Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Lissu - Nikikutana na Rais Magufuli Nitamsimanga na Kumpa Vidonge Vyake..!!!

0
0

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesema uongozi wa chama hicho umemwandikia Rais John Magufuli kutaka kukutana naye Ikulu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi na kufanya mazungumzo.

“Ni mkutano baina ya Rais na rais,” alisema Lissu katika mahojiano na gazeti hili alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.

Lissu, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki, alichaguliwa kuwa rais wa chama hicho mapema mwezi huu, na Rais ni mmoja kati ya viongozi kadhaa waliowaandikia kuomba kukutana nao.

Aliwataja wengine kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na marais wawili wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Alisema tayari Jaji Mkuu ameshakubali ombi lao.

Kuhusu ombi lao kwa Rais Magufuli, Lissu alisema atatumia fursa hiyo vizuri, iwapo watakubaliwa.

“Nikifika nitaanza kwa kumshukuru Rais kwa kuwafundisha Watanzania maana ya utawala wa sheria, uhuru wa mawazo, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Mahakama na Bunge,” alisema Tundu Lissu.

Lissu alifafanua baadaye kuwa Rais Magufuli amefumbua wengi macho kujua vitu hivyo kutokana na jinsi anavyoendesha nchi, ndio maana atamshukuru.

“Tumeomba appointment na Rais Magufuli tuzungumzie utawala wa sheria,” alisema Lissu.

“Leo ni Jumatano? Barua tulimpelekea Jumatatu. Tutaenda kujitambulisha na kuzungumzia utawala wa sheria na mwelekeo wa taifa hili. Ni between presidents. Tuna imani kwamba atatukaribisha. Tutamweleza maoni yetu, pale tunapoona amekosea tutamweleza na pale anapoona tuna matatizo atatueleza.”

Alisema wanajua kuwa Rais ana shughuli nyingi, lakini wanatarajia atatenga muda kwa ajili yao.

“Tunafahamu yuko busy, lakini kama anaweza kuangalia Shilawadu, atakuwa na muda hata nusu saa au saa nzima ya kuongea na kiongozi wa chama cha mawakili wa Tanganyika,” alisema.

Lakini akaonyesha jinsi alivyopania kueleza matatizo anayoyaona katika utawala wa sasa.

“Nakwenda kumpa vidonge vyake, kabisa! Wala sitammezea. Nitamwambia kwa heshima zote kwamba Mheshimiwa Rais, sisi kama mawakili wa Tanganyika tuna wasiwasi mkubwa na mwelekeo wa Serikali yako,” alisema.

“Wamenituma nikueleze mwelekeo na matendo ya Serikali yako. Unatawala vibaya, nje ya Katiba, wameniambia nije nikwambie ujirekebishe. Nakwenda kumsimanga tu. Halafu tukitoka pale namwambia Mheshimiwa Rais tupige picha, wajue nilikuja.”

Alisema iwapo Rais hatakubali kuwaalika, ataueleza umma.

“Atakuwa amenirahisishia, nawaita waandishi wa habari nawaambia. Tulimwambia Bwana mkubwa tumsalimie na tumweleze kwamba haturidhiki na utawala wake, yeye amekataa amekimbia,” alisema Lissu.

Hata hivyo, mkuu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa amemtaka Lissu kusubiri taratibu za kiutawala.

Msigwa alimshangaa Lissu kwa kitendo chake cha kuzungumza katika vyombo vya habari ilhali anajua utaratibu wa kiutawala.

“Yeye kama ameandika barua barua si asubiri majibu? Muulizeni inakuwaje kabla hajapewa majibu anaenda kutangaza katika vyombo vya habari? Si asubiri utaratibu wa kiutawala,” alisema Msigwa.

Lissu alisema ofisi nyingine walizopeleka maombi kama hayo ni ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba Kabudi alisema hana taarifa juu ya barua hiyo kwa kuwa tangu ateuliwe hajaingia ofisini.

“Nimekuwa katika vikao vya Kamati za Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma, hivyo sina habari hiyo,” alisema.

Hata hivyo, Profesa Kabudi alisema inawezekana ni kweli rais huyo wa TLS amewasilisha barua hiyo ofisini kwake lakini yeye bado haijamfikia.

Dakika 180 za Makonda Kuwekwa Kitimoto Bungeni...!!!

0
0

HATIMAYE. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhojiwa kwa dakika 180 na kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na kauli aliyoitoa  Februari mwaka huu inayodaiwa kudhalilisha hadhi ya mhimili huo wa Dola.

Makonda akiwa amevaa shati ya maua na suruali nyeusi aliwasili bungeni jana saa 4 asubuhi kuitikia  wito huo uliopitishwa na Bunge Februari 8 mwaka huu, ikiwa zimebaki siku saba tu kabla ya kuanza vikao vya Bunge la Bajeti.

Siku hiyo ya Februari 8, Bunge lilitumia dakika 45 kupitisha kwa kauli moja maazimio manne, likiwemo la kuitwa kwa Makonda na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti kutokana na hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara akisema wateule hao wa Rais wametoa kauli zinazodhalilisha Bunge.

Wakati Makonda akisema wakati mwingine wabunge hulala bungeni kwa kukosa cha kuzungumza, Mnyeti aliandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa wabunge ni wapuuzi kutokana na michango yao wakati walipohoji hatua ya Ma-DC na Ma-RC kutoa amri za kuwaweka ndani viongozi wa siasa.

Hata hivyo,  jana ilikuwa zamu ya mkuu huyo wa mkoa ambaye habari za ndani kutoka katika kamati hiyo zinaeleza kuwa alikiomba radhi chombo hicho cha kutunga sharia, baada ya kubanwa kwa maswali ambayo mengine alishindwa kuyajibu.

Kuhojiwa kwa mteule huyo wa Rais, huenda kukawatuliza baadhi ya wabunge walionukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari wakieleza kuwa iwapo Bunge lingeshindwa kumhoji mkuu huyo wa mkoa, moto ungewaka katika vikao vya Bunge la bajeti.

Hata hivyo, mteule huyo wa Rais bado anaweza kuzua gumzo bungeni kutokana na kauli na matukio mbalimbali yanayomhusu, likiwamo la kuvamia kituo cha Clouds ambalo aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye aliliundia tume iliyothibitisha Makonda kuvamia kituo hicho, ambayo hata hivyo yanatajwa kusababisha Nape kuvuliwa uwaziri.

Jingine ni utata wa elimu ya Makonda na madai ya kughushi na kutumia vyeti vya kidato cha nne vya mtu mwingine, ambayo mashtaka yake yamefikishwa Tume ya Maadili ya Viongozi na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob.

Akizungumza baada mahojiano hayo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika alisema, “Leo (jana) tumekutana baada ya kuagizwa na Spika kwa mujibu wa kanuni za Bunge.  Kamati yetu hukutana pale tu inapoagizwa na Spika.”

“Spika aliagiza kamati yetu imuite makonda ili kumhoji kufuatia azimio la Bunge lililopitishwa Februari 8. Pamoja ana mambo mengine alitakiwa kufka mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili.”

Mkuchika alisema kwa mujibu wa azimio hilo, Makonda alidaiwa kutoa kauli hiyo kupitia kituo cha Televisheni cha Clouds kwamba wabunge wanasinzia, jambo alilosema kuwa lilionekana kama dharau kwa Bunge.

“Napenda kutoa taarifa kuwa Makonda leo (jana) amekuja mbele ya kamati na ametupa ushirikiano mzuri, tumepokea maelezo yake na naweza kusema kuwa kamati imemaliza kazi yake iliyoagizwa,” alisema Mkuchika.

Alisema kwa mujibu wa taratibu na kanuni za chombo hicho cha kutunga sheria, kamati yake itakabidhi taarifa ya mahojiano hayo kwa Spika ambaye ndiye atakayeamua namna ya kutoa taarifa kuhusu kazi ya kamati hiyo.

Jide Afunguka ya Kuachwa na Mnigeria Wake

0
0

Jide afunguka ya kuachwa na Mnigeria wake


Wakati maneno ya chini chini yakiwa yanaendelea kuhusu kupigwa kibuti na mpenzi wake mpya Spicy kutoka Nigeria, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amefunguka na kusema wabongo wengi wanapenda wenzao waharibikiwe na kuwataka kuacha kuwaziana mabaya.


Jide amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya maneno kuzagaa kuwa amepigana kibuti na Mnigeria huyo ikiwa ni siku wiki chache baada ya kuandika maneno yaliyomo kwenye wimbo wa  Rosella katika mtandao wa Instagram.


“Niko vizuri na Spicy, yale maneno niliandika kwa ajili ya muziki, watu wanapenda kuona wenzao wanaharibikiwa, kwanini wanakimbilia kuamini nina matatizo na Spicy na hawafikirii kuhusu kazi yangu? Niwakaribishe waje kwenye show yangu ya uzinduzi pale Lugalo Uwanja wa Gofu Ijumaa hii,” alisema Jide.


Lady Jaydee anayetamba na wimbo wa Rosella alioshirikiana na h_art the band kutoka Kenya anatarajiwa kuzindua albamu yake ya saba tarehe 31 ya mwezi huu.

Heh! Kumbe kuna Harmonize...!!!!

0
0

NI nadra sana kwa sasa kama utatembelea kwenye mitandao ya kijamii usikutane na jina la Harmorapa akizungumziwa kwa ishu yoyote ile, iwe kwa kupondwa, kusifiwa na hata kusanifiwa, yeye kila kitu ni sawa tu ilimradi atimize ndoto zake. Harmorapa ambaye hana hata mwaka mmoja kwenye gemu la muziki, asiye na hit songs hata mbili tu kwenye tasnia hiyo, lakini ni mmoja wa wasanii ambao wanazungumziwa zaidi kwenye mitandao kuliko hata Darassa mwenye zaidi ya miaka kumi kwenye gemu, Fid Q au Joh Makini. Kila kona ni Harmorapa.

Upepo alionao si wa mchezomchezo, hakuna anayemzungumzia Harmonize tena pamoja na kumpa umaarufu kijana huyu wa Kimakua kutoka Masasi, Mtwara kutokana na kufanana kwao, ingawa Harmonize hakubaliani na hilo! Inawezekana Harmonize anaamini kama alivyosema Dancer wa Diamond Platnumz, Moses Iyobo kuwa Harmorapa hafanani naye bali anafanana na nyani huku chuki dhidi yake akiionesha waziwazi.

Kuhusu Harmonize kwa sasa hadi ukutane na habari zake ndiyo unashtuka; “Heh! Kumbe kuna Harmonize!” Kila mtu anamzungumzia Harmorapa tu.

Harmorapa ambaye kimuziki bado anajikongoja kutokana na uwezo wake lakini inaonekana uongozi wake ni mzuri katika suala zima la kumtengezea kiki. Kimchezomchezo anazidi kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha bila kujali ametengeneza kwa kudhihakiwa, kulia, kupiga magoti, kutukanwa na mambo mengine mengi lakini mwisho wa siku ni yeye kufahamika.

Kwa mambo yanavyoenda si ajabu kusikia Harmonize amesahaulika kabisa kama Harmorapa ataendelea kukua kama ilivyo sasa. Ni ukweli kuwa wakati ‘dogo’ huyo alipoanza kuchomoza na kupata kiki kwenye midia mbalimbali, baadhi ya watu walikuwa wanamuhesabia siku za kupotea, wengine wakampa wiki kadhaa, wengine miezi lakini upepo umekuwa tofauti na mitazamo ya wengi na sasa Harmorapa anazidi kupaa tu.

Nyota ya kinda huyo inaonekana kung’ara kila kukicha, hivi karibuni ‘alimeki headline’  kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari kufuatia kitendo chake cha kutimua mbio baada ya kuona ‘mdomo wa bata’ (bastola) aliyotolewa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye.

Baada ya Harmorapa kutimua vumbi kwenye sakata la Nape, vibonzo, magazeti na video mbalimbali zilisambaa mitandaoni jambo lililosababisha kinda huyo kupewa Ubalozi wa Kinywaji cha Swala huku akipata mashavu ya shoo kadhaa ikiwemo ya kukata na shoka ya Dar Live kwenye Usiku wa Pasaka. Katika nukuu zake, Fid Q aliwahi kusema kuwa mafanikio hufuata kile unachofanya. Hilo linajidhihirisha kwa Harmorapa, mafanikio yake yanatokana na juhudi zake pamoja na kujitoa ufahamu katika kila jambo ambalo haijalishi litaacha gumzo kwa kupondwa au kusifiwa na watu.

Mbali na kutafuta mafanikio kwa njia yake ya vituko, kimuziki pia rapa huyo anaonesha mabadiliko na kukua, hasa kwenye kibao chake cha Kiboko ya Mabishoo alichomshirikisha Juma Nature. Wimbo huo umepiga hatua kubwa kwa kuanza kuchezwa kwenye kituo kikubwa cha Runinga cha MTV Base.

Ushauri kwa Harmonize ni vyema akawekeza nguvu nyingi kwenye kazi zake, hana sababu ya kuonyesha chuki kwa Harmorapa kwa sababu hawezi kuzuia mafanikio yake! Hivi tatizo liko wapi Harmorapa kufanana na Harmonize? Mbona kuna vijana wengi wameibuka na kudai wanafanana na bosi wake, Diamond Platnumz?

Kwani Harmonize ni mtu wa kwanza kufananishwa na mtu? Ni wakati wa kufanya kazi, Harmonize asipoangalia atazidi kupotea na kushindwa kuelewa ni wapi alipoteleza, huku akimshuhudia huyo ‘nyani’ akizidi kupanda kwenye matawi ya juu ya mti wa mafanikio.

Kimenukaa..Mama Yake Hamisa Mobeto Atolea Kichambo Hiki Zari the Boss Lady,Amtaka Akome Kumtajataja Mwanae Mitandaoni..!!!

0
0

DAR ES SALAAM Skendo ya mjini iliyotapakaa mjini na kwenye mitandao ya kijamii inamgusa modo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto akidaiwa kujichora ‘tatuu’ ya mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ishu iliyosababisha mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumporomoshea matusi.

Kuhusu sakata hilo, mama mzazi wa Mobeto ameshindwa kujizuia na kujikuta akimtolea povu Zari juu ya mwanaye huyo. Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu alipoulizwa kuhusu sekeseke hilo la mwanaye, mama Mobeto alisema kuwa, hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.

“Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,” alisema mama Mobeto. Alifunguka kuwa, habari ambayo imesambaa kuhusu mwanaye kujichora tatuu ya Diamond, anaona ni mambo ambayo hayana msingi wowote zaidi ya kumchafua na kumdhalilisha mwanaye.

“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta kumuwekea jambo baya,  kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” alisema mama Mobeto.

Hivi karibuni Zari alimtolea matusi Mobeto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akimtahadharisha juu ya habari zilizozagaa kuwa, huwa anachepuka na Diamond kwa siri hasa mwanamama huyo anapokuwa nyumbani kwake, Afrika Kusini na kumwacha baba watoto wake huyo jijini Dar.


Ubuyu wa Moto Moto..Mama Wema Atuhumiwa Kudendeka na Alex Msama,Ubuyu Wote Uko Hapa..!!!

0
0

 Hatari! Mama mzazi wa muigizaji mkubwa wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, Miriam Sepetu anadaiwa kuitikisa ndoa ya mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Msama, Risasi Mchanganyiko limepewa mchongo mzima.

ANA KWA ANA NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na ishu hiyo, mtikisiko huo mkubwa ulitokea ndani ya familia ya muandaaji huyo wa matamasha ya Injili baada ya mkewe kukuta ujumbe mfupi wa maneno katika simu ya mumewe, hivyo kusababisha mtafaruku.

“Sijui hasa nini kilitokea, lakini nilicho na uhakika nacho ni kuwa ndoa ya wawili hao ilikuwa katika majaribu makubwa wakati huo, maana kulionekana kuwepo kwa mawasiliano ya mara kwa mara baina ya Msama na Mama Wema, kitu ambacho mkewe alishindwa kuelewa. “Msama alijitahidi sana kupooza mambo kwa kujaribu kumuweka sawa mkewe, lakini bado ikawa ngumu hadi baadhi ya marafiki wa karibu wa pande

WAANDISHI WETU, RISASI zote mbili walipoingilia kati na kuliweka sawa jambo hilo na hivyo kupoa,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilisema wakati mmoja katika mtafaruku huo, wanandoa hao walikuwa hawazungumzi, kitu ambacho kilitishia sana uhai wa ndoa hiyo. Baada ya kupata taarifa hizo, Risasi Mchanganyiko lilifanya juhudi kubwa za kuwatafuta wawili hao, likifika ofisini na nyumbani kwa nyakati tofauti lakini mara zote likiambulia patupu. Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Msama alipatikana kupitia simu yake ya mkononi.

HUYU HAPA ALEX MSAMA

“Ni kweli, ndoa yangu ilipata mtikisiko mkubwa sana kwa sababu ya Mama Wema, mke wangu alikuta mawasiliano baina yangu na yule mama kwenye simu, akaja juu. Alikuwa akiniuliza huyu ni nani na kwa nini nawasiliana naye mara kwa mara.

“Nilikuwa nawasiliana naye mara kwa mara kwa sababu nilikuwa na biashara naye. Unajua kuna kipindi nilitaka kununua nyumba yake, nikawa wakati mwingine ninampa hela kidogokidogo, sasa katika biashara kubwa kama ile ni lazima mtakuwa mnawasiliana mara kwa mara.

“Mke wangu alipokuwa anaona meseji nyingi kutoka kwake, akawa anahisi kuna kitu, lakini nilijitahidi kumweleza kuwa ni kwa sababu ya biashara tu, hatimaye alinielewa, mambo yakaisha na sasa kila kitu kiko vizuri,” alisema Msama. Mke wa Msama ni mtangazaji wa kituo kimoja cha Redio, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

VIPI KUHUSU PESA ZAKE?

Risasi Mchanganyiko lilimuuliza Msama hatima ya fedha zake za maudhiano ya nyumba ambazo hivi karibuni alilazimika kutumia Polisi ili kumkamata, baada ya kudai kuwa mama huyo alichukua fedha, lakini badala yake akamuuzia mtu mwingine.

“Hapa ni lazima niwe mkweli, siwezi kukubali huyu mama achukue tu fedha zangu kirahisi atoweke, ninasikia faili lake tayari limeshafika kwa Mwendesha Mashtaka wa serikali, ninachotaka mimi ni vyombo vya sheria kufanya kazi yake ili haki itendeke.

“Sitakubali mazungumzo, maana watu kama hawa wapo wengi sana hapa mjini, wanafanya mambo makusudi, wakitegemea huruma, siwezi kuwa na huruma na mtu ambaye anadhani udanganyifu ni jambo zuri, suala hilo ninataka limalizike mahakamani,” alisema Msama ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Habari ya Msama Media Group.

MSAKO WA MAMA WEMA

Mbio za kumsaka Mama Wema zilishika kasi na kulifikisha Risasi Mchanganyiko hadi nyumbani kwake, Sinza Mori, lakini msichana aliyefungua mlango alisema mwanamama huyo, aliyegonga vichwa vya habari wiki chache zilizopita kufuatia sakata lake na Steve Nyerere, hakuhitaji kuonana na mtu yeyote kwa wakati huo.

Kuona hivyo, waandishi wetu walimtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi, lakini licha ya kuonyesha kuwa ujumbe huo ulifika na kusomwa, hakurudisha majibu.

TUJIKUMBUSHE

Alex Msama na Miriam Sepetu wamejikuta wakiingia katika mtafaruku baada ya kushindwa kuelewana katika suala lao la mauziano ya nyumba ya mama huyo iliyopo Sinza Lion.

Taarifa za awali zilizoandikwa na gazeti hili, zilisema mama huyo alitaka kuiuza nyumba hiyo kwa Msama, lakini mfanyabiashara huyo alichelewesha malipo na kumfanya aiuze kwa mtu mwingine. Hadi anafikia uamuzi wa kufanya biashara na mtu mwingine, inadaiwa kuwa tayari alikuwa ameshachukua kiasi cha shilingi milioni 16 kutoka kwa Msama.

Namna Mchezo wa Ku-Bet Unavyofanana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya...!!!!

0
0

Madawa ya kulevya ni addictive kwa sababu mtumiaji anapotumia kwa mara ya kwanza kuna raha kubwa anaipata anapoyatumia kwa mara ya kwanza

Baada ya kuipata hii raha basi atajaribu kutumia tena madawa haya kuitafuta ile raha aliyokuwa ameipata mwanzo..lakini huwa haipati raha kama ya mwanzo, na inampelekea kuongeza kiasi cha dozi kila mara akijaribu kuitafuta na kuirudia rudia hadi anaharibikiwa kabisa

Kwenye ku bet sasa..
kutokana na kuwa na marafiki wa kiume wanao bet nime observe kubet nako ni sawa na matumizi ya narcos tu.

Kubet na kwenyewe kunaleta furaha kubwa sana endapo yule anaye bet atafanikiwa kupatia utabiri wake na kushinda fedha nyingi

Ule mshawasha wa kusubiria matokea na kisha utabiri wako kutimia kunaleta excitement kubwa kwa mcheza kamari

Sasa mcheza kamari anaposhinda hupata furaha kubwa na pia kujiamini kuwa yeye ni mtaalamu kwenye kubashiri

Kwa hiyo ataendelea kucheza kamari kwa sababu ya furaha ya kupata pesa za bure kutoja kwenye mchezo anaoupenda na kujiamini ni mtaalamu

Na kwa kuwa mchezo wa kamari upo based kwenye kanuni za probability ambazo zinampa nafasi kwa mchezaji na mwenye kampuni nafasi za kushindaa lakini chances za mcheza kamari kushinda always zinakuwa ni ndogo kuliko za kampuni...yaani hazipo 50%/50%, ni lazima mchezaji ataumia tu in the long run

Na kwa kuwa saikolojia yake ishaathirika yeye anajua atashinda kesho kama akikosa leo kwa kuwa keshashinda mwanzo

atacheza atashindwa ila hata akimaliza fedha yake atakopa ili airudishe fedha yake aliyopoteza

so atashinda na kushindwa (lakini atashindwa mara nyingi zaidi kwa kuwa odds always zinakuwa favourable kwa betting company)

so mwisho wake atauza hata mali zake kupata fedha ya kamari kama hana self control na ku realise kuwa yeye ni ndiye loser kwenye huu mchezo

Mbinu 5 Kali za Jinsi ya Kutongoza Msichana Yoyote Mrembo na Akubali...!!!

0
0

Je , unamtamani msichana mrembo ambae kwa sasa ni kama marafiki ? au unavutiwa na yule demu unayemuona kila siku mtaani na unashidwa kujizuia sema hujui uanzaje ? Haijalishi kama unamjua au hamjuani , ila inapokuja kwenye kumtongoza mwanamke unachotakiwa kujua ni uelewa wa vitu kadhaa kuhusu jinsi kutamani kunavyokua na jinsi ya kufanyia kazi ili ufanikiwe .

Kumtongoza demu na vitu unavyotakiwa kujua

kwanza kabisa kama unataka kumtongoza msichana au kumfanya tu akupende tu , inabidi uwe mtu poa ambae anaweza kuvuta macho ya wasichana.

Kama hautaweza kua mtu anayeweza kumvutia msichana kirahisi , utakua bado unauwezo wa kumtongoza mwanamke unayempenda lakini itakua ngumu kuwezesha yeye akukubali .

Kiufupi fatisha njia hizi 11 rahisi na kiukweli kabisa utakua vizuri katika kutongoza na hata kwa mambo mengine yatakayofuata baada ya hapo.

Tumia njia hizi moja baada ya nyingine na ijapokua utacheza karata zako vizuri basi lazima umpate mrembo yoyote unayemtaka hata kama kuna watu wengine kibao wanamfukuzia .

1 . Kua karibu nae

Siku zote , kama unataka kumtokea msichana njia muhimu kabisa ni kuweza kumjua kwa undani .Usikurupuke kurupuke tu ukaanza kutongoza , msichana ataogopa au atakuona mtu rahisi kua nae na mwisho wa siku utaishia kumboa tu .

Ongea nae na upate kumjua vizuri . Mtumie message na usiwe na mzuka , mfanye awe kama rafiki kwanza . Usimtokee kwanza sema pia usisubiri sana maana ataanza kukuchukulia poa .

2 . Kua mtu unayependeka

Hii ni hatua muhimu sana . Na huu ndio wakati utagundua kama anahisia na wewe kweli au anakuchezea akili . Pia unapoongea nae mara kwa mara jaribu kugundua vitu anavyovipenda. Jaribu kuweka ukaribu nae kwenye kitu ambacho wote mnakipenda.

3 . Usilale Usiku

Ndio maana mitandao mingi ya simu ikawapa ofa za usiku watu kama nyie muongee usiku kucha . Usiku ndio muda sahihi wa kuweza kutoa ya moyoni na kueleza hisia zako kwa msichana . Anza kwa kuweka maongezi ya kawaida na kadiri unavyoendelea weka vionjo fulani vitakavyomfanya aanze kuingia line bila kugundua kama unamtokea.

4 . Ishi Maisha mawili

Unapoongea nae usiku , mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi sema mkikutana ana kwa ana mchana usiongelee mambo ya mapenzi kabisa labda aanze yeye na hivyo kumaanisha ashaingia line na anapenda maongezi hayo .

Pia epuka kuongelea kuhusu mambo yenu ya kimapenzi mnapokua na marafiki wengine bali fanyeni hivyo mkiwa wawili . Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuna uhusiano motomoto wa siri unapikika kati yenu.

5 . Usimfanye ajue unampenda

Wanaume wengi ufanyaga kosa hili kubwa . Wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao . Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari . Au hajui ? Unampigia simu kila saa , mnataniani kimapenzi na anaona uhusiano wenu kabisa .

Kwahiyo japokua anahisi unampenda , usije kuonyesha hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihakikishia hisia zake . Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake , kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo .

Acha Kubaka Wewe...Fahamu Njia Adimu za Kumfanya Mwanamke Afike Kileleni Haraka !!!!

0
0

Kuna njia mbalimbali za kumuongezea wigo mwanamke kufika kileleni na kuna kitu kimoja wanawake wote husema, "Kufika kileleni huitaji utulivu wa akili na hisia ".

Kama ukimweka mwanamke kwenye mazingira mazuri kiakili na kihisia, kuna uwezekano mkubwa na mwili wake kufuata na kumfanya afike kileleni.

Japo wanawake wanatofautiana, imejaribu kuongea na baadhi ya wanawake na wametumegea siri na kutupa njia nzuri ya kumfikisha kileleni mwanamke kwa haraka, japo ilikua mpaka tulipowapa baadhi ya siri zetu za kiume kidogo ndo wakalainika kutuambia...

Kama ukitaka kumfikisha kileleni kwa haraka, ni vizuri mwanamke ukamweka juu yako ili aweze kudhibiti kasi, msuguano na engo ya uume wako ndani yake, japo nawe unaweza kupata matamanio ya kumsaidia, ila ni vizuri ukamwacha mwenyewe ili usije kumharibia kasi anayoitaka yeye na kuitumia.

Inabidi upambane na matamanio yako na uendelee kutulia na umsikilize anataka wewe ukaeje ili ajiongezee msisimko zaidi na kwa sasa inabidi uutulize mwili huku mikono yako ikishughurika na uitumie vizuri, unaweza kuwa unampapasa sehemu za makalio yake au nyuma ya kichwa chake sehemu za shingoni mpaka kisogoni kwa hali ya kimahaba, na kama umekaa wima utajiongezea pointi zaidi kwa kumbusu shingoni na kuongea maneno mazuri ya kimahaba na kumsifia kwa uzuri wake na sifa nyingine

Soma kwa Makini Hii Kitu Itakusaidia...!!!

0
0

HAKUNA anayebisha kwamba ndoa ni jambo la msingi sana katika maisha ya kila binadamu. Aidha, kuoa ama kuolewa ni heshima katika jamii na ndiyo maana leo hii wapo wanaofanya kadiri wawezavyo kuhakikisha wanapata watu wa kuwa nao kama mwili mmoja pale wanapofikia umri wa kufanya hivyo.

Kufunga ndoa kuna wakati wake, siyo kwamba pale unapojisikia kufanya hivyo basi ufanye hata kama mazingira, umri na hali yako kimaisha havikuruhusu. Lakini sasa, kibaya ambacho nimekuwa nikikishuhudia katika jamii yetu kila siku ni kwamba wapo ambao huchukulia kuoa ama kuolewa kama ‘fasheni’, hali ambayo huwasababishia kuingia katika matatizo ambayo hawakuyatarajia.

Ieleweke kwamba hadi kufikia hatua ya kutamka kwamba unataka kufunga ndoa ni lazima uwe umefanya uchunguzi wa hali ya juu na kuhakikisha kwamba unaingia katika maisha ambayo hutajutia. Suala la kuoana si la kukurupuka, ni lazima kwanza uangalie, je ni kweli unastahili kuoa ama kuolewa kwa wakati huo? Hili ni swali la msingi kujiuliza na kama jibu litakuja akilini mwako kwamba muda bado, basi unatakiwa kusubiri. Suala la kuoa ama kuolewa ni la heri na halitakiwi kuharakishwa eti kwa kufuata mkumbo. Kumbuka waswahili wanasema, mambo mazuri hayataki haraka.

Kwako wewe mwanamke, unapodhani umefikia umri wa kuolewa, kwanza unatakiwa kuangalia mwanaume sahihi, ambaye hata utakapoingia kwenye maisha hayo ya ndoa, utadumu na kufurahia. Epuka sana wanaume walaghai ambao mara nyingi hutumia gia za kuoa ili wakubaliwe kimapenzi.

Anapokutokea mwanaume na kukuambia anakupenda na angependa kuwa wako wa maisha, mchunguze kwa muda mrefu kabla hujafanya maamuzi sahihi. Usimkubalie haraka ili nawe uitwe mke wa mtu kama ilivyo kwa rafiki au ndugu yako aliyeolewa hivi karibuni. Kwa ujumla ni kwamba kabla ya kumtamkia yule ambaye ungependa umuite mke na yeye akuite mume ni lazima kwanza mtaanza kuwa wapenzi wa kawaida kisha baada ya kuona kwamba, mmependezana kitabia ndipo mtafikia hatua moja kati yenu kugusia suala la kuoana.

Kama mtaafikiana katika hilo, mnaweza kuingia katika hatua nyingine ambayo ni kwenda kutambulishana kwa wazazi wenu na baada ya hapo mtakuwa ni wachumba ambao mnatarajia kufunga pingu za maisha.

Jambo la msingi ni kuwa makini sana na nyendo za mpenzi wako katika maisha yenu ya kila siku. Mchunguze kwa undani, je anafaa kuwa mke ama mume wako? Anakufaa au umedondoka katika penzi ambalo siyo sahihi? Isije ikatokea eti kwa sababu mmekuwa wapenzi kwa muda mrefu basi atakapokutamkia kwamba anataka kukuoa, basi ukubali tu hata kama umeona kwamba maisha ya ndoa yenu yanaweza kutokuwa ya amani kutokana na kuwepo kwa migongano ya mara kwa mara pindi mlipokuwa wapenzi wa kawaida.

Wapo wapenzi ambao wanaonekana hata wakija kuoana watakuwa na maisha mazuri. Ni dhahiri kwamba wapenzi ambao wamekaa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja na haijawahi kutokea wamegombana, kutukanana, kuvunjiana heshima kwa namna moja ama nyingine, hawa wanaweza kuoana na wakaishi maisha ya raha mustarehe.

Nimalizie kwa kusema waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi na kikubwa zaidi unatakiwa kuwa na imani. Amini kwamba huyo uliyempata ambaye unataka awe mwandani wako ndivyo alivyo na ndivyo atakavyokuwa hata mtakapokuja kuoana. Usiwe na mawazo kwamba anaweza kuja kukugeuka ilimradi tu uwe umempenda na umethibitisha na yeye anakupenda.

Amini ni wako na mnastahili kuwa mke na mume na maisha ya furaha na amani yatakuwa upande wenu.

Mwenye Uume Mdogo Usiwe na Shaka Fuata Ushauri Huu Utakusaidia Kumridhisha Mpenzi..!!!

0
0

Je, ni urefu au unene?
Je, urefu wa uume ni suala muhimu kwa mwanamke kuridhika kimapenzi?Hii ni imani potofu ambayo imewafanya wanaume wengi kujiingiza kufanya surgery za gharama kubwa na wengine kupoteza pesa zao kwa ajili ya kutafuta dawa za kienyeji ili kuongeza maumbile kuwa marefu zaidi.

Huko ni kupoteza muda na pesa.
Ingawa urefu wa uume hauna umuhimu kama imani potofu inavyodai bado suala la msingi ni uimara wa misuli ya uume; kwani misuli ya uume ikiwa imara basi mwanaume huwa na uwezo (strength/flexibility) ambayo itaweza kumpa sifa mume kwa mke wake kuliko kushabikia kuwa na jumbo size.


Hii ina maana bila kujali una urefu kiasi gani au ufupi kiasi gani, kama una misuli imara hilo ndilo jambo la msingi kwa mwanaume.


Tuweke suala la hiyo imani potofu pembeni hivi ni kitu gani mwanamke huhitaji physically ili afurahie tendo la ndoa?Suala la muhimu ni kuwa na ufahamu wa anatomy kuhusu mwanamke (uke); ukweli ni kwamba nervesnyingi zipo within inches mbili kutoka mlango wa uke (vaginal opening) na asilimia kubwa ya nerves zipo katika mzunguko wa mlango wa uke.

Hii ina maana mwanaume yeyote mwenye uume wa inches mbili kama anajua namna ya kumfikisha mke kuridhika au kufika kileleni kupitia uke (vaginal climax) basi ataweza kumfikisha mke wake kileleni.

Je, ni unene (thickness) wa uume huweza kumridhisha mwanamke kimapenzi?Ni kweli unene inaweza kuwa ni factor hasa kutokana na uwezo wa mwanamke alionao kukaza misuli ya uke.

Je mwanamke ana umri gani, amekuwa na partners kiasi gani na amezaa watoto wangapi na zaidi amefanya kitu gani kuhakikisha misuli yake (uke) inakuwa imara.

Mfano:Ingawa suala la thickness si tatizo kwa wanawake wa nchi za Asia kama Japan, Singapore au Philippines kwa kuwa suala la kukaza misuli kwa wanawake ni moja ya sanaa.

Wanawake wa huko hucheza michezo ya kuingiza ping pong-ball (mipira mfano wa tennis) sita kwenye uke na kuzirusha futi 15 ili kuingia kwenye ndoo huku kila kimpira kinapotoka kinaendana na popping sound bila kukosa hata kimoja.

Pia huweza kuingia ndizi iliyomenywa kwenye uke huanza kuzikata ndizo (slice) vipande vipande huku vikidondoka.

Fikiria sasa likija suala la mapenzi hii inaonesha kwamba hao wanawake wanajua jinsi ya kuridhishana na kwao size does not matter.

Bahati mbaya ni kwamba tamaduni nyingi za Africa, ulaya na Amerika hazina mazoea ya kuwa na mazoezi ya kukaza misuli ya uke au uume.

Hivyo thickness ni muhimu kwa mwanamke ambaye uke wake ni loose na weak pia kama misuli yake hoi.

NB:
Hapa sina maana mwanamke ajihusishe na mchezo huu, it is illegal; najaribu kuelezea uwezo wa misuli ya uke ukifanyiwa mazoezi vitu inaweza kufanya.

Je, inakuwaje kama mwanaume ana uume mkubwa (unene na urefu) zaidi ya wastani ambao wanaume wengi huwa?Tafiti nyingi zinaonesha wanawake wengi hulalamika pale mwanaume anapokuwa na uume mkubwa zaidi ya kawaida na hasa kama hajui namna ya kuutumia.

Wanawake wengi huona ni huge barrier kwa ajili ya ku-enjoy sex kama mke na mume na wakati mwingine mwanamke hujisikia uncomfortable na huishia kukwepa.

Pia wanaume wenyewe ambao wana uume mkubwa tafiti zinaonesha kwamba wengi hujikuta katika huzuni na wanaombolezo kwa sababu partners wao kujisikia maumivu na kuumia na hata imesababisha mahusiano ya kimapenzi kati ya mke na mume kuzolota.

Je, hutokea nini pale mwanaume mwenye jumbo size akakutana na mwanamke mwenye uke uliobana?

Na wanaume ambao ukubwa wa uume (thickness ni zaidi ya kawaida wanapokutana na mwanamke ambaye ana size ndogo ya uke, au hakuwa wet sawasawa au hajazaa mtoto kabisa au bikira suala la sex linakuwa shughuli nzito kuihimili kwani lazima mwanamke akubaliane na pressure na pain za kuta za uke zinapochanwa.

Na pia kama mwanaume ana urefu unaozidi inches 6 ambayo ni average size kwa wanaume basi mwanamke anaweza kujikuta anajuta kwani anaweza kuhisi mwanaume anagonga hadi kwenye kizazi (internal reproductive organs).

Na matokeo yake mwanamke hujikuta anakaribisha magonjwa kama cysts ambayo huhitaji surgery na pia huweza kupata infections ambazo huweza kusababisha kukosa watoto.
Nini kifanyike?Jambo la msingi ni kwa mwanaume kufahamu namna ya kutumia tool yake vizuri, hii ni pamoja na kuwa caring, kufanya maandalizi ya kutosha.

Je, nini faida ya kuwa na uume mkubwa au uume mdogo?Kama mwanamke ana uke ambao ni loose na hawezi kuthibiti mwendo (misuli imelegea) basi tool kubwa kama hiyo huweza kumsaidia kupata feelings za kufurahia mapenzi hapa haijalishi mwanaume ana skills zozote au la.

Na mwanaume ambaye ana uume mdogo kuliko kawaida anaweza kuwa na faida kwa mwanamke ambaye ana uke mdogo (tight).

Hii ina maana mwanaume mwenye uume mkubwa ana match na mwanamke mwenye uke loose na hii combination huwezesha hao wawili kuwa na ridhiko kimapenzi.

Na mwanaume mwenye umbile dogo ana match na mwanamke mwenye uke tight.

Wakili kaeleza sababu za Mbunge Lijualikali kuachiwa huru

0
0


Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam March 30 2017  imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubali kuwa hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na mapungufu.

Mmoja wa mawakili waliokuwa wakisimamia rufaa ya mbunge Lijualikali, Fred Kiwelo amesema sababu mojawapo iliyopelekea kuachiwa huru ni pamoja na hati mashtaka kuwa na mapungufu ambapo kosa ambalo alikuwa amehukumiwa nalo limetofautiana na maelezo ambayo amesomewa.

Mashabiki wa Muziki Wamdhihaki Diamond Mtandaoni

0
0

MASHABIKI  wa muziki wa  Bongo Fleva nchini wamekuwa wakisambaza picha ya mwanamuziki nyota, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’,  ikimuonyesha akiwa katika hali duni tofauti na ukwasi alionao hivi sasa.

Mashabiki hao wamekuwa wakiisambaza picha hiyo kwa lengo la kumdhihaki ili kuonyesha kuwa maisha huanzia mbali,  hivyo watu wasisahau walikotokea.

Picha hiyo imekuwa ikisambazwa pamoja na ujumbe tofauti hivyo kuwaudhi  mashabiki wa mwanamuziki huyo na kuwafurahisha mahasimu wake.

Aidha  picha hiyo inawaonyesha Diamond na mwigizaji Irene Uwoya ambapo Diamond anaonekana katika taswira ya kijana mwenye hali duni tofauti na alivyo hivi sasa.

Hatarii..Siwema Amvua Nguo Hadharani Nay a Mitego ,Aanika Siri Zake Zote..!!!

0
0

MZAZI mwenziye na Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,  Siwema Hudson amesema kitendo cha serikali kumpa kashikashi kutokana na wimbo wake wa Wapo hakikumshangaza kwani alitarajia hayo yatokee kwa kuwa zilipendwa wake huyo ni mtu wa kukurupuka.

Akizungumza na gazeti hili juzi baada ya Nay kutoka polisi, Siwema alisema yeye amekaa na Nay kwa muda mrefu na mara nyingi akiamua jambo ndiyo hivyo wala hakuna mtu anayeweza kumshauri.

“Unajua Nay anapenda kukurupuka na wala hataki mtu apinge wazo lake, kama ameamua kufanya kitu anafanya tu na nilifahamu kuwa ipo siku hilo lingemtokea, sasa kama limepita anatakiwa kujitathmini upya,” alisema Siwema

Sakata la Vyeti Feki ..Ikulu Yatupa Mpira kwa Waziri Huyu..Kuhusu Vyeti vya Makonda Amefunguka Haya Mazito..!!!

0
0

WAKATI uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma unakamilika leo, Ikulu imemtwisha mzigo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, kuwa ndiye mhusika mkuu wa suala hilo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Machi 20, mwaka huu na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro, uhakiki wa vyeti vya elimu na taaluma pamoja na namba za mitihani kwa watumishi wa umma ulioanza Machi 12, mwaka jana, utakamilika rasmi leo.

Katika tangazo hilo, Dk. Ndumbaro anaeleza kuwa uhakiki huo haujalenga kumkoma mtumishi wa umma bali kuhakikisha kunakuwa na watumishi wenye sifa stahiki na kitaaluma na kitaalamu ili kutoa huduma zilizo bora na kwa weledi kwa wananchi.

"Serikali inasisitiza kuwa mtumishi wa umma atakayeshindwa kutumia muda uliotolewa kuwasilisha nakala za vyeti au namba za mitihani kwa wale waliopoteza, atakuwa amejiondoa mwenyewe katika ajira serikalini," linaeleza tangazo hilo ambalo Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Utumishi, aliithibitishia Nipashe kuwa ni lao.

Alipoulizwa na Nipashe kama uhakiki huo unawahusu pia wateule wa Rais, Temba alisema ni kwa watumishi wote wa umma, lakini akadai kuwa vyeti vya wateule wa Rais vinahakikiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi.

Nipashe ilipomtafuta Simbachawene kuzungumzia suala hilo, alidai masuala ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wakiwamo wateuliwa unafanywa na Wizara Nchi, Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

"Utumishi ndiyo wanaofanya hiyo kazi ya uhakiki na utunzaji wa taarifa zote za watumishi na wateuliwa, hivyo siwezi kujibu hilo suala," alisema Simbachawene.

Kutokana na majibu hayo ya Simbachawene, Nipashe ilimtafuta tena Temba ambaye alisisitiza kuwa wanaohakikiwa na wizara yao ni watumishi wa umma na kwamba vyeti vya elimu na kitaalamu vya wateule huwa wanavipeleka kwenye mamlaka husika za uteuzi.

Akizungumza na Nipashe kwa simu jana mchana kuhusu uhakiki wa vyeti vya elimu na kitaalamu vya wateule wa Rais, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, alisema Simbachawene ndiye anayepaswa kuzungumzia uhakiki huo.

"Muulize huyo huyo Simbachawene. Vyeti vinahakikiwa huko huko Tamisemi. Simbachawene yuko Ofisi ya Rais Tamisemi ambako mambo ya uhakiki (kwa wateule) yanafanyikia huko," alisema Msigwa.

Jitihada za Nipashe kutaka kuzungumza na Simbachawene jana hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopokewa na hakujibu ujumbe mfupi wa maandishi tuliomtumia kuhusu suala hilo.

Kwa miaka mingi, ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zimekuwa zikionyesha upotevu wa mabilioni ya shilingi kutokana na malipo ya watumishi hewa.

Kutokana na changamoto hiyo, Machi 12, mwaka jana, serikali ya awamu ya tano ilielekeza kufanyika kwa uhakiki wa watumishi hewa kwa kukagua vyeti vya kazi wanavyotumia ili kuwe na usimamizi na uwajibikaji.

Juni 22, mwaka jana, Rais John Magufuli akatangaza kusitisha ajira serikalini ili kuhakiki watumishi wote wa umma.

Kutokana na uamuzi huo, nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali vya likizo ya bila malipo vilisitishwa kwa muda hadi uhakiki utakapokamilika.

Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, baada ya kusitishwa kwa ajira, taarifa zilisambazwa katika halmashauri zote na idara za serikali kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na wizara Juni 13, jana kusitisha ajira hadi pale uhakiki utakapokamilika.

Kutokana na uamuzi huo, ajira 71,496 zilizokuwa zimepangwa kutolewa mwaka huu wa fedha na serikali kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwandani hazijatolewa, huku zikiwa zimebaki siku 91 kabla ya kumalizika kwa mwaka wa bajeti.

Kwa mujibu wa Temba, sekta ya elimu mwaka huu ilitarajiwa kuwa na ajira mpya 28,957, afya 10,870, kilimo 1,791, mifugo 1,130, huku maeneo mengine ambayo hayakutajwa, yakitarajiwa kuwa na ajira 28,748.

Ofisa huyo wa serikali aliiambia Nipashe kuwa hadi kufikia Agosti 2016, watumishi 839 walikuwa wamefikishwa kwenye mamlaka za kiuchunguzi likiwamo Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kutoa maelezo kabla ya kufikishwa mahakamani kutokana na kunufaika kwa kujipatia fedha kupitia watumishi hewa.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani Novemba 5, 2015, serikali yake imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kukomesha vitendo vya ufisadi vikiwamo hivyo vya kuwapo kwa malipo ya kila mwezi yanayokwenda mifukoni mwa maofisa wachache wasio waaminifu badala ya fedha hizo kuelekezwa katika shughuli nyingine za maendeleo.

Credit - Nipashe

OFA: Jipatie Water Dispenser Yenye Warrant Ya Mwaka (1) kwa Bei nafuu Mnoo!

0
0

*OFA YA ZA PASAKA!*

Jipatie Water Dispenser Yenye Warrant Ya Mwaka (1) kwa Bei nafuu Mnoo!

Dispenser mashine ya Friji chini Tsh *290000*

Dispenser Ya Maji baridi&Moto Tsh 195000/=
Kuweka Oda
🔴0743 757575

Tufollow instagram

@beinafuu_Shop
@beinafuu_Shop

Dkt Slaa Afunguka Haya Mazito Kuhusu Wanaomchukia Rais Magufuli..!!!!

0
0

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt Willbrod Slaa alipozungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli amesema kuwa watu waelewe hakuna nchi hata moja ambayo kiongozi atakubalika na watu wote kwa asilimia 100.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania akiwa nchini Canada Alhamisi hii, Dk. Slaa ambaye amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.

Dkt Slaa alisema wako watu ambao maslahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima watapiga kelele.

“Hatua zote zimechukuliwa,zinapaswa kuwa endelevu. Kwa bahati mbaya mchwa wengine waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na Serikali na huwezi kufagia Serikali nzima kwa siku mmoja. Kwa jinsi Rais ambavyo hayumbi na wala hayumbishwi, nina hakika atafikia malengo na kurudisha Taifa kwenye misingi ya tunu za Taifa ya uwazi, ukweli, uadilifu, kuheshimiana na kuthaminiana na hasa kujali utu,” alisema.

“Hii ndiyo hali ambayo Rais Magufuli kila siku anaiita ‘Transition’ (kipindi cha mpito). Tutafika tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli ana nia njema ya kufikisha Taifa mahali pazuri. Hii inahitaji kuweka pembeni maslahi yetu binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa Serikali au hata wa kisiasa.”

Chirwa Bwana...Soma Hapa Alichokisema Baada ya Kunyoa Upara Danga..!!!

0
0

STRAIKA wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa, amebadili mwonekano mpya kichwani kwake baada ya kunyoa nywele zote huku ikielezwa ni kutoa mikosi ili awafunge wapinzani wao Azam FC.

Yanga na Azam zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mzambia huyo amekuja na staili hiyo huku akiachia ndevu, muonekano ambao ameanza kuonekana nao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Rafiki wa Chirwa amelsemakuwa Chirwa ameipania mechi dhidi ya Azam, hivyo amepanga kufanya kila jitihada kuhakikisha anawafunga kisha bao atakalofunga liwe zawadi kwa mtoto wake aliyezaliwa wiki iliyopita.

Alipotafutwa Chirwa kuzungumzia hilo alisema:  “Sitaweza kuongea hadi nikapopata ruhusa kutoka kwa kocha.”

Lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha yake akiwa mazoezini akiwa na upara na kuandika ‘new look’.

ShyRose Bhanji Amvua Nguo Rais Magufuli..Adai Alimfanyia Ubabe kwenye Kamati Kuu..!!!

0
0



Katika Hali ya Kuonyeshwa kuwa hakuridhishwa na jina lake kukatwa na kamati kuu ya chama cha mapinduzi katika kuwania ubunge wa bunge la jumuiya ya afrika mashariki,Aliyekuwa Mbunge wa Bunge Hilo Kutoka Tanzania Shyrose Banji amefunguka Makubwa ya kushangaza.

Kupitia Ukurasa wake wakijamii wa instagram ,Shyrose ameonyesha kukerwa na kile alichokiita ni ubabe wa Mwenyekiti wa CCM,Rais Dk John Magufuli,ambapo kwa madai yake anasema kuwa Lilipofika jina lake,Rais Magufuli Alisema Kuwa Hataki hata kulisikia tupa kule.

Zaidi ni Hivi Alivyoandika katika ukurasa wake huo.

"Kwa habari nilizoziskia ni kwamba Mwekekiti wa Chama Rais JPM katika kikao cha CC ilipofikia jina langu kujadiliwa akasema: "Huyu wala sitaki tumjadili sitaki hata kumsikia" Naambiwa wajumbe kama wanne walinyoosha mkono lakini akawakatalia na kusema mjadala umefungwa #FullUbabe CC @hpolepole"

 

Ukweli Mchungu..Ushahidi wa Wazi kwa Uvamizi wa ,Makonda Alioufanya Clouds TV..!!!

0
0

Wakuu, naomba Leo tuweke ushabiki pembeni tudadavue  uvamizi wa RC pale Clouds TV. Naomba tuangalie mazingira yote kwa uwazi kabisa tuje na conclusive evidence juu ya tukio hilo la kulaaniwa. 

1. CCTV FOOTAGE 
Anaonekana mkuu wa mkoa akiingia kwenye mlango wa kwanza akifuatiwa na mtu mmoja aliyevaa kiraia hana silaha kisha askari askari mwenye silaha aliyefunga mlango huo. Jumla ya walioingia ni watatu. Halafu anaonekani mkuu wa mkoa akifungua mlango wa pili (wa kuingilia studio?). Anapoanza kuingia ndani footage inakoma

2. USHAHIDI WA MAZINGIRA
Masaa kadhaa baadaye taarifa zinazagaa kwamba clouds wamevamiwa na mkuu wa mkoa akiwa na askari wanane wenye silaha na kuwapiga vibaya sana licha ya kuwatisha watangazaji. Na hapa ndipo shida inapoanzia 

...ile footage haithibitishi tykio polite la uvamizi. 
*Ukiitazama haioneshi ubabe wowote kwenye kuingia ndani studio. RC aliingia kwa kufungua mlango taratibu

*Nje walikuwapo walinzi ambao hawakushuhudia nia yoyote ya uvamizi mpaka pale walipopigiwa simu na Ruge (aliyekuwa nyumbani kwake). Wao walimwona RC akiingia kawaida tu hapo studio. 

*Mazingira ya studio ya tv huwa na camera nyingi tu. Ni ajabu sana kusiwe na kipande japo kifupi cha kile kilichotokea ndani ya studio. Hats hiyo footage, ni kwa nini inakoma pale tu RC anapoanza kuingia ndani? Je, ni kweli kuwa clouds wameweka camera hapo mlangoni tu? Au labda mkuu wa mkoa aliamuru kamera zizimwe kabla ya kuingia ndani? 

*Kama kamera zilikuwa mbovu walau tungepata hata audio ya kile kilichitokea ndani basi. Sio masimulizi tu. Hapo ni studio na vifaa vyote vipo. Kwa nini tusadiki masimulizi? 

3. RIPOTI YA KAMATI
Kamati ilitoa ripoti kwamba RC alivamia akiwa na askari watano? na si nane. Pia wafanyakazi hawakupigwa kama ilivyoarifiwa hapo awali. Ni kwa nini ilitolewa taarifa kinzani hapo awali? 

4. URAFIKI WA RC NA CLOUDS 
Ruge anakiri kuwa hawa ni marafiki wa siku nyingi. Tena anatoa kauli tata kuwa RC anatabia ya kwenda hapo studio kupiga stori. Swami hapa, je, kila anapokwenda hutumia utaratibu gani kuingia studio? Je, huwa anaacha wapi walinzi wake? Kuna rekodi yoyote ya clip za cctv za huko nyuma ili tuone ilivyokuwa? 

5. Kilichopo mpaka sasa ni ushahidi wa masimulizi ya wanaodaiwa kuvamiwa. Ushahidi wa clip ulikuwa na lengo la kuandaa akili ili wasikilizaji wafanye mwendelezo wa uvamizi akilini mwao. Mtu wa kwanza kabisa kuripoti uvamizi huu alipaswa kuwa mlinzi. 

Ni mtazamo wangu tu, baada ya tafakuri ya kina. Twende na constructive criticism kama nilivyofanya mimi, ile timu matusi mkae kando kuruhusu mjadala. Nawasilisha.

Maswali yatokanayo na mjadala unaoendelea : 


**kwa nini Gwajima aliripoti kuvamiwa na kupigwa watangazaji? Nani aliyewasiliana naye kumpa habari ili alipue? Was it a coordinated move? 

**kwa nini clouds hawataki kuripoti tukio hili polisi? Kwa nini walisubiri liwe magnified na mitandao kwanza? Je, yawezekana walikuwa wanapima upepo? Je kuna yawezekana kuna ofisi ambayo walitarajia itaingilia kati ili kulishughulikia suala hili tofauti na vyombo husika? 

**Kwa nini ililazimu waziri kukemea vikali hata kabla ya kujiridhisha usahihi wake? Kwa nini jinai hii haikuhusisha vyombo rasmi vya uchunguzi? Kwa nini haikufanyika coordination na mamlak teuzi ya RC? Kulikuwa na haraka gani ya kukimbilia kwenye press utadhani studio iliteketezwa? What is behind all this!?
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images