Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Rasmi..CCM Yaweka Kizingiti Kingine..!!!

$
0
0

Wakati CCM ikitangaza makatibu wapya wa mikoa na wilaya, chama hicho kimesema kitahakikisha kinajenga urafiki usio na shaka kwa kuchunguza uadilifu wa wahisani watakaotaka kukichangia chama hicho, kabla ya kupokea michango yao.

Uamuzi huu umefikiwa na CCM kutokana na kile kinachoonekana chama kutaka kisitekwe na wafadhili kutokana na nguvu yao ya fedha. Hii ni pamoja na kuondoa uwezo wa wafadhili kuamua nani agombee nafasi ipi.

Kukiweka mkononi chama kutokana na michango inayotolewa na marafiki hao ambao huwa na uwezo wa kushawishi nani agombee nafasi ipi.

CCM pia imeamua kuendesha shughuli zake muhimu, kama uchaguzi mkuu kwa kutumia fedha zinazotokana na vyanzo vyake vya ndani.

“Chama kitaendelea kupokea michango kutoka kwa matajiri wanaotaka kukiunga mkono kwenye miradi na shughuli mbalimbali,” alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika mahojiano maalumu na waandishi wa Gazeti la Mwananchi.

“Marafiki wa CCM bado wapo na wataendelea kukisaidia chama, ila sasa ni lazima tujiridhishe kwamba si wakwepa kodi, hawauzi unga na wanafanya biashara halali.

Polepole pia alisema CCM itataka kujihakikishia kuwa misaada ya wafadhili hao haikigawi chama.

CCM imekuwa ikisemekana kutegemea kwa kiasi kikubwa michango ya wafadhili kujiendesha, hasa inapotaka kuitisha vikao vyake vya juu kama Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu.

Pia chama hicho kinategemea misaada ya marafiki zake katika shughuli za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na uchapishaji vifaa vya kampeni kama fulana, vipeperushi na khanga.

“Yote yaliyoafikiwa hayakufanywa kwa kumtazama mtu,” alisema Polepole.

“Tumeweka mfumo mzuri utakaodhibiti rushwa kwa kuwa awali wapo waliothubutu hata kuchapisha kadi za uanachama na kuunda makundi yao ndani ya chama.”

Wakati ikitegemea wafadhili kuendesha shughuli zake, CCM inamiliki mali nyingi kubwa kama majengo ya kukodisha, viwanja vya michezo na kumbi za mikutano

“CCM ina mali zake yenyewe wala haijapewa na Serikali kama wengi wanavyodhani. Tumefanya mabadiliko ya katiba ambayo yanalenga kuongeza usimamizi wake,” alisema Polepole.

Ili kufikia uwezo huo, Polepole alisema utaratibu wa kuhakiki mali zote za chama umewekwa na utahusisha mapato na matumizi kwa namna ambayo ziada itapelekwa makao makuu kwa mipango ya kitaifa.

Polepole alisema hadi mwaka 2011, CCM ilikuwa inamiliki viwanja 32 vya michezo na kati ya hivyo, 22 vinatumika kwa mechi za soka za ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza.

Kutoka kwenye vitega uchumi vyote walivyonavyo, alisema kutakuwa na mapato ambayo yanapelekwa makao makuu huku wanaovisimamia wakitoa kiasi kinachotosha kukidhi gharama za uendeshaji.

Polepole alisema mkakati mwingine wa chama hicho ni kuongeza thamani ya mali ilizonazo ili zitumike au kukodishwa kulingana na hali ya soko la sasa pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Alisema vikao vya juu vya chama hicho vimekuwa vikighartimu fedha nyingi.

Alisema kikao cha Halmashauri Kuu, ambacho kabla ya mabadiliko ya katiba ya CCM kilikuwa na wajumbe takriban 400, kilikuwa kikitumia Sh600 milioni lakini baada ya kuwapunguza mpaka 163, sasa kitatumia Sh100 milioni tu.

“Halmashauri inakutana mara tatu kwa mwaka. Unaweza kuona ni kiasi gani kitaokolewa kwa mabadiliko haya ambayo hayajaathiri uwakilishi wa wajumbe,” alisema Polepole.

Kwa hatua hizo, alisema katika mkakati wa chama kuhakikisha kinaongeza uwajibikaji na kuziba mianya yote ya rushwa, ipo mikakati thabiti.

Licha ya hatua hizo, Polepole alisema kingine kilichofanywa na chama hicho tawala ni kuwaondoa makamanda na makatibu wasaidizi wilaya na mkoa ambao walikuwa wanalipwa mishahara kwamba ni moja ya dhamira za kupunguza matumizi.

Sambamba na marekebisho hayo alisema ajira za watumishi wa jumuiya zake; Umoja wa Vijana (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Wanawake (UWT) litafanywa chini ya sekretarieti moja tofauti na ilivyokuwa awali.

Licha ya watumishi hao wa chama, alisema hata gharama za mikutano zimepunguzwa baada ya kushusha idadi ya wajumbe watakaokuwa wanahudhuria.



Mabadiliko

Katika mabadiliko hayo yaliyopitishwa na Mkutano Mkuu, CCM imeondoa kofia mbili za uongozi kwa wale wanaoshika nafasi za utendaji.

Lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano ataendelea pia kuwa mwenyekiti wa chama.

“Mwenyekiti ndiyo kichwa, ndiye kiongozi kwenye chama chetu. Tumekubaliana tunampa dhamana ya kuwa mgombea wa chama chetu ili atupe uongozi mmoja wa chama na atumie nafasi hiyo kuongoza Serikali,” alisema Polepole.

Alisema nchini China mwenyekiti wa chama ni rais wa nchi hiyo, lakini chini ya cheo hicho watendaji wengine wote hawaruhusiwi kulimbikiza mamlaka.

“Bado tunahitaji mtu mmoja atubebee dhamana ya nchi na huu ni msimamo tuliokubaliana. Rais wetu, ndiye tunampa uenyekiti wa chama. Ni ku- maintain na kuhuisha ukubwa wa nchi na chama,” alisisitiza Polepole. 

“Diwani ambaye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya kwa nafasi hiyo na anaweza akagombea nafasi kwenye kamati ya siasa ya mkoa pia,” alisema.

Akiwa na nafasi hizo zote na akakosea, alisema hakuna kamati inayoweza kumuwajibisha kwa sababu kote ni mjumbe.



Urais

Akizungumzia madai ya kuwapo kwa mpango wa kuweka pingamizi la kugombea bila kupingwa katika kipindi cha pili kwa Rais aliyepo madarakani, Polepole alisema hayana ukweli wowote.

“Hili jambo la kupinga ni uongo. Hakuna kikao chochote tulichojadili suala la kugombea kwa maana ya kuomba nafasi ya kupeperusha bendera mwaka 2020,” alisema. 

Alisema suala hilo lipo kwenye utamaduni wa CCM wa siku nyingi kwamba Rais aliyepo anapitishwa kwa muhula unaofuata ingawa hakuna anayezuiwa kuchukua fomu ya kumpinga.

“Kila baada ya miaka mitano watu wanaruhusiwa kuchukua fomu. Hata mwaka 2010 walifanya hivyo. Lakini kwa aliyefanya kazi nzuri tutampa tena nafasi. Hatujaondoa haki hiyo ya kidemokrasia ndani ya chama,” alisema.



CCM yapanga upya makatibu wa mikoa, wilaya

Wakati huo huo CCM jana kilitangaza safu yake mpya ya watendaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, baada ya kukamilisha uteuzi wa makatibu wake katika ngazi hizo mbili kwa upande wa Bara, huku Zanzibar ikiwekwa kiporo.

Uteuzi wa makatibu hao ulitangazwa jana na Polepole, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Katika uteuzi huo wapo watendaji waliopandishwa kutoka ngazi ya wilaya kwenda mikoa, huku wengine wakihamishwa katika vituo vyao vya kazi.

Ingawa uteuzi wa makatibu wa mikoa yote 31 tayari umeshakamilika, lakini Polepole alitaja makatibu wa mikoa 25 tu huku wa mikoa mitano ya Zanzibar akisema yatatangazwa baadaye sambamba na makatibu wa wilaya zote za Zanzibar, ambao bado hawajateuliwa.

Polepole alisema kwamba watendaji hao kwa upande wa Zanzibar watatangazwa baada ya kumalizika kwa tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, na hali ya kisiasa ya Zanzibar.

“Uteuzi huu umezingatia maadili, weledi, jinsia na mpango wa kuachiana vijiti kwa kuzingatia rika.”, alisema Polepole.

Polepole alifafanua kuwa makatibu wa mikoa 11 na makatibu wa wilaya 75 ni wapya.

Wateule hao wapya hawajawahi kushika nafasi hizo bali wamekuwa wakitumika ndani ya chama katika nafasi mbalimbali na kwamba zaidi ya asilimia 30 ni wanawake.

“Makatibu wengi tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra” alisema.

Alifafanua kuwa lengo la kuteua watendaji hao wapya ni kuendana na dhana ya CCM mpya kutokana na mpango wa mageuzi yanayofanywa ndani ya chama hicho, ili kuingiza mawazo mapya yatakayoshirikiana na yale ya wazoefu.

Alisema kuwa jukumu la kwanza la watendaji hao ni kusimamia uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho, unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Awali, Polepole alisema kufuatia mageuzi yanayaoendelea ndani ya chama hicho nafasi za utendaji zitakuwa zinatangazwa ndani ya chama kwa kuwapa fursa wenye sifa za kitaaluma, waadilifu, weledi na uzoefu.

Alisisitiza kuwa wanataka mtawanyiko wa jinsia na viongozi wanaokidhi misingi ya kuendana na utamaduni wa kupokezana vijiti kwa marika ili vijana waweze kujifunza na kupata uzoefu wa uongozi kutoka kwa viongozi watu wazima waliopo.

JPM Atoa Agizo kwa CAG Kukagua Sekta ya Madini

$
0
0

Rais Magufuli amemuagiza CAG kufanya ukaguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini mianya yote ambayo inasababisha nchi kukosa mapato makubwa hususani katika misamaha ya kodi, mikataba mbalimbali na ulipaji wa kodi.

Ametoa agizo hilo leo wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo imewasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Juma Assad katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

“Haiwezekani Watanzania wanakosa dawa hospitali wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa maji wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa umeme wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa barabara wakati dhahabu zao zinaondoka, nataka ukakague kwa kina hii sekta ya madini ili watanzania wajue chao nini na kama kinapatikana sawasawa?” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Dkt. Magufuli pia amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kuitisha kikao cha pamoja kitakachomkutanisha CAG na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wa wizara zote, Gavana wa Benki Kuu na Wakuu wa taasisi za umma ili kila mmoja aambiwe hali ya hesabu katika taasisi yake na kuchukua hatua.

“Mhe. Waziri Mkuu ukaongoze hicho kikao na wewe CAG uwaambie kila mmoja katika eneo lake juu ya dosari zake, sitaki kuona dosari zinajirudia zilezile kila wakati” amefafanua Mhe. Rais Magufuli.

Ripoti hiyo imegusa maeneo mbalimbali yakiwemo ukaguzi wa hali ya hesabu za Serikali, misamaha ya kodi, ukusanyaji wa kodi na maduhuli ya Serikali, uandaaji na utekelezaji wa bajeti, hali ya deni la Taifa, usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa mali na madeni ya Serikali na usimamizi na uendeshaji wa taasisi za umma zikiwemo taasisi muhimu za kifedha na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Prof. Mussa Juma Assad amesema pamoja na hatua kubwa iliyopigwa na Serikali katika kuzingatia taratibu za fedha bado kuna mapungufu mbalimbali ambayo yameendelea kujitokeza na ameshauri hatua zichukuliwe kukabiliana nayo ikiwemo kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma katika madini, kuiepusha TANESCO kununua umeme wa gharama kubwa, matumizi mabaya ya misamaha ya kodi na kuongeza mashine za kutoa risiti (EFD).

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CAG anapaswa kuwasilisha ripoti ya hesabu za Serikali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya tarehe 31 Machi ya kila mwaka, na baada ya hapo ripoti hiyo huwasilishwa bungeni katika kikao kinachofuata.

Ukweli Mchungu Kuhusu FARU John, Kamati Yabaini ni Kweli Alikufa

$
0
0
Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuchunguza kifo cha Faru John imetoa taarifa kuwa mnyama huyo alikufa katika hifadhi ya Sasakwa Gruneti kwa kukosa matibabu alipoumwa.

Akiwasilisha ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Samwel Mnyele alisema faru John alikosa matunzo na uangalizi wa karibu.

Mnyele ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali alisema hakukuwa na kibali rasmi cha kumhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Grunet.

Alisema kamati hiyo imeshauri hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori na Mhifadhi wa Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipongeza kamati hiyo na kusema serikali itayafanyia kazi mapendekezo ili kulinda maliasili.

Chanzo: Mwananchi

VIDEO:Alichoongea Ney wa Mitego Baada ya Serikali Kuamua Kumwachia na Kutoka Selo

$
0
0
Ney wa Mitego amewashukuru wasanii wote walioonyesha sapoti kwake kipindi alichokuwa matatizoni
pia amemshukuru Rais Magufuli na waziri wake Mwakyembe, ila kuhusu kuonana na Mwakyembe Dodoma kama waziri alivyotaka amesema mpaka afikirie kwanza
Bonyeza Play

Barnaba Alizwa na Wezi, Aomba Walau Wamrudishie Passport yake

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo Barnaba ameibiwa begi lake lililokuwa ndani ya gari lake likiwa na vitu vya thamani ambavyo ni pamoja na baadhi ya kazi zake ambazo hazijatoka zilizokuwa kwenye hard disc, kamera na laptop mbili.



Barnaba amepost ujumbe Instagram kuwaomba wasamaria wema kumrudishia na kutoa maelezo jinsi ya kuwasiliana naye na kati ya vitu vilivyopotea ipo pia hati yake kusafiria(passport).

Ameandika:

“Za asubui Ndugu Zangu wapendwa Usiku wa kuamkia Leo Nimeibiwa Begi langu Dogo Tu si Kubwa Sana ambalo lilikuwa ndani ya Gari langu | lakini ndani Yake Kulikua Na Laptop 💻 za mac mbili moja Pro x moja Letina ya ukubwa Kidogo Theni Kuna external mbili moja Rangi Ya orange 🍊 moja Ya kijani Na Kuna File Zangu zilikua Na Mikataba Mbali Mbali lakini Kikubwa zaidi Ndani Yake Kuna PASPORT Yangu ambayo Ukifungua ndani Inasoma Jina La ELIASI BARNABASI INYASI and Kuna Vitu Vingi Sana Vidogo vidogo Vyenye Thamani Kubwa Kama Camera 🎥Na vingine Lakini Naomba sana Sana Waungwana Kama Kuna mtu Yotote atabaini au kujua Vilipo au hata kupelekewa Basi Naomba wasamalia Wema mnirudishie Au kuniletea Na Napatikana kwa No 0743505010 Mungu Awabariki Na naamini Aliyenavyo ajaiba Bali amepitiwa katika njia ya kutafuta Ridhiki Nami kwa jina la mungu nitamsamehe Na nimesamehe ila Kama Ana Rohoo nzuri Na ameguswa Basi Naomba waungwana mnipigie hata Kama Umeokota 😰😭” Alipost Barnaba

Maneno ya Nape Nnauye Baada ya Nay wa Mitego Kuachiwa

$
0
0
Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, March 27, 2017 kutoa agizo kwa Jeshi la Polisi  kumuchia huru msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uchezwe kwenye vyombo mbalimbali.

Sasa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter hakuweza kuficha hisia zake juu ya maamuzi ambapo aliyaandika haya……
 “Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!” – Ney wa Mitego.

Alichokiandika Mwanasheria Alberto Msando kuhusu Msanii Harmorapa

$
0
0
Siku chache baada ya msanii Harmorapa kupata Ubalozi wa kinywaji kinachoitwa cider ‘swala’, Mwanasheria maarufu Alberto Msando ambaye amekuwa akizishughulikia kesi za watu maarufu kama Wema Sepetu na wengineo, ametoa pongezi kwa msanii huyo.

Msando alitoa pongezi hizo kwa Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram akimpongeza kwa hatua aliyopiga na kujitahidi kutengeneza umaarufu ambao wengi wameshindwa. 

Alberto Msando ameyaandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram…
"I really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi hawawezi.
"Wengi wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu. Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider ‘swala’. Its a big step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby 😂😂😂😂.;- Msando
"Kisa tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama wengine. #TheDon#HarmoMbio #HarmoBastola#KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa 😂😂#NusuUsoNusuPua;-Msando

Zitto: Rais Hana Haki Kuhalalisha Nyimbo ya Msanii Yeyote Kuchezwa au Kutochezwa..!!!


Ukweli Mchungu ...Rais Magufuli Anaenda Kinyume na Mitizamo ya Wananchi..!!!

$
0
0

Bila shaka mmepatwa na mshangao kwa uamuzi uliochukuliwa dhidi ya msanii Ney wa Mitego. Nimejaribu kupitia matukio kadhaa yaliyotokea hivi karibuni ndani ya nchi yetu Tanzania yaliyokua yanategemea maamuzi kutoka kwa mh rais. 

Nimegundua rais amekua akitenda tofauti na mitazamo/hukumu zetu. Mfano tukianza na swala la Mkuu wa Mkoa wa Dar na tuhuma dhidi ya kugushi vyeti na kuvamia Clouds matumaini na mitizamo yetu ilikua ni kwamba mh rais angemuondoa ktk nafasi yake na kuchukuliwa hatua za kisheria lakini kachukua maamuzi ambayo kila mtu hadi sasa amebaki na mshangao. 

Ukija katika ishu ya Ney wa Mitego kuhusu wimbo wake kuoneka kuwa na baadhi ya maneno yanayomlenga mh rais watu wengi walishatoa hukumu kuwa msanii huyu. atafungwa au kupotezwa kabisa hasa baada ya msanii huyo kukamatwa na Jeshi la Polisi mjini Morogoro lakini imekua tofauti pia na uamuzi aliochukua mh rais wa kuagiza msanii huyo aachiwe na wimbo wake uendelee kupigwa na vituo vyote vya redio nchini hivyo kutengua uamuzi wa BASATA walioufungia wimbo huo. 

Hili la Masogange na Madawa ya Kulevya Linahitaji Hakimu Mwanamke;wa Kiume Anaweza Kufuta Kesi...!!!

Je, Kuwa na Gari ni Kivutio Kwa Wadada Katika Mahusiano?

$
0
0
Sijui kwa wengine hili limekaaje ila binafsi naona gari nalo ni kivutio kwa hawa dada zetu, kuna binti hapa mtaani enzi hizo sina gari aliniwekea ngumu ila mwaka jana nilivyomiliki gari yani alilegeza hata sikuamini.

I mean kuna siku kuna bidada anajiheshimu sana tu nilimpa lifti tukabadilishana contacts kesho yake kiutani nikamwambia tumeet akakubali fasta yani nikawa nacheka tu maana ilikuwa natania.

Kuna matukio mengi sana ambayo yalinithibitishia kuwa hawa dada zetu wana kaugonjwa kwa wanaume wenye magari, Japo haya matukio huwa yananitokea mimi najiheshimu na nampenda sana mpenzi wangu sipo tayari kutake advantage kwa hawa mabinti wa lifti.

Je unaonaje Mdau ni kweli wadada wanapenda wanaume wenye magari au la?

Noma Sana..Nape Aibuka na Haya Baada ya Rais Magufuli Kuruhusu Wimbo wa Nay wa Mitego...!!!

$
0
0

ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amechapisha ujumbe wenye kutaka itumike busara na siyo nguvu katika kufanya maamuzi.

Aidha ujumbe huo ulikwenda sambamba na picha ya msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

Nape ameonyesha kuguswa baada ya kukamatwa kwa mwanamuziki huyo na alipoachiwa huru amepongeza uamuzi uliofanyika na kusisitiza mara zote busara inastahili kutumika.

Kwa Wale Msiopenda Uzee,Msosi Huu Unawahusu..!!!

$
0
0

Kuna wakati nilipata mwaliko wa kwenda nchini Uganda, tulifika Kampla na kupokelewa na mwenyeji wetu. Tulikuwa kikundi cha watu watano, tulipelekwa kwenye hoteli tuliyoandaliwa na kuambiwa tujiandae, baada ya masaa mawili mwenyeji wetu atarudi kutuchukua kwa chakula cha jioni.

Nyumbani kwa mwenyeji wetu ile karamu ilikuwa ya kukata na shoka, kulikuwa na vyakula vingi kuanzia; matoke, wali, samaki sato, nyama ya mbuzi (choma), mbuzi mchuzi, chapati, salad, matunda, nuts na vinginevyo. Katika kujitengea chakula, kaka mmoja nilimuona anakula salad tu, baada ya chakula tulijiwekea matunda na story za hapa na pale ziliendelea.

Baadae niligundua kaka yule ni daktari, alinifahamisha alipata scholarship baada ya kumaliza form six kwenda kusoma medicine China, alipofika kule aliamua kubadili na kusomea Chinese Medicine na katika process ya kusoma herbs ndiyo aligundua uharibifu wa chakula katika harakati za mapishi mpaka kumfikia mlaji.

Daktari yule aliniambia kwa miaka takriban 25 ameacha kula chakula kilichopikwa, alipoanza ilikuwa ngumu lakini sasa hivi hawezi tena kula chakula chochote kilichopitia moto. Kwa muonekano yule daktari anaonekana ana miaka 35, nilishangaa aliponiambia ameshagonga 50 kama miaka miwili iliyopita.

Dieat yake:
Breakfast; embe na ndizi mbivu au papai na ndizi mbivu pamoja na kikombe cha mchanganyiko wa nuts hii ndiyo supplement ya protein. Chai na kahawa ni sumu kubwa ya mwili, kunywa maji tu ukimaliza kula hivyo. Kwasababu digestion ya matunda ni haraka, hakikisha una matunda yaliyotaarishwa na unaweza kula baada ya saa moja au masaa mawili.

Lunch;
Kabich lililokatwa katwa, matango (cucumber), nyanya, unaweza kuweka limao kwa ladha pia ni source ya vitamin C, vipande vya mhogo au viazi vitamu unatafuna vibichi na kikombe cha mchanganyiko wa nuts unamalizia na maji. 

In between hakikisha unaandaa matunda na cucumber kama bites kwasababu digestion inakwenda haraka.

Dinner;
Carrots zilizokatwa katwa, kachumbari ya nyanya kitunguu na cucumber unanyunyiza olive oil kijiko kimoja cha chakula, nanasi na kikombe cha mchanganyiko wa nuts na glass ya maji.

Wengine wanafanya water therapy yaani in between meals wanakunywa maji haya yanasaidia pa kutokusikia njaa.

Ukianza hivyo hutaweza kuwa na excess fat.

Kama Kweli Una Ndoto za Kufanikiwa, Kaa Mbali na Hawa!

$
0
0

WIKI hii msomaji wangu nataka kuwazungumzia baadhi ya watu ambao wao wapowapo tu, wameridhika na maisha yao duni lakini haohao ndiyo wako mstari wa mbele kuwakatisha tamaa wenzao wanaopambana kutimiza ndoto zao.

Ukweli ni kwamba, maisha ya sasa yana changamoto nyingi, wanaoweza kuishi kwa furaha ni wale ambao kila siku wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii, lengo likiwa ni kuyaboresha maisha yao pamoja na wale wanaowategemea.

Achilia mbali hao ambao wanapambana kuyaboresha maisha yao, wapo ambao wamekuwa wakiota kuwa na mafanikio makubwa sana. Wamekuwa wakiumizwa vichwa vyao juu ya nini wafanye ili mwisho wa siku ndoto zao ziweze kuwa kweli.

Hawa ni wale wanaojua maana halisi ya maisha. Wanajua mafanikio ni kwa kila mtu na kwamba anayeishi ilimradi siku zinakwenda, hawezi kuwa na faida yoyote kwenye jamii anayoishi. Wenye mawazo hayo ndiyo wale ambao siku hadi siku huona mabadiliko katika maisha yao.

Wanaaga umaskini kwa kasi huku wakiona mwanga wa kutimiza ndoto zao. Mimi na wewe tunatakiwa kuwa hivyo.

Kuamini kwamba maisha ya kuwa na uhakika wa kula, kulala na kuvaa tu siyo tuliyopangiwa. Maisha sahihi tuliyopangiwa ni kuwa na uhakika wa kujipatia mahitaji hayo muhimu lakini pia kuwa na ziada ambayo itatufanya tuwasaidie wale ambao hawana uwezo.

Hapa nawazungumzia walemavu, watoto yatima na wazee. Hawa wanahitaji msaada wako, sasa kama utaridhika na maisha eti kwa kuwa umeweza kujikimu wewe na familia yako, utakuwa unakosea. Lakini sasa wakati wewe na mimi tukiwa kwenye jitihada za kutimiza ndoto zetu, wapo watu ambao wanashangaza sana.

Nawazungumzia wale ambao wamekuwa na tabia ya kuwakatisha tamaa wenzao
wenye uchu wa mafanikio. Watu hawa wapo huko mtaani. Unakuta wewe unakesha usiku na mchana, unapambana ili kutimiza ndoto zako, anatokea mtu kwa chuki zake anakuendea kwa mganga ili usifanikiwe au anakutia maneno ya kuvunja moyo ili usitimize malengo yako.

Watu hawa ni wabaya sana na unatakiwa kukaa nao mbali. Inawezekana kabisa wewe huna shida ya kufanikiwa, umeridhika na maisha yako duni unayoishi, kwa nini sasa uwe kizuizi kwa wengine wanaotaka kuzifanya ndoto zao ziwe kweli? Siku zote safari ya kuelekea kwenye mafanikio siyo ya ‘lami’, ina mashimo, milima na mabonde kiasi kwamba ili kufika kule unakotaka, inahitaji moyo na sapoti pia kutoka kwa watu wanaokuzunguka.

Ukiwa umezungukwa na watu wenye wivu, chuki na husuda, kufanikiwa kwako itakuwa ni kazi sana, waepuke hao! Ndiyo maana unashauriwa kuchagua marafiki, washauri
sahihi ambao unaamini ukiwashirikisha kwenye mawazo yako, wanaweza kukuunga mkono na kukupa sapoti inayostahili badala ya kukuvunja moyo.

Pointi ya msingi leo ni kwamba, mimi na wewe tunatakiwa kuhakikisha ndoto zetu zinatimia. Kikubwa ni kuzishughulisha akili zetu na kuweka malengo kwa kupita kule walikopita wale waliofanikiwa kabla yetu. Kingine ni kuhakikisha tunachagua watu sahihi wa kuwashirikisha mipango yetu ya kusaka mafanikio.

Siyo kila mtu atakuunga mkono, wengine watakukatisha tamaa, hiyo chukulia ni changamoto. Mwisho nishauri tu kwamba, kama wewe huna tamaa ya kufanikiwa, waache wenzako wanaojua lengo la kuletwa hapa duniani watimize ndoto zao.

Kama unajua huna uwezo wa kufanikiwa labda kutokana na sababu unazozijua, basi watie moyo wenzako kwani kufanikiwa kwao kunaweza kuwa na faida kwako.

Kama Una Tabia Hizi, Mafanikio Utayasikia kwa Wenzako Tu...!!!!

$
0
0

Najua fika wapo ambao wamemaliza mwaka wa 2016 wakiwa hawajatimiza malengo yao ya kuwa miongoni mwa watu waliofanikiwa. Wewe unayesoma makala haya unaweza kuwa miongoni mwao, inaumiza sana!

Hata hivyo, huu siyo wakati wa kujilaumu bali unatakiwa kujipanga upya na kuanza tena pale ulipoishia, naamimi Mungu atakuwekea mkono na huenda mpaka mwaka unaisha utakuwa umefanikiwa.

Lakini sasa, nikupe angalizo tu kwamba, kama utakuwa ni mtu mwenye tabia hizi nitakazozieleza hapa chini, mafanikio utayasikia kwa wenzako tu.

Kutenda kabla ya kufikiri
Tabia ya kwanza ya watu wasioweza kufanikiwa kimaisha ni hii ya kutenda jambo kabla ya kufikiria. Watu wa aina hii huwa wepesi sana kununua vitu barabarani mara tu wanaposhawishiwa na macho au wauzaji.

Utakuta mtu bila hata kujiuliza faida za kitu hicho anaamua haraka kukipata. Ataamua kwa haraka kuoa, kuolewa, kukubali kujiingiza katika mapenzi na hata kufanya jambo lolote bila kujiuliza atanufaika vipi?

Kupenda kuzungumza zaidi ya kusikiliza
Watu ambao pia wako katika hatari ya kutofanikiwa ni wale ambao daima ni wazuri katika kuzungumza kuliko kusikiliza. Wao huwa ni wajuaji wa kila kitu, hawako tayari kupokea ushauri.

Siku zote wanapokuwa kwenye makundi ya watu, pengine wajuzi zaidi yao wao huwa hodari kujenga hoja kutetea mambo yao hata kama hayafai. Unaweza kumkuta mtu ni kiongozi wa ngazi za juu, amefanya kosa na watu wote wameona kuwa kakosea lakini mhusika hujiona si mkosaji.

Mtu anapokuwa muongeaji sana huwa mgumu kupokea ushauri wa yeyote, anachoamua yeye hukifanya kwa imani kuwa kinafaa. Ukiwa mtu mwenya tabia ya aina hii huwezi kufanikiwa kabisa katika maisha yako.

Watafiti wa masuala ya biashara ulimwenguni waliwahi kushauri kuwa, mipango mizuri ya kibiashara hutoka kwa watu maskini, ambao walisema hufikiri zaidi namna ya kujikomboa kuliko matajiri wanavyofikiri katika kujiendeleza, hivyo wakasema kama mtu anataka kufanikiwa kibiashara lazima asikilize mawazo ya maskini si kuwapuuza kwa kujiona ni bora zaidi yao.

Kukata tamaa mapema
Watu wanaotaka kufanikiwa huchukulia kushindwa kama hatua ya kuelekea kwenye mafanikio, lakini watu wasioweza kufanikiwa wanapojaribu mara moja au mbili kuvuka kikwazo fulani cha kimaisha na kushindwa, hukata tamaa na kutotaka kujaribu tena kusonga mbele.

Wenye tabia ya kushindwa kimaisha hawako tayari kudumu na jambo moja linaloonekana kushindikana kwao kwa muda mrefu. Akiona mwanamke ambaye ni mkorofi kidogo, haraka hukimbilia kumwacha na kutafuta mwingine, mara nyingi si watu wavumilivu.

Akijaribu biashara ya vitumbua kwa wiki moja na akaona havinunuliwi, anaanza kupika maandazi, wiki moja baadaye yuko kwenye mihogo, basi ilimradi kuhangaika kusikokuwa na tija katika maisha.

Usioghope Kuachika, Ogopa Kuchanika...!!!!

$
0
0

JAMANI salama huko mliko maanti zangu wa kisasa? Leo nimeamka nimechokachoka hata sijui kwa sababu gani, maana jana nimelala mapema tena nikiwa hata sijafanya kazi ngumu. Ingekuwa zamani ningesema wachawi wamenifanyisha kazi, lakini siku hizi, wanipate wapi, nalala na kitabu kitakatifu, waje wauone moto wake!

Hata hivyo, nikasema siwezi kuwaangusha mashosti zangu, lazima niwape kitu roho inapenda, si ndiyo makubaliano yetu bwana? Basi leo sasa ndiyo nataka niwape makavu mubashara, maana kila siku tumezoea kubembelezana hatutaki kupeana live!

Tunalo tatizo moja sisi wana wa kike, tukishawekwa ndani na hao watu wetu, kuachika tunaona kama mikosi, tunaogopa kuchekwa, kunangwa na hata kudharauliwa, kwa sababu tu, eti umeachika.

Nataka niwaambie kitu kimoja, katu usiogope kuachika, ilimradi tu kuachika kwenyewe, kuwe kwa haki. Ndiyo, sasa kwa nini uogope kuachika, yaani hata kama unachanika? Aka babu, usijikwaze.

Maana kuna wengine unapatwa na makwazo kwelikweli ndani ya nyumba, huyo bwana ana gubu, mawifi wana magubu, ilimradi hupumui! Ya nini bhana, mtoto wa kike jiondokee zako, tena uwe na tabasamu usoni!

Niwaambie ukweli, hapa mnaponiona, nimeishi na mabwana watatu na nimeolewa mara mbili, yaani kama hunielewi, wakati nakua natafuta mji wangu, nimeshakaa na wanaume watatu tofauti, wote nikaona wananizingua, nikaachana nao. Ndiyo nikampata mwanaume akanioa, nikazaa naye watoto watatu, nikaachika!

Unadhani hata nilikonda? Siku hiyohiyo narudi nyumbani kwetu, usiku nikaenda ngomani. Afu anicheke nani, kila mtu alikuwa anajua jinsi gani nilimvumilia yule mbaba. Ndiyo baadaye nikampata huyu mzee, ninayeishi naye hadi Mungu atutenganishe.

Kwa hiyo ninachowaambia, msiogope kuachika kuliko mchanike moyoni, kitu cha msingi ni je, wewe ndiye mkosaji au yeye. Kama ni wewe, ona aibu kabisaaa, usikimbie ndoa yako, jishushe, zungumza na mwenzio myamalize, maana katika maisha ya kinyumba, kugongana ni jambo la kawaida.

Lakini kama mkosaji ni yeye, msome. Kuna wengine ujue wanakosea lakini wenyewe hawajui kama wanakosea. Unaweza kuwalaumu kumbe walaaa, hawajui kama wanakukwaza. Sasa hapa lazima uwe makini, unatakiwa umwambie, mwenzangu hivyo unavyofanya mie sipendi!

Anatakiwa ajue kabisa kuwa hupendi, yaani hupendi. Sasa ukiona kila ukimwambia yeye ndiyo kwanza anaendelea, ujue huyo ana lake jambo, usije msichana ukanyauka wakati bado, akhaa. Hata pawe na hela vipi, maisha ya moyo kusononeka hayana ubora!

Na ili uende sawa, usijiondokee tu kama mtu asiye na kwao, wahabarishe wazazi, kwamba jamani mie huku nimeshindwa. Ninavyojua, wao watajaribu kuweka sawa na najua kama huyo mwenzio ndiyo tabia yake, siku zote tabia mazoea, atashindwa tu.

Muda wa kusepa ukifika, usikonde, chukua kilicho chako ujirudie kwenu. Cha msingi, mtaji mkubwa wa mwanamke, ni thamani ya mwili wake, utunze ukusitiri mbele ya safari!

Ukweli Mubashara...Muache Achague Mwenye Kumpa Raha!..!!!

$
0
0

NI Jumatatu nyingine yenye kila neema machoni pa Mungu, zipo changamoto za hapa na pale zinazokukabili msomaji wangu , lakini nikutie moyo tu kuwa kamwe usithubutu kukata tamaa, hayo ndiyo maisha.

Amini tu! Bila shaka kila mzazi anapenda au anatamani mwanaye aangukie mikononi mwa mpenzi mwenye sifa anazotaka yeye. Kwa mfano, anatamani mwanaye kipenzi awe wa kike au wa kiume apate mpenzi mwenye elimu, fedha, mali na kadhalika.

Kama ni suala la kutoa mapendekezo kwa mwanao siyo jambo baya lakini ni lazima ujue kuwa hata mwanao naye ana chaguo lake. Hivyo ni vyema yeye ndiye ukampa nafasi ya kumchagua mtu wa kumpa raha katika maisha yake.

Katika makala haya ngoja nijikite zaidi kwa wazazi wenzangu, maana hata mimi nina mtoto anayeweza kuoa au kuolewa muda ukiwadia.

Wazazi wamekuwa na tabia ya kulazimisha kijana au binti yao aoe au aolewe na f’lani kwa sababu ya kitu f’lani. Hii si sawa, huko ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi, labda kama ameridhia au kaomba mzazi umsaidie kumtafutia, jambo ambalo nalo pia si sahihi.

Lakini si kwa matakwa yako au kumlazimisha, hii ni hatari sana hasa kwa karne hii ya sayansi na teknolojia. Kama kweli raha jipe mwenyewe, basi muache mwanao amchague mwenyewe wa kumpa raha na siyo kumchagulia.

Maana ukimchagulia, akienda huko yakamshinda, lazima ujue lawama zote atazielekeza kwako. Kila akikorofishana na mwenza wake, ataanza kulia na kulaumu kama kuwa isingekuwa wewe kumchagulia mwanamke au mwanaume wa kumuoa, basi asingekuwa anapata mateso kama anayopata katika kipindi husika atakachokuwanacho.

Kusema kweli, suala hili la kuchaguliwa mwanaume au mwanamke wa kuoa linazitesa ndoa nyingi kwa sasa, linawatesa watoto wetu kama ulikuwa hujui kadiri zinavyozidi kusonga mbele, suala la harusi au ndoa linaonekana kupungua siku baada ya siku, vijana wa kike na wa kiume ni mara chache sana kufikia hatua ya kuoana kama zamani zaidi ya kufanya uasherati.

Hivi kama mwanao amerukaruka huku na kule, kijiji kizima anajulikana kwa mawenge yake, leo amepata mchumba wa kumuoa au kuolea naye, una sababu zipi za kumkataa mchumba wake na kutaka aolewe au amuoe unayemtaka wewe? Ingawa unaweza ukachaguliwa na ukabahatika kumpata mwenza mwenye upendo na mapenzi ya dhati, lakini katika kipindi tulichonacho ni heri kila mtu akabeba msalaba wake.

Wajue Mabinti wa Kimbulu (Wairaq) Katika Masuala ya Mapenzi..!!!

$
0
0

Leo nimeona niwajuze machache kuhusu hili kabila la wambulu(wairaq) hususani mabinti yani tabia zao, wawapo katika uhusiano na kadhalika!

Kwanza mabinti wa kiiraq asilimia kubwa ni weupe kwa maana ya rangi ya ngozi zao, kwa upande wa nyele(za kichwani) sio siri wamejaliwa kwani ni laini, ndefu na zinazong'aa hususani ukutane na yule ambaye hajachanganyika na kabila jingine.

Mabinti wa kimbulu si wafupi kwani utafiti niliofanya nimegundua kuwa wengi ni warefu japo si sana ila kimo chao wengi wanavutia! 

Kwa upande wa sura ni wazuri sana tuu, ila wengi hawana maumbo ya kibantu(namba nane) na kwa upande wa makalio ni kawaida si kama wale wa kitanga au kwingine waosifika kwa makalio ya haja!Huo ndio muonekano wa hawa dada zetu wa kimbulu ki maumbo!

Saa acha nikujuze kuhusu mtazamo wao wa maisha ya mapenzi japo siwezi kuwa sahihi aslimia mia moja ila nitakuwa nimepatia kiasi fulani!

Wengi wao wanapenda sana kuna na mpenzi wa kabila lao, na hii inasababisha walio waoa mademu wa kiiraq halafu wakaenda nao mjini na ikitokea wakakutana na mtu wa kabila lao huku jua upo uwezekano mkubwa ukaibiwa kiurahisi sana!

Si wavumilivu wa mambo hususani pale kukiwa na financial problems jua uwezekano wa kukimbiwa ni mkubwa sana, kamahii haitoshi madem hawa wanasifa ya kupenda sana madereva wa magari ya tours companies (hapa bado nachunguza nijue ni kwa nini) maana nimegundua kuwa asilimia kubwa ya hawa mabinti wanamegwa na hawa jamaa!

Na kunako majamboz wengi wao hawana mbinu za kiuchokozi kama yale makabila ya pwani kwani unaweza maliza dakika 90 bila kupewa ushirikiano unaostahili.

Ndugu zangu hao ndio mabinti wa kimbulu aka wairaq.

Note: kama unatafuta demu mwenye sura nzuri tena natural basi hawa wanafaa sana ila kwa upande wa uaminifu na uvumilivu majibu ni hayo hapo juu!

Bunge Liko Kwenye Majaribu Makubwa- Lema

Kimenukaa..Nape Nnauye Aaanza Kuichana Serikali ..Amtaja Magufuli na Mwakyembe..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote.

“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!" 

Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia juzi ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao unaikashifu serikali. 

Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, jana mchana alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi  kumuchia huru msanii huyo na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uendelee kuchezwa  kwenye vyombo mbalimbali,
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images