ya zamani kumalizana na SC Villa ya Uganda anayochezea kwa sasa.

BINGWA lilizungumza na Kaburu kuhusu mchezaji huyo ambapo alisema, Kamati ya Utendaji ya Simba haina pingamizi kuhusu usajili wa Okwi kama benchi la ufundi litahitaji huduma yake.

Alisema kwa muda ambao Okwi ameishi na kutumikia kikosi cha Simba, hawana wasiwasi naye na kwamba Msimbazi ni sawa na nyumbani kwa Mganda huyo.

“Okwi, Simba ni nyumbani kwake, kama kocha atahitaji huduma yake, basi hatuna pingamizi,” alisema Kaburu.

Credit - Bingwa

Lady Jay Dee Afunguka Mahaba yake Kwa Hamorapa...Adai Watu Wamuache Afanye Kazi

$
0
0

LadyJaydee amefunguka kuhusu #Harmorapa ambaye amekuwa akiteka vichwa vya habari kutokana na stori zake zikiwemo nyingi za kuvunja mbavu.

#Jaydee amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa haoni tatizo kwa rapper huyo chipukizi kwa kuwa kila msanii ana njia zake ambazo anatumia za kufikisha sanaa yake inapotakiwa kufika.

#Ladyjaydee👉 “Tumuache afanye yake, unajua kila mtu ni ambavyo anaweza kuiwakilisha sanaa yake, kwahiyo mimi naona yuko poa,” ..
.
.
#Jide ameongeza kuwa alifurahi sana baada ya kuona clip ya video ikimuonyesha #Harmorappa akitoka nduki baada ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kuonyeshewa bastola Alhamisi hii.

Spika Ndugai :Makonda Hachomoki ..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 26/3/2017..!!!

Kimenukaa..Lissu Aaanza Kumtia Kashkash Rais Magufuli,Adai Anamvizia Tu Ajichanganye Juu ya Uteuzi wa Jaji Mkuu...!!!!

$
0
0

HATUA ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania imeibua utata kuhusu dhamira yake kwenye kufanya hivyo, Raia Mwema limeambiwa.

Tangu Uhuru wa Tanganyika, hakuna Rais aliyewahi kumteua mtu kuwa Kaimu Jaji Mkuu; baada ya Jaji Mkuu aliyekuwepo madarakani kumaliza muda wake wa utumishi kwenye mhimili huo wa dola.

Profesa Juma ambaye anachukuliwa kama mgeni kwenye mhimili huo, aliteuliwa na Rais Magufuli mapema mwaka huu kuwa Kaimu Jaji Mkuu akichukuwa nafasi ya Chande Othman aliyefikia umri wa kustaafu.

Mazungumzo baina ya gazeti hili na wandani wa Mahakama hapa nchini yameeleza hali hiyo kuleta utata kwa vile tukio hilo halijawahi kutokea na halina maelezo ya maana kulitetea.

“Sikiliza, hii nchi haijawahi kuwa na Kaimu Jaji Mkuu aliyeapishwa wakati Jaji Mkuu akiwa amestaafu. Hii ni mara ya kwanza na kwa kweli imeleta mkanganyiko mkubwa.

“ Kaimu Jaji Mkuu anaweza kuapishwa wakati Jaji Mkuu akiwa kwenye safari ya muda mrefu nje ya nchi au akiwa na tatizo linaloweza kuathiri utendaji kazi wake. Hapo Kaimu anaweza kuapishwa lakini si kwa ilivyo sasa. Jaji Mkuu kastaafu sasa Rais anateua Kaimu wa nini?” alihoji  mmoja wa majaji mashuhuri nchini aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa majina yake.

Jaji huyo alisema mtu akiwa anakaimu nafasi yoyote anakuwa hajiamini na hawezi kuchukua uamuzi mzito kwa sababu hajui kama atamfurahisha aliyemteua au la.

“Kama Rais alikuwa anamtaka Profesa Juma, angemteua tu kuwa Jaji Mkuu, hii kaimu haina maana sana. Imeleta mkanganyiko na utata tu,” alisema Jaji huyo.

Ingawa baadhi ya wanaharakati kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii wameenda mbali kiasi cha kusema kuna uvunjwaji wa Katiba kwenye uteuzi huo wa Kaimu Jaji Mkuu, Raia Mwema limebaini hakuna uvunjwaji wa Katiba uliofanyika kwenye jambo hilo.

Ibara ya 118 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toleo la mwaka 197, imeeleza kwa kirefu kuhusu nafasi hiyo ya Jaji Mkuu kama ifuatavyo:-

“118.-(1) Kutakuwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani

(ambaye katika ibara zifuatazo kwenye Katiba hii atatajwa tu kwa kifupi kama "Jaji Mkuu" na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani wasiopungua wawili, isipokuwa kwamba kikao maalumu cha Mahakama nzima kitakuwa kamili kikiwa na Majaji wa Rufani wasiopungua watano.

(2) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais na atakuwa ndiye Kiongozi wa Mahakama ya Rufani na pia Mkuu wa Idara ya Mahakama kama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 116 ya Katiba hii.

“(3) Majaji wengineo wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyoelezwa katika ibara ya 109 ya Katiba hii au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa

kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa Sheria zinazotumika Zanzibar.

“(4) Iwapo itatokea kwamba:-

(a) Kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi; au

(b) Jaji Mkuu hayupo Tanzania; au

(c) Jaji Mkuu atashindwa kutekeleza kazi yake kwasababu yoyote na Rais akiona kuwa kwa muda watukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu Jaji Mkuu, basi Rais aweza kumteua Kaimu Jaji Mkuu kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kustahili kuteuliwa kuwa Majaji wa Mhakama ya Rufani.

“Na huyo huyo Kaimu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpaka atakapoteuliwa Jaji Mkuu au mpaka Jaji Mkuu mwingine ambaye hakuwapo Tanzania au alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea kazini.”

Kwa mujibu wa vifungu hivyo vya Katiba, Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu endapo “Kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi”; lakini haijafafanua uwazi upi kwani inaweza kuwa kwa sababu ya kifo, kustaafu, kusafiri, kuumwa au sababu nyingine yoyote inayokubalika.

Ukaimu wa Profesa Juma

Baadhi ya wandani hao wa Mahakama, wameliambia gazeti hili ingawa imekuwa ni kawaida kwa majaji kukaimu Ujaji Mkuu, mara nyingi wanaokaimu huendelea kutumia ofisi zao zilezile na magari yaleyale, jambo ambalo ni tofauti na sasa.

Raia Mwema limeelezwa kwamba Profesa Juma anatumia gari la Jaji Mkuu, anafanya kazi kwenye ofisi ya Jaji Mkuu na kutendewa kama Jaji Mkuu kamili, ilhali wadhifa wake huo haujathibitishwa.

Wakati wa Jaji Mkuu Francis Nyalali, Raia Mwema limeelezwa, mara kadhaa aliwahi kutibiwa nje ya nchi na nafasi yake kukaimiwa na Jaji Augustino Ramadhani, lakini hakuwahi kutumia gari wala ofisi ya Jaji Mkuu.

Ilikuwa hivyo hivyo kwa Jaji Eusebia Munuo ambaye aliwahi kukaimu nafasi ya Chande wakati alipokuwa nje ya nchi kwa muda mrefu lakini hakuwahi kutumia ofisi ya Jaji Mkuu wala gari lake.

“ Kwa mujibu wa Sheria za Utumishi, muda wa kukaimu nafasi ni miezi sita. Sasa tunasubiri kwa hamu baada ya kupita kwa miezi hiyo sita nini kitafuata.

“ Je, Rais Magufuli atamuita tena Jaji Juma kwa ajili ya kumuapisha kuwa Jaji Mkuu? Kama hatamuapisha, atatoa sababu za kutomuapisha? Je, watu wakisema amemtoa kwa sababu alikataa kuburuzwa itakuwaje?” Raia Mwema limeambiwa.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hili, Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, alisema hatua ya Rais Magufuli kuteua Kaimu Jaji Mkuu ni dharau kubwa kwa majaji wa Tanzania.

Alisema kitendo cha Rais kuteua Kaimu Jaji Mkuu wakati kulikuwa na fursa ya kuteua Jaji Mkuu kamili kinatoa picha mbili kubwa; moja kwamba hakuwa tayari kwa uteuzi huo na pili hakuna majaji wenye sifa ya kuchukua wadhifa huo.

“Je, Rais anataka kuonyesha kwamba nchi hii haina majaji wenye uwezo wa kushika wadhifa huo kiasi kwamba ateue Kaimu Jaji Mkuu? Kwangu, naichukulia hii kuwa ni dharau kwa majaji wetu.

“ Mimi nasema Rais hajavunja sheria yoyote kwa kuteua Kaimu Jaji Mkuu lakini kinachogomba hapa ni picha anayoionyesha kwa mhimili huu. Kinachogomba ni dhamiri yake kwenye Idara ya Mahakama,” alisema Lissu.

Lissu alisema kazi iliyopo sasa kwa wanasheria, asasi za kijamii na vyombo vya habari ni kumkumbusha Rais kwa nguvu zote kwamba Idara ya Mahakama inatakiwa kuongozwa na Jaji Mkuu mwenye mamlaka kamili na si ya kukaimu.

“Na nyie mjiulize, Jaji Mkuu amestaafu, Kaimu Jaji Mkuu wa nini? Kaimu inakubalika tu wakati mhusika anapokuwa nje ya nchi au kwa sababu nyingine kama zilivyoelezwa kwenye Katiba. Hili la kuteua Kaimu wakati Jaji Mkuu amestaafu ndiyo kalileta Magufuli,” alisema.

Jaji Ibrahim Hamis Juma ni msomi mbobezi wa masuala ya sheria akiwa amewahi kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Aliapishwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu Januari mwaka huu na kwa mara ya kwanza aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2008.

Credit - Raia Mwema

Kalianzisha Tena..Lema Achochea Vyama vya Upinzani Kufanya Haya Dhidi ya Utawala wa Rais Magufuli...!!!

$
0
0

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amekuja na staili mpya katika ulingo wa kisiasa mara hii akihimiza ushirikiano wa wapinzani kudai utawala bora.

Lema amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kumbizi ya miaka 50 ya Azimio la Arusha mjini hapa, akisema huu ni wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana.

Lema alisema amehudhuria mkutano huo kutokana na kampeni ya ushirikiano wa vyama vyote vya upinzani waliokubaliana kupinga mwenendo wa Serikali.

 “Mkiwa na mkutano semeni niwaalike na wanachama wa Chadema waje wawape ushirikiano, lengo letu ni kuhakikisha haki inatendeka bila matabaka ya walionacho na wasionacho wala makabila,” amesema.

Katika mkutano huo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amezungumzia ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa na kusema kuna idadi kubwa ya kampuni za uwekezaji ambazo zinafanya hivyo.

Hatarii..Prof Lipumba Azidi Kumganda Maalim Seif,Adai ni Msaliti..!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa CUF anayetambulia na Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amemlalamikia Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad kufungia akaunti zote za chama hicho za wilaya.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la uongozi linaloongozwa na upande wake, Profesa Lipumba amesema kutokana na uamuzi huo ruzuku ya chama kutoka serikalini wameikosa.

Mwanasiasa huyo amesema CUF ipo katika mtihani kwa sasa, hivyo uwapo wa Maalim katika kikao hicho ungesaidia kuiimarisha.

“Wajumbe nawashukuru kwa kuja ili kupata fursa ya kujenga chama. Chama chetu kipo ndani ya mtihani ambao kwa kweli chanzo chake ni katibu mkuu wetu kutoheshimu katiba yetu na kutoheshimu taratibu za kidemokrasia,” amelalamika Profesa Lipumba.

Amesema kuwa Maalim Seif alitakiwa kuhudhuria kikao hicho na alipewa taarifa lakini hakuweza kufika, hali iliyosababisha majukumu yake kusimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara), Magdalena Sakaya kama katiba yao inavyoelekeza.

 “Fedha zimekwama kwenye mabenki hasa NMB kwa sababu akaunti za wilaya zinafunguliwa na kamati za utendaji za wilaya, hazifunguliwi na makao makuu, lakini wenzetu wametumia mitandao ya wapambe wao kutoa shinikizo zifungwe,” amesema.

Akijibu tuhuma hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui amesema kuwa hatua ya kufunga akaunti za benki imelenga kulinda fedha ya chama ili zisitumiwe vibaya na upande wa Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba yupo kwenye mgogoro na CUF baada ya kuandika barua ya kujiuzulu na baadaye kuifuta, lakini mkutano mkuu ulikubali kujiuzulu kwake na kuteua kamati ya uongozi chini ya Julius Mtatiro.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa bado anamtambua kwa madai kuwa hakutaarifiwa kuhusu uamuzi huo na kwamba, baadhi ya taratibu hazikufuatwa, msimamo ambao CUF chini ya Maalim Seif imeukataa.

Noma Sana Aisee..Askofu Gwajima Awavuta Stan Bakora na Kitale Katika Kanisa Lake la Ufufuo na Uzima ..!!!

$
0
0

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Ministries, Josephat Gwajima amesema Jumapili hii atatembelewa na wachekeshaji Kitale ‘Mkudesimba’ pamoja na Stan Bakora.

Gwajima amekuwa akitamka mara kadhaa kwamba anavutiwa na wachekeshaji hao ambao wamekuwa maarufu kutokana na vichesho vyao ambavyo vilikuwa vinarushwa kupitia redio ya EFM.

Jumamosi hii mchungaji huyo ambaye amekuwa akizuru katika vituo mbalimbali vya redio kutoa pole kuhusiana na tukio la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media siku chache zilizopita, ametoa taarifa ya kutembelewa kanisani kwake na wachekeshaji hao.

“Tutakuwa na ugeni wa waigizaji na wachekeshaji wawili rafiki yangu Mkude Simba (Kitale) na Stan Bakora watapata nafasi ya kuperform live pia, kwa niaba ya familia ya Ufufuo na Uzima tunawakaribisha. Ufufuo na uzima tunasapoti vipawa mbalimbali ambavyo watu wamepewa na Mungu,” aliandika Gwajima Instagram.

Askofu huyo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hivi karibuni baada ya kutajwa kwenye sakata la dawa za kulevya na RC Makonda.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>