Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Kimenukaa..Siku Chache Baada ya Kutoa Wimbo Unaoiponda Serikali,Nay wa Mitego Akamatwa na Polisi..!!!

0
0

Nay wa Mitego amedai amekamatwa na polisi wilayani Mvomero, Morogoro alikokuwa ameenda kwaajili ya show.

Hajasema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake Wapo ambao umemkosoa vikali Rais Dkt John Magufuli. “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police,” ameandika rapper huyo mtata.
“Nawapenda Watanzania wote.✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo,” ameongeza.

Kwa Taarifa Yako Hii Ndio Mijengo ya Maana 6 Anayomiliki Samatta Bongo...!!!!

0
0

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.

Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.

Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.

“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.

Banda Mchezaji Bora Simba kwa Mwezi wa Pili...!!!

0
0

Klabu ya Simba Sports Club imejiwekea utaratibu wa kila mwezi kutoa tuzo ya heshima na zawadi kwa mchezaji ambaye anakuwa amefanya vizuri katika mwezi husika ili kuwapa motisha wachezaji wao na kuwapa moyo wa kufanya vyema.

Katika mwezi wa pili, Simba Sports Club imemtangaza mchezaji wake Abdi Banda kuwa ndiye mchezaji bora wa mwezi wa pili.

Zoezi la kuwapata wachezaji bora katika klabu ya Simba linafanyika kwa mashabiki kutuma jina la mchezaji husika kupitia ukurasa wao wa Facebook 

Zitto - Rais Magufuli Kaitia Nchi Hasara ya Trilioni 1.8 kwa Amri Zake za Kiholela..!!!

0
0

Jana nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongozi lazima ujue unatoa kauli gani wakati gani. Niliwaeleza wanachama na wageni wengjne katika mkutano wa ACT Wazalendo kuwa Amri ya kiholela aliyoitoa Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu imepelekea nchi yetu kupoteza USD 880m Kama kodi ya ongezeko la Mtaji kutokana na mauzo ya Acacia Mining. 

Hivi sasa nchini kwetu kuna sheria ya kutoza 20% ya thamani ya mauzo iwapo kampuni zinauziana hisa. Tozo inayotozwa inaitwa Capital Gains Tax. Kodi hii mpya ilitungwa mwaka 2012 ili kukabili wawekezaji waliokuwa wanauziana makampuni juu Kwa juu bila Tanzania kupata lolote. Tanzania imeshafaidika na kodi hiyo Kwa mauzo mbali mbali ambayo yamekwisha fanyika kwenye sekta mbalimbali. 

Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika. 
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni. 

Tafiti zinaonyesha kuwa gharama ya kujenga ' refinery ' ya kuchenjua dhahabu hapa nchini ni USD 800m. Hivyo mapato ambayo yangepatikana kutokana na kodi ya mauzo ya Acacia yangewezesha nchi kujenga refinery na kufikia lengo la Rais la kuwa na uchenjuaji wa mchanga ule hapa hapa nchini. Rais angetulia angeweza kuua ndege wawili Kwa jiwe moja, 1) kiwanda cha kuchenjua kingejengwa nchini na 2) mchanga usingesafirishwa tena kwenda China na Japan. 

Hata hivyo Tanzania haina mchanga wa kutosha wa kushibisha hiyo refinery Kwa mujibu wa teknolojia ya sasa ( soma maelezo yangu hapa chini Kwa Mhariri wa RaiaMwema). Hivyo Rais angeweza kutumia mapato hayo Kwa matumizi mengine ya Maendeleo. Kwa mfano Bunge lilitenga kama USD 430m hivi kujenga Reli ya kisasa na tayari Serikali imeshaingia mkataba na kampuni kutoka Uturuki kujenga Reli hiyo kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro. Lakini gharama ya kipande hicho ni USD 1.2bn. Kwahiyo Rais angeweza kutumia mapato haya ya mauzo ya Acacia kuongezea kwenye kipande hiki na hivyo kuepuka kukopa kuziba nakisi ya USD 800m iliyopo Sasa na Bunge kwenye Bajeti ya 2017/18 lingetenga fedha za kuanzia Morogoro kwenda Dodoma. 

Kama Mipango ya Reli ipo sawa, Rais angeweza kutumia fedha za capital gains tax kutoka Acacia kujenga vyuo vya VETA kila Wilaya na kila Kambi ya JKT na chenji ingebaki. Tanzania inahitaji tshs 750 bilioni kujenga vyuo vya VETA kila Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji nchini. 

Rais angejifunza kujizuia kutoa matamko barabarani angeisaidia Sana nchi na kujisaidia yeye mwenyewe kutimiza ndoto zake kwa nchi anayoongoza. Mimi binafsi naunga mkono kuwa ni lazima tuchenjue dhahabu hapa hapa nchini badala ya kupeleka mchanga Japan na China. Lakini ni muhimu maamuzi hayo yawe na ushahidi wa kisayansi badala ya matamko holela ambayo madhara yake Kwa nchi ni makubwa mno. 

Zitto Kabwe, Mb 
Arusha 
26/3/2017

Breaking News..Rais Magufuli Afanya Utenguzi Wizara ya Nishati na Madini

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa kuanzia leo tarehe 26 Machi 2017.

Katibu Mkuu Ntalikwa aliteuliwa Desemba 2015 na kuapishwa Ikulu Januari 2, 2016.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, nafasi yake itajazwa hapo baadaye.

Exclusive..Polisi Waweka Wazi Sababu ya Kumkamata Nay wa Mitego Leo...!!!

0
0

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.

Kama Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.

Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.

Za Chini ya Kapeti..Mgogoro Mkubwa Waibuka Chadema,Chanzo Chatajwa ni Ubunge wa Afrika Mashariki na Hali Mbaya ya Kifedha..!!!

0
0

Chama chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kimeingia katika wingu zito na kutishia kukisambaratisha chama hicho.

Chanzo cha Mgogoro ni nafasi za Ubunge wa Africa mashariki, Uchaguzi wa kanda ya Mashariki na Hali ya kifedha ndani ya chama.

Chanzo cha ndani ya CHADEMA kinasema kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe aliingia na majina mawili ndo akawaambia wayachague ambapo aliingia na Majina hayo ni Masha na Wenje hakukua na utaratibu sahihi wa kuwapata wagombea katika Bunge la Africa Mashariki.

Uchaguzi wa kumpata Viongozi ndani ya kanda ya Mashariki ulijaa kasoro nyingi ambapo wananchama wanaulinganisha na ule wa kanda ya Nyasa ambapo Ole Sosopi alitupwa nje ya kinyang'anyiro kwa kuwa mwenyekiti wa chama aliingia na Jina lake.

Idara ya fedha ndani ya CHADEMA haijakaa vizuri hivyo kuleta sintofahamu kwa wadhamini ambao wanataka ukaguzi wa fedha kupitia mkaguzi huru akague ili wajiridhishe wadhamini ndani ya CHADEMA wamekua wagumu kutoa fedha zao Hali ambayo inaisababishia chama ukata kwani Tajiri na Mdhamini mkubwa ndani ya CHADEMA ndugu Sabodo Alishajitoa na Kuungana na Rais Magufuli baada ya kuona Utendaji wake uliotukuka.

Kinachokupotezea Mafanikio Yako Sana Ni Hiki Hapa..!!!

0
0

Acha kujidanganya kwamba unatafuta mafanikio wakati hata unashindwa kubadili tabia ndogo ndogo za kukupeleka kwenye mafanikio yako, huo utakuwa ni uongo mkubwa.

Acha kuendelea kujidanganya kwamba kesho yako itakuwa bora wakati hata leo hii hufanyi kitu cha uhakika cha kubadilisha maisha yako. Maisha yako kiukweli hayataweza kubadilika.

Acha kuendelea kulaumu watu wengine kwa maisha yako kuendelea kuwa mabaya. Mtu wa kwanza unayetakiwa kumlaumu ni wewe mwenyewe hasa kutokana na mienendo na tabia zako.

Sio kwa sababu maisha ni magumu kwa sasa, basi unachanganyikiwa na kuona kila kitu hakifai kwako na kwa wengine. Maisha yanahitaji sana utulivu wa hali ya juu ili ufanikiwe, unatakiwa ujue hili.

Kama unaona maisha yako yamekweda hovyo, jichunguze, panga mipango yako upya kwa umakini na utulivu na hata wala usikurupuke katika hilo. Utulivu ni kitu cha msingi sana ambacho kinaweza kukupa mafanikio.

Tabia mbaya na mienendo mibovu ulionayo hiyo ndiyo inaokufanya au naweza kusema inaharibu maisha yako moja kwa moja. Angalia hilo halafu utaujua ukweli ambao ninakwambia.

Kila wakati jiulize, unaendelea kukua kimafanikio, au unarudi nyuma? Kama unarudi nyuma, kama nilivyosema kuwa makini sana na tabia na mienendo yako, hiyo ndiyo inayokukwamisha.

Kama umefika wakati kwako wa kusema uko 'serious' na mafanikio yako, basi hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kubadilisha tabia zako na kujenga tabia zitakazokuwezesha kufanikiwa.

Kumbuka pia kinachokupotezea mafanikio yako, ni tabia ambazo unazo na unazibeba kila wakati, hicho ndicho kitu kikubwa kinachokupotezea mafanikio yako ya leo na kesho.

Nikutakie siku njema na kila kheri,

Hatua Nne Za Kufikia Malengo Yako Kwa Uhakika Mkubwa...!!!

0
0

Kila mtu katika maisha yake ana malengo maalumu ambayo anakuwa amejiwekea na anakuwa ana waza kwamba kwa namna yoyote ni lazima baada ya muda fulani malengo yake yatatimia.

Pia sina shaka na wewe, naamini umejifunza kwa sehemu namna au mbinu ambazo mtu anaweza akazitumia kuweza kufikia malengo yake. Lakini leo hii, si vibaya kama nitakung’ata sikio kukumbushia tena jinsi unavyoweza kufikia malengo yako kwa uhakika mkubwa.

Najua kila mtu ana njia zake na mbinu ambazo anazitumia kuweza kufikia malengo yoyote katika maisha. Leo hii, naomba nikuonyeshe mbinu ambazo zinatumiwa karibu na watu wote wenye mafanikio makubwa kufikia malengo yao kila wakati.

Andika malengo yako chini.

Yaweke malengo yako kwenye karatasii ili yawe rahisi kuyaona. Yawe ni malengo mahsusi ambayo utekelezaji wake unafikika na uwe tayari umejiwekea tarehe maalumu ya kuyafikia. Hio ndiyo sifa ya malengo unayotakiwa kuwa nayo.

Anza kuweka mipango.

Umesha andika malengo yako tayari. Hatua inayofuata ni kwa wewe sasa, kuweka mipango ya kufanya. Kumbuka unapofanya jambo unapata nguvu zaidi ya kuweza kulifanikisha kuliko ukitulia. Hivyo ni lazima mipango yako iwe hai na ya kiutekelezaji.

Lipa gharama.

Kubali kulipia kila gharama inayohitajika ili kufikia malengo yako. Gharama hizo zinaweza zikawa ni muda au nidhamu binafsi. Lakini gharama yoyote fanya kila ufanyalo hakikisha unailipa. Kama utakwepa kulipa gharama yoyote ile naomba nikwambie sahau mafanikio.

Yapitie malengo yako kila siku.

Hakuna namna ya nyingine ya kuwa mshindi zaidi ya wewe kukomaa kupitia malengo yako kila siku. Unapopitia malengo yako kila siku yanakupa nguvu na hamasa kubwa ya kuona ni jinsi gani yanawezekana na unaweza kuyafikia.

Hivyo ndivyo, unaweza kutimiza malengo kwa kufuata hizo hatua rahisi kabisa.

Nikutakie siku njema na kila kheri,

Kama Unaogopa Kufanya Kitu Hiki, Sahau Kuhusu Mafanikio Katika Maisha Yako Yote...!!!

0
0

Fikiria kila unachokijua na kukikumbuka kuhusu mabadiliko unayotaka yawe katika maisha yako, halafu  uone ukweli huu  kama kweli nawe ni mmoja kati ya watu wanaotaka mafanikio au uko nje ya mstari wa mafanikio na pengine tu wewe hujijui. Kama kweli unataka mafanikio, ni kwanini  mara kwa mara umekuwa ukisita au kuogopa kufanya jambo ambalo lingeweza kubadili maisha yako na kukuletea mafanikio mkubwa? Hili ndilo tatizo walilonalo watu wengi wanahofia sana kufanya mabadiliko kwa namna moja au nyingine hata kwenye yale malengo waliojiwekea wao wenyewe kuna wakati huwa wanaogopa pia.

Kimaumbile, kila binadamiu anahofia mabadiliko, lakini hofu ya mabadiliko inapozidi kuwa kubwa na kukuzuia kufanya mambo ya maana kwako, hofu hii  sasa hugeuka kuwa ni maradhi yanayokuzuia wewe kufanikiwa. Hebu fikiria tena, ni mara ngapi umekuwa ukitaka kufanya mabadiliko Fulani  katika maisha yako, lakini umekuwa ukijikuta ukishindwa kufanya hivyo kutokana na kuogopa kufanya vitu Fulani? Ni mara ngapi umekuwa ukitaka kuingia kwenye biashara lakini umekuwa na hofu nyingi zinakuzuia? Hivi ndivyo ilivyo mabadiliko huogopwa, wakati mwingine bila sababu ya msingi.

Wengi wetu kutokana na kuogopa mabadiliko, hujikuta ni watu wa kutoa sababu ambazo hata hazina mashiko zinazosababisha wao washindwe kutekeleza malengo na mipango waliojiwekea. Utakuta mtu anakwambia  hawezi kufanya biashara ni kwa sababu hana mtaji, ukija kuchunguza kidogo utagundua kuwa hiyo ni sababu ambayo amekuwa akiitoa kwa muda mrefu, iweje kila siku mtu huyohuyo awe hana mtaji tu. Kama uko hivi una hofu tu hata kwa vitu vidogo ambavyo ungeweza kuvifanyana , tambua kuwa kuanzia sasa unaye adui mkubwa ndani mwako anayekuzuia kufanikiwa. Na unapoogopa kufanya mabadiliko ambayo unaahitaji sasa ili ufanikiwe, sahau kuhusu mafanikio katika maisha yako yote.

Tatizo kubwa utakalokuwa nalo linalosababishwa na hofu hii ya kuogopa kufanya mabadiliko ni lazima utakuwa mtu wa kutaka mafanikio ya harakaharaka. Watu wengi wenye mawazo ya kutaka kufanikiwa leoleo hata kama wameanza biashara leo, wengi wao huwa wana hofu hii kubwa ya mabadiliko ndani mwao, unaweza  kufanya utafiti mdogo utagundua ukweli huu ulio wazi. Hawa ni watu ambao kiuhalisia hawaijui wala kuiamini subira ndani mwao, bali ni watu wakutaka mfumo wa maisha uwe ambao unaanza leo biashara na wiki ijayo uwe tajiri ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Hivi ndivyo walivyo watanzania wengi wanaogopa mabadiliko na kuamini katika miujiza, sio katika wao wenyewe kutenda na kuona matokeo.  Hebu jaribu kukagua maisha ya walio wengi utakuja kugundua ukweli huu ni watu wanaofikiria sana leo, sasa hivi, siyo baadaye. Hata malengo yao ni ya karibu sana na hawataki shida, wanataka wafanye leo, wamudu leo na kila kitu kimalizike leo. Sijui kesho watafanya kitu gani? Ukimwambia mtanzania aanzishe mradi ili aje faidi baada ya miaka 10 kutoka sasa kwanza atakushangaa, kisha atakucheka we hadi mbavu zimuume. Anataka leo hata kama ni kwa miujiza.

Ndiyo maana wengi kati ya Watanzania hawana malengo, wanaishi tu na kutawaliwa na hofu za mabadiliko. Kuweka malengo siyo sehemu ya maisha yao, kwani malengo yanataka mtu mwenye subira, mtu anayeamini kwamba maisha ni kuanguka na kusimama. Wanachojua kikubwa ni kulalamika na kulaumu, kuponda na kukejeli, kwa sababu wao wamekata tamaa bila kujijua. Ndiyo maana ni watanzania wanne tu kati ya kumi ambao wanafanya kazi, wanatoka jasho na wanaweza kusubiri bila kukata tamaa, wengine waliobaki wanasubiri ujanja ujanja tu ilimradi wafanikiwe hata kama ni kwa kufanya uhalifu wa aina yoyote.

Ni watu ambao wanataka kuishi kihadithi, wawe na pete ambayo wanaweza kuiamuru iwape wakitakacho na wakipate. Maisha ni ya kibunuasi- abunuasi tu, watu hawa kwao mabadiliko ni kitu kigumu sana kwao na kinaogopwa kweli. Kama unataka mafanikio ya kweli yawe kwako, unatakiwa kubadilisha fikra za zako na kuamua kukubali kuwa mafanikio yanahitaji mabadiliko makubwa sana ambayo wewe mwenyewe unatakiwa uyafanye kwa kujitoa hasa. Acha kuwa na hofu zisizo na maana zinazokuzuia wewe usifanikiwe, chukua hatua katika maisha yako, kuyafikia maisha unayoyataka.

Polepole Amtwisha Rais Magufuli Sakata la Paul Makonda

0
0


Kupitia mkutano wa Katibu Mwenezi Ndg Humphrey Polepole na Wanahabari leo Jijini Dar es salaam juu ya mageuzi ya CCM kiutendaji na kiutawala pamoja na CCM kufanya uteuzi mpya. pia Mwenezi huyo aliulizwa Swalli kuhusu CCM kulishughulikia sakata la RC Makonda,

Na haya ndiyo yalikuwa majibu yake... 


"Kuhusu RC Paul Makonda, CCM inautaratibu wake wa kushughulikia viongozi wake. Chama kitakapokuwa tayari kitalishughulikia suala hili."


"Pili, RC Paul Makonda ni mteule wa Rais Magufuli, na yeye anapomteua mtu anaweza pia kumchukulia hatua."

PICHA: Nay Wa Mitego alivyokuwa ndani ya kituo cha polisi Morogoro

0
0


Hapo chini ni Picha ikimuonesha Nay wa Mitego akiwa ndani ya kituo cha Polisi Morogoro baada ya kukamatwa. (Picha kwa hisani ya Group la WhatsApp la Waandishi wa Morogoro)

Mashabiki Walivyomliza Jana Nape

0
0


UPENDO ambao mashabiki wa mpira wa miguu waliuonesha jana kwa Nape Nnauye, aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo ulimliza kiongozi huyo.


Mashabiki wa soka waliojitokeza Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa – Taifa Stars dhidi ya Botswana, walisimama kwa muda na kumshangilia Nape Nnauye alipoingia uwanjani hapo, ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono.


Katika ukurasa wake wa Instagram leo, Nape ameweka video inayonesha mashabiki wakimshangilia kama ishara ya kumtia moyo, huku akiandika “Jana mlinitoa machozi.”


Nape ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi aliondolewa katika nafasi yake Alhamis ya wiki hii na Rais John Magufuli, ikiwa ni siku moja tu baada ya kueleza kuchukizwa na kitendo cha uvamizi wa ofisi za kituo cha Clouds TV, uliongozwa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Siku hiyohiyo pia Nape alikabiliwa na maofisa usalama, ili kuzuiwa kuzungumza na wanahabari baada ya kuenguliwa katika wadhifa wake. Tukio la kumzuia Nape liliambatana na mmoja wa maofisa usalama kumnyoshea bastola ili kumshinikiza aingie kwenye gari lake na asizungumze na wanahabari.


Tangu kutokea kwa tukio hilo watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, wasanii, wananchi na wasomi wamejitokeza na kulaani kitendo alichofanyiwa Nape, huku wakimtia moyo.

Kudadeki..Diamond Afanya Kufuru ya Pesa,Anunua Cheni na Pete kwa Milioni 158...!!!

0
0

Pete na cheni mpya za Diamond Platnumz alizozivaa kwa wakati mmoja zina thamani ya shilingi milioni 158!

Hitmaker huyo wa Marry You amepost Instagram picha mbili zikionesha madini hayo kwa kile anachosema kuwainspire mashabiki wake.

“Thanks God for my new GOLD & DIAMONDS collection…i never thought i would be able to hang 50,000$ on my neck,” ameandika kwenye picha ya kwanza.

Kwenye picha nyingine ameandika, “Thanks God for your daily blessings never thought i would be able to walk with 22,000 $ on my Hand!!!… jus get inspired @sallam_sk don’t hate.”

Muimbaji huyo wikiendi iliyopita alitumbuiza show ya nguvu humo Muscat, Oman.

Breaking News..Rais Magufuli Aagiza Nay wa Mitego Aaachiliwe,Ataka Pia Wimbo Wake Uendelee Kuchezwa Kwenye Radio Station Kama Kawa,Ampa Masharti Haya

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumuachia huru Rapa Emmanue Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kukamatwa juzi wilayani Mvomero mkoani Morogoro kisha kusafirishwa jana kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake wa WAPO alioutoa hivi karibuni hauna maadili na una maneno ya kichochezi.

Akitoa agizo la Rais Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli ametaka Nay aachiwe huru na wimbo wake aufanyie maboresho kwa kuongelea pia kuhusu wauza madawa ya kulevya na wakwepa kodi kisha uendelee kupigwa kwenye vyombo vya habari.

Aidha amesema kuwa, mara tu atakapoachiwa huru, Nay anapaswa kuonana na Waziri Mwakyembe ili ampe maelekezo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wimbo huo.

Kimenukaaa..Bakwata Yatoa Tamko Kuhusu Masheikh Walioenda Kusali Kanisani kwa Gwajima Jumapili...!!!

Mwanasheria Maarufu Alberto Msando Ammwagia Sifa Msanii Harmorapa

0
0

Baada ya msanii Harmorapa kupata Ubalozi wa kinywaji kinachoitwa cider ‘swala’, Mwanasheria maarufu Alberto Msando ambaye amekuwa akizishughulikia kesi za wasanii maarufu kama Wema Sepetu na wengineo, ametoa pongezi kwa msanii huyo.


Msando ametoa pongezi hizo kwa Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram akimpongeza kwa hatua aliyopiga na kujitahidi kutengeneza umaarufu ambao wengi wameshindwa.


"I really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi hawawezi.


"Wengi wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu. Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider ‘swala’. Its a big step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby 😂😂😂😂

 

"Kisa tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama wengine. #TheDon#HarmoMbio #HarmoBastola#KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa 😂😂#NusuUsoNusuPua"

Inasikitisha..Mtoto wa Miaka Minne Alawitiwa na Kijana wa Kazi Hadi Kufikia Hatua ya Kuwa Shoga...!!!

0
0

Kuna familia moja ni walimu walikuwa na mtoto wao wa kiume wa miaka minne alikuwa anasoma chekechea baada ya kuona kipato hakitoshi wakaamua kuanzisha kilimo na ufugaji. 

Kwa kuwa walikuwa ni wafanyakazi wakaamua kutafuta kijana toka Iringa atakayekuwa anasimamia shughuli za kilimo na ufugaji na kumuangalia mtoto baada ya msichana wa kazi kuondoka walipokuwa wanafanya mchakato wa kupata dada mwingine kazi ya huyo kijana kwa mtoto ilikuwa kwenda kumchukua shule, kumbadilisha nguo za shule, kumpatia chakula na kumuangalia asipate matatizo wakati wazazi hawapo.

Kilichotokea yule kijana akawa anamlawiti mtoto wazazi wake pale wanapokuwa hawapo, baada ya muda afya ya mtoto ikaanza kuzorota, kuharisha yaani akawa haeleweki, na majirani wakawa wanamwambia yule mwalimu kuwa kuna muda mtoto analia sana na ukienda kumuangalia utakuta kijana kajifungia naye bafuni anamwogesha, yule dada akachukulia ni mtoto kutokuyapenda maji/kuoga, hakutilia maanani

Kuna siku mtoto akawa hana furaha usiku mama akaamua kwenda kuomba ruhusa kazini ili arudi aje amchukue mtoto ampeleke hospitali, alivyofika ghafla akakuta kijana anamlawiti mtoto chumbani kwake na kawasha redio kwa sauti kubwa ili majirani wasisikie kelele alivyofumania akaita majirani wakampeleka polisi yule kijana na yule mtoto akapelekwa hospitali.

Baada ya kumfanyia vipimo vyote ikaonekana ameathirika/UKIMWI wakamuanzishia dozi ya ARV na yule kijana akakubali kosa mahakamani na alikuwa chini ya miaka kumi na nane na akajieleza kuwa ni mgonjwa wa UKIMWI anatumia dawa na huo ugonjwa alitoka nao kwao Iringa hivyo anaombwa asamehewe baada ya muda yule mtoto akaendelea vizuri lakini akawa anawaomba watu wazima wamuingize kitu nyuma means ameshakuwa shoga tayari sijui kama atakuja kuachana na hii hali.

Fahamu Mambo Kumi ya Kushangaza Kuhusu Mnyama Simba...!!!

0
0

Simba kama afahamikavyo kuwa ni mfalme wa pori anasifa mbalimbali ambazo nyingi unaweza ukawa unazijua kulingana na uelewa wako, lakini kwa sifa kabambae na za uhakika juu ya hayawani huyu ni kama ifuatavyo:-

1. Simba ni miongoni mwa jamii ya paka wakubwa akiwa ni wapili kwa ukubwa nyuma ya chui.

2. Simba dume katika ‘group’ la simba huwa ndiye wa kwanza kula windo kabla ya wengine kula,tofauti na inavyoelezwa kuwa jike ndiyo huwa wa kwanza.

3. Jina lingine la Simba dume ni Tom, wakati jina la simba jike ni lioness.

4. Kuna aina saba za Simba ambao ni Simba wa kiafrika,simba wa marekani, simba wa milimani, simba weupe, simba wa kiasia na simba aina ya cave.

5. Simba ana uwezo wa kutembea zaidi ya siku nne au tano bila kunywa maji.

6. Familia ya simba inaitwa ‘pride’na inaundwa na dume mmoja na jike mmoja huku watoto wakiwa kuanzia wawili hadi watatu huku miongoni mwa watoto hao mmoja akiwa ni dume.

7. Uzito wa simba kijana ni kati ya pound 330 hadi 500,kwa kawaida simba dume kijana anakuwa mrefu kuliko simba jike kijana.

8. Kwa kawaida Simba hutumia zaidi ya saa 16 hadi 20 kwa ajili ya kulaa na kupumzika kila siku.

9. Endapo katika famila ya Simba,akapatikana dume jipya,dume huyo huwauwa simba wadogo na kuwala.

10. Kiumbe pekee ambacho kinaogopwa na Simba ni binadamu

Toyota Coaster Inauzwa Bei Nafuu

0
0

Toyota coaster inauzwa
170,000km
Bei 20m(mazungumzo yapo)
Gari inatembea iko Mwenge DSM
Piga simu namba 0759252600

Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images