Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YATEKETEA KWA MOTO

0
0
MABWENI saba ya wavulana wa Shule ya Sekondari Ivumwe, mkoani hapa, inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yameteketea kwa moto na kuteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi wa shule hiyo.

Moto huo ulizuka jana majira kati  ya saa tatu na nne asubuhi wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani kuendelea na masomo yao.

Akitoa taarifa mbele ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi taifa, Abdallah Majura Bulembo, aliyefika mkoani hapa kujionea janga hilo, Mkuu wa shule hiyo, Emmery Muhondwa, alisema mbali na kuteketeza mabweni hayo, hakuna madhara ya kibinadamu.

Mwalimu Muhondwa alisema moto huo uliteketeza vitanda 93, magodoro 186, mashuka 372, blanketi 186, mabegi 186, matranker 186 pamoja na vitabu na madaftari, vyote vikiwa na jumla ya  thamani ya sh milioni 30.

“Katika kukabiliana na hali hiyo, tumewahamishia wanafunzi katika madarasa yaliyokuwa yanatumiwa na kidato cha sita ili walale humo, tumeazima magodoro 169 kutoka Shule ya Sekondari ya Loleza na tunawasiliana na wazazi ili wawanunulie nguo za kushindia na za shule huku tukiendelea kukarabati mabweni,’’ alisema Mwalimu Muhondwa.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa, Bulembo, aliwapa pole wanafunzi na kuwataka wawe wavumilivu katika kipindi hiki.

Pia alitoa mchango aliouita wa dharura wa sh milioni tatu  kwa ajili ya ukarabati wa mabweni na mahitaji mengine ya haraka na kuahidi kuwashirikisha wadau wengine wa elimu ili kuwasaidia wanafunzi hao.

Mbali na mchango huo, alitoa tamko kuzitaka shule zote zinazomilikiwa na jumuiya hiyo kuwa na bima ya moto.

“Kuanzia sasa, suala la bima ya moto ni la lazima kwa shule zote za jumuiya ya wazazi wa CCM. Baraza Kuu tutakutana kwa dharura mjini Dodoma Mei 17, mwaka huu na tutakachokipata tutakileta haraka kwenu ili kusaidia janga hili la moto,’’ alisema Bulembo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Dk. Victoria Kanama, alimshukuru mwenyekiti huyo kwa mchango wake.

“Tutahakikisha tunakarabati mabweni haya ndani ya mwezi mmoja na kufanya jitihada za kuongeza ufanisi wa ufaulu katika shule yetu,” alisema Dk. Kanama.

Ivumwe, ni kati ya shule zenye sifa ya kufaulisha ambapo katika mtihani wa utamilifu (Mock), kidato cha sita mwaka huu, shule hiyo imeshika nafasi ya pili kati ya shule 26 zilizokuwa na watahiniwa 30 Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

DAWA ZA DICLOPA NA DICLOFENAC ZADAIWA KUWA NI HATARI KWA MATUMIZI YA BINADAMU

0
0
Dawa za Diclopa na Diclofenac zadaiwa kuwa ni hatari kwa matumizi ya binadamu!
Radio Dutch Velle ya mjini Kolon Ujerumani jana ilitangaza kuwa Dawa Diclopa na Diclofenac ni hatari kwa matumizi ya binadamu, Imegundulika Vidonge hivyo husababisha kansa ya Ini na Ubongo,Ugonjwa wa moyo, Kiharusi, Vidonda vya Tumbo au kifo cha ghafla.

Chanzo: Radio Dutch Velle

UHURU" I WILL MAKE EAST AFRICA THE PRIDE OF AFRICA"

0
0
The President, who is the sitting chair of the regional bloc, wants the Community to become a shining example to the rest of Africa.
He said the EAC integration process is aimed at making it easier for the movement of people and goods which will in turn increase trade and thus improve the lives of the people.
The President spoke when he met the World Trade Organisation (WTO) Director General Robert Azevedo at State House Nairobi.

The President said the benefits of integration far outweighs all risks, adding that trade is an important tool in enhancing peace and stability in Africa.

He said trade will help create job opportunities, adding that he is willing to partner with WTO to increase trade in the region and throughout Africa.
He cited trade cooperation between countries as one way of achieving political stability.

TRADE FOR PEACE

“Trade can be used as an instrument of peace in Africa,” the President said.

President Kenyatta said time has come for Africa to move away from an agrarian continent to an industrialised one.

“This is the time for Africa. We won’t confine ourselves to agricultural activities but also industrial and commodity exports,” he said.

Mr. Azevedo assured of the global trade organization’s support to president’s vision of accelerated East African Community integration.

Mr. Azevedo --who is on his first Africa trip, commended President Kenyatta’s efforts in mobilising East Africa leaders and citizens towards integration.

He said President Kenyatta has effectively used trade to unite people and advocate peace and stability in the region.

He said his organisation is in the process of setting up programmes to help member countries in capacity building in the integration process.

CHINA SET TO OVERTAKE U.S.A AS THE BIGGEST ECONOMY IN THE WORLD

0
0
China is poised to overtake the U.S. as the world’s biggest economy this year, while India has vaulted into third place, ahead of Japan, using calculations that take exchange rates into account.
China’s economy was 87 percent of the size of that of the U.S. in 2011, assessed according to so-called purchasing power parity, the International Comparison Program said in a statement in Washington yesterday.
The figures, compiled by the International Comparison Program hosted by the World Bank, are the most authoritative estimates of what money can buy in different countries and are used by most public and private sector organisations, such as the International Monetary Fund. This is the first time they have been updated since 2005.
The US has been the global leader since overtaking the UK in 1872. Most economists previously thought China would pull ahead in 2019.
Changes in methodology contributed to the speed of China’s rise and India jumping to third-biggest in 2011 from 10th in 2005. Purchasing power parity seeks to compare how far money goes in each country. Using market rates, U.S. gross domestic product was $16.2 trillion in 2012, compared with China’s $8.2 trillion.
In 2005, the ICP thought China’s economy was less than half the size of the US, accounting for only 43 per cent of America’s total. Because of the new methodology – and the fact that China’s economy has grown much more quickly – the research placed China’s GDP at 87 per cent of the US in 2011.
For 2011, the report says: “The US remained the world’s largest economy, but it was closely followed by China when measured using PPPs”.
With the IMF expecting China’s economy to have grown 24 per cent between 2011 and 2014 while the US is expected to expand only 7.6 per cent, China is likely to overtake the US this year.

YALIYO TOKEA JANA NI AIBU..RUGE AGOMBANIWA KWENYE SOCIAL MEDIA

0
0



YALIYOTOKEA JANA NI AIBU...
Sorry to say ila Siamini kama Wanawake wanaweza kukosa akili kwa kiwango hiki...Nilijua Maturity ya Wanawake comes with age lakini nadhani I was wrong!
Kugombea Babe Ake kwenye Social Media kuprove Mchepuko NDIO DILI....NGACHOKA MIE

KIKWETE "MISHAHARA ITAPANDA NA KODI (PAYE) NITAIPUNGUZA"

0
0
Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi yao.

Alisema malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.

“Mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo, tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo,” alisema.

WAMACHINGA WAPAMBANA NA POLISI KARIAKOO

0
0
Jeshi la Polisi limelazimika  kutumia mabomu ya machozi kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) katika Soko Kuu la Kariakoo.

Hamisha hamisha hiyo yenye baraka za uongozi wa mkoa zilianza mapema mwezi uliopita kwa lengo la kuondoa biashara zisizo rasmi katikati ya jiji la Dar es Salaam, pamoja na bodaboda, bidhaa zimwagwazo chini, mama ntilie na vibanda vya vocha.

Majira ya saa tisa alasiri magari ya polisi yaliwasili sokoni hapo huku yakiwa na askari polisi na mgambo waliokuwa wamevaa fulana na kofia za Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu), zenye rangi ya njano, na kuanza kuwakamata wamachinga hao.

Askari hao waliokuwa katika magari aina ya Land Rover Defender na Toyota LandCruiser waliuvamia mitaa ya Kongo na Mchikichini kufanya oparesheni hiyo kabla hawajalazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwaondoa walengwa katika  eneo hilo.

Hali hiyo ilizua tafrani kwa wateja waliokuwa wakinunua bidhaa kwenye maduka hayo  walioenda kwa ajili ya kupata mahitaji yao walikimbia hovyo  ili kujiokoa kutokana na vurugu hizo.

Maduka mengi ya mtaa huo, kuanzia kituo cha daladala hadi sokoni, yalilazimika kufungwa kwa hofu ya kupoteza mali kutokana na vibaka wanaotumia nafasi kama hizo kuiba vitu.

Kazi haikuwa rahisi kwa askari hao kwani wamachinga kadhaa hawakuwa tayari kuona wakikamatwa au kupoteza mali zao hivyo kulazimika kupambana kwa kile kilichoonekana kama kuwa radhi ‘kufia mali’ zao. Wamachinga hao waliokaidi amri halali ya jeshi hilo, walikamatwa na kuingizwa kwenye gari la polisi .

Watu walionekana wakikimbia hovyo na wengine wakipanda gari lolote bila kujali linaelekea wapi ili mradi waondoke eneo la tukio kabla hawajapatwa na lolote  na kuumia au kuibiwa. “Sisi tutaenda wapi bwana. Acha wafanye mambo yao wakiondoka tunarudi tena kuendelea na biashara zetu,” alisema Hamis Jumanne, anayefanya biashara ya kuuza  maji.

Kamanda wa Polisi Mkoa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa zoezi la kuondoa wamachinga jijini ni endelevu.

KWA WANAO MPONDA PENNY NA HALIMA KIMWANA KUWEKA TATTO YA BRO AKE INAKUHUSU HII

0
0

Huku Instagram leo .....Teamukwelinauwazi Aibuka na Kuwatetea Penny na Halima Kimwana baada ya Watu fulani fulani kuwasema sana ...Jisomeee hapa chini:






PICHA MTOTO ATAKA KUMUUA BABA YAKE HUKO MWENGE JIJINI DAR

0
0
Katika tukio la kushangaza, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Anord Michael mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya vurugu kubwa nyumbani kwao, akidaiwa kutaka kumuua baba yake mzazi kwa sababu ambazo hazikueleweka sawasawa. 
Huku majirani na watu wengine wakishangazwa na kitendo hicho, Anord alimfungia ndani baba yake mzazi na kuanza kumshambulia kwa silaha mbalimbali kabla ya kuchukua panga kwa lengo la kutaka kummaliza kabisa.

Mzee Michael, kuona kijana wake amepania kummaliza, alipiga mayowe ya kuomba msaada, kitu ambacho kilifanikiwa kwani mara moja wasamaria wema walijitokeza na kumuokoa kwa kumhifadhi katika chumba kingine ndani ya nyumba hiyo. 

Pamoja na hivyo, kijana huyo ambaye bado watu wana mashaka na utimamu wa akili yake, aliendelea kufanya fujo huku akivunja mlango wa chumba alichohifadhiwa baba yake ili aweze kumtoa roho, huku pia akitishia kumuua mtu yeyote ambaye angejaribu kumsogelea.

Baba Aliyetaka kuuwawa

 Akiwa katika hatua za mwisho kuvunja mlango huo huku baba yake naye akianza kusali sala ya mwisho kabla ya mauti kumfika, ghafla askari wenye silaha waliwasili eneo hilo na kuanza kumdhibiti kijana huyo.Hata hivyo, zoezi la kumdhibiti kijana huyo halikuwa rahisi, kwani bado alisababisha timbwili kubwa kabla ya maafande hao kutumia ujuzi wa kikazi bila kutumia risasi na kumweka chini ya ulinzi. 

Katika hali ya kushangaza, baada ya askari polisi kumuuliza sababu iliyomfanya afikie uamuzi wa kumuua baba yake mzazi, Anord alidai mzee huyo ndiye chanzo cha yeye kuharibikiwa kimaisha.
Baadaye maafande hao walimzoa kijana huyo na baba yake kuelekea Kituo cha Polisi Mabatini  Kijitonyama  kwa mahojiano zaidi.

LIVE AUNT EZEKIEL AKIDENDEKA...AMUIGA DIAMOND NA WEMA

0
0
Aunt ezekiel afata nyayo za wema sepetu na diamond the platnumz, ni jana tu tuliona diamond the platnumz na wema sepetu waliamua kuachia picha ikionyesha huku wakinyonyana ndimi, basi na aunt yake akaona isiwe shida, na yeye huko alipo dubai akaamua kufanya yake kwa kufanya mapenzi na mpenzi wake, na baada ya hapo akaamua kufotoa picha huku wakinyonyana ndimi na kuficha sura ya mwanaume wake 


SAKATA LA MIL 13:KAJALA AFUNGUKA KUWA "SIMLIPI WEMA MIL.13 NG'O"

0
0
JAMBO limezua jambo! Zile shilingi milioni 13 alizolipa staa mkubwa wa kike Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ mahakamani ili kumnusuru Kajala Masanja kwenda gerezani, zinaendelea kusababisha fukuto na sasa Kajala amejibu mapigo, akisema hatamlipa Wema fedha hizo.


Wema na Kajala wapo kwenye gogoro zito kwa muda mrefu huku mashabiki wa mastaa hao waliojipa majina ya Team Wema (wanaomuunga mkono Wema) na Team Kajala (walio upande wa Kajala) wakiukuza ugomvi huo kwa kushambuliana kwa maneno makali kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
 WEMA KUFUNGUKA
Katika gazeti hili, toleo namba 877 la Aprili 25-Mei Mosi, 2014 la wiki iliyopita, liliandika habari ya Wema iliyokuwa na kichwa; Kwa mara ya kwanza Wema afunguka, asema: NAJUTA KUMLIPIA KAJALA MIL. 13!
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Wema kufunguka baada ya bifu la kimyakimya la muda mrefu ambapo alifafanua chanzo cha bifu lao na namna anavyojuta kumlipia Kajala fedha hizo.
 “Kusema kweli najuta kumlipia (Kajala) ile faini ya Sh. milioni 13. Bora angeenda jela miaka saba kuliko kunisababishia matatizo na maumivu kiasi hiki. Mimi sijawahi kumsema vibaya K kisa eti nilimlipia fedha hizo,” alisema Wema katika gazeti hilo.
Alipoambiwa kama Kajala yupo tayari kurudisha fedha hizo alisema:
“Kama anataka kunilipa, anilipe kisha aende jela maana mimi sikumkopesha, nilitoa kwa moyo.”


 HABARI ZA MOTO
Baada ya gazeti hilo kuruka mitaani na Kajala kulipata ndipo akaeleza mambo mazito.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Kajala alisema katika vitu ambavyo Wema anatakiwa kuvisahau ni pamoja na kumlipia mahakamani hizo milioni 13.
 “Siwezi kumlipa ng’o. Namlipa nini sasa na kivipi? Kwani tulikopeshana? Hakuna anachonidai Wema, hata kama akisema nimlipe, siwezi kufanya hivyo,” alisema Kajala.
 Huku akimwaga machozi, Kajala aliendelea: “Unajua haya mambo yanachukuliwa kirahisi tu na wadandiaji wa mambo, ni vile watu hawajui ni kwa kiwango gani hili suala linaniumiza.
“Wema alinisaidia, alinilipia fedha mahakamani wakati ambao nilikuwa na uhitaji na sikuwa na zile fedha. Kama asingejitokeza kunilipia nilikuwa nakwenda jela.
 “Lile ni jambo kubwa. Thamani yake haifananishiki na fedha. Ule ulikuwa ni utu tu, sasa leo iweje ligeuzwe kuwa kama deni? Siwezi kufanya hivyo.”
 YUPO TAYARI KWA SULUHU
Kwa mara nyingine tena, Kajala alisema kuhusu kupatana na Wema yupo tayari muda wowote, maana haoni sababu ya kuendelea kwa ugomvi huo.
 Hii ni mara ya tatu Kajala kuzungumzia suluhu akisisitiza: “Nakosa amani kabisa na huu mzigo. Natamani kuutua. Nipo tayari kukutanishwa naye hata leo tuyamalize.”


HABARI YA MJINI
Habari ambazo zimeenea mjini lakini bado hazijathibitishwa zinadai kuwa, Kajala anajiamini kwa sababu anajua fedha alizolipiwa na Wema si zake, zililipwa na aliyekuwa mwanaume (boyfriend) wa Wema, yule kigogo wa Ikulu anayetajwa kwa jina la CK.
 “Lile lilikuwa agizo, Wema hakuwa na fedha zote zile kwa ajili ya kumlipia Kajala. Alipewa na CK na kuambiwa amlipie ili asiende jela,” alisema mmoja wa watu wa karibu na mastaa hao kwa sharti la kutotajwa gazetini.
 ETI ULIKUWA MPANGO!
Chanzo kinaendelea: “Alivyoingia mitaani, CK akajiweka karibu na Kajala na kumweleza mchongo mzima, kuwa yeye ndiye aliyetoa  hizo fedha kwa hiyo asiwe na wasiwasi.
“Ndiyo maana hata Wema na CK walivyoachana ikawa rahisi kwa CK kujimilikisha Kajala moja kwa moja kwa sababu anaujua ukweli.”
Haya ni madai ya chanzo chetu ambayo hayajathibitishwa na wahusika.
 SAFARI ZA CHINA VIPI?
Habari nyingine ambazo bado zinafuatiliwa ili zithibitishwe, zinasema kuwa, safari nyingi za Kajala kwenda China kwa mapumziko huwa anamfuata au kuongozana na CK.
“Hata sasa hivi (juzi Jumatano) wapo safarini China wanakula bata. Yaani haya mambo yamejifunga sana. Yanahitaji hekima sana kuyamaliza,” aliendelea kudai.
 BIFU HADI LINI?
Wadau wa tasnia ya filamu Bongo, kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipiga simu na kutuma ujumbe mfupi katika chumba cha habari cha magazeti pendwa Tanzania, Global Publishers na kueleza jinsi ambavyo mtaani kunazidi kuchafuka kuhusu sakata hilo huku wengi wakiwataka wayamalize.
 “Haya mambo yanakuzwa na watu. Hawa ni wasanii wazuri, wana majina makubwa na wanaendana, nashauri wazungumze, wayamalize. Bifu lao halijengi badala yake linabomoa,” Maimuna Sadallah wa Majani Mapana, Tanga alieleza katika ujumbe wake.
 Msomaji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la mama Mwaija mkazi wa Mbagala - Maji  Matitu, Dar alikuwa na haya ya kusema: “Haya mambo ya wanangu Wema na Kajala yananichoma sana. Napenda sana filamu zao, nafurahia namna wanavyoshirikiana na kusaidiana. Hebu wamlaani shetani.”
 WAZAZI WAOMBWA KUINGILIA KATI
James Sukae wa Kimara-Baruti, Dar alisema: “Hili jambo na umri wao naona ni kubwa sana kwao kulimaliza. Tukisema tusubiri wayamalize wenyewe, haitawezekana ila litazidi kuwa kubwa.
“Kajala ana wazazi wake, Wema naye kadhalika.
 Tena hapa nisisitize, wazazi wanaopaswa zaidi kushughulikia hili ni mama zao. Mama Kajala na mama Wema wanatakiwa kukutana na watoto wao ili wawakalishe na kuzungumza.
“Kwangu mimi, mbele ya wazazi ni jambo dogo sana. Hekima zao ni kubwa na bila shaka watalimaliza kuliko kuacha likielea kama ilivyo sasa. Wakipuuzia hili suala litasababisha janga kubwa.”

GPL

TAARIFA NYINGINE WALIOPEWA NDUGU WA ABIRIA WALIOPOTEA NA NDEGE YA MALAYSIA

0
0
Toka March 8 2014 mpaka leo ikiwa ni May, ndege ya Malaysia iliyokua imebeba zaidi ya watu 200 haijulikani ilipo baada ya kupotea ikiwa inatokea Malaysia kwenda Beijing China.
Kwa siku zote hizo toka imepotea ndugu wa abiria wa ndege hiyo wamekua wakishinda kwenye hoteli ambazo pia zimekua zikitumiwa na shirika hilo la Malaysia kukusanyika na kutoa taarifa kuhusu kinachoendelea kwenye kuitafuta ndege hiyo.
May 1 2014 taarifa zimeanza kusambaa kwamba ndugu hao sasa wamepewa maagizo waondoke kutoka kwenye hoteli zote walizofikia Beijing na Kuala Lumpar na kurudi nyumbani kwao ambapo taarifa za chochote kitakachotokea watazipata wakiwa hukohuko majumbani.

Hii iliwafanya ndugu kadhaa kuangua tena vilio na kupiga mayowe baada ya kujua kwamba taarifa ya shirika hilo la ndege inamaanisha haitakuwepo tena ile mikusanyiko ya kila siku kwenye chumba cha mikutano kwa ndugu hao kupewa taarifa za kinachoendelea kwenye zoezi la utafutaji wa ndege hiyo.
Kwenye hoteli ya Lido Beijing ambako kampuni hiyo ya ndege imekua ikiwalipia ndugu hao wa abiria toka ndege ipotee, kulikua na watu wanaozidi 500 ambao wote ni ndugu wa abiria waliopotea.
Hata hivyo kampuni hii ya ndege itaanza kutoa malipo ya pesa kwa ndugu hao siku za karibuni ambapo japo haijasema itatoa kiasi gani, sheria inasema ndugu wanaweza kulipwa kuanzia dola za kimarekani laki moja na nusu mpaka laki moja na elfu 75.
Ripoti mpya iliyotoka inasema maafisa hawakua wamegundua kupotea kwa ndege hiyo mpaka dakika 17 baadae na walichelewa kwa dakika 240 kuanza kuitafuta ndege hiyo baada ya kupotea kwenye radar.

TAARIFA KUTOKA YANGA KUHUSU WACHEZAJI WAKE WAWILI WALIO SIGN KUICHEZEA AZAM

0
0
Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao 2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu
Uongozi wa Yanga uliandikia TFF barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya kufuatia Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa na wachezaji watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata majibu juu ya utaratibu utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.
Hivyo makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na uongozi wa Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni na katika hali ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini kuichezea timu ya Azam FC.
Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013, alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo alisema hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda wa mwaka mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walishindwa kuwa wakweli kwa viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango yao ya kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga SC.
Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na ripoti ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa hivi karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na kuafikiana mipango ya msimu ujao.
Aidha uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na washabiki wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani Yanga bado ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea kuboresha kikosi chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu ujao

KAJALA "NAIGOPA SIMU YANGU" ADAI UGOMVI WAKE NA WEMA UMEKUZWA NA WATU

0
0

Muigizaji wa filamu nchini, Kajala Masanja amesema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaigopa simu yake zaidi ya kupiga na kupokea.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV wiki hii, Kajala amesema amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo. Kajala amesema ugomvi wake na Wema haujatokana na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana yake’ na kwamba umetokana na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao. Amesema pamoja na ugomvi wao kusababisha na mambo ya kawaida, umekuzwa mno na watu pamoja na vyombo vya habari kiasi cha kuwafanya wajikute maaudui kweli.

Kuhusiana na tetesi kuwa alianza kumdharau Wema baada ya Miss Tanzania huyo wa zamani kuishiwa fedha, Kajala amesema amekuwa rafiki yake tangia enzi hana chochote. “Alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwahiyo kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela mimi sio rafiki yangu tena, sio kweli,” amesema.

Kajala amekiri kuwa kukosana kwake na Wema kumeathiri maisha yake.

“Inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nammiss,” amesema.

Kajala ameeleza kuwa ameshawahi kumtaka Wema wamalize ugomvi wao lakini ilishindikana japo amesema kwakuwa ugomvi ni wao wenyewe, ipo siku utaisha na watakuwa marafiki tena.

RAY C AKANUSHA KURUDIANA NA MWISHO MWAMPAMBA

0
0
Rehema Charamila aka Ray C amekanusha kilichoandikwa na gazeti la Visa kuwa amerudiana na aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa mara mbili Mwisho Mwampamba. Wawili hao waliwahi kuwa na uhusiano miaka kadhaa iliyopita.

Kupitia Instagram Ray C ameandika: Sijamuona Mwisho na Kama mwaka wa Sita huu!!!udaku Mwingine umezidi kwakweli sipendi……..He is happily married and I respect him!!!!ati I met him last week n we exchanged numbers that’s a big big lie jamani……Am happy and Single….Am loving my life

WEMA NA SEPETU WAKIJIACHIA CHUMBANI KWA RAHA ZAO

0
0


MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa katika pozi la kimahaba kitandani Naf beach hotel. Picha hizi Wema  amezitupia katika akaunti yake ya Instagram na kuandika maneno yafuatayo "Thank God tumemaliza salama...Nd we are Happy it went well...Alahamdulillah....Baadae inshallah...Tulale kwanza alafu yale mapichapicha na kila kitu, leteeeeers.."

LULU AWATETEA MABOSI WAKWARE

0
0
Stori: Gabriel Ng’osha
STAA wa filamu ya Foolish Age, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewatetea mabosi wa wasanii akidai si wote wana tabia ya ‘kuduu’ na wafanyakazi wao.

Akijibu swali aliloulizwa na paparazi wetu kuhusiana na mabosi wakware, Lulu alitiririka:
“Imezoeleka kuwa mabosi wote hawawezi kufanya kazi na msanii bila kuomba penzi, si wote, wapo wasioomba,” alisema Lulu ambaye aliwahi kutajwa kuwa anatembea na mmoja wa mabosi wake wa sasa.

KIKWETE AUNDA TUME KUCHUNGUZA OPERATION TOKOMEZA UJANGILI

0
0

Rais Jakaya Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi, kuhusu vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ilisema, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.

Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Vilevile, Rais Kikwete amewateua Jaji Mstaafu Stephen Ihema na Jaji Mstaafu Vincent Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.

Hatua ya Rais Kikwete kuunda tume hiyo inakuja baada ya Operesheni Tokomeza Ujangili kusitishwa na Bunge kutokana ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu wakati wa utekelezaji wake.

Operesheni hiyo iliayoanza Oktoba 2013 na kusitishwa Nobemba 4 mwaka jana, ndiyo iliyowang’oa mawaziri wanne kwa kushindwa kusimamia vizuri utekelezaji wake.

Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.

Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, na kutaja majukumu ya tume hiyo kuwa ni pamoja na kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.

Majukumu mengine ni kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza na kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.

Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.

Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.

Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.

WATOTO WASIMULIA JINSI WENZAO WALIVYOKUFA MAJI KWENYE BWAWA LA KUOGELEA HOTELINI

0
0

Ilikuwa ni safari ya kawaida ambayo ilitarajiwa kuwapa faraja watoto. Lakini hali imekuwa tofauti baada ya matarajio hayo kugeuka majonzi kwa mtaa mzima kutokana na kuondokewa na watoto watatu kwa wakati mmoja.

Ni mara chache sana watoto hutoka pamoja kwenda mbali kufurahia na wenzao. Hivyo Janet, Ndimbumi na Eva waliamini kuwa siku hiyo ingewapa furaha na pengine hadithi za kwenda kusimulia shuleni, lakini haikutokea kama walivyotarajia; simulizi zikawa tofauti.

“Tulistuka kuuona mwili wa Janeth ukiwa unaelea juu ya maji,” anasema kaka yake, Goodluck Kihoko (14) ambaye siku hiyo alienda pamoja na watoto wengine 20 kwenye Hoteli ya Landmark iliyo Mbezi Beach, jijini Dar es salaam.

“Tuliwaita walinzi, lakini wakapuuza. Tuliwaita walinzi kwa muda mrefu ndipo wakafika na wakati huo mama na wale vijana walikuwa mbali na pale tulipokuwa tukiogelea. Baada ya muda walikuja na tukauona mwili wa pili ukiibuka,” anasimulia Gooluck kwa uchungu.

Wakisimulia tulio hilo, watoto waliokuwa katika msafara huo Florian Masonda (12) anasema  walichukuliwa na jirani yao, Anita Mboka kwenda kusherehekea nao siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake, Derick Mboka aliyekuwa anatimiza umri wa mwaka mmoja.

Florian anasema baada ya kufika hotelini hapo walianza kucheza mpira wa kikapu huku watoto wengine wakiogelea na mama Mboka aliyewapeleka pamoja na wale vijana wakiwa wamekaa wakipata vinywaji.

“Tulikuwa tunacheza mpira wa kikapu na ghafla tulisikia kelele baada ya mtoto mmoja kuja kutuita na kutupatia taarifa kuwa kuna watoto wamezama chini ya maji na hawaonekani. Tuliondoka na baada ya kufika kwenye bwawa la kuogelea ndipo tulipowaona wakiwa tayari wamekunywa maji mengi,” anasema Florian.

Naye Goodluck anasema yeye na watoto wenzake zaidi ya 20 waliondoka Kijitonyama wakiwa na vijana wanne kwenda kwenye sherehe hiyo.

“Tuliondoka hapa saa kumi na moja jioni, baada ya kufika kule tulianza kuogelea kwenye bwawa. Watoto wengine walikuwa wanakwenda kuogelea kwenye maji marefu, walizuiliwa mara tatu, lakini baada ya walinzi kuondoka walirudi na kuzama,” anasema.

Kwa uchungu alionao Bahati Sisala alikuwa amekaa akiwa ameduwaa macho yake yamevimba na mekundu kutokana na machozi yaliyomtoka kwa muda mrefu.

Akiwa amejiinamia bado haamini mkasa uliomkuta binti yake kipenzi Ndimbumi Sisala (9) uliosababisha kifo chake ambacho kilimkuta ghafla katika hoteli hiyo Aprili 27.

Lugano Mwakyosi, ambaye ni msemaji wa familia hiyo inayoishi Kijitonyama Mpakani A, anasema Sisala amechanganyikiwa kutokana na kifo cha binti yake aliyempenda sana.

DOGS FOR SALE....GERMANY SHEPHERD ..CALL 0768570703

0
0


These two healthy, clean and medically cared germany shepherd dogs on sale. Call now 0768570703 price 750,000/ or 460$ each
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images